DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI JUMATANO APRILI 17, 2019
↧
↧
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMAENDELEO TEMEKE WAMFURAHISHARC MAKONDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa, vyoo na mabweni katika shule ya msingi Tuangoma jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Kijichi ambapo alizungumza na wanafunzi na kuwataka kuzingatia masomo na kuweka mbele nidhamu, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi akizungumza na wanahabari mara baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa, mabweni na vyoo katika shule ya msingi Tuangoma jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitoa maelekezo mara baada ya kukagua ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wenye ulemavu wa macho katika shule ya msingi Tuangoma, jijini Dar es Salaam.
*Azindua mabweni ya wanafunzi wenye ulemavu wa macho Tuangoma
* Aiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi kwa tenda za miradi ya DMPD
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya Temeke ambapo amekagua ujenzi barabara ya Usalama Chang'ombe, ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya Sekondari kijichi mradi unaofadhiliwa na TAMISEMI, ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wenye ulemavu wa macho ambapo pia ameweka jiwe la msingi, ujenzi wa mradi wa kisima cha maji katika kata ya Charambe pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Yombo Vituka.
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara hiyo Makonda ameipongeza halmashauri hiyo kwa kusimamia vyema miradi hiyo hasa ya barabara ambapo wameokoa gharama kubwa na kujenga barabara imara kwa milioni 900 kwa kilomita moja ukilinganisha na halmashauri ya Kinondoni inayojenga barabara ya kilomita moja kwa zaidi ya shilingi bilioni 2 ambapo amemuagiza Mkurugenzi wa TAKUKURU wa Mkoa huo kufanya uchunguzi wa utaratibu wa upatikanaji wa tenda kwenye miradi inayofadhiliwa na benki ya dunia (DMDP) baada ya kubaini matumizi mabaya ya fedha za serikali katika miradi hiyo kwa baadhi ya maeneo ya miradi.
Makonda amesema haiwezekani Kilomita Moja ya barabara ya Wilaya ya Kinondoni ikajengwa kwa Shilingi Billion 2.7 wakati kwa Wilaya ya Temeke barabara kama hiyo inajengwa kwa shilingi Milioni 900 pekee na yote inafadhiliwa na benki ya dunia.
Aidha Makonda amesema kuwa wazawa wawe mstari wa mbele kuomba tenda za kusimamia miradi ya fedha nyingi ili kuweza kujitangaza na kuongeza ujuzi zaidi na sio kuyaachia makampuni makubwa pekee.
Vilevile Makonda ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuwatazama watu wenye mahitaji maalumu kwa kujenga mabweni ya wanafunzi wenye ulemavu na amewataka kuwatazama watoto kutoka sehemu nyingine ili waweze kunufaika na fursa hiyo.
Ameeleza kuwa nafasi zitakazosalia katika bweni hilo wachukuliwe wanafunzi kutoka maeneo mengine kwa kuwa mradi huo ni wa pekee na maalumu katika mkoa huo na amezitaka halmashauri nyingine kuiga kutoka kwa wana Temeke.
↧
MGONJWA MARIAM RAJAB WA SINGIDA AWASILI MUHIMBILI KWA MATIBABU.
Mariam Rajab (25), mkazi wa Singida ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, amewasili saa 6:00 usiku huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Hivi sasa Mariam amepokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura ambapo anaendelea kufanyiwa vipimo vya awali na kisha atalazwa ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu Zaidi siku ya Alhamisi.
“Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika familia ya kimasikini, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo langu, tatizo ambalo ninalo, tatizo lenyewe ambalo ninalo ni kidonda ambacho kipo hapa mgongoni, naombeni Watanzania wenzangu muweze kunisaidia niweze kwenda Hospitali ya Muhimbili ili niweze kupata matibabu. Sina cha kuwalipa bali Mungu atawalipa, asanteni” hayo ni maelezo aliyotoa Mariam kupitia picha ya video iliyoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki hii.
Kutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (MB) aliuagiza Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kumtafuta Mariam ili apelekwe Hospitalini hapa kwa ajili uchunguzi na matibabu.
↧
Betri la kuongoza Taa barabarani latia hasara serikali
Na Editha Edward- Tabora
Zaidi ya shilingi Milioni Tatu zimetumika kununua betri la kuongozea taa za barabarani lililoibiwa katika makutano ya barabara la isevya wilaya ya Tabora mjini mkoani Tabora, Jambo ambalo limesababisha hasara kwa serikali ili hali fedha hiyo ingetumika kwa maendeleo mengine
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha barabarani TANROADS Raphael Mlimaji amesema wizi wa betri hiyo imesababisha kusimama kwa kutumika Taa katika eneo husika,jambo ambalo limesababisha ongezeko la ajali za barabarani
"Hii hasara imesababishwa na mtu mmoja lakini pia imeaathiri wananchi, Kati yetu wanamfahamu na nchi inataka kusonga mbele mnarudisha nyuma ni kinyume cha Sheria"Amesema Mlimaji
Naye kamanda wa jeshi la polisi wilaya ya Tabora John Mfinanga amesema kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake ili kuweza kuwafikisha wahalifu kwenye vyombo husika ili kuweza kuimarisha usalama katika jamii
"Unapo iba vifaa vya barabarani si kwa kuikomoa serikali bali unakomoa wananchi wote ni vyema tushirikiane kuwafichua wezi hawa kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mkoa wetu"Amesema Mfinanga
Aidha Kamanda wa usalama barabarani Ame Malawi,amewataka wananchi mkoani Tabora kufuata Sheria za barabarani ili kuweza kusaidia kuondokana na ajali za Mara kwa Mara.
Zaidi ya shilingi Milioni Tatu zimetumika kununua betri la kuongozea taa za barabarani lililoibiwa katika makutano ya barabara la isevya wilaya ya Tabora mjini mkoani Tabora, Jambo ambalo limesababisha hasara kwa serikali ili hali fedha hiyo ingetumika kwa maendeleo mengine
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha barabarani TANROADS Raphael Mlimaji amesema wizi wa betri hiyo imesababisha kusimama kwa kutumika Taa katika eneo husika,jambo ambalo limesababisha ongezeko la ajali za barabarani
"Hii hasara imesababishwa na mtu mmoja lakini pia imeaathiri wananchi, Kati yetu wanamfahamu na nchi inataka kusonga mbele mnarudisha nyuma ni kinyume cha Sheria"Amesema Mlimaji
Naye kamanda wa jeshi la polisi wilaya ya Tabora John Mfinanga amesema kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake ili kuweza kuwafikisha wahalifu kwenye vyombo husika ili kuweza kuimarisha usalama katika jamii
"Unapo iba vifaa vya barabarani si kwa kuikomoa serikali bali unakomoa wananchi wote ni vyema tushirikiane kuwafichua wezi hawa kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mkoa wetu"Amesema Mfinanga
Aidha Kamanda wa usalama barabarani Ame Malawi,amewataka wananchi mkoani Tabora kufuata Sheria za barabarani ili kuweza kusaidia kuondokana na ajali za Mara kwa Mara.
