Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhusiano wa Tanzania na China

$
0
0
Waziri wa Elimu Sayansi ya Tekenolojia Prof. Joyce Ndalichako Akizungmza katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China, iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
Balozi wa China Nchini Tanzania Wang Ke, akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
Waziri wa Elimu Sayansi ya Tekenolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Balozi wa China Nchini Tanzania Wang Ke mara baada ya kumaliza kuhutubia katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China, iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
Waziri wa Elimu Sayansi ya Tekenolojia Prof. Joyce Ndalichako, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.Damas Ndumbaro na Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda na mkewe Tunu Pinda, wakifuatilia hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Faraji Mnyepe(kushoto), akifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu Sayansi ya Tekenolojia Prof. Joyce Ndalichako, katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
Balozi wa China Nchini Tanzania Wang Ke (wa pili kushoto) akifuatilia burudani katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019, kushoto kwake ni Waziri wa Elimu Sayansi ya Tekenolojia Prof. Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.Damas Ndumbaro na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Agustine Mahiga.

Wasanii kutoka China wakitoa burudani katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019.
Kikundi cha ngoma za asili kutoka Mwananyamala Jijini Dar es Salaam, kikitoa Burudani katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China iliyofanyika katika Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jumatano 24 April 2019. (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO).

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, zimeadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia ulioasisiwa na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mao Ze Dong, Rais wa kwanza wa China.

Akiongea katika maadhimisho hayo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, amesema kuwa uhusiano huo umejenga urafiki mkubwa kwa Tanzania na China katika Nyanja zote za maendeleo.

“Napenda kuanza na Nukuu ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere ambaye alisema kuwa “sisi tunataka kuwa rafiki wa kila mtu na hatuwezi kuwa na rafiki ambaye anatuchagulia adui yetu”, China ilionyesha dhamira ya kuwa rafiki wa Tanzania, rafiki ambaye tulizuiwa kuwa rafiki yetu kipindi cha ukoloni, maneno haya ya Baba wa Taifa yalionyesha namna gani alivyokuwa anathamini urafiki wa Tanzania na China, kwa hiyo China ni rafiki yetu mkubwa”. Amesema Prof. Ndalichako.

Prof. Ndalichako ameeleza kuwa miaka 55 ya uhusiano huo umechochea kuwa na urafiki mkubwa ambao umeleta faida kwa kila nchi kwa sababu ya kujenga historia kubwa, kuthaminiana, kuheshimiana, kwa hiyo huo ni urafiki ambao kila mtu anamuheshimu mwenzie.

Prof.Ndalichako amesema kuwa katika maadhimisho ya miaka 55 kumekuwa na mafanikio makubwa katika Nyanja ya kiuchumi kwa kuwepo na miradi mbalimbali inayotokana na uhusiano China na Tanzania, miradi ambayo imetekelezwa ni Reli ya TAZARA, Kiwanda cha Urafiki, Kiwanda cha UFI, Kiwanda cha dawa keko, Kiwanda cha sukari Mahonda Zanzibar na Shamba la mpunga Mbarali.

Miradi mingine iliyotekelezwa kwenye urafiki huo ni Uwanja cha mpira wa Taifa, Uwanja wa mpira Amani Zanzibar, Bwawa la maji Chalinze, Kituo cha Mikutano Julius Nyerere, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Maktaba ya Chuo Kikuu Dar es Salaam ambayo ni maktaba kubwa kuliko zote ukanda wa Afrika pamoja na jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Prof. Ndalichako amesema kuwa China imekuwa ikiifadhili Tanzania nafasi 100 za wanafunzi kusoma China katika fani mbalimbali zikiwemo za uhandisi na udaktari “Kila mwaka China imekuwa ikitoa nafasi 100 kwa wanafunzi wetu kusoma nchini China, lakini pia katika maeneo muhimu kama udaktari kuna nafasi 20 za madaktari bingwa kwenye fani ya upandikizaji uboho na nafasi 30 kwa madaktari kwenda kusoma mafunzo mafupi, hakika huu ni urafiki mzuri na umekuwa na mafanikio makubwa”, amesema Prof.Ndalichako.

Kwa upande wa Miradi ya uwekezaji Prof.Ndalichako amesema kuwa tokea mwaka 1990 hadi Desemba mwaka jana tayari China ina miradi 723 ambayo imefanywa na wawekezaji kutoka China ambayo imetengeneza ajira 87,126, pia kwenye utalii Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu sasa.

“Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano mkubwa pia katika sekta ya utalii na sekta ya utamaduni, ikiwemo kwa Chuo chetu cha Dar es Salaam na Dodoma kuwa na taasisi za kufundisha utamaduni wa China, lakini pia tumeanza kufundisha lugha ya kichina na mpaka sasa shule 15 zinafundisha lugha hiyo, kwenye utalii uzinduzi wa safari ya ndege yetu ya Dreamliner 787 itaanza safari zake moja kwa moja mpaka China na kuleta watalii wengi kutoka china kuja kutalii nchini”.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alisema kuwa uhusiano huo ulioasisiwa na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania na Mao Ze Dong Rais wa kwanza wa China, umeleta urafiki mkubwa kwa watu wa Tanzania na China.

“Hatuna budi kuulinda urafiki huu kwani ni urafiki wa faida, tumekuwa tukishirikiana katika miradi mbalimabli ikiwemo ujenzi wa reli ya TAZARA na miradi mingine ya maendeleo ambayo inaleta faida na manufaa kwa watu wetu”, alisema Wang Ke. Urafiki wa Tanzania na China ulianza mwaka 1964 mara baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

JAJI MKUU AWAAGIZA MANAIBU WASAJILI WA MAHAKAMA KUU KUANDAA KUMBUKUMBU ZA RUFAA KWA UFASAHA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa kwanza kulia) akiwa katika kikao cha mwaka cha Majaji wa Mahakama ya Rufani cha kutathmini utendaji wa mwaka 2018 na kuweka malengo ya mwaka 2019. Kikao hicho kilifanyika kwa siku mbili (2) Aprili 23 na 24, 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimewashirikisha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani, Manaibu Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, Wasaidizi wa Kisheria wa Majaji, Makarani na Watunza kumbukumbu wa Mahakama ya Rufani.

