Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WATU WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUCHANGAMKIA MKOPO USIO NA RIBA

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Stellah Ikupa (kulia), akiwa meza kuu pamoja na Rais wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga (katikati) na Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel kwenye Tamasha la Kitaifa la kupinga Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia kwa Watuwenye Ulemavu lililoandaliwa na umoja  huo lililofanyika Jijijini Dodoma wiki iliyopita. 


Viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Tamasha hilo.
Mtoto Bilal Donald Nyawenga mwenye ulemavu anayedaiwa kufungiwa tangu 1997
Rais wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga, akijaribu kuzungumza na mtoto huyo.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WATU Wenyeulemavu wametakiwa kuchangamkia fedha za mkopo bila riba walizotengewa na Serikali ambazo zipo katika Halmshauri ya miji nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Stellah Ikupa wakati akihutubia kwenye Tamsha la Kitaifa la kupinga Unyanyasaji na Ukatili wa kijinsia kwa watu wenye ulemavu lililoandaliwa na Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) lililofanyika Jijijini Dodoma wiki iliyopita. 

"Changamukieni fedha hizo ambazo ni asilimia mbili zipo kwenye halmshauri zetu tena mnakopa bila ya kuwa riba yoyote waambieni na wenzenu" alisema Ikupa.

Alisema awali wanawake na vijana kila kundi lilitengewa asilimia 5 ya fedha kwa ajili ya kukopeshwa lakini baada ya waziri huyo na wenzake kuomba kusaidiwa walemavu kila kundi lilitoa asilimia moja na kuwa mbili kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Ikupa alisema Serikali imekuwa ikiwajali sana watu wenyeulemavu ndio maana imetenga wizara hiyo ambayo inashughulikia masuala yote yanayo wahusu walemavu.

Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga aliiomba serikali kuendelea kusimamia sheria zote zinazowalinda walemavu ikiwa pamoja na kuwajengea miundombinu mizuri kama ngazi za kushukia na kupandia katika majengo makubwa.

"Kumekuwa na ukihukaji wa sheria za kuwalinda walemavu kama kuwaficha majumbani na kukosa haki zao za msingi kama kupata elimu na huduma zingine za kijamii tunaiomba serikali iendelee kusimamia sheria hizo na kuchukua hatua kali kwa watuhumiwa" alisema Dk.Kisanga.

Baada ya Tamasha hilo wananchi waliweza kuwaongoza viongozi wa TAMUFO kwenda kumshuhudia mtoto Bilal Donald Nyawenga mwenye ulemavu ambaye yupo Kijiji cha Chogola Kata ya Sama wilayani Mpwapwa ambaye inadaiwa anafungiwa ndani  tangu azaliwe mwaka 1997.

Mtoto huyo mwenye ulemavu wa baadhi ya viungo vyake na mwenye kichwa kikubwa amekosa haki ya kusoma lakini licha ya baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kujua changamoto aliyonayo hakuna hatua yoyote iliyochukulia ya kuweza kumsaidia.

SPIKA NDUGAI AFUNGUA MAADHIMISHO WIKI YA WANASAYANSI WA MAABARA ZA AFYA NYERERE SQUARE JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokelewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Kanda ya Ziwa, Ndg. Joseph Gimboya alipowasili kufungua maadhimisho ya wiki ya Wanasayansi wa Maabara za Afya katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde na Rais wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya, Ndg. Yahya Mnung’a.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mteknolojia Maabara, Ndg. Habiba Malima wakati akikagua Mabanda katika Maadhimisho ya wiki ya Wanasayansi wa Maabara za Afya yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akimsikiliza Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha damu salama Dodoma, Dkt. Leah Kitundya akimuelezea kuhusu changamoto wanazokutana nazo ikiwemo wakina Mama wako nyuma kwenye zoezi la kuchangia damu wengi wanaogopa sindano wakati akikagua mabanda katika Maadhimisho ya wiki ya Wanasayansi wa Maabara za Afya yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Wanasayansi Mbali mbali wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) akizungumza katika Maadhimisho ya wiki ya Wanasayansi wa Maabara za Afya yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wanasayansi, Wageni Mbali mbali katika Maadhimisho ya Wiki ya Wanasayansi wa Maabara za Afya yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. (PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA BALOZI BRAZIL NCHINI TANZANIA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Heshima wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Zanzibar Abdulsamad Abdulrahim, alipowasili katika ukumbi wa mkutano Ikulu Zanzibar, katikatika Balozi wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Nchini Tanzania Antonio Augusto Cesar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Nchini Tanzania. Antonio Augusto Cesar, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo,7-5-2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wac Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifurahia jambo wakati akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Nchini Tanzania  Antonio Augusto Cesar, alipofika Ikulu Zanzibar kwa kujitambulisha na mazungumzo leo 7-5-2019.


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Mlango (Zanzibar Door) Balozi wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Nchini Tanzania Antonio Augusto Cesar, baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo,7-5-2019.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja kushoto Balozi wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazili Nchini Tanzania Antonio Augusto Cesar, Afisa wa Ubalozi wa Brazil Bi. Daniella Xavier na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu na kulia Balozi wa Heshima Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Zanzibar.Bwa. Abdulsamad Abdulrahim na Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar,Balozi Mohammed Hamza. wakiwa katika picha ya pamoja. 

Upatikanaji dawa waimarika 94%,Viwanda vya dawa vyajengwa,Tozo zafutwa

VIPAUMBELE IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII VYATAJWA

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amewasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20 kwa kutaja majukumu ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na kuongeza kuwa Idara hiyo itatumia kiasi cha takribani bil. 415 ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwemo matumizi ya kawaida na mishahara.

Waziri Ummy amevitaja vipaumbele vya idara hiyo pamoja na majukumu ya utekelezaji wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kuwa ni Kuamsha Ari ya Wananchi Kushiriki katika Shughuli za Kuleta Maendeleo Wizara yake iliratibu ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia nguvukazi pamoja na rasilimali zinazowazunguka.

Waziri Ummy ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa skimu ya umwagiliaji katika Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro, ujenzi wa Shule Shikizi katika Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani kwa ajili ya watoto wadogo wasioweza kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 5 kufuata shule ilipo.

Mengineyo ni ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Kirare Tanga Jiji, ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Mikaranga mkoa wa Ruvuma, ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Mhagawa Asili, Wilayani Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma pamoja na ujenzi wa wodi ya mama na mtoto kwenye Kituo cha Afya Kaloleni Arusha Jiji mkoani Arusha.