Kamanda wa Jeshi la polisi wilaya ya Tabora, John Mfinanga
↧
MAGAZETI YA LEO AL HAMISI ,APRIL 18,2019
↧
↧
WATUMISHI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WATAKIWA KUBORESHA ZAIDI MIFUMO YA UKUSANYAJI MAPATO YA SERIKALI
Na Farida Ramadhani & Josephine Majura. WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji , amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya ndani na kupanua wigo wa walipakodi pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, wizarani hapo.
Alisema Wizara ya Fedha na Mipango imebeba majukumu ya kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali na matumizi ya rasilimali fedha yanasimamiwa kikamilifu.
“Watendaji na watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha na ufuatiliaji wa matumizi ili kuhakikisha rasilimali fedha zilizopo zinatumika kwa ufanisi” ,alisema Dkt. Kijaji.
Alisema ni jukumu la Watumishi wa Wizara kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016-2021) wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.
Aliwataka Watumishi kufanyakazi kwa ushirikiano, umoja , mshikamano, ufanisi na uadilifu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyopo.
“Ni wajibu wetu pia kutumia busara na hekima, hususan pale tunaposhughulikia maslahi ya watumishi na wananchi kwa ujumla”, alisisitiza Dkt. Kijaji.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Doto James, amemhakikishia Dkt. Kijaji kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa haraka na ukamilifu kwa maendeleo ya nchi kwa kuwa Wizara hiyo ni nguzo ya kusimamia uchumi wa nchi.
Alisema uzoefu unaonesha kwamba vikao vya Baraza la wafanyakazi vimekua na umuhimu mkubwa mahala pa kazi na kwa kuzingatia umuhimu huo Wizara ya Fedha na Mipango imehakikisha kuwa vikao vya Baraza vinafanyika kila mwaka kulingana na Mkataba kati ya Wizara na Chama cha Wafanyakazi cha Serikali na Afya (TUGHE).
Alisema kupitia Baraza la wafanyakazi Wizara imefanikiwa kuongeza mshikamano kati ya Wafanyakazi hivyo kuamsha ari kwa watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali.
Aliongeza kuwa hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwenye Baraza zimeboresha huduma kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia watumishi vitendea kazi pamoja na kuwelimisha watumishi kuhusu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu (BP), Kifua kikuu, HIV na UKIMWI.
Meza Kuu (waliyokaa) ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),(watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Doto James akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma .
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (watatu kushoto) wakiimba wimbo wa kudumisha umoja kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma .
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa kudumisha umoja na mshikamano "solidarity forever" kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuapishwa hivi karibuni , Bw. Adolf Ndunguru, katika Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo , Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw.Doto James akitoa salam za utangulizi kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), katika ukumbi wa Kambarage Dodoma ambapo Watendaji wa Wizara walitakiwa kutekeleza jukumu la kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akizungumza wakati wa kufungua Baraza la Wafanyakazi, Jijini Dodoma, ambapo aliagiza Watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya kukusanya mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa walipa kodi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akipongezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.Doto James, baada ya kumaliza hotuba yake alipofungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
↧
TIGO YAWAKUNA MAWAKAWALA WAKE,YAWAMWAGIA FEDHA TASLIMU NCHI NZIMA
Baadhi ya wafanyakazi wa Tigo Mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na Wakala wa huduma ya Tigo Pesa Shine Murtazah ambaye ni mmoja kati washindi wawili wa kanda hiyo waliojishindia zawadi za fedha taslimu kwenye promosheni ya ‘Cash In’ iliyomalizika mwishoni mwa mwezi Machi. Tigo imetoa zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya Tshs 1m/- kwa Mawakala wa Tigo Pesa nchi nzima.
Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Mashariki Abbas Abdulrahman akiagana na na Wakala wa huduma ya Tigo Pesa Shine Murtazah wa Iringa ambaye ni mmoja kati washindi wawili wa kanda hiyo waliojishindia zawadi za fedha taslimu kwenye promosheni ya ‘Cash In’ iliyomalizika mwishoni mwa mwezi Machi. Tigo imetoa zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya Tshs 1m/- kwa Mawakala wa Tigo Pesa nchi nzima
Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Mashariki Abbas Abdulrahman (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja Wakala wa huduma ya Tigo Pesa Shine Murtazah wa Iringa ambaye ni mmoja kati washindi wawili wa kanda hiyo waliojishindia zawadi za fedha taslimu kwenye promosheni ya ‘Cash In’ iliyomalizika mwishoni mwa mwezi Machi. Tigo imetoa zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya Tshs 1m/- kwa Mawakala wa Tigo Pesa nchi nzima
Meneja wa Tigo kanda ya Kusini Mashariki Abbas Abdulrahman (kulia) akiteta jambo na Wakala wa huduma ya Tigo Pesa Shine Murtazah wa Iringa ambaye ni mmoja kati washindi wawili wa kanda hiyo waliojishindia zawadi za fedha taslimu kwenye promosheni ya ‘Cash In’ iliyomalizika mwishoni mwa mwezi Machi. Tigo imetoa zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya Tshs 1m/- kwa Mawakala wa Tigo Pesa nchi nzima
↧
AGAPE YAENDESHA KIKAO CHA USHAWISHI NA UTETEZI WA MASUALA YA AFYA NA UJINSIA
Shirika la Agape AIDS Control Program limeendesha kikao cha ushawishi na utetezi wa masuala ya afya ya uzazi na ujinsia katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumatano Aprili 17,2019 katika shule ya msingi Shingida na kukutanisha pamoja viongozi wa ngazi ya kata,walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari,viongozi wa dini na kimila,wawakilishi wa wanafunzi na wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya idara ya elimu na maendeleo ya jamii.
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana unaotekelezwa na Shirika la Agape kwa ufadhili wa shirika la Sida na nchini Sweden, Lucy Maganga alisema mbali na kutokomeza mila na desturi kandamizi pia washiriki wa kikao hicho watakuwa chachu ya mapambano dhidi ya mimba za utotoni hasa kwa watoto wa shule.
“Kupitia kikao hiki cha ushawishi na utetezi washiriki hawa wa kikao watakuwa mstari wa mbele kuishauri halmashauri ya wilaya kuongeza bajeti ya masuala ya afya ya uzazi ikiwemo miundombinu rafiki shuleni hasa vyoo,maji na vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike”,alisema Maganga.
Kwa upande wake,Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Lucas Mambile alisema tayari halmashauri imeshatenga bajeti kwa mwaka 2019/2020 kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kike shuleni.
