Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109583 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: HAKIMU WA MAHAKAMA WILAYA NA MAWAKILI WA SERIKALI KIZIMBANI ARUSHA KWA MASHITAKA 11

0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha 
Hakimu wa mahakama ya wilaya mkoani Arusha Benard Nganga, na wenzake wanne wakiwemo mawakili wa serikali wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 11 yakiwemo ya uhujumu wa uchumi na utakatishaji wa fedha. 
 Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu mfawidhi Niku Mwakatobe wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Mwendesha mashtaka wa serikali Javelin Rugailuza amewataja washtakiwa wengine ni Maneno Mbunda wakili wa shirika la hifadhi za Taifa (Tanapa), Fortunatus Mhalila na Tumaini Mdee wote ni mawakili wa serikali na mfanyabiashara Nelson Kangero. 
Mwendesha mashtaka huyo ameeleza kuwa kati ya tarehe 1 mwezi wa sita mwaka 2018 katika maeneo tofauti jijini Arusha na mkoani Arusha washtakiwa kwa pamoja walitenda makosa mbali mbali ya uhujumu wa uchumi na kujipatia rushwa na uundwaji wa genge la mtandao wa uhalifu. Makosa mengine wanayokabiliana nayo ni pamoja na kutoa na kupokea rushwa ya million 31.5 kwa lengo la kushawishi wa kuwezesha kuwachiwa huru kwa mhalifu na kuhuaribu ushahidi, na kuchoma jalada la kesi, pamoja na kuwasilisha nyaraka za uongo.
Baada ya mwendesha mashtaka huyo kuwasomea mashataka hayo hawakutakiwa kujibu chochote kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo kuahirishwa hadi tarehe 20 mwezi huu. 
Wakati huo huo Mshatakiwa Nelson Kangero alisomewa shtka mmoja la kukutwa na meno 15 ya Tembo ambayo ni nyara za serikali zenye thamani ya shilingi million 100.8 kinyume cha sheria. Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mfawidhi Mwakatobe Mwendesha mashtaka wa serikali Javelin Rugailuza alisema kuwa mnamo Disemba 15 mwaka 2017 katika eneo la Kichwa cha Nyumbu Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro mtuhumiwa alikutwa na Meno ya tembo yenye thamani ya dola za Kimarekani 15000 mali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo kupelekwa rumande hadi mei 20 mwaka huu kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Wakati huo huo Mkurugenzi wa Makosa ya jinai wa Jeshi la Polisi (DCI) Robert Boaz amesema kuwa hali ya uhalifu nchini imepungua kwa asilimia 3.4 ukilinganisha na makosa kama hayo mwaka jana ambayo yalikuwa 14,866 na robo mwaka huu ni 14,355. 
Akizungumzia makosa makubwa yakiwemo ya Unyang’anyi wa kutumia silaha na Ujangili Boaz alisema yamepungua kwa asilimia 4.7 ambapo mwaka jana yalikuwa 6897 na mwaka huu ni makosa 6573,hatua hiyo imetokana na Jeshi hilo kuunda timu ya kufuatilia uhalifu na kufanikisha kuwatia mbaroni wahusika na vifaa vyao vya kazi.
 Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Arusha na washtakiwa wenzie wakiwasili mahakamani kupandishwa kizimbani Kwa makosa 11 ya utakatishaji fedha, uhujumu uchumi na mtandao wa genge la uhalifu sanjari na ujangili. Picha na Ahmed Mahmoud, Arusha



TAFITI NI MOYO WA TAALUMA KATIKA KULETA MAENDELEO NCHINI-PINDA

0
0

"Atembelea na kujifunza utekendaji wa kazi katika baadhi ya Ndaki na Shule Kuu"


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amesema tafiti ni duru inayotanua mawanda ya taarifa na kuchangia katika kuleta maendeleo nchini na kwenye jamii kwa ujumla. 

Amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Tano ya Tafiti akiwa mgeni rasmi wa wiki hiyo iliyoanza leo katika Chuo Kikuu Dar es Salaam tarehe 6 Mei,2019. 

"Wiki hii itachochea ushirikiano kati ya Chuo Kikuu na serikali na kusaidia kuhabarisha umma kuhusu tafiti zitakazo oneshwa na kuzisikia na jinsi zitakavyosaidia kuleta maendeleo katika jamii", alisema Pinda. 

Maendeleo ya jamii yanahusiana moja kwa moja na maendeleo ya tafiti kwani ukuaji jumuishi wa uchumi katika masuala ya maendeleo huenda sambamba na matumizi bora ya rasilimali, alisema. 

Pinda amepongeza uongozi wa chuo kikuu kwa jitihada ya maboresho katika upande wa elimu kwa kuchagua njia mbadala ya ufundishaji kwa vitendo, amekitaka chuo kutumia vema mfumo huo mpya wa ufundishaji ili kuondoa changamoto zilizopo pale wanafunzi wanapohitimu mafunzo yao kuweza kufikiria kujiajiri wenyewe. 

MAPEMA: Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof. William Anangisye alisema, tafiti hizi huleta maendeleo na ukuaji wa misingi muhimu sana inayochochea katika kuhamasisha uchumi wa viwanda, kwani tafiti nyingi zinatusaidia katika kuongeza thamani za shughuli chuo kikuu kwa ujumla kwakuwa tunazingatia mihimili mitatu ufundishaji, tafiti na elimu, alisema. 

Maonesho ya Wiki ya tafiti ya Chuo Kikuu Dar es Salaam yatafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Jumatatu tarehe 6 hadi Jumatano tarehe 8 Mei 2019 yenye kauli mbiu isemayo "Utafiti kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu" . 

Imetolewa na Afisha Habari na Uhusiano 

Imetolewa na Afisa Uhusiano 
Kitengo cha Huduma kwa Umma 
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam 











Waganga Wakuu wa Mikoa wapewa mwezi mmoja kutathmini utendaji wa Kamati za afya za Mikoa na Wilaya zao

0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na Kamati ya uendeshaji ya huduma za afya ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea jana
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuja kupata huduma za afya katika kituo cha afya cha Mjimwema kilichopo Manispaa ya Songea
baadhi ya wajumbe wa kamati ya uendeshaji ya huduma za afya wa mkoa wa ruvuma wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima jana mjini Songea.


Na Mathew Kwembe, songea 

Waganga wakuu wa Mikoa Tanzania Bara wamepewa mwezi mmoja kuhakikisha kuwa wanazifanyia tathmini ya kina Kamati za Uendeshaji Huduma za Afya za Mikoa na Wilaya zao kuona kama zinaendana na kasi ya mabadiliko yanayokusudiwa na Serikali ya Awamu ya Tano. 

Agizo hilo limetolewa jana mjini Songea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji Huduma za Afya ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na Wajumbe wa Kamati za Uendeshaji Huduma za Afya kutoka Halmashauri ya Namtumbo, Halmashauri ya Wilaya ya Songea pamoja na Manispaa ya Songea. 

Amesema anawapa siku 30 Waganga Wakuu wa Mikoa yote kuhakikisha kuwa wanafanya tathmini ya Wajumbe waliopo katika ofisi zao kama wanatosha kuendelea na nyadhifa zao za kusimamia jukumu la uendeshaji huduma za afya katika mikoa na halmashauri zao. 

Dkt Gwajima ameongeza kuwa endapo itabainika kuwa baadhi ya Wajumbe wa Kamati hizo hawana sifa zinazowafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao ya usimamizi na uendeshaji huduma za afya katika maeneo yao, Waganga Wakuu wa Mikoa watalazimika kuwaweka pembeni Wajumbe hao na kuunda upya Kamati ambazo zitaweza kuiendeleza agenda ya mabadiliko katika sekta ya afya. 

“Kinyume na hapo katika ziara hizi ninazoendelea kuzifanya mikoani nikikuta yupo Mganga Mkuu wa Mkoa ambaye ametulia tu, mapungufu katika vituo bado yapo na amewezeshwa na Serikali, ajue wazi kuwa wa kutokutosha wa kwanza atakuwa yeye,” amesema Dkt Gwajima na kuongeza: 

“Haiwezekani tukute mapungufu madogo kabisa katika vituo, ambayo yangeweza kuonwa na wao walioko huko eti hayaonekani hadi tuje sisi kutoka Tamisemi ndiyo mapungufu hao yafanyiwe kazi,”amesisitiza Dkt Gwajima. 

