Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji mstaafu Dkt. Steven James Bwana (kulia) akizungumza katika mahojiano maalum na bwana Rutengano Haonga wa TBC 1 (kushoto) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na PO PSC)
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji mstaafu Dkt. Steven James Bwana (kulia) akiteta jambo na bwana Rutengano Haonga wa TBC 1 (katikati) jijini Dar es Salaam . (Picha na PO PSC)

Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea wa Kimarekani la Peace Corps lawaapisha Wafanyakazi wa Kujitolea 59 wa sekta za Afya na Kilimo

0
0
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson ameongoza hafla ya kuapishwa kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps wapatao 59 watakaohudumu nchini Tanzania kwa miaka miwili katika sekta za Afya na Kilimo. Wafanyakazi hawa watapangiwa kufanyakazi katika wilaya 35 nchini kote Tanzania.

Kaimu Balozi Patterson aliongoza kiapo rasmi cha wafanyakazi hao wapya wa kujitolea mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara.  Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi wa serikali, wafanyakazi wa kujitolea wa zamani wa Peace Corps, wawakilishi wa taasisi wabia na wanafamilia wa familia za Kitanzania ambazo wafanyakazi hawa wa kujitolewa waliishi nazo.

Kaimu Balozi Patterson aliwaeleza wafanyakazi wapya wa kujitolea kuwa: “Kupitia programu hii mtaweza kuleta mabadiliko kwa Watanzania mtakaofanya nao kazi n ahata kwenu ninyi wenyewe.Wakati ambapo ninyi mnaweza kuwa Wamarekani wa kwanza kukutana na kufanya kazi na wafanyakazi wenzenu na majirani zenu wa Kitanzania, ni dhahiri kwamba katika mawazo yao mtaendelea kuwa wawakilishi wa watu wa Marekani na ubia wa muda mrefu kati ya Wamarekani na Watanzania.”

Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa zaidi ya miaka 50, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao, Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea,kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.

Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolewa wa Peace Corps 3000 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1961. Peace Corps hutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wenye utaalamu katika nyanja mbalimbali ambao hupangiwa kufanyakazi katika jamii wakifundisha katika shule za sekondari (hisabati, sayansi na Kiingereza), wakitoa elimu ya afya na utunzaji wa mazingira.



Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson akiwaapisha wafanyakazi wapya wa kujitolea wa Peace Corps 59 ili kuanza utumishi wao wa miaka miwili nchini Tanzania katika hafla imeyofanyika tarehe 17 Aprili 2019 katika ukumbi wa CCT Kilakala Morogoro. Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa Kimarekani watakao pangiwa kuhudumu katika wilaya 35 nchini, watafanyakazi na jamii katika sekta za afya na kilimo. Hafla ya kuapishwa kwao ilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara, Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania Dk. Nelson Cronyn, wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps waliohudumu hapo zamani pamoja na maafisa kutoka mashirika mengine yanayojihusisha na wafanyakazi wa kujitolea. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson wakiwa kwenye picha ya pamoja Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania Dk. Nelson Cronyn na wafanyakazi wapya wa kujitolea wa Peace Corps 59 wa miaka miwili nchini Tanzania hafla hii imemefanyika tarehe 17 Aprili 2019 katika ukumbi wa CCT Kilakala Morogoro.

KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA IMEZINDULIWA MKOANI ARUSHA

0
0

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama umefanyika mkoani Arusha ikiwa na lengo la ''Kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi'' na kuhakikisha mama na mtoto wanakuwa salama kabla na baada ya kujifungua.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa watendaji wote wa wizara ya afya ngazi ya mkoa watende kazi kwa weledi ili waweze kupunguza vifo vya wakina mama wakati wa kujifungua ambapo kwa ngazi ya mkoa ni 40%na Kitaifa ni 28%

Kampeni hiyo iliyobeba Kauli mbiu isemayo''Jiongeze Tuwavushe Salama''na Maudhui yasemayo '' Kila mmoja wetu anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi, maneno basi, sasa vitendo''

Amesema kuwa kampeni hiyo ni ya muhimu kwani inakwenda sambamba na lishe kwa mama mjamzito ili aweze kujifungua salama na mtoto atakayezaliwa awe mwenye afya njema,''Mwanaume ni wajibu wako kutambua kuwa mwanamke anapokuwa mjamzito ndio wakati wako wa kuwa karibu na mkeo, msindikize Kliniki, pimeni afya pamoja leeni mimba pamoja na mtoto akizaliwa mtamfurahia''. Alisema Gambo.

Ameainisha sababu kuu ambazo zinasababisha vifo kwa akina mama wajawazito ni pamoja na mama kutohudhuria kliniki mapema,kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua na baada ,shinikizo la damu.Amesema lishe duni imekuwa sababu kubwa ya wakina mama kujifungua watoto njiti ambapo pia vifo vya watoto hao ni 25 kati ya kila vizazi hai 1000husababishwa na kushindwa kupumua na wengine kuzaliwa kabla ya wakati.

Kwa upande wake Daktari mkuu wa mkoa Wedson Sichalwe amesema Tafiti zilizofanyika mwaka 2015/2016 zinaonyesha kiwango cha vifo vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na vifo 11,000 kila mwaka,sawa na wanawake 30 hufariki kila siku, kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi.

Dkt. Sichalwe ameainisha kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni ukosefu wa dawa lishe,ukosefu wa virutubisho ambavyo hupelekea matatizo kwa mtoto akiwa tumboni hata kuzaliwa njiti au akiwa amefariki.Dkt amesema hiyo changamoto ya lishe katika mkoa imesababisha watoto wengine kuzaliwa wakiwa na udumavu halo inayopelekewa kuja kuwa na taifa lenye watoto wengi wenye tatizo hilo endapo hatua za haraka hazitachikiliwa.

Baadhi ya washiriki na wadau wa afya akiwemo Dkt. Emmanuel Maeda amesema swala la elimu kwa jamii ni changamoto hivyo wao wamekuja na kitu kiitwacho Vunja ukimya kwaajili ya kumkumbusha mwanaume kutambua wajibu wake pale mke anapokuwa mjamzito.

'' Mwanamke anapokuwa mjamzito inamuhitaji mwanaume kuelewa, anapaswa atambue mama mjamzito anahitaji lishe bora ili ajifungue salama, ikiwa kwenda pamoja kliniki na kutambua changamoto anazopitia na siyo wao kukaa pembeni na kusema kwani mimi ndo nimebeba mimba''alisema Dkt. Maeda.

Nae Munga kutoka Japayco nae alishauri kuwa kuwepo na siku ya afya vijijini ina lazima juhudi ziongezwe kuhakikisha kuangalia zaidi mama na kichanga anavuka salama na kila mjamzito lazima aende kliniki na hospitali kujifungua.

Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan 6Novemba 2018 mkoani Dodoma. ampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama inatekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo UNICEF.
 Baadhi ya washiriki na wadau wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama wakiwa katika uzinduzi huo
Katibu Tawala wa Jiji la Arusha Richard Kwitega akizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa Jijini Arusha.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akibadilishana jambo na Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe kwenye Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama

Asasi ya LSF yateuaOfisaMkurugenziMkuumpya

0
0
Shirika la Legal Services Facility (LSF) jane limetangaza rasmi uteuzi wa Bi Lulu Ng’wanakilala kama Ofisa Mkurugenzi Mkuu mpya. Katika kutekeleza kazi hii, anachukua nafasi ya Bw Kees Groenendijk, ambaye ameongoza asasi hii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011.

