Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

BREAKING NYUZZZZZZ........: MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA IPP, DKT. REGINALD MENGI AFARIKI DUNIA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii inaeleza kuwa, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi amefariki dunia. Taarifa zaidi zitakufikia kupitia hapa hapa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Mpendwa wetu, Dkt. Reginald Mengi.

Ameen.

WANANCHI JENGENI TABIA YA KUJILETEA MAENDELEO ,WENYEVITI SITA WARUDI CCM

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha.

Wananchi wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya shuhghuli za maendeleo katika vijiji vyao na sio kutegemea serikali kuwafanyia kila kitu .

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakati akizindua ofisi ya kijiji cha Nsongoro kilichopo Wilayani Arumeru mkoani hapa ,ofisi iliojengwa kwa nguvu za wananchi. 

Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiacha kufanya maendeleo katika vijiji vyao kwa kudai kuwa serikali ndio inatakiwa kufanya au kuwaletea maendeleo katika vijiji vyao kitu ambacho sio cha kweli .

"napenda kutumia wakati huu kuwapon geza sana wanakijiji wa kijiji cha Nsongoro kwa hatua mliofikia ya kuuza miti ya kijiji pamoja na kujichangisha na kujenga ofisi hii ya kijiji ambayo kwa miaka yote tang mwaka 1976 mlikuwa hamna ofisi ya kijiji na mlikuwa mnatumia ofisi ya chama cha mapinduzi , unajua wananchi wengi wanafikiriaga maendeleo kama haya yanaletwaga na serikali tu kitu ambacho sio chakweli kwani wananchi pia mnaweza kufanya wenyewe vitu kama hivi”alisema Muro

Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Arumeru mwalimu Jemsi Mchembe aliwapongeza wananchi hao na kuwaambia maendeleo ya kweli yanaletwa na watu wenyewe hivyo ni vyema kila mwananchi kujituma ili kuleta maendeleo katika nchi yake na sio kutegemea tu serikali iwaletee maendeleo .

Aidha aliwaambia maendeleo pia hayana chama hivyo ni vyema wananchi kushirikiana bila kujali chama wala kabili kufanya vitu ambavyo vitawanufaisha wananchi kwa ujumla na sio wananchi wale waliopo kipini hiki pia itawasadia ata wajukuu na vitukuu watakao kuja baadae.

Naye mwenyekiti wa kijiji Cha Nsongoro alisema kuwa ofisi hiyo ya kijiji imejegwa kwa nguvu za wananchi kwa ambao walikaa na kukubaliana kuuza miti ya iliopo katikashamba la kiijiji ambapo walipouza walipata jumla ya shilingi milioni 19 na katika fedha hizo shilingi milioni 17 zilitumika kujenga ofisi hiyo ya kijiji na shilingi milioni 2 ilitumika kwa ajili kuvuna miti ilioyokuwa shambani

Wakai huo huo Baada ya kumtuhumu Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro kuamuru kushushwa kwa bendera za chadema , Wenyeviti wa vijiji vitano na vitongoji viwili wa kata ya Songoro wameamua kukihama chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) nakujiunga na chama cha mapinduzi (CCM) kwa lengo la kumuunga mkono mkuu wa wilaya ya Arumeru katika harakati zake za kuleta maendeleo.

Wenyeviti ambao Walirudi CCM ni pamoja na Eliah Mathayo Mbise aliekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Songoro,Pokeali latiaeli Nnko wa kijiji cha mulala, Sadikiel Solomon Ayo wa kijiji cha Sura pamoja na Elifasi sunguroi Nassari wa kijiji cha Kilinga.

Pia wamo wenyeviti wawili wa vitongoji Anathe Eliah mbise kitongoji cha meto kijiji cha mulala, pamoja na Sinyaeli ndetaulo mbise wa kitongoji cha kiuta kijiji cha songoro mbali na hao pia aliekuwa katibu Mwenezi wa Chadema kata ya Songoro George peter Pallangyo pamoja na mwenyekiti wa Bawacha Bi Ekael felix wamelitangaza rasmi kurudi chama cha mapinduzi hivyo Kwa sasa kata ya Songoro vijiji vyake vyote sita vimerejea chama cha mapinduzi.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea katibu wa CCM wilayani Arumeru Shabani Mdoe alisema kuwa wamefanya uhamuzi mzuri kwani wameamua kuja kuung amkoano juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro.
 Katibu tawala wa wilaya ya Arumeru Mwalimu Jemsi Mchembe akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo ya kijiji 
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza moja ya mwenyekiti kwa uhamuzi aliochukuwa wa kuhamia CCM.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akifungua rasmi ofisi ya kijiji iliojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Songoro.

SIKU YA WAFANYAKAZI (MEI MOSI) MKOA WA ARUSHA ILIVYONOGESHWA

$
0
0
Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya mkoa wa Arusha wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Mei Mosi jijini Arusha 
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Mei Mosi jijini Arusha. 
Wafanyakazi wa kampuni ya Lodhia wakiwa na furaha wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi 2019. 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha(Auwsa) wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Mei Mosi jijini Arusha. 
Mkuu wa wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Idd Kimanta akimkabidhi kombe la ushindi katika michezo ya Mei Mosi 2019,Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shanna. 
Wafanyakazi wa kiwanda cha A to Z wakifurahia ushindi wa kwanza 
Viongozi jukwaa kuu wakiimba wimbo wa mshikamano. 

MAGAZETI YA LEO AL HAMIS APRIL 3,2019

WAAJIRI WAASWA KUTOWANYANYASA WAFANYAKAZI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Kimanta akihutubia siku ya wafanyakazi duniani mkoani Arusha,ambapo alimuwakilisha mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.
Maandamano ya wafanyakazi kama yanavyoonekana pichani Jijiji Arusha.
Maandamano yakiendelea kuelekea katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Karume Jijiji Arusha.




Na Vero Ignatus,Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Kimanta amekenea vikali tabia ya baadhi ya Waajiri wakorofi wanaowanyanyasa Wafanyakazi wao na kuwataka Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kuwachukulia hatua mapema pale watakapobainika.

Amesema hayo wakati akitubia katika Siku ya Wafanyakazi mkoani Arusha akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo Mrisho Gambo ambapo amewataka waajiri wajiepushe na vitendo vya unyanyasaji kwani sheria itafuata mkondo wake.

"Hatutamfumbia macho baadhi ya waajiri wakorofi wanaowanyanyasa wafanyakazi wao vyama vyavwafanyakazi fanyeni jitihada kuwabaini ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.alisema Kimanta.''

Mhe.Kimanta amewataka Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi kutatua kero za wafanyakazi badala ya kusubiri siku ya wafanyakazi na kutoa kero zao.