Na Mary Gwera, Mahakama

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Manaibu Wasajili wa Mahakama Kuu nchini na wote wanaoshughulika na uandaaji wa kumbukumbu za rufaa kuzingatia sheria na kanuni muhimu katika uandaaji wa nyaraka hizo ili kuondoa mapungufu yanayoweza kusababisha usikilizaji wa rufaa kukwama.

Akizungumza wakati wa kufunga rasmi kikao cha siku mbili (2) cha Majaji wa Mahakama ya Rufani nchini kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) Aprili 24, 2019, Mhe. Jaji Mkuu alisema kwa kufanya hivyo kutapunguza makosa yanayojitokeza ambayo kwa wakati mwingine hupelekea ucheleweshaji wa usikilizwaji wa rufaa hizo kwa kufanya marekebisho mara kadhaa.

“Ni vyema Manaibu Wasajili na Watumishi wanaohusika katika utayarishaji wa nyaraka hizo, kuandaa vyema kumbukumbu za rufaa ‘records of appeal’ kwa kuibua makosa mbalimbali yanayoonekana pindi wanapoandaa kumbukumbu za rufaa ili kuzuia kesi kuchukua muda mrefu Mahakamani,” alieleza Mhe. Jaji Mkuu.

Awali, akitoa taarifa ya Utendaji wa Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2018, Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Elizabeth Mkwizu alisema kwa mwaka huo Mahakama ya Rufani iliweza kushughulikia jumla ya mashauri 1230 katika jumla ya vikao 38 vilivyofanyika katika Kanda 11 kote nchini.

Mhe. Mkwizu alisema kuwa jumla ya Mashauri 1108 kati ya 1230 yaliyopangwa katika vikao hivyo yalimalizika ikiwa ni asilimia tisini (90%) ya mashauri yote yaliyopangwa kusikilizwa.

“Hiki ni kiwango kizuri pamoja na kuwa lengo la kumaliza mashauri kwa asilimia mia moja (100%) halikutimia, hata hivyo tunatoa pongezi kwa wote waliochangia mafanikio hayo,” alieleza Mhe. Mkwizu.

Akizungumzia muda wa mashauri kukaa Mahakamani, Mhe. Mkwizu alisema kuwa takwimu za mashauri zinaonyesha kushuka kwa wastani wa muda wa rufaa za jinai kukaa Mahakamani kutoka siku 5240 mnamo Februari, 2017 hadi siku 898 kufikia mwishoni mwa Desemba 2018 na kusema hii ni hatua kubwa.

Kwa upande mwingine, kwa mwaka huu 2019 Mahakama ya Rufani imejiwekea malengo ya kuendelea kusikiliza mashauri na kuimarisha masjala.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mpango kazi wa Mahakama ya Rufani ya mwaka 2019 Mahakama ya Rufani tayari imepitia Rejista na kukusanya takwimu za mashauri, kufanya ‘stock taking’ ya mashauri yaliyopo katika masjala, kuainisha idadi ya mashauri yaliyopo kwa kanda na kwa umri lengo likiwa ni kuweka mkakati wa uondoshaji wa mashauri ya zamani kulingana na mzigo uliopo kwa kila kanda.

Mkutano wa mwaka huu wa Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani pia uliwashirikisha Manaibu Wasajili, wasaidizi wa kisheria wa Majaji, Makarani na watunza kumbukumbu ambao walitoa taarifa za utendaji kazi pamoja na changamoto zinazowakabili ili waweze kusaidiana kwa pamoja kupanga mikakati ya kumaliza mashauri kwa wakati.

VACANCY ANNOUNCEMENT

$
0
0

PRESS RELEASE


Vacancy notice

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received Vacancy Notice for the post of Director General available at the African Development Bank (AfDB) for qualified individuals to apply. 


Application details can be found through the following website: http://www.afdb.org. Closing date for application is 1st May, 2019.

The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply.

Issued by:

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

Dodoma.

25th April, 2019.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA KENYA, KUWAIT

$
0
0
*Asisitiza uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na mabalozi wa Kenya na Kuwait na kuwasisitizia kwamba Tanzania inakaribisha wawekezaji kutoka kwenye nchi zao na hasa eneo la ujenzi wa viwanda.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 25, 2019) alipokutana kwa nyakati tofauti na Balozi wa Kenya nchini, Bw. Dan Kazungu na Balozi wa Kuwait nchini, Bw. Mubarak Alsehaijan ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda, tutafurahi tukipata wawekezaji kutoka Kenya ili waje wawekeze kwenye viwanda kwani tunajua Kenya ilianza mapema kujihusisha na ujenzi wa viwanda wakati sisi tukiwa bado na mfumo wa ujamaa,” amesema.

Waziri Mkuu alimweleza Balozi Kazungu kuwa anatambua kwamba miongoni mwa nchi za Afrika, Kenya inaongoza kwa uwekezaji hapa nchini lakini kwa fursa ambazo Tanzania inazo, bado wanayo nafasi ya kuja kuwekeza.

“Kwa kuzingatia kuwa Mheshimiwa Rais ameleta Waziri, Katibu Mkuu na TIC kwenye ofisi yangu, hii maana yake ninapaswa nisimamie suala la uwekezaji kwa karibu zaidi. Tumetengeneza blueprint, tumeweka taasisi 11 pale TIC za kurahisisha usajili na hivi sasa mwekezaji siyo lazima aje Tanzania, anaweza kujisajili mtandaoni hukohuko aliko,” amesema.

Pia alisisitiiza suala la kulinda amani katika nchi hizo mbili na hasa ulinzi wa mipakani. “Wenzetu mmepata mitisikiko ya ugaidi hivi karibuni, lakini ulinzi wa uhakika wa pamoja ni jambo linalojadilika na linalowezekana. Sisi tuko tayari kuwaunga mkono katika vita dhidi ya ugaidi, uharamia, na usafirishaji wa dawa za kulevya,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Balozi Kazungu amemshukuru Waziri Mkuu kwa ushirikiano ambao Serikali ya Kenya imekuwa ikiupata kutoka Tanzania na kuahidi kudumisha udugu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.

“Sisi ni ndugu, tena ni majirani na mtu huwezi kuchagua jirani yako awe nani. Tunahitaji tuwe karibukaribu na kama ni biashara, basi watu wetu wawe wanafanya biashara kama majirani,” alisema Balozi Kazungu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemshukuru Balozi wa Kuwait kwa misaada ambayo nchi hiyo imekuwa ikiipatia Tanzania kupitia taasisi zake za kijamii.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu amesema Serikali ya nchi hiyo kupitia Kuwait Fund, imesaidia ujenzi wa barabara ya Chaya-Nyahua (Tabora), mradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe na ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja huko Zanzibar.

