Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

TANESCO YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WA MTWARA, LINDI WAKATI WA KIMBUNGA

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limewataarifu wateja wake wa Mikoa ya Mtwara na Lindi kuchukua tahadhari kutokana na taarifa ya uwezekano wa kuwepo kwa kimbunga katika mikoa hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu inasema  inawashauri wananchi kuwa mbali na miundombinu ya umeme, na iwapo kimbunga kitaambatana na mvua kutokujikinga chini ya nguzo ama transfoma ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Imesema iwapo mwananchi ataona miundombinu imeathirika kwa kuanguka ama waya kukatika, ni vema akatoa taarifa TANESCO huku ikizuia kushika wala kukanyaga waya uliokatika.

Pia iwapo kimbunga kitaambatana na tadi, upepo mkali, au umeme kuwa unapungua nguvu na kuongezeka ndani ya nyumba, unashauriwa kuzima umeme kwenye Main Switch hadi hali hiyo itakapotulia.

AUAWA NA TEMBO AKIWA NJIANI KWENDA SHAMBANI

0
0
MKAZI wa kijiji cha Mpanji kata ya Mbati wilayani Tunduru Awetu Mussa(52) amefariki Dunia baada  ya kujeruhiwa sehemu mbalimbali ya mwili wake  na kundi kubwa la Tembo.

 Tukio hilo lilitokea tarehe 22 Mwezi huu, ambapo marehemu alipatwa na mkasa huo wakati  akielekea shambani na mumewe Ahmad Kisanje ambapo  wakiwa njiani majira  ya asubuhi walikutana na kundi  hilo la Tembo ambao walipumzika chini ya mti na mara baada ya kuwaona walibadili mwelekeo wa safari yao na kuanza kuwafuata.

Kwa Mujibu wa mume wa marehemu  Ahmadi Kisanje ni kwamba,  licha ya marehemu kujitahidi kukimbia kwa lengo la kuokoa maisha yake lakini alizidiwa mbio na Tembo hao ambao walimuangusha chini na kumkanyaga  ambapo Awetu  alifariki Dunia papo hapo.

Kisanje alisema,yeye aliweza kunusurika kutokana na kujificha nyuma ya kisiki kikubwa  huku akishuhudia mke wake akipoteza Dunia kwa kukanyagwa maeneo mbalimbali ya mwili.

Tembo hao ambao wanatembea makundi makubwa kuanzia 20 na kuendelea, wanatoka katika Hifadhi ya Selou na mapori yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa misitu  wamekuwa wakiharibu mazao mashambani na  kuleta tahuruki kubwa kwa wananchi  hivyo  kusababisha hata kushindwa kwenda  katika shughuli zao mashambani.

Ameiomba Serikali kupeleka Askari  wa Wanyama poli wengi katika kijiji hicho ili kurudisha hali ya amani na utulivu kwani kama Tembo wataachwa  bila kudhibitiwa kuna hatari ya wananchi kushindwa kwenda katika shughuli za uzalishaji mali.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru  ambaye alifika nyumbani kwa Marehemu kwa lengo la kuipa pole familia ya  iliyompoteza mpendwa wao alisema, Serikali imesikitishwa na tukio hilo  na imeshapeleka Askari  kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama poli(TAWA)kanda ya Songea  ambao wameanza kazi ya kufukuza tembo kurudi katika makazi yao ya kawaida.

Homera ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Tunduru amewataka Wananchi wa kijiji hicho na maeneo mengine kuchukua taadhari pindi wanapokwenda mashambani na  kuaghailisha safari zao pindi wanapoona dalili za uwepo wa wanyama hao.

Alisema, serikali inathamini sana maisha ya wananchi,lakini ni lazima nao wawe na tabia ya kuchukua taadhari ikiwemo kutolima jirani na maeneo ambayo yamehifadhiwa  kwa ajili ya wanyama.

Akiongea katika mkutano na wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa wilaya alisema, serikali haitalipa fidia wala  kutoa kifuta jasho  kwa mtu yoyote atakayejeruhiwa  na wanyama ambaye anafanya shughuli zake katika maeneo yasioruhusiwa kufanya shughuli za kibinadamu.

Kwa upande wake, mkuu wa kikosi cha  Mamlaka ya usimamizi Wanyamapoli kanda ya kusini Ruben Joseph amewataka wananchi kuwa makini pindi wanapokwenda mashambani na ikiwezekana kusubiri kwa muda wakati huu ambao wanaendelea kurudisha makundi hayo ya Tembo katika hifadhi.

Wakati huo huo kundi  kubwa la Tembo linakadiliwa kufikia 30 wamevamia shamba lenye ukubwa wa ekari tano  la mtendaji wa kijiji cha Mbesa wilaya ya Tunduru Rasso Kundeka na kuharibu  na kula matikiti zaidi ya  elfu tano.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera kulia akimpa pole Mzee wa kijiji cha Mpanji kata ya Mbati Ahmed Kisanje baada kufiwa na mkewe Awetu Musa kutokana na kushambuliwa na kuawa na Tembo alipokuwa njiani kuelekea shambani .
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori kanda ya Kusini Ruben Joseph akiongea na wananchi wa kijiji cha Mpanji wilaya ya Tunduru baada ya kutokea kifo cha mkazi wa kijiji hicho baada ya kushambuliwa na Tembo wakati akienda shambani,katikati Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mpanji wilaya ya Tuunduru wakinyanyua mikono kama ishara ya kukubali kuanza ujenzi wa zahanati baada ya wananchi hao kukosa huduma za Afya kwa miaka mingi ambapo Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera(hayupo pichani) kuchangia mifuko 100 ya saruji na Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori kanda ya Kusini nayo kutoa mifuko 10.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera wa pili kushoto akiangali mabaki ya Tikiti baada ya kundi kubwa la Tembo kuvamia na kufanya uharibifu wa mazao katika shamba la mtendaji wa kata ya Mbesa Rasso Kudeka.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akikagua shamba la Afisa Mtendaji wa kata ya Mbesa Rasso Kundeka ambalo kundi la Tembo lilivamia na kufanya uharibu mkubwa wa mazao ikiwemo Matikiti,viazi na mbaazi.

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI,WAJUMBE WA TASAF

TAARIFA YA MSIBA

0
0
Ndugu Ephraim Kinabo Lyaruu wa Sinon Lemara Arusha anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Engineer  Isaac Hipollyte Lyaruu , kilichotokea tarehe 22/04/2019 katika hospital ya Mount Meru, Arusha .

 Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwake AICC Arusha, Mazishi yatafanyika siku ya jumamosi Tarehe 27/04/2019 Shambani kwake Himo Moshi,njia panda ya Kilema ,habari ziwafikie  ndugu,jamaa na marafiki .

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MIAKA 10 YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE (UCSAF)

0
0
Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Eng. Peter Ulanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo kuhusiana na maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo yanayofanyika jijini Dodoma yakibebwa na kauli mbiu ya "Mawasiliano kwa Wote ni Kichocheo cha Kuufikia Uchumi wa Kati".

MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE (UCSAF)

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) unatarajia kufanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Maadhimisho hayo ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mfuko ni sehemu ya Utekelezaji wa Kauli Mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuufikia Uchumi wa Kati. Kauli mbiu katika maadhimisho haya ni Mawasiliano kwa Wote ni Kichocheo cha Kuufikia Uchumi wa Kati.

Maadhimisho haya yatafanyika hapa Dodoma kuanzia tarehe 27 Aprili hadi kilele chake tarehe 30 Aprili, 2019 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge). 

Katika maadhimisho haya, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umeandaa shughuli mbalimbali katika kipindi cha muda wa maadhimisho, yakiwemo maonesho ya watoa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 27 Aprili hadi siku ya kilele tarehe 30 Aprili 2019. Mfuko unachukua fursa hii kuualika umma wa wananchi wa Jiji la Dodoma pamoja nanyi waandishi wa habari kuhudhuria maonesho hayo yatakayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (maarufu kama Nyerere Square) jijini Dodoma.

Sambamba na maonesho hayo, Mfuko utazindua Klabu za TEHAMA katika Shule za Sekondari za Dodoma pamoja na Msalato zilizoko Dodoma siku ya tarehe 28 April 2019. Aidha Mfuko utagawa Kompyuta kwa Wilaya ya Gairo pamoja na kuzindua mnara wa mawasiliano uliopo wilaya ya Bahi siku ya tarehe 29 Aprili 2019, ikiwa ni kielelezo cha miradi ambayo inatekelezwa maeneo mengi nchini Tanzania Bara na Visiwani. 