Aidha alisema halmashauri inaendelea kushirikiana na jamii kujenga na kujenga vyumba vya watoto wa kike kujistiri. Kwa upande wao,wajumbe wa kikao hicho waliahidi kuendelea kutoa elimu katika jamii ili iondokane na mila na desturi zinazochangia ukatili dhidi ya watoto lakini pia kulea watoto katika maadili mema.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Aisha Omary akizungumza katika kikao hicho na kueleza kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuwa walinzi wa watoto wao na kuwalea katika maadili mema.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumatano Aprili 17,2019 katika shule ya msingi Shingida na kukutanisha pamoja viongozi wa ngazi ya kata,walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari,viongozi wa dini na kimila,wawakilishi wa wanafunzi na wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya idara ya elimu na maendeleo ya jamii.
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana unaotekelezwa na Shirika la Agape kwa ufadhili wa shirika la Sida na nchini Sweden, Lucy Maganga alisema mbali na kutokomeza mila na desturi kandamizi pia washiriki wa kikao hicho watakuwa chachu ya mapambano dhidi ya mimba za utotoni hasa kwa watoto wa shule.
“Kupitia kikao hiki cha ushawishi na utetezi washiriki hawa wa kikao watakuwa mstari wa mbele kuishauri halmashauri ya wilaya kuongeza bajeti ya masuala ya afya ya uzazi ikiwemo miundombinu rafiki shuleni hasa vyoo,maji na vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike”,alisema Maganga.
Kwa upande wake,Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Lucas Mambile alisema tayari halmashauri imeshatenga bajeti kwa mwaka 2019/2020 kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kike shuleni.
Aidha alisema halmashauri inaendelea kushirikiana na jamii kujenga na kujenga vyumba vya watoto wa kike kujistiri. Kwa upande wao,wajumbe wa kikao hicho waliahidi kuendelea kutoa elimu katika jamii ili iondokane na mila na desturi zinazochangia ukatili dhidi ya watoto lakini pia kulea watoto katika maadili mema.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Aisha Omary akizungumza katika kikao hicho na kueleza kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuwa walinzi wa watoto wao na kuwalea katika maadili mema.
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape ACP Lucy Maganga akizungumza wakati wa kikao cha ushawishi na utetezi wa masuala ya afya ya uzazi na ujinsia katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo katika shule ya msingi Shingida- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape ACP Lucy Maganga akizungumza ambapo wajumbe wa kikao hicho watakuwa mabalozi wa kuishauri halmashauri ya wilaya kuongeza bajeti ya masuala ya afya ya uzazi ikiwemo miundombinu rafiki shuleni hasa vyoo,maji na vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike.
Wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Lucy Maganga.
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Lucas Mambile akielezea mikakati iliyopo katika halmashauri katika kusaidia masuala ya afya ya uzazi na ujinsia kwa wanafunzi ambapo alisema wametenga bajeti kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kike shuleni.
Kaimu Ofisa Elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mary Maka akiwaomba viongozi wa kata na walimu kuwa na mawasiliano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa inapobainika watoto wa kike wamepewa ujauzito ili watuhumiwa wakamatwe na kuchukuliwa hatua.
Wajumbe wa kikao wakimsikiliza Lucy Maganga.
Kiongozi wa kimila,Lucas Kiyenze akizungumza katika kikao hicho.
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape ACP Lucy Maganga akiangalia kazi ya kundi la walimu wakuu shule za msingi katika kata ya Usanda wakijadili mikakati mbalimbali ya kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.
Viongozi wa jamii wakiwemo watendaji wa vijiji na maafisa maendeleo ya jamii wakijadili mikakati ya kumaliza mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi.
Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga idara ya elimu na maendeleo ya jamii wakijadili mikakati wanayoendelea nayo kuongeza bajeti ya masuala ya afya ya uzazi na ujinsia ikiwemo miundombinu rafiki shuleni hasa vyoo,maji na vyumba vya kujisitiri kwa watoto wa kike .
Afisa Idara ya Miradi kutoka shirika la Agape Prosper Ndaiga akifuatilia majadiliano ya wawakilishi wa wanafunzi shule za sekondari Shingita na Samuye kuhusu mikakati yao ya kutokomeza mimba kwa watoto wa shule.
Afisa Mtendaji kijiji cha Singita akiwasilisha kazi ya kundi la viongozi wa jamii kuhusu mikakati ya kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.Alizitaja baadhi ya mila hizo kuwa ni 'watoto kuogeshwa dawa ' samba' ili wapendwe, watoto kusindikiza bibi harusi.
Mkuu wa shule ya sekondari Samuye,Jackson Mganga akiwasilisha kazi ya kundi la wakuu wa shule namna walivyoweka mikakati kutokomeza mimba kwa watoto wa shule.
Sheikh Soud Ally wa msikiti wa Usanda akielezea mikakati ya kulea kwenye maadili ya dini watoto ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Mchungaji Lameck Makungu kutoka kanisa la AICT Busanda akielezea namna kanisa linavyotoa elimu kwa watoto ili kuepuka mimba na ndoa za utotoni.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
↧
Wananchi Waonywa wengine wakamatwa baada ya kuishambulia gari ya Serikali Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaonya wananchi wa Kijiji cha Nankanga, Kata ya Nankanga, Wilayani Sumbawanga kuacha tabia ya kuharibu mali za serikali ili kutafuta suluhu ya migogoro iliyopo baina yao na askari wa hifadhi ya Pori la Akiba Uwanda katika bonde la ziwa Rukwa huku akimuagiza kamanda wa polisi Mkoa kuwasaka na kuwakama wote waliohusika na uharibifu huo.
Ametoa maagizo hayo baada ya gari ya hifadhi hiyo kushambuliwa na wavuvi waishio katika kambi ya uvuvi ya Kijiji cha Nankanga kilichopo pembezoni mwa ziwa Rukwa, tukio lililotokea tarehe 10.4.2019 ambapo wavuvi hao walivunja vioo vya gari, kuchomoa tairi pamoja na kuchukua vitu vilivyokuwamo ndani ya gari huku dereva wa gari hiyo kukimbia na kuicha gari hiyo.
Alisisitiza kuwa wananchi hawawezi kufanya uhalifu ili kuhalalisha madai yao na uhalifu haulipwi kwa uhalifu na kuongeza kuwa mahali popote penye uhalifu, sheria huchukua mkondo wake, sio kuanza uharibifu na vitendo vingine vya uvunjifu wa amani mpaka kutishia uhai wa watu hivyo aliwataka wana Nankanga kujitafakari kwa kina na kujitambua.
