Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WAZIRI KAIRUKI ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI WAZAWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI ZILIZOPO NA KUSAJILI MIRADI YA UWEKEZAJI

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.  Angela Kairuki ametoa wito kwa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato  Tanzania (ATAPE) na wawekezaji wengine wazawa kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini na kusajili miradi  yao ya Uwekezaji katika Tume ya uwekezaji ya Taifa (TIC).

Kairuki ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa 20 wa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato  Tanzania (ATAPE) Mjini Bariadi, ambapo amebainisha kuwa kwa mwaka huu 2019 wawekezaji wazawa zaidi ya asilimia 72 wamesajili miradi yao ya uwekezaji TIC.

“ Kwa mwaka huu peke yake tumepata wawekezaji wazawa waliosajili miradi yao ya uwekezaji TIC zaidi ya asilimia 72, hii inanipa faraja sana kama waziri wa nchi ninayesimamia uwekezaji ninapoona Watanzania wenzangu wanachangamkia fursa”

"Naomba mchangamkie fursa hizo kwa sababu wawekezaji wa nje tunapenda waje tu endapo watakuja kuungana nasi kwenye mtaji, kubadilishana nasi ujuzi na uzoefu " alisema Kairuki.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara, uwekezaji na kuweka vipaumbele kwa ajili ya kuvutia wawekezaji katika sekta ambazo zitakuwana athari na tija kubwa kiuchumi kwa wananchi, ili kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo,uvuvi, na mifugo ambayo ni maeneo yanayoajiri Watanzania wengi zaidi.

Aidha, Waziri Kairuki amezitaja sekta nyingine za kipaumbele kuwa ni  uzalishaji wa mafuta ya kula kwa kutumia mbegu zinazozalishwa nchini, uzalishaji wa sukari, uzalishaji wa dawa za binadamu, vifaa tiba na kemikali, ujenzi wa miundombinu ya uvuvi wa kisasa, viwanda vya kuchakata samaki, kusindika nyama, viwanda vya kubangua korosho, viwanda vitakavyotumia pamba na viwanda vya  pembejeo na mbolea.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ameipongeza ATAPE kwa jinsi  inavyoshirikiana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji pamoja na huduma nyingine.

Kairuki amesema serikali pekee  haiwezi kutatua changamoto zote hivyo  kwa kushirikiana na wadau ikiwemo taasisi za dini wanaweza kuwahudumia wananchi na kuleta mabadiliko chanya ikiwa ni pamoja na  kuhubiri amani, huku akisisitiza kuwa masomo ya ujasiriamali yanayotolewa kwa wana ATAPE wayatumie kwa manufaa ya kanisa na jamii kwa ujumla.


Awali akimkatibisha waziri Kairuki, mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkutano huo umewasaidia  watu wa  Simiyu  kukutana na watu wa maeneo mengine hatua iliyopelekea kubadilishana uzoefu  sambamba na kuongeza na kupata masoko mapya .

‘’watu wetu wameongeza wigo wa masoko, mmebadilishana uzoefu ....huu ni mkoa wa kibiashara na ni mkoa wenye fursa nyingi;  tunajenga tawi la chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) hivyo ninawaalika wafanyabiashara na Watanzania wote kuja kuwekeza ujenzi wa hosteli eneo lile linalojengwa tawi hilo"alisisitiza Mtaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ATAPE Freddie Manento amesema kwa miaka mitatu ATAPE imewekeza miradi ya bilioni 1.2 katika miradi yenye manufaa kwa kanisa, wanajamii na wana ATAPE.

Alisema wamewekeza kwenye miradi ya maji kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa, miradi ya miti ya matund), korosho na miradi ya mashamba ya mihogo kwa kutengeneza ajira na faida katika vijiji walivyolima mashamba yao.

‘’Wana ATAPE wamejitoa kwelikweli na wameitikia dhana yetu ya kutumia vipaji na rasilimali zetu kwa ajili ya kazi ya MUNGU, hii iko katika mathayo 28;19, 20…hii ndio dhana yao’’ alisema Manento.

Mkutano wa Wanataaluma na Wajasiriamali (ATAPE) kutoka kanisa la Waadventista Wasabato umefanyika mkoani Simiyu kwa muda wa siku sita ambapo umehudhuriwa na wananchama zaidi ya 1500.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi
 Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi
 Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), Bw. Freddie Manento akimtambulisha rasmi  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki (mwenye skafu) kama mwanachama mpya mbele ya wanachama, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho Mjini Bariadi
 Kutoka kushoto Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki, Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati(nchi 11) , Mchungaji Emanuel Pelote, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na Mchungaji Joshua Njuguna kutoka nchini Kenya, wakifurahia jambo wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),  hicho Mjini Bariadi
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka(mwenye shati la Kitenge kushoto) akiimba pamoja na wanakwaya ya Bulka kutoka Jijini Arusha, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),  hicho Mjini Bariadi
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akionesha ngao/tuzo alichopewa na Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),   kama shukrani ya kuwezesha mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho kufanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho Mjini Bariadi
Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la Kaskazini , Dkt. Godwin Lekondayo akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi

ANAYEFELI SOMO LA ELIMU YA DINI ASIAJIRIWE - ASKOFU RWEYONGEZA

$
0
0
Abdullatif Yunus wa Michuzi Tv.