Kwa miongo mingi Sekta ya Mawasiliano imekuwa ikikuwa kwa kasi ndogo katika nyanja zote za simu, posta na utangazaji. Mabadiliko ya Sekta ya Mawasiliano yalianza miaka ya 90 ambapo mfumo wa uendeshaji wa sekta ulibadilishwa na kuingiza uwepo wa wadhibiti wa sekta (Tume ya Mawasiliano na Tume ya Utangazaji) na kuanza kuingiza ushindani katika sekta ya mawasiliano. 

Miaka 10 baadaye mabadiliko zaidi ya kisekta yalifanyika kwa kuunganisha Tume ya Mawasiliano na Tume ya Utangazaji na kuunda Mamlaka ya Mawasiliano mwaka 2003. Katika kuongeza ushindani katika soko la mawasiliano lilijitokeza ombwe katika muundo wa sekta katika ngazi ya kiutendaji. Ombwe hilo lilitokana na nguvu za ushindani kujikita kupeleka mawasiliano katika maeneo yenye mvuto wa kibiashara na kuyaacha maeneo ya vijijini na ya mijini yasio na mvuto wa kibiashara. 

Serikali ililiona hilo kuanzia mwaka 2003 mpaka mwaka 2006 ambapo sheria ya kuanzisha Mfuko Mahsusi kwa ajili ya Mawasiliano ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mfuko huo ulianzishwa kama taasisi ya serikali inayojitegemea chini ya Wizara inayohusika na mawasiliano. Kanuni za kuanzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote zilisainiwa mwezi Aprili 2009. 

Sekta ya Mawasiliano katika kipindi kirefu cha tabribani miaka 30 iliyopita imepitia mabadiliko makubwa sana ambapo sekta imetoka kwenye kuwa na kampuni moja ya umma kabla ya mwaka 1993 ambayo ilikuwa inatoa huduma za simu za mezani, posta na hata telegramu na telex mpaka kuwa na soko kubwa la ushindani lenye makampuni makubwa ya simu za mkononi. Sekta ya mawasiliano imefaidi sana kwa uwepo wa mdhibiti wa mawasiliano aliyethabiti na kutoa mwongozo ambao umeifanya sekta ya mawasiliano kuwa sekta inayochangia maendeleo makubwa ya uchumi wa Tanzania. 

Mabadiliko ya kisekta yaliyofanywa na Serikali mwaka 2005 yaliongeza kasi ya ushindani katika sekta ya mawasiliano na mabadiliko ya aina hiyo yalitokea kwenye sekta ya utangazaji na sekta ya posta. Kuongezeka kwa ushindani kulisababisha ushindani wa bei na kufanya gharama kuanza kupungua hata hivyo kutokana na hali hiyo watoa huduma walichelea kupeleka mawasiliano ya aina zote maeneo ambayo yataonekana kukosa mvuto wa kibiashara hasa maeneo ya vijijini. 

Serikali ilianzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote mwaka 2006 na kusainiwa na Mheshimiwa Raisi mwaka 2007. Hata hivyo kanuni za kuanzisha Mfuko zilisainiwa Aprili 2009. Lengo kuu la kuanzishwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni kuhakikisha Mtanzania popote alipo ataweza kupata huduma za uhakika za mawasiliano iwe ni mawasiliano ya simu za mkononi, utangazaji, huduma za posta au intaneti. 

Toka kuanzishwa kwake Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umejikita kutambua mahitaji ya mawasiliano nchi nzima, kushirikisha wadau mbali mbali wa mawasiliano nchini, kushirikisha wananchi katika kutambua na kutatua kero za mawasiliano. Wakati Mfuko unaanza takriban asilimia 45 tu ya watanzania walikuwa wanaishi katika maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu. Mpaka tunavyoongea leo takriban asilimia 94 ya watanzania wanaishi kwenye maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu ambapo zaidi ya asilimia 70 ni watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu. Asilimia 10 imechangiwa na Mfuko wa Mawasiliano.

Imetolewa na

Eng. Peter Ulanga
Mtendaji Mkuu
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA JENGO LA NHIF NA KUHUTUBIA MAMIA YA WANANCHI WA JIJI LA MBEYA

0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi za NHIF lililopo jijini Mbeya leo tarehe 26/04/2019.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kufungua Jengo la Ofisi za NHIF lililopo jijini Mbeya leo tarehe 26/04/2019.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa Bodi ya  Mfuko huo wa Bima ya Afya Anna Makinda akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo hilo.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye jengo hilo la NHIF mara baada ya kulifungua.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia na kuwashukuru wananchi wa Mbeya waliokusanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili.
67
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia na kuwashukuru wananchi wa Mbeya waliokusanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili.
8910
Sehemu ya Wananchi wa Mbeya waliohudhuria Mkutano wa hadhara katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mbeya katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mbeya katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.
131415
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiwa na wananchi wengine akifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya. PICHA NA IKULU

DK.MABODI AMWAGA NEEMA KIJIJI CHA KIKOBWENI

0
0



 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza katika Mkutano wa Jimbo wa Jimbo la Chaani wa  kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
IMG_3592A
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi(kulia) akimsikiliza Mkaazi wa Kijiji cha Kikobweni Ndugu Hassan Nganja(kushoto) aliyetoa maoni yake juu ya kuwepo na upungufu wa huduma za Maji Safi katika Kijiji hicho.
IMG_3545A
BAADHI ya Wananchi wa Jimbo la Chaani wakisikiliza kwa makini taarifa mbali mbali za Utekelezaji wa Ilani katika Jimbo hilo.
IMG_3578A
MWAKILISHI wa Jimbo la Chaani Unguja Mhe.Nadir Abdul-Tif Yussuf akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa Jimbo hilo katika uwanja wa Mpira wa Kijiji cha Kikobweni Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
…………………….

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abudlla Juma  Saadalla Mabodi amesema CCM itachimba Kisima cha Maji Safi na Salama kwa  muda wa Wiki mbili ili kuondosha changamoto ya ukosefu wa huduma hiyo  kwa Wananchi wa Kijiji cha Kikobweni Jimbo la Chaani Wilaya ya Kaskazini  ‘A’ Unguja.

Ahadi hiyo ameitoa katika Mkutano wa Jimbo la Chaani wa kueleza  utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Chama na Serikali,ambapo baadhi ya  Wananchi wa kijiji hicho wamedai  kukabiliwa na upungufu wa huduma za maji safi na kwa sasa wanatumia maji ya kisima cha zamani cha kuvuta kwa kamba  kisichokidhi mahitaji yao.

Dk.Mabodi alisema kwa hatua ya awali anatoa kiasi cha shilingi milioni  1.5 kwa ajili ya maandalizi ya uchimbaji wa kisima hicho ili wananchi wa  kijiji hicho na vijiji jirani wapate huduma hiyo kwa wakati hasa katika  mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Alisema wananchi wana haki ya kueleza changamoto zinazowakabili kwa  viongozi wao waliowapa ridhaa ya kuwaongoza katika ngazi mbali mbali za kiuongozi katika Chama na Serikali.

Alisema CCM ni Taasisi ya Kisiasa inayoahidi na ikatekeleza kwa vitendo na kwa wakati mwafaka na haitoi ahadi za kuwalaghai wananchi kama vinavyofanya baadhi ya vyama vya upinzani kuwa wataijenga Zanzibar kwa  Siku 100 iwe kama Nchi ya Singapore.

Alisema maendeleo hayana itikadi wala misimamo ya kisiasa kwani inapotekelezwa Ilani ya CCM kwa kuwafikishia wananchi huduma za maji,Umeme,Bababara na Vituo vya Afya fursa hizo hazitumiwi na Wanachama wa CCM pekee yao bali wananufaika wananchi wote.

Alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sasa inatekeleza Ilani ya CCM kwa kujenga Barabara yenye kiwango cha Lami katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ili kurahisisha huduma za Usafiri kwa wananchi wa Mkoa huo.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi aliwambia wananchi wa Jimbo la Chaani kwamba Serikali ipo katika hatua za kutekeleza Mradi mkubwa wa Maji Safi na Salama ambapo ukikamilika utamaliza changamoto ya upungufu wa huduma za maji Mkoani humo.

Kupitia Mkutano huo Dk.Mabodi alielezea kuridhishwa kwake na Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo hilo, licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo zinazotafutiwa ufumbuzi wa kudumu na viongozi wa jimbo hilo.
Aliwataka Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo watatue changamoto zilizopo katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo ili Chama kishinde bila vikwazo  katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema CCM inapozungumzia ushindi wake wa Kihistoria katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020, ni kutokana na utekelezaji mzuri wa ahadi zilizotolewa kupitia Uchaguzi Mkuu uliopita.

