Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109924 articles
Browse latest View live

ZRB YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA WAJIBU WAO KATIKA KODI

$
0
0
Na Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar
Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) imefanya mafunzo kwa Waandishi wa habari juu ya ulipaji Kodi ikiwa ni mkakati wake wa utekelezaji wa ajenda ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Katika mafunzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwao Mazizini, ZRB imewataka Waandishi wa Habari kuielimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa kulipa Kodi kwa maendeleo ya nchi na watu wake.

Akizungumza na Waandishi hao Meneja uhusiano na huduma kwa walipa Kodi ZRB Shaban Yahya Ramadhan amesema Waandishi wana wajibu wa kuijengea hamasa Jamii juu ya ulipaji Kodi kupitia vipindi na taarifa wanazozitoa katika Vyombo vyao.

Amewataka Waandishi hao kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Kodi ili kufanikisha makusanyo ya Kodi yaliyopangwa.

“Lengo la 17 la SDGs linatutaka sisi kushirikiana na Wadau wengine katika kufikia malengo tuliyojipangia na miongoni mwa Wadau wetu muhimu ni nyinyi ambao muna wajibu wa kutengeneza hamasa jamii ilipe Kodi” Alisema Meneja Uhusiano.

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa ZRB Makame Khamis Mohamed wakati akielezea umuhimu wa Kodi amesema hutumika kuendeshea Serikali ikiwemo kulipa Mishahara ya Wafayakazi, Wawakilishi na watoa huduma nyingine.

Amesema Kodi inayokusanywa na ZRB huingizwa katika Hazina ya Serikali na baadaye hurudishwa kwa Wananchi kwa kuhudumia shughuli mbali mbali ikiwemo miundominu ya barabara, elimu, umeme na maji.

Ameongeza kuwa Kodi hiyo hutumika pia kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi kwa kulipa mishahara kwa wakati watendaji wa Vikosi vya ulinzi na usalama.

Akielezea changamoto zinazoikabili ZRB Makame amesema ni pamoja na kuwepo kwa Wafanyabiashara wanaofanya biashara bila kusajiliwa kulipa kodi. Changamoto nyingine ni Wauzaji kutotoa Risiti kwa Wateja na Wanunuzi kushindwa kudai Risiti wakati wa manunuzi.

Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru ZRB kwa kuwajengea uwezo kuhusu Kodi na kuahidi kuifanyia kazi elimu waliyoipata kwa faida yao na jamii kwa ujumla.

Aidha Waandishi hao wametoa wito kwa Taasisi zingine kuiga mfano wa ZRB katika kushirikiana na wadau wake ili kufikia malengo yaliyopangwa.

Mafunzo hayo yamekuja ikiwa ni utekelezaji wa lengo la 17 la ajenda ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu (SDGs) linalohusu ushirikiano na Wadau katika kufikia Malengo.
 Meneja Uhusiano na Huduma kwa Walipa Kodi Shaban Yahya Ramadhan (kushoto) akitoa Elimu kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Utekelezaji wa SDGs katika mafunzo ya siku moja ya Wajibu wa Muandishi wa Habari katika Kodi na Utekelezaji wa SDG yaliofanyika Ofisi ya ZRB Mazizini mjini Unguja.
 Afisa Uhusiano Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB)Makame Khamis Mohd akitoa elimu kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mahusiano na Huduma kwa Walipa Kodi katika mafunzo ya siku moja ya Wajibu wa Muandishi wa Habari katika Kodi na Utekelezaji wa SDG yaliofanyika Ofisi ya ZRB Mazizini mjini Unguja. 
 Muandishi wa Habari wa Hits Fm Kudra Mawazo akiuliza maswali katika mafunzo ya siku moja ya Wajibu wa Muandishi wa Habari katika Kodi na Utekelezaji wa SDG yaliofanyika Ofisi ya ZRB Mazizini mjini Unguja.
Muandishi wa Habari wa Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza maswali katika mafunzo ya siku moja ya Wajibu wa Muandishi wa Habari katika Kodi na Utekelezaji wa SDG yaliofanyika Ofisi ya ZRB Mazizini mjini Unguja.

SEND OFF YA BINTI RWEIKIZA YAVUNJA REKODI BUKOBA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Sherehe za Kumuaga Mtoto wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mhe. Jasson Rweikiza zimefanyika Jana katika viwanja vya Shule za Rweikiza zilizopo Maeneo ya Kyetema Bukoba.

Sherehe hizo zilizofanyika mnamo Aprili 23, 2019 zikiwa zimehudhuliwa na watu zaidi ya 5000 wakiwemo Viongozi wa Dini, Serikali, Chama Tawala, Madiwani, watumishi wa serikali, wananchi kutoka Kata zinazounda Halmashauri ya Bukoba na wengine kutoka nje ya Mkoa wa Kagera.

Kivutio kikubwa katika sherehe hiyo ni Mshereheshaji wa shughuli mbali mbali za Kitaifa Ndg. Mavunde akionyesha umahiri mkubwa wa kuongoza shughuli aina zote na akiacha waalikwa wakiumwa mbavu kwa Vicheko.

Miongoni mwa wasanii waliotoa burudani ni pamoja na  Saida Karoli aliyetamba kwa kibao maalum cha "Obugenyi"  kinachofanya vizuri sana katika sherehe za Harusi.
Familia ya bibi harusi wakiongozwa na Baba na Mama Mzazi wakati wakiingia Ukumbini katika Sherehe ya Kumuaga Binti yao.
Mapema Viongozi mbali mbali wakiwasili katika Send off ya Hope Jasson Rweikiza, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Bukoba, Mh. Deodatus Kinawiro.
Pichani kushoto ni Mkurugenzi Wa Nyanza Bottling Co. Ltd Christopher Mwita Gachuma, akiwasili Ukumbini akisindikizwa Na Diwani Wa Kata ya Kaibanja Mh. Jasson Lwankomezi.


Wazazi wa Aloyce Kutoka Usukumani wakicheza Wimbo wa Kubyala wakisaidiwa na Mshereheshaji Bwn. Mavunde
Kikundi cha burudani (Brigthers) maarufu kama Kibeta One kikisafisha njia kabla ya maharusi kuingia Ukumbini.
Bi Harusi Mtarajiwa Hope Jasson Rwekiza akiingia ukumbini huku akicheza kufurahia siku yake, akisindikizwa na Ndugu yake.

Wanameremeta wapendanao hawa Aloyce na Hope ambao baadae watakuwa Mwili mmoja.
Karibu senene baba watoto mtarajiwa
Muonekano wa Keki Maalumu iliyoaandaliwa kwa ajili ya Hope Rweikiza
Pichani Mpambe wa Hope akimsaidia kuandaa keki kabla ya kukatwa
Burudani ya Saida Karoli ikamsababisha Mhe. Abdallah Bulembo (MB) kunyanyuka akisindikizwa na Mbuge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Rweikiza, kuongoza wageni waalikwa kwenda kutunza.
Mama mzazi wa Hope, Bi. Stella akicheza ngoma ya Saida Karoli pamoja na Mwenyekiti wa Wazee Mzee Sadru Nyangasha.
Bibi Harusi mtarajiwa Hope akigonga glasi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Mama Buhiye wakati wa sherehe za Kumuaga zilizofanyika katika shule za Rweikiza Bukoba.
Pichani Mh. Rweikiza akitoa neno lake kwa bintiye kikubwa akiwa amemuusia Upendo na Kumcha Mungu.
Pichani Mh. Jasson Rweikiza  (MB) akifurahi pamoja na Bintiye Hope Rweikiza katika sherehe ya Kumuaga Binti hiyo (send off).

