Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

USAFIRISHAJI WA MKAA

$
0
0
Mmoja waendesha Pikipiki katika kata ya Mwandege Wilaya ya Temeke mkoani Pwani akiwa amepakia Mzigo wa Mkaa kuzidi uwezo wa chombo chake akiwa hajavaa kofia ngumu akipita katika Barabara ya Kilwa kuelekea Dar es Salaam, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wake.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Wasafirishaji wa Mkaa kwa kutumia pikipiki wakikatiza katika viunga vya Mwandege.

TAHADHARI KUTOKA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI KUHUSU KIMBUNGA KENNETH

$
0
0
Kutokana na utabiri uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuhusu kutokea kwa Kimbunga kikali (KENNETH) na mvua kubwa leo tarehe 25 Aprili 2019 kitakachoathiri maeneo ya Pwani ya Kusini mwa nchi na kusababisha madhara mbalimbali. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatoa rai kwa Wananchi wote waishio katika maeneo hatarishi, maeneo yaliyopo pembezoni mwa bahari na kandokando ya Mito, kuchukua tahadhari katika kipindi hiki kwa kuyahama maeneo hayo haraka.

Wananchi wanatahadharishwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki na kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania na kusikiliza vyombo vya habari pamoja na kuzingatia tahadhari zinazotolewa, ushauri na miongozo ya kitaalam ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Tuchukue tahadhari kwa kuepuka kukaa au kuegesha vyombo vya Usafiri na Usafirishaji chini ya miti mikubwa, maana matawi au mti vyaweza kuangukia chombo na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mali hata kudhuru Maisha.

Kutokana na Kimbunga hiki kikali kinachoambatana na mvua kubwa kuna uwezekano wa mawe makubwa au udongo kuporomoka kutoka milimani au miti kuanguka na kuziba barabara, hivyo madereva wanapaswa kuwa makini kwa kuendesha vyombo kwa mwendo unaokubalika ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limejipanga na liko imara kuhakikisha linatoa huduma bora, sahihi na kwa wakati.

Imetolewa na;
Billy Mwakatage
Kamishna wa Operesheni
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

TCRA CCC YAWATOA HOFU WATUMIAJI WA SIMU ZA MKONONI

MNYETI AWASHUKIA VIKALI WANASIASA SIMANJIRO

$
0
0
Na Joseph Lyimo, Globu ya Jamii-Manyara.

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewashukia vikali wanasiasa nane wa Kata ya Kitwai Wilayani Simanjiro wanaorudisha nyuma maendeleo kwa kukataza wanafunzi wasisome kwenye madarasa ya shule ya msingi Kitwai B yaliyojengwa na mdau wa maendeleo hivyo kuyasusia.

Akizungumza wakati akizindua madarasa matatu mapya ya shule hiyo, Mnyeti alisema wanasiasa hao atawachukulia hatua kali wanaoshawishi wananchi kususia maendeleo.

Alisema hatakubali kuona watu wachache wanaopinga maendeleo, hivyo serikali itamuunga mkono mdau huyo wa maendeleo Sanare Mollel ambaye pia ana mpango wa kumalizia majengo ya zahanati ya kijiji hicho.

"Wanasiasa hao wanampinga mdau huyo kwa sababu ni mfugaji mkubwa ambaye amefuata taratibu na kanuni zote za kuingia ndani ya kijiji hicho lakini hajavunja sheria kwani mtanzania anaruhusiwa kuishi popote," alisema Mnyeti.

Alisema haiwezekani mdau wa maendeleo Sanare Mollel ajitolee kujenga madarasa matatu kisha baadhi ya wanasiasa wanawaambia wananchi wasisomeshe watoto.

Diwani wa kata hiyo Nyika Shawishi alisema wapinzani wake wa kisiasa ndiyo wanaosababisha hali hiyo kwani wanaona maendeleo yakifanyika sifa zitakuwa kwake.

"Maboma matano yanayoongozwa na viongozi niliowashinda kwenye uchaguzi uliopita ndiyo wanasababisha uchochezi wa kugomea maendeleo," alisema Shawishi.

Ofisa elimu msingi wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Silvanus Tairo alisema shule hiyo imegharimu sh47.3 milioni ambapo mdau wa maendeleo alijitolea sh30 milioni na nguvu za wananchi zimegharimu sh12.3 milioni.

Tairo alisema jamii ya eneo hilo bado haioni elimu ni muhimu ndiyo sababu wanawasikiliza wanasiasa wenye kuwachochea wakatae maendeleo kutokana na ufinyu wa uelewa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizindua madarasa matatu ya shule ya msingi Kitwai B Wilayani Simanjiro iliyojengwa na mdau wa maendeleo Sanare Mollel.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akiwa na mavazi ya jadi aliyovishwa na wazee wa kimila wa kimasai wa Kijiji cha Irkujit Kata ya Edonyongijape Wilayani Simanjiro, baada ya kuendesha harambee ya papo kwa papo na kupatikana shilingi milioni 17 za ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kwenye kijiji cha Irkujit Kata ya Edonyongijape.

TEMESA YAFUNGA TAA KUZUNGUKA UKUTA WA MACHIMBO YA MERERANI

$
0
0
Muonekano wa taa ambazo zimefungwa katika ukuta uliozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la Mererani, Wilayani Simanjiro mkoani Arusha. Mradi huo umesimamiwa na Mameneja Wakala wa Ufundi na Umeme nchini TEMESA kutoka mikoa ya Dodoma, Arusha pamoja na Kilimanjaro.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kushoto akikagua mojawapo ya taa ambazo zimefungwa na Wakala huo katika ukuta uliozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la Mererani, Wilayani Simanjiro mkoani Arusha.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kushoto akitoa maagizo kwa mameneja wa Wakala huo ambao wameshirikiana kusimamia ufungaji wa taa katika ukuta uliozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la Mererani, wilayani Simanjiro mkoani Arusha. Kutoka kushoto ni Meneja mkoa wa Arusha Mhandisi Heriel Mteri, Meneja wa Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo, pamoja na Meneja mkoa wa Dodoma Mhandisi Liberatus Bikulamchi (wa kwanza kulia).
Muonekano wa taa ambazo zimefungwa katika ukuta uliozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la Mererani, Wilayani Simanjiro mkoani Arusha. Mradi huo umesimamiwa kwa pamoja na Mameneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kutoka mikoa ya Dodoma, Arusha pamoja na Kilimanjaro.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa nne kushoto pamoja na mameneja wakikagua kazi ya ufungaji wa taa katika ukuta uliozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la Mererani, Wilayani Simanjiro mkoani Arusha. Mradi huo umesimamiwa na meneja wa Wakala huo kutoka mikoa ya Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo (wa pili kushoto), meneja wa Arusha Mhandisi Heriel Mteri (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja wa mkoa wa Dodoma Mhandisi Liberatus Bikulamchi (wa tatu kulia).

INTRODUCING "I Don't Care" By Lady Jaydee

NEWZ ALERT: WANANCHI WAKUSANYIKA UWANJA WA NDEGE MTWARA KUCHUKUA TAHADHARI YA KIMBUNGA KENETH,WAOMBWA KUJIORODHSESHA KWENYE KITABU CHA KUMBUKUMBU

$
0
0
Na Joseph Mpangala-Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evodius Mmanda amewataka Mananchi waliofika eneo la Uwanja wa Ndege Mkoani Mtwara kwa ajili ya kujihifadhi kuhakikisha wanajiorodhesha katika kitabu cha Kumbukumbu ili kuepuka kupoteana.

Mmanda ameyasema hayo wakati akitembelea maeneo maalum  yaliyotengwa kwa ajili ya kujihifadhi kufuatia tahadhali iliyototelewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA ya kuwepo kwa Kimbunga Keneth ambacho kilitabiriwa kutokea Alhamis Wiki Hii.

Aidha Mmanda amewaomba wananchi hao kuwapa taarifa wenzao ambao wamekaidi kuondoka majumbani mwao na kuelekea maeneo yaliyotajwa.

Maeneo yaliyoandaliwa kwa Mwananchi kujihifadhi ni Shule ya Mitengo,Sabasaba,Uwanja wa Ndege,Naliendele pamoja na Shule ya sekondari ya Sabodo.

