Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Balozi wa Utalii Tanzania atambua mchango wa wasanii na serikali kutangaza Utalii


MIGOGORO YA NDOA YATAJWA KUCHANGIA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

0
0


Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akizungumza kwenye kikao cha mrejesho wa kazi za viongozi wa jamii kata ya Usanda katika kutokomeza mila na desturi kandamizi katika jamii.

Imeelezwa kuwa migogoro ya wanandoa imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa watoto kukosa haki zao matokeo yake wanafanyiwa vitendo vya kikatili. 

Hayo yamesemwa leo Jumanne Aprili 16,2019 na Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo kwenye kikao cha mrejesho wa majukumu ya viongozi wa jamii kata ya Usanda katika kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

Kikao hicho kimeandaliwa na Shirika la Agape ACP ambalo linalenga kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kupunguza mimba na ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU na UKIMWI. 

Afisa ustawi huyo wa jamii aliwataka wanandoa kuvumiliana panapotokea migongano kwani hakuna ndoa takatifu huku akibainisha kuwa pale wanandoa wanapoachana wanaoteseka zaidi huwa ni watoto. 

“Wanaume mmekuwa na kasumba na kuuza mazao na kuamua kuoa wanawake wengine matokeo yake mnaacha watoto wakiteseka,mnasahau hadi majukumu ya kuwalea na kuwasomesha matokeo yake watoto hawa wanaanza kuiga tabia za makundi mabaya”,alisema Mweyo. 

“Mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama,ndoa inaposambaratika watoto wanakosa pa kwenda,wengine wanaamua kuacha hata kwenda shule na kujiunga kwenye makundi yasiyofaa,mbaya zaidi wanaume wakipata mke mpya wa kwanza anamsahau,anasahau hadi kuwapatia haki watoto wake”,alieleza Mweyo. 

Aidha aliwashauri wananchi kuwa mstari wa mbele kubadilisha mila na desturi zisizofaa katika jamii ikiwemo kurithi wajane, kuozesha watoto na kutopeleka watoto shule akieleza kuwa mabadiliko yataletwa na wao wenyewe. 

Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape unaofadhiliwa na shirika la Sida la nchini Sweden, Lucy Maganga aliwaomba viongozi wa jamii kufanya kazi ya kutokomeza mila na desturi kandamizi kwa weledi ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto na wanawake. 

Kwa upande wao,viongozi hao wa jamii walilishukuru shirika la Agape kwa kuwafikia na kuwapatia elimu ya kukabiliana mila na desturi kandamizi huku wakisema hivi sasa jamii ya Usanda imebadilika na matukio ya mimba na ndoa za utotoni yamepungua. 

“Tumeendelea kutoa elimu kwa jamii,kwa kweli mwitikio umekuwa mzuri ,na sasa ile kasumba ya kwamba baba ndiyo kila kitu katika familia imeisha”,alisema Juma Katabuka kutoka Shabuluba. 

“Hivi sasa jamii imeanza kuacha tabia ya kurithi wajane kwani imeshatambua madhara yake kwani huko ni kumfanyia ukatili mwanamke lakini pia ni chanzo cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI,kwani huwezi kujua marehemu alifariki kwa ugonjwa gani”,alisema Ramadhan Kulwa ambaye ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwagala. 

Naye Singu Njegi kutoka kitongoji cha Munge alisema kutokana na elimu waliyopata wataendelea kuzifikia kaya na makundi mbalimbali ili kila mtu atambue mila na desturi kandamizi zinachangia ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 
Afisa Mtendaji wa kata Usanda Emmanuel Maduhu akizungumza wakati wa kikao cha mrejesho wa kazi zilizofanywa na viongozi wa jamii kata ya Usanda kilichofanyika leo katika shule ya msingi Shingida. Maduhu alisema Shirika la Agape limesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua mimba na ndoa za utotoni katika eneo hilo- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akiwahamasisha viongozi wa jamii kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watoto na wanawake ambao wamekuwa waathirika wakubwa wa mila na desturi kandamizi katika jamii.
Viongozi wa jamii wakiwemo viongozi wa kimila na Wazee maarufu kata ya Usanda wakimsikiliza afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga.
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akizungumza wakati wa kikao hicho. 
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akiwataka viongozi wa jamii kuwakumbusha wanandoa kuvumiliana ili familia zisitawi vizuri kwa maslahi ya kulinda haki za watoto kwani ndoa zinaposambaratika watoto wengi hukosa mwelekeo wa maisha matokeo yake wanajiingiza kwenye makundi yasiyofaa.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akizungumza katika kikao hicho.
Mzee Singu Njegi kutoka kitongoji cha Munge akitoa mrejesho wa kazi anazofanya kutokomeza mila na desturi kandamizi katika jamii.
Kikao kinaendelea.
Kaimu Mwenyekiti wa kitongoji cha Kanyenye,Daudi Michael akielezea namna anavyohamasisha wazazi kupeleka watoto shule.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Nzega kijiji cha Shigita,Mwinyi Albinus akielezea namna anavyoendelea kuielimisha jamii kuachana na mila na desturi kandamizi zinazochangia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kikao kinaendelea.
Mwakilishi wa kundi la watu wenye ulemavu Mayunga Mayunga akielezea jinsi anavyotoa elimu kwa jamii kuachana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Washiriki wa kikao hicho wakiwa ukumbini.
Mwakilishi wa kundi la vijana,Suzana Amos kutoka kitongoji cha Munge akielezea jinsi anavyotoa elimu kwenye kaya mbalimbali kuhusu madhara ya mila na desturi kandamizi.
Simon Makenza kutoka Nzagaluba akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Muelimisha rika kata ya Usanda,Hamis Malundi akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwagala, Ramadhan Kulwa akizungumza wakati wa kikao hicho.
Ng'wanzalima Malimi kutoka kitongoji cha Buchamike akizungumza wakati wa kikao hicho cha viongozi wa jamii.
Afisa Ustawi wa Jamii kata ya Usanda, Halima Tendeja akifunga kikao cha mrejesho wa kazi za viongozi wa jamii katika kutokomeza mila na desturi kandamizi. Tendeja alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanaume kushauriana na wenza wao kupanga uzazi kwani bado baadhi ya wanawake wamekuwa wakiogopa kupanga uzazi kwa kuogopa waume zao.

