Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

Dc Muro atinga sokoni kugawa vitambulisho vya machinga

$
0
0
Na woinde Shizza globu ya jamii Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amefanya ziara ya kustukiza kukagua zoezi la utoaji wa vitambulisho vya wajasiliamali na wafanyabiashara ndogondogo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Arumeru .

katika hali ya kuonesha kukerwa na kasi ndogo ya utoaji wa vitambulisho,Dc Murro  ilimlazimu kuvigawa vitambulisho hivyo yeye mwenyewe ,ziara hiyo ambayo aliifanya katika soko la Tengeru, kisha katika soko la usa River na hatimaye kumalizia katika soko la Ngaramtoni 

Muro amelazimika kwanza kutoa elimu kwa wafanyabiashara ndogondogo na wajasiriamali hatua ambayo iliongezeka mwitiko mzuri wa wafanyabiashara hao kuvichukua vitambulisho hivyo baada ya kuelimishwa na kuelewa umuhimu wa kuvitumia vitambulisho hivyo ambapo pia wananchi hao walimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapatia vitambulisho 

Kwa upande Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa masoko ya Tengeru na USA River Abia Mbise amesema kuwa awali wafanyabiashara walikuwa na mwamko mdogo kutokana na kutopatikana kwa urahisi kwa vitambulisho hivyo.Aidha alipongeza kitendo cha mkuu wa wilaya kutoka ofisini na kuwafuata na kutoaelimu Wa umuhimu wa kuwa na vitambulisho hivi pamoja na kuvigawa yeye mwenyewe hatua hii imewasaidia kuongeza mwitiko kwa wafanyabiashara wengi kuchukua vitambulisho hivyo.

Akizungumza mara baada ya kutoa elimu na kugawa vitambulisho hivyo, alisema mkuu Wa Wilaya hiyo alisema ameamua kutoa vitambulisho hivyo Mara baada ya kuona zoezi hilo limezorota.

"nimelazimika kuingia mitaani kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa utoaji wa vitambulisho hivi nimetoa maelekezo kwa wakurugenzi wa Halmashauri ya Meru na Arusha Dc pamoja na Maafisa Tarafa na watendaji wa kata na vijiji kuacha tabia ya kuwasubiria wafanyabiashara maofisini na badala yake watoke na kuwafuata ili kuwapunguzia usumbufu wa kwenda umbali mrefu kuchukua vitambulisho hivi" alisema Muro 
 Mkuu  wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akieleza jambo wakati wa kugawa vitambulisho vya machinga katika solo la Tengeru
Picha malimbali zikionesha Mkuu  wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akigawa vitambulisho vya machinga katika solo la Tengeru

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

$
0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha jumla ya Shilingi bilioni 55,175,163,302 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Katiba na Taasisi zake.

Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 47,283,566,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara na shilingi Bilioni 7,891,598,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Fedha zilizopitishwa ni kwa ajii ya Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria, Tume ya Utumishi wa Mahakama,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Tume ya Kurekebisha Sheria.

Wizara pia iliomba Bunge liidhinishe shilingi Bilioni 126,162,464,756 kwa ajili ya Mfuko wa Mahakama . Kati ya Fedha hizo shilingi Bilioni 104,004,564,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi Bilioni 22,157,900,576 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Towards a financially equitable society

$
0
0
Tanzania endeavors to become a middle-income economy by 2025 with a desired per capita income of USD 3000; this will be a monumental step towards economic development and growth for the country. 

These aspirations can only be achieved by investing in human capital, in particular creating equal opportunities for women and men.

Human capital is the driver of economic transformation and according to the National Bureau of Statistics (NBS) the population currently stands at 54 million and is projected to reach 67 million by 2025. Currently, women comprise 51.3 percent of the population, and while they play a key role in household resilience and sustaining livelihoods within Tanzania’s current economy, they face considerable challenges in other areas. 

For Tanzania to realize its development ambitions to attain middle-income status, these obstacles need to be addressed in order to create a level playing field that empowers women to be involved in the economy at the same rate as men. 

Poverty rates are higher for female-headed households, especially in the rural areas -according to the Ministry of Health, 60 percent of Tanzanian women live in absolute poverty. Women struggle to access vital resources, such as educational opportunities, credit and financial services on a daily basis, hindering their chances for income stability and economic opportunities. While these challenges are not unique to women they are a particularly disadvantaged group. 

Additionally, when it comes to accessing financial services, women are underserved. A 2018 report by FinScope notes that only 60% of women in Tanzania have access to financial services compared to 70% of men - while 30 percent are completely excluded from financial services due to qualifying criteria. Sadly, women are trailing behind men in the efforts to advance financial inclusion in Tanzania. 

Mama Ntilie’s are a common feature of the urban landscape and when it comes to the business arena, women surpass men as founders of micro, small and medium enterprises (MSMEs) accounting for 54 percent of all MSMEs in Tanzania. As such, women should warrant more attention; they can catalyze the economy into Tanzania’s desired middle-income status by 2025. 

Stanbic Bank Tanzania has joined forces with the United Nations (UN) Women HeForShe movement, which invites men and women to stand in solidarity for gender equality. We encourage all genders to partake as agents of change and act against negative stereotypes and behaviors. 

It is imperative that financial services provide not only credit options but also equip women with information and direction to succeed in the market. Products and services need to be tailored to support their business and personal financial activities, provide convenience to carry out daily transactions such as transferring funds, paying bills and monitoring the activities on their accounts while allowing them to focus on running and scaling up their businesses.

 Stanbic Bank’s UHURU Banking is one such solution. It is a simple, easy, transparent and accessible way of banking that can contribute to balancing the scale between the genders by also providing women the right advice and support for their financial growth. 

In Tanzania’s social framework, the function of women in bolstering a household cannot be overstated; they carry a large financial load when it comes to sustaining their households. Women are the doorway towards improving standards of living within homes in a qualitative and quantitative manner. 

In order to empower women and carve out a level playing field, they must have the tools to participate in economic and social activities as equal citizens, which requires access to opportunities, information and capabilities. Once this becomes a reality their input will lead to a significant improvement in the livelihoods of the population, creation of jobs and household resilience. The spirit of Tanzanian women will have transformative powers on the nation. 
Head, Personal Banking, Ruth Mwaiselage .