Pamoja na hayo aliwasihi wananchi wa Jimbo hilo kuthamini miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwani kuna baadhi yao wamekuwa wakihujumu miradi hiyo kwa makusudi hali inayokwamisha baadhi ya fursa za kimaendeleo.
” Nimeshuhudia katika Mkoa huu inahujumiwa miondombinu ya Maji Safi na Salama kwa kuiba vifaa vya umeme,kuharibiwa kwa Gari ya wagonjwa na matukio mengine ya kukatisha tamaa na yote hayo yanatekelezwa na watu wachache wapinga maendeleo.

Kupitia Mkutano huu nawambia waache Tabia hizo mara moja vinginevyo mtu yeyote atakayebainika anatekeleza uhalifu huo litakalomkuta litakuwa ni fundisho kwa watu wengine, kwani haiwezekani mtu kuharibu miundombinu inayotegemewa na makundi mbali mbali ya wananchi wakiwemo Wenye Mahitaji Maalum. “,alifafanua Dk.Mabodi.

Aliwaonya baadhi ya Watendaji na Viongozi wa Ngazi za Majimbo katika Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, wanaojihusisha na mipango ya kuwaandaa wagombea wa ngazi mbali mbali za uongozi kabla ya muda wa kufanya hivyo kufika kwani kufanya hivyo ni kukiuka Katiba ya CCM ya mwaka 1977 na miongozo yake. 
Pamoja na hayo alisema kwamba CCM itaendelea kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa gharama yeyote na atakayejaribu kubeza atakuwa ni msaliti na adui wa Taifa.

 Akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe.Nadir Abdul-Tif Yussuf alisema kwa kipindi cha mwaka 2016-2017 alitekeleza masuala mbali mbali yakiwemo kuvipatia fedha za mitaji vikundi vya ujasiriamali,alinunua Gari maalum la Wagonjwa,kuweka Taa za umeme za kuwasha usiku Viwanja Vitatu,kujenga visima vya Maji Safi na Salama pamoja na kununua mashine za Kilimo za Power Tiller kwa ajili ya shughuli za Kilimo.

Miradi mingine iliyotekelezwa ni pamoja na matengenezo ya Ofisi mbali mbali za CCM,ununuzi wa Dawa za Binadamu katika Vituo vya Afya mbali mbali mbali pamoja na ununuzi wa Vyarahani 10 kwa ajili ya vikundi vya Jimbo.

Mhe.Nadir alitoa alitoa tahadhari kwa baadhi ya Watu wanaotengeneza makundi ya kuwagawa na kuwafitinisha viongozi wa Jimbo hilo uku wakipanga wagombea kinyume na utaratibu na kuongeza kwamba watu hao hawakitakii mema Chama Cha Mapinduzi.

Wakizungumza kwa wakati tofauti Wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya Mkutano huo,walieleza kwamba wamenufaika sana na miradi inayotekelezwa na fedha za Mfuko wa Jimbo wa Mwakilishi.

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA TCRA KUTOZIFUNGA LAINI ZA SIMU AMBAZO HAZIJASAJILIWA

0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema mchakato wa kusajili laini za simu kwa kuunganisha na Kitambulisho cha Taifa(NIDA) usogezwe mbele hadi Desemba mwaka huu huku akiagiza Watanzania wasiokuwa na vitambulisho vya NIDA wasihukumiwe kwa laini zao kufungiwa.

Kabla ya kauli hiyo ya Rais Magufuli ambayo ameitoa leo Aprili 26,2019 akiwa mkoani Mbeya ,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) walitangaza kuwa watazima laini za simu ambazo hazitakuwa zimesajiliwa na kuunganishwa na NIDA kwa kuweka alama ya kidole kigumba ambapo pia walitangaza kuanza kwa usajili wa laini za simu kuanzia tarehe moja ya mwezi ujao.

Akizungumza leo akiwa ziarani mkoani Mbeya pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amezungumzia usajili wa laini za simu uliotangazwa na TCRA ambapo amesema hakuna sababu ya kuwahukumu Watanzania kwa kuzima laini zao za simu kwa kigezo kwamba hawajasajili laini za simu.

Amesema ifahamike si kwamba anazuia usajili wa laini kwani ni muhimu na usajili huo una faida zake na ni nyingi lakini amefafanua Tanzania kuna Watanzania zaidi ya milioni 50 na wenye vitambulisho vya NIDA hawafiki milioni 15.

Hivyo amesema ni vema TCRA waongeze muda wa kusajili laini za simu kwa kwenda sambamba na utoaji wa vitambulisho vya Taifa. "Watu wasihukumiwe kwa kutosajili simu kwasababu ya NIDA.Mchakato uende pamoja ili watazania wasiopata wasihukumiwe," amesema Rais Magufuli .
 
Amesisitiza kadri NIDA wanavyotoa vitambulisho ndivyo kasi yake iendane na usajili wa laini za simu,hivyo wasifungue laini kwa kipindi hiki kwani kufanya ni sawa na kuwahukumu Watanzania.

Wakati huo huo Rais Magufuli ameagiza Jeshi la Polisi mkoani Songwe kuanza kuchunguza upya madai ya mtoto wa miaka minne wa kiume kulawitiwa.Rais ametoa maagizo hayo baada ya mmoja aliyekuwa katika mkutano wa Rais kupata nafasi ya kuzungumza mbele take ambapo alitoa malalamiko ya mtoto wake kulawitia.

Mama huyo baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza amemwambia Rais Magufuli kuwa mtoto wake wa kiume amelawitiwa na sasa anajisaidia muda wote na baada ya kitendo hicho aliamua kwenda kwenye vyombo vya ulinzi na usalama lakini hadi sasa haana msaada wowote zaidi ya kuzungushwa.

Amesema kuwa amekwenda kuonana na Kamanda wa Polis Mbeya,Mkuu wa Jeshi la Polisi ncbini IGP pamoja na Jaji Mkuu lakini anaona anazungushwa tu,hivyo matumaini yake yamebaki kwa Rais Magufuli ambaye ni Rais wa wanyonge.

"Rais wangu naomba msaada wako,nimekwenda kila mahali hadi kwa Jaji Mkuu,nisaidie mheshimiwa Rais ,nyaraka za note ambako nimekwenda ninazo.Mtoto aliyelawitiwa ni mwanaume na picha yake ninayo,lakini kwenye makaratasi wanasema ni mwanamke," amesema mama huyo wakati anamuleza Rais.

Hata hivyo Rais alimuuliza kama amekwenda na mtoto huyo mkutano hapo lakini mama huyo akajibu ameshindwa kwenda naye kwani anajisaidia Mara kwa mara,hivyo hakuweza kufika naye

Kutokana na maelezo hayo Rais Magufuli alimhakikishia mama huyo kuwa uchunguzi utafanyika na haki itatendeka ambapo ameomba nyaraka akabidhiwe mwanasheria ili kuanza ufuatiliaji.

Pia Rais Magufuli alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha mama huyo hasumbuliwi huku akimpa fedha kwa ajili ya kujikimu na mtoto wake.

KIMBUNGA KENNETH CHAISHIA ARDHI YA MSUMBIJI, KASI YA UPEPO YAPUNGUA

0
0
*Mtwara hali shwari, wananchi washauriwa kuzidi kufuatilia taarifa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa

Na Leandra Gabriel Blogu ya jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agness Kijazi amesema kuwa kimbunga Kenneth kipo katika ardhi ya Msumbiji na kinaenda katika maeneo ya kusini na kasi ya upepo ikiwa ni kilometa 70 kwa saa huku mzingo wake ukiwa umepungua kwa kilometa 200 na hakitaweza kufika hata kwenye mpaka wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo amesema kuwa matarajio ni kwamba mgandamizo huo ni mdogo na utaendelea kupungua nguvu huku kikisogea kuelekea kusini mwa Mashariki mwa Msumbiji ifikapo mchana wa tarehe 27 Aprili na mchana wa leo tarehe 26 mgandamizo huo mdogo ulifikia kuwa umbali wa takribani kilomita 297 kusini mwa Mtwara.

Aidha amesema kuwa mgandamizo huo mdogo hautarajiwi kutua katika ardhi ya Tanzania huku ikiwa wazi kuwa sio mbali sana na mpaka wa Tanzania.

Dkt. Kijazi amesema kuwa  mifumo ya hali ya hewa katika maeneo mengi ya nchi itaendeshwa na mgandamizo huo huku vipindi vya mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali vinaweza kujitokeza kufuatia mgandamizo huo.

Matazamio ya siku zijazo kwa kimbunga hicho ambazo kwa sasa ni mgandamizo Kijazi ameeleza kuwa, utarudi baharini na kikipata joto kitakuwa kimbunga kikubwa zaidi, na wao kama Mamlaka wanafuatilia kwa ukaribu ili kuweza kuzuia kutokea kwa maafa.

