Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

MUHIMBILI KUMUAMISHIA MARIAMU RAJABU HOSPITALI YA SARATANI OCEAN ROAD

$
0
0
 Na Humphrey Shao, Michuzi TV
Jopo la Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lililokuwa likimfanyia Uchunguzi Mwanadada Mariamu Rajabu kuhusu kidonda chake cha Mgongoni limekubalina kwa pamoja kumuamishia mgonjwa huyo katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ibrahim Mkoma amesema kuwa mara baada ya jopo la madaktari wa Hospitali ya Tiafa Muhimbili kufanya uchunguzi kwa kina wameamua kumpa rufani mgonjwa huyo kwenda hospitali ya Ocean Road hili aweze kupata matibabu zaidi.

Hata hivyo waandishi wa habari walipohoji nini matokeo ya uchunguzi wa na kwanini wanamuamishia katika Hospitali ya Saratani Dk Mkoma alikataa kutoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi wake na kusema kuwa matokeo hayo ya ugonjwa huo ni siri ya Daktari na Mgonjwa kama kanuni za kitabibu zinavyohitaji.

Hata hivyo Globu ya Jamii ilipomuuliza Mariamu Rajabu juu ya ugonjwa wake alisema kuwa awezi kuzungumzia ugonjwa huo kwa sasa na hayupo tayari kuzungumzia ugonjwa wake.

Muhimbili (MNH) ilianza  kumfanyia uchunguzi Mariam Rajab kubaini chanzo cha kidonda alichonacho mgongoni. Taarifa za ugonjwa wa Mariam zilisambaa siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha binti huyo akiomba msaada wa matibabu kufuatia kidonda hicho kilichodumu kwa muda mrefu.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari  amesema hospitali hiyo imechukua jukumu la kumtibia Mariam baada ya kupata maelekezo kutoka wizara ya afya na serikali itabeba gharama zote.

 Alisema waliona ile video nakufanya juhudi za kumtafuta na hatimaye ametoka Singida na kukaa naye wodini, kwa  matibabu  yanaendelea na tayari madaktari wamechukua vipimo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

 Mariam alieleza kuwa kidonda hicho amekuwa nacho kwa muda mrefu na amekuwa akikitibia mara kwa mara ila Agosti 2018 kimefuka upya na kumsababishia maumivu makali. Mkuu wa idara ya upasuaji MNH, Ibrahim Mkoma amesema matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa ndiyo yatakayotoa mwongozo ni aina gani ya matibabu ambayo Mariam anatakiwa kupatiw

 Mwanadada Mariamu Rajabu akiwa amelala kwenye kitanda akisaidiwa  na muhudumu wa afya katika hospitali ya Tiafa Muhimbili.
Jopo la Madaktari waliokuwa wakimuhudumia Mwanadada Mariamu Rajabu aliyelala kwenye kitanda katika hospitali ya Tiafa Muhimbili.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake leo bungeni Jijini Dodoma.
 Wageni Mbali mbali wakifuatilia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Mkutano wa 15 Kikao cha 15 Kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma.

 Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Kanda Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akielezea jambo uku akisikilizwa na Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe (katikati) na Katibu wa Bunge la Jimbo la Free State, Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri ya Jarida la Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika (SCOTT Africa Journal), Ndg. Thabo Mofokeng ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kulia) akimkaribisha Katibu wa Bunge la Jimbo la Free State, Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri ya Jarida la Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika (SCOTT Africa Journal), Ndg. Thabo Mofokeng (kushoto) pale ugeni kutoka Chama cha Makatibu Mezani (SOCATT Kanda ya Afrika) wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Kanda Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai na Kulia ni Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe (katikati) na Katibu wa Bunge la Jimbo la Free State, Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri ya Jarida la Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika (SCOTT Africa Journal), Ndg. Thabo Mofokeng walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa tatu kushoto) akutana na kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Chama cha Makatibu Mezani (SOCATT Kanda ya Afrika) wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Ugeni huo ulioongozwa na Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe (kushoto kwake)
  Spika wa Bunge,  Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya asali mbili kutoka Zambia na zawadi ambayo haijafunguliwa na  Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha Makatibu Mezani (SOCATT Kanda ya Afrika) wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, walioongozwa na Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe (wa pili kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Kanda Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai

 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Afya AAR Tanzania na Mdau wa TIRA, Ndg. Violet Modechai.
Spika wa Bunge, Job Ndugaiakutana na kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA) wakiongozwa na Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo Saqware (kushoto kwake) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 33 na Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware pale ugeni kutoka Mamlaka hiyo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kwa ajili ya Ujenzi wa vyoo vya Mfano kwa ajili ya kuboresha Mazingira ya Mtoto wa kike Mashuleni. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) na Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta.
 Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Kanda Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Kanda Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe (katikati) na Katibu wa Bunge la Jimbo la Free State, Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri ya Jarida la Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika (SCOTT Africa Journal) ), Ndg. Thabo Mofokeng walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Kanda Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe (kulia) na Katibu wa Bunge la Jimbo la Free State, Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri ya Jarida la Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika (SCOTT Africa Journal) ), Ndg. Thabo Mofokeng walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Kanda Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kushoto) akimsikiliza Katibu wa Bunge la Jimbo la Free State, Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wahariri ya Jarida la Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika (SCOTT Africa Journal) ), Ndg. Thabo Mofokeng wakati wakiongozana wakielekea katika Ofisi ya Spika Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu wa Bunge la Zambia na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani Kanda ya Afrika, Ndg. Cecilia Mbwewe (kulia) Wengine ni Maafisa kutoka Bunge la Tanzania na Zambia
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)


Mchungaji kizimbani kwa kusafirisha dawa za kulevya

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
 Mchungaji Henry Ogwany (44),  raia wa Nigeria na wenzake watatu,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa zaidi ya kilogramu 19.

 Mchungaji Ogwanyi, amepandishwa kizimbani pamoja na mshitakiwa mwengine, Onyebuchi Ogbu (34), raia wa Nigeria anayeishi eneo la Msimbazi,  ambao kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi huku washitakiwa wengine aliopandishwa nao kizimbani mchungaji huyo ni raia wawili wa Lativia, Linda Mazure (21) ambaye ni mwanafunzi na Martins Plavins (20), mkandarasi na mkazi wa Lativian na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwizile.

Mbele ya Hakimu Rwizile, imedaiwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula akisaidiana na Batilda Mushi kuwa Aprili 17, 2019,  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) washitakiwa Mazure, Ogwanyi na Plavins walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa kilogram 4.87.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washitakiwa hawakiruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka  ya kusikiliza kesi huyo hadi Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) atakapotoa kibali.

Kwa mujibu wa  upande wa mashitaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili wa Serikali Batilda Mushi amedai kuwa, Ogwany na Ogbu wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Nigeria na Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Amedai, Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Msimbazi wilayani Ilala jijini humo washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya heroini zenye kilogramu 15.8.

Hakimu Shaidi amesema washitakiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kwa saba mahakama hiyo haina mamlaka na kwamba mashitaka wanayoshitakiwa nayo hayana dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Waliodaiwa kufa sasa kuibukia Mahakamani kutoa Ushahidi

$
0
0
Na Karama Kenyunko wa Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, watu wanne wanaodaiwa kuuliwa na askari polisi Mkoani Kigoma wapo hai na watafika Mahakamani kutoa ushahidi.

Mpelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Maruru amedai hayo leo Aprili 24, 2019 wakati alipofika mahakamani hapo kutoa ushahidi dhidi ya kesi ya uchochozi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ambayo imeanza  leo kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, kutoa ushahidi wake, Mururu ambae ni shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri amedai kwatu hao wanne ambao Zitto alidai kuwa walikuwa majeruhi na kupelekwa kituo cha afya Nguruka, na kwamba polisi waliwachukua na kuwaua sio kweli kwani watu hao wanne pamoja na Mganga wa Kituo cha Afya Nguruka, watakuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, amedai,  Oktoba 28, mwaka huu Zitto akiwa katika mkutano na waandishi wa habari alitoa maneno ya uchochezi ambayo yamesababisha kuwachonganisha wananchi na jeshi la polisi kwamba sio watumishi bali ni wauaji wa wananchi.

