Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live

AJALI YA NDEGE YAUA 41, YAJERUHI 11 NCHINI URUSI

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TAKRIBANI watu 41 wamefariki dunia kufuatia ajali ya ndege ya Aeroflot Sukhoi Superjet ya nchini Urusi baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kushika moto na kulazimika kutua kwa dharura mjini Moscow hapo jana, shirika la utangazaji la Al jazeera limeripoti.

Video zimeonesha  ndege hiyo ya Sukhoi Superet -100 ilipata hitilafu na kulazimika kutua kwa dharura huku sehemu za ndege hiyo ikiwaka moto katika uwanja wa ndege  wa Sheremetyevo Moscow.

Baadhi ya picha za video zimeonesha baadhi ya abiria wakiruka kutoka katika sehemu zilizokuwa zinawaka na kuruka katika nyasi na sehemu salama.

Imeelezwa kuwa watoto wawili ni moja kati ya watu waliopoteza maisha na tayari wapelelezi kutoka Urusi wameshaanza kufanya uchunguzi kufuatia tukio hilo.

Waziri wa Afya wa Moscow Dmitry Matveyev amesema kuwa katika ajali hiyo watu 11 wamejeruhiwa, na watatu kati yao wameruhusiwa kutoka hospitali na hali zao zinaendelea vizuri.

Mamlaka ya uwanja wa ndege Moscow Urusi umesema kuwa ndege hiyo ilitua kwa dharura baada ya tatizo la kiufundi kutokea ikiwa angani na  wachunguzi watafanya utafiti kupitia mashahidi, wahanga pamoja na wafanyakazi wa ndege wa la shirika hilo.

Ndege hiyo ya Sukhoi  aircraft ilikuwa inaruka kutoka Moscow kuelekea mji wa kaskazini wa Urusi (Murmansk) kabla ya kurudi uwanjani na ilibeba abiria 73 na wafanyakazi wa ndege 4.

TRFA YATOA MSAADA WA CHUPA 500 ZA DAWA ZA KUTIBU SARATANI KWA WATOTO MUHIMBILI

$
0
0
*Wadau waombwa kujitokeza kusaidia watoto haoNa Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

MAMLAKA ya  udhibiti wa mbolea nchini imetoa msaada wa chupa 500 za dawa ya kutibu magonjwa ya saratani kwa watoto ili kuweza kuokoa maisha ya watoto wanaosumbuliwa na tatizo la saratani.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Dkt. Stephan Ngailo amesema kuwa dawa hizo zimegharimu Shilingi Milioni 11.

Amesema kuwa, "Msaada huu ni kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya na kuwahudumia wananchi ili wawe na afya njema," amesema Dkt. Ngailo. 

Amesema kuwa kwa kuwasaidia watoto hao itawasaidia wazazi wao kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa.

"Watoto hawa wakipata matibabu basi muda  mwingi wa wazazi wao utatumika katika kujenga taifa kuliko sasa ambako muda wao mwingi unatumika Hospitalini wakiwauguza watoto" ameeleza. 

Aidha amesema kuwa, "Tunaamini sasa kuwa dawa hii ikitolewa na kutibu  watoto hawa basi wazazi wao watasaidia katika shughuli mbali mbali za maendeleo na kukuza uchumi na pia wanaweza kununua mbolea ili kukuza kilimo na kuongeza uzalishaji na tija na  kuchangia kwenye uchumi wa viwanda kwenye nchi yetu," amesema.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya taifa  Muhimbili Mary Charles  ameishukuru TRFA kwa msaada wa dawa walizowapatia na amewaomba wadau wengine wajitokeze na kujitolea misaada ya namna hiyo  kwani matibabu ya saratani huwa ni ghali sana.

