Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI IKUPA ALIPONGEZA SHIRIKA LA COMPASSION INTERNATIONAL KWA KUSAIDIA WATOTO NA VIJANA NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amelipongeza Shirika lisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania (CIT) kwa kuwahudumia na kuwapatia watoto na vijana stadi za maisha zinazowawezesha kujitegemea.
Naibu Waziri Ikupa ametoa pongezi hizo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya Shirika hilo yaliyofanyika leo Aprili 27, 2019 katika ukumbi wa Kanisa la TAG lililopo Mipango, Jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yalikuwa na Kauli Mbiu isemayo; “Wekeza kwa Watoto na Vijana kwa Uchumi Endelevu.”
Alieleza kuwa Shirika la Compassion International Tanzania limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto na vijana nchini wanahudumiwa na kuondokana na hali ya umasikini kwa kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii na Taifa.
“Shirika hili ni la mfano na limeendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwalinda watoto na kuwapa fursa ya kufikia ndoto zao na kuwapatia vijana ujuzi wa stadi za maisha zinazoleta mabadiliko chanya kwao na kuwaletea maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla,” alisema Ikupa
Aliongeza kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekuwa akionesha watanzania namna gani nchi yetu imeweza kujitegemea katika kutekeleza shughuli mbalimbali, hivyo Mhe. Rais ni mfano tosha wa kuigwa na vijana nchini kwa kuona wanauwezo wa kujitegemea.
Aidha, Naibu Waziri Ikupa alitoa rai kwa vijana kuacha kukaa kwenye vijiwe bila sababu za msingi na kubadili mitazamo, bali watumie muda wao kutafakari shughuli za kufanya kwa bidii ambazo zitawaletea maendeleo na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
“Serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa vijana ili waweze kuanzisha shughuli mbalimbali zitakazo wawezesha kukua kiuchumi, tumieni fursa ya ujuzi mliopata kupitia shirika hili na ubunifu mlionao kuchangamkia fursa hiyo muhimu itakayowawezesha kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo viwanda,” alisema Ikupa
Pia alitoa wito kwa jamii kuripoti haraka vitendo vya unyanyasaji wa watoto katika madawati ya jinsia na watoto yaliyopo kwenye vituo vya polisi nchini na kwa maafisa ustawi wa jamii ili kutokomeza vitendo hivyo kwa kumjengea mazingira salama motto na kumuonesha jamii yake imejaa upendo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanawatetea na kuwasimamia watoto na kuwapatia nafasi vijana ya kujitambua kwa kuchangamkia fursa ambazo zipo katika jamii na kuleta ufumbuzi wa kimaendeleo.   
“Maono ya shirika ni kuona wanufaika wanatoka katika uhitaji na kujijengea dhana ya kujitegemea, vilevile kuwa wahisani wa watu wengine,” alisema Hotay
Shirika la Compassion International Tanzania (CIT) ni sehemu ya Compassion International ambalo ni shirika la kimataifa la Kikristo linalojihusisha kuhudumia watoto na vijana wanaotoka katika kaya maskini kwa njia ya ufadhili. Shirika hili limekuwa likifanya huduma hii hapa nchini toka mwaka 1999.
Kwa sasa Shirika hilo lipo katika Mikoa 19 ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Kigoma, Manyara, Pwani, Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Lindi, Geita, Mtwara, Simiyu na Kagera.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akizungumza na washiriki waliohudhuria katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Shirika la Compassion International Tanzania yaliyofanyika Aprili 27, 2019 katika ukumbi wa Kanisa la TAG lililopo Kata ya Miyuji, Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay akielezea kuhusu huduma zinazotolewa na Shirika la Compassion International Tanzania wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (wa pili kutoka kushoto) akifuatilia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanakwaya ya Muunganiko wa Makanisa ya Kiinjili wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 20 ya Shirika la Compassion International Tanzania.
Afisa Maendeleo ya Vijana, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Happy Mwaipopo akielezea jambo kuhusu Mikopo inayotolewa na Ofisi hiyo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
 Baadhi ya Maaskofu kutoka kwenye Makanisa ya Kiinjili hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa hafla hiyo.

 Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa hafla hiyo.

 Sehemu ya Washiriki wa walioudhuria kwenye hafla ya Maadhimisho ya Miaka 20 ya Shirika la Compassion International Tanzania yaliyofanyika Jijini Dodoma, Aprili 27, 2019.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa Shirika la Compassion International Tanzania na watendaji wa Ofisi yake. Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhe. Lolensia Bukwimba, (wa tatu kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Taifa wa Shirika la Compassion International Tanzania, Bi. Agness Stanley Hotay.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA KWA ASKOFU GERVAS NYAISONGA KUWA ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU KATOLIKI MKOANI MBEYA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Jimbo hilo.
8
9..
 Mke wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli  Mama Janeth Magufuli akimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Jimbo hilo.
1
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiongoza Ibada ya kumsikima Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya katika Ibada iliyofanyika katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
23
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa amekaa kwenye kiti wakati Ibada ya kusimikwa kwake ikiendelea katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
5
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akisalimiana na Mapadre wa Kanisa Katoliki mara baada ya kusimikwa Rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya.
6
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa ameketi kwenye Kiti cha Uaskofu pamoja na Maaskofu wengine wa Kanisa Katoliki nchini.

9.11
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akipongezwa na Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki mara baada ya kusimikwa Rasmi. PICHA NA IKULU
12
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga akiwa amekaa kwenye kiti wakati Ibada ya kusimikwa kwake ikiendelea katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
034A1097
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikusanya Sadaka kwa waumini mbalimbali waliokusanyika katika uwanja wa Sokoine katika ibada ya Kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mkoa wa Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga
034A1098034A1101034A1135034A1143034A1190034A1215034A1218

Naibu Waziri Shonza awataka Watanzania Kuandaa Mashindano ya Kusaka Vipaji vya Muziki kuanzia ngazi ya Wilaya Mpaka Mkoa

$
0
0


Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kulia) akiwasili katika viwanja vya   Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) jana na kupokewa na vijana wanaoshiriki mashindano  ya Kabati Star Search ambapo mashindano hayo yanafanyika hapo, watatu kushoto ni  Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa ambaye ndiye mwandaaji wa mashindano hayo.
PIX 4 B
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili kushoto)akisalimiana na mchekeshaji maarufu Baraka Mwakipesile anayeigiza kama Rais Magufuli ambapo kwa sasa anajulikana  kama Baraka Magufuli mara baada ya uzinduzi wa mashindano ya Kabati Star Search yaliyofanyika jana Mkoani Iringa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufundi Bw.Netho Ndilito.
PIX 4PIX 5
Mmoja ya washiriki wa mashindano ya  Kabati Star Search Yahya Hamadi  kutoka Kata ya Mwangata  Mkoani  Iringa  akionyesha uwezo wake kwa kuimba  wimbo wa Msanii Young Killer katika mashindano hayo yaliyofanyika jana ambapo yalizinduliwa na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (hayupo pichani).
PIX 6
Mmoja ya washiriki wa mashindano ya  Kabati Star Search Sophia Kalinga kutoka Kata ya Gangilonga  Mkoani  Iringa  akionyesha uwezo wake kwa kuimba  wimbo wa You Raise Me Up  kutoka kwa msanii Josh Groban katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Mkoani hapo.
PIX 7
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kushoto ) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Shindano la Kabati Star Search mara baada ya uzinduzi wa shindano hilo lililofanyika jana  Mkoani  Iringa, wapili kushoto ni muandaaji wa shindano hilo Ritha Kabati Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa .
PIX 8
Msanii wa Mkoa wa Iringa Ezra Msiliova maarufu kama Eze Nice akiimba  kwa hisia wimbo  wa kuisifia Tanzania mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa uzinduzi wa Shindano la Kabati Star Search lilofanyika jana Mkoani Iringa.
………………………………………………………………………………

