Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live

DC KASESELA: MARUFUKU KUFANYA BIASHARA IRINGA KAMA HULIPI KODI AU HUNA KITAMBULISHO CHA MACHINGA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizunguza na wafanyabiashara wa bidha za kusindika walikuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali 
Wafanyabiashara wa bidha za kusindika wakiwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali na wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa bidhaa za kusindika



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wafanyabiashara wa wilaya ya Iringa wametakiwa kufanya biashara wakiwa wamelipa kodi au wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama kitambulisho cha machinga.

Akizungumza na wajasiliamali waliokuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema ni marufuku kwa sasa kufanya biashara yoyote wilaya ya Iringa bila kulipa kodi na zile ambazo hazijafikia hatua kodi zitalipa tozo

“Sasa tunaanza kufanya mchakato wa kuchunguza kujua wafanyabiashara wangapi wanafanya kazi hizo bila kulipa kodi na tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyosema” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wafanyabiashara wadogowadogo wote wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanapata kitambulisho cha kwa shilling elfu ishirini ambacho kinatamruhusu kufanya biashara sehemu yoyote hapa nchini kwa mujibu wa Rais.“Jamani ili ufanye biashara kwa uhuru katika wilaya ya Iringa ni lazima uwe na kitambusho cha wafanyabisahara wadogo au uwe umelipia leseni kutoka katika mamlaka husika la sivyo huwezi kufanya biashara hiyo wilaya ya Iringa” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wananchi wote wanaopenda kufanya biashara kuhakikisha wanafanyabiashara kwa kufuata taratibu zilizowekwa na nchi ili wasipate usumbufu wowote ule kutoka kwa mamlaka za wilaya ya Iringa.

“Jamani wananchi wa Iringa changamkieni kuchukua vitambulisho vya wafanyabishara wadogo wadogo ili kufanya biashara zenu mkiwa na uhuru wa kutosha ila mkikahidi mkono wa sheria utawahusu” alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwashauri wafanyabishara ya bidhaa za kusindika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata kanuni za kisheria kwa kuhakikisha wanalipa kodi kama inavyostahili.Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo walimuadi mkuu wa wilaya hiyo kuwa watahamasishana kuhakikisha wote wanakuwa na vitambulisho hivyo ili wafanye biashara kwa uhuru na haki.

“Mkuu tunakuhakikishia kuwa tutafanyabiashara huku tukiwa tumevaa vitambulisho hivi kwa kuwa Rais wetu katupa uhuru wa kufanya biashara zetu mahali popote pale bora mradi tuwe na vitambulisho hivyo” walisema wafanyabiashara hao.

StarTimes Kids yatambulishwa shule za Msingi Mchikichini

$
0
0
Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Jumatano hii ilikuwa ni zamu ya Shule ya Msingi Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 3 na 4 kutoka shule hiyo.

Mbali na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi cha Dish kwa uongozi wa shule na zawadi kadha wa kadha kwa wanafunzi waliojibu vizuri maswali na wale wanaofanya vizuri darasani. “Tunashukuru sana kwa ugeni huu wa StarTimes kuja shuleni kuzungumza na wanawafunzi na kuwapatia chachu ya kujifunza zaidi na kuwasaidia kupata msukumo wa kufanikiwa kwenye masomo yao”, alisema Mwl. Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Mchikichini Bw. Amani Levison Kidiala.

“Pia maudhui ya chaneli hii yamewachangamsha wanafunzi na pia itakuwa ni sehemu ya ukuaji wao kwa sababu kuna vitu vingi wanavyoweza kujifunza kupitia vipindi ambavyo vinafundisha sanaa na stadi mbali mbali za kimaisha.” Aliongeza. ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambay wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.

“Vipindi vingine vina mafunzo ya ustadi ambao utawasaidia watoto kujijijenga kiakili na kujiamini zaidi. Lengo letu kuja shule ya Mchikichini ni kwa sababu wanafunzi wa shule hii wanabeba uhalisia wa watoto wengi wa kitanzania”. Zamaradi Nzowa Meneja Maudhui, StarTimes Tanzania.
Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini iliyoko Mbagala Zakhem wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios akiuliza maswali na kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala(katikati) akitoa shukrani kwa Startimes Tanzania kwa kuweza kuwakumbuka wakati wa kukabidhiwa zawadi ya King'amuzi cha Startimes wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. Kulia ni Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa na kushoto ni Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kulia) akimkabidhi zawadi ya dishi la Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. Kulia ni Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa.
Meneja Maudhui  wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa(kushoto) akimkabidhi dekoda ya Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mchikichini, Amani Levison Kidiala(kulia) wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. 
Wanafunzi wa darasa la 3 na 4 kutoka shule ya msingi Mchikichini wakiangalia iliyoko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam wakiangalia katuni zinazopatikana kwenye chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Picha ya pamoja

VODACOM YAHITIMISHA KILELE CHA WIKI YA AFYA NA USALAMA JIJINI DAR

$
0
0
Emmanuel Mabula wa BestOne Company (shati la grey) akiwaelekeza wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc jinsi ya kutumia kifaa kimojawapo cha umeme katika hafla ya kuhitimisha wiki ya afya na usalama iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo inaendelea kutimiza wajibu wa kuhakikisha kwamba wanafanyakazi wake wapo katika mazingira bora na kuzingatia sheria za afya na usalama makazini.
Acky Charles wa Dartcom Miles (reflector ya kijani) akiwaelekeza wafanyakazi wa Vodacom Tanzania juu ya matumizi ya vifaa mbali mbali vya usalama, katika hafla ya kuhitimisha wiki ya afya na usalama iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampuni hiyo inaendelea kutimiza wajibu wa kuhakikisha kwamba wafanyakazi wake wapo katika mazingira bora na kuzingatia sheria za afya na usalama makazini. 
Mkurugenzi wa Rasilmali Watu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Vivienne Penessis (kulia) akimkabidhi cheti cha ushiriki Hilda Ndakidemi wa kampuni ya BMTL katika hafla ya kuhitimisha mwezi wa afya na usalama iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania mapema wiki hii jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo inaendelea kutimiza wajibu kuhakikisha kwamba wafanyakazi wake wapo katika mazingira bora na kuzingatia sheria za afya na usalama makazini.