Nae Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya Wafanyakazi mkoani Arusha (TUCTA) Lota Laizer ameiomba serikali itoe nyongeza ya mishahara pamoja na ongezeko la asilimia la 1 la kila mwaka kama ilivyo matakwa ya sheria.

Aidha Laizer amewataka Wafanyakazi kuwa viongozi wa kisiasa wanatekeleza majukumu yao bila kukiuka sheria za wafanyakazi na kutumia lugha za kuwadhalilisha wafanyakazi.

RAIS DKT MAGUFULI AMLILIA DKT REGINALD MENGI

Karibu kwenye ibada Maalum ya kuombea Elimu/ mtihani wa kidato cha sita 2019

$
0
0
Kituo cha Huduma ya Maombi na Neno la Mungu Jijini Mwanza kinakukaribisha kwenye Ibada Maalum ya kuombea elimu/ mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza nchini Tanzania Mei 06 hadi 23, 2019. Ibada hiyo itakafanyika siku ya jumapili Mei 05, 2019 kuanzia saa tisa na nusu alasiri hadi saa kumi na mbili jioni eneo la Pasiansia/ Iloganzara jirani na kiwanda cha mabondo cha wachina.

Dkt. Ndumbaro akutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini leo tarehe 1 Mei, 2019, katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es salaam. Mazungumzo hayo yamejikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na EU hususan katika nyanja za elimu na udhibiti wa biashara haramu ya dawa za kulevya. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo. 
Kaimu Balozi Stuart akielezea jambo wakati wa mazungumzo hayo. 
Afisa Mambo ya Nje wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Albert Philipo akifuatilia mazungumzo hayo. 
Juu na chini mazungumzo yakiendelea. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.) akiagana na Kaimu Balozi Charles Stuart mara baada ya mazungumzo. 

NHIF TANGA YATUMIA MAADHIMISHO YA MEI MOSI KUWAKUMBUSHA WAAJIRI KUTOA MICHANGO YA WATUMISHI WAO

$
0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga umetumia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi dunia (Mei Mosi) kuwakumbusha waajiri kuhakikisha wanatoa michango kwa ajili ya watumishi wao. 


Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Happines Sima ambapo aliwataka waajiri kuzingatia suala hilo. 

Alisema pia wametumia fursa hiyo kuweza kuhamasisha waajiri ambao watumishi wao ambao hawajajiunga na mfuko huo wajiunge ili waweze kunufaika na fursa zilizopo ndani ya mfuko huo. 

“Lakini pia katika maadhimisho haya tumeweka banda letu ili kuweza kuwasikiliza wafanyakazi na kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili “Alisema Meneja huyo. 

Hata hiyo aliwataka wazazi na walezi kuwaandikisha watoto wao kwenye mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu pindi wanapougua . 

 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Happines Sima akizungumza wakati wa maadhimisho hayo leo
 Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto ni Meneja wa Mfuko huo mkoa wa Tanga Happines Sima akiweka sawa mwamvuli wakipita mbele ya mgeni rasmi
 Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

RC Mongella agoma kufungua mradi, rungu lamuangukia Mhandisi

$
0
0
Ukaguzi wa mradi wa maji wa kisima kirefu katika Kijiji cha Matela, Kata ya Isangijo wilayani Magu.
Ukaguzi wa mradi wa uzalishaji mali wa kikundi cha ESM Kangara ambapo kinajihusisha na ufugaji wa kuku, bata, njiwa, mbwa na paka.
 Ukaguzi wa Zahanati ya Bundilya wilayani Magu.
Jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha kwanza kujengwa wilayani Magu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwenye ukaguzi wa Kituo cha Afya Nyerere kilichopo Kata ya Kangara wilayani Magu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa pamoja na viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya anaendelea na ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Mwanza. Hapa Mongella akiwasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Lumnve iliyopo Kata ya Bujora wilayani Magu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kwenye ukaguzi wa kisima kirefu cha maji Isangijo ikiwa ni moja ya visima 16 vinavyochimbwa wilayani Magu ili kuondoa adha ya maji kwa wananchi.
Ukaguzi wa shamba la miti la Bahati Kwangu ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Busekwa, Kata ya Bujashi wilayani Magu lenye miti zaidi ya elfu 10 likiwa na ukubwa wa Hekali saba, lengo likiwa ni kuhifadhi mazingira pamoja na kitega uchumi kwa baadae.
Ukaguzi wa Zahanati ya Isangijo wilayani Magu.

Ukaguzi wa shughuli za kikundi cha wazalishaji mali cha "Meremeta Leather Group" wilayani Magu kinachojihusisha na utengenezaji wa bidhaa za ngozi ikiwemo viatu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alitembelea Shule ya Musabi wilayani Magu ambapo kuna klabu ya TAKUKURU kwa wanafunzi wa shule ya msingi.
Wanafunzi wakafurahi kukutana na viongozi wao.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akaweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Maligisu wilayani Kwimba.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alipotembelea Shule ya Sekondari Maligisu wilayani Kwimba.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aligoma kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Kadashi wilayani Kwimba ambao ulianza mwaka 2013 ambapo aliagiza mradi huo ukamilike na kutoa maji katika magati yote 21 ifikapo Juni Mosi 2019.
Tazama BMG Online TV hapa chini

HOTUBA YA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI, MBEYA

Makala ya kuadhimisha Ushirikiano wa miaka 55 Kati ya China na Tanzania

$
0
0


Mwandishi Phelisters Wegesa Marwa

Nyumbani mbali na Nyumbani Jamhuri ya Watu wa China, nashukuru sana hii yote ni kwa sababu ya urafiki mwema kati ya China na Tanzania naishi kama nyumbani. Mnamo Agosti 2016 nilifunga mizigo yangu na kusafiri angani takriban maili 5,340 kutoka Dar es Salaam, mji wa kibiashara wa Tanzania hadi Beijing nchini China kutafuta maarifa. 
Hapo awali nilikuwa nimeshaenda nje ya nchi Tanzania kwenye vikao, semina, kazi Afrika na hata Ulaya, ambapo nilikaa wiki chache au miezi michache. Lakini China bila shaka ni tofauti na nchi zinazozungumza Kiingereza na Kiswahili na kwa nchi ya China Kichina ni lugha inayotumika zaidi. Watu wengi wana dhana kuwa kuja China zaidi ni kufanya biashara na sio Kusoma: Lakini bado nilisisitiza nitakuja China, nilitaka kueleza uamuzi wangu wa kujifunza nje ya nchi na kwamba kuna mengi zaidi duniani ya kujifunza zaidi ya Marekani na mimi niilitamani kuyajua haya .