Shirika la Sun Flower kujenga kiwanda nchini

$
0
0
Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha Alizeti {Sun Flower } la Alemdar kutoka Nchini Uturuki limeonyesha nia ya kutaka kujenga kiwanda kitakachozalisha Bidhaa tofauti kwa kutumia malighafi ya Maua hayo katika azma ya kuitikia wito wa Serikali wa kuwa Nchi ya Viwanda katika kipindi kifupi kijacho.

Ofisa Mkuu wa Shirika hilo Bibi Fatma Atala alieleza hayo wakati Ujumbe wa Viongozi wa Shirika hilo ulioongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Oktay Alemder ulipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Bibi Fatma Atala alisema Mradi huo wa Kibiashara endapo utafanikiwa kuanzishwa Visiwani Zanzibar unalenga pia kuwashirikisha moja kwa moja Wakulima Vijini kwa kulima Maua ya Alizeti katika baadhi ya maeneo yao ya Kilimo.

Alisema Maua ya Alizeti ni bidhaa inayoendelea kuwa na hadhi kubwa katika masoko ya Kimataifa ambayo inaweza kusaidia kunyanyua mapato ya washiriki katika ukulima wake sambamba na kuongeza Mapato ya Taifa.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alueleza Ujumbe huo wa Viongozi wa Shirika la Alemdar kutoka Nchini Uturuki kwamba Tanzania tayari imeshaamua kuwa Nchi ya Viwanda ifikapo Mwaka 2025.

Balozi Seif alisema Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi wana fursa ya kuitumia nafasi hiyo katika Ushiriki wao wa Uwekezaji utakaokwenda sambamba na azma hiyo ya Serikali.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Ujumbe huo unapaswa kuzingatia zaidi mazingira halisi ya Zanzibar yanayoendelea kukumbwa na changamoto la ufinyu wa Ardhi.

Balozi Seif aliushauri Ujumbe wa Viongozi hao kutayarisha maombi na kuyawasilisha kwa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} kwa hatua ya kuangalia uwezekano wa kuufanyia uchambuzi yakinifu Mradi wao na mazingira halisi ya Ardhi yaliyopo Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Ujumbe huo wa Viongozi wa Shirika la Alemdar kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari muda wowote kuunga mkono jitihada za Shirika hilo za kutaka kuitumia fursa ya Uwekezaji Vitega Uchumi iliyopo Nchini Tanzania. 
 Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha Alizeti (Sun Flower) la Alemdar Bwana Oktay Alemder Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika na Ujumbe wake kwa mazungumzo. Kati kati yao ni Mwakilishi wa Shirika hilo hapa Zanzibar Bibi Batuli. 
 Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha Alizeti (Sun Flower) la Alemdar Bibi Fatma Atala Kushoto akitoa maelezo ya utendaji wa Shirika lake kwa Balozi Seif.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Shirika la Alemdar kutoka Nchini Uturuki Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Viongozi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha Alizeti (Sun Flower) la Alemdar wa Uturuki na wale waliopo Zanzibar wakifuatilia mazungumzo yao na Balozi Seif hayupo pichani. Picha na – OMPR – ZNZ.

ASKARI POLISI 400 WANAISHI URAIANI, DKT MGHWIRA AOMBA WADAU KUSAIDIA UJENZI WA NYUMBA KWA ASKARI HAO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Hamis Issah wakipokea msaada wa mifuko 200 ya saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jun Yu , inayotengeneza saruji ya Moshi Cement ,Tian Haifeng . 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

FAMILIA 400 za askari Polisi kati ya 1600 katika mkoa wa Kilimanjaro wanaishi uraiani hali inayochangia kupungua kwa maadili katika utendaji kazi kwa baadhi ya askari kutokana na kuishi maeneo yasiyokuwa kambi za Polisi.

Kutokana na hali hiyo tayari Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limeanza ujenzi wa nyumba sita katika eneo la kambi za Polisi mjini Moshi kwa ajili ya makazi ya askari hao baada ya kupokea kiasi cha Sh Milioni 150 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John Pombe Magufuli.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji kutoka kampuni ya kichina ya Jun Yu investment ,watengeneza wa saruji ya Moshi Cement ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh Bilioni 10 zilizotolewa na Rais.

“Nimshukuru mh. Raisi wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za dhati za kuboresha ustawi wa askari kwa kutoa shilingi Bilioni 10 kwa ajii ya kujenga nyumba za kuishi askari polisi na familia zao katika mikoa yote nchini.”alisema kamanda Issah.

“Aidha siku ya leo kwa niaba ya maofisa,wakaguzi na askari wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro ,niushukuru uongozi wa kampuni ya Moshi Cement kwa kutupatia mifuko 200 ya saruji na huu ni mwanzo mzuri kwa wadau kuendelea kutusaidia.”alingeza Issah.

Kamanda Issah alisema uongozi wa kampuni ya Moshi Cement wamejitoa kuchangia baada ya kufahamu umuhimu wa jeshi la polisi katika shughuli zao za uwekezaji na pia katika kumuunga mkono Mh. Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ,Dkt Magufuli katika juhudi za kuboresha jeshi la Polisi.

“Nyumba hizi zinatakiwa zikamilike ifikapo Juni 31 mwaka 2019 hivyo tunajitahidi kuwashirikisha wadau wa jeshi la polisi na wadau wengine wapenda maendeleo ili kukamilisha ujenzi huu kwa wakati,na pia ikiwezekana tuongeze nyumba nyingine katika eneo hili .”alisema Kamanda Issah .

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akizungumza mara baada ua kupokea msaada huo alisema ni jukumu la serikali kuhakikisha askari wake wanaishi kwenye maeneo yaliyo safi na salama huku akieleza kuwa shauku yake ilikuwa ni kuona ujenzi huo ni wa nyumba za Ghorofa.

“Nilipokuja kutembelea uwanja huu binafsi nilitamani sana kama tungekuwa tumejipanga haya majengo yangeenda Juu ili kuacha nafasi ya kutosha kwa ajili ya watoto wa askari na jumuiya inayoshi hapa ,kupata sehemu mbalimbali zikiwemo za mapumziko na biashara kidogo “alisema Dkt Mghwira.