Wafanyakazi wa Serikali pamoja na wanafunzi wameagizwa kutokwenda kutokana na Utabiri wa Uwepo wa Kimbunga Keneth siku ya alhamis.
 Baadhi ya Wananchii wamekusanyika katika Eneo la Uwanja wa Ndege Mkoani Mtwara kwa Tahadhari ya kujilinda na Kimbunga Kenneth kilichotabiriwa kutokea Leo na Mamlaka ya Hali ha Hewa Tanzania TMA.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini Mh.Evodius Mmanda  akizungumza na baadhi ya Wananchi waliokusanyika katika uwanja wa ndege  Mkoani Mtwara kwa tahadhari ya kujilinda na Kimbunga Kenneth kilichotabiriwa kutokea leo na Mamlaka ya Hali ha Hewa Tanzania TMA.
 Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika kwa pamoja 

MAHAKAMA YAMTEUA KABIDHI WASII MKUU KUWA MSIMAMIZI WA MIRATHI YA MAREHEMU MTUI

$
0
0
MAHAKAMA ya Mwanzo ya Maji ya Chai wilayani Arumeru,mkoani Arusha imemteua Kabidhi Wasii Mkuu,kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Anderson Mtui na kumpa muda wa miezi minne kutambua,kukusanya na kugawanya mali za marehemu kwa warithi stahiki.

Baada ya mgao huo atatakiwa  kupeleka taarifa ya mgawanyo na hesabu mahakamani hapo.Aidha Mahakama hiyo imemvua usimamizi wa mirathi,Aunieli Mtui baada ya kuandika jina marehemu(baba yake mzazi),Anderson Mtui,kama moja ya mashahidi wake waliofika mahakamani hapo wakati wa kufungua mirathi.

Katika shauri hilo la mirathi namba 39 la mwaka 2008,waombaji Royson Mtui na Rehema Mtui,ambao pia ni watoto wa marehemu waliiomba  Mahakama hiyo imtengue Aunieli  kuwa Msimamizi wa mirathi ya marehemu Anderson Mtui kwa madai kuwa msimamizi huyo siyo muaminifu kufanya kazi hiyo.

Akitoa hukumu hiyo juzi,Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Rweyemamu Kashero,alisema Mahakama hiyo imeamua kumteua Kabidhi Wasii Mkuu huyo baada ya Aunieli kuonesha taswira mbaya ya kushindwa kusimamia na kugawa kwa usawa mali za marehemu.

Alisema baada kwa kuzingatia wingi na thamani ya mali za marehemu,Mahakama hiyo inamteua Kabidhi Wasii Mkuu huyo kuwa msimamizi na kugawanya mali hizo ili mirathi hiyo ili iweze kufungwa.

Aidha baada ya Mahakama hiyo kumtengua msimamizi wa awali ya mirathi hiyo, ilimwagiza msimamizi huyo(Aunieli),kurudisha nyaraka zote alizopewa na Mahakama hiyo kuhusiana na mirathi hiyo ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

"Kwa kuzingatia kwamba marehemu alikuwa amezaa watoto wake na wamama wanne tofauti na msuguano uliopo katika familia hii ambao unathibitishwa na shauri hili,ni vigumu kumpata msimamizi wa miirathi asiyekuwa na upande katika  familia hii,si tu kwamba haki itendeke bali ionekane kuwa imetendeka namteua Kabidhi Wasii Mkuu kuwa msimamizi wa mirathi hii,"alisema.

Alisema Mahakama imefikia uamuzi hul baada ya kusikiliza hoja za mashahidi  wa pande zote ambapo mahakama iliona msimamizi wa mirathi hakuwa sahihi kwani alitumia majina ya marehemu kama shahidi wakati wa kufungua mirathi.

"Kwa namna yoyote ile marehemu asingeweza kufufuka na kuja kutoa ushahidi katika mirathi yake mwenyewe,"alisema Hakimu huyo

Hakimu Kashero alitaja sababu za kumtengua msimamizi huyo ni pamoja na kwenda tofauti na mashahidi wake kuhusiana na baadhi ya mali za marehemu pamoja na msimamizi huyo  kufanya  kinyume na masharti ya usimamizi wake kwa makusudi ikiwemo kushindwa kuwa msimamizi na kumkasimisha mama yake ambaye ni mke mkubwa kuwa msimamizi wa mali hizo.

Hakimu huyo akirejea ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo,alisema mahakama imebaini msimamizi wa awali alichanganya mali ambazo hazikuwa za marehemu,ambapo mali hizo marehemu alizigawa kabla ya kifo chake.

Hakimu Kashore alisema suala la msimamizi kujiamulia mali zote ni za mama yake kwa kigezo kuwa ni mke wa marehemu hivyo mali hizo walizitafuta wote siyo sawa kwa sababu suala lililopo mbele ya mahakama hiyo ni la mirathi halipaswi kuchanganywa na suala la ndoa.

"Kwa kuzingatia kwamba marehemu alikuwa amezaa watoto 14 na wamama wanne tofauti,kwa kusingatia msuguano uliopo katika familia hii ambao unathibitishwa na shauri hili,ni vigumu kumpata msimamizi wa mirathi asiyekuwa na upande katika familia hii,"alisema na kuongeza

"Kwa kuzingatia wingi na thamani ya mali za marehemu mahakama hii inamteua Kabidhi Wasii Mkuu kuwa msimamizi wa mirathi kuanzia leo na kumpa muda wa miezi minne kutambua,kukusanya na kugawanya mali za marehemu kwa mujibu wa sheria kwa warithi stahiki na kuleta taarifa ya mgawanyona hesabu ili mirathi hii ifungwe,"

Awali waombaji hao waliiomba Mahakama imtengue kuwa msimamizi wa mirathi kwa madai kuwa hakutenda haki,hajawahi kuwaonyesha mali zao huku akigawa mali kwa kuwapendelea watoto wa familia ya mke mkubwa ambaye ana wa watoto saba na kuwabagua watoto wengine saba waliozaliwa na mama watatu tofauti.

Vodacom yawadatisha wateja wake na data

$
0
0


 Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa (Mbele) akizungumza na wananchi wakati wa uzindunzuzi wa kampeni ya Data Datani iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti. 
 Wasanii wakitumbuiza katika uzinduzi wa kampeni ya Data Datani iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti. 


 Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa  (wapili kulia) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifurahia uzinduzi wa kampeni ya Data Datani, iliyofanyika viwanja vya Mbagala Zackiem hapo jana. Data Datani ni huduma inayowezesha wateja wa Vodacom kupata Mb hadi mara mbili zaidi ya kiwango walichonunua kila wanunuapo bando la intaneti.  



Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc, leo imezindua kampeni kabambe ya data iitwayo “Data Datani’ ambayo inawezesha wateja wake kupata bonus Mb hadi mara mbili zaidi kila wanunuapo bando la intaneti. Kampeni hiyo imezinduliwa katika viwanja vya Mbagala Zackhem jijini Dar es Salaam.

Kampeni ya Data datani inalenga kuwawezesha watumiaji wa intanet kufaidi zaidi matumizi ya vifurushi vyao na pia kuwajuza mbinu mbali mbali za kutunza data isiishe kwa haraka, jambo ambalo limekuwa likiwatatiza wateja wake kwa muda mrefu.

Ili kupata ofa hii, wateja wa Vodacom Tanzania Plc wanatakiwa kupiga *149*01# kisha chagua intaneti, halafu chagua intaneti bando kisha nunua kifurushi, hii itakuwezesha kupata hadi mara mbili ya bando uliyonunua awali kwa bei ile ile.

Katika Uzinduzi wa kampeni hiyo kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa alitilia mkazo umuhimu wa data katika maisha ya kila siku. “Tukiwa ni Kampuni inayoongoza nchini kwa kutoa intaneti yenye kasi zaidi nchini, ni muhimu kuzingatia pande zote mbili za sarafu, yaani huduma na wateja wetu. Ndio maana tumeleta kampeni hii ili kuwawezesha wateja wetu kupata zaidi ya kile walicholipia kila wanaponunua bando la data,” alisema Linda huku akiongeza kwamba wanafahamu umuhimu wa data hasa katika zama hizi za kidijitali, habari zote na biashara ziko mitandaoni, hivyo wasingependa ukosefu wa data uwe kikwazo kwa wateja wao katika kufanikisha shughuli zao za kila siku.

Mwaka 2017 Kampuni ya Vodacom Tanzania ilizindua mtandao wa 4G katika mkoa wa Dar es Salaam ili kuwawezesha wateja wake kupata intaneti yenye kasi zaidi, na mpaka sasa mtandao huu wa 4G umesambaa kufikia mikoa 24.

Mfanyabiashara na mkaazi wa Mbagala Justin Joseph aliyehudhuria uzinduzi huu nae alisema, “Sasa ni wakati wa kudata datani, internet sio tu teknolojia bali pia ni kiuwezeshaji. Inatuwezesha kupata habari haraka, inatuwezesha kufanya biashara za mtandaoni, inawezesha serikali kupata kipato na kuwezesha shughuli za kijamii, yani kudata, ni zaidi ya data tu”.

Kampeni hii inalenga kuwezesha wateja kutumia data zaidi na kikamilifu kwa shughuli zao zote za mtandaoni bila kuwa na wasiwasi wa data kuisha.