Maruru amedai baada ya taarifa hiyo walianza kufuatilia kwa kina ikiwemo kuwasiliana na SSP Mark Njela wa Kigoma ili wapate kujua hali ikoje kama ilivyotamkwa na Zitto ambapo SSP Njela alimwambia kuwa mambo yaliyosemwa ni ya uongo na dhamira ni kuchonganisha  jeshi na wananchi kwani katika kufuatilia taarifa hiyo, alienda  maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam na kukuta wananchi wakijadiliana kuhusu taarifa iliyotolewa na Zitto na kwamba walionesha kuchukizwa na taarifa hiyo.

Amedai, kufutia hayo, alirudi ofisini na kuwaita makachero wazoefu  na maofisa wa makosa ya mtandao ili kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na tulipeana majukumu ikiwemo kufuatilia na kukusanya ushahidi kuhusu tuhuma hizo na kuitisha mashahidi.’’ alisisitiza.

Aliendelea kudai kuwa kauli zilizotoka kwenye nakala ya taarifa kwa vyombo vya habari ilionesha kuwa jeshi hilo ni wauaji kwani Zitto alisema ‘Polisi wameenda kituo cha afya Nguruka na wamewachukua majeruhi wanne waliopelekwa na kuwaua’.

Pia katika taarifa hiyo ilionesha ‘polisi wakiwa kwenye operesheni hiyo wameua watu wengi sana’. Maruru alidai kwamba maneno hayo ni ya uchochezi na yanalenga kuwachonganisha na wananchi.

Shahidi huyo alidai kitengo cha makosa ya mtandao walifanikiwa kupata ushahidi wa video na walimkamata mshitakiwa na walipompekuwa walimkuta na taarifa kwa vyombo vya habari.

Katika kesi hiyo, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2019  akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki

Anadaiwa kusema, watu waliokuwa ni majeruni katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka, Polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospital kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua".

RITA KUANZA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WANAOJIANDAA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetangaza rasmi kuanza kupitia maombi ya vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu mwaka huu ambapo matarajio yao ni kuhakiki vyeti vya wanafunzi 100,000.

Kwa mujibu wa RITA ni kwamba ili mwanafunzi mwenye sifa ya kupata mkopo kwa ajili ya masomo ya vyuo vikuu anapaswa cheti chake cha kuzaliwa kufanyiwa uhakiki ili kujiridhisha na taarifa zake na baada ya kuhakikiwa majibu yanayorudishwa kwa mwanafunzi na kutumwa Taasisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Kendelea na mchakato wa kutoa mkopo.

Hivyo katika kufanikisha wanafunzi wanapata mikopo kwa wakati RITA imeamua kuanza mchakato wa kuhakikiwa vyeti vya kuzaliwa mapema wakiamini itasaidia wanafunzi hao kuwa na uhakika wa taarifa zilizomo kwenye vyeti vyao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam , Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu/ Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) Emmy Kalomba Hudson amesema uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi unaanza leo na kuendelea huku akifafanua kuwa moja ya kielelezo au kiambatanisho ambacho kinatakiwa na taasisi ya mikopo ni uthibitisho wa mwanafunzi anayeomba mikopo.

"Hivyo tumeona ni busara kuanza mchakato mapema ili wanafunzi waweze kupata mikopo. Tunajua kuna taasisi nyingi zinahusika lakini kwa upande wetu tumeona tuanze mapema. Kwanini tunahakiki? Tunajua watu ambao tunawasajili wanavyeti lakini lengo ni kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili kupata mikopo basi wapate," amesema Hudson.

Ameongeza kuwa cheti cha kuzaliwa mwenye mamlaka yenye kuthibitisha uhalali wake ni RITA,na kwa kutambua jukumu hilo wameona ni bora wakaanza mapema na kwamba gharama za kuhakikiwa Sh.3000 huku akitoa rai kwa wanafunzi au wazazi kufungua akaunti email ili kurahisisha kujaza maombi na kutuma RITA yakahakikiwe

"Wale ambao tutahakiki vyeti vyao na kuthibitisha taarifa zao tutawajibu na kisha taarifa zao kupeleka bodi ya mikopo kwa maana wanastahili kupata mkopo na wale ambao taarifa zao hazitakuwa RITA nao watajulishwa ili waangalie namna ya kufanya.

"Pia uhakiki huu mbali ya kuhakiki cheti cha mwanafunzi,tunafahamu wakati mwingine mwanafunzi anaweza kuwa amepoteza mzazi mmoja wapi au wote, na hivyo mwenye kuthibitisha cheti cha kifo ni sisi RITA," amesema na kuongeza ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa kuwa na vyeti vya kuzaliwa mapema ili kuepuka unaoweza kujitokeza mbele ya safari.


Amefafanua zaidi kuwa kuna haja ya kuanza mapema ili kufanya zoezi kuwa rahisi na kupata muda unaofaa na kwamba wanaanza leo na kama mtoto yupo shule wanajua  wazazi wanatunza vyeti, na kama hawana basi ndio muda mzuri wa kufuatilia na kwamba maombi 100,000 ndio ambayo yatahakikiwa kwa mwaka huu.

 Amesema kuwa " Ada ya uhakiki wa maombi ni Sh.3000 tu,mwaka jana tulisikia wanafunzi wametapeliwa kwenye vibanda vya Intaneti, wapo waliotozwa hadi Sh.30,000 na hiyo imekuwa kero.

Wazazi wafungue akaunti wenyewe za email ili kupunguza gharama. Wapo wengine ambao walilipa fedha na maombi yao hayakwenda. Wanafunzi waache kuzembea wajitume kwa kujaza maombi wenyewe. Zoezi hilo ni endelevu na vizuri wakaanza mapema kabla ya muda wa kuomba mikopo haujafika,"amesema Hudson

Hata hivyo amesema maombi yatumwe kwa njia ya mtandao kwani hiyo itasaidia kupitia.maombi mengi na ndani ya siku tatu wahusika watakuwa wamejibiwa huku akitoa rai kwa makatibu tawala walioko wilayani ambao wanatambuliwa na RITA kuhakikisha wanafunzi wanajaza maombi kwa njia ya mtandao kwani mwaka jana wapo ambao walijaza maombi bila kutumia mtandao na hivyo kusababisha maombi kuchelewa RITA.

Akizungumzia changamoto ambazo zilijitokeza mwaka jana wakati wa uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi, Hudson amesema kulikuwa na changamoto katika upigaji picha wa vyeti ambapo zilikuwa hazionekani kwa uharaka, wengine walikosea nywila(paswadi) hivyo hata majibu yalipotumwa wengine walichelewa kupata kwasababu ya kusahau nywila.

Pia changamoto nyingine kuna wanafunzi wengine walikuwa wazembe maana walikuwa wanajipiga selfie na kisha kutuma Rita,jambo ambalo haliko kwenye utaratibu."Changamoto nyingine wapo ambao walikuwa wamezaliwa nje ya nchi lakini nao wanakuja RITA.Hao tulikuwa tunawapa maelekezo ya namna ya kufanya.

"Kulikuwa na changamoto pia ya mtandao kuzidiwa kutokana na idadi kubwa ya waombaji.Ndio maana tumeanza mapema kuondoa changamoto hiyo.Na baada ya kuona changamoto tumeamua kuboresha mtandao wetu kwa mfano iwapo mwanafunzi atasahau nywila basi Luna sehemu ataiona," amesema Hudson.

Alipoulizwa kuhusu vyeti vyeki,amejibu ni kweli vipo kwa watu wachache ambao wamevipata kutoka kwa wahuni ambao wamekuwa wakitengeneza vyeti feki,view vya kuzaliwa au vya kielimu na vyeti vingine,na wanapobaini wanachukua hatua za kuwafikisha wahusika katika vyombo vingine vya kisheria."Ndio vipo huwa tunaona kwenye televisheni wakionesha watu wamekamatwa na mitambo ya kutengeneza vyeti.Hata hivyo vyeti vyeti vinausalama wa kutosha ."

Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa iwapo watabaini kuna mtu au watu wanatengeneza vyeti.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria Lina Msanga amesema kinachohakikiwa na RITA ni cheti cha kuzaliwa au cheti cha kifo na sio matangazo,hivyo kinachotakiwa kutumwa RITA ili kihakikiwe ni cheti.
 Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu /Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Kalomba Hudson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam wakati akitangaza kuanza uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wanaojiandaa kujiunga na masomo ya elimu ya juu ambao wanasifa za kupata mkopo
Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Haki za Kisheria kutoka RITA Lina Msanga akifafanua jambo kuhusu uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi wanaosubiri kupata uhakiki wa mkopo baada ya RITA kuthibitisha taarifa zao

 

TATIZO LANGU LILIANZIA KWENYE JIPU - MARIAM

$
0
0
Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV 
Mkazi wa Singida, Mariam Rajab Juma anayesumbuliwa na tatizo la kidonda kikubwa kilichopo sehemu ya mgongoni ameeleza kuwa tatizo hilo chanzo chake kilianzia kwenye Jipu ambalo baadae lilipasuka nakupelekea kidonda hiko. 

Mariam aliyelazwa kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) amezungumza hayo alipokuwa akihojiwa na Waandishi wa Habari hospitalini hapo. 

Mariam ameeleza kuwa tangu kufika Muhimbili ameona kuna mabadiliko makubwa, amesema kwa sasa anatembea vizuri tofauti na zamani.

"Naishukuru Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa hali niliyonayo sasa, kuna mabadiliko makubwa tangu tatizo hili lianze miezi Saba iliyopita", amesema Mariam.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma amethibitisha kuwepo kwa Mgonjwa huyo takriban wiki moja iliyopita, amesema wamefanya uchunguzi kwa Mariam nakujiridhisha kile kinachomsumbua. 

Dkt. Mkoma amesema baada ya upembuzi yakinifu kuhusu kinachomsumbua Mariam, ataendelea na matibabu katika hospitali ya Ocean Road kwa muda na baadae atafanyiwa uchunguzi tena na Jopo la Madaktari. 

Amesema baada ya uchunguzi huo, Jopo hilo la Madaktari litakaa tena kufanya tathmini kujua anaendelea na matibabu ya aina gani. 

Kuhusu tatizo zaidi lilonalomsumbua Mariam, Dkt. Mkoma amesema suala hilo litabaki kuwa siri kati ya Madaktari na Mgonjwa.

Hata hivyo, Dkt. Mkoma ametoa wito kwa Wananchi kuwa na tabia yakuchunguza afya mara kwa mara, amesema inapokea kuwa na kidonda chochote kwenye kovu la zamani lazima kufanya kipimo kujua ni aina gani ya kidonda.

RAIS DKT. MAGUFULI AMEWASILI NCHINI MALAWI KWA ZIARA YA KISERIKALI YA SIKU MBILI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka ndani ya ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa na Mizinga 21 ya Rais mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Malawi kwa heshima yake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Malawi waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Prof. Arthur Peter Mutharika wakiwasalimia baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika, Mama Janeth Magufuli pamoja na Prof. Gertrude Mutharika kabla ya kuweka mashada ya maua katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi Lilongwe nchini Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa wameshika mashada ya maua tayari kuyaweka katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiweka mashada ya maua katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi. April 24, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mara baada ya kuweka mashada ya maua katika kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi, Prof. Bingu Mutharika,katika eneo la Bunge la Malawi. April 24, 2019.

Kaburi la Rais wa Tatu wa Malawi Hayati Prof. Bingu Mutharika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Bunge Malawi (nyuma yake ni mkewe Mama Janeth Magufuli akishuhudia) April 24, 2019.

MHANDISI MTIGUMWE AKIAGIZA KIKOSI KAZI CHA CARD TANZANIA KUKAMILISHA MPANGO KAZI WA KUENDELEZA ZAO LA MPUNGA KABLA YA JUNI 2019

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye wa kikao cha kazi cha maandalizi ya uandaaji wa Mpango mkakati wa pili wa kuendeleza uzalishaji wa zao la Mpunga nchini (National Rice Development Stratergy II - NRDS II) kilichofanyika katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro, leo tarehe 24 Aprili 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kazi cha maandalizi ya uandaaji wa Mpango mkakati wa pili wa kuendeleza uzalishaji wa zao la Mpunga nchini (National Rice Development Stratergy II - NRDS II) kilichofanyika katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro, leo tarehe 24 Aprili 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Kikosi Kazi cha CARD kwa kushirikiana na Mshauri wa CARD, kimeagizwa kuandaa rasimu ya awali ya mkakati wa kuendeleza zao la mpunga nchini mapema kabla ya June, 2019.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 24 Aprili 2019 wakati wa kikao cha kazi cha maandalizi ya uandaaji wa Mpango mkakati wa pili wa kuendeleza uzalishaji wa zao la Mpunga nchini (National Rice Development Stratergy II - NRDS II) kilichofanyika katika Hoteli ya Edema Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa ili kikamilishe hiyo kazi lazima kuwe na takwimu sahihi zinazoonyesha hali halisi ya uzalishaji wa mpunga nchini. ” Ni lazima kutoa takwimu zenye uhakika zitakazowezesha mpango wa pili wa kuendeleza zao la mpunga kukamilika ipasavyo, Timizeni wajibu wenu mliopewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais wetu mpendwa, Mhe Dr. John Pombe Joseph Magufuli” Alikaririwa Mhandisi Mtigumwe

Alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa takwimu hizo kikosi kazi hicho kitaanza kuandika rasimu ya mpango mkakati wa kuendeleza zao la mpunga, awamu ya pili kwa kuzingatia kuwa CARD wameazimia kuongeza uzalishaji mara mbili zaidi hivyo Tanzania inapaswa kuzalisha mara mbili zaidi ya mwaka jana.

Alilitaja lengo kuu la Mpango Mkakati wa Tanzania katika uzalishaji wa zao la Mpunga nchini, kuwa litakuwa ni kuzalisha kutoka tani 2,219,628 za sasa na kufikia tani 4,500,000 ifikapo mwaka 2030.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Mpango mkakati wa kuendeleza zao la Mpunga unaandaliwa kwa kushirikiana na "Coallition for African Rice Development" (CARD), ambapo makao makuu yake yako Nairobi, nchini KENYA. Tanzania ni moja kati ya chi 32 ambazo ni wanachama.

Pamoja na CARD kumaliza kipindi cha awamu ya kwanza, mwaka 2018, nchi wanachama pamoja na wafadhili walikutana Octoba 2018 huko Tokyo, Japan ambapo walifanya tathmini ya awamu ya kwanza na ilionyesha kuwa lengo lilifikiwa.

Aidha, walikubaliana kuanzisha awamu ya pili ya CARD, kuanzia 2018 hadi 2030. Awamu hii inatarajiwa kuzinduliwa nchini Japan, mwezi wa Agosti, 2019. Moja ya jambo muhimu na linalozingatiwa ili kila nchi ipate nafasi ya kupata miradi itakayonufaika na CARD, ni kuwa na Mpango Mkakati wa Kuendeleza zao la Mpunga Awamu ya Pili (2018-2030). Lengo kuu la CARD, awamu ya pili ni kuongeza uzalishaji wa mpunga kutoka tani 28 milioni (zilizofikiwa katika awamu ya kwanza mwaka 2018) hadi tani 56 milioni mwaka 2030 kwa nchi zote wanachama.

Mtigumwe alisema kuwa kama ilivyofanyika kwa nchi nyingine, na kwa kuzingatia kwamba zao la mpunga ni mojawapo ya zao muhimu la chakula na biashara linalozalishwa takribani mikoa yote hapa nchini, mwaka 2008 Wizara ya Kilimo iliandaa pia Mpango Mkakati wa Kuendeleza zao la Mpunga (NRDS I). Mpango huo ulikuwa ni wa miaka 10 na ulikamilika mwaka 2018 ambapo ulitoa matokeo chanya ikiwemo kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga kutoka tani 899,000 mwaka 2008 hadi tani 2,219,628 mwaka 2018.

CARD ni Muungano wa Wabia ambao hupokea maandiko mbalimbali ya miradi ya uzalishaji na usindikaji wa mpunga  na kuyatafutia fedha  kwa ajili ya utekelezaji, na huongozwa na Sekretariati ya CARD, iliyoundwa na Wabia wanachama. Hadi sasa kuna Wabia 23. Miongoni mwa Wabia hao, kama alivyokwishawataja Mkurugenzi ni JICA, Benki Kuu ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na wengineo.