Naibu Katibu Mkuu huyo ameonya tabia iliyojengeka miongoni mwa Wajumbe wa Kamati za Uendeshaji Huduma ya Afya kukimbilia kuomba msamaha pindi zinaposhindwa kutekeleza majukumu yake kwa makusudi. 

Amesema huu ni wakati wa kuboresha sekta ya afya katika vituo vya afya na zahanati kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya utoaji huduma yanaboreshwa ili yaweze kuwavutia wananchi wengi kukimbilia kupata huduma katika zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na serikali ikiwemo hospitali za halmashauri. 

Dkt Gwajima amesema kuwa kamwe hatawapa nafasi Wajumbe wa Kamati za Uendeshaji Huduma za Afya wa Mikoa na Wilaya ambao siku zote wamekuwa ni watu wa visingizio vya kuomba kusamehewa ama kupewa muda kuwa wamefahamu mapungufu yao wakati mapungufu husika ni yale yale ambayo kila siku Serikali inatoa maelekezo kuwa yafanyiwe kazi. 

Amesema angependa kuona Kamati za Uendeshaji Huduma za Afya katika Mikoa na Halmashauri zikijikita katika kuongelea mambo ya ubora wa huduma kwa mteja “’quality care” na kuwa, mteja ni mfalme na si vinginevyo. Serikali imeshirikisha Wananchi na kutuwezesha miundombinu safi na dawa za kutosha, bajeti ya kufuatilia huduma inatolewa, semina za uongozi zinafanyika, maelekezo yanatolewa je, tatizo huwa linatokea wapi? 

“Hivi vitu vidogo vidogo vya kitaalamu tubebe sisi wenyewe, Wananchi wametuunga mkono, tumeweza kushirikiana nao kujenga zahanati na vituo vya afya katika mikoa na halmashauri zetu hivyo ni jukumu letu sasa kuhakikisha kuwa tunatoa huduma bora za afya kwa Wananchi na kuondoa hii tabia ya kuwepo kwa malalamiko yanayosababishwa na uzembe katika kufuatilia na kusimamia,” amesema. 

Kwa mujibu wa Dkt.Gwajima, katika ziara zake alizokwisha zifanya katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Njombe na Songea amejionea mapungufu mbalimbali ya utoaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya na zahanati ambayo yapo ndani ya uwezo wa Kamati za Usimamizi na Uendeshaji Huduma za Afya katika mikoa na halmashauri husika. 

Ameongeza kuwa mapungufu hayo ambayo ameyashuhudia kwenye vituo vya afya na zahanati zinazomilikiwa na umma yametokana na watoa huduma waliopo katika vituo hivyo kutopata usimamizi unaostahili kutoka kwa Kamati za Usimamizi na Uendeshaji wa Huduma za Afya za Mikoa na Halmashauri husika. 

Dkt Gwajima anaamini kuwa, kushindwa kwa Kamati za Uendeshaji na Usimamizi wa utoaji huduma za afya katika ngazi za mikoa na halmashauri kutekeleza majukumu yao, ndiko kulikopelekea kukithiri kwa uchafu katika majengo ya vituo vya afya na zahanati, kushindwa kufanyiwa matengenezo muhimu ya kuboresha mazingira ya zahanati na vituo hivyo licha ya vituo hivyo kuwa na fedha za uendeshaji wake. 

“Unakuta kituo kina fedha za kutosha kwenye akaunti lakini mapungufu madogo madogo ya kukera yamejaa,” ameeleza Naibu Katibu Mkuu. 

Amesema hali hiyo imesababishwa na kushindwa kwa Kamati za Uendeshaji Huduma za Afya za Mkoa (RHMT) na zile za Halmashauri (CHMT) kwa kutofanya kazi ya ufuatiliaji wa utoaji huduma bora na utaalam kwenye vituo vya afya nchini licha ya kuwezeshwa na Serikali. 

Sambamba na kuwataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuzitathmini Kamati hizo, Dkt Gwajima pia amewataka wajumbe wa Kamati hizo kutambua kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ipo na agenda moja tu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya na kuwagusa watumiaji wa huduma hizo kwa huduma zenye ubora unaostahili. 

“Hatutapimwa kwa idadi ya semina au uwepo wa kituo cha afya tu karibu na Wananchi bali kwa ubora huduma zinazotoleewa katika vituo hivi, vinginevyo Wananchi watakuwa karibu na vituo husika lakini hawavitumii,” amesema. 

Dkt Gwajima amebainisha mapungufu kadhaa aliyoyaona kwenye ziara yake kuwa ni pamoja na Kamati za Uendeshaji Huduma ya Afya kushindwa kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye vituo vyao vya afya na zahanati, kuwepo kwa malalamiko toka kwa wagonjwa, kukosekana kwa takwimu sahihi za utendaji kazi na Wajumbe wa Kamati za uendeshaji huduma za Afya kushindwa kuandika vizuri kumbukumbu za taarifa za kazi za ikiwemo mihutasari ya vikao na wengine kutokaa kabisa vikao muhimu. 

Akiwa katika kituo cha afya Mjimwema Manispaa ya Songea Naibu Katibu Mkuu Dkt.Gwajima alipokea kero za wagonjwa kuhusu uwepo wa kauli mbaya toka kwa baadhi ya watumishi wakiwemo wauguzi na matabibu, tatizo la ukosefu dawa na vifaa tiba muhimu hususan vya akina mama wajawazito. 

“Hapa Mjimwema nimebaini kasoro nyingi mojawapo kauli mbaya za watumishi na tatizo la dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa ” ameonya Dkt .Gwajima. 

Aidha, alimpongeza tabibu msaidizi mmoja aliyeibuliwa na mteja kwamba, anatamani watoa huduma wote wangekuwa kama tabibu huyo anayeitwa Lidya Mwakyusa Hii ni mara ya pili kwa wateja kuwataja hadharani watumishi watoa huduma wenye huduma inayojali mteja akiwemo Edward Mapunda wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Njombe. 

Dkt. Gwajima amewapongeza watoa huduma wanaotambua wajibu wao kuwa, mteja ni mfalme na amewataka kutovunjwa moyo na baadhi ya watumishi wasiozingatia maadili ya kazi na kuleta kero kwa wateja. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Jairy Khanga ameahidi kuchukua hatua za mapema kufanya mabadiliko ya utendaji kazi wa Kamati za Usimamizi wa Huduma za Afya katika Mkoa wa Ruvuma 

MERU KUONDOKANA NA TATIZO LA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

0
0
Na Woinde Shizza, Michuzi TV
Wananchi Wa Wilaya ya Arumeru wapo mbioni kuondokana na adha ya ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) baada ya kujengewa mochwari Mpya ya kisasa na serikali. 
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mkuu wawilaya hiyo mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Cosmas Kalasala alisemakuwa chumba hicho chakuhofadhia maiti mpaka kiishe kitagarimu kiasi cha shilingi milioni 160. 
 Alisema kuwa mpaka sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 80% na kwamba wanatarajia kukamilisha ujenzi huo hivi karibuni ili wananchi waweze kutumia jengo hilo waondokane na usumbufu wa kwenda kuhifadhi miili ya marehemu nje ya Wilaya. 
Mkuu wawilaya hiyo Jerry Muro alisema serikali ya awamu ya tano imeona tatizo hili la ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti hivyo wakaamua watoe fedha za mfuko wa jimbo na kijengea chumba hicho katika hospital ya wilaya ya Arumeru 
"Unajua fedha hizi za maendeleo ya mfuko wa jimbo ni za maendeleo ya wananchi wa Meru hivyo tumefata utaratibu wa kushirikisha wananchi tukachukua fedha hizi kwa ajili ya kuwajengea wananchi wa Meru chumba cha kuhifadhia miili  ya marehemu ndugu zao"alisema Muro. 
 Alisema kuwa wananchi hao walikuwa wanapata taabu sana pindi ndugu zao wanapofariki kwani hospital ya wilaya ilikuwa haina huduma hiyo hivyo walikuwa wanalazimika kwenda kuhifadhi miili ya marehemu ndugu zao katika hospital ya mkoa ya Arusha (Mount meru hospital ) ambapo ni zaidi ya kilometa 20 kutoka hospital hiyo  ya Wilaya. 
DC  Muro alisema jengo hilo linalojengwa ni kubwa na litakuwa na uwezo kuhifadhi miili 45 hadi 50 ya marehemu kwa wakati mmoja na kwamba  wanatarajia kulizindua rasmi na Mwenge wa Uhuru mapema Mwezi Juni mwaka huu.


 Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kalasala akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru jinsi chumba hicho cha kuhifadhia maiti kilivyofikia 
 Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kalasala akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru jinsi chumba hicho cha kuhifadhia maiti kilivyofikia 
 Mkurugenzi wa Jalmashauri ya Meru akifafanua jambo katika ziara hiyo ya mkuu wa wilaya ya kukagua ujenzi wa mochwari hiyo ulipofikia

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema jengo hilo la kuhifadhia maiti litasadia sana wananchi wa wilaya yake kwani walikuwa wanapata taabu sana ya kusafirisha miili pindi ndugu zao wanapofariki dunia.

MERU KUONDOKANA NA TATIZO LA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

0
0

Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Wananchi Wa Wilaya ya Arumeru wapo mbioni kuondokana na adha ya ukosefu wa chumba chakuhifadhia maiti (mochwari) baada ya kujengewa mochwari Mpya ya kisasa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mkuu wawilaya hiyo mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Cosmas Kalasala alisemakuwa chumba hicho chakuhofadhia maiti mpaka kiishe kitagarimu kiasi cha shilingi milioni 160.

Alisema kuwa mpaka sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 80%na wanatarajia kukamilisha ujenzi huo hivi karibuni ili wananchi waweze kutumia jengo hilo waondokane na usumbufu wa kwenda kuhifadhi miili ya marehemu nje ya Wilaya.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro alisema serikali ya awamu ya tano imeona tatizo hilo la ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti, hivyo wakaamua watoe fedha za mfuko wa jimbo na kijengea chumba hichi katika hospital ya wilaya ya Arumeru

"unajua fedha hizi za maendeleo ya mfuko wa jimbo ni zamaendeleo ya
wananchi wa meru hivyo tumefata utaratibu wa kushirikisha wananchi
tukachukua fedha hizi kwaajili ya kuwajengea wananchi wa meru chumba cha kuhifadhia mihili ya marehemu ndugu zao"alisema Muro.

Alisema kuwa wananchi hao walikuwa wanapata tabu sana pindi ndugu zao
wanapofariki kwani hospital ya wilaya ilikuwa haina huduma hiyo kwakipindi kirefu hivyo walikuwa wanalazimika kwenda kuhofadhi miili ya marehemu ndugu zao katika hospital ya mkoa ya Arusha(mounti meru hospital ) ambapo ni zaidi ya kilometa 20kutoka hospital ya Wilaya.

Muro alisema jengo hilo linalojengwa nikubwa nalinaeza kuhifadhi miili 45
hadi 50 ya marehemu nawanatarajia kulizindua rasmi na mwenge wa uhuru
mapema Mwezi June.
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru Cosmas Kalasala akimuonyesha Mkuu wa wilaya ya Arumeru jinsi chumba hicho cha kuhifadhia maiti kilivyofikia .
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema jengo hilo la kuhifadhia maiti litasadia sana wananchi wa wilaya yake, kwani walikuwa wanapata tabu sana ya kusafirisha miilii pindi ndugu zao wanapofariki dunia

MAKAMU WA RAIS AZINDUA RIPOTI YA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia  ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira mara baada ya kuizindua  katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (kushoto) mara baada ya kuzindua  ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hotel ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Ifikapo Juni 30, mitaa yote ya majiji iwe imesambaziwa umeme aamuru Waziri wa Nishati Dkt Kalemani

0
0
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akionyesha nyumba bado hazijaunganishiwa umeme katika eneo la Ntyuka jijini Dodoma wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo ya mijini ambayo hayana umeme. Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikagua maeneo ambayo hayajaunganishwa na umeme katika eneo la Mkonze jijini Dodoma.Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikagua maeneo ambayo hayajaunganishwa na umeme katika eneo la Mkonze jijini Dodoma.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka  (kulia) na Mhandisi Ahmed Chinemba kutoka Wizara ya Nishati (kushoto).
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maeneo ya mijini ambayo hayana umeme. Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2019, mitaa yote isiyo na umeme katika Majiji yote nchini iwe imesambaziwa umeme.

Dkt Kalemani aliyasema hayo tarehe 5 Mei, 2019, mara baada ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma ambayo bado yana nyumba nyingi ambazo hazijaunganishwa na umeme.

Katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka, Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.

" Mwisho wa kuunganisha umeme kwenye maeneo haya ya Majiji ni Juni 30 mwaka huu, iwe Ntyuka, Mkonze, jijini Dodoma, au Murieti jijini Arusha, haya maeneo yana kero ya umeme lazima yapatiwe nishati hii haraka ili yafanane na hadhi ya Majiji hivyo jukumu la mwananchi ni kufanya wiring na kulipia huduma ya umeme." alisema Dkt Kalemani.

Dkt. Kalemani alisema kuwa kazi ya uuganishaji umeme katika mitaa isiyo na umeme katika mikoa mingine ambayo si majiji itaendelea hadi mwezi Desemba mwaka huu.

Aidha, Waziri wa Nishati aliwataka Wataalam kutoka TANESCO kutokataa malipo ya wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme bali wanapaswa kupokea malipo hayo na kuwasambazia umeme wateja.

Kabla ya kufanya ziara hiyo, Waziri wa Nishati, alifanya kikao na watendaji wa TANESCO ambapo pamoja na kuwapongeza kwa jitihada mbalimbali wanazofanya katika kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na umeme wa kutosha na uhakika, aliwata kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za umeme zinazoendelea kujitokeza.

Dkt. Kalemani alisema kuwa moja ya changamoto wanayopaswa kushughulikia ni kuunganishia umeme wateja waliolipia huduma ya umeme na hawajaunganishwa kwa muda mrefu ambapo aliagiza kuwa mwisho wa kuwaunganishia umeme wateja hao ni mwezi wa Tano mwaka huu.

Aidha aliiagiza TANESCO kuhakikisha kuwa, ifikapo mwisho wa mwezi wa Tano mwaka huu, maeneo yaliyounganishwa na umeme wa gridi yanapata umeme wa kutosha na wa uhakika ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli mbalimbali bila kikwazo cha uwepo wa nishati ya kutosha.

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII MHE.KANYASU APIGA MARUFUKU UKAMATAJI MCHANGA PORI LA AKIBA LA RUNGWA

0
0



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amepiga marufuku ukamataji wa  vifurushi vya mchanga unaodaiwa kuwa na madini ya dhahabu unaochimbwa na wachimbaji wadogo wadogo ndani ya Pori la Akiba la Rungwa wilayani Manyoni, mkoani Singida kinyume cha sheria na kuuagiza Uongozi wa Pori hilo kuhakikisha unaimarisha   ulinzi  katika maeneo yote yanayodaiwa kuwa na madini ndani ya pori hilo ili kuzuia Wachimbaji  kuingia na kuendesha shughuli ya uchimbaji wa mchanga kinyume cha sheria.

Marufuku hiyo imekuja kufuatia taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Maafisa Wanyamapori  ambao wamekuwa wakiwaruhusu Wachimbaji hao kuingia ndani ya Pori hilo nyakati za usiku  kwa ajili ya  kuchimba mchanga unaodaiwa kuwa una madini kwa makubaliano yaliyo nje ya utaratibu.

Akizungumza  na Watumishi wa geti la Doroto katika Pori hilo wilayani Manyoni mkoani Singida, Mhe.Kanyasu amesema kuwa tuhuma hizo za rushwa zitaisha tu pale watakapoimarisha ulinzi katika eneo hilo na sio kukamata vifurushi vya mchanga kwenye geti hilo.

