Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

CCM MANISPAA YA IRINGA NA NAIBU MEYA WAMVAA TENA MBUNGE PETER MSINGWA SWALA BARABARA

0
0
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata kupitia chama cha mapinduzi akikagua utekelezaji wa ahadi waliyoitoa kwa wananchi wa kata ya Mkimbizi mtaa wa Ugele manispaa ya Iringa
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na mwenyekiti wa vijana kata ya Mkimbizi wakikagua utekelezaji wa ahadi yao
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula wakifurahi jambo na wananchi wa mtaa wa Ugele mara baada ya kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara
Naibu meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir pamoja na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula wakifurahi jambo na wananchi wa mtaa wa Ugele mara baada ya kutekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

NAIBU meya wa manispaa ya Iringa amewataka wananchi wa manispaa ya Iringa kumkataa mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wa kuleta maendeleo kwa wananchi waliompa kura.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Mkimbizi mtaa wa Ugele,Naibu meya Joseph Lyata alisema kuwa mfuko wa mbunge unapesa nyingi za kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi lakini hali imekuwa tofauti kwa mbunge huyo kushindwa kutatua changamoto za wananchi.

“Mbunge anauwezo wa kuwatembelea wananchi wa Ugele na kuja kutatua changamoto mlizonazo kwa kuwa anapesa za mfuko wa mbunge ambao anauwezo wa kutoa pesa kwa ajili ya kukarabati barabara hii ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika kuleta maendeleo ya eneo hili” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa wananchi wa mtaa wa Ugele wanakabiliwa na tatizo la kukosa huduma bora za afya kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo hayupo tayari kuwasaidia kutatua changamoto hizo.

“Mlifanya kosa kubwa sana kumchagua mbunge huyo kwa kuwa hajawai kuja kuwasikiliza kero zeo na kuzitatua ndio maana maumivu hayo mnayapa hii leo kwa kuwa hakuna maendeleo ambayo mmefanyiwa na mbunge huyo” alisema Lyata

Lyata amewataka wananchi wa mtaa wa Ugele kutomchagua tena mbunge huyo kuwa kuwa hana faida ya kimaendeleo kwa wananchi kwa kuwa ameshindwa kuleta maendeleo kwa kushindwa kuboresha sekta ya afya,elimu na miundombinu.

“Mmemchagua kiongozi ambaye hawasikilizi na anashindwa kutatua kero za wananchi ndio maana hadi hii leo mnateseka kwa kushindwa kutatuliwa kero zenu huyo sio kiongozi na hafai tena kuwa kiongozi” alisema Lyata

Aidha Lyata alisema kuwa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimeamua kutatua kero zenu kwa kuwa hamna kiongozi ambaye anaweza kuwatatulia kero kwa kuwa mbunge mliyemchagua ameshindwa kutatua kero hizo.Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Manispaa ya Iringa Edwin Bashir aliwataka wananchi wa mtaa huo kuendelea kuwa na imani na chama cha mapinduzi kwa kuwa kinafanya kazi ya kuleta maendeleo kwa vitendo.

“Tulikuja hapa kukiwa hakuna barabara lakini tulifanya mkutano wa hadhara na kuwasikiliza kero zetu hatimaye mkatupa kero ya barabara na zahanati hivyo sasa tumeanza kutengeza barabara kwa kiwango bora kinachosaidia kuleta maendeleo kwa wananchi” alisema Bashir

Bashir alisema kwa sasa hakuna chama kinachoweza kutekeleza ahadi zake kwa umakini kama chama cha mapinduzi hivyo wananchi mnatakiwa kuendelea kuwa na imani na chama hicho.“Jamani mnatakiwa kuendelea kukienzi na kukitunza chama hiki bora ambacho ndio chama bora kwa kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake na sio vyama vingine” alisema Bashir

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa chama cha mapinduzi na naibu meya wa manispaa ya Iringa walikuwa hawalali kwa ajili ya kutatua tatizo la barabara ya Ugele kwa kuwa wananchi hao wanahitaji kufanya kazi za kimaendeleo

“Wananchi wa kata ya Ugele wanahitaji kufanya maendeleo kwa kuwa wamekuwa wachapa kazi wakubwa lakini mbunge wao amekuwa hawasaidie kwa lolote hivyo ndio chama na Naibu Meya walipobebe jukumu la kutatua changamoto hiyo” alisema Chegula

Chegula alisema kuwa kipaumbele kilikuwa kutatua changamoto ya barabara ndipo wanatafuta njia nyingine ya kutatua changamoto nyingine zilizopo katika mtaa wa Ugele ili wananchi wafanye kazi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyotaka.

Nao wananchi wa Mtaa wa Ugele Manyigi Uliopo Kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa wameishukuru serikali Chini ya Naibu Meya Manispaa ya Iringa kwa kuwakarabatia barabara ambayo ilikuwa awali ilikuwa kero kwao.

“Baadhi ya wananchi wa Mtaa huo wamesema kuwa awali kabla ya ukarabati wa barabara hiyo, wajawazito walikuwa wanapata shida pindi wanapoelekea mjini kupata huduma za afya” walisema wananchi

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ugele Manyigi Aloyce Laurent amemshukuru Naibu Meya Joseph Lyata kwa kupeleka Greda katika Mataa wake na kurekebisha barabara ambayo ilikuwa kero kwa wananchi wake.

MAKAMPUNI,MASHIRIKA YAUNGANA NA LA PRINCE PUB KUTOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

0
0
Wadau wa Maendeleo mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Kampuni ya La Prince Pub inayojihusisha na biashara ya uuzaji vinywaji na chakula Mjini Shinyanga wamesherehekea Sikukuu ya Miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kutembelea na kuwapatia misaada mbalimbali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa akina mama na watoto ni pamoja na sabuni,mafuta ya kujipaka juisi,poda, miswaki,dawa za meno,matunda, toilet papers,biskuti,maji na zawadi zingine.

Wadau walioungana na wafanyakazi wa La Prince Pub kutembelea na kutoa misaada kwa wagonjwa leo Aprili 26,2019 ni pamoja na Kampuni ya Lulekia,Jambo Food Products Co. Ltd,Astro Secure Co. Ltd,Uptown Holdings Co.Ltd,Msirikale Microfinance,24 Security Tanzania,Ommy Fashion, Gvenwear,Shirika la TVMC,Dellah Car Traders,Luxury Pub,Friends of Bhoke na Malunde 1 blog.


