Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

INTRODUCING “SHILINGI” (official video) by Aky Banguliny


INTRODUCING “SOLEMBA” (official music video) by Kassim Mganga

MICHEZO YA BONAZA LA PASAKA VIWANJA VYA MAO: IKULU ZANZIBAR NA IKULU DAR ES SALAAM ZAPAMBANA VIKALI

$
0
0
 WAFANYAKAZI wa Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuaza kwa mchezo wa mpira katika Bonaza la Michezo ya Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's. Zanzibar 
 NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Kassim Ali akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam, kabla ya kuaza kwa mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar.
 MCHEZAJI wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Azori Ndege mwenye mpira akimpita beki wa Timu ya Ikulu Sports Clun Zanzibar Khamis Bakari wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Pasaka uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Zanzibar imeshinda bao 6-2
 MSHAMBULIAJI wa Timu ya Ikulu Sports Club Zanzibar Rajab Wakil akimpita Beki wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Hokororo Sadiq, wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Sports Club Zanzibar imeshinda mchezo huo kwa bao 6-2.
 MSHAMBULIAJI wa Timu ya Ikulu Sports Clun Zanzibar Omar Hamad akijaribu kumpita Beki wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Hassan Econ, wakati wa mchezo wao wa kusherehekea Michezo ya Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Zanzibar imeshinda bao 6-2.
 MSHINDI wa mbio za Mita Mia Moja kutoka Ikulu Zanzibar Vuai Suleiman akiongoza mbio hizo na kufuatiwa mshindi wa Pili kutoka Ikulu Dar es Salaam Mwabora Richard
 WASHIRIKI wa mchezo wa kufukuza Kuku kutoka Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam wakishiriki mbio hizo za kufukuza kuku mshindi kutoka Ikulu Zanzibar Bi. Susiati Nyange.


WANAMICHEZO kutoka Timu ya Ikulu Sports Clun Dar es Salaam, wakisoma dua wakati walipotembelea Kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwangui Zanzibar, baada ya kumaliza mchezo wao leo.(Picha na Ikulu Zanzibar)

JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO

$
0
0
 Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV 

Klabu ya Soka ya Juventus ya Italia imeweka rekodi mpya barani Ulaya na nchini Italia baada yakutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini humo maarufu kama Serie A mara nane mfululizo. 

Juventus inakuwa timu ya kwanza kuweka rekodi hiyo, ambapo hakuna timu katika Ligi tano bora la Ulaya iliyofanya hivyo. 

Juventus maarufu kwa jina la Bianconeri ilikuwa ikihitaji alama moja tu katika mchezo wake waliotandikwa bao 2-1 na SPAL, hivyo ikashindikana kutangaza ubingwa huo, katika mchezo wake dhidi ya Fiorentina, Juventus iliondoka na ushindi wa bao 2-1, hivyo kutangaza ubingwa huo. 

Katika mchezo huo dhidi ya Fiorentina, Juventus walitoka nyuma kwa bao la Nikola Milenkovic dakika ya 6, kabla ya Alex Sandro kusawazisha dakika ya 37 na bao lakujifunga la Beki wa Kati wa Fiorentina, Germàn Pezzella dakika ya 53, hivyo kufanya jumla ya bao 2-1.

Ushindi huo umepelekea Juventus kutwaa taji la Serie A mara 8 mfululizo, rekodi ambayo haijawekwa na timu yoyote katika bara la Ulaya. 

Ikiwa na mchezo 150 katika Uwanja wake wa nyumbani, imeshinda michezo 127, mabao yakufunga 335.

MAX ALLEGRI AWEKA REKODI YA KOCHA WA KWANZA KUTWAA MATAJI MATANO MFULULIZO 

Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri baada ya timu hiyo kutwaa Ubingwa wake mara nane mfululizo, anakuwa Kocha wa kwanza kutwaa mataji matano ya Ligi (Serie A).

Allegri anatwaa mataji hayo matano baada yakuachiwa mikoba na Kocha Antonio Conte aliyetwaa mataji hayo mara tatu. 

Rekodi hiyo inamuweka Kocha huyo katika nafasi ya pili, nyuma ya Giovanni Trapattoni anayeshikilia mataji Saba ya Serie A.

Juventus watakabidhiwa Kombe lao katika mchezo unaofuata dhidi ya Atalanta, nyumbani.

SERENGETI BOYS YAAGA MASHINDANO WAKISHIKILIA MKIA KUNDI A

$
0
0
Wenyeji wa mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON)  kwa chini ya vijana wa miaka 17 timu ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ wameondoshwa kwenye mashindano hayo wakiwa na alama sifuri. Serengeti Boys Wamemaliza kundi A wakiwa hawajafanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo wowote kati ya mitatu waliyoicheza.

Kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Angola Serengeti Boys walihitaji ushindi wa goli 4-0 na kumuombea Uganda apoteze mchezo wake dhidi ya Nigeria.

Katika mchezo wa leo, Serengeti Boys ndio wa kwanza kuliona lango la Angola katika dakika ya 12 kupitia kwa beki wake Omary Omary aliyeandika goli la kwanza akimalizia kona safi kutoka upande wa kushoto.

Vijana wa Serengeti wakiendelea kusaka goli lingine, ilichukua dakika 5 kwa Angola kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa beki wake wa kati Mimo kwa kichwa .


Dakika ya 41,Omar anamfanyia madhambi mchezaji wa Angola na mwamuzi kuweka tuta’ mkwaju wa penati’ na kufanikiwa kuandika goli la pili na katika dakika ya 43 Agiri Ngoda anaisawazishia timu yake na kwenda mapumziko wakiwa 2-2.


