Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Airtel Money Branch kutumika kusajili bure laini za Airtel kwa kutumia alama za vidole nchini nzima

$
0
0
*Usajili wa laini za Airtel kwa kutumia alama za vidole ni BURE kwa wote.

Dar es Salaam Alhamisi 2 Mei 2019 … Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetangaza maduka ya Airtel maoney Branch kila kona rasmi kusajili laini za simu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole kwa mteja walioko kila mkoa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuanza kwa zoezi hilo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “Kama utakumbuka mwaka jana Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilizindua mfumo huu kwa majaribio. TCRA pia siku hiyo ilitoa mwongozo kwa makampuni yote ya simu kuweka utaratibu na kufanya usajili wa laini za simu mpya kwa kutumia mfumo huu mpya katika maeneo ya mikoa sita ya majaribio. Baada la zoezi hilo serikali ilitoa taarifa za kuanza usajili kwa kutumia alama za vidole kwa wateja wote. Leo hii Airtel Tanzania tunatangaza rasmi kuanza kwa zoezi hili kwenye Airtel Money Branch zaidi ya 600 pamoja na maduka ya Airtel yote bila gharama yoyote yaani BURE”

“Usajili huu wakisasa unaotumia alama za vidole ni wa uhakika zaidi na vigumu kughushi, ni muhimu sana wateja wote wapya ambao wanajiunga na Airtel kwa sasa kusaijili kwa mfumo huu’ alisema Mmbando.

Vile vile Airtel itaweka vituo maalum kwenye maeneo ya taasisi za serikali na ofisi za makampuni mbalimbali kurahizisha zoezi hili. Kadhalika, makampuni na taasisi zinaweza kuomba kutembelewa na Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel ili kufanyiwa usajili kwenye maeneo yao ya kazi kwa kuwa sisi tunathamini muda wa wateja wetu tutajipanga na tutakwenda’ alisema Mmbando.

“Wateja wetu hasa wale wa zamani tunawasihi kuhakiki taarifa zenu za usajili kwa kupiga *106# endapo taarifa zako za usajili haziko sahihi tembelea duka letu lililopo karibu yako ili kukamilisha usajili wako kwa kutumia mfumo huu mpya wa kutumia alama za vidole” aliongeza Mmbando.

“Tunasisitiza Usajili huu ni bure na unaendelea kwenye Airtel Money Branch zote na maduka yote ya Airtel, mteja anachotakiwa kuwa nacho ili kusajili ni kitambulisho cha uraia au namba ya kitambulisho kutoka NIDA, alisema Mmbando

Tunaendelea kuongeza Maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 600 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini. Ni imani yetu tutaendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kadri muda unavyokwenda.
 Wakazi wa jijini Dar es Salaam wanaotumia Mtandao wa simu wa Kampuni ya Airtel wakifanya usajili katika makao Makuu kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Usajili wa alama za vidole umeanza juzi na utaendelea hadi Decemba mwaka huu.
 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson MMbando akiongea na baadhi ya wateja waliojitokeza jana katika maduka ya Airtel ili kusajili laini zao kwa alama za vidole na kuwashauri kutembelea pia maduka ya Airtel huduma kwa mteja zaidi ya 20yalioko popote karibu nao pamoja na Airtel Money branch zaidi ya 600. Usajili wa alama za vidole umeanza juzi na utaendelea hadi Decemba mwaka huu.

WIKI YA NENDA KWA USALAMA KUZINDULIWA KESHO SIMU 2000

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Jeshi la Polisi nchini kanda maalum ya Dar es Salaam kitengo cha usalama barabarani, kesho kitazindua kampeni yake ya wiki ya nenda kwa usalama katika viwanja vya kituo cha Daladala simu 2000.

Akizungumza na Waandishi wa habari kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani kanda Maalum ya Dar es Salaam Marison Mwakyoma amesema uzinduzi huo utafanyika sambamba na ukaguzi wa magari katika eneo hilo.

“tunawaalika wakazi wote wanaotumia vyombo vya moto na ambavyo vinapita barabrani kufika katika viwanja vya Simu 2000 maarufu kama Mawasiliano kwa ajili ya kupata elimu ya usalama barabarani na taratibu zingine ambazo jeshi la polisi imeziandaa"amesema Mwakyoma

Akizungumza kwa niaba ya Wasanii wa filamu nchini Mwenyekiti wa kundi la Uzalendo kwanza Steve Nyerere amesema moja ya vitu vitakavyofanyika kesho ni wasanii wote wakiongozwa na yeye watafika katika eneo hilo kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi wa magari yao.

Amesema ni jambo la aibu msanii anatembea barabarani uku gari yake ikiwa haijakaguliwa, hivyo anatoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam na wasaniii wote kujitokeza kwa wingi 

kwa upande wake mkuu wa kituo cha ukaguzi wa mabasi Ubungo Ins Ibrahim Samwix ametaja kuwa yeye na askari wengine wamejipanga vizuri hivyo kuwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wale waliokuja kutembea kujitokeza kwa wingi ili waweze kukaguliwa magari yao.
Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam Marison Mwakyoma akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya wiki ya Uslama barabarani ytakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya simu 2000 maarufu kama Mawasiliano
 Mkuu wa  Kituo cha Ukaguzi wa mabasi cha ubungo , Ibrahim Samwix akieleza jinsi walivyojipanga kufanya ukaguzi katika wiki ya nenda kwa usalama  
 Msanii wa Filamu na Vichekesho ambaye ni mwenyekiti wa kundi la Uzalendo kwanza, Steve Nyerere akizungumza uwepo wa Wasanii katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama pale mawasiliano
Mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam akitoa Maoni yae juu ya wiki ya nenda kwa usalama