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo,Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William alisema wameamua kuungana na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka.

Alisema zawadi hizo kwa wagonjwa zimetolewa kupitia Mpango maalumu ulioanzishwa na La Prince Pub unaojulikana kwa jina la ‘La Prince Charity Movement’ kwa lengo la kuisaidia jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali,makampuni na wafanyabiashara mbalimbali. 

“Tumefika hapa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa pole kwa wagonjwa na kuwapa misaada mbalimbali,tumejumuika sisi wafanyakazi wa La Prince na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo kutoka kwenye mashirika na makampuni ambao tumeungana kuja kurudi kurudisha fadhila kwa jamii kwa kutoa misaada kwa wagonjwa katika wodi za akina mama na watoto",alisema.

“Tukiwa sehemu ya jamii tumeona ni busara zaidi katika siku hii ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo hatufanyi sherehe za kitaifa,sisi tumeona tufanye sherehe ndogo ya kuwapa pole wanaoumwa na wenye mahitaji maalumu”,aliongeza William.

“Kilichotusukuma sisi ni moyo wa upendo,sisi tuna mpango maalumu unaitwa La Prince Movement ambapo kila mwezi tumeamua kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga kutoa misaada mbalimbali katika kada mbalimbali, leo tumeanza na hospitali na hivi karibuni tutambelea magereza”,alieleza Mkurugenzi wa La Prince Pub.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakati wadau mbalimbali wa maendeleo walipotembelea wagonjwa na kuwapatia zawadi akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali hiyo leo Aprili 26,2019 ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mmoja wa wafanyakazi wa La Prince Pub akiweka sawa zawadi mbalimbali zilizotolewa na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya wafanyakazi wa La Prince Pub wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali.
Wadau wa maendeleo wakiwa na zawadi zao wakijiandaa kuingia katika wodi mbalimbali katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kugawa zawadi hizo kwa wagonjwa.
Wadau wa maendeleo wakielekea katika wodi za watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika moja ya wodi akielezea lengo la wadau kufika katika hospitali hiyo.
Wadau wa maendeleo wakiwa wodini na zawadi zao kabla ya kuanza kuzigawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimiana na mmoja wa Madaktari katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga aliyekutwa wodini.
Wadau wakitoa zawadi kwa mama aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika moja ya wodi za akina mama.
Wafanyakazi wa Ommy Fashion wakitoa zawadi kwa mgonjwa.
Wafanyakazi wa La Prince Pub wakitoa zawadi katika wodi ya watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimia akina mama katika wodi ya watoto.
Utoaji zawadi ukiendelea katika wodi ya akina mama waliojifungua. katikati ni Bhoke Wambura, muanzilishi wa Friends of Bhoke.
Wadau wakiongozwa na Mkurugenzi wa shirika la TVMC,Musa Jonas Ngangala (katikati) wakikabidhi zawadi ya ndoo ya sabuni na zawadi zingine kwa mama aliyejifungua watoto mapacha wa kiume.
Wafanyakazi wa La Prince wakimsalimia na kumpa pole pamoja na zawadi mama wa mmoja mfanyakazi mwenzao aliyelazwa katika wodi ya wanawake.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

SERIKALI YAAJIRI WALIMU WAPYA 4,549 ,YAWAPANGIA SHULE ZA KUFUNDISHA

0
0
*Waziri Jafo asema mwisho wa kuripoti ni Mei 27,watakaochukua posho na kuondoka kukiona.

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema jumla ya walimu 4,549 wamepangiwa moja kwa moja kufundisha katika shule za msingi na Sekondari.

Kwa mujibu wa Jafo ni kwamba TAMISEMI ilipata kibali cha kuajiri jumla ya walimu 4, 549 na kibali hicho kilikuwa kwa ajili ya walimu was shule hizo na hasa katika maeneo yaliyokuwa na upungufu.

Akizungumza leo Aprili 27,2019 jijini Dar es Salaam Jafo amesema jumla ya waombaji 91,108 walojitokeza kutuma maombi ya nafasi mbalimbali zilizotangazwa na kati ya hao maombi 43,770 sawa na asilimia 48.04 ya waombaji wote walikuwa na viambatisho  vyote vilivyohitajika.

Ameongeza na jumla ya waombaji 47,338 sawa na asilimia 51.96 maombi yao hayakuwa na vigezo ikiwa ni pamoja na kukosa viambatisho muhimu vilivyohitajika.

"Kutokana na mahitaji makubwa ya walimu katika shule za msingi na walimu wa shule za msingi wa masomo ya sayansi(Fizikia,Kemia na Bailojia) na hisabati .Ofisi ya TAMISEMI imefanya uchambuzi na kutoa kipaumbele katika ajira ya walimu wa kada za walimu daraja la tatu A(cheti)kwa ajili ya kufundisha shule za msingi.

" Walimu daraja la tatu B (Stashahada) wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kufundisha shule za sekondari kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.Walimu daraja la tatu C wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kufundisha katika shule za sekondari za kidato cha tano na sita.

"Na walimu daraja la tatu C (Shahada) wa masomo ya elimu maalum ,biashara ,uchumi,kilimo na maarifa ya nyumbani kwa ajili ya kufundisha shule za sekondari. Mchakato wa kupitia maombi ulijumuisha uhakiki wa uhalali wa vyeti vy elimu na taaluma vya waombaji na ukamilifu wa nyaraka zilizohitajika," amesema Jafo.

Amefafanua anatumia nafasi hiyo kuwataarifu waombaji wote wa masomo ya Sana'a ,sayansi na masomo mengine ambao walitimiza vigezo na hawakufanikiwa kupata nafasi katika kipindi hiki kuwa maombi yao yote yamechambuliwa na yamehifadhiwa kwenye kanzidata yao na kuwa fursa za ajira zitakapojitokeza utaratibu wa ajira utatolewa.

Kuhusu walimu waliopata ajira ambao ni hao 4,549 wamepangiwa moja kwa moja na kati ya hao jumla ya walimu 3,059 sawa na asilimia 67.25 wamepangiwa kufundisha shule za msingi na walimu 1,490 sawa na asilimia 32.75 wamepangwa kufundisha shule za sekondari.