“Hebu fikiria hiyo gari kama ingechomwa moto na uvunjifu mwingine wa amani mkubwa ungetokea mnadhani mngelala kwenye Kijiji chenu hiki, wengine mngetumbukia kwenye maji, wengine mngepanda mlima bila ya kujua na wengine msingekaa kurudi hapa, kwahiyo mimi ninawaonya na ninawakanya iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho, ninyi kama wanakijiji kuleta uvunjifu wa amani ndani ya Kijiji, msije mkagusa tena mali ya serikali, bahati mbaya sikujua gharama za uharibifu mlioufanya mngechanga Kijiji kizima kulipa huo uharibifu ambao mmeshaufanya,” Alisisitiza.
Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Uwanda Jovine Nachihangu alisema kuwa mgogoro huo ulitokana na askari wa hifadhi hiyo kukamata mitumbwi sita na wavuvi 18 waliokuwa wakivua katika eneo la hifadhi ndani ya ziwa Rukwa ambapo hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilomita za mraba 5000 huku eneo la nchi kavu likiwa na kilomita za mraba 490.
“Wakati nipo Mbeya, nilipokea simu kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kwamba kuna watu wanataka kuvamia kambini kwahiyo nichukue tahadhari, kwahiyo nilianza kuwasiliana na watu waliomo humu kuwa kuna jambo hili na hili linataka kutokea, gari ilipata pancha Kijiji kwasababu tunakawaida ya kumchukua mwenyekiti wa Kijiji ili kuwatambua watu wake lakini muda huo dereva alinipigia simu kunambia hali siyo nzuri na ameiacha gari kijijini, hivyo tuliwasiliana na polisi ili kuomba msaada,” Alieleza.
Wakati akifafanua tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule alisema kuwa mahusiano baina ya wananchi na askari wa hifadhi hiyo sio mazuri lakini kitendo cha wananchi kuvamia gari ya serikali kuipiga mawe na kuiba hakifai na kuongeza kuwa hifadhi hiyo ina mipaka ya muda na mipaka ya kudumu bado infanyiwa tathmini na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala.
“Waziri Kigwangala mwaka jana alikuwa hapa na miongoni mwa matatizo tuliyomueleza ni mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi na wavuvi, nchi kavu huku tunashukuru alama zimewekwa na zimepunguza migogoro iliyopo kati ya wananchi na hifadhi, bado tuna changamoto ya mifugo nae neo la wavuvi bado wavuvi wanaingia hifadhini,” Alisema.
Wakati huo huo Diwani wa Kata ya Nankanga Anyisile Kayuni alisema kuwa tukio lililotokea limetokana na chuki kati ya wavuvi na wahifadhi na kudai kuwa wavuvi wanahisi wanaonewa wakati wahifadhi wanatekeleza majukumu yao ya kisheria.
“Mgogoro huu nimeukuta tangu naingia udiwani umepitia hatu anyingi sana hadi kufikia Waziri Dkt. Kigwangala kuwasimamisha watumishi 27 wa wanayapori lakini mgogorio huu bado haujaisha, Mh. Mkuu wa Mkoa wakazi hawa wa Nankanga wamepungua idadi uliyoikuta wakati ule wa masika sio hii asilimia kubwa wamekimbilia forodha ya masuche jirani hapo (wilaya ya) Momba (Mkoani Songwe) wakitokea mwalo huu hapa,” Alieleza.
Katika hatua nyingine Mh. Wangabo aliwatahadharisha askari wa wanayamapori kutotumia sheria vibaya na hatimae kuwaonea wananchi kwa kuwapiga bila ya mpangilio na huku akiwataka wananchi hao kuhakikisha wanatii sheria na inapotokea wanakiuka sheria hizo basi waache ubishi wakati wanapokamatwa.
Katika kipindi cha mwezi Novemba mwaka 2018 hadi Machi 2019, Wanyama walioonekana katika pori hilo la Akiba la Uwanda lililopo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Wanyama walioonekana ni Nyati, Swala, Fisi na Tembo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (katikati) akitoa maelekezo kwa meneja wa pori la Akiba la Uwanda Jovine Nachihangu (kulia) juu ya kuhakikisha alama zinazowekwa kwenye mipaka ya hifadhi hiyo inakuwa na maandishi yanayoosomeka kuwa unaingia katika hifadhi ili kupunguza migogoro na wananchi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt Khalfan Haule.
↧
↧
WATUMISHI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WATAKIWA KUBORESHA ZAIDI MIFUMO YA UKUSANYAJI MAPATO YA SERIKALI
Na Farida Ramadhani & Josephine Majura. WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji , amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya ndani na kupanua wigo wa walipakodi pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, wizarani hapo.
Alisema Wizara ya Fedha na Mipango imebeba majukumu ya kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali na matumizi ya rasilimali fedha yanasimamiwa kikamilifu.
“Watendaji na watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha na ufuatiliaji wa matumizi ili kuhakikisha rasilimali fedha zilizopo zinatumika kwa ufanisi” ,alisema Dkt. Kijaji.
Alisema ni jukumu la Watumishi wa Wizara kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016-2021) wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu.
Aliwataka Watumishi kufanyakazi kwa ushirikiano, umoja , mshikamano, ufanisi na uadilifu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyopo.
“Ni wajibu wetu pia kutumia busara na hekima, hususan pale tunaposhughulikia maslahi ya watumishi na wananchi kwa ujumla”, alisisitiza Dkt. Kijaji.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Doto James, amemhakikishia Dkt. Kijaji kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa haraka na ukamilifu kwa maendeleo ya nchi kwa kuwa Wizara hiyo ni nguzo ya kusimamia uchumi wa nchi.
Alisema uzoefu unaonesha kwamba vikao vya Baraza la wafanyakazi vimekua na umuhimu mkubwa mahala pa kazi na kwa kuzingatia umuhimu huo Wizara ya Fedha na Mipango imehakikisha kuwa vikao vya Baraza vinafanyika kila mwaka kulingana na Mkataba kati ya Wizara na Chama cha Wafanyakazi cha Serikali na Afya (TUGHE).
Alisema kupitia Baraza la wafanyakazi Wizara imefanikiwa kuongeza mshikamano kati ya Wafanyakazi hivyo kuamsha ari kwa watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali.
Aliongeza kuwa hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwenye Baraza zimeboresha huduma kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia watumishi vitendea kazi pamoja na kuwelimisha watumishi kuhusu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu (BP), Kifua kikuu, HIV na UKIMWI.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Doto James akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma .
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (watatu kushoto) wakiimba wimbo wa kudumisha umoja kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma .
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa kudumisha umoja na mshikamano "solidarity forever" kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kushoto) akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aliyeteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuapishwa hivi karibuni , Adolf Ndunguru, katika Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo , Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Doto James akitoa salam za utangulizi kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe walioshiriki Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), katika ukumbi wa Kambarage Dodoma ambapo Watendaji wa Wizara walitakiwa kutekeleza jukumu la kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akizungumza wakati wa kufungua Baraza la Wafanyakazi, Jijini Dodoma, ambapo aliagiza Watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya kukusanya mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa walipa kodi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akipongezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, baada ya kumaliza hotuba yake alipofungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
Meza Kuu (waliyokaa) ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),(watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasilino Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
↧
Chelsea na Arsenal washindwe wenyewe tu kwenye UEFA Europa League leo
Chelsea na Arsenal wanaingia katika michezo ya leo wakiwa na matarajio makubwa ya kufuzu kuingia nusu fainali. Arsenal walishinda 2-0 nyumbani kwao dhidi ya Napoli katika mchezo wa kwanza, huku Chelsea wakishinda ugenini dhidi ya Slavia Prague kwa bao 1-0.
Hata hivyo Chelsea walifungwa 2-0 ugenini kwa Liverpool na wako hatarini kumaliza msimu nje ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, hii inawaongezea sababu zaidi za kupambana ili kushinda taji la Europa.
Mshindi wa Europa hupata tiketi ya moja kwa moja kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya na kwa kusema ukweli hapo ndipo Chelsea na Arsenal wanatamani kucheza.
Naye mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Chelsea alisema kwamba mchezo wao dhidi ya Slavia Prague ndio mchezo mgumu zaidi ambao wamecheza katika Europa msimu huu. “Watajitahidi kufanya kila kitu ili kufuzu hatua inayofata. Tunajua kiwango chao, kwa hiyo tutajitahidi kumaliza kazi kwenye uwanja wetu”. Alisema
Mchezo wa Chelsea dhidi ya Slavia Prague utarushwa LIVE kupitia ST Sports Premium pekee, saa 4:00 Usiku. Arsenal wanasafiri hadi Italia siku nne tu baada ya kucheza na Watford kwenye ligi na iko wazi kwamba wachezaji wengi hawatacheza kwenye mechi zote mbili kutokana na uchovu na kuepuka majeruhi.
‘Gunners’ walilalamikiwa na mshambukiaji wao wa zamani Paul Mariner, ambaye alisema Arsenal walipoteza nafasi nyingi sana kwenye mchezo wa kwanza. “Cha msingi ni ilikuwa ni kumaliza kabisa mchezo. Walikuwa na nafasi ya kufanya hivyo nyumbani.
“Sijali wanakwenda wapi, 2-0 kwenye mechi za Ulaya bado mechi haijaisha. Kwa sababu lolote linaweza kutokea, hujui kama mwamuzi atafanya maamuzi sahihi au la, au wachezaji wanaweza wasicheze vizuri,” aliwaambia waandishi. Mchezo wa Napoli dhidi ya Arsenal utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee, saa 4:00 Usiku.
Kwenye michezo mingine, Valencia walimaliza nusu ya kazi tayari baada ya kushinda ugenini kwa Villarreal 3-1 na sasa wanaweza kufuzu hata wakipoteza mchezo wa nyumbani kwa magoli machache dhidi ya wenzao wa La Liga.
Mchezo mwingine ni Eintracht Frankfurt dhidi ya Benfica Lisbon, huu bado uko wazi kwa timu zote, japokuwa wareno hao walifunga mabao manne, waliruhusu magoli mawili nyumbani pia.
Hii inawapa moyo Frankfurt na matumaini ya kufuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1979/80, walipowafunga Borussia Moenchengladbadch kwa bao la ugenini kwenye robo fainali ya wajerumani (kipindi hicho Europa ilijulikana kama UEFA Cup).
Hakikisha hupitwi na mchezo wowote – angalia kupitia StarTimes pekee, katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa zaidi kwa kulipia Tsh 18,000 tu kwa watumiaji wa Antenna.
↧
Ujio wa Sevilla Fc ni fursa ya kukuza Michezo na Kuitangaza nchi: Shonza
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amesema kuwa ujio wa timu ya Sevilla Fc kutoka Laliga nchini Hispania ni fursa kubwa ya kukuza na kuendeleza michezo hapa nchini.
Naibu Waziri ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati Kampuni ya SportPesa ilipotangaza ujio wa Klabu hiyo kubwa inayoshiriki ligi ya Laliga ikiwa nafasi ya tano ambayo inatarajiwa kuja nchini Mei 21 kucheza na mojawapo ya timu kubwa inayoshiriki ligi Kuu hapa nchini.
“Ujio wa Sevvila Fc ni fursa kubwa sana kwa nchi yetu kwani itasaidia kutangaza na kuinua wachezaji na ligi yetu Ulimwenguni kote,”alisema Shonza.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kingwangalla ameeleza kuwa ujio wa timu hiyo utachangia kutangaza utalii wa nchi yetu na ameahidi kuipeleka kutembelea moja ya hifadhi pamoja na kisiwa cha Zanzibar.
Kwa upande wake Mkurugenzi na Mdhibiti wa Kampuni ya SportPesa Bw. Abbas Tarimba amesema Kampuni yake inaendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza michezo ikiwa ni pamoja na kuleta timu kubwa Duniani ambazo zinatangaza soka la hapa nchini.
“Sevilla inakuja kucheza hapa nchini na timu ya Yanga au Simba ambazo zinatengenezewa mfumo maalum wa kupatikana timu mojawapo kati ya hizo mechi itakayochezwa mnamo Mei 2019”, alisema Bw.Tarimba.
Vilevile Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw.Wilfred Kidau ameeleza kuwa maandalizi ya kuipokea timu hiyo yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kusajili Mechi hiyo ya kimataifa katika Shirikisho la mpira wa miguu Duniani.
Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza akizungumza na Waandishi wa Habari Aprili 17, 2019 Jijini Dodoma kuhusu ujio wa Klabu ya Sevilla Fc kutoka Laliga unaoratibiwa na Kampuni ya SportPesa ambayo itacheza na timu ya Yanga au Simba Mei 23,2019.Kulia ni Mdhibiti na Utawala wa Kampuni hiyo Bw.Abbas Tarimba.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kingwangalla (mwenye suti ya kijivu) pamoja na Viongozi wa Kampuni ya SportPesa baada ya mkutano na waandishi wa Waandishi wa Habari Aprili 17, 2019 Jijini Dodoma kuhusu ujio wa Klabu ya Sevilla Fc kutoka Laliga unaoratibiwa na Kampuni hiyo ambayo itacheza na timu ya Yanga au Simba Mei 23,2019.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw.Nicholas William.
↧
ATAPE KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA MAJI, UJENZI WA HOSTELI SIMIYU
Na Stella Kalinga, Simiyu
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE), kinakusudia kuwekeza katika ujenzi wa mradi wa maji kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi na ujenzi wa hosteli ili kutoa huduma za malazi katika Mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Freddie Manento, Aprili 17, 2019 wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi, ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho kwa takribani siku saba ambao umeanza Aprili 16 na utahitimishwa Aprili 21, 2019.