Ili mteja aweze kufurahia huduma hii anapaswa kununua kifurushi kupitia mfumo wowote iwe ni M-Pesa, vocha, My Voda App, na ataweza kuperuzi habari, kuangalia video, kusikiliza muziki au kununua bidhaa mtandaoni. Changamkia fursa hii kwa kubofya *149*01, pata kifurushi chako cha intaneti uendelee kudata datani.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA TAHADHARI NCHINI KUHUSU KIMBUNGA KENNETH

LUKUVI ATATUA MGOGORO WA WAFUGAJI WA KIMASAI NA WAWEKEZAJI MONDULI

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemaliza mgogoro uliodumukwa muda mrefu baina ya wananchi wa vijiji vya Lengiloriti na Naalarami vilivyopo wilayani Monduli mkoani Arusha na wawekezaji wa mashamba yanayomilikiwa na TANFOAM na SLUIS kwa kuamua kumega sehemu za mashamba na kuwapatia wananchi wa vijiji hivyo.

Lukuvi alifikia umauzi huo baada ya kukutana na pande zote mbili tarehe 23 Aprili 2019 wilayani humo na kujadiliana kwa kina kwa takriban saa tano kwa lengo la kupata suluhu ya mgogoro huo ambao umeleta sintofahamu kati ya wananchi wa vijiji hivyo na wawekezaji wa mashamba.

Katika makubaliano hayo iliamuliwa ekari kati ya 850 hadi 900 zimegwe kutoka kwa muwekezaji TANFOAM na kugawiwa kwa kijiji cha Lengiloriti wilayani Monduli kutoka shamba namba 44 lenye ukubwa wa ekari 3098. Aidha, upande wa muwekezaji SLUIS jumla ya ekari 2000 za muwekezaji zimetolewa kwa kijiji cha Naaralami, NAFCO, Lokisari na Tukusi ambapo sasa muwekezaji atabaki na aekari 2217 badala ya 4,217 alizokuwa nazo awali.

Kwa mujibu wa Lukuvi, ardhi iliyomegwa na kurudishwa katika vijiji hivyo itakuwa chini ya mamlaka ya kijiji ambacho ndicho kitakuwa na jukumu la kuigawa upya kwa wananchi wa vijiji husika na baadaye kupangwa matumizi bora ya ardhi.

Akizungumzia kijiji cha Lengiloriti, Waziri wa Ardhi aliwataka wananchi wenye Maboma yaliyokuwa ndani ya eneo la shamba la muwekezaji TANFOAM kuhamia eneo jipya walilotengewa katika kipindi cha miezi mitatu ili kupisha muwekezaji kuendelea na shughuli za kilimo na kutotekelezwa kwa aina yoyote agizo hilo kutaifanya serikali kuchukua hatua.

Aidha, ameagiza kuanzia wiki hii timu ya upimaji ardhi mkoani Arusha iende ktika eneo hilo kwa ajili ya kuweka mipaka/alama za kudumu ili kuepuka uvamizi mwingine unaoweza kutokea na kuagiza wawekezaji na wananchi wa vijiji vilivyopatiwa ekari hizo kuchangia fedha kwa ajili ya upimaji ambapo muwekezaji na wananchi walikubali kutoa milioni tano kwa ajili ya upimaji.

Kuhusu mgogoro wa muwekezaji SLUIS, Lukuvi alisema muwekezaji huyo amekubali kutoa ekari 520 kwa kijiji cha Naaralami pamoja na ekari 300 kwa ajili ya kupitishia mifugo ya wananchi wa kijiji hicho huku ekari 513 zikitolewa kwa NAFCO, 366 kwa Lokisari na ekari 301 kwa kijiji cha Tukusi.

Lukuvi alisema serikali inawaeshimu sana wawekezaji wa sekta ya ardhi kwa kuwa wanalipa kodi inayosadia utoaji wa huduma za jamii huku wananchi nao wakipata ajira na kusisisitiza kuwa wawekezaji wanaomiliki mashamba kisheria serikali itawalinda na kuonya baadhi ya viongozi wa vijiji kujigawia maeneo bila ya kushirikisha wananchi wa vijiji husika.

‘’Nimekuja kusuluhisha mgogoro siyo kunyanganya wawekezaji mashamba, wawekezaji wamekubali kupunguza mashamba yao na hayo mashamba siyo mali ya wananchi wanaoishi katika maboma yaliyohamishwa bali ni mali ya kijiji ambacho kitakuwa na jukumu la kugawa maeneo hayo’’ alisema Lukuvi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa, baada ya makubaliano ya pande zote mbili anategemea kila upande utaheshimu maamuzi yaliyotolewa na mtu yoyote atakayekiuka basi serikali ya mkoa itachukua hatua kali dhidi yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanfoam Riaz Lemtula amepongeza jitihada iliyofanywa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi mpaka kufikia muafaka wa suala hilo na kuahidi kutekeleza makubaliano waliyoafikiana kwa lengo la kuleta maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai alimshukuru Waziri wa Ardhi kwa niaba ya Kijiji chake kwa kazi anayoifanya ya kutatua migogoro ya ardhi na kuahidi kushirikiana na wawekezaji waiokubali kumega maeneo yao kwa ajili ya kijiji.

Wawekezaji wanaomili mashamba katika vijiji hivyo wamekuwa wakiendesha mashamba yao katika shughuli za kilimo ambapo hulima mazoa ya Maharage, Mtama, Ngwara na mahindi na kusafirisha mazo hao katika nchi za Sweden, Canada na Uholanzi.

WASAFIRISHAJI MKAA WAKIWA KAZINI

$
0
0
Mmoja waendesha Pikipiki katika kata ya Mwandege Wilaya ya Temeke mkoani Pwani akiwa amepakia Mzigo wa Mkaa kuzidi uwezo wa chombo chake akiwa hawajavaa kofia ngumu akipita katika Barabara ya Kilwa kuelekea Dar es Salaam, jambo ambalo ni hatarisha kwa usalama wake.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV).
Wasafirishaji wa mkaa kwa kutumia pikipiki wakikatiza katika viunga vya Mwandege.

ABDALLAH GAMA MWENYE HISTORIA NDEFU KATIKA MUZIKI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
Nina uhakika wale mashabiki wa bendi DDC Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde’ Ngoma ya Ukae’ wakati huo ambao walikuwa vijana wa zamani, watakuwa wanakumbuka mbali kila pale linapotajwa jina la mwanamuziki Abdallah Gama.

Gama ni mkung’utaji mahiri wa gitaa la kati, Rhythm, aliyepata kusumbua akili za wapigaji magitaa wengine wengi enzi zile, hususani alipokuwa katika bendi hiyo ya Sikinde.

Nguli huyo ni mmoja miongoni mwa wanamuziki 12 ambao mwaka 1978 walijiengua kwenye kundi la Dar International kwa madai ya kupinga uongozi mbovu wa mmiliki wao, Zachariah Ndabameiye na kuanzisha bendi ya Mlimani Park Orchestra.

Waliondoka kwa madai ya kupinga uongozi uliokuwa mbovu wa mmiliki wao, ambapo imeelzwa kuwa baada ya kujiengua walikwenda kuungana na wanamuziki wengine akina Abel Bartazal, George Kessy, Haruna Lwali na Ibrahim Mwinchande na kuwa waanzilishi wa bendi ya Mlimani Park Orchestra.

Baadhi ya wanamuziki wengine waliochomoka Dar International na kwenda kuanzisha bendi hiyo walikuwa ni Michael Enock, aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote za muziki, Cosmas Chidumule, Abel Bartazal, Joseph Mulenga’King Spoiler’, George Kessy na Machaku Salum. Wengine ni Haruna Lwali, Ibrahim, Mwinchande, Joseph Benard na Habib Jeff.

Wakati akiwa kwenye bendi ya Dar International aliyoitumikia kuanzia mwaka 1977, Gama alishiriki kupiga Rhythm kwenye vibao vingi, baadhi yake vikiwa ni ‘Sikitiko’, ‘Mwana Rudi Uoe’ na ‘Mwalimu Nyerere’.

Alipoingia katika bendi hiyo ya Mlimani Park Orchestra, Gama kwa kipindi kifupi aliweza kujipatia umaarufu mkubwa, hasa kwa umahiri aliokuwa nao katika kulicharaza ipasavyo gitaa la Rhythm kwenye vibao vingi vya bendi hiyo.

Abdallah gama ni mwanamuziki aliyefaulu kwa kiasi kikubwa kuzigusa nyoyo za mashabiki wengi kutokana na tungo zake zenye maudhui maridhawa yaliyoshiba ujumbe mzito, za ‘Hadija’, ‘Dar es Salaam Airport’, ‘Maudhi ya Nyumbani’, ‘Linda’ na ‘Nawashukuru Wazazi’.

Akielezea wasifu wake Gama alianika mambo mengi hususani historia yake kimuziki na maisha kwa ujumla.

“Baba yangu alikuwa fundi Cherahani, ndiye aliyenivuta kwenye muziki kwani alikuwa akipiga gitaa lisilotumia umeme la Galatoni, kujifurahisha na wakati mwingine akiwaburudisha rafiki zake…” anasema Gama.