Na Anitha Jonas- Iringa

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ameto wito  kwa  wadau mbalimbali nchini kujitokeza kuandaa Mashindano ya kusaka vipaji vya Muziki kwa vijana kwa kuanzia ngazi za Mikoa na Wilaya.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo jana Mkoani Iringa alipokuwa akizindua Tamasha la Ritha Kabati Star Search lililolenga kusaka  vipaji vya vijana wanaojua kuimba muziki na tamasha hilo limekusanya vijana zaidi ya 150 kutoka maeneo mbalimbali ya wa Mkoa wa Iringa.

“Ninapenda kumpongeza Mhe.Ritha Kabati  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kwa kuandaa Tamasha lenye tija kwa taifa kama hili, pia ninaomba wadau mbalimbali wenye uwezo kuandaa matamasha kama haya kwa kuanzia ngazi za mbalimbali ndani ya mikoa na wilaya zetu kwa ndiko waliko vijana wenye vipaji,  tuwasaidie kufikia ndoto zao kwa manufaa ya taifa,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo wa Kabati Star Search Naibu Waziri huyo alimtaka Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Iringa kuandika barua kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ya kuomba wataalamu kuja kutoa mafunzo kwa wasanii chipukizi wa muziki wa mkoa huo kwa lengo la kuwa ongezea maarifa wasanii hao.

Naye muandaaji wa Tamasha hilo Mhe.Ritha Kabati alieleza kuwa amekuwa akiwaona  vijana wa mkoa huo na kuwa wanavipaji  ila wamekuwa wakikosa jukwaa la kuonyesha vipaji vyao na ndiyo maana aliamua kuanzisha mashindano hayo ambayo yatawainua vijana wa mkoa wa Iringa nao kuanza kusikika Kitaifa na Kimataifa kama wasanii wengine maarufu hapa nchini.

“Katika kuhakikisha mashindano haya yanaleta mafanikio nilizungumza na mmoja wa walezi  wasanii wa Muziki  nchini  Bw. Said Fella Maarufu kama Mkubwa Fella kuhusu kuwasaidia washindi wa mashindano haya na tukakubaliana kuwa mshindi wa kwanza mpaka watatu  atawachukua na kwenda kuwafunza vizuri kisha watarekodi  nyimbo zao na pia wataimba na wasanii maarufu hapa nchini na atahakikisha na hizo nyimbo zao zinapigwa katika vituo vya redio na televisheni mbalimbali nchini,”alisema Kabati.

Pamoja na hayo Kabati alieleza kuwa vijana wa Iringa wamesema wanataka nao Mkoa wao uonyesha  kuwa unavipaji vyenye uwezo mkubwa wakufikia ngazi za Kimataifa kwani  kupitia mashindano ya mpira wa miguu ya Kabati Challenge Cup vijana watatu tayari wamechukuliwa na timu za mpira za Afrika Kusini kwa lengo la kwenda kuchezea timu za vijana na watakuwa wanasomeshwa huko pia .

Halikadhalika na mmoja wa washiriki wa mashindano hayo  Yahya Hamadi alimshukuru mbunge huyo wa viti maalum kwa kuandaa mashindano hayo na ameahidi kuwa atajitahidi kufanya vizuri kwani  anaamini  kupitia jukwaa hilo nae anaweza kuja kuwa msanii maarufu katika Taifa.

Hata hivyo Naibu Waziri Shonza aliwasihi majaji wa mashindano hayo kutenda haki katika maamuzi wanayoyafanya kwani  wao ndiyo wenye dhamana ya  kutoa msanii atakayetangaza mkoa na taifa kwa ujumla katika ngazi za Kimataifa,ambapo mmoja  wa majaji hao Bw.Roger Magoha kwa niaba ya wenzake aliahidi kusimamia hilo.

WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE UWANJA WA NDEGE WA KIA

$
0
0


Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mlango (geti) la kielektroniki kwa ajili ya ukaguzi wa abiria, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Watalii kutoka Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, kutoka kushoto ni Naomi Moscovich, akiwa na binti zake, Dana Moscovich(kulia) na Lihi Moscovich (katikati). Aprili 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
…………………………………………………………………….

*Ni yenye kuonyesha wanyama, milima, fukwe, mambo ya utamaduni
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa bodi ya KADCO uhakikishe unaweka mabango ya kielektroniki yenye kuonesha vivutio vya utalii kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

 “KADCO na Wizara ya Maliasili na Utalii, shirikianeni kuweka utaratibu wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii hasa wanyama kwenye viwanja vyote vya ndege. Tunazo mbuga, milima, fukwe za bahari na ngoma za makabila mbalimbali, wekeni mabango yanayobadilisha picha.” 

 “Screens zenye wanyama wanaobadilikabadilika zinaleta mvuto lakini pia ni fursa ya kutangaza vivutio vyetu. Nimezunguka humu ndani, kuta zote ni nyeupe tu, tumieni fursa hiyo kutangaza tamaduni zetu na vivutio tulivyonavyo,” Waziri Mkuu alimweleza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), Mhandisi Christopher Mukoma. 

Alitoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Aprili 27, 2019) wakati akikagua miundombinu ya uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kuwaaga watalii 274 kutoka Israeli wanaowawakilisha wenzao 1,000 walioondoka nchini jana kurejea kwao.

Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alikagua eneo la mapokezi, sehemu ya abiria wanaoondoka na wanaowasili, sehemu ya uhamiaji, mashine za kukagua mizigo ya wanaoondoka na wanaowasili, sehemu za kutolea huduma na maduka.
Pia alimwagiza Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji kwenye kiwanja hicho cha ndege, Bw. Filbert Ndege awasiliane na makao makuu yake ili waangalie uwezekano wa kuongeza madirisha ya kutolea huduma za uhamiaji (counters) ili huduma hiyo itolewe kwa kasi zaidi. 

 “Angalieni cha kufanya, ikibidi eneo hili lipanuliwe na counters nyingine ziongezwe ili kufasttrack utoaji wa huduma hasa msimu ambao watalii wengi huingia nchini.”

