Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

HUU SIO UBINADAMU, MNAHATARISHA AFYA ZA WATOTO- RC MWANGELA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akitazama makazi ya wananchi wa Mtaa wa Shule ulioko jirani na Shule ya Msingi Mlowo, Wilayani Mbozi ambapo takataka zimemwaga katikati ya makazi ya wananchi kabla ya kuagiza kufungwa kwa dampo hilo.
Wananchi wa Mtaa wa Shule wakitazama takataka zilizomwagwa jirani na makazi yao mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela kupita mtaani hapo na kuagiza dampo hilo lifungwe.

……………………

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ameagiza kushikiliwa na polisi kwa masaa 24 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo Seriadi Mbugi kutokana na kurundika takataka jirani na makazi ya wananchi pamoja na shule ya Msingi Mlowo na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Brig. Jen. (Mst) Mwangela amefikia uamuzi huo mapema leo wakati akifanya ukaguzi wa hali ya usafi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo na kukuta takataka zimemwagwa katikati ya makazi ya wananchi ikiwa ni siku saba tangu amuelekeze Kaimu Mkurugenzi huyo kuhakikisha mji huo unakuwa Msafi.

“Nilifanya Mkutano na wananchi wa Mji wa Mlowo na malalamiko yao makubwa yalikuwa mrundikano wa takataka na madampo katikati ya miji yao, nilimuagiza na kumpa siku saba Mkurugenzi wa Mji mdogo wa Mlowo kuhakikisha anausafisha mji huu lakini leo siku saba zimepita ninakagua na kukuta takataka zimemwaga katikati ya makazi ya watu, naambiwa watoto wanacheza na kuokota taka hapa, huu sio ubinadamu”, amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela

Ameongeza kuwa Mkurugenzi huyo amekiuka agizo lake na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi hao kwa kuwawekea takakata wananchi katikati ya makazi yao kinyume na taratibu za kiafya zinavyoelekeza.

“Huu sio utendaji wa serikali kabisa, licha ya Kaimu Mkurugenzi wa Mji Mdogo kukaa ndani, namuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha ndani ya masaa manne takataka hizo ziwe zimetolewa na dampo hilo lifutwe”, amesisitiza Brig. Jen. (Mst) Mwangela

Kwa upande wake mkazi wa mtaa wa shule Bi Salehemu Filimon Mwaihojo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea eneo hilo na kutatua kero hiyo kwakuwa wamekuwa wakipata hofu ya magonjwa kutokana na uwepo wa takataka hizo

“Hii ni wiki ya pili wanamwaga matakataka hapa, watoto wanachezea na kuokota makopo wanachota maji machafu na kunywa kwenye makopo hayo machafu wengine unakuta wanaokota kondomu zinazomwaga hapa wanapuliza wao wanajua mipira, kwakweli tulikuwa na hali mbaya, kwakuwa tuliona wametumwagia magonjwa hapa”, amesema Mwaihojo

Ameongeza kuwa dampo hilo lipo pia jirani na Shule ya Msingi Mlowo na hivyo wanafunzi hupita na kuchezea hapo hali ambayo wangeweza kudhuriwa na vipande vya chupa na taka ngumu zinazo mwagwa hapo huku wengine wakiokota na kula mabaki ya vyakula yanayotupwa hapo na hivyo kuhatarisha afya zao.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Azindua Soko la Madini Chunya

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Soko la Madini Chunya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.
Kutoka kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula wakifungua kitambaa kama ishara ya uzinduzi wa Soko la Madini Chunya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (katikati waliokaa mbele) Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (wa pili kushoto waliokaa mbele) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi ( wa nne kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya mara baada ya uzinduzi wa soko hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (katikati waliokaa mbele) Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (wa pili kushoto waliokaa mbele) na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi ( wa nne kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa madini ya dhahabu Chunya mara baada ya uzinduzi wa soko hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi (katikati) mara baada ya kuzindua Soko la Madini la Chunya lililopo Mjini Chunya Mkoani Mbeya tarehe 02 Mei, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akisoma hotuba ya uzinduzi kabla ya kuzindua Soko la Madini Chunya.
Watendaji kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Idara nyingine za Serikali wakifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Soko la Madini Chunya iliyokuwa inatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila. (hayupo pichani).
Sehemu ya wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa Soko la Madini Chunya wakifuatilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa inatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila. (hayupo pichani).

……………………

Na Greyson Mwase, Chunya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amezindua Soko la Madini Chunya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wilaya ya Chunya kuhakikisha imekamilisha na kuzindua soko la madini ndani ya kipindi cha siku saba. Rais Magufuli alitoa agizo hilo tarehe 27 Aprili, 2019 wilayani Chunya katika mkutano wake na wachimbaji na wachenjuaji wa madini.

Uzinduzi huo ulishirikisha Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Anthony Tarimo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Migodi kutoka Wizara ya Madini, Ali Ali.

Wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, Dk. Venance Mwase, wawakilishi wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya habari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Msanjila alisema kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.

Akielezea mafanikio ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa rasilimali za madini, Profesa Msanjila alisema kuwa, ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufahika na rasilimali za madini, Serikali ilitunga Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili Namba 5 ya Mwaka 2017; Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi Namba 6 ya mwaka 2017 pamoja na kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123.

Aliendelea kueleza kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.

Alisema kuwa, kuwekwa kwa mazingira mazuri ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali zinazofikia asilimia 23 kutaondoa utoroshwaji wa madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.

Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila aliwataka wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini kuendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.

Akielezea manufaa ya soko jipya la madini Chunya, Profesa Msanjila alisema soko litaziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa Soko la Madini Chunya kutawezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la kuuza na kununua madini.

Profesa Msanjila aliendelea kufafanua manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa na kuondoa vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.

“Soko hili litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana, nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli tu” alisema Profesa Msanjila.

Katika hatua nyingine Profesa Msanjila aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Chunya, wafanyabiashara wa madini kwa kuhakikisha Soko la Madini Chunya limezinduliwa ndani ya muda uliopangwa.

Wakati huo huo akizungumzia hali ya uanzishwaji wa masoko ya madini nchini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alisema kuwa, hadi kufikia sasa masoko matano ya madini yameshafunguliwa katika mikoa ya Geita, Singida, Kahama, Arusha – Namanga na Chunya.