Amesema dawa wanazotumia kutibu saratani ni za aina nyingi kwa mfano hii Dawa ya Actinomycin inaweza kutumika na dawa nyingine mbili au tatu yenyewe peeke yake hawezi kutibu saratani mpaka iwe na mchanganyiko hivyo wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza ili kuwasaidia watoto hao.
 Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya udhibiti mbolea nchini Dkt. Stephen Ngailo (kushoto) akimkabidhi dawa hizo Daktari bingwa  wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya taifa Muhimbili Dkt. Mary Charles leo jijini Dar  es Salaam.
 Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya mbolea nchini Dkt. Stephen Ngailo akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi dawa hizo ambapo wadau wameombwa kujitokeza ili kuwasaidia watoto hao, leo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya taifa Muhimbili Mary Charles akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea dawa hizo ambapo ametoa wito zaidi kwa wadau kutoa misaada ya namna hiyo, leo jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA RIPOTI YA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia  ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira mara baada ya kuizindua  katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (kushoto) mara baada ya kuzindua  ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hotel ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Bungeni jijini Dodoma Mei 6.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe, Bungeni jijini Dodoma Mei 6.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Mei 6.2019.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Mei 6.2019. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, Mbunge wa Bukoba vijijini Jason Rweikiza, Mbunge wa Sumve Richard Ndasa, Mbunge wa Sengerema William Ngeleja.

MAELFU YA WANANCHI DAR WAJITOKEZA BARABARANI KUUPOKEA MWILI WA MENGI

$
0
0
Jeneza lenye Mwili wa marehemu Dk. Reginald Mengi ukiingizwa kwenye gari maalumu baada ya kuwasili nchini nchini ukitoa Dubai, tayari kwa safari ya kuelekea Hospitali ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es salaam kwa kuhifadhiwa.

*Ni baada ya mwili wake kuwasili nchini ukitokea Dubai 
 *Wengine waamua kukimbilia gari ili kugusa jeneza lake

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAELFU ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam leo Mei 6,2019 wamejitokeza kwa wingi kuupokea na kuulaki mwili wa aliyekuwa mfanyabishara maarufu nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi ambaye amefariki dunia Mei 2 mwaka huu akiwa Dubai.

Mwili wa marehemu Dk.Mengi umewasili nchini saa nane mchana ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wastaafu na wananchi wa kada mbalimbali walijitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuupokea.

Pia Mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete alikuwa miongoni mwa waliofika uwanjani hapo kuupokea mwili huo wa Dk.Mengi. Baada ya kuwasili na kupokelewa na kufanyika maombo kabla ya kuanza safari ya kuelekea Hospitali ya Lugalo.
Mjane wa Marehemu Dkt. Mengi, Bi. Jacquenine akiwana wa waombolezaji wengine pamoja na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete waliofika kwenye uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere kumlaki.

Maelfu ya wananchi waliamua kuweka kambi katika barabara ambazo mwili wa Mengi umepitishwa ambapo wapo baadhi ya wananchi walionekana wakigusa jeneza ambalo limebeba mwili kama ishara ya kuonesha upendo.

Wakati mwili unapitishwa katika barabara ya Nyerere, Buguruni, Ilala,Kigogo, Magomeni, Kinondoni na  Morroco wakati ukielekea Mwenge na kisha Lugalo idadi ya watu ilizidi kuongezeka kuusubiri mwili wa Dk.Mengi.

Simanzi na majonzi yalikuwa yametawala katika nyuso za wananchi walioamua kwenda kuulaki mwili wa Dk.Mengi huku wengi wao wakionekana kukimbilia gari iliyobeba mwili huo kwa lengo la kulishika. Mengi enzi za uhai alijipambanua kuwa karibu na jamii ya Watanzania ambapo alitumia sehemu ya fedha zake kutoa misaada.
Kutokana na idadi ya watu waliokuwa wamejipanga barabarani, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliyekuwa kwenye msafara huo alionekana akihakikisha msafara huo unakwenda katika mazingira yaliyotulivu huku akisaidiwa na Jeshi la Polisi kupita Kikosi cha Usalama barabarani.

Katika msafara huo waendesha bodaboda nao hawakuwa nyuma kwani nao walikuwa sehemu ya wananchi ambao walihakikisha wanakuwepo katika mapokezi ya mwili huo.

