Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 286 | 287 | (Page 288) | 289 | 290 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0
 • 12/04/13--08:59: KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO
 • Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 4, 2013.
  Waziri wa Nci,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) akiteta na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema,Bungeni jijini Dar es salaam Novemba 4,2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Vyama vya wafugaji nyuki kutoka mkoa wa Tabora kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi, Kazi na Utumishi wa Umma,katika kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Ofisi hiyo,wa mwaka wa fedha 2012-2013 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,(wa pili kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee .
  Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa Ofisi ya Rais, Kazi,na Utumishi wa Umma,wakiwa katika cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Ofisi hiyo,wa mwaka wa fedha 2012-2013 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

  0 0

  Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Leonard Akwilapo akieleza kwa waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) Kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi hiyo ikiwamo uendeshaji wa Mafunzo ya Mitaala kwa walimu nchini, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na Uboreshaji wa Mitaala Bi. Angela Katabaro.(Picha na Hassan Silayo)

  Na Kiza Sungura

  Taasisi ya Elimu Tanzania  [TET]imedhamiria kuendelea kuboresha utendaji wake ili kuinua kiwango cha elimu nchini. 

  Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wataasisi hiyo Dr.Leonard Akwilapo wakati akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam.

  Dr. Akwilapo alisema kuwa kwa kuzingatia mpango mkakati wamaendeleo wamiaka mitano (2011- 2016), taasisi hiyo inatarajia kufanya maboresho katika majukumu yake mbalimbali kwa lengo la kuleta tija katika sekta ya elimu nchini.

  Akitaja mipango ya taasisi hiyo Dr. Akwilapo alifafanua kuwa ni pamoja na kufanya tahakiki ya mitaala katika ngazi zote, kuandaa vifaa vya kujifunzia nakufundishia vikiwemo vitabu, vifaa vya kielektroniki na vipindi vya redio na televisheni.

  Aidha TET inatarajia kukamilisha andiko la Mwongozo wa Taifa wa Ukuzaji Mitaala, kufanya tathmini ya utekelezaji wa mitaala ya elimu ya awali hadi sekondari na kuendesha makongamano ya kitaifa na kimataifa kuhusu mitaala.

  Pia Dr. Akwilapo aliongeza kuwa wana mpango wakujenga kituo cha kisasa cha mafunzo ya ukuzaji mitaala eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, kuandika sera ya utafiti na uelekezi wa kitaalam pamoja na kuendesha mafunzo elekezi kwa walimu na watekelezaji wa mitaala.

  Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu naUboreshaji Mitaala ya taasisi hiyo Bi Angela Katabaro alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita taasisi imeweza kuboresha mihtasari ya masomo 26 ya ualimu ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi.

  Pia Bi Katabaro aliongeza kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI ilichapisha na kusambaza mihtasari na miongozo ya masomo yote ya shule za msingi.

  Kwa upande waelimu ya sekondari taasisi iliweza kuboresha mihtasari 25 ya kufundishia kidato cha tano na sita na kuendesha mafunzo ya utekelezaji wa mtaala wa sekondari kwa walimu wa shule mbalimbali za sekondari hapa nchini.

  0 0

   Semina ikiendelea ikiongozwa na Dada Grace huku wanachama wakisikiliza kwa makini
   Kijana kutoka  Mzizima branch akifafanua jambo kwa wanachama wenzake huku semina ikiendelea.
   Dada Grace akifafanua jambo kwa vijana wake

  0 0  0 0  0 0

   Rais Francois Hollande wa Ufaransa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jijini Paris kwenye mkutano unaohimiza kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na Afrika. Akizungumza katika mkutano huo Rais Kikwete alisema kuwa mbali na kuwa bado bara la Afrika linahitaji  misaada ya uchumi nchi zilizoendelea lazima ziwekeze mitaji katika nchi za Afrika

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Francois Hollande wa Ufaransa,Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast na Rais Mac Sall wav Senegal wakiwa katika mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Afrika na nchi za kiafrika. Picha na mdau Freddy Maro wa IKULU