Kipindi cha pili kilianza kwa kila upande kusaka nafasi ya kupata goli la ziada, na katika dakika ya 62  Mchezaji wa Angola Davidi anaiandikia timu yake goli la tatuna Mfungaji wa goli la pili Capita  anaiandikia timu yake goli la nne na kuzizima ndoto za watanzania kwenda kombe la Dunia la Vijana nchini Peru mwaka huu.

Baada ya matokeo hayo, Serengeti Boys wanapoteza mchezo wa tatu kwa jumla ya magoli 12 wakifungwa 5-4 dhidi ya Nigeria, 3-0 na Uganda na 4-2 kwa Angola.


Kwenye mchezo mwingine wa kundi B, Nigeria na Uganda wanatok sare 1-1 na kuipa nafasi Angola kuungana na Nigeria kwenda hatua inayofuata akiwa nyuma ya Nigeria wenye alama 7 na Angola akiwa na alama 6.

Mechi zingine za kundi B zitachezwa hapo kesho.

Death announcement from the Semakula family in Minnesota, USA

$
0
0



The Semakula family would like to thank you for the generosity, love and support you have given them as they grieve the loss of their beloved mother, Ruth Semakula, which occurred on 4/16/2019 at Hennepin County Medical Center in Minneapolis, MN. 
The following is the itinerary of events; 
◦ Thursday, 4/18/19, 6:00PM: A fundraising event was held at the residence of Dr Crispin and Sally Semakula.
6451 Pheasant Hills Drive, Lino Lakes,
Minnesota 55038
◦ Saturday, 4/20/19, 1:00PM-4:00PM: Special Memorial service for Mama Semakula at the Swahili Church (Holly Trinity Lutheran Church.
2730 East 31st Street,
Minneapolis MN 55406)
◦ Sunday, 4/21/19, 11:00AM-1:00PM: Viewing of the body at Anderson Funeral Home.
 1401 North Arcade Street, St. Paul,
 MN 56106

◦ Monday, 4/22/19: Flight to Tanzania via KLM.
Your financial contribution to help cover the funeral and travel expenses would be highly appreciated. Financial contributions can be sent using the following means:
◦ Wellsfargo account # 3012151001 - Crispin Semakula 
◦ CashApp: $CrispinSemakula 
phone# 651-983-7637
◦ CashApp; $charlessemakula 
phone# 9524651130

CashApp: George Semakula 
Phone # 3472081771

JUVENTUS YAWEKA REKODI MPYA ULAYA NA ITALIA BAADA YAKUTWAA TAJI LA LIGI MARA 8 MFULULIZO

$
0
0

Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV 

Klabu ya Soka ya Juventus ya Italia imeweka rekodi mpya barani Ulaya na nchini Italia baada yakutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini humo maarufu kama Serie A mara nane mfululizo. Hii  inakuwa timu ya kwanza kuweka rekodi hiyo, ambapo hakuna timu katika Ligi tano bora la Ulaya iliyofanya hivyo. 

Juventus maarufu kwa jina la Bianconeri ilikuwa ikihitaji alama moja tu katika mchezo wake waliotandikwa bao 2-1 na SPAL, hivyo ikashindikana kutangaza ubingwa huo, katika mchezo wake dhidi ya Fiorentina, Juventus iliondoka na ushindi wa bao 2-1, hivyo kutangaza ubingwa huo. 

Katika mchezo huo dhidi ya Fiorentina, Juventus walitoka nyuma kwa bao la Nikola Milenkovic dakika ya 6, kabla ya Alex Sandro kusawazisha dakika ya 37 na bao lakujifunga la Beki wa Kati wa Fiorentina, Germàn Pezzella dakika ya 53, hivyo kufanya jumla ya bao 2-1.

Ushindi huo umepelekea Juventus kutwaa taji la Serie A mara 8 mfululizo, rekodi ambayo haijawekwa na timu yoyote katika bara la Ulaya. Ikiwa na mchezo 150 katika Uwanja wake wa nyumbani, imeshinda michezo 127, mabao yakufunga 335.

MAX ALLEGRI AWEKA REKODI YA KOCHA WA KWANZA KUTWAA MATAJI MATANO MFULULIZO 

Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri baada ya timu hiyo kutwaa Ubingwa wake mara nane mfululizo, anakuwa Kocha wa kwanza kutwaa mataji matano ya Ligi (Serie A).

Allegri anatwaa mataji hayo matano baada yakuachiwa mikoba na Kocha Antonio Conte aliyetwaa mataji hayo mara tatu. 

Rekodi hiyo inamuweka Kocha huyo katika nafasi ya pili, nyuma ya Giovanni Trapattoni anayeshikilia mataji Saba ya Serie A.

Juventus watakabidhiwa Kombe lao katika mchezo unaofuata dhidi ya Atalanta, nyumbani. 


