Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KONGAMANO LA MKUTANO WA KIMATAIFA LINAYOSHUGHULIKIA MASUALA YA USTAWI WA JAMII LIMEZINDULIWA RASMI LEO.

$
0
0
Na Agness Francis, Michuzi Tv

Mwenyekiti wa bodi ya magavanazi wa taasisi ya ustawi wa Jamii Sophia Simba leo amefungua kongamano la  mkutano wa kimataifa  inayoshuhulika na  maswala ya ustawi wa jamii ili kuleta chachu ya maendeleo endelevu ya uchumi wa viwanda,  ambao umehudhuriwa na watu kutoka Sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi  utakao malizika mei 10 mwaka huu. 

Sophia Simba amezungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi  huo ambapo amesema kuwa  mkutano huo una lengo la kujua ni jinsi gani maswala ya ustawi wa jamii utakavyo saidia katika kukuza  uchumi na mabadiliko ya viwanda hapa nchini. 

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa ni vizuri jamii ikaelewa hata nchi nyingine duniani kama Korea, China na Malaysia wamepitia misukosuko mingi mpaka hapo walipofikia  kwa kujitolea kwa hali ya juu. 

"Juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakisha tunafika pale tunapokakusudia kama tukiwa wote tunapeleka elimu Katika jamii, na serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa sheria na taratibu  mbali mbali zilizopo ili kulinda ustawi wa jamii katika utendaji wake wa kazi"amesema Sophia Simba. 

Vile vile ameongezea kwa kusema  kuwa Taasisi ya Elimu ya juu ikiwemo na ya ustawi wa jamii zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba taaluma hiyo inatoa mchango mkubwa katika kuleta mapinduzi ya viwanda hapa nchini. 

Hata hivyo  Makamu mkuu wa Taasisi  ya mipango, fedha na utawala Zena Mabeyo amesema kuwa inatakiwa tuwe na rasilimali watu  kuweza kuwashawishi watu kuwa na mfumo bora ili kuweza kuwafikia wananchi katika safari ya kuelekea kuboresha Tanzania ya viwanda. 

"Hatuishii hapa tu kwa kadri ya miaka inavyozidi kuendelea tutakuwa tunaandaa makongamano  ya aina hii yatakayoangalia michango ya fani nyinginezo katika kutoa  mchango wa nchi. 

Pia Mabeyo amemalizia kwa kusisitizia usalama na ulinzi kwa wazee, watoto pamoja na watu wenye ulemavu  katika kuleta mapinduzi ya uchumi wa Viwanda tukiamia kila mtu ana mchango katika kuleta maendeleo.
 Mwenyekiti wa bodi ya magavanazi wa taasisi ya ustawi wa Jamii Sophia Simba akizungumza wakati wa uzinduzi na wadau mbali mbali leo Jijini Dar es Salaam waliohudhuria Kongamano hilo linaloshughulika na maswala ya ustawi wa jamii ili kuleta chachu ya maendeleo  endelevu ya kukuza uchumi wa viwanda hapa nchini.
 Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya magavanazi wa taasisi ya ustawi wa Jamii Lucian Msambichaka akizungumza na wadau mbali mbali katika Kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Makamu mkuu wa Taasisi  ya mipango, fedha na utawala Zena Mabeyo akifafanua jinsi Taasisi ya Ustawi wa Jamii jinsi inavyoweza kufanya kazi zake kwa jamii leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kongamano hilo ambalo hufikia tamati Mei 10 mwaka huu.
 Wadau kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi waliohudhuria leo Jijini Dar es Salaam  Kongamano hilo linalolenga kuunga mkono juhudi za Rais wa amu ya tano  John Pombe Magufuli za kukuza Tanzania ya viwanda.
 
 picha ya Pamoja

WAZIRI MKUU KUONGOZA MAZISHI YA DK. MENGI KESHO

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi yatakayofanyika kesho Mei 9, 2019 kijijini kwake, Kisereni, Machame, wilayani Hai, Kilimanjaro.

Waziri Mkuu anatarajiwa kuongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali. Ibada ya mazishi itafanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Kisereni, Machame.

Mwili wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia alfajiri ya Mei 2, mwaka huu akiwa kwenye matibabu huko Dubai, Falme za Kiarabu, umewasili Moshi leo ukitokea Dar es Salaam na kupokekelewa na mamia ya wananchi waliojipanga barabarani.

Jana, (Jumanne, Mei 6, 2019) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa Serikali, waliongoza maelfu ya wananchi kutoa heshima za mwisho wakati wa shughuli za kuaga mwili huo katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hadi mauti yanamfika, Dkt. Mengi alikuwa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania (Chairman of the Media Owners Association of Tanzania - MOAT). Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF).

Baadhi ya nyandhifa ambazo Dkt. Mengi aliwahi kushika ni pamoja na Kamishna wa kamati inayoshughulikia mishahara (Salary Review Commission); Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA); Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mazingira Tanzania (NEMC); Mwenyekiti wa vyombo vya habari vya Jumuia ya Madola Tanzania (Chairman of the Tanzania Chapter-Commonwealth Press Union-CPU); Kamishna wa TACAIDS na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano TCRA amiminiwa pongezi

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jones Kilimbe (kushoto) akipongezwa na Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Derek Murusuri, baada ya kumalizika kwa hafla ya kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja (Client Service Charter) wa Mamlaka hiyo jijini Dodoma leo.

Akizindua Mkataba huo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Isack Kamwelwe (hayuko pichani), ameipongeza Bodi na Menejimenti ya TCRA kwa kuwa mfano bora kwa taasisi nyingine za umma kuandaa Mkataba wenye lengo last kuboresha huduma.

Waziri Kamwelwe amempongeza Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Eng. James Kilaba (katikati) kwa ubunifu na umakini mkubwa katika kufanikisha uandaaji wa mkataba huo utakaowafanya watanzania wajivunie huduma bora na kujaliwa katika taifa lao.

Waziri Kamwelwe amesema kuwa uboreshaji wa huduma za Mawasiliano nchini pia utasaidia kuondoa rushwa kabisa kwani katika e-government, mteja atahudumiwa pasipo kuonana na mtoa huduma uso kwa uso.

"Ni katika kuonana uso kwa uso vitendo vya rushwa vinafanyika, katika simu ukioomba rushwa utamulikwa tu," alisema.Tanzania chini ya Rais Magufuli, inapigiwa mfano katika bara la Afrika kwenye vita dhidi ya rushwa.

Akiongea katika hafla hiyo kubwa iliyofanyika katika ukumbi ya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe George Mkuchika, amezitaka taasisi nyingine zote za umma kuiga mfano wa TCRA na kuandaa mikataba ya wateja.

Ameitaka Mamlaka hiyo kuutekeleza Mkataba huo ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini, hasa ukizingatia unyeti wa sekta ya Mawasiliano.

Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, mbali na kuipongeza TCRA kwa kazi nzuri ya kuwahudumia watanzania, ameishukuru Mamlaka kwa mahusiano mazuri ya kikazi baina yao.