Aidha Waziri ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wadau Wizara yake imeendelea kuhakikisha uwepo wa haki za mtoto za kuishi,kuendelezwa, kushiriki, kulindwa na kutobaguliwa katika jamii akiongeza kuwa Mwezi Desemba, 2018, Wizara kwa kushirikiana na wadau iliwezesha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa hadi Machi, 2019, ushiriki wa watoto katika ajenda ya maendeleo ulifanyika kupitia mabaraza ya watoto 1,669 yaliyopo katika ngazi ya Taifa, Mikoa, Halmashauri, Kata na Vijiji/Vitongoji na klabu za watoto 2,475 zilizoanzishwa katika shule za msingi na sekondari.

Kuhusu usawa wa Kijinsia Waziri ummy ameliambia Bunge kuwa Wizara yake imeandelea kukuza Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ambapo uwezeshaji wanawake kiuchumi ni suala muhimu katika kufikia usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini wa kipato katika jamii.

Aidha ameliambia Bunge katika hotuba yake kuwa Wizara yake imeendelea kusimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili yachangie katikakuleta maendeleo kwa Taifa. Katika kipindi cha mwaka 2018 hadi Machi, 2019, jumla ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 617 yamesajiliwa na kupatiwa cheti cha usajili ikilinganishwa na mashirika 385 yaliyosajiliwa mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 60.

Aidha Waziri Ummy aliongeza kuwa kati ya mashirika 617 yaliyosajiliwa, mashirika 44 yamesajiliwa katika ngazi ya Kimataifa, mashirika 551 katika ngazi ya Kitaifa, mashirika 15 ngazi ya Wilaya na mashirika saba katika ngazi ya Mkoa.

Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2019/20 yanaendelea kujadiliwa Bungeni Jijini Dodoma na yanatarajia kuhitimishwa hapo kesho kwa Bunge kuidhinisha Bajeti ya Wizara hiyo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA VIZURI KALAMU ZAO.

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Michael Ngayalina amewataka wanahabari kutumia kalamu zao vizuri ili kuepuka kuleta migogoro na uchochezi katika jamii badala yake wazitumie katika kuleta mabadiliko hasa katika sekta ya uchumi.

Kanali Ndayalina ameyasema hayo kwenye ukumbi wa NSSF uliopo Manispaa ya Kigoma mjini  kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari.

Mkuu wa Wilaya huyo ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alisema kuwa wanahabari wana nafasi kubwa ya kuchochea kukua kwa uchumi wa Taifa iwapo watatumia vizuri nafasi zao.

"Nyie wanahabari ni kiungo kizuri kati ya jamii na serikali yao endapo mtatumia vizuri kalamu kuelimisha jamii mambo mbalimbali ya kuchochea maendeleo uchumi wa Taifa letu utapanda"Alisema

Pia amewataka wanahabari kuandika habari zao kwa usahihi kama sheria inavyowaelekeza hasa katika kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu.

Naye Rais wa umoja wa muungano wa vilabu vya waandishi Tanzania(UTPC)Deogratius Nsokolo lengo kubwa ni kuona waandishi wanafuata maadili ya kazi za uandishi na kuwataka waandishi wa habari nchini kuwa sehemu ya mabadiliko hasa kwenye kipindi hiki kinachoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Baadhi ya wadau wa habari waliohudhuria katika maadhimisho hayo wamewataka wadau kutoa ushirikiano kwa waandishi ili habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
 Rais wa UTPC Deo Nsokolo akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo  vya habari katika ukumbi as nssf manispaa ya Kigoma
 Wanahabari wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja
 Katibu Mkuu wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma(KGPC)Fadhil Abdallah akisoma hotuba kwa wadau waliohudhuria maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari.
 Mmoja wa Wadau aliyehudhuria maadhimisho hayo akichangia mada

Wabunge wafanya usajili kwa kutumia alama za vidole

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum, Sonia Magogo akiwa katika meza ya usajili wa laini za simu za Airtel kwa kutumia alama za vidole, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum, Anna Gidaria akiwa katika meza ya usajili wa laini za simu za Airtel kwa kutumia alama za vidole, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Wabunge wakiwa katika meza ya usajili wa laini za simu za Airtel kwa kutumia alama za vidole, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Wabunge wakiwa katika meza ya usajili wa laini za simu za Airtel kwa kutumia alama za vidole, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Mbunge wa Mikumi, Joseoh Haule (kulia) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo wakiwa katika meza ya usajili wa laini za simu za Airtel kwa kutumia alama za vidole, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. (Picha na Airtel).
Mbunge wa Mikumi, Joseoh Haule (kulia) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (kushoto) wakiwa katika meza ya usajili wa laini za simu za Airtel kwa kutumia alama za vidole, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. (Picha na Airtel).

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akiwa kwenye banda la Kampuni ya simu ya Airtel lililopo katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwaajili ya kusajili laini kwa alama za vidole. (Picha na Airtel).

MAADHIMISHO YA REDCROSS KITAIFA KUFANYIKA KIGOMA KESHO

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

TANZANIA Red Cross leo inaungana na Nchi 191 ulimwenguni katika maadhimisho ya siku ya Red Cross Duniani Mei 8, 2019 ambapo mwaka huu kitaifa yanafanyika Mkoani Kigoma katika Viwanja vya Mwanga community center.

Akiongea na waandishi wa habari ofisa habari wa Red cross Tanzania Godfrida Jola amesema kuwa Mgeni rasmi katika madhimisho hayo kesho anatarajiwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce L. Ndalichako.

Alisema katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi atazindua bweni la wanafunzi katika shule ya Bitale Maalum iliyopo Mkoani humo iliyojengwa kwa michango ya wanachama na wafanyakazi wote ili kuwasaidiawatoto wenye ulemavu watimize ndoto zao.

Kauli Mbiu ya mwaka huu kimataifa ni " Upendo ". Ujumbe huu unamaanisha kwamba Red Cross inawafikia na kuwahudumia watu na jamii nyakati zote katika hali mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote kwa upendo.

Tanzania Red Cross Society inafanya kazi kwa bidii na kutoa huduma za Kibinadamu kwa kufuata Kanuni zake saba za Ubinadamu, Uadilifu, Kutopendelea, Uhuru, kujitolea, Umoja, na Kushirikiana Kimataifa, hii inaifanya jamii kuiamini na kukisaidia kutimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Jola alisema Red Cross imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma wakati wa maafa na dharura mbalimbali ikiwemo mafuriko, njaa, tetemeko, ajali mbalimbali za nchi kavu na majini, kushiriki juhudi za kuboresha afya ya jamii na kuhamasisha upatikanaji damu salama, huduma kwa watu wanaoishi na maambukizi.