Amesisitiza kuwa bado Tanzania na Kuwait zinahitaji kuimarisha mahusiano yao katika maeneo mengine ya kiuchumi.

Naye Balozi Alsehaijan wa Kuwait amemshukuru Waziri Mkuu na kuahidi kuwa nchi yake iko tayari kuendelea kutoa misaada na huduma za kijamii.

Alisema kupitia taasisi za kujitolea, kuna mashirika manne (charity groups) ambayo yamejenga vituo vya watoto yatima Singida na Mwanza lakini kwa Mwanza, pia wameanza kuwahudumia na watu wenye ulemavu. “Pia wanajenga hospitali huko Zanzibar,” alisema.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akijibu swali, katika kipindi cha maswali na majibu, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu, ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma, Aprili 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu, ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma, Aprili 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Alsehaijan, ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma, Aprili 25, 2019.
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Alsehaijan, ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma, Aprili 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KIMBUNGA KENNETH CHASHIKA KASI , TMA YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI ILI KUEPUKA MAAFA

$
0
0
*Kesho asubuhi kutua nchi kavu, mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma yatajwa
*Kasi yake ya upepo yazidi kuongezeka kadri kinavyosogea katika nchini yetu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imetoa muelekeo wa kimbunga Kenneth ambacho kwa sasa kipo Bahari ya Hindi ambapo hadi asubuhi ya leo kilikuwa tayari kipo katika Pwani ya nchi yetu na Pwani ya Msumbiji na kimeshakuwa na jicho na hivyo kuwa na nguvu kubwa.

Hivyo TMA imeendelea kusisitiza wananchi kusikiliza na kufuata ushauri unaotolewa na Serikali kwa lengo la kuhakikisha athari zitokanazo na kimbunga hicho ikiwemo ya maafa yanapungua huku ikifafanuliwa kimbunga hicho kesho kitatua nchi kavu katika ardhi ya Msumbuji lakini upepo wake utafikia mikoa ya Kusini ya Lindi, Ruvuma na Mtwara.

Akizungumza leo Aprili 25,2019 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnnes Kijazi amesema wamefuatilia muelekeo wa kimbunga hicho ambacho kutokana na muelekeo wake kipo pia Visiwa vya Comorro.

"Muelekeo wa kimbunga hiki kwa sasa kipo Bahari ya Hindi na kinaendelea kusogea kuelekea maeneo ya nchi yetu na mpaka kufika leo kilikuwa kimeshafika Pwani ya nchi yetu lakini pia Pwani ya Msumbiji."Kimbunga hiki tayari kimekuwa na jicho, hivyo kina nguvu kubwa zaidi na jinsi kinavyoendelea kusogea kuelekea katika Pwani kinaendelea kuongezeka nguvu na kwa sasa kina mgandamizo wa 936 ambao ni mdogo.


"Mgandamizo huo unavuta upepo kuekelea kwenye kimbunga hicho na kasi ya upepo kwa sasa ni kilometa 130 kwa saa lakini kadri kinavyozidi na kasi inaongezeka na hivyo tunatarajia kuwa na kasi ya kilometa 140 kwa saa,"amesema Dk.Kijazi.

Amefafanua kesho Aprili 26, 2019 kimbunga Kenneth kitakuwa kinatuka nchi kavu nchini Msumbuji na kitakuwa na umbali wa kilometa 237 kutoka eneo la Pwani ya Mtwara. Kwa kawaida kimbunga kinapotua kinapunguza nguvu ya ule upepo lakini upepo huo lazima utasababisha athari katika maeneo ya nchi kavu.

"Kwa kasi ya upepo wa kimbunga hicho ambacho ni kikubwa kuwahi kutokea athari zake zinaweza kuikumba mikoa ya Lindi,Ruvuma na Mtwara yenyewe, hivyo ni vema wananchi wakachukua tahadhari kuepuka maafa ya watu na uharibifu wa mali na miundombinu na hasa kwa kuzingatia kitaongeza pia kna cha bahari.

Amefafanua kwa Mkoa wa Mtwara mvua ambazo zimeanza kunyesha wananchi wanaweza kuziona ni za kawaida lakini kadri kimbunga kinavyosogea ndivyo ambavyo mbunga kinavyoongezeka." Kimbunga kitakuwa katika nchi kavu hadi Jumatatu kabla ya kurudi tena baharini.Hivyo tuchukue tahadhari kwa kipindi chote hicho na TMA tutaendelea kutoa taarifa ya muelekeo wa kimbunga Kennethi,"amesema Dk.Kijazi.

TIC YAMSHUKURU RAIS MAGUFULI,YAKASIRIKA KUFUNGWA KWA BIASHARA, VIWANDA KWASABABU YA MADENI KATIKA KODI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kimemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa namna anavyokipigania kituo hicho kufanikisha majukumu yake huku kikitoa rai kwa taasisi nyingine nchini kuacha kufungia viwanda na biashara kwani madhara yake ni makubwa.

Akizungumza leo Aprili 25,2019 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe amesema wanamshukuru Rais kwani anawapigania sana akiwa katika ziara yake ya Lindi,Mtwara,Ruvuma na Njombe ametoa maagizo na maelekezo kwa TIC na taasisi nyingine zinazohusika na uwekezaji.

"Huu ni wakati wa kuacha kufikiria misaada na badala yake ni kuweka mipango kufanya uwekezaji, Rais anataka rasilimali zetu zitumike kuleta maendeleo. Kwa rasilimali ambazo nchi yetu inazo ni matajiri,nchi nyingine wanamiliki milima na barafu tu.  

"Kwetu sisi TIC Rais anatusaidia sana na imefika mahali akasema iwapo TIC haipewi nguvu kama yeye anavyotaka yupo tayari kituo cha uwekezaji kihamie katika ofisi yake lakini Waziri Mkuu naye amesema hayuko tayari kuona inaondoka kwake,"amesema.

Amefafanua pamoja na mafanikio ambayo yamepatikana TIC bado shida iko katika upatikaji huduma kwa wawekezaji na hiyo haiko kwao na tayari Waziri Mkuu amesema yupo tayari kukaa na wadau wengine kuweka mikakati itakayofaniksha wote kuzungumza lugha moja ya uwekezaji.