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA HOSPITALI, AZUNGUMZA NA WANANCHI WA INYALA, IGURUSI, MSWISWI NA CHIMALA WAKATI AKIELEKEA MBARALI MKOANI MBEYA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako kuashiria uzinduzi wa Hospitali ya Uamsho wa Wakristo Tanzania (UWATA) iliyopo Mwakibete jijini Mbeya ambayo inatoa huduma za afya kwa mkoa wa Mbeya pamoja na nchi jirani za Zambia na Malawi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya, Wabunge, Mawaziri, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hospitali ya Uamsho wa Wakristo Tanzania (UWATA) iliyopo Mwakibete jijini Mbeya ambayo inatoa huduma za afya kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya pamoja na nchi jirani za Zambia na Malawi.

 Mandhhari ya hospitali ya UWATA iliyopo jijini Mbeya ambayo inatoa huduma za afya kwa mkoa wa Mbeya pamoja na nchi jirani za Zambia na Malawi.



  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika katika uzinduzi wa Hospitali ya UWATA jijini Mbeya mara baada ya kuizindua.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Inyala wakati akiwa njiani kuelekea Igurusi mkoani Mbeya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mswiswi wakati akiwa njiani kuelekea Chimala.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Igurusi hawaonekani pichani mara baada ya kuwasili katika eneo hilo akitokea jijini Mbeya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Chimala Wilayani Mbarali mkoani Mbeya. PICHA NA IKULU

UMOJA wa wanawake wajasiliamali 'SINGLE MOTHERS'waendelea na mafunzo jijini Dar es salaam.

$
0
0
Mwenyekiti wa umoja huo Neema Steven amesema ni muhimu wanawake wangejitambua na kujua changamoto ambazo wanazikabili bila kuwepo kwa wenza wao na badae kutafuta suluhisho ili kusaidia familia zao pasipo kujihusisha na vitendo viovu kama kushiriki kwenye uchangudoa na wizi.

Pia ameweka bayana jinsi kikundi hicho mbali na kupatiwa mafunzo ya ujasiriliamali wanawake hao pia wanafundishwa jinsi ya kujitambua,kujiari,kupatiwa mitaji kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali na kupatiwa masoko nje na ndani ya nchi kupitia biashara zao.

"Ni fursa sasa Kwa wanawake nchi kote kujiunga na umoja huo ambao utaleta mabadiliko katika familia zao na taifa kwa ujumla na kupunguza idadi ya omba omba barabarani na badala yake wanawake kujiari ili kupata fedha zitakazowawezesha kujikimu kiuchumi," alisema steven.

Aidha, ameeleza kuwa tayari kwenye warsha hiyo ya siku tano itawawezesha wanawake ambao tayari wameshajiunga kwenye kikundi hicho kupika chakula ambacho kitauzwa kwa bei nafuu lengo likiwa ni kukusanya fedha hizo na kusaidia watoto yatima kwenye vituo mbalimbali nchini ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali wameshaunga mkono Jambo hilo .

" Wasanii wengi kama dayna,madee,dk.cheni wameshafika kwenye warsha hii na wamelipia vyakula hii ikiwa ni mchango ambao umeingia kwenye mfuko wa kikundi wenye lengo la kusaidia watoto yatima," alimalizia steven


Kwa upande wake msanii wa tasnia ya bongofleva ambae alijizolea umaarufu kutokana na kujihusisha na Uhusiano wa kimapenzi na mvulana mwenye umri mdogo hollystar ,sister Fay amesema licha ya kuwa na mikasa ya kuwa ni miongoni mwa wanawake ambao wanatunza familia zao pamoja na watoto bila kuwepo kwa baba au waume zao.

"Ifike pahala wasanii tushiriki kwenye majukumu ya kijamii sio kuwapa burudani tu au kutaka kulipwa pesa katika majukumu au shughuli za kijamii tu bali kuna muda tuwe tunaisaidia na kujitoa kwa hali na mali kusaidia jamii inayotuzunguka," alisema fey.

Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wanaolea familia pasipo kupata ushirikiano kutoka kwa mzazi mwenzie ina lengo la kupunguza kasi ya madanguro ,pamoja na wanawake wanazurura mitaani kwa ajili ya kutafuta riziki kwa familia zao

Hata hivyo ametoa rai kwa wanawake wote ambao wangependa kujiunga na kikundi hicho kuwa ni sehemu salama na utaweza kupata mafunzo ya kujitambua na elimu juu ya kuanzisha biashara na jinsi ya kukuza biashara yako pamoja na kupatiwa mitaji na masoko.
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiAliamali hasa wanaotafuta ridhiki na kulea familia pasipo kupata msaada kutoka kwa mzazi mwenzie Neema Steven pamoja na mdau wa kikundi hicho ambae ni msanii wa bongofleva sister fey wakizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanawake wanaolea familia zao bila kuwepo kwa mzazi mmoja (SINGLE MOTHER'S)