Serikali Kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeombwa kuangalia upya mtaala wa Elimu, hasa somo la Elimu ya Dini ili kuwafanya Viongozi wajao kuwa waadilifu.

Kauli hiyo imetolewa na Askofu Almachiusi Rweyongeza wa Kanisa la Mt. George Parokia ya Kayanga Jimbo la Kayanga Wilayani Karagwe, katika Ibada ya Pasaka iliyoadhimishwa Kitaifa Jimboni hapo.

Katika Ibada hiyo iliyohudhuliwa na Viongozi Mbalimbali waandamizi  Askofu Rweyongeza amesema Viongozi wamekuwa wakiapa kwa Kutumia vitabu vitakatifu pale waingiapo Madarakani, au Ofisi wanazozisimamia ajabu ni kuwa utendaji wao wa kazi hawamshiriki wala kumtanguliza Mungu, hivyo kwa yule atayekuwa amefeli somo la Dini asiajiriwe popote katika sekta yoyote na Ofisi za Umma.

Aidha ameongeza kuwa Serikali kupitia mfuko wa Kunusuru kaya Maskini, TASAF waangalie upya namna ya mfuko huo kuzisaidia kaya hizo katika suala la afya kwa kuzitafutia bima ya afya badala ya kuwapatia pesa tu.

Akitoa salaam zake kwa Niaba ya Serikali Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesisitiza juu ya suala la Ulinzi na Amani wa mipaka ya Nchi, na wananchi kujiepusha na viashiria vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani hiyo huku akiwataka wale wanoingia Nchini kufuata taratibu za Uhamiaji, na wale wanaofanya biashara za magendo kuacha mara moja na pindi wakibainika hakuna msamaha.
 Askofu Almachius Rweyongeza Wa Kanisa la Mtakatifu George akiongoza Ibada ya Pasaka Kitaifa iliyofanyika Kayanga Karagwe Kagera.
 Pichani ni Viongozi Wa Serikali , Kushoto Mkuu Wa Wilaya Karagwe Godfrey Muheluka, Naibu Waziri Wa Kilimo, Innocent Bashungwa (MB), Mkuu Wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco E. Gaguti na Katibu Tawala Wa Mkoa Prof Faustine Kamzola wakiendelea na Ibada ya Pasaka katika Kanisa Mt. George Kayanga


 waumini Wa Dini ya Kikirsto wakiendelea na Ibada ya Pasaka, wakisherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo.
Askofu Almachius Rweyongeza akisalimiana na Viongozi Mbalimbali, Ofisini kwake Mara baada ya kuwasili Jimboni hapo kabla ya kuanza kwa Ibada ya Pasaka.

PASAKA YAWA CHUNGU SRI LANKA, MILIPUKO YAUWA MAMIA

$
0
0
 Makanisa na hoteli zashambuliwa, raia wa kigeni 35 wapoteza maisha.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAKATI  Waumini wa Madhehebu ya kikristo ulimwenguni wakisherekea sikukuu ya Pasaka leo Machi 21, Wananchi wa Sri Lanka wameamshwa na milipuko mikubwa katika Makanisa na Hoteli jijini Colombo.

Katika mashambulio yapatayo matano watu 156 wamethibitika kupoteza maisha huku ikihofiwa kuwa idadi inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengi kuwa katika hali mbaya. Mji mkuu wa nchi hiyo, Colombo kumetokea shambulio linaelezwa kupigwa katika hoteli iliyo karibu na  hifadhi kubwa ya wanyama nchini humo na polisi wameeleza kuwa watu wawili wamefariki dunia.
Aidha milipuko mitatu imetokea katika makanisa (katoliki) na milipuko mingine imetokea katika hoteli za kitalii za Cinnamon Grand, Kingsbury na Shangri -La- iliyopo katikati ya mji wa Colombo.

Mashambulio hayo yamesababisha majeruhi 400 waliokuwa wamekwenda kuabudu katika sikukuu ya Pasaka.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Aljazeera makanisa yaliyoshambuliwa ni pamoja na kanisa la Mtakatifu Anthony Shrine Colombo, kanisa la Mtakatifu Sebastian Negombo linalopatikana kilometa 30 kutoka mji mkuu pamoja na kanisa la Batticaloa lililopo kilometa 250 Mashariki kutoka Mji wa Colombo.
Waziri mkuu nchini humo Ranil Wickremesinghr ameitisha kikao cha dharura cha viongozi wa juu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo na kuelekeza kuwepo kwa kikao cha dharura cha Bunge mapema Jumatatu.

Msemaji wa polisi Ruwan Gunasekera amesema kuwa majeruhi wamekuwa wakiokolewa huku Polisi wakiendelea na uchunguzi.

Picha katika mitandao ya kijamii zilionyesha paa za makanisa hayo zikiwa zimeharibiwa kwa milipuko hiyo huku watu wakionekana wametapakaa damu.
Vilevile imeelezwa kuwa kati ya watu waliopoteza maisha watu 35 ni raia wa kigeni na bado washambuliaji hawajafahamika.