Kocha Mkuu wa Juventus, Max Allegri

INTRODUCING MSANII MPYA WA PRODUCER SHIRKO ALLY MAHABA - SIELEWI


MAELFU WAJITOKEZA KAMBI YA MATIBABU YA MACHO JIJINI TANGA,WAZIRI UMMY AELEZA TATIZO LILIVYO KUBWA NCHINI

$
0
0







Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kambi ya macho kwenye shule ya Sekondari Maawal Jijini Tanga chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania wakishirikiana na Mbunge huyo chini ya Ufadhili wa better Charity ya nchini Uingereza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Mwenyekiti wa Bilal Muslim Africa Mohsin Abdallah (Shein) 
Mwenyekiti wa Bilal Muslim Africa Mohsin Abdallah (Shein) akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto ni Mkuu wa Maawal Sheikh Mohamed Hariri
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo 
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Clemence Marcel akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mratibu w Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharriff akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na Mratibu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Sharrif mara baada ya kufanya uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi ambaye alijitokeza kwenye kambi hiyo ya matibabu ya macho mara baada ya kuizindua 
Sehemu ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri Ummy wakati akizindua matibabu hayo
Wananchi kutoka maeneo 
Sehemu ya wananchi wakisubiriwa kupata huduma ya matibabu wakati wa kambi hiyo
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye kambi hiyo ya macho


MAELFU ya Wakazi wa mji wa Tanga wamejitokeza kwenye kambi ya Matibabu ya Macho inayoendelea kwenye shule ya shule ya Sekondari Maawal mjini hapa chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission tanzania wakishirikiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto chini ya Ufadhili wa better Charity ya nchini Uingereza

Akizungumza wakati akizindua kambi hiyo ya matibabu ya Macho Waziri Ummy alisema kuwa tatizo la ugonjwa wa macho nchini limekuwa kubwa ambapo kila watanzania mia moja wanne wanakabiliwa na matatizo ya macho. Alisema takwimu hizo zimefafanua kuwa katika idadi hiyo kila mtanzania mmoja anakabiliwa na tatizo la upofu wa mamcho na watanzania watatu wanakabiliwa na matatizo ya upungufu wa uoni wa kati na hali ya juu tatizo ambalo limekuwa kubwa sana. 

Aidha alisema kwa mujibu wa takwimu wizara ya afya katika kila watanzania 100 mmoja ana tatizo la upofu huku kwa ikieleza kwa watanzania 100 kati yao watatu wana matatizo ya upungufu wa kuona wa kati na hali ya juu tatizo hilo ni kubwa kwa sababu kati ya watu 100 wa nne wana matatizo ya macho. 

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy alitoa wito kwa watanzania kujiwekea utaratibu wa kuhudhuria kwenye vituo vya Afya ili waweze kupata matibabu pindi wanapoona kuwepo dalili za ugonjwa wa macho. “Ukiona una tatizo la macho nenda kwenye vituo vya afya upate matibabu haraka lakini niwaambie pia wana tanga na watanzania hakikisheni mnachunguza afya ya macho na afya ya kinywa mara moja kila mwaka “Alisema .

Waziri huyo aliwataka watanzania kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa hasa vyenye vitamin ikiwemo kuhakikisha wanakula mbogamboga huku akiwataka kuacha dawa kwenye macho bila kuandikiwa na daktari kwa sababu inaweza kupelekea kuharibu macho yao .Awali akizungumza katika halfa hiyo Mwenyekiti wa Bilal Muslim Afrika Mohsin Abdallah (Shein) alimshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuhakikisha huduma za afya nchini zinaimarika kwenye maeneo mbalimbali na kuondosha changamoto zilizopokuwepo awali.

“Namshukuru Rais Magufuli miaka yote tumefanya kazi tunatumia hospitali za serikali huduma zilikuwepo lakini hazikuwa kama ilivyo sasa lakini leo serikali ya awamu ya tano hospitali zimekuwa na vifaa muhimu kwenye hospitali”Alisema 

Aidha alisema wao kama bilal Muslim wamekuwa wakienda kwenye maeneo ambayo yana matukio makubwa lakini kutokana na ombi la Waziri Ummy tumeona kuja hapa kumuunga mkono pia tunashukuru mwamko umekuwa mkubwa sana,

JENGO KONGWE LA HOSPITALI YA MNAZIMMOJA KUFANYIWA MATENGENEZA YA PAA NA DARI

$
0
0
Na Ramadhani Ali - Maelezo Zanzibar 

Jengo kongwe la Hospitali Kuu ya Mnazimmoja linatarajiwa kufanyiwa matengenezo ya paa na dari kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Jumatano ijayo kutokna na kuvuja kwa muda kirefu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Msemaji Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Hassan Makame alisema kuvuja kwa jengo hilo kumepelekea sehemu kubwa ya dari kuharibika na kuhitaji matengenezo makubwa.

Alisema kutokana na ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mji Mkongwe, paa la Hospitali hiyo halitavunjwa bali litafanyiwa marekebisho sehemu za misumari inayovujisha na kuwekwa misumari mipya.

Alisema hatua hiyo ni miongoni mwa juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Wizara ya Afya kuhakikisha Hospitali hiyo inafikia lengo la kuwa Hospitali ya rufaa.

Hassan aliwata wananchi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa Hospitali kutokana na usumbufu utakaojitokeza kwa sababu wagonjwa ambao hawatakuwa na sababu kubwa ya kulazwa wataruhusiwa na upasuaji unaoweza kusubiri utasogezwa siku za mbele.

Hata hivyo Msemaji huyo aliwahakikishia wananchi kuwa upasuaji wa dharura na ambao hauwezi kusubiri utafanywa wakati wote wa matengenezo.

Katika kudumisha hali ya usafi ndani ya wodi za wagonjwa, msemaji Hassan aliwashauri jamaa wa wagonjwa wanaolazwa kuacha tabia ya kuchukua mizigo mingi kwani huduma nyingi zinapatikana hapo hapo.

Matengenezo ya paa na dari katika Hospitali kongwe ya Mnazimmoja yatafanywa na Kampuni ya Ujenzi ya Mamba na yatagharimu shilingi milioni 154 hadi yatakapo kamilika.