 Ameuagiza Uongozi huo kuhakikisha  unakamata vifurushi wanavyohisi ndani yake kuna madini  na lazima Afisa Madini awepo ili kuhakikisha anataja thamani ya madini  pamoja na taratibu zinazotakiwa kufuatwa  ili kukidhi matakwa ya sheria ya utaifishaji wa mali iliyokamatwa.

 Baadhi ya Wachimbaji wadogo walionyang'anywa mchanga wao wamedai kwamba Maafisa hao wamekuwa wakikagua magari kwenye geti la kutokea la Doroto na pale wanapokamata vifurushi hivyo bila kujua mchanga huo una madini kiasi gani wamekuwa wakimruhusu mtuhumiwa aende zake bila kumueleza taratibu zozote zile jambo ambalo ni kinyume na sheria. 

Amesema kitendo hicho ni unyang'anyi na uonevu wa hali ya juu na ni kinyume cha sheria kwa sababu sheria ya utaifishaji wa mali iliyokamatwa inampa nafasi mtuhumiwa kujua thamani ya mali aliyokamatwa nayo  na ndipo taratibu za kesi kwenda mahakamani hufuata.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewaonya Maafisa Wanyamapori katika pori hilo kuacha tabia ya kuwaonesha wachimbaji hao mahali wanapohisi  kuwa kuna madini kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Amesema ni ngumu kwa Mwananchi yeyote kujua sehemu ambako kuna madini ndani ya Pori bila kudokezwa na wenyeji ambao ni Wahifadhi wa Pori hilo

Amesisitiza kuwa endapo uchimbaji huo wa madini ndani ya Hifadhi utaendelea kufanyika itakuwa ni ushahidi tosha kuwa Meneja wa Pori hilo kashindwa kazi.

Aidha, Mhe.Kanyasu amewataka kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Pori hilo ili kukomesha ujangili wanyamapori pamoja na ukataji miti ndani ya Pori hilo.

Kwa upande wake, Meneja wa Pori la Akiba la Rungwa, Patrick Kutondolana amekiri kuwa wamekuwa wakikamata mchanga huo kwa mashirikiano kati ya Kamati ya Ulinzi wa Wilaya hiyo ili kukomesha tabia hiyo ya uchimbaji mchanga ndani ya Hifadhi.

Amesisitiza kuwa si kweli kuwa wamekuwa na ushirikiano na Wachimbaji hao kwa makubaliano ya kupata rushwa ni kwamba hiyo imekuwa njama ya kutaka kuwachafua kwa lengo la kuwakatisha nia.




 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Pori la Akiba la Rungwa  lililopo katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida mara kuhusu ukamatajii wa vifurushi vya mchanga unaodaiwa kuwa una madini ya dhahabu baadala ya kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo ndani ya Pori hilo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Pori hilo,Patrick Kutondolana  
 Baadhi ya watumishi wa Pori la Akiba la Rungwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kuhusu ukamataji wa mchanga unaodaiwa kuwa na madini ya dhahabu wakati alipofanya ziara katika geti la Doroto katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida

RAMADHAN KAREEM WADAU WOTE WA GLOBU YA JAMII POPOTE MLIPO

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA KUAGA MWILI WA DK.MENGI VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk. John Magufuli amewasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga na kutoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Dk.Reginald Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 akiwa Dubai.

Dk. Magufuli amefika katika viwanja hivyo saa 4:30 asubuhi ambapo baada ya kufika waombolezaji wengine waliokuwa msibani hapo walisimama ambapo alikwenda moja kwa moja hadi lilipo jeneza lenye mwili wa Dk.Mengi. Baada ya hapo Rais alikwenda kukaa na kisha kuanza kusikiliza viongozi wa dini ambao walikuwa wakiendelea kutoa mahubiri kuhusu kifo cha Mengi na mchango wake kwa Watanzania.

Mbali ya Rais Magufuli , pia viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria kuaga mwili wa Dk.Mengi. Pia marais wastaafu nao wamehudhuria pamoja na kada nyingine za makundi mbalimbali ya Watanzania,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, pamoja na Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma wakiwa katika ukumbi wa Karimjee, kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi.

Hata hivyo wakati Rais anafika viwanja vya Karimjee, Askofu wa CCT Nelson Kisare alikuwa akiendelea kutoa mahubiri kabla ya kufanya maombi kwa ajili ya mzee Mengi.Wakati anahubiri Askofu Kisare amesema kuwa Dk.Mengi amekuwa mmoja wa Watanzania wachache ambao wametumia fursa zilizopo khakikisha anatatatua changamoto.

Amesema Dk. Mengi enzi za uhai wake amefanya mambo mengi makubwa na ya mfano wa kuigwa na kutaka jamii ya Watanzania kuiga matendo mema ya mpendwa wetu."Dk.Mengi kupitia biashara zake amekuwa akilipa kodi na kodi hiyo imeleta maendeleo kwa Watanzania, mzunguko wa fedha zake umekwenda kwa watanzania,na wapo ambao wamepata ajira kupitia biashara zake.Hivyo ametoa mchango mkubwa na amegusa maisha ya wananchi mbalimbali.

Askofu Kisare amesisitiza yale ambayo yana sifa njema na matendo mema ambayo amefanya Dk.Mengi maisha yake ya hapa duniani ni vema kila mmoja wetu akatafakari.

Wakati huo huo Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Father Kitima kabla ya kutoa maombi kwenye shughuli za kuaga mwili wa Dk.Mengi, amesema kuwa Dk.Mengi alikuwa karibu sana na Kanisa Katoliki kwa kushiriki katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo zinahosu Kanisa hilo ."Kanisa Katoliki Tanzania limeguswa na msiba wa Dk.Mengi.Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Arusha aliyefanya kazi kwa karibu na Mzee Mengi amesema rafiki yake amemuacha lakini ameacha alama kutokana na mchango wake.
Mjane wa Marehemu Dkt. Mengi, Jacqueline Mengi akiwa pamoja na watoto wa Marehemu.

"Imani ya Dk.Mengi , sisi tunaamini maisha ya mwanadamu , ni maisha yaliyoungwanishwa na maisha ya muumba wake. Katika Injili ya Yohana sura ya 11 tunaelezwa jinsi Yesu anavyoeleza kifo hakina ushindi kwa mwanadamu. Tunapofurahia kazi nzuri za Dk. Mengi katika kuwafanya watanzania wakutane kupitia vyombo vya habari na kuhimiza kufanya mambo mema , ni jukumu letu kuenzi na kuendeleza mema ambayo ameyatenda,"amesema.

Pia Futher Kitima amesema  binadamu hapa duniani anakabiliana na nguvu za uovu na anapambana nazo na hivyo wanahitaji msaada wa Mungu. Dk.Mengi ametenda mengi lakini bado tunayo kila sababu ya kuzidi kumuombea na kubwa zaidi kuungana na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

WAZIRI KABUDI NA SALAM ZA SERIKALI KUFUATIA KIFO CHA DKT. MENGI, AZUNGUMZIA MCHANGO WAKE KWA WATANZANIA

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akitoa salamu za Serikali wakati wa kuaga mwili wa Dk. Mengi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imesema imesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha aliyekuwa mfayabishara maarufu nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Reginald Mengi aliyefariki dunia Mei 2, 2019 akiwa Dubai .

Akitoa salamu za Serikali leo Mei 7, 2019 wakati wa kuaga mwili wa Dk. Mengi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema  kwa niaba ya Rais, Serikali na watanzania wote wanatoa pole nyingi kwa familia ya Dk. Mengi, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na kifo cha Dk.Mengi.

"Serikali tunatoa pole nyingi kwa mke na watoto wa marehemu Dk.Mengi na tunamuomba Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu kwenu na kwa watanzania.Pia tunatoa pole kwa wafanyakazi wote wa kampuni ya IPP kwa kuondokewa na mpendwa wao na mpendwa wetu.Tunatambua upendo wa dhati ambao Dk.Mengi amekuwa nao kwa watumishi wake.Kifo chake ni pigo kubwa kwao.

"Kama ilivyo kwa familia, serikali nayo imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Dk.Mengi.Kifo chake kimekuwa cha ghafla sana kwani aliondoka nchini akiwa mzima na alipofika Dubai amefariki.Baada ya taarifa za kifo hicho, Serikali kupitia Ubalozi wetu uliopo katika nchi za Falmeza Kiarabu ulianza mchakato wa kuhakikisha mwili unarudishwa nyumbani na unafika salama na leo hii uko mbele yetu.