Wananchi mbalimbali ambao walikuwa barabarani na kupata fursa ya kumzungumzia Dk.Mengi wamesema kuwa na mambo mengi ya kujifunza kutoka katika maisha ya Mengi ambaye enzi za uhai wake alikuwa na upendo kwa kila mtu na kubwa zaidi alihakikisha utajiri wake unawanufaisha na wengine kwani hakuwa mchoyo.
Sehemu ya waombolezaji wakiwa wamejitokeza kwa wiki maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam kuulaki mwili wa marehemu Dk. Reginald Mengi uliowasili nchini mchana wa leo. Picha kwa hisani ya CloudsFM
Mjane wa Marehemu Dkt. Mengi, Jacqueline Mengi akilia kwa uchungu.

VOA Swahili: Duniani Leo May 6, 2019

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO MEI 6, 2019

WADAU WA USALAMA BARABARA WAKUBALIANA KUWEKA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

$
0
0
--
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Fatma Toufiq akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani ulioandaliwa na Chama Cha Wanasheria wanawake TAWLA

 Mratibuwa Masula ya Uslama barabra kutoka Umoja wa Mataifa Marry Kessy akizungumzia malengo mawili ya milenia ambayo yamegusia usalama barabarani na muda uliongezwa wa maalengo ya milenia kufikia 2030
 Mkurugenzi wa Chama Cha Wanasheria Wanawake TAWLA, Tike Mwambipile akizungumza na Washiriki wa Semina hiyo juu ya masuala ya usalama barabarani
 Mmoja wa Washiriki wa Semina hiyo na Mdau wa Masuala ya Usalama Barabrani Mzee Hamza Kasongo akichangia katika mjadala wa nini kifanyike kupunguza ajali nchini

Sehemu ya Washiriki wa Semina juu ya Masuala ya Usalama Barabarani yaliyoandaliwa na TAWLA Kwa kushirikiana na Azaki nyingine za kiraia

NEMC YATAJA MCHANGO WA MAREHEMU WA DR REGINALD MENGI KATIKA UANZISHWAJI WAKE

$
0
0

Na Humphrey Shao, Michuzi Blog

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka  amezungumza na Waombolezaji walikusanyika nyumbani kwa marehemu na kutaja mchango wake katika uhifadhi wa mazingira nchini
Akizungumza na vyombo vya habari na waombolezaji Nyumbani kwa marehemu kinondoni Dar es Salaam,Dr Gwamaka ametaja namna Marehemu alivyoshiriki katika uanzishwaji wa baraz ala Mazingira nchini.
"Dr. Mengi ndio alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa baraza na aliyeshiriki kuunda baraza na sheria yake ambayo imeleta mabadiliko makubwa ya uhifadhi wa mazingira nchini kulinganisha na uko nyuma.
Ametaja kuwa Dk. Mengi amedumu katika nafasi hiyo kwa miaka kumi ambayo ndio wakati baraza liliweza kuimarika sana na kujilikana kila mahali hivyo tunatambua mchango wako mkubwa katika uhifadhi wa Mazingira.
 Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo wa msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Marehemu Dr Reginald Mengi
  Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka akisaini kitabu cha Maombolezo
  Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC, DK.Samuel Gwamaka akisalimiana na wadau mbalimbali pembeni yake ni Mwanasheria wa NEMC Eche Saguda akisikiliza kwa makini
 Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu, Omary Mahita akisaini katika kitabu cha Maombolezo Nyumbani kwa Marehemu Kinondoni
Viongozi wa Vyama Vya Siasa Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanachi Cuf, Prof Ibrahim Lipumba na kulia kwake ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa CCM Keisha

KC YASAINI MKATABA WA KUWAUZIA VIWANJA WASANII KIGAMBONI

$
0
0

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando akitoa nasaha zake kwa wasanii na wanachama wa Uzalendo kwanza walifika katika hafla ya chakula cha pamoja kwa ajili ya kusaini mkataba wa ununuzi wa Viwanja katika Wilaya ya Kigambani kupitia kampuni ya Kc Developing Plan.