Kwa heshima ya kuchaguliwa na Ofisi ya Uchumi na Biashara ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, kwa ufadhili kutoka Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China (MOFCOM) katika Chuo Kikuu cha Beijing ambacho kwa sasa pia ni Taasisi ya Utafiti wa Belt na Road. 

2019 ni mwaka wa kusherehekea miaka 55 ya mahusiano ya kidiplomasia ya China na Tanzania; China na Tanzania wana ndoto ya pamoja. Ndoto ya ushirikiano wa kiuchumi na ushirikiano wa maendeleo ya pamoja, ndoto hii na ushirikiano kati ya China na Tanzania inarudi nyuma ya kumbukumbu ya miaka kadaa iliyopita wakati hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alikutana na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong. 

Historia ya Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), mradi mkubwa zaidi wa msaada wa kigeni nchini Afrika hadi sasa na uwekezaji mwingine unaoungwa mkono na serikali ya Kichina; Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Urafiki, Shamba la mpunga la Mubarali, Mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Kiwanda cha miwa cha Mahonda, Uwanja wa Taifa , Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Maktaba ya Kimataifa ya sanaa ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, bandari ya New Bagamoyo pamoja na mtandao wa reli unaounganishwa na reli nyingine za Tanzania na kadhalika. Historia hii ina maana kubwa sana katika uhusiano kati ya China na Tanzania na hata Afrika kwa ujumla. 
Mwenyekiti wa muda mrefu China, Mao Zedong pamoja na Rais wa kwanza wa Tanzania, J. K. Nyerere, Machi 25, 1974.

China na Tanzania wanaendelea kuimarisha uaminifu wa kisiasa kwa njia ya ziara za mara kwa mara za viongozi wa serikali. Rais wa China Xi Jinping alichagua Tanzania kuwa kituo chake kwanza cha ziara yake ya Afrika mwaka 2013 baada ya kuchukua madaraka na hii inathibitisha umuhimu wa mahusiano ya China na Tanzania. 

Aidha, kumekuwa na ziara nyingi za juu za kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili kwa uzinduzi wa miradi mbalimbali zaidi; ikiwa ni pamoja na Elimu, Miundombinu, Afya, Utalii, Mbinu za Kilimo za Kisasa, Mauzo ya Nje na Uagizaji ambayo umeimarisha uhusiano zaidi na kubadilishana uzoefu. 
Rais wa China Xi Jinping (Kulia) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa FOCAC mjini Beijing, Septemba 6, 2019.

Tanzania imejihusisha kushiriki kikamilifu katika Mpango wa Belt na Road na Septemba iliyopita, Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwenye Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika (FOCAC) walikubaliana na Rais Xi Jinping kuendelea kuimarisha ushirikiano wenye manufaa kati ya pande zote mbili. China inasaidia juhudi za Tanzania katika kulinda haki na maslahi yake, kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu, na iko tayari kuimarisha na kubadilishana uzoefu wa utawala, maendeleo na mikakati ya kupunguza umaskini. 

China bila shaka ni kinara duniani katika kupunguza umaskini na kuna mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wake. China inachukua jukumu zaidi katika hatua ya kimataifa na Tanzania ina nafasi nzuri ya kuendelea kushirikiana zaidi na nchi nyingine zinazoendelea kujifunza kutoka China na kufanya kazi pamoja kuwekeza katika nguvu zake za viwanda na uvumbuzi. 

Wizara ya Afya na wadau muhimu kutoka Tanzania na China wamekutana mara kwa mara kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Afya kwa njia ya miradi ambayo tayari imeanzishwa. Mfano mkubwa ni Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ndio taasisi ya moyo ya kwanza nchini Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mnamo Oktoba 2015, JKCI imefanikiwa kutibu maelfu ya wagonjwa wa moyo na kufanya upasuaji wa moyo zaidi ya 1,500 kwa gharama nafuu, na hivyo kuleta faida kubwa kwa watanzania. 

Hivi sasa, kuna madaktari watatu wa kichina wanaofanya kazi JKCI, waliobobea katika upasuaji wa moyo na magonjwa ya watoto. Hivi karibuni JKCI imesaini mkataba wa makubaliano na Hospitali ya Fuwai iliyopo nchini China ambayo ni kituo kikubwa kinachoshughulikia matatizo ya moyo na kinachojulikana duniani na kimataifa kwa matibabu sugu ya aina tofauti sumbufu ya moyo. 
China imeonyesha kujitolea kwa kupanua upatikanaji wa huduma za afya, kuanzia na Mfumo wa Matibabu wa Ushirika, upatikanaji wa ubora wa huduma za afya ambayo imekuwa mojawapo ya eneo la msingi la Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China na Wizara ya Afya Tanzania na ni kupitia miradi hii ya pamoja na mafunzo ya wataalam na ushirikiano wa taasisi za afya. 

Zaidi Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu alikutana na Waziri wa Afya wa China Ma Xiaowei na kusema kuwa China itaendelea kupeleka timu za matibabu Tanzania kwa kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika matibabu ya angiocardiopathy, kansa, afya ya umma, pamoja na mafunzo ya madaktari wa kitaaluma na ujanibishaji wa bidhaa za dawa. Ilihitimishwa kwa kusaini mkataba wa ushirika kati ya Hospitali ya Saratani ya Kichina ya Sayansi ya Matibabu ya China na Taasisi ya Saratani Ocean Road Tanzania. 
Waziri wa Afya Mheshimiwa Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki na wataalamu wengine wa afya kutoka China na Tanzania wakati wa ziara ya Hospitali ya Kimataifa ya Peking University (PUIH). 

Watanzania wana kila sababu ya kudumisha uhusiano wa China na Tanzania na mustakabali wa mahusiano haya yapo mikononi mwa vijana wote waliopata nafasi ya kuja kujifunza nchini China na kujifunza hata kwa Wachina nyumbani. Ni jukumu la vijana kufanya bora zaidi kwa yale tuliyojifunza, ni funguo katika kukuza maendeleo mapya na mafanikio ya nchi ya Tanzania. Hii itasaidia kuongeza kasi ya mageuzi na mabadiliko yaliyopangwa na Mheshimiwa Rais wetu Mheshimiwa John Joseph Magufuli. 

China kama mshirika muhimu wa maendeleo na Tanzania, Tanzania inahitaji China katika mkakati wa viwanda ili iweze kufikia lengo la kuwa uchumi wa katikati mwaka 2025 kwa kuzingatia taarifa ya "2019 ni mwaka wa uwekezaji". 