Mwambe amesema kila taasisi ijitoe kwa ajili ya maendeleo ya nchi na hivyo wanatoa ahadi kwa Rais kuwa wataendelea kupambana na kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Tano iweze kutimia katika kufanikisha uwekezaji nchini.

Kuhusu kufungiwa kwa wafanyabiashara na viwanda kwasababu ya kudaiwa kodi au vibali vingine kwa wawekezaji, Mwambe ametoa ushauri badala ya kufungia ni vema hiyo ikawa hatua ya mwisho kabisa kwani madhara yake ni mengi kuliko faida.

 " Ni vema taasisi nyingine zifahamu kufunga biashara za watu na kufunga kiwanda ni kuongeza hasara na iwapo kuna ulazima wa kufunga basi iwe hatua ya mwisho. Hivyo hakuna saabu ya kufunga biashara zipo njia nyingi za kufanya na biashara zikaendelea Unapofunga biashara kwa sababu ya kudai kodi , ukweli hutapata hiyo kodi na hakutakuwa na biashara,"amesema.

Amefafanua yeye ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na katika vikao vya bodi  wamekuwa wakijadili kuhusu namna bora ya kudai kodi na wamekuwa wakikataa kufungia biashara na akaunti za wafanyabiashara.

"Mkurugenzi Mkuu wa TRA mara kadhaa amekuwa akieleza kufunga akaunti ni mchakato mgumu na sio kazi rahisi  na pale ambapo kutakuwa na kesi maalum kuna taratibu za kuafuatwa,"amesema Mwambe.

Amesisitiza "Kuna wimbi la watumishi wa TRA kwenda kufunga biashara za watu jambo ambalo si sawa. Kuna biashara ambazo kodi wanalipa kila siku,hivyo kufunga biashara maana yake TRA haitapata kodi na deni halitalipwa.Ninaumia sana ninapoona yale ambayo tunayazungumza kwenye bodi hayapo kwa watumishi wengine".

Wakati huo huo amesema ni wakati muafaka kwa kila taasisi kuhakikisha inafanya kazi kwa bidii ili kuondoa malalamiko yanayotolewa na wawekezaji nchini na iwe mwisho kuendelea kusikia malalamiko yakitolewa.

Pia Mwambe amesema Rais Magufuli amekuwa akishangazwa na idadi ndogo ya walipaji kado ambayo ni milioni mbili wakati kuna Watanzania zaidi ya milioni 50, hivyo ni wajibu wao kuhamasisha uwekezaji na hatimaye kuongeza idadi ya walipa kodi.

Mwambe pia amesema wanamshukuru Rais kwa kuwapa Jengo jipya lililopo pembeni mwa Jengo la ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuwa makao makuu ya TIC na hivyo watahamia katika ofisi hizo siku za karibuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geoffrey Mwambe akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu jitihada za kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Geoffrey Mwambe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia namna ambavyo Rais Dk.John Magufuli ambavyo amekuwa karibu na kituo hicho ili kitekeleze vema majukumu yake.
 Mkurugenzi Mtendaji was Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)Geoffrey Mwambe (wa kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo Aprili 25,2019

VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

NYOTA wa muziki kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva Said Juma a.k.a Chege amewapa zawadi mashabiki wake kwa kuipua wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Njegeka ambayo amemshirikisha Vanessa Mdee.

Akipiga stori ya Michuzi Blog jijini Dar es Salaam Chege amesema kibao hicho ambacho tayari kina video yake amesema ameamu kumshirikisha Mdee ili kuleta ladha hasa kwa kuzingatia ni mwanadada mwenye kipaji cha hali ya juu katika muziki.

"Nimekuwa nikitamani kufanya kazi na Vanessa Mdee zaidi ya miaka mitatu iliyopita lakini sasa nimefanikiwa kumshirikisha kwenye wimbo wangu mpya.Vanesa ni msanii wa kipekee na tofauti kutokana na kujitoa kwake kwenye ngoma pale anaposhirikishwa, kushauri ,ikiwezekana hata kuongeza baadhi ya vionjo na kuifanya kazi ikapendwa,"amesema.

Ameongeza mashabiki wataona ngoma yake Njegeka ilivyokuwa tofauti na ya kipekee na kwamba Njegeka maana yake ni mapenzi yasioeleweka yani ya kudanganyana.

Akizungumzia Meneja anayemsimamia kwenye shughuli zake za muziki, Chege amesema bado yupo kwenye mikono ya Meneja Said Fella lakini kwa sasa kutokana na majukumu ya kijamii inamlazimu asionekane nae kwenye mizunguko yake katika kazi za sanaa.

Wakati huo huo amesema kuwa mitandao ya kijamii ni sehemu kubwa ya kufahamiana na mashabiki wake kwani amekuwa akijifunza mengi na kujua mashabiki wake wanahitaji nini kutoka kwake.

RAIS DKT. MAGUFULI NA RAIS PROF.MUTHARIKA WAZINDUA MSIMU WA SOKO LA TUMBAKU KANENGO - LILONGWE NCHINI MALAWI.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tumbaku ambayo ipo tayari kwa kuuzwa alipotembelea pamoja na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe kabla ya kuzindua rasmi msimu wa Soko la biashara  Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.
 Tumbaku ambayo ipo tayari kwa kuuzwa katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe 
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akikagua Tumbaku ambayo ipo tayari kwa kuuzwa alipotembelea katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe kabla ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika kuzindua rasmi msimu wa Soko la biashara  Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishangiliwa na Wanawake wa Lilongwe waliojitokeza katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe kumlaki  mara baada ya kukagua Tumbaku ambayo ipo tayari kwa kuuzwa alipotembelea pamoja na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika kabla ya kuzindua rasmi msimu wa Soko la biashara  nchini Malawi.Aprili 25, 2019.

 Watanzania wanaoishi nchini Malawi wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kukagua Tumbaku alipotembelea katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe pamoja na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika kabla ya kuzindua rasmi msimu wa Soko la biashara  nchini Malawi.Aprili 25, 2019.



 Sehemu ya Wananchi wa Malawi wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli huku mmoja akionyesha Picha yake wakati wa Sherehe ya Uzinduzi wa msimu wa Soko la biashara ya Tumbaku katika shehere zilizofanyika  Kanengo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika,Mama Janeth Magufuli, Prof.Gertrude Mutharika Mke wa Rais wa Malawi huku wimbo wa Taifa wa Malawi Ukipigwa wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Msimu mpya wa Soko la Tumbaku zilizofanyika katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika sherehe ya Uzinduzi wa Soko la Msimu mpya wa biashara ya Tumbaku katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe nchini Malawi.Aprili 25, 2019.