  0 0
 • 12/04/13--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Ngoma ya Chicco ya 'We Miss You Manelo' iliturusha sana Disko Toto enzi hizo

  0 0

  Chuo cha Diplomasia Dar es salaam, katika kuendeleza wito na wajibu wa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu, kati ya  tarehe 25 na 29 Novemba 2013 kilifanya kozi fupi ya ITIFAKI NA MAHUSIANO YA UMMA (PROTOCOL AND PUBLIC RELATION) Chuoni Kurasini, Dar es salaam
  Washiriki  walitoka maeneo mbali mbali katika sekta binafsi na mabenki kama CRDB Plc na Sekta ya Umma, Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa J.K.Nyerere(JNIA), Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Mhe. Sophia Mjema na kadhalika.
   Wawezeshaji wa Mafunzo haya ya muda mfupi kawaida huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea sana katika mambo ya Diplomasia hivyo kuwapa washiriki uzoefu na kesi halisi zilizowahi kutokea katika eneo husika la mafunzo ili kuwajengea uwezo na waweze kwenda kufanyia kazi moja kwa moja mafunzo na utaalam walioupata. 
   Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bwana, Juma M. Kanuwa akisisitiza  umuhimu wa utaalam wa mambo ya Itifaki na Mahusiano ya Umma, katika sehemu za kazi, alisema kuwa mafunzo hayo  yatarudiwa tena mnamo tarehe 16th – 20th Desemba 2013 hapo Chuo cha Diplomasia ili wale wote walioshindwa kuhudhuria hapo awali wajitokeze  kwa wingi na kupata mafunzo hayo toka kwa mabalozi na wataalam waliobobea na wenye uzoefu wa miaka mingi.
   Washiriki wakimsikiliza na kufuatilia kwa makini mafunzo ya Itifaki (Protocol) toka kwa mmoja wa wawezeshaji Balozi C. A. Sanga ( hayupo pichani)
  Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Mhe. Sophia Mjema akishiriki katika moja ya mijadala
  Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa  Taaluma, Utafiti na Ushauri, Dr. Wetengere Kitojo (aliyekaa katikati mwenye shati la mikono mirefu)

  0 0

  Katibu mkuu  wa  Chadema  Dr  Wilbroad Slaa akiwahutubia  wananchi  wa Kahama mara  baada ya  kuwasili mjini hapo kwa  ziara  yake  ya  kichama jana
  Dr Slaa akisalimiana na  wananchi waliofika  kumpokea mjini Kahama  jana. leo Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya mjini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
   Katibu NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.

   Sehemu ya Wakazi wa jiji la Mbeya Mjini wakishangilia jambo wakati Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye alipokuwa akihutubia,katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana  jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yao katika mkoa huo.
   Pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia mikono wakazi wa jiji la Mbeya waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika uwanja wa Rwanda Nzovwe,nyuma ni Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa Dkt.Asharose Migiro.
    Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Bajaj huku akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara,anaekimbia pichani kulia ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
   Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara.


  0 0

  Na Kiza Sungura- MAELEZO_Dar es salaam

  Shirika la Madini la Taifa [STAMICO] limeingia mkataba wa ubia na Kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited [Tanzanite One] kuhusu uchimbaji wa pamoja wa madini, ya Tanzanite katika kitalu C, Mirerani.
  Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Gray Mwakalukwa wakati akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari mara baada ya hafla fupi ya kusaini mkataba huo.

  Mwakalukwa alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kutoa leseni ambayo inawawezesha STAMICO  kumiliki asilimia 50 na TanzaniaOne watabaki na  asilimia 50.
  Alisema kuwa umiliki huo unatokana na Serikali kusimamia utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ambapo chini ya sharia hiyo, Kampuni za kigeni haziruhusiwi kumiliki hisa zaidi ya asilimia 50 katika uchimbaaji wa vito.

  Mwakalukwa aliongeza kuwa mkataba huo umezingatia makubaliano ya awali yaliyotiwa saini mapema mwaka huu ambayo yataka STAMICO na Tanzanite One kuwa  na gawio sawa la asilimia 50 kwa hamsini litakalotokana na faida.  