 Kwa miaka zaidi ya 20 imekuwa ikitoa huduma za kibinadamu kwa Wakimbizi, kwa sasa inatoa huduma za afya kwa zaidi ya wakimbizi 300,000 katika kambi za Nyarugusu (Wilaya ya Kasulu) na Mtendeli (Wilaya ya kakonko), pia inatoa huduma za kuwaunganganisha wana ndugu waliopoteana (Restoring Family Links).

Katika maadhimisho ya mwaka huu, kupitia matawi yake ya mikoa na wilaya Tanzania Red Cross imefanya shughuli za kijamii ikiwemo, kusafisha mazingira, kusaidia vikundi vilivyo katika mazingira hatarishi na kuhamasisha watu uchangiaji damu kwa hiari, michezo, kambi ya vijana, kupanda miti na mafunzo kuhusu huduma za afya ikiwemo huduma ya kwanza.

Alisema pia Wilaya ya Kasulu, kwa kushirikiana na Halmashauri husika TRCS imejenga maabara za kisasa katika vituo vya afya vitatu kikiwemo cha Rusesa katika kata ya Rusesa, Nyenge (Kurugongo)na hospitali ya Kimwanya iliyopo katika Kata ya Nyachenda.

Pia katika Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma TRCS kwa ushirikiano na Belgium Red Cross inaendelea kutekeleza mradi wa Maji na afya ya msingi kwa kuwasaidia wanachi kujenga vyoo vya kisasa na kujenga uzio katika vyanzo vya maji katika vijiji saba vya Buhigwe, Kavomo, Murela, Songambele, Bulimanyi, Nyamugali na Munyegera ambapo hadi sasa familia 200 wamesaidiwa vifaa na kujenga vyoo vya kisasa.

"Tunaiomba jamii kuendelea kutoa huduma za kijamii kwa kufuata maadili ya kibaadam na kyifikia jamii popote ilipo na kila wakati"alisema

TFS YAWAPELEKA AMINI NA LINNA MSITU WA MAGAMBA KUFANYA YAO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umeamua kuwapeleka wasanii Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga katika hifadhi ya Msitu wa asili wa Magamba uliopo wilayani Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya kurekodi nyimbo yao mpya ya Nimenasa.

Vivutio vilivyomo kwenye msitu huo ndio sababu pekee ya wasanii hao kwenda kurekodi sehemu ya video itakayokuwa kwenye wimbo huo wa Nimenasa ambapo TFS imeamua kutoa nafasi kwa wasanii hao kwa kutambua wanayo nafasi ya kutumia misiti ya asili kurekodi video yao.

Akizungumza na Michuzi Blog akiwa katika msitu wa Magamba Amini ndani ya msitu wa Magamba kuna kila kitu na pengine ambavyo havipatikani nchi nyingine yoyote zaidi ya Tanzania.

"Nimenasa ni wimbo wangu mpya ambao nimemshikirisha dada Linna.Ni moja ya wimbo matata sana, hivyo niliona nina kila sababu ya kufanya video yake katika eneo ambalo kwangu naliona ni sahihi,"amesema.

Pia amesema anafahamu kuwa TFS wanasimamia hifadhi nyingi za misitu ya asili. "Binafsi kwa hapa Magamba pamenivutia sana , kuna maporomoko ya maji yanayotiririka kwa mpangilio ambao umapengwa na Mungu ukapangika.

"Kuna eneo ambalo unaweza kukaa na kuiona Wilaya yote ya Lushoto na Korogwe.Video ya Nimenasa itakuwa mtata sana,"amesema Amini huku akisisitiza kutambua fursa ambayo amepewa na TFS kwa ajili ya kwenda kutengeneza video yake hiyo.

Amini amesema kuwa video ya wimbo wa Nimenasa itatoka siku za hivi karibuni."Nawashukuru sana TFS kwa kunipa nafasi hii, nitoe rai kwa wasanii wenzangu kuhakikisha wanarekodi video zao hapa hapa nchini Tanzania."

Pia amesema TFS wamethibitisha namna wanavyotamani kuona wasanii wa fani mbalimbali ikiwemo ya Bongo Fleva wanarekodi video zao katika mazingira ya nyumbani.

"Wanazo hifadhi nyingi za misitu inayovutia na msanii anaweza kuchagua eneo ambalo anataka kwenda kurekodi kulingana na maudhui ya kazi aliyonayo,"amesema Amini.

Hata hivyo pamoja na maelezo hayo ya Amini ukweli ni kwamba msitu wa Magamba umeficha siri kubwa ya Amini na Linna .Siri hiyo itawekwa wazi baada ya kukamilika kwa video hiyo.
 Msanii wa Bongo Fleva Amini Mwinyimkuu akiwa na Linna Sanga wakati wakirekodi video ya wimbo wao mpya wa Nimenasa.Wasanii hao walikwenda hifadhi ya msitu wa asili wa Magamba uliopo wilayani Lushoto mkoani Tanga kwa ajili ya kurekodi video hiyo chini ya ufadhili wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu (kushoto) akiwa amemshikia kipaza sauti msanii Linna Sanga wakati wakirekodi video ya Nimenasa katika msitu wa Magamba uliopo Lushoto mkoani Tanga.
Msanii maarufu katika muziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu akizungumzia video yake ya Nimenasa ambayo ameirokodi kwenye msitu wa Magamba .
Wasanii Amini Mwinyimkuu na Linna Sanga wakiendelea kurekodi wimbo wao mpya wa Nimenasa katika msitu wa Magamba ambao upo chini ya usimamizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)

Balozi wa Kenya “ayapigia debe” Maporomoko ya kalambo

$
0
0
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amewaomba wawekezaji kutoka kila pande ya dunia kujitokeza kwa wingi kuwekeza kwa kujenga hoteli na nyumba za kupumzikia wageni katika eneo linalozunguka maporomoko ya Kalambo (Kalambo Falls) yaliyopo katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.

Amesema kuwa eneo hilo ni zuri kwa wanafamilia kulitumia katika siku za mapumziko, siku za sikukuu na pia kujitokeza ili kuyaona maajabu hayo ambayo yametambuliwa na Shirika la umoja wa mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (UNESCO) kuwa ni urithi wa dunia.

“Tunaomba wawekezaji waje hapa kwa wingi, hapa kuna kivutio ambacho kimejulikana na umoja wa mataifa UNESCO kama hifadhi ya urithi wa dunia, mje wawekezaji hapa, pahali ambapo siku za mwisho wa wiki watu wanaweza kuja kujipumzisha ama siku za sikukuu kuja na familia yao kwaajili ya “picnic”, wanajenga “lodges” lakini tunaomba “lodges” zijengwe nyingi zaidi za hadhi ya ubora wa juu zaidi ili tufurahie na familia zetu,” Alisema.