Aliongeza kuwa masoko mengine ya madini yanatarajiwa kufunguliwa kabla ya tarehe 05 Mei, 2019 ikiwa ni pamoja na Soko la Madini ya Dhahabu na Vito vya Thamani Ruvuma, Soko la Madini Shinyanga, Soko la Madini Dodoma na Soko la Madini Mbeya. Profesa Kikula alitaja masoko mengine ambayo yanatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kuwa ni pamoja na Soko la Madini ya Bati (tin) na Soko la Madini ya Dhahabu Handeni.

Alisisitiza kuwa mikoa mingine ipo katika hatua za mwisho kukamilisha vigezo mbalimbali vikiwemo vya kiusalama na miundombinu.

TUMIENI HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA KUTAFUTA MIKOPO YA UWEKEZAJI–DC UYUI

$
0
0

  Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Gift Msuya akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo jana katika Kijiji cha Miyenze.

Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akieleza faida za mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui Mkoani Tabora wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo jana katika Kijiji cha Miyenze.

Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui mkoani Tabora kikitoa burudani wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wakulima wa Kijiji ya Miyenze yaliyoandaliwa na Kuratibiwa na Ofisi ya Rais MKURABITA ili kuwawezesha wakulima hao kuwa na kilimo chenye tija.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wazee maarufu wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo jana baada ya kukabidhi hati 100 kwa wakazi wa eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wakulima waliopata hati miliki za kimila za kumiliki ardhi wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo.
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Miyenze wakimsikiliza jana Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa hafla ya ugawaji wa hati za hakimiliki za kimila za ardhi kwa wakazi 100.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Masele Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Rufunga Maguki. Picha na WHUSM

………………….
NA TIGANYA VINCENT ,TABORA

WAKAZI wa Kijiji cha Miyenze wilayani Uyui wametakiwa kutumia hati za hakimiliki za kimila walizopewa kuomba mikopo kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi ili kujiletea maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa Kijiji cha Miyenze na kukabidhi hati za hakimiliki ya ardhi za kimila kwa wakazi 100.

Alisema wakazi walipata hati za haki miliki hizo za kimila wanao usalama wa zao za ardhi na wameiongezea thamani ambayo inawafanya kuwa na fursa za kupata pesa. Msuya aliongeza kuwa hati hizo zitawasaidia kupata dhamana hata kwenye vyombo vya kisheria kama vile Mahakama pindi wanatakiwa kuweka mali isiyo hamishika.

Alisema hati walizopata ni fursa pia ya kuwawezesha kuingia ubia na wawekezaji mbalimbali ambao wanatafuta ardhi inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuwekeza katika sekta za viwanda, hoteli, maduka na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa Kijiji hicho na maeneo mengine katika wilaya hiyo ambao mashamba yao hayajapimwa kuhakikisha wanaypima ili kuyaongezea thamani na kuwaondoa katika umaskini na kupunguza migogoro.

Alisema hakuna haja ya wananchi kukumbatia maeneo makubwa ambayo hayajapimwa kwa kuwa hayawezi kuwasaidia kupata maendeleo yao na nchi kwa ujumla kwa kuwa ni sawa na mali mfu.

Kwa upande wa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema kuwa pamoja na kutoa hati hizo watawajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 jinsi ya kuendesha kilimo bora na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara.

Alisema maeneo mengine ni jinsi ya kutafuta fursa na kuzitumia na ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na uandishiwa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi.

Naye mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Miyenze William Mauye aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupima mashamba yao na hatimaye kuwapatia hati za haki miliki za kimila kwa kuwa zitawasaidia kuinua kipato chao kwa kuwa watakuwa na fursa ya kupata mikopo ya benki.

Alisema mkopo atakaochukua utamwezesha kununuza zana za kilimo za kisasa kwa ajili ya kuboresha kilicho chake cha mpunga na mahindi na hivyo kuongeza uzalishaji.

Mauye aliiomba Serikali kupitia MKURABITA kuendelea kuwasaidia wananchi wa vijiji ili wapimie ardhi yao na kuepuka baadhi ya watu ambao wakuwa wakichukua fedha zao bila hata kuwapimia maeneo yao.

ARUMERIU YAOMBOLEZA KIFO CHA MZEE MENGI

Reginald Mengi na safari ya ufukara mpaka utajiri

$
0
0
"Nimezaliwa katika umasikini wa kutupwa, lakini jambo hilo hata siku moja halikunikatisha tamaa," ni moja ya kauli ambazo Reginald Abraham Mengi alikuwa hacoki kuzisema kila alipopata wasaa wa kuzungumzia alipotokea maishani.

Ni jambo hilo pia ndilo lilomsukuma kuchapisha kitabu cha maisha yake mwaka 2018 kiitwacho I can, I must, I will (Ninaweza, Lazima nifanye, Nitafanikisha) kinachoangazia historia ya maisha yake toka alipozaliwa mpaka kufanikiwa kibiashara.

Mzee Mengi amefariki Jumatano usiku jijini Dubai, Falme za Kiarabu alipokwenda kwa matibabu, familia yake imethibitisha.Umauti umemfika akiwa na umri wa miaka 77, huku akicha mke na watoo wanne.

Reginald Mengi ni jina kubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, lakini wajua ametokea wapi.

Mengi alizaliwa wilayani Machame, Kilimanjaro, Tanzania mwaka 1942, akiwa mmoja wa watoto saba wa Bw Abhraham Mengi na Bi Ndeekyo Mengi.

"Familia yetu ilikuwa masikini sana, kila siku ilikuwa ni vita ya kupambana na umasikini. Tulimiliki sio zaidi ya ekari moja tukiishi kwenye vibanda vya udongo tukichanganyika na ng'ombe wachache na kuku. Ninaporudisha fikra na kutazama nyuma ni vigumu napatwa na ugumu wa kufikiri namna tulivyoweza kuishi katika hali ile," alipata kusema kwenye uhai wake.

Alianza safari yake kielimu shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School. Kwa ufadhili wa Chama cha Ushirika kilichokuwa na nguvu ya kifedha ushawishi KNCU Mengi alisomeshwa masomo yake ya shahada ya kwanza ya uhasibu nchini Uingereza.