  Alitaja baadhi ya mambo waliokubaliana ni pamoja na mitambo ya uchimbaji na uzalishaji itabaki kuwa ni mali ya Tanzanite One itaendelea  kutumika na wabia wataifanyia matengenezo itakapoharibika.

  Mwakalukwa alisema kuwa jambo jingine waliokubaliana ni pamoja na kuanzisha kitengo maalum cha ufuatiliaji na tathmini ya shughuli zote za mgodi kitakachoundwa kutoka kwa wajumbe wa kila pande.

  Naye Mwenyekiti wa Tanzanite One, Balozi  Ami Mpungwe alisema kuwa hatua ya Kampuni yake kusaini  mkataba huo ni sehemu ya  kutekeleza sera ya uchimbaji  wa madini nchini na ni  hatua nzuri  ya  kuhakikisha ulinzi na usalama madini ya Tanzanite.

  0 0

  Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Ujumbe wa Wataalam kutoka Idara ya Afya ya Jimbo la Nanjing,nchini China,waliofika Ikulu Mjini Zanzibar,wakiongozwa na Kiongozi wao Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya Wang Hua,(wa pili kulia).Picha na REamadhan Othman Ikulu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Kongamano la Kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Disemba 5,2013.
  Baadhi ya washiriki wa kongamano la kitaifa la Ajira barani Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua Kongamano hilo leo Disemba 5,2013 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalim Julius nyerere Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika mara baada ya kufungua kongamano hilo leo Disemba 5-2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka mara baada ya kufungua kongamano la kitaifa la Ajira kwa bara la Afrika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Disemba 5,2013. (Picha na OMR)

  0 0  0 0


  Taarifa ya mkutano wa wanachama wa chama cha mapinduzi wa maeneo ya District of Colombia, Maryland na Virginia ( DMV)

   Tunaombwa kwa umoja wetu kuhudhuria mkutano wa wanachama wote ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuimarisha tawi letu.Pia fomu za kugombea nafasi ya wajumbe 10 wa halmashauri kuu ya tawi, katibu UWT, katibu Wazazi na Mwenyekiti umoja wa vijana zinapatikana, tafadhali wasiliana na viongozi ili upewe maramoja ujaze na kuziwakilisha kabla ya mkutano. Tunawakaribisha  wote wanaotaka kujiunga na CCM uandikishwaji wa wanachama wapya utakuwepo siku ya mkutano.

  Tafadhali usikose kuhudhuria ili sauti yako isikike na ushiriki kikamilifu kukijenga chama chetu na kuleta maendeleo ya nchi yetu.

  MAHALI:  1400 University Boulevard Langley Park, Maryland 20783                        ( TABEER RESTAURANT)

  SIKU:          Jumapili, DECEMBER 15,   2013

  SAA:           5.00 p.m -8 pm

  1.     Taarifa fupi ya Tawi

  2.     Mikakati juu ya uimarishaji wa tawi letu

                                      3.   Uchaguzi wa viongozi wa tawi( NAFASI ZILIZOWAZI)

                             4.  Mengineyo


  Tafadhali tujitokeze kwa wingi kama ilivyo desturi yetu kina Baba tunaomba maji na soda na kina Mama Vitafunio. Tafadhali zingatia muda.