Mnazi Mmoja yaichabanga Muhimbili 40-16 katika mpira wa pete

$
0
0
Timu ya mpira wa pete ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar imeibuka mshindi baada ya kuichabanga Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) bao 40-16 kwenye michezo ya Bonanza la Pasaka inayoendelea mjini humo.

Katika mchezo huo uliofanyika uwanja cha Gymkhana Zanzibar hadi kipindi cha kwanza kinaisha timu ya Mnazi Mmoja iliongoza kwa bao 16-5. Mara baada ya mchuano huo kuisha nahodha wa timu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja, Maneno Shaame amesema mtangane huo ulikuwa mzuri na ushindi wao umetokana timu yake kufanya mazoezi ya kutosha na hivyo kujiandaa kikamilifu.

“Tunashukuru tumecheza vizuri na mpaka sasa hivi timu tunaijenga ili kufikia mafanikio mazuri zaidi kwa michezo ijayo” amesema Shaame. Naye kocha wa timu ya Muhimbili Zainabu Kassim amekiri kuwa kufungwa kwa timu yake kumetokana na makosa waliyofanya wakati mchezo huo ukiendelea hivyo wamejifunza na kwamba wataijenga zaidi timu hii.

“Mchezo ulikuwa mzuri na hivyo kwa kuwa tunaijenga timu yetu, tumejua tuko wapi na tunaelekea wapi, changamoto tumeiona japo tumefungwa lakini tumejifunza,” amesema Zainabu Bonanza la Michezo ya Pasaka linaendelea Zanzibar kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Mnazi Mmoja ambalo linajumuisha mpira wa miguu na pete.
 Kikosi cha timu ya mpira wa pete kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifanya mazoezi kabla ya mchezo huo kuanza.
 Mchezaji wa Timu ya Muhimbili Nzitu Msengi (WD) akitoa pasi kwa Kuruthum (c ) katika mchezo uliofanyika kwenye kiwanja cha Gymkhana
 Julieth Jabu (GA) akiifungia timu ya Muhimbili goli la nane katika mchezo huo.
 Baadhi ya washabiki wa mpira wa pete wakifuatilia mechi kati ya Muhimbili na Mnazi Mmoja

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM AKEMEA VITENDO VIOVU VUNAVYOWEZA KUHATARISHA AMANI HAPA NCHINI

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema Chama hicho kimejizatiti kutatua kero za wananchi pamoja na kusimamia Demokrasia kwa kukemea vitendo viovu vinavyohatarisha Amani na Utulivu wa Nchi.

Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kukagua Uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja, amesema vipaumbele vya CCM ni kutekeleza kwa kasi ahadi zilizotolewa na Taasisi hiyo kwa wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu uliopita.

Alisema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kuaminiwa,kupendwa na kuthaminiwa na Mamilioni ya Watanzania kutokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Sera zake, kwa kutatua changamoto za kijamii kwa wakati mwafaka.

Aidha alisema katika kusimamia dhana ya Demokrasia CCM haitosita kukemea vitendo viovu vinavyoashiria kuvunja Sheria za Nchi, hasa vinavyotekelezwa na baadhi ya Vyama vya upinzani.

“Tumekubali kuingia katika mfumo wa Vyama vingi ili tushindane kwa Sera na sio kushindana kwa vituko na vurugu ni muhimu kila mwanasiasa kujitathimini juu ya mwenendo wake kwa jamii anayoiongoza.”, alisema Dk.Mabodi.

Alisema katika zama za CCM mpya imekuwa imekuwa ni kimbilio la wananchi wanaoamini katika siasa za maendeleo ambao wametelekezwa na Vyama vyao na kupokelewa  vizuri ndani ya CCM ili wanufaike na Demokrasia iliyotukuka.

Aliwataka Viongozi na Watendaji wa CCM kutowawekea vikwazo Wananchi wanaotaka  kujiunga na Chama na badala yake wapewe fursa hiyo bila masharti magumu sambamba na kuwasomesha miongozo na itikadi za kitaasisi.

Aliwaagiza Wabunge,Wawakilishi na Madiwani kufanya mikutano katika maeneo yao ya kuwaeleza Wananchi mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Ilani ili wananchi hao wawe Mabalozi wa kufikisha taarifa hizo kwa jamii.

Aliwambia wananchi kuwa CCM imesimamia kwa ufanisi miradi ya maendeleo ukiwemo wa TASAF ambao upo katika Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020, ambao umewaondosha wananchi katika wimbi la umasikini na kuwa na kipato cha kati.  

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo Runinga (Television) pamoja na Fedha kwa vikundi 11 vya Saccos ya Shehia ya Mzuri katika Maskani ya CCM ya Kisonge Makunduchi Dk.Mabodi amesisitiza kuwa uhai wa Taasisi hiyo ya kisiasa unaanza kuimarishwa kuanzia ngazi ya mashina.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe.Haroun Ali Suleiman alisema tayari Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo imetekelezwa kwa asilimia 90, na kwa sasa wanaendelea kutatua baadhi ya changamoto ili kuzimaliza kabla ya 2020.

Mhe.Haroun alisema kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa ya Jimbo hilo amefanya ziara katika Shehia zote 13 za Jimbo kwa kuratibu changamoto zinazowakabili wananchi na nyingi zimetatuliwa sambamba na kueleza fursa na miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ameir Haji Timbe alisema maendeleo yaliyopatikana katika Jimbo hilo yametokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya viongozi na wananchi.

Akizungumza Mwenyekiti wa Maskani ya CCM ya Kisonge iliyopo Makunduchi Abdallah Hassan Haji alisema wanaendelea kuvuna wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani huku wakijipanga kufuta masalia ya upinzania ndani ya Jimbo hilo.

Naye Mwenyekiti wa Maskani ya CCM ya Hapa Kazi Tu Yussuf Abeid Haji, akizungumza katika uzinduzi wa Maskani hiyo alisema eneo la maskani yao litatumika kuwa chachu ya kujenga umoja,mshikamano pamoja na kuwa kituo mbadala cha kubuni miradi mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya Wana CCM.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa amebeba mtoto mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kibuteni alipoenda kukagua uwanja wa mpira wa kisasa unaojengwa katika Kijiji hicho.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwahutubia Wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla katika ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani katika Maskani ya CCM ya Kisonge, iliyopo Shehia ya Mzuri Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa amebeba ndoo yenye udongo katika ujenzi wa Tawi la CCM Miwaleni Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
  MWAKILISHI wa Jimbo la Makunduchi Mhe.Haroun Ali Suleiman akisomba udongo wa kifusi wa kuweka katika Tawi la CCM la Miwaleni katika ziara ya kukukagua uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo hilo Wilaya ya Kusini Unguja.
 MKUU wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrisa Mustafa Kitwana (aliyebeba kifaa cha kubebea udongo wa kifusi wa pili kushoto) akishiriki katika ujenzi wa Taifa wa Tawi la CCM Miwaleni Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizindua Maskani ya CCM ya Hapa Kazi Tu iliyopo Mtende Mndo Makunduchi.