 Pia aliwataka KADCO waboreshe eneo la maegesho ya magari kwa kufanya upanuzi na kujenga maturubai ya vivuli (shades) ili kuyakinga na jua kali magari ya wateja

MTANZANIA ANG'ARA MBIO ZA MARATHONI UJERUMANI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
FAILUNA Abdi Matanga kutoka Tanzania ameshika nafasi ya tatu  katika mbio za Hispa Hambarg marathoni kwa upande wa wa wanawake mashindano yaliyomalizika leo mchana nchini Ujerumani na kuvunja rekodi ya muda wake wa awali.

Failuna amekimbia kwa muda wa saa 2:27:56 na kutunukiwa medali ya shaba huku mkimbiaji mwingine kutoka Tanzania Gloria Makula akishiaka nafasi ya 30 baada ya kukimbia kwa muda wa 2:49:07.

Failuna aliachwa kwa muda wa dakika tatu na mshindi wa medali ya dhahabu wa mbio hizo Dibabe Kuma kutoka nchini Ethiopia ambaye alitumia saa 2:24:42 huku nafasi ya pili ikishikiliwa  Magdalyne Masai kutoka Kenya aliyekimbia kwa saa 2:26:04.

Kupitia ujumbe wa Whatsap Failuna amesema kuwa alitamani kushinda medali ya dhahabu lakini alipitwa dakika za mwishoni.

Katika mashindano hayo kwa upande wa wanaume Tadu Abate  kutoka Ethiopia ameshinda baada ya kukimbia kwa saa 2:08:26 huku raia mwingine kutoka Ethiopia Ayele Abshero akimaliza nafasi ya pili kwa kutumia saa 2: 08:27 wakimwacha mshindi na bingwa wa Olympiki wa mwaka 2012 Stephen Kiprotich kutoka Uganda aliyeshika nafasi ya tatu.

USAJILI LAINI ZA SIMU KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE, WANANCHI WOTE KUFIKIWA.

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv, Morogoro

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Mashariki imesema kuwa wananchi wote wenye laini za simu za simu watafikiwa na huduma ya usajili wa laini za simu kwa vitambulisho vya Uraia na alama za vidole na watoa huduma wa kampuni za simu nchini.

Hayo yamesemwa kutokana na kuibuka kwa sintofahamu ya namna wananchi watakavyofikiwa na watoa huduma kwa ajili ya kusajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na kitambulisho cha uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Mamlaka hiyo imewatoa hofu wananchi wote na kuwahakikishia kwamba watafikiwa na watoa huduma za mawasiliano.

Akizungumza katika Mnada wa Dakawa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema wananchi wote watapata usajili wa laini zao kwa kutumia alama za vidole kwa kuwa na vitambulisho vya taifa.

Mhandisi Odiero amesema kazi yao ni kutoa elimu kwa wananchi wote hivyo watawafikia kwa njia yoyote kuhakikisha wananchi hawapati changamoto wakati wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Amesema usajili ni jitihada za Serikali katika kuhakikisha usalama wa watumiaji wa huduma za Mawsiliano kutokana na changamoto kwa baadhi ya watumiaji kutumia mawasiliano kinyume na utaratibu uliowekwa lakini kwa sasa ni kitambulisho kimoja tu ambapo mtu akifanya uharifu ni rahisi kumfikia na hatua zitachukuliwa.

Mhandisi Odiero amesema awali TCRA iliruhusu vitambulisho vingi hata barua za Serikali za Mtaa katika kusajili hali iliyofanya baadhi ya watumiaji kukiuka taratibu ikiwemo kudanganya na kutoa taarifa za uongo wakati wa usajili na hivyo na kutoa mwanya hata kwa wahali kutumia vitambulisho hivyo kujisajili na kufanya utapeli wa kujipatia kipato kisichokuwa halali.

Naye Eng. Robson Shaban (Mhandisi mwandamizi wa Mamlaka hiyo) ameasihi wananchi ambao tayari wana vitambulisho vya Uraia kusajili mapema (Ifikapo tarehe 01/05/2019 ambayo ndio mwanzo wa Usajili) laini zao na sio kusubiri mwisho na kuonekana usajili una changamoto wakati muda ulikuwepo na wakashindwa kufanya hivyo.

Katika Mnada huo watu wengi waliuza maswali na kujibiwa na maofisa kutika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Mashariki. Mamlaka inaendelea kuwaelimisha watumiaji juu ya umuhimu wa zoezi hilo.
 Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Robson Shaban akiwapa maelezo ya kitabu cha muongozo wa mawasiliano katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.
Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Robson Shaban akitoa elimu ya usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.

 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mfumo mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akimpa maelekezo mwananchi wakati wa otoaji wa elimu ya namna ya usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.

Dc amsweka Ndani Mwkiti wa Kijiji kwa kutafuna mamilioni ya fedha za Kijiji

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud,Longido

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ewor ndeke katika kata ya Kimokokua wilaya ya Longido, Moses Lesikar Leng'ese Ole Nasuaku, anashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya hiyo akituhumiwa kujipatia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 135 zilizolipwa na wakala wa umeme vijijini Rea kama fidia ya kupisha usambazaji wa umeme.

Akiongea na vyombo vya habari Mkuu wa wilaya hiyo ,Frank Mwaisumbe amesema hatua hiyo imekuja kufuatia malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho wakimtuhumu mwenyekiti wao kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mradi wa Rea baada ya kudanganya kuwa maeneo yanayopitiwa na mradi huo ni mali yake wakati si kweli.

Mwaisumbe alifafanua kuwa mwenyekiti huyo alilipwa mara mbili akitumia majina tofauti ,ambapo alilipwa kiasi cha sh,milioni 66 kwa hekari saba na sh,milioni 69 kwa hekari 10 huku akitumia majina ya Lesikar Leng'ese na Moses Leng'ese na kujipatia kiasi hicho cha fedha.

Alisema kuwa kabla ya kutiwa mbaroni kwa mwenyekiti huyo Wanakijiji saba waliohojiwa ,watano walidhibitisha maeneo hayo ni ya kijiji huku wawili ndio walisema ni Mali ya mwenyekiti huyo anayemiliki tangu mwaka 2013 ,ingawa hatua ya upimaji maeneo ya mradi ilishapita tangu mwaka ,2008 .

"Ni kweli tumemkamata kwa kosa la kujipatia fedha kinyume cha SHERIA na kosa hilo ninaangukia kwenye uhujumu uchumi ,nimempa siku saba arejeshe fedha hizo na baada ya hapo tutampeleka mahakamani" Alisema Mwaisumbe

Aliwataja wengine waliotumia mpango huo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia maeneo hayo ya Kijiji ambao wanatafutwa ni pamoja na Elia Shapashina Kool na Luka Sambeke Ole Mboloso

Wengine ni mwenyekiti wa kitongoji cha Maatiani aliyetambulika kwa jina moja la Kerimboti ,Sindiyo Leakui na Nengolo Sadaka wote wakazi wa Kijiji cha Ewor ndeke.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa fedha hizo zimelipwa wiki tatu zilizopita kama fidia kwa maeneo yaliyopitiwa na mradi huo wa Rea baada ya kupimwa na kuthaminishwa mwaka 2008 ambapo fedha hizo ziliopaswa kuwekwa kwenye akaunti ya Kijiji lakini mwenyekiti huyo na wenzake walitumia akaunti binafsi kujinufaisha.