LUKUVI ATATUA MGOGORO WA WAFUGAJI WA KIMASAI NA WAWEKEZAJI MASHAMBA MONDULI

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto), Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Arusha Miundombinu Mahmoud Mansour (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TANFOAM Riaz Lemtula (katikati) na Mshauri wa TANFOAM Victor Njau wakijadiliana na namna ya kumega eneo kwa ajili ya wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Lengiroliti wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha wakati Waziri wa Ardhi alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya kijiji hicho na Mwekezaji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuviu akijadiliana na wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Lengiroliti wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi kati ya kijiji hicho na mwekezaji wa Shamba TANFOAM. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lengiroliti na Naaralami wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya vijiji hivyo na wawekezaji wa mashamba TANFOAM NA na SLUIS. Kulia ni Mkurugenzi wa TANFOAM Riaz Lemtula (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).

Na Munir Shemweta, WANNM MONDULI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemaliza mgogoro uliodumukwa muda mrefu baina ya wananchi wa vijiji vya Lengiloriti na Naalarami vilivyopo wilayani Monduli mkoani Arusha na wawekezaji wa mashamba yanayomilikiwa na TANFOAM na SLUIS kwa kuamua kumega sehemu za mashamba na kuwapatia wananchi wa vijiji hivyo.

Lukuvi alifikia umauzi huo baada ya kukutana na pande zote mbili jana tarehe 23 Aprili 2019 wilayani humo na kujadiliana kwa kina kwa takriban saa tano kwa lengo la kupata suluhu ya mgogoro huo ambao umeleta sintofahamu kati ya wananchi wa vijiji hivyo na wawekezaji wa mashamba.

Katika makubaliano hayo iliamuliwa ekari kati ya 850 hadi 900 zimegwe kutoka kwa muwekezaji TANFOAM na kugawiwa kwa kijiji cha Lengiloriti  wilayani Monduli  kutoka shamba namba 44 lenye ukubwa wa  ekari 3098. Aidha, upande wa muwekezaji SLUIS jumla ya ekari 2000 za muwekezaji zimetolewa kwa kijiji cha Naaralami, NAFCO, Lokisari na Tukusi ambapo sasa muwekezaji atabaki na aekari 2217 badala ya 4,217 alizokuwa nazo awali.

Kwa mujibu wa Lukuvi, ardhi iliyomegwa na kurudishwa katika vijiji hivyo itakuwa chini ya mamlaka ya kijiji ambacho ndicho kitakuwa na jukumu la kuigawa upya kwa wananchi wa vijiji husika na baadaye kupangwa matumizi bora ya ardhi.

Akizungumzia kijiji cha Lengiloriti, Waziri wa Ardhi aliwataka wananchi wenye Maboma yaliyokuwa ndani ya eneo la shamba la muwekezaji TANFOAM kuhamia eneo jipya walilotengewa katika kipindi cha miezi mitatu ili kupisha muwekezaji kuendelea na shughuli za kilimo na kutotekelezwa kwa aina yoyote agizo hilo kutaifanya serikali kuchukua hatua.

Maboma yaliyohamishwa ni pamoja na linaloongozwa na mwenyekiti wa kijiji cha Lengiloriti Baraka Lemai. Maboma mengine ni la Kaay Rao, Remi Paraleti, Kelemo Kipara, Yamat Miriliali, Bete Kabulua, Barik Simon, Rais Ramadhani, Ramadhani Hamis na Lakalai Olodo  ambapo Waziri wa Ardhi alisisitiza wamiliki wa Maboma hayo kupewa kipaumbele wakati wa kugawiwa ekari zilizotolewa na kiasi kitakachobaki wapatiwe wananchi wengine.

Aidha, ameagiza kuanzia wiki hii timu ya upimaji ardhi mkoani Arusha iende ktika eneo hilo kwa ajili ya kuweka mipaka/alama za kudumu  ili kuepuka uvamizi mwingine unaoweza kutokea na kuagiza wawekezaji na wananchi wa vijiji vilivyopatiwa ekari hizo kuchangia fedha kwa ajili ya upimaji ambapo muwekezaji na wananchi walikubali kutoa milioni tano kwa ajili ya upimaji.

Kuhusu mgogoro wa muwekezaji SLUIS, Lukuvi alisema muwekezaji huyo amekubali  kutoa ekari 520 kwa kijiji cha Naaralami pamoja na ekari 300 kwa ajili ya kupitishia mifugo ya wananchi wa kijiji hicho huku ekari 513 zikitolewa kwa NAFCO, 366 kwa Lokisari na ekari 301 kwa kijiji cha Tukusi.

Lukuvi alisema serikali inawaeshimu sana wawekezaji wa sekta ya ardhi kwa kuwa wanalipa kodi inayosadia utoaji wa huduma za jamii huku wananchi nao wakipata ajira na kusisisitiza kuwa wawekezaji wanaomiliki mashamba kisheria serikali itawalinda na kuonya baadhi ya viongozi wa vijiji kujigawia maeneo bila ya kushirikisha wananchi wa vijiji husika.

‘’Nimekuja kusuluhisha mgogoro siyo kunyanganya wawekezaji mashamba, wawekezaji wamekubali kupunguza mashamba yao na hayo mashamba siyo mali ya wananchi wanaoishi katika maboma yaliyohamishwa bali ni mali ya kijiji ambacho kitakuwa na jukumu la kugawa maeneo hayo’’ alisema Lukuvi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa, baada ya makubaliano ya pande zote mbili anategemea kila upande utaheshimu maamuzi yaliyotolewa na mtu yoyote atakayekiuka basi serikali ya mkoa itachukua hatua kali dhidi yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanfoam Riaz Lemtula amepongeza jitihada iliyofanywa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi mpaka kufikia muafaka wa suala hilo na kuahidi kutekeleza makubaliano waliyoafikiana kwa lengo la kuleta maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Lengiroliti Baraka Lemai alimshukuru Waziri wa Ardhi kwa niaba ya Kijiji chake kwa kazi anayoifanya ya kutatua migogoro ya ardhi na kuahidi kushirikiana na wawekezaji waiokubali kumega maeneo yao kwa ajili ya kijiji.

Wawekezaji wanaomili mashamba katika vijiji hivyo wamekuwa wakiendesha mashamba yao katika shughuli za kilimo ambapo hulima mazoa ya Maharage, Mtama, Ngwara na mahindi na kusafirisha mazo hao katika nchi za Sweden, Canada na Uholanzi.

SERIKALI YAKABIDHI SHILINGI BILIONI 688.615 KWA MKANDARASI ANAYEJENGA MRADI WA UMEME WA MTO RUFIJI, TANESCO WAFURAHISHWA ....WATOA NENO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SERIKALI ya Tanzania imekabidhi hundi ya fedha yenye thamani ya Sh. Bilioni 688.615 kwa mkandarasi wa Kampuni ya Arab Contractors kutoka nchini Misri anayejenga mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP).

Fedha hizo ni malipo ya awali kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo huku ikielezwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kutoa fedha nyingi kiasi hicho tena kwa mkupuo kwa ajili ya kulipa malipo ya awali kwa ajili ya mradi huo.

Wakati Serikali inakabidhi fedha hizo kwa mkandarasi, wa ujenzi huo baadhi ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), Mkurugezi Mtendaji wa TANESCO, Mwakilishi wa Benki Kuu(BoT) pamoja na viongozi wa Wizara ya Nishati walikuwepo kushuhudia tukio hilo.

Akizungumza baada ya kukabidhi hundi hiyo leo Aprili 24, 2019 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James amesema Wizara hiyo kwa niaba ya Serikali imekabidhi fedha hizo kwa mkandarasi wa kampuni ya Arab Contractors na fedha nyingine zilizobaki zitaendelea kulipwa hatua kwa hatua kulingana na maendeleo ya ujenzi.

" Hazina kwa niaba ya Serikali tumekabidhi fedha Sh.bilioni 688.615 kwa mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji ni mradi wa kihistoria kwani ni utekelezaji wa wazo la muasisi wa Taifa hili Mwalim Julius Nyerere aliyelitoa mwaka 1971 na Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kutekeleza kwa kuanza ujenzi.