TANGULIA OLIVER MUTUKUDZI ‘TUKU’

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam.
Kifo cha mwanamuziki wa muziki wa Jazz kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ‘Tuku’ kimewaacha katika majonzi makubwa baadhi ya wapenzi wamuziki huo. Tuku alifariki dunia Januari 23, 2019 katika hospitali ya Avenues mjini Harare nchini Zimbabwe akiwa na umri wa miaka 66.

Oliver alikuwa amelezwa hospitalini humo kwa ajili ya kupaitiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kabla hajalazwa mwanamuziki huyo alikuwa katika ziara za kimuziki katika nchi mbalimbali duniani. Ilimlazimu kuzikatiza sababu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Tuku aliibeba Tuku Music kama beji ya heshima na kuipa hadhi sanaa ya Afrika, alifariki dunia tarehe sawa na ile ambayo rafiki yake, mkongwe wa muziki, Hugh Masekela alifariki dunia, Afrika Kusini, mwaka jana 2018. Aliwahi kuja nchini Tanzania mwaka 2011 kwa kazi hiyo, akaimba nyimbo nyingi kuhusu Ukimwi, ukiwemo Todii ambao ni Lifetime song.

Oliver atakumbukwa kwa vibao vyake vingi vilivyotikisa Ulimwengu wa muziki, hasa wimbo wa 'Neria' na 'Todii'. Baadhi ya Wabunge nchini Zimbabwe walitoa pole kwa familia na mashabiki wa Mtukudzi huku wakimtaka Rais kutangaza msiba wa Kitaifa.

"Tumepoteza nembo ya Taifa namwandikia rais Emmerson Mnangagwa kuomba atangaze msiba wa taifa kwa heshima ya shujaa huyu kwa mchango wake wa kitaifa kwenye sekta ya muziki, sanaa na utamaduni'', alisema mbunge wa Norton Temba Mliswa.

Moja ya viongozi wengine waliotoa pole ni Waziri wa zamani wa Elimu, Michezo, Sanaa na Utamaduni nchini Zimbabwe David Coltart ambaye amesema "Pumzika kwa amani Oliver Mtukudzi, kama kuna mtu yeyote amewahi kuitangaza Zimbabwe ni wewe. Asante kwa kutufanya tufurahi kwa muda mrefu."

Mtukudzi maarufu kama ‘Tuku’ alikuwa ni msanii na mwandishi mashuhuri wa ngoma mbalimbali huku akiwa ni moja ya wasanii wenye albam nyingi zaidi akiwa nazo zaidi ya 60. Mapema mwaka jana 2018, alilazwa katika hospitali moja mjini Harare kwa shinikizo la damu. Hata hivyo aliruhusiwa na hali yake ikaimarika.

Mwanamuziki huyo alishawahi kufanya muziki na msanii wa Bongo Fleva, Lady JayDee wimbo unaoitwa “I am who I am” au ka lugha yetu ya Kiswahili 'Mimi ni Mimi' wakiimba kwa lugha za Kishona na Kiswahili. Baada ya kifo cha nguli huyo Lady JayDee alisema Oliver Mtukudzi alikuwa mwanamuziki mrahisi kufanya naye kazi kutokana na tabia yake ya kumpokea mtu jinsi alivyo.

Alitamka kuwa mara baada ya yeye kukutana na Oliver Mtukudzi, alimshauri vitu vingi kuhusu muziki kitu ambacho kimempa faida. "Baada ya hapo mambo yalibadilika kutokana na ushauri aliyonipa, namna ya kufanya muziki wa ‘live’ na kuhusisha vionjo vya Kiafrika kwenye muziki wangu," alisema Lady JayDee.

Kwa upande wake msanii wa mkongwe wa muziki nchini, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ alieleza kuguswa na kifo cha Oliver Mtukudzi kwa kuwa alikuwa akiupenda sana muziki wake. "Nimeshtushwa na kifo chake pili imeniuma sana kwa sababu nilikuwa nampenda na napenda kazi zake" alisema Kiki.

Mdua wa muziki Songoro Mnyonge wa Dar es Salaam, kwa upande wake alimuelezea Oliver kuwa Afrika imempoteza mwanamuziki nguli aliyekuwa mcheshi, akiimba kwa hisia huku akilicharaza gitaa lake. Mnyonge amesema kuwa muziki wake utaishi milele, kwani vionjo vyake ni vya kipekee. Songoro alisema aliwahi kuzungumza na marehemu Tuku katika jiji la Harare ambapo alimwambia kuwa robo tatu ya maisha yake amehudumu katika muziki.

Licha ya kuitangaza Zimbabwe duniani kote kupitia kwa muziki wake, Tuku pia alikuwa ni mpigania haki za binadamu duniani pamoja na kuwa balozi wa hisani wa Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Wasifu wake

Oliver Mtukudzi alizaliwa Septemba 22, 1952 mjini Highfield, Harare nchini Zimbambwe. Alikuwa ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Oliver alianza kutambulika zaidi kimuziki baada ya kuingia katika Kundi la Wagon Wheels mwaka 1977, akiwa na wenzake kadhaa akiwamo Thomas Mapfumo.

Wimbo wake wa kwanza ulikuwa wa ‘Dzandimomotera’ ulioheshimika sana, na hapo ndipo alipotoka na albamu yake ya kwanza iliyomletea mafanikio makubwa zaidi. Nguli huyo alitoa alitoa albamu kuanzia mwaka 1978, za Chokwadi Chichabuda na Muroi Ndiani za mwaka 1979. Mwaka 1981 alitoa albamu ya Shanje na Pfambi na katika kipindi cha mwaka 1982, akaacxhia albamu ya Maugira na Please Ndapota wakati mwaka 1983, alikuja na alamu ya Nzara na Oliver’s Greatest Hits.

Albamu nyingine za mhenga huyo zilikuwa za Hwema Handirase, Mhaka, Gona,Zvauya Sei, Wawona, Nyanga Yenzou, Strange, Isn’t It?, Sugar Pie, Grandpa Story, Chikonzi, Pss Pss Hallo na Shoko. Mtukudzi hakuishia hapo kwani aliachia albamu zaingine za Mutorwa, Rombe, Rumbidzai Africa, Ziwere MuKobenhavn, Was My Child, The Other Side na Live in Switzerland.

Zingine ni pamoja na Ndega Zvangu, Dzangu Dziye, na Tuku Muzic na nyingine nyingi.

Aidha, Mtukudzi aikuwa ni mmoja wa wanakundi la Mahube, lililokuwa ni la muziki la nchi za Afrika Kusini. Alikuwa ni baba wa watoto watano na wajukuu wawili. Watoto wawili kati ya hao, ni wanamuziki.