HAKUNA SIKUKUU KWENYE KAZI ZA UMEME – WAZIRI KALEMANI

$
0
0


HAKUNA SIKUKUU KWENYE KAZI ZA UMEME – WAZIRI KALEMANI

Na Veronica Simba – Kongwa

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kuendelea na kazi katika maeneo yao kwa siku zote zikiwemo sikukuu.

Alitoa maagizo hayo Aprili 18, 2019 Kongwa, Dodoma alipokuwa akikagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini; ambapo pia aliwasha umeme katika vijiji vya Ngonga na Mjini Mashariki B.

“Wakandarasi, najua kuna sikukuu lakini hakuna sikukuu kwenye kazi za umeme. Jipangeni na magenge yenu. Mameneja na vibarua muendelee na kazi. Hakuna Pasaka kwenye umeme. Umeme ni usalama na umeme ni uhai,” alisema.

Aidha, Waziri pia alimwagiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Kongwa, kuwaunganishia umeme wananchi wa kijiji cha Ngonga ambao nyumba zao zimerukwa.

“Sitaki kuona nyumba haina umeme. Nyumba hizi zote mzipelekee umeme. Mmeziruka mkidhani ni za hovyo-hovyo, hakuna nyumba ya hovyo. Nawapa hizi UMETA (Vifaa vya Umeme Tayari), kesho muwaunganishie umeme,” alisisitiza Waziri.

Akihamasisha kuhusu matumizi ya UMETA, Waziri Kalemani aliwataka viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Vijiji na Wilaya kuhakikisha wanatumia kifaa hicho katika Taasisi za Umma ambazo majengo yake hayana vyumba vingi ili kupunguza gharama za kutandaza nyaya za umeme.

Aidha, aliwahamasisha wananchi wenye nyumba zenye vyumba vichache (visivyozidi vinne) kutumia vifaa hivyo ili kuepukana na gharama za kutandaza nyaya za umeme.

Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia gharama za kuunganishiwa umeme kwenye makazi yao ambazo ni shilingi 27,000 kwa wananchi wa vijijini.

“Siyo lazima ulipe yote kwa mkupuo. Unaweza kulipia kidogo kidogo hadi ukafikisha 27,000 na TANESCO watakuunganishia umeme.”

Katika ziara hiyo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, ambaye ndiye Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, alitoa salamu za shukrani kwa serikali kwa kuwapelekea wananchi wake umeme kwa ajili ya maendeleo yao.

“Nasimama kwa niaba yenu (wananchi), kutoa shukrani nyingi kwa serikali, kwa será hii nzuri ya kutuletea umeme. Umeme ni maendeleo, umeme ni maisha, umeme ni uhai. Kinachotakiwa sasa ni tuutumie umeme huu.”

Aidha, Mheshimiwa Ndugai alimpongeza Dkt. Kalemani kwa kuwa Waziri wa kwanza tangu Tanzania ipate Uhuru, kufika katika Kijiji cha Mjini Mashariki B, kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kuhakikisha wananchi wanapelekewa huduma za maendeleo.

Waziri aliambatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na REA.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Mjini Mashariki B, kilichopo wilayani Kongwa, alipokuwa katika ziara ya kazi, Aprili 18, 2019. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme kwenye nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Mjini Mashariki B, Lilia Boma (katikati), alipokuwa katika ziara ya kazi wilayani Kongwa, Aprili 18, 2019. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwagawia bure vifaa cha Umeme Tayari (UMETA), wakazi wa Kijiji cha Mjini Mashariki B, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma ili waweze kuunganishiwa umeme pasipo kuingia gharama za kutandaza nyaya. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Aprili 18, 2019.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Kijiji cha Ngonga, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) na kushangilia alipowaahidi kuwa serikali itasambaza umeme katika vitongoji vyote vya kijiji hicho. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Aprili 18, 2019.