JAPAN KUIPIGA JEKI TANZANIA SHILINGI BILIONI 794 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

KING MWALUBADU ndani ya Alasiri Lounge ya AZAM TV

LUKUVI AONYA WENYEVITI WA MITAA MAUZIANO YA ARDHI

0
0
Na Munir Shemweta

Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William lukuvi amewaonya wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutojihusisha na masuala ya uuzaji ardhi katika maeneo mbalimbali kwa kuwa hapaswi kisheria kufanya kazi hiyo.

Lukuvi alitoa onyo hilo jana wakati alipokwenda kusuluhisha mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kikwajuni Vijibweni maarufu kama kwa Mkorea wilayani Kigamboni mkoa wa Dar es Salaam na Mwekezaji ‘Registered Trustee of Korea Church Mission’ katika eneo hilo la ukubwa wa ekari 305.

Lukuvi alisema sheria ya ardhi haisemi kama wenyeviti wa mitaa wanaruhusiwa kusimamia uuzaji ardhi na kusisitiza kuwa wenyeviti hao hawana mamlaka ya kufanya hivyo na mwenye jukumu la kusimamia masuala ya ardhi katika miji ni halmashauri za mji au Manispaa.

Waziri wa Ardhi alisema mtu yeyote atakayeuziwa ardhi kupitia wenyeviti hao wa mitaa au mtu mwingine asiyetambuliwa kisheria basi atakuwa ameuziwa ‘bomu’ na kuwataka wananchi kuwa makini na suala hilo na kuwashauri kabla ya kununua eneo lolote ni vyema wakaiuliza mamlaka husika iwapo eneo husika limepangwa kwa matumizi ya aina gani ili kuepuka kubomolewa.

‘’Ukitaka kununua kiwanja kwanza kaulize Manispaa maana unaweza kununua eneo kumbe ni la kuzikia kwani manispaa ndiyo inayojua kama eneo hilo ni salama’’ alisema Lukuvi

Katika hatua nyingine, Waziri Lukuvi ametoa siku kumi kwa halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kufanya uhakiki kwa wananchi wote wanaoishi eneo lenye mgogoro na Mwekezaji la Kikwajuni Vijibweni Kigamboni maarufu kwa Mkorea ili kupata taarifa sahihi za wananchi hao.

Aidha, amemtaka Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam Methew Mhonge kupata nakala ya hukumu ya kesi ya wananchi hao dhidi ya Mwekezaji ‘Registered Trustees Korea Church Mission’ inayoonesha kuwa wananchi wa eneo hilo wameshindwa kesi na wanatakiwa kuondoka.

Maagizo hayo ya Lukuvi yanafuatia kuelezwa na wananchi 22 wa Kikwajuni kupitia mwakilishi wao Meja Mstaafu Peter Ismail kuwa haki haikutendeka wakati wa zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi wa eneo hilo jambo lililosababisha kukataa kuchukua fidia na wengine 6 kudai nyongeza ya fidia huku wananchi 95 wakilalamika.

Meja Mstaafu Ismail alisema, wao walichukua uamuzi wa kutokubaliana na mwekezaji aliyetaka kuwafidia laki nne kwa ekari moja wakati wao walitaka kulipwa shilingi milioni moja kwa ekari moja na kufafanua kuwa kilichowashangaza ni Mwekezaji kulipa fidia mwaka 2015 wakati zoezi hilo lilitakiwa kufanyika miezi sita baada ya Agosti 2004.

Kwa upande wa wananchi sita wanaotaka kuongezewa fidia wananchi hao kupitia mwakilishi wao Hamza Rashid walidai kesi yao iliamuliwa kupatiwa taarifa halisi ya uthamni na siyo nakala kama walivyofanyiwa jambo walilolieleza kuwa halikufanyika.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Lukuvi aliagiza taarifa zote muhimu zipatikane kipindi cha siku kumi ikiwemo Mwekezaji kuwasilisha mpango wa jinsi atakavyolitumia eneo hilo la ekari 305 sambamba na chanzo cha mtaji wa uwekezaji huo.

Eneo la Kikwajuni Vijibweni maarufu kwa Mkorea kwa muda mrefu tangu mwaka 2004 limekuwa na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa eneo hilo na Mwekezaji ‘Registered Trustees Korea Church Mission’ anayetaka kujenga chuo Kikuu.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Wakazi wa Kikwajuni Vijibweni wilaya ya Kigamboni alipokwenda kutatua mgogoro kati ya Mwekezaji Registered Trustees Korea Church Mission  jijini Dar es Salaam jana.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  akitembea kuelekea eneo lenye mgogoro kati ya Wananchi wa Mkwajuni Vijibweni wilaya ya Kigamboni maarufu kama kwa Mkorea na Mwekezaji wakati alipokwenda kutatua mgogoro katika eneo hilo jana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimsikiliza mwananchi wa Mkwajuni Vijibweni  Mariam Kange alipokwenda kuatatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa eneo hilo maarufu kwa Mkorea na Mwekezaji Registered Trustees Korea Church Mission (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

WASAFI TV: MSANII BARAKA MWAMKIPESILE ANAYEMUIGIZA RAIS MAGUFULI

MKAZI WA GEITA AJISHINDIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI TANO KUTOKA BIKO

0
0
Mfanyabiashara mdogo wa Geita Mjini, Alyoce Masamaki, amefanikiwa kuibuka milionea kwa kukabidhiwa fedha zake sh milioni tano kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko.