Alisema kuwa, akiwa na umri wa miaka 28, alikuwa tayari anafahamu kikamilifu jinsi ya kulikung’uta gitaa. Bendi yake ya kwanza kupigia ilikuwa ni Safari Trippers aliyojiunga nayo mwaka 1973.

“ Nikiwa Safari Trippers nilishiriki kupiga gitaa la solo kwenye vibao kadhaa, vikiwamo ‘Ooh Lila’ na ‘Mateso’ ambavyo vyote ni matunda ya marehemu Marijani Rajabu...” alibainsha Abdallah Gama.

Ni mwanamuziki asiyependezwa na tabia ya wanamuziki kuhamahama makundi, alisema kwamba mwaka 1975 alijiunga na bendi ya Tanzania Stars ambayo maskani yake yalikuwa katika hoteli ya Margot.

Hoteli hiyo ilikuwa katika mtaa wa Independence (siku hizi ni mtaa wa Samora) jijini Dar es Salaam. Ikumbukwe kuwa, mwaka 1984 Gama alijiunga katika bendi ya Bima Lee iliyokuwa ikimilikiwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC)

“Nikiwa na bendi ya Bima Lee, iliyokuwa ikipiga muziki kwa mtindo wa “Magnet tingisha” nilitunga kibao cha ‘Fungua Macho’, pamoja na kushiriki kucharaza gitaa kwenye vibao kama vile; ‘Makulata’ na ‘Tujemaso…” anafafanua Gama.

Abdallah Gama atakumbukwa kwa kazi zake alipokuwa bendi ya Bima Lee Orchestra akishirikiana vyema na watunzi na waimbaji akina Jerry Nashon, Shaaban Dede, wapiga magitaa Joseph Mulenga ‘Kig Spoiler’ kwa upande wa solo na Suleiman Mwanyiro kwa upande wa gitaa zito la besi.

Wanamuziki hao walichukuliwa kwa mpigo na Shirika hilo la Bima kwa ajili ya kuimarisha bendi ya Bima Lee Orchestra kufuatia ushindani mkubwa wa bendi zilikuzokuwepo wakati huo. Abdallah Gama wakati huo alikuwa mithiri ya Kito cha thamani kwani aliitumikia bendi Bima Lee Orchestra kwa mwaka mmoja.

Mwishoni mwa mwaka 1985, alihitajika kurejea tena katika bendi yake ya zamani ya ‘Wana Sikinde’. Wimbo wa ‘Gama Unisamehe’ kilichoporoshwa na bendi yake wakati huo ya Mlimani Park Orchestra, baadhi ya wapenzi na mashabiki hudhani kwamba mtunzi wa wimbo huo kuwa alikuwa yeye. Lakini Gama pasipo kujigamba ametamka kwamba pasipo kumung’unya maneno akisema:

“Kibao kile kilitungwa na Tshimanga Kalala Asossa, tukiwa Zanzibar kwenye shoo, mimi nilikuwa Kiongozi wa Jukwaa, sasa kabla hatujaanza kutumbuiza nilipanda jukwaani na kuwaita wanamuziki kwa kutumia mlio wa gitaa langu...”

Nguli huyo aliendelea kueleza kuwa, ghafla alimuona Asossa aliyekuwa anapenda kutembea na redio ndogo ya kurekodia sauti, akarekodi kipande alichokuwa anakipiga kisha akaondoka.

Waliporejea Dar es Salaam wakiwa kwenye mazoezi, Tshimanga Kalala Asossa alikuja na mashairi ya wimbo huo, akiambatanisha kile kipande alichokipiga Gama kule Zanzibar.

Wakaufanyia kazi wimbo huo na kuamua kuupa kumbukumbu kwa kuuita ‘Gama Unisamehe’. Tshimanga Asossa alijiunga na bendi hiyo ya Mlimani Park Orchestra mwaka 1981, baada ya uongozi wa Mlimani Park kumfuata kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuja kupiga muziki na bendi hiyo kwa mkataba.

“Maisha ni kutafuta…” usemi huo ulijionesha wazi kwa mwanamuziki Abdallah Gama, ambaye mwishoni mwa mwaka 1985, alivuka mpaka wa Tanzania na kiungia nchini Kenya kwa kupitia bandari ya Tanga.

Alipotua katika jiji la Nairobi, alijiunga na bendi ya Super Mazembe iliyokuwa ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Garden Square, jijini Nairobi. Alishirikiana kikamilifu na wapiga magitaa wa bendi hiyo ya Super Mazembe akina Loboko Bua Mangala, Bukasa wa bukasa ‘Bukalos’, Atia Joe ‘Mwanza wa Mwanza’ aliyekuwa akiliungurumisha gitaa la besi

Matarajio ya kila kazi ni kupata mafanikio mazuri yanayoweza kumnemesha muhisika pamoja na familia yake. Kwa upande wa mafanikio aliyoyapata mwanamuziki huyo Abdallah Gama anasema “…Mafanikio niliyokwishayapata kwenye muziki ni kutembea nchi nyingi duniani, jambo ambalo sikutarajia hapo kabla…” Gama kati ya ziara alizowahi kuzofanya nje ya nchi, anaikumbuka mno ziara yake alipokuwa katika bendi ya Malembe Stars.

Aidha anazikumbuka baadhi ya nchi alizowahi kufika kuwa ni pamoja na Japan, Malaysia, Ufilipino, Pakistan na Misri. Bila kusita Gama amesema kuwa yeye ni baba wa watoto wanne anawataja kuwa ni Mgeni, Pili, Hadija na Maimuna. Gama elimu kwa familia yake aliipa kipa umbele na sasa anajivunia kwa kuweza kusomesha watoto wake wote hadi elimu ya Chuo Kikuu.

Ili kutunza kumbukumbu za kazi zake alizokwisha kuzifanya awali, Gama ana mpango wa kurudia kuvirekodi upya vibao vyake vya zamani, alivyovitunga akiwa na bendi za Mlaimani Park Orchestra ‘Wana Sikinde’ na Bima Lee Orchestra, kutokana na shinikizo kubwa la mashabiki wake. Abdallah Gama hivi sasa yuko katika bendi ya Excel ya jijini Dar es Salaam, wakati akiwa katika mkakati wa kuanzisha bendi yake binafsi.

MIAKA SITA BILA KABEYA BADU

$
0
0
Na Moshy Kiyungi

Kabeya badu alikuwa mwimbaji mahiri katika bendi ya La Capitale, aliyewaacha wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi hapa nchini, wakiwa bado wanamhitaji.

Mwaka huu ametimiza miaka sita atngu aiage dunia Machi 06, 2013 akiwa katika hospitali wa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa maradhi ya figo, akiwa amefikisha umri wa miaka 68.

Mpaka alipofikwa na umauti, alikuwa ni mwanamuziki mwenye vipaji vya kutunga na kuimba katika bendi ya La Capitale ‘Wazee Sugu’ inayoongozwa na mkongwe Kikumbi Mwanza Mpango ‘King iki’.

Msimba wa Kabeya uliwatia simanzi na majonzi makubwa waombolezaji waliofika katika hospitali ya Muhimbili kuuaga mwili wake na katika mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni Machi 07, 2013. umati wa watu walibubujikwa machozi mara walipoona mwili wake ukishushwa kaburini.

Kabeya Badu toka alipoanza safari yake katika muziki, kamwe hakuwa mtu mwenye soni, alikuwa tayari kuiacha bendi na kwenda nyingine wakati wowote, ili mradi maslahi yawe mazuri. Alipitia bendi nyingi akiwa huko kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na hapa Tanzania, ambapo alipigia katika bendi si chini ya tano tofauti.

Si vyema kumsifia mtu baada ya kufa, lakini kwa Kabeya ninalazimika kufanya hivyo kwa kuwa mwishoni mwa mwaka jana 2012, nilipata fursa ya kufanya mahojiano naye ili kujua Wasifu wake.

Nilizungumza na Kabeya Badu kwa takribani saa mbili mfululizo, akinisimulia historia ya maisha yake kwa ujumla. Aliaza kwa kutaja majina yake akisema anaitwa Kabeya Chibangu Badu, alizaliwa Januari 22, 1945 katika mji wa Likasi, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Elimu ya msingi alipata katika shule ya Ecole Officialle Laique de Kolwezi, akamaliza mwaka 1959.

Kabeya alisema muziki alianza kuupenda tangu akiwa bado mdogo na alipopata umri wa kwenda kanisani, alijiunga katika kwaya akiimba nyimbo injili. Akiwa kanisani humo, alijifunza jinsi ya kutengeneza ‘Melody’ baadaye mwaka 1963, akajiamini kwamba anaweza kufanya muziki. Alikwenda kujiunga na bendi ya muziki wa dansi ya Ricco Jazz, iliyokuwa katika wilaya ya Kolwezi. Akiwa huko Kabeya alijiunga na chuo cha ufundi ambako alichukua masomo ya useremala na uashi.