"Ubalozi wetu ulifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha taratibu zote za kuusafirisha mwili zinapatikana na Serikali ilihakikisha mwili unafika kwa wakati. Balozi wa Tanzania katika nchi za Falme za Kiarab Mbarouk Nassoro Mbarouk amefanya kazi kubwa kuhakikisha mwili unarudishwa kwa wakati.Hata hivyo pamoja na majonzi tuliyonayo tunajua kifo ni fumbo kama ambavyo viongozi wote wa dini wamesema , na mwenye kujua fumbo hilo ni Mungu, hivyo tunamuachia yeye,"amesema Profesa Kabudi.

Pia amesema Serikali imeguswa sana na msiba wa Dk.Mengi kwani amekuwa msaada mkubwa katika kujenga uchumi wa nchi yetu na kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania na kwamba uzalendo wake kwa nchi yake uliweza kuvuta wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini.

"Dk.Mengi enzi za uhai wake mara kadhaa ameshauri namna bora ya kujenga uchumi na wazawa kupewa nafasi na kubwa zaidi alikuwa na majawabu ya nini kifanyike. katika Serikali ya Awamu ya tano, Dk.Mengi alikuwa mwenye maono ya kutekeleza kauli mbiu ya Serikali ya viwanda ambapo alikuwa na mkakati wa kuanzisha kiwanda cha magari na ukweli ni kwamba mchango wake kufanikisha Serikali ya viwanda ni mkubwa.

"Serikali inatambua mchango wa Dk.Mengi katika kusaidia wanyonge, watu wenye kipato cha chini, walemavu na watu wenye ulemavu na utaratibu wake wa kukutana na watu wenye ulemavu inadhihirisha upendo wake kwa kada za watu mbalimbali. Tunatambua mchango wa Dk.mengi katika mazingira kwani amekuwa mchago mkubwa katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa na alianzisha kampeni ya kupanda miti katika mlima kilimanjaro,"amesema.

Waziri Kabudi wakati anaendelea kutoa salamu za Serikali, amesema Rais Dk.John Magufuli alizindua kitabu cha Dk.Mengi mwaka jana na kwamba kitabu hicho ni hazina kwani kinafundisha mambo ambayo ameyafanya Dk.Mengi na kupitia kitabu hicho iwe sehemu ya kuwa somo la kusaidia watanzania wengi.

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MWILI WA DKT REGINALD MENGI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja  na viongozi wengine wakiwa wamejiunga na waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Jukwaa la fawakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019
 Maafisa waandamizi wa IPP Limited na waombolezaji wengine

 Mahubiri
 Mahubiri
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja  na viongozi wengine wakiwa wamejiunga na waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja  na viongozi wengine wakiwa wamejiunga na waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019








 Viongozi mbalimbali na waombolezaji
 Viongozi mbalimbali na waombolezaji




 Viongozi mbalimbali na waombolezaji

 Balozi Juma Mapachu akisoma wasifu wa marehemu wakati wa kuuaga mwikli wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019




 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea machache wakati wa kuuaga mwikli wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja  na viongozi wengine wakiwa wamejiunga na waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Waombolezaji wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Waombolezaji wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Waombolezaji wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi akitoa salamu za serikali wakati wa kuuaga mwikli wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019


 Jukwaa la fawakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019
Mkurugenzi wa Radio One Deo Rweyunga ndiye aliyekuwa MC
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwili kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwili kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwili kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa karibu wa marehemu wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa mtoto wa Marehemu Bw. Abdiel Mengi wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa shemeji wa marehemu Bi. Shimimana Ntuyabaliwe wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa mjane wa marehemu Bi. Jacquiline Mengi wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa watoto mapacha wa marehemu wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa binti wa marehemu Bi. Regina Mengi wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa watoto mapacha wa marehemu wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa Mama Rose Mwapachu wakati akiaga baada ya kuongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019













RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA KUAGA MWILI WA DK.MENGI VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amewasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga na kutoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Dk.Reginald Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 akiwa Dubai.

Dk.Magufuli amefiwa katika viwanja hivyo saa 4:30 asubuhi ambapo baada ya kufika waombolezaji wengine waliokuwa msibani hapo walisimama ambapo moja kwa moja hadi lilipo jeneza lenye mwili wa Dk.Mengi.Baada ya hapo Rais alikwenda kukaa na kisha kuanza kusikiliza viongozi wa dini ambao walikuwa wakiendelea kutoa mahubiri kuhusu kifo cha Mengi na mchango wake kwa Watanzania.

Mbali ya Rais Magufuli , pia viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria kuaga mwili wa Dk.Mengi.Pia marais wastaafu nao wamehudhuria pamoja na kada nyingine za makundi mbalimbali ya Watanzania,

Hata hivyo wakati Rais anafika viwanja vya Karimjee, Askofu wa CCT Nelson Kisare alikuwa akiendelea kutoa mahubiri kabla ya kufanya maombi kwa ajili ya mzee Mengi.Wakati anahubiri Askofu Kisare amesema kuwa Dk.Mengi amekuwa mmoja wa Watanzania wachache ambao wametumia fursa zilizopo khakikisha anatatatua changamoto.

Amesema Dk.Mengi enzi za uhai wake amefanya mambo mengi makubwa na ya mfano wa kuigwa na kutaka jamii ya Watanzania kuiga matendo mema ya mpendwa wetu."Dk.Mengi kupitia biashara zake amekuwa akilipa kodi na kodi hiyo imeleta maendeleo kwa Watanzania, mzunguko wa fedha zake umekwenda kwa watanzania,na wapo ambao wamepata ajira kupitia biashara zake.Hivyo ametoa mchango mkubwa na amegusa maisha ya wananchi mbalimbali.

Askofu Kisare amesisitiza yale ambayo yana sifa njema na matendo mema ambayo amefanya Dk.Mengi maisha yake ya hapa duniani ni vema kila mmoja wetu akatafakari.

Wakati huo huo Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Futher Kitima kabla ya kutoa maombi kwenye shughuli za kuaga mwili wa Dk.Mengi, amesema kuwa Dk.Mengi alikuwa karibu sana na Kanisa Katoliki kwa kushiriki katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo zinahosu Kanisa hilo ."Kanisa Katoliki Tanzania limeguswa na msiba wa Dk.Mengi.Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Arusha aliyefanya kazi kwa karibu na Mzee Mengi amesema rafiki yake amemuacha lakini ameacha alama kutokana na mchango wake.

"Imani ya Dk.Mengi , sisi tunaamini maisha ya mwanadamu , ni maisha yaliyoungwanishwa na maisha ya muumba wake. Katika Injili ya Yohana sura ya 11 tunaelezwa jinsi Yesu anavyoeleza kifo hakina ushindi kwa mwanadamu. Tunapofurahia kazi nzuri za Dk. Mengi katika kuwafanya watanzania wakutane kupitia vyombo vya habari na kuhimiza kufanya mambo mema , ni jukumu letu kuenzi na kuendeleza mema ambayo ameyatenda,"amesema.

Pia Futher Kitima amesema binadamu hapa duniani anakabiliana na nguvu za uovu na anapambana nazo na hivyo wanahitaji msaada wa Mungu. Dk.Mengi ametenda mengi lakini bado tunayo kila sababu ya kuzidi kumuombea na kubwa zaidi kuungana na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa watoto mapacha wa marehemu wakati alipoongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited marehemu Dkt. Reginald Abraham Mengi kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Jumanne Mei 7, 2019.

MKAZI WA MOROGO AKABIDHIWA KITITA CHAKE CHA SH MILIONI 5 KUTOKA BIKO

YOULOU MABIALA ALIOA BINTI WA FRANCO MAKIADI

0
0
Wapenzi wa muziki wa ‘soukous’ uliokuwa ukitawaliwa na wanamuziki toka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kongo Brazzaville, majina ya Youlou Mabiala hayawezi kuwa mageni kwao.

Mabiala ni mwanamuziki aliye na vipaji vya kutunga na kuimba, aliyepiga muziki kati ya miaka ya 1960 hadi 2008.