Manento amesema ATAPE imedhamiria kuwekeza kwenye miradi itakayokuwa na tija kwa Watanzania wote kwa ujumla huku akieleza kuwa timu ya wataalam wa uwekezaji wa chama hicho inaendelea kufanya utafiti, ili kubaini eneo litakalofaa kuchimba kisima cha maji na kujenga hosteli mkoani Simiyu. “Tumedhamiria kuacha alama katika Mkoa wa Simiyu kupitia mkutano wetu wa 20 wa ATAPE, tumepewa fursa ya kiwanja kwa ajili ya kujenga hosteli katika kukabiliana na changamoto ya malazi, lakini pia wataalam wetu wanaendelea na utafiti kubaini mahali tutakapochimba kisima kwa ajili ya huduma ya maji kwa Wanasimiyu” alisema Manento
Pamoja na miradi hiyo inayotarajiwa kutekelezwa mkoani Simiyu, Manento amesema ATAPE imewekeza katika kilimo kwenye mashamba ya miti, miwa, mikorosho, miti ya maparachichi ambayo kwa ujumla yana ukubwa wa ekari 10,000 na ekari zaidi 3500 ambazo zinatarajiwa kufanyiwa uwekezaji mwingine.
Amesema hadi sasa ni takribani shilingi bilioni 1.039 imewekezwa katika miradi hiyo ambayo pia imechangia kutoa ajira za kudumu na za msimu kwa Watanzania walio katika maeneo yenye miradi hiyo, huku akibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo hayo ATAPE imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii husika.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa ATAPE ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu hususani Bariadi kutumia mkutano huo kama fursa kiuchumi kupitia biashara ya bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo usafiri wa kuwatoa na kuwapeleka wajumbe katika eneo la mkutano
Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu wamesema Mkutano wa ATAPE umekuwa fursa kwao kwa kuwa utawasaidia kujiingizia kipato na kupata ujuzi mpya kupitia huduma na bidhaa zitakazouzwa kwenye mkutano huo.
“ Binafsi ninashukuru uwepo wa mkutano huu, mimi kama mjasiriamali nimepata pesa, nimepata ujuzi mpya kutoka kwa wenzetu waliotoka nje ya Simiyu, hivyo ninaendelea kuwaomba viongozi wetu waendelee kutuletea matukio kama haya ili tupate pesa zaidi” alisema Bw. John Bubinza mjasiriamali kutoka Bariadi.
Nao wajasirimali wanaoshiriki katika mkutano huo kutoka nje ya mkoa wa Simiyu wametoa wito kwa Wananchi mkoani Simiyu kufika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kusekwa Memorial kujifunza na kujionea kazi mbalimbali za ujasirimali ili waweze kupata ujuzi na maarifa mapya ya kufanya kazi za ujasiriamali kwa ufanisi na kununua bidhaa mbalimbali.
“ Binafsi nawakaribisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufika katika viwanja hivi waje wajionee, wakifika hapa watapata bidhaa kwa bei za jumla na rejareja, laikini pia nawasisitiza wanawake wainuke waje waone maana ujasiriamali unatuinua sana wanawake” alisema Mjasiriamali Esther Jichogo kutoka Jijini Dar es salaam.
Wanachama zaidi ya 1500 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE) wanaendelea na mkutano wao wa 20 mkoani Simiyu, ukiwa na Kauli mbiu “KUSONGA MBELE NA MUNGU” ambao utachukua takribani siku saba kuanzia tarehe 16/04/2019 hadi 21/04/2019.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Freddie Manento akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, ukanda wa AfrikaMashariki na Kati(nchi 11), Mchungaji Emanuel Pelote akizungumza na Wanachama wa Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya Wanachama wa Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) wakiwa katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano mkuu wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), wakiwa katika vipindi maalum vinavyoendelea katika Mkutano wa Chama hicho unaofanyika katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019. PICHA 5:-Baadhi ya wananchi wakinunua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali ambao ni Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho unaofanyika Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Jusline Gilbert mkazi wa Bariadi akaingalia baadhi ya bidhaa za Wajasiriamali ambao ni Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkuu wa Chama hicho Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya mabanda ya watoa huduma mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unaofanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019.
Baadhi ya mabanda ya watoa huduma mbalimbali katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi ambako unafanyika Mkutano mkubwa wa hicho unaofanyika Mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE), Mkoani Simiyu kuanzia Aprili 16 hadi Aprili 21, 2019
↧
↧
Wawili wakamatwa, mmoja afutiwa mkataba ujenzi wa hospitali ya Wilaya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kusitisha mkataba na fundi anayehusika na ujenzi wa jengo la maabara katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kalambo huku akimtaka Mkurugenzi huyo kutafuta chumba katika eneo hilo ili asimamie kwa karibu ujenzi unaoendelea na kuhakikisha unaisha kwa wakati.
Ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo hivi karibuni baada ya kuitaka mikoa yote kusimamia ujenzi wa hospitali za wilaya na kufikia tarehe 13 hadi 25 Mei, 2019 majengo yote yawe yameshapauliwa na mikoa hiyo kutuma picha za majengo saba ya hospitali hizo.
Kwa kutekeleza hayo Wangabo amewaagiza mafundi wote wanaosimamia ujenzi wa majengo hayo saba kuhakikisha wanafikia usawa wa linta ifikapo tarehe 10 mwezi Mei mwaka huu na hatimae kumalizika kwa wakati.
Wangabo ameyasema hayo alipotembelea eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kalambo na kukutana na wataalamu wa halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Msongela Palela pamoja na mafundi waliopewa mkataba kwaajili ya ujenzi wa hospitali.
Baada ya kutembelea alisema kuwa hakuridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali hiyo ya Wilaya ya Kalambo kwakua kasi ni ndogo pamoja na kujua kuwa kulikuwa na changamoto nyingi hasa kipindi cha mvua ambapo barabara zilikuwa hazipitiki hivyo vifaa mbalimbali kushindwa kufika kwenye eneo la ujenzi na kutahadharisha kuwa sasa mvua zimeisha hivyo hakuna sababu ya kuendelea na kasi ile iliyokuwepo.
“Lakini pia nimegundua kuwa kuna wajenzi wengine hata ‘saiti’ hawapo na ujenzi wa majengo yao unasuasua, sasa yule mjenzi wa maabara kule Mkurugenzi sitisha mkataba wake mara moja na utafute mjenzi mwengine ambaye ataleta mafundi wengi na hili jambo lichukue muda mfupi iwezekanavyo ili tarehe 10 mwezi Mei majengo yote haya saba yawe yamefika kwenye hatua ya linta na sio vinginevyo,” alisisitiza.