UMEFIKA WAKATI SASA WASOMI KUANDIKA NA KIUBUA MASHUJAA WA FANI MBALIMBALI-BALOZI SEID ALI IDDI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Wasomi au Watu wa kawaida wenye uwezo na Taaluma ya kuandika kuibua na kuiweka hadharani hazina ya Mashujaa wa fani mbali mbali ili Vizazi vya sasa na vile vijavyo viweze kufaidika na michango yao.
Alisema Visiwa vya Zanzibar vimebahatika kukaliwa na mashujaa wa fani tofauti ikiwemo, Uchumi, Siasa na Utamaduni, lakini kwa bahati mbaya Wasomi wengi wamekuwa wavivu kutafiti maisha yao na hatimae kuyawasilisha kwa Jamii kwa nia ya Vitabu.
Balozi Seif Ali Iddi aliseMa hayo wakati akizindua Tamthilia ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad iliyotungwa na Mwandishi Mahiri na mpenzi mkubwa wa Lugha ya Kiswahili Nchini Profesa Emmanuel Mbogo hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idiss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Alisema kunakili hadhithi na kuzichapisha kwenye Vitabu ni njia murua na muwafaka  ya kuwaenzi mashujaa hao na itapendeza zaidi iwapo simulizi zao zitachapishwa kwa kutumia Lugha Mama na sanifu iliyozoeleka ya Kiswahili ili zipate wasomaji wengi zaidi.
Balozi Seif alieleza anaamini kuwa Historia ya Zanzibar haiwezi kukamilika bila ya kuelezea maisha ya Msanii maarufu wa Taarabu Afrika Mashariki Bibi Siti Binti Saad ambapo kwa bahati nzuzi Profesa Emmanuel Mbogo ameifanya kazi hiyo ya kuinawirisha Historia ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba Uandishi wa Historia za Mashujaa wa Fani mbali mbali Visiwani Zanzibar na Mwambao wa Afrika Mashariki ni muhimu kwa Jamii kwa vile Hadithi zao husaidia kuchangamsha na kushajiisha kuiga mwenendo wa maisha yao.
“ Kwa hakika Hadhithi za Maisha ya Mashujaa zikisomwa na kuzingatiwa hutuangazia mwanga  wa kuona uwezekano wa kubadilisha maisha yetu pengine siku moja na sisi tukaweza kugeuka tukawa kama wao au zaidi”. Alisema Balozi Seif.
Alimpongeza na kumshukuru Profesa Emmanuel Mbogo kwa mchango wake wa kupanda mbegu ya mashujaa wa baadae kupitia Tamthilia  yake  inayohusu Maisha ya Siti Binti Saad inayoweza kuzalisha katika Jamii hii akina Siti Binti Saad wengine  katika siku zijazo.
Balozi Seif alitoa wito kwa Vijana wa sasa kuisomaTamthilia hiyo ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad na kuizingatia kwa vile inatoa funzo la umuhimu wa kung’ang’ania ndoto mpaka itowe matunda anayoyakusudia Mtu.
Alisema Vijana wengi kwa sasa wamejenga hulka ya kutojiamini na kuacha ndoto zao za Kimaisha na badala yake hutafuta njia za mkato ambazo mara nyingi haziwezi kuwaletea hatma njema ya maisha yao.
Balozi Seif aliwanasihi Vijana kuiga  mfano bora wa Marehemu  shujaa Bibi Siti Binti Saad kutokana na ujasiri wake aliyoujenga wakati alipoamua kuzisimamia ndoto zake zilizompa shime ya kujifunza kusoma na kuimba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akichambua baadhi ya maneno yaliyomo ndani ya Tamthilia hiyo ya kurasa 88 kwenye onyesho la kwanza katika kichwa cha Habari kisemacho Uchumba, akijikita zaidi kwenye lugha ya Mahaba alisema kwa sasa imetoweka katika jamii Nchini.
Alisema kutoweka kwa maneno matamu kunachangia kwa kiasi kikubwa Vijana wengi walio kwenye Ndoa kutumia njia ya mkato ya kutoa Talaka kwa Wake zao kutokana na kushindwa kuwashawishi kudumu kwenye ndoa kwa kutumia lugha ya Mahaba.
Balozi Seif  alifahamisha kwamba kukosekana kwa maneno matamu Mitaani hata katika Familia kipindi hichi cha kizazi cha sasa inawezekana ikawa ndio chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano katika Jamii.
“ Tafadhali egesha sikio lako kifuani kwangu ili upate kusikia jinsi moyo  wangu unavyodunda, ukikutaja, ukikuita na kusema  - Mtumwa,  nakupenda”. Balozi Seif akikariri baadhi ya maneno matamu kutoka kwa Bwana Khamis akitafuta penzi la Mkewe Bi. Siti.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Taasisi ya Siti Binti Saad Zanzibar kwa juhudi iliyochukuwa ya kufanikisha tukio hilo muhimu la uzinduzi wa Tamthilia ya Shujaa huyo wa Sanaa Afrika Mashariki ambayo itaendelea kubakia  sehemu ya Urithi wa Taifa hili.
Akitoa maelezo ya siku ya Urithi wa Utamaduni Duniani Mshika Fedha wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Bibi Aziza Saleh alisema Taasisi hiyo kupitia Azimio linaloshajiisha Nchi zilizomo katika Uhifadhi wa Urithi wa Kimataifa limeandaa mambo yanayorithisha Vijana kurithi Tamaduni za Taifa.
Bibi Aziza alisema zipo hatua ambazo tayari zimeshachukuliwa kutekeleza Malengo hayo ikiwemo Makongamano ya Watu na Jumuiya tofauti, kutoa mafunzo ya uchoraji wa aina mbali mbali hata kuendeleza Lugha adhimu ya Kiswahili ambayo kwa sasa inashika nafasi ya Kumi Duniani.
Alieleza kwamba Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad bado inazingatia kutosahau thamani ya Utamaduni wa asilia unaopaswa kuonyeshwa kwa Vijana wa kisasa hasa upishi na vyakula vya Ladu za mtama, vileja, visheti pamoja na kashata za nazi na njugu  ili wathamini cha asili.
Akimkaribisha kuzindua Tamthilia ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,  Bibi Nasra Hilal alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana tokea kuasisiwa kwa Taasisi hiyo Miaka Mitano iliyopita.
Bibi Nasra alisema ushirikiano wa karibu uliopatikana baina ya Wana Taasisi hiyo na Wadau wa Utamaduni wa Mswahili umewezesha kupiga hatua kubwa Malengo ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ikiwemo matayarisho ya ujenzi wa Jengo la Utamaduni la Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikabidhi Hati za Uanachama wa Heshima kwa washirika wa Taasisi hiyo.
Uzinduzi huo wa Tamthilia ya Mtumwa hadi Siti Binti Saad umefanyika ukiambatana ndani ya Wiki ya Uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni Duniani { World Culture Heritage Day } inayoadhimishwa na Umoja wa Mataifa { UN } kila ifikapo Tarehe 18 Aprili ya Kila Mwaka.
Mji Mkongwe wa Zanzibar { Maarufu Stone Town } umebahatika kuwemo miongoni mwa Miji iliyoidhinishwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Elimu, Sayansi na Utamaduni {Unesco} kuwa ndani ya Urithi wa Kimataifa.
 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad kilichoandikwa na Profesa Em,manuel Mbogo.
 Waswahili wakijimwaga kwenye burdani ya muziki wa asili uliokuwa ukitumbuizwa na Kikundi cha Taarab cha Akheri Zamani hapo katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad kilichoandikwa na Profesa Em,manuel Mbogo.
 Balozi Seif Kulia akikabidhi Hati ya Uwanachama wa  Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
  Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Mwanaharakati ya Bibi Siti Binti Saad Bwana Mbarawa akimkabidhi Balozi Seif picha mahiri ya kuchora ya Bibi siti na Kikundi chake wakati wa enzi zake ya uimbaji.
 Balozi Seif Kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad mara baada ya uzinduzi wa Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati huyo.
Balozi Seif Kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Taarab cha Akheri zamani kilichokuwa kikitoa burdani kwenye hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Tamthilia ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad.