Mwenyekiti wa Tanzania Uzalendo Kwanza Steve Nyerere akizungumza kabala ya kusaini maktaba na kampuni ya Uuzaji Ardhi ya Kc Development
 Mkurugenzi wa Kc Land Development Plan, Khalid Mwinyi akizungumza na Wasanii kabla ya kusaini makataba wa mauziano ya Viwanja.
 Mkurugenzi wa Kc Land Development Plan, Khalid Mwinyi na Mwenyekiti wa Tanzania Uzalendo Kwanza Steve Nyerere wakisaini Mkataba wa muziano ya Viwanja na wasanii katika eneo la kigamboni
  Mkurugenzi wa Kc Land Development Plan, Khalid Mwinyi na Mwenyekiti wa Tanzania Uzalendo Kwanza Steve Nyerere wakibadilishana Mkataba.

Katibu wa Uzalendo Kwanza , Kulwa Kikumba maarufu kama Dude akitoa neno la Shukrani kwa Wasanii
 Wasanii wa Filamu ambao ni wanachama wa kundi la Uzalendo kwanza wakfatilia
 Wasanii wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi

SERIKALI YA UJERUMANI YAKABIDHI HOSPITAL YA JESHI KANDA YA KASKAZINI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi TV, Monduli. 
 SERIKALI ya Ujerumani kupitia Balozi wake nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter imekabidhi funguo za Hospitali ya Kanda ya Jeshi iliyopo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli wilayani humo iliyogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.6. 
 Akikabidhi funguo kama ishara ya ufunguzi na makabidhiano kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Balozi Dkt Waechter alisema kuwa hospitali hiyo ni moja ya mkataba kati ya Wizara ya Ulinzi nchini Ujerumani na Wizara ya Ulinzi nchini Tanzania kupitia sekta ya afya huku akiahidi kuendelea kufadhili katika miradi ya serikali ya Tanzania. 
 "Mradi huu ulianza 2017 ulitakiwa kuisha mwaka 2020 lakini tumeongeza muda wa mradi hadi 2024 ili kuendelea kusaidia serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ulinzi"alisema Balozi huyo. 
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi aliiomba Serikali ya Ujerumani kuendelea kutoa msaada kwakuwa hospitali za Kanda hazihudumii wanajeshi pekee bali zinasaidia wananchi kwa asilimia 80 huku wanajeshi asilimia 20. 
 "Wenzetu wa Ujerumani wametusaidia sana walitusaidia katika ujenzi wa chuo cha wataalam wa tiba,vifaa na maabara na niwashukuru kwa kuongeza muda wa mradi..... 
 "Lakini Hospitali hii ina vifaa bora na vya kisasa pengine kuliko hata hospitali nyingine na itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wakienda nje kutibiwa" alisema Waziri Mwinyi. 
 Naye Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo alisema kuwa hadi kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hiyo kumeghalimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.6 ambapo Bilioni 2.8 zilitumika kwa  ajili ya vifaa tiba na Bilioni 2.8 kwa ajili ya miundombinu kwa ufadhili wa serikali ya Ujerumani. 
 "Aidha pia mbali na hii Walijenga chuo cha Tiba Dar es salaam, Mbeya, Mwanza na hapa na zote ni za viwango vya juu" alisema Generali  Mabeyo. 
 Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Tiba wa Jeshi la Wananchi Tanzania Meja Jenerali Denis Janga alibainisha matibabu yataanza mapema ambapo kutakuwa na wataalam wa Idara zote ikiwemo Meno,Uzazi na picha(Xray) huku akibainisha kuwa hospitali hii ina uwezo wa kulaza wagonjwa 50 kwa siku na kuhudumia wagonjwa wa nje 300 kwa siku.
 balozi wa Ujerumani nchini Tanzania pamoja na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa akikata utepe ishara ya kuonyesha hospital hii ipo tayari kutumika
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi  akionyeshwa moja ya chumba kwa ajili ya Upasuaji
Balozi wa Ujerumani  nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter akimkabidhi funguo za Hospitali ya Kanda ya Jeshi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi .
waziri wa ulinzi na jeshii la  wananchi wa Tanzania pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania akiwa pamoja na maofisa mbalimbali wa jeshi hilo pamoja na ujerumani.