Baada ya masomo ughaibuni, Mengi alirudi Tanzania 1971 na kuajiriwa na kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ( sasa Prince water house Cooper) mpaka mwaka 1989 alipoamua kujikita kwenye ujasiriamali.

VGS 20 WAPATIWA MAFUNZO YA UJASILIAMALI NAMTUMBO

$
0
0
NA Yeremias Ngerangera ,Namtumbo.

Askari 20 wanaosaidia kazi ya uhifadhi katika vijiji (VGS)hivi karibuni walipatiwa mafunzo ya ujasiliamali wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao pamoja na kuiendeleza jamii .

Mafunzo hayo yalikuwa ya siku nne yaliyolenga kuwapa ujuzi ,maarifa na stadi juu ya ujasiliamali ili kuwaepusha na vishawishi visivyo vya lazima na kujikita katika kazi zao pamoja na kujiongezea kipato.

Waliopata mafunzo hayo walikuwa 20 ambapo kati ya hao wasichana walikuwa 5na wavulana 15 huku mada za ujasiriamali zilizokuwa zinafundishwa zilikuwa kumi na tatu.

Chuo cha kijamii cha uhifadhi wa maliasili Likuyusekamaganga ndio eneo lililotumika kutolea mafunzo hayo huku Ofisi ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ndiyo iliyohusika kutoa mtaalamu wa kutoa mafunzo hayo.

Perez Kamugisha mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alisema idara yake ilimteua Buyeke Rutaihwa kutoa mafunzo hayo ya siku nne kwa VGS hao.

Kamugisha alidai vijana waliopatiwa mafunzo ya siku nne ni vijana kutoka wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya ,Sikonge mkoa wa Tabora na Manyoni mkoa wa Singida.

Wakiongea kwa niaba ya VGS wenzao Lucy Moses na Ramadhani Issa walidai mafunzo hayo yamewasaidia kuwaongezea uelewa wa namna ya kuepuka vishawishi na namna ya kujikita katika ujasiriamali ili kujiongezea kipato katika jamii.

Hata hivyo VGS hao walimhakikishia mwendesha mafunzo hayo kuwa watazingatia mafunzo waliyopata kwa muda wa siku nne na kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyofundishwa ili kujiongezea kipato jamii zao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Buyeke Rutaihwa kutoka katika idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo aliwapongeza VGS wote hasa kwa kufanya vizuri mitihani yao iliyotokana na mafunzo hayo na kufauri vizuri na kisha kuwataka kwenda kutumia mafunzo hayo waliyoyapata kwa vitendo ili kujiongezea kipato katika familia zao na jamii kwa ujumla aliwaambia Buyeke.

Katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo VGS wanapatikana katika jumuiya za uhifadhi (WMA)zilizopo katika Halmashauri ya wilaya Namtumbo ambazo ni Kimbanda,Kisungule na Mbarang”andu .

TUMIENI HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA KUTAFUTA MIKOPO YA UWEKEZAJI–DC UYUI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Kijiji cha Miyenze wilayani Uyui wametakiwa kutumia hati za hakimiliki za kimila walizopewa kuomba mikopo kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi ili kujiletea maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa Kijiji cha Miyenze na kukabidhi hati za hakimiliki ya ardhi za kimila kwa wakazi 100.

Alisema wakazi walipata hati za haki miliki hizo za kimila wanao usalama wa zao za ardhi na wameiongezea thamani ambayo inawafanya kuwa na fursa za kupata pesa.

Msuya aliongeza kuwa hati hizo zitawasaidia kupata dhamana hata kwenye vyombo vya kisheria kama vile Mahakama pindi wanatakiwa kuweka mali isiyo hamishika.

Alisema hati walizopata ni fursa pia ya kuwawezesha kuingia ubia na wawekezaji mbalimbali ambao wanatafuta ardhi inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuwekeza katika sekta za viwanda, hoteli, maduka na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa Kijiji hicho na maeneo mengine katika wilaya hiyo ambao mashamba yao hayajapimwa kuhakikisha wanaypima ili kuyaongezea thamani na kuwaondoa katika umaskini na kupunguza migogoro.

Alisema hakuna haja ya wananchi kukumbatia maeneo makubwa ambayo hayajapimwa kwa kuwa hayawezi kuwasaidia kupata maendeleo yao na nchi kwa ujumla kwa kuwa ni sawa na mali mfu.

Kwa upande wa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema kuwa pamoja na kutoa hati hizo watawajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 jinsi ya kuendesha kilimo bora na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara.

Alisema maeneo mengine ni jinsi ya kutafuta fursa na kuzitumia na ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na uandishiwa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi.

Naye mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Miyenze William Mauye aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupima mashamba yao na hatimaye kuwapatia hati za haki miliki za kimila kwa kuwa zitawasaidia kuinua kipato chao kwa kuwa watakuwa na fursa ya kupata mikopo ya benki.

Alisema mkopo atakaochukua utamwezesha kununuza zana za kilimo za kisasa kwa ajili ya kuboresha kilicho chake cha mpunga na mahindi na hivyo kuongeza uzalishaji.

Mauye aliiomba Serikali kupitia MKURABITA kuendelea kuwasaidia wananchi wa vijiji ili wapimie ardhi yao na kuepuka baadhi ya watu ambao wakuwa wakichukua fedha zao bila hata kuwapimia maeneo yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Gift Msuya akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo jana katika Kijiji cha Miyenze.
 Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akieleza faida za mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui Mkoani Tabora wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo jana katika Kijiji cha Miyenze.
 Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui mkoani Tabora kikitoa burudani wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wakulima wa Kijiji ya Miyenze yaliyoandaliwa na Kuratibiwa na Ofisi ya Rais MKURABITA ili kuwawezesha wakulima hao kuwa na kilimo chenye tija.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wazee maarufu wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo jana baada ya kukabidhi hati 100 kwa wakazi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wakulima waliopata hati miliki za kimila za kumiliki ardhi wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo.
  Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Miyenze wakimsikiliza jana Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa hafla ya ugawaji wa hati za hakimiliki za kimila za ardhi kwa wakazi 100. PIX7. Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Masele Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Rufunga Maguki. Picha na WHUSM

FAINALI YA MAVUNDE CUP KIKUYU KASKAZINI YAIBUA VIPAJI,MBUNGE MAVUNDE AAHIDI MAKUBWA

$
0
0
Fainali ya Mavunde Cup kata ya Kikuyu Kaskazini imemalizika jana kwa kishindo kikubwa kwa Timu ya Kikuyu Football Club kuibuka kidedea na kunyakua ubingwa huo baada ya kuitandika Timu ya St John’s University kwa bao moja kwa bila katika Mchezo uliochezwa katika Viwanja vya Chuo kikuu cha St John’s na kuhushuriwa na maelfu ya wananchi wa Dodoma.