KC,UZALENDO KWANZA KUWAMILIKISHA WASANII ARDHI

$
0
0

 Mwenyekiti wa kundi la Uzalendo Kwanza na Mugizaji wa Filamu Nchini, Steve Nyerere akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Makubaliano ya Wasaniii wa kampeni ya uzalendo kwanza na kampuni ya KC Land Development Plan Ltd kuhusu Mpango wao wa kukopeshwa Viwanja kwa gharama nafuu pasipokuwa na riba Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya KC Land Development Plan Ltd,Khalid Mwinyi akitoa maelezo juu ya mradi na Viwanja vitakavyojulikana kama mji wa Wasanii Msaniii wa na Meneja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akieleza ni namna gani bendi yake itakavyotumbuzi siku ya chakula cha pamoja baina ya Wasanii na Kampuni ya KC Land Development Plan Ltd Msanii mkongwe wa Filamu nchini Chick Mchoma akieleza faida za wasanii watakaochukua Viwanja vya Kampuni ya KC Land Development Plan Ltd ambavyo vinalipwa ndani ya miaka miwili kwa gharama nafuu Msanii mMahaurufu wa mvchezo wa Bongo Dar es Salaam, Kuwa Kikumba maharufu kama Dude akieleza nini kama wasanii watakwenda kufanya kuhakikisha kuwa wanamiliki viwanja hivyo  Promota wa Mchezo wa Ngumi ambaye ni Mwanachama wa kundi la Uzalendo kwanza akieleza faida za Viwanja hivyo kwa mabondia ambao wamekuwa wakipata pesa na kufanya anasa pasipo kumiliki ardhi Msanii wa kike wa Siku nyingi Maya akieleza namana wasanii wakike watakavyokwenda kumiliki nyumba zao na kuacha kunyanyasika Wasanii kwa pamoja wakiwa wamesimama kama ishara ya kumkumbuka Mzee Reginald Mengi aliyetutoka usiku wa kuamkia leo.Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki mkutano huo wakitimiza majukumu yao kama wanavyoonekana pichani

DAMPO LA ILEMBO LITACHAFUA MAJI- RC MWANGELA

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imetakiwa kubadilisha mahali pa kutupa takataka (dampo) kutoka eneo la Ilembo lilipo sasa kwakuwa maji yanayotiririka kutoka katika eneo hilo yanaweza kuelekea katika chanzo cha maji cha Mantengu ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika muda si mrefu.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji iliyopo Wilayani humo.

Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema zoezi la kubadilisha eneo lakutupa takataka lifanyike haraka kwakuwa mradi wa Maji wa Vwawa ambao unatumia chanzo cha Maji cha Mantengu umekamilika na hivi karibuni utaanza kuwafikia wananchi.

“Ile sehemu ya dampo ibadilishwe, maji yameshaanza kutoka na yatawafikia wananchi hivi karibuni, hivyo nawaagiza halmashauri utekelezaji wa hili ufanye haraka,”amesisitiza Brig. Jen. (Mst) Mwangela

Ameongeza kuwa licha ya kuwa eneo la kutupa takataka litabadilishwa lakini wahakikishe wanazoa takataka zilizopo kwakuwa zikibaki pale zitaendelea kuchafua maji.

“Ili chanzo cha Mantengu kibaki salama na maji yawe salama zile takataka zitolewe mara baada ya kuhamisha dampo, licha ya kuwa tunafahamu kuna utaratibu wa kuyachuja na kuyawekea dawa maji hayo bado kuna baadhi ya sumu haziwezi kumalizwa na madawa hayo”, amefafanu Brig. Jen. (Mst) Mwangela

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Mbozi itatekeleza agizo hilo na sasa eneo la kutupa takataka litahamishiwa Mbozi Mission ili kulinda chanzo hicho cha maji cha Mantengu.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akipanda katika tenki la maji litakalotumika katika mradi wa maji wa Vwawa-Mantengu wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.

NI PIGO KWA TAIFA... VIONGOZI WA SERIKALI WABUNGE WAMLILIA DK. REGINALD MENGI....

$
0
0


*Wasema atakumbukwa kwa wema wake, kujitoa kwa kusaidia jamii ya Watanzania
*Wengine wasema ameacha somo...
Nape akumbuka kikao chao cha mwisho

 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


VIONGOZI wa ngazi mbalimbali nchini katika Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na wabunge wamesema wamesikitisha na taarifa za kifo cha mfanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi.

Mengi aliyezaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo(Mei 2,2019) akiwa Dubai katika moja ya nchi za Falme za Kiarabu.
Akizungumzia kuhusu taarifa za kifo cha Mengi, Rais Dk.John Magufuli amesema " Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dk. Reginald Mengi. 

"Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo ktk kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara."
Wakati huo huo Makau wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema moja ya vitu alivyotuachia Mzee Mengi ni ule wepesi wake wa kusaidia masuala ya kijamii na kwamba Watanzania daima atakukumbuka.

Kwa upande wake Mbunge wa Mtama mkoani Lindi Nape Nnauye amesema kuwa Mengi ameacha alama kubwa."Nimejifunza mengi kwako, Rafiki, Mshikaji, Kiongozi na Mzazi! Ulinifundisha kuwa kukata tamaa ni dhambi! 

"Msalimie mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu Cha mwisho nyumbani kwako.Pumzika kwa Amani Dk. R.A Mengi,"amesema Nape wakati anaelezea masikitiko yake kutokana na kifo cha mzee Mengi. 

Akizungumzia kifo cha Mengi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Januari Makamba amesema "Pole kwa Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins - na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi."

Kwa upande wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hivi " Pumzika kwa amani Dk.Reginald Mengi, asante kwa ushirikiano mzuri ulionipatia katika kutekeleza majukumu yangu lakini zaidi kwa kunihimiza mara kwa mara nitamani/kufanya mambo makubwa. 

"Pengo lako ni gumu kuzibika! Pole nyingi kwa Madam JNtuyabaliwe ,watoto, ndugu, jamaa na marafiki. Poleni sana,"amesema Waziri Mwalimu.
Naye aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumzia kifo cha Mengi ametoa pole kwa wana familia, ndugu, jamii na marafiki wa Mengi kutokana na taarifa za kifo chake.