"Mradi huu utakapokamilika utakuwa na megawati 2,115 ambazo zitazalishwa na kwa sasa nchi yetu kwa ujumla wake inazo mewagati 1, 602 kutoka vyanzo vyote vilivyopo nchini lakini kwa mradi huu peke yake tutakuwa tumeongeza megawati zaidi ya 2000,"amesema Katibu Mkuu James.

Amefafanua mradi huo utakamilika baada ya miezi 36 na fedha za mradi zinatolewa na Serikali kwa asilimia 100 Kwa umuhimu wa mradi huu ndio maana Serikali imetoa fedha nyingi kwa mkupuo. "Hakuna mradi mwingine wowote ambao fedha za awali zimetolewa nyingi kiasi hicho tena kwa mara moja.Miradi mingi fedha zake hazikuwahi kuzidi Sh.bilioni 50,"amesema James.

Amesisitiza mradi huo utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu hasa kwa kuzingatia muelekeo wa Serikali ni kuwa na Tanzania ya viwanda ambapo nishati ya umeme wa uhakika inahitajika zaidi ili kuvutia wawekezaji huku akieleza faida nyingine ya mradi huo ni kwamba utakapokamilika hata bei ya umeme itapungua.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa wakati wa ujenzi wa mradi huo ajira zitaongezeka kati ya 4500 hadi ajira 6000 wakati wote wa ujenzi, hivyo ni fursa kwa wananchi wa Tanzania. Pia eneo la mradi kutakuwa na uhakika wa maji kwa ajili ya umwagiliaji kutokana na maji ya maporomoko hayo.

"Pia shughuli za utalii katika pori la Selous na faida nyingi ujenzi wa mradi huo ni kwamba hakutakuwa na mafuriko kwani maji yatajengewa kuta imara na hivyo kzuia mafuriko. Faida nyingine mradi utakapokamilika na umeme kusambaa sehemu kubwa ya nchi utasaidia utnzaji wa mazingira,"amesema James.

Hata hivyo amefafanua kiasi cha fedha ambacho kimetolewa hadi sasa kwa ajili ya mradi huo wa umeme wa maporomoko ya Mto Rufiji ni Sh.trilioni moja kati ya Sh.trilioni sita ambazo zinahitajika kuukamilisha mradi huo. Pia amesema Serikali kupitia hazina imejipanga kufanikisha mradi huo wa kimkakati na wamejiandaa kikamilifu katika kuutekekeza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dk.Hamis Mwinyimvua ameongeza kuwa Aprili 15, mwaka huu Benki ya CRDB na UBA walitoa dhamana ya fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi huo wa Rufiji. "Kutolewa kwa dhamana hizo kuliwezesha kuanza kwa baadhi ya hatua kwa mkandarasi Kwa mujibu wa mkataba asilimia 70 ni fedha zitakuwa za kigeni na asilimia 30 ni fedha za ndani.

Fedha za kigeni tayari imelipwa kwa asilimia 70 na ndani zitaendelea kulipwa.
"Mkandarasi kama ambavyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango alivyosema , tunakuhakikishia fedha zipo na hivyo asiwe na wasiwasi.Malipo ya awali kwa ajili ya mradi huu ni muhimu na tayari yamelipwa, hivyo ni matarajio yetu sasa vifaa vyote vinavyotakiwa kwa ajili ya kuanza ujenzi vitakwenda eneo la mradi,"amesema Dk.Mwinyumvua.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Dk. Alexandra Kyazuri amesema Tanesco wamefurahi sana na kwamba umeme uliopo ni megawati 1600 na sasa kupitia mradi huo zitapatikana megawati 2000

"Tunaishukuru Serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuamua kuanza kwa mradi huo.Kwa siku ya leo hii TANESCO hatutaki kuwa na maneno mengi zaidi ya kuwa na furaha sana,"amesema Dk.Kyaruzi .
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua akionyesha Hundi yenye thamani ya Tsh.Bilioni 688 fedha zilizolipwa kama malipo ya awali  kwa Mkandarasi(Arab Contructors) kwa  utekelezaji wa Mradi wa kufua umeme mto rufiji, kulia ni Mwenyekti wa Bodi  TANESCO , Alexander Kyaruzi  na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka.
 

NIDA, TCRA na Makampuni ya Simu nchini kuwezesha zoezi la uandikishaji wa watumiaji wa simu kwa kutumia Namba za Utambulisho wa Taifa

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Makampuni ya Simu nchini, itawezesha zoezi la uandikishaji wa watumiaji wa simu nchini kwa kutumia Namba za Utambulisho wa Taifa au Kitambulisho cha Taifa.  Zoezi la Uandikishaji wa laini za simu linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 01-Mei-2019. Mazoezi ya majaribio ya zoezi hili yamefanyika katika baadhi ya Mikoa na Taasisi na kuonyesha mafanikio.

NIDA tayari imesajili asilimia 88 ya watu wote wanaostahili kusajiliwa kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa nchi nzima. Zoezi la Utambuzi na usajili ni endelevu, hivyo asilimia 12 ya lengo la usajili lililobaki linaendelea kutekelezwa katika wilaya zote nchini kwa kusajili watu ambao hawakusajiliwa kwenye zoezi la usajili wa umma (Mass Registration) na ambao wamekisha umri wa miaka 18, ambacho ni kigezo cha kisheria kinachoruhusu mwananchi kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa.  Vile vile usajili wa umma unafanywa tena katika mikoa ambayo watu wengi hawakusajiliwa katika usajili wa awali. Mikoa hiyo ni pamoja na Dar es salaam, Tanga, Pwani na Kigoma.

NIDA tayari imetengeneza Namba za Utambulisho wa Taifa Milioni 12, sawa na asilimia na 59 ya usajili uliofanyika. Zoezi la uhakiki, kuchakata na kutengeneza Namba za Utambulisho wa Taifa linaendelea kutekelezwa kwa kasi usiku na mchana. Aidha tunatoa rai kwa wale wote ambao wamejulishwa kuwa vitambulisho vyao vipo tayari wafike Ofisi za NIDA au Ofisi za Serikali za Mitaa walipo jiandikishia kuvichukua. Vitambulisho vya Taifa vinaendelea kuzalishwa na kusambazwa kwa wananchi. Namba za Utambulisho wa Taifa zitatumika katika usajili wa Namba za simu na matumizi mengine. Hivyo wale ambao tayari wana Namba za Utambulisho wa Taifa wazitumie kujisajili wakati vitambulisho vinazalishwa.

Wananchi mnaweza kupata Namba ya Utambulisho wa Taifa na huduma zingine zitolewazo na NIDA kwa njia zifuatazo:-
a.Kupiga namba * 152 *00#; chagua Ajira na Utambuzi; Chagua NIDA
b.Kupakua nakala ya Kitambulisho cha Taifa kwa kutembelea tovuti: https://services.nida.go.tz/nidportal/NID_Copy.aspx au tovuti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.
c.Kupiga simu huduma wateja; 0673 333444, 0743 202020, 0743 201020, 
d.0759 102010, 0765 201020. 
e.Kufika ofisi za NIDA ya Wilaya ilyopo karibu.

Ni Muhimu kwa Wananchi wote wenye sifa za kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa kufanya hivyo sasa pasipo kusubiri mpaka wanapokuwa na hitaji la haraka kwani uhakiki wa taarifa zako lazima ufanyike kabla ya utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Taifa na baadae kitambulisho cha Taifa.

“Utambulisho wa Taifa kwa Maendeleo na Ustawi wa Nchi Yetu”


Imetolewa na

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
23 APRILI, 2019.

MAMLAKA HALI YA HEWA YAWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KUFUATIA TAARIFA ZA UJIO WA KIMBUGA KENETH

$
0
0
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa na ushauri unaotolewa na mamlaka hiyo ili kupunguza athari zinazowezeza kujitokeza endapo kutakuwa na uwepo wa kimbunga Kenneth.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Aprili 24, 2019 Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TMA Tanzania Dkt. Pascal Waniha amesema wanatoa ufafanuzi huo ikiwa ni moja ya njia ya kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza.