Alisema ujenzi wa nyumba za Ghorofa zingetoa nafasi kwa askari Polisi kuishi maisha ya Staha wanapokuwa kambini tofauti na ilivyo sasa hali iliyowalazimu askari kuongeza vyumba katika nyumba wanazo ishi ili waweze kuenea na familia zao.

“Nilitamani sana msingi huu ungetengenezwa kwa ajili yakupanda juu lakini tukasema kwa sababu serikali imetupa fursa hii ebu tuitumie hii kuwa kichocheo kwa ajili ya makazi mengine yatakayo endelea yasibaki kuwa ya chini .” alisema Dkt Mghwira .

Kutokana na hali hiyo Dkt Mghwira alimuagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamisi Issah kukaa na waandisi kwa ajili ya kufanya tathimini ya makazi yanayohitajika kwa ajili ya askari Polisi pamoja na gharama za ujenzi wa nyumba hizo.

“ RPC kakae na wahandisi waturetee utaratibu wa kujenga makazi yote yanayohitajika tukipandisha juu na tutahitaji fedha kiasi gani ,…tunaweza kuanza kukusanya kidogo kidogo kama hivi ninavyoona sasa,maana tunaweza tukamaliza ujenzi hata kabla hatujaigusa ile pesa iliyotolewa na Rais Magufuli.”alisema Dkt Mghwira .

“Na mimi kwa hili naomba niwahamasishe tena wana Kilimanjaro ,yeyote anaye jisikia kutenda lolote katika hili alete mchango wake kama sadaka yake kwa ajili ya maisha na ustawi wa askari wetu ,kama mnavyoona eneo hili liko wazi na linapakana na makazi ya watu na hakuna ukuta unaotenganisha maeneo hayo , hili ni upungufu mkubwa sana ,”aliongeza Dkt Mghwira.

Tayari hadi sasa wadau mbalimbali wameendelea kutoa michango yao ikiwemo kampuni ya Rocktronic iliyotoa Loli pamoja na Greda kwa ajili ya kusafisha eneo la ujenzi ,Ravj aliyetoa kokoto tani saba , mfanyabiashara Mr Ngowi aliyetoa mifuko 200 ya saruji pamoja na askari namba E 1708 Koplo Dickson Mwakabuta ambaye ametoa mchanga Lori moja kwa hiari yake.
Sehemu ya mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na Kampuni ya Jun Yu inayoendeshwa na raia wa China iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari Polisi .

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira ,akiongizwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hamis Issah kwa kutizama maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari zinazojengwa katika kambi ya Polisi Moshi. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira ,akizungumza jambo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hamis Issah mara baada ya kutizama maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari zinazojengwa katika kambi ya Polisi Moshi. 

Baadhi ya Mafundi wakiendelea na ujenzi katika eneo hilo la kambi ya askari Polisi. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akizungumza wakati wa kupokea msaada wa saruji kutoka kampuni ya Jun Yu. 
Baadhi ya wageni waliofika katika hafla hiyo. 
Baadhi ya Raia wa China wanaoendesha kiwanda cha kutengeneza saruji wakiwa katika hafla hiyo. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Jun Yu , Tian Haifeng akimwaga maji wakati Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akinawa Mikono.
Dkt Mghwira akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jun Yu , Tian Haifeng mara baada ya hafla fupi ya kupokea msaada wa Saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari Polisi.

MAREKANI YAWAAPISHA WAFANYAKAZI 59 WA KUJITOLEA KUSAIDIA AFYA NA KILIMO

$
0
0
Na Hussein Stambuli, Morogoro

Ubalozi wa marekani umewaapisha wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2 katika sekta ya kilimo na afya lengo kuongeza uzoefu na maarifa mapya katika sekta hizo…

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuwaapisha wafanyakazi hao kutoka shirika la wafanyakazi wa kujitolea wa kimarekani peace corps kaimu balozi wa marekani dk inmi patterson amesema kuwa wafanyakazi hao wataongeza uzoefu na maarifa katika sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo huku katika upande wa afya wakiwa na lengo la kujenga uelewa juu ya ugonjwa wa hiv na utapiamlo.

“Kupitia program hii mtaweza kuleta mabadiliko kwa watanzania mtakaofanya nao kazi na hata kwenu nyinyi wenyewe” amesema dr inmi patterson

Naibu waziri ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) mwita mwikabe amesisiti viongozi wa wilaya walizopangiwa wafanyakazi hao wameombwa kudumisha ushirikiano na wafanyakazi hao ili kuhakikisha maarifa waliyonayo wanayapokea pamoja na kulitangaza taifa katika nyanja mbalimbali na kutaka kuenziwa kwa ushirikiano huo wa kupokea wafanyakazi wa kujitolea ulioasisiwa na rais wa taifa hilo john f kennedy mwaka 1961.

“ningeomba kuweza kuwasisitiza wakuu wa wilaya na viongozi wote watakao husika moja kwa moaja kuwapokea wageni hawa ni muhimu kuwapa ushirikiano kwani kubadilishana maarifa kutasaidia wananchi wetu kujifunza mambo mapya ambayo yatasaidia kukua katika sekta ya kilimo na afya na umoja huu ni muhimu ukaenziwa” amesema mwikabe, Naibu waziri ofisi ya rais (tamisemi)

Wafanyakazi kutoka marekani waliopata mafunzo ya lugha na tamaduni kwa muda wa wiki 10 wameonesha kuvutiwa na aina ya maisha ya watanzania na wakiahidi kutoa ushirikiano zaidi kwani wanaamini watanzania wengi wanapenda kujifunza na wao watajitahidi kurithisha maarifa waliyonayo hasa kwenye sekta ya kilimo na afya bora.