Akihitimisha mashindano hayo,Mfadhili wa mashindano hayo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amezipongeza timu zote kwa ushiriki wao na kuonesha uwezo mkubwa wa vipaji vikubwa kwa muda wote wa mashindano na kuahidi kwamba atahakikisha anaendelea kuvikuza na kuvilea vipaji hivyo ili Vijana hao pia waweze kufikia malengo yao katika mchezo wa mpira wa miguu ambao sasa umekuwa ni fursa ya Ajira kwa Vijana wengi.

Akishukuru kwa niaba ya Vijana wenzake,Mratibu wa mashindano hayo *Comrade Elibariki **alimshukuru Mbunge Mavunde kwa Ufadhili wa mashindano hayo na vifaa vya michezo kwa Timu *10 ambazo zimeshiriki katika mashindano haya lakini pia na namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Vijana katika Jimbo la Dodoma Mjini katika nyanja mbalimbali.

MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA MUUNGANO WA TANZANIA SAUDI ARABIA

$
0
0
Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh nchini Saudi Arabia iliadhimisha miaka 55 ya MUungano wa Tanzania kwa shuguli mbalimbali yakiwemo maonyesho ya utamaduni wa Mtanzania, vyakula vya asili ya Tanzania, utalii na bidhaa za kilimo na zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania. 
Balozi Hemedi Mgaza akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi, Viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio Riyadh wakiwapokea wageni waalikwa waliohudhuria siku hiyo.
Balozi Hemedi Mgaza akiwa na mgeni rasmi Meya wa Jiji la Riyadh Eng. Tariq Al Faris wakisimama kwa heshima wakati nyimbo za taifa za Tanzania na Saudi Arabia zikiimbwa.
Baadhi ya wakinamama Watanzania na wanadiaspora walioandaa sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano mjini Riyadh.
Wageni walikwa wakiwemo Watanzania wanaofanya kazi nchini Saudi Arabia na wanadiplomasia wakisikiliza hotuba wakati wa maadhimisho hayo.
Balozi wa Tanzania ncini Saudi Arabia Hemedi Mgaza akiwa na mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanzania Meya wa Jiji la Riyadh Eng Tariq Al Faris wakikata keki kuzindua shere za maadhimisho.
 Wageni walikwa waliofika katika Ukumbi wa Utamaduni (Diplomatic Quarters Cultural Palace Hall) wakisikiliza hotuba ya Balozi iliyozungumzia kuitangaza Tanzania katika utalii, utamaduni, uwekezaji, masoko ya bidhaa za Tanzania na shughuli za madakatari wa hisani.
Mabalozi wawakilishai wa nchi za Cameroon, Nigeria na Ghana wakiwa na Balozi wa Tanzania wakionja vyakula vya asili ya Tanzania vilivyoandaliwa na Watanzania waishio Riyadh.
Baadhi ya bidhaa za utamaduni wa Tanzania zilizoonyeshwa wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanzania.

TFDA YATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATI KIFO CHA DKT REGINALD MENGI

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA TLS- AG

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, amesema, Serikali inatambua mchango wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika ( TLS) katika kuimarisha na kudumisha Utawala wa Sheria nchini. Akasema wakati wote Serikali ipo tayari kupokea maoni na ushauri kutoka TLS ilimradi kwamba, maoni au ushauri huo unajikita katika kujenga, kuimarisha, hauegemei upande wowote, wenye staha na usio na mashinikizo.

“ Kwanza niwashukuru sana kwa kuja kukutana na kufanya mazungumzo nami, niwapongeze wewe Rais kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa TLS pamoja na wote mliochaguliwa katika baraza la uongozi. Ni matumaini yangu kwamba, hamtawaangusha wanachama wenu waliowachagua, msiwaagushe tafadhali” Akasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuongeza

“Wakati wote Serikali imekuwa ikithamini sana mchango wenu na maoni yenu. Na kwa kweli mmekuwa mkitoa mchango na maoni mazuri sana, niwahakikishe kwamba Serikali wakati wote ipo tayari kushirikiana nanyi. Jambo la muhimu ni kuwa na majadiliano ( dialogue) pale ambapo mnaona kunajambo la kujadiliana kabla ya kulitolea matamko.

“Niwahakikishe kwamba, Serikali kwa ujumla na hasa Mhe. Rais John Pombe Magufuli katika uongozi wake anapenda sana Sheria na anataka mambo yafanyike kisheria na kwa kuzingatia sheria ” akasisitiza Profesa Kilangi Profesa Kilangi ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumza na ujumbe wa Balaza la Uongozi la TLS likiongozwa na Rais wake Dk. Rugemeleza Nshala.

Mazungumzo kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ujumbe wa Balaza la Uongozi yaliyochukua zaidi ya masaa matatu, yalifanyika siku ya Alhamisi katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mitumba- Ihumwa Jijini Dodoma. “Niwaombe sana katika uongozi wenu msimamie sana weledi wa tasnia ya Sheria, hili nawaomba sana, sisi sote ni maofisa wa Mahakama, ni katika mkutadha huu tunatakiwa kutekeleza majukumu yetu ya uofisa Mahakama kwa welidi wa hali ya juu sana na kwa kuzingiatia misingi na maadili ya kazi zetu. Lisimamieni sana hili, simamie professionalism” akasisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais wa TLS Dk, Rugemeleza Nshala pamoja na kumshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwakubalia ombi lao na kukutana nao. Alisema kuna mambo kadhaa ambayo walitamani au waliona ni vema wakabilishana naye mawazo. Dk Nshala aliyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na kuangalia namna bora itakayowawezesha TLS na wadau wengine wa Sheria nchini, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kushirikiana katika kuhakikisha kwamba Mawakili wa kujitegemea na Mawakili wa Serikali wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia maadili na miiko ya kazi zao.