WAKUU WA IDARA WANAOFANYA KAZI KWA MAZOEA WAHAMISHWE VITUO VYA KAZI -RC MAKONDA

0
0

*Awataka madiwani Manispaa ya Ilala kuendana na kasi katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati

* Utendaji kazi wa RC Makonda katika sekta ya elimu wamvutia balozi wa nchi za kiarabu nchini atoa Milioni 20 kusaidia watoto wa kike katika sekta ya elimu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote jijini humo kuwahamisha kazi wakuu wote wa idara  wanaofanya kazi kwa mazoea hali inayopelekea kusuasua kwa kasi maendeleo inayoenda sasa.

Akizungumza katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani  wa Manispaa ya Ilala  Makonda amesema kuwa baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakikwamisha maendeleo, huku akieleza kuwa wakuu wa idara zote waliokwama kwenye idara zao watolewe Dar es Salaam na  kupelekwe Mikoani hadi kufikia mwezi June mwaka huu.

Amesema kuwa baadhi yao wamekuwa wakikwamisha shughuli za kimaendeleo pamoja na kutotoa ushirikiano kwa wakurugenzi wao na hata ubadilishwaji wa vituo vya kazi kwa wakuu wa idara hao umekuwa ni kutoka halmashauri moja kwenda nyingine hivyo ni vyema wakapelekwa katika Mikoa mingine ili kuboresha utendaji wao.

Kuhusiana na mradi wa ujenzi wa soko la kisutu Makonda amesema kuwa haoni sababu ya mradi huo kukwama huku fedha zikichezewa na kutumika kiholela na amefurahi baada ya  kuona leo   mradi huo umeanza kutekelezwa na hiyo ni baada ya kutoa maagizo ya siku tatu kwa Mkuu wa Wilaya na watendaji wake kushughulikia suala hilo.

Pia amesema kuwa kusuasua kwa mifereji na mto msimbazi hakufurahishi kwa kuwa watu wanapoteza maisha kunakosababishwa na mafuriko, amesema kuwa licha ya kuwepo kwa fedha lakini mradi huo bado hauridhishi na amewaagiza watendaji kufanya kazi usiku na mchana kwa kuwa Serikali tayari imetoa fedha ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Vilevile amewataka madiwani hao kusimamia miradi ya kimkakati ipasavyo na kujenga tabia ya kuokoa fedha za wapiga kura.

Akitoa taarifa ya manispaa hiyo Naibu Meya wa Ilala OMari Kumbilamoto amesema kuwa makusanyo ya mapato yamefikia asilimia 70 huku akieleza kuwa zaidi ya bilioni moja zitatolewa kesho kwa makundi mbalimbali wakiwemo wajane, walemavu na wanawake.

Amesema kuwa takribani watoto 21 elfu wamerudi shule huku  madarasa mengi zaidi yakizidi kujengwa ili kutatua changamoto ya elimu na amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuendelea kuonesha ushirikiano katika kuleta maendeleo.

Wakati huo huo RC Makonda amepokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa balozi wa  nchi za kiarabu nchini Balozi Khalifa Abdullahman al- Marzouqi  ambaye ametoa fedha hizo katika kuunga mkono juhudi za RC Makonda za kuwasomesha watoto wa kike  100 waliofaulu masomo ya sayansi na wanaoishi kwenye mazingira magumu kila mwaka.

Balozi Khalifa amesema kuwa utendaji kazi wa Makonda unavutia hasa kwa kuwagusa watu wenye mahitaji muhimu na amehaidi kuendelea kusaidia zaidi kwa siku za baadaye sambamba na kuboresha zaidi mahusiano ya nchi hizo mbili. Pia balozi huyo atafadhili ujenzi wa uwanja wa michezo (basketball) kwa ajili ya wanafunzi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na madiwani wa manispaa ya Ilala kwenye kikao cha dharura ambapo amewataka kuwa mstari wa mbele katika kusimamia miradi ya kimkakati jijini humo, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kushoto) akiteta jambo na Balozi nchi za kiarabu nchini Khalifa Abdullahman al-marzouqi (kulia) mara baada ya balozi huyo kukabidhi hundi ya shilingi milioni 20 zitakazowasaidia watoto wa kike katika sekta ya elimu, leo jijini Dar es Salaam.


Maambukizi ya Ukimwi kwa Wasichana na Wanawake yamezidi kuongezeka

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

 Maambukizi ya Ukimwi kwa vijana yamezidi kuongezeka na kufanya serikali kushindwa kufikia malengo kutokana vijana ndio nguvu kazi ya taifa.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi Bengi Issa kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu wa Binge ,Vijana na Walemavu wakati Mkutano wa Wadau wanaotekeleza Afua za Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Tanzania uliondaliwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwa Nchini (TACAIDS) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Issa amesema kuwa kutokana na hali hiyo vijana lazima muambiane ukweli kuhusiana na maambukizi ya Ukimwi kwa vijana wasichana walio katika balehe.Amesema serikali imekuwa ikitekeleza miradi ya Ukimwi ambapo aliongeza kuwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa katika kufikia malengo ya kutomeza ugonjwa huo.

Issa amesema kuwa vijana katika kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi lazima teknolojia zilizopo zitumike katika kupeana habari.Bengi amesema mapambano ya ukimwi yafanyike kwa kila mtu katika nafasi yake kwani bila kufanya hivyo tutapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo wahanga wakubwa ni wasichana walio katika Balehe na wanawake vijana.

Amesema afua hizo zimefanyika katika mikoa tisa lakini serikali itaendelea kushirikiana katika kumaliza mikoa yote.Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Jumanne Isango amesema mkutano wa wadau wa muhimu katika kupeana mrejesho kwa utekelezaji wa mradi.