"Walimu wote waliopata ajira wanatakiwa kuripoti kwa wakurugenzi wa halmashauri zilipo shule walizopangwa kwa ajili ya uhakiki wa vyeti halisi vya elimu na taaluma,kujaza mikata ya ajira na taratibu nyingine za kiutumishi na kisha kuripoti katika shule walizopangiwa.

" Walimu wote waliopata ajira wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya Nazi kuanzia Mei 7,2019 hadi Mei 21,2019 .Walimu wapya ambao hawataripoti katika vituo vyao vya kazi ifikapo Mei 21,2019 nafasi zao zitajazwa mara moja bila kuwataarifu kwa kuwapanga walimu wenye sifa ambao hawakupangwa katika awamu hii.

"Aidha Wakurugenzi wa halmashauri wasibadilishe vituo vya kazi  vya walimu hao bila kibali maalum cha Katibu Mkuu TAMISEMI .Mwajiriwa atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kisha akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa atachukuliwa hatua kali za kisheria," amesema Jafo.

Pia amewomba wakurugenzi wote wa halmashauri zilizopangiwa walimu wa ajira mpya kuwapokea walimu hao na kukamilisha taratibu za ajira kwa kuzingatia sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo inayosimamia utumishi wa umma.

TCRA: Changamoto Vitambulisho vya Taifa itatatuliwa na Mamlaka husika sambamba na zoezi la Usajili

0
0
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV, Morogoro
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  Kanda ya mashariki imesema kuwa changamoto ya wananchi kukosa vitambulisho vya Taifa kwa ajili ya kusajili namba za simu kwa kutumia namba za vidole itatatuliwa na Mamlaka inayotoa vitambulisho hivyo (NIDA).

Changamoto ya vitambulisho hivyo imeibuka wakati Kanda ya Mashariki ilipokuwa inatoa elimu maeneo mbalimbali ya mkoani Morogoro kwa wananchi kuhoji vitambulisho vya taifa namna ambapo watavipata kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa muda uliowekwa kwa ajili ya usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole unafanya kila mwananchi atapata kitambulisho cha Taifa na kuweza kusajili laini kwa kutumia alama za vidole.

Aidha amesema kuwa baadhi ya watu walikuwa wanatumia simu ambazo zimesajiliwa na kwa majina ya watu wengine ambapo ni kosa kisheria. Amesema kuwa usajili wa laini kwa alama za vidole inaondoa mtu kumiliki laini kwa jina la mtu mwingine. Amesema kuwa katika kipindi hiki cha usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole kwa wenye vitambulisho wajisajili na wasiokuwa navyo wafuate utaratibu kwa kuvipata katika mamlaka husika kuweza kuvipata kwani mwisho wa kusajili ni Desemba 31 mwaka huu ambapo wasiosajili simu zao zitafungiwa.
 Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki  Robson Shaban akimpa maelezo mwananchi wa kijiji cha Mkuyuni.
 Mhandisi  Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Christopher John akitoa maelezo namna kutumia mawasiliano na umuhimu wa kusajili laini kwa kutumia alama za vidole wakati kanda hiyo ilivyokwenda kutoa elimu katika kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro.
 Wananchi wakipata elimu ya mawasiliano pamoja na usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole katika mnada wa kijiji cha Mkuyuni mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi wa Mkuyuni Mkoani Morogoro katika mnada wa kijiji hicho walipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano na Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole
 Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Violet Eseko akitoa maelezo ya kisheria ya kumiliki simu zisizokuwa na majina yao wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi Mkuyuni mkoani Morogoro.
Mwananchi wa kijiji cha Mkuyuni akiuliza swali kwa TCRA Kanda ya Mashariki ilipokwenda kutoa elimu katika kijiji hicho.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na Abood Tv mara baada ya kumaliza kipindi cha utoaji elimu katika Radio Abood mkoani Morogoro

VETA kushirikiana na DIT kuboresha utoaji mafunzo katika sekta ya ngozi

0
0
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesaini makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa lengo kuu la kuboresha utoaji mafunzo katika sekta ya ngozi ili kuchangia kukuza sekta hiyo nchini na kusaidia  juhudi za kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Akizungumza wakati wa tukio la utiaji saini makubaliano hayo Aprili 25, 2019  katika Taasisi ya DIT Dar es Salaam, Mkuu wa DIT Profesa Preksedia Ndomba amesema makubaliano hayo yanalenga kupanua wigo wa utoaji mafunzo na kuimarisha mafunzo ya ufundi na kuzalisha nguvu kazi mahiri ya kuhudumia sekta ya ngozi kupitia mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Alisema DIT inalenga kutumia baadhi ya programu zinazotolewa katika vyuo vya VETA ili kupata vijana walioiva katika fani mbalimbali watakaojiunga kwenye programu zinazotolewa na Taasisi hiyo katika ngazi ya ufundi Sanifu.

Profesa Ndomba alisema kupitia makubaliano hayo taasisi hizo zitaanza utekelezaji wa utoaji na uboreshaji wa mafunzo hayo katika vyuo vya DIT- Kampasi ya Mwanza, Chuo cha VETA Dakawa na Chuo cha VETA Dodoma ikiwa ni pamoja na kuboresha karakana na kuweka vifaa vya kisasa vya utoaji mafunzo hayo.

Alisema kwa sasa DIT–Kampasi ya Mwanza inafanya usajili wa kutoa mafunzo ya ngazi ya tatu ya ufundi ili kuwezesha vijana wanaohitimu katika chuo cha VETA Dakawa kwa ngazi ya pili ya ufundi stadi kujiunga na chuo cha DIT Mwanza na kuendelea hadi ngazi ya Ufundi Sanifu.

“Tunaamini kupitia ushirikiano huu tutaweza kuongeza udahili katika chuo chetu cha Mwanza na kuzalisha wataalamu zaidi watakaoweza kuitumikia sekta ya ngozi na walimu wa kufundisha fani hii katika vyuo vya VETA.” Alisema

Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu amesema ushirikiano huo utaisaidia VETA kuongeza uzalishaji wa mafundi stadi kwa ajili ya viwanda vya ngozi na bidhaa zitokanazo za ngozi.

Alisema kwa sasa VETA kupitia chuo chake cha VETA Dakawa inatoa mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi katika ngazi ya kwanza na ya pili ya ufundi na kwamba kupitia ushirikiano huo wahitimu wa chuo hicho wataweza kupata nafasi za kujiendeleza na mafunzo kwa ngazi ya tatu kupitia DIT-Kampasi ya Mwanza.