Kwa Mujibu wa Dkt Pascal Waniha kimbunga Kenneth kinatarajiwa kuambatana na upepo mkali wa kasi ya kilometa 80 kwa saa ambacho kitaathiri zaidi katika maeno ya Mtwara, Lindi Pwani na maeneo jirani ya mikoa hiyo kwa umbali wa kilometa 500.

Amesema, Kimbunga Kenneth kilichopo eneo la kaskazini magharibi mwa kisiwa cha Madagascar kinaambatana na mvua kubwa na upepo mkali huku eneo la pwani ya Kusini yaani Lindi na Mtwara kinatarajiwa kufikiwa na hali hiyo.

"Kimbunga hicho kinaendelea kutawala mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini, hivyo kisababisha ongezeko la mvua zinazoambatana na ngurumo za radi pamoja na upepo mkali kadri kinavyokaribia maeneo ya ukanda wa pwani", amesema DkWaniha.

Ameongeza, kama kimbunga cha Kenneth kitaingia nchi kavu kwa nguvu inayotarajiwa baei madhara makubwa kwa maisha ya watu na Mali yanaweza kutokea ikiwa ni pamoja na mtawanyiko mkubwa wa mafuriko, uharibifu wa miundombinu, kuongezeka kwa kina cha Maji baharini katika kipindi kifupi, kuathirika kwa shughuli za usafirishaji kwa njia ya anga, Maji na hata nchi kavu.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Waniha amebainisha athari ambazo zinaweza kujitokeza ikiwemo mafuriko na uharibifu wa mali na makazi .

Katika hatua nyingine Dkt Waniha amebainisha sababu za vimbunga vinavyotokea maeneo mbalimbali ya dunia kupewa majina hususan ya binadamu ambapo amesema kuwa majina vinapewa kutokana na wadau wanaokutana kujadili masuala hayo ya vipunga ambap Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinashiriki katika kujadili masuala hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini, TMA, Dkt. pascal Waniha akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uwepo wa Kimbunga Kenneth, kinachotarajiwa kutokea April 26,2019 na Athari zake na kueleza jinsi ambavyo wananchi wanavyotakiwa kuchukua tahadhari ikiwa ni moja ya njia ya kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza.

Wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong nchini China kuja Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kambi maalum

$
0
0
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godfrey Mbawala akizungumza na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Na Zawadi Masinde - JKCI

24/04/2019 Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong nchini China wanatarajia kuja nchini mwezi wa nane mwaka huu kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya matibabu ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Makubaliano hayo yamefikiwa leo katika kikao cha pamoja cha viongozi kutoka Hospitali hiyo na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kilichofanyika jijini Dar es Salaam..

Akizungumza katika kikao hicho Kiongozi wa msafara huo Wang Zhifeng alisema wataalamu hao ambao watakuja nchini watafanya upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua pia watabadilishana ujuzi wa kazi na wenzao wa JKCI “Wataalamu wetu kutoka Hospitali ya Shandong wakija hapa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete watakuja na vifaa tiba ambavyo watavitumia katika upasuaji watakaoufanya. Pia mtatuambia ni vifaa gani vingine ambavyo mnavihitaji ili wataalamu wetu watakapokuja waje navyo”, alisema Zhifeng.

Aliendelea kusema kuwa kabla ya kuja kwa wataalamu hao hapa nchini kutaanza na program ya madaktari, wauguzi, wataalamu wa usingizi, mafundi sanifu wa moyo na Wahandisi wa vifaa tiba kwenda katika Hospitali hiyo kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi ya magonjwa ya moyo na mashine za moyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliwashukuru viongozi hao kwa kutembelea Taasisi hiyo na kusema kuwa kuja kwa wataalamu hao ni matokeo ya mkataba wa mahusiano uliosainiwa mwezi wa nane mwaka jana.

Makubaliano yaliyosainiwa katika mkataba huo ni kutolewa kwa mafunzo ya muda mfupi kwa madaktari, wauguzi, mafundi sanifu wa moyo na wahandisi wa vifaa tiba, kujenga jengo jipya la Taasisi hiyo, kutoa msaada wa vifaa tiba na kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo ambazo zitasaidia kuwajengea uwezo wataalam wa hapa nchini.

Naye Mratibu wa ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta ya Afya Dkt. Ligile Vumilia alisema makubaliano yaliyofikiwa katika kikao hicho ni lazima yafanyike kwa wakati na kwa manufaa ya nchi kwani hakuna Taasisi itakayotoa matibabu ya moyo zaidi ya wataalamu waliopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Hospitali kuu ya jimbo la Shandong inautaalamu wa hali ya juu wa kutibu magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na kufanya upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua ambapo kwa mwaka 2018 ilifanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 85,000.
Daktari wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China anayejitolea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zhao Lijian akiwaelezea madaktari wenzake kutoka China namna ambavyo anatoa huduma ya matibabu ya moyo kwa watoto walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo na kuahidi kushirikiana na taasisi hiyo kuboresha sekta ya afya ikiwemo afya ya moyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (katikati) akipokea zawadi ya picha ya Shandong kutoka kwa kiongozi wa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China Wang Zhifeng walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam na kuahidi kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kubadilishana ujuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi katika picha ya pamoja na menejimenti ya taasisi hiyo na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika sekta ya afya ikiwemo magonjwa ya moyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akifafanua jambo alipokua akizungumza na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Angela Muhozya akielezea namna idara ya upasuaji inavyofanya kazi alipokua akizungumza na baadhi ya madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: JKCI.

Radi Yauwa Watu Watano Wa Familia Moja

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Watu Watano wa Familia moja katika kijiji cha Isonge Kata ya Sikonge Mkoani Tabora wameuawa na watatu kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na Mvua na Upepo  mkali 

Tukio hilo lililoibua simazi kubwa limetokea usiku wa saa tano  katika kijiji hicho

Nae kaimu Mathew Sipemba ni kaimu Mganga Mfawidhi Wilaya ya Sikonge amesema alipata taarifa hiyo kutoka polisi juu ya tukio hilo na kukuta watu Watano walikuwa tayari wamepoteza maisha

"Ajali ya radi sio nzuri ni kama moto watu hawa wamejikuta wanavuta hewa ya harufu kali na kuunguza mapafu jambo ambalo limepelekea kupoteza maisha kwa watu hawa"Amesema Sipemba

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishina msaidizi Emmanuel  Nley amesema Radi hiyo ilisababisha ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala familia hiyo kupasuka na kusababisha vifo hivyo
"Nyumba Ilikuwa imejengwa kwa udongo na makuti na kuezekwa kwa nyasi Mvua iliponyesha  ilisababisha ukuta kupasuka na kupelekea tukio hilo kutokea "Amesema Nley

Kamanda Nley amesema katika tukio hili waliopoteza maisha ni Mhindi Peter, Vailleth Juma, Gress Juma Kulwa Lukanya na Nyanzobe Juma

Peter Nzalalila ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge amesema tukio hili lkmeibua simanzi kubwa na amewataka Wananchi wa eneo hilo kuacha kuhusisha tukio hilo na Imani za kishirikina.

CHAGUENI VIONGOZI WENYE UWEZO WA KUTATUA KERO ZENU -RC MAKONDA

$
0
0


*Akagua mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani Mbezi Louis, aridhishwa na kasi

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MEYA wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob leo amekuwa na wakati mgumu baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumtolea uvivu Meya huyo kwa kile kilichoelezwa ni kukosa nidhamu kwa kudanganya wananchi kuwa yeye ndio amefanikisha mradi wa ujenzi wa Kisima cha maji Kata ya Mbezi Makabe wakati Rais Dkt.John Magufuli ndiye aliyetoa fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni 611 kwa ajili ya kumaliza kero za maji kwa wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati wa mwendelezo wa ziara ya ukaguzi miradi ya Maendeleo Mkoa wa Dar es salaam ambapo Makonda ameshangazwa kuona Meya anakijinadi mbele ya wananchi na viongozi kuwa yeye ndiye aliyefanikisha upatikanaji wa fedha hizo na ndio aliyeweka saini badala ya kumshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa  kutoa fedha hizo.

 Makonda amesema kitendo hicho ni utovu wa nidhamu kwa viongozi wanaotoa fedha kwa ajili ya kutatua kero za wananchi ambapo amemtaka Meya huyo kuwa na shukrani kwa viongozi bila kujali itikadi za kisiasa.