Hafla hiyo imehudhuriwa viongozi mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Atashasta Nditiye na Naibu mwingine katika Wizara hiyo, anayeshughulikia sekta ya Ujenzi, Eng. Elias Kuandikwa.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Mary Sassabo, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo, Dk Jim Yonazi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

WAZIRI PROFESA NDALICHAKO:UDSM IMEONA MBALI KATIKA KUWEKEZA KWENYE UTAFITI WA MATATIZO YA WANANCHI.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwa kutenga sh. bilioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wanataaluma kufanya tafiti zaidi hasa zinazogusa matatizo ya jamii moja kwa moja.

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya tano ya Wiki ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo amesema tafiti ni muhimu katika kuleta maendeleo kwa kujenga na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

Prof. Nalochako amesema serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda lengo likiwa kuhakikisha kunakuwa na viwanda ambavyo vinatumika kuzalisha bidhaa na kutoa huduma zitakazotosheleza jamii ya Kitanzania na kusaidia kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumzia Wiki ya Utafiti Waziri Ndalichako amesema inawapa wadau wa utafiti na ubunifu jukwaa la kufahamu shughuli za utafiti zinazofanyika; sehemu gani kuna mapengo na changamoto; na mikakati gani ya kimipango inahitajika ili kuziba mapengo pamoja na kutatua changamoto zilizobainika.

"kama taifa, tuna wajibu mkubwa na fursa nyingi za kuweza kutumia utafiti, ubunifu na ujasiriamali hususan kupitia sekta ya elimu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda nchini. Kufanya hivyo, kutawezesha kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Dira ya Taifa ya 2015, ya kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia viwanda." Amesisitiza Waziri Ndalichako.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye amesema kuwa tafiti zinazofanyika zinafanya Chuo kuweza kutambulika kimataifa.

Amesema wanataraji kutenga sh.bilioni moja kwa ajili ya kazi za utafiti ili kuweza matokeo katika maendeleo katika utengenezaji sera mbalimbali.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema kuwa tafiti ndizo kiungo na serikali katika kusaidia wananchi kutatua changamoto mbalimbali.

 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo katika maonesho ya Utafiti katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifunga wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) uliofanyika katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo hicho.
 Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam -Profesa William Anangisye akitoa maelezo kuhusiana na Wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
 

 Baadhi ya wadau katika wiki ya Tano ya Utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

NYUMBA 300 HATARINI KARAKATA RELINI, DIWANI ATOA OMBI MANISPAA YA ILALA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANANCHI wa Karakata Relini wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam wameiomba Serikali kuwasaidia ili kuepukana na maafa yanayoweza kutokea baada ya nyumba zao zaidi ya 300 kuzingirwa na maji.

Wananchi wa maeneo hayo wamesema kwa sasa hatma ya usalama wao umebaki mikononi mwa viongozi wa Wilaya ya Ilala hasa kwa kuzingatia maji hayo yamekosa pakupita kutokana na ujenzi wa reli unaondelea.

Wakizungumza na Michuzi Blog leo Mei 8, 2019 jijini Dar es Salaam wananchi hao wamesema maji yalianza kujaa katika nyumba zao kuanzia jana jioni na leo hii hali imekuwa mbaya zaidi kwani hakuna anayeweza kuingia ndani ya nyumba na baadhi ya watu wamekaa juu ya paa za nyumba kujinusuru.

Mmoja wa wananchi ambaye naye nyuma yake imejaa maji amesema baadhi ya wananchi wananchi wanachokifanya ni kujaribu kuyaondoa maji yaliyokuwa ndani ya nyumba lakini wameshindwa kuyaondoa kwani maji ni mengi.

"Jana wananchi tuliamua kuchukua majembe ili kwenda kuchimba mirefeji ya maji ambayo imezibwa kutokana na ujenzi wa reli. Hata hivyo Polisi walituzuia na kwa kuwa tunaheshimu mamlaka zilizopo, tunasubiri ingawa tuko kwenye wakati mgumu sana.Hatujui maisha yetu yatakuwa katika mazingira gani,"amesema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Karakata Kennedy Simioni amesema jana jioni walipata taarifa kuhusu nyumba hizo kujaa maji ambazo ni zaidi ya 300.Pia Kanisa la Anglikaa na Msikiti nayo imezingiwa maji.

"Baada ya taarifa hizo mimi na Mwenyekiti wangu wa Mtaa Olutu tulikwenda eneo hilo na kwa kweli hali ni mbaya sana.Hivyo kwa siku ya jana tulichukua hatua kwa kuwasiliana na mamlaka zote zinahusika ikiwemo Kamati ya maafa ya Wilaya.

"Pia tumewasiliana na wahandisi wa Manispaa ya Ilala pamoja na Kampuni inayojenga reli ya kisasa.Lengo letu ni kupata ufumbuzi kwani kabla ya ujenzi wa reli maji yalikuwa yanakwenda vizuri lakini baada ya ujenzi kuanza maji yamekosa njia ya kupita kama zamani,"amesema Simioni.

Diwani Simioni amesema wamekwenda Wakala wa Ujenzi wa Barabara TARURA kutoa taarifa na wakaambiwa waandike barua na wakafanya hivyo na walishaiwasilisha.

"Kitu ambacho tumekifanya kwanza ni kutoa taarifa kwa wanaohusika ili wao wachukue hatua ikiwemo ya kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi wetu .Hali ni mbaya sana kwani maji yamejaa katika nyumba na Mkuu wa Wilaya ya Ilala nimempa taarifa hizi,"amesema.




WAJASILIAMALI WADOGO WAIOMBA SERIKALI KUWATAFUTIA MUWEKEZAJI ATAKAYE FUNGUA KIWANDA CHA VIFUNGASHIO

$
0
0
Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Wajasiriamali wadogo wameiomba serikali kuwatafutia Muwekezaji atakaewaletea mashine za kutengeneza vifungashio pamoja na lebo ili kupunguza usumbufu na adha wanayoipata. 

Iwapo tutapata vifungashio bora na vizuri itasaidia kukuza biashara yetu na kufanya bidhaa zetu kuwa kuwa zenye ubora Kitaifa na Kimataifa zaidi. 

Hayo yamebainishwa  leo na Mjasiliamali Annet Kivuyo alipokuwa akizungumza katika semina ya wajasiliamali ilioandaliwa na shirika la Uthibiti wa Viwango (TBS) kwa kushirikiana na SIDO, ambapo alisema kuwa changamoto ya vifungashio inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza soko la bidhaa za hapa nchini kwa sababu vifungashio vyetu havipo kwenye ubora unao kubalika. 

"vifungashio bora vya kuvutia vitasaidia bidhaa zetu ziwe kwenye viwango vyenye ubora , serikali itusaidie tuwe na mtu atakae wekeza mashine za lebo na kutengeneza vifungashio kama wenzetu wa nchi jirani, kwani kwa sasa tunaagiza nchi za nje na vinavyokuja pia vinakuwa vichache havitoshelezi mahitaji  ni gharama kubwa inatumika"alisema Annet

Alisema Tanzania  inabidhaa nzuri na zenye ubora, ila changamoto kubwa inayotusumbua ni vifungashio, hivyo ameiomba Serikali ijitahidi kupata mwekezaji atakae saidia kuondoa tatizo hilo. 