Dkt Bujulu aliongeza kuwa kupitia DIT, VETA itapata waalimu wa kufundisha fani hiyo mpaka ngazi ya tatu katika chuo cha Dakawa na kuweza kupanua wigo wa utoaji mafunzo katika vyuo vingine vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini, hasa maeneo ya wafugaji ili kusaidia wafugaji  kuongeza thamani ya mifugo yao.

“kwa sasa tuna changamoto ya wataalam pamoja na vifaa vya kufundisha fani hii katika vyuo vyetu na ndiyo maana hatujaweza kutoa mafunzo hayo hadi ngazi ya tatu ya ufundi….kupitia ushirikiano huu tunaamini changamoto hii itapata ufumbuzi.” Alisema

Alisema pia VETA itaanzisha mafunzo ya usindikaji na uchakataji ngozi katika chuo cha VETA Dodoma ambacho kwa sasa kinaendesha fani ya Usindikaji Nyama ili kujihakikishia upatikanaji wa malighafi bora ya ngozi itakayotumika katika uzalishaji wa bidhaa za ngozi.
 Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Profesa Preksedia Ndomba (kushoto) wakitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha utoaji mafunzo katika sekta ya ngozi tukio lililofanyika Dar Salaam. Waliosimama ni Wanasheria wa VETA na DIT walioshuhudia zoezi hilo.
 Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu (kulia) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Profesa Preksedia Ndomba (kushoto) wakitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha utoaji mafunzo katika sekta ya ngozi tukio lililofanyika Dar Salaam. Waliosimama ni Wanasheria wa VETA na DIT walioshuhudia zoezi hilo
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu (aliyeketi kulia) na Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Profesa Preksedia Ndomba (aliyeketi kushoto) na baadhi ya wataalamu  wa VETA na DIT baada ya zoezi la utiaji saini makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha utoaji mafunzo katika sekta ya ngozi tukio lililofanyika Dar Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA MBEYA-LWANJILO-CHUNYA KM 72 NA KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA CHUNYA-MAKONGOLOSI KM 39 CHUNYA MKOANI MBEYA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, pamoja na viongozi mbalimbali Wabunge, Mawaziri, Viongozi wa Mkoa wa Mbeya, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Chunya hadi Makongolosi km 39 itakayojengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Chunya mkoani Mbeya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chhalamila mara baada ya kufungua barabara ya kutoka Mbeya-Lwanjilo-Chunya yenye jumla ya kilometa 72.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara itakayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Chunya hadi Makongolosi km 39.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, pamoja na viongozi mbalimbali Wabunge, Mawaziri, Viongozi wa Mkoa wa Mbeya, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya  Mbeya-Lwanjilo-Chunya yenye jumla ya kilometa 72 iliyokamika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Chunya mkoani Mbeya.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Sabasaba Wilayani Chunya kwa ajili ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa Hadhara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwasalimia wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Sabasaba Chunya kabla ya kuwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mhandisi Profesa Ninatubu Lema kutoka Wizara ya Ujenzi wakati alipowasili katika uwanja wa Sabasaba Chunya mkoani Mbeya. PICHA NA IKULU

MWILI WA MAREHEMU MZEE LUTUMBA SIMARO MASIYA KUZIKWA JUMAPILI JIJINI KINSHASA

0
0
Mwili wa mwanamuziki mkongwe wa muziki rhumba wa nchini DR Congo, Marehemu Lutumba Simaro Masiya ukifanyiwa ibada ya kuuaga katika moja ya kanisa huki jijini Paris, Ufaransa leo, ambapo unatarajiwa kuusafirisha na ndege ya "Air France" kuelekea Kinshasa, nchini Congo kwa mazishi.

Mwili wa Marehemu Lutumba Simaro Masiya ukiwasili jijini Kinshasa, moja kwa moja utapelekwa kuhifadhiwa "Mortuary katika hospitali De Cinquantenaire, na baadaye kupewa heshima za mwisho bungeni, kabla ya kufika bungeni, atapitishwa nyumbani kweke, na kufikishwa pia kwenye "Lutumba Monument"sehemu yenye mnara wa kumbukumbu yake ili kuwapa nafasi wapenzi wa muziki wake kuuaga mwili wa mpendwa wao.

Mwili wa marehemu Lutumba Simaro Masiya utalazwa kwenye makazi yake ya milele kwenye makaburi ya "Nécropole Entre Terre et Ciel", jijini Kinshasa siku ya jumapili Aprili 29, 2019..

Marehemu Lutumba Simaro Masiya ambaye jina lake halisi ni "Apa Simon Lutumba Ndomanueno" alifariki Machi 30, 2019 jijini Paris nchini Ufaransa, akiwa na umri wa miaka 81. Atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi ikiwemo "Maya" (unaweza iangalia hapa chini).

Sehemu ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Lutumba Simaro Masiya, walipokuwa wakitoka kanisani kulikofanyika ibada maalum ya kuaga, jijini Paris Ufaranza.
Ankal pia anamkumbuka Mkongwe huyo wa Muziki wa Rhumba. Mungu ailaze pema peponi roho yake - Ameen

Mvua yaleta mafuriko Kahama mjini leo

0
0
 Hivi ndivyo hali ilivyo kwa sasa huko mjini Kahama, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha. nyumba nyingi zimekubwa na mafuriko kama inavyoonekana pichani. 


WAZIRI MKUU MAJALIWA, SPIKA NDUGAI WASHUHUDIA MECHI TIMU YA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR JIJINI DODOMA

0
0
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokelewa na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyochezwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mwenye Kijani ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mbunge Viti Maalum, Mhe. Salma Kikwete (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Pastobas Katambi (katikati). Mechi hiyo iliisha kwa timu zote mbili kufunga magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo.
Wachezaji wa timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kulia) wakisalimiana na Wachezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki baina yao iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mechi hiyo iliisha kwa timu hizo kufungana magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) wakifuatilia mechi kati ya timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyochezwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Watatu kushoto ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Pastobas Katambi.
Mbunge wa Kilolo, Mhe. Venance Mwamoto (katikati) ambae pia ni Kocha Mchezaji na Mfungaji wa bao la kwanza la timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Wachezaji wa timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapumziko katika mechi iliyowakutanisha timu hiyo na timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mechi hiyo iliisha kwa timu hizo kufungana magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishangilia goli walilofunga dhidi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar mchezo uliochezwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto ambaye pia ni mfungaji wa goli hilo na nyuma ni Ndg. Onesmo lau lau. Katika mchezo huo timu hizo zilifungana magoli 2 -2, Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano baina ya Mabunge hayo.