JESHI LA POLIS KANDA MAALUM DSM LAANZA UCHUNGUZI WA VIDEO YA NGONO INAYOSAMBAA MITANDAONI IKIDHANIWA KUWA NI MCHUNGAJI GWAJIMA.

Benki Ya Exim Yamtangaza Rasmi Mtendaji Mkuu Mpya

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (Kulia) kizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Exim Tanzania pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Exim Tanzania anaemaliza muda wake Bw Said Mwema (Kulia) akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Exim Tanzania pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya wajumbe ya Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Exim Tanzania wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu (Kulia) wakati wa hafla maalumu ya kumpongeza Mkurugenzi huyo pamoja na wafanyakazi wengine iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.


Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Exim Tanzania Bw Yogesh Manek (Kulia) akiwapongeza Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo anaemaliza muda wake Bw Said Mwema wakati wa hafla hiyo.
 


Spika Ndugai Ahamasisha Wananchi Kusajili Upya Laini Zao za Simu

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba wakiwasili katika vwanja vya Bunge kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili Mpya wa Simu kwa kutumia akitembelea baadhi ya mabanda ya wadau wa Mawasiliano ya Simu katika viwanja vya katika zoezi la Usajili Upya wa Laini za Simu kutumia Kitambulisho cha Taifa liloratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikisha Kampuni za simu Bunge leo jijini Dodoma. 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akitembelea baadhi ya mabanda ya wadau wa Mawasiliano ya Simu katika viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma katika zoezi la Usajili Upya wa Laini za Simu kutumia Kitambulisho cha Taifa liloratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikisha Kampuni za simu. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi na Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akichukuliwa alama ya kidole alipotembelea moja ya mabanda ya Kampuni za Simu na Kusajili Laini katika viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma katika zoezi la Usajili Upya wa Laini za Simu kutumia Kitambulisho cha Taifa liloratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikisha Kampuni za simu. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi na Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye. 
 Baadhi ya Wabunge na Wafanyakazi wa Bunge wakisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa TTCL walipotembelea Banda la Kampuni hiyo katika viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma katika zoezi la Usajili Upya wa Laini za Simu kutumia Kitambulisho cha Taifa liloratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikisha Kampuni za simu. 

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Iramba Mashariki, Lameck Mwigulu Nchemba(MB), akisajili laini alipotembelea moja ya mabanda ya Kampuni za Simu na Kusajili Laini katika viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma katika zoezi la Usajili Upya wa Laini za Simu kutumia Kitambulisho cha Taifa liloratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikisha Kampuni za simu. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi na Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye.

NAIBU WAZIRI SHONZA MGENI RASMI TANAPA LUGALO OPEN 2019

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh Juliana Shonza anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufungaji mashindano ya TANAPA Lugalo Open  Mashindano yanayotarajia kutimua Vumbi kesho Mei 10 katika Viwanja vya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema ni bahati kwa mchezo wa Gofu kupata Mgeni Rasmi kutoka Ngazi ya Juu ya Uongozi wa Wizara Husika.

“ Tumekuwa na wageni rasmi Kila Mara Lakini kutoka katika Wizara Husika kupata kiongozi wa Juu ni Fursa itakayowawezesha kuufahamu mchezo na Changamoto zake kwa Ukaribu” Alisema Mweyekiti.

Aliongeza kuwa mashindano haya ni makubwa na  ni moja kati ya mashindano ya ratiba na kusimamiwa naa Chama cha Gofu Tanzania na  Lugalo tumepewa dhamana ya kuyaendesha huku yakijumuisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali.

“ Licha ya kuwa Wazi lakini Klabu tarajiwa ni wenyeji Lugalo, Dar es Salaam  Gymkhana, Arusha Gymkhana, Moshi Gymkhana, TPC Moshi, Morogoro Gymkhana na Mufindi Gofu klabu na wachezaji wengine Wa ndani na nje watakaojitokeza”  Alisema Brigedia Luwongo.

Kwa Upande wake Afisa tawala wa Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule Alisema kutokan na ukubwa wa mashindano Uchezaji Utagawanyika katika makundi matatu kwa kujumisha  Wachezaji wa kulipwa wachezaji wa ridhaa na kwa kuwa ni shindano la wazi, linatoa fursa pia kwa wachezaji wasaidizi (Caddies)

 Aliongeza kuwa  wachezaji Wasaidizi na  kulipwa watacheza siku ya Alhamisi na Ijumaa ya tarehe 10 na Jumamosi na Jumapili kwa Wachezaji wa Ridhaa  na imepangwa kufanyika hivi ili wachezaji wa kulipwa waweze kusimamia mchezo siku zingine za Mashindano.

Kwa upande wake mwakilishi wa TANAPA  Dattomax Sellanyika Alisema Tanapa itaendelea kudhamini na imefanya hivyo kwa mara ya pili ili kutoa fursa nzuri kwa Wadau wa mchezo huu kupata taarifa na kutembelea hifadhi na vivutio  kutokana na kuchezwa na Wageni Wengi.