Mtukudzi amefariki akiwa na umri wa miaka 66, alikuwa baba wa watoto watano na wajukuu wawili. Alikuwa kati ya watoto sita dada zake wanne na wa kiume wawili, mmoja ambaye alikuwa kaka yake alikwishafariki.

Licha ya muziki Tuku alikuwa akifurahia kuogelea katika bwawa lake (swimming pool) ambalo lina umbo la gitaa la solo. Mwanamuziki huyo wa Kimataifa alikwisha tunukiwa tuzo ya tatu na kuweza kutoa zaidi ya albamu 40.

Oliver alishinda tuzo nyingi mno hata nyingine hakuweza kuzikumbuka. Moja ya tuzo hizo ni ile iliyobeba heshima ya udaktari kutokana na kuwa mshauri na balozi mzuri wa muziki.

Mwaka 2003 alitunukiwa tuzo kubwa ya heshima na Chuo Kikuu cha Zimbabwe kwa kutambua mchango wake na kujitolea katika kujenga muziki na msukumo kwa wasanii wa kizazi kipya nchini Zimbabwe, huku akionesha ushawishi kwenye kazi za wasanii hao kwa miongo kadhaa.

Mwaka 2009, Chuo Kikuu cha Wanawake cha Afrika kilimpatia tuzo ya shahada ya sanaa na kumwelezea mwanamuziki huyo kama mbunifu wa hali ya juu kuwahi kutokea nchini Zimbabwe katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita.

Wengi wanamfahamu Mtukudzi kutokana na umahiri wake mkubwa katika medani ya muziki, utambulisho wake mkubwa ukiwa ni sauti yake nzito na ya kipekee. Licha ya Oliver kuwa mwanamuziki, pia ni mfanyabiashara, mwanaharakati wa haki za binadamu na balozi wa UNICEF Kusini mwa Bara la Afrika.

Mara nyingi Tuku alikuwa akiimba nyimbo katika lugha tatu tofauti za Kishona, Kindebele na Kiingereza. Alikuwa akichanganya ala za muziki wa kiasili kwenye nyimbo zake, jambo lililompa umaarufu mkubwa dunia nzima.

Tofauti na wenzake katika kundi la Wagon Wheels waliokuwa wa kimwimba vibaya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe, Mutukudzi alikuwa akimsifia sana na kusababisha anufaike kwa misaada mbalimbali kutoka serikalini.

Kati ya wasanii wenzake waliokuwa wakiunda kundi la Wagon Wheels, ni yeye pekee aliyekuwa amebakia kufuatia wenzake wote kufa kwa Ukimwi. Mwaka 2010, mwanawe kipenzi, Sam Mutukudzi, ambaye naye alikuwa mwanamuziki, alifariki dunia kutokana na ajali mbaya ya gari. Mutukudzi amekuwa akidaiwa mara kwa mara kwamba alikuwa mwathirika wa ugonjwa wa Ukimwi, ingawa mwenyewe alikuwa akikanusha vikali madai hayo.

Hivi karibuni, mashabiki wake nchini humo walipatwa na mshangao mkubwa baada ya kitabu kiitwacho ‘Tuku Backstage’ kuvuja kikiwa na kashfa nyingi za ngono zinazomhusu gwiji huyo, mwandishi akiwa ni Shepherd Mutamba.

Oliver Mutukudzi ameacha albamu za nyingi baadhi yake ni kama ‘Ndipeiwo Zano’ ya mwaka 1978, ikarudiwa tena mwaka 2000, ‘Chokwadi Chichabuda’ na ‘Muroi Ndiani?’ za mwaka 1979, ‘Shanje’ na ‘Pfimbi’ za mwaka 1981, ‘Nhava’ ya mwaka 2005, ‘Wonai’ ya 2006, ‘Tsimba Itsoka’ na nyingine nyingi.

Safari yake ya muziki ilianza mwaka 1977, alipojiunga na bendi ya Wheels ambako alikuwa akiimba na Thomas Mapfumo ambako walitoa muziki wao wa kwanza wa Dzandimomotera ambao ulifanya vizuri sana na kupelekea utoaji wa albamu yao ya kwanza ambayo pia ilifanya vizuri katika soko la muziki.

Sauti yake yenye mvuto wa kukwaruza , ilikuwa ndio utambulisho mkubwa ndani na nchi ya Zimbabwe. Nyimbo zake nyingi alikuwa akiimba kwa lugha yake ya Kishona na kundi lake la Zimbabwe KoreKore. Pia alikuwa akichanganya na lugha na midundo ya asili na kufanya muziki wake uwe na mvuto wa kipekee.

Wanamuziki wengi wa Zimbabwe na wa Afrika wamenufaika na mafunzo ya kimuziki kwa njia moja ama nyingine katika kipindi chote cha maisha yake ya kimuziki. Mwaka 2010 alituzwa Tuzo kutoka chuo kikuu cha Zimbabwe, ya The international Council of Afrinana Womenism Award. Hiyo ilitokana na mchango wake mkubwa wa kuwainua wanawake kupitia Sanaa ya muziki.

Hata hivyo kila mtu kwa ujumla huwa anamapenzi ya kitu fulkani kwenye maisha yake ya kkila siku anapokuwa akipata fulsa ya kupumzika baada ya kazi ya kutafuta riziki yake. Wapo wanapenda kuangalia mpira wa miguu, sinema, kufanya mazoezi, kuangalia mifugo yao, bustani, na wengine kuwatembelea wagonjwa na ndugu zao na kuongelea. Hali hiyo hufanywa na baadhi ya nyota ili kupunguza mawazo, yao baada ya kazi zao nzito.

Mwanamuziki Oliver Mtukudzi ‘Tuku’ kila mara alipokuwa akipata muda wa kupumzika, alikuwa anapenda sana kuogelea kwenye bwawa lake (swimming pool) ambalo limejengwa kwa umbo la gitaa. Alikuwa anafurahi sana kupumzika hapo huku akiangalia umbo laeneo la bwawa hilo ambappo aliwahi kudai kuwa lilikuwa linampa faraja kujua wajibu wa kazi yake.

Aidha Tuku alikuwa amejaaliwa vipaji vingi kikiwemo cha uigizaji. Aliweza kutengeneza filamu ya Jit, Neria na Tsisi Dangarembga mwaka 1993. Oliver Mtukudzi ‘Tuku’ haupo duniani ila muziki wako utadumu daima milele. Mungu aipumzishe roho yako pahala pema peponi, Amina.

JAJI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA KUTATHMINI UTENDAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAJAJI wa mahakama ya Rufani wametakiwa kuzingatia sheria na katiba katika kutoa haki, na pia kutosahau kutumia tabia za utamaduni ambazo hazijaandikwa mahali popote katika kusaidia utoaji wa haki.

Amesema, tabia ya  uvivu, uchonganishi, ulalamishi na ubishi usioeleweka ni moja kati ya tabia za kibinadamu zinazochangia  kutotolewa kwa haki kwa wakati. Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameyasema hayo leo Aprili 23, 2019, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kutathmini utendaji wa Mahakama ya Rufani.