NAIBU WAZIRI KANYASU ATOA ONYO KWA WAHIFADHI NCHINI KUHUSU WANANCHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amezionya na kuzitaka Taasisi za Uhifadhi kuacha tabia ya kuwabughudhi wananchi wanaoishi katika vijiji na vitongoji 366 vilivyokutwa ndani ya Hifadhi katika maeneo mbalimbali nchini mpaka hapo maamuzi ya Kamati ya Mawaziri saba iliyoundwa kushughulikia suala hilo itakapokamilisha kazi iliyopewa na kuwasilisha ripoti kwa Mhe. Rais.

Hatua hiyo ni kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji wanaoishi katika vijiji na vitongoji hivyo kudai kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na mifugo yao kukamatwa mara mara kwa madai ya kukutwa imeingia ndani ya Hifadhi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Mhe. Kanyasu amezitaka taasisi hizo kufuata na kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.

Aidha, Mhe. Kanyasu ametumia fursa hiyo kuwaonya wananchi ambao wamekuwa wakivamia maeneo mapya ya Hifadhi kwa kisingizio cha kauli aliyoitoa Mhe. Rais kuacha mara moja na kwamba yeyote atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

" Wananchi ninao walenga ni wale tu ambao walikuwa wakiishi Hifadhini kabla ya kauli ya Rais aliyoitoa mwanzoni mwa mwaka huu" Alisisitiza.

Hata hivyo, Mhe Kanyasu amebainisha kuwa Kamati ya Mawaziri saba iliyoundwa na kuzunguka nchi nchi nzima imebaini kuwa kuna zaidi ya vijiji 820 ambavyo vimo ndani ya Hifadhi mbali ya vile 365 vilivyobainishwa awali na kuwasihi wananchi wasiendelee kuvamia maeneo mengine.

Mhe.Kanyasu ameowanya baadhi ya askari wa wanyamapori wanaoomba rushwa Kutoka kwa wafugaji pindi wanapokamata mifugo yao ili waweze kuiachia waache mara moja tabia hiyo akisisitiza kwamba askari yeyote atakayethibitika atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria za utumishi wa Umma.

Mkuu wa wilaya ya Kondoa, Mhe. Sezaria Makota amewataka wananchi hao kuendelea kuwa walinzi wa maeneo hayo huku wakisubili hatma ya taarifa ya kamati ya Mawaziri saba itakayotolewa hivi karibuni.

" Baada ya taarifa hiyo mtajua hatma yenu na kama hapa mtabaki au mtahamishwa na kama mtahamishwa tutajua tutawapeleka eneo gani kwa ajili ya malisho na kilimo." Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi, Mwenyekiti wa kijiji cha Kisondoko, Ismail Said amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa baadhi ya askari wa wanyamapori wamekuwa wakikamata mifugo yao na kuomba rushwa na pale makubaliano yanaposhindikana huondoka na mifugo yao.

Amesisitiza kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikichochea chuki baina ya wananchi na askari hao jambo linalorudisha nyuma jitihada za Uhifadhi nchini.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine  Kanyasu wa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo ameagiza wananchi hao wasibughuziwe hadi hapo maamuzi yatakapotolewa juu ya hatma yao. Wengine ni kmati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo pamoja na Maafisa wa kutoka  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Sezaria Makota. 
  Mkuu wa wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu katika kijiji  ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyoomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo ameagiza wananchi hao wasibughuziwe hadi hapo maamuzi yatakapotolewa juu ya hatma yao.   
 .Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kisondoko wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akizungumza nao kuhusu mifugo yao kukamatwa mara kwa mara na askari wanyamapori wa Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
Diwani wa kata ya Kisondoko, Mhe. Ismail Juma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya  Mhe. Sezaria Makota katika kijiji  ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyoomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.                                                          (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 21,2019

TAARIFA MUHIMU KWA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI KUHUSIANA NA PASIPOTI ZA KIELEKTRONIKI


DK.MABODI ANENA KUHUSU MUUNGANO.

$
0
0


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi amesema muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni tunu ya taifa inayotakiwa kuenziwa kwa vitendo na wananchi kutokana na kuimarika kwa nyanja za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kimaendeleo.

Rai hiyo ameitoa leo katika hafla ya kutoa vifaa vya skuli kwa wanafunzi wa skuli ya Kidagoni Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja vilivyotolewa na Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo wa CCM, amesema muungano huo licha ya kuunganisha nchi mbili umeenda mbali zaidi na kuwaunganisha watu wa pande zote mbili kiundugu, kidamu na kijamii.