Amesema mapambano ya Ukimwi yanaendelea kwani bila kufanya hivyo nguvu kazi ya taifa itapungua na kushindwa kufikia katika ukuaji wa uchumi.Amesema vijana wasichana wanaoshiriki katika mradi wa sauti wameaswa kuendelea kuwa mabalozi ya kutoa elimu ya ukimwi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia zilizopo katika karne ya 21.

Mwakilishi wa Unicef Urike Gilbert-Nandra amesema kuwa Unicef itaendelea kushirikiana na Tacaids katika mapambano ya ukimwi ili kuweza kufikia malengo.
 Mgeni Rasimi akiwa katika picha ya pamoja na wasichana walio katika mradi.
 Wadau katika mkutano wa TACAIDS
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini (TACAIDS) Jumanne Isango akitoa maelezo ya uandaji wa mkutano wa Mwaka wa Wadau Wanaotekeleza Afua Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wadau wa Mkutano Tacaids
 Mwakilishi wa Unicef. Urike Gilbert-Nandra akitoa maelezo namna Unicef inavyoshiriki katika mapambano ya Ukimwi katika mkutano wa mwaka wa Wadau wanaotekeleza afua za wasichana Balehe na wanawake vijana Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi Bengi Issa akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Wadau wanaotekeleza Afua za Wasichana Balehe na Wanawake vijana Tanzania Uliofanyika jijini Dar es Salaam.

WATEJA 15 WAFAIDIKA NA PROMOSHENI YA TIA VITUUZ.

0
0
Na.Khadija seif,Globu ya jamii

HATIMAE washindi 15 wa wiki ya saba ya promosheni ya “Tia kitu pata vituz” inayoendeshwa na Kampuni ya MultiChoice Tanzania watangazwa rasmi.

Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya michezo ya kubahatisha Bw. Jehud Ngolo amesema Kampeni hiyo ni ya kipindi cha wiki 8, ambapo washindi 15 hutangazwa kila wiki hivyo jumla ya washindi 120 katika kipindi chote cha promosheni hiyo.

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania Grace Mgaya wakati wa kufanya droo ya wiki ya saba ya promosheni hiyo amesema promosheni hiyo ni wazi kuwa inawalenga wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla havijakatika. 

“Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na ana fursa ya kujishindia kifurushi chake kwa muda wa miezi miwili mfulilizo” alisema Mgaya.


Akizumgumza baada ya kupatiwa taarifa kuhusu ushindi wake huo Angelina Michael  ambaye ni mteja wa DStv aliyepo mkoani Arusha amesema kuwa anafurahishwa na jitihada zinazofanywa na DStv siku hadi siku katika kuwajali na kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zilizo na ubora wa hali ya juu. 
.
Huku Deus Nyakriga kutoka mkoani Mara, ameishukuru sana DStv kwa zawadi hiyo na kueleza kuwa licha ya kuwapatia huduma nzuri DStv inawajali sana wateja wake. 

Pia amewapa ujasiri wateja wengine wa DStv kulipa kwa wakati ili kujipatia nafasi hiyo ya kuingia kwenye droo hiyo ya kushinda miezi miwili bila malipo.
Afisa Uhusiano MultiChoice Tanzania Grace Mgaya {katikati} Akizungumza kwa simu na moja ya washindi wa promosheni hiyo. Kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Jehud Ngolo na kushoto ni Benson Urio wa Kitengo cha Teknohama. Promosheni hiyo ni kwa wateja wanaolipia kwa
wakati kabla vifurushi vyao havijakatika hivyo kupata fursa ya kushinda kifurushi cha miezi miwili. Promosheni hii itaendelea kwa kipindi cha wiki 5 zijazo ambapo jumla ya washindi 120 
watapatikan 

SERIKALI IMEJIPANGA KUENDELEZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI-MHE MGUMBA

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Katika mpango kabambe wa Tanzania wa kufanya kilimo cha umwagiliaji kuwa kipaombele kikuu yaani ASDP II kauli ya kuwa kilimo ni maji inajipambanua zaidi kwani inazingatia matumizi bora ya ardhi na maji.

Katika kuongeza ufanisi na tija katika kilimo kupitia umwagiliaji Serikali imejipanga vyema kuimarisha sekta ya kilimo kupitia mbinu bora za kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Rehema Juma Migila aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji katika Manispaa ya Tabora, kwa kutumia maji kutoka Bwawa la Igombe baada ya ujio wa maji kutoka Ziwa Victoria kufika Tabora.

Mhe Mgumba alisema kuwa wakati wa kupanga matumizi ya maji kutoka katika chanzo, utunzaji wa mazingira na matumizi ya jamii hupewa umuhimu zaidi kabla ya matumizi mengine. 

Ujenzi wa miundombinu ya kutoa maji kutoka Ziwa Victoria umelenga zaidi katika kupunguza upungufu wa maji uliopo kwenye Manispaa ya Tabora ambayo kwa sasa inahudumiwa na Bwawa la Igombe. Maji hayo ni kwa ajili ya matumizi ya kijamii tu kwani hayatatosha kwa kilimo cha umwagiliaji.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa tija na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Wizara ya kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji unaotekelezwa kuanzia 2018/2019 hadi 2035/2036 ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo katika Manispaa ya Tabora, mpango huo umejumuisha uboreshaji na ujenzi wa skimu za umwagiliaji za Imalamihayo, Inala, Magoweko na Bonde la Kakulungu.

Aliongeza kuwa rasilimali maji ni muhimu katika jamii na kama itawekwa vizuri matumizi yake katika kila hatua huleta manufaa makubwa kwa kilimo kupitia umwagiliaji na kupata nishati ya umeme kwenye maporomoko.

SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO NA NCHI ZA MISRI NA ALGERIA KUANDAA MAKUBALIANO YA KUUZA TUMBAKU YA TANZANIA

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeanzisha mazungumzo na nchi wanachama wa COMESA na nchi kama Misri na Algeria kupitia balozi zake ili kuandaa Makubaliano Maalum (Bilateral Agreement) yatakayoiwezesha Tanzania kupeleka tumbaku kwa kodi nafuu. 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mhe Edwin Amandus Ngonyani Mbunge wa Namtumbo aliyetaka kufahamu Wizara ya Kilimo inashirikianaje na Wizara nyingine zinazohusika na uwekezaji wa mambo ya nje kutafuta soko la tumbaku nchini Misri badala ya kulazimika kutumia nchi za Uganda na Kenya pekee.

Mazungumzo hayo yamefikia hatua nzuri na matarajio ni kufungua milango ya soko hilo na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na taifa kwa ujumla. Aidha, Makubaliano hayo yakikamilika Tanzania inaweza pia kuuza chai nchini Misri na Algeria kwa faida kuliko ilivyo hivi sasa au badala ya kuuza chai kupitia mnada wa Mombasa nchini Kenya.

Mhe Bashungwa alisema kuwa mwaka 2014/2015 uzalishaji wa tumbaku ya moshi (Dark Fire Cured Tobacco – DFC) ulisimama mkoani Ruvuma kutokana na kukosa soko. 

Hata hivyo, Jitihada za Serikali ikawezesha Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited (PATL) kuonesha nia ya kununua tumbaku hiyo ya DFC ambayo nchini Tanzania huzalishwa katika Wilaya ya Namtumbo na Songea Vijijini Mkoani Ruvuma. 

Alisema Kampuni hiyo ilieleza kuwa lipo soko kubwa la tumbaku aina ya DFC nchini Misri na Algeria lakini tumbaku ya Tanzania inauzwa kwa bei ya juu kutokana na kodi inayotozwa ikilinganishwa na aina hiyo ya tumbaku kutoka nchi za Uganda na Kenya kwa kuwa nchi hizo (Uganda, Kenya, Algeria na Misri) ni wanachama wa jumuiya ya COMESA na kwa hiyo kodi za kuingiza tumbaku, chai na bidhaa nchini Algeria na Misri kutoka Uganda na Kenya ni za chini. 

Mhe Bashungwa alisisitiza kuwa, ili Tanzania iuze tumbaku, chai na bidhaa nyingine katika nchi za Algeria na Misri kwa faida, inatumia nchi zilizo kwenye jumuiya hiyo kama Uganda na Kenya.

Kadhalika, Mhe Bashungwa alisema kuwa Wizara ya Kilimo inaendelea kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo tayari soko la mahindi limepatiwa ufumbuzi kwa Wizara kuingia mkataba wa mauziano na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuingia mikataba ya masoko ya uhakika kwenye mazao ya kimkakati na mazao mchanganyiko.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MASOKO NCHINI

0
0
Afisa Mradi wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika masoko ya Mbagala Rangitatu na Kampochea ujulikanao kama Mpe Riziki si Matusi, Shabani Rulimbiye (kushoto), akitoa mada wakati akitoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ukatili wa kijinsia kwa maofisa wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mafunzo hayo ya siku moja yaliandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).
Afisa Ustawi wa Jamii, Getruda Nyagabona (kushoto) kutoka Manispaa ya Temeke akizungumza katika semina ya siku moja ya namna ya kupinga ukatili wa kijinsia masokoni iliyoandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii, Magrida Mumba.
Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada kwa makini.
Mwenyekiti wa Soko la Kampochea, Hemed Said Njiwa akichangia jambo. 
Majadiliano katika makundi.
Majadiliano wa kazi za makundi.
Ofisa Mtendaji wa Mbagala Rangitatu, Morris Ssendi (kushoto), akichangia jambo wakati wa kazi za makundi.
Afisa Ustawi wa Jamii, Magrida Mumba, akichangia jambo.
Katibu wa Soko la Mbagala Rangitatu, Frank Mapolu akichangia jambo kwenye semina hiyo.


Na Dotto Mwaibale


HALMASHAURI za miji zimetakiwa kuboresha miundombinu ya masoko kwa kuwa yanachangia asilimia kubwa ya pato la Serikali za mitaa nchini.

Ombi hilo limetolewa na Afisa Mradi wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika masoko ya Mbagala Rangitatu na Kampochea ujulikanao kama Mpe Riziki si Matusi, Shabani Rulimbiye unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG) wakati akitoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ukatili wa kijinsia kwa maofisa wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Maofisa walionufaika na mafunzo hayo ni maofisa ustawi wa jamii,maendeleo ya jamii, watendaji wa kata, askari polisi kutoka dawati la jinsia na viongozi `wa masoko. 

Alisema masoko mengi ambayo yanaendeshwa na sekta binafsi ambayo imetoa ajira mara tano ya ajira zilizo sekta rasmi na kuokoa wanawake wengi na watoto wao miundombinu yake ni mibovu na hayajawekewa sera na usimamizi wa kisheria kuanzia mazingira ya kazi, kipaumbele kwa makundi maalumu na zaidi ukatili wa `kijinsia `uliokithiri.

"Pamoja na kua ni kimbilio la wahanaga wa mfumo dume, sekta hii pia ni chachu kubwa sana ya maendeleo ya mwanannchi binafsi, serikali za mitaa na Taifa kwa ujumla ambapo takwimu zinaonesha kuwa Halmashauri zinategemea zaidi masoko kwa kuchangia kipato" alisema Rulimbiye.

Aliongeza kuwa pamoja na sekta hii isiyo rasmi kuwa ni chanzo kikubwa cha ajira na kuchangia asilimia kubwa ya pato la Taifa, mazingira yake yanafanywa kama chaka la utovu wa nidhamu na wahanga wakubwa ni wanawake, ambao ni wengi ambao pia wakati mwingine hujumuika na watoto wao.

Afisa Ustawi wa Jamii, Getruda Nyagabona alisema kesi nyingi za ukatili wa kijinsia zimekuwa zikitatuliwa kwa ushiriano baina yao na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini jambo ambalo limesaidia kupunguza vitendo hivyo.

Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia wafanikiwa kupata ufadhili wa masomo (scholarship) 160 kwa Watanzania

0
0
Katika jitihada za kutafutia Watanzania nafasi za masomo nje ya nchi, Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia umefanikiwa kupata ufadhili (scholarships) kwa wanafunzi 160 katika fani mbalimbali. 


Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt Ramadhani Dau, Ufadhili huo ambao umetolewa na Chuo Kikuu cha UNISEL (University of Selangor) kilichopo Kuala Lumpur una thamani ya USD 1,851,860 sawa na shs 4,287,084,410 za Tanzania.

Dkt. Dau amesema ufadhili huo wa masomo utahusu fani zifuatazo:

1. Bachelor of Civil Engineering 

2. Bachelor of Electrical Engineering 

3. Bachelor of Mechanical Engineering 

4. Bachelor of Occupational Health and Safety 

5. Bachelor of Medical Laboratory 

6. Bachelor of Industrial Biotechnology 

7. Bachelor of Computer Science 

8. Bachelor of Information Technology 

Chuo Kikuu cha Selangor ni miongoni mwa vyuo vya Serikali ambacho kilianzishwa mwaka 1999 na kina program za masomo zaidi ya 90 kwenye ngazi mbalimbali kuanzia stashahada hadi shahada ya uzamivu (PhD).  Kwa sasa UNISEL ina wanafunzi
13,500 

 Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akipokea barua rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa 
Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akipokea barua rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa 

Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
 Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa barua rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
 Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akitembezwa kwenye maeneo mbalimbali ya chuo baada ya kukabidhiwa barua rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau akitembezwa kwenye maeneo mbalimbali ya chuo baada ya kukabidhiwa barua rasmi ya ufadhili huo wa masomo kutoka kwa Profesa Dkt. Mohammad Ridhwan Othman wa Chuo Kikuu cha UNISEL University of Selangor jijini Kuala Lumpur leo


TECC YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA WILAYANI KIBAHA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

0
0
VICTOR MASANGU, KIBAHA

VIJANA wapatao 35 katika halmashauri ya mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani ambao walikuwa wanakabiliwa na wimbi la ukosefu wa upatikanaji wa ajira wamepatiwa mafunzo maalumu ya ujasiriamali kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na tatizo la umasikini.
Hayo wamebainishwa na Meneja wa Taasisi ya ujasiramali na ushindani Tanzania (TECC) Anna Manuti wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku 11 ya ujasiliamali kwa baadhi ya vijana waliopo katika halmashauri ya mji Kibaha ambayo yameandaliwa kwa lengo la kuwapa mbinu mbali mbali zitakazoweza kuwasaidia kujiajiri na kuacha na kuwa tegemezi.
Aidha Meneja huyo amebainisha kuwa katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili baadhi ya vijana wameamua kuwakutanisha vijana hao kwa lengo la kuwawezesha kwa kuwapatia elimu ambayo itawapa fursa ya kuanzisha biashara zao wenyewe lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
“Hii programu ya kuwawezesha vijana mafunzo ya ujasiriamali tunaifanya kwa kipindi cha miaka miaka mine na inatarajia kumalizika mwaka 2020 na kwa sasa huu ni mzunguko wa sita ambapo katika halmashauri ya mji wa kibaha vijana wapatao 35 wamepata fursa ya kupatiwa mafunzo haya ambayo yatawea kuwasaidia kuweza kujiajiri wao wenyewe,”alisema Anna.
Kwa upande wake Meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani Behata Minga amesema programu ya kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali itawasaidia vijana kujiajiri wao wenyewe kutokana kuanzisha viwanda vidogovidogo lengo ikiwa ni kujikwamua kiuchumi na kupambana na wimbi la umasikini.

“Kwa kweli mradi huu wa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana hasa katika Mkoa wetu wa Pwani na sisis kama Sido tutahakikisha tunashirikiana bega kwa beda na taasisi hii ya TECC ambayo imefanikisha kuwakusanya vijana hawa na kuwapa mahalifa ambayo yatawasaidia kupata ajira pamoja na kuanzisha viwanda vidogividogo,”alisema Mlinga.

Nao baadhi ya vijana ambao wameshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Selemani Shabani pamoja na Azaria Namga wamesema kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na ajira, ukosefu wa mitaji ya biashara hivyo wameiomba serikali ya awamu yatano kuwasaidia kwa halina mali ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.
MRADI huo wa kuwawezesha vijana kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali unatekelezwa katika mikoa mine ya Jiji la Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara pamoja na Pwani ambapo hadi sasa katika mikoa yote hiyo vijana wapatao 894 wamenufaika na programu hiyo ambayo inatarajia kumalizika mwaka 2020.

BUNGE KUISHAURI SERIKALI KUTEKELEZA AZIMIO LA MALABO KUTENGA ASILIMIA 10 KWENYE BAJETI YA KILIMO

0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa bunge limejipanga kuishauri serikali kutekeleza azimio la Malabo la kutenga Asilimia 10 ya bajeti kwa ajili ya usalama wa chakula na suala la lishe bora kwa jamii.

Akizindua jukwaa la majadiliano ya Usalama wa chakula ya mabunge ya Afika mashariki na kusini iliyoandaliwa na Bunge la Afrika mashariki Ndugai alisema kuwa changamoto kubwa kwenye sekta ya kilimo bado bajeti yake haijatekelezwa kwa asilimia japo 30 hivyo kwa kuanzia angalau kwenye bajeti za maendeleo za nchi zetu tukaanzia na asilimia 10

Amesema kuwa pamoja na serikali kujitahidi bado kunachangamoto kubwa ya lishe duni na udumavu katika jamii hivyo kama tunataka kufikia kwenye maendeleo ya kiuchumi tunahitajika kujenga miundombinu ya kufikika kwa wakulima wetu sanjari na kuhimiza kilimo na ufugaji kwa kutenga bajeti inayoakisi kufikia huko.