 Jaji Profesa Juma amesema,  majaji wana wajibu mkubwa wa kutoa haki kwa mujibu wa sheria na kutoa uamuzi hata katika mambo yasiyo na sheria na kwamba tabia za kutotoa haki kwa wakati ni pamoja na uvivu, uchonganishi, ubishi usioeleweka na ulalamishi kwani mambo haya yakiingia katika mfumo wa utoaji haki yanachelewesha.

Amesema pamoja na kutakiwa kutegemea sheria na katiba, yapo mambo ya kiutamaduni na tabia ambazo hazijaandikwa sehemu yoyote hivyo wanapaswa kuyazingatia katika kutoa haki.

"Mnatakiwa kuwa na uelewa wa sheria kwani wananchi wanategemea watapata haki kwa wakati, pia tuwe na ujuzi wa sheria na msisahau kuelewa tabia za watu  mbalimbali hususani majaji waliostaafu ili isije kuwa kikwazo katika utoaji haki," alisisitiza.

Amesema,  mkakati wa miaka mitano wa mahakama unajenga tabia ya kutoa haki  kwa kutumia utamaduni na kuwa hakuna mahali ambapo pameandikwa kuwepo kwa uharakishaji wa utoaji haki, lakini majaji wanapaswa kutambua suala hilo kwani wananchi wanawategemea kuendana na karne ya 21.

Jaji Profesa Juma amesema, kutumia tamaduni nzuri za nchi husika ni sehemu mojawapo inayosaidia utoaji wa haki, hivyo kama mahakama watazitumia tamaduni zetu, basis itasaidia sana kwani yapo mambo mengi ya kuwezesha utoaji haki kwa wakati ambayo hayakuandikwa.

Ameongeza kiwa, ongezeko la Majaji wa Rufani kutoka 15 tuliowazoea hadi 21,  imeongeza nguvu kwa mahakama na lengo ikiwa  kuondoa mashauri yaliyokuwa yakichelewa kwani ni Lazima tuwasaidie wananchi kupata suluhu ya haraka katika masuala ya uchumi na jamii.

Katika mkutano huo wa mafunzo wa siku mbili ulioandaliwa na chuo cha mafunzo ya uongozi Lushoto,  Majaji wa Mahakama ya Rufani watapata mafunzo ya namna ya kuendesha majopo mahakamani yatakayowawezwsha utoaji wa haki kwa wakati.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma akifungua  mkutano wa mwaka wa kutathmini utendaji wa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wastaafu unaofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wastaafu wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma alipokuwa akifungua  mkutano wa mwaka wa kutathmini utendaji wa mahakama ya Rufani unaofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wastaafu  mara baada ya kufungua mkutanowa mwaka wa kutathmini utendaji unaofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

SPIKA NDUGAI AZINDUA MTAALA WA KOZI YA SHAHADA YA UCHUMI NA FEDHA YA CHUO CHA IFM

$
0
0
 Spika wa Bunge Job Ndugai akionesha Mtaala wa Kozi ya Shahada ya Uchumi na Fedha aliyezindua upande wa Kushoto ni Mawaziri kushoto wa Kwanza Waziri Kilimo Japhet Hasunga akifuatiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhanga Mpina upande wa Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mahamoud Mgimwa akifuatiwa Mkuu wa Chuo cha IFM Profesa Tadeo Satta.
 Baadhi ya Wabunge wakifatilia muhadhara  juu ya mwelekeo wa upatikanaji  wa Chakula, Kukuza   Mnyororo wa thamani ya Uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na Kilimo kwa Chakula Duniani.
 Picha ya Pamoja ya Spika wa Bunge Job Ndugai  akiwa na Naibu Spika wa Bunge  Dkt Tulia Ackson, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga , Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhanga Mpina na Uongozi wa Chuo cha IFM baada ya kumaliza Muhadhara.

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mnamo tarehe 17 Aprili 2019  katika viwanja vya Bunge ukumbi wa Pius Msekwa Dodoma waliendesha muhadhara  kwa umma unaohusu Mwelekeo wa Upatikasnaji wa chakula- Kukuza Myororo wa Thamani ya Uzalishaji wa Bidhaa zinazotokana na Kilimo kwa chakula Duniani. Baada ya muhadhara huo kulikuwa uzinduzi wa Shahada ya Sayansi ya Uchumi na Fedha katika matukio haya Mgeni Rasmi alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Job Ndugai (MB). 

Akizumgumza katika muhadhara huo Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa TadeoSsatta, alisema chuo kimeona umuhimu kuendesha mihadhara kwa umma ili kutoa elimu stahiki na kusaidia Serikali ya awamu ya tano katika kukuza sekta ya Viwanda na Uchumi. 

Pia Prof. Satta, alisema kuongeza shahada hii ya Uchumi na Fedha ikiwa na lengo la kuongeza taifa elimu juu ya Uchumi na Fedha ambayo pia sekta muhimu katika awamu hii ya tano. 

Alisema kwa sasa chuo kimekua kwa kasi sana na kwa sasa kinaendesha kozi zaidi ya 35 katika fani mbalimbali.

Akizumza na hadhara ilioyo hudhuria wakiwemo waheshimiwa Wabunge na wananchi, Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Kilimo, Mifugo na Chakula Mahmoud mgimwa(MB)  alisema IFM kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliona umuhimu wa chakula nchi hivyo wakaona umuhimu wa  kuwashirikisha wabunge na wananchi wahudhurie mhadara huu muhimu.  

Mgeni rasmi Spika wa Bunge Job Ndugai (MB) alifurahishwa na IFM kuona fursa yakuwakutanisha pamoja watendaji wa sekta mbalimbali katika masuala ya kuongeza thamani na kuboresha bidhaa zinazotokana na kilimo kubadilishana uzoefu kuhusu namna za kuondokana na changamoto zinazojitokeza katika sekta ya kilimo. 

Pia alisizitiza kwamba Mihadhara kama hii inasaidia kutoa elimu  kuwa ukulima katika kiwango chochote ni sehemu ya biashara. Na shughuli yoyote ya kibiashara inahitaji kuangaliwa katika upana wake ikiwa ni pamoja na kuangalia mnyororo wa thamani, kutoka katika uzalishaji kwenda kwenye usindikaji, soko na mwisho kwa mlaji.

Kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais John Pombe Joseph Magufuli imefanya juhudi kubwa inayolenga kufikia hali ya kuwa na usalama wa chakula na viwanda vya uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo nchini.

Mwendesha mhadhara wa mada iliyohusu  mwelekeo wa upatikasnaji wa chakula- kukuza myororo wa thamani ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo kwa chakula Duniani Profesa Daktari Jan Willem Velthuizen  kutoka Chuo kikuu cha Groningen cha Uholazi, alisema sababu kubwa za upungufu wa chakula unasabishwa na Ongezeko la watu, Mabadiliko ya ladha za vitu, Mabadiliko ya tabia nchi, Uhaba wa maji, Uchumi, Rasilimali na Ukuaji wa miji.