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA UKAGUZI WA HATUA ZA MAANDALIZI YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI JENGO LA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi ulipofikia.

Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako amemwelekeza Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019 ujenzi wa Jengo hilo kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.

Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa mbali na kumbi za mikutano na ofisi za uendeshaji. Jengo hilo linatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli Mei 1, 2019.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (katikati) akikagua mahali litakapojengwa jiwe la msingi ambalo litawekwa rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Mei 1, 2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni Mkadarasi wa Ujenzi Injinia Thedeus Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu) akifuatiwa na Profesa Ernest Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.

Waziri Ndalichako akiongozwa na Mkandarasi wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara alipowasili kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Taaluma na Utawala linalotazamiwa kumalizika mwezi Juni,2019. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu Mawakamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenzi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya mbeya mara tu baada ya kuwasili. Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto).
Profesa Joyce Ndalichako alikagua muonekano wa nje wa jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya pamoja na kukagua usafi wa mazingira, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi kabla Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajafika kuweka jiwe la msingi.

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AITAKA SUMA JKT KUMKABIDHI JENGO JIPYA LA UHAMIAJI JIJINI DODOMA BAADA YA MIEZI 18, WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO, LEO

0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, wakisaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo litakua na ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Katibu Mkuu ameitaka Suma JKT kumkabidhi jengo hilo kwa wakati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na wa Wizara yake, kabla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma JKT wanatarajia kujenga jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane, na litakamilika baada ya miezi 18. Kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Martin Busungu. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, akizungumza kabla ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, leo. Suma JKT ndiyo Mkandarasi wa jengo hilo lenye urefu wa ghorofa nane, na linatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kushoto), akimuaga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taida (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, mara baada ya kumaliza kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, jijini Dodoma, leo. Suma JKT wanatarajia kujenga jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane, na litakamilika baada ya miezi 18

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (watatu kushoto), Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu (watatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa JKT na Wizara, mara baada ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa Jengo hilo ambalo litakua na urefu wa ghorofa nane unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 18. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

………………..

Na Mwandishi Wetu, MOHA

KATIBU Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu amelitaka Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT), kujenga jengo la Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kwa ufanisi mkubwa na akabidhiwe jengo hilo baada ya miezi 18.

Akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa jengo hilo, kati ya Wizara yake na Suma JKT ambayo iliongozwa katika kikao hicho na Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, iliyopo Mji wa Serikali, Kata ya Mtumba, jijini Dodoma, leo, alisema hana shaka na uwezo wa Mkandarasi huyo, ila anaamini ujenzi huo utakua bora na utakamilika kwa wakati.

“Baada ya maandalizi ya ujenzi huu kuchukua muda mrefu lakini hatimaye tumekamilisha, hivyo nawaomba ndugu zangu tufanye kazi vizuri kabisa, na leo ndio siku ya kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi huu,” alisema Meja Jenerali KIngu.

Meja Jenerali Kingu alisema Wizara yake itafuatilia kwa karibu ujenzi huo, ambapo Mkandarasi ni Suma JKT na Mshauri Elekezi ni Chuo Kikuu cha Ardhi, hivyo jengo hilo anatarajia kuwa bora zaidi kutokana na uwepo wa wadau hao.

Kwa upande wake, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Busungu, alisema aliishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuwa na imani na Suma JKT na kuipa kazi ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya uhamiaji jijini Dodoma.

“Tunaishukuru Wizara yako kwa kutupa kazi hii ya ujenzi wa jengo hili ambalo ni la ghorofa nane, tunaahidi kulikamilisha baada ya miezi 18, na tutapiga kadiri inawezekana, tupo tayari kwa kazi yenye uweledi wa kuzingatia muda na ubora ambao utawauza zaidi Suma JKT,” alisema Meja Jenerali Busungu.

Mkataba huo ulisainiwa na viongozi hao huku ukishuhudiwa na wanasheria wa taasisi hizo ambao ni Mkurugenzi wa Sheria, Marlin Komba wa Wizara hiyo na Kapteni Joyce Mwaikofu kutoka JKT.

UBALOZI URUSI WAADHIMISHA MUUNGANO KW KUTANGAZA BIDHAA ZA TANZANIA

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akitoa neno la ukaribisho kwa wageni mbalimbali walioalikwa kushiriki kilele cha kuadhimisha Siku ya Taifa ya Tanzania (Maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano) yaliyofanyika jijini Moscow tarehe 26 Aprili 2019. Maadhimisho hayo yalipambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Maonesho ya bidhaa na vivutio vya utalii vya Tanzania; kukabidhi vyeti kwa wadau mbalimbali ili kutambua mchango wao katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania, hususan katika sekta ya utalii, uwekezaji, sanaa, lugha na utamaduni pamoja na kutoa fursa ya kubadilishana mawazo baina ya Mabalozi na taasisi za Urusi zinazojihusisha na masuala ya uwekezaji. Mwingine katika picha ni Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk. 
Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk akisoma hotuba katika maadhimisho hayo. 
Wageni waalikwa wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi Urusi wakisikiliza hotuba. 
Mhe. Balozi Mumwi na Waheshimiwa Mabalozi wa mbalimbali wa nchi za Afrika zenye uwakilishi nchini Urusi wakikata keki ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanzania. 
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wadau wanaochangia maendeleo na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. 
Mdau akipokea cheti chake ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Tanzania. 
Picha ya pamoja ya baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi, wageni, maafisa wa ubalozi na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Urusi walioshiriki katika maadhimisho hayo. 

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 7 KWA WAKUU WA MIKOA INAYOZALISHA DHAHABU KUFUNGUA MASOKO YA MADINI

0
0
Na Ripota Wetu-MAELEZO

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku saba kwa Wakuu wa Mikoa inayozalisha dhahabu nchini kushirikiana na Wizara ya Madini katika kufungua masoko ya madini ikiwemo dhahabu ili kuifanya sekta ya madini kuweza kuleta tija ya kiuchumi kwa Watanzania wote hususani wachimbaji wadogo.

Akizungumza Mkoani Mbeya leo Jumamosi (April 27, 2019) wakati wa katika hafla ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi la barabara ya Mbeya-Lwanjilo-Chunya-Makongosi yenye urefu wa Kilometa 111, Rais Magufuli alisema Serikali anayoiongoza kamwe haitokubali kuona wachimbaji wadogo wakiendelea kuteseka nchini.