RAIS WA SHIRIKISHO LA BARAZA LA TAIFA LA FALME ZA KIARABU (UAE) AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA AFRIKA

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi amefungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika ulioanza leo Mei 6,2019 jijini Johannesburg,Afrika Kusini kwa kukutanisha wabunge kutoka nchi 54 barani Afrika.
Akitoa hotuba yake, Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi alisema Bunge la Nchi za Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) zimekubaliana kushirikiana na Bunge la Afrika katika kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi barani Afrika.
“Uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Bara la Afrika umekuwa mkubwa,tumekuwa tukisaidia mambo kadha wa kadha barani Afrika,tunataka kuona usalama unazidi kuimarika Afrika,kwani bila usalama katika nchi zetu hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa”,alisema Dr. Amal.
“Masuala ya vitendo vya kigaidi yana athari kubwa,tunatakiwa kwa pamoja kushirikiana kuyatafutia ufumbuzi ili wananchi wetu wawe salama lakini pia kuwa na suluhisho la kudumu juu ya wakimbizi wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani,tunafurahi kuona wakimbizi wakirudi kwenye nchi zao kwa amani”,alisema.
Kwa upande wake,Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang alisema ili ushirikiano na umoja madhubuti unahitajika ili kufikia suluhu za kudumu juu ya masuala ya amani na usalama barani Afrika.
Ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika litakalofungwa Mei 17,2019 umekwenda sanjari na wabunge 26 wapya wa bunge la Afrika kutoka nchi mbalimbali kuapishwa.
Kauli mbiu ya Bunge la Afrika mwaka huu ni "2019 mwaka wa Wakimbizi,wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani : Kuelekea kupata masuluhisho ya kudumu katika kulazimishwa kuhama makazi katika Afrika".
Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa Bunge la Afrika likifunguliwa leo..Tazama hapa chini
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi akitoa hotuba yake wakati akifungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019 Midrand, jijini Johannesburg,Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akitoa hotuba yake Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019.
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi (katikati),Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang na washiriki wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuimba wimbo  wa Umoja wa Afrika.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wakiimba wimbo  wa Umoja wa Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (kulia) na viongozi mbalimbali wa bunge la Afrika wakiwa katika ukumbi wa bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa ukumbini.
Bunge linaendelea.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Aliyekuwa Mjumbe wa Uongozi wa Bunge la Afrika Dr. Bernadette Lahai kutoka Sierra Leone akitoa tamko na ujumbe wa mshikamano barani Afrika.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Wabunge wapya wa bunge la Afrika kutoka Swaziland wakila kiapo bungeni leo. Hao ni miongoni mwa wabunge 26 kutoka nchi mbalimbali walioapishwa leo.
Wabunge wapya wa bunge la Afrika wakiendelea kiapo
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika.

RC Wangabo awasihi wafanya biashara kutoongeza bei za bidhaa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 06.05.2019

The 5th UDSM Research Week Exhibitions. 6th to 8th May 2019.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 7,2019

WADAU WA USALAMA BARABARA WAKUBALIANA KUWEKA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Fatma Toufiq akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa kujadili masuala ya usalama barabarani ulioandaliwa na Chama Cha Wanasheria wanawake TAWLA

Mratibuwa Masula ya Uslama barabra kutoka Umoja wa Mataifa Marry Kessy akizungumzia malengo mawili ya milenia ambayo yamegusia usalama barabarani na muda uliongezwa wa maalengo ya milenia kufikia 2030
Mkurugenzi wa Chama Cha Wanasheria Wanawake TAWLA, Tike Mwambipile akizungumza na Washiriki wa Semina hiyo juu ya masuala ya usalama barabarani
Mmoja wa Washiriki wa Semina hiyo na Mdau wa Masuala ya Usalama Barabrani Mzee Hamza Kasongo akichangia katika mjadala wa nini kifanyike kupunguza ajali nchini
Sehemu ya Washiriki wa Semina juu ya Masuala ya Usalama Barabarani yaliyoandaliwa na TAWLA Kwa kushirikiana na Azaki nyingine za kiraia

Marais Kagame, Sall kuungana mkutano wa Tony Elumelu Foundation

$
0
0

*Kukutanisha wajasiriamali 5,000 wa Bara la Afrika

Na Ripota wa Michuzi TV -Abuja, Nigeria

Taasisi ya Tony Elumelu Foundation (TEF) ambayo inapambania wajasiriamali kutoka Afrika itakuwa mwenyeji wa awamu ya 5 ya mkusanyiko mkubwa wa wajasiriamali kutoka Afrika itakayofanyika Julai 26 na 27, 2019, ambapo mkutano huo wa siku mbili utafanyika Hoteli ya Transcorp Hilton, Abuja nchini Nigeria.