 Sehemu ya Wananchi wa Malawi wakimshangilia kwa nyimbo  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe wa Sherehe ya Uzinduzi wa msimu wa Soko la biashara ya Tumbaku katika shehere zilizofanyika  Kanengo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa zawadi na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe kabla ya kuzindua rasmi msimu wa Soko la biashara  Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya kumkabidhi zawadi katika sherehe zilizofanyika Kanengo Jijini Lilongwe kabla ya kuzindua rasmi msimu wa Soko la biashara  Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika na wananchi wa Malawi  katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe kabla ya kuzindua rasmi msimu wa Soko la biashara  Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma pamoja na Mke wa Rais wa Malawi Prof.Grtrude Mutharika na Wanawake wa Malawi  katika eneo la Kanengo Jijini Lilongwe wakati wa sherehe za Uzinduzi wa msimu wa Soko la biashara  Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyeji wake na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania unapigwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu kabla ya kuanza safari ya kurejea Nchini Tanzania.Aprili 25, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride Lililoandaliwa na Jeshi la Malawi  kwaajili ya kumuuga katika  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu kabla ya kuanza safari ya kurejea Nchini Tanzania.Aprili 25, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyeji wake na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu kabla ya kuanza safari ya kurejea Nchini Tanzania. Aprili 25, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kumuaga Mwenyeji wake na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika  na Wananchi wa Malawi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu kabla ya kuanza safari ya kurejea Nchini Tanzania.Aprili 25, 2019.

Picha na Ikulu


RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI MBEYA NA KUWASALIMIA WAKAZI WA MBALIZI, NZOVWE, IYUNGA NA MAFIATI JIJINI MBEYA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili akitokea nchini Malawi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Mbeya waliofika katika uwanja wa ndege wa Songwe kumpokea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) aliyefika katika uwanja wa ndege wa Songwe kumpokea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mbalizi wakati akielekea Mbeya mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Mbalizi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.
Wananchi wa Mafiati jijini Mbeya wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika eneo hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) katika eneo la Mafiati mara baada ya kuhutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nzovwe mara baada ya kuwasili katika eneo hilo. PICHA NA IKULU.



WAFANYABIASHARA KIZIMBANI KWA TUHUMA YA KUJIPATIA ZAIDI YA SHILINGI 150 KWA NJIA YA UDANGANYIFU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
WAFANYABASHRA wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kula njama na kijipatia zaidi ya sh. Milioni 150 kwa njia ya udanganyifu .

Washtakiwa hao, Laurean Wambura (60) anaishi Mbezi Mshikamano na Allan Kwayu (25) wa Bunju Baharini wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando.

Imedaiwa, katika siku tofauti tofauti kati ya Oktoba 2018 na Februari 2019, jijini Dar es Salaam, washtakiwa walitenda kosa la kujipatia RedHawks kwa njia ya udanganyifu.

Katika shtaka la pili, imedaiwa kati ya Januari 29 na February 27 mwaka huu, katika benki ya Exim tawi la Samora Avenue, washtakiwa kwa nia ya kudanganya au kutapeli, walijipatia USD 66,000 ambazo ni sawa na Sh. 150,678000  kutoka kwenye Akaunti ya Apollo international.  Kwa kudanganya kuwa wangewauzia copper Cathodes huku wakijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kuwasilisha hati ya Mali isiyohamishika yenye thamani ya nusu ya fedha wanazodaiwa kutapeli.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu.

MKUU WA MKOA WA MTWARA AWATOA WANANCHI KUFUATIA KIMBUKA KENNETH

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa akizungumza pamoja na kuwatoa hofu wakazi wa mkoa huo na watanzania kwa ujumla juu ya hali ya uwepo wa kimbunga Kenneth kinachoelezwa kutokea katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo, wakati alipotembelea kwenye eneo la uwanja wa ndege wa mkoa huo na kuwatoa hofu juu ya taarifa zinazoenea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa hali siyo shwari, RC Byakanwa amesema hali ni shwari hadi hivi sasa siyo kama taarifa hizo zinavyoenezwa.(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU).
Wakazi mkoani Mtwara leo wakiyakimbia makazi yao na kukimbila shule ya msingi Tandika mkoani hapa eneo ambalo serikali ya mkoa wa mtwara imetangaza kuwa yatakuwa salama kwao hata kama kimbunga keneth kitatokea kwani madhara hayatakuwa makubwa kwao.

MKAZI WA TANGA ASHINDA AHATI NASIBU YA BIKO,AKABIDHIWA KITITA CHA MILIONI 10

TASAC YAONYA VYOMBO VYA MAJINI JUU YA KIMBUNGA KENNETH

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mhandisi Japhet Loisimaye akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Kimbunga Kenneth ambacho kimesogea ukanda wa Kusini mwa Bahari ya Hindi na kwamba maeneo ambayo yataathariwa ni Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Kisiwa cha Mafia.

Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)  limetoa tahadhari kwa Vyombo vya Majini kufuatia Kimbunga Kenneth kilichosogea ukanda wa Kusini mwa Bahari ya Hindi na kwamba  maeneo ambayo yataathariwa ni Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Kisiwa cha Mafia. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Japhet Loisimaye amesema Kimbunga hicho sio rafiki kwa Vyombo vya Majini kutokana na mawimbi yake kutembea kwa kasi ya KM 150 -      450 kwa Saa.

Mhandisi Loisimaye ametoa tahadhari kwa Vyombo vidogo vya Majini visiende majini, hata hivyo amesema Vyombo vikubwa  vichukue tahadhari kutokana Kimbunga hicho kutokana na kuwa na vifaa vyenye uwezo wakuchukua tahadhari ya haraka.

‘’Vyombo vinavyofanya safari za Dar es Salaam – Zanzibar au Zanzibar – Dar lazima kuwa makini nakuchukua tahadhari zaidi vikiwa majini lakini hata Vivuko vyetu lazima vichukue tahadhari’’, amesema Mhandisi Loisimaye 

Pia ameeleza kuwa kutokana na majukumu yao wanaowajibu wa kuhakikisha wanaotumia Vyombo vya usafiri wa majini wanakuwa salama na Rai kubwa Vyombo vidogo visiende kabisa majini.