Kwa upande wake Mmkurugenzi wa TBS Jabir Abdi alisema kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo kwa wafanyabiashara wachakataji wa bidhaa za ngozi,  lakini pia huo ni muendelezo wa kuhakikisha wanapata elimu sahihi itakayo wasaidia kufikia viwango vya Kitaifa ili waweze kuuza bidhaa zao, sio tu hapa nchini pia waweze kuuza nje ya nchi

Aidha alifafanua kuwa wanatoa elimu hiyo pia ili  kupata alama za ubora pamoja na kuwawezesha kufikia malengo yao, kitu pekee kitakachowawezesha wajasiliamali kufikia malengo ni kufuata sheria ya kufika viwango vya kitaifa.

Atakayekamatwa anakata mti hovyo Sukuma Ndani-RC Mwanri

$
0
0
Na Editha Edward-Michuzi TV Tabora 

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa onyo kwa mtu atakaye haribu mazingira kwa njia ya ukataji wa miti hovyo.

Kauli hiyo ameisema wakati akishiriki zoezi la upandaji wa miti na wanafunzi wa chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (D. I. T) katika kata ya kanyenye manispaa ya Tabora ikiwa ni juhudi za kuboresha Mazingira 

"Mtu atakayekamatwa anafanya Uharibifu wa Mazingira atasukumwa ndani, tunachofanya hapa ni kuotesha miti kila Halmashauri iwe na vitalu vyake kuanzia kwa mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya mtendaji wa kata, Mtendaji wa kijiji pamoja na Mtendaji wa mtaa, tunataka tuhakikishe miti hii inapandwa katika Taasisi zote"Amesema Mwanri

Aidha kiongozi wa Wanafunzi wa Chuo cha D. I. T Machage Emmanuel amesema Lengo la kushiriki zoezi hilo la upandaji wa miti ni kuimarisha Mazingira na kupata uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuifanya Tabora kuwa ya kijani.
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ambaye ameshiriki zoezi la upandaji wa miti pamoja na wanafunzi wa chuo cha D. I. T.

MACHIFU MBEYA WATOA ZAWADI KWA RAIS MAGUFULI, WAMPONGEZA KWA KUIFUNGUA TANZANIA


Miss Mbeya na Bodaboda yake azungumzia ishu nzima ya mchuano huo

BENKI ZILIZOTUMIKA KUWEKA BILIONI 14 ZA DECI ZAONYWA KUTOZIGUSA,ZIKIBAINIKA KUKIUKA HATUA KALI KUCHUKULIWA IKIWEMO KUPELEKWA MAHAKAMANI

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, (DPP) Biswalo Mganga ameziasa benki zote nchini, zilizotumika kuweka sh. Bilioni 14 za kampuni ya kusimamia shughuli za upatu (DECI), kwa mtindo wa kupanda mbegu na kuvuna fedha kutozigusa fedha zozote zilizoamriwa kutaifishwa na mahakama na wakibainika kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kupelekwa mahakamani

DPP amesema hayo leo Mei 8, 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake kufuatia amri ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam iliyotolewa jana na kuamuru mali zote za Deci zitaifishwe na kuwa mali ya serikali.

Amesema, mameneja wa benki hizo wanapaswa kuwa makini na kutambua kuwa mahakama tayari imeshatoa agizo na wasiruhusu kurubuniwa kuzihamisha kwenda kwenye akaunti nyingine.

Akieleza sababu za kutoa onyo hilo, Dpp amesema, Januari 10, mwaka huu kulikuwa na kesi inayowahusu wakurugenzi wa Kampuni ya Rifaro Afrika ambayo inajihusisha na kuchezesha upatu ambao walikiri makosa na mahakama iliwaamuru fedha zilizokuwa benki ya biashara ya Kenya (KCB) sh milioni 149 zitaifishwe na kuwa mali ya serikali.

Amesema, hatua hiyo ilikuja baada ya mahakama kuwaachiwa kwa kulipa faini ya zaidi ya Sh milioni 204, ambapo baada ya kulipa faini hiyo, fedha zilizokuwemo kwenye account KCB, benki walihamisha Sh milioni 109 na kuziweka kwenye akaunti maalum na kuacha Sh milioni 40 pekee.

Amesema kufuatia kitendo hicho, ameshatoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufanya uchunguzi kwa meneja wa benki hiyo ya KCB na wahakikishe kwamba fedha hizo zinarudi mapema iwezekanavyo na waende mahakamani akaeleze kwa nini fedha hizo walieza kuziamisha kutoka kwenye akaunti husika huku wakijua zilikuwa zimezuiwa kwa amri ya mahakama kwa kutaifishwa.

Aimezitaja mali zilizotokana na DECI ambazo ni nyumba nne, viwanja vitano na magari 11 na fedha hizo zilizoko kwenye akaunti za Benki ya NMB, DCB na KCB, ambazo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliamuru mali hizo zitaifishwe na kuwa za serikali.

Aidha DPP amewaasa wananchi wanaojishughulisha na upatu kuacha mara moja kwa sababu ni kosa la jinai na kwamba watakapokamatwa watashitakiwa na watapoteza mali na fedha zao kwa sababu zitataifishwa.

"Ninafahamu kuna watu ambao bado wanajishughulisha na upatu, niwaombe waache, tulianza na Deci 2009, ikaja Rifaro ambayo tayari fedha zao zimetaifishwa na zote huko wataendelea kupoteza fedha, ninafahamu kuna watu walijiingiza kwenye upatu katika kampuni nyingine tuko kwenye upelelezi muda ukifika tutasema, lakini yeyote anayejiingiza kwenye upatu kwa kutafuta fedha za haraka haraka atapoteza fedha sake"amesema Mganga.

Amesema watu watafute biashara halali ya kufanya uwekezaji kuliko kujiingiza kwenye upatu. Kwani sheria inasema yeyote anayejiingiza kwenye upatu anafanya kosa la jinai na akikamatwa atashtakiwa.

Mganga alizitaja mali ambazo zimetaifishwa kuwa ni nyumba namba UKMMD/1237 iliyoko Mwembe Madafu, Ukonga, Dar es Salaam, kiwanja namba 651, kitalu ‘M’ kilichopo Forest area, Mbeya, nyumba iliyoko kiwanja namba 7, kitalu ‘P’ ikiwa na hati namba 033004/23 kilichopo mtaa wa Rufiji, Manispaa ya Mwanza.

Pia mali nyingine ni kiwanja namba 2/283/2 kitalu “E” Mabibo, Kinondoni, Dar es Salaam, kipande cha ardhi ambacho hakijapimwa kilichopo kijiji cha Manyinga, Turiani, Mvomero, Morogoro, kiwanja namba 467 kilichopo kitalu “H” kikiwa na hati ya usajil;i namba 48170 kilichopo eneo la Tegeta, Dar es Salaam, nyumba iliyoko kiwanja namba MM/19/P kilichopo Manzese karibu na barabara ya Morogoro, Dar es Salaam na nyumba iliyoko katika kiwanja namba KND/MXS/MNM/Z ikiwa na leseni ya makazi namba KND 008337 Kinondoni, Dar es Salaam.