RAIS WA ZANZIBAR AHUDHURIA MAHAFALI YA 14 CHUO CHA TAIFA SUZA TUNGUU

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA Dkt. Ali Mohamed Shein, akiingia katika ukumbi wa Mahafali ya 14 YA SUZA, akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Profesa Idrisa Rai.(Picha na Ikulu)
 /BAADHI ya Wahitimu wa Mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano wakiingia katika ukumbi wa Mahafali wa Dk. Ali Mohamed Shein, Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 WAHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano ya Mahafali ya 14 ya SUZA wakiingia katika ukumbi wa hafla hiyo ya Dkt.Ali Mohamed Shein, Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt. Ali Mohamed Shein, akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili Ndg. Ali Saleh Khalfan, ya Utafiti wa Istilahza Kiswahili :Mfano wa Istalahi za Sayansi ya Komyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, wakati wa hafla ya Mahafali ya 14 ya (SUZA) leo katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein. Tunguu Zanzibar(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt Ali Mohamed Shein, akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili ya Vitendo Neni katika Hutuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka 2015 na Athari zake kwa Wanajamii wa Kisiwani Unguja -Zanzibar. Ndg. Mahmoud Yussuf Haji, wakati wa hafla ya Mahafali ya 14 ya (SUZA) yaliofanyika katika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein. Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar yaliofanyika katika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu)


 WAHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla hiyo ya Mahafali ya 14 ya (SUZA) yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein,Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 WAHITIMU wa Shahada ya Utabibu (Madaktari) wakila kiapo baada ya kutunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa DK.Ali Mohamed Shein Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu)


YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza umuhimu wa waandishi wa Habari kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kulinda tunu za Taifa leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza akijibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimisha  mjadala wa hoja zilizotolewa kwa wabunge wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim  Majaliwa akimpongeza Waziri wa  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wake  Juliana Shonza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Susan Mlawi wakifuatilia majadiliano ndani ya ukumbi wa ubunge leo kabla ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa Wizara  mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kushughulikia makosa ya jinai ikiwemo kufanya  uchunguzi dhidi tuhuma husika na kubaini ukweli.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu utaratibu unaotumiwa na Shirika la Fedha Duniani kutoa taarifa ya hali ya uchumi kwa nchi wananchama Leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa sehemu ya wasanii leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Mmoja wa wasanii akimpongeza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo leo Jijini Dodoma. (Picha zote na Frank  Mvungi- MAELEZO, Dodoma)

WAZIRI MKUU AKAGUA OFISI ZA SERIKALI MTUMBA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ofisi mpya za wizara saba katika mji wa Serikali ulioko Mtumba, Dodoma na kusisitiza waweke vibao vya ofisi na kukamilisha mazingira ya nje.

“Kuna wizara hazina majina kwa nje. Hakikisheni majengo yote yanawekwa majina haraka ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaokuja huku kutafuta huduma. Kama kuna wizara mbili ziko jirani, pale njia panda wekeni kibao kuonesha majina ya wizara zote mbili. Nia ya Serikaili ni kutoa huduma zote kutokea hapa Mtumba,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumanne, Aprili 23, 2019) wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo fupi kwa maafisa wa Serikali waliokuwepo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara ya nishati ambako ndiko alimalizia ziara yake.

Waziri Mkuu ametembelea wizara saba ambazo ni Maliasili na Utalii; Ofisi ya Rais - TAMISEMI; OWM - Sera, Uratibu na Bunge; Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora; Mifugo na Uvuvi, Ulinzi na JKT na ya mwisho ilikuwani ni Wizara ya Nishati. 

“Nimefurahi kukuta Mawaziri, Naibu wao na Makatibu Wakuu pamoja na wakuu wa idara wako huku na kazi zinaendelea, lakini ni lazima nisisitize kwamba idara zinazohamia huku ziwe ni zile zenye kutoa huduma za kila siku kwa wananchi,” amesema.

“Ni lazima tuwaeleze wananchi na wadau wetu ili watambue kwamba Serikali imehamia huku, lakini wakija kutaka huduma wasikute idara inayowahusu iko mjini au wengine wako huku na wengune wako kule.”

Kuhusu miundombinu ya barabara, umeme na TEHAMA, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma inasimamia kazi hiyo ikiwemo suala la ujenzi wa kituo kikubwa cha afya ambacho kitakuwa na huduma zote kwa viongozi lakini pia pia kitatoa huduma kwa wananchi waishio vijiji vya jirani.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka mawaziri walioko Mtumba wajiandae kwani kuna siku atakwenda kufanya vikao vyake kwenye wizara zao kwa sababu amebaini kuwa kila wizara ina ukumbi mkubwa wa mikutano.

Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema jumla ya watumishi 64 wameshamia kwenye ofisi za wizara hiyo ambapo kuna vyumba 25 vya ofisi na ukumbi mmoja wa mikutano. Pia alisema waligawa miche ya miti 13,570 kwa wizara mbalimbali na kwamba katika ofisi yake, wamepanda miti 980.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi (OR-TAMISEMI), Bw. Suleiman Jafo alisema wamekwishahamia tangu Jumatatu iliyopita na kwa sasa wanatumia ofisi za muda ambazo ni za mabati huku wakisimamia ujenzi wa ghorofa yao hadi ukamilike.

Akielezea kuhusu ujenzi wa ofisi hizo ulipofikia, Bw. Jafo alisema ifikapo mwishoni mwa wiki watakuwa wamekamilisha kazi ya kuweka mabati na kupiga plaster. “Tunatarajia kukamilisha kazi ya ujenzi Mei 30, kama ilivyopangwa. Jengo lilikamilika litakuwa na kumbi mbili za mikutano na ofisi za kuchukua watumishi 88,” alisema.

Naye Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alisema kuwa hadi sasa watumishi 73 kati ya 153 ndiyo wamehamia kwenye ofisi mpya za Mtumba. Alisema kwa sasa wanatenegeza eneo la maegesho ya magari na wameshatenga eneo la mgahawa kwa ajili ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa mfano wa nyamera na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala, kwenye ofisi ya Wizara hiyo, wakati akikagua ofisi za Wizara katika mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma, Aprili 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Suleiman Jaffo, kwenye ofisi ya Wizara hiyo ya muda, wakati akikagua ofisi za Wizara kwenye mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma, Aprili 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Suleiman Jaffo, wakati akikagua ofisi za Wizara kwenye mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma, Aprili 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akitoka kwenye jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, wakati akikagua ofisi za Wizara kwenye mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma, Aprili 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi,  wakati akikagua ofisi za Wizara kwenye mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma, Aprili 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MKAZI WA KILOSA,MOROGORO AKABIDHIWA KITITA CHAKE CHA MILIONI TANO KUTOKA BIKO

SABA WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA GEREZANI

$
0
0
 

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu raia saba wa Somalia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya uharamia wa kuvamia meli na kuipiga risasi.

Washtakiwa hao walihukumiwa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Yose Mlyambina baada mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi 14 wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mlyambina amesema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa na wote wametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kufungwa jela maisha.

Washtakiwa waliotiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo hicho ni Mohammed Nuru, Bashir Rooble, Muhsin Haji, Abdulwaidi Abdallahamani, Farahani Abdul, Ally Ally na Omary Mohammed.