Balozi Kazungu ameyasema hayo alipotembelea maporomoko ya kalambo katika ziara yake ya siku moja Mkoani Rukwa iliyolenga kutafuta fursa za uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huku akitembelea kiwanda cha Nyama cha SAAFI pamoja na ujenzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga.

Aidha, Balozi Kazungu alitoa ushauri kwa wakala wa misitu Tanzania wanaoshughulika na uhifadhi wa msitu wa Kalambo pamoja na kuimarisha miundombinu ya maporomopko hayo kuona uwezekazo wa kuweka nyaya pamoja na vigari vitakavyopita kwenye nyaya hizo ili watalii waweze kuyaona maporomoko hayo vizuri zaidi pamoja na msitu huo.

Wakati akisoma taarifa ya maporomoko hayo ya Kalambo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Misitu Wilaya ya Kalambo Helman Ndanzi amesema kuwa pindi ujenzi wa ngazi za kushukukia kutoka maporomoko yanapoanzia hadi kufikia sehemu maji yanapodondokea utakapokamilika, ngazi hizo zitakuwa na urefu wa mita 1277 na kugharimu shilingi 852,789,066.70.

“Changamoto zilizopo ni kutotangazwa vya kutosha maporomoko hayo hali inayopelekea kutojitokeza kwa wawekezaji katika eneo hilo ambalo mawasiliano ya simu pia bado ni tatizo na hivyo tunaiomba mitandano mbalimbali ya simu kujitokeza kuweka minara katika maeneo haya ili mawasiliano yawe rahisi,” Alisema.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alimhakikishia Balozi huyo kuwa mkoa umejipanga kuhakikisha unakamilisha miundombinu inayohitajika ili kuwarahisishia wawekezaji kutekeleza shughuli zao kwa urahisi na hatimae kuinua uchumi wa wananchi katika mkoa lakini pia uchumi Tanzania kwa ujumla.

“Sisi tupo kwenye mpango ule wa viwanja vya ndege vile vinne, kuna kiwanja hiki cha Sumbawanga, Tabora, Shinyanga pamoja na Kigoma, karibu kila kitu kipo tayari kimazingira, vitu vyote vinavyotakiwa kufanyika kabla ya kuanza upanuzi wa uwanja tayari vimekwishafanyika, mhandisi mshauri yupo, mkandarasi yupo, mikataba tayari, fidia kwa wananchi waliohusika nae neo la upanuzi tayari, kila kitu kipo tayari, bado serikali haijaruhu lakini bila ya shaka wakati wowote ruhusa itatoka,” Alisisitiza.

Maporomoko ya Kalambo ni maporomoko ya pili kwa urefu kutoka maji yanapoanzia kumwagika hadi yanapodondokea kwa mita 235 na upana wa mita kuanzia 3.6 hadi mita 18 (single drop waterfall) ambapo maporomoko ya kwanza ni ya TUGELA yaliyopo Afrika ya Kusini yenye urefu wa mita 947.
 Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Dan Kazungu akitoa ushauri kwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Kalambo juu ya kuboresha eneo hilo la Maporomoko.

 Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Dan Kazungu (mbele kulia) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele kushoto) wakati wakiteremka ngazi za kuelekea kwenye kina cha maporomoko ya Kalambo. (Kalambo Falls)

  Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Dan Kazungu baada ya kufika eneo ambalo unaweza kuyaona maporomoko hayo vizuri.
Sehemu ya Maporomoko ya Kalambo (Kalambo Falls)

BREAKING NEWZZZZ: MAHAKAMA KUU YAAMURU MALI ZOTE ZA DECI ZITAIFISHWE NA SERIKALI

$
0
0
Na Mwene Said, Michuzi TV
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeamuru mali zote zinazomilikiwa na Kampuni ya Development Enterpreneuship for Community Initiative (DECI) ikiwamo magari, mali zisizohamishika (nyumba) na Sh.Bilioni 14.3 kutaifishwa kuwa nali ya serikali.

Pia, imemwagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kubadilisha umiliki wa magari kutoka Deci kwenda kuwa ya serikali,  Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP)kuwasilisha maombi mahakamani ili madalali wakawahamishe wananchi wanaoishi kwenye nyumba hizo kuwa za serikari.
Leo Mei 7, 2019 hukumu hiyo imesomwa  mahakamani hapo mbele ya Jaji Stephen Magoiga. Alisema mali zisizohamishika ikiwamo nyumba zibadilishwe majina ya umiliki kutoka Deci kuwa kwa jina la Msajili Hazina.

Jaji alisema akaunti za kampuni hiyo zilizopo, Benki ya Nmb tawi la Msasani, benki ya Community tawi la Uhuru na KCB tawi la Samora wahamishe  Sh. Bilioni 14.3 kutoka kwenye matawi yao kwenda Serikalini mara watakapopokea amri ya mahakama yake.

Alisema baada ya kupitia maombi  ya mlalamikaji (DPP) na utetezi walalamikiwa  Wakurugenzi wa DECI Jackson Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Saiguran Ole Loitg’nye na Samwel Mtares, bila kuacha shaka walalamikiwa wameshindwa kuthibitisha kwamba mali na fedha taslimu zimepatikana na chanzo tofauti kampuni hiyo.

"DPP katika maombi yake amewasilisha vielelezo kuthibisha kwamba mali zote zilipatikana kwa fedha za upatu, zilizopatikana kwa njia isiyo halali lakini walalamikiwa hawajawasilisha majibu yoyote yanayopinga maombi hayo au kufafanua upatikaji wa mali hizo tofauti na vielelezo vya mlalamikaji, mahakama yangu inaamuru mali zote zitaifishwe kuwa mali za serikali." Alisema Jaji Magoiga.


Alisema DPP aliwasilisha maombi akitaka kutaifisha mali hizo kuwa za serikali baada ya kubainika kuwa zimepatikana isivyo halali na kwamba ni fedha chafu. Hata hivyo, walalamikiwa hawajawasilisha utetezi kuonyesha kwamba walikuwa na biashara nyingine zaidi ya upatu.

Jaji aliendelea kuichambua hukumu kwamba walalamikaji wameshindwa kujitetea kwamba fedha na mali zote hazihusiani na upatu uliotokana na makusanyo kutoka kwa wananchi bila kuwa na leseni ya kufanya hivyo.

Alisema lengo la DPP si kuitajitisha serikali bali ni kuwataka watu wafuate taratibu na sheria kuendesha shughuli zao.

Walalamikiwa waliwakilishwa na Wakili Majura Magafu.
Mapema mahakamani hapo Magafu akijibu hoja za mlalamikaji  alidai kuwa akaunti zilizowasilishwa na DPP, kati ya hizo moja inamilikiwa na kanisa na ya pili inamilikiwa na mlalamikiwa wa kwanza.