Jambo jingine ambalo Dk. Nshala kwa niaba ya jumbe wake aliliwasilisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni la namna ya kuangalia jinsi ya kuifanyia marekebisho baadhi ya vifungu vya Sheria ya TLS hasa katika kifungu cha uchaguzi wa Viongozi unaotakiwa kufanyika kila mwaka. “Katika mkutano wetu wa Arusha wanachama tulilijadili hili la uchaguzi wa kila mwaka, ni hitajio la kisheria lakini gharama za kukutana kila mwaka ni kubwa sana na zinabebwa na wanachama, hivyo tulijadiliana kuona namna gani tunaweza kuliboresha hili kwa kujadiliana na wadau wengine na kwa kuangalia mifano ya nchi nyingne akasema “ Rais wa TLS.

Dk. Nshala pia alizungumzia kuhusu mitaala ya mafunzo Sheria katika Vyuo Vikuu na kushauri kwamba wadau wa Sheria wanapashwa kukaa na kujadiliana namna bora ya kuuboresha ili iendane na wakati. Kwa mujibu wa Rais huyo wa TLS amesema kwa uzoefu wake na katika utekelezaji wa majukumu yake kuna mifano hai ya mapungufu ya kiutendaji kwa kwa baadhi ya mawakili ambayo mengi kati ya hayo ni ukosefu wa mafunzo Stahiki

Katika hilo la uboreshaji wa mfumo wa ufundishaji, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema anakubaliana nalo kwa asilimia kubwa, na kwamba , tatizo ambalo yeye analiona ndiyo changamoto kubwa katika tasnia ya Sheria ni mafunzo kwa vitendo. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Kilangi na Uongozi wa TLS walijadili pia kuhusu namna bora ya kuhakikisha kwamba Sheria zinazofanyiwa urekebu na mara zikisha pitishwa na Bunge Ofisi ya Mwanasheria Mkuu isisambaze ili zinawafikia wadau kwa wakati.

Vile vile walibadilishana mawazo kuhusu haja na umuhimu wa kuzifanyia urekebu baadhi ya Sheria ambazo zinamatatizo au changamoto katika utekelezaji wake. Baadhi ya Sheria hizo ni pamoja na baadhi ya vifungu vya Sheria ya Jinai na Sheria ya Usuluhishi wa migogoro nje ya Mahakama.

Walibadilishana mawazo pia kuhusu mazingira ya utendaji kazi wa Mawakili hasa mawakili wa kujitegemea ambao Dk. Nshala alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopashwa kutafutiwa ufumbuzi. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Evaristo Longopa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na Utoaji wa Huduma Dk. Gift Kweka.
 Ujumbe wa Baraza la Uongozi la TLS wakiwa katika mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni kuhusu namna bora ya kuhakikisha sheria ambazo zimefanyiwa urekebu na baada ya kupitishwa na Bunge zinawafikia wadau kwa wakati. Pia walijadiliana kuhusu haja na umuhimu wa kuzifanyia urekebu wa baadhi ya sheria zenye changamoto.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akisisitiza kwa Baraza la Uongozi la TLS likiogozwa na Rais wake Dk. Rugemeleza Nshala kwamba Serikali itashirikiana na TLS,Wakati Baraza hilo lilipomtembelea na kufanya mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ofisini kwake Mitumba- Ihumwa Jijini Dodoma. Mazungumzo hayo yalifanyika jana alhamisi.
  Rais wa TLS Dk. Rugemeleza Nshala akimkabidhi Mwanasheria Mkuu wa Serikali shajala za TLS mara baada ya mazugumzo yao yaliyowajumuisha pia wajumbe wa Baraza la Uongozi la TLS.
Picha ya pamoja baada ya majadiliano baina ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Baraza la Uogozi wa TLS. Walioketi mbele kuanzia kushoto ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Evaristo Longopa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, Rais wa TLS Dk. Rugemeleza Nshala na CEO wa TLS. Picha na habari kwa hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI TANZANIA IKULU ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania Maniza Zamani, alipofika Ikulu Zanzibar, kuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi Nchini, kushoto akiwa na Mwakilishi wa UNICEF anayefanyika Kazi zake Zanzibar Maha Damaj.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania  Maniza Zamani, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi Tanzania akiwa na Mwakilishi wa UNICEF Anayefanyika kazi zake Zanzibar B. Maha Damaj.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa picha na Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania  Maniza Zamani , yenye Ujumbe Unaoashiria Upendo kwa Watoto, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumuaga leo.3-5-2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa nac mgeni wake Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania  Maniza Zamani, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini Tanzania.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania  Maniza Zamani, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo,3-5-2019.(Picha na Ikulu)

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, akifurahia jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Stella Ikupa, Bungeni jijini Dodoma Mei 3, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, Bungeni jijini Dodoma Mei 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma Mei 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Katibu Mkuu Wizara ya Madini azindua Soko la Madini Chunya

$
0
0
Na Greyson Mwase, Chunya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amezindua Soko la Madini Chunya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wilaya ya Chunya kuhakikisha imekamilisha na kuzindua soko la madini ndani ya kipindi cha siku saba. Rais Magufuli alitoa agizo hilo tarehe 27 Aprili, 2019 wilayani Chunya katika mkutano wake na wachimbaji na wachenjuaji wa madini.

Uzinduzi huo ulishirikisha Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi,  Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Anthony Tarimo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Migodi kutoka Wizara ya Madini, Ali Ali.

Wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, Dk. Venance Mwase, wawakilishi wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya habari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Msanjila alisema kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.

Akielezea mafanikio ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kwenye usimamizi  wa rasilimali za madini, Profesa Msanjila alisema kuwa,  ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufahika na rasilimali za madini, Serikali ilitunga Sheria ya Mamlaka ya Nchi  Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili Namba 5 ya Mwaka 2017; Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi Namba 6 ya mwaka 2017 pamoja na kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123.

Aliendelea kueleza kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.