Magari yaliyotaifishwa ni Toyota Premio lenye namba T 132 AWJ, Toyota Land Cruiser namba T 480 AUP, Toyota Rav 4 namba T 274 ATQ, Toyota Mark II namba T 676 AYP, Subaru Legacy namba T 682 AUT, Toyota Ipsum namba T 850 AXY, Toyota Ipsum T455 ADM, Toyota Mark II T 186 AYX, Mitsubishi Pajero T 852 AAV, Toyota Land Cruiser T 789 AUX, Nissan Terrano namba T 899 AYU.

Aidha, Mganga alisema fedha zilizotaifishwa na kuwa mali za serikali ni Sh 12,503,068,647.89 zilizopo NMB, tawi la Msasani, Sh 1,457,700,462.49 zilizoko benki ya Dar es Salaam Community Bank (DCB), tawi la Uhuru na Sh 57,933,304.10 zilizoko KCB, tawi la Samora, Dar es Salaam.

Alisisitiza kuwa mahakama hiyo iliamuru magari hayo yabadilishwe umiliki na kubadilishwa matumizi kwa namna serikali itakavyopenda na kiwanja ambacho hakijapimwa kinatakiwa kusajiliwa kwa jina la Katibu Mkuu hazina.

Pia mahakama iliagiza DPP kupeleka maombi mahakamani hapo kuomba watu wanaoishi kwenye nyumba hizo watolewe kupitia kampuni ya udalali.

UBALOZI WA USWISI WATOA MILIONI 170 KWA VIKUNDI VYA SANAA KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UBALOZI wa Uswisi nchini Tanzania umetoa zaidi ya milioni 170 kwa ajili ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Uswisi nchini Florence Mattli amesema kuwa fedha hizo ni jitihada za kuchangia ukuaji wa sekta ya sanaa na utamaduni nchini Tanzania kwa mashirika na vikundi kupata fedha hizo na kuonesha vipaji vyao.

Amesema, Shirika la maendeleo na Ushirikiano la Uswisi kupitia programu yake ya utamaduni ilitoa wito wa mapendekezo ulioitwa Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

"Taka yangu, Hazina yangu inatoa wito kwa kila mtu kuangalia taka kwa mtazamo tofauti, kwani taka zingine zinaweza kuwa na thamani iwapo zikitumika tena kwa njia nyingine," amesema Florence.

"Lengo la mradi huu ni kutafakari kwa kutumia sanaa juu ya tabia zetu na wajibu wetu kama raia, namna tunavyotumia na kutupa taka inaweza kuwa na athari za mazingira yetu,"

Mkurugenzi wa Makumbusho Achiles Bufure amesema kuwa mradi huu utasaidia katika kutunza na kuboresha mazingira na takataka na kuwa fursa.Bufure amesema, kwa kipindi cha miaka mitatu Ubalozi wa Uswisi wamekuwa wanashiriki kwenye masuala ya Kijamii ambapo walianza na Masuala ya rushwa, mimba za utotoni na sasa hivi mazingira.

Mbali na hilo, amesema watashirikiana na wasanii kutumia sanaa kuleta maendeleo na mradi wao unaangalia zaidi kuwa takataka ni dili na fursa kwa maendeleo ya nchini.Kwa upande wa Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamale amesema wasanii wanapopewa fedha hizo wanatakiwa wakafanyie kazi kwa ajili ya maendeleo na kutumia sanaa walizonazo kama fursa ya ajira.

" mradi huu unalenga kuboresha taka kuwa fursa kupitia sanaa kwani takataka zimekuwa kikwazo kikubwa tofauti na nchi zingine," amesema Nyangamale.Aidha, ametoa pongezi kwa Ubalozi wa Uswisi katika ushiriki wao wa masuala ya kimaendeleo na kuonesha ni namna gani wanapambana kuhakikisha tunatoka hapa tulipo na kwenda mbele zaidi kiuchumi na kimaendeleo.

Naye Kiongozi wa Kikundi cha Wasanii 14+, Twahiri Sabuni amewashukuru ubalozi wa Uswisi kwa kupata nafasi hiyo na kuwa moja ya vikundi vitano vilivyopata nafasi ya kuonesha ubunifu wao kupitia takataka na kutengeneza kazi za sanaa kubwa matumizi mbadala.

Amesema, watashirikiana na wanamchi, watoto, vijana na watu wenys uhitaji maalumu katika kutimiza azma ya kulinda mazingira na kutumia taka kama fursa ga kiuchumi.Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania umekuwa ukichangia katika kuendeleza masuala mbalimbali ya utamaduni wa Tanzania tangu mwaka 2005 na kutoa asilimia 1 ya bajeti yake kuunga mkono sekta ya sanaa na utamaduni.

Mashirika na vikundi vilivyofanikiwa kupata fedha hizo baada ya kupelekea maombi ni pamoja na Makumbusho ga Taifa la Tanzania, CDEA, Chuma Art Worksho, Alama Art and Media Production na Wasanii 14+ na aina mbalimbali za sanaa zitatumika katika uhamasishaji na kufikia kwenye mikoa mballimbali nchini.
 Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Florence Mattli akikabidhiana mkataba na  Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Achiles Bufure  kwa ajili ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa. Ubalozi huo umetoa kiasi cha Shillingi Milioni 170 kwa mashirika na vikundi vitano nchini vitakavyotumia takataka na kuzigeuza fursa wakitumia kauli ya  Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

 Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Florence Mattli akipeana mkono na  Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Achiles Bufure, Kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamale baada ya makabidhiano ya mkataba   kwa ajili ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa. Ubalozi huo umetoa kiasi cha Shillingi Milioni 170 kwa mashirika na vikundi vitano nchini vitakavyotumia takataka na kuzigeuza fursa wakitumia kauli ya  Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania Florence Mattli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mashirika na vikundi vilivyofanikiwa kuingia kwenye mradi wa  umuhimu wa kuhifadhi mazingira kupitia sanaa. Ubalozi huo umetoa kiasi cha Shillingi Milioni 170 kwa mashirika na vikundi vitano nchini vitakavyotumia takataka na kuzigeuza fursa wakitumia kauli ya  Taka Yangu hazina yangu unaolenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Shirika la AGPAHI lasaidia wananchi mkoani Simiyu kupima afya bure

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi nchini Tanzania, limetoa huduma ya upimaji afya bure kwa wananchi mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 ambayo kilele chake ni Mei 05 kila mwaka.

Huduma hiyo imetolewa katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi yalikofanyika maadhimisho hayo ambapo wananchi hususani akina mama walipata fursa ya kufanya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi pamoja na VVU kuanzia Mei 02, 2019.

Akitoa takwimu za awali jana kabla hatujaenda mitamboni, Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka alisema zaidi ya akina mama 200 walifanyiwa uchunguzi na kati hao, mmoja aligundulika kuwa na dalili za awali za Saratani ya Mlango wa Kizazi na kuanzishiwa huduma ya mgandisho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Simiyu, Somanda huku wengine wawili wakipewa rufaa.

“Lakini pia akina mama wawili walikutwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo tuliwapa rufaa ya kwenda Bugando (Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa) kwa ajili ya matibabu zaidi” alieleza Shiluka.

Shiluka pia aliongeza kwamba akina mama 166 walikubali kupima maambukizi ya VVU ambapo kati yao, mmoja alikundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuanzishiwa dawa kupitia Kituo cha Afya Muungano.