Maafa yaliyojitokeza kwa sehemu kilichopiga kimbunga hicho ambao nyumba na miti vimeharibiwa ni pamoja na Moeada, Muidumbe na Ilhadoibo  na Mji wa Pemba nchini Msumbiji, Kisiwa cha Komoro ambapo nyumba na miti vimeathirika huku nchini Tanzania upepo ukiongezeka kwa kilomita 60 kwa saa katika maeneo ya Mtwara.

Amesema kuwa Mamlaka ya hali ya hewa itaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa uliopo Kaskazini-mashariki mwa Msumbiji na mienendo mingine ya hali ya hewa kwa ujumla na kutoa taarifa za mrejeo kila itakapobidi.

Amewashauri wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka hiyo na kuzingatia tahadhari pamoja na kufuata ushauri na miongozo ya wataalamu katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya uratibu wa maafa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Matamwe amewashakuru wadau mbalimbali zikiwemo kampuni za simu zilizokuwa zinatoa jumbe na taarifa kwa wananchi kuhusiana na kimbunga hicho pamoja na wananchi wa Mtwara, Ruvuma na Lindi kwa kushirikiana na kamati za maafa katika maeneo yao ambapo kama kimbunga hicho kingepiga zaidi ya wakazi milioni moja wangeathirika na ametoa rai kwa kamati za maafa kote nchini kujiimarisha na kujiandaa dhidi ya majanga yoyote yanayoweza kujitokeza.

DKT. KALEMANI AWATAKA MAMENEJA AMBAO HAWAJAUNGANISHIA UMEME WANANCHI KUACHIA MADARAKA

0
0
Na Veronica Simba – Manyara
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa karipio kwa mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao wamekaidi agizo alilolitoa kuhakikisha wanawaunganishia umeme wananchi waliolipia huduma hiyo kwa wakati na kuwataka wajisalimishe makao makuu ya Shirika hilo Mei 5 mwaka huu, wakiwa na barua za kuachia nyadhifa zao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Dosidosi wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, jana Aprili 25, akiwa katika ziara ya kazi, Waziri Kalemani alisema hawezi tena kutoa msamaha kwa mameneja ambao hawajawaunganishia umeme wateja kwa wakati kuanzia kipindi cha nyuma hadi kufikia mwezi uliopita (Machi).

“Siwezi kusamehe tena mameneja ambao hawajawaunganishia umeme wateja kwa muda mrefu. Hii ni kwa sababu wamesababisha kuleta kero kwa wateja, usumbufu pamoja na kupotezea mapato Shirika la Umeme,” alisisitiza Waziri.

Katika hatua nyingine, Waziri alikerwa na hali aliyoishuhudia katika kijiji cha Nchinira wilayani humo, ambapo nguzo za umeme zinaonekana kusimikwa kwa muda mrefu pasipo kutundikwa nyaya ili kuwaunganishia wananchi.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Kalemani alilazimika kutoa onyo kali kwa mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini wilayani humo pamoja na kumtaka Meneja wa TANESCO wa Wilaya kuwasilisha maelezo makao makuu ya Wizara, Dodoma ni kwanini eneo hilo halijaunganishiwa umeme ilhali nguzo zilishasimikwa kitambo.

“Natoa onyo kwa Mkandarasi. Maeneo yote mliyosimika nguzo; sitaki kuona nguzo zimesimama bila kuwa na nyaya na bila kuwaunganishia umeme wananchi. Ni marufuku. Nguzo zikisimikwa, zitundikiwe nyaya na wananchi waunganishiwe umeme.”

Waziri alielekeza eneo hilo liwe limeunganishiwa umeme ifikapo wiki ijayo.

Aidha, akiwasha umeme katika shule ya sekondari iliyopo Kijiji cha Dodisdosi, Waziri Kalemani alitoa wito kwa walimu na viongozi mbalimbali wa ngazi za vijiji na mitaa nchi nzima, kulipia gharama za uunganishaji umeme ili Taasisi mbalimbali za Umma katika maeneo yao, hususani shule zipatiwe nishati hiyo muhimu.

Alisema siyo vema shule ikakamilika ujenzi na kuanza kutoa huduma kwa takribani miaka miwili au zaidi ikiwa haina umeme kwani inaweza kusababisha uduni wa maendeleo ya elimu katika shule husika.

“Uwepo wa umeme katika shule husaidia kuongeza hali ya ufaulu kwani pamoja na mambo mengine, kwa sababu walimu wataweza kufanya vizuri zaidi maandalizi yao ya kufundisha,” alifafanua.

Waziri aliwaeleza wananchi wa Kiteto kuwa vijiji vyote vya Wilaya hiyo pamoja na vitongoji vyake, ambavyo havijaunganishiwa umeme, vitapata nishati hiyo kwani viko katika orodha ya Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza ambao unatarajiwa kukamilika Juni mwakani.

Hata hivyo, alisema serikali imemuagiza Mkandarasi husika kuhakikisha anakamilisha kazi ya kuviunganishia vijiji vyote umeme kabla ya Septemba mwaka huu ili libaki zoezi la kuunganishia umeme wananchi ambalo nalo litatakiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mkataba wake.

Katika ziara hiyo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme wilayani Kiteto, Waziri Kalemani alifuatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo husika Emmanuel Papian, Kaimu Kamishna wa Nishati Juma mkobya, mameneja wa TANESCO wa Kanda na Wilaya pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani na REA.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), akizungumza na mafundi wanaounganisha umeme katika kijiji cha Osteti wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme wilayani humo, Aprili 25, 2019.
 Mafundi wakiunganisha umeme katika nyumba ya mmoja wa wakazi wa kijiji cha Osteti wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara. Taswira hii ilichukuliwa Aprili 25, mwaka huu wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kijijini humo kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini wilayani Kiteto, akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo, Aprili 25, 2019 kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme na kuzungumza na wananchi.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kabla ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Dosidosi wilayani Kiteto, mkoani Manyara akiwa katika ziara ya kazi, Aprili 25, 2019.

TIMU ZA BUNGE, WAWAKILISHI ZATOKA SARE 2-2

0
0
TIMU ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoka sare kwa kufungana mabao 2-2 na timu ya Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mtanange huo umechezwa leo (Ijumaa, Aprili 26, 2019) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa suluhu.

Timu ya Wabunge ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kwenye dakika ya pili ya kipindi cha pili   lililofungwa na Venance Mwamoto. Iliwachukua dakika mbili tu, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kusawazisha bao hilo lililofungwa na Juma Ally baada ya kupiga shuti kali la umbali wa mita 20.

Hata hivyo, goli hilo lilizua utata na kusababisha mpira huo kusimamia kwa dakika tano ili wavu wa goli urekebishwe kwa sababu mpira ulipita kwenye wavu ambao umechanika, upande wa kushoto juu ya goli.

Ilimlazimu mwamuzi Byrceson Msuya wa Dodoma awasiliane na mshika kibendera wake na hatimaye wakaridhia kuwa hilo lilikuwa ni goli.

Mara baada ya mpira kuanza, kapteni wa BLW, Hamza Hassan aliipatia timu yake bao la pili kwenye dakika ya nane baada ya kupigwa kichwa kupitia mpira wa krosi uliopigwa na Masoud Abraham.

Mpira uliendelea kwa kasi huku kila timu ikijaribu kutafuta goli ambapo kwa upande wa BLW, wachezaji Mohammed Mgaza na Juma Ali walikuwa mwiba kwa ngome ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha kwa upande wa Jamhuri ya Muungano washambuliaji Venance na Yona Kirumbi ambaye aliingia kipindi cha pili, walikuwa mwiba kwa ngome ya Baraza la Wawakilishi lakini ustadi wa golikipa wa BLW, Fakhi Suleiman ulikuwa kikwazo kikubwa kwao kwani akiokoa michomo mingi ya washambualiaji wa timu ya Bunge.

Ikiwa imebakia dakika moja mchezo huo kumalizika, mchezaji wa timu ya Bunge, Yona Kirumbi aliisawazishia timu yake bao la pili baada ya kupikea pasi ndefu kutoka kwa Onesmo Raurau.

Akitoa maoni juu ya mchezo huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alihudhuria mechi hiyo alisema mechi ulikuwa nzuri na imetumiaka kudumisha Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Pia aliahidi kwamba, kwenye maadhimishi ya mika 56 ya Muungano, timu ya Bunge itakenda kucheza uwanaja wa Aaman, Zanzibar pamoja na timu ya Baraza la Wawakilishi.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai alisemw timu ya Bunge imecheza vizuri sana na ameshuhudia timu ya Baraza la wawakilishi kiwa imezidiwa, na kama wangeongeza dakika tano, ni lazima timu yale ingetoka na ushindi.

Kwa upande wake, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zuberi Ali Maulid aliwapongeza wachezaji wa timu zote mbili kwa umahiri waliounyesha na kuongeza kwamba watawasubiria mwakani timu ya Bunge Sports Club katika mtanange utakaofanyika huko Zanzibar.