Alisema kuwa, kuwekwa kwa mazingira mazuri ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali zinazofikia asilimia 23 kutaondoa utoroshwaji wa madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.

Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila aliwataka  wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini  kuendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali  za Serikali katika kutekeleza majukumu  yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali  inayotolewa na Serikali.

Akielezea manufaa ya soko jipya la madini Chunya, Profesa Msanjila alisema soko litaziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa Soko la Madini Chunya kutawezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la kuuza na kununua madini.

Profesa Msanjila aliendelea kufafanua manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa na kuondoa  vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa  vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.

“Soko hili litaondoa  uwezekano wa wanunuzi  wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya  kuwa na madini wakati hawana, nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli tu” alisema Profesa Msanjila.

Katika hatua nyingine Profesa Msanjila aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Chunya, wafanyabiashara wa madini kwa kuhakikisha Soko la Madini Chunya limezinduliwa ndani ya muda uliopangwa.

Wakati huo huo akizungumzia hali ya uanzishwaji wa masoko ya madini nchini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alisema kuwa, hadi kufikia sasa masoko matano ya madini yameshafunguliwa katika mikoa ya Geita, Singida, Kahama, Arusha – Namanga na Chunya.

Aliongeza kuwa masoko mengine ya madini yanatarajiwa kufunguliwa kabla ya tarehe 05 Mei, 2019 ikiwa ni pamoja na Soko la Madini ya Dhahabu na Vito vya Thamani Ruvuma, Soko la Madini Shinyanga, Soko la Madini Dodoma na Soko la Madini Mbeya.

Profesa Kikula alitaja masoko mengine ambayo yanatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kuwa ni pamoja na Soko la Madini ya Bati (tin) na Soko la Madini ya Dhahabu Handeni.

Alisisitiza kuwa mikoa mingine ipo katika  hatua za mwisho kukamilisha vigezo mbalimbali vikiwemo vya kiusalama na miundombinu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi (katikati) mara baada ya kuzindua Soko la Madini la Chunya lililopo Mjini Chunya  Mkoani Mbeya tarehe 02 Mei, 2019.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akisoma hotuba ya uzinduzi kabla ya kuzindua Soko la Madini Chunya.
 Watendaji kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Idara nyingine za Serikali wakifuatilia hotuba  ya uzinduzi wa  Soko la Madini Chunya iliyokuwa inatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila. (hayupo pichani).
 Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa Soko la Madini Chunya wakifuatilia hotuba  ya uzinduzi iliyokuwa inatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila. (hayupo pichani).
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Soko la Madini Chunya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.
 Kutoka kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula wakifungua kitambaa kama ishara ya uzinduzi wa Soko la Madini Chunya.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (katikati waliokaa mbele) Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (wa pili kushoto waliokaa mbele) na   Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi ( wa nne kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya mara baada ya uzinduzi wa soko hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (katikati waliokaa mbele) Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (wa pili kushoto waliokaa mbele) na   Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi ( wa nne kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara wa madini ya dhahabu Chunya mara baada ya uzinduzi wa soko hilo.

MBUNGE JUMANNE KISHIMBA AJITOSA KUUCHAMBUA MFUMO WA ELIMU,ATAKA UANGALIWE UPYA

$
0
0
*Asisitiza  wenye digrii ni kama viazi vilivyoshindwa kuiva...aeleza changamoto ya ajira kwa waliosoma

*Aweka wazi elimu ya sasa haina tofauti na kifungo cha maisha, ambacho wanafunga wazazi na watoto

Na Ripota Wetu,Michuzi TV

HATIMAYE Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, mkoani Shinyanga Jumanne Kishimba (CCM), ameamua kujitosa kwa kuzungumzia mfumo wa elimu uliopo sasa ambao umeshindwa kumwandaa mwanafunzi kujitegemea na kwamba hiyo ni dalili mbaya kwa Taifa la Tanzania.

Kishimba amesema umefika wakati l kwa Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kuangalia namna bora ya kutoa elimu ya kumwandaa mwanafunzi pamoja na kuangalia mitaala ya elimu kama inakidhi vigezo vya elimu na ikiwezekana ifanyiwe maboresho.

Amefafanua ni bora akazungumzia mfumo wa elimu kwani wengi wamekuwa wakiogopa kueleza ukweli,lakini kwake anaona ni wakati wa mfumo wetu wa elimu kuangaliwa upya kama ambavyo amewahi kushauri Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Akizungumza bungeni Mjini  Dodoma, wakati anachangia mjadala wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Kishimba amesema kuwa alishtushwa na taarifa ya watu 40,000 kuwasilisha maombi ya ajira 70 zilizotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivi karibuni.

Amesema suala hilo linapaswa kuisikitisha, kuiogofya na kuishangaza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na vyuo vikuu kwa sababu kama waombaji ni 40,000 na wanaopata kazi ni 50 hawa wengine wanakwenda wapi.

“Elimu yetu hii tulirithi kutoka kwa wakoloni Waingereza, haina pingamizi. Waingereza wakistaafu watu 900,000, watakaomaliza shule au ‘University’ (chuo kikuu) watakuwa milioni moja, kwa hiyo 900,000 watapata kazi hawa 100,000, Serikali inaweza kuwatunza na kuwahifadhi, lakini kwetu wanaomaliza shule wanaweza kuwa milioni moja wanaopata kazi ni 50,000, "amesema.

Ameongeza kuwa “Kwahiyo tukiendelea na utaratibu huu mwenyekiti tunatengeneza bomu kubwa, kwenye suala hili naona kila mtu anaogopa kupasema, lakini ukweli mwenyekiti ni vizuri tukubaliane na Wizara ya Elimu ambao wao ndio watunga sera za elimu, iundwe kamati au tume ambayo itachunguza suala la elimu kwa Tanzania".

Kishimba ameongeza kuwa “Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amejaribu kuliongelea hili suala mara mbili mara tatu, lakini naona watu hawalichukulii uzito, lakini mwenyekiti watu 40,000 kama wangekuwa Uwanja wa Taifa wakasema hawatoki mle uwanjani, utakuwa na kazi ngumu ya kuwatoa." 