Naye katibu mkuu wa Chama cha Golf Tanzania Boniface Nyiti aliipongeza klabu ya Lugalo kuwa Chachu ya Mchezo wa Golf na kuwa kivutio cha Wachezaji wengi kufuatia michuano wanayokuwa  wameiandaa.

NAIBU WAZIRI SHONZA MGENI RASMI TANAPA LUGALO OPEN 2019

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh Juliana Shonza anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufungaji mashindano ya TANAPA Lugalo Open Mashindano yanayotarajia kutimua Vumbi kesho Mei 10 katika Viwanja vya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema ni bahati kwa mchezo wa Gofu kupata Mgeni Rasmi kutoka Ngazi ya Juu ya Uongozi wa Wizara Husika.

“ Tumekuwa na wageni rasmi Kila Mara Lakini kutoka katika Wizara Husika kupata kiongozi wa Juu ni Fursa itakayowawezesha kuufahamu mchezo na Changamoto zake kwa Ukaribu” Alisema Mweyekiti.

Aliongeza kuwa mashindano haya ni makubwa na ni moja kati ya mashindano ya ratiba na kusimamiwa naa Chama cha Gofu Tanzania na Lugalo tumepewa dhamana ya kuyaendesha huku yakijumuisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali.

“ Licha ya kuwa Wazi lakini Klabu tarajiwa ni wenyeji Lugalo, Dar es Salaam Gymkhana, Arusha Gymkhana, Moshi Gymkhana, TPC Moshi, Morogoro Gymkhana na Mufindi Gofu klabu na wachezaji wengine Wa ndani na nje watakaojitokeza” Alisema Brigedia Luwongo.

Kwa Upande wake Afisa tawala wa Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule Alisema kutokan na ukubwa wa mashindano Uchezaji Utagawanyika katika makundi matatu kwa kujumisha Wachezaji wa kulipwa wachezaji wa ridhaa na kwa kuwa ni shindano la wazi, linatoa fursa pia kwa wachezaji wasaidizi (Caddies)

Aliongeza kuwa wachezaji Wasaidizi na kulipwa watacheza siku ya Alhamisi na Ijumaa ya tarehe 10 na Jumamosi na Jumapili kwa Wachezaji wa Ridhaa na imepangwa kufanyika hivi ili wachezaji wa kulipwa waweze kusimamia mchezo siku zingine za Mashindano.

Kwa upande wake mwakilishi wa TANAPA Dattomax Sellanyika Alisema Tanapa itaendelea kudhamini na imefanya hivyo kwa mara ya pili ili kutoa fursa nzuri kwa Wadau wa mchezo huu kupata taarifa na kutembelea hifadhi na vivutio kutokana na kuchezwa na Wageni Wengi.

Naye katibu mkuu wa Chama cha Golf Tanzania Boniface Nyiti aliipongeza klabu ya Lugalo kuwa Chachu ya Mchezo wa Golf na kuwa kivutio cha Wachezaji wengi kufuatia michuano wanayokuwa wameiandaa.


MAHAKAMA INAYOTEMBEA KURAHISISHA UPATIKANAJI WA HAKI

$
0
0
Katika kuboresha huduma zake kwa wananchi, Mahakama ya Tanzania imeamua kuanzisha Mahakama inayotembea (Mobile Court) ili kuendelea kusogeza huduma za kimahakama karibu zaidi na wananachi. Lengo la kuanzishwa kwa kwa huduma hii muhimu pia ni kuwapunguzia wananchi gharama za kufuata huduma za Mahakama na Kuongeza imani ya wananchi kwa Mahakama.

Mahakama inayotembea ni kitendo cha Mahakama kuhamisha huduma zake na kuzitolea katika sehemu mbalimbali ndani ya mamlaka husika. Dhana hii pia inamaanisha kuwa Mahakama inaweza kuhamisha huduma zake na kuzitolea sehemu mbalimbali kwa kutumia gari maalumu lenye chumba kilichotengenezwa mithili ya ofisi ya Hakimu, kinachoweza kutumika katika kusikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi.

Gari litakalotumika kutoa huduma za Mahakama lina nyenzo zote za kimahakama kama vile sehemu ya kusikilizia mashauri, vitendea kazi vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya kisasa ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kama vile kamera, mfumo wa matangazo (PA system) na mwavuli kwa ajili ya kivuli na viti vya kupumzikia wateja. Aidha, mahakama hii ni gari maalumu lenye sehemu mbili (2) Chumba cha hakimu ambacho kitakuwa na meza ya hakimu, meza ya wadaawa, meza ya karani/mpiga chapa, Televisheni, Kompyuta “Printer”, Kabati la kutunzia majalada, Vyombo vya kurekodi mashauri na vifaa vya kutangazia (vipaza sauti) pamoja na chumba cha faragha.


Historia ya Mahakama inayotembea Tanzania
Dhana hii ya Mahakama inayotembea ilikuwepo tangu miaka ya 1920 ambapo Mahakama Kuu kwa wakati huo ilitumia behewa la treni kutoa huduma za kimahakama kwenye ukanda ambao treni ilipita. Sababu za kuhamisha mahakama zilikuwa kumfuata shahidi kwa sababu ni mgonjwa au kuwapunguzia gharama mashahidi au iwapo kielelezo hakihamishiki kirahisi.

Huduma zitolewazo katika Mahakama inayotembea

Aidha, huduma zitakazotolewa na Mahakama inayotembea ni pamoja na kupokea, kusajili na kusikiliza mashauri, kutoa taarifa za mashauri, kutoa fomu za viapo na kuthibitisha nyaraka mbalimbali. Huduma nyingine zitakazotolewa ni kufanya usuluhishi kwa wadaawa na kutoa elimu kuhusiana na masuala mbalimbali ya Mahakama.