  Asanteni


                                                              Uongozi wa  CCM Tawi la DMV


  0 0

  Kinana akimkabidhi Mwenyekiti wa Vijana wa Tarafa ya Ikuwo, Tunsume Shemgogo ufunguo ikiwa ni ishara ya kukabidhi Trekta kwa vijana wa Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kusaidia Kilimo.Trekta hilo limetolewa na CCM kwa vijana wa mkoa huo,aidha makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye kambi ya vijana iliyopo kweneye kijiji cha Mlengu,kata ya Kiangala,tarafa ya Ikuwo wilayani Makete,mkoani Njombe,ambapo kambi hiyo ina eneo la ekari 300 za mashamba,Ndugu Kinana aliahidi kutoa Trekta hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo mnamo Agosti mwaka huu,baada ya kuelezwa jinsi vijana hao walivyojiunga pamoja katika kikundi na kuamua kujishughulisha na kilimo ili kujikwamua na suala zima la umaskini.
  Kinana akilima shamba la vijana wa Tarafa ya Ikuwo kwa kutumia trekta wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Kijiji cha Mlengo, wilayani Makete mkoani Njombe leo jioni.shamba  hilo  la Vijana
   wapatao  252 wakiwa na shamba lenye ukubwa wa ekari 300,wamekabidhiwa Trekta lenye thamani ya sh. mil 42.
  Kinana (kulia), Dk. Asha Rose Migiro wakiangalia vyerehani vya kisasa walipotembelea Chuo cha Ufundi Stadi cha Makete-VETA.
  Injinia Asifiwe Swalo akielezea mashine mojawapo ya mbao inayofanya kazi ya kuchana mbao katika mianguko mbalimbali ikiwemo na kuweka urembo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mara baada ya kutembelea karakana ya ufundi Selemara.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda mti nje ya eneo la chuo hicho cha VETA,kushoto kwake anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini,Bi.Monica Mbele.
  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akishiriki upandaji miti nje ya eneo la chuo hicho cha VETA,mapema leo Wilayani Makete mkoani Njombe.
  Pichani katini katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Makete,Mh. Josephine Matiro (kushoto) na  Mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini,Bi.Monica Mbele.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0


  TANZANIANS THANKS FOR YOUR VOTES –3 DAYS TO GO TO THE FINALE!
  now
  HISIA is among the 6 finalists!

  3 DAYS to go before East Africa’s favorite music reality show produces an East African star for the 6th time through Tusker.
  You have a say on who takes the grand price home.  Our Tanzanian representative HISIA depends on your votes to win.

  EVERY SINGLE VOTE COUNTS!

  HOW TO VOTE
  a)      Create your account on https://tusker.mobi/register to have a say on who wins the grand price ( ONE VOTE PER DAY)

  Or

  b)      SMS the words Tusker12 to the number 15324 ( 5 SMS PER PERSON PER DAY)

  ITS YOUR TIME TO TAKE THE STAGE / UZALENDO MBELE!

  0 0

   Jumuiya ya WaTanzania Manchester pamoja na  familia ya Bwana Rajab Mbeyu  tunasikitika kuwatangazia kifo cha Ndugu yetu / Mtanzania mwenzetu Bw. HASSAN MBEJU  (pichani) kilichotokea hapa Manchester. 
   Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu . 
  Tunaomba kuwapa ratiba rasmi pale itakapokuwa tayari.

  Kwa sasa tunawaomba Watanzania wote popote pale mlipo michango yenu ya hali na Mali ili kuweza fanikisha hili. Michango yote tafadhali tunaomba iwasilishwe kwa wahusika  wafuatao:-
      
   Abdul Dau (Leicester ) : 07792104495 
               Abeid   Hamis (London)
  NATWEST BANK
  Sort Code :61 01 37
  Account No: 52724743
  Victor Mashamba (Manchester): 07979 656 165 
  Tanzania Association in Greater Manchester 
  NATWEST BANK
  Account No: 21148066
  Sort Code : 01 01 97

  TAFADHALI WEKA REFERENCE "MBEJU".
   Kwa Maelezo zaidi tafadhali wasiliana na 
  wahusika wahusika hapo juu au  wafuatao:
  Sophie Mbeyu (Sweden)  +46762898798
  Ishaqa Mbeyu (Norway)   +4798473806 or +4796659593
  Jestina George  07404332910
  Dr.Mohamed Zahrani (London)  07931706414
  TANZANIA
  Sheikh Issa Othman (Msikiti wa Maamur Dar es salaam) 0719372319
  Nuru Mbeyu (Dar es salaam) 0713432565
  "INNA LILLAH WA INNA ILAYHI RAJIUUN"
   "KWA HAKIKA SISI SOTE NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA "
  TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU ZA DHATI
  MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI .
       

older | 1 | .... | 286 | 287 | (Page 288) | 289 | 290 | .... | 3270 | newer