Hata hivyo, hati ya kiapo iliyowasilishwa na DPP hakuna mahali inaonyesha ushahidi kwamba mali zote zimetokana na fedha za ujanjaujanja.

Jopo la mlalamikaji liliongozwa na Dpp Biswalo Mganga akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu Paul Kadushi, Mawakili wa Serikali Waandamizi, Theophil Mutakyawa na Shadrack Kimaro.

Akijibu hoja za walalamikiwa, DPP alidai kuwa walalamikaji walikuwa wanaendesha mchezo wa upatu kinyume cha sheria na kwamba mali zote ni mali ya DECI zinafaa kutaifishwa.

Alidai kuwa fedha na mali hizo zimethibitika kuwa zilitokana na upatu na ndiyo maana Mahakama ya rufaa katika hukumu yake ilimuelekeza kufungua maombo hayo Mahakama Kuu.

Alidai kwamba,Deci haikuwa na shuguli nyingine yeyote  mbali ya kukusanya fedha  na kwamba wajibu maombi hawakuleta ushahidi wa kulinga hilo hivyo   
biashara haramu ya upatu ndiyo ilikuwa kazi yao.


Kuhusu uhusiano wa mali za kanisa na Deci,Dpp Mganga alidai kuwa fedha zilizokuwa katika akaunti ya kanisa zilikuwa za Deci kwasababu wakàti huo hawakuwa na akaunti kwani walikuwa bado hawajakamilisha usajili.

Katika maombi ya msingi, DPP Mganga aliwaailisha maombi hayo mahakamani hapo, akiiomba itoe amri ya kutaifishwa kwa mali za kampuni hiyo yakiwamo magari 11, nyumba na viwanja vinane na fedha ziwe nali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika maombi hayo, DPP anaiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kutaifishwa na kuwa mali ya serikali, nyumba namba UKMMD/1237 iliyoko Mwembe Madafu, Ukonga, Dar es Salaam, kiwanja namba 651, kitalu ‘M’ kilichopo Forest area, Mbeya, nyumba iliyoko kiwanja namba 7, kitalu ‘P’  ikiwa na hati namba  033004/23 kilichopo mtaa wa Rufiji, Manispaa ya Mwanza.

Mali nyingine ni ardhi iliyoko katika kiwanja namba 2/283/2 kitalu “E” Mabibo, Kinondoni, Dar es Salaam, kipande cha ardhi ambacho hakijapimwa kilichopo kijiji cha Manyinga, Turiani, Mvomero, Morogoro, kiwanja namba 467 kilichopo kitalu “H” kikiwa na hati ya usajili namba 48170 kilichopo eneo la Tegeta, Dar es Salaam, nyumba iliyoko kiwanja namba MM/19/P kilichopo Manzese karibu na barabara ya Morogoro, Dar es Salaam na nyumba iliyoko katika kiwanja namba KND/MXS/MNM/Z ikiwa na leseni ya makazi namba KND 008337 Kinondoni, Dar es Salaam.

Magari ambayo DPP anaiomba mahakama kutoa amri ya kutaifishwa na kuwa mali ya serikali ni Toyota Premio lenye namba  T 132 AWJ, Toyota Land Cruiser namba T 480 AUP,   Toyota Rav 4 namba T 274 ATQ, Toyota Mark II namba T 676 AYP, Subaru Legacy namba T 682 AUT, Toyota Ipsum namba T 850 AXY, Toyota Ipsum  T455 ADM, Toyota Mark II T 186 AYX, Mitsubishi Pajero  T 852 AAV, Toyota Lande Cruiser T 789 AUX, Nissan Terrano namba T 899 AYU.

Pia, DPP anaomba mahakama kutoa amri ya kutaifishwa kwa fedha zilizoko benki katika akaunti namba 22601601056 iliyoko National Microfinance Bank (NMB), tawi la Msasani  Sh. 12,503,068,647.89.

Fedha nyingine taslimu ni zilizoko katika akaunti namba 000120100000194/1 iliyoko Dar es Salaam Community Bank (DCB), tawi la Uhuru ikiwa na Sh. 1,457,700,462.49 na fedha taslim zilizoko katika akaunti namba 021140019558 iliyoko Kenya Commercial Bank (KCB), tawi la Samora, Dar es Salaam, ikiwa na Sh. 57,933,304.10.
Viongozi wa DECI Arbogast Kipilimba, Jackson Mtares, Samwel Mtares, Dominick Kigedi na Timotheo Saiguran ole Loiting’ye wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam. Picha ya Maktaba.

Mc Pilipili kizimbani kwa tuhuma za makosa ya mtandao

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
 MSHERESHAJI maarufu nchini, Emmanuel Mathias (34) anayejulikana zaidi kwa jina la MC Pilipili na mwenzake Heriel Clemence (25) wamepandishwa katika kizimbani cha Mahakama ya Hakimu Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha maudhui kwenye mtandao bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 

 Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Costantine Kakula akisaidiana na Batrida Mushi leo Mei 19,2019 amedai mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando kuwa washtakiwa wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kuchapisha maudhui bila kuwa na leseni. 

Amedai, MC Pilipili ambae ni mkazi wa Mbezi Beach na Clemence Mkazi wa Kawe wanadaiwa, kati Novemba 17, 2013 na Mei 2, 2019 katika maeneo tofauti tofauti ndani ya jijii la Dar es Salaam kwa kupitia televisheni za mtandaoni inayojulikana kama Pilipili TV bila kuwa na leseni kutoka TCRA.
Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na MC Pilipili amekamilisha masharti hayo na ameachiwa kwa dhamana, huku Clemence akishindwa kukamilisha masharti na amerudishwa rumande. 

 Hakimu Mmbando amesema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana kila mmoja anatakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho halali ambao watasaini bondi ya sh milioni tano kwa kila mmoja. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

 Katika kesi nyingine, mshereheshaji, Julius Warioba(23) maarufu kama Mc Warioba, naye amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kujibu shtaka la kuchapisha maudhi katika Mtandao bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini( TCRA). Warioba anayeishi Ubungo, anadaiwa kuwa, kati ya Januari 2016 na April 30, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam mshtakiwa Warioba alichapisha maudhui kupitia Televisheni ya mtandaoni ( Tv online) inayojulikana kwa jina Mc Warioba, bila kuwa na kibali kutoka TCRA huku akijua kuwa ni kinyume cha sheria ya Mtandao. 

Mshtakiwa amekana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo yamemtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata na barua hiyo, ipitishwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa, anakotokea mdhamini huyo.

 "Mshtakiwa nakupa dhamana ila kesho ulete barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata yako na vitambulisho vyako vitazuiliwa hapa mahakamani hadi hapo utakapolea barua", amesema Hakimu Mtega. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi kesho ajili ya mdhamini kuwasilisha barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata.