Katika kikao cha dharura kilichofanyika mapema baada ya tukio hilo waziri wa uchumi na masuala ya umma Harsha de Silva kupitia mtandao wa tweeter ameandika kuwa mashambulio mawili yametekelezwa nchini humo wengi wameathirika wakiwemo wageni na amewataka wananchi kuwa watulivu na kubaki majumbani.

Introducing No more Fear (Official Music Video) by Ritha Komba

Ibada ya Pasaka Karagwe/Askofu Almachius wa Kanisa la Mt. George Jimbo la Kayanga atoa neno hili..

BONANZA LA PASAKA: Muhimbili yaicharaza Mwera FC ya Zanzibar Goli 1-0

$
0
0
Timu ya mpira wa miguu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendelea kuonyesha ubabe kwa timu mbalimbali zinazoshiriki michezo ya Pasaka inayofanyika Zanzibar baada ya kuichapa timu ya Mwera Fc goli 1-0 katika Viwanja vya Mbweni.

Tangu kipindi cha kwanza timu hizo zimeonyesha kandanda safi huku zikishambuliana kwa zamu lakini hadi zinakwenda mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeona goli la mwenzake. 

Aidha, mara baada kipenga kupulizwa kipindi cha pili timu ya Muhimbili ilianza kwa kasi hivyo kupata goli la mapema dakika ya 51 kupitia kwa kiungo hatari Emmanuel Teophil.

Ushindi huo umeshuhudiwa na Mkurugenzi wa Kinga, Zanzibar Dkt.Fadhili Mohamed na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. Praxeda Ogweyo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Naye kocha wa timu ya Muhumibili  Teophil Joseph amesema mchezo ulikuwa mgumu na kwamba ushindi umepatikana kutokana na  maelekezo ya kocha. 

“Tunashukuru tumeshinda mechi japo kipindi cha kwanza kulikuwa na makosa madogo madogo hivyo kipindi cha pili tumerekebisha makosa hayo na kuweza kupata ushindi," amesema kocha Teophil.
 Mkurugenzi wa kinga Dkt. Fadhili Mohamedi akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kuanza kwa mchezo huo katika uwanja wa Mbweni,Zanzibar.
 Baadhi ya washabiki na wachezaji wa timu ya Muhimbili wakifuatilia mtanange huo kwa makini.
Mchezaji wa  timu ya muhimbili, Emmanuel Teophil akifunga goli la kwanza dhidi ya Mwera Fc  ya Zanzibar.

DC KINONDONI AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI KULIPA KWA WAKATI KODI YA MAJENGO,MABANGO

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar as Salaam Daniel Chongolo amezindua kampeni maalum ya kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulipa kwa wakat kodi ya majengo pamoja na kodi ya mabango.

Kampeni hiyo itakwenda sambamba na kampeni ya nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuhakikisha wamiliki wote wa majenga wanalipa kodi kwa wakati na lengo la Wilaya ya Kinondoni ni kukusanya Sh.bilioni saba katika majengo.

Akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar as Salaam wakati wa kuzindua kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Bunju, Chongolo amesema lengo la kuzinduliwa kampeni hiyo ni kuhamasisha wananchi kuanza kulipa kodi ya majengo na mabango mapema.

Ameongeza kuna tabia ya wananchi wengi kujitokeza siku ya mwisho katika kulipa kodi ya majengo kiasi cha kusababisha msongamano mkubwa wa watu,hivyo Wilaya ya Kinondoni imeona ni vema ikaanza kampeni hiyo ili wananchi waanze kulipa kuanzia sasa  na mwisho ni Juni 30,2019.

Chongolo amesema katika kufanikisha kampeni hiyo viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya wakiwamo watendaji wa mitaa na kata watashirikiana na.maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwenda kufanya hamasa hiyo kwa wananchi na kubwa zaidi kutambua umuhimu wa kulipa kodi ya majengo na mabango.

"Kutakuwa na utaratibu maalumu wa kila mwenye jengo kupewa stakabadhi inayoonesha kodi anayostahili kulipa na kisha atakwenda kulipa na watendaji watakuwa wakiwaelekeza wananchi pakwenda kulipa kodi yao.

"Serikali kwa kuwajali wananchi wake imeamua kodi ya jengo kuwa moja tu iwe ni Sh.10,000 tu.Hivyo mwenye nyumba moja atalipa kiasi hicho na mwenye nyumba mbili atalipia kila nyumba kwa Sh. 10,0000.

"Kwa wenge ghorofa kila floo italipiwa sh.50,000.Makadirio yetu na matarajio ambayo tumejiwekea ni kukusanya Sh.bilioni saba kutoka kwenye majengo.Kampeni hii ambayo tumeizundua tunaomba wananchi washiriki kikamilifu ili kufikia malengo ambayo Wilaya ya Kinondoni tumejiwekea," amesema Chongolo.

Hata hivyo amesema baada ya kampeni ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya majengo,yeye mwenyewe kwa kushirikiana na viongozi wa Kara,mitaa na maofisa wa TRA watakwenda nyumba hadi nyumba kuangalia nani amelipa na na hajalipa kodi.Hivyo amesema cha msingi wananchi kulipa ndani ya muda uliowekwa.