Bi Ng’wanakilala, ambayeana Shahada ya Pili katika Sheriaya Kimataifa na Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Livraserpool nchini Uingereza na Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, amedhamiria kufanya mabadiliko ya kitaasisi lengo kuu likiwa ni kuifanya LSF kupanua wigo utoaji wa msaada wa kisheria kwa mamilioni ya wanaume na wanawake maskini Tanzania wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.

Anachukua uongozi wa asasi isiyo ya kiserikali ambayo imewezesha uwepo wa wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar, wanaotao msaada wa kisheria kwa watanzania wenye matatizo ya kisheria na kuwawezesha kupata haki zao.

Akitoa mtazamo wake, Afisa Mkurugenzi anayemaliza muda wake, Bw. Mkurugenzi Bw Groenendijk, anasema: “Tangu mwanzoni kwa msaada wa washirika wa maendeleo DANIDA naDfID, LSF imefanya kazi kubwa ya kuweka mazingira yaliyowezesha upatikananji wa huduma za kisheria kwa watu maskini hasa wanawake, kuwa rahisi na wakuaminika.”

Kwa kupitia mtandao mkubwa wa takriban wasaidizi wa kisheriahai 3,000 nchi nzima, “tumeweza kuleta mabadiliko chanya kwa maisha ya watu maskini, mpaka kwa wale waishio wa pembezoni. Kwa umuhimu unaofanana ni ukweli kwamba LSF inafanya kazi na asasi zingine za kiraia na serikali kuwezesha mabadiliko ya sera na sheria kwa lengo la kuhakikisha haki inabakikuwa sifa muhimu ya maisha ya kila siku ya mamilioni ya Watanzania. Ofisa Mkurungenzi Mkuu mpya atakuta misingi bora yenye lengo la kutekeleza maono yake, na hatimae kukuboresha misingi na maono hayo zaidi na zaidi.”

“Ng’wanakilala analeta nguvu na kasi mpya ya uongozi wenye mawazo mapya, uzoefu na maarifa mapana aliyonayo katika taaluma na nyadhifa mbalimbali alizoshika ambazo ni muhimu katika kuipeleka LSF mbele na kuwawezesha maelfu ya wananchi kuendelea kupata na kutambua hakizao,” anaongezaBw Groenendijk.

Akimkaribisha Ofisa MkurugenziMkuumpya, Mwenyekiti wa Bodiya LSF, Dk Benson Bana anasema: “Huduma za kutoa msaada wa kisheria ni kiini kinachoelezea kazi ya LSF. Kwa miaka hii michache asasi hii imebadilisha maisha ya watu wengi wa kawaida kwa kutilia mkazo kuwainua wanawake ambao kwa mfumo dume uliopo wamekuwa hawafaidiki sana. LSF, kwa ushirikiano kutoka serikalini, inaendelea kuwezesha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kila siku bila malipo yoyote. Ofisa Mkurugenzi Mkuu anayekuja ataunganisha vizuri watu hawa na kwa kutumia utajiri wa uzoefu wake ataweza kuiwezesha LSF kukuza fursa kwa watu wengi zaidi kunufaika na kujitoa kwetu kwa upatikanaji wa haki.”

Kablayauteuzi wake LSF, Ms Ng’wanakilala alishika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Mtandao wa UtepeMweupe kwa Uzazi Salama Tanzania (WRATZ), mjumbe wa KamatiyaUtendajiyaMradiUnaoongoza wa Uamzi Salama (LSC), Mkurugenzi wa BodiyaWanawake wa Mafanikio Tanzania (TWA) namwanzilishinamjumbe wa BodiyaKituo cha MawasilianonaMaendeleo Tanzania (TCDC).

Amefanya kazi kubwa katika mabadilikoya sera na kwenye vikundi vya kitaalamu vinavyoratibu, wezesha na ameshiriki katika hatua mbalimbali za utekelezaji, ikiwani pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupungu za Umaskini Tanzania (Mkukuta). Bi Ng’wanakilalanimwanachama pia wa Chama cha WanasheriaTanganzania Bara (TLS).

Uteuzi wa Bi Ng’wanakilalaunaanzarasmi Mei 1, 2019.

Benki ya Exim Yazindua Kituo Cha Huduma za Kubadilishia Fedha Za Kigeni Kariakoo

0
0
Benki ya Exim leo imezindua Kituo chake maalum kwa ajili ya kutoa huduma za kubadilisha fedha za Kigeni (Bureau de Change) katika soko la Karikakoo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kusogeza huduma zake zaidi kwa wateja.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho, Mkuu wa huduma ya rejareja wa benki ya Exim, Bw. Andrew Lyimo alisema uamuzi wa kufungua kituo hicho kinachohamishika umekuja kufuatia ongezeko la mahitaji ya sasa ya wateja wanaotafuta huduma za uhakika za fedha za kigeni hususani katika eneo hilo ambalo ni kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika mashariki na Kati.

"Benki ya Exim imekuwa ikihudumia wateja wengi sana kupitia tawi letu lililopo hapa Karikakoo na uamuzi wa kufungua huduma hii kubadilisha fedha za kigeni imekuja baada ya kugundua kuwa kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma hii na hivyo tumeamua kuchukua hatua mapema ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu,’’ alisema.

Aliongeza kuwa jukumu la benki hiyo litabaki katika kuwezesha jumuiya ya wafanyabiashara kukuza biashara zao huku benki hiyo ikiwasogezea huduma kwa ukaribu zaidi.

“Tunaamini kuwa kupitia kituo chetu hiki kinachohamishika, jumuiya ya wabiashara Kariakoo, itafurahia huduma zetu kwa kuwa wataweza kuuza na kununua fedha za kigeni papo hapo bila gharama yoyote.’’ Alibainisha.

Lyimo alisema kuwa huduma hiyo inaifanya benki hiyo izidi kuimarisha uwezo wake wa kutoa huduma na inadhihirisha kujitoa kwake kwa wafanyabiashara hasa wa kati na wadogo katika jiji la Dar es Salaam na kitaifa kwa ujumla.

“Inafahamika kuwa Kariakoo ni eneo la biashara na ni kitovu cha waagizaji, wafanyabiashara na wasambazaji ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji huu wa uchumi. Benki ya Exim inawahakikishia viwango vya ushindani kwenye soko na ndio maana tunawakaribisha waweze kufurahia huduma za fedha za kigeni kwenye kituo chetu cha hapa Kariakoo na kwenye mtandao wetu mkubwa wa matawi thelathini na mbili. "Aliongeza.

"Ikiwa ni benki ya tano kwa ukubwa hapa nchini na benki ya kwanza ya Tanzania kufungua matawi yake katika visiwa vya Comoros, Djibouti na Uganda, tunasimamia ahadi yetu ya kuboresha mazingira rafiki ya upatikanaji wa huduma za kifedha hapa nchini. Tunaamini kituo hiki kitasaidia kutoa ushirikiano wa muda mrefu na wa manufaa kati ya Exim Bank na wafanyabiashara wa wadogo na wa kati hapa nchini,’’ alihitimisha.
 Baadhi ya wafanyabiashara eneo la Kariakoo wakiingia kwenye kituo kipya  kinachohamishika cha huduma za kubadilisha fedha za Kigeni (Bureau de Change) cha Benki ya Exim katika soko la Karikakoo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kusogeza huduma zake zaidi kwa wateja. 
Baadhi ya wateja benki ya Exim eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam wakipata huduma ya kifedha kwenye kituo kipya cha kubadilisha fedha za Kigeni (Bureau de Change) kinachohamishika cha cha Benki ya Exim katika soko hilo ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kusogeza huduma zake zaidi kwa wateja. 