Majina yake halisi ni Gilbert Youlou Mabiala, alizaliwa Machi 03, 1947 katika kitongoji cha Linzolo, jirani na Brazzaville, ambao ndio mji mkuu wa nchi ya Jamhuri ya Kongo.

Msomaji wa makala hii, nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Jamhuri ya Kongo ni nchi mbili tofauti. Sehemu kubwa nchi hizo zimetengenishwa na mto Kongo.

Anajulikana sana kwa jina bandia ‘Prince Youlou’, alianza muziki kwenye bendi za mitaani katika jiji la Brazzaville, nchini Jamhuri ya Kongo.

Youlou mwaka 1963, alijiunga katika bendi ya T.P.OK Jazz, katika jiji la Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akiwa kama mtunzi na mwimbaji. Bendi ya T.P.OK. Jazz, ilikuwa ikiongoza katika muziki wa Wakongo kwenye miaka ya 1960 hadi ya 1980.

Baadhi ya nyimbo alizotunga au kushiriki kuimba akiwa katika bendi ya T.P.OK. Jazz ni Télé Zaire ya mwaka 1975, Siddikh, Aboubacar za mwaka 2008 , "Asumani” , Ngaira na Amos.

Mwaka 1972, Youlou alikuwa mmoja kati ya wanamziki walioondoka katika bendi ya T.P.OK. Jazz, wakaenda kuunda bendi iliyoitwa Lovy du Zaïre, iliyoongozwa na Vicky Longomba.

Kwa taarifa yako mpenzi msomaji wa makala haya, Vicky Longomba ndiye aliyekuwa baba wa wanamuziki mashuhuri Awillo na Lovy Longomba.
Katika harakati za kutafuta maisha, Youlou baadaye aliiacha bendi hiyo, akaenda kuunda bendi ya Orchestra Somo Somo.

Aliwakusanya wanamuziki wengine akina Jean Kwamy Munsi, Diatho Lukoki, Master Mwana Congo na Nona Simon.

Kama wasemavyo Waswahili kuwa “ Ngoma ya watoto haikeshi” Mabiala mwaka 1975, aliamua kuondoka katika bendi aliyoianzisha na kurudi kwa gwiji la muziki Franco Luambo Makiadi aliyekuwa kiongozi wa bendi ya T.P.OK. Jazz.

Katika bendi hiyo aliachia kibao ‘matata’ sana cha ‘Kamikaze’ ambacho kilikuja kuwa maarufu sehemu nyingi Afrika na kwa baadhi ya Waafrika waishio nchi za Ulaya na Marekani ya Kaskazini.

Mabiala aliimba nyimbo nyingine za Ledi, Massi na Lekwey alioutunga akiwa pamoja na Franco Makiadi.Baada ya kuchota ‘maujuzi’ zaidi toka katika bendi ya T.P.OK. Jazz, mwaka 1977, Youlou aliondoka katika bendi hiyo jumla.

Akaenda kuunda bendi iliyopewa jina la Trois Frères akiwa na wanamuziki akina Loko Massengo, Mose Fan Fan, Michel Boyibanda na wengine wengi, wakipiga muziki hususani katika jiji la Brazzaville.

Watanzania watalikumbuka jina la Mose Fan Fan, aliyewahi kuishi humu nchini akipiga gitaa la solo katika bendi za Orchestra Makassy na Orchestra Matimila.Mnamo miaka ya 1980, Youlou aliimba katika bendi ya Kamikaze Loningisa, ambako alitunga na kuimba wimbo wa Djeliba na zingine.

Akitoa burudani za muziki katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa nchi ya Kongo Brazzaville Agosti 15 2004, zilizofanyika hoteli ya Présidence de la République huko Pointe Noire, Youlou Mabiala alipatwa na ugonjwa kiharusi.Baada ya kupatiwa kuhuduma na kupata nafuu, katika hospitali ya jijini Brazzaville, alisafirishwa kwa ndege kupelekwa Paris, nchini Ufaransa kwa matibabu zaidi.

Hata baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, alibakia katika nchini Ufaransa kwa ajili ya kujiimarisha kiafya.Youlou Mabiala baba wa familia aliye na mke. Mke huyo ni mmoja kati ya mabinti wa aliyekuwa ‘bosi’ wake Franco Luambo Makiadi.

BENDI YA MSONDO NGOMA ILIKOTOKEA

0
0
Zilikuwepo bendi nyingi humu nchini zilizokuwa zikitoa burudani katika sherehe mbalimbali hata kabla ya kupata Uhuru wa Tanganyika.

Mara baada ya kupatikana kwa Uhuru, kuliundwa bendi iliyopewa jina la NUTA Jazz ambayo ni kongwe miongoni mwa bendi zilizokuwepo hapa nchini.

Mwaka huu ni takribani miaka 55 tangu ianzishwe mwaka 1964 katika jiji la Dar es Salaam, ikiwa chini ya ummiliki wa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania (National Union of Tanzania) kwa kifupi NUTA.

Mwaka huohuo wa 1964 Muhidini Gurumo aliitwa kujiunga na bendi hiyo ya hiyo akitokea katika bendi ya Rufiji Jazz, na kuwa mmoja wa waasisi wa bendi.Gurumo aliungana na wanamuziki wengine akina Hamis Sama, Mnenge Ramadhani, Wilfred, Boniface na wengine.

Muhidin Maalim Gurumo nyimbo zake za kwanza kurekodi akiwa na NUTA Jazz zilikuwa Baba Nyerere, uliokuwa ukimsifia Mwalimu Nyerere kwa kuleta Uhuru wa Tanganyika. Nyingine zilikuwa Kilimo ni kazi yetu na Mwengele.

Mwaka 1966 mwanamuziki mwingine mahiri John Simon alijiunga na bendi hiyo ya NUTA Jazz.Mpiga gitaa la solo Amed Omar ndiye aliyechaguliwa kuwa kiongozi wa bendi.

Jumuiya hiyo ilipobadili majina kuwa ‘Organization of Tanzania Trade Unions’ kwa kifupi OTTU, bendi nayo ikawa OTTU Jazz.Baada ya kipindi kingine kupita Jumuiya hiyo ikabadili majina kuwa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania, kwa kifupi JUWATA.

Wakati wa uhai wake marehemu Gurumo aliwahi kusema kuwa mpiga solo Ahmed Omar kuwa ndiye aliyechaguliwa kuwa kiongozi wa NUTA Jazz wakati huo.Mzee Gurumo ambaye ndiye aliyekuwa muasisi wa mtindo wa Msondo, ukiwa ni wa asili ya kabila la Kizaramo, aliweza kutamba katika nyimbo.

Baadhi ya nyimbo zilizorekodiwa wakati huo, Mpenzi Sofia, Tumeishi toka zamani, na Walinicheka. Zingine zilikuwa Aziza, Tukiwa na Monica shuleni, Sakina, Maneno ya Nyerere, Mipacha Ngui na nyingine nyingi.

Wakati huo huo mpiga gitaa la solo Saidi Mabera alichaguliwa kuwa kiongozi wa bendi hiyo.Baadhi ya wanamuziki waliounda Juwata Jazz ni pamoja waimbaji Muhidini Gurumo, wengine ni Hassan Rehani Bichuka, na mpiga kinanda Waziri Alli ambaye hivi sasa ni mmoja kati ya viongozi wa bendi ya The Kilimanjaro Band (Wana Njenje).

Waziri kabla ya kujiunga katika bendi hiyo, alikuwa katika bendi ya taarabu ya Lucky Star ya mjini Tanga. Alifika katika jiji la Dar es Salaam akiwa na nia ya kwenda nchini Marekani kujifunza muziki. Juhudi zake hazikufanikiwa akapelekwa na nduguze kwenda kujiunga katika bendi hiyo. Alipotuwa alikabidhiwa kupiga Kinanda.

Miaka hiyo ya 1980 hadi 1990, takribani kila bendi ilikuwa na wapiga vinanda. Ikumbukwe katika bendi ya Maquis du Zaire, alikuwa akibofya Mbuya Makonga ‘Adios’, alikuwepo mwanamama pekee Asia Darwesh aliyekuwa akikipapasa kinanda hususani katika bendi ya MK Group, iliyokuwa ikiga muziki wake katika ukumbi wa Bandari Grill, kwenye hotel ya New Africa, ya jijini Dar es Salaam.