Alisema hakuna kiongozi, taasisi wala mtu wa kuvunja muungano huo uliodumu kwa miaka 55 toka kuasisiwa kwake.Alieleza kwamba wapo baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa na kauli zisizofaa za kubeza tunu hiyo iliyowaunganisha wananchi wa nchi mbili na kuishi kwa amani na utulivu.

Alisema wakati umefika wa wananchi wa wilaya hiyo ya Kaskazini 'A' hasa shehia ya Kidoti na vitongoji vyake kupuuza maneno ya ulaghai yanayotolewa na vyama vya upinzani na badala yake kuthamini juhudi za kimaendeleo zinazotekelezwa na Serikali chini ya usimamizi wa CCM.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 alisema Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa mijini na vijijini ili wanufaike na Sera imara zinazosimamiwa na CCM.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi alifafanua kwamba maendeleo yaliyofikiwa nchini yametokama na misingi imara ya kiuongozi, kiitikadi na kimfumo iliyoasisiwa na waasisi wa Mapinduzi ya 1964,Muungano 1964 pamoja na waasisi wa TANU na ASP.

Katika hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wa skuli hiyo Dk. Mabodi amesema CCM itatoa itatoa mabati ya kuezeka Kituo cha Afya cha Ndagoni pamoja na ujenzi wa choo, kuchangia shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa matano ya skuli hiyo ya mandalizi, msingi na kati pamoja na vifaa mbali mbali vya kutumia maskulini kwa wanafunzi watakaofaulu michipuo.

Aidha aliongeza kuwa ataikumbusha Serikali kuu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'A' kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la ukosefu wa barabara, umeme na umaliziaji wa kituo cha Afya.

"CCM inapoahidi inatekeleza kwa wakati na hakuna jambo lolote lililowahi kushindikana mbele yetu, nakuombeni muendelew kuwa pamoja na Chama Cha Mapinduzi kwani ndio taasisi pekee inayozunguka usiku na mchana kuratibu matatizo yenu na kuyatatua kwa wakati", alisema Dk. Mabodi.

Pamoja na hayo aliongeza kwamba kwa mujibu CCM ilivyotekeleza Ilani yake visiwani humo, hakuna mtu yeyote wa kuzuia ushindi wa kishindo wa CCM mwaka 2020 kama ilivyosisitizwa katika ibara ya Tano ya Katiba ya Chama ya mwaka 1977.

Akizungumza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo ya CCM Mwinyi Ahmed Mwinyi alisema lengo la kutoa vifaa hivyo kwa wanafunzi ni kuunga mkono juhudu za Serikali na CCM katika kuisaidia jamii ya wananchi wa kijiji cha Ndagoni.

Alisema fedha za kununua vifaa hivyo zumetokana na michango mbali mbali ya vijana wazalendo wa CCM ambao ni wanachama waliounda jumuiya hiyo kwa kutoa fedha za mishahara yao ili isaidie jamii katika masuala ya elimu.

Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni sale za wanafunzi wa ngazi zote za skuli hiyo, viatu, mikoba, mabati, mabembea ya kisasa kwa ajili ya wanafunzi wa maandalizi pamoja na mabati ya kuezekea majengo ya skuli hiyo.

Katika risala ya skuli hiyo iliyosomwa na Mwl. Neema Othman Khamis aliishukru Jumuiya hiyo kwa maamuzi yake ya kuwasaidia vifaa wanafunzi wa skuli hiyo na kueleza kuwa wamekuwa ni mfano bora wa kuigwa na jumuiya zingine nchini.

Alizitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni upungufu wa madarasa, ukosefu wa barabara, ukosefu wa vifaa vya masomo ya ICT zikiwemo komputa.

Naye Mwakilishi wa Jimbo Mhe. Ame Haji Ali alisema ametekeleza masuala mbali mbali ya kimaendeleo katika kijiji hicho na vijiji jirani vikiwemo kuimarisha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za Afya, vikundi vya ujasiriamali zikiwemo Sacoss kwa ajili ya akina mama pamoja na kuimarisha sekta ya michezo kuwapatia vijana vifaa vya michezo katika ligi mbali mbali za jimbo hilo.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kidagoni mara baada ya kukabidhi vifaa na zawadi mbali mbali kwa wanafunzi wa skuli ya Kidagoni.(PICHA NA IS-HAKA OMAR-AFISI KUU YA CCM ZANZIBAR).
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akishangiliwa na Wanafunzi wa Skuli ya Kidagoni ya wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
 WANAFUNZI wa Skuli ya Maandalizi,Msingi na Kati ya Kidagoni Wilaya ya Kaskazini ‘A’  wakiwa katika skuli hiyo kwa ajili ya hafla ya kukabidhiwa vifaa vya wanafunzi zikiwemo sale,viatu,mikoba ya kuhifadhi madaftari pamoja na mabembea na Jumuya ya Vijana wapenda maendeleo ya CCM Zanzibar.
 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo Mwinyi Ahmed Mwinyi (wa kulia wa mwanzo aliyenyanyua shungi la sale ya wanafunzi wa kike) akikabidhi vitu mbali mbali vilivyotolewa na jumuiya hiyo kwa uongozi wa skuli hiyo.
VIONGOZI wa Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo pamoja na Walimu wa Skuli ya Kidagoni na wanafunzi wa maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea vifaa vya skuli zikiwemo Sale,viatu na mikoba ya kuhifadhi madaftari.