RAIA wa uingereza mahakamani kwa utapeli

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
RAIA wa Uingereza,  anayeishi Mikocheni jijini Dar es Salaam, Derick Tweedley (85),  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na  shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi  cha sh. Milioni 717 mali ya Gulam Dewji.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Wankyo Simon, amedai mbele ya Hakimu Mkazi.  Maira Kasonde leo Jumanne, Mei 7, 2019 kuwa, Desemba 9 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alijipatia USD 300,000, ambazo ni sawa na Sh milioni  717milioni kutoka kwa Gulam Dewji.

Imedaiwa kuwa mshitakiwa huyo alijipatia kiasi hicho cha fedha baada ya kumdanganya Dewji kuwa atahamisha umiliki wa kiwanja namba 16066 na 7902 kwenda kwenye Kampuni ya  Mohamed Enterprises (Tanzania) wakati akijua kuwa sio kweli.

Mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo
Yalimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho watakao wasilisha fedha taslimu sh. Milioni 353.5 kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi  hadi Mei 20, mwaka huu, itakapotajwa.

MASELE AIKINGIA KIFUA SERIKALI YA TANZANIA KWENYE BUNGE LA AFRIKA

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akisisitiza jambo wakati akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.Picha na Kadama Malunde- Malunde1 blog


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua za haraka kusaidia nchi za Kusini mwa Afrika (Msumbiji,Malawi na Zimbabwe) zilizoathirika na Kimbunga cha Idai. 

Mheshimiwa Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini ametoa pongezi hizo leo Mei 7,2019 akiongoza kikao cha Bunge la Afrika kinachofanyika Jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini wakati wabunge wakijadili kuhusu Ripoti ya kazi ya Umoja wa Afrika (AU). 

Mhe. Masele alilazimika kutoa ufafanuzi baada ya hoja kuibuka hoja bungeni kuwa nchi za Umoja wa Afrika zimekuwa hazichukui hatua za haraka panapotokea majanga mbalimbali. 

“Nitumie fursa hii kuipongeza sana serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kuchukua hatua za haraka kusaidia chakula na madawa kwa nchi zilizokumbwa na Kimbunga Idai”,alisema Mhe. Masele. 

“Serikali ya Tanzania ilikuwa mstari mbele kutoa msaada wa chakula,dawa na vifaa vya kujiihifadhi kwa nchi ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika”,aliongeza Mhe. Masele.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha Bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Katikati ni Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Roger Nkodo Dang akitoa taarifa ya kazi ya Bunge la Afrika.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Kikao cha bunge kikiendelea.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA BUNGE LA AFRIKA

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akimpokea Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika “Pan- African Parliament” yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini leo Mei 7,2019.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akimkaribisha ofisini Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete. 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang (katikati) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele. 
Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akizungumza jambo wakati wa majadiliano hayo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa majadiliano yake na Viongozi wa Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu hali ya uchaguzi Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete ambaye anaongoza Timu ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019 akiongoza kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi huo nchini Afrika Kusini.
Kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini kati ya Viongozi wa Bunge la Afrika na timu ya waangalizi ya Umoja wa Afrika inayoongozwa na Dkt. Jakaya Kikwete kikiendelea.
Waheshimiwa Mabalozi kutoka Kenya,Nigeria wa kiongozwa na Balozi Naimi Aziz wa kwanza kulia anayeiwakilisha Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika ambao wameambatana na Mheshimiwa Kikwete.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (wa tatu kulia) akizungumza wakati wa kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2019 nchini Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akitembelea ukumbi wa Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akipiga picha ya kumbukumbu ofisini kwake na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Jijini Johannesburg, Afrika Kusini. 


****

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete ametembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika “Pan- African Parliament” yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Dkt. Kikwete ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika wa Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019 amepokelewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele leo Jumanne Mei 7,2019.

Amelipongeza Bunge la Afrika kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kusimamia Demokrasia, Utawala na Masuala ya Ulinzi na Usalama barani Afrika.

“Mimi nilikuwa miongoni mwa Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao tulikutana kule Sirte Libya kuandaa kanuni za kuanzishwa kwa Bunge la Afrika,hivyo ninayo furaha kubwa kuona hatua kubwa ya maendeleo ya bunge,Nawapongeza sana Rais na Makamu wa Rais kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuendeleza bunge hili na Waafrika wote tunawatagemea”,amesema Dkt. Kikwete

“Leo na timu yangu ya uangalizi ambao tupo hapa Afrika Kusini kwa ajili ya uangalizi wa Uchaguzi mkuu wa mwaka huu,na ninashukuru miongoni mwa timu yangu wabunge wa bunge la Afrika ni miongoni mwa wajumbe wangu,nawapongeza sana Bunge la Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika kusimamia demokrasia”,ameongeza Dkt. Kikwete.

Kwa upande,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele amemshukuru na kumpongeza, Mheshimiwa Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa bara la Afrika kwenye nyanja za afya,elimu na demokrasia.

"Sisi viongozi vijana tuna mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wako mkubwa kwenye masuala ya uongozi na siasa za kimataifa, binafsi nakushukuru sana kwa malezi yako ambapo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nimeweza kufika hapa nilipo kiuongozi",amesema Mhe. Masele.

Aidha amemuahidi Mheshimiwa Kikwete kuwa Bunge la Afrika litatoa ushirikiano wote unaohitajika ili kuweza kutimiza majukumu yake katika uangalizi wa uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019.


Na Kadama Malunde - Johannesburg,Afrika Kusini

KAFULILA ASITISHA MKATABA NA TBA UJENZI WA NYUMBA ZA VIONGOZI

$
0
0


Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akizungumza na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas katika eneo la ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa, Kafulila amevunja Mkataba na TBA wa ujenzi wa Nyumba hizo kutokana na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
Eneo likionyesha hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa ambapo kwa muda wa miezi miwili tangu wakabidhiwe eneo la ujenzi TBA wamefikia hatua hiyo huku wakibakiwa na miezi mingine miwili ya kukamilisha ujenzi huo, hali iliyopelekea Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila kuvunja mkataba na TBA kutokana na kutoridhishwa na kasi hiyo.

……………………..

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amesitisha Mkataba wa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa uliokuwa kati ya yake na Shirika la Ujenzi la Taifa (TBA), kutokana na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo.

Kafulila akiambatana na wakuu wa Sehemu wa Sekretarieti ya Mkoa wa Songwe amefikia uamuzi huo jana mara baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa nyumba hizo na kukuta hatua ya ujenzi iliyofikiwa hairidhishi.