Aliongeza kuwa tangu mwaka 2017, Serikali imepitisha Sheria Bungeni inayotoa maelekezo kuhusu usimamizi wa sekta ya madini nchini na hivyo anashangwa na baadhi ya Viongozi wake hususani Wakuu wa Mikoa inazozalisha dhahabu kusuasua katika kusimamia maelekezo ya maelekezo yake aliyoyatoa katika siku za nyuma.

Alisema kuwa Serikali pia imefuta kodi mbalimbali za madini na kuendelea kuwahamasisha wachimbaji wadogo kupeleka dhahabu zao katika masoko hayo, lakini hadi sasa baadhi ya Wakuu wa Mikoa wameshindwa kujenga masoko hayo, pamoja na faida mbalimbali zinazopatikana katika masoko hayo ikiwemo kuepusha dhuluma kwa wachimbaji, kupata dhahabu yenye ushindani pamoja na kuzuia upotevu wa kodi ya Serikali.

Aliongeza kuwa katika mkutano wake alioufanya hivi karibuni na Viongozi wa Wizara ya Madini na Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara inayozalisha Dhababu, alitoa maelekezo ya kufungua masoko ya madini katika maeneo yao, ingawa ni Mkoa wa Geita pekee uliyotekeleza maelekezo hayo wakati ujenzi huo hauhitaji nyumba au eneo kubwa.

“Kama Mkoa wa Geita, umeweza kuwa na Kituo cha soko la kuuzia madini, nashangazwa kwanini Wakuu wengine wa Mikoa wanashindwa kutekeleza maelekezo hayo, hivyo hili ni agizo kwa Wakuu wa Mikoa ya Katavi, Singida na Arusha kuhakikisha kuwa watatekeleza maagizo haya” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema Serikali anayoiongoza haiwezi kuwa na Viongozi na Watendaji wasiotaka kutekeleza maagizo, hivyo ametoa kipindi cha muda huo kuhakikisha kuwa vituo hivyo vinafunguliwa na hivyo kuwahakikishia masoko ya uhakika wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakidhulumiwa dhahabu zao na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

Aidha Rais Magufuli aliutaka Uongozi wa Mkoa wa Mbeya hususani Wilaya ya Chunya kuhakikisha kuwa soko hilo la dhahabu linafunguliwa haraka iwezekanavyo kwa kuzingatia kuwa rasilimali zote muhimu za kufanikisha maagizo hayo zipo ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vitatumika kwa ajili ya ulinzi wa madini ya dhahabu wakati wa mauzo hayo yakifanyika.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, alisema kuwa suala la kujiletea maendeleo kwa Watanzania linacheleweshwa na baadhi ya Viongozi Watendaji Serikali kwani wananchi hususani wachimbaji wadogo wa madini wamekuwa na juhudi kubwa za kujiletea maendeleo yao lakini wamekuwa wakikatishwa tamaa pamoja na juhudi kubwa wanazozionyesha katika kuchimba dhahabu.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema tangu kutungwa kwa Sheria ya Madini mwaka 2017, Serikali imeweza kuokoa kiasi kikubwa cha madini kutoroshwa nje ya nchi, ambapo katika Wilaya ya Chunya ambayo ni Wilaya ya pili kwa uzalishaji wa dhahabu Serikali imeweza kutoa jumla ya kilo 30 zilizokuwa zikitoroshwa nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa mtambo wa kuchenjulia madini.

Mara baada ya kujiridhisha na taratibu zote za kisheria, tumeweza kufungua mitambo 38 ya kuchenjulia dhahabu hapa Chunya, ambayo tulisimamisha shughuli hizi huko nyuma kutokana na utoroshaji mkubwa uliokuwa ukifanyika” alisema Biteko.
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli

TAASISI YA USIMAMIZI WA VIHATARISHI YASEMA KUNA VIHATARISHI VYA KIUSALAMA KATIKA MITANDAONI

0
0
Viongozi na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania(IRMT) wakiwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa mahafali ya tatu ya taasisi yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
Mgeni rasmi katika mahafali ya tatu ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania Anderson Mlabwa( watatu kulia)ambaye ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Vihatarishi kutoka Benki ya CRDB akifuatilia hotuba wakati wa mahafali hayo.Wengine ni viongozi na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa taasisi hiyo
Mgeni rasmi katika mahafali ya tatu ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Mkurugenzi wa Menejimenti ya Vihatarishi kutoka benki ya CRDB Anderson Mlabwa akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Makamu mkuu wa Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania( IRMT)Buyamba Buyamba akizungumza kwenye mahafali ya tatu ya taasisi hiyo yaliyofanyika leo Aprili 27,2019 jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania(IRMT) Dk.Mashaka Mkandawile akizungumza wakati wa mahafali hayo
Sehemu ya wahitimu wa Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi wakiwa kwenye mahafali ya tatu yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wahitimu 25 wametunukiwa vyeti
Mgeni rasmi katika Mahafali ya tatu ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Anderson Mlabwa ambaye ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Vihatarishi kutoka Benki ya CRDB akikabidhi cheti kwa moja wa wahitimu wa taasisi hiyo Fredrick Mgaya



*Yahamasisha Watanzania wengi kujiunga na taasisi hiyo ili kuongeza idadi ya watalaam

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

TAASISI ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania(IRMT) imesema kwa sasa kuna vihatarishi vingi vya kiusalama kwa njia ya mtandao huku akieleza wazi uhalifu mtandaoni nao umeshika kasi, hivyo ameshauri ni wakati muafaka kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kupata mafunzo yanayohusu Usimamizi  wa Vihatarishi.

Hayo yamesemwa na Makamu wa taasisi hiyo Buyamba Buyamba wakati wa mahafali ya tatu ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania(IRMT) ambayo yamefanyika leo Aprili 27, 2019 jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu 25 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu. 

"Tasnia hii ya Usimamizi wa vihatarishi inagusa maeneo mengi  sana na katika kipindi hiki ambacho teknolojia ndio inayotumika zaidi katika kufanya kila jambo , ni wazi watu wenye tabia ya wizi nao wanaitumia kufanya uhalifu wa mtandaoni na ukweli vihatarishi vya kiusalama mtandaoni ni vingi.Tunafaamu pia nchi yetu malipo mengi ya Serikali yanafanyika kwa njia ya mtandao, hivyo lazima idadi ya watalamu waliobebea kwenye usimamizi wa vihatarishi ikaongezeka na bahati nzuri taasisi yetu  ipo kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo,"amesema Buyamba.