Aina za mashauri yanayosikilizwa katika Mahakama inayotembea

Kama ilivyo kwa Mahakama tulizozizoea, Mahakama inayotembea itasikiliza mashauri ya aina zote yanayosikilizwa na Mahakama za Mwanzo kama vile migogoro ya ndoa, madai, mirathi pamoja na jinai. Mahakama hii itasikiliza mashauri katika operesheni maalumu.


Ratiba ya utoaji huduma

Baada ya kuanzishwa kwa Mahakama inayotembea, Mahakama ya Tanzania inatarajia kutoa huduma kwa kufuata Kalenda na ratiba maalumu pamoja na taratibu zilizowekwa. Ratiba (causelist) zitatoa taarifa na maelekezo ya siku na muda ambao shauri litasikilizwa.


Utekelezaji Hukumu (kukaza hukumu)

Utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama inayotembea utafanywa katika Mahakama za kawaida katika eneo/mamlaka husika. Mfano, hukumu iliyotolewa na mahakama inayotembea katika kituo cha Bunju utekelezaji wake utafanyikia kwenye Mahakama ya Mwanzo Kawe.

Haki ya Kukata Rufaa katika Mahakama inayotembea

Mhusika yeyote katika shauri asiyeridhika na uamuzi wa Mahakama inayotembea ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama ya juu. Kwa upande wa Mahakama ya Mwanzo, mhusika anaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Wilaya kwa kufuata taratibu zilizopo. Kwa upande wa Mahakama ya Wilaya mhusika anaweza kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Faida zitakazopatikana baada ya kuanzishwa kwa Mahakama inayotembea

Baadhi ya faida zitakazopatikana kutokana na Mahakama ya Tanzania kuanzisha Mahakama inayotembea ni pamoja na kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au kuondoa kabisa mlundikano wa mashauri mahakamani. Mahakama inayotembea pia itasaidia kuwapunguzia gharama wananchi za kufika Mahakamani kufuatilia haki zao na kupitia Mahakama hii ustawi wa jamii utaimarika. Aidha, Mahakama hii itakuwa ni fursa pekee ya kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi kwa kuwa wananchi hawatatumia muda mrefu kufuatilia haki zao kwa kuwa Mahakama inayotembea uitarahisisha upatikanaji wa haki.

Maeneo yatakayohudumiwa na Mahakama inayotembea

Kwa kuanzia, huduma hii itatolewa katika mikoa ya Dar es salaam na Mwanza. Katika mkoa wa Dar es salaam, huduma ya Mahakama inayotembea itatolewa katika maeneo ya Bunju “A” (kwenye viwanja vya ofisi ya Serikali za mitaa), Kibamba (kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni), Chanika (pembeni ya kituo kipya cha Polisi Chanika) na Buza (eneo la kituo cha mabasi Buza).

Katika Mkoa wa Mwanza, huduma za Mahakama inayotembea zitatolewa katika maeneo ya Buhongwa (eneo la wazi karibu na kituo cha Polisi Buhongwa), Igoma (eneo la kuegesha Malori Igoma-Terminal Trucks ground) na Buswelu katika Viwanja vya Soko Buswelu.

Licha ya kuanzisha huduma ya Mahakama inayotembea kwa baadhi ya maeneo nchini, Mahakama ya Tanzania inao mpango la kutanua wigo wa utoaji wa huduma kwa njia ya magari maalum katika mikoa mingine hapo baadaye ili kuendelea kusogeza huduma za kimahakama karibu zaidi na wananchi na kurahisisha upatikanaji wa haki.


Rais azindua Mahakama inayotembea

Akizindua Mahakama inayotembea hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kuanzisha huduma hii kwa kuwa itasaidia kutoa haki kwa wananchi wengi na kuitaka Mahakama kuongeza idadi ya magari hayo ili kufikia maeneo mengi zaidi nchini.

Akizungumza wakati wa sherehe za kilele cha wiki ya Sheria na Siku ya Sheria nchini, Mhe. Rais pia aliipongeza Benki ya Dunia kwa ufadhili wa ununuzi wa magari hayo ya Mahakama inayotembea.

“Nakupongeza sana Mhe. Jaji Mkuu pamoja na Watumishi wote wa Mahakama kwa ujumla kwa maboresho ya Mahakama yaliyofanyika na vilevile napongeza uanzishwaji wa huduma ya Mahakama inayotembea kwani itawasaidia wananchi kutatua migogoro mbalimbali” alisema Mhe. Dkt. Magufuli.

Hata hivyo, Mhe. Rais aliitaka Mahakama kuelekeza huduma hiyo katika kutatua matatizo ya wananchi hususani wanawake wajane ambao wanahangaika muda mrefu kufuatilia mirathi hatua ambayo wakati mwingine inawasababisha kukosa haki zao za msingi.

“Maombi yangu, huduma hii iwasaidie pia wanawake ambao wengi wanahangaika kwa muda mrefu kushughulikia mirathi, ikibidi liwepo gari maalum ambalo ikiwezekana awekwe Jaji/Hakimu mwanamke kwa ajili ya kuwasaidia wamama wajane kuhusu masuala ya mirathi,” alisisitiza Mhe. Rais.

Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumzia Mahakama inayotembea wakati wa siku ya Sheria nchini alisema Mahakama zinazotembea zitasaidia kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi hasa sehemu zisizo na Mahakama, kusikiliza kesi na kuzimaliza.