"Hakika, siku za maisha yetu zimehesabiwa na kuandikwa kitabuni. Ameimaliza safari yake hapa duniani. Iwe heri kwake huko ng'ambo ya mto. RIP baba yetu,"amesema Nyalandu.

Kwa upande wake Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa haijalishi tunaishi muda gani hapa duniani, cha msingi unatoa mchango gani hapa duniani kabla ya kifo. "Dk.Mengi si tu uliwavutia wengi ,bali uligusa sana maisha ya wengi , umetuonesha kuziacha jamii zetu bora zaidi kuliko tulivyo zikuta.Pumzika kwa Amani,"amesema.

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amesema " Msiba mkubwa kwa Taifa na haswa kwa familia ya Mzee Reginald Mengi. Pole sana JNtuyabaliwe na Watoto, The twins. "Poleni sana Regina, Abdiel na familia nzima ya Makampuni ya IPP. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi mahala pema anapostahili."

Mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji 'MO' ameandika hivi "Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un. Mwenyezi Mungu ampe pumziko na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Ameen.RIP Mengi."

Kwa upande wa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema watu wanagopa kifo, kimsingi tunacho ogopa ni kuwahi kufa kwani kifo hakizuiliki.
"Katika maisha ni vyema kuishi maisha ya baraka na watu wote,ili utakapotangulia maisha yako yaweze kuwa na thamani. Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dk. Mengi,kwani alijua thamani ya ubinadamu,"amesema Lema.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee amesema amepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha ndugu Reginald Mengi.Ametoa pole kwa familia , ndugu, jamii na marafiki.

"Mwaka 2019 unaendelea kuwa wa majonzi kwetu kama Taita, tunapoteza watu makini waliokuwa na mchango mkubwa sana katika ujenzi wa nchi yetu.Upumzike kwa amani Mkuu,"amesema Mdee.
Katika Enzi za Uhai wake Dkt Reginald Abraham Mengi akiwa na familia yake. 

EAGLES SEKONDARI YAFICHUA MBINU YA KUWAJENGA WANAFUNZI

$
0
0
*Yajiegemeza katika kujenga maadili na kuwatumia wanasaikolojia kama mbinu mbadala ya adhabu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

MAADILI na malezi katika kuwakuza  vyema vijana katika sekta ya elimu imeelezwa kuwa ni nyenzo muhimu ya kuwajenga na kuwandaa vijana   ambao ndio nguzo kwa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya sekondari ya wavulana Eagles iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani Adam Mgonde amesema kuwa katika kuhakisha zao linalotokana na elimu nchini linakuwa bora zaidi shule hiyo imeenda mbali zaidi kwa kuwa na mtaalamu wa ushauri nasaha (mwanasaikolojia) pamoja ushauri na kuwahudumia watoto wote shuleni hapo.

Amesema kuwa watoto wa kipindi hiki ni tofauti sana kwa kuwa wanajua mambo mengi kutokana na maendeleoya sayansi na teknolojia na kuwaadhibu wanapokosea sio suluhisho bali ni kuwaelekeza kuhusiana na maadili mema pamoja na malezi.

Aidha amesema kuwa baada ya serikali kuridhia mabadiliko kadhaa ya muundo wa shule hiyo rasmi wameandaa tahasusi mpya kabisa ambazo hazikuwahi kutolewa nchini pamoja na masomo na hiyo inakuja baada ya malengo ya taifa kuelekea uchumi wa viwanda ambao unahitaji wataalamu wa kutosha.

Akieleza kuhusu masomo na tahasusi zilizoongezwa Mgonde amesema kuwa masomo ya kilimo yameanza kutolewa shuleni hapo na kwa kushirikiana na ubalozi wa Ufaransa wameanzisha somo la Kifaransa mwaka huu na ifikapo Julai tahasusi ya KLF (Kiswahili, English Language na French) itatolewa shuleni hapo.

Kwa upande wake mwalimu wa biashara na mkuu wa Masoko shuleni hapo Gadi Lameck amesema kuwa tahasusi mpya za masomo ya sayansi yanayojumisha masomo ya kompyuta zitatolewa kwa mara ya kwanza shuleni hapo na hiyo ni katika kwenda sambamba na matakwa ya taifa ya kujenga uchumi imara wa viwanda na wao kama Eagles High School wanatoa mafunzo kwa kilimo kwa utendaji ili kuzalisha vijana wenye mawanda mapana ya kusaidia taifa.

Katika kukuza sekta ya elimu nchini imeshauriwa kukuza malezi ya vijana, maadili, ubunifu na afya njema ili kutimiza ndoto za kizazi cha kesho na nguzo ya taifa.
 Mkuu wa shule ya sekondari ya wavulana Eagles Adam Mgonde (katikati) akizungumza na wanahabari kuhusiana na kukuza sekta elimu, leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa shule ya Sekondari ya wavulana Eagles, Adam Mgonde wakati akiwasilisha taarifa ya uboreshwaji wa sekta ya elimu katika shule hiyo leo jijini Dar es Salaam.