Timu ya Bunge iliwakilishwa na Ally Salum, Abdallah Haji, Salum Rehani/ Pascal Haonga, Ally King/Chiza Amani, Yusuf Kaiza, Venance Mwamoto, William Ngeleja/ Yona Kirumbi, Cosato Chumi, Sixtus Mapunda/Onesmo Raurau, Godfrey Mgimwa/Peter Msigwa na Alex Gashaza/Rajab Kipilo.


Timu ya Wawakilishi ilikuwa na Fakhi Suleima, Ali Salum, Ramadhani Hamisi, Amour Mohammed, Juma Ali, Miraji Khamis, Mohammed Mgaza, Masoud Abrahman, Rashid Ali Juma/Dau Maulid, Hamza Hassan na Suleiman Sarahan.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, wakati akiwasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019, kushuhudia mpira kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid, Mbunge wa Viti maalum, Salma Kikwete.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapa mkono Wabunge wa Bunge la Tanzania, wakati akikagua timu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, katika mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapa mkono Wabunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati akikagua timu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, katika mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akirusha shilingi kabla ya mechi kuanza, kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akipuliza firimbi, kwenye kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Mbunge wa Jang’ombe Ali King, akicheza mpira wa juu, katika mechi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid, kwenye kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Wabunge wakiangalia mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aprili 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KAMPUNI YA HAFFIYY ENTERTAINMENT KUWA MKOMBOZI KWA WASANII WA BONGO FLEVA

0
0
Mkurugenzi wa kampuni ya Haffiyy entertainment Hafidh Mkongwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mikakati ya kampuni hiyo kuinua vipaji na kuirudhisha Iringa kwenye ramani ya burudani








NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


KAMPUNI ya Haffiyy entertainment ya mkoani Iringa imejipanga kuhakikisha inainua vipaji vya wasanii wa bongo fleva mkoani Iringa kwa lengo la kuwakomboa vijana kuirudisha Iringa kwenye ramani ya Muziki kama ilivyokuwa hapo awali.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa mkurugenzi wa kampuni ya Haffiyy entertainment Hafidh Mkongwa alisema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha wanakuza vipaji vya wasanii wa bongo flava kwa kuongeza ajira kwa vijana.

“Kuna wasanii wengi wanavipaji lakini wanakosa wasimamizi wazuri hivyo kampuni yangu imejipanga kuhakikisha inawasimamia vilivyo kwenye sanaa hii na kuwaongezea kipato lakini kukuza pia vipaji vyao” alisema Mkongwa,Mkongwa alisema kuwa mkoa wa Iringa umepotea kwenye ramani ya burudani kwa muda mrefu hivyo kmapuni hiyo imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha kuwa Iringa inarudi kwenye ramani ya burudani.

“Miaka ya nyuma Iringa ilikuwa kwenye ramani ya burudani na ilikuwa inazalisha vipaji vingi hivyo hapa katika tumepotea kwenye ramani hiyo hivyo kamapuni yangu imejipanga vilivyo kuhakikisha wasaniii wa mkoa wa Iringa wanarudi kwenye ramani ya burudani” alisema Mkongwa 

Mkongwa alisema kwa sasa kampuni ya Haffiyy Entertainmet imeanza kuwasimamia baadhi ya wasanii kutoka mkoani Iringa na nyanda za juu kusini na sasa wameanza kumsimamia msanii aitwaye Meda Classic na msanii aitwaye Casso anatoka katika wilaya ya Temeke

“Hawa ndio baadhi tu ya wasanii ambao tumeingia nao mikataba ya kusimamia kazi zao lakini bado nawasaidia wasanii wengi ambao bado hawana mikataba na kampuni yangu hivyo mtaona jitihada zangu zimeanza kwa kasi kubwa” alisema Mkongwa

Aidha Mkongwa aliwaomba wananchi na wadau wa burudani mkoani Iringa kuendelea kuwaunga mkono kwa juhudi ambazo zinazofanywa na kampuni hiyo ili kukuza burudani na kuirudisha Iringa kwenye Ramani ya burudani.

“Iringa tulikuwa tunafanya kazi vizuri mno hivyo baada ya kupotea kwenye ramani niwaombe wadau tushirikiane kuhakikisha tunarudi kwenye ramani ya burudani” alisema Mkongwa

Mkongwa alimalizia kwa kuwaomba wasanii wenye vipaji na nidhamu ya kazi basi wamtafute ili kuhakikisha kuwa wanapata nafasi kwenye kampuni hiyo yenye leongo la kuinua vipaji vyao na kuwaongezea ajira vijana hao. 

POLISI ARUSHA WAJENGA NYUMBA ZAO SIKU YA MUUNGANO

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akishiriki kubeba matofali wakati wa ujenzi wa nyumba za askari polisi eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za Muungano.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathani Shana akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kushiriki ujenzi wa nyumba Sita za Polisi eneo la Njiro mjiani Arusha jana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano.
 Askari na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakishiriki usaombaji wa matofauri wakati wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa askari hao eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sherehe za Muungano. 
 Askari Polisi wakiwa chini ya msingi kwa ajili ya kumwaga zege wakati wa ujenzi wa nyumba za askari eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Muungano.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mwenye jacket akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathan Shana wakishiriki kubeba zege wakati wa ujenzi wa nyumba za polisi eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya sherehe za Muungano.
  Askari na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakishiriki usaombaji wa matofauri wakati wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa askari hao eneo la Njiro mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sherehe za Muungano. 
 
 

'TUNATAKA WATOTO WAZALIWE BILA VVU' - AGPAHI

0
0


Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akizungumza wakati wa kufunga warsha ya MAMA RIKA mkoa wa Mwanza Aprili 25,2019.



Tunataka Taifa la Tanzania liwe na watoto wanaozaliwa bila kuwa na Maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU)!

Haya ni maneno ya Cecilia Yona ambaye ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii wa asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI, wakati akifunga warsha kwa MAMA RIKA mkoa wa Mwanza iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

MAMA RIKA ni Waelimishaji wa akina mama wajawazito na wanaonyonyesha wanaoishi na VVU ambao wanapata huduma za tiba na matunzo katika kliniki ya mama,baba na mtoto (RCH) ili kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto. Warsha hiyo ya siku mbili imemalizika Alhamis Aprili 25,2019 jijini Mwanza na kuhudhuriwa na MAMA RIKA 70,wauguzi, waratibu wa huduma ya afya ya uzazi,waratibu wa huduma za VVU na UKIMWI katika jamii mkoa wa Mwanza.

Afisa Miradi huyo wa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona alisema ili kuwa na watoto wanaozaliwa bila maambukizi ya VVU katika taifa la Tanzania ni lazima akina mama wanaoishi na VVU wapewe elimu ya kutosha kuhusu namna ya kuzuia maambukizi wakati wa ujauzito, kujifungua na wakati wa kunyonyesha.

“Hatuwezi kupata watoto ambao ni Free From HIV (watoto wasio na HIV),bila akina mama kuwa na elimu,ndiyo maana AGPAHI tumewakutanisha MAMA RIKA ili tuwajengee uwezo juu ya masuala ya VVU na UKIMWI na namna ya kusaidiana kupitia uzoefu kutoka ujauzito mpaka watoto wanapopata kipimo cha mwisho cha uhakiki”,alieleza Yona.

“Lengo la kuwa na MAMA RIKA kwenye vikundi ni kusaidia kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,hivyo tunaamini mama akielewa vizuri,akipata elimu ya kutosha na akafuatilia yale aliyoelekezwa mtoto hatapata maambukizi ya VVU”,alisema.

“AGPAHI iko bega kwa bega kufanya kazi na MAMA RIKA,tunaamini kwamba huyu mama akijengewa uwezo vizuri kwa njia ya wataalamu na kufundishana wao kwa wao,wanapata nafasi kubwa ya kujifunza wenyewe kwa wenyewe kwa kutumia uzoefu walionao,yule ambaye ameshajifungua atamfundisha mjamzito, yule amemaliza kunyonyesha atamfundisha anayeanza kunyonyesha, kwa hiyo wanafundishana kwa njia ya uzoefu na elimu hiyo inakuwa sehemu ya maisha yao na kuwasaidia akina mama wengine”,aliongeza Yona.

Yona alitoa wito kwa washiriki wa warsha hiyo kuwa mabalozi na wasimamizi kwa akina mama wengine ili watakaporudi wakawasaidie akina mama waliopo katika kitengo cha kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Hata hivyo MAMA RIKA walioshiriki warsha hiyo walisema hivi sasa suala la ubaguzi na unyanyapaa limepungua kutokana na watu wengi kupata elimu kuhusu VVU na UKIMWI na wengi kujiweka wazi wakibainisha kuwa kupata maambukizi siyo mwisho wa maisha.