“Katika dhana hii mpya ya Mahakama inayotembea mahakama itahamishia shughuli zake katika chumba maalumu kilichotengenezwa ndani ya gari lakini kuna huduma zote muhimu kama ilivyo ofisi au “chambers” ya hakimu ambapo itasikiliza mashauri na kuyatolea maamuzi”, alisema Jaji Mkuu.

Alisema dhamira ya Mahakama baadaye ni kuwa na magari ya aina hii nchi nzima kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi kwa mfano jamii za wafugaji na wavuvi ili kuwapunguzia wananchi wote kero. Mahakama hizi zitakuwa chini ya mamlaka ya Mahakama husika za Wilaya na Mwanzo na Mahakimu walioteuliwa kuzisimamia wamepatiwa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya kuhudumia wateja (customer care). Aliongeza kuwa Mahakama inayotembea inatarajiwa kuwa kimbilio la wananchi wengi kwa huduma nzuri zitakazotolewa katika mahakama hizo.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN MAGUFULI AKIZINDUA MAHAKAMA INAYOTEMBEA WAKATI WA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI NA SIKU YA SHERIA. WA TATU KUSHOTO NI JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA NA KULIA KWA RAIS NI SWPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MHE. jOB nDUGAI AKIFUATIWA NA ALIYEKUWA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. PROF. PALAMAGAMBA KABUDI. KUTOKA KUSHOTO NI MWAKILISHI WA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA TEMEKE, SOPHIA MJEMA AKIFUATIWA NA MUWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI BIBI BELLA BIRD.
 MUONEKANO WA NDANI GARI LITAKALOTOA HUDUMA ZA MAHAKAMA INAYOTEMBEA INAYOTARAJIWA KUANZA KUFANYA KAZI HIVI KARIBUNI.   

VIDEO CHAFU YA NGONO YAIMUIBUA GWAJIMA...AJIPANGA KUJIBU MAPIGO

$
0
0

*Atuma salamu kwa TCRA kuchukua hatua kwa aliyesambaza 

*Asema anachafuliwa kwasababu mwakani ni mwaka wa uchaguzi

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amejitokeza hadharani kujibu mapigo baada ya kusambaa video chafu ya ngono inayomuonesha akiwa kitandani akifanya mapenzi na mwanamke.

Video ya Askofu Gwajima ilianza kusambaa jana asubuhi na kadri saa zilivyokuwa zikienda ndivyo habari yake ilivyozidi kusambaa na kuwa gumzo. Katika mitandao ya kijamii kwa sasa habari ya mjini ni Gwajima.

Akizungumza leo Mei 8, 2019 Askofu Gwajima amesema amewaita waandishi wa habari ili kuzungumzia tukio ambalo lilitikisa siku za nyuma na akaamini limekwisha na kwamba alijua vita imeisha na aliamua kuweka silaha chini.

"Ukiona mtu amebeba makombora yake basi unachokifanya na wewe unachukua silaha zako.Nimeona leo nizungumze na watu wangu wa Ufufuo. Kuanzia jana niliona mtandao fulani wa Oroginali Isragramu ambaye alianza kupost picha zinaoonesha mambo yasiyofaa dhidi yangu.Nilianza kuona tangu asubuhi na baada ya hapo niliamua kufuatilia kwa kufanya utafiti kwanza maana nilitakakujua nani yuko nyuma ya hili. Nataka kurudisha adabu maana naona anataka kunizoea tena,"amesema.

Amefafanua kwanza video hiyo haina ukweli wowote bali ni ya kutengeneza na inaonesha lengo ni kumchafua ili kumnyima sauti ya kuzungumzia maovu lakini ukweli yeye atabaki imara kuliko ilivyokuwa sasa.

"Kuna mkakati wa kunichafua, hivi hata tukio hili lingekuwa la kweli iweje mambo ya chumbani yaletwe hadharani? Huwezi kuchukua mambo ya faragha ya watu wazima waliokuwa chumbani na kisha ukaanza kuyasambaza mtandaoni.

"Nia ya mtu huyo sio nzuri na hata sheria ya nchi inaleza wazi kuna picha za aina fulani ambazo hazitakiwi kuonwa hadharani .Tayari ninayo RB kama hatua ya awali ambayo nimechukua, pia naitaka TCRA imkamate mtu huyo na sheria ichukue mkondo wake.Nitashangaa kama TCRA itakaa kimya bila kumchukulia hatu myu ambaye ameamua kumchafua,"amesema Askofu Gwajima.

Amongeza aliyesambaza video hiyo anajua kabisa Askofu Gwajima ana mke, anajua ana watoto wakubwa, anajua siku za karibuni alikuwa Marekani alikokwenda kuhubiri Injili na anajua anayo makanisa 400.

"Hivyo aliyefanya kitendo cha kusambaza video hii ashindwe kwa jina la Yesu. Kwanini mimi ? Najua mwakani ni mwaka wa uchaguzi hivyo aliye nyuma ya hilii anatumia mbinu chafu kunichafua ili kuninyima sauti.Na sasa kinachoonekana yanaletwa matukio ya kunizima lakini sitakubali na nitajibu mapigo,"ameseam Askofu Gwajima.

Hata hivyo amesema katika video hiyo kuna picha za wasichana tofauti tofauti ambazo zimeunganishwa ili kumchafua na baadhi ya picha zinaonesha mwili mwingine na kichwa ni kingine huku akifafanua kwa mwanaume mwenye akili hawezi kujipiga picha mwenyewe na kisha kusambaza.