Hata hivyo amesema kwa kuwa tasnia inayohusu majanga bado changa muamko wa Watanzania kujiunga na Taasisi hiyo kwa lengo la kupata mafunzo na hatimaye kuwa watalaam bado ndogo lakini kinacholeta faraja Serikali imeweka kipaumbele katika kuhakikisha eneo la kuangalia vihatarishi linapewa kipaumbele na ametoa mfano wa taarifa za uwepo wa kimbunga Kenneth ambapo Serikali ilichukua tahadhari zote kuhakikisha hata kikitokea madhara yanakuwa si makubwa sana.

Pia amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa taasisi mbalimbali ambazo zinahitaji watumishi wake kupata mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi ambapo amesema wamefurahishwa na hatua ambazo Mamalaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutokana na uwepo wa taarifaza kimbunga Kenneth."Taasisi yetu ilipata nafasi ya kutoa mafunzo kwa watumishi wa TMA na hakika wameonesha ukomavu katika kuchukua tahadhari baada ya kuona kuna vihatarishi vitatokea kutokana na kimbunga Kenneth,"amesisitiza.

Kuhusu mahafali hayo amesema , mwaka huu ni mahafali ya mwaka wa tatu, na jambo ambalo linawapa matumaini idadi ya wahitimu inaongezeka mwaka hadi mwaka na kufafanua mahali ya kwanza yalikuwa na wahitimu 17 lakini safari hii idadi ya wahitimu imeongezeka na hayo ni mafanikio ambayo wanajivunia nayo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo ambaye ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Vihatarishi na Matekelezo kutoka Benki ya CRDB Anderson Mlabwa aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela , ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa pamoja na ongezeko lilitokana na wahitimu hao bado pengo la watalaam wa fani ya Usimamizi wa Vihatarishi  bado kubwa katika sekta ya umma na bifasi.

Hivyo amesema bado jitihada zinazohusisha wadau wote zinahitajika ili kuhuisha mfumo utakaowezesha wataalam wengi zaidi  kuzalishwa  na kwamba CRDB itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kukuza taaluma hiyo hiyo kwa kudhamini wafanyakazi wao kushiriki katika mafunzo mbalimbali yanayotolewa na taasisi hiyo pamoja na kuchangia utalaam wenye lengo la kuziba mapengo ya kitaaluma kwa kadiri  watakavyohitajika na pia kudhamini matukio ya kukuza na kuendeleza taaluma ya usimamizi wa vihatarishi.

"Tumekusanyika hapa kufurahia na kushuhudia kutambuliwa rasmi matunda ya jasho la watahiniwa hawa.Ninafahamu wazi wahitimu hawa waliposajiliwa kwenye taasisi kama wanafunzi walikabiliwa na changamoto kubwa mbele yao.Kwa kuhitimu wamedhihirisha umahiri wao na kupa wasaa wa kushuhudia matunda ya juhudi zao.Hivyo sina budi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB kupogeza kwa dhati uongozi , walimu na wafanyakazi wote kwa kuwapika watalaamu hao,"amesema.

Ameongeza kama ambavyo inafahamika nchi yetu  inaelekea kwenye uchumi wa viwanda kama ilivyo kauli mbiu ya Serikali iliyotolewa na Rais Dk.John Magufuli.Hivyo uchumi wa viwanda unahitaji watalaam waliobobea wa masuala ya usimamizi wa vihatarishi ili kutoa taarifa mapema ya tahadhari za mbeleni na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingepotea kwa kutojua yaliyoko mbele.


"Sekta binafsi  inatambua na kufurahishwa na mchango wenu na jitihada mnazofanya hasa kwa kuzingatia mazingira magumu mnayokabiliana nayo.Kadiri idadi ya watalaamu inavyoongezeka , ndivyo tunavyosonga mbele kufikia lengo letu la kuokoa fedha nyingi katika uzalishaji kwa kutoa tahadhari ya mbele kwa ufasaha na kitaalum.Nisisitize IRMT imetengeneza mtaala wake ambao umetumika kupima watunukiwa hawa kulingana na mahitaji ya ndani ya nchi na viwango vya kimataifa na hivyo kuzalisha watalaam waliojaa vitendo zaidi kuliko nadharia kitu ambacho ni tofauti sana na taasisi nyingine za nje,"amesema Mlabwa.

Pia amesema watalaam waliohitimu leo si tu mabalozi wa Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania bali pia wanategemewa kuwa dira ya muelekeo wa taasisi hiyo na kwamba tunu zao ni dhamana , na zinabeba wajibu kwa wanataaluma hao wa kuaminiwa.Hivyo lazima wazitumie kwa uadilifu , uaminifu ,bidii na kuzingatia kanuni za nidhamu na tabia njema ikiwa ishara ya kuwa wawazi na wakweli na hivyo ndivyo vitu vinavyosisitizwa sana na Serikali.

Hata hivyo amesema wahitimu hao wanapaswa kufahamu kuwa Taifa linaamini kwamba wameandaliwa vizuri na hivyo wanaweza kujiunga na kufanya kazi kwa umahiri katika Serikali na taasisi binafsi au kuendesha shughuli zao wenyewe au kwa vikundi.Hivyo popote watakapokuwa na kwa wadhifa wowote watakaokuwa nao wasisahau matendo yao tabia, hekima zao zitakuwa kioo na taswira ya taasisi hiyo na mafunzo waliyoyapata yatapimwa kwa shughuli zao za kila siku sehemu za kazi.

Wakati huo huo amesema iwapo nchi itakuwa na watalaam wa kutosha wenye ujuzi wa namna ya kusimamia vihatarishi , Taifa litaokoa fedha nyingi  kutokana na matukio ya hatari ambayo yangeepukwa kama vile mikopo chechefu, wizi katika mitandao, mikataba mibovu , miradi isiyokwisha, manunuzi hewa, mfumuko wa bei na upotevu wa mali za umma.