Mustakabali wa kesho unaonekana kuwa mzuri na wenye mafanikio, nikitizama mbele naamini na naona kuwa kuunganisha umuhimu wa ushirikiano wa elimu ya juu, sayansi na teknolojia, utafiti ni suluhisho muhimu kuimarisha uchumi wetu. Nina hakika kwamba msingi wa urafiki uliojengwa na China na Tanzania utafikia kizazi cha baadaye kwa kufanya kazi pamoja ili kujenga jumuiya yenye nguvu zaidi ya baadaye. Siku hiyo itakuja wakati taifa la Kichina litafikia ndoto yake ya upyaji wa kitaifa na Tanzania itafahamu na kuelewa ndoto yake ya umoja na kuendelea kuimarisha! 


Udumu Urafiki wa China na Tanzania! 

Phelisters Wegesa Marwa 

Mtumishi wa Umma anayefanya kazi 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Tanzania na ni mwandishi wa kujitegemea wa makala ya Uchumi, Vijana, Elimu na Ushirikiano wa China na Afrika. 

WAAJIRI WATAKAO WANYANYASA WAFANYAKAZI KUCHUKULIWA HATUA KALI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
SERIKALI ya awamu ya tano imehaidi kushughulikia changamoto za wafanyakazi kote nchini na kuwataka wawe na subira wakati Serikali ikiendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuwahimiza wafanyakazi kutekeleza wajibu wao.

Akijibu changamoto za wafanyakazi kupitia risala  iliyosomwa katika siku ya kilele cha siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimata akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo  amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi kupeleka matatizo ya wafanyakazi katika ofisi husika za Serikali ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa mara moja. 

Aidha ameweka wazi kuwa serikali haitamfumbia macho mwajiri  binafsi ambaye atabainika anamnyanyasa mfanyakazi,na iwapo itabainika  amemnyanyasa mfanyakazi kwa namna yoyote  hatua kali itachukuliwa dhidi take.

"Kuna waajiri ambao wananyanyasa wafanyakazi nimesikia wanawatolea maneno machafu ,wanawapiga ,na wengine hata kuwanyima haki zao sasa nasema viongozi wa wafanyakazi naomba  hatua kali zichukuliwe na sio hivyo tu iwapo  mwajiri yeyote ambaye atabainika anawanyayasa wafanyakazi leteni taarifa ili tuwachukulie hatua Kali" alisema kamanta.

Aidha amesema  kuwa wiki mbili zijazo kiwanda cha matairi general trye kitazinduliwa na serikali itaanza mchakato huo na maagizo ya kuvifuatilia viwanda vingine vilivyofungiwa unaendelea hivyo sherehe za mei mosi sio siku za kuleta changamoto bali ziwe ni furaha.

"Tukae pamoja kabla ya sherehe tuzungumze mapema na tusingoje hadi wakati sherehe hizi za wafanyakazi ndio tunaleta changamoto haileti afya kwani sherehe ni furaha na milango ipo wazi kutatua kabla ya sherehe"amesema kimanta

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe za mei mosi Mwenyekiti Wa chama cha walimu mkoa Wa Arusha Lootha Laizer ameiomba serikali kuwachukulia hatua Kali waajiri wote ambao wanawanyanyasa wafanyakazi.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya waajiri wa sekta binafsi wamekuwa na tabia ya kuwanyanyasa wafanyakazi kwa kwa kuwapiga, kuwatolea lugha za matusi na hata kuwanyima haki zao  taarifa zao zimetakiwa haraka iwezekanavyo ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.

Akisoma  risala mbele ya mgeni rasmi mratibu wa wafanyakazi Mkoa wa Arusha Samweli Maghero kwa niaba ya wafanyakazi wameiomba serikali kupunguza kodi ya mapato kwa wafanyakazi kwakuwa kodi hiyo ni kubwa na mshahara ni mdogo ukilinganisha na hali ya uchumi.

Aidha pia wameiomba serikali kupandisha madaraja (vyeo )kwa wafanyakazi waliokaa kwa kipindi kirefu bila kupandishwa vyeo ,huku wakiomba  serikali iwape ruhusa ya walimu kuhama vituo vyao vya kazi.
 Mratibu wa wafanyakazi Mkoa Wa Arusha Samweli Maghero akisoma Risala kwa niaba ya Wafanyakazi katika kilele cha siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Baadhi ya wafanyakazi wakifatilia hutuba ya mgeni
  Mwenyekiti Wa chama cha waalimu mkoa Wa Arusha, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Arusha Lootha Laize rakiongea katika maadhimisho hayo ambayo ameiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waajiri wanaonyanyasa wafanyakazi.
 Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimata akihutubia wafanyakazi waliojitokeza kusherekea siku hiyo ambapo amewahimiza kufanyakazi kwa bidii na kuwasilisha matatizo yao kwa wakati.

Kampuni ya Vodacom Tanzania yatoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa wafanyakazi wake

$
0
0
 Mkuu wa mauzo wa kanda ya Dar na Pwani wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, George Lugata (aliyelala chini) na Msimamizi wa mifumo ya kompyuta Emmanuel Lenduyayi (aliyesimama) akitoa mfano wa namna ya kumhudumia mtu aliyeanguka ghafla katika semina ya mafunzo ya huduma ya kwanza, yaliyofanyika makao makuu ya kampuni jijini Dar es Salaam karibuni jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom hutoa mafunzo mbalimbali ya uokoaji kwa wafanyakazi wake na wafanyakazi wa majumbani kwao ili kuwawezesha kukabiliana na ajali mbalimbali ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake. Aliyesimama kulia ni mwalimu wa mafunzo hayo Bw Adam kutoka kampuni ya Knight Support Company.

Mfanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Neema Mgombelo, akionyesha mfano wa jinsi ya kumtambua mgonjwa aliezimia katika semina ya mafunzo ya huduma ya kwanza, iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom hutoa mafunzo mbalimbali ya uokoaji kwa wafanyakazi wake na wafanyakazi wa majumbani kwao ili kuwawezesha kukabiliana na ajali mbalimbali ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake. Kushoto ni Mwalimu wa mafunzo hayo Bw Adam kutoka kampuni ya Knight Support Company.

Dkt Gwajima ataka Timu za Uendeshaji Huduma za Afya za Mikoa kutumia muda wao vizuri kufuatilia na kusimamia huduma za afya

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Njombe
Serikali imezitaka timu za uendeshaji huduma za afya za mikoa kuelekeza nguvu zaidi na muda zaidi katika kusimamia  shughuli zote za utoaji wa huduma bora za afya katika mikoa yao badala ya kutumia nguvu na muda mwingi kukaa ofisini au kuwa safarini.

Agizo hilo limetolewa leo mjini Njombe na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima wakati akizungumza na timu ya uendeshaji huduma za afya ya mkoa wa Njombe.