Wakati mkuu huyo wa wilaya akichukua hatua hiyo wananchi wa Kijiji hicho wakiwemo wanawake wametishia kufunga ofisi ya kijiji hicho kama njia pekee ya kushinikiza kiongozi huyo kuachia ngazi .

Mmoja ya wananchi wa Kijiji hicho, Mbayo Olotito alisema kuwa mwenyekiti wao amekosa uaminifu kwa muda mrefu na wanajipanga kupeleka kilio chao kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ili kushinikiza kuweza kuchukuliwa hatua zaidi kwa mwenyekiti huyo na wenzake walioshiriki kuhujumu maeneo ya Kijiji na kujinufaisha wenyewe.

"Huyu mwenyekiti kwa muda mrefu amekuwa akichochea migogoro ya Ardhi kwa wananchi na kujinufaisha " Amesema Olo Tito.

TANZANIA NA KENYA WAANZA KUJADILI KUONDOA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA MIPAKANI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Longido

Mawaziri wa Kenya na Tanzania wamekutana kutatua changamoto za mipakani Kati ya nchi hizo mbili ili kuongeza ufanisi na kuondoa changamoto Kwa Wafanyabiashara wa pande hizo mbili.

Mawaziri wa Biashara kutoka nchi za Kenya na Tanzania wamekutana kujadili na kutatua changamoto za kibiashara katika mipaka ya nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuskiliza kero za wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi ili kuondokana na usumbufu wanaoupata wafanyabiashara.

Wafanyabiashara hao wameeleza changamoto ya mizigo yao kukaa muda mrefu mipakani humo pamoja na changamoto ya hati za muda za kusafiria madereva kutolewa kwa muda mfupi hivyo kuathiri biashara hivyo wameomba hati hizo zitolewe kwa muda wa mwaka mmoja na si kwa safari moja pekee 

Waziri wa biashara nchini Kenya Chris Kibito amesema kuwa asilimia 45% ya biashara ya afrika mashariki inafanyika kati ya Tanzania na Kenya hivyo ni vyema kuimarisha mahusiano ya kibiashara ili nchi zote mbili ziweze kunufaika pia ameahidi kushughulikia kwa karibu changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara mipakani humo 

Amesema kuwa mbali na biashara kuchelewa mipakani kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo suala zima la upimaji wa viwango vya bidhaa zinazovuka watajitahidi kuhakikisha masuala yote yanatatuliwa ndani ya miezi mitatu.

Amesema malengo ya biashara ni kukuza uchumi Kwa upande mmoja na hivyo kama suala hilo halikuchukuliwa Kwa kuliangalia Kwa ndani kuondoa changamoto basi hatutapiga hatua kiuchumi.

Waziri wa biashara na viwanda nchini Tanzania JOSEPH KAKUNDA amesema kuwa changamoto zilizofikishwa na wafanya biashara hao wanazifanyia kazi kwa kushrikiana na maslahi mapana ya nchi zote hivyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuwa na uvumilivu wakati wakisubiri majibu ya changamoto hizo.

Amesema kuwa hakuna nchi hata moja ambayo inataka kuona changamoto za kibiashara kwenye mipaka hivyo ndio maana wamekutana kujadili na kuona namna nzuri ya kuondoa changamoto za kibiashara mipakani mwa nchi hizo

Mawaziri kutoka nchi za Kenya na Tanzania wameweka saini ya makubaliano ya kukutana mara mbili kwa mwaka ili kutatua changamoto za kibiashara na kuimarisha mahusiano.


RC Tabora Aapa, Atakaye Hujumu Mradi Wa Trekta Hatamuonea Aibu

$
0
0
Na Editha Edward, Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) amekabidhi Mradi wa Matrekta 14 yenye thamani ya Shilingi  bilioni 2.5 kwa vyama vya ushirika vya mkoa huo katika hafla iliyofanyika wilayani Igunga Mkoani Tabora na kutoa onyo kwa wale watakaoenda kuyaegesha bila ya kufanyia kazi.

Mbali na vyama vya ushirika Mwanri amekabidhi Matrekta kwa watu binafisi wakiwemo mapdri, Maaskofu, na Masheikh wa mkoa huo huku akisisitiza kuwa Matrekta hayo yatumike katika Shughuli za kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kwa ujumla

Pia mkuu huyo wa Mkoa mbali na kulishukuru Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)  kwa mpango wake wa kutoa Matrekta kwa Wakulima ameliomba Shirika hilo Kuchangamkia Fursa nyingine za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Tabora

Hata hivyo mkoa wa Tabora una fursa za uwekezaji kwenye wilaya zake zote katika Sekta za  Nyama,  Asali,  Ngozi, na Tumbaku ikiongoza kwa asilimia 60 huzalishwa nchini.

Benki ya NMB Yazidi kujitanua, yazindua Rasmi Tawi lake Mbogwe

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la NMB Mbogwe lililopo wilayani Mbogwe Mkoani Geita mwishoni mwa juma. Wakishuhudia tukio hilo ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse (kushoto), Meneja wa Tawi la NMB Mbogwe – Daudi Mkanza na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara – Donatus Richard, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe - Martha Mkupasi na Meneja Uhusiano Biashara ya Serikali NMB – Suma Mwainunu.


Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert (Kushoto) akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mbogwe mkoani Geita. Tawi la NMB Mbogwe linafanya Benki ya NMB kuwa na matawi 229 na ATM Zaidi ya 800 nchi nzima. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Tawi la NMB Mbogwe – Daudi Mkanza na Mkuu wa Kitengo cha Biashara – Donatus Richard.




Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert (mwenye Kofia) akimpongeza Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi – Sospeter Magesse mara baada ya kuzindua rasmi tawi la NMB Mbogwe la wilayani Mbogwe mkoani Geita. Tawi la NMB Mbogwe linafanya Benki ya NMB kuwa na matawi 229 na ATM Zaidi ya 800 nchi nzima. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara – Donatus Richard.
Mkuu wa Mkoa wa Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert akitoa hotuba kwenye muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Tawi la NMB Mbogwe, wilayani Mbogwe mwishoni mwa juma. Tawi la NMB Mbogwe linafanya Benki ya NMB kuwa na matawi 229 na ATM Zaidi ya 800 nchi nzima.


Benki ya NMB imezindua tawi jipya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kwa lengo la kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi katika kanda ya Magharibi. Hilo ni tawi la 25 kwa mkoani Geita na la 229 nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua tawi hilo, mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Geita Eng. Gabriel Luhumba amesema ufunguzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka kwa kuwa ofisi za serikali zinampango wa uchumi wakimkakati ambao utafanya Geita kuwa chachu ya maendeleo nchini.

Akiongea na wananchi wa wilaya ya Mbogwe Eng. Gabriel Luhumba pia ametoa rai kwa wananchi kubadilika na kuacha mazoea ya kuweka pesa majumbani na kuwataka kuwa na tabia ya kuweka benki na kwenye taasisi za fedha.