Mradi wa ujenzi wa kisima cha Maji Mbezi Makabe unagharimu zaidi ya Shilingi Million 611 zilizotolewa na Rais Magufuli na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya Wakazi 75,000.

Wakiwa katika ujenzi wa ofisi za Manispaa ya Ubungo Meya Jacob amewahimiza wasimamizi wa mradi huo ambao ni wakala wa majengo nchini (TBA) kukamilisha mradi huo kwa wakati kabla ya mwaka kuisha na wao kama viongozi watasimamia hilo.

Wakati huo huo Makonda ametembelea ujenzi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo Mikoani na nchi jirani mradi unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 50 na hadi kufikia Machi mwaka huu ulikua umekamilika kwa asilimia 12.5.

Akiwa katika mradi huo Makonda amehimiza kuzingatia ushirikishwaji wa wazawa katika miradi hiyo mikubwa ili waweze kunufaika zaidi na hata malighafi zinazotumika katika ujenzi zitumike zile zinazozalishwa nchini ili kuongeza kipato kwa wananchi na taifa zaidi.

Akiwa Wilayani humo RC Makonda ametembelea miradi ya ujenzi wa kituo kipya cha mabasi, ujenzi wa ofisi za Manispaa, ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na mradi wa maji kupitia kisima kinachojengwa Mbezi Makabe.

Waziri wa Afya ashiriki kwenye ungawaji wa vyandarua ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

$
0
0

Waziri wa Afya ashiriki kwenye ungawaji wa vyandarua ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,amesema kuwa Serikali imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.

Hayo ameyasema leo wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya ya Dodoma.

Aidha,amesema kuwa halmashauri kutenga fedha za ndani kwa ajili ya kununua viuwadudu ikiwa ni katika kupambana na maambukizi ya Malaria katika maeneo yao.

Waziri Ummy amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 2 ya utawala wa Rais John Magufuli, Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia 50 kutoka wastani wa asilimia 14 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 7.

Hata hivyo amesema kuwa serikali imekuwa na mikakati mingi ya kupambana na maambukizi wa ugonjwawa malaria ambayo yamekuwa ikiuwa Watanzania wengi kuwa mbali na kugawa vyandarua pia wanapulizia dawa katika mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi.

”Serikali imenunua takribani lita 60,000 ya viuawadudu kwa ajili ya kuua mazalia ya mbu na kuzigawa katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya malaria kama vile Mkoa wa Kagera, Geita, Kigoma, Lindi na Mtwara lakini pia niwaombe wananchi kutunza mazingira ili kujiepusha na mbu waenezao malaria,” amesisitiza Mwalimu

Aidha, Mwalimu alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 angalau wajawazito 80 kati ya 100 waweze kuhudhuria kiliniki angalau mara nne hivyo kutoa fursa ya kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwamo malaria.

Kwa upande wake mratibu wa ugonjwa wa malaria mkoa wa Dodoma, Fransis Bujiku amesema kuwa Mkoa huo umefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 1 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 0.6 kwa sasa.
Bujiku amesema kuwa kwa pamoja wamefanikiwa kwa kutuna mazingira ikiwa ni pamoja na kunyunyiza dawa ya kuua mbu kipindi cha masika na kufukia madimbwi yote yanayotuamisha maji pamoja na kuwahamasisha wananchi kulala kwenye vyandarua.

Siku ya malaria duniani inafanyika kesho ambapo kitaifa itafanyikia mkoani Lindi ikiwa na kauli mbiu isemayo Ziro malaria inaanza na mimi .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akionesha nchandarua kwa akina mama wajawazito (hawapo pichani) wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwapongeza baadhi ya wanaume ambao waliwaleta watoto klinik wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimia na baadhi ya viongozi wa wilaya ya mkoa wa Dodoma alipowasili kwa ajili ya kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali hiyo iliyopo Makole jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa na ambaye ni mratibu wa Malaria mkoa wa Dodoma, Francis Bujiku,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma
Sehemu ya akina mama wajawazito wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.

WIZARA YA KILIMO KUKUZA UZALISHAJI MPUNGA MPAKA TANI MILIONI 4.5 IFIKAPO MWKA 2030…

$
0
0
Katibu mkuu wizara ya kilimo mhandisi mathew mtigumwe amekitaka kikosi kazi kinachojihusisha na uandaaji wa mpango mkakati wa kuendeleza uzalishaji wa zao la mpunga nchini kuhakikisha kinaanda rasimu itakayowezesha uzalishaji wa zao hilo kukuwa mara mbili zaidi kutoka tani milioni 2.2 hadi kufikia tani 4.5 ifikapo 2030.
Akizungumza na wataalam hao na wadau kutoka taasisi binafsi katika katibu mkuu mtigumwe amesema kufuatia wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuanzisha mpango mkakati wa kuendeleza zao la mpunga yaani national rice development strategy (nrsd) 1 mwaka 2008 kuwa na matokeo chanya ya kuongeza uzalishaji wa mpunga kutoka tani laki  899,000 hadi kufikia tani milioni 2.2 mwaka 2018 ambapo ili kukuza zaidi uzalishaji imeanzishwa nrds 2 itakayokwenda mpaka mwaka 2030 huku lengo likiwa ni kufikia tani za mpunga milioni 4.5…
"Mpango huu utatekelezwa kwa muda was miaka 12 kuanzia mwaka 2018 had I mwaka 2030 na tayari maandalizi Yake yalianza mwaka 2018 kwa kuanzia kuainishwa takwimu zinazohitajika" amesema mtigumwe.
Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho  joseph lubiloh, amesema kuwa matarajio waliyonayo mara baada ya kukamilika kwa mpango wa awamu ya pili na hadi sasa kikosi hicho kimefanikisha kukusanya takwimu kamili za kufanikisha mpango huo huku wadau wengine wakifafanua mipango iliyopo katika kufanikisha mpango huo kuwa ni kushirikiana na serikali kukamilisha juhudi hizo.
 Katibu mkuu wizara ya kilimo mhandisi mathew mtigumwe akizungumza jambo na wanakikosi kazi pamoja na wadau mbalimbali.
 kikosi kazi kinachojihusisha na uandaaji wa mpango mkakati wa kuendeleza uzalishaji wa zao la mpunga nchini pamoja na Katibu mkuu wizara ya kilimo mhandisi mathew mtigumwe aliyekaa katikati
 wadau mbalimbali na kikosi kazi kinachojihusisha na uandaaji wa mpango mkakati wa kuendeleza uzalishaji wa zao la mpunga nchini

VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha

Tatizo la ajira kwa Vijana ni changamoto kubwa nchini na ulimwengu mzima kwa ujumla, hivyo Vijana wametakiwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali zenye heshima na staha.

Hayo yamebainishwa katika mahafali sita ya kidato cha sita ya shule ya
Sekondari St. Mary’s Duluti hayo yamebainishwa na Father Fr.Peter Makao alipokuwa mgeni rasmi wa mahafali ya sita katika shule hiyo ambapo alisema katika ulimwengu wa sasa ajira ni chache sana ukilinganisha na idadi ya watu wanaoingia katika soko la ajira.

Alibainisha kuwa ushindani katika soko la ajira ni kubwa sana hivyo ni vyema Vijana wengi waliopo majumbani na mitaani kuliko kukaa bila kazi yeyote ile wakajihusisha na shughuli za ujasilia mali zenye heshima na staha, pia wawe wabunifu

Aliongeza kuwa Vijana walio wengi wa leo wanapenda kuwa huru(freedom) katika kufanya mambo ,Uhuru si jambo baya lakini uhuru usiokuwa na mipaka na uwajibikaji huo sio uhuru,Lazima mtu awajibike kwa matendo yake mwenyewe Hivyo basi uhuru wa kweli lazima uendane na uajibikaji

Akiongea katika mahafali hayo mkuu Wa shule hiyo brother Essau Mlengule aliwaambia kuwa hatua waliofikia ni kwa sababu ya bidii kubwa, nidhamu na kujituma katika masomo mbali na hivyo pia kumtegemea Mwenyezi Mungu, akazibariki nguvu na bidii zao katika kuyatekeleza majukumu yao mema.