Amesema jukumu kubwa la timu za usimamizi huduma za afya mikoa ni kuhakikisha kuwa timu za usimamizi huduma za afya halmashauri zinaimarisha usimamizi wa timu za uendeshaji huduma za vituo husika ili, zihakikishe huduma zinatolewa kwa ubora stahiki.

Aidha, kupitia ufuatiliaji wa kina, timu za usimamizi wa afya mkoa na halmashauri  zinapaswa kupata mwenendo wa huduma kutoka vituo vyote na maeneo yote ya huduma za afya jamii kisha,  kufanya uchambuzi wa takwimu na taarifa hizo na kuzijadili ili, kutoa ushauri, mapendekezo, maelekezo ya kuwesha kuwa na mipango stahiki inayojibu hoja husika kwa wakati.

Dkt. Gwajima amezikumbusha timu zote za usimamizi huduma za afya za mikoa na halmashauri kuwa, huduma za afya zinazotolewa katika vituo na katika ngazi ya jamii zina uhusiano wa moja kwa moja na umakini wa utendaji wa timu za afya za mikoa na halmashauri hivyo, watambue kuwa, wanalo jukumu kubwa la kuelekeza nguvu na muda wa kutosha katika kufuatilia utoaji wa huduma husika badala ya kutumia muda mwingi kukaa ofisini na kusafiri hata safari ambazo wanaweza kuwakilishwa.

Hivyo, amesema kipimo cha ubora, umahiri na tija ya utendaji wa timu za afya mkoa na timu za afya za halmashauri ni ubora wa huduma zinazotolewa ngazi ya vituo vya afya na siyo vinginevyo.

Dkt Gwajima amesema, takwimu zinaonesha baadhi ya timu za usimamizi huduma za afya mikoa na halmashauri hazitumii muda wa kutosha kufanya ufuatiliaji wa kina wa utoaji huduma za afya katika vituo na jamii na badala yake muda mwingi unatumika kukaa ofisini, safarini au kuendekeza malumbano yatokanayo na kukataa kupokea mabadiliko katika uwajibikaji (resistance to change) kitu ambacho, amesema hakikubaliki kwani kinapoteza muda.

 Amesisitiza kuwa, lazima muda mwingi utumike kwa timu hizi kuwa karibu zaidi na ufuatiliaji wa mwenendo wa utoaji huduma za afya kwa wateja ili, kubaini changamoto zinazojitokeza, kuziwasilisha, kuzichambua na kuzijadili kama timu kisha, kuzitumia kutoa ushauri, maelekezo, mapendekezo na kupanga mipango inayogusa huduma kwa uhalisia wa takwimu.

Dkt. Gwajima amesema, kila mjumbe wa timu ya usimamizi wa huduma za afya anatakiwa kuwa na taarifa fupi ya utekelezaji wa ufuatiliaji wa mwenendo wa huduma siyo tu kila mwezi na kila robo bali kila siku kwani, vipo viashiria muhimu vya kufutilia na kuvifanyia uchambuzi kila siku na kinyume na hapo, haikubaliki maana hakutakuwa na maelezo ya nini hasa kimefanyika siku husika.

Kuhusu eneo la upatikanaji wa huduma Dkt. Gwajima amesema, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imeendelea kuinua ubora wa huduma za afya kwa kujikita katika kuboresha maeneo mengi na baadhi yake ni ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya na kuongeza bajeti ya dawa.

Hivyo, jukumu la timu za usimamizi huduma za afya ni kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa kina ili, juhudi hizi zizidi kuzaa matunda makubwa zaidi na kuondoa kero zinazoepukika hususan, matukio ya kukosekana kwa dawa yatokanayo na kutozingatia taratibu za manunuzi ya umma na tabia za baadhi ya watoa huduma kutumia dawa hizo bila kuzingatia Mwongozo wa Matibabu.

Amesema, tabia zinazokwamisha juhudi za Serikali zinachangiwa na baadhi ya timu za usimamizi huduma za afya mikoa na halmashauri kutoweka nguvu na muda wa kutosha katika kufuatilia mwenendo wa utoaji huduma katika vituo husika.

Dkt Gwajima amesema, timu za usimamizi huduma za afya zina jukumu la msingi la kuhakikisha huduma za tiba zinakuwa bora katika vituo na kuvutia watumiaji wengi wenye uhitaji.

Aidha, kwa kuwa miongoni mwa watumiaji ni wanachama wa mifuko mbalimbali ya bima za afya ni dhahiri kuwa, watachangia huduma na hivyo, kuwezesha vituo vya huduma kupunguza utegemezi kwa Serikali na hii ndiyo itaongeza tija zaidi.

Amesema, kupunguza utegemezi wa vituo kwa serikali inawezekana kwa kuwa, bado fedha nyingi za marejesho ya mfuko wa taifa wa bima ya afya zinaenda kwa watoa huduma wanaomiliki vituo binafsi ambao ni wachache ukilinganisha na idadi ya vituo vya Serikali hivyo, kuna haja ya kuzingatia hili.

Dkt. Gwajima amesema, uzembe katika kujaza kumbukumbu za huduma iliyotolewa ikiwemo, kumbukumbu za madai ya fedha unachangia kuwepo kwa makato yanayoepukika.

Aidha, baadhi ya watoa huduma kutojali uwepo wa dawa na vipimo kunachangia wateja wengi kwenda kununua dawa nje ya kituo ikiwemo, baadhi ya watoa huduma  kuanza biashara bubu za kuuza dawa kwa wateja hivyo, tabia hizi zidhibitiwe mara moja na timu za usimamizi huduma za afya mikoa na halmashauri.

Dkt. Gwajima amesema, mapungufu mbalimbali mara nyingi hayaripotiwi na timu za usimamizi huduma za afya na sababu kubwa ni wajumbe wengi wa timu hizi kutotoa muda na nguvu za kutosha kufanya ufuatiliaji wa huduma.

Aidha, amempongeza mfamasia wa kituo cha afya cha njombe mjini bwana Ben Ngogo kwa kuwezesha uwepo wa rekodi nzuri za kumbukumbu za dawa pamoja na kuwa anakabiliwa na ufinyu wa stoo ya dawa. Pia, Dkt. Gwajima amempongeza Muuguzi wa Wodi ya Kujifungua katika kituo hicho bibi Diana Simime kwa umakini wake katika kusimamia usafi pamoja na changamoto ya ufinyu wa chumba na uchakavu wa miundombinu. Amemtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Dkt.Thomas Ndailo kuongeza kasi ya kutimiza malengo ya kujenga kituo cha afya kwenye eneo lenye nafasi.