Eng.Luhumba alisema wananchi wa mkoa wa Geita wenye neema nyingi ya madini aina ya dhahabu wamekuwa na tabia ya kutunza fedha zao nyumbani hali ambayo imekuwa ni hatari kwa usalama wa maisha yao na kuwataka kuacha tabia hiyo.

Alisema mazoea na tabia ya kuweka fedha kwenye vitanda , kuchimbia chini au kwenye mazizi ya mifungo ilishapitwa na wakati kwa kipindi hiki na kuwataka vipato vyao vya pesa wanapopata kwenda kuziweka benki na kwenye taasisi za zinazotunza fedha.

“Ndugu zangu wananchi uhai katika maisha yetu ni bora sana, katika familia zetu , tabia ya kuendelea kukaa na fedha majumbani kwetu ni hatari sana kwa sababu unaweza kuvamiwa na watu waharifu wakawashambulia na kupoteza maisha kwa hiyo rai yangu mnapopata pesa iwe hata kidogo lazima tupeleka kuziweka benki,, Alisema Eng.Luhumba.

Eng. Luhumba katika hotuba yake alitoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Mbogwe kutumia fursa zinazotolewa na benki hiyo kujiletea mafanikio kiuchimi katika maisha yao na kuwataka kuwa wakopaji wazuri wa mikopo na kulejesha kwa wakati.

Mbali na kuipongeza menejimenti ya benki hiyo, aliipa changamoto ya kuhakikisha inaweza kuandaa Kongamano la biashara katika mkoa wa Geita ilikuwapa msasa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu kuchangamkia fursa zilipo mkoani humo ilikuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yenye tija ndani na nje ya kanda ya Magharibi na Afrika Mashariki.

Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi alisema anaishukuru benki ya NMB kwa kuwasogezea huduma za kibenki kutokana na kuwa wananchi walikuwa na kilio cha siku nyingi kwa serikali kuitaka benki kwa sababu walikuwa wasafiri zaidi ya kilimita 50 kufaata huduma hizo wilaya jirani za Bukombe na Kahama mkoa wa Shinyanga.

Mkupasi alisema kufunguliwa kwa tawi hilo la benki hiyo kumewaondolea aza waliyokuwa wanaipata kusafiri na fedha umabari mrefu hali iliyokuwa inahatarisha maisha yao kwa kuhofia kuvamiwa na majambazi , kwa kusogezewa huduma hiyo na kuwahimiza kutumia fursa hiyo kuichumi na kujiletea maendeleo.

Awali katika hotuba yake mkuu wa kitengo cha biashara wa benki ya NMB , Donatus Richard alisema sasa tawi hilo ni la 229 kwa nchi zima na huo ni wajibu wao katika kuwasogezea huduma hizo wananchi, wafanyabiashara wa dogo, wa kati na wakubwa ili kuwawezesha watu kupata mitaji kwa ajili ya biashara na shughuli mbalimbali nalengo la kuwanyanyua kiuchumi na kuwaomba wachangamikie fursa zionazotolewa na benki ili kujiletea maendeleo.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 29,2019

SHETA, NICK WA PILI WAMCHEZESHA KIDUKU NAIBU WAZIRI WA MAJI

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa kizazi Bongo fleva , Shetta akicheza na Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso wakati wa uzinduzi wa AWESO CUP Katika Wilaya ya pangani mkoa ni Tanga
 Msanii wa Hip Pop nchini Nick wa Pili akiimba kwa pamoja na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso wakati wa uzinduzi wa AWESO CUP iliyofanyika katika Viwanja vya Kumba Wilaya ya Pangani
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Madee akiimba na wakazi wa pangani katika uzinduzi wa AWESO CUP Wilaya ya Pangani Madee ni mmoja ya Wasanii wazawa katika mkoa huo alitumia muda huo kutoa hamasa kwa viajana wa Wilaya pangani kutokata Tamaa.
 Kiongozi wa kundi la Uzalendo kwanza na Msanii wa Vichekesho Nchini,Steve Nyerere akizungumza na wakazi wa pangani ni namna gani kupita uzalendo kwanza watakavyoweza kuipaisha wilaya hiyo .
 Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara akishukuru kwa wakazi wa pangani kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono mbunge wao na kusema kuwa wao wapo bega kwa kuakikisha pangani inapata maendeleo.
 Msanii wa Muziki wa Singeni Dulla Makabila akiwasha moto juu ya jukwaa wakati wa kuhitimsiah uzinduzi wa Mashindano ya AWESO CUP Katika Wilaya ya Pangani.
 Kiungo wa Coast Union ya Tanga akipiga mpira kwenda lango la Pangani Kombaini wakati wa mchezo wa uzinduzi wa ligi ya AWESO CUP
 Wachezaji wa Coast Union ya Tanga wakimtoka beki wa Pangani Kombani katika Mchezo wa uzinduzi wa AWESO CUP Ambapo Coast Union iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
 Mchazaji wa Coast Union ya Tanga na Mchezaji wa Pangani Kombaini wakiwania mpira wakati wa mchezo wa uzinduzi wa ligi ya AWESO CUP iliyofanyika katika uwanja wa Kumba na Coast Union ilipata ushindi wa bao 1-0
 Wasanii walioshiriki Tamasha hilo wakiangalia mpira
  Wasanii walioshiriki Tamasha hilo wakiangalia mpira a
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Pangani akiwashukuru wakazi wa Pangani kwa kuweza kufika katika uzinduzi wa AWESO CUP

KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU ZITAKUWA ENDELEVU - RC MTAKA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa.wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani humo, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.
Aliyekuwa mlezi(Patron) wa kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita kwa wanafunzi wa kidato cha Sita mkoani Simiyu, Mwl.Pimbili Chalya kutoka Mwandoya, akitoa tathmini ya kambi hiyo , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Joseph Mathias Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Bariadi akitoa tathmini ya kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita mkoani Simiyu, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mwanafunzi wa kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, akitoa burudani ya wimbo, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato kutoka Mkoani Mwanza, Nicodemo Ntabindi akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mwalimu Dennis Wasagara ambaye pia ni mzazi akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Mwl. Kuyunga Jackson akitoa tathmini ya kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita mkoani Simiyu, wakati wa kufunga kambi hiyo , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Kambi za Kitaaluma mkoani Simiyu kwa wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha Sita, ambayo ni madarasa yanayofanya Mitihani ya Taifa ya kuhitimu elimu ya Msingi na Sekondari zitakuwa endelevu.

Mtaka amesema hayo Aprili 28, 2019 wakati akihitimisha Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ikihusisha wanafunzi 1166 kutoka katika shule 12 mkoani hapa.

Amesema Mkoa utaendelea kufanya jitihada na kuboresha zaidi kambi hizo huku akieleza kuwa ameshawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya motisha kwa walimu na wanafunzi watakaokuwa wakifanya vizuri.