“AGPAHI tunatoa huduma za tiba na matunzo kwa wanaoishi na maambukizi ya VVU katika Wilaya zote za Mkoa Simiyu ambapo tuna jumla ya Vituo 73 ambavyo tunavihudumia kwa ajili ya huduma hiyo na Vituo vinane kati ya 73 vinatoa huduma ya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi” alisema Shiluka.

Shiluka alitoa rai kwa wananchi hususani akina mama kuwa na desturi ya kujitokeza kupima saratani ya mlango wa kizazi kwenye Vituo vya Afya na Hospitali zinazotoa huduma hiyo tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi hujitokeza tu kwenye makongamano mbalimbali mkoani Simiyu.

Baadhi ya akina mama waliojitokeza kufanya uchunguzi kwenye maadhimisho hayo walitoa shukrani kwa Shirika la AGPAHI kwa kutoa huduma hiyo na kuahidi kuitumia vyema elimu waliyoipata ikiwemo kuhamasisha wenzao kwenda katika Vituo vya Afya na Hospitali kufanya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na Matiti.

“Tumefundishwa jinsi ya kuambukizwa na jinsi ya kujikinga, ukikutwa hauna Saratani ya Mlango wa Kizazi hautakiwi uwe na wanaume wengi, tujikinge, tuwe watulivu na tupime mara kwa mara” alisema Pendo Mboje.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, Dkt. Faustine Ndungulile ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto aliwahamasisha wananchi kupima afya zao ikiwemo VVU na Saratani ya Mlango wa Kizazi huku akiongeza kwamba Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya nchini ili kuwaondolea wananchi adha ya kupata matibabu.
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka akizungumza na BMG kwenye maadhimisho hayo.
Pendo Mboje ambaye ni Mkazi wa Bariadi akizungumza na BMG kuhusu huduma ya upimaji iliyotolewa na Shirika la AGPAHI.
Mkuu wa Wilaya Busega, Festo Kiswaga akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Washiriki wa Siku ya Wakunga Duniani 2019 yaliyofanyika kitaifa Bariaadi mkoani Simiyu wakiwasili uwanjani.
Viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya Busega Festo Kiswaga (wa pili kulia),  Rais wa TAMA Feddy Mwanza (wa tatu kulia), Makamu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Hashina Begum (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Simiyu (wa kwanza kushoto).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisikiliza ufafanuzi alipotembelea banda la Shirika la AGPAHI.
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka (kushoto) akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na Shirika hilo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile  (kulia).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akipokea kipeperusha chenye elimu kuhusu Saratani ya Mlango wa Kizazi alipotembelea banda la Shirika la AGPAHI.
Sehemu ya akina mama waliojitokeza kupata huduma ya uchunguzi kwenye banda la Shirika la AGPAHI.
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu, Dafrosa Shiluka akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda la Shirika hilo.
Sehemu ya akina mama waliojitokeza kupata huduma ya uchunguzi kwenye banda la Shirika la AGPAHI.
Baadhi ya Wakunga waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2019 kitaifa mjini Bariadi.
Tazama BMG Online TV hapa chini
Attachments area

KWA MOYO NA UPENDO HUU WA TFS, WASANII MKISHINDWA KUITUMIA MUNGU 'ATAWALAANI'

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KWANZA kabisa naomba nitumie fursa hii kukusabahi na natumai uko poa na mambo yanasonga.

Pia sote tunafahamu Taifa letu lipo katika majonzi kutokana na kifo cha mpendwa wetu Dk.Reginald Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 12019 akiwa Dubai. Mungu ilaze roho yake mahala pema peponi.Amina.

Baada ya hapo sasa tuendelee iko hivi ukweli uliopo wasanii nchini Tanzania na hasa wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva wamekuwa wakitumia fedha nyingi sana pindi wanapohitaji kurekodi video za nyimbo zao.

Ni mara kadhaa tumeshuhudia wakifunga safari kwenda nje ya Tanzania ili kupata maeneo ya kurekodi nyimbo zao. Wanamini nje ndiko kuzuri kwa kurekodi video zao kuliko nyumbani.Jamani sio kweli, ninao ushahidi.

Nikiri Watanzania walio wengi tunayo kasumba nikiwemo mimi kasoro wewe tu unayesoma hapa ya kuamini vya nje ni bora zaidi kuliko vya kwetu.Na ndicho kinachowasumbua wasanii wetu.Si wote ila wengi wao wako hivyo.Usikatae ndio ukweli.

Sasa umefika wakati kwa wasanii kubadili matazamo na fikra kwasababu katika ardhi ya Tanzania ambayo Mungu ameipagilia na ikapangika kuliko mahali popote tuna kila kitu.

Ndio maana Wazungu wanafunga safari kuja nchini kwetu kutalii.Tunavyo ambavyo wao hawana.Mungu ametupendelea Watanzania.Tunayo sababu ya kumshukuru kwa kusema Ahsante Mungu.

Chonde chonde wasanii wa Tanzania.Narudia tena chonde chonde, nyumbani kuna maeneo mazuri ya kurekodi video zenu.Niwahakikishie hamtajuta kutumia mazingira ya nyumbani kwa ajili ya video zenu.

Nashukuru Mungu baadhi ya wasanii wameona haja ya kubadili mtazamo wao na sasa wameamua kubaki na Tanzania yao katika kufanya kazi zao za muziki.

Wasanii Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga wameonesha njia kwa wasanii wenzao.Unajua ambacho wamekifanya? Nikukumbushe wasanii hao wametoa nyimbo yao mpya inayofahamika kwa jina la Nimenasa.Nyimbo tamu balaa.

Katika kuhakikisha video ya wimbo huo inakuwa bora na ya kuvuta wakaona isiwe taabu, wakafunga safari hadi kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kwa ajili ya kuomba eneo la kurekodi video yao.

Kwa moyo wa upendo walionao TFS kwa wasanii wa nchi yetu, wala wahakujiuliza mara mbili, walikubali ombi la wasanii hao. Na sio kukubali tu bali waliamua kufadhili na gharama ya video yenyewe kwa asilimia 80.Hongereni TFS.

Kwa dhamira njema ya TFS kwa wasanii, ni wajibu wa kila msanii iwe wa Bongo Fleva,Bongo Movie na hata wale wa filamu za 'Action' kuhakikisha mnakuwa karibu nao.Wameamua kutoa maeneo yao kwa ajili yenu pale mnapotaka kufanya kazi zenu.

Wapo tayari kusaidia hata kama isiwe fedha basi hata kutoa watalaam wao ili kushauri sehemu nzuri itakayofaa kwa msanii kurekodi kazi yake kulingana na mahitaji yake. Mnataka nini tena?

Kaimu Meneja Mawasiliano wa TFS Tulizo Kilaga amefafanua kwa kina sababu za kuamua kuwawezesha wasanii Amini na Linna kurekodi video yao ambapo amesema msingi mkubwa ulitokana na ombi la wasanii hao la kuomba eneo lenye mazingira asili zaidi ili kupata muonekana wanaouhitaji.