Vijana Jazz walikuwa na Hassan Shaw, ambaye hivi sasa yupo Ughaibuni akipiga muziki katika kumbi mbalimbali za Kitalii. Bima Lee Orchestra walikuwa na Kassimu Magati wakati Abdul Salvador ‘Father Kidevu’ alikuwa akipata ‘ulaji’ ala hiyo.

Ushindani kati ya bendi za muziki wa dansi ulipoongezeka, wanamuziki mwaka 1978 wanamuziki Muhidini Gurumo na Hassan Reheni Bichuka walihamia bendi ya Mlimani Park Orchestra.Gurumo alipofika katika bendi hiyo akawa kiongozi wa bendi sanjari na kuasisi mtindo wa ‘Sikinde ngoma ya ukae’.Mtindo huo ambao aliwahi kuelezea ni wa asili ya ngoma za kabila lake la Kizaramo.

Baada ya muda mfupi Hassani Bichuka naye aliindoka bendi hiyo Juwata kwenda kuungana na Gurumo katika bendi ya Mlimani Park Orchestra.
Baada ya Bichuka kupondoka, uongozi ukamchukuwa mwimbaji aliyekuwa akishabihiana naye kwa sauti, Shaban Dede ‘Kamchape’ alikitokea katika bendi ya Dodoma International ya mjini Dodoma wakati huo, sasa ni jiji.

Gurumo alirejea tena katika bendi yake ya Juwata mwaka 1991, akapewa wadhifa wa kuwa kiongozi wa bendi hiyo, baada ya kupiga muziki katika bendi hiyo ya Mliamani Park Orchestra pamoja na Orchestra Safari Sound (OSS) kwa nyakati tofauti.

Nyimbo walizotoka nazo zilikuwa za Nidhamu ya kazi, Ete, Queen Kasse, Mariamu ninakujibu, Usia wa baba, Msafiri kafiri, Tupa tupa, Ndugu Kassimu na nyingine lukuki.

Baadaye bendi hiyo ilibadilishwa jina na kuwa OTTU Jazz kufuatia kubadilika kwa jina la Chama cha Wafanyakazi kuwa OTTU. Hakuna ubishi kwamba bendi ya OTTU Jazz au kwa jina lingine wakajiita ‘Baba ya Muziki’, ilitikisa jiji la Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla wakipigia kwa mtindo wa wa ‘Msondo Ngoma, magoma Kitakita’ au ‘Mambo hadharani’.

Wakati huo ilikuwa katikati ya wimbo wapenzi na mashabiki wa Msondo walikuwa wakiimbishwa kibwagizo cha “Msondo yee Msondo Waa…” wapenzi na walikuwa wakiitikia “Afyaaaa”.Bendi hiyo ilikuwa ikipiga muziki wake katika ukumbi wa Amana uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, ikipakana na hospitali ya Amana.

Katika kipindi hicho bendi hiyo ilikuwa imesheheni wengi wenye vipaji vinavyotofautiana.Wanamuziki hao walikuwa akina Joseph Lusungu, Mnenge Ramadhani, Muhiddin Maalim, Hassan Rehani Bitchuka, Saidi Mabera na TX Moshi William. Wengine ni pamoja na

Nicko Zengekala, Selemani Mbwembwe, Joseph Maina, Mustapha John Ngosha, Suleimani Mwanyiro ‘Computer’, Tino Maselenge (Masinge) ‘Arawa’ na Athuman Momba.


Abdull Ridhiwan Pangamawe, Roman Mng’ande ‘Romario’

Wengine ni Salehe Bangwe ‘mwana Kigoma’, na bila kuwasahau Huruka Uvuruge na mzee mzima Said Mabera mpiga solo mahiri ambaye tangia ajiunge katika bendi hiyo hajathubutu kuiondoka.

Kufuatia Hospitali ya Ilala kupanuka, OTTU Jazz walitakiwa kuondoka kwa kile kilichodaiwa ni kuwabughudhi wagonjwa kwa makelele ya vyombo vya muziki wao.Hivyo walilazimika kuhamia katika ukumbi wa AfriCenter uliopo barabara ya Kigogo, ambako nako hawakudumu kipindi kirefu na hivi sasa wanapiga muziki wao katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni.

Baadhi ya nyimbo zilizogongwa na OTTU Jazz zilikuwa za Kicheko, Mawifi mnanionea, Ndoa Ndoana, Nimezama katika dimbwi, Mti mkavu na Mizimu.

Zingine ni Wabakaji, Tabu, Pricila, Penzi la mlemavu, Piga ua talaka utatoa, Tuma, Wapambe, Asha mwana Sefu, Ajali, Mtanikumbuka, Barua ya kusikitisha, Mwana mkiwa, Kalunde, Kaza moyo, Jesca, Kwenye penzi, Binti maringo, Dalili na nyingine nyingi.

Chama cha Wafanyakazi Tanzania baadaye kijiondoa katika ufadhili wa bendi hiyo, kikawaachia vyombo wajitegemee. Walijikusanya kutengeneza mikakati na kuamua kuipa jina la bendi kuwa Msondo Ngoma ikiwa imesheheni wanamuziki wengi wakiwemo wa zamani na wapya.

Msondo Ngoma ina jumla ya wanamuziki 18 na fundi mitambo mmoja. Kiongozi wao ni Said Mabera ambaye pia ni mpigaji wa gita la Solo. Waimbaji wa bendi hiyo ni akaina Juma Katundu, Fresh Jumbe, Shaaban Dede, Twaha Mohamed, Hassan Moshi William ‘TX Junior’ na Hussein Kalembo.

Wakung’utaji magita ni akina Abdull Ridhiwani Pangamawe ambaye ni bingwa wa kupiga kinanda, Solo na Rhythm, Huruka Uvuruge naye pia ni mpigaji wa Solo na Rhythm, Kassimu Mponda, Mustafa Hamis ‘Pishuu’ na Zahoro Bange wakicharaza gitaa la rhythm.

Kwa upande wa gita zito la besi wapo Ally Lindunga na Saad Ally ‘Sure Boy’. Drums huchanganywa na Saad Ally ‘Mashine’ na Arnold Kang’ombe.Tarumbeta hupulizwa na kijana machachari Roman Mng’ande ‘Romari’ na Hamis Mnyupe.Dorice George hupiga Tumba, Drums ambaye pia ni Mwimbaji wakati Amiri Said Dongo naye ni mpigaji wa Tumba.

Mtunzi na mwimbaji mahiri Shabani Dede ‘Kamchape’ alirejea tena katika bendi hiyo akitokea bendi ya Mlimani Park Orchestra ‘Wana Sikinde’.Talanta za kutunga na kuimba za marehemu TX Moshi William, ambaye inasemekana yeye ndiye alikuwa mtunzi mkuu katika bendi hiyo.

Inaaminika kuwa katika albamu moja waliokuwa wakiifyatua, TX alikuwa katunga nyimbo 8 hadi 9 wakati zilizobaki zinatungwa na Jumuiya.

Tofauti kabisa na miaka ya nyuma upinzani kati ya bendi za Mlimani Park na Msondo Ngoma Classic uliokuwa ukishihudiwa nyakati zile, umepungua kwa kiasi kikubwa. Bendi hizo hufikia kuandaa siku ya kupiga muziki kwa pamoja katika viwanja vya TTC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.

Bendi ya Msondo Ngoma Classic bado ipo ikiwa na makao yake katika baa ya Dimax iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanamuziki wanaotajwa katika makala hii wamekwisha tangulia mbele za mungu akiwemo Mzee Muhidini Gurumo.

Wengine ni TX Moshi William, Nicko Zengekala, Selemani Mbwembwe, Joseph Maina, Hamis Kitambi, Mustafa John Ngosha, Suleiman Mwanyiro, Tino Maselenge ‘Arawa’, Athuman Momba na wapulizaji wa saxophone Mnenge Ramadhani na Alli Rashidi aliyefariki dunia siku ambayo bendi hiyo ikitimiza miaka 50, Oktoba 10, 2014.

Mungu azipumzishe roho zao pahala pema peoni, Amina.