“Kambi za kitaaluma  zitaendelea kuwepo katika kipindi chote nitakacho kuwepo na tutaendelea kuboresha; mwaka huu nimewaambia Wakurugenzi ni lazima kila Halmashauri itenge fedha kwa ajili ya motisha katika elimu, motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka amewashukuru walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali waliochangia kufanikisha kambi ya kidato cha sita, huku akiwasisitiza wanafunzi wa hao kuendeleza juhudi walizozionesha wakiwa kambini na kutumia mbinu walizopewa na walimu mahiri ili waweze kufanya vizuri mitihani yao ya mwisho.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato kutoka Jijini Mwanza, Nicodemo Ntabindi amewaonya wanafunzi wa Kidato cha sita kutojihusisha na masuala ya mapenzi badala yake wajikite katika masomo tu kwa sasa ili waweze kufikia ndoto zao.

Kwa upande wao wanafunzi waliokuwepo katika kambi hiyo ya Kitaaluma wamesema kambi hiyo imekuwa msaada kwa wanafunzi kwa kuwa imechangia kuwasaidia kupata ufumbuzi wa mada ngumu zilizokuwa zinawapa shida na kuahidi kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa kutokana na namna walivyoandaliwa vema.

“Tunashukuru uwepo wa kambi hii maana imetusaidia kupata maarifa ya namna ya kujibu maswali kwenye mitihani, lakini tumeweza kusaidiwa na walimu kutatua mada ngumu ambazo zilikuwa zinatushinda, ninaamini kwa namna tulivyoandaliwa hatutamuangusha Mkuu wetu wa Mkoa” alisema mwanafunzi Farida Omary.

“Kambi hizi hazijafanyika popote hapa nchini tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kuja na wazo la kuwa na kambi kwa sababu tumejifunza mengi, tumekutana na wenzetu wa shule mbalimbali hapa mkoani kwetu na tukapata maarifa ambayo awali hatukuwa nayo, tuna imani tufanya vizuri “ alisema mwanafunzi Casto Nyakarungu.

Katika kambi hii Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, imetoa shilingi milioni 12 kwa ajili ya motisha kwa walimu waliokuwa wakifundisha kambini hapo na imeahidi kutoa shilingi milioni nne kwa mwanafunzi atakayepata ‘division one, pointi tatu’ na kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa.

Mradi wa umeme wa Kinyerezi I Extension kukamilika mwezi Agosti mwaka huu

$
0
0
Na Teresia Mhagama

Imeelezwa kuwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi wa Kinyerezi I extension utakamilika mwezi Agosti mwaka huu ambapo utazalisha umeme wa kiasi cha megawati 185.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2019 na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya umeme ambapo aliambatana na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Juma Mkobya  na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Tito Mwinuka.

Alisema kuwa, Kituo cha Kinyerezi I tayari kinazalisha megawati 150 hivyo kuongezeka kwa megawati 185 kutafanya kituo hicho kuzalisha umeme kiasi cha megawati 335.

Aliongeza kuwa, mradi huo wa Kinyerezi I Extension unatekelezwa kwa fedha za ndani ambapo jumla ya Dola za Marekani milioni 188 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo na malipo yamekwishafanyika kwa asilimia 60.85.

Awali, Meneja Miradi kutoka TANESCO, Mhandisi Stephen Manda alieleza kuwa, mradi wa Kinyerezi I Extension unahusisha ununuzi, usanifu na utengenezaji wa mitambo na viambata vyake, ujenzi wa laini ya msongo wa kV132 kutoka Kinyerezi hadi Gongo la Mboto na upanuzi wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme.

Alisema kuwa, tayari mitambo minne ya kuzalisha umeme itakayofungwa kwenye eneo hilo imeshafika nchini na kwamba mitambo miwili inatarajiwa kuwashwa na kuungwa kwenye gridi ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu na mitambo inayobaki itawashwa mwezi Agosti mwaka huu.

Alitaja baadhi ya kazi zilizokamilika hadi sasa kuwa ni ujenzi wa misingi ya mitambo, ujenzi wa kituo cha kupoza umeme na ujenzi wa laini ya msongo wa kV 220 kutoka katika mitambo ya umeme ya Kinyerezi I hadi Kinyerezi II, hivyo kwa ujumla mradi umetekelezwa kwa asilimia 82.

Awali, Waziri wa Nishati, alikagua kazi ya ufungaji wa transfoma kubwa yenye uwezo wa megawati 240 katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam na kutoa maagizo kwa watendaji wa TANESCO kuwa kazi hiyo ikamilike tarehe Moja mwezi wa Saba mwaka huu ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Vilevile, Dkt. Kalemani alikagua kituo cha kupoza umeme cha Kurasini na kukuta kimeshakamilika hivyo kimeanza kazi ya kusambaza umeme katika eneo la Kigamboni hali itakayopelekea eneo hilo kupata umeme wa uhakika.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akitoka kukagua kazi ya ufungaji wa mitambo itakayozalisha kiasi cha umeme cha megawati 185 kupitia mradi wa Kinyerezi I Extension jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi kutoka TANESCO, Mhandisi Stephen Manda (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) kuhusu utekelezaji mradi wa Kinyerezi I Extension utakaozalisha megawati 185. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Juma Mkobya akizungumza na Mhandisi Edson Ngabo kutoka Wizara ya Nishati, wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati katika mradi wa umeme wa Kinyerezi I Extension jijini Dar es Salaam.

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI-MBEYA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde (wa kwanza kulia) na wa kwanza kushoto ni katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe wakitembea katika viwanja vya Bustani ya Jiji wakati wa kukagua mabanda ya maonesho katika kuadhimisha Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Aprili 28, 2019 yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokelewa na watumishi wa OSHA alipowasili katika viwanja vya bustani ya Jiji Mkoani Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika mkoani hapo kitaifa.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Bi. Khadija Mwenda akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa maaadhimisho hayo, wa kwanza kushoto ni Naibu wake Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipewa maelezo ya vifaa saidizi kazini kutoka kwa Mtaalamu kutoka Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiuliza jambo kwa wataalam kutoka Idara ya Kazi wa ofisi hiyo alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la maonesho la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista pamoja na naibu wake Mhe. Anthony Mavunde wakiangalia mfano wa namna ya kuokoa mtu aliyepata madhara awapo kazini walipotembelea banda la MUST (Mbeya University of Science and Technology) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista pamoja na baadhi ya viongozi wa TUGHE wakifurahia jambo wakati alipotembelea banda la TUGHE katika maonesho hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akifuatilia takwimu za ajari zitokananazo na shughuli za uchimbaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu alipotembelea banda la ofisi hiyo kujionea namna wanavyofanya kazi wakati wa maadhimisho ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Mkoani Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akihutubia wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya kilele maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya Aprili 28, 2019.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akifurahia pamoja na watumishi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kupokea tuzo nyingi kuliko washiriki wengine wa maonesho ya Siku Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

SHEGELLA AWATAKA MA DC NA WABUNGE KUJIFUNZA KWA AWESO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Pangani

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amewaagiza Wakuu wa Wilaya na wabunge wote wa Majimbo katika mkoa wa Tanga kuhakikisha wanasimamia michezo katika maeneo yao ya kazi kama ilivyoelekeza ilani ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015.