WAFANYABIASHARA WAWALI KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SH.MILIONI 50 KWA NJIA YA UDANGANYIFU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jami

WAFANYABASHRA wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kula njama na kijipatia zaidi ya sh. Milioni 150 kwa njia ya udanganyifu .

Washtakiwa hao, Laurean Wambura (60) anaishi Mbezi Mshikamano na Allan Kwayu (25) wa Bunju Baharini wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando.

Imedaiwa, katika siku tofauti tofauti kati ya Oktoba 2018 na Februari 2019, jijini Dar es Salaam, washtakiwa walitenda kosa la kujipatia RedHawks kwa njia ya udanganyifu.

Katika shtaka la pili, imedaiwa kati ya Januari 29 na February 27 mwaka huu, katika benki ya Exim tawi la Samora Avenue, washtakiwa kwa nia ya kudanganya au kutapeli, walijipatia USD 66,000 ambazo ni sawa na Sh. 150,678000  kutoka kwenye Akaunti ya Apollo international.  Kwa kudanganya kuwa wangewauzia copper Cathodes huku wakijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kuwasilisha hati ya Mali isiyohamishika yenye thamani ya nusu ya fedha wanazodaiwa kutapeli. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu.

TCRA Kanda ya Mashariki yaendelea na utoaji wa elimu ya mawasiliano

$
0
0


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Kanda ya Mashariki ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) imeendelea kutoa elimu ya mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja kuwataka wananchi wasajili namba zao kwa kutumia alama za vidole.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyandira mkoani Morogoro Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa serikali imeshatangaza wananchi juu ya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole hivyo ni vyema wasajili kwani baada ya muda uliowekwa ukimalizika namba za simu zisizosajiliwa zitafungwa na watoa huduma.
Odiero amesema kuwa usajili huo ni usalama kwa mtumiaji wa mawasiliano ambapo kwa alama hizo hawawezi kuingiliana na mtu mwingine yeyote duniani.
Amesema kuwa wananchi watumie mawasiliano kwa mujibu wa sheria zilizopo bila na mtu atakaye kwenda kinyume na sheria zilizowekwa anaweza kufungwa jela au faini na wakati mwingine ni faini pamoja na kifungo kwa wakati mmoja.
Odiero amewasaa wananchi wa Nyandira kutumia simu kwa kutengeneza ajira kwani mawasiliano yanarahisha kufanya biashara na kuweza kujiingizia kipato.
Aidha amesema kuwa kitambulisho kinachotakiwa ni cha uraia /kitambulisho cha Taifa na serikali imetoa vitambulisho hivyo na inaendelea kutoa kwa wale wasiokuwa navyo wafuatilie mamlaka husika na kuweza kuwa navyo na hatimaye kujisajili namba za simu kwa alama za vidole.
Hata hivyo amesema kuwa mtu anaweza kuwa na laini moja au zaidi isipokuwa hawezi mtu kumiliki laini mbili kwa mtandao mmoja.
"Tumejipanga kuhakikisha wananchi wetu tunawafikia popote mlipo ili kuwapa elimu ya mawasiliano msiweze kupata changamoto katika kutumia mawasiliano hayo"amesema Odiero.
Katika utoaji wa elimu kwa wananchi kanda hiyo pia inatoa elimu kupitia vituo radio pamoja na Luninga ili kwa wale wasiweza kufika katika mihadhara hiyo kupata taarifa katika vyombo vya habari.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kanda hiyo katika kijiji cha Nyandira.
 Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Annastella Mchomvu akiwasikiliza wananchi wa Kijiji cha Nyandira wakati kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano katika kijiji hicho.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyandira wakati walipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano wa kijiji hicho
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akitoa kitabu cha muongozo kwa mwananchi wakati wa utoaji wa elimu ya mawasiliano  kwa kanda hiyo.
Wananchi wakiangalia vipepelushi mbalimbali wakati wa utoaji wa elimu kwa Kanda ya Mashariki ya TCRA
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akiwasomea wananchi juu matumizi ya mawasiliano kwa kuzingatia sheria na wataokiuka adhabu ambazo zimewekwa katika jarida hilo
 Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaolet Eseko akitoa maelezo kuhusiana na matumizi ya simu wakati kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano katika Kijiji cha Nyandira mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero na maafisa wa Kanda hiyo wakiwa katika kituo cha Radio cha Top Fm mkoani Morogoro kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano.
 Wananchi wa Nyandira wakipeana maelezo mara baada ya kupata elimu ya mawasiliano kutoka Kanda ya Mashariki ya TCRA

Vijana 200 kuhudhuria mkutano wenye mfumo kama Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Morogoro

$
0
0

ZAIDI ya vijana 200 kutoka nchini na nje ya nchi wanatarajia kuhudhuria mkutano mkubwa utakaoendeshwa kwa mfano wa mfumo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kisheria na kikanuni.

Mkutano huo utakaofanyika Morogoro unatambuliwa kimataifa kama Tanzania International Model United Nations (TIMUN) unajumuisha vijana kuanzia miaka 15-30.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari, mratibu wa tukio hilo Bw. Kelvin Edward alisema: “Nimefurahishwa sana kuona washiriki wengi wa tukio la mwaka huu wanataka kuhakikisha kwamba vijana wa leo na kesho wanawezeshwa . Nashukuru sana mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kuwezesha jukwaa la vijana kubadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu kufikia mwaka 2030. Katika mkutano huo vijana watapata nafasi ya kubadilisha mawazo  na kuelezea matumaini yao .”

Mkutano wa mwaka huu utazingatia zaidi kuangalia maendeleo endelevu (SDGs). majadiliano yatalenga zaidi ushiriki wa vijana katika kipengele cha tatu cha SDG kinachogusa Afya na ustawi; Kipengele cha nane kazi zenye staha na ukuaji wa uchumi; kipengele cha 13 mabadiliko ya tabia nchi na kipengele cha 16 cha amani, haki na taasisi zenye uwezo .

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa , Msemaji wa umoja huo kitaifa, Bi. Didi Nafisa  amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia vijana katika utekelezaji wa SDGs.  “Vijana wanafanya idadi kubwa  ya wananchi. Ni muhimu kwa wao kupewa taarifa na pia kuhusishwa na utekelezaji wa malengo ya  maendeleo endelevu hasa kwa sasa ambapo kinachoangaliwa zaidi ni matokeo.”