Wote walikuwa wanakabiliwa na kosa la uharamia kinyume cha kifungu cha 66(1)(a)((I) na (2) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Katika kesi hiyo upande wa Jamuhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Cecilia Shelly na Wakili wa Serikali, George Barasa huku washtakiwa wakijitetea wenyewe.

Katika hati ya mashtaka imedaiwa, Oktoba 3 mwaka 2011 majira ya saa moja na nusu usiku maeneo ya Bahari ya Hindi, maharamia hao walifanya uvamizi kwenye meli ya Sams All good kwa kuipiga risasi hadi wanajeshi wa majini walipoanza kuipiga boti ndogo aina ya Skiff.

Wanajeshi hao walifanikiwa kuwakamata na kuwafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Pwani na February 29, mwaka huu ikasikilizwa na kutolewa maamuzi.

Wakati wa keai hiyo, washtakiwa waliwakilishwa mahakamani hapo na mawakili, Aloyce Komba, Domicus Mkwera, Rupia Abraham, Omary Msemo, Dennis Tumaini, Benedict Pius na Velasquez Severine.

RC Wangabo apongeza mshikamano na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Jaochim Wangabo akitembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika hospitali ya Wilaya ya Nkasi wakati jengo hilo likiwa katika hatua ya msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Jaochim Wangabo akimpatia fredha ya “kunywa maji” mmoja wa wakinamama kwa niaba ya wakinamama wenzie wanaoshiriki ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Nkasi kama vibarua.

Baadhi ya vibarua wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi wakiendelea na pirika zao wakati Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( hayupo pichani) alipokwenda kutembelea maendeleo ya ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akisaidia kuweka mchanga kwenye viroba kwa mmoja wa kinamama walioshiriki ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi wakati alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Hoachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akipokea maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Nkasi kutoka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Said Mtanda (wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Hoachim Wangabo (wa kwanza kulia) akipokea maelezo ya ufyatuaji wa matofali kwaajili ya ujenzi wa majengo saba ya hospitali ya wilaya ya Nkasi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Said Mtanda na kueleza kuwa matofali yanayohitajika ni 78,000 na hadi tarehe 18.4.2019 tayari wamefyatua matofali 58,000.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akijaribu uimara wa matofali hayo ambayo aliambiwa kuwa mfuko mmoja wa saruji unatoa matofali 20 kwaajili ya kujenga kuta za majengo saba ya hospitali ya wilaya ya Nkasi.

…………………………………………………………………………….

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amepongeza mshikamano uliopo katika uongozi wa wilaya ya Nkasi unaongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mh. Said Mtanda baada ya kuona namna uongozi huo ulivyojipanga katika kuhakikisha maelekezo na maagizo ya serikali yanatekelezwa kwa wakati hasa maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi.

Amesema kuwa mshikamano huo ni tunu kwa wanarukwa katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo na hasa linapokuja suala la utekelezaji wa upatikanaji wa huduma ambazo zinawagusa moja kwa moja wananchi waliokuwa wakisubiri huduma hizo kwa muda mrefu.

“Nimeona kwamba mmejipanga kwa kuleta vifaa, na kama hakuna vifaa ujenzi utasuasua, kuna mawe naona yanakwenda kwasababu yanahitajika kwa kasi kubwa, basi hilo eneo liwekewe nguvu kubwa sana, ndio eneo lenye hitaji kubwa kwa sasa na kama hakuna mawe tutashindwa kusogea hatua ya kuweka matofali hadi kufikia hatu ile ya linta,” alisema

Aliongeza kuwa hivi sasa mvua hakuna, hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha vifaa vyote vinavyohitajika kwaajili ya ujenzi vinakuwa katika eneo hilo la ujenzi ili kila hatua ya ujenzi isikumbane na kikwazo cha kukosa vifaa na kutoa sababu ya mvua kuharibu barabara na hivyo vifaa kushindwa kufika.

Halikadhalika ametoa pongezi kwa namna vibarua wa ujenzi huo wanavyolipwa kwa wakati na kufanya kazi wakiwa wameridhika na malipo wanayopewa jambo linaloashiria kuwa ujenzi huo unakwenda bila ya dosari zozote na kuagiza kuwa hadi kufikia tarehe 10 Mei, 2019 majengo yote saba ya hospitali hiyo yawe yamefikia usawa wa linta ili kwenda na kasi ya utoaji huduma kwa jamii.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipokwenda kuona maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa katika makao makuu ya wilaya ya Nkasi mjini Namanyere ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa juu ya kuwataka Wakuu wa Mikoa kusimamia kwa karibu ujenzi wa hospitali hizo na hatimae kumalizika kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda alisema kuwa ili kuhakikisha vibarua na wagonga kokoto wanalipwa na mafundi walioingia nao mkataba, wameweka utaratibu wa mafundi hao kuwalipa mbele yake, zoezi linalofanyika katika ukumbi wa ofisi yake ya wilaya na wakati huo huo wakitumia fursa hiyo kuwapatia wagonga kokoto hao vitambulisho vya ujasiliamali.

Imeelezwa kuwa ili majengo saba ya hospitali hiyo yakamilike yanahitajika matofali 78,000 huku hadi tarehe 18 Aprili,2019 matofali 58,000 tayari yameshafyatuliwa ili kuendelea na ujenzi huo.

RAIS DKT MAGUFULI AIONGEZEA MUDA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB)

SERIKALI YAKUSANYA KODI YA SH.MILIONI 5554 ZA TAULO ZA KIKE

$
0
0

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)



Serikali imesema kuwa imekusanya Sh. Milioni 3,010.5 kwa mwaka fedha 2016/17 na Sh. Milioni 2,545.6 kwa mwaka wa fedha 2017/18 za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika taulo za kike(sanitary pads) zilizozotengenezwa nchini na zilizoingizwa kutoka nje ya nchi.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Upendo Peneza (Chadema) aliyetaka kujua Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokusanywa na Serikali katika mwaka wa fedha wa 2016/17 na 20017/18.

Dkt. Kijaji alisema kiasi hicho cha kodi kilikusanywa kabla ya kuondolewa kwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)Juni, 2018.

Katika maswali ya nyongeza, yaliyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Dkt. Immaculate Swale kwa niaba ya Mhe. Peneza, alisema pamoja na Serikali kuondoa baadhi ya kodi katika uzalishaji wa taulo za kike lakini bado bei ya bidhaa hiyo ipo juu, na kutaka kujua mkakati wa Serikali kushusha bei ya bidhaa hiyo ili kuhakikisha inawafikia walengwa.

“Kama Serikali imeshindwa kusimamia kushuka kwa bei, haioni kwamba iendeleze zile kodi za awali lakini kodi hii ikusanywe na iwe refinance ili kuweza kununulia hizi taulo za kike na izigawe bure mashuleni”, aliongeza Dkt. Swale.

Akijibu maswali hiyo, Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali haijashindwa kusimamia bei ya bidhaa hizo na kwa sasa inaendelea kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi ili kuona namna bora ya kuwafikia walengwa.

Alisema Serikali inaendelea kufanya tafiti mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuona namna ya kuwasaidia watoto wa kike ila kuna changamoto kodi inakusanywa ikiwekwa kwa ajili ya kununua na kugawa taulo za kike mashuleni.