Aidha walishauri elimu iendelee kutolewa zaidi kwa akina mama wajawazito wahudhurie kwenye vituo vya afya wafundishwe mambo muhimu badala ya kufuata maneno mtaani na kujinyanyapaa matokeo yake wanajifungua watoto wenye maambukizi.
Afisa Miradi huyo wa Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akifunga warsha ya siku mbili ya MAMA RIKA mkoa wa Mwanza iliyofanyika katika ukumbi wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Cecilia Yona akiwasisitiza washiriki wa warsha hiyo kuwa mabalozi kwa akina mama wengine wawape elimu ya kutosha kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI ili wazaliwe watoto wasio na maambukizi ya VVU.

Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Cecilia Yona akionesha kitabu cha mwongozo wa kuendesha vikundi vya akina mama wanaoishi na VVU wenye ujauzito na wanaonyonyesha kutoka kitengo cha kuzuia maambukizi ya toka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT).
MAMA RIKA,wauguzi, waratibu wa huduma ya afya ya uzazi na waratibu wa huduma za VVU na UKIMWI katika jamii wakionesha vitabu vya mwongozo wa kuendesha vikundi vya akina mama (PMTCT) baada ya kugawiwa wakati wa warsha hiyo. Kushoto ni Mwezeshaji wa kitaifa wa masuala ya Vijana,VVU na UKIMWI, Dkt. Happiness Wimile Mbeyela.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.

Awali,Mwezeshaji wa kitaifa wa masuala ya Vijana,VVU na UKIMWI, Dkt. Happiness Wimile Mbeyela akitoa mada kuhusu unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU. Dkt. Happiness Wimile Mbeyela akisikiliza swali kutoka mmoja wa washiriki wa warsha hiyo.
Mwezeshaji katika warsha hiyo, Edwiga Zumba akitoa mada ukumbini.

Mwezeshaji katika warsha hiyo,Yahaya Isangula akiwasisitiza akina mama wajawazito na wanaonyonyesha wenye maambukizi ya VVU kuendelea kuwa wafuasi wazuri wa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs).
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akiuliza swali.
Mratibu wa huduma ya afya ya uzazi halmashauri ya wilaya ya Ilemela,Grace Kusaya akiwahamasisha MAMA RIKA kuwapa elimu akina wajawazito na wanaonyesha ili watoto wasipate maambukizi ya VVU.
Mratibu wa huduma ya afya ya uzazi halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Flora Kuzenza akichangia hoja.

Kaimu mratibu wa huduma ya afya ya uzazi halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Laurencia Damas akizungumza ukumbini.
Picha ya pamoja washiriki wa warsha.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Soma pia : AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA MAMA RIKA MKOA WA MWANZA

DC MSHAMA AWAASA MADEREVA BODA KULIPIA VITAMBULISHO VYA UJASIRIAMALI

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

MKUU wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama ,amewaasa madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda ,kulipia vitambulisho vya wajasiriamali na endapo watashindwa kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria.

Aliyasema hayo mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na madereva hao na kusema ,wao ni moja ya kundi ambalo linapaswa kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ambapo wanatakiwa kulipia shilingi 20,000.

Mshama alisema kuwa agizo la watu wanaofanyabiashara ambayo mtaji wake hauzidi kiasi cha sh.milioni nne wanapaswa kuwa na vitambulisho hivyo .

“Mnapaswa kununua vitambulisho hivyo na kwa wale ambao hawatakuwa na vitambulisho hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo hivyo hakuna budi kila mmoja wetu kuhakikisha analipia kiasi hicho ili waweze kufanya kazi bila ya usumbufu,” alisema Mshama.

Aliwataka wafanyabiashara wengine nao kulipa ili wapatiwe vitambulisho ambavyo Rais ametaka wajasiriamali wadogo wawe navyo kwani nao wanachangia uchumi wa taifa.

“Tunaendelea kuwahamasisha wajasiriamali wadogo wachangamkie fursa hiyo kwani ushuru waliokuwa wakilipa kwa sasa utakuwa haupo na kitambulisho hicho ndicho kitakuwa kimefidia na haitaruhusiwa kufanya bishara kama hawana vitambulisho hivyo,” alisema Mshama.

Kwa upande wake Bakari Kapera wa kitengo cha elimu ya mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Pwani alisema kuwa fedha wanazolipia leseni siyo kodi bali ni ada ili mtu kutambulika kuwa ni dereva.

Stanley Ndunguru kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga na Majini (SUMATRA) alisema kuwa malipo hayo yanalipwa na mmiliki wa chombo na siyo wao kama madereva kwani hawaruhusiwi kulipa ikiwa ni pamoja na bima. 

Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Jenifa Omolo alisema kuwa waendesha boda boda nao wametajwa kuwa nao ni mwiongoni mwa wanaotakiwa kulipia vitambulisho hivyo.

Katibu wa Chama cha Wamiliki na Waendesha Pikipiki wilaya ya Kibaha (CHAWAMAPIKI) Shaban Kambi alisema kuwa kilichosababisha wakashindwa kuchukua vitambulisho hivyo ni kutopatiwa elimu juu ya wanaopaswa kulipia.
MKUU wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama

TANZANIA KUWA MWENYEJI KARATE

0
0

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa michuano ya kimataifa ya Karate ambayo yamepangwa kuanza kurindima nchini Mwezi July jijini Dar es salaam, kwa kushirikisha mataifa ya bara la Afrika bara la Asia.

Taarifa za kufanyika kwa tukio hilo la kimataifa katika radhi ya Tanzania upande wa mchezo wa Karate, zimetolewa na Mkufunzi mkuu wa Karate tawi la Tanzania Jorome George Mhagama alipozungumza na kipindi hiki jijini Dar es salaam.

Mhagama amesema ni faraja kwa viongozi wa chama cha Karate nchini kuendelea kupata nafasi ya kuandaa michuano hiyo ya kimataifa, jambo ambalo ambaamini linaendelea kuitangaza nchi ndani ya Afrika na ulimwenguni kwa ujmla.

Mhagama amesema lengo kubwa la kufanyika kwa michuano hiyo, ni kuendelea kutoa nafasi ya kujifunza kwa wachezaji wan chi shiriki, kujenga urafiki na uhusiano ambao utaendelea kuifanya Tanzania kuwa na nafasi ya kutambulika zaidi kimataifa.

Pia ameelezea shughuli nyingine ambazo zitakwemnda sambamba na michuano hiyo ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa semina na mitihani nadharia na vitendo.

Wakati huo huo Mhabama akaweka wazi ratiba ya matukio yote kuelekea michuano hiyo ya kimataifa pamoja na semina itakayofanyika nchini Tanzania.

WAZIRI MHAGAMA AWAPA HAMASA TUCTA KUANZISHA VIWANDA

0
0



 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Mkutano wake na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kujadili masuala ya Wafanyakazi nchini leo Aprili 26, 2019, katika ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma. (Kushoto) ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Phillip Mpango, (wa tatu kutoka kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jaffo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika na rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
????????????????????????????????????
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Phillip Mpango akielezea jambo wakati wa mkutano huo, Kulia ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika (wa pili kutoka kulia) akisisitiza jambo kwa Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kujadili masuala ya Wafanyakazi nchini leo Aprili 26, 2019, Jijini Dodoma. (Kushoto) ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Phillip Mpango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na (wa tatu kutoka kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jaffo.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde(wa kwanza kushoto) pamoja na  Katibu mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe (katikati) na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kulia) wakifuatilia mada wakati wa Mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Mkutano huo.
????????????????????????????????????
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akieleza jambo kuhusu masuala ya Wafanyakazi nchini walipokutana Aprili 26, 2019 Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akichangia mada wakati wa Mkutano huo walipokutana kujadili masuala ya wafanyakazi nchini wakati wa kikao hiko kilichofanyika Jijini Dodoma. 
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akielezea jambo wakati wa Mkutano huo
????????????????????????????????????
Mwenyekiti Kamati ya Wanawake, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa Pili kutoka Kushoto) wakiimba kwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Kushoto), (wa tatu kutoka kushoto) ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika na rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa Pili kutoka Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo. (Kushoto) ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Phillip Mpango, (wa tatu kutoka kushoto) ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamghokya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………………..


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi kuanzisha viwanda ili kuinua uchumi na kuchangia adhma ya Serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda.

Ametoa kauli hiyo hii leo Aprili 26, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na viongozi hao uliohudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo pamoja na Naibu Waziri anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde ili kujadili masuala yanayohusu wafanyakazi nchini.

Waziri mhagama aliwataka viongozi hao kuwa wabunifu kwa kuanziasha viwanda vitakavyowezesha kujikwamua kiuchumi pamoja na kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kukuza mapato ya vyama vyao.