“Tumefurahishwa na uwepo wetu hapa katika nchi hii tunahakika ushirikiano uliopo utatuwezesha kubadilishana uzoefu wa kiufundi na tamaduni tunauhakika tumeishi vyema na kutambua changamoto ambazo zinatukabili tumejipanga katika uvumilivu na tunaamini mwishoni wote tutafurahi kuyaona mafanikio” amesema sidney cech, muwakilishi wafanyakazi

Peace corps ni taasisi ya seriakli ya marekani iliyoanzishwa mwaka 1961 chini ya rais john f kennedy ambayo mpaka hivi sasa wafanyakazi wapatao 7000 wanahudumu katika nchi 70 duniani kwa zaidi ya miaka 50 huku lengo likiwa ni kuendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na tamaduni.
 Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson akiwaapisha wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2 katika sekta ya kilimo na afya.
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson akizungumza jambo na wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani.
 Wafanyakazi wa kujitolea wapatao 59 raia wa Marekani watakao hudumu nchini ndani ya wilaya 35 kwa muda wa miaka 2.

IGP SIMON SIRRO AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO.

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simoni Sirro amefanya ziara katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo kwa lengo la kutaka kujua hali ya kiusalama katika maeneo hayo, zaidi ikiwa kuwasikiliza wananchi wan maoni gani juu ya ushirikiano wao na Jeshi la Polisi katika utendaji kazi wa kila siku.

Aidha amewashukuru wananchi na wafanyabiashara wa Kariakoo kwa ushirikiano wao huku akiwataka waendelee kuwafichua wahalifu wa mifukoni na wale wanaotumia udanganyifu wa kuwaibia watu kwa kuwauzia sabuni na kusema mwisho wao hauta kuwa mzuri maana uhalifu hauna nafasi nchini.

IGP Sirro amewataka wananchi wote kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi hasa pale wanapokuwa na shaka na jambo fulani ili hatua z mapema ziweze kuchukuliwa kwa lengo la kuulinda usalama na amani iliyopo nchini, lakini pia amewahakikishia wananchi kuwa katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha kuwa linasimamia usalama wa raia na mali zao ili waweze kusherekea wakiwa salama.

Mariam afanyiwa uchunguzi kubaini ugonjwa alionao

$
0
0
Daktari Bingwa Upasuaji (plastic surgery), Dkt. Ibrahim Mkoma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma ya matibabu ambayo Bi. Mariam Rajab Juma ameanza kupatiwa katika hospitali hiyo.


Na John Stephen Massawe.


Wataalam wabobezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo wameanza kufanya vipimo mbalimbali vya uchunguzi kwa Mariam Rajab Juma mwenye kidonda sehemu ya mgongoni ili kubaini chanzo cha ugonjwa alionao.

Akizungumza na Wanahabari juu ya mwenendo wa matibabu ya Mariam, Daktari Bingwa wa Upasuaji Dkt. Ibrahim Mkoma amesema vipimo hivyo ni pamoja na kuchukuliwa sampuli ya nyama kutoka sehemu ya kidonda na kupelekwa maabara kwa watalaam wa patholojia ili kubaini kama kuna saratani au la. 

Aidha Mariam ameandikiwa kufanya vipimo mbalimbali ikiwemo CT-scan ya kifua na kichwa, Ultrasound pamoja na vipimo mbalimbali vya damu.

Dkt. Mkoma amesema kidonda kilichopo sehemu ya mgongo wa Mariam ni kidonda sugu na kwamba hadi sasa haijabainika kama mgonjwa huyo ana tatizo la saratani au la mpaka hapo majibu ya wapatholojia yatakapo patikana ndani ya siku nne kuanzia sasa. 

Mariam amesema aliwahi kuugua moto akiwa na umri wa miaka mitano ambapo alitibiwa na kupona ingawa alibaki na kovu kubwa kuanzia sehemu ya mgongo wake hadi kwenye kisogo. 

Amesema mwezi wa nane mwaka jana alipata kipele kwenye kovu na baadae kipele hicho kugeuka kuwa jipu. Alipotumbua jipu lilitoa usaha na kisha kuanza kuota kidonda kilichoendelea kuongezeka siku hadi siku.

“Nilienda kutibiwa katika Hospitali ya Makiungu iliyopo Manispaa ya Singida, lakini pia kutokana na wazazi wangu kutokua na uwezo wa kifedha niliacha kwenda hospitalini na kuanza kusafisha kidonda mwenyewe, huku nikiwaomba marafiki zangu niliosoma nao sekondari wanichangie fedha ili niweze kununua dawa,” amesema Mariam.

Amesema wakati anatibiwa katika Hospitali ya Makiungu wataalam walimshauri kuja Muhimbili ili kupatiwa matibabu zaidi, lakini kutokana na wazazi wake kukosa fedha alimtafuta rafiki yake aitwaye Seif ambaye pia alisoma naye sekondari akamrekodi kwa simu yake na kutuma kwenye mitandao ya kijamii na huo ukawa mwanzo wa yeye kuanza kupata msaada.

Mariam anaishukuru Serikali kupitia kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuitikia wito wa kumsaidia na kuanza kumpa huduma.

Aidha, anawashukuru Watanzania kwa jinsi walivyompigia simu na kutaka kumsaidia baada ya kuona picha ya video kwenye mitandao ya kijamii.

Habari kwa hisani ya Muhimbili National Hospital

RPC WANKYO APIGA MARUFUKU DISKO TOTO NA KUJAZA KUMBI ZA STAREHE KWENYE PASAKA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

JESHI la polisi mkoani Pwani, limepiga marufuku kupiga disko toto pamoja na kuwaasa wamiliki wa kumbi za starehe kuacha kujaza watu wengi kuzidi uwezo wa kumbi zao, kwenye sikukuu ya pasaka.

Aidha limejipanga kufanya msako na doria ili kuhakikisha hakuna tukio la kihalifu litakalofanikiwa kuelekea sikukuu hiyo.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa aliwatahadharisha, wamiliki hao kuzingatia sheria na atakaekiuka agizo hilo hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Katika hatua nyingine ,aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuzuia ajali katika barabara za mkoa huo.

Wankyo alisema, madereva wasiendeshe baada ya kutumia vileo kwani askari wao wa kikosi cha usalama barabarani wapo kila kona hivyo hawatoweza kupita mkoani humo,pasipo kukaguliwa .

"Kwa wamiliki wa magari yanayosafirisha abiria kuzingatia uwepo wa madereva wawili na magari yatakayobainika kuwa na dereva mmoja hayataruhusiwa kuendelea na safari"

Kamanda huyo hakusita kuwaomba wazazi na walezi kuweka ulinzi majumbani mwao endapo watatoka kwenda kwenye nyumba za ibada na kuwawekea waangalizi watoto watakapowaacha nyumbani.