NAIBU MEYA MANISPAA YA IRINGA APIGA MARUFUKU KUNUNUA CHAKI NJE YA KIWANDA DUSTLESS SMART CHALK

0
0
Hizi ni baadhi ya chaki zinazotengenezwa katika kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

NAIBU meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata amepiga marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa kununua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora na zinazofaa kutumiwa katika shule zote.

Akizungumza na blog Naibu meya,alisema kuwa kiwanda cha chaki kilichopo katika manispaa ya Iringa kinatengeneza chaki zilizo na kiwango bora cha kutumiwa na walimu wakati wa kufundisha ili kuinua uchumi wa kiwanda hicho.

“Mimi nimekuwa mwalimu kwa takribani miaka nane katika shule mbalimbali na nimefundisha na kuandikia chaki kutoka katika kampuni mbalimbali ila hizi chaki ambazo zinatengemezwa hapa manispaa ya Iringa zinaviwango vinavyotakiwa” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa haiwezekani kunakiwanda cha kutengeneza chaki lakini walimu wanatumia chaki kutoka nje ya manispaa ya Iringa kutasababisha kuua mitaji na viwanda hivi vya vijana wabunifu ambao wapo manispaa hapa.

“Tusipo waunga mkono vijana na kiwanda hiki cha kutengeneza chaki tutakuwa tuaua uchumi wa wananchi wa manispaa ya Iringa hivyo lazima walimu wa manispaa ya Iringa kuwaamuru kutumia chaki zinazotengenezwa na kiwanda chetu kilichopo hapa manispaa ya Iringa” alisema Lyata

Aidha Lyata aliwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuwasaidia vijana hao wenye kiwanda cha Dustless Smart Chalk ambacho bado kinahitaji vitu vingi ili kuwa na kiwanga kikubwa zaidi na kuongeza ajira kwa vijana wengine.

“Wadau naombe mjaribu kuwatembelea wale vijana walipo pale Ipogolo SIDO kwa kuwa wanafanya kazi kubwa na ubunifu mkubwa kwa lengo la kufanikiwa kuja kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitasaidia kuongeza ajira kwa vijana wengine” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa kiwanda cha Dustless Smart Chalk kinakabiliwa na upungufu wa vifaa na vitendea kazi ambavyo vinarudisha nyuma kazi zao hivyo wadau wanatakiwa kujitokeza na kuwasiadia kununua vifaa pamoja kukiboresha kiwanda hicho kuwa cha kimataifa.

Lakini Lyata alimalizia kwa kusema kuwa chaki hizo zinaubora wa kimataifa kwa kuwa hazina vumbi wala madhara kwa binadamu yeyeto yule hivyo sasa ni muda muafaka kwa walimu kutumia chaki hizo.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu meya mmoja wa wanakikundi wa kiwanda cha Dustless Smart Chalk Prisca Masalanga alisema kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za vifaa bora vya kuzalishia bidhaa hii ya chaki.

“Tunazalisha chaki zenye kiwango bora lakini tunakumbana na uhaba wa vifaa vinavyopelekea kuanika chaki hizi kwenye meza kwa kuwa hatuna sehemu sahihi ya kuanikia chaki hizi,bado hatuna mashine kubwa bado tunatumia mashine ndogo” alisema Masalanga

Masalanga alisema kuwa changamoto kubwa ambayo wanakumbana nao ni kukosa soko la kudumu la chaki kutoka katika kiwanda hicho cha Dustless Smart Chalk ambacho kinauwezo wa kuazalisha chaki zenye ubora unaotakiwa kufundishia mashuleni.

“Kwa kweli ndugu mwandishi kiwanda chetu bado hatuna soko tunazalisha tu hizi chaki huku tukitafuta soko na kuwaomba wadau kutusaidia kutafuta soko ili tuweze kuuza chaki hizi na kukuza mitaji yetu na kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitaajili vijana wanzetu wengi hapo baadae” alisema Masalanga
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa kiwandani hapo na kupiga marufuku kwa shule zote za manispaa ya Iringa kununua chaki kutoka nje ya kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kwa kuwa kiwanda hicho kinatengeneza chaki zilizo bora.
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiandika kwa kutumia chaki zinazotengenezwa na kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa kinachotengeneza chaki zilizo bora.
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akipata maelezo ya jinsi gani chaki hizo zinavyotengenezwa katika kiwanda Dustless Smart Chalk kilichopo manispaa ya Iringa.

Dkt. Ndumbaro afanya mazungumzo na Mwakilishi wa JICA nchini

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.), amefanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) nchini, Bw.Naofumi Yamamura, hivi karibuni katika ofisi za wizara Dodoma. Mazungumzo hayo, yanalenga kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia shirika hilo katika masuala ya miundombinu. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) nchini, Bw. Naofumi Yamamura,mara baada ya kuwasili katika ofisi za wizara.
Afisa Mambo ya Nje wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Bi. Bertha Makilagi na Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Charles Faini, wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Afisa Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Takusaburo Kimura, akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo. 
Wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) nchini, Bw. Naofumi Yamamura na Afisa Mwandamizi wa shirika hilo, Bw. Takusaburo Kimura, wakimsikiliza Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (hayupo pichani).

MWENYEKITI TUGHE PWANI CATHERINE KATELE AFANYA ZIARA BAGAMOYO KUSIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYAKAZI AMBAO NI WANACHAMA WA CHAMA HICHO.

0
0
NA ELISA SHUNDA,BAGAMOYO.

MWENYEKITI wa Chama Cha wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) wa Mkoa wa Pwani Ameanza Ziara ya Kutembelea Taasisi Mbalimbali za Wilaya ya Bagamoyo ambapo Kuna Wafanyakazi Ambao ni Wanachama Wao kwenye Chama Hicho kwa Ajili ya Kuwasikiliza,Kupokea Changamoto zao na Kuzitatua Pale Inapobidi kwa Haraka Zaidi.

Akizungumza na wafanyakazi wa taasisi ya sanaa Bagamoyo (Tasuba) baada ya kuwatembelea Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Pwani,Catherine Katele alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kutoa semina fupi juu ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) jinsi unavyofanya kazi zake katika kuwahudumia watumishi wa umma lakini pia kusikiliza kero na changamoto za wafanyakazi hao na kuzichukua kuzifikisha sehemu husika pamoja na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa kiongozi wao kwa kipindi cha miaka mitano.

“Tangu nimechaguliwa nafasi hii sikuwahi kuja kuwatembelea ndugu zangu watumishi wenzangu wa serikali japo kuwashukuru kwa kunichagua kwa kura za kishindo lakini pia sikuja bure nimeongozana na wenzangu kutoka ngazi ya mkoa ambapo leo hii mtanufaika kwa kupata semina fupi juu ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) jinsi unavyofanya kazi katika kumsaidia mtumishi wa umma pindi anapopatwa na matatizo akiwa kazini pamoja na kusikiliza kero na changamoto zenu tuzibebe na tuzifikishe sehemu husika zishughulkikiwe;

“Kwa sasa katika taasisi nyingi kumekuwa na hali ya sintofahamu ambayo inaleta mkanganyiko katika kipindi cha kutoa mfanyakazi bora mfano katika taasisi yenu hii kuna wafanyakazi ambao wapo katika vyama vingine vya wafanyakazi ukiachia chama chetu cha tughe sasa muda ukifika badala ya kuangalia mfanyakazi gani ameiletea taasisi mafanikio kinachoangaliwa kila watumishi na vyama vyao wanavutia upande wao,mimi niseme hatuendi hivyo niwasihi tumchague mfanyakazi kwa manufaa aliyoiletea taasisi yake na ubora wa utendaji kazi wake” Alisema Mwenyekiti Katele.