“tangu nikiwa mdogo, nilipenda sana nyimbo na uimbaji wa Tabu Ley Rochereau na Kabasele Yampanya ‘Pepe Kale’ nikatamani siku moja nifikie hadhi yao…” anasema Kabeya. Familia yake ilijitahidi kumpa moyo ili aweze kufanya vizuri katika muziki, hivyo ilimshauri kabeya kujifunza lugha ya Kifaransa ambayo inazungumzwa nchini mwao.

Kabeya alikubaliana na ushauri huo, akaingia katika chuo kilichokuwa kikimilikiwa na dhehebu la dini ya Protestant huko Kananga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kiu cha Kabeya kilipozwa pale alipopokea cheti baada ya kufuzu somo hilo la Kifaransa. Harakati za kutafuta maisha zilimfikisha kufanya kazi katika gazeti moja la Reality Congolese la mjini Kananga, kwenye kitengo cha usambazaji mwaka 1967.

“Baada ya miaka miwili kupita, mmiliki wa gazeti hilo alikamatwa baada ya gazeti hilo kuandika habari zilizo muudhi rais wa wakati huo Mobutu Seseseko, hatima yake gazeti likafungiwa, tukakosa kazi….” anaeleza Kabeya Badu.

‘kuvunjika kwa koleo si mwisho wa ujenzi’ msemo huu aliufanyia kazi Kabeya ambaye mwaka huo huo alianza safari yake ya muziki kikamilifu. Akajiunga katika bendi ya Lupe Jazz, baadae akaenda katika bendi nyingine ya Amide Success. Kabeya hakuishia hapo kwani aliondoka tena na kwenda kujiunga na bendi ya Santa Fee, baadae akajiunga katika bendi ya Lupina Nationale, ambako alikutana na Kasongo Mpinda ‘Clayton’ huko Kananga.

Utulivu katika bendi kwake haukuwepo kabisa, kwani aliondoka tena na kwenda kujiunga katika bendi ya Lupe Revolution, iliyokuwa ya vijana kama yeye. Jina na sifa za uimbaji wake zikazagaa kila pembe. Ndipo alipochukuliwa na Omer Baba Gaston Ilunga wa Ilunga, akajiunga katika bendi yake ya Baba Nationale Septemba 1968. Mwaka 1970, Kabeya alishawishika kwenda kutafuta ajira katika mji wa Kinshasa. Huko alibahatika kupata ajira katika bendi ambayo baadae akagundua kwamba ilimpa ahadi za uongo za maslahi, naye akaachana nayo.

Kati ya mwaka 1971 na 1972 Kabeya Badu alipiga muziki katika bendi ya Festival du Zaire katika jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kabeya alirudi Likasi mwaka huohuo wa 1972 na kujiunga na bendi ya Fouvette ambayo baadae ilibadilishwa mnajina ikaitwa Safari Nkoi. Alikuwa ni mwanamuziki Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ aliyemuita kwenda kujiunga katika bendi hiyo.

Hapo alikutana na wanamuziki wengine magwiji Ndala Kasheba na Baziano Bweti. Kabeya Badu nasema kwamba alisoma darasa moja na Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’, katika shule ya msingi ya shule ya Ecole Officialle Laique de Kolwezi, ambako walimaliza masomo yao mwaka 1959.

“Tangu tukiwa vijana tulikuwa tukielewana sana na Kiki. Ndiyo sababu nimekuwa naye sambamba tukienda sehemu mbalimbali hadi leo ninaye…” alisema Kabeya. Walipokuwa Kolwezi wakipiga muziki katika bendi ya Safari Nkoi, walikuwa wamepanga nyumba moja, walichangia bajeti ya chakula kwa pamoja kila mwisho wa mwezi.

Mwaka 1973 uongozi wa Safari Nkoi ulianza kuwafanyia ‘mtimanyongo’ wanamuziki wake akiwemo ‘King Kiki’ lakini Kiki, aligundua mapema hali hiyo. Akamshawishi Kabeya mwaka huohuo wa 1973, kuondoka na kwenda kuanzisha bendi yao.

‘mwenye bahati habahatishi’ msemo huo ulijionesha dhahiri kwani kabla hawajaazisha bendi yao, akajitokeza tajiri mmoja aliyejulikana kwa jina la Paradizo, akimtaka Kiki kwenda Lubumbashi kuanzisha bendi yake. “Kiki hakuniacha mwaka 1974 tukaenda Lubumbashi kuunda bendi ya tajiri huyo ya Buka Buka Mabele. “Ukiritimba wa tajiri ulisababisha bendi hiyo kufa baada ya miezi sita…” alielezea mwanamuziki huyo.

Kabeya akaongeza akisema baada ya kufa kwa bendi ya Buka Buka Mabele, Kiki mwaka 1974 mwishoni aliamua kwenda mji mkuu wa DRC wa Kinshasa. Lakini kabla hajaondoka, aliwashawishi yeye na wanamuziki wenzake warejee Safari Nkoi. Walikubali ushauri hou nao wakarejea na wakapokewa na uongozi wa Safari Nkoi kwa mara nyingine tena.

Kwa kipindi hicho akiwa Safari Nkoi, Kabeya akawa na mawasiliano ya karibu na Kiki, akimshawishi aendelee kubakia Safari Nkoi kwa hali ya utulivu katika bendi ilikuwa ni imeimarika. King Kiki alirejea Lubumbashi mwaka 1976, akitokea Kinshasa pasipo kumafamamisha mtu yeyote. Kabeya anasema “ tulikuwa tunapiga muziki katika ukumbi mmoja wa Rele Night Club mjini Lubumbashi, ghafla Kiki akapanda jukwaani na kushika ‘Mic’ akaanza kuimba. sote tukabutwaika tukaona kama vile ‘shetani’ aliyetua kimiujiza jukwaani”

Mwaka 1977 Kikumbi Mwanza Mpango alifuatwa na Chibangu Katayi ‘mzee Paul’ aliyetokea Maquis du Zaire iliyokuwa hapa nchini. Kiki alimuuliza mzee Paul iwapo wanamuziki waliopo Maquis du Zaire wanakidhi viwango? mzee Paul alijibu kwa wasiwasi na kupendekeza bora kuchukua wanamuziki huko drc. Kiki alipendekeza wanamuziki wa kuondoka nae kuj Tanzania akiwemo Kanku Kelly, Mutombo Sozy, Ilunga Banza ‘mchafu’.

Wakiwa safarini kuja nchini walipitia mji wa Kamina ambako walimpata mnenguaji mwanadada Ngalula Tshiandanda aliyekuwa akinengua katika bendi ya Sakayonsa ya mjini humo. Kabeya badu alikuwa akiwasiliana na King Kiki, akamuahidi kwamba atajitahidi aje Tanzania.

Ahadi ya Kiki kwa Kabeya ikatimia baada ya kufika Maquis du Zaire, ambako alibaini kuwa safu ya uimbaji ikaonekana kupwaya. Aipendekeza kuongezwa kwa wanamuziki zaidi ili kuimarisha bendi hiyo ya Maquis du zaire. Chibangu Katayi ‘ mzee Paul’ kwa mara nyingine tena akatumwa kwenda congo kuwaleta wanamuziki waliopendekezwa na Kiki.

“ tulichukuliwa mimi Kabeya Badu na Kalala Mbwebwe, tukiwa ni watunzi na waimbaji, Monga Kiyombo aliyekuwa na uwezo wa kupiga gita la rhythm na saxophone. Wengine waliochukuliwa ni Ngoi Mubenga kwa upande wa tarumbeta na Khatibu Iteyi Iteyi aliyekuwa mpulizji wa saxophone tukaletwa tanzania mwaka 1978…” alitamka Kabeya.

Kabeya alisema mara alipotua Maquis du Zaire, alitunga na kuimba nyimbo nyingi, baadhi yake ni “Ndoa ya kwangu na mama Kazi”, ‘Pondamali’, ‘Kibwe Mutombo’ na zingine za Muntanda Muli, Lwembe na maneno, ambazo hazikuwahi kurekodiwa.

Kabeya Kadu alipiga na Maquis du Zaire kwa miaka miwili, mwaka 1980 alichoropoka na kwenda akijunga na King Kiki katika bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS) iliyokuwa ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu Hugo Kisima. Akiwa na OSS, Kabeya alitunga na kuimba nyimbo za Nani atashika Jembe na Pole ndugu.