 Kwa upande wake Meneja wa TRA Wilaya ya Kinondoni jijini Dar as Salaam Masawa Masatu amesema wamejipanga kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na watafanya hamasa maeneo yote ndani ya Wilaya huku akifafanua changamoto ya wananchi kusubiri tarehe za mwishoni wanataka kuiondoa.

"Kuna tabia ya baadhi ya wananchi ambao wao wanasubiri tarehe ya mwisho ndio wanakwenda kulipa kodi ya majengo.Kinondoni tunasema watu walipe kodi ndani ya muda uliopo kwani itaondoa msongamano kwenye maeneo ya kulipia kodi.Katika majengo tunakadiria kukusanya Sh.bilioni saba," amesema Masatu.

Wakati huo huo Mtendaji wa Kara ya Bunju Ibrahim Mabewa amesema kuwa jukumu lao ni kushiriki kikamilifu kuhakikisha hamasa ya wananchi kulipa kodi inafika kwenye.mitaa yote na hatimaye kodi ikusanywe kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.

Naye Msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba ambaye naye alishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo amesema wasanii wanalojukumu la kuhamasisha ulipaji wa kodi na kufafanua tena wanapaswa kuhamasisha kwa lugha rahisi ambayo itafanya mwananchi alipe kodi.

Amesema suala la kodi hata huko miaka ya nyuma inaelezwa namna lilivyokuwa ugumu maana unapozungumzia kodi unazungumzia fedha,hivyo kazi ya wasanii ni kutoa lugha rahisi lakini yenye kuzungumzia umuhimu ya wananchi kulipa kodi.
WASANII wa kundi la  ngoma za asili linaloongozwa na msanii nyota Mrisho Mpoto, wakitoa burudani kwa kutumia nyoka aina ya chatu, Barabara ya Bagamoyo eneo la Bunju A, ikiwa ni kuhamasisha wananchi kulipa kodi ya nyumba na mabango, wakati wa uzinduzi wa wiki ya ulipaji kodi hiyo, Wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, jana.(Picha na Christopher Lissa).

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 22,2019


AJALI YAUA WATU 2 NA KUJERUI WENGINE 5 ARUSHA

$
0
0

Na. Vero Ignatus Arusha

Watu wawili wamefariki na watano kujeruhiwa, katika ajali iliyotokea majira ya saa tisa alasiri, katika barabara itokayo Arusha kwenda Namanga, eneo la Oldonyosambu ambapo imeusisha magari mawili madogo toyota T612 saloon na Mitsubish saloon KCH 665

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema chanzo chake ni uzembe na mwendo kasi. 

'' Dereva wa gari la dereva wa gari ya nyuma alikuwa anakata kona kuelekea ngarenanyuki mkono wa kulia na gari ya nyuma ikaovatake mkono wa kulia ndipo yakagongana. Amesema Kamanda Shanna '' 

Kamanda Shanna amewataja waliofariki ni dereva aliyetambuliwa kwa jina la Onesmo Machia Mwangi miaka 20 ni mfanyabiashara raia wa Kenya na mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Hendry

Amesema majeruhi wote wanatibiwa katika hospitali ya Serilani Ngaramtoni ila hali zao bado ni mbaya.

Aidha amesema Jeshi la Polisi halikubaliani uzembe wowote unaofanywa na madereva wakiwa barabarani na ametoa onyo kwa madereva ambao wanaendesha magari wakiwa wamelewa sheria itachukua mkondo wake. 

TANZIA: Mwenyekiti Chama cha mpira wa Miguu Kinondoni (KIFA) Mzee Lupiana afariki Dunia

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu cha Manispaa ya Kinondoni (KIFA) na  mjumbe wa Chama Cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Simon Lupiana (72) maarufu kwa jina la Mzee Lupiana (pichani) amefariki Dunia baada ya kugua muda mfupi.
Mtoto wa marehemu, Lupiana Lupiana alisema kuwa baba yake alilazwa Hospitali yaTaifa ya Muhimbili siku ya Ijumaa Kuu akisumbuliwa na shinikizo la damu (Pressure) na Kisukari ambayo yalisababisha matatizo ya figo na kufariki dunia saa 5.30 usiku wa sikukuu ya Pasaka.
Lupiana alisema kuwa msiba kwa sasa upo nyumbani kwao, Kimara Stop Over na wanatarajia kuzika siku ya Jumatano kwenye makaburi ya Kinondoni.
 “Kwa sasa tupo katika harakati za kukamilisha masuala mbalimbali ya msiba wa mpendwa Baba yetu na matarajio ni kumpunzisha katika nyumba yake ya milele siku ya Jumatano kwenye makaburi ya Kinondoni, taratibu nyingine zitatolewa baadaye,” alisema Lupiana.
Hiki kilikuwa kipindi cha pili cha uongozi cha marehemu Mzee Lupiana ambapo mwakani alikuwa anamalizia muda wake.
 Mbali ya kuwa kiongozi wa mpira, marehemu pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wa wadogowadogo madini ya kujengea (DACOREMA) na aliwahi kuwa diwani wa Kata ya Kinondoni.
Attachments area

Diamond Platnumz's new hit "The One" (Official Music Video)

maadhimisho Siku ya Malaria nchini kufanyika April 25, Mkoani Lindi.