“Changamoto ninaoyoiona leo kwetu kama nchi za bara la afrika ni kutoona umuhimu wa kujipanga kutekeleza azimio la Malabo baada ya viongozi wetu wa mataifa ya bara hili kuipitisha mwaka 2014 kuhusu usalama wa chakula hivyo muhimu kama nchi zetu kuweka maazimio kama mabunge linalotaka kila nchi kwenye bajeti yake ikaweka asilimia 10 kwa ajili ya sekta ya kilimo mifugo na uvuvi”alisisitiza Ndugai.

Kwa Upande wake Mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Asha Abdallah Juma(Mshuwa)ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuwa na usalama wa chakula ili kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto kwa kukosa lishe bora kwenye miaka mitatu ya mwanzo.

Amewataka wa Bunge kutotunga Sheria pekee na wajikite kuwa na mashamba ya mfano Kwa wananchi wanaowaongoza kuibua uzalishaji na kilimo kikue hapo tutapata maendeleo ya kiuchumi.

"Sisi Kwa mfano tulianzisha chuo maeneo ya chukwani Kwa lengo la kuwezesha jamii kutumia eneo dogo kuzalisha Kwa tija ili tunapopata nafasi tuitumie vizuri kuzalisha chakula Kwa wingi"

Mshuwa alieleza kuwa warsha hizo ni nzuri Sana kwani zinasaidia nchi zetu kuondoa changamoto zinazotukabili ikiwemo ukosefu wa Ardhi Kwa ajili ya uzalishaji inayotufanya kutokuwa na usalama wa chakuli na lishe duni.

Nae mbunge wa Babati vijijini Jituson alisema kuwa mkoa wa Manyara ni wazalishaji wakubwa lakini udumavu bado ni changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa lishe Bora Kwa watoto wanaozaliwa hivyo kuiomba serikali kuona umuhimu wa kuongeza bajeti yetu kwenye kilimo mifugo na uvuvi.

Ameitaka jamii kurudi Kula vyakula vya asili ambavyo havina wanga mwingi na kuacha Kula vyakula ambavyo vitasababisha miili kukosa afya Bora.

ZIARA YA RC MAKONDA YAZIDI KUIBUA MADUDU UJENZI WA BARABARA

0
0
*Afurahishwa na ujenzi wa ofisi za walimu kwa hisani ya mkandarasi Madale

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

ZIARA ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda imeendelea kwa kutembelea Manispaa ya Kinondoni na kukagua miradi ya kimaendeleo huku akiibua ubadhirifu mkubwa wa fedha unaofanywa katika miradi hiyo hasa barabara.

Akikagua barabara ya Kilonga wima inayojengwa kwa hisani ya benki ya dunia Makonda amegundua fedha ya ziada takribani shilingi milioni 800 inayotumiwa na kandarasi hiyo ukilinganisha na barabara zinazosimamiwa na wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA)

Mshauri wa mradi mhandisi Henry Ngogolo amemweleza mkuu wa Mkoa kuwa barabara hiyo inajengwa kwa shilingi bilioni 2.5 kwa kilometa huku TARURA wakijenga barabara za kilometa hizo kwa shilingi bilioni 1.5.

Makonda amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kutafuta namna kuhusiana na ujenzi wa barabara za jiji hilo hasa katika usimamizi na washauri wa miradi hiyo ili kuweza kuokoa fedha na kusaidia wananchi kutatua kero nyingine na sio kurundika fedha kwenye mradi mmoja ambao bado hautekelezwi vizuri.

Aidha Makonda ametembelea na kukagua ujenzi barabara ya Salasala iliyosimamiwa na TARURA na imekamilika kwa gharama ya shilingi milioni 900 kwa mita 700 walizopatiwa kwa matengenezo.

Pia akiwa Salasala amekutana wananchi ambao walieleza hofu zao za kubomolewa nyumba zao ambazo zimepita katika mkondo wa maji na reli na RC Makonda amewatoa hofu kwa kuahidi kushughulikia suala hilo.

Aidha ziara yake imemulika katika Shule ya Sekondari ya Kisauke Madale ambayo ilikuwa na changamoto ya kukosa ofisi za walimu na vyoo hali iliyopelekea walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja.

Akiwa shuleni hapo Makonda amefurahishwa kasi ya ujenzi wa ofisi za kisasa kwa ajili ya walimu zinayojengwa na kandarasi inayojenga barabara ya Goba, Madale hadi Wazo bure ikiwa ni mchango wao katika kusaidia sekta elimu.

"Nilipofika hapa kwa mara ya kwanza mazingira ya utendaji kazi kwa walimu yalinihuzunisha, hasa kwa kukosa ofisi na kuchangia vyoo na wanafunzi, na nilimwomba mkandarasi anayekarabati barabara ya Goba Madale awaangalie kwa hilo na ninafurahi kwa kazi nzuri na ya mfano inayofanywa na kandarasi hii" ameeleza Makonda.

Aidha amewataka wanafunzi kuangalia malengo yao na kuweka nidhamu mbele ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao ambapo kupitia mkuu wa shule hiyo Fadhili Mutarubukwa wamemshukuru mkuu wa Mkoa kwa moyo na uthubutu wa kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili tangu mwaka 2009 na wamehaidi kutokomeza  daraja sifuri katika matokeo ya kidato cha nne ili kuonesha thamani ya elimu bure inayotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kisauke iliyopo Madale jijini humo ambapo amewataka wazingatie masomo yao na kuwa na nidhamu kwa walimu wao, jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitoa maelekezo kwa viongozi alioambatana nao mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Salasala na kuzungumza na wananchi waliotoa kero zao hasa hofu ya kubomolewa nyumba zao, jijini Dar es Salaam.
Muonekano ya barabara ya Salasala jijini Dar es Salaam.