"Kwa mfano katika hizo picha iko moja ambayo nilipiga nikiwa na familia yangu ambayo sikuwa nimevaa shati na ilikuwa ni mwaka Oktoba 20, 2018 .Kupiga picha na familia yangu sio tatizo lakini kinachoonekana watu wameamua kuunganisha picha ili kuninyamazisha,"amesema Askofu Gwajima.

Hata hivyo amesema waliosambaza video hiyo badala ya kumchafua wamedhirisha yeye ni mwanaume rijali na kwamba kila kila silaha itakayofanyika juu yake haitafanikiwa .

"Kuanzia Jumapili hii nitaanza kujibu mapigo ...nataka iwe kama Jumali zilee ambazo watu walikuwa wanasikiliza Gwajima anatasema kitu gani.Dunia ina watu wa ajabu ambao wanapenda kuwekea wenzao mambo ambayo hayapo.
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima aalipokuwa akizungumza na Vyombo vya Habari leo,kuhusu kujibu mapigo baada ya kusambaa video chafu ya ngono inayodaiwa ikimuonesha akiwa kitandani akifanya mapenzi na mwanamke.

Namibia’s Nam Radio Ignitions Voice Coaching Initiative for Africa

$
0
0

Nam Radio, an all African music channel that gives power to the upcoming African artist by creating a platform for those typically lacking media access, proudly present Vocals Quick Fix Africa Project to provide essential training that will equip artists with skills and knowledge to attract their recognition by mainstream platforms.
In collaboration with their in-house artist development brand Talent Showcase Africa (TSA), Nam Radio is launching the first ever radio jingle and social media campaign in Africa that offers a very unique opportunity for listeners across Africa and the Diaspora to connect with a celebrated voice coach for the purpose of getting professional training to help them become better singers.
Joett, voice coach to afro pop superstar Vanessa Mdee and the author of new singers’ handbook 101 Letters from a Vocal Coach, is creator of the ‘Complete Vocals Overhaul’ concept in association with Nam Radio and heads up its pan-African training division. “When it comes to singing, you are the instrument!” said Joett. “With proper training, almost anyone can learn to sing like a pro—with no pain and no strain.”
Referring to their flagship voice training program, Joett explains: “we have created something that is tailored to the mindset of African singers; a program that doesn’t involve a lot of time and requires absolutely no long-term commitment from the artist whatsoever. It is what it is. A ‘Vocals Quick Fix’ for pre-studio recording sessions and live gigs. Plain and simple! This, I feel, should work well for Africa.”
Citing shouting and putting weight on the throat as being one of the most endemic problems afflicting African singers, Joett advocates vocal rebalancing using specific tailor-made vocal exercises, as the key solution to freeing the singer from all the pain and strain associated with the untrained voice.  
With private voice lessons conducted by Joett via Skype, Nam Radio brings convenient, affordable, professional help to both upcoming and established artists across the African continent, and the Diaspora.

To book your place visit their website today, at: Nam-Radio.com

WAZIRI MKUU KUONGOZA MAZISHI YA DK. MENGI KESHO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi yatakayofanyika kesho Mei 9, 2019 kijijini kwake, Kisereni, Machame, wilayani Hai, Kilimanjaro.

Waziri Mkuu anatarajiwa kuongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali. Ibada ya mazishi itafanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Kisereni, Machame.

Mwili wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia alfajiri ya Mei 2, mwaka huu akiwa kwenye matibabu huko Dubai, Falme za Kiarabu, umewasili Moshi leo ukitokea Dar es Salaam na kupokekelewa na mamia ya wananchi waliojipanga barabarani.

Jana, (Jumanne, Mei 6, 2019) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa Serikali, waliongoza maelfu ya wananchi kutoa heshima za mwisho wakati wa shughuli za kuaga mwili huo katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Hadi mauti yanamfika, Dkt. Mengi alikuwa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania (Chairman of the Media Owners Association of Tanzania - MOAT). Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF).

Baadhi ya nyandhifa ambazo Dkt. Mengi aliwahi kushika ni pamoja na Kamishna wa kamati inayoshughulikia mishahara (Salary Review Commission); Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA); Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mazingira Tanzania (NEMC); Mwenyekiti wa vyombo vya habari vya Jumuia ya Madola Tanzania (Chairman of the Tanzania Chapter-Commonwealth Press Union-CPU); Kamishna wa TACAIDS na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.