Kafulila amesema kasi ya ujenzi wa nyumba hizo inatia mashaka kutokana na kuwa kazi iliyokwisha fanyika kwa muda wa siku sitini ni ndogo ukilinganisha kazi na muda uliobakia kufikia tarehe ya makubaliano ya kukamilika ujenzi.

“Kazi iliyobaki kiuhalisia haiwezekani TBA wakaikamilisha kwa muda uliobakia, kwani tuliwakabidhi eneo la ujenzi tarehe 2-2-2019 na tulikubaliana ikifika tarehe 30-06-2019 nyumba hizo mbili ziwe zimekamilika lakini kwa kipindi cha miezi miwili hakuna kitu wamefanya na kuna dalili zote za kutokamilisha kwa muda”, ameeleza Kafulila.

Ameongeza kuwa TBA wamekuwa na tabia ya kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kasi ndogo mkoani Songwe na hivyo kusababisha fedha kurudishwa hazina kuu kutokana na kutozitumia kwa muda unaotakiwa yaani ndani ya mwaka wa fedha wa serikali ambapo fedha hizo zinakuwa zimetolewa.

“TBA mmekuwa na kawaida ya kutekeleza miradi yetu kwa kasi ndogo na hivyo kusababisha fedha kurudishwa hazina, mfano ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamesababisha takribani Bilioni 3.8 zirudishwe na sasa tunahangaika kuziomba tena, uzembe huu tunaona unelekea kujirudia tena na sisi kama Mkoa hatuko tayari kila mara tunapewa fedha za ujenzi halafu zinarudishwa kwa uzembe wa TBA”, ameongeza Kafulila.

Amesema kuwa Mkoa hauna matatizo na Wizara ya Ujenzi wala shirika hilo la TBA ila lazima hatua za kusitisha mkataba huo zichuliwe ili kunusuru fedha hizo kurudishwa hazina kuu kutokana na kuchelewa kuzitumia ndani yam waka wa fedha wa serikali pia ili nyumba hizo zikamilike kwa muda na kuwezesha makazi ya viongozi.

“Naomba ifahamike mimi na mkoa kwa ujumla hatuna matatizo na Wizara ya Ujenzi pamoja na TBA lakini tukilifumbia macho hili hata sisi tutapimwa utimamu wa akili zetu, nimetembelea eneo la ujenzi zaidi ya mara nne lakini hakuna maendeleo yoyote, kiuhalisia kwa kasi hii TBA Mtatuangusha, sisi tunapenda kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya Rais wetu”, amesisitiza Kafulila.

Amesema gharama ya Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa ni shilingi milioni 499.9 na tayari TBA walipewa malipo ya awali ya shilingi milioni 74.9 huku nyumba ya Katibu Tawala Mkoa ikiwa na gharama ya shilingi milioni 499.7 na malipo ya awali yaliyotolewa ni shilingi milioni 74.9

Imeelezwa kuwa TBA hawajawahi kuwasilisha taarifa ya kazi iliyokwisha fanyika lakini pia hawajaomba fedha zozote tangu walipwe malipo ya awali huku muda uliobaki ukionyesha kuwa hataweza kukamilisha kazi iliyobaki.

Msimu wa pili wa MultiChoice Talent Factory Wafunguliwa

$
0
0
Vijana wenye kiu ya kuwa wabobezi wa filamu kupata udhamini
Mafunzo ya kitaalamu ya mwaka mzima kutolewa
Ni kwa udhamini wa MultiChoice
Mpango wa umoja wa Afrika unatafuta wabunifu 60 wa filamu na televisheni barani kote Afrika kuwa sehemu ya darasa la mwaka 2019.

Vijana 60 kutoka kote barani Afrika – ikiwemo Tanzannia watapata fursa ya udhamini wa kujifunza uzalishaji wa filamu na vipindi vya televisheni kwa mwaka mzima katika  awamu ya pili ya program ya MultiChoice Talent Factory

Kuanzia tarehe 7 Mei 2019 hadi tarehe 14 Juni 2019, vijana wenye uchu wa kuwa wabobezi wa filamu watapata fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya usaili utakaotoa wanafunzi 60 watakaodhaminiwa kwa mafunzo hayo ya kitaalamu ya mwaka mzima yanayoendeshwa katika vituo vitatu barani afrika ikiwemo Nairobi, Lusaka na Lagos.

Kwa upande wa Tanzania, kuna nafasi nne za udhamini katika awamu hii ya pili ambapo wanafunzi hao wataungana na wenzao kutoka Kenya, Uganda na Ethiopia katika kituo cha mafunzo cha Nairobi.

Kwa wanaotaka kushiriki ni rahisi sana. tembelea  www.multichoicetalentfactory.com  kabla ya tarehe 14/06/2019 na kisha fuata maelekezo ya namna ya kujisajili. Kwa watakaopata tatizo lolote wanaweza kutuma e-mail info@multichoicetalentfactory.com Au kupiga simu +255756753201 kwa maelekezo zaidi.

Program ya MultiChoice Talent Factory ilizinduliwa rasmi mnamo Mei 2018, kwa lengo la kuwanoa vijana wa kiafrika katika tasnia ya filamu ili kuwapa upeo, uwezo, ujuzi na weledi wa kiwango cha kimataifa katika uzalishaji na biashara ya filamu kwa ujumla.

Cituo hivyo vya mafunzo vinaongozwa na wakufunzi mahiri wenye ujuzi mkubwa na pia vina vifaa na miundombinu ya Kisasa kuwawezesha wanafunzi kujifunza uzalishaji filamu wa Kisasa na wa kibiashara.

Kama sehemu ya programu, watengenezaji wa filamu wadogo watapatiwa mafunzo na uzoefu wa vitendo katika tasnia ya filamu, kwa kuzingatia simulizi za visa, uzalishaji, sauti na kuongoza na maeneo mengine muhimu. Vituo hivi pia vinatoa fursa kwa wanafunzi ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa sekta hiyo, kufanya kazi za kuzalisha  vipindi vya televisheni, maigizo na kuanda maudhui asilia ambayo yatakuwa yakirushwa hewani kwa njia mbalimbali ndani ya M-Net kwa kupitia  (DStv)

Darasa la kwanza la programu hii ambalo litakamilika mwezi Oktoba mwaka huu, tayari limeonyesha mafanikio makubwa ambapo wanafunzi wameshiriki katika kazi mbalimbali  ikiwemo utengenezaji wa vipindi halisia vya muziki kama Coke Studio, Pambio, Turn-Up na telenovela ya kiswahili maarufu kama Selina.