MKUTANO WA SABA WA TAPSEA WAANZA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakifatilia mada mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa na wakufunzi kutoka nyanja tofauti katika siku ya kwanza ya Mkutano wao wa saba, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha. Kauli mbiu: 'Tutumie muda wetu vizuri kufanyakazi kwa ufanisi na kuleta tija kazini'.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akizungumza jambo katika siku ya kwanza ya Mkutano Mkuu Chama hicho, ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha. 
Mhadhiri wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles George Magaya akizungumza wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa "Katibu Mahsusi kutunza siri na mzalendo katika kazi na Taifa kwa ujumla" wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha. 
Wakili wa Serikali, Berious Nyasebwa akizungumza wakati akiwasilisha mada yake iliyoelezea "Umuhimu wa Haki za Binadamu na Utawala Bora" wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha.

















































IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA ZA RUNGWE NA KYELA MKOANI MBEYA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo ambapo IGP Sirro aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akinunua matunda kutoka kwa mmoja wa wajasiliamali katika eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani humo kwa lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajasiliamali ndogo ndogo katika eneo la Ushirika, Tukuyu mkoani Mbeya leo, IGP Sirro yupo mkoani hapa kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akikagua gwaride aliloandaliwa kwa ajili yake wakati alipowasili katika Kituo Kikuu cha Polisi wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Claudia Kitta, wakati alipowasilia wilayani humo kwa ziara ya kikazi yeye lengo la kuona utendajikazi unaofanywa na askari wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.


Je, Arsenal watawaweza Valencia?

$
0
0
Timu za Uingereza zina nafasi ya kuandika historia kwa kuwa ligi ya kwanza Ulaya kuingiza vilabu vinne kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa na Europa. Liverpool na Tottenham Hotspur bado ziko kwenye ligi ya mabingwa, wakati Alhamisi hii Arsenal na Chelsea zinacheza na Valencia na Eintracht Frankfurt kwenye nusu fainali za ligi ya Europa.

Arsenal wamepoteza michezo mitatu mfululizo kwenye ligi ya Uingereza – kipigo cha mwisho wakikipata dhidi ya Leicester kwa mabao 3-0 walipotembelea dimba la King Power. Kipigo hicho kimefifisha matumaini ya Arsenal kumaliza katika nafasi nne za juu ili kuweza kushiriki ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matumaini yao ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao ni kushinda Europa pekee. Wanacheza dhidi ya Valencia dimbani Emirates katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali huku Valencia wakiwa katika nafasi ya uhakika kushiriki lii ya mabingwa msimu ujao.

Kocha wa Arsenal Unai Emery alisema walijisikia vibaya kupoteza dhidi ya Crystal Palace, Wolves na Leiceste City “Lakini tunahitaji kuendelea. Tuna ligi mbili ambazo bado tunahitajika kucheza vizuri ligi ya Uingereza na Europa. Zote hizi zina nafasi ya kutufikisha kwenye ligi ya mabingwa ambalo ndio lengo letu.

“Tunatakiwa kuendele kuwa imara kiakili na kujiamini kwamba tunaweza,” alisema. Chelsea ni timu ambayo imenufaika na kiwango kibovu cha Arsenal, hivyo wameweza kujiimarisha katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi – wao watacheza dhidi ya Eiintracht Frankurt.
Timu hiyo kutoka ligi ya Bundesliga sio ya kupuuzwa, ushindi wao dhidi ya Inter Milan na Benfica kwenye hatua zilizopita inaonyesha jinsi gani walivyo wazuri. Ikiwa ndiyo timu pekee kutoka Bundelsiga katika mashindano ya Ulaya, matumaini yote ya Ujerumani yapo mabegani mwao hivyo Chelsea watakuwa na kazi ya ziada kuwatoa.

Chesea wanacheza mchezo huu baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United Jumapili iliyopita. Eden Hazard anasema yeye pamoja na wachezaji wenzake wataingia katika mchezo huo wakiwa na kujiamini zaidi baada ya mchezo wa Man United. “Ilikuwa ni vizuri (sare dhidi ya United) ila tungeweza kufanya vizuri zaidi” alisema baada ya mchezo. “Sare sio matokeo mabaya kwetu nadhani kama tungejiamini zaidi tungepata bao jingine na kushinda mchezo”

Mechi hizi zitaonyeshwa kupitia StarTimes pekee. Arsenal vs Valencia utakuwa LIVE kupoitia ST World Football saa 4:00 Usiku na Eintracht Frankfurt vs Chelsea LIVE kupitia ST Sports Premium saa 4:00 Usiku. Kwa wateja wa Antenna ni kifurushi cha UHURU kwa Tsh 18000 tu na wateja wa Dish ni kifurushi cha SMART kwa Tsh 21,000.

RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA MAJENGO YA OFISI ZA SMZ PEMBA

$
0
0
 MAJENGO ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliojengwa katika eneo la Gombani Kisiwani Pemba Wilaya ya Chakechake yaliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Magengo Matatu ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilioko katika eneo la Gombani Wilaya ya Chakechake Pemba, kulia Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kufungua majengo ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kushoto Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa na kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Khamis Juma Maalim, wakishiriki katika ukataji wa utepe huo wakati hafla ya ufunguzi wa majengo hayo.(Picha na Ikulu)

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri wa Ujenzi wa Majengo Matatu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ndg. Mbarouk Juma, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Majengo hayo eneo la Gombani Pemba.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiuliza mswali wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa majengo hayo katika eneo la Gombani Pemba.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mjenzi wa Majengo ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ndg. Khamish Ali Khamis, ( na kushoto Mshauri Elekezi wa Mradi wa Ujenzi huo Ndg. Mbarouk Juma.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Kaimu Afisa Mdhamini Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Pemba Ndg. Hakim Vuai Shein, kulia, wakati akitembelea jingo la Wizara hiyo.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea majengo hayo baada ya kuyafungua rasmin leo kisiwani Pemba katika eneo la Gombani.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mjenzi wa Majengo hayo wakati alitembelea majengo hayo baada ya kuyafungua rasmin leo.(Picha na Ikulu)

UBA yaadhimisha miaka 70 ya utumishi

$
0
0
LAGOS, NIGERIA

BENKI ya United Bank of Africa (UBA) imeadhimisha miaka 70 tangu ianze kutoa huduma za kibenki kwa wateja wake wakati wa sherehe zilizoongozwa na Mwenyekiti wa kundi la kampuni Tony O. Elumelu.