Mkutano huo wa kila mwaka  huandaliwa kupitia Programu ya Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship ambayo imewapa mafunzo Waafrika chipukizi 3,000 ambao walichaguliwa kutoka zaidi ya waombaji 216,000. 

Tukio hilo linawapa nafasi wanawake na wanaume chipukizi kutoka nchi zote 54 za Afrika kukutana, kujifunza na kubadilishana mawazo yenye mlengo wa kuwa wawekezaji bora Afrika na duniani.

Pia ni fursa muhimu kwa viongozi wanasiasa na watunga sera kukutana uso kwa uso na kizazi kipya cha wafanyabiashara viongozi Wafrika ambao wanabadilisha uchumi wa Afrika.

Wazungumzaji wakuu katika warsga hiyo muhimu ni Rais wa Rwanda, Paul Kagame, na Rais wa Senegal, Macky Sall, ambao wataungana na Mwanzilishi wa TEF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Heirs Holdings na United Bank for Africa (UBA), Tony O. Elumelu, katika majadiliano ya wazi.

Uwepo wa marais hao unawapa fursa wajasiriamali kutoka Afrika wanaohudhuria kuwa na mjadala wa kina na kutoa ushuhuda namna serikali inavyoweza kufanya kuchochea ukuwaji wa biashara.

Ajenda ya mkutano huo inahusisha majadiliano na wataalamu kutoka Afrika na duniani ambao watawapa mafunzo washiriki kuongeza ujuzi katika biashara yao. Aidha warsha hiyo itawapa fursa baadhi wajasiriamali wateuli kuelezea bidhaa na huduma wanazotoa mbele ya jopo la majaji.

Kwa mara ya kwanza, warsha hiyo itafanyika Abuja, Nigeria na kuwaleta pamoja watunga sera wakubwa, wafanyabiashara wakubwa na wale waliowahi kufaidi Programu hiyo.

Mwaka jana, tukio muhimu lilikuwa uzinduzi wa TEFConnect ambayo ni sehemu ya wajasiriamali kutoka Afrika kubadilishana mawazo kupitia mfumo wa digitali.

Mikutano hiyo imewahi kuhudhuriwa  na marais kadhaa wakiwamo Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, Waziri Mkuu wa mstaafu wa Benin na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri, Lionel Zinsou na Makamu wa Rais wa Nigeria, Profesa Yemi Osinbajo.

Taasisi ya Tony Elumelu imedhamiria kuleta mabadiliko Afrika nzima kupitia ujasiriamali kwa kutaka zaidi Waafrika kujitegemea, Africapitalism, chini ya mwanzilishi huku akitambua zaidi kuwawezesha vijana wa Afrika kiuchumi hususan karne hii ya 21.

Mwaka 2015, taasisi hiyo ilijitolea dola za Marekani milioni 100 million kuwawezesha wajasiriamali 10,000 kutoka kote barani kwa zaidi ya miaka 10 ambapo kwa sasa inakwenda kutimiza miaka mitano.

Pia Tony Elumelu Foundation imetoa mchango wa  kushauri na kutoka mafunzo ya menejementi kwa zaidi ya watu 7,500 wanaoanzisha na wenye biashara ndogo kwa nchi zote 54 za Afrika.

“Warsha ya TEF Entrepreneurship haitaleta tu watu wadau muhimu katika mabadiliko ya ujasiriamali wa Afrika lakini pia kumpa nafasi kila mtu kupanua biashara yake kwa nia ya kuleta maendeleo barani.

“Tunafarijika kupokea habari kutoka kwa wajasiriamali wetu ambao wanatengeneza ajira, wanaajiri watu na kubadilisha maisha ya jamii inayowazunguka barani Afrika. Tunaamini hawa wajasiriamali ni tegemeo wetu wa baadaye. Wekezeni kwao sasa na kuvuna ndoto ya kesho ya Afrika,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa TEF.Ifeyinwa Ugochukwu.

Manzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu Foundation, Tony Elumelu, akiwa katika moja ya mikutano ya wajasiriamali wa Afrika nchini Nigeria.
Washiriki wa moja ya mikutano iliyopita wakiwa katika picha ya pamoja na mwasisi wa Tony Elumelu Foundation.

RAIS WA SHIRIKISHO BARAZA LA TAIFA FALME ZA KIARABU (UAE) AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA AFRIKA

$
0
0

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi akifungua Mkutano wa Bunge la Afrika leo nchini Afrika Kusini

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi amefungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika ulioanza leo Mei 6,2019 jijini Johannesburg,Afrika Kusini kwa kukutanisha wabunge kutoka nchi 54 barani Afrika.

Akitoa hotuba yake, Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi alisema Bunge la Nchi za Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) zimekubaliana kushirikiana na Bunge la Afrika katika kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi barani Afrika.

“Uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Bara la Afrika umekuwa mkubwa,tumekuwa tukisaidia mambo kadha wa kadha barani Afrika,tunataka kuona usalama unazidi kuimarika Afrika,kwani bila usalama katika nchi zetu hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa”,alisema Dr. Amal.

“Masuala ya vitendo vya kigaidi yana athari kubwa,tunatakiwa kwa pamoja kushirikiana kuyatafutia ufumbuzi ili wananchi wetu wawe salama lakini pia kuwa na suluhisho la kudumu juu ya wakimbizi wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani,tunafurahi kuona wakimbizi wakirudi kwenye nchi zao kwa amani”,alisema.

Kwa upande wake,Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang alisema ili ushirikiano na umoja madhubuti unahitajika ili kufikia suluhu za kudumu juu ya masuala ya amani na usalama barani Afrika.Ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika litakalofungwa Mei 17,2019 umekwenda sanjari na wabunge 26 wapya wa bunge la Afrika kutoka nchi mbalimbali kuapishwa.

Kauli mbiu ya Bunge la Afrika mwaka huu ni "2019 mwaka wa Wakimbizi,wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani : Kuelekea kupata masuluhisho ya kudumu katika kulazimishwa kuhama makazi katika Afrika".Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa Bunge la Afrika likifunguliwa leo..Tazama hapa chini

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi akitoa hotuba yake wakati akifungua Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019 Midrand, jijini Johannesburg,Afrika Kusini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akitoa hotuba yake Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika leo Mei 6,2019.

Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi (katikati),Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang na washiriki wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika wakiwa wamesimama kuimba wimbo wa Umoja wa Afrika.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wakiimba wimbo wa Umoja wa Afrika.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (kulia) na viongozi mbalimbali wa bunge la Afrika wakiwa katika ukumbi wa bunge la Afrika leo Jijini Johannesburg.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa ukumbini.
Bunge linaendelea.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Aliyekuwa Mjumbe wa Uongozi wa Bunge la Afrika Dr. Bernadette Lahai kutoka Sierra Leone akitoa tamko na ujumbe wa mshikamano barani Afrika.

Wabunge wakiwa ukumbini.

Wabunge wapya wa bunge la Afrika kutoka Swaziland wakila kiapo bungeni leo. Hao ni miongoni mwa wabunge 26 kutoka nchi mbalimbali walioapishwa leo.
Wabunge wapya wa bunge la Afrika wakiendelea kiapo Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.

Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA RIPOTI YA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira mara baada ya kuizindua katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (kushoto) mara baada ya kuzindua ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hotel ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Mazingira Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
…………………. 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua ripoti ya hali ya Hali ya Mazingira nchini Tanzania ambapo ripoti hiyo imetaja sababu mbalimbali ikiwemo ya kasi ya ongezeko la watu na ukuaji wa maendeleo unachangia kwa sehemu kubwa uharibifu wa mazingira.

Akizungumza leo Mei 6,2019 wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mama Samia amesema ripoti hiyo imefanywa kati ya Serikali ya Tazania na Benki ya Dunia na lengo ni kuangalia kwa kina kuhusu hali ya mazingira nchini na hatua za kuchukua katika kutafuta ufumbuzi wake. 