WAKATI HUO HUO, jeshi hilo linamshikilia Mwamini Shomary (37) ,mkazi wa Yombo Bagamoyo kwa kosa la kusafirisha mafuta ya kula dumu kumi yenye thamani ya laki tano, ambayo hayajalipiwa ushuru.

"Askari wetu wakiwa doria maeneo ya Kwamatias, huko Kibaha walimkamata mtuhumiwa akiwa na mafuta hayo aina ya mico gold ujazo wa lita 20 kila moja akitokanayo Bagamoyo.

Wankyo alielezea kwamba, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kamanda huyo aliongeza kusema, pia wamekamata bangi puli tano, kete 155 na pombe aina ya gongo lita 11.

BENKI YA UBA YAJIVUNIA USHIRIKI WAKE KATIKA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO NCHINI TANZANIA

$
0
0
*Yaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa njia ya kidigitali, wagusia changamoto ya mikopo
 
Na Agnes Francis ,Globu ya jamii

BENKI ya UBA imesema inajivunia uwepo wake wa miaka 10 nchini kwani imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kuchangia maendeleo ya nchi ya Tanzania huku ikieleza wazi moja ya changamoto kubwa iliyopo katika taasisi za kibenki ni urejeshwaji wa mikopo iliyokopwa na wateja.

Kuhusu mikakati yao katika kujiimarisha kutoa huduma kwa Watanzania katika sekta hiyo ya kibenki, imesema imeweka nguvu zaidi kutoa kutoa huduma kwa njia ya mtandao(Kidigiali) hasa kwa kuzingatia kuna idadi kubwa ya watumiaji wa simu, hivyo imetoa siri benki hiyo iko mbioni wateja watatumia WhatsApp kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali ya kifedha kwa maana ya kutuma au kupokea tena kwa usalama zaidi.

Wakizungumza leo Aprili 18,2019 jijini Dar es Salaam na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, viongozi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Usman Isiaka wamesema wanajivunia kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha uchumi unaimarika na kubwa ambalo linawapa faraja ni namna ambavyo benki yao imekuwa mstari wa mbele kusaidia miradi ya maendeleo na hivi karibuni wameungana na Benki ya CRDB kutoa fedha ili kusaidia ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji.

Mkurugenzi Mkuu wa United Bank For Afrika(UBA) nchini Tanzania Usman Isiaka amesema benki yao imetimiza miaka 10 tangu ifungue tawi lake nchini Tanzania na imefikisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo ina matawi katika nchi mbalimbali Afrika na nje ya Afrika na lengo kuu la uwepo wake ni kusaidia katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

"Tumekuwa tukishiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo na hii imetupa nafasi ya benki yetu kuwa mstari wa mbele kutoa fedha kwa ajili ya kuwa sehemu ya kufanikisha miradi ya maendeleo.Uwepo wetu wa miaka 10 nchini Tanzania tumekuwa tukichangia ukuaji wa uchumi kwa kutoa mikopo kwa wananchi wa kada mbalimbali,"amesema na kuongeza wataendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kwa Serikali ili iweze kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Hata hivyo, amesema benki hiyo imeweka mkakati wa kuendelea kuwa karibu na wananchi ikiwa pamoja na kujitangaza ili ifahamike zaidi na kuongeza kwa kipindi cha miaka miwili sasa wamefanikiwa kujitambulisha na huduma za kibenki ambazo wanazitoa huku akisisitiza wameamua kujikita katika kutoa huduma kidigitali zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Corporate Mussa Kitambi ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa pamoja na mafanikio ambayo benki hiyo imeyapata kwa kutoa huduma bora kwa wateja wao, changamoto kubwa inayowakabili ni urejeshwaji wa mikopo kutoka kwa wateja wao na kwamba kwa mazingira ya sasa hata walioweka hati ya nyumba kama dhamana ya mkopo nako hakuko sawa kwani bei ya nyumba imeshuka.

"Changamoto ambayo tunakabiliana nayo ni katika eneo hili la mikopo, wapo ambao wamekopa lakini katika kurejesha kuna shida, wapo ambao waliweka hati ya nyumba lakini nako soko la bei ya nyumba limeporomoka, hivyo inakuwa ngumu fedha iliyokopwa kurejea yote.

"Pia changamoto nyingine iliyokuwa inatukabili ni katika eneo la kubadilisha fedha ambako benki zilikuwa katika wakati mgumu kwani hakukua na uhakika wa bei ya kubadilisha fedha lakini baada ya BoT kuamua kuweka mfumo mzuri sasa mambo yanakwenda vizuri.Hiyo changamoto iliyotokana na kubadilisha fedha za kigeni haiko tena,"amesema.

"Tunafahamu kuwa Serikali iliamua fedha zake zote ziwekwe Benki Kuu, hivyo baada ya kuondolewa kwa fedha hizo ilileta changamoto kwetu, hivyo baada ya kuziondoa ndio maana mtaona hivi sasa benki zote zimekimbilia kwa wananchi kwa kuwa karibu nao na kuwahudumia,"amesema Kitambi.

Ameongeza changamoto nyingine ambayo wamekuwa nayo ni kwamba walikuwa wanafanya kazi kwa sehemu kubwa na Serikali na hasa ya kuweka fedha katika benki binafsi la kwetu ni eneo hili la urejeshwaji wa mikopo kutoka kwa wateja wetu ambao tuliwakopesha.Wapo walioweka hati za nyumba lakini ukweli hivi sasa soko la nyuma liko chini.Hivyo hata unapotaka kuuza nyumba kurejesha mkopo bado haitishi.Changamoto nyingine ilikuwa ni kupanda kwa Dola lakini tunaishukuru Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa kuwema mfumo rasmi wa kubadilisha fedha za kigeni.

"Kabla ya BoT kutoa maelekezo katika eneo hili la kubadilisha fedha za kigeni benki yetu na huenda hata benki nyingine zilikuwa katika wakati mgumu lakini sasa kuna unafuu maana kuna mfumo mzuri katika kubadili fedha za kigeni.Kwa sasa mambo yanakwenda vizuri,"amesema Kitambi. 