“Niwaombe sana muwe na mitazamo chanya katika kuchangia adhma ya Serikali kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vitakavyowawezesha kukuza uchumi mfano viwanda vya chaki, mbao na vingine vingi”, alieleza waziri Mhagama

Aidha aliwaeleza umuhimu wa kuanzisha viwanda hivyo ikiwa ni pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi nchini, kusaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuongeza motisha na kutoa fursa za ajira kwa wananchi kwa ujumla.

“Hii leo nimeona niwape changamoto ya kuona umuhimu wa kuwa na viwanda vyenu kwa kuangalia mchango wenu katika jamii na kuendelea kuwa na tija kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na viwanda nchini,” alisisitiza Mhagama

Kwa upande wake rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Bw. Tumaini Nyamhokya alishukuru mchango wa serikali na maoni yao kwa kuwapa chachu ya kuona umuhimu wa kuwa na viwanda na kuahidi kulifanyika kazi suala hilo.

“Kipekee nimefurahishwa na maoni na mawazo ya serikali hivyo hatuna budi kuanza kulifanyia kazi suala hilo ili kuendelea kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu”, alisema Nyamhokya

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bi. Rehema Ludanga alieleza alivyopokea ushauri huo wa serikali na kuona ni namna bora ya kujishirikihsha katika uchumi wa viwanda na kuonesha utayari wa kufanyia kazi suala hilo.

“Binafsi nikiwa kama mwenyekiti Kamati ya Wanawake nimelichukua kwa dhati kabisa na nitajitahidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo ili wanawake nao waweze kunufaika na fursa hii hasa upande wa sekta ya kilimo,” alieleza Bi. Rehema.

DKT MSONDE ATOA ONYO KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA

0
0



Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita mkoani Simiyu walio katika kambi ya Kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, wakati alipotembelea kambi hiyo Aprili 25,2019.
PICHA B
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato Cha Sita mkoani Simiyu wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde (hayupo pichani) wakati alipowatembelea katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 25, 2019.
PICHA C
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde azungumze na wanafunzi wa Kidato Cha Sita mkoani Simiyu, walio katika kambi ya Kitaaluma  Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa  Aprili 25, 2019.
PICHA E
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa,  Julieth John akitoa shukrani kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde alipowatembelea Wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, Aprili 25, 2019  katika kambi ya Kitaaluma Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa
PICHA F
Mwanafunzi wa Kidato Cha Sita Shule ya Sekondari Simba wa Yuda,  Innocent Leonard  akitoa shukrani kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taiga(NECTA), Dkt. Charles Msonde alipowatembelea Wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, Aprili 25, 2019  katika kambi ya Kitaaluma Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
PICHA G
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Mwl. Kuyunga Jackson akizungumza kwa niaba ya walimu wakati wa ziara ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde katika kambi ya Kitaaluma kwa Wanafunzi wa KIDATO Cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Aprili 25, 2019.
PICHA I
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), Dkt. Charles Msonde(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Elimu Mkoa wa Simiyu, walimu na wanafunzi wa Kidato Cha Sita mkoani Simiyu, Mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
 …………………..


Na Stella Kalinga, Simiyu

Katibu MTENDAJI wa Baraza la Taifa la Mitihani nchini (NECTA) amewataka wanafunzi wa kidato cha sita nchini wanaotarajia kufanya mtihani wao wa mwisho mapema mwezi Mei, 2019 kuepuka aina yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani huo.

Dkt. Msonde ameyasema hayo wakati akiongea na wanafunzi wa kidato cha sita mkoani Simiyu waliopo kwenye kambi ya kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, ambayo inayohusisha wanafunzi 1166 kutoka shule 12 zikiwemo 10 za umma na mbili za binafsi zenye kidato cha sita.

“Niwatake msifanye asilani habari yoyote ya udanganyifu kwenye mtihani wenu, mkifanya hayo tu kwanza yatawafanya mshindwe lakini pili tutakaponusa tu harufu yoyote ya udanganyifu tutawafutia matokeo”alisema Dkt. Msonde.

Wakati huo huo Dot. msonde amewataka wanafunzi hao kuondokana na dhana kwamba mtihani wa Taifa ni mgumu hali inayopelekea kuwa na homa ya mtihani(hofu), badala yake wajiamini na wajiandae vema kwa kuzingatia waliyofundishwa na walimu wao.

Pamoja na hayo amewapongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu kwa ubunifu wao wa kuanzisha kambi za kitaaluma hatua inayopelekea mkoa huo kupiga hatua ya katika ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na kidato cha nne.

Awali akimkaribisha Katibu Mtendaji wa NECTA, Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema kuwa awali mkoa ulikuwa na ufaulu mbaya lakini kupitia kambi ufaulu umepanda kuanzia matokeo ya kidato cha sita kutoka nafasi ya 26 mwaka 2017 hadi nafasi ya 10 mwaka 2018 na kidato cha nne kutoka nafasi ya 12 mwaka 2017 hadi nafasi ya 9 mwaka 2018.

Akiongea kwa niaba ya walimu mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Maswa Mwl. Kuyunga Jackson amesema kuwa vijana wa kidato cha sita Simiyu wamepikwa vizuri kitaaluma hivyo matarajio yao ni kuingia tatu bora kitaifa.

Katika hatua nyingine wanafunzi waliopo kambini hapo wamesema kuwa ujio wa katibu mtendaji NECTA umekuwa chachu ya ufaulu wao na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoyaeleza ikiwemo kuepuka udanganyifu pamoja na kuondoa homa ya mtihani.

“Tunakushukuru Sana kwa ujio wako umetujenga na kutuondolea hofu ya mtihani, tutafanyia kazi uliyotueleza, tunakuhakikishia hatutajihusisha na udanganyifu wowote kwa sababu walimu wametuandaa vizuri na tunajua udanganyifu unaweza kusababisha tusifikie ndoto zetu; tutazingatia yote tuliyofundishwa na walimu wetu” alisema Julieth John.

Taasisi ya APHFTA yashiriki Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2019

0
0
Kila mwaka Aprili 25 huwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambapo kwa mwaka huu 2019, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya imekuja na mkakati wa “Zero Malaria” unaolenga kutokomeza Malaria hadi kufikia mwaka 2030. Kitaifa maadhimisho ya siku ya Malaria 2019 yamefanyika mkoani Lindi yakiwa na kaulimbiu isemayo “ZeroMalaria inaanza na mimi” huku mikoa mingine nayo ikipata fursa ya kuandaa maadhimisho yake.

Katika Mkoa wa Geita, Chama cha Watoa Huduma Binafsi za Afya Tanzania (APHFTA) kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine wa afya, kimeandaa maadhimisho haya kimkoa katika shule ya msingi Mkapa iliyopo Mji Mdogo Katoro ambapo huduma mbalimbali ikiwemo upimaji wa Malari bure kutolewa kwa wananchi.

Chama cha APHFTA kimekuwa ikitekeleza mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita kuanzia mwezi Januari mwaka 2017 unaotarajiwa kufikia tamati mwezi Disemba mwaka huu ambapo mradi huo na mikakati mingine, umesaidia kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/16 hadi asilimia 17.3 mwaka 2017/18.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita kwenye Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2019 mkoani humo yaliyofanyika kwenye viunga vya Shule ya Msingi Mkapa iliyopo katika Mji Mdogo wa Katoro.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita kwenye Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2019 mkoani humo.
Mratibu wa Udhibiti Malaria Mkoa Geita, Dkt. Moses Simon akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Tanzania inazidi kupiga hatua kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambao vimelea vyake huenezwa na mbu jike aina ya “Anopheles” ikielezwa kwamba maambukizi yameshuka kwa  asilimia 50. Malaria ni hatari kwa sababu mtu mmoja hupoteza maisha duniani kila baada ya dakika moja kutokana na ugonjwa huo.

Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi (katikati) akiwa ameshika bango la "Ziro Malaria, Inaanza na Mimi" ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mkakati wa Serikali kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030.
Wakati chanjo mpya ya Malaria inayotambulishwa na Shirika la Duniani (WHO) ikitarajiwa kufanyiwa majaribio katika nchi za Kenya, Malawi na Ghana, Serikali ya Tanzania imetenga shilingi Bilioni 12.5 ili kutekeleza program mbalimbali za kupambana na Malaria hususani katika wilaya 10 nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi.

Wilaya zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya Malaria Tanzania ni Kakonko yenye asilia 30.8, Kasulu asilimia 27.6, Kibondo asilimia 25.8, Uvinza asilimia 25.4, Kigoma asilimia 25.1, Buhigwe asilimia 24, Geita asilimia 22.4, Nanyamba asilimia 19.5, Muleba asilimia 19.4 na Mtwara asilimia 19.1.