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso, amewataka vijana wadogo kuchangamia fursa hiyo adhimu. “Nawasihi vijana wetu wa Tanzania wenye ari na nia ya kuwa nyota wa uzalishaji wa filamu duniani kuhakikisha kuwa hawakosi nafasi hii. Wajiandikishe ili waweze kupata fursa hiii muhimu”


Jiunge na mazungumzo ya mitandao ya kijamii ya MTF kwa kuandika #MultichoiceTalentFactory na jiunge:
Instagram: @multichoicetalentfactory
Twitter: @MCTalentFactory
Facebook: @multichoiceafricatalentfactory

SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBOLEA YA ASILI-MHE MGUMBA

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 8 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 8 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali kwa kushirikiana na taasisi za sekta binafsi imeendelea kutoa elimu ya kilimo bora inayojumuisha matumizi sahihi ya mbolea za asili, viuatilifu vya asili, mbegu bora na hifadhi ya mazingira ili kuzalisha mazao kwa tija na kuwa na kilimo endelevu.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 8 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Chambani Mhe Yussuf Salim Hussein aliyetaka kufahamu Serikali imeweka mikakati gani ya kutoa elimu ya mbolea ya asili kwa wakulima na hatua Serikali inayoichukua ili kuona kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kuzalisha mazao yasiyotumia mbolea za viwandani. 

Alisema kuwa katika kutekeleza mpango wa muda mrefu wa matumizi sahihi ya virutubisho vya udongo, Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inafanya utafiti wa afya ya udongo katika Kanda zote saba za kiikolojia za kilimo nchini. 

Utafiti huo unalenga kubaini aina za virutubisho na tabia za udongo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kiasi, aina na matumizi sahihi ya mbolea za viwandani na asili. Utafiti huo umeanza kwa kuchukua sampuli za udongo katika Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini na sehemu ya Kanda ya Mashariki (Mkoa wa Morogoro) na utaendelea katika maeneo mengine nchini na kukamilika Juni 2020.

Alisema, kwa kutambua ongezeko la mahitaji ya mazao na bidhaa za kilimo zinazozalishwa kwa kutumia mbolea za asili na viuatilifu vya asili, Serikali imeboresha mtaala wa mafunzo katika vyuo vya kilimo ambapo mada za kilimo hai na hifadhi ya mazingira zimejumuishwa ili kuwawezesha maafisa ugani na wakulima kupata elimu hiyo. 

Mhe Mgumba aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na Tanzania Organic Agriculture Movemet (TOAM), Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), Ecology Agriculture chini ya SWISSAID, Zanzibar Organic Producers (ZANOP), Tanzania Alliance for Biodiversity (TABIO) na TANCERT inatoa elimu ya kilimo hai kwa wakulima na kutoa vyeti vya ubora wa mazao kwa ajili ya masoko maalum. Baadhi ya mazao ambayo yanazalishwa katika mfumo wa kilimo hai hapa nchini ni pamoja na kakao, kahawa, pamba na viungo. 

Kadhalika, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe Easter Michael Mmasi aliyetaka kufahamu kuhusu ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya kilimo, Mhe Mgumba alisema kuwa Sekta ya Kilimo inajumuisha sekta ndogo za kilimo mazao, mifugo, uvuvi na misitu. 

Bajeti za Wizara za Sekta ya Kilimo zinajumuisha bajeti za Wizara za sekta husika, Bodi za mazao na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara za Kisekta. Utekelezaji wa bajeti hizo huwawezesha wanaume na wanawake katika shughuli za kilimo. Wanawake wanachangia asilimia 90.4 ya nguvukazi ya wanawake inayotumika katika shughuli za kilimo na kuchangia wastani wa asilimia 70 ya mahitaji ya chakula nchini. 

Mhe Mgumba alisema kuwa katika kutatua changamoto hizo Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 kupitia mifuko ya uwezeshaji ikiwemo Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake (Women Development Fund - WDF) ambao huchangiwa asilimia 4 ya mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kila mwaka. Katika mwaka 2017/2018, jumla ya Shilingi 15,633,312,764.91 zimetolewa kwa vikundi 2,919 vya wanawake na vijana vyenye jumla ya wanawake wajasiriamali 29,190 katika Halmashauri mbalimbali nchini. 

Aidha, alisema kutokana na umuhimu wa wanawake katika kilimo Serikali imeielekeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo (Tanzania Agricultural Development Bank – TADB) katika mikopo inayotoa asilimia 20 ya mikopo itolewe kwa vikundi vya wanawake. Hadi Januari 2019, asilimia 33 ya mikopo imetolewa katika vikundi vya wanawake kupitia Benki ya TADB. Vilevile, benki za NMB na Azania zimeanzisha dirisha maalumu la kutoa mikopo kwa vikundi vinavyo jishughulisha na kilimo na miradi mbalimbali. Pia Serikali imehamasisha wanawake kujiunga kwenye vikundi vya ushirika wa akiba na mikopo kama SACCOS, VICOBA ili kupata huduma za kifedha na mikopo kwa urahisi ili kuongeza mitaji yao katika kilimo.

Mhe Mgumba aliongeza kuwa, Serikali imeuelekeza Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (Agricultural Input Trust Fund - AGITF) kutoa kipaumbele kwa vikundi vya wanawake vinavyoomba mikopo ya kuendeleza kilimo. Vile vile, Serikali imeendelea kutoa hati miliki za ardhi za kimila na hati miliki za ardhi kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kumiliki ardhi na kuzitumia kama dhamana kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha ili waweze kupata mitaji ya kununua pembejeo na zana bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji, tija na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindikaji wa mazao ya kilimo.

MILIONI 700 ZA RAIS MAGUFULI ZAANZA KUTOA MATOKEO POLISI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akipita kukagua ujenzi wa majengo mapya na ya kisasa yanayojengwa katika Chuo cha Maofisa wa Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es salaam, ujenzi unaotokana na fedha iliyotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kiasi cha shilingi milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa Chuo hicho cha Maofisa. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akifurahia jambo huku akiwa amembeba mtoto aliyefika katika hospitali Kuu ya Polisi iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam leo, akiwa na mzazi wake kwa ajili ya kupata huduma za matibabu hospitalini hapo, IGP Sirro amefanya ziara ya ghafla ya ukaguzi yenye lengo la kuona namna huduma za matibabu zinavyotolewa pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na Maofisa wa Polisi wanaofanyakazi katika hospitali Kuu ya Polisi iliyopo Kurasini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya ghafla ya ukaguzi yenye lengo la kuona namna huduma za matibabu zinavyotolewa pamoja na changamoto wanazokutananazo ambapo IGP Sirro amewataka viongozi hao kutoa huduma bora kwa wateja. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu Dkt. C. Msenga wa hospitali ya Jeshi hilo iliyopo Kurasini Jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya ghafla ya ukaguzi hospitalini hapo. Picha na Jeshi la Polisi.

MKURABITA YAPONGEZWA KWA URASIMISHAJI ARDHI UYUI

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images