Amefafanua ripoti ioanesha kuwa kasi ya ongezeko la watu na kasi ya ukuaji wa uchumi nchini unachangia uharibifu wa mazingira, hivyo ni jukumu la Watanzania pamoja na watalaam wa kada mbalimbali na wadau wa maendeleo kuangalia namna bora itakayowezesha idadi ya watu inayoongezeka na ukuaji wa uchumi hauwi sehemu ya kuharibi mazingira nchini. 

“Ripoti inaposema ukuaji wa uchumi na kasi ya ongezeko la watu ndio sababu za uharibifu wa mazingira, lazima watanzania na watalaamu kwa ujumla kutusaidia kutafuta ufumbuzi wake.Kama kasi ya ongezeko la watu ni sababu sasa tufanyeje ?Inaana nusu ya watu ipungue, au kasi ya ukuaji wa uchumi ambayo nayo inatajwa kama sehemu ya chanzo cha kuharibu mazingira inachangia. 

“Ni lazima Watanzania tuangalie namna bora itakayofanikisha mazingira yanatunzwa na shughuli za maendeleo na kasi ya ukuaji wa watu inaendelea.Ndani ya ripoti imeonesha namna ambavyo rasilimali za Tanzania namna ambavyo zinaharibiwa. 

“Imeonekana kuwa matumizi mabaya ya maji, uharibifu wa hali ya hewa, kilimo na mambo mengine kadhaa yanachangia kuharibu mazingira.Watalaamu wanayo nafasi ya kushauri na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike ili kulinda mazingira yetu,”amesema Makamu wa Rais. 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Januari Makamba amesema kuwa “Leo ni siku muhimu kwa watu tunaohusika na mazingira kwasababu tumezindua ripoti ya hali ya mazingira ambayo imefanywa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.Ripoti hii inaeleza hali ya uchambuzi nchini Tanzania. 

“Chimbuko la ripoti hii ni mazungumzo ambayo tumekuwa nayo muda mrefu na wenzetu wa Benki ya Dunia pamoja na wadau wa maendeleo kuhusu namna gani nchi yetu inapata maendeleo kwa namna endelevu zaidi. Tunaposema maendeleo endelevu maana yake ni mchakato mzima wa kutafuta maendeleo ambayo yatadumu. Tutafute maendeleo huku tukitunza mazingira. 

“Ripoti inaonesha hali halisi ya uharibifu wa mazingira na bahati nzuri inaelekeza namna bora na nzuri ya kuhakikisha tunalinda mazingira yetu.Tumeona kuna changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira na wakati huo huo tunayo matumaini makubwa kwani kuna hatua ambazo zimependekezwa ndani ya ripoti hiyo ili kuhakikisha tunabaki salama katika eneo la mazingira. 

Amefafanua katika ripoti hiyo kuna sababu nyingi ambazo zimetajwa kama sehemu ya kuchangia uharibifu wa mazingira na sababu kubwa inatajwa kasi ya ongezeko la ukuaji wa watu na kasi ya ukuaji wa uchumi.Pia amesema kilimo cha umwagiliaji maji nacho kimetajwa moja ya sababu ya kuharibifu wa mazingira. 

Kuhusu mapendekezo ambayo yametajwa ndani ya ripoti hiyo , Waziri Makamba kuna mapendekezo manne ambayo yametolewa na pendekezo namba moja ni kuhakikisha taasisi za uharibifu wa mazingira na uchafuzi wa hali ya hewa zinaimarishwa kuongeza udhibiti. 

Makamba amefafanua katika ripoti inaonesha watu 26000 wanafariki dunia ka mwaka kutokana na uharibifu wa hali ya hewa huku akieleza kuwa kila dakika misitu inayoharibiwa ni urefu wa kiwanja cha mpira, hivyo kuna kila sababu ya kuendeleakuchukua hatua ili mazingira yabaki salama. 

Hata hivyo amesema baada ya kuzinduliwa kwa ripoti hiyo, kinachofuata ni mjadala katika kuichambua na kisha kuwekwa mikakati mbalimbali ambayo itaifanya nchi yetu iendelee kutunza mazingira yake hasa kwa kuzingatia kuna hatua nyingi zinachukuliwa kuhakikisha mazingira yabanaki salama.
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live

Latest Images