Halikadhalika, alisikiliza kilio cha vibarua wanaoendelea na ujenzi wa majengo ya hospitali hiyo na kugundua kuwa kuna kusuasua kwa malipo ya vibarua hao na hivyo kumuagiza Kamanda wa polisi wa Wilaya hiyo kuwakamata fundi anayehusika na ujenzi wa jengo la utawala Fadhili Salum pamoja na msaidizi wake Amir Rajabu kwa kushindwa kuwalipa vibarua wao tangu ujenzi huo uanze mwanzoni mwaka huu na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufuatilia malipo ya vibarua hao kwa karibu ili wasiharibu kazi.
Serikali imetoa jumla ya Shilingi bilioni 105 kwa wilaya 67 kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa hospitali za wilaya ambapo kila Wilaya ilipewa Shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi wa majengo saba ya hospitali hizo ambapo mwisho wa ujenzi huo na majengo hayo kuanza kutumika ni tarehe 30 June, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (wa mbele) alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa majengo saba ya hospitali ya Wilaya ya Kalambo iliyopo Matai mjini ambapo ndio makao makuu ya wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (mwenye rainboot za kijani) akitoa maagizo kwa timu ya wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Msongela Palela (kulia) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo Julieth Binyura (kushoto).
Jengo la Mionzi (X - Ray) linaloendelea kujengwa katika hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
Sehemu ya Jengo la Wodi ya akinamama ikiendelea kujengwa katika hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
Jengo la Utawala la hopitali ya Wilaya ya Kalmbo likiendelea kujengwa.
↧
Mbunge wa Goodluck Ulanga Mlinga aomba dawa za kifafa jimboni kwake
↧
BODI YA URATIBU WA NGOs YAFUTA USAJILI WA MASHIRIKA SITA
* Mashirika matatu yaenda kinyume na maadili na utamaduni wa Nchi.
* Mengine matatu yaomba kufutwa kwa kukiri kukiuka Katiba zake.
Kikao cha 40 wa Bodi ya Nne ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kimeyafutia usajili Mashirika 6 Yasiyo ya Kiserikali kufanya kazi na kutoa huduma zake hapa nchini kufuatia kukiuka Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali lakini pia kufanya kazi kinyume na Katiba zao kama zilivyowasilishwa kwa Msajili wa Mashirika hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa Bodi ya Uratibu wa NGOs jijini Dodoma Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya ripoti ya uchunguzi wa Mashirika hayo kuwasilishwa katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 17 Aprili, 2019.
Ameyataja Mashirika yaliyofutwa kwa kutozingatia Sheria, Kanuni, taratibu na maadili ya nchini kuwa ni Shirika la Community Health Education Services & Advocacy (CHESA), Kazi Busara na Hekima (KBH Sisters), AHA Development Organization Tanzania, Pathfinder Green City, Hope and Others na HAMASA Poverty Reduction(HAPORE).
Aidha Mwanga alifafanua kuwa Mashirika ya Community Health Education Services & Advocacy (CHESA), Kazi Busara na Hekima (KBH Sisters), pamoja na AHA Development Organisation Tanzania yamefutiwa usajili kutokana na kosa la kukikuka Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali pamoja na Katiba iliyowasilishwa katika Ofisi ya Msajili kwa kuhamasisha matendo yasiyofaa katika jamii mambo ambayo ni ukiukaji wa Sheria, maadili na utamaduni wa Tanzania.
Aidha Mwanga aliongeza kuwa Mashirika ya Pathfinder Green City, Hamasa Poverty Reduction (HAPORE) na Shirika la Hope and Others yenyewe yaliomba kujitoa kwenye Orodha ya Msajili baada ya kutuhumiwa kuendesha kazi zao kinyume na Katiba zake na hivyo Bodi ilielekeza Mashirika hayo kufutwa kwenye daftari la usajili.
Aidha, Msajili amefafanua kuwa ufutwaji wa Mashirika hayo umefanywa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1) (c) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 inayosema kuwa pale Msajili wa Mashirika hayo atakapopokea tuhuma kuhusu Shirika au Mashirika yanayofanya kazi zake pasipo kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za nchini Msajili hupeleka notisi au onyo kwa Shirika husika kujiteteta kabla ya kufikia maamuzi ya kufutiwa usajili.
Msajili ameongeza kuwa endapo Ofisi ya Msajili isiporidhika na utetezi wa Shirika au Mashirika yanayotuhumiwa kukiuka Sheria, Kanuni na taratibu itapeleka mashauri hayo katika Kikao cha Bodi ya Uratibu wa Mashirika hayo na hao ndio wenye Mamlaka ya kutoa idhini ya kufutwa au kutofutwa kwa Shirika.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Nne ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Dkt. Faustine Sambaiga amesema kuwa wameielekeza Sekretarieti kuyafutia usajili Mashirika yote Yasiyo ya Kiserikali ambayo yamekuwa hayafuati Sheria, Kanuni na taratibu za nchini ili kukidhi matakwa ya kisheria.
“ Kama Bodi tunamuagiza Msajili kuyafutia usajili Mashirika hayo kwani Bodi ndio yenye Mamlaka ya kutoa idhini kwa Msajili wa NGOs kuyafuta Mashirika au kutoyafuta” alisisitiza Dkt Sambaiga.
Mwenyekiti huyo wa Bodi ameyasisitiza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za nchi na kuzingatia uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuchochea Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Hatua hii ya kuyafutia usajili Mashirika sita Yasiyo ya Kiserikali Nchini imekuja mara baada ya kuundwa kwa Bodi ya Nne ya Uratibu wa Mashirika hayo chini ya uwenyekiti wa Dkt. Faustine Sambaiga aliyeteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni kuongoza Bodi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nne ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Dkt. Faustine Sambaiga (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Bodi wakati wa kikao cha 40 cha Bodi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kulia ni Kaimu Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Neema Mwanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akizungumza na Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Nne ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Dkt. Faustine Sambaiga (kulia) mara baada ya kikao cha 40 cha Bodi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma wa pili kushoto ni Kaimu Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Neema Mwanga na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Usajili Bw. Leornard Baraka. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
↧
ZANTEL YAPATA VYETI VYA KIMATAIFA VYA ISO VYA MAZINGIRA, AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI
Kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imepata vyeti 2 vya ubora wa kimataifa (ISO), kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa katika kutekeleza kwa ufasaha kuendesha biashara zake kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira (ISO 14001:25),na cheti kipya cha utekelezaji wa mifumo ya Afya na Usalama mahali pa kazi (ISO 45001:2018).
Mafanikio haya ni mwendelezo, mwaka jana mwishoni baada ya kufanyiwa ukaguzi ilipata cheti cha kimataifa cha ISO kutokana na kukidhi vigezo vya utekelezaji mifumo ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kwa ufasaha (OHSA 18001:2007).