Mbunge huyo aliyekuwa anachambua mfumo wa elimu kwa kujiamini huku wabunge wakionesha kuguswa na mchango wake ili kuboresha elimu ya Tanzania, ametoa ushauri kutungwa sera mpya ya elimu itakayowawezesha kujifunza shughuli za biashara, kilimo na ufugaji badala mfumo uliopo sasa ambao mwanafunzi anahitimu elimu ya juu kwa kupewa cheti ambacho hakimwezeshi kupata ajira popote.

Kishimba amesema mfumo huo unapaswa kuhakikisha kuwa asilimia 50 ya maksi wanafunzi wazipate katika masomo hayo na asilimia 50 zitokane na masomo ya darasani.

Aeeleza kwamba  mfumo huo utamsaidia mwanafunzi pale anapohitimu masomo yake ya sekondari au chuo kikuu, akiambiwa akajitegemee anakuwa na sababu ya msingi ya kufanya hivyo kwa sababu atakuwa akifahamu akajitegemee vipi.

“Lakini leo kumwambia mtu mwenyekiti aende akajitegemee, wewe umechukua fedha zake za ‘University’ alafu wewe ukampa unayosema ni digrii, lakini kiukweli umempa karatasi, ni sawa sawa na mtu amecheza Deci, hii digrii hakuna mahala inapotambuliwa popote, hata kama unaumwa huwezi kuiweka dhamana famasi, huwezi kuiweka dhamana benki, sasa inawezekana kweli?

“Binafsi  nimesomesha mtoto wangu, nimeuza mifugo yangu, nimelipa milioni 10, wewe umenipa digrii halafu wewe unaniacha mimi nikazunguke mtaani na ile digrii. Mimi mwenyewe ni mwathirika wa hizo digrii, ninao watoto sita wana digrii, kwa kweli mwenyetiki inahuzunisha sana, ingekuwa bora watunga sera tukubaliane kwamba vyuo vikuu kabla havijatangaza nafasi za shule zikatafute ajira zenyewe.

"Zieleze na mishahara, ziseme tumepata NBC mshahara ni Sh 800,000, tumepata NSSF Sh 500,000, sasa tunaanza kusajili, leta milioni tano nikupe digrii kazi hii hapa,” amesema na kuongeza suala hilo linaweza kuonekana kama la kuchekesha, lakini hali ni mbaya mitaani kwa sababu watu wanazo digrii kila kona, hawana ajira.

Pia amesema  muda wa kusoma vilevile watunga sera waangalie ni nani alifanya ‘research’ kwamba ubongo wa binadamu unahitaji kila mwaka darasa moja, kama yupo atwambie. "Wakati huu nafasi za ajira hakuna unachukuliwa mtoto wako miaka 17, unarudishiwa ana miaka 25 mnaambiwa katafuteni kazi ya kujitegemea, mnajitegemeaje mwenyekiti?

“Kama watakubali watunga sera mwaka mmoja wasome madarasa matatu au manne ili watu wamalize shule mapema, itatusaidia sana ili mtu akimaliza shule arudi huku tuje tuendelee na maisha kijana akiwa bado mdogo. Leo wanakaa naye muda wote wanakuja kukurudishia wewe ana miaka 25," amesema.

Kishimba amesema ukienda kwenye familia zilizoathirika kwenye suala hilo la elimu ukasema elimu ni ufunguo wa maisha watasema hapana elimu ya Tanzania ni kifungo cha maisha, maana ni kifungo kigumu, umefungwa wewe, amefungwa mtoto, amefungwa mama na fedha zimeenda, wote mna vyeti viko ukutani na majoho ya siku ya ‘graduation’, cha kufanya hamna mnatazamana.

Amesema kuwa lengo lake si kubeza elimu, lakini ni lazima yafanyike mabadiliko makubwa na kwamba nchi nyingi duniani zina matatizo kama hayo ikiwamo Afrika Kusini kwa sababu wao pia wamefuata mfumo huo wa elimu wa Uingereza ambao unakwenda kwa mfumo wa sukuma, sukuma, sukuma na kupewa cheti, lakini hakuna kitu wanachokipata.l

Pia kwa sasa wanapokwenda kwenye majimbo vijijini wakiuliza ni mtoto gani ana faida kati ya aliyesoma na ambaye hajasoma, wanajibu kuwa ambaye hajasoma ndiye mwenye faida kijijini, anayefuata wa darasa la saba, kisha wa kidato cha nne ndiyo anafuata wa chuo kikuu.

Ameongeza  kuwa wananchi wanasema mhitimu wa chuo kikuu ni kama viazi vilivyoshindwa kuiva kwa sababu hawezi kufanya kazi yoyote ikiwamo kulima, anabaki kusubiri ajira ambazo hazipo.

“Kama zimetangazwa nafasi 50 walioomba ni 40,000 na hawa ndio wana e-mail na internet, je ambao hawana e-mail na internet na walioghairi. Je, watu hawa wako wapi sasa hivi na wanafanya nini?” alihoji.

Alisema kuwa waziri amekuwa akisema anaboresha elimu, lakini hajui ni elimu ipi inayoboreshwa kwa sababu waliohitimu hawajapata kazi.

“Bidhaa inaboreshwa pale ambapo bidhaa uliyopeleka sokoni wateja wamesema tunataka bidhaa ya aina fulani. Ukisema unataka kuboresha elimu, unaboresha ipi kama watu walio bora hawajapata kazi,” amesema.

MWILI WA DKT. REGINALD MENGI KUWASILI NCHINI JUMATATU MEI 6, 2019

$
0
0
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi utawasili nchini Jumatatu 6, 2019 na ndege ya Shirika la ndege la Emirate ukitokea Dubai, Falme za Kiarabu, Mwanasheria wa familia ya Dkt. Mengi, Bw. Michael Ngalo amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 3, 2019. 

Mwili wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia akiwa huko Dubai usiku wa kuamkia Mei 2, 2019, ukishawasili jijini Dar es Salaam, utahifadhiwa kwenye hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo na siku inayofuata yaani Jumanne Mei 7, 2019, shughuli ya kuaga mwili huo itafanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar. 

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa baada ya shughuli hiyo ya kutoa salamu za mwisho, mwili wa Dkt. Mengi utasafirishwa Jumatano Mei 8, 2019 kuelekea mahala alikozaliwa Machame, Mkoani Kilimanjaro ambapo shughuli za mazishi zitafanyika Alhamisi Mei 9, 2019.