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jisnia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema mapambano dhidi ya Malaria yanaonesha mafanikio makubwa kutokana na kushuka kwa Maambukizi hayo kutoka aslimia 14.5 mwaka 2015 hadi kufikia aslimia 7 mwaka huu.

Waziri Ummy amesema licha ya kushuka kwa maambukizi hayo lakini bado kuna mikoa kadhaa ambayo bado maambikizi ya ugonjwa wa Malaria yapo juu na hivyo kutoa wito kwa wadau kuongeza jitihada katika kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.

Mhe. Waziri ameitaja mikoa ambayo maambukizi ya ugonjwa Malaria yapo juu kuwa ni pamoja na Mara, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo amewataka wananchi kuongeza jitihada katika kupunguza kiwango cha Ugonjwa huo.

"Licha ya jitihada zinazofanywa kumaliza ugonjwa huu lakini bado jitihada zinahitajika zaidi katika kufikia lengo la ZERO MALARIA ifikapo 2030". Amesisitiza Mhe. Ummy.

Kuhusiana na maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Malaria Duniani, Mhe. Ummy amewataka wananchi wote kushiriki katika kufikia lengo la Zero Malaria kwa kutomeza mazalia ya Mbu, kutumia vyandarua vilivyowekwa Dawa, kwenda hospitalini pindi wanapohisi wana viashiria vya Malaria na kumaliza dozi kama watakavyo elekezwa na watalaamu wa Afya.

"Wito wangu kwa watanzania wote ni kuhakikisha wanafuata maelekezo ya watoa huduma za afya pindi wauguapo Malaria na pia kuweka mazingira yao safi ili kukabiliana na mbu waenezao Ugonjwa wa Malaria" Alisema Mhe. Waziri.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Malaria kwa Mwaka huu ni ZIRO MALARIA INAANZA NA MIMI huku maadhimisho ya Siku ya Malaria hapa nchini yanatarajiwa kufanyika April 25, Mkoani Lindi.

KITAMBI NOMA YATWAA UBIGWA BONANZA LA PASAKA

$
0
0

Na woinde Shizza ,Michuzi TV Arusha

Timu kitambi noma ya jijini Arusha imefanikiwa kuutwaa ubigwa na kuondoka na kombe Mara baada ya kuichapa timu ya Moshi veteran bao 1 kwao.

Hayo yote yalijiri Jana katika fainali ya bonanza la pasaka lililoandaliwa na timu ya kitambi noma ya jijini hapa ambapo katika bonanza hilo timu zaidi kumi imeshiriki zikimo za ndani ya nchi pamoja na nje ya nchi.

Timu ambazo zimeshiriki bonanza hill no pamoja na Moshi veteran ,mango garden veteran ya jijini dar es salaam, lushoto veteran ,Nairobi west ya Kenya ,Green Yard ya Kenya ,Sua Veterans ya Morogoro,Paris Fc Wa Nair obi, Makabe veterans pamoja na Arusha Coaches.

Akiongelea mashindano hayo Mwenyekiti Hamis Tembele alisema kuwa wameandaa mashindano haya kwa nia ya kukutanisha wadau na kubadilishana ,ujuzi ,biashara pamoja na undugu .

Alisema mashindano haya yanashindikisha Wazee ambao ni maveteran kutoka sehemu mbalimbali Wa ndani ya nchi pamoja na nje ya nchi.

Kwa upande wake msemaji Wa klabu ya kitambi noma ambaye ni waandaaji Wa bonanza hili LA pasaka Imma Diah alisema kuwa kwakuwa michezo ni furaha ajira na pia inatengeneza afya wameona waandae ili Wazee waendelee kujiburudisha na kuweka miili yao katika hali nzuri ya kiafya.

Kwa upande wake mthamini mkuu Wa mashindano haya Meneja masoko kanda ya kaskazini Wa kampuni Wa TBL Goodluck Kway ambao wamethamini bonanza hili kupitia kinyaji chao cha Konyagi alisema kuwa wameamua kuthamini bonanza hili kwakuwa linaamasisha michezo na wao kama wapo tayari kusaidia vitu vyote vinavyohamasisha amani na upendo.

Akiongea kwa niaba ya mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo,ambaye alikuwa mgeni rasmi Wa mashindano haya Afisa utamaduni Wa jiji LA Arusha Benson Maneno alisema aliwapongeza waandaaji Wa mashindano haya na kusema kuwa wamefanya jambo jema sana kuwakutanisha maveteran kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi

Aliwasihi wasiishie pia kushabikia timu za verterani tu Bali waendelee at a katika timu zetu za mikoani pamoja na taifa.