Alieleza kuwa wimbo wa ‘Yuyu’ ulipigwa na kurekodiwa katika kipindi cha Klabu raha leo show kilichokuwa kikirushwa na Radio Tanzania Dar es Salaam. (RTD) badu alikuwa akihitajika sana katika bendi hizo mbili pinzani wakati huo za maquis na oss. hivyo akawa mithiri ya ‘muigizaji’ kwa kuhamahama. alirejea tena maquis kwa kipindi kifupi kisha mwaka 1986 akatakiwa kurejea kwa mara nyingine tena katika bendi ya orchestra safari sound.

aliporejea oss tayari bendi ilikuwa chini ya uongozi wa ndala kasheba na haichukua muda mrefu akatoka na wimbo uliowapagaisha wapenzi wa oss wa ziada. wimbo huo aliuimba peke yake kwa hisia kali akimlilia ziada, na ukamuongezea sifa kubwa miongoni mwa waimbaji wa muziki wa dansi hapa nchini. zingine zilikuwa za ‘ kuruthumu’, ‘simba wala watu wamevamia mji’ mama mwita, kayanda na nyingine nyingi.

kabeya badu anamwelezea kikumbi mwanza mpango ‘king kiki’ kuwa ndiye anayejua umuhimu wake na hapa anasema… “ kiki ndiye aliyekuwa akijua umuhimu wangu katika muziki toka mwanzo hadi akanipachika jina la ‘ changa cha mkonyoyo’ ikiwa na maana ya siri iliyofichika…” alipewa jina hilo baada ya kufyatua wimbo wa changa cha mkonyoyo’ anaoulezea kuwa ni ujumbe mzito japokuwa wimbo huo haukuwahi kurekodiwa.

aliondoka oss na kwenda kujiunga kwa mara nyingine tena na maquis du zaire mwaka 1988, hapo napo hakadumu akachukuliwa na kwenda kujiunga na bendi ya tancut almasi iliyokuwa ikipiga muziki wake mjini iringa. ‘msahau kwao mtumwa’ kabeya alitamani kurejea kwao congo, ndipo mwaka 1990 akaamua kurudi kwao likasi katika jimbo la katanga.

kama nilivyokujuza mwanzoni kwamba kabeya alikuwa mtafutaji wa maslahi murua, hivyo alirejea tena tanzania mwishoni mwa mwaka 1998. mwaka uliofuatia wa 1999, akapewa kazi ya kuanzisha bendi ya magoma sound ya jijini dar es salaam. mwaka 2001 alijiunga katika bendi ya la capitale inayoongozwa na kikumbi mwanza mapango ‘king kiki’ au ‘bwana mukubwa’ hadi mauti yake yalipomfika jumatano iliyopita ya tarehe 06 machi, 2013.

kabeya alisema kwamba ana matarajio makubwa anayotamani kufikia. “nina mpango wa kununua vyombo vyangu vya muziki, pia natarajia kurekodi nyimbo zagu zote nilizotunga na kuziimba, nziuze mimi mwenyewe…” anasema kabeya akiwa mwingi wa tabasamu usoni. ninasikitika kwa kusema kuwa kumbe kauli hiyo ikifuatiwa na tabasamu hilo, ilikuwa la ndiyo mwisho, tukiagana naye! kabeya badu alinisisitiza kwamba mara tu makala hii ikitoka, nimualifu ili awahi kununua gazeti hili, lakini mpangaji wa yote ni mungu.

kiongozi wa bendi ya la capitale, kikumbi mwanza mpango king kiki’ alimuelezea kuwa pengo la kabeya kamwe halitazibika. “ kabeya pengo lake halitazibika kamwe ametuachia ukiwa usio na kifani. alikuwa ni mtunzi na mwimbaji mzuri si hivyo tu pia alikuwa msikivu, mtu wa kazi tulishauriana kutengeneza ‘melody’na kwa kwa ushirikiano huo tulikuwa tukichokozana na kutoa vibao ‘matata’ sana. tumempoteza kabeya…” kwa masikitiko na majonzi anasema kiki.

kabeya chibangu badu, ameacha mjane na watoto wanane kati yao watano ni wa kike. wapenzi na wadau wa muziki wa dansi hapa nchini, kamwe hatamsahau kabeya badu kwa jinsi alivyokuwa na uwezo wa kulishambulia jukwa kwa kucheza na kupaza suti yake iliyokuwa nyororo wakati akiimba. Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi, amina.

KATIBU TAWALA ATUMIA WAANDISHI WA HABARI WA KASKAZINI KUTUMA SALAM KWA WAFANYABIASHARA

$
0
0
Na Woinde Shizza, Michuzi TV Kilimanjaro.

KATIBU Tawala wa Mkoa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour amewataka wafanyabiashara kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kuitumia Bandari ya Tanga katika kusafirisha mizigo yao kwani hivi sasa imeboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza katika kikao kati yake na waandishi wa waandishi wa habari wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo amesema wafanyabiashara wengi kutoka mikoa hiyo wamekuwa wakitumia kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya kutokana na changamoto ambazo zilikuwepo hapo nyuma lakini kwa sasa Bandari ya Tanga imeboreshwa.

Ametumia nafasi hiyo kuipongeza Mamalaka ya Bandari ya Tanzania chini ya uongozi wa Mhandishi Deusdedit Kakoko kwa jitihada kubwa za kuboresha miundombinu na utoaji wa huduma katika kiwango cha hali ya juu katika bandari ya Tanga na kuwa mkakati huo utaifanya bandari hiyo kuwa kimbilio la wafanyabiashara na wawekezaji. "Tunawaomba wafanyabiashara watumie hii Bandari ya Tanga kwani sasa hivi imeboreshwa zaidi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mitambo mikubwa ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kurahisisha utoaji huduma,"amesema Mhandishi Aisha. 

Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Tanga, Percival Salama amesema kuwa bandari hiyo imeweza kuhudumia tani 506,000 Kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 ambapo hadi kufika Juni mwaka huu watakuwa wamehudumia tani 700,000.Amesema bandari hiyo ina jumla ya mitambo 42 kwa sasa, ambapo kwa mwaka 2018/2019 imeagiza mitambo 20 kati ya hiyo mitambo 16 imeshawasili sawa na asilimia 80 .

Ameongeza hivi sasa changamoto ya suala la mitambo katika bandari hiyo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu, hivyo kuwataka wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro kujitokeza Kwa wingi kuitumia bandari hiyo.

"Bandari ya Tanga ya sasa hivi si ile tuliyoizoea zamani, sasa hivi bandari imeboreshwa sana ikiwa ni jitihada za Mkurugenzi Mkuu wa bandari Tanzania, Mhandisi Deusdedit Kakoko lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wote waliokuwa wakitumia bandari zingine wanarudi nyumbani kwani sasa kumenoga,"amesema Salama. 

Amefafanua bandari ya Tanga ndio bandari pekee Afrika yenye uwezo wa kuhudumia nchi saba kwa kutumia mpaka mmoja, ambapo nchi hizo ni Malawi, Zambia, DRC Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.
 Katibu Tawala  wa mkoa wa  Kilimanjaro muhandisi Aisha Amour akiongea na waandishi Wa habari  katika mkutano  Wa waandishi Wa  habari   ulioandaliwa na mamlaka ya bandari ya Tanga  uliofanyika Leo katika ukumbi Wa mikutano Wa mkuu Wa mkoa Wa Kilimanjaro.

 Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo


DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 


MKUU wa wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani Assumpter Mshama ,amedhamiria kuyafuta mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO's) wilayani humo ambayo ni ya mifukoni huku yakifanya shughuli kwa utapeli na ubabaishaji.

Aidha amedai atayaandikia barua ya kujieleza mashirika yale ambayo yaliitwa kwenye kikao chake lakini viongozi wake hawakuweza kutokea ambapo kati ya mashirika zaidi ya 100 yaliyofika yalikuwa 21 pekee.

Assumpter aliseyama hayo wakati wa kikao chake na viongozi wa mashirika hayo ili kubadilishana mawazo na kujua changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi wao.

Alieleza, watatoa taarifa kwa wafadhili wao kuwa mashirika hayo ni ya kitapeli na hayafanyi kazi kama wanavyojieleza wanapoomba ufadhili.

"Hawa walioshindwa kuja lazima waandike barua za kujieleza kwa nini hawakufika kwenye kikao na nadhani ndo haya tunayoyasema na wakishindwa kujieleza tutawafuta na tutapeleka taarifa kwa msajili wa mashirika haya ili ayaondoe kwenye usajili," alisisitiza Assumpter. 

Hata hivyo, amewataka viongozi wa mashirika hayo kupeleka taarifa zao za utendaji kazi na wawe wanatoa taarika serikalini za kila robo mwaka na ataomba wafadhili kabla ya kutoa fedha waulize juu ya mashirika hayo kwani mengine yako kwa ajili ya maslahi binafsi .

Nae ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya mji Kibaha ,Mkami Noela Hangaya alisema ,alitoa taarifa kwa mashirika yote lakini yaliyohudhuria ni machache na hakuna sababu walizotoa kwamba hawatafika.