Dkt. Gwajima amesema, ana imani kuwa, watoa huduma walioko vituoni watafanya vizuri zaidi iwapo, timu za usimamizi huduma za afya mikoa na halmashauri zitaelekeza nguvu na muda wa kutosha katika kufuatilia utekelezaji unaofanyika katika vituo hivi, kuchambua takwimu na taarifa, kujadili, na kushauri na kuelekeza na siyo vinginevyo.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Bumi Mwamasage ameahidi kusimamia kwa nguvu zote yote yaliyo elekezwa na kuhakikisha kuna uwajibikaji mkubwa zaidi wa timu zote za usimamizi huduma za afya katika halmashauri zote.

Dkt. Gwajima anaendelea na ziara ya ufuatiliaji wa ufanisi wa timu za afya mikoa na halmashauri katika mikoa ya Ruvuma na Iringa baada ya kukamilisha kwenye mikoa ya Dodoma, Morogoro na Njombe kauli mbiu ikiwa ni ‘ubora na uhai wa mifumo ya utoaji huduma za tiba na kinga kipimo cha ufanisi wa timu za usimamizi huduma za afya mikoa na halmashauri’.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima  akizungumza na timu ya uendeshaji huduma za afya ya mkoa wa Njombe.

 Baadhi ya wajumbe wa timu ya uendeshaji huduma za afya ya mkoa wa Njombe  wakimsikiliza  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia sekta ya Afya Dkt Dorothy Gwajima leo mjini Njombe

MADAKTARI BINGWA WA HUDUMA ZA GANZI BADO CHANGAMOTO

$
0
0
Imeelezwa kuwa Upungufu wa wataalamu wa kutosha wa kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi umekuwa ukisababisha  changamoto kwa wagonjwa kukosa huduma stahiki.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof Laurence Museru wakati wa Mkutano uliowakuwanisha wataalamu wa kutoa huduma za dawa ya usingizi na ganzi wa ndani na nje ya nchi.



Prof. Museru amesema kuwa wataalam wa kutoa dawa hizo kwa Tanzania wapo 40 ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafika 50.

“Hapo awali nchini kulikuwa na wataalam 10 na baadae wakaongezeka na kufikia 40 ila huitaji tunaitaji kufikia wataalam 200”. Amesema museru.

Ameongeza kuwa serikali imekuwa ikiongeza juhudi kwa kuwasomesha wauguzi ili kuzidi kuboresha huduma hiyo.



Pia amesema kumekua na ongezeko la ajali hivyo kupitia wataalam waliopo na watakao ongezeka watasaidia kuhuisha majeruhi mahututi na wanopoteza fahamu.Naye Rais wa chama cha watoa huduma wa dawa za usingizi na ganzi SATA, Dk. Mpoki Ulisubisya amesema lengo la mkutano huo ni kuweza kuweza kuboresha huduma na kuona ni namna gani tunaweza kutoa elimu ili kuongeza wataalam.

“Tutakuwa tukiweka ushawishi kwa vijana kuweza kusomea ili kuongeza idadi yetu y’all madaktari kwani kwa nchi nzima atufiki 50 ivyo tunataka tuwe wengi”. Amesema Dkt. Mpoki.Pia Dk. Mpoki aliongeza kuwa nia yao kila hospitali ya rufaa na mkoa kuwa na angalau daktari bingwa mmoja.
 Balozi Dkt Ulisubisya Mpoki  akifungua  Mkutano wa  wataalamu wa kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi  iliyofanyikakwenye hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof Laurence Museru akizungumza kwenye Mkutano wa  wataalamu wa kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi  iliyofanyikakwenye hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam.Baadhi ya wataalamu wa kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi wakiwa kwenye mkutano uliofanyika katika  hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)Muonekano wa viifaa tiba vinavyotumiwa na  wataalamu wa kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi.Wataalam hao wakiwa katikapicha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo.

Wafanyakazi Rukwa waaswa kupunguza matumizi ya simu za mikononi muda wa kazi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaasa wafanyakazi mkoani Rukwa kupunguza matumizi ya simu za mikononi kwaajili ya shughuli binafsi nje na majukumu ya kazi hasa muda wa kazi wanapokuwa ofisini wakiendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Amesema kuwa dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kumtumikia mwananchi kwa nguvu zote hivyo kila mfanyakazi anapaswa kuongeza bidii katika kufanya kazi, lakini kutumia simu na kuacha kuwahudumia wananchi kwa wakati mfanyakazi anakuwa anapata mshahara ambao hausmtahili kutokana na kutotumia muda wake alioajiriwa kwa ufanisi.

“ Ndugu wafanyakazi, hizi simu zimekuwa ni changamoto kubwa sana sehemu zetu za kazi, unakuta mtu badala ya kufanya kazi, hata kutoa huduma kwa mwananchi yeye “ana-chat” kwenye simu, vidole viko kwenye simu, yeye na simu, simu na yeye, kazi haziendi na kama zinakwenda basi zinakwenda kwa mapungufu, kunakuwa hakuna ufanisi na umakini, suala hili la simu tuliangalie sana ndugu waajiri pamoja na waajiriwa,” alisisitiza

Ameongeza kuwa wafanyakazi wamekuwa wakidai maslahi kuliko kupima uwajibikaji wao katika kazi ambazo wanapaswa kuzitekeleza na hali inayopelekea kuzorota kwa kazi nyingi kutokana na wafanyakazi kujishughulisha na matumizi ya simu za mkononi kuliko kuwajibika.

Ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kimkoa katika mkoa wa Rukwa yalifanyika katika viwanja vya mpira mji mdogo wa Laela, Wilaya ya Sumbawanga alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maeneo nane yenye kulenga kuimarisha utendaji wa kazi ili kuleta maslahi kwa wananchi pamoja na wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi, ikiwemo uwajibikaji, kushughulikia kero za wananchi, uadilifu, usimamizi wa miradi, ubunifu, ushirikiano,kupambana na Rushwa,na kuunda mabaraza ya kazi.

Wakati akisoma risala ya wafanyakazi kwa mgeni rasmi katibu wa shirikisho la vyama huru vya wafanayakazi (TUCTA) Mkoani Rukwa Nashoni Kabombwe alisema kuwa kuna baadhi ya waajiri hawataki kabisa zoezi la kupata wafanyakazi bora kwenye taasisi zao lifanyike kwa kisingizio kwamba hawana fedha wala zawadi yoyote ya kuwalipa.

Katika kushinikiza hilo alisema, “kiwango cha zawadi kwa wafanyakazi bora zinazotolewa na baadhi ya waajiri ni kidogo na hakiendani na mabadiliko ya kiuchumi TUCTA inawataka waajiri kuanzia sasa kiwango cha chini cha zawadi kiwe shilingi 500,000 au kitu chenye thamani isiyopungua fedha hiyo.”