TIMUN  inaendeshwa na Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA), na hufanyika  kila mwaka kwa vijana kuletwa pamoja kutoka mataifa mbalimbali duniani .

Akizungumza na mwenyekiti wa YUNA Bw. Jolson Msaki amesema matukio  kama ya TIMUN yanaleta vijana karibu na Umoja wa Mataifa na kuongeza uwezo wa vijana kujadili masuala yanayogusa dunia na kupata fursa ya kutoa suluhu ya utekelezaji wa  SDGs .


Tukio la mwaka huu limedhaminiwa na Umoja wa Mataifa Dar es salaam, ofisi ya Waziri Mkuu, UNICEF, UNFPA, UNIC, Ubalozi wa Marekani, Pathfinder, Plan International na International Youth Foundation.
Mratibu wa TIMUN 2019, Kevin Edward (kulia) akitoa maelezo kuhusu namna vijana wanavyonufaika na Mkutano wa vijana unaoendeshwa kwa mfumo wa Mikutano ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa, nchini Bi Didi Nafisa.
Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi Didi Nafisa akielezea namna ambavyo vijana wanavyokutanishwa kujadili namna ya kutekeleza vipengele vya maendeleo endelevu (SDGs) kwa kuwasilisha hoja za kitaifa; na namna Umoja wa Mataifa unavyosaidia makundi ya vijana kufikia usitawi wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa YUNA Tanzania, Bw. Jolson Masaki (kushoto) akitoa ushuhuda namna TIMUN inavyosaidia vijana. TIMUN hufanyika mara moja kwa mwaka na hii ni TIMUN ya 22. Katika mkutano huo vijana hujadiliana kuhusu mambo mbalimbali ya duniani na kutoa nafasi ya kupata suluhu yenye ubunifu mkubwa.

JK katika Mkutano wa “Belt and Road Forum” mjini Beijing, China

$
0
0
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kulia) akiwa pamoja na Viongozi Wastaafu wenzake wakati Mkutano wa “Belt and Road Forum” unaofanyika mjini Beijing, China. kushoto kwake ni Mhe. Madhva Kumar Waziri Mkuu Mstaafu wa Nepal, kulia kwake Waziri Mkuu Mstaafu Japan Mhe. Yukio Hatoyama na Rais Mstaafu wa Ujerumani Mhe Christian Wulff.

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MIAKA 10 YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE (UCSAF)

$
0
0

Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Eng. Peter Ulanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo kuhusiana na maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo yanayofanyika jijini Dodoma yakibebwa na kauli mbiu ya "Mawasiliano kwa Wote ni Kichocheo cha Kuufikia Uchumi wa Kati".


MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE (UCSAF)


Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) unatarajia kufanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Maadhimisho hayo ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mfuko ni sehemu ya Utekelezaji wa Kauli Mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuufikia Uchumi wa Kati. Kauli mbiu katika maadhimisho haya ni Mawasiliano kwa Wote ni Kichocheo cha Kuufikia Uchumi wa Kati.


Maadhimisho haya yatafanyika hapa Dodoma kuanzia tarehe 27 Aprili hadi kilele chake tarehe 30 Aprili, 2019 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge).


Katika maadhimisho haya, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umeandaa shughuli mbalimbali katika kipindi cha muda wa maadhimisho, yakiwemo maonesho ya watoa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 27 Aprili hadi siku ya kilele tarehe 30 Aprili 2019. Mfuko unachukua fursa hii kuualika umma wa wananchi wa Jiji la Dodoma pamoja nanyi waandishi wa habari kuhudhuria maonesho hayo yatakayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (maarufu kama Nyerere Square) jijini Dodoma.


Sambamba na maonesho hayo, Mfuko utazindua Klabu za TEHAMA katika Shule za Sekondari za Dodoma pamoja na Msalato zilizoko Dodoma siku ya tarehe 28 April 2019. Aidha Mfuko utagawa Kompyuta kwa Wilaya ya Gairo pamoja na kuzindua mnara wa mawasiliano uliopo wilaya ya Bahi siku ya tarehe 29 Aprili 2019, ikiwa ni kielelezo cha miradi ambayo inatekelezwa maeneo mengi nchini Tanzania Bara na Visiwani.


Kwa miongo mingi Sekta ya Mawasiliano imekuwa ikikuwa kwa kasi ndogo katika nyanja zote za simu, posta na utangazaji. Mabadiliko ya Sekta ya Mawasiliano yalianza miaka ya 90 ambapo mfumo wa uendeshaji wa sekta ulibadilishwa na kuingiza uwepo wa wadhibiti wa sekta (Tume ya Mawasiliano na Tume ya Utangazaji) na kuanza kuingiza ushindani katika sekta ya mawasiliano.


Miaka 10 baadaye mabadiliko zaidi ya kisekta yalifanyika kwa kuunganisha Tume ya Mawasiliano na Tume ya Utangazaji na kuunda Mamlaka ya Mawasiliano mwaka 2003. Katika kuongeza ushindani katika soko la mawasiliano lilijitokeza ombwe katika muundo wa sekta katika ngazi ya kiutendaji. Ombwe hilo lilitokana na nguvu za ushindani kujikita kupeleka mawasiliano katika maeneo yenye mvuto wa kibiashara na kuyaacha maeneo ya vijijini na ya mijini yasio na mvuto wa kibiashara. 

Serikali ililiona hilo kuanzia mwaka 2003 mpaka mwaka 2006 ambapo sheria ya kuanzisha Mfuko Mahsusi kwa ajili ya Mawasiliano ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mfuko huo ulianzishwa kama taasisi ya serikali inayojitegemea chini ya Wizara inayohusika na mawasiliano.  Kanuni za kuanzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote zilisainiwa mwezi Aprili 2009.


Sekta ya Mawasiliano katika kipindi kirefu cha tabribani miaka 30 iliyopita imepitia mabadiliko makubwa sana ambapo sekta imetoka kwenye kuwa na kampuni moja ya umma kabla ya mwaka 1993 ambayo ilikuwa inatoa huduma za simu za mezani, posta na hata telegramu na telex mpaka kuwa na soko kubwa la ushindani lenye makampuni makubwa ya simu za mkononi.  Sekta ya mawasiliano imefaidi sana kwa uwepo wa mdhibiti wa mawasiliano aliyethabiti na kutoa mwongozo ambao umeifanya sekta ya mawasiliano kuwa sekta inayochangia maendeleo makubwa ya uchumi wa Tanzania.