Aidha Mwenyekiti Katele amewaambia uongozi wa tawi la Tughe katika taasisi ya Tasuba kuwa Viongozi wamehakikisha wanasimamia haki za wanachama wao kwa kuhakikisha asilimia 20% zao za matawi zinaanza kutolewa na madeni Yote ya Nyuma  yanalipwa.

 Hata Hivyo Katibu wa Tughe wa Mkoa wa Pwani,Shadrack Mkodo wakati akitoa semina kuhusu mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa watumishi hao wa Tasuba aliwaambia kuwa kazi inaanzia unapotoka mlangoni kwako au getini unaanza kuhesabika upo kazini hadi unafika ofisini unasaini hadi muda wa kuondoka hadi unafika nyumbani kwako lolote litakalokutokea utahesabika umepatwa na tatizo hilo ukiwa kazini ila endapo utakutwa na tatizo ukiwa umekwenda sehemu nyingine tofauti na maelekezo ya kazi yako inavyosema utakuwa umepatwa na matatizo hayo nje ya kazi akatolea mfano kama ukiumia bar na kumbi za starehe.

Naye mmoja kati ya wafanyakazi wa Tasuba ambaye ni mwanachama wa tughe,Mkufunzi,Haji Maeda aliwashukuru uongozi wa chama cha wafanyakazi kwa mkoa wa pwani kufanya ziara hiyo ambayo kwa namna moja itasaidia kutatua kero na changamoto zao walau kwa kiasi na kuwaomba kuwatembelea mara kwa mara ili kuzidi kuwasaidia katika kutatua matatizo yanayowakabili pamoja na kuwapatie elimu juu ya stahiki na haki zao kama wafanyakazi.

Katika msafara wa Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) Mkoa wa Pwani ambao ulikuwa ukiongozwa na Mwenyekiti wake,Catherine Katele na Katibu wake,Shadrack Mkodo pia uliambatana na Mwakilishi wa Vijana Mkoa wa Pwani Tughe,Dk.Christian Benedict,Katibu wa Tughe Mkoa wa Dar es Salaam,Litson Magawa,Mratibu Tughe Wilaya ya Bagamoyo,Timothy George Twalib,Mratibu Tughe Wilaya ya Kibaha,Dk.Baraka Makayo.







NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO,ATASHASTA NDITIYE AFUNGUA BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI SHIRIKA LA RELI TANZANIA - TRC.

0
0
                                

Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe, Mhandisi Atashasta Nditiye afungua rasmi Baraza jipya la wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC katika ukumbi wa Bandari jijini Dar es Salaam hivi karibuni Aprili 2019.                                                        




Hafla hiyo ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi TRC kwa mara ya kwanza 
tangu kuunganishwa kwa iliyokuwa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli – RAHCO na kuanzishwa TRC.

Baraza jipya la wafanyakazi lina jukumu la kusimamia na kutetea maslahi ya wafanyakazi kupitia wawakilishi kutoka idara na vitengo vya taasisi pamoja na wajumbe wa kamati tendaji wanaotokana na wajumbe wa baraza.

kulingana na katiba ya baraza na taratibu za kisheria Baraza lina kazi ya kupitia na kutoa maoni na kuboresha utendaji wa Shirika,pia baraza ni chombo cha kuleta upendo na umoja baina ya wafanyakazi. 

Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Baraza hilo naibu waziri Mhe. Atashasta Nditiye amelipongeza Shirika la Reli Tanzania kwa kufanya uamuzi huo wa kuundwa Baraza jipya na kuwataka wajumbe kulifanya Baraza kama sehemu wa kuwawakilisha wafanyakazi kwa lengo la kutatua matatizo changamoto na kuleta tija katika Shirika. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC alisema kuwa serikali inafuatilia Mali za Shirika ambazo zinamilikiwa na watu binafsi wamejibinafisha kwa njia zisizo halali na kuomba wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania kushirikiana katika kutoa taarifa sahihi ili rasilimali hizo zirudi kuongeza mapato kusaidia kuendesha Shirika ikiwemo kuinua maslahi ya wafanyakazi.


Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe, Mhandisi Atashasta Nditiye akifungua rasmi Baraza jipya la wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC katika ukumbi wa Bandari jijini Dar es Salaam hivi karibuni Aprili 2019.
Picha tofauti za matukio katika Hafla ya ufunguzi wa Baraza la kwanza la wafanyakazi TRC tangu kuunganishwa kwa kampuni mbili zilizokua TRC,yaani Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) na kampuni hodhi ya Reli (RAHCO) 

ILALA YATOA MKOPO KWA BILIONI 1.7/-, DC MJEMA AWATAKA WALIOPEWA KUREJESHA KWA WAKATI

0
0

*Pia kuna mikopo ya Bajaji, bodaboda ili kuinua maisha ya wananchi

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imetoa mkopo wa Sh.bilioni 1.7 kwa vikundi 295 kwa lengo la kuwajengea uwezo kiuchumi, huku Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema akiwataka waliopewa mkopo huo kurejesha kwa wakati ili wengine nao wakopeshwe.

Kwa mujibu wa Ilala utolewaji wa mkopo huo wa fedha kwa wananchi uliokwenda sambamba na utoaji wa mikopo ya bajaji 30 na bodaboda 29, ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo inazungumzia kuwawezesha wananchi kiuchumi .

Pia imeelezwa ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli iliyodhamiria kuinua maisha ya wananchi wanyonge kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi.

Akizugumza leo Aprili 17, 2019 wakati wa kukabidhi mkopo huo kwa vikundi 295, Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema amesema waliopewa mkopo huo wanapaswa kurejesha kwa wakati ili wengine nao wakope na kwa kufanya hivyo wananchi wengi watakuwa wameinuka kiuchumi.

"Leo hii Wilaya ya Ilala tumetoa mkopo wa fedha wenye thamani ya Sh.bilioni 1.7 kwa alili ya kukopesha vikundi mbalimbali ndani ya Wilaya yetu.Hata hivyo lengo letu ni kutoa mkopo zaidi na kati ya Mei na Juni mwaka huu tutatoa tena mkopo wenye thamani ya Sh.bilioni mbili na lengo letu ni kutoa Sh.bilioni nne.

"Mbali ya kutoa mkopo wa fedha, tumetoa mkopo wa bajaji, pikipiki na mkopo wa vifaa vya kilimo kulingana na mahitaji ya vikundi ambavyo vimepwa mkopo huu.Kazi yetu kubwa wasaidizi wa Rais wetu mpendwa ni kutimiza ndoto zake ambazo anataka kuona wananchi wa hali ya chini wanakuwa na maisha mazuri.

"Hivyo kitendo cha kutoa mkopo huu Ilala tunakwenda kuinua maisha ya wananchi wetu, tunaamini wapo ambao wamepata mkopo huu na baada ya kipindi kifupi watakuwa matajiri wakubwa,"amesema Mjema.

Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kumuombea Rais Magufuli awe na maisha marefu na hatimaye aweze kutimiza ndoto zake za kuwaletea maendeleo Watanzania wote na kwamba Ilala itaendelea kuweka mikakati ya kuendelea kuinua maisha ya wananchi.

Mjema amesema viongozi wa Chama na Serikali wameungana na wataendelea kufanya kazi kwa bidii. "Kila jambo ambalo linafanyika katika taifa hili yamo kwenye Ilani ya uchaguzi. Kutoa bajaji, boda boda ,kutoa mikopo ya fedha ni utekelezaji wa Ilani".

Wakati huo huo Mjema amesema Rais Magufuli anawapenda Watanzania na kwamba alianza kutoa vitambulisho vya wajasirimali na sasa wanatamba na kuwataka waendelee kutamba na kwamba mikopo iliyotolewa haina riba. 

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam amesema kuwa jumla vikundi 295 vimenufaika na mkopo huo na kwamba wataendelea kutoa na kwamba wamejipanga kutoa Sh.bilioni nne licha ya kwamba leo tayari wametoa Sh.bilioni 1.7.

"Hadi sasa jumla ya 3, 209 wanafuika na mkopo ambao umetolewa na kati ya hao wanawake ni 2, 744 na kwa upande wa vijana ambao wamenufaika hadi sasa ni 332.Hata hivyo tunaamini waliokopeshwa bajaji na pikipiki watarudisha fedha kwa wakati,"amesema.

Ameongeza mikopo inalenga kupunguza umasikini wa kipato kwa wananchi wa Manispaa ya Ilala na kufafanua kuna vikundi ambavyo vimeomba mikopo ya vifaa vya kilimo.Pia kutokana na mkopo huo wapo ambao wamekopa kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo , hivyo matarajio ni kuanzishwa viwanda vidogo 150 ndani ya Wilaya hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema akijiandaa kukabidhi bodaboda ambazo zimetolewa na wilaya hiyo ili kukopesha wananchi.Mikopo hiyo ya bodaboda imetolewa leo viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema(wa pili kushoto) akifurahia jambo baada ya kutoa hutuba kwa vikundi mbalimbali ambavyo vimekabidhiwa mkopo wa bajaji,bodaboda na fedha
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa amepakizwa kwenye pikipiki baada ya kukabidhiwa kwa vikundi ambavyo vimepewa mkopo wa bodaboda
 Viongozi wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema wakicheza muziki kabla ya tukio la kukbidhi mkopo kwa wananchi ambao wamejiunga kwenye vikundi mbalimbali
 Bajaji ya mkopo iliyotolewa na Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ikiwa na ujumbe maalum kuhusu bajaji hizo ambazo ni za mkopo
 Sehemu ya wananchi wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakicheza muziki wakati wa utolewaji wa mikopo ambapo baadhi ya wamepata mkopo wa fedha, bajaji na bodaboda
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa katika moja ya bajaji ambayo ni ya mkopo iliyotolewa na wilaya hiyo

SERIKALI YASHUSHA GHARAMA ZA URASIMISHAJI

0
0
Na Munir Shemweta, WANNM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuanzia sasa gharama za urasimishaji haitazidi shilingi 150,000 badala ya 250,000 iliyopangwa awali na makampuni yatakayoenda kinyume yatachukuliwa hatua ikiwemo kufutwa.

Lukuvi alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Makampuni ya Upangaji na Upimaji yanayofanya kazi ya urasimishaji katika mitaa mbalimbali nchini pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, baada ya Wizara yake kuona zoezi la urasimishaji linasuasua wamegundua asilimia 30 pekee ndiyo iliyorasimishwa tangu kuanza zoezi hilo na hali hiyo imechangiwa na uwezo mdogo wa wananchi wengi kumudu gharama za urasimishaji.

Waziri Lukuvi alisema, alichotegemea kwa makampuni yaliyopewa kazi ya urasimishaji ni kuwa na uzalendo kwa kushusha gharama lakini yameshindwa kupunguza gharama jambo lililoifanya serikali kuona haja ya kupitia upya gharama hizo na kubaini gharama za msingi ili kumuwezesha mwananchi kupata hati na kusisitiza punguzo hilo halitawahusu waliolipia gharama za urasimishaji.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameyataka makampuni yanaoyoendesha zoezi la urasimishaji kuhakikisha kiasi cha fedha inachowatoza wananchi kinaishia hatua ya Hati na gharama itakayolipwa na mwananchi baada ya kurasimishwa ni kodi ya ardhi na kuyatahadharisha kutochukua muda mrefu kukamilisha zoezi hilo.

Amewataka wananchi wote wanaoishi kwenye maeneo yasiyo rasmi kuhakikisha wanaingia katika zoezi la urasimishaji ili kupata hati itakayowawezesha kiuchumi na kusisitiza kuwa suala hilo linafanyika kwa nia njema kwa nia ya kuwaongezea mtaji wananchi kwa kupatiwa nyaraka itakayowasiadia kukopa fedha benki.

Akigeukia suala la Leseni za Makazi, Waziri Lukuvi alisema zoezi hilo linaendelea vizuri katika jiji la dar es Salaama kwa gharama ya shilingi elfu tano hadi hatua ya upatiwaji leseni ya makazi na kusisitiza kuwa leseni hiyo siyo ya kudumu bali itakuwa kwa miaka mitano na kuwataka wananchi walio katika maeneo ya urasimishaji kuendelea na zoezi hilo kwa kuwa wizara inayo kanzi data itakayotunza takwimu za mazoezi yote mawili.

‘’Tunataka kuwa na database ya nani anamiliki ardhi kiasi gani na kila mwananchi lazima awe na leseni ya makazi au hati kwa lengo la kushiriki kulipa kodi’’ alisema Lukuvi

Hata hivyo, Lukuvi alisikitishwa na baadhi ya Makampuni ya urasimishaji kushindwa kutoa takwimu wakati wa zoezi la upimaji zinazoendana na miongozo ya wizara na kuyataka yote yaliyoenda kinyume kurudia zoezi na kuongeza kuwa kuna makampuni 34 yaliyotuma takwimu ambazo ni chafu na kuyapongeza makampuni mawili ya Visible Planners na Afro Max kwa kufuata taratibu zote za urasimishaji.

Lukuvi alionya baadhi ya makapuni ya urasimishaji kuacha kuwalaghai wananchi kwa kuwapatia leseni za makazi badala ya hati kwa gharama za urasimishaji na kusema kufanya hivyo ni kosa la uhujumu uchumi na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Vile vile Lukuvi amewataka watendaji wa serikali ambao wana makampuni yanayofanya kazi ya urasimishaji kuchagua jambo moja la kuitumikia serikali ama makampuni yao kwa kuwa wanatumia muda mwingi kufanya kazi katika makampuni yao badala ya kuitumikia serikali.

‘’Ninyi watendaji wa serikali badhi yenu mna makampuni ya urasimishaji na ndiyo mnaoharibu zoezi mnataka squatters ziendelee ili mnufaike na mnapima halafu michoro mnapitisha ninyi hii ni conflict of interest’’ alisema Likuvi.