Aidha Mkuu wa Kitengo cha kuhudumia Serikali na mashirika ya Umma Dominick Thimoth amefafanua wamekuwa wakisaidia kwa kutoa mikopo kwa Serikali kwenye miradi pamoja na kuchangia bajeti ya Serikali.Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Wateja UBA Asupya Nalingigwa ametumia nafasi hiyo ya kuzungumza na wahariri kuelekeza namna ambavyo wamejipanga kutoa huduma kimtandao kwa kutumia simu za mkononi na hivi karibuni watazindua huduma ya Whtsap kwa ajili ya wateja kufanya miala.
 Pia amesema katika kurahisisha namna ya kujiunga na benki yao, wanayo huduma ya mwananchi kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi kwa kusaidia huduma ya Leo ambayo ni ya kisasa.
 Mkurugenzi wa UBA Usman Isiaka akizungumza na waandishi wa habari akifafanua huduma zinazotolewa na banki ya UBA kwa serikali na hata sekta binafsi leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu Kitengo cha wateja  UBA Asupya Nalingigwa akielezea namna ya kufungua akaunti ya benki hiyo kwa kutumia mfumo wa kisasa kupitia simu kwa lengo la kutaka kuwafikia watanzania wengi leo Jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa Benki ya UBA wawakisikiliza maswali ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam
Viongozi wa UBA katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali leo Jijini Dar es Salaam.

SHERIA YA NDOA YA 1971 NI SHERIA YA KIMAPINDUZI, ILIYOKUJA KWA WAKATI MUAFAKA- PROF KABUDI ALIAMBIA BUNGE.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ni Sheria ya kimapinduzi ambayo ilikuja nchini kwa wakati muafaka na kufafanua kuwa anaiona sheria hiyo kuwa ni ya kimapinduzi kwa kuwa nchi nyingi duniani zimeshindwa kuwa na Sheria kama hiyo.

Prof. Kabudi amesema hayo bungeni jana wakati alipokuwa akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wake Dkt. Augustine Mahiga.

“Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ni Sheria ya kimapinduzi na nchi nyingine mpaka leo zimeshindwa kutunga sheria ya aina hii, ilikuja kwa wakati muafaka na ni ya kimapinduzi kwa kuwa watu wengi wameshindwa kuwa na Sheria kama hiyo,” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi aliongelea suala hilo baada ya wabunge waliokuwa wakichangia hoja ya Dkt. Mahiga kutaka Sheria hiyo ya Ndoa ifanyiwe marekebisho hasa katika kipengele cha umri wa mtoto  wa kike kuolewa.

Amewataka Wabunge waache kuchukulia kipengele cha umri wa mtoto wa kike kuolewa kama kigezo cha kuifanya sheria hiyo kuwa mbaya na kwamba yapo mambo maengi mazuri ndani ya sheri hiyo kama vile muwezesha mwanamke alieolewa kumiliki mali huku akitumia jina la baba yake , enzi za ukoloni jambo hilo lilikuwa haliwezekani.

“Tusichukulie suala moja tu kuwa ndio kigezo cha kusema sheria hii  ni kandamizi, kifungu hicho cha umri wa kuoa au kuolewa hakizungumzii msichana tu bali pia kinazungumzia mvulana, ndani ya sheria yetu wako wavulana wanaoweza kuoa chini ya umri mdogo, sheria hii ni sheria ya kimapinduzi kwasababu ni sheria kwanza iliyowakomboa wanawake wa kitanzania hasa wenye ajira, kwa kuweza kwenda kufanya kazi na kutpanda vyeo kwa sababu kabla ya hapo Sheria tuliyoachiwa na Muingereza ilikuwa inasema mwanamke lazima akae mahali alipo mmewe na hili liliwanyima wanawake fursa,” alifafanua Prof. Kabudi.

 Amesema kuwa umri wa mtoto wa kike kuolewa ni jambo nyeti sana na litasababisha ugomvi hata miongoni mwa wabunge kwani hata nchi zilizoendelea akiitolea mfano Uingereza umri wa mtoto wa kike kuolewa ni miaka 16 na kuongeza kuwa wasichana hawaolewi kwa sababu ya fursa mbalimbali za elimu na mwamko.

Amewataka wabunge kuisoma vizuri sheria hiyo kwani ina mambo mengi mazuri ambayo imeyaweka n ani makubwa hivyo ni vizuri tukaielewa.

Kangi Lugola: Watumishi Kitengo cha Malalamiko tekelezeni wajibu wenu

$
0
0
NA VERONICA MWAFISI, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa wito kwa watumishi wa Wizara hiyo kitengo cha kushughulikia malalamiko ya wananchi, kutekeleza wajibu wao wa kufuatilia na kuyapatia ufumbuzi wa haraka malalamiko wanayopokea. Lugola aliyasema hayo jijini Dodoma juzi katika kikao kazi kilichoshirikisha watumishi wa kitengo hicho.

Aliwataka wafuatilie malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi ya taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). “Hakikisheni malalamiko mnayoletewa, mnayapatia ufumbuzi wa haraka bila kufika ngazi ya juu, tekelezeni wajibu wenu kwa ufanisi ili kujenga imani kwa wananchi (walalamikaji).

“Kama wananchi watajiridhisha kuwa kitengo hiki ni msaada mkubwa kwao, mtakuwa mmejijenga uaminifu na kuifanya Wizara ijitegemee kushughulikia malalamiko,” alisema. Lugola alisisitiza umuhimu wa viongozi wanaoshughulikia malalamiko yanayotolewa na wananchi kuchukuliwa hatua kama itabainika wameshindwa kutimiza wajibu wao.

Alisisitiza umuhimu wa kubadili mfumo wa kushughulikia malalamiko akisema yanapofikishwa katika kitengo hicho yachunguzwe hapo hapo wizarani.
“Malalamiko yasirudishwe kwenye taasisi zinazolalamikiwa kama Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na NIDA…pia walalamikiwa waitwe na kuhojiwa.