"Walikuja kwetu kuomba maeneo ya kwenda kurekodi video ya Nimenasa.Kwetu TFS tukaona hii ni fursa kwa umaarufu wa wasanii haoa na kampeni yetu ya kuhamasisha utalii wa ndani basi tunaamini ujio wao utatusaidia kuongeza idadi ya watalii wa ndani.

"Hivyo tuliwaelekeza video yao wakaifanyie Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Magamba ulikopo wilayani Lushoto mkoani Tanga. Kuna maeneo mengi mazuri yakiwemo maporomoko ya maji , wanyama , mimea , ndege, pango la Mjerumani na kila aina ya kivutio kilingana na mashairi ya wimbo wao,"amesema Kilaga.

Amefafanua kwa kuwa wasanii hao walionesha nia TFS imeona ni jukumu lake kuhakikisha kila ambacho wanakihitaji kinapatikana na uzuri wao wanasimamia hifadhi za misitu 17 nchini kote.

"Sababu za kufanya hivyo tunataka wasanii hawa baada ya kwenda Magamba wawe mabalozi kwa wasanii wengine kwa kuwaambia hakuna sababu ya kuumiza kichwa kwa ajili ya maeneo ya kufanya video zao kwani hapa nyumbani yapo.TFS tunasimamia hifadhi ya misitu 17 na kote huko kuna kila kitu ambacho msanii anahitaji.

"Kikubwa wasanii wanatakiwa kufika katika ofisi za TFS na kisha kueleza tu wanataka maeneo ya aina gani na sisi tutawapa maelekezo ya mahali pa kwenda na si kwa wanamuziki wa kizazi kipya hata wale ambao wanarekodi video za ngumi,"anasema.

Ameongeza kuna maeneo mengi ambayo wasanii wanaweza kutayatumia kurekodi na kazi zao zikapendwa na msanii haitaji kutumia nguvu kutafuta maeneo, bali wao wafike tu TFS.

Ameongeza wasanii wanapaswa kujivunia uwepo wa misitu iliyopo nchini Tanzania, kwani ina kila kitu ambacho kinaweza kuwepo kwenye kazi zao na kwamba TFS ipo tayari kutoa ushauri kwa wasanii.

Amesisitiza " Tupo katika kipindi cha kufanya promosheni hasa kwa kuzingatia tunaelekea kwenye msimu wa utalii.Hivyo ujio wa Linna na Amini ni sehemu ya kufanya hamasa ya kuvuta Watanzania wengine kwenda maeneo ya utalii".

Pamoja na mambo mengine, Tulizo anasema msanii anaweza kwenda katika Istagram ya TFS na kisha akatoa mawazo na ushauri wake na baada ya hapo wao wataufanyia kazi.

Kwa upande wake Amini anasema anatoa rai kwa wasanii nchini kuhakikisha wanaitumia hifadhi za misitu ya asili kwa ajili ya kufanya kazi zao za sanii kwani hakuna ambacho kinakosekana huku akieleza kuwa anao ushahidi kwani yeye amepata nafasi ya kurekodi video ya Nimenasa katika msitu wa Magamba.

Wakati Linna anasema hakuwahi kufikiria kama nchini kwetu kuna maeneo mazuri ya asili ambayo yaaweza kutumiwa na wasanii kurekodi kazi zao, hivyo naye amesema ni wakati muafaka kwa wasanii kutumia mazingira ya nyumbani kufanya kazi zao za muziki.

 Msanii Linna Sanga akiwa amekanyaga mgongo wa Kaimu Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Tulizo Kilaga ili kumsaidia kupita aende kurekodi kipande cha video kitakachokuwemo kwenye wimbo wa Nimenasa.Aliyeshika mkono ni msanii Amini Mwinyimkuuu.
 Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga wakiwa katika Msitu wa Magamba baada ya kupewa kibali na TFS warekodi video yao ya wimbo unaofahamika kwa jina la Nimenasa.



SERIKALI YA DENMARK WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO KATIKA KUBORESHA SEKTA ZA HAKI ZA BINADAMU NCHINI

$
0
0

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Serikali ya Denmark kupitia ubalozi wake nchini wamesaini mkataba wa makubaliano wa kifedha katika mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubaliano hayo balozi wa Denmark nchini Mheshimiwa Einar Hebogard Jensen amesema kuwa mkataba huo umeelekezwa katika sekta tatu ambazo ni programu za utawala bora, upatikanaji wa haki na haki za binadamu.

Katika makubaliano hayo Serikali ya Denmark imetoa msaada wa Krona milioni 7 sawa na takribani dola za kimarekani milioni 1, 049, 776 huku tafiti zikionesha kuwa kwa mwaka 2018 walitoa jumla ya dola za kimarekani milioni 63.

Balozi Jensen amesema kuwa Denmark inaamini kuwa ili kufikia maendeleo lazima misingi ya uwazi, uwajibikaji na usawa wa kijinsia iwepo na wamekuwa na ushirikiano duniani kote na kupitia UNDP nchini Tanzania wamekuwa wakishiriki na kufanya kazi kwa pamoja katika  kuboresha shughuli za bunge, utawala bora pamoja na taasisi na vituo mbalimbali za haki za binadamu.

Aidha amesema kuwa watanzania wanazijua haki zao kwa kufuata sheria na hiyo ni kutokana na ukomavu wa demokrasia nchini.

Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Natalie Boulcy amesema kuwa Denmark ni moja kati ya nchi 10 zinazoshirikiana na kutoa msaada mkubwa kwaUNDP hasa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora na ulinzi.

Natalie amesema kuwa msaada utawafikia watu wengi zaidi hasa vijijini pamoja na  kusaidia sekta mbalimbali zikiwemo tume ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG) hasa katika kuwajengea uwezo, ikiwa ni pamoja na kuwezesha uchapishaji wa ripoti za haki za binadamu kwa kila mwaka na kuzimbaza kote nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na katiba na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali .

Pia msaada huo utaelekezwa katika makundi mbalimbali wakiwemo wanawake na watoto, ofisi ya Mwendesha Mashtaka mkuu wa serikali (DPP) kupitia Wizara ya sheria pamoja na vituo vya haki za binadamu na utawala bora.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely  wakikabidhiana mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely  wakisaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidmkatabaresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam. Kulia ni mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovely .
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Natalie Bovel(kulia) akimpa zawadi Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen  mara baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano wa kifedha kwa ajili ya mwendelezo wa kusaidia maboresho ya sekta za haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na utawala bora na ulinzi kupitia programu ya msaada wa sheria na upatikanaji wa haki. Mpango huo ni wa miaka mitatu yaliyofanyika katika Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam.

KWA HERI DKT. REGINALD MENGI......

$
0
0
 Sehemu ya waombolezaji wakiwa ndani ya kanisa la kiinjili la Kilutheli (KKKT) usharika wa Moshi, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa Dkt Reginald Mengi zinazoendelea hivi sasa.
 Familia ya Marehemu Dkt Reginald Mengi ikiwa ni yenye huzuni kubwa kwa kuondokewa na mpendwa wako, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake inayoendelea hivi sasa katika katika la kiinjili la Kilutheli (KKKT) usharika wa Moshi.
Nje ya kanisa hivi ndivyo hali ilivyo wakati watu mbalimbali wakiendelea na zoezi la kuaga mwili wa Dkt Reginald Mengi katika kanisa la kiinjili la kilutheli usharika was Moshi mjini.