Mabadiliko ya kisekta yaliyofanywa na Serikali mwaka 2005 yaliongeza kasi ya ushindani katika sekta ya mawasiliano na mabadiliko ya aina hiyo yalitokea kwenye sekta ya utangazaji na sekta ya posta. Kuongezeka kwa ushindani kulisababisha ushindani wa bei na kufanya gharama kuanza kupungua hata hivyo kutokana na hali hiyo watoa huduma walichelea kupeleka mawasiliano ya aina zote maeneo ambayo yataonekana kukosa mvuto wa kibiashara hasa maeneo ya vijijini.


Serikali ilianzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote mwaka 2006 na kusainiwa na Mheshimiwa Raisi mwaka 2007. Hata hivyo kanuni za kuanzisha Mfuko zilisainiwa Aprili 2009. Lengo kuu la kuanzishwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni kuhakikisha Mtanzania popote alipo ataweza kupata huduma za uhakika za mawasiliano iwe ni mawasiliano ya simu za mkononi, utangazaji, huduma za posta au intaneti. 


Toka kuanzishwa kwake Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umejikita kutambua mahitaji ya mawasiliano nchi nzima, kushirikisha wadau mbali mbali wa mawasiliano nchini, kushirikisha wananchi katika kutambua na kutatua kero za mawasiliano. Wakati Mfuko unaanza takriban asilimia 45 tu ya watanzania walikuwa wanaishi katika maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu. Mpaka tunavyoongea leo takriban asilimia 94 ya watanzania wanaishi kwenye maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu ambapo zaidi ya asilimia 70 ni watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu.  Asilimia 10 imechangiwa na Mfuko wa Mawasiliano.


       Imetolewa na

Eng. Peter Ulanga

Mtendaji Mkuu

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,530 KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 55 YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0
Katika kuadhimisha Miaka 55 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2019 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-

(i)Wafungwa wote wapunguziwe robo (1/4) ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58, wafungwa hao  sharti wawe wametumikia robo (1/4) ya adhabu zao gerezani isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i – xxi).

(ii)Wafungwa walioingia gerezani kabla ya tarehe 15 Machi, 2019.

(iii)Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Saratani (Cancer) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa hawa wathibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

(iv)Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi.  Umri huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

(v)Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

(vi)Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability). Ulemavu huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

2.Aidha, Msamaha wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:- 

(i)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa au kwa makosa ya kujaribu kuua, kujaribu kujiua au kuua watoto wachanga (attempt to murder, attempt suicide or infanticide).
(ii)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.

(iii)Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

(iv)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhangi n.k.

(v)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji na upokeaji au utoaji rushwa.

(vi)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempted robbery).

(vii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (fire arms, ammunitions and explosives).

(viii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti, ukatili dhidi ya watoto au kujaribu kutenda makosa hayo.

(ix)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

(x)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki, uharibifu wa miundombinu au kujaribu kutenda makosa hayo.

(xi)Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994), Sheria ya Huduma kwa Jamii (Act. No. 6/2002) na Kifungo cha Nje {The Prisons (Extra Mural Penal Employment) Regulation}.

(xii)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao, utakatishaji fedha  na kuhujumu uchumi.

(xiii)Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mhe. Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki. 

(xiv)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.

(xv)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, ukatili dhidi ya watoto, kupoka na kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking).

(xvi)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.

(xvii)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na nyara za Serikali na ujangili (poachers).

(xviii)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali.

(xix)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali au kusaidia kutendeka kwa makosa hayo na bado wangali wanatumika adhabu hizo.

(xx)Wafungwa waliowahi kufungwa gerezani (warudiaji) na wale wenye makosa ya kinidhamu gerezani.

3.Wafungwa 3,530 watafaidika na Msamaha huu ambapo 722 wataachiliwa huru tarehe 26 Aprili, 2019 na 2,808 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu. Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

Meja Jenerali Jacob G. Kingu, ndc
KATIBU MKUU.

Achomwa Kisu Tumboni Kisa Wivu Wa Kimapenzi

$
0
0
Binti mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Wilaya ya Urambo amejeruhiwa vibaya sehemu ya Tumboni baada ya Kuchomwa Kisu na Msichana mwenzake Chanzo ikiwa ni Wivu wa mapenzi 


Tukio hili limetokea katika mnada wa kitongoji cha mwenge kata ya Urambo mjini likimuhusisha mmoja anayetajwa kwa jina la Kalunde Madua mwenye Umri wa miaka 20 baada ya kumchoma mwenzake Joyce Isaya kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi na kumshuku kuwa anatoka na mvulana wake 

Baada ya tukio hilo Kalunde alishambuliwa na Wananchi waliokuwepp kwenye eneo hilo na kupelekwa kituo cha polisi huku Joyce akikimbizwa Hospitali  ya Wilaya ya Urambo

Kwa mujibu wa Mama yake mzazi na Joyce bi. Cesilia Mathias alipozungumza na Michuzi Blog akiwa katika hodi aliyolazwa Mwanae Joyce amesema

"Ugomvi baina ya binti yangu Joyce na Kalunde ulianza zamani Licha ya wazazi na Majirani Kujaribu kuwakalisha kikao cha kuwasuluhisha Lakini bado wameendelea kuhitalafiana mara kadhaa 

Mganga Mkuu Wa Wilaya Ya Urambo Paul Swakala amekili kumpokea Mgonjwa huyo na kuongeza kuwa 

"Baada ya kuwa amechomwa Kisu sehemu ya kushoto ya tumbo kwa baahati nzuri Kisu hakikuweza kuingia ndani hivyo anaendelea na matibabu mpaka sasa  tunaendelea na uchunguzi wa kina kuhakikisha anapata nafuu na bado yupo chini ya uangalizi wa Hospitali "Amesema Swakala

Naye Mwenyekiti wa kitongoji cha msufini kata ya Kapilula Bw. Lameck Zakayo ameiomba Serikali kumchukulia hatua kali za kisheria na watu wenye tabia kama  hizo 

Hata hivyo kwa mujibu wa Daktari Swakala amesema binti huyo aliyejeruhiwa atapatiwa ruhusa hivi karibuni kutokana na majereha yake kutokuwa ya kutisha na kwa upande wa Kalunde bado anashikiliwa na jeshi la polisi.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images