Mwenyekiti wa shirika la kituo cha msaada wa kisheria, Kibaha (KPC) Catherine Mlenga alifafanua ,wamekuwa wakitoa taarifa serikalini ofisi ya ustawi wa jamii na kwa viongozi wa serikali za mitaa na kata hivyo wao wanafuata taratibu zote.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA WELEDI

$
0
0
WAANDISHI wa habari wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na kusaka vyanzo tofauti katika habari zao badala ya kuegemea chanzo kimoja.

Hayo yalielezwa jana katika uzinduzi wa machapisho ya matatu ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), ambayo ni ripoiti ya hali ya tasnia ya habari nchini ya mwaka 2017/2018 iliyoandikwa na Dr. Joyce Bazira, Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Dr Ali Uki na Henry Muhanika, chapisho la pili ni ukiukwaji wa maadili kwenye tasnia ya uandishi wa habari kilichoandikwa na Mhariri wa Gazeti la Daily News Pudenciana Temba na Attilio Tagalile, wakati chapisho la tatu ni fani ya uwandishi katika habari za kiuchunguzi zinavyoathirika ikitolea mfano kesi ya waandishi wa habari Ruvuma , ambapo kimeandikwa na Hamis Mzee, Lucas Liganga na Florence Majani.

Katika utafiti huo wa MCT unaonyesha kuwa vyombo vingi vya habari nchini vinakabiliwa na ugonjwa wa chanzo kimoja cha habari (SSS).

Akisoma ripoti hiyo, Mwenyekiti mstaafu wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda alisema kinachosikitisha zaidi kuhusu chanzo kimoja cha habari ni kwamba hutawaliwa na sauti za wanaume.

“Utafiti mmoja mahususi uliofanywa na MCT umeonyesha gazeti la Mwananchi lilikuwa na habari 99 za chanzo kimoja, ya vyanzo viwili zilikuwa 63 na habari za vyanzo vingi zilikuwa 158, habari zenye sauti za wanaume 1,913 sawa na asilimia 95 wakati zenye sauti za wanawake ni 93 sawa na asilimia tano.

Alisema utafiti huo pia umeonyesha gazeti la Nipashe lilikuwa na habari za chanzo kimoja ni 184, zenye vyanzo viwili ni 133 na habari za vyanzo vingi ni 103, habari zenye sauti za wanaume 1,307 sawa na asilimia 94 na zenye sauti za wanawake zilikuwa 88 sawa na asilimia sita wakati gazeti la Uhuru lilikuwa na habari za chanzo viwili zilikuwa 155 na habari za vyanzo vingi zilikuwa 204, huku zenye sauti za wanaume 3,111 sawa na asilimia 95 wakati sauti za wanawake zilikuwa 237 sawa na asilimia nane.

“Takwimu hizo zinaonyesha ukubwa wa tatizo ambalo lazima lishugulikiwe haraka na vyombo vya habari vya ndani, mfano kuna wakati Zito Kabwe anageuzwa yeye ndio waziri wa fedha, ndio profesa wa uchumi, ndio CAG, mchambuzi wa mambo ya uchumi, habari ukiikuta ni Zito alisema, aliongeza, alifafanua, waandishi toeni haki ya kujibu, hii itasaidia kukwepa vitanzi vya kisheria.”alisema Kibanda na kuongeza

“The Citizen walifungiwa wiki mbili, mimi namuunga mkono Dr Abbas kwa vile waliegemea upande mmoja walipaswa kupata upande wa pili lakini walikuwa na haraka, juzi kuna vyombi vya habaru vimeandikiwa barua baada ya kuandika ripoti aliyotoa Zito, ni sahihi kwa vile hawakutoa haki kwa mamlaka nyingine kujibu, hii ingesaidia, wasingepata kitanzi cha kisheria.”alisema Kibanda

Alisema changamoto kubwa kwa sasa hali ya uandishi wa habari ina wasomi lakini kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa kimaadili, msingi ya kitaaluma leo hii kuliko miaka ya nyuma ambapo wasomi walikuwa wachache.

“Waandishi wanatakiwa kujitazama na kujitathmini kama wanatimiza wajibu wao kitaaluma, mnapaswa kuwa makini kuliko wakati mwingine wowote.”alisema na kutolea mfano waandishi wa mitandao ya kijamii hususani you tube ambayo wamekuwa wakitoa kipande kidogo kwa makusudi na kuharibu maana nzima ya habari.

Akitolea mfano online tv alisema misingi ya kitaaluma inabidi ielekezwe huko kwani wamekuwa wakipotosha zaidi, bila kujali usahihi ulivyo na kusababisha mkanganyiko kwa jamii.

“Usahihi ni msingi namba moja hasa kwenye mitandao ya kijamii ambayo inafatiliwa kwa haraka, Uhuru uliopo usipitilize, misingi, maadili na miiko ya taaaluma inabidi itimizwe, la sivyo tusipotimiza hili, tutakwisha.”alisema

Alisema waandishi wa mitandao ya kijamii wanapaswa kufuata msingi wa kutoegemea upande wowote, na kuzingatia misingi ya kutoa haki na wajibu.

Kwa upande wa gwiji la habari, Pili Mtambalike ambaye alifanya rejea ya chapisho la Ukiukwaji wa Maadili kwenye Tasnia ya Uandishi wa Habari alisema ripoti hiyo imechukua miaka miwili ambayo ni 2017 na 2018 ambayo imepitia masuala ya sheria, sera, kanuni na changamoto mbali mbali zinazotokana na sheria za vyombo vya habari, kanuni na athari zitokanazo na sheria mpya ya vyombo vya habari.

Naye Atilio Tagalile akizungumzia ripoti ya Ruvuma ambayo waandishi wameenda kinyume na maadili ya vyombo vya habari alisema waandishi wanapaswa kushikamana na sio kuumizana na wasikubali kutumika.

“Waandishi wengi wa sasa ni wasomi, lakini inasikitisha baadhi yao hawana weledi kwenye kazi yao, nawakumbusha kwa nyakati hizi mnapaswa kufanya kazi zenu kwa umakini na weledi wa hali ya juu, la sivyo kuna anguko zaidi katika tasnia ya uandishi iwapo hatua hazitachukuliwa haraka.”alisema

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga alisema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imeporomoka kwa nafasi 47 katika nchi ndani ya miaka mitatu kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2018, ambapo mwaka 2016 iliporomoka nafasi 12, mwaka 2017 ikaporomoka nafasi 10 na mwaka 2018 imeporomoka nafasi 25.

DPP aipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili ‘Mpemba wa Magufuli'

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MKURUGENZI  wa Mashitaka Nchini (DPP), ameipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli' na wenzake watano.

Hatua hiyo imekuja leo Aprili 25, 2019 kufuatia wakili wa serikali Eliya Athamasi akisaidiana na Candid Nasua ,kuwasilisha hati na ridhaa ya kuruhusu Mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo iliyowasilishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kuwasilishwa kwa nyaraka hizo,upande  wa mashitaka uliwasomea upya washitakiwa hao mashitaka yao ambayo waliyakana na upande wa mashitaka umeomba  tarehe ya kuwasomea washitakiwa hao Maelezo ya awali na kesi hiyi imeahirishwa hadi Mei 7 mwaka huu.

Yusuf na wenzake watano, wanakabiliwa na mashitaka manne, likiwemo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chuma, Ahmed  Nyagongo  na Pius Kulangwa.

Katika hati ya mashtaka imedaiwaaiwa kwamba Kati ya Januari 2014 na Oktoba 2016  katika Mkoa wa Dar es Salaam, Ilinga, Morogoro, Tanga na Mtwara kwa dhamira,waliendesha na kujihusisha na shughuli za kihalifu kwa kupokea,kumiliki na kujihusisha na biashara haramu ya vipande 50 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Sh. 392, 870,000 bila kibali kutoka kwa mkurugenzi wa Wanyamapori.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kwamba,Oktoba 26 mwaka 2016 eneo la Mbagara Zakiem,Temeke Dar es Salaam walikutwa wakimiliki vipande 10 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh. 60,496,000 bila kuwa na kibali.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Oktoba 27 2016 huko Tabata Kisukuru, wastihakiwa hao walikutwa  wakimiliki vipande vinne vya meno ya tembo vyenye thamani ya sh 32,734,800 kinyume cha shehria. Pia washtakiwa hao wanadaiwa Oktoba 29, walikutwa wakimiliki vipande 36 vya meno ya Tembo  vyenye thamani ya Sh. 294,613,000 bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wanyama pori nchini.

MTENDAJI MKUU WA BODI YA FILAMU ATENGULIWA

$
0
0
KATIBU MKUU wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi ameagizwa ampangie kazi nyingine Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Bi. Joyce Fisoo na ateue mtu mwingine kushika nafasi hiyo.

Agizo hilo lilitolewa jana jioni (Jumatano, Aprili 24, 2019) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akihitimisha kikao chake na wasanii zaidi ya 100 kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania kilichofanyika Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.