MOMBASA READIES FOR 9TH EAST AFRICAN PETROLEUM CONFERENCE AND EXHIBITION 2019

0
0
The 9th East African Petroleum Conference and Exhibition 2019 (EAPCE’19) is set to be held in Mombasa, Kenya at the Pride Inn Resort, from 8th to 10th May, 2019.

The 9th edition of the biennial oil and gas regional event, themed East African Region - the destination of choice for Oil and Gas Investment Opportunities to enhance Socioeconomic Transformation, will provide a unique forum for dialogue for all players in the Petroleum industry regionally and internationally. Technical papers, posters and exhibitions aligned to the conference theme are lined up to produce stimulating interactions among conference delegates.

The Conference offers a wide range of technical presentations reflecting developments in the oil and gas industry in East Africa and around the world. The EAPCE’19 provides a forum for discussing the legal and policy framework and the overall business environment prevailing in the region.

Preceding the Conference, on 7th May, 2019, is a Pre-Conference workshop under the theme Skills Gap and Local Content Requirements for Sustainable Oil and Gas Development in East Africa.
Facilitated by Norwegian Petroleum Directorate (NPD) and Bridge Consult, the Pre-Conference Workshop aims at the identification and development of skills in order to maximize national benefits from petroleum exploitation, as well as how local content can be identified and understood through increased local purchase, higher employment of nationals or larger local ownership in the oil and gas sector.

Further, the Ugandan Minister of Energy and Mineral Development, Hon. Eng. Irene N. Muloni is scheduled to launch the country’s second licensing round on 8th May, 2019.  Five (5) Exploration Blocks ranging from 400 to 1300 km2 are expected to be launched for this licensing. This licensing round follows the first licensing round through competitive bidding which was successfully undertaken in 2017.

Uganda made its first commercial oil discovery in 2006. To date, over 121 wells have been drilled with a success rate of over 88%. Preparations are under way to commence production following the issuance of production licenses to Total E&P Uganda B.V, Tullow Uganda Operations Pty Ltd, and CNOOC Uganda Ltd. The commercialization of the oil in Uganda will involve export of part of crude oil by the East Africa Crude Oil Pipeline through Tanga Port in Tanzania.

The Conference’s programme also incorporates Field excursions to selected sites of geological and touristic importance in the region to give the delegates an unforgettable experience.

UFARANSA WATOA NENO WAKATI WA KUAGA MWILI WA DK. MENGI, WAKUMBUKA TABASAMU LAKE LILILOJAA UPENDO

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UBALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania umesema umesikitishwa na kifo cha mfanyabishara maarufu na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dk.Reginald Mengi huku ukielezea namna ambavyo walikuwa wakishirikiana naye katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza leo Mei 7,2019 wakati wa kuaga mwili wa Dk.Mengi katika viwanja vya Kamrijee jijini Dar es Salaam, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frediric Clavier amesema kifo cha Dk.Mengi ni pigo kwa Taifa la Tanzania na kwamba ubalozi wa Ufaransa umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hiyo.

"Ubalozi wa Ufaransa pamoja na wafanyakazi wake wote, tumesikitishwa na kifo cha Dk.Mengi.Binafsi kwangi mimi naweza kusema nilipata bahati kwani nimeshauriana naye mambo mengi yenye kulenye kulenga kuimarisha taasisi mbalimbali.Tulibadilisha mawazo kuhusu shughuli za kibiashara,"amesema Balozi Clavier.

Amefafanua kuna mambo mengi ambayo yamefanywa na Dk.Mengi wakati wa uhai wake na kwamba amekuwa akikumbuka vikao vyao mbalimbali ambavyo amekaa na Dk.Mengi kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na kubwa zaidi anakumbuka tabasamu lake lililojaa upendo wakati wote.

"Dk.Mengi alikuwa akishirikiana na Ubalozi wa Ufaransa lakini pia tunatambua pigo kubwa ambalo Taifa la Tanzania limepata kutokana na kuondokewa na mtu muhimu.Ubalozi wa Ufaransa tutakumbuka namna ambavyo Mengi alijitoa kwa ajili ya kusaidia makundi ya watu wasiojiweza,"amesema.

Amesisitiza "Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kumuomba Mungu ampumzishe ndugu yetu mahala pema peponi.Amina."

ROSE NDAUKA AWASHAURI WASANII WA BONGOMOVIE KUBORESHA SOKO LA FILAMU.

0
0

         Na.Khadija seif,Globu ya jamii.

MSANII wa tasnia ya filamu nchini Rose Ndauka amefungua biashara ya saloon jijini Dar es salaam.

Ndauka amesema ukimya wake katika filamu kwa muda mrefu umetokana na majukumu ya kifamilia pamoja na biashara ambayo ameianzisha hivi karibuni ya saloon ya kike na kiume.

"Rose ni yule yule na kadri navozidi kukua  majukumu ndio yanazidi ila bado niko vizuri na ninapenda kazi yangu ya sanaa kwani ndio ilionitambulisha kwenye ramani ya Tanzania na watu wanaifahamu kupitia sanaa", alisema ndauka.

Hata hivyo ameeleza ukimya huo pia umemuwezesha kujinoa upya na kurudi kwenye tasnia akiwa mpya kwani ameweza kuyafanyia kazi malalamiko ambayo mashabiki kila kukicha hutoa na kusema kwa sasa filamu nyingi hazina ubora na zinapelekwa sokoni pasi na ubunifu na utofauti kwenye kazi hizo.

Pia amewapa ushauri wasanii na watengenezaji wa filamu kuboresha kazi zao ili ziweze kupewa thamani katika jamii na kupata wanunuzi wengi kwani soko bado lipo na wasanii wazuri bado wapo .

Aidha ndauka amewapa rai mashabiki wake kuwa waendelee kununua kazi zake na kumshauri pale anapokosea kwani bila wao hata Leo hii asingeweza kufungua biashara zingine kutokana na kuwa wadau wakubwa wa kazi za filamu na kununua pia .

WAFANYABIASHARA MKOANI TANGA WATAKIWA KUACHA KUPANDISHA BEI ZA BIDHAA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

0
0
WAFANYABIASHARA mkoani Tanga wametakiwa kuacha kupandisha bei za bidhaa hususani za vyakula kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuwa na moyo wa huruma kwa wale watakaofunga kwani ni mwezi wa toba ambao waumini hujinyima kwaajili ya watu wengine.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Waziri Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa mwezi wa ramadhani.
Alisema kuwa mwezi wa ramadhani ni kipindi ambacho waumini humrudia Mwenyezi Mungu kwa nguvu zote hivyo sio kipindi cha wafanyabiashara hao kujinufaisha kwa watu wanaofunga kwani waumini wamekuwa wakijidunduliza ili kusaidia wasiojiweza lakini wafanyabiashara hao wanaona ni fursa ya kujinufaisha.
 “Hiki ni kipindi ambacho wanawasaidia watu mbalimbali kwa nguvu zao zote, sasa akamsaidie mtu mwingine na wakati huo huo akusaidie wewe ambaye unataka kujinufaisha kwa manufaa yako mwenyewe ukijua kabisa kwamba hiki ni kipindi maalum cha kumrudia Mwenyezi Mungu lakini pia ndugu zangu kwenye tuongeze ibada,tupendane ikiwemo kutembelea wagonjwa“Alisema
Katibu huyo aliwasihi wafanyabiashara kuacha kuongeza bei bei ya vyakula mbalimbali huku akiwaomba ikiwezekana washushe bei za vyakula ili kuweza kupata thawabu kwenye kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtufuku wa ramadhani.
Aidha aliwatakia mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani Waislamu wote Tanzania pamoja na wale waumini wa dini mbalimbali watakaosindikiza mwezi huo na kumuomba mwenyezi Mungu atupe baraka kutokana na mwezi huo ndani ya Mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.
Hata hivyo pia aliwataka makatibu wote wa hamasa na chipukizi wilaya za mkoa huo kuendelela kushikamana ikiwemo kuchangamkia fursa za kimaendeleo zilizopo kwenye maeneo yao ili ziweze kuwa na tija kwao na jamii zinazowazunguka.
Viewing all 109583 articles
Browse latest View live




Latest Images