Katika bonanza hili timu ya kitambi noma ilishika nafasi ya kwanza na kuondoka na kombe kubwa pamoja na zawadi ya box LA konyagi,mshindi Wa pili alikuwa ni Moshi veteran ambao wameondoka na kombe huku nafasi ya tatu imechukuliwa na timu ya Lushoto veteran ambao imeondoka na kombe Dogo.
Mdhamini Mkuu wa mashindano Meneja masoko kanda ya kaskazini Wa kampuni Wa TBL Goodluck Kway akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Afisa utamaduni wa jiji la  Arusha Benson Maneno kwa kuwashukuru kuhudhuria katika bonanza hilo

Tanzania kuwakillishwa na waogeleaji wanne mashindano ya Dunia

$
0
0
Chama Cha mchezo wa kuogelea nchini (TSA) kimetangaza majina ya waogeleaji wanne ambao wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika katika mji wa Gwangju, Korea Kusini.

Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro amewataja waogeleaji hao ni Hilal Hemed Hilal na Collins Saliboko ambao watashindana kwa upande wa wanaume ambapo kwa upande wa wasichana ni Sylvia Caloiaro na Shivani Bhatt.

Waogeleaji hao kwa sasa wapo katika maandalizi makali kwa ajili ya mashindano hayo yaliyopangwa kuanza Julai 18 mpaka 29.

Hilal kwa sasa anafanya mazoezi Dubai kufuatia udhamini wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (Fina), nchini Dubai na Collins anajifua shuleni kwake, St Felix Uingereza huku Sylvia na Shivani wanatoka klabu ya Taliss-IST wanafanya mazoezi hapa hapa nchini.

Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa aaogeleaji hao wamepata nafasi hiyo baada ya kukidhi vigezo mbalimbali vilivyowekwa.

Inviolata alisema kuwa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (Fina) litagharimia waogeleaji watatu na kocha mmoja katika mashindano hayo huku muogeleaji wanne atatakiwa kugharimiwa na chama husika kwa kupitia wadau wa mchezo.

“Waogeaji watatu, kocha na kiongozi wa TSA mmoja watagharimiwa na Fina. Waogeleaji watatu ni Hilal, Collins na Sylvia. TSA inaomba wadau kufanikisha safari ya muogeleaji wan ne ambaye ni Shivani ili naye kwenda kushindana,” alisema Inviolata.

Alisema kuwa waogeleaji hao kwa sasa wapo katika maandalizi kuelekea mashindano hayo ambapo Tanzania itakuwa inawakilishwa na waogeleaji wanne kwa mara ya kwanza.

“Waogeaji wetu wamepania kuhimarisha muda wao wa kuogelea ‘Personal Best time’ katika mashindano hayo ambayo ni makubwa sana duniani. Kutokana na hilo, wameamua kujiandaa vilivyo ili kufikia malengo yao na kupromoti mchezo kwa ujumla,” alisema.

MBUNGE VULLU NA DAU WATOA MSAADA WA VIFAA MAFIA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,  Mafia

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Pwani ,Zaynabu Vullu, ametoa kitanda na vifaa tiba katika zahanati ya Kijiji cha Malimbani ,wilayani Mafia.

Aidha mbunge wa Jimbo la Mafia Mbaraka Dau nae amekabidhi mashine ya kusambazia maji, kata ya Kiegeani ili kuwarahishia wakazi hao kupata huduma hiyo kupitia kisima kilichochimbwa eneo hilo.

Vullu alikabidhi vifaa hivyo ,wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku mbili wilayani Mafia, kwa lengo la kutimiza ahadi yake ya kukabidhi vifaa hivyo vinavyolenga kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wakazi hao, ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Dau.

Alisema , anaunga mkono juhudi za serikali  kwa kununua kitanda, na vifaa tiba vitavyosaidia wagonjwa wataokwenda kupatiwa huduma kwenye zahanati hiyo.
"Niwapongeze kwa umoja, upendo na mshikamano ambao mnaendelea kuuonyesha katika kujiletea maendeleo, nami leo nimekuja kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuelekeza nguvu katika kuboresha sekta ya afya" alisema Zaynab.

Nae Dau alielezea kwamba ,amenunua mashine hiyo inayolenga kuboresha upatikanaji wa maji katika kisima kilichopo, ambacho kwa sasa ni cha mdundiko.

Alielezea, baada ya kufungwa mashine maji yatakuwa yanasambazwa umbali wa mita 1,000. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwajupi Abdallah Sharifu aliwashukuru wabunge hao kwa namna walivyojitoa katika sekta hizo.

RPC SHANNA ATAJA MAJINA YA MAJERUHI WA AJALI/DC MURO ATEMBELEA MAJERUHI

$
0
0


Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna alipotembelea eneo la oldonyosambu ajali ilipotokea jana na kusababisha vifo vya watu wawili.
Kamanda wa wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akitolea ufafanuzi ajali iliyotokea jana eneo la Oldonyosambo barabara ya Arusha Namanga.,Kulia kwakwe ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa Joseph Bukombe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akipokea maelezo kitoka kwa Dkt. Wa Halmashauri ya Arusha Petro Mboya katika hospital ya Seliani
Mkuu wa wilaya ya Arumeru jerry Muro akimjulia hali mmoja wa majeruhi aliyelazwa katika hospitali ya Seliani Ngaramtoni.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Arusha Dkt Petro Mboya akifafanua jambo kwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro.