Shigella amesema hayo alipokuwa akifungua Mashindano ya Aweso Cup yaliyofanyika katika Wilaya ya Pangani katika Viwanja vya Kumba na kudhaminiwa na Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso.

"nimeridhika na jinsi gani Mbunge wa jimbo hilo anavyomsaidia Rais Dk John Pombe Magufuli katika kutekelezaa Ilani kwani kwa kudhamini Tamasha kubwa kama hili na kufanikiwa kwa kiasi hichi sio jambo la bahati mbaya bali anazingatia maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo katika uchaguzi wa mwaka 2015 CCM iliahidi kusimamia michezo katika kila wilaya hivyo nawaagiza Wakuu wa Wilaya wote mliopo hapa mjifunze kutoka kwa Aweso na Mkafanye hivi kila mmoja katika wilaya zenu"Amesema Rc Shegella.

alisisitiza kuwa maelekezo hayo anyatka yaanze kutekelezwa mapama tu mara baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani hivyo kila mmmoja kajipange kwa namana yake.

kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdalah amesema kiuwa uwepo wa ligi hiyo umesaidia kupaza kuchochea Maendeleo katika Wilaya ya pangani na kuinua vipaji kwani ligi hiyo ya Aweso Cup inafanyika kwa kipindi cha Miaka miatatu mfulululizo sasa chini ya udhamini wa mbunge huyo wa pangani.

Nae Mbunge wa Pangani na Naibu waziri wa Maji, Juma Awesu amemshukuru mkuu wa mkoa  Martin Shigella kwa kufika katika na kuzinfdua ligi hiyo ambayo imekuwa kivutio na kuwaunganisha wana pangani wote ambao wanpenda michezo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shegella akizungumza na Wakazi wa Wilaya ya Pangani waliofika kushuhudia uzinduzi wa Awesu CUP Uliofanyika katika Viwanja vya Kumba.
 Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani, Juma Awesu, akipiga magoti kuwashukuru wakazi wa Wilaya ya Panagani kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa ligi ya Awesu Cup inayofanyika katika wilya hiyo chini ya udhamini wake yeye kama Mbunge wa Jimbo.
 Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdalah akitoa Historia fupi ya Mashindano ya Awesu Cup katika wilaya hiyo na mafanikio yake katika kipindi cha miaka mitatu mfululuzo.
 Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa(CCM), Khadija Shabani(Keisha), akitoa salamu za CCM na namna gani Rais John Pombe magufuli alivyoweza kutekeleza ilani katika mkoa wa Tanga na wilaya zake
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shegella, akikabidhi cheti cha Shukrani kwa Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara kwa mchango wake kwa kipindi cha miaka mitatu


 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akizungumza katika Tamasha hilo juu ya kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na Kufanya jambo hilo katika mkoa wake.
Sehemu ya Wananchi wa mkoa wa Tanga wakifatilia hotuba mbalimbali za viongozi wakati wa uzinduzi wa Tamasha hilo.

Wasanii wa Vichekesho Kupa na Mtanga ambao ni Wazawa wa Pangani wakisherehesha wakati wa uzinduzi huo
 Uwanja wa Kumba unavyooneka kwa juu kwa jinsi ulivyofurika

Dkt Kalemani azindua uunganishaji wa Gesi ya asilia Kiwanda cha Cocacola

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria kukiunganishia Gesi asilia kiwanda cha Cocacola cha jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Profesa Sufian Bukurura.

Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amezindua upelekaji wa Gesi asilia katika kiwanda cha Cocacola kilichopo jijini Dar es Salaam ambacho sasa kitaanza kutumia gesi hiyo kwa shughuli zake za uzalishaji.

Uunganishaji wa Gesi asilia katika kiwanda hicho ni matokeo ya kazi iliyofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika mwaka wa fedha 2018/2019 ya kuunganisha bomba la kusafirisha gesi asilia  linalotoka Mtwara na Songo songo hadi Dar es Salaam kwenye bomba la usambazaji gesi asilia linalotoka Ubungo hadi Mikocheni  jijini Dar es Salaam.

Dkt Kalemani alifanya uzinduzi huo tarehe 28 Aprili, 2019 ambapo pia amekagua shughuli za usambazaji gesi majumbani katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mikocheni na Savey.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo alisema "yapo mabomba manne yanayotumika kwa shughuli hizi za usambazaji gesi hivyo ni matumaini ya Serikali kuwa viwanda vingi zaidi vitatumia gesi hii kwa shughuli za uzalishaji ili kuleta tija kwenye  gesi, kupunguza gharama za uendeshaji wa viwanda  na pia kwa ajili ya utunzaji wa mazingira."

Kuhusu kupitisha miundombinu ya usambazaji gesi katika maeneo ambayo hayajapimwa, Dkt Kalemani aliitaka TPDC na kampuni yake tanzu ya Usambazaji Gesi (GASCO) kuhamasisha viongozi wa mitaa na wananchi ili kuitikia wito wa kupitisha miundombinu hiyo kwenye maeneo yao hivyo kuunganishia gesi wananchi wengi zaidi.

Aidha, aliagiza kuwa, zaidi ya robo ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wasambaziwe Gesi Asilia katika miaka mitatu ijayo na kueleza kuwa kuna umuhimu kwa vyombo vya usafiri kama magari, majumbani na viwanda kutumia gesi hiyo ambapo kwa sasa magari zaidi ya 200 yameunganishwa na gesi hiyo nchini.

Pia alisisitiza matumizi ya vifaa vinavyozalishwa nchini katika kazi za usambazaji wa gesi kama vile mabomba na viunganishi ili kutochelewesha kazi hizo, kuepusha usumbufu na kupunguza gharama katika usambazaji gesi asilia.

Kuhusu bajeti ya usambazaji gesi asilia,  alisema kuwa Serikali inalipa kipaumbele suala hilo na imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kazi hizo ambapo kwa sasa imetenga zaidi ya shilingi bilioni 50 kwa ajili ya mradi huo.

katika ziara hiyo, Waziri wa Nishati aliambatana Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu , Mhandisi Innocent Luoga na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa pili kushoto) akiangalia miundombinu ya usambazaji gesi majumbani katika eneo la Mlalakua jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba na wa Tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Profesa Sufian Bukurura.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba ( wa pili kutoka kulia) akimuonesha Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa kwanza kulia) miundombinu ya usambazaji gesi majumbani katika eneo la Mlalakua jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kutoka kushoto) akikagua miundombinu ya usambazaji gesi majumbani katika eneo la Mlalakua jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Profesa Sufian Bukurura na kushoto kwa Waziri ni Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya usambazaji gesi majumbani katika eneo la Mlalakua jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba na Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Profesa Sufian Bukurura. Kushoto kwa Waziri ni Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya.