Sherehe hizo zilizohudhuriwa na wateja, wafanyakazi na marafiki pia zilienda sambamba na hafla ya utoaji Tuzo za kila mwaka za Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO).

Tuzo hizo zilitolewa mbele ya maelfu ya wageni kwa wafanyakazi wa UBA kutoka nchi zote 23 ambako inaendesha shughuli zake kutokana na utendaji wao uliotukuka wa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Miongoni mwa watu mashuhuhuri katika usiku huo pamoja na makadhi, magavana wa zamani na sasa wa majimbo mbalimbali ya Nigeria.

Aidha marais wa zamani Olusegun Obasanjo na Ibrahim Babaginda, ambao walishindwa kuhudhuria kutokana na dharura walituma barua za kuipongeza benki hiyo kwa ufanisi na mafanikio makubwa yaliyopatikana.

Mwenyekiti wa UBA Plc, Tony Elumelu, ambaye aliambatana na mkewe Dk. Awele, alisema UBA imebakia kuwa taasisi ya kifedha inayoongoza barani Afrika na kutimiza kwake miaka 70 ni mafanikio makubwa.

Alisema, “Huu ni wakati wa kusherehekea urithi tajiri wa kipindi cha miaka mingi na kumwambia kila mtu aliyechangia kile kinachoifanya UBA isimame imara leo hii, kuwa tunashukuru kwa yote na jinsi walivyohakikisha uwekezaji uliowekwa katika benki kipindi cha miongo iliyopita unalipa.”

Shukrani kama hizo zilitolewa pia na CEO wa Kundi la Kampuni, Kennedy Uzoka huku Mwenyekiti wa Benki ya Zenith, Jim Ovia, akiisifu menejimeni na wafanyakazi wa UBA kwa kuifikisha hapo ilipo. Ovia alisema; “ UBA inabakia kuwa moja ya benki kubwa kabisa Kusini mwa Sahara Afrika. UBA imeanzishwa kwa ajili ya kudumu. Nawapongeza wafanyakazi wote na wanahisa. Najuta kutonunua hisa za UBA, lakini nadhani sijachelewa kufanya hivyo.



Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya United Bank for Africa, Tony Elumelu, akifurahia jambo na washiriki wengine kwenye sherehe ya miaka 70 ya utoaji huduma kwa benki hiyo kwa nchi zaidi ya 50 za Afrika. Sherehe hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Lagos nchini Nigeria 

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA MAMIA YA WANANCHI WA MBARALI MKOANI MBEYA

$
0
0
  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Barafu Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kuwahutubia wanachi. 



 Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili katika uwanja huo wa mkatano wa Barafu.
 Wananchi wa Mbarali wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika uwanja wa Barafu.


 Sehemu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Barafu Mbarali kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Barabara ya TANZAM highway sehemu ya  Igawa-Mbeya eneo la Igawa ikiwa katika mandhari ya kupendeza mara baada ya ukarabati mkubwa wa Barabara hiyo. PICHA NA IKULU

RELI YA KATI NAYO YAUNGWA UPYA KWA UMEME KUTOKA DAR ES SALAAM HADI ISAKA


WASANII WA UZALENDO KWANZA WAHIMIZWA KUMILIKI VIWANJA VYA KC

$
0
0
 Na Khadija Seif, Michuzi TV

KAMPUNI  ya KC Land Development Plan imesema imejipanga ili kuweza kuwasaidia wananchi waishio katika hali ya chini Viwanja kwa bei rahisi, na imeahidi kuwapatia wasanii ambao ni wanachama wa Uzalendo Kwanza viwanja kwa ajili ya kumiliki ardhi na kupata makazi.

Akizungumza na waandishi wahabari Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Khalid Mwinyi amesema, wamefikia uamuzi huo lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Mwinyi amesema kwa sasa utoaji wa Viwanja hivyo utaanzia  mikoa ya Dar es Salaam, Pwani pamoja na  Dodoma na kwamba malipo yatakuwa ni kwa mwaka mmoja hadi miwili. Ametoa rai kwa wasanii wa Bongofleva pia kumiliki viwanja hivyo kwa bei  ambayo anahisi kila msanii ataweza kumudu kulipia.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Uzalendo Kwanza Steve Mengere maarufu kama Steve Nyerere ameshukuru kampuni hiyo kwa kuwaona kwenye jambo hilo muhimu na kuwapa kipaumbele. Amesema anaamini sifa kubwa kama msanii ni kumiliki Kiwanja, ambapo amemshukuru Mkurugenzi wa KC na kusema kuwa jambo hilo limekuja kwa wakati sahihi.
 "Nikweli wasanii tumekuwa tukitangatanga katika nyumba za kupanga tunawashukuru KC kwa kutuona na kutuwezesha kupata ardhi kwa kuwa heshima ni kuwa na nyumba na si gari, kaulimbiu yetu ni Maisha ni nyumba"alisema Steve. 
Aidha Kampuni hiyo imejipanga kufanya hafla ya chakula cha jioni katika ukumbi la Lamada siku ya mei 5,2019 lengo likiwa ni kuwaweka pamoja wasanii na kujadiliana nao jinsi ya upatikanaji wa viwanja hivyo na jinsi gani wataweza kuwa mabalozi wa wananchi na kuwahamasisha kumiliki viwanja vyao.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya KC Land  Khalid Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 02.05.2019