Shirikisho la Filamu Tanzania linajumuisha vyama 11, ambapo 10 vimesajiliwa na kimoja hakijakamilisha usajili. Vyama hivyo ni vya waigizaji, waongozaji, watayarishaji, wahariri, wachekeshaji na wapigapicha. Wengine ni waandishi wa miswada (script writers), watafutaji mandhari, wasambazaji wa filamu, walimu na chama cha wanawake wa tasnia ya filamu ambacho bado kiko kwenye mchakato wa usajili.

Kikao hicho ambacho kilidumu kwa zaidi ya saa saba, kilihudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakiongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Bibi Juliana Shonza.

“Katibu Mkuu mtafutie eneo jingine la kufanya kazi. Hana tuhuma zaidi ya mahusiano mabaya na wadau wake, ana historia nzuri, lakini tatizo ni mahusiano. Mpeleke idara nyingine na hapa mlete mtu mwingine,” alisema Waziri Mkuu.

“Mama Fisoo wewe uko clean, sina tatizo na utendaji wako lakini ukikaa hapa hutaweza kwenda mbele na wala hawa wote hawatakuja kufanya kazi na wewe. Tunataka hii tasnia iende mbele, tunataka maendeleo kwenye tasnia ya filamu,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Alimuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania, Profesa Frowin Nyoni ajipange upya na Bodi yake na kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa wasanii kama ambavyo imeainishwa kwenye sheria ya kuanzishwa kwa Bodi hiyo.

“Bodi yako inao wajibu wa kutoa elimu kwa makundi tofauti ya wasanii. Sheria yenu imeainisha kuwa mnapaswa kutoa elimu. Wapeni refresher courses ili waongeze ujuzi na wakienda huko wanatoa uzoefu walionao kwa wanachuo, nao pia wanakuwa wamejifunza,” alisema.

“Nimeangalia makundi ya wasanii na kukuta kuna wachoraji na wachongaji; wasanii wa filamu, wasanii wa maigizo, wabunifu wa mitindo na wote hawa wana Bodi zao. Timizeni majukumu yenu. Bodi pia mna kazi ya kupromote brand kwa kutumia wasanii wetu,” alisema.

Kuhusu utitiri wa tozo ambao umelalamikiwa na wasanii hao, Waziri Mkuu alisema kuna haja ya kulinda soko la ndani la kazi za wasanii wa Kitanzania tofauti na hali ilivyo sasa ambapo wazawa wanatumia gharama kubwa kutengeneza kazi zao lakini wanapata shida kuziuza ilhali wageni wanapata faida zaidi kwa kazi kama hizo.

“Wasanii wamesema kuna tozo 11 lakini Mtendaji Mkuu kataja tozo chache tu. Hebu Waziri aitishe kikao baina yenu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Viwanda na Biashara, Kamishna wa TRA, Bodi ya Filamu na TCRA, mkutane mara moja na kuziangalia upya hizi tozo ili zipunguzwe kama tulivyofanya kwingine. Lazima tulinde soko la ndani,” alisisitiza.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaonya wasanii juu ya fukuto linaloendelea ndani kwa ndani baina ya vyama tofauti, baina ya vyama na shirikisho na baina ya shirikisho na taasisi nyingine za kiutendaji.

Kuhusu maudhui ya filamu zinazotengenezwa na wasanii wa Tanzania, Waziri Mkuu alisema inashangaza kuona masuala ya mapenzi yanaongoza kwenye filamu za Kitanzania kwa kushika nafasi ya kwanza ikiwa ni sawa na asilimia 68, ikifuatiwa na vichekesho ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa sawa na asilimia 12.

“Je, wote ni lazima muigize masuala la mapenzi kwenye filamu zenu au huwa mnaambiana mtoe maudhui yanayohusu mapenzi. Je, ni kweli kwamba Watanzania wengi wanapenda kuangalia mambo ya mapenzi?”

“Ni lazima muangalie maudhui yenu na mpanue wigo. Kwa kuwa mna shirikisho, ni vema mkagawana maeneo ya kuigiza ili kupanua soko na mkiingiza filamu zenu sokoni, zote zipate mashabiki.”

Alisema nafasi ya tatu kwenye maudhui imechukuliwa na filamu za masuala ya utamaduni na mambo ya uchawi ambayo ni sawa na asilimia 10 huku nafasi ya nne ikichukuliwana na filamu zinazohusu mapigano ambazo ni sawa na asilimia saba. “Hizi ni chache kwa sababu zinahitaji mtaji mkubwa wakati wa kuzitengeneza na pia ni risky,” alisema.

Wakitoa maoni yao ni kwa nini tasnia ya filamu imedidimia, wasanii hao ambao waliwakilisha wenzao kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Katavi na Rukwa, walidai kwamba Bodi ya Filamu imeua tasnia hiyo kwa hiyo hawana imani na Bodi na hawako tayari kufanya nayo kazi.

Waliomba pia kuwe na taratibu za kuvutia wawekezaji kwenye tasnia hiyo, uwekwe mkakati wa haraka wa kuinua soko la filamu kupitia lugha ya Kiswahili ambayo walisema ni bidhaa adimu. Pia waliomba sera ya filamu nchini ikamilishwe haraka ili iweze kulinda maslahi ya wasanii wa filamu.

Wananchi wahimizwa kushiriki mashindano ya Hearth Marathon ili wachangie upasuaji wa moyo kwa watoto

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mashindano ya mbio za Heart Marathon zitakazofanyika siku ya jumapili 28 Aprili 2019 katika viwanja vya Coco Beach kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo leo katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI Naiz Majani.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya mbio za Heart Marathon zitakazofanyika Jumapili 28, 2019 katika viwanja vya Coco Beach kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo leo katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu kutoka Damu salama kanda ya mashariki Judith Goshashi. Picha na JKCI.

Na Zawadi Masinde- JKCI

25/04/2019 Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na mikoa jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki katika mashindano ya Heart Marathoni ili waweze kuchangia matibabu ya moyo kwa watoto. Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mashindano ya mbio hizo yatakayofanyika tarehe 28/04/2019.

Prof. Janabi alisema mtoto anaweza kuwa na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nayo hii inatokana na sababu za kurithi, mama kutokupata chanjo wakati akiwa mjamzito, unywaji wa pombe pamoja na uvutaji wa sigara. Lakini pia mtoto anaweza kupata ugonjwa wa moyo kwa njia ya mfumo wa hewa au chakula ambapo mtoto asipopata matibabu kwa wakati bakteria wanashambulia valvu za moyo.

“Kwa upande wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nao kila watoto 100 wanaozaliwa hai mmoja anatatizo la moyo. Kwa mwaka Taasisi yetu inapokea zaidi ya watoto 1000 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo na ya kuambukizwa . Kwa sasa watoto 512 wako katika orodha ya kufanyiwa upasuaji wa moyo”,.

“Mwananchi akishiriki mbio za Heart Marathoni kwa kujisajili kwa Tshs. 30,000/= au kumthamini mtoto mmoja kati ya hao 1000 kwa kumlipia gharama ya upasuaji wa Tshs. 2,000,000/= kutapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji”, alisema Prof. Janabi.

Prof. Janabi alimalizia kwa kusema lengo kuu la mashindano hayo ni kupata fedha za kuchangia matibabu ya watoto walio na matatizo ya moyo ambao wazazi wao hawana uwezo.

Naye Mkuu wa Idara ya ukusanyaji Damu kutoka Damu Salama kanda ya Mashariki Judith Goshashi aliwaomba wananchi kujitokeza siku hiyo ili waweze kuchangia damu kwa ajili ya watoto watakaofanyiwa upasuaji wa moyo. Alisema mtoto mmoja anayefanyiwa upasuaji wa moyo anatumia chupa tano hadi saba za damu hivyo basi kujitoa kwa wananchi kuchangia damu kutasaidia kuokoa maisha ya watoto watakaofanyiwa upasuaji.

Judith alisema, “Kuna baadhi ya makundi ya damu ni adimu kupatikana na yamekuwa yakituletea changamoyo pindi anapotokea mgonjwa mwenye kundi hili la damu, makundi hayo ni O-,B- na AB- . Ninawaomba wananchi wenye makundi haya ya damu waje kuchangia damu kwa ajili ya watoto wetu”.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo atakuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu .

Washiriki wote wa mashindano hayo watapewa zawadi za medali pamoja na T- shirt ambapo washindi wa kwanza hadi wa tatu kwa Km. tano na kumi watapewa fedha taslimu. Mshindi wa kwanza hadi wa kumi kwa Km. 21 kukimbia na kuendesha baiskeli watapewa fedha taslimu. Kwa upande wa watoto watakaoshiriki mbio za mita 700 mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapewa fedha taslimu.

Kauli mbiu ya mashindano hayo ni “KIMBIA SAIDIA WATOTO WENYE UGONJWA WA MOYO”,.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images