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA DKT REGINALD MENGI

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UPANUZI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA MBEYA MKOANI SONGWE

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria upanuzi wa Kiwanda cha Saruji cha Mbeya kilichopo Songwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Saruji inayotengenezwa na kiwanda cha Saruji cha Mbeya kilichopo Songwe. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Songwe wakati akielekea kwenye kiwanda cha Saruji cha Mbeya ambapo aliweka jiwe la msingi la upanuzi wa kiwanda hicho.
PICHA NA IKULU

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS) JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dkt. Rugemeleza Nshala alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dkt. Rugemeleza Nshala (katikati) na Mjumbe wa Chama hicho, Ndg. Harold Sungusia walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akizungumza na Ugeni kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi ya ‘note book’/daftari ndogo ya dondoo kutoka kwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dkt. Rugemeleza Nshala alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu
Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa sita kulia) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa tano kulia ni Rais wa Chama hicho, Dkt. Rugemeleza Nshala

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

UJERUMANI YATOA MSAADA WA SH. BILIONI 330 KWA AJILI YA MRADI WA MAJI MKOA WA SIMIYU

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
SERIKALI ya Ujerumani kupitia Benki yake ya  Maendeleo (KfW), imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 127.7, sawa na sh. bilioni 330, kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria katika mkoa wa Simiyu.

Makubaliano ya msaada huo kupitia mikataba miwili yamesainiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, (KfW) anayeshughulikia nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya, Dkt. Klaus Mueller.

Katika mkataba wa kwanza, kiasi cha Euro 102.7, sawa na shilingi bilioni 265 kimetolewa na Mfuko wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Green Climate Fund) na mkataba wa pili unahusisha Euro milioni 25, sawa na sh. bilioni 65 ambazo zimetokelewa na Benki ya Maendeleo ya UJerumani (KfW).

Mbali na mradi wa maji  wa Simiyu ambao chanzo chake cha maji ni kutoka Ziwa Victoria, miradi mingine itakayonufaika na msaada huo ni kilimo endelevu cha umwagiliaji, usafi wa mazingira, maji na malisho ya mifugo na kuzijengea uwezo taasisi zitakazotekeleza mradi huo hasa mamlaka za maji katika Wilaya tano za Bariadi, Itilima, Meatu, Busega na Maswa zitakazonufaika na mradi huo.

"Kutokana na umuhimu wa mradi huo wa maji, Serikali kwa upande wake itachangia Euro milioni 40.7 sawa na sh. bilioni 104 na wananchi watakao nufaika na mradi huo watachangia Euro milioni 1.5 sawa na sh. bilioni 3.8 na kufanya gharama za mradi mzima kufikia zaidi ya Euro milioni 171 sawa na zaidi ya sh. bilioni 446" alisema Bw. Doto James

Aliishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia Mfuko wake wa Kimataifa wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi (GCF) na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) kwa kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kitakachotumika kutekeleza mradi huo utakachukua miaka mitano hadi kukamilika kwake.

"Katika kipindi cha miaka  mitatu Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania zaidi ya Euro 202.8 sawa na shilingi bilioni 518.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, nishati, uhifadhi wa maliasili, udhibiti wa fedha za umma na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi" alisisitiza Bw. James

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya KfW amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Mfuko wa Kimataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutoa kiasi kikubwa cha fedha cha Euro milioni 102.7 kwa mkupuo katika nchi za kiafrika tangu mfuko huo uanzishwe.

"Tunaamini kuwa zaidi ya watu 500,000 watanufaika na mradi huu wa maji kutoka Ziwa Victoria unaohusiana na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kutuhifadhi vyanzo vya maji, usafi wa mazingira, kuendesha kilimo bora chenye kuhifadhi mazingira" aliongeza Dkt. Mueller.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuipatia Wizara yake zaidi ya shilingi trilioni 3 katika kipindi kifupi cha miaka mili kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji inayoendelea kujengwa nchini kote.

Alitaja sababu za mkoa wa Simiyu kunufaika na msaada huo kuwa ni mkoa unaokabiliwa na hali mbaya ya hewa ukiwemo ukame na kwamba mradi huo utawawezesha wananchi kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kwamba katika ukanda huo wa Ziwa kutakuwa na miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.2 itakayokuwa inatekelezwa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Mahamoud Mgimwa amesema Bunge litahakikisha linausimamia mradi huo utekelezwe kwa wakati kwa sababu Serikali imedhamiria kwa dhati kuona kwamba wananchi wanapata maji safi na salama kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakisaini Mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi  wa maji kutoa Ziwa Victoria kupitia mradi wa kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia nchi katika Mkoa wa Simiyu, hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)  na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakibadilishana mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji katika Mkoa wa Simiyu, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)  na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakionesha mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji katika Mkoa wa Simiyu baada ya kusainiwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), akieleza kuwa licha ya msaada wa Sh. bilioni 330 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW), kwa ajili ya  mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Mkoa wa Simiyu, Serikali ya Tanzania itachangia kiasi cha Euro milioni 40.7 ambayo ni sawa na Sh. 104.1 kutokana na umuhimu wa mradi huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mahamouud Mgimwa (Mb)(wapili kushoto), Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedhja na Mipango Bw. John Rubuga (wa pili kuli) na Kamishna wa Sera wa Wizara hiyo Bw. Mgonya Benedicto wakiwa katika  hafla ya utiwaji saini mikataba miwili yenye jumla ya kiasi cha Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji katika Mkoa wa Simiyu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, akieleza kuwa Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  zitawanufaisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kupitia miradi ya maji, kilimo cha umwagiliaji na usafi wa mazingira, wakati wa hafla ya kusaiiniwa kwa msaada wa fedha hizo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti  wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Mahamoud Mgimwa (Mb), akieleza kuwa msaada wa Sh. bilioni 330 zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi utasaidia kuondoa malalamiko ya mda mrefu ya wabunge wa wilaya zitakazonufaika na mradi huo kuhusu ukosefu wa maji Mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati)  na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Benki ya KfW ya Ujerumani baada ya kukamilika kwa hafla ya kusainiwa mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria kwenda Mkoa wa Simiyu.

(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Latest Images