OFISA OPERESHENI WA KIPOLISI KINONDONI ATOA USHAHIDI KESI YA KINA MBOWE

0
0
MRAKIBU Mwandamizi wa Polisi, SSP Gerald Ngiichi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliamuru askari kupiga risasi hewani kwa ajili ya kusambaratisha maandamano ya viongozi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Baada ya kuona njia ya kutumia mabomu ya Moshi imeshindikana kuwatanya.

Amedai baada ya kuamuru risasi zipigwe hewani na utekelezaji kufanyika, kulitokea sauti kubwa ambayo ilifanya waandamanaji wakiongozwa na Mwenyekiti  wa chama hicho, Freeman Mbowe kukimbia ambapo amesema  hakujua kama Mbowe alikuwa na mbio kiasi kile.

Amedai, baada ya waandamanaji kusambaratika, alifanya tathmini na kubaini kuna majeruhi wawili ambapo alikuwepo Akwilina aliyewashishwa Hospitali ya Mwananyamala na baadae kuripotiwa kuwa amefariki.

Ngiichi ambae ni Ofisa Operesheni wa Kipolisi Kinondoni, na shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho amedai hayo leo Aprili 17,2019 alipokuwa akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, shahidi huyo amedai Februari 16, mwaka jana wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Kinondoni,  kulikuwa na mikutano mikubwa mitatu ya Chama cha Wananchi (CUF) iliyofanyika viwanja vya Vegas Makumbusho, mkutano wa Chadema ulifanyika viwanja vya Buibui Mwananyamala na mkutano wa CCM Uliofanyika viwanja vya Biafra Kinondoni.

Amedai, akiwa kama kiongozi, alihakikisha kila mkutano unakuwa na ulinzi wa kutosha huku wakisimamiwa, lakini viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe waliwaongoza wafuasi wao kuandamana kutoka kwenye viwanja vya kampeni kwenda kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Kinondoni ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi.

Amedai, katika mikutano hiyo kila mkutano alipangwa ofisa wa kusimamia mikutano hiyo ya kampeni pamoja na askari wa kutosha ambapo mkutano wa Chadema ulisimamiwa na SSP Dotto, mkutano wa CUF ulisimamiwa na SP Batseba na wa CCM ulisimamiwa na SP Magai.  Lakini kati ya saa 11:30 kwenda saa 12 jioni alipokea taarifa kutoka kwa Dotto kuwa kwenye mkutano wa Chadema kuna dalili za kuwepo kwa uvunjifu wa amani kwa sababu viongozi wanaopanda jukwaani na kuhamasisha chuki na uvunjifu wa amani kwa wananchi.

Amedai, alimuelekeza ofisa huyo kusimamia kwa weredi mkutano huo na kuelekeza askari kuchukua kumbukumbu ya vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na ndipo Baada ya muda mfupi alipigiwa simu na SSP Dotto na kumueleza kuwa viongozi wa Chadema wanahamasisha wananchi kuondoka kwenye mkutano na kwenda kwa Mkurugenzi wa Kinondoni.

Ameongeza, alimwambia SSP Dotto awaonye viongozi hao kwamba kinachoendelea ni mkutano na sio kuondoka kwenda kwenye eneo lingine kwa sababu hawajajipanga kwa ajali ya hilo na kwenda kwenye ofisi za serikali wakati  zimefungwa, haikuwa sahihi lakini walikataa na kuhamasishana kuondoka kwenda barabarani 

Kufuatia hali hiyo niliagiza askari wengine ikiwemo kutoka vikosi vya doria, magari, pikipiki na wa usalama barabarani kwenda kwenye makutano ya barabara ya Kawawa na Mwananyamala kwa ajili ya kuzuia maandamano hayo ambapo Mbowe na wenzake walikaidi amri iliyotolewa kitu kilichomfanya yeye mwenyewe kuamua kwenda eneo la tukio na kwamba alipofika alikuta watu wengi zaidi ya 600 wakiingia barabarani wakiwa wamevalia sare na magwanda ya Chadema huku wakiimba kwamba ‘hatupoi, hatutishwi ‘ wakionekana kuwa na jazba  mawe, chupa za soda, maji na fimbo.

Amedai baada ya kuona hali hiyo, alimuamuru dereva wake awashe king’ora na honi ili wapite kwenye barabara ya mwendokasi na walifanikiwa kufanya hivyo lakini waandamanaji walipoona kuwa ni gari la polisi waliendelea kusogea mbele hivyo alitoa ilani mara tatu ya kuwataka kutawanyika lakini walikataa kutii amri.

‘’Ilani ilani ilani mimi SSP Gerald Ngiichi kwa jina la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkusanyiko huu ambao sio halali mliokusanyika hapa nawaamuru mtawanyike mara moja vinginevyo nguvu itatumika kuwatawanya,’’ alidai kutoa ilani hiyo kwa kutumia kipaza sauti cha kwenye gari analotumia huku akiendelea mbele.

Amedai kufuatia kugoma kutawanyika, pamoja na kutoa ilani hiyo, aliamuru askari waliokuwa na mabomu ya moshi kupiga mabomu hayo lakini hakukuwa na muitikio wa kutawanyika kwa waandamanaji kwa sababu mabomu yaliathiriwa na upepo hivyo moshi ulikuwa ukirudi upande wa askari kitendo kilichopelekea waandamanaji hao kuwarushia mawe na kusababisha kujeruhiwa askari wawili ambao ni PC Fikiri na Koplo Rahim ambao walianguka chini hivyo aliomba askari kutoa msaada kwao.

‘’Baada ya kuona hali hii, niliamuru vikosi vya mabomu kurudi nyuma na vikosi vyenye risasi za moto kusonga mbele kwa ajili ya kupiga risasi hewani ambapo baada ya kupigwa kwa risasi hizo, kulitokea kishindo kikubwa na niliona waandamanaji wakitawanyika ikiwemo Mbowe akikimbia, sikuamini kama alikuwa na mbio kiasi kile,’’ amedai SSP Ngiichi.

Pia alidai baada ya kutawanyika kwa watu hao, walifanikiwa kuwakamata wafuasi 43 na kuwapeleka kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kuwafungulia kesi ya kufanya maandamano isivyohalali.


Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji ,  Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji,  Mbunge wa Kawe,  Halima Mdee,  Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda,  Ester Bulaya.

Kesi hiyo itaendelea Mwezi ujao kwa Siku tatu mfululizo. Mei 13, 14 na 15

Serikali Yajipanga Kuimarisha Mfumo Madhubuti wa Kikatiba na Kisheria

0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imejipanga kuimarisha mfumo madhubuti wa kikatiba na kisheria ili kufanikisha utekelezaji wa sera na mipango kwa maendeleo ya Taifa.

Hayo yamesemwa leo Bungeni  jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) alipokuwa akiwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Balozi Mahiga amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha, wizara hiyo itaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kisheria kwa Umma  ambapo imeainisha maeneo mahususi ya vipaumbele na kuyawekea mikakati ya utekelezaji.

"Ili kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele hivyo vitakavyoisaidia nchi kusonga mbele, katika Bajeti ya Mwaka 2019/20 Wizara yangu inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 55,175,163,302 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo", alisema Balozi Mahiga.

Balozi Mahiga amevitaja baadhi ya vipaumbele vya Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo vikiwemo vya  kukamilisha maandalizi ya Sera ya Taifa ya Sheria kwa ajili ya mambo ya kisheria na utekelezaji wake kuwa; kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali ya maboresho katika mfumo wa utoaji haki nchini pamoja na kushiriki katika masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa yanayoihusu wizara.