Juhudi za kupambana na Malaria ni pamoja na kutokomeza mazalia ya mbu, kugawa bure na kuhamasisha matumizi ya vyandarua vyenye dawa, kunyunyizia dawa za kuua mbu majumbani, kutoa elimu kwa wananchi ili kuweka mazingira yao safi, kuwahi hospitalini wanapohisi viashiria vya Malaria ikiwemo joto kali na kutapika.

Sehemu ya wananchi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2019 kwa Mkoa Geita yaliyofanyika katika Mji Mdogo wa Katoro.
Mgeni rasmi, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa Geita, Frank Moshi akikagua zoezi la upimaji Malaria kwenye maadhimisho hayo.
Tanzania inazidi kupiga hatua kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambao vimelea vyake huenezwa na mbu jike aina ya “Anopheles” ikielezwa kwamba maambukizi yameshuka kwa  asilimia 50. Malaria ni hatari kwa sababu mtu mmoja hupoteza maisha duniani kila baada ya dakika moja kutokana na ugonjwa huo.

Mwaka 2015 Tanzania ilikuwa na asilimia 14.4 ya maambukizi ya Malaria ambapo juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zimesaidia kiwango hicho kitaifa kupungua hadi asilimia 7.3 mwaka huu. Hata hivyo juhudi zaidi zinahitajika kwani kwa mujibu wa ripoti ya mwaka jana kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania ina asilimia 80 ya vifo vitokanavyo na Malaria.

Idadi kubwa ya wananchi ilijitokeza kupima Malaria bure.
Mmoja wa wakati wa Katoro mkoani Geita (katikati) akiwa kwenye bango la "Ziro Malaria, Inaanza na Mimi" ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mkakati huo wa kutokomeza Malaria Tanzania ifikapo mwaka 2030. Kushoto ni Mratibu wa Udhibiti Malaria Mkoa Geita, Dkt. Moses Simon na kulia ni Bigeso Makenge ambaye ni Mratibu wa Mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita unaotekelezwa na APHFTA kuanzia Januari 2017 hadi Disemba 2019.
Mwaka 2015 Tanzania ilikuwa na asilimia 14.4 ya maambukizi ya Malaria ambapo juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zimesaidia kiwango hicho kitaifa kupungua hadi asilimia 7.3 mwaka huu. Hata hivyo juhudi zaidi zinahitajika kwani kwa mujibu wa ripoti ya mwaka jana kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania ina asilimia 80 ya vifo vitokanavyo na Malaria.

Aidha matokeo ya utafiti wa viashiria vya Malaria Tanzania mwaka 2017 yanaonyesha Mkoa wa Kigoma unaoongoza kwa kiwango kikubwa cha ugonjwa huo ukiwa na asilimia 24 ukifuatiwa na Geita asilimia 17, Kagera na Mtwara asilimia 15, Tabora, Ruvuma na Lindi asilimia 12 hii ikiwa ni mikoa yenye kiwango cha juu cha maambukizi.

Taasisi ya APHFTA iligawa vipeperushi vyenye elimu kuhusu Malaria kwenye maadhimisho.
 Mikoa inayofuatia ni Mara yenye asilimia 11, Morogoro asilimia 10, Mwanza asilimia nane, Katavi asilimia saba, Simiyu na Shinyanga asilimia sita, Pwani asilimia tano, Mbeya asilimia nne, Tanga asilimia tatu, Singida, Rukwa na Iringia asilimia mbili, Dar es salaam, Dodoma na Mjini Magharibi Zanzibar asilimia moja.

Tazama BMG Online TV hapa chini

Halmashauri Zakusanya Bil 449 Mapato Ya Ndani

0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI 

IKIWA imepita robo tatu ya mwaka wa fedha 2018/2019, halmashauri zote zimekusanya Sh bilioni 449.8 ambayo ni asilimia 61 kati ya Sh bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo vya ndani huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkoa wa Dar es Salaam zikiongoza kwa mapato ghafi. 

Hayo yabamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alipokuwa akitoa taarifa za makusanya kwa halmashauri kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu na kusisitiza kuwa vyanzo vya mapato vinavyokuswanywa na serikali kuu havijumuishi katika makusanyo hayo. 

Akifafanua zaidi Jafo alisema halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi(asilimia 113), Geita (asilimia 109), Wanging’ombe(asilimia 105), Kilolo (asilimia 103) na Sumbawanga (asilimia 92) huku zile zilizofanya vibaya kuwa ni Newala na Tandahimba (asilimia 15), Momba na Masasi (asilimia 13) na Nanyamba (asilimia 12) 

Kwa kigezo cha pato ghafi, Jafo alisema halmashauri zinazongoza kwa wingi wa mapato kuwa ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma 9 (Sh bilioni 49.9), Ilala (Sh bilioni 44.8), Kinondoni(Sh bilioni 23.5) Temeke Sh bilioni 20.6) na Jiji la Arusha (Sh bilioni 12.5) wakati halmashauri tano zilizofanya vibaya katika kundi hili ni Madaba(Sh milioni 293.7), Newala (Sh milioni 268.3) Kakonko (Sh milioni 238.6) Buhigwe (Sh milioni 177.3) na Momba(Sh milioni 170.4). 

Aidha, katika kundi la mikoa kwa kigezo cha asilimia, Jafo alisema mikoa inayoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani ni Mkoa wa Iringa (asilimia 77), Geita (asilimia 73), Dar es salaam (asilimia 72), Dodoma na Songwe (asilimia 68) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Shinyanga (asilimia 46), Katavi (asilimia 43), Kigoma na Lindi (asilimia 42) na Mtwara (asilimia 26). 

Kwa upande wa mikoa kwa kigezo cha pato ghafi, Jafo alitaja mikoa inayoongoza kuwa ni Dar es Salaam (Sh bilioni118.4) Dodoma (Sh bilioni 57.30), Mwanza (Sh bilioni 22.9) Arusha (Sh bilioni 22.8) na Mbeya (Sh bilioni 19.8) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Manyara (Sh bilioni 6.5) Lindi (Sh bilioni 6.1), Rukwa (Sh bilioni 5.8) Kigoma (Sh bilioni 4.5) na Katavi Sh bilioni 3.8). 

Aidha, Jafo alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza katika kundi la halmashauri za majiji kwa asilimia kwa kukusanya asilimia 87 ya makisio huku jiji la Tanga likiwa la mwisho katikakundi hilo baada ya kukusanya asilimia 57 ya makisio. 

Alisema Halmashauri ya Dodoma inaongeza kwa kigezo cha patoghafi ambapo imekusanya Sh bilioni 50 na halmashauri ya jiji la Tanga imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya Sh bilioni 8.7. 

Aidha, Jafo alisema halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imeongoza kundi la halmashauri za Manispaa kwa kukusanya asilimia 92 ya makisio huku Lindi ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya asilimi 23 ya makisio. 

Jafo alisema kwa upande wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeoongoza katika kundi la halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha mapato ghafi baada ya kukusanyw Sh bilioni 50 huku Tanga ikiwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 8.7. 

Aidha, JAfo alisema halmashauri ya Mji wa Kondoa imeongoeza kundi la halmashauri za miji kwa kigezo cha asilimia ambapo wamekusanya kwa asilimia 92 ya makisio huku halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya asilimi 12 ya makisio. 

“ Katika kigezo ya pato ghafi kwa halmashauri za mji, Geita inaongeza baada ya kukusanya Sh bilioni 5.9 na halmashauri ya mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho ikiwa imekusanya Shilingi milioni 293.9. 

Kwa upande wa halmashauri za wilaya, Jafo alisema Mbozi inaongoza kwa kukusanya kwa asilimia 113 ya kamkisio nay a mwisho ni Masasi iliyokusanya asilimia 13 ya makisio wakati kwa upadne wa pato ghafi, Chalinze inaoongoza kwa kukusanya Sh bilioni 4.6 na ya mwisho katika kundi hili ni Momba iliyokusanya Sh milioni 170.4. 

Aidha, Jafo aliwataka wakurugenzi ambao makusanyao yao hayajafika asilimia 50 kuaza kujitathimini huku asikisisitiza kuwapo taarifa za baadhi ya watumishi kuhujumu ukusanyaji wa mapato. 

“ Mkurugenzi usikubali kurudishwa nyuma na watendaji wasio waamini, maana kuna baadhi ya maeneo watu wamekuwa wahatumii mifumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kieletroniki na wengine hawatumii kabisa,” 

Aidha, Jafo ameendelea kusisitiza wakurugenzi kuhakikisha fedha za mapato ya ndani asilimia 40 au 60 kuelekezwe kwenye miradi ya maendeleo eneo husika sambamba na utoaji wa asilimia 10 za fedha za ndani kwa walemavu, vijana na wanawake na kusisitiza kuwa mwisho wa mwaka mambo hayao yatakuwa ni tathimini ya utendaji wa wakurugenzi hao. 




Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images