“Yapo makundi mengine ambayo kodi zinazotozwa kwenye bidhaa zinazotumika na makundi hayo, tutatengeneza ombwe la kila kundi kuja kuomba kodi inayotozwa kwenye makundi hayo waweze kupewa wao”, alisema Dkt. Kijaji.

Aidha, Dkt. Kijaji alishauri kuwa kinachotakiwa kufanywa ni kubuni njia nyingine ili kuona watoto wa kike wanaweza kupata bidhaa hii bila kuhusisha kodi, au tozo zozote zinazotozwa katika bidhaa hii kwasababu imebainika kuwa inapoondolewa kodi wanaonufaika ni wazalishaji kwa kuwa taifa lipo katika soko huria.

Imetolewa na;

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

RC MAKONDA ARIDHISHWA NA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA ILALA

$
0
0
* Asisitiza wazawa kupewa vipaumbele katika utekelezaji wa miradi mikubwa
*Atoa fursa kwa vijana wajasiriamali, neema yanukia

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ilala mradi ambao unatekelezwa na fedha takribani shilingi bilioni 1 na milioni 500 zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo ni soko la kisasa la ghorofa tatu la Kisutu ambalo litakamilika ndani ya miezi 18 (Septemba 9, 2020) kituo cha afya Buguruni na barabara Makonda amesema kuwa kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ilala yenye majengo saba inayojengwa Kivule jijini humo inaridhisha na baada ya kukamilika kwake itawasaidia wananchi wengi wa maeneo hayo pamoja na kupunguza msongamano katika hospitali ya rufani ya Amana huku mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema amehaidi hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu mradi huo utakuwa umekamilika.

Makonda amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo makini katika kuhakikisha wananchi wa chini wanapata huduma muhimu bila kizifuata kama ilivyokuwa awali na amehaidi barabara korofi ya eneo hilo zitashughulikiwa mapema iwezekanavyo.

Aidha amesema kuwa wataalamu wanaosimamia miradi hiyo watoe nafasi kwa wazawa ili nao waweze kunufaika kwa kuwa Mkoa huo una zaidi ya miradi ya shilingi trilioni 3 hivyo ni vyema wazawa wakanufaika.

Akiwa Lumumba Kariakoo Makonda amekutana na vijana wa fani mbalimbali na kuahidi kuwa Serikali itatoa mafunzo bila malipo ya ufundi kupitia VETA kwa vijana wengi kwa fani za ufundi gereji, umeme na vyuma ili kuwajengea uwezo na kuwapa fursa zaidi.

Kwa upande Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema amewataka wananchi kuunga mkono jitihada za serikali katika kuleta maendeleo na wao kama wawakilishi watasimama imara ili huduma muhimu ziweze kuwafikia kwa urahisi.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ukaguzi wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa jijini humo na katika Manispaa ya Ilala amekagua ujenzi wa soko la kisasa la Kisutu, ujenzi wa barabara kata ya Kilawani, Hospitali ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kivule pamoja na ukaguzi wa majengo mapya katika kituo cha afya Buguruni.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  akikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ilala ambayo inajengwa kwa fedha (bilioni moja na milioni 500) zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha huduma za afya leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa ameambatana na  viongozi wa Wilaya hiyo wakati wa kukagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo na amewataka kufanya kazi kwa kasi zaidi na kumaliza miradi hiyo kwa wakati, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya hiyo mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo na amewataka kufanya kazi kwa kasi zaidi na kumaliza miradi hiyo kwa wakati, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na vijana wajasiriamali katika mtaa wa Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo amewahaidi kutolewa bure kwa mafunzo ya ufundi ili kuwajengea fursa na uwezo zaidi leo jijini Dar es Salaam.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 23.04.2019

WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA - DKT. GEORDAVIE KASAMBALE

$
0
0
Na Woinde Shizza  wa Michuzi TV, Arusha
Watanzania dumisheni amani na upendo  uliopo  katika nchi yetu kwani ndio zawadi  pekee tulioachiwa na mwenyezi Mungu, amesema Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako Dkt. Geordavie  Kasambale (pichani) jijini hapa wakati akiongea na waumini Wa kanisa hilo katika ibada ya Chuo cha Manabii kilichopo Kisongo.  

Alisema kuwa Watanzania tunayo amani ambayo tumezawadiwa na Mungu hivyo ni wajibu wa kila MTU kuienzi, kuidumisha   pamoja na kuilinda.

"Unajua Mungu anatupendelea sana Watanzania. Ametupa amani ya nchi yetu...ametufanya tunaishi kwa upendo. Hebu  angalieni nchi zingine wanapigana kila siku... Kuna vita ndugu kwa ndugu hawapendani. Lakini sisi Watanzania tunaishi kwa amani hivyo ni vyema amani hii tuliopewa tuilinde kama vile mboni ya jicho letu" alisema Geordavie

Aidha aliwataka Watanzania kutoruhusu mtu yeyote yule kuingilia amani yetu na kuivuruga kwani hii ni zawadi ya pekee tuliopewa na mwenyenzi Mungu. Pia alimtaka kila Mwananchi kupitia imani yake kuendelea kuombea  nchi yetu ya Tanzania iendelee  kuwa na amani, na pia aliwakumbusha kuwaweka viongozi wetu wa kitaifa akiwepo Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania katika maombi kila siku ili mungu aendelee kuwaongoza na kuwapigania.

Dkt. Kasambale amewataka Watanzania kutii Sheria za nchi bila vurugu, huku akisisitiza wanasiasa kutopandikiza chuki miongoni mwa wananchi badala yake wawaunganishe na kuwafanya kitu kimoja.

HABARI ZA UN LEO

WAFANYABIASHARA WALIOWEZESHWA NA BENKI YA CRDB KWENDA CHINA WAREJEA NCHINI, WAELEZA FURSA WALIZOZIONA

$
0
0
Baadhi ya wafanyabiashara waliopata fursa ya kuhudhuria maonyesho ya kibiashara yaliyoambatana na mafunzo ya uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini China ambao waliwezeshwa safari yao na Benki ya CRDB kwa ushirikiano na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) wakiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es salaam walioporejea nchini baada ya kutembelea viwanda mbalimbali vya nchini China kwa mafunzo. Jumla ya wafanyabiasahara 60 kutoka maeneo mbalimbali nchini walihuhudhulia mafunzo hayo ya siku kumi (10) yatakayo wawezesha kutanua mtandao na kufungua soko jipya la kibiashara baina yao na wale wa kutoka China.
Mmoja wa viongozi wa safari hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Francis Lukwaro akizungumza na waandishi wa habari juu ya fursa za kibiashara walizoziona nchini China ambazo wameahidi kuzifanyia kazi hapa nchini.

Afisa Mahusiano wa Benki ya CRDB, Agnes Ngalo akizungumzia na waandhishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea nchini wakitokea China, walikokwenda pamoja na wafanyabiasha hao kuhudhulia maonyesho ya kibiashara yaliyoambatana na mafunzo ya uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini China ambao waliwezeshwa safari yao na Benki ya CRDB kwa ushirikiano na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) 


Viewing all 109924 articles
Browse latest View live




Latest Images