Kwa upande wake Afisa mfawidhi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) katika mikoa ya Rukwa na Katavi Oscar Ngaluka katika mwaka wa fedha 2017/2018 Tume ilipokea jumla ya migogoro ya kikazi 127, wakati iliyomalizwa katika hatua ya usuluhishi ni 93, na inayoendelea na migogoro ni 10 na kuongeza kuwa sekta inayoongoza kwa migogoro mahala pa kazi katika mikoa ya Rukwa na Katavi ni ujenzi wa barabara.

“Sababu zinazoweza kumfanya mfanyakazi afungue mgogoro wake katika Tume ni pamoja na kuachishwa kazi bila ya kuwepo sababu ya kufaa na utaratibu wala kosa, mwajiri kuzuia vyama vya wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ya kichama, madai ya stahili mbalimbali na manyanyazo sehemu za kazi,” Alisema.

Kauli mbiu ya siku ya wafanyakazi ni “Tanzania ya Uchumi inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora kwa wafanyakazi ni sasa” ambapo Tanzania nzima ina vyama vya wafanyakazi 31 huku Mkoa wa Rukwa ukiwa na vyama vya wafanyakazi 9.
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo wakipita na bango lao katika maadhimisho ya sherehe ya siku ya Wafanyakazi bora iliyofanyika katika viwanja vya mpira mji mdogo laela Wilayani Sumbawaga.
 Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akimkabidhi Michale Mongomongo dereva wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa cheti pamoja na shilingi laki tatu ikiwa ni zawadi ya mfanyakazi bora katika sherehe za siku ya wafanyakazi 2019 Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (waliokaa mwenye skafu) katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi bora (waliosimama) katika sherehe ya siku ya Wafanyakazi bora iliyofanyika katika viwanja vya mpira mji mdogo laela Wilayani Sumbawaga.

MAKATIBU WAKUU TANZANIA NA UGANDA WAHITIMISHA MKUTANO WA MAHUSIANO NA KUSAINI MAKUBALIANO

$
0
0
Na Munir Shemweta, BUKOBA

Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, Kiuchumi na Kimazingira umemalizika Bukoba mkoani Kagera kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot kusaini makubaliano yaliyofikiwa.

Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi za Tanzania na Uganda kutoka Wizara zinazoshughulika na masuala ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mambo ya Nje, Mifugo na Uvuvi, Maji pamoja na Nishati.

Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta zinazohusika kutoka nchi hizo mbili walikutana na kujadiliana namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda katika eneo la Mpaka na baadaye kuwasilisha mapendekezo kwa Makatibu Wakuu kwa lengo la kujadiliwa kwa manufaa ya nchi hizo.

Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango Kabambe wa Utunzaji Mto Kagera na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera kati ya Tanzania na Uganda.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel alisema katika siku mbili za mkutano huo, nchi washiriki zilijadili namna bora ya kuendeleza mahusiano ya mipakani kwa lengo la kurahisisha mambo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira sambamba na kujadili jinsi ya kuboresha matumizi endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera ili ziweze kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Okidi Ollot alisema, mkutano huo ni njia sahihi ya kuonesha kuimarika kwa mahusiano ya Tanzania na Uganda na kusisitiza kuwa kilichofanyika ni kuonesha uhalisia wa ushirikiano kwa lengo la kuwafanya wananchi wa pande zote kunufaika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alizishukuru pande zote mbili za nchi za Tanzania na Uganda kwa kufanikisha kufikiwa makubaliano aliyoyaeleza kuwa yana lengo la kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) akibadilishana hati za makubaliano na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot baada ya kusainiwa kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot wakionesha hati za makubaliano baada ya kusainiwa kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot (Wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe akizungumza wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira Bukoba mkoani Kagera. (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
 Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (wa kwanza kulia) na Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa kufungwa Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira Bukoba mkoani Kagera.
 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera.
 Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima akizungumza kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika Bukoba mkoani Kagera (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WA WIZARA YA ARDHI)

Benki ya NMB yaahidi kusaidia Wakulima wa zao la Zabibu

$
0
0
Dodoma. Benki ya NMB wamekubali kusaidia wakulima wa zao la zabibu mkoani Dodoma,ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali wa kuwainua wakulima.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NMB Albert Jonkergouw katika hafla fupi ya benki hiyo kwa taasisi za serikali, viongozi wa taasisi na wafanyabiashara iliyofanyika katika ukumbi wa new Dodoma hotel.Mkurugenzi huyo alisema nguvu kubwa imeelekezwa kwa wakulima kutokana na sera ya Tanzania ya viwanda lakini akasifu mpango wa serikali kuhamia Dodoma ambao umeungwa mkono na benki hiyo.

Jonkergouw alisema katika kuunga mkono uhamiaji Dodoma, NMB wameshapeleka tawi la benki tembezi katika mji wa kiserikali Mtumba na kwamba mipango ya baadae ni kufanya maboresho makubwa ya huduma za benki katika eneo hilo.

“Tutaendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara, mimi niseme kuwa benki hii ni mali yenu mna haki ya kuitumia nasi ni wajibu wetu kuwahudumia,” alisema Mkurugenzi.

Akizungumza katika halfa hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge aliomba uongozi wa NMB kuutazama mkoa wa Dodoma kwa jicho la pekee kutokana na ongezeko la watu kufuatia ujio wa makao makuu.

Dk Mahenge aliomba benki kurahisisha masharti katika upatikanaji wa mikopo ikiwemo kuwapa kipaumbele zaidi wakulima wa zabibu zao linalotajwa kuwa mkombozi kwa wenyeji w amkoa huo.

Mkurugenzi wa hospitali ya Benjamini Mkapa ya Jijini hapa Dk Alfonce Chandika alisema benki ya NMB ni rafiki kwa makundi yote kutokana na huduma zake kuyagusa makundi yote.

Dk Chandika alisema kwa sasa huduma zinazotolewa na benki hiyo zinapaswa kuwa mfano kwa taasisi zingine jambo litakalotoa tafsiri chanya kwa Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Albert Jonkergouw akiongea na watumishi wa Serikali na wafanyabiashara kwenye chai ya Asubuhi iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia Serikali jijini Dodoma jana. 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DR. Binilith Mahenge (Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Albert Jonkergouw (Kulia) kwenye chai ya Asubuhi iliyo andaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya kuelezea utayari wa Benki hiyo katika kuhudumia Serikali jijini Dodoma jana.

Kongamano la QNET huko Malayasia lahudhuriwa na wajasiriamali 13 000 wakiwemo waAfrika 2600

$
0
0
Kampuni maarufu ya kimataifa ya mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia, QNET imeendesha kongamano la siku tano la kimataifa ambalo linaleta pamoja takribani wajasiriamali 13,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani katika kisiwa cha Penang, Malaysia Takribani wajasiriamali wa kiafrika wenye shauku wapatao 2600  walishiriki katika kongamano la mwaka huu.