Vile vile kwa upande wa Mahakama ya Tanzania. baadhi ya vipaumbele ni kuanza ujenzi wa majengo ya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma pamoja na kuendelea na ujenzi wa Mahakama nchini kote zikiwemo Mahakama Kuu mbili zinazoendelea kujengwa mkoani Kigoma na Mara; na kuanza kujenga nyingine katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Dodoma na Singida.

Aidha, Balozi Mahiga ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa vipaumbele vya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19 vikiwemo vya wananchi kuwa na uhakika kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za kimahakama,, kupatikana kwa ofisi za kudumu za Wizara na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa huduma za kisheria kupitia TEHAMA pamoja na kupatikana kwa  kiasi kikubwa cha fedha na mali nyingi kilichookolewa na kurejeshwa Serikalini.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA MAURITIUS NA MWEKEZAJI IKULU

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Sugar Investment Trust (SIT) ya Mauritius Bw. Gansam Boodram, Balozi wa Mauritius nchini, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede  pamoja na Maafisa wa Kituo cha uwekezaji na wa Ikulu baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na balozi huyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Mauritius nchini Mhe. Jean Pierre Jhumun pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt Edwin Mhede, Maafisa wa Kituo cha uwekezaji na wa Ikulu baada ya kuonana na kufanya mazungumzo na balozi huyo Ikulu jijini Dar es Salaam.Aprili 17, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari akiwa na Mhe. John Chiligati aliyeongozana na Balozi wa Mauritius  nchini Mhe. Jean Pierre Jhumun, Mwenyekiti wa Kampuni ya Sugar Investment Trust (SIT) ya Mauritius Bw. Gansam Boodram baada ya kuonana na kufanya mazungumzo na balozi huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Aprili 17, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mhe. John Chiligati aliyeongozana na Balozi wa Mauritius  nchini Mhe. Jean Pierre Jhumun, Mwenyekiti wa Kampuni ya Sugar Investment Trust (SIT) ya Mauritius Bw. Gansam Boodram pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede baada ya kuonana na kufanya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Aprili 17, 2019.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Ackson (kulia), na Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa Bungeni jijini Dodoma Aprili 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa viti Maalum, Upendo Peneza, Bungeni jijini Dodoma Aprili 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Wawi (CUF) Ahmed Ngwali, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma Aprili 17, 2019. Katikati ni Mbunge wa Mafinga Cosato Chumi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungunza na Mbunge wa Mtwara Mjini (CUF), Maftah Nachuma, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma Aprili 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SAHARA TANZANIA LIMITED YAANZISHA KAMPENI KUWASAIDIA SERENGETI BOYS

0
0
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Sahara Wakiongozwa Afisa Maendeleo ya Biashara Bi Mwajabu Mrutu (Watatu Kulia) Wakiwa Kwenye Kampeni ya Kuwasaidia Vijana wa Serengeti Boys ili kuweza kufanya Vizuri Kwenye Michuano ya Kombe la Afrika (AFCON -U17) Inayoendelea Nchini.

Na Mwanishi Wetu 

KAMPUNI  ya Sahara Tanzania Limited imeamua kuanzisha kampeni ya kuwasaidia vijana wa Serengeti Boys kwa lengo la kuhakikisha wanafanya vema katika michuano ya Kombo la Africa (AFCON) chini ya miaka 17 inayoendelea nchini. 

Akizungmza leo Aprili 17, 2019 jijini Dar es Salaam Ofisa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo Mwajabu Mrutu amesema kampeni hiyo inajulikana kama 'KeepYourEyeOnTheBall' ambayo inatoa hamasa kwa vijana hao ili wajiamini na kufanya vizuri.

Hivyo amesema kupitia kampeni hiyo,  Sahara Tanzania Limited inatoa msaada wa kuwajengea uwezo vijana hao wa Serengeti wanaoshiriki AFCON 2019.

"Licha ya kuwa tunatoa hamasa kwa vijana katika kufanya vizuri siku za usoni, pia tunatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kufanya vizuri zaidi,"amesema na kuongeza kampuni yao inatoa hudumu ya kuwapeleka wachezaji na mashambiki uwanjani kwa ajili ya kuwapa hamasa vijana wa Serengeti.

Mrutu ametoa ombi kwa vyombo vya habari nchini na wadau  wengine wakiwemo mashabiki wa Serengeti Boys kusaidia katika kutekeleza kampeni hiyo inayolenga kuwasaidia vijana.

"'KeepYourEyeOnTheBall' si ujumbe wa wachezaji tu, tunaamini ni ujumbe ambao unakuja wakati mwafaka kwa vijana wote wa Tanzania kwa ajili ya kupenda na kuhamasika katika suala la  mpira wa miguu nchini Tanzania,"ameongeza Mrutu.

Wakati huo huo amesema kupitia kampeni hiyo, Sahara Tanzania Limited inatoa pia msaada wa masuala ya ujasiriamali na uchumi kwa ajili ya kuandaa wachezaji vijana kuona kama mpira ni sehemu nzuri ya kutengeneza maisha ya yao ya baadae.

"Tuna imani kuhusu vijana wa Tanzania na hii inatufanya  Sahara tuendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia maendeleo endelevu kwa vijana  wetu," amesema.

Amefafanua kuwa Sahara Tanzania Limited kupitia Sahara Foundation inatekeleza miradi mbalimbali nchini ukiwemo mradi wa kupandisha  hadhi maabara katika Shule ya Sekondari Pugu inayohudumia wanafunzi  zaidi ya 1000. Miradi mingine ni School Sanitation Wash and Hygiene (SWAH) ambao unahusisha utoaji wa vyoo na bafu katika shule ya Sekondari ya Salma Kikwete.

WAZIRI MKUU ASHIRIKI KWENYE MSIBA WA MTOTO WA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Cheka Kaviga, baada ya kufiwa na mtoto wake Samson Cheka,katika kanisa la Mchungaji Mwema Ipagala jijini Dodoma Aprili 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima ya mwisho kwa mtoto wa Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Cheka Kaviga, baada ya kufiwa na mtoto wake Samson Cheka,katika kanisa la Mchungaji Mwema Ipagala jijini Dodoma Aprili 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SEVILLA FC KUFANYA ZIARA NCHINI

0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii 

*Kutangaza Utalii wa Tanzania 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ameipongeza SportPesa kwa kufanikisha ujio wa timu hiyo na kueleza kuwa kampuni ni mdau mkubwa wa michezo nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma leo, Shonza amesema ujio wa Sevilla nchini utaitangaza Tanzania duniani na hivyo kusaidia kuwatangaza hata wachezaji wa Tanzania watakaocheza dhidi ya timu hiyo Mei 23. "Hivi sasa, Tanzania imeanza kuonesha mafanikio makubwa katika mchezo wa soka na michezo mbalimbali na kutia imani kwa wananchi kwamba pale tunapotaka kufika, itawekana," amesema.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kigwangalla, ameipongeza SportPesa kwa kuamua kuwaleta Sevilla Tanzania, amesema wizara yake itautumia ujio wa timu hiyo kama fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini. 

Amesema timu hiyo itakapowasili nchini, wataipeleka kwenye hifadhi moja au mbili kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii nchini. "Tunaamini kwa kufanya hivi tutaongeza idadi ya watalii. Tutaangalia pia uwezekano wa kuwapeleka Zanzibar kutembelea fukwe," amesema.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Ndugu Tarimba Abbas amesema ziara hiyo ni muendelezo wa ahadi ya kampuni hiyo ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.