Kutokana na ukaguzi huo, ilibainika inatekeleza vizuri mifumo ya Afya na Usalama, wakaguzi walipendekeza ZANTEL ibadilike kutoka cheti cha zamani cha OHSA 18001:2007 na kupatiwa cheti kipya cha ISO ambacho kimeanza kutolewa kwa makampuni yanayokidhi vigezo mwaka jana.
Akiongelea mafanikio haya ya kampuni kupata vyeti vya kimataifa vya ISO,Mkuu wa kitengo cha Teknolojia Mawasiliano wa Zantel,John Sicilima alisema “Tunayo furaha kukidhi viwango vya ukaguzi na kupewa vyeti vya ubora vya kimataifa.Hatua hii inadhihirisha umakini wetu tunavyozingatia suala la afya na Usalama kuanzia kwa wafanya kazi ,wadau mbalimbali tunaoshirikiana nao na katika mazingira tunayofanyia shughuli zetu,kama malengo yetu tuliojiwekea mojawapo ni kuendesha shughuli zetu tukiwajibika kulinda usalama wa jamii katika maeneo tunayofanyia biashara sambamba na kuongeza hadhi ya kampuni yetu”.
Alisema baada ya kupata vyeti vya kimataifa vya ISO, Zantel itahakikisha inafanikisha dhamira yake katika maeneo ya afya na tahadhari katika usalama, athari za mazingira, Kutekeleza kanuni za usalama kwa vitendo, mifumo ya uharibifu wa mazingira wa sauti na kuhakikisha tahadhari zaidi na athari zinadhibitiwa ipasavyo.
“Utekelezaji wa maelekezo yanayoendana na vyeti hivi yatawezesha taswira ya Zantel kuwa nzuri zaidi, kuongeza uhusiano mzuri na jamii na kupanua wigo wa masoko ya biashara zetu na wadau wengine,” aliongeza Sicilima. Cheti cha kimataifa cha ubora cha ISO 45001 taasisi yenye kuwa nacho, inapaswa kuwa inatekeleza mifumo ya Afya na Usalama kwa ufasaha, lengo kuu likiwa ni kulinda Afya na usalama kwa wafanyakazi na watu wengine.
Utoaji wa cheti kipya cha ISO 45001, umeanza mwezi Machi mwaka 2018, kuhakikisha kanuni za Afya na Usalama zinapewa kipaumbele duniani kote. Taasisi ya Kimataifa ya Kusimamia Ubora (ISO) imelenga kuhakikisha matukio ya ajali na magonjwa yatokanayo na shughuli za kazi yanapungua sambamba na kuwezesha umri wa kuishi kuogezeka. Kutokana na kuanza kutolewa kwa cheti cha ubora cha kimataifa cha ISO 45001, taasisi ambazo zilikuwa katika mfumo wa cheti cha zamani cha ISO ikiwa ni pamoja na cheti cha OHSAS 18001 yanapaswa kubadilika na kupata cheti kipya kabla ya kufikia mwezi Machi mwaka 2021.
↧
↧
Wizara ya Habari yawasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2019/20
Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2019/20.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akimpongeza Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe baada ya kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2019/20.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakifuatilia hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2019/20 bungeni leo mjini Dodoma. Picha na Kelvin Kanje-MAELEZO
↧
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWEKA WAZI MPANGO MKAKATI WAKE KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA
Katika kuelekea sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga kikamilifu kuhakikisha wakazi wa Mkoa wa Mbeya, wageni na wakazi wa mikoa jirani wanasherehekea sikukuu hii kwa amani na utulivu.
Kwa kutambua kuwa Mkoa wetu unapakana na nchi jirani ya Malawi pia barabara kuu inayounganisha nchi yetu na nchi jirani pamoja na mikoa jirani imepita hapa, tumejipanga vizuri kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara wakiwemo madereva na watembea kwa miguu.
Wito wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ni kwa watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Sambamba na hilo, tumejipanga vizuri kuhakikisha maeneo yeto tete kama vile Mlima Nyoka, Mlima Iwambi, Mlima Igawilo na Mwansekwa ulinzi na usalama umeimarishwa katika kipindi chote cha sikukuu ya Pasaka kama ilivyo kwa siku nyingine.
Kuelekea kipindi hiki cha sikukuu, waumini wa madhehebu ya Kikristu ushiriki katika ibada/misa kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba zao, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama katika makanisa hasa katika misa au ibada za mkesha.
Aidha tunatoa wito kwa viongozi katika makanisa kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri hasa katika suala la ulinzi kwa kuzitumia kamati za ulinzi na usalama ili kuhakikisha ulinzi katika maeneo ya ndani na nje ya makanisa hasa sehemu za maegesho ya magari panakuwa salama kabisa.
Pia tunatoa rai kwa wamiliki wa kumbi za starehe kufuata sheria hasa kuzingatia leseni zao za biashara zinavyowaelekeza ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda wa kufungua na kufunga sehemu zao za biashara, wenye kumbi za muziki kuhakikisha kumbi zao zinaingiza idadi ya watu inayohitajika [capacity] pamoja na kuweka walinzi katika maeneo yanayowazunguka.
Kuelekea msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, ni wito wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi na usalama wa mtoto, pia kuwasaidia watoto kuwavusha katika maeneo tete kama vile barabara au maeneo yenye mito ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata.
Pia ili kuepuka watoto kupotea katika kipindi hiki, wazazi na walezi wanapaswa kuongeza umakini, uangalizi kwa watoto wao kila mahali wanapokwenda iwe ni makanisani, misikitini au katika maeneo yenye michezo ya watoto.
Pia tunasitiza ulinzi na usalama katika makazi yetu, kuhakikisha kwa wale wanaotoka kwenda katika misa au ibada za mkesha kuacha waangalizi pia kuhakikisha tunajilinda kwa kufunga milango na madirisha ili kuepuka uhalifu katika nyumba zetu.
Aidha tunasisitiza utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia namba za simu za viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo:-
RPC…………………………………………………………….0715 009 931
RCO [Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa]………0658 376 052
STAFF OFFICER [Msaidizi wa RPC]………………….……0658 376 006
OPERATION OFFICER [Mkuu wa Operesheni Mkoa]..…..0754 466 924
RTO [Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa]……0658 376 472
OC FFU [Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia]……..…….0658 376 009
OCD MBEYA………………………………………………….0659 884 996
OCD MBALIZI………………………………………………..0655 248 381
OCD CHUNYA………………………………………………..0782 746 543
OCD MBARALI……………………………………………....0659 885 948
OCD RUNGWE……………………………………………….0659 885 253
OCD KYELA………………………………………………….0659 887 919
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
↧
INTRODUCING NO MORE FEAR OFFICIAL MUSIC VIDEO BY RITHA KOMBA
↧
More Pages to Explore .....