Kongamano ambalo hufanywa mara mbili kwa mwaka la (V-Convention) ni tukio la kipekee ambalo huleta pamoja wateja na wasambazaji wa QNET kutoka maeneo mbalimbali duniani, washirika wake wa kibiashara, na pia maofisa wa serikali kuja kujionea bidhaa na huduma za QNET na kuelewa vyema biashara yake. 

Kongamano la siku tano ilijumuisha mfululizo wa programu za mafunzo, hotuba za uhamasishaji, kutambulisha bidhaa mpya za mtindo wa maisha wa QNET na matukio ya burudani. Kivutio kikubwa mwaka huu ni QNET Carnival ambayo ilionyesha zaidi ya nembo au lebo 30 za bidhaa za QNET katika moja ya maonyesho makubwa kuwahi kufanywa na kampuni hiyo. Bidhaa mpya zilizozinduliwa mwaka huu ni pamoja na virutubisho vipya kwaajili ya afya ya wanaume vinavyoitwa QAlive, na toleo lenye ukomo la saa za kifahari kwaajili ya kumbukizi ya miaka mitano ya ushirikiano kati ya QNET na klabu ya mpira wa miguu ya jiji la Manchester  (Manchester City Football Club). Moja kati ya dondoo zilizoshika hisia za watu ni sherehe za mahafali ya wateja ambao wamekamilisha kozi zao kwa njia ya mtandao kupitia qLean, bidhaa ya elimu ya QNET, ambayo ni maarufu sana miongoni mwa wateja katika kanda ya Sahara ya Afrika. 

Washiriki vile vile walipewa fursa ya kusikiliza kutoka kwa wazungumzaji rasmi ambao wameshinda vikwazo vikubwa na kufanikisha ndoto zao.  Farouk Saad Hamad Al-Zuman, raia wa kwanza wa Saudi Arabia kupanda mlima Everest, na Sparsh Shah, mvulana mwenye umri wa miaka 15 raia wa marekani mwenye asili ya India aliyezaliwa na tatizo la mifupa dhaifu (brittle bones), ambaye alipewa siku 2 za kuishi na madaktari baada ya kuzaliwa, na sasa ni nyota katika mtandao wa Youtube kwa mtindo wake wa kipekee wa mziki ambao anaunganisha pamoja muziki wa classical na rap.  

Bwana Koné Doupin, Mwakilishi wa Kujitegemea anayeshiriki katika kongamano hilo la (V-Convention) kutokea Ivory Coast alisema:  "Nina furaha sana kuwa hapa mwaka huu.  Tangu nilipojiunga na QNET miaka kumi iliyopita, sijawahi kukosa kongamano la -V lolote kwa sababu ni fursa ya kipekee kukutana na viongozi wetu wa juu, kujifunza kutoka kwao, kukutana na watu kutoka sehemu mbalimbali na kugundua upekee wa bidhaa mpya.  Nina shauku kubwa ya kujaribu bidhaa mpya ya QAlive, kirutubisho kipya cha wanaume na kugundua ni jinsi gani kinaweza kuboresha maisha yangu."

Sherehe za ufunguzi ziliongozwa na watu mbalimbali maarufu kutoka Malayasia na Asia ya Kusini Mashariki.  Mgeni rasmi kutoka Afrika, Bwana Cissé Ibrahim Sory vile vile alikuwepo katika sherehe za ufunguzi, Bwana Cissé Ibrahim Sory ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri kutoka ofisi ya Rais katika Jamhuri ya Guinea-Conakry.

Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa QNET aliyeteuliwa, Bi. Malou Caluza alisema: "Matukio kama haya ya Kongamano (V-Convention) hutupa fursa ya kuwahudumia wasambazaji wetu na kuwapa fursa ya kuona na kushuhudia mtindo wa Kuishi Kikamilifu (Absolute Living) ambao inaongoza biashara yetu, Vile vile ni jukwaa bora la kusherehekea ari ya ujasiriamali ambayo kampuni ya mauzo ya moja kwa moja kama QNET inachochea kwa mamilioni ya watu duniani kote, kuwasaidia kuboresha maisha yao na kuchangia katika jamii."

Akiongeza katika hilo, Meneja Mkuu wa QNET wa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Bwana Biram Fall, alisema: "V-Malayasia inafuata msimu wa kongamano la QNET Expo wa mwaka 2019 wenye mafanikio wenye jina la Kuisi Kikamilifu (Absolute Living), linaloenda sambamba na kanuni ya kampuni ya mauzo ya moja kwa moja QNET na falsafa yake ya  RYTHM - Jiinue Uweze Kuwasaidia Wanadamu (Raise Yourself to Help Mankind) Kongamano la mwaka 2019 lilianzia jijini Dar es salaam, Tanzania mwezi uliopita, kisha likahalia Kumasi, Ghana na sasa nchini Malayasia kwaajili ya kongamano la kiulimwengu la V-Convention.  Baadae nchi zingine za Afrika zitakuwa wenyeji wa kongamano la Kuishi Kikamilifu (Absolute living expo)."

QNET, inauza reja reja bidhaa mbalimbali za Afya na ustawi, huduma binafsi na urembo, sikukuu, utunzaji wa nyumba na kozi kwa njia ya mtandao miongoni mwa nyingi zingine ambazo zinaboresha maisha ya kila siku ya wateja wake duniani kote. QNET iliwekwa katika moja kati ya makampuni 100 makubwa na imara ya MLM  (Solid Top MLM Companies) kwa mwaka 2018 na Portal ya habari za mauzo ya moja kwa moja ya Business for Home.

Katika Afrika Magharibi, Chama cha Ghana cha CSR (GHACEA) mwaka 2018 kiliitunukia QNET kuwa Kampuni ya Mwaka ya Biashara ya Mtandao (E-Commerce Company of the Year.)
 Afisa Mtendaji Mkuu wa QNET,  Ms. Malou Calouza(wa kwanza kushoto)  na Maofisa wa serikali ya Malaysia wakikata  utepe kuzindua rasmi kongamano la V-Convetion lililofanyika mjini Penang, Malaysia hivi karibuni. Wengine ni wajumbe wa Bodi wa QNET.
Meneja wa QNET wa kusini mwa Afrika, Biram Fall (kushoto)akiwa amepozi na Mjumbe wa Baraza la Mawaziri Ofisi ya Rais, Guinea-Conakry, Ndugu Cissé Ibrahim Sory wakati wa kongamano la QNET la V-Convetion lililofanyika mjini Penang, Malaysia hivi karibuni.
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images