Dkt. Kalemani aitaka TANESCO kuendeleza miradi ya umeme vijijini

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendelea kusambaza umeme vijijini mara wakandarasi wa umeme vijijini wanapomaliza kazi kwa mujibu wa mkataba.

Dkt. Kalemani aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini katika Wilaya za Mpwapwa na Bahi mkoani Dodoma ambapo aliambatana na Wawakilishi wa wananchi katika maeneo hayo, Watendaji wa Wizara ya Nishati, TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Yapo maeneo ambayo yalishasambaziwa umeme kutoka zamani kupitia miradi ya usambazaji umeme vijijini hivyo kazi ya TANESCO ni kuendelea kusambaza umeme kwenye maeneo hayo kwa muda wote badaala ya kuyaacha tu yakikosa umeme.” alisema Dkt Kalemani.

Akiwa kwenye Wilaya hizo, Dkt Kalemani aliwasha umeme katika Kijiji cha Igoji na Chinoje vya wilayani Mpwapwa, pia aliwasha umeme katika Kijiji cha Chikola kilichoko wilayani Bahi na kuahidi umeme utawaka tarehe 12 Mei, 2019 katika Kijiji cha Chipanga wilayani Bahi.

Akizungumzia kazi za usambazaji umeme katika Wilaya hizo mbili alisema kuwa, Wilaya ya Bahi ina vijiji 59 ambapo vijiji 19 tayari vimeshambaziwa umeme na vijiji 40 vilivyosalia vinasambaziwa umeme kupitia mradi wa REA wa Awamu ya Tatu.

Aidha kwa Wilaya ya Mpwapwa alisema kuwa, Wilaya hiyo ina Vijiji 113 ambapo Vijiji 78 tayari vimesambaziwa umeme huku kazi ya usambazaji umeme ikiendelea kwenye Vijiji vilivyosalia.

Akizungumza na wananchi katika Vijiji hivyo, Dkt Kalemani aliwaagiza Mameneja wa TANESCO kwenye Wilaya hizo kuhakikisha kuwa wanafungua vituo kwa ajili ya kuhudumia wananchi badala ya wananchi kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma TANESCO.

Kuhusu wakandarasi wa umeme vijijini wanaosuasua katika kazi zao, Dkt Kalemani alisema kuwa Serikali itachukua hatua kali dhidi yao hivyo ni vyema wakaongeza kasi katika utekelezaji wa kazi walizopewa na Serikali.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachwene pamoja na kupongeza Wizara ya Nishati kwa ufuatiliaji wa karibu wa miradi ya umeme vijijini alitoa ombi kwa Serikali kuhakikisha wakandarasi wa umeme vijijini wanasambaza umeme kwa wigo mkubwa na pale mkandarasi anapomaliza muda wake TANESCO waendelee na kazi ya kusambaza umeme kwa wananchi.

Vilevile alisema kuwa, kazi ya upangaji wa vijiji au vitongoji vinavyopaswa kupelekewa umeme ushirikishe wawakilishi wa wananchi ili kuboresha utaratibu wa usambazaji umeme na hivyo kuepusha malalamiko yanayoweza kutokea kwa baadhi ya vijiji au vitongoji kuona kuwa vimerukwa bila sababu za msingi.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika Kijiji cha Chinoje wilayani Mpwapwa. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene. Kulia kwa Waziri ni Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika Kijiji cha Chikola wilayani Bahi. Kulia kwa Waziri ni MKuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda na kushoto kwa Waziri ni Mbunge wa Bahi, Omary Badwel.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza katika Kijiji cha Chinoje wilayani Mpwapwa kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho. Wa kwanza kulia ni Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (mwenye shati ya bluu) akizungumza na baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Chikola wilayani Bahi mara baada ya kuzindua huduma ya umeme kijijini hapo. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda.

MAELFU WAJITOKEZA KUMUAGA DKT.MENGI

$
0
0

 Mke wa Marehemu Jacline akiwa pamoja na watoto katika katisa la KKKT usharika wa moshi mjini
 Mtoto wa Marehemu Regina Mengi akiwa kanisani tayari kwa ibada katika Kanisa la KKKT usharika wa Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro
 Waombolezaji wakiwa kanisani tayari kwa ibada
Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi mjini mahali ambapo wenyeji wa Mkoa wa kilimanjaro,wageni mbalimbali wanapouaga Mwili wa Dkt.Regnald Mengi 
Watu mbalimbali wakiendelea kuuaga Mwili wa Dkt.Regnald Mengi KKKT Usharika wa Moshi Mjij
 Waombolezaji wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuagana na mpendwa wao Regnald Mengi
 Waombolezaji wakiwa kwenye foleni
 Waombolezaji wakiingia kanisani
 Lango kuu la Kanisa kama linavyoonekana
 Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika foleni kwaajili ya kuingia kanisani kuuagana na mpendwa wao Regnald Mengi leo.
Na Vero Ignatus,Moshi

MAELFU ya wakazi wa  mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Manyara na maeneo jirani wamejitokeza kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni tanzu za IPP Regnald Mengi,kwenye ibada ya mazishi katika kanisa la kiinjili la Kilutheri usharika wa Moshi Mjini.

Mwili wa marehemu Dkt Regnald Mengi,umewasili katika kanisa Hilo majira ya saa 2:00 asubuhi,ambapo ulipokelewa na na baadhi ya viongozi mbalimbali ambao ni wabunge Nape Mnauye,Godbles Lema,Freeman Mbowe,Luhaga Mpina,Anna Kilango na James Mbatia.

Hata hivyo Mara baada ya mwili huo kuwasili pia ulipokewa na vilio,simanzi na majonzi kwa wanachi ambao walionekana wamefurika katika maeno yote ya viunga vya kanisa hilo.

Kutokana na umati wa watu kuzidi skauti ambao walikuwa katika lango kuu la kuingilia watu  polisi walilazimika kuingilia katika ili kunisuru Hali iliyokuwepo ambayo ilihatarisha usalama.

Hata hivyo baada ya zoezi la kutoa heshima za mwisho,Mwili wa Mengi,safari ya kuelekea machame Kijiji Nkuu Sinde kuulaza mwili huo utaanza,ambapo Waziri Mkuu anatarajiwa kuongoza maelfu ya wanachi katika mazishi hayo.

MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA DKT. MABODI SONGEA MJINI

$
0
0
 MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akiwasili katika Wilaya ya CCM Songea Mjini kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya kuimarisha Chama na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Wilaya hiyo.
 WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi Songea Mjini wakimvisha Vazi la Heshima la Kimila la kumtambua Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa kuwa ni Kiongozi Muadilifu aliyetambuliwa rasmi na Wazee wa Wilaya hiyo ambao ni Utaratibu wa Kimila uliasisiwa na Kiongozi Mkuu wa Kijadi ambaye ni Mzee Songea Mbano.
 MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akiwa katika Kikao cha ndani na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Songea  Mjini.
 WANACHAMA wapya waliojiunga na CCM wakila kiapo cha Uanachama mara baada ya kukabidhiwa Kadi za CCM na kupokelewa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Taifa huko katika Shina namba 4 Tawi la CCM Mtakuja na Kata ya Majengo Wilaya ya CCM Songea Mjini.
 WALIOKUWA Viongozi wandamizi wa CHADEMA waliojiunga na CCM na kupokelewa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Mabodi ambao ni Thimoth Tililo (kulia) aliyekuwa Mjumbe wa Mtaa wa Unangwa kupitia CHADEMA Wilaya ya Songea Mjini na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Kata ya Misufini ndugu Juma Marwa Kionyori (kushoto) wakizzumgumza mara baada ya kujiunga na CCM na kupokelewa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi.
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Killian Mwisho akizungumza katika Kikao cha ndani cha Viongozi na Watendaji wa Serikali kilichohitishwa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi'.