Na. Vero Ignatus, Arusha

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa onyo kali kwa madereva ambao wanendesha magari bila kufuata sheria usalama barabarani na kusababisha ajali katika kupoteza maisha ya watu sababu ya uzembe.

Onyo hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kutokana na ajali iliyotokea jana eneo la Oldonyosambu na kusababisha vifo vya watu 2 na wengine 5 kujeruhiwa vibaya, amesema kwa dereva atakayekutwa na kosa la uzembe sheria itafuata mkondo wake.

Vilevile RPC Shanna ametoa onyo mitandao ya jamii ambayo inatoa taarifa ambazo siyo sahihi hazijathibitishwa, amesema mitandao mingi hapo jana ilieneza uvumi kwamba watu waliofariki ni 8 wakati siyo kweli na ikaleta taharuki katika jamii.

Amewataja majina kuwa ni bwana Robby Alan (kenya) Rajab Essa (mmakoe) (31)mkazi wa Arusha, Robby Mkurya (kenya) Anold Twahir (mshirazi) mkazi wa Arusha Shadrack Anold (13)ni mwanafunzi mkazi wa Arusha, Stellah Mathon Mngai(kenya ) (21)Bosco Mshanga mkazi wa Arusha wote hawa walikuwa abiria ndani ya magari hayo na wawili kati yao hali zao ni mbaya.

RPC amesema mbali na tukio hilo lililoleta majonzi, mkoa wa Arusha upo swari hakuna matukio mengine katika msimu huu wa sikukuu wala uhalifu kwani jeshi la polisi lilijipanga vilivyo na wananchi walionyesha ushirikiano mkubwa.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya Oldonyosambu inayodaiwa kuwa katika ajali hiyo watu nane Walifariki dunia kitu ambacho siyo kweli katika ajali hiyo watu wawili ndio Walifariki dunia.

Muro Ameyasema hayo mara baada ya kuwatembelea Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Selian Lutheran Ngaramtoni ambapo ilitokea katika eneo la Oldonyosambu na kuwataka wananchi kuacha kukurupuka na kuandika ovyo katika mitandao ya kijamii vinavyozua taaruki pindi tatizo linapotokea badala yake wasubiri taarifa kutoka mamlaka husika.

Amewataka wananchi wa Arumeru na mkoa wa Arusha iwapo watataka kufanya matukio yoyote ambayo yatakuwa na kusanyiko lolote linalolenga shughuli pembezoni mwa barabara lazima tukio hilo liripotiwe kwa serikali ili serikali iwaandalie vitu vya Usalama na watu waache kufanya vitu kwa mazoea kwani serikali haiendeshwi kwa mazoea.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Petro Mboya amekiri kupokea miili miwili ya watu waliofariki hapo jana,majeruhi ambao wanaendelea kutibiwa ambapo wawili wameumia vichwani, mmoja uti wa mgongo na wengine wapo ICU ambapo mmoja wamemuhamisha kwaajili ya kufanyiwa vipimo zaidi.

VODACOM YATOA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA ZA KIFEDHA KWA WANAFUNZI IFM

$
0
0

Meneja wa Biashara na Mkakati wa Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Caleb Majo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Semina hiyo imefanyika chini ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Green Hope ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapata ufahamu wa teknolojia hizo na mchango wake katika kuchochea ushirikishwaji wa kifadha.
Meneja wa Biashara na Mkakati wa Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Caleb Majo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja mauzo wa eneo la katikati ya jiji wa Vodacom Tanzania Plc, George Nyanda (kulia) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jana jijini Dar es Salaam. Semina hiyo imetolewa chini ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Green Hope ili kuhakikisha vijana wanapata ufahamu wa teknolojia hizo na mchango wake katika kuchochea ushirikishwaji wa kifedha.
Meneja mauzo wa eneo la katikati ya jiji wa Vodacom Tanzania Plc, George Nyanda (kulia) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa teknolojia za kifedha jana jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 23,2019

Serikali yazitaka Muhimbili na Mnazi Mmoja kudumisha ushirikiano

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Harusi Suleiman amezitaka Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- na Mnazi Mmoja kudumisha uhusiano na ushirikiano uliopo ili kuwaenzi waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Naibu Waziri Suleiman ametoa kauli hiyo katika hafla ya kuhitimisha tamasha la Pasaka   2019 lililofanyika Visiwani Zanzibar na kuhusisha timu za michezo za Muhimbili pamoja na Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo visiwani humo.

Akizungumza katika hafla hiyo amesisitiza kwamba timu hizo zimekuwa zikikutaka kila mwaka kwa lengo la kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya pande hizo mbili ambapo mwaka jana tamasha hilo lilifanyika Tanzania Bara. “Ndugu zangu tumefarijika kuja kututembelea katika pasaka hii tunaomba ushirikiano huu uendelezwe kwa faida ya pande zote mbili, pia kikubwa nilichofurahishwa kutoka kwenu ni nidhamu pamoja na maadili kwani hata katika michezo tunasisitiza nidhamu na maadili hakika mnastahili pongezi”. Amesema Naibu Waziri wa Afya Zanzibar.