BONAZA LA PASAKA LAFANA VIWANJA VYA MAO ZANZIBAR

$
0
0
 WAFANYAKAZI wa Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuaza kwa mchezo wa mpira katika Bonaza la Michezo ya Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's. Zanzibar (Picha na Ikulu Zanzibar )  
 NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Kassim Ali akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam, kabla ya kuaza kwa mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar.(Picha na Ikulu Zanzibar)
 MCHEZAJI wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Azori Ndege mwenye mpira akimpita beki wa Timu ya Ikulu Sports Clun Zanzibar Khamis Bakari wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Pasaka uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Zanzibar imeshinda bao 6-2.(Picha na Ikulu Zanzibar)
 MSHAMBULIAJI wa Timu ya Ikulu Sports Club Zanzibar Rajab Wakil akimpita Beki wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Okororo Sadiq, wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Sports Club Zanzibar imeshinda mchezo huo kwa bao 6-2.(Picha na Ikulu Zanzibar)
 MSHAMBULIAJI wa Timu ya Ikulu Sports Clun Zanzibar Omar Hamad akijaribu kumpita Beki wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam Hassan Econ, wakati wa mchezo wao wa kusherehekea Michezo ya Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya Ikulu Zanzibar imeshinda bao 6-2.(Picha na Ikulu Zanzibar)
 MSHINDI wa mbio za Mita Mia Moja kutoka Ikulu Zanzibar Vuai Suleiman akiongoza mbio hizo na kufuatiwa mshindi wa Pili kutoka Ikulu Dar es Salaam Mwabora Richard (Picha Ikulu Zanzibar)
 WASHIRIKI wa mchezo wa kufukuza Kuku kutoka Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam wakishiriki mbio hizo za kufukuza kuku mshindi kutoka Ikulu Zanzibar Bi. Susiati Nyange.(Picha na Ikulu Zanzibar)
WANAMICHEZO kutoka Timu ya Ikulu Sports Clun Dar es Salaam, wakisoma dua wakati walipotembelea Kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwangui Zanzibar, baada ya kumaliza mchezo wao leo.(Picha na Ikulu Zanzibar)

WILAYA YA KILOSA YAEPUKANA NA UPOTEVU WA ZAO LA MPUNGA KUTOKA ASILIMIA 45 HADI 30

$
0
0
Wilaya za kilosa na mvomero mkoani morogoro zimefanikiwa kupunguza changamoto kubwa ya upotevu wa mazao ya mpunga mashambani kutoka asilimia 45 zilizokuwepo kufikia asilimia 30 jambo ambalo litawanufaisha wakulima wanaojihusisha na kilimo cha zao hilo.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa mradi wa kuwezesha makundi ya wanawake na vijana wanaojihusisha na kilimo cha mpunga kupunguza upotevu wa mpunga kabla na baada ya mavuno (ripoma) ulio chini ya shirika la elvetas tanzania, daniel kalimbiya ambaye amebainisha wameweza kudhibiti tatizo hilo kwa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora, wanalima na kuvuna kisasa na kuhifadhi mazao yao kwenye maghala bora waliyojenga.

“wakulima walikuwa na changamoto kubwa hasa kwenye uzalishaji na kutunza mazao, hivi sasa upotevu wa mazao umepungua kutoka asilimia 45 hadi asilimia 30 huku pia tumefanikisha kuwafahamisha namna bora ya kutunza mazao kwa ubora Zaidi, amesema kalimbiya

Mkuu wa wilaya ya kilosa adam mgoyi akawasisitiza maafisa kilimo na mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo kusimamia vyema miradi yenye tija kwa wananchi kama ilivyo kwa mradin huo ili kuwa na muendelezo hata baada ya kumalizika ili ulete tija na mabadiliko kwa wakulima wa wilaya hiyo.

“ningependa kuwashauri wataalam kutoka halmashauri tuwe na mwenendo mzuri wa kushiriki katika kutunza na kufahamisha miradi yenye tija kama hii na tunatakiwa kuongeza umakini katika usimamizi hasa usimamizi mara baada ya kumalizika kwa mradi” amesema Mgoyi

meneja wa ripoma greyson regemalila akasema licha ya kudhibiti upotevu, kwa kushirikiana na mamlaka ya chakula na dawa tfda na shirika la viwango vya ubora nchini tbs wame7ongeza thamani ya mazao ya wakulima na kutoa msimbo milia yaani barcode kwa baadhi yao ili kuongeza thamani ya mazao kuuzwa ndani na nje ya nchi.



introducing All Eyes (Official Music Video) by Hennesseyy

WAZIRI WA NISHATI AKUTANA NA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME VIJIJINI GEITA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Geita, wataalamu kutoka wizarani, TANESCO na REA katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Aprili 20, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.

Na Veronica Simba – Chato

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amekutana na wakandarasi wa miradi ya umeme vijijini katika Mkoa wa Geita na kujadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo kwa ufanisi zaidi.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo, Aprili 20, 2019 katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato, makubaliano maalum yaliyofikiwa ni kwa wakandarasi husika kuhakikisha wanakamilisha Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa kwanza, mkoani humo ifikapo Septemba mwaka huu.

Akiwapa hamasa ya kufanya kazi kwa viwango na kasi, Waziri Kalemani amewaambia wakandarasi hao kuwa siyo dhambi kukamilisha kazi waliyopewa kabla ya muda ulioanishwa katika Mkataba wao.

Aidha, amewataka kujenga utaratibu wa kuwashirikisha viongozi wa maeneo wanakotekeleza miradi husika wakiwemo Wakuu wa Wilaya, wabunge na madiwani ili pamoja na mambo mengine waweze kuwaelimisha wananchi na kufuatilia ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Wataalamu kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), pia wameshiriki kikao hicho.

Waziri wa Nishati yuko mkoani Geita kwa ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images