“Lengo ni kupata suluhisho la malalamiko yanayotolewa ili kuleta uhuru, malalamiko yajibiwe kwa haraka na uwazikwa njia ya barua ama simu, malalamiko ambayo yataonekana hayana ukweli walalamikaji wapewe taarifa,” alisisitiza Lugola. Aliongeza kuwa, malalamiko mengine hayapaswi kuchukua muda mrefu ili kutatuliwa akitolea mfano malalamiko ambayo aliyapokea kwa wananchi na kuyapatia ufumbuzi wa haraka kwenye ziara alizofanya katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, alitumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa kitengo hicho kwa kuyafuatilia malalamiko yanayotolewa na wananchi pamoja na kuyafanyia kazi kwa haraka. Alisema kitendo cha kupokelewa, kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi ndani ya muda mchache, kitawezekana kama kila mtumishi anayeshughulikia malalamiko atawajibika ipasavyo ili kupunguza mrundikano wa malalamiko yanayotolewa.

Alitoa wito kwa watumishi wa kitengo hicho kwenda maeneo mbalimbali ambayo yana malalamiko ili kupata usahihi wa taarifa, kuzifanyia kazi na kutoa maamuzi. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo na kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, NIDA na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wakisikiliza maoni, hoja mbalimbali kwenye kikao kazi kilichoshirikisha watumishi wa Wizara hiyo kitengo cha kushughulikia malalamiko ya wananchi Kilicofanyika juzi Mjini Dodoma.
(Picha na Veronica Mwafisi-MOHA).

WIZARA YA AFYA IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII YAANZA KAZI RASMI MJI WA SERIKALI

$
0
0
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imeanza rasmi kutoa huduma za Ofisi katika mji wa Serikali uliopo Mtumba nje kidogo ya Jiji la Dodoma na kuwataka wananchi kufuata huduma za kiofisi katika ofisi hizo mpya. .

atibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kimsingi Ofisi yake kwa sasa inatoa huduma zake katika ofisi zake zilizoko Mtumba na kuwataka wateja wake kufuata huduma hapo ambazo zitakuwa wazi muda wote

"Nawakaribisha sana wananchi wote kuanza kutumia ofisi zetu hapa eneo la Mtumba na tuko hapa kama hatua muhimu ya kutekeleza kikamilifu agizo la Rais kwa vitendo." Aliongeza Dkt.Jingu. .

Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na Wizara na Rasilimali Watu Leornad Mchau amesema ni uamuzi muhimu sana wa kuweka Ofisi za Serikali mahali pamoja ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa haraka na kwa gharama nafuu. .

Ameusifu uamuzi wa Serikali kuwa wa msingi sana akitofautisha na Dar es Salaam ambapo Wizara za Serikali zilitapakaa maeneo mbalimbali ya Jiji lakini kwa sasa hata kama ukitokea Jijini Dar es Salaam ni rahisi kupata huduma za Serikali katika eneo moja.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza ametoa rai kwa uongozi wa Jiji la Dodoma kuharakisha miundombinu ya usafiri ili wananchi wanaoitaji huduma za kiofisi waweze kufika katika eneo la Mtumba na kupata huduma hiyo kwa haraka.

Magwiza ameongeza kuwa kwa maoni yake wateja watu wanahitaji miundombinu rafiki ili waweze kuhudumiwa na ofisi yake kwa haraka lakini ana imani uongozi wa Jiji utaharakisha au kulifanyia kazi jambo hili na kuwezesha wananchi kupata huduma ya haraka na kuwataka kuweka tayari mipango miji ili wawekezaji waweze kuwekeza jilani na eneo hilo.

Wizara za Serikali tayari zimeanza kutolewa katika Jiji jipya la Serikali kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka Viongozi wa Setikali kuanza kutoa huduma zao Mtumba baada ya kukamilika kwa Ofisi hizo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akifurahia jambo mara baada kuanza kazi Makao Makuu Mapya ya Wizara yake yaliyoko eneo la Mtumba nje kidogo ya Jiji Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Mwajuma Magwiza wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii mara ya kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya zilizoko Mtumba nje Kidogo ya Jiji la Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Leornard Mchau mara ya baada kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya zilizoko Mtumba nje Kidogo ya Jiji la Dodoma.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MENEJIMENTI YA PSSSF

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Menejimenti ya PSSSF, katika jengo la ofisi hiyo, jijini Dodoma Aprili 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2019

$
0
0

 Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akimtangaza mfanyakazi bora wa ofisi yake wakati wa kikao cha uchaguzi wa mfanyakazi bora kilichofanyika jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akifafanua jambo kwa watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge.
 Baadhi ya wafanyakazi bora wa Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mwenendo wa uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akisimamia zoezi la kuhesabu kura kwa ajili ya kumchagua wa mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni wawakilishi wa wafanyakazi bora walioingia kwenye ushindani.
 Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (katikati) akimpa mkono wa pongezi mfanyakazi bora wa mwaka 2019 wa ofisi yake Bw. Jafari Kalaghe, Afisa Tawala baada ya uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge na kushoto ni Mkurugenzi wa  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
 Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi, Bw. Kamugisha Lufulenge akitoa ufafanuzi wa kanuni za kumchagua mfanyakazi bora kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) kabla ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa Ofisi hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni  Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Musa Joseph.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji akiwa tayari kuwasilisha kura yake baada ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi hiyo uliofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni  Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw Ayoub Banzi na kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Mary Mwakapenda.

 Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsilikiza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (hayupo pichani) alipokuwa akitangaza mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Utumishi katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imefanya uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa mwaka 2019 kwa kuwashindanisha wafanyakazi bora saba (7) kutoka Idara na Vitengo vya ofisi hiyo ambao wamepatikana kwa kigezo cha utendaji kazi mzuri kupitia Mfumo wa Wazi wa Mapitio ya Utendaji Kazi (OPRAS).

Mfanyakazi bora aliyechaguliwa ni Afisa Tawala, Bw. Jafari Kalaghe kutoka Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu. 
Mara baada ya kumtangaza Bw. Kalaghe kuwa mfanyakazi bora, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba, amempongeza kwa ushindi na kuwashukuru watumishi kwa kufanya uchaguzi uliozingatia vigezo.