Aliwataka wakaendelee kujituma, kuwa na bidii na nidhamu pindi tu warudipo nyumbani pia wasiache hata siku moja kumtegemea Mungu katika kilajambo walifanyalo

Alisema kuwa kuhitimu kwao kwa masomo ni ishara ya kuwa wamekomaa kiakili, kiroho na kimwili na wapotayari kuelekea hatua mpya ya maisha kitaaluma, na maisha ya kujitegemea kiujumla.

"Ninyi kama wasomi wa kidato cha sita, mnajukumu kubwa la kuwa wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya maisha yenu binafsi, maendeleo ya familia, jumuniya zenu na hatimaye maendeleo ya Taifa zima la Tanzania kwa fikra yakinifu, kwa matendo na kwa njia halali zinazokubalika na jamii ya watu walioelimika." Alisema Mlengule

Alisema kwamba mafanikio/maendeleo ya kweli hayaji kwa njia za mkato, kutokufuata taratibu za jumuiya husika, Kujichukulia maamzi bila ruhusa ya mamlaka husika, bali kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa malengo, kujiamini, kuwa weledi (kuwa wabobezi) katika kazi zenu, elimu ya fedha pamoja na kuwa na nidhamu ya fedha.

Alisema Elimu yenu ya kidato cha sita iwasaidie kuwa na ujasiri wa kuishi kwa mifano maisha ya uadilifu katika familia na jumuiya pia Elimu mliopata iwasaidie kuepukana na uvivu, ulevi, uzushi, kiburi, wizi, matumizi ya madawa ya kulevya, uasherati na matendo mengine maovu yasiyokubaalika katika jamii yetu ya Tanzania kwani jamii inatarajia kuona ndani yenu maisha ya fadhila, utulivu, usikivu, uwajibikaji, ushiriki wenu katika kazi za kiuchumi na kijamii

Alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili shule hiyo ni pamoja na upungufu Wa mabweni ,ukosefu Wa jengo la utawala pamoja na viwanja vya michezo.

CHUO KIKUU MZUMBE CHAJIZATITI KUIMARISHA UTOAJI ELIMU KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA WILAYANI MVOMERO

$
0
0
Maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliadhimishwa kwa aina yake na Chuo kikuu Mzumbe Aprili 23; 2019 ambapo mbali na maonyesho ya machapisho yaliyoandikwa na Wanazuoni; Chuo hicho kilikabidhi msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule za Msingi na Sekondari zilizopo kwenye Kata hiyo.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvombero Bw. Florian Kyombo ambaye pamoja na mambo mengine alipongeza jitihada zinazofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe katika kuchangia na kuboresha sekta ya elimu nchini hususani matumizi ya teknolojia hasa kipindi hiki cha Awamu ya Tano ya Uongozi ambapo elimu ni agenda inayopewa kipaumbele na hivyo kutolewa bila malipo kwa ngazi ya elimu ya Awali, Msingi na Sekondari.

“Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa msaada wa vitabu, shelfu na elimu mnayoendelea kuitoa kwa shule zetu kuhusu matumizi sahihi ya vitabu hivyo, sambamba na matumizi ya teknolojia ya utunzaji. Kwangu hili ni deni kuhakikisha tunatenga bajeti kuwezesha shule zingine za Msingi na Sekondari kwenye Kata 30 zilizopo kwenye Wilaya ya Mvomero zinaiga mfumo huu kwa kuifanya Kata ya Mzumbe kuwa ni ya kujifunzia.” alisisitiza.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka amesema Chuo hicho kina wajibu wa kuhakikisha jamii inayokizunguka inanufaika na uwepo wake kwa kusaidia katika masuala ya maendeleo ikiwemo kuinua kiwango cha elimu kwa kujenga hamasa ya usomaji wa vitabu, kuwakuwa hiyo ndiyo mbinu pekee inayoweza kuwapatia Wanafunzi maarifa ya kutosha na kuweza kufikia ngazi zote za elimu hadi Chuo Kikuu.

Amesema “ Mpango wa kuzifikia na kutatua changamoto za Shule za Msingi na Sekondari kwa jamii inayotuzunguka ni endelevu na ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa nne (IV) wa Chuo Kikuu Mzumbe ambapo kwa awamu hii, tumetoa Vitabu vya kiada na ziada kwa shule za Msingi Tangeni, 
Mnyanza,Vikenge, Masanze, Changarawe na Mzumbe na shule tatu za Sekondari ambazo ni Mongola,Askofu Adrian Mkoba na Mzumbe; na tayari tumetoa msada wa Komputa na kutoa mafunzo ya matumizi ya programu mbalimbali ili kuziwezesha shule zetu kuendeshwa kisasa kwa kutoa mafunzo yanayoendana na wakati tulionao”.

Aidha; ameahidi Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kuwa chachu katika kuhamasisha usomaji na utunzaji vitabu wenye lengo la kurithishana elimu na ujuzi kwa manufaa mapana ya Taifa.

Siku ya Vitabu Duniani huadhimishwa kila mwaka Aprili 23; kwa lengo la kuhamasisha usomaji wa vitabu na kuwaenzi watunzi wa Vitabu duniani kote.
Mwanafunzi wa Kidato cha sita Mark Malekela wa shule ya Sekondari Mzumbe, akionyesha moja ya kitabu alichotunga kwenye maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro. Maadhimisho hayo yalilenga kuhamasisha usomaji na utunzi wa vitabu Duniani.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - kushoto), kwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Pro. Lughano Kusiluka wakikabidhi msaada wa Vitabu kwa shule ya Sekondari ya Mzumbe na Adrian Mkoba zote za Kata ya Mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliyofanyika Kampasi Kuu Morogoro.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - kushoto), kwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Pro. Lughano Kusiluka wakikabidhi msaada wa Vitabu kwa shule ya Sekondari ya Mzumbe na Adrian Mkoba zote za Kata ya Mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya Vitabu Duniani yaliyofanyika Kampasi Kuu Morogoro.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - kulia), akikabidhi msaada wa vitabu kwa shule ya msingi Mnyanza. Kulia kwake ni Prof. Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe (mwenye sare ya kitenge) na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Myanza Bw. Robert Ngelima na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Wakiwa katika picha ya pamoja ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florian Kyombo (mwenye kaunda suti - katikati), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Pro. Lughano Kusiluka (mwenye sare ya kitenge – kulia), Mhe. Rachel Kingu Diwani wa Kata ya Mzumbe (Kushoto), Dkt. Albogast Musabila Mkurugenzi wa Makitaba na huduma za Kiufundi Chuo Kikuu Mzumbe ( mwenye sare ya Kitenge wa kwanza kulia) na Dkt. Hawa Petro Tundui ( wa kwanza kushoto) akimwakilisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma. Kwa nyuma ni baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS PROF.MUTHARIKA IKULU YA KAMUZU,LILONGWE NCHINI MALAWI

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika pamoja na Mawaziri na Watendaji wa Serikali kabla ya Kusaini Mikataba ya Makubaliano ya Masuala mbalimbali yanayohusu Nchi zote mbili  katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika pamoja na Mawaziri na Watendaji wa Serikali kabla ya Kusaini Mikataba ya Makubaliano ya Masuala mbalimbali yanayohusu Nchi zote mbili  katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.
3.34
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika pamoja na Mawaziri na Watendaji wa Serikali kabla ya Kusaini Mikataba ya Makubaliano ya Masuala mbalimbali yanayohusu Nchi zote mbili  katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.
56789
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof.  Arthur Peter Mutharika kwa Zawadi aliyompatia mara baada ya Mazungumzo ya Kiserikali katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Picha ya Twiga na Mlima Kilimanjaro Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya Mazungumzo ya Kiserikali katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kinyago Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya Mazungumzo ya Kiserikali katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika mara baada ya kumkabidhi zawadi ya kinyago katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Nchini Malawi.Aprili 24, 2019.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Prof. John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Dkt.Lois Fabiano pamoja na Mawaziri na Viongozi wengine wa Sreikali ya Tanzania na Malawi katika Ikulu ya Kamuzu iliyopo Jijini Lilongwe Malawi.Aprili 24, 2019.Picha na Ikulu
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images