“Lakini pia yapaswa kuwashukuru viongozi wetu ambao walianzisha muungano wetu ambao umetuwezesha kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo michezo hivyo hatuna budi kuwaenzi kwa kuendeleza na kuiboresha zaidi michezo hii ambayo ilianzishwa mwaka 1972”. Amesisitiza Mh. Suleiman.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi kutoka Muhimbili Dkt. Praxeda Ogweyo, amewapongeza wanamichezo wote walioshiriki katika tamasha la Pasaka 2019 na kueleza kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ipo mstari wa mbele katika kuhakikisha michezo inaendelezwa katika taasisi hiyo na kutoa fursa kwa watumishi wengi kushiriki.
Naibu Waziri wa Afya Mh. Harusi Suleiman akizungumza na wanamichezo katika hafla ya ufungaji wa tamasha la pasaka liliofanyika Zanzibar na kuhusisha timu za Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt. Praxeda Ogweyo, akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga tamasha hilo.
Baadhi ya wanamichezo wakikiliza neno kutoka kwa Naibu waziri wa Afya.

Wateja wa Tigo Kilolo wapata huduma ya kasi zaidi ya 3G

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kililo Mkoani Iringa Philemon Namwenga  (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete, Wilaya Kilolo, mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani na wa kwanza kulia ni diwani wa viti maalum kata ya Idete Elina Kivegele na anayemfuatia ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai.
 Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kililo Mkoani Iringa Philemon Namwenga (wa pili kulia) muda mfupi baada ya uzinduzi wa mnara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai  diwani wa viti maalum kata ya Idete Elina Kivegelea
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Philemon Namwenga pamoja na Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani, wakisalimiana na wananchi wa kijiji cha Idete Wilayani Kilolo mkoani Iringa muda mfupi baada ya uzinduzi wa manra mpya wenye uwezo wa 3G kijijini hapo.
Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Abbas Abdurahamani (wa pili kushoto) akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Philemon Namwenga baadhi ya smart phone za gharama nafuu zinazouzwa na kampuni ya Tigo muda mfupi baada ya uzinduzi wa mara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete wailayani Kilolo. Wa kwanza kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai.

Kampuni ya mawasiliano ya simu, Tigo, leo imezindua mnara wa 3G katika kata ya Kidete, mkoani Iringa kama moja ya jitihada zake za kufikisha huduma bora za kupiga na kupokea simu, intaneti na kutuma na kupokea pesa kwa wateja wake.
Akizungumza katika uzinduzi huo katika kata ya Idete, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo, Aloyce Kwezi, aliwakaribisha na kuwashukuru Tigo kwa kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka teknolojia ya 2G hadi 3G.

Serikali ya Tanzania imefanya suala la viwanda kuwa agenda yake kuu. Na sisi kama serikali tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika kufanikisha hii dira. Tunapenda kuwashukuru sana kwa kuifikiria Kilolo na wananchi wake, maana sekta hii ya mawasiliano ni chachu kubwa sana katika ukuaji na ubunifu wa viwanda mbalimbali,” alisema Kwezi. 

Kwa upande wake, Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini, Abbas Abdurahamani, alisema kwamba kipaumbele ya Tigo ni kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma za kisasa za kiteknolojia za simu kama ya 3G.
Uzinduzi wa leo unaofanyika Kilolo ni mwanzo wa kampeni ya nchi nzima ambapo kutakuwa na uzinduzi wa minara 52 kutoka Tigo zitakazo zinduliwa kutoka kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini. 

Uzinduzi wa minara uaenda sambamba na ofa maalum. Wateja ambao watahudumiwa na minara ambayo imeongezewa uwezo kutoka 2G hadi 3G. Wateja watazawadiwa kiasi cha MB 100 za data kila mara watakaponunua kifurushi chochote cha intaneti. Huku wateja katika maeneo ya minara ya 4G itakayozinduliwa, watazawadiwa GB 4 za data bure pale wanapobadilisha laini zao za simu kuingia 4G. 

“Kuongeza ubora wa mnara huu kutoka 2G kwenda 3G ina maana kwamba wateja wetu wa Kilolo sasa wataweza kupata huduma rahisi na kasi zaidi. Kwa mfano, 3G itaweza kuwapatia huduma ya intaneti iliyo bora ambayo itafungua jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma. Jambo hili litabadilisha namna watu watakavyojifunza na kufanya biashara,” alisema Abdurahamani. 

Abdurahamani pia alisisitiza kuhusu kazi ambayo Tigo inafanya kuwezesha sera ya TEHAMA ya Taifa na kuunga jitihada ya serikali katika viwanda kwa kupanua na kuboresha wigo wa mtandao ili kuwezesha nchi kufaidika katika nyanja mbali mbali za kijamii kama uchumi na elimu kupitia mfumo wa kidijitali. 

Minara mengine ambayo imeboreshwa na zitazinduliwa hivi karibuni katika Kanda ya Kusini ukiondoa Kilolo zinapatikana katika maeneo ya Sumbawanga, Katavi, Mufindi, Njombe, Songwe, Mbeya and Songea.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images