Bw. Kiliba amesema kuwa, Bw. Kalaghe ni mchapakazi hodari anayeonekana na kila mtu na amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza kabla ya uchaguzi, Bw. Kiliba, aliwataka watumishi kumchagua mtumishi ambaye utendaji kazi wake unaonekana kuwa ni bora badala ya kuchagua kwasababu za kufahamiana.

“Tunapopiga kura, tusimchague mtumishi kwasababu unamfahamu au anatoka kwenye idara au kitengo kimoja, bali tumchague kwa uchapakazi wake unaoendana na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, inayohimizwa na Serikali ya Awamu ya Tano,” Bw. Kiliba ameongeza.
Kwa upande wake, mfanyakazi bora aliyechaguliwa, Bw. Jafari Kalaghe amewashukuru watumishi kwa kuona utendaji wake na kuahidi kuendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano.



RAIS DKT. MAGUFULI ASALI MISA YA ALHAMISI KUU KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki akishiriki Misa Takatifu ya Alhamisi Kuu katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.



Waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakiwa katika Misa Takatifu ya Alhamisi Kuu kanisani hapo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WALIOTUMIA JINA LA MAMA JANETH MAGUFULI KUTAPELI WAPANDISHWA KIZIMBANI

Mtoto mchanga wa siku mbili atupwa katika Choo cha shule ya sekondari ya kazima manispaa ya tabora

$
0
0

Na Editha Edward wa Michuzi Blog, Tabora

Maiti ya mtoto mchanga anaekadiriwa kuwa na umri wa siku mbili amekutwa kwenye choo cha wasichana katika shule ya sekondari Kazima iliyopo manispaa ya Tabora na kusababisha taharuki kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo 

Akizungumza na Michuzi Blog katika eneo la tukio mara baada ya kuvunja choo hicho mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa Bi.Vailleth Machechu amekemea kitendo hicho cha kikatili kilichofanywa mkoani humo.

Aidha mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya kazima Bw. Mrisho Kuvuluga amesema kuwa kitendo hicho kinaweza kuwa kimefanywa na wananchi kutoka nje ya shule kutokana na kichanga hicho kuonekana na umri wa siku mbili na shuleni hapo utaratibu wa kupima ujauzito wanafunzi wa kike unafanywa kila  msimu wa masomo.

 Wauguzi wakiandaa mwili wa kichanga hicho baada ya kuuopoa chooni

Choo cha wasichana katika shule ya sekondari Kazima manispaa ya Tabora kilipokutwa kichanga hicho. Picha na Edith Edward

MSAKO WA WEZI WA BETRI YA KUWASHIA TAA ZA BARABARANI MJINI TABORA WAANZA

$
0
0
Na Editha Edward wa Michuzi Blog, Tabora

Zaidi ya shilingi Milioni Tatu zimetumika  kununua betri ya mashine ya kuongozea taa za barabarani iliyoibwa katika makutano ya barabara ya Isevya katika wilaya ya Tabora mjini mkoani Tabora na kusababisha adha kubwa. 

Akithibitisha hilo, Kamanda wa jeshi la polisi wilaya ya Tabora mjini Afande John Mfinanga amesema msako wa kuisaka betri hiyo umeanzishwa na yeyote atakayekutwa nayo mkono mrefu wa sheria utamshughulikia.

Kamanda huyo ametanabahisha kwamba kila mwananchi anatakiwa awe mlinzi wa mali za umma ili kuweza kurahisisha kuwabaini na  kuwafikisha wahalifu kwenye vyombo husika ili kuweza kuimarisha usalama wa mali za umma na watu katika jamii.
"Unapoiba vifaa vya barabarani sio kwamba unaikomoa serikali bali pia unakomoa wananchi wote. Ni vyema tushirikiane kuwafichua wezi hawa kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mkoa wetu", amesema Afande Mfinanga 
Mkuu wa kitengo cha Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Bw.  Raphael Mlimaji amesema wizi wa betri hiyo umesababisha kusimama kwa kutumika taa katika eneo hilo na kusababisha foleni zisizo lazima pamoja na ongezeko la ajali.
"Hii hasara imesababishwa na mtu mmoja lakini inaathiri wananchi wengi sana. Tutaendeleaje wakati nchi inataka kusonga mbele lakini kuna wachache wanaotaka kuturudisha. Hili jambo sio tu  nyuma ni kinyume Cha sheria bali pia limekera wengi na kutia hasara serikali", amesema Mlimaji.
Aidha Kamanda wa usalama barabarani  Afande Ame Malawi amewataka wananchi mkoani Tabora kufuata Sheria za barabarani ili kuweza kusaidia kuondokana na ajali za Mara kwa Mara.
  Kamanda wa jeshi la polisi wilaya ya Tabora mjini Afande John Mfinanga 
 Nguzo na mashine ya taa za barabarani katika makutano ya barabara ya Isevya katika wilaya ya Tabora mjini
Taa za barabarani katika makutano ya barabara ya Isevya katika wilaya ya Tabora mjini

MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU.

$
0
0
Mariam Rajab (25), mkazi wa Singida ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, amewasili saa 6:00 usiku wa kuamkia leo  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) yarai kuanza matibabu kwa udhamini wa serikali.

Mariam alipokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura ambapo amefanyiwa vipimo vya awali na kisha na kupelekwa kulazwa wodini ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu Zaidi siku ya Alhamisi.

“Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika familia ya kimasikini, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo langu, tatizo ambalo ninalo, tatizo lenyewe ambalo ninalo ni kidonda ambacho kipo hapa mgongoni, naombeni Watanzania wenzangu muweze kunisaidia niweze kwenda Hospitali ya Muhimbili ili niweze kupata matibabu. Sina cha kuwalipa bali Mungu atawalipa, asanteni” hayo ni maelezo aliyotoa Mariam kupitia picha ya video iliyoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki hii na kuvuta hisia za watu wengi.
Kutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (MB) aliuagiza Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kumtafuta Mariam ili apelekwe Hospitalini hapa kwa ajili uchunguzi na matibabu.
Mariam ameletwa na gari la wagonjwa (ambulance) kutoka Singida lililoanza safari yake saa 8:00 mchana jana. Tutaendelea kuwapa taarifa juu ya mwenendo wa matibabu yake.
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images