Matukio Mbalimbali ya Fainali za AFCON U17

$
0
0
Wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 wakishangilia mara baada ya kuibuka mabungwa wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya kuifunga Guinea kwa mikwaju ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Mpoto Theatre kikitoa burudani kwa watazamaji wa fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyokutanisha Cameroon na Guinea hapo jana na Cameroon kutwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi ya penati 3 za Guinea.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Susan Mlawi wakati Naibu Waziri alipowasili  kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad wakati Naibu Waziri alipowasili  kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, kati ya Guinea na Cameroon jana jijini Dar es Salaam.
Vikosi vya timu za vijana chini ya miaka 17 toka Guinea na Cameroon wakiimba nyimbo za mataifa yao kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali hapo jana ambapo Cameroon waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi penati 3 za Guinea.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad (katikati) akimkabidhi bendera ya CAF Balozi wa Morocco Nchini Tanzania Abdelilah Benryane ikiwa ishara ya kuwa muandaaji wa mashindano hayo, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Wallace Karia.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimkabidhi zawadi ya kombe mchezaji ambayealiibuka kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 jana jijini Dar es Salaam.
Washindi wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, timu ya Cameroon wakivalishwa medali mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad akimkabidhi nahodha wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 mara baada ya kuibuka mabingwa kwa ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.

Picha na WHUSM – Dar es Salaam

Vodacom yafungua fursa za kiuchumi mkoani Katavi.

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc imeendelea kuwasogezea huduma wateja wake kwa kuzindua duka kubwa la kisasa katika wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi. Duka hili litawezesha kufungua fursa mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo yanayoizunguka. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka hilo, Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mh Mizengo Pinda, aliipongeza kampuni ya Vodacom huku akisisitiza kwamba duka hilo litarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja na kuchochea shughuli za kiuchumi za wilaya na mkoa huo. 

“Karibuni nyumbani Vodacom, hongereni sana kwa kutufungulia duka kubwa zaidi hapa Mpanda kwani wilaya hii ina wananchi wachapakazi, wenye muamko wa kukuza uchumi na wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Ni furaha kuona sasa watapata huduma za simu kwa ukaribu, lakini pia, wajasiriamali watapata fursa zaidi” alisema Mh Pinda huku akihamasisha wakazi wa wilaya hiyo kuona duka hilo kama kichocheo cha kukuza uchumi wilayani humo. 

Duka hilo jipya Iina vifaa vya kisasa, wafanyakazi waliopata mafunzo sawia na walio tayari kutoa huduma bora kwa wakazi wa wilaya ya Mpanda kwa kuzingatia ongezeko la idadi ya watu katika mkoa wa Katavi. 

Naye Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Nyanda za Juu kusini, MacFydine Minja alisema, uzinduzi wa duka hilo unaenda sambamba na mkakati wa kampuni hiyo wa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta fursa kwa watanzania. Pia Vodacom imelenga kupanua wigo wa huduma za simu Tanzania na kuzifikisha karibu na wananchi. 

“Tumejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wetu katika mkoa huu, ambapo tayari tuna huduma ya 4G ambayo inatoa nafasi ya kupata intaneti yenye kasi zaidi, pia tuna madawati matano ya huduma kwa wateja. Kipaumbele chetu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma kiurahisi na kwa ufanisi zaidi, hivyo uwepo wa Vodacom wilayani hapa ni fursa kwani duka na madawati ya huduma kwa Mteja tayari yameajiri wafanyakazi 15 na kutoa fursa lukuki za huduma mbalimbali katika duka hili kwa wajasiriamali mkoani hapa” aliongeza Minja. 

Aliongeza kwamba kwa sasa wateja wa Vodacom wanaweza kupata huduma tofauti kwenye duka hilo kama vile usajili wa laini za simu, ushauri wa huduma za Vodacom kama M-Koba, kurudisha laini zilizopotea au kuharibika, kununua simujanja kwa bei nafuu kabisa na mengine mengi kutoka Vodacom. 

Huduma za simu hasa miamala ya fedha imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini na kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ujumla. “Nimekuwa nikipanga kuwa wakala wa M-Pesa kwa muda mrefu sana na sasa naishukuru Vodacom kwa kutufungulia duka hili, kwani leo naanza hatua ya kwanza ya kutimiza ndoto yangu” alisema Helena Lao, mkazi wa wilaya hiyo huku akionesha vitambulisho husika vitakavyomuwezesha kuwa wakala wa kwanza kusajiliwa katika duka hilo. 

Kwa sasa Vodacom Tanzania Plc ina jumla ya maduka 100, madawati ya huduma kwa mteja (Service Desks) 350 yanayotoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo maeneo mbalimbali nchini. 

UCSAF YAZINDUA CLUB ZA ICT SHULE ZA SEKONDARI DODOMA, MSALATO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye (kulia) akifurahia jambo baada ya kutazama kazi iliyofanywa na mwanafunzi wa Dodoma Sekondari wakati akizindua Club ya ICT na Maabara ya Kompyuta sjuleni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). UCSAF wamekabidhi kompyuta 10 katika maabara hiyo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (katikati) akikata utepe kuzindua maabara ya Compyuta na ICT Club katika Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yanayofanyika Mkoani Dodoma kitaifa. Wengine pichani toka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule, Naibu Katibu Mkuu, Mawasiliano, Dk Jim Yonazi , Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Peter Ulanga, Mwenyekiti wa Bodi ya CSAF, Joseph Kilongola, Mwalimu Mkuu Dodoma Sekondari, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Maria Sasabo pamoja na watumishi wa UCSAF na walimu .UCSAF imetoa wamekabidhi Computa 10 kwa shule hiyo. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kulia) akiangalia mwanafunzi wa shule ya Sekondari Msalato wakitumia maabara ya Computa baada ya kuzindia maabara hiyo jijini Dodoma jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya UCSAF ambao ndio wamekabidhi Computa 10 kwa shule hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Mawasilino na Uchukuzi, Dk. Jim Yonazi akiangaklia kazi iliyofanywa na mwanafunzi wa Sekondari ya Msalato. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Peter Ulanga wakiangalia wanafunzi wa shule ya Sekondari Msalato wakitumia maabara ya Computa baada ya kuzindia maabara hiyo jijini Dodoma jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya UCSAF ambao ndio wamekabidhi Computa 10 kwa shule hiyo
Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye akizungumza na na wanafunzi wa Sekondari ya Msalato. 
Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye akiangalia kazi za wanafunzi katika maabara hiyo. 
Wanafunzi wakiwa maabara ya Compyuta 
Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Peter Ulanga akizungumza
Naibu Waziri wa Mawasilono na Uchukuzi, Atashasta Nditiye akizungumza na kusisitiza umuhimi wa matumizi sahihi ya TEHAMA katika kufikia uchumi wa kati. 
Wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma masomo ya Sayansi Dodoma Sekondari wakifuatilia hotuba za viongozi 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kushoto) akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Peter Ulanga (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya CSAF, Joseph Kilongola, wakati wa hafla hiyo Dodoma Sekondari.
Picha ya pamoja
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live




Latest Images