Article 6

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, Bahi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani S. Jafo amepongeza Uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya unaoendelea katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza kati ziara yake ya kikazi wilayani humo Jafo ameonyesha kuridhishwa kwake na wakati anapokea Taarifa ya Wilaya hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Afya na kisha kutembelea ujenzi wa Hospital ya Wilaya ambayo ipo katika hatua ya lenta.
“Hakika Bahi mmefanya kazi nzuri  mmejenga kwa kasi ya ajabu huku ubora ukizangatiwa katika majengo yote na  bado mmesimamia matumizi mazuri ya fedha za mradi kwa kuwapa vibarua kazi hii ya ujenzi.
Niseme wazi  kuwa Bahi mmenifurahisha kwa sababu mmeweza kutafsiri vizuri mfumo wa ujenzi pasipo kutumia MKandarasi yaani “Force Account” ambao unatumia fedha kidogo na mmeweza kutumia nguvu kazi mliyonayo ya mgambo kufyatua matofali na vibarua ambao ni vijana kutoka hapa hapa Bahi kujenga majengo ya Afya hongereni sana kwa hili” Alisema Jafo.
Sambamba na kuwapongeza viongozi hao pia aliwataka kumaliza tofauti zilizopo kati ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na Mbunge kwa kuwasisitiza kila mmojawao kutekeleza majukumu yake pasipo kuingiliana wala kukwamishana.
“Lengo letu sote ni kuleta maendeleo kwa Wananchi kwahiyo Mwenyekiti wa Halmashauri tekeleza majukumu yako pasipo kumuingilia Mbunge na Mbunge naye aendelee kutekeleza majukumu yake ya Kibunge tena anafanya vizuri sana na miradi yote hii mnayopata ni jitihada zake Bungeni kwahiyo msimkwamishe mpeni ushirikiano wa kutosha” Alisema Jafo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Belinith Mahenge amemueleza Waziri Jafo kuwa Wilaya ya Bahi ni moja kati ya Wilaya za Dodoma zinazofanya vizuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa ujenzi wa vituo vitatu vya Afya umeshakamilika na vitafunguliwa hivi karibuni wakati hospotali ya Wilaya ikiwa katika hatua ya lenta.
“Pamoja na changamoto chache ambazo tunakutana nazo katika utekelezaji wa miradi hii kama vile ushiriki mdogo wa wananchi katika kuchangia nguvu kazi, kukosekana kwa Mhandishi wa Halmashauri lakini tumeweza kukabiliana nazo na kuhakikisha hazikwamishi ujenzi wa miradi yetu ya Afya” Alisema Munkunda.
Ujenzi wa Hospital za Wilaya unaondelea kote Nchini unatarajiwa kukamilika Juni 30, 2019
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda wakati wa zaiara yake ya kukagua ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati akikagua ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Bahi  
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiendelea na ukaguzi wa Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Bahi
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiangalia matofali ambayo yanafyatuliwa na mgambo ambao wamepewa kazi hiyo kwa ajili ya kurahisisha kazi ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya.
Muonekano wa moja ya jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya Hospital ya Wilaya ya Bahi.

MSHAMBULIAJI JOHN BOCCO NA KOCHA PATRICK AUSSEMS WA SIMBA SC WATWAA TUZO LIGI KUU

$
0
0

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, John Bocco, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019. 

Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Emmanuel Okwi wa Simba na Heritier Makambo wa Yanga alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Kwa mwezi huo wa Aprili, Simba ilicheza michezo sita na kushinda mitano na kupoteza mmoja, ambapo Bocco alitoa mchango mkubwa kwa timu yake akifunga mabao matatu na kuifanya Simba ipande hadi nafasi ya pili ikitoka ya tatu iliyokuwepo mwezi uliopita.

Kwa upande wa Makambo yeye aliiongoza Yanga iliyocheza michezo mitano ikishinda mitatu, sare mmoja na kupoteza mmoja, ambapo alifunga mabao matatu na alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Yanga kuendelea kubaki nafasi ya kwanza mwezi huo, wakati Okwi aliyefunga pia mabao matatu alikuwa chachu ya mafanikio ya Simba.

Pia Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems kuwa Kocha Bora wa mwezi Aprili  akiwashinda Kocha Mkuu wa Azam, Abdul Mingange na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera. 

Aussems ameifanya Simba iendelee kung’ara katika ligi hiyo, ambapo kwa mwezi huo ilishinda michezo mitano na kupoteza mmoja ikipanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili, wakati Mingane aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare mmoja na kupoteza mmoja, lakini timu hiyo imeshuka kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili.

Kwa upande wa Zahera kwa mwezi huo timu yake ilicheza michezo mitano ikishinda mitatu, sare mmoja na kupoteza mchezo mmoja ikiendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayoshirikisha timu 20. Timu nyingi kwa mwezi huo ukiacha Simba, Yanga na Azam zilicheza mechi chache.

Washindi kila mmoja atazawadiwa sh. 1,000,000 (milioni moja) pamoja na kikombe (trophy) kutoka kwa wadhamini Biko Sports, na kisimbusi kutoka Azam Tv ambao ni wana haki ya matangazo ya Ligi Kuu. 

BODI YA LIGI YAWALALAMIKIA 9 KAMATI YA NIDHAMU
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewasilisha malalamiko mbalimbali ya kinidhamu dhidi ya viongozi, makocha na wachezaji kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Walalamikiwa ni kutoka katika klabu za Ligi Kuu ya Tanzania (TPL), na Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Makocha waliolalamikiwa ni Athuman Bilal wa Stand United, Mwinyi Zahera (Yanga), Nassoro Mrisho (Geita Gold FC), na Ramadhani Nsanzurwimo (Mbeya City).

Viongozi ni Herry Chibakasa wa Friends Rangers FC, Mohamed Hussein (Kagera Sugar FC),Walter Harrison (KMC) na Hussein Salehe wa Geita Gold FC wakati mchezaji aliyelalamikiwa ni Deus Tulusubya wa Pamba SC.

Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana Mei 12,2019

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akizungumza Bungeni jijini Dodoma Mei 8.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki Bungeni jijini Dodoma Mei 8.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama Bungeni jijini Dodoma Mei 8.2019.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba,  kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Mei 8.2019, katikati ni Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge David Silinde (kushoto) wa Mbozi Magharibi na Peter Serukamba (katikati) wa Kigoma Kaskazini, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Mei 8.2019


NEWS ALERT: Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa atumbuliwa

$
0
0
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amefanya mabadiliko ya Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) kuanzia leo tarehe 08 Mei, 2019.


Kufuatia mabadiliko hayo, Mhandisi Gonsalves Rwegasira Rutakyamirwa anakuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa DDCA.

Kabla ya nafasi hiyo, Mhandisi Gonsalves (juu kulia) alikua akifanya kazi Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA), akisimamia miradi ya maji ya pembezoni.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Florence Lawrence, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, hatua hiyo imetengua uteuzi wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa DDCA Domina Msonge (kushoto).