WAOMBOLEZAJI WAMIMINIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DKT. REGINALD MENGI, WAMMIMINIA SIFA LUKUKI

$
0
0
Waombolezaji wamesema Mwenyekiti wa makampuni ya IPP marehemu Dkt. Reginald Mengi atakumbukwa na Watanzania wote kwa jinsi alivyojitoa maisha yake kwa ajili ya maisha ya wengine, hasa wanyonge na wenye mahitaji maalumu.
Wamesema hayo walipomiminika nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es salaam kutoa pole na rambirambi kwa wafiwa. Dkt. Mengi alifariki dunia mapema asubuhi ya  Alhamisi akiwa Dubai kwenye matibabu.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema  wakati alipofika nyumbani hapo kwamba msiba wa Mengi ni mkubwa na umeligusa Taifa kutokana kwa  kujitoa kwake katika kuisaidia jamii. 
"Mzee Mengi alikubali kujitoa kwa watu maskini kwenye jamii ambapo aliahidi kuwajengea uwezo walemavu ili kuondokana na umaskini" amesema Makonda. "Matamanio yangu mazishi ya Mzee mengi watu wajitokeze kwa wingi ili kumuenzi mzee wetu huyu." 
Mkuu huyo wa mkoa amesema baada ya ratiba ya mazishi kufahamika kutoka kwa wanafamilia angependa watu wajitokeze kwa wingi kumpa marehemu upendo na heshima anayostahili. 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe amesema kifo cha Dkt. Mengi ni pigo kwa taifa na itakuwa vigimu kumpata mtu kama huyo kirahisi.
Akizungumza nyumbani hapo, Mhe.  Mbowe amesema ndugu wa karibu wa familia ndio wanaanza kufika hivyo taratibu nzima kuhusiana na msiba huu zitatolewa baadae"
Mhe Mbowe amesema Marehemu Mzee Mengi alikuwa mtu wa watu wote na kwamba alijali sana walemavu, wanamichezo pamoja na tasnia nzima ya mambo ya habari. 
 "Kwa niaba ya wanachi wa Moshi,wanachama wa vyama vyote hasa wanachama wa wa chadema pamoja na watanzania wote nitoe pole kwa walioguswa na msiba huu.
"Niwaambie tu itachukua miaka muda mrefu kuziba pengo aliloacha Mzee Mengi kwani alikuwa mdau wa uwekezaji aliyejali wanyonge na kuondoka kwake ni pigo kubwa kwa Taifa"amesema.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda  akiwasili kwenye Msiba wa Mwenyekiti wa kampuni za IPP Regnaldi Mengi nyumbani kwa marehemu Kinondoni  jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  akizungumza na waandishi wa habari leo alipofika kufariji wafiwa nyumbani kwa Dkt  Regnaldi Mengi Kinondoni  kufwatia kifo cha Mwenyekiti huyo aliefariki usiku wakuamkia Mei 2,2019 dubai.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mwanasheria wa familia,Michael Ngalu  akizungumz na waandishi wa habari ambapo amesema  kwa sasa maandalizi yanaendelea na kwamba taarifa za msiba zitatolewa kesho mchana.
 Waombolezaji wakiwa nymbani kwa  Dkt  Regnaldi Mengi Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakiwa katika majukumu yao nyumbani kwa Dkt  Regnaldi Mengi  Kinondoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)


DR. REGINALD ABRAHAM MENGI KWA UFUPI

$
0
0


Dr. Reginald Abraham Mengi alizaliwa katika kijiji cha Nkuu huko Machame, Kilimanjaro, Tanzania. Baba yake Mr. Abhraham Mengi alizaliwa Marangu, Kilimanjaro, Tanzania lakini baada ya babu yake kufariki ilitokea mivutano juu ya urithi hasa kwenye masuala ya ardhi hivyo alilazimika kuhamia Machame ambapo napo licha ya kukutana na changamoto nyingi lakini aliweza kukaa akatulia. 

Baba yake Mzee Abraham Mengi na mama yake Ndeekyo walibarikiwa watoto saba yeye Dr. Mengi akiwa kama mtoto wa tano kuzaliwa - yaani Apaanisa, Elitira, Asanterabi, Karileni, Dr. Mengi mwenyewe, Evaresta na Benjamin.


Dr. Mengi alianza shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School. Katika maisha yake ya shule tukio kubwa analolikumbuka ni wakati shule yao ya Old Moshi ilipohamishwa kutoka Old Moshi, Kolila na kuhamia Moshi mjini.



Baada kumaliza shule ya sekondari alipata ufadhili wa KNCU(Kilimanjaro Native Cooperative Union), alikwenda Uingereza kuchukua masomo ya uhasibu. Dr. Reginald Mengi ni moja kati ya watanzania wa mwanzo kabisa kusoma UK, Scotland na kufanikiwa kuwa Mhasibu anayetambulika na Taasisi ya Wahasibu ya Uingereza na Walesi



Mwaka 1971 Reginald mengi alirudi Tanzania na kuajiriwa kwenye kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ambayo kwa sasa inajulikana kama Prince water house Cooper. Baada ya kufanya kazi muda mrefu kwenye kampuni hiyo akiwa kama chairman and partner mwaka 1989 aliondoka kwenye kampuni hiyo na kwenda kuanzisha kampuni yake. Dr. Reginald Abraham Mengi ni mwanzilishi, mmiliki na Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Limited na Taasisi ya teknolojia na ugunduzi ya IPP(IPP Institute of Technology and Innovation).