“SportPesa inapenda kuendelea kushirkiana na La Liga ambayo inatajwa kuwa Ligi bora duniani ili kuvinadi vipaji vilivyopo nchini pamoja na kukuza kiwango cha soka nchin.
Picha ya Pamoja kati ya Kampuni ya Kubashiri ya Sportpesa na Viongozi wa Serikali, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangalla na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza. 

Ikiwa nchini Tanzania, Sevilla FC ambao wanagombea nafasi ya kushiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao, watashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.

Muendelezo wa historia “Mwaka 2017 dunia ilishuhudia klabu ya Everton ikitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza na muitikio ulikuwa ni wa kipekee. Hivyo tukaona umuhimu wa kuendeleza historia hiyo kupitia ushirika na LaLiga

“Kutokana na kuwa na ushirika na taasisi kubwa za soka duniani, tukaona basi ni vyema kuendeleza kuleta msisimko wa soka nchini Tanzania wenye hadhi sawa na ule wa Everton kwa kuileta timu ya Sevilla nchini Tanzania ambayo ni moja ya vilabu bora barani Ulaya kwa kushirikiana na wenzetu wa LaLiga,” alisema Ndugu Tarimba

“Lengo ni kuionesha dunia kuwa Tanzania ni mahala sahihi kwa vilabu vikubwa duniani kuja kwa ajili ya ziara za maandalizi ya Ligi bila kusahau kuvinadi vipaji adhimu vya soka vilivyosheheni nchini”.

Mwaka juzi, Kampuni ya SportPesa ilifanikisha ujio wa timu ya Everton inashiriki Ligi Kuu ya England (EPL). Ikiwa nchini, Everton ilikipiga dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

TAKUKURU PWANI IMEWAFIKISHA MAHAKAMANI MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA RAZABA NAMBA 4 PAMOJA NA WENZAKE WANNE

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani imewafikisha mahakamani mwenyekiti wa Kitongoji cha Razaba ,namba 4 ,Makurunge Bagamoyo Siasa Kasanura, na wenzake wanne kwa kosa la kutoa hongo ya sh.270,000 kwa askari polisi kinyume na kifungu cha 15(1)(b) cha 
Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007. 

Washitakiwa hao,wakiwemo wafanyabiashara wawili Idrisa Machano na Ndaju Kivalia, pamoja na mlinzi wa kampuni ya Bagamoyo Sugar Shabani Funga kwa kosa la kutoa rushwa hiyo machi, 2019 kwa askari polisi wa ofisi ya mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Pwani ili wasiwakamate wakati wakiendelea kufanya biashara haramu ya mkaa na magendo katika kitongoji hicho.

Kamanda wa TAKUKURU Pwani, Susan Raymond alieleza, askari hao walikuwa kwenye operesheni maalumu ya kudhibiti uhalifu katika kitongoji cha Razaba . 

Alisema, kitendo cha askari hao kudhibiti mianya ya biashara haramu ya mkaa na magendo kilipelekea wafanyabiashara haramu, wakiongozwa na mwenyekiti wao Siasa Kasanura kwenda kuwashawishi polisi kwa kuwapa hongo kwa ili wasiwakamate na wawaruhusu waendelee na biashara hiyo haramu. 

Susan alibainisha, washtakiwa hao wamefunguliwa mashitaka ya ya jinai namba 146 ya mwaka 2019 katika Mahakama ya wilaya Bagamoyo kwa kosa la kutoa hongo hiyo, kinyume na kifungu cha 15(1)(b) cha Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba. 11/2007. 

"Washtakiwa wote wanne wakisomewa mashtaka na mwanasheria wa TAKUKURU, Beatrice Ngogo mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Tumaini wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo, walikiri kutende kosa"

"Na ikumbukwe kwamba mtoaji na mtoa rushwa wote ni kosa"alisisitiza Suzan. 

Kamanda huyo alifafanua, kutokana na kukiri kutenda kosa hilo mahakama imewatia hatiani na kutoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila mmoja ama kulipa faini ambapo watuhumiwa wameamua kulipa faini na wamewekwa mahabusu wakisubiri kukamilisha malipo 
hayo.

WAZIRI KAIRUKI AMPONGEZI BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA KWA KUHAMASISHA UWEKEZAJI

0
0
 Waziri wa Uwekezaji, Angellah Kairuki akizungumza wakati ufunguzi wa mkutano wa majadiliano kati ya wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania na China uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.

Na Khadija Seif, Globu ya jamii

SERIKALI imetoa pongezi kwa Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke kwa namna ambavyo ameendelea kujenga ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo sekta ya uwekezaji.

Pongezi hizo zimetolewa leo Aprili 17,2019 na Waziri wa Uwekezaji Angellah Kairuki wakati ufunguzi wa mkutano wa majadiliano kati ya  wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mbali ya wawekezaji na wafanyabishara, pia mkutano huo umehusisha taasisi, kampuni za kibiashara pamoja na maofisa wa wizara mbalimbali ambazo zinahusika na mambo ya biashara na uwekezaji.
Kairuki wakati anazungumza kwenye mkutano huo amesema "Nampongeza pongezi Balozi wa China nchini Tanzania kwa kuendelea kuamini nchi ya Tanzania na kutengeneza ushirikiano mzuri baina ya nchi mbili hizo katika kila nyanja ya kimaendeleo ,"amesema Waziri Kairuki.
Ameongeza  umoja wa jamii ya watu wa China uliopo nchini umewezesha kuwekwezwa kwa Dola za Marekani bilioni saba ambazo kwa sehemu kubwa zimewanufaisha Watanzania huku akifafanua  wapo raia wa China ambao wameamua kuifanya Tanzania sehemu ya makazi yao ya kudumu.

Waziri Kairuki amesema mikutani ya aina hiyo itaendelea kufanyika na huo ni mwanzo tu kwani pamoja na jamii hiyo ya Wachina kuwekeza katika nchini Tanzania na kutengeneza baadhi ya bidhaa na kufanya biashara bado wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upatikanaji wa vibali na hivyo kusababisha malalamiko madogo madogo.

Kwa upande wake Balozi Wang Ke ametoa pongezi kwa Rais Dk.John Magufuli kwa kuendelea kuwakaribisha raia wa China kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini Tanzania.

Balozi Ke amesema mbali na mkutano huo kujenga ushirikiano wa kibiashara, pia utasaidia kutoa ujuzi kwa wawekezaji wa nchini zingine akitolea mfano Watanzania wenyewe kujaribu kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia ujuzi utakaotolewa na Wachina.
Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Daniel Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari.

"Tunafahamau mshikamano uliopo baina ya nchi ya China na Tanzania unafanya nchi hizi mbili kuendelea kushirikiana kwa hali na mali japo changamoto hazikosekani ,"amesema Balozi Ke.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Damas Daniel Ndumbaro amesema ushirikiano wa nchi hizo mbili utaendelea kuimairishwa kwani ni muhimu katika kukuza maendeleo ya Watanzania.

Dk.Ndumbaro amesema nchi ya China imeshaonesha utayari wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kujenga urafiki  katika biashara,uchumi na kukuza teknolojia nchini.
Balozi wa China nchini Tanzania Wang ke akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufungua mkutano wa wawekezaji kati ya nchi ya China na Tanzania jijini Dar es salaam
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live




Latest Images