Serikali Yawalipa Wananchi Fidia Bonde la Mto Ruhila

$
0
0

Wizara ya Maji imelipa jumla ya Shilingi 1,913,832,491 ikiwa ni fidia kwa wananchi waliokuwa na makazi kando kando ya Bonde la Mto Ruhila ambalo ni chanzo cha maji cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA).

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara iliyotolewa leo, Wananchi hao wamekuwa wakifuatilia malipo yao kwa miaka 15 iliyopita tangu mwaka 2003. Malipo hayo yamefanyika kwa awamu tatu (3); awamu ya kwanza kiasi kilicholipwa ni Shilingi 500,000,000/= na awamu ya pili na ya tatu kiasi kilicholipwa ni Shilingi 1,413,832,491.

Kazi hiyo ya kuwalipa wananchi hundi zao imesimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA).

Idadi ya wananchi waliolipwa fidia ni 723. Hata hivyo, idadi ya wananchi wapatao 80 hawakujitokeza kuchukua hundi zao ambazo bado zipo katika Ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA),wananchi waliobaki wanaombwa kufika katika ofisi hizo kuchukua hundi zao.

TANZANIA KUPOKEA UGENI MZITO WA NCHI 16 KUTOKA SADC AGOSTI MWAKA HUU KUTOKA SADC

$
0
0
*Wafanyabiashara na wajasiriamali washauriwa kutumia fursa hiyo kutangaza biashara zao

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAFANYABIASHARA na wajasiriamali wametakiwa kutumia fursa ya kutangaza biashara zao kupitia mkutano wa 39 wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) mkutano unaotarajiwa kufanyika nchini  tarehe 17 na 18 Agosti mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa kwa mara ya pili SADC wanatembelea Tanzania na hiyo ni baada ya taifa kupewa jukumu la kuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa umoja wa nchi za kusini mwa Afrika huku Rais Magufuli ambaye kwa sasa ni makamu mwenyekiti wa umoja huo atakuwa mwenyekiti kwa muda wa mwaka mmoja akipokea kijiti kutoka Namibia.

Profesa Kabudi amesema kuwa mkutano wa namna hiyo ulifanyika nchini mwaka 2003 na Rais wa awamu tatu Benjamin Mkapa alihudumu kama mwenyekiti kwa mwaka 2003/2004.

Amesema kuwa mkutano huo utaanza na maadhimisho ya wiki ya viwanda ya SADC  na kuwataka wajasiriamali na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo katika kujitangaza.

Aidha amesema kuwa majukumu ambayo mwenyekiti atakuwa nayo ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za kikanda, kusimamia mikutano ya kisekta kama vile afya na elimu.


Kwa upande wake naibu katibu mtendaji kutoka SADC Balozi Joseph Nourrice amesema kuwa wana amini katika ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja katika kuhakikisha nchi zilizopo katika umoja huo zina piga hatua.

Mkutano huo utakaokutanisha wakuu wa nchi 16 utaanza kwa mikutano ya ndani itakayoanza tarehe 6 Agosti kabla ya kuhitimishwa tarehe 18 mwezi huo na masuala mbalimbali nyeti na ya kidharura kama mafuriko na maafa katika nchi za Malawi, Zimbabwe na Msumbiji yatajadiliwa.

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA SIKU TANO NA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA

MWENYEKITI UVCCM MKOA WA TANGA AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KATIBU HAMASA KATA YA CHUMBAGENI JIJINI TANGA

$
0
0
 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Omari Mwanga kulia akiwa kwenye msiba huo katikati ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo kushoto ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa (UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed
 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Omari Mwanga kulia akiwa kwenye msiba huo katikati ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo kushoto ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa (UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed
 Sehemu ya Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga wakiwa msibani leo
Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa (UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed akifuatilia matukio mbalimbali kwenye msiba ambapo aliyefariki alikuwa akifanya naye kazi

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Omari Mwanga leo amewaongoza viongozi mbalimbali wa jumuiya kwenye mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Hamasa na Chipukizi (UVCCM) Kata ya Chumbageni Jijini Tanga Marry Dominic Dawa yaliyofanyika Bombani Muheza.

Kabla ya mwili huo kusafirishwa kuelekea wilayani Muheza aliagwa eneo la Kange Kasera Jijini Tanga ambapo Jumuiya ya Umoja wa Vijana mkoa wa Tanga walitoa salamu zao wakati wa halfa hiyo

Akizungumza wakati kuagwa mwili huo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Mwanga aliwapa pole wafiwa na kuwataka kuwa wavumilivu kwenye kipindi hicho kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Alisema wao kama Jumuiya wapo pamoja na familia kwenye kipindi hicho kigumu huku wakimuelezea namna katibu huyo alivyokuwa mchapakazi na hodari katika utendaji wake.

Kwa kweli hapa tumepata pigo kubwa hasa ukizungatia Marry alikuwa kiongozi hodari na shupavu kwenye kuwajibika kwenye nafasi aliyokuwepo huku wakieleza mchango wake utaendelea kukumbukwa.

Hata hivyo aliwataka viongozi waliobakia kuiga mazuri yaliyofanywa na kiongozi huyo katika kuhakikisha Jumuiya hiyo inapata mafanikio makubwa .

Msiba huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo,Katibu wa (UVCCM) wilaya ya Tanga Fahad Siraji,Katibu Hamasa wilaya ya Tanga (UVCCM) Kipanga Juma,Mjumbe wa Baraza Taifa (UVCCM) Mbaruku Asilia.


Imetolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Tanga Katibu wa Hamasa na Chipukizi (UVCCM) Mkoa wa Tanga   
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live


Latest Images