Kupitia kampuni yake hiyo Reginald Mengi aliweza kumiliki vyombo mbalimbali vya habari mfano kwa upande wa TV alimiliki ITV, EATV na Capital Tv na kwa upande wa Radio anamiliki Radio one, Capital radio na EATV radio. Dr. Reginald Mengi alimiliki magazeti kadhaa, mfano wa magazeti hayo ni Nipashe, kulikoni, Taifa letu , The Guardian , Financial time na Sunday observer.



Mwaka 1992 Dr. Mengi alianzisha makampuni mengi zaidi yaliyokuwa yanazalisha bidhaa mbalimbali za kawaida ambazo zilikuwa ni adimu sana kwa wakati huo. Alikuwa tayari anamiliki biashara kadhaa ambazo ni;- Tanzania Kalamu Company Limited, Anche-Mwedu Limited, Tanpack Industries Limited, Industrial Chemicals Limited ambacho baadaye ilibadili jina na kuitwa Bodycare Limited pamoja na Bonite Bottlers Limited.



-Mwaka 1981 Dr. Mengi alianzisha kampuni kubwa ya uwekezaji iliyokwenda kwa jina la Mengi Associates Limited ambayo mwaka 1988 ilibadili jina na kuitwa Industrial Projects Promotion Limited na baadaye IPP Limited. IPP Limited kwa sasa ni jina linalojulikana sana Tanzania. Dr. Mengi anasema karibia fedha yote anayotumia kuanzisha makampuni haya inatokana na faida inayopatikana natoka kampuni zilizopo.



-Dr. Mengi alikuwa anasita sana kuwekeza katika vyombo vya habari kutokana na uhalisia wa mazingira ya kitanzania kisiasa lakini kufikia mwaka 1993 aliamua kuingia huko kwa kuanzisha Radio One, Itv kisha magazeti kama vile Nipashe, The Guardian n.k.



Reginald Mengi alimiliki viwanda baadhi ambavyo vinazalisha vinywaji mbalimbali hapa Tanzania. Alimiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji, Bonite Bottlers inayoongoza kwa kinywaji cha Coca-Cola na maji ya chupa ya Kilimanjaro. Dr. Mengi pia amewekeza katika madini, mafuta, gesi, gesi asilia, madawa, kilimo cha mboga mboga katika maeneo makubwa, magari(kuunganisha magari ya umeme), saruji na mambo mengine zaidi katika sekta ya utengenezaji(manufacturing sector).



Dr. Mengi amewahi pia kuwa katika nafasi kadhaa za uongozi wa umma ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa magazeti Tanzania(Chairperson of Tanzania Standard Newpapers); Kamishna wa kamati inayoshughulikia mishahara(Commissioner of Salary Review Commission); Mwenyekiti wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania(NBAA);  na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa La Mazingira Tanzania(National Environmental Council of Tanzania(NEMC)

Alikuwa pia Mwenyekiti wa Vyombo vya habari vya Jumuia ya Madola Tanzania(Chairman of the Tanzania Chapter Commonwealth Press Union(CPU)); Mkurugenzi wa bodi ya LEAD(Leadership for Environment and Development International); Kamishna wa kamati ya Ukimwi Tanzania (Commissioner of Tanzania Commission for AIDS(TACAIDS).

Pia alikuwa Mwenyekiti wa Muungano wa viwanda Tanzania(Chairman of the Confederation of Tanzania Industries(CTI); Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki(Chairman of the East African Business Council); Mwenyekiti wa ICC Tanzania (a National Committee of the Intenational Chamber of Commerce); Na Mkurugenzi wa Bodi Ya Baraza la Biashara la Jumuiya ya Madola(Director of the Board of Commonwealth



Kuanzia mwaka 1987 Dr. Mengi amekuwa akisaidia upandaji miti kuzunguka mlima Kilimanjaro kwa sababu amekuwa akiona msitu ukipungua katika mlima Kilimanjaro. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2014 zaidi ya miti milioni 24 ilikuwa imepandw. Kwa mchango huu katika mazingira, Rais Mkapa alimchagua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la kusimamia Mazingira Tanzania(NEMC)National Environmental Management Council licha ya kwamba anatokea katika sekta binafsi.



Dr. Mengi hadi mauti unamkuta alikuwa ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania(Chairman of the Media Owners Association of Tanzania(MOAT) na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania(the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)



Dr. Mengi alikuwa mtu anayejulikana sana kwa kutoa sana misaada ya kijamii(philanthropist). Amepewa tuzo mbalimbali kitaifa, kikanda na kimataifa akitambulika sana kwa kazi yake ya kujitolea kwa watu. 
*Amepewa tuzo ya “The Order of the United Republic of Tanzania” mwaka 1994 na “The Order of The Arusha Declaration of the First Class” zilizotolewa na Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania mwaka 1995. 
*Amepewa tuzo ya “The Martin Luther King Jr. Drum Major for Justice iliyotolewa na Marekani mwaka 2008. 
*Amepewa tuzo ya “The International Order of the Lions Club iliyotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Lions Club mwaka 2014; na “The 2012 Business For Peace Award” iliyotolewa na Taasisi ya Oslo Sweden ya “Business for Peace Foundation” baada ya kupendekezwa na kamati inayotoa tuzo za Nobeli.



Kwa kutambua juhudi zake za kupambana na rushwa na ufisadi nchini mwaka 2008 serikali ya Marekani ilimpatia tuzo ya “Martin Luther King Jr. Drum Major Award”



Mwaka 2014 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alimpatia Dr. Mengi tuzo ya taifa katika mambo ya kuisaida na kuiwezesha jamii hasa katika ujasiriamali wa kijamii “The National Philanthropy Award” katika sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.




MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 3,2019

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images