9TH EAST AFRICAN PETROLEUM CONFERENCE AND EXHIBITION 2019 OPENS IN MOMBASA

$
0
0
Kenya’s Cabinet Secretary for Petroleum and Mining, Hon. John Munyes on Wednesday 8th May, 2019 graced the official opening of the 9th East African Petroleum Conference and Exhibition 2019, themed East African Region - the destination of choice for Oil and Gas Investment Opportunities to enhance Socioeconomic Transformation.
Kenya’s Cabinet Secretary for Petroleum and Mining, Hon. John Munyes, delivering his speech at the EAPCE’19. 
The Cabinet Secretary disclosed that Kenya was on course with the exploitation of its oil fields with the country expected to ship its first 200,000 barrels of crude oil in June 2019 after hitting the 200,000-barrel mark set by the government for it to be able to ship out the product. 

The Cabinet Secretary also disclosed that Tullow Oil had so far transported 87,000 barrels of crude oil to the Kenya Petroleum Refineries storage tanks in Mombasa. 

According to Hon. Munyes, Kenya has a total of 94 wells of oil that have been drilled, 63 exploration blocks that have been gazetted, 276 blocks licensed and 36 blocks open to investors, adding that “the government was constructing a 820km 20-inch diameter, South Lokichar – Lamu Crude Oil pipeline that will connect Turkana to Lamu Port, which will be operational by 2022.”
Kenya's Petroleum and Mining Minister, Hon. John Munyes, accompanied by his Ugandan counterpart, Hon. Eng. Irene Muloni, and other Ministers tour the Uganda Exhibition stand.
The Cabinet Secretary revealed other major petroleum infrastructure that have been put in place/or whose construction is ongoing including the 450km, 20-inch diameter multi-product Line 5 from Mombasa to Nairobi, which has been completed; construction of four tanks of 133,000 cubic metres in Nairobi to ensure adequate storage of products coming through Line 5; the 122 km, 10-inch diameter multi-product line from Sinendet to Kisumu, and; completion of the Kisumu Oil Jetty.

Hon. Munyes called upon investors to come to the EAC not only to invest in the Oil and Gas sectors but also to support the Partner States develop their fledgling petroleum industries.

“There are challenges in this area and we really need your support,” said the Cabinet Secretary.

On his part, the Tullow Oil Executive Vice President for East Africa, Mr. Mark MacFarlane, disclosed that Tullow Oil had invested $2 billion in Kenya, and it was upbeat that they will hit the 200,000 barrels required for shipment. Tullow discovered crude oil in Uganda in 2006 and later in Kenya in 2012 but no exports have been made as yet.

Addressing delegates on behalf of the Secretary General of the EAC, Amb. Liberat mfumukeko, the Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo, said that a few years ago, the East African region did not attract significant investments in the oil and gas sector but that today, the region had benefited from advances in technology and management of exploration and production, which has led to the discovery of commercially viable oil and gas deposits.

“Recent discoveries were very impressive; Uganda has 6.5 billion barrels of oil and 500 Billion cubic feet (Bcf) of gas; Kenya 754 million barrels of oil, Tanzania 57.25 Trillion cubic feet (Tcf) of gas, Rwanda 63 billion cubic metres of methane gas and huge commercial reserves in South Sudan, and reports at hand indicate that exploration process in Burundi is also on going and that it has reached an advanced stage,” said Hon. Bazivamo.

The Deputy Secretary General informed the delegates that the ongoing event aims at fulfilling one of the objectives of the Community enshrined in Chapter 19, Article 114 of the EAC Treaty and Article 40 of the EAC Common Market Protocol of promoting sustainable utilization of the natural resources of the Partner States and putting in place measures that would effectively protect the natural environment of the Partner States.

Hon. Bazivamo said that exploitation of petroleum resources on the Continent, had certainly not achieved the intended socio-economic transformation, hence, “we have the obligation to draw lessons and ensure we are better off in the EAC region.”

"Since the inception of the EAPCE in, impressive achievements have been reported in every subsequent conference and I am happy to report that the EAC Partner States have established clear, harmonized, stable, regulatory, legal and fiscal frameworks that are supporting the achievements and developments in the sector," he said.

At the Conference, Uganda’s Minister of Energy and Mineral Development, Hon. Eng. Irene Muloni launched Uganda’s second open competitive licensing round in petroleum exploration, development and production in Uganda.

At the launch, Hon. Eng. Muloni disclosed that the licensing round covers five (5) Exploration Blocks in the Albertine Graben, which is the most prospective area of exploration, development, and production in Uganda. The Blocks are:-LR2_2019_Block01 (Avivi), area coverage of 1026km2; LR2_2019_Block02 (Omuka), area coverage of 750km2; LR2_2019_Block03 (Kasuruban), area coverage of 1285km2; LR2_2019_Block04 (Turaco), area coverage of 637km2; and LR2_2019_Block05 (Ngaji), area coverage of 1230km2.

The Minister hailed President Yoweri Kaguta Museveni for his visionary leadership and strong guidance he has given to the sector since 10th February, 1986. She also commended the EAC Partner States for the support they have provided in facilitating the development of the oil and gas sector in Uganda and the region at large.

The licensing round was driven by a number of factors including, among others, the establishment of additional resources and reserves to the current confirmed 6 billion barrels of oil, out of which about 1.4 billion barrels are recoverable, and 500 billion cubic feet of non-associated gas; and existence of comprehensive and robust legal, regulatory and institutional frameworks which guarantee certainty to investors. The second launch follows the first licensing round through competitive bidding undertaken in 2017.

Uganda made its first commercial oil discovery in 2006. To date, over 121 wells have been drilled with a success rate of over 88%. Preparations are under way to commence production following the issuance of production licenses to Total E&P Uganda B.V, Tullow Uganda Operations Pty Ltd, and CNOOC Uganda Ltd. The commercialization of the oil in Uganda will involve export of part of crude oil by the East Africa Crude Oil Pipeline through Tanga Port in Tanzania.

The 9th East African Petroleum Conference and Exhibition 2019 is being attended by Ministers in charge of the sectors in the Partner States; Members of the East African Legislative Assembly; Members of National Parliaments; Members of the Diplomatic Corps, Development Partners and investors; Petroleum Sector Business Community; and Members of the EAC Regional Petroleum Conference and Exhibition Steering Committee.

ASKARI JESHI AJINYAKULIA BODA BODA NA MILIONI MOJA BAHATI NASIBU YA BIKO

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images