Awali Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi hiyo Dk.Mashaka  Mkandawile amesema kutokana na maendeleo ya kukua kwa teknolojia, taasisi hiyo imeona haja ya kutoa mafunzo hayo ya usimamizi wa vihatarishi ili kukabiliana na kila aina ya vihatarishi nchini."Kukua kwa teknolojia kumeongeza vihatarishi na kunachangamoto nyingi hata katika sekta ya mabenki .Hivyo ni wajibu wetu kuendelea kuandaa na watalaamu wengi zaidi watakaokabiliana na kila aina ya changamoto.

"Pia ndio wakati sahihi wa waalaamu katika usimamizi wa vihatarishi kuweka mikakati ambayo itasaidia kukomesha vihatarishi vilivyopo na kutoa muelekeo wa nini kifanyike ili tuendelee kuwa salama .Tunafahamu wanaofanya uhalifu mtandaoni kila siku wanabadili mbinu, hivyo nasi kupitia watalaam wetu wanakatakiwa kuwa na mbinu mpya ili kukabiliana na wahalifu wa mitandaoni,"amesema Dk.Mkandawile.

EAC-IGAD-IOC LAUNCH ADVANCED TRAINING FOR POLICE OFFICERS ON CRIMINAL INVESTIGATIONS

0
0

EAC Secretariat

The East African Community, in partnership with the Intergovernmental Authority on Development (IGAD) and the Indian Ocean Commission (IOC) have over the last three years been implementing the ESA-IO Maritime Security Strategy with a Euro 37.5 Million seed funding from the European Union. Among the interventions envisaged is the enhancement of the Capacity of the Criminal Investigations Authorities of the participating states to effectively and efficiently investigate crimes at sea in a manner that provides a successful legal finish. The EAC was entrusted with this result area and commenced training of investigators on General Investigations, Forensic Investigations and Criminal Analysis. Six intermediate trainings, targeting 50 officers per cluster were held between January and June 2018.

The advanced trainings for the same officers in each of the clusters commenced with the training of 50 officers on Criminal Analysis that commenced on 23rd April 2019 in Mauritius. The trainings will take place within a two week period ending May 5th 2019. The trainings are being held at the Mauritius Prisons Training School in Port Louis. INTERPOL, within the context of the MoU between EAC and it (INTERPOL) concluded in 2012, is providing the technical expertise.

The trainings were formally launched by the Attorney General and Minister for Justice, Human Rights and Constitutional Reforms of the Republic of Mauritius Hon Maneesh Gobin. In his speech the Minister underscored the need for collective action by regional states in combating transnational organized crime. He noted that with the increase in the movement of people, money and goods, the level of sophistication of crime that rides on economic and social integration has increased. He called for the intensification of both horizontal and vertical information sharing among and within agencies and across states. He re-emphasized the need to strengthen commonality of purpose and where possible expansion of the training program to encompass more states particularly the French Speaking island states whose legal systems are different yet whose security is inextricably tied to other regional states (both littoral and inland).

The opening session was also graced by the Deputy Head of the EU Delegation in Mauritius Mr. Michael Gobalek, the Deputy Commissioner of Police Mr. Muktar Din Taujoo, and the Commissioner of Prisons, Mr. Premananda Apadoo. 
Participants for the trainings are drawn from Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia, Seychelles, Mauritius, South Sudan, Tanzania, and Uganda.

The Attorney General and Minister for Justice, Human Rights and Constitutional Reforms of the Republic of Mauritius, Hon Maneesh Gobin (far left) being welcomed at the venue by the Commissioner of Prisons, Mr. Premananda Apadoo (in the middle) and the EAC Peace and Security Expert, Mr. Leonard Onyonyi (far right).
 The Attorney General addresses the course participants. Seated (far left to right)  are the INTERPOL Training Mission Leader, Ms. Irina Koulatchenko; the Deputy Commissioner of Police, Muktar Din Taujoo; and the Deputy Head of EU Delegation, Michael Gobalek.

Group Photo Opportunity with the Chief Guest.

RC Mongella amwakilisha vyema Pinda kwenye harambee wilayani Sengerema

0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella jumamosi Aprili 27, 2019 amemwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana wilayani Sengerema.

Harambee hiyo imelenga kukusanya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya kwaya ya “New Life” ya kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji Leonard Giligwa pamoja na gari kwa ajili ya Parishi ya Bomani wilayani humo ambapo zaidi ya shilingi milioni 20 zimepatikana ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana Sengerema, Leonard Giligwa (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) picha maalum ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Mizengo Peter Kayanza Pinda kwenye harambee hiyo ambapo Pinda alikuwa mgeni rasmi na akawakilishwa na Mongella.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, Mchungaji wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana Sengerema Leonard Giligwa, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi pamoja na Mkuu wa Wilaya Ukerewe Colonel Magembe wakiwa kwenye harambee hiyo.
Mlezi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Lweru, Askofu Godfrey Mbelwa akiwa kwenye harambee hiyo.
Baadhi ya washirika na wananchi waliohudhuria harambee hiyo.
Tazama Vidio hapa chini

WAZIRI MKUU AWAAGA WATALII 1000 KUTOKA NCHINI ISRAEL

0
0
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kigwangala, wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, kuwasalimia na kuwaaga Watalii kutoka nchini Israel Aprili 27, 2019
 Wasanii wa kabila la Kimasai, wakitoa burudani kwa Watalii kutoka nchini Israel Aprili 27, 2019, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kigwangala, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, alipofika kuwasalimia na kuwaaga Watalii kutoka nchini Israel
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Another World Shlomo Carmel, iliyoleta Watalii 1000 kutoka nchini Israel, akiongea na kushukuru kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Watalii kutoka nchini Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, wakati akiwaaga Aprili 27, 2019.
 Watalii kutoka nchini Israel, wakimsikiliza Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, kabla ya kuondoka nchini
 Watalii kutoka nchini Israel, wakimsikiliza Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, kabla ya kuondoka nchini
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Watalii kutoka nchini Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA, wakati akiwaaga Aprili 27, 2019.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akimvalisha kikoi Mkurugenzi wa Kampuni ya Another World Shlomo Carmel, iliyoleta Watalii 1000 kutoka nchini Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kigwangala.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiagana na watalii kutoka nchini Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Another World Shlomo Carmel.
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiagana na watalii kutoka nchini Israel, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA Aprili 27, 2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Another World Shlomo Carmel.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

INTRODUCING "PULL UP" BY FRIDA AMANI ft. GiftedSon

Harmonize's "Niteke" Cover By Zahra

INTRODUCING "KARAOKE NIGHT" BY BAYO

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images