AJALI ZA MAJINI 300 HUTOKEA KILA MWAKA MKOANI MWANZA

0
0

Na. OWM, MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amebainisha kuwa takribani ajali za majini  zaidi ya mia tatu huripotiwa kuwa zimetokea mkoani humo. Ajali hizo ni zile ambazo huripotiwa rasmi  tu  katika mamlaka husika , aidha inasadikika zipo ajali nyingi ambazo hutokea lakini huwa haziripitiwi  kutokana na jiografia ya mkoa huo. Mkoa wa Mwanza una visiwa zaidi ya 162 ambapo kati ya Visiwa hivyo vipo ambavyo watu wanayo makazi ya kudumu na vingine watu huishi kwa muda mfupi.

Akiongea wakati  akifungua Mafunzo kwa Kamati  ya  Usimamizi wa maafa  ya mkoa huo,  yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughulii za maafa Leo, tarehe 17 Aprili, 2019, jiijini Mwanza, Mongella amefafanua kuwa ajali za vyombo vya usafiri hasa vya majini zinaweza kupunguzwa sana kama wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivyo watazingatia sheria na Kanuni  zinazotawala uendeshaji wa vyombo hivyo.

“Suala muhimu la Kuzingatia ni kuhakikisha mamlaka zetu za serikali za mitaa zinaimarisha utawala bora unaotoa nafasi kwa  jamii kushiriki katika kuzuia na Kupunguza madhara ya majanga, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali baada ya maafa kutokea ikiwa ni pamoja na kutoa elimu, taarifa za tahadhari ya awali kwa wakati muafaka na kuandaa rasilimali zinazohiotajika , Ni wajibu wetu kuhakikisha sheria zinasimamiwa kikamilifu ili kuepuka maafa“ alisisitiza Mongella.

Naye Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, ameitaka Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya mkoa huo  kuandaa Mkakati wa Kupunguza madhara  ya maafa pamoja na Mpango wa kujiandaa na kukabili maafa, Aidha, ameeleza kuwa  Ofisi ya waziri Mkuu imeendesha mafunzo hayo  ili kuijengea uwezo kamati hiyo ambayo ni chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathimini na kutekeleza masuala ya kitaalam kuhusu usimamizi wa maafa, kuzuia na kupunguza madhara ya majanga ya aina zote katika mkoa.

“Upunguzaji wa madhara ya maafa ni suala mtambuka linalohusika katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii sekta zote. Suala la usimamizi wa maafa linahitaji utashi wa kisiasa na kuwajibika kitaalam, kisheria, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi, mipango makini ya maendeleo, ufanisi wa utekelezaji wa sera, mifumo ya tahadhari inayojibu matakwa ya jamii” alisema  Kanali., Matamwe.

Mwaka jana, Mwezi Septemba, mkoa wa Mwanza ulipata maafa makubwa baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kuzama na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200 na wengine 40 waliokolewa. Kufuatia maafa hayo Mkoa huo umeendelea na jitihada za kuzijengea uwezo kamati za Usimamizi wa Maafa za mkoa huo

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughuli za maafa, yamehudhuriwa na wajumbe wote wa Kamati ya Usimamizi wa maafa kwa kuzingatia Kifungu cha 13 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya mwaka 2015.
 Mkuu wa  Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella  akifafanua umuhimu wa kuwa na Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi za serikali za mitaa wakati wa Mafunzo kwa Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Mkoa huo, leo tarehe 17Aprili, 2019, jijini Mwanza., kulia ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri  Mkuu, Jimmy Matamwe, Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu Maafa.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati  wa Usimamizi wa Maafa ya Mkoa wa Mwanza wakifuatilia mafunzo ya Kuijengea Kamati hiyo uwezo wa Usimamizi wa Maafa , leo tarehe 17Aprili, 2019, jijini Mwanza, Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu Maafa.
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri  Mkuu, Jimmy Matamwe akifafanua  umuhimu wa kuwa na Mkakati wa Kupunguza madhara ya maafa, katikati ni Mkuu wa  Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Christopher Kadio, wakati wa Mafunzo kwa Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Mkoa huo, leo tarehe 17 Aprili, 2019, jijini Mwanza, Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu Maafa.
Mkuu wa  Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella  akisalimiana na mjumbe wa  Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Mkoa huo, Shekh, Hassan Kabeke mara baada ya kufungua mafunzo ya kuijengea uwezo  Kamati hiyo, leo tarehe 17Aprili, 2019, jijini Mwanza, Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu Maafa.

Mkuu wa  Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati  wa Usimamizi wa Maafa ya Mkoa wa Mwanza mara baada ya kufungua  mafunzo ya Kuijengea Kamati hiyo uwezo wa Usimamizi wa Maafa , leo tarehe 17Aprili, 2019, jijini Mwanza.Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu Maafa.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

LIVIGHA ATIWA HATIANI KWA KOSA LA KUFUJA FEDHA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Mkuranga, mkoani Pwani, imemtia hatiani, Sifa Livigha kwa kumpa adhabu ya kifungo cha nje na kutotenda kosa katika kipindi cha miezi sita (conditional discharge) baada ya kufuja fedha kiasi cha sh. milioni mbili.

Aidha mshitakiwa ameamriwa kulipa fedha kiasi cha sh. milioni 2 ,alizokuwa anashitakiwa kuzifuja kinyume na kifungu cha 28 cha sheria ya kuzuiana kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 .

Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mkuranga, Janet Kinyage amemtia hatiani ,Livigha kwa mujibu wa kifungu cha 38(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Anasema Livigha alifikishwa mahakamani hapo tarehe 03/05/2018 kwa kosa moja la kufanya ubadhilifu na ufujaji wa fedha hizo kinyume na kifungu cha 28 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mtuhumiwa alikuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Mivule, kijiji cha Mwanambaya wilayani Mkuranga na alifikishwa mahakamani baada ya mwaka 2104 kupokea fedha za ushuru wa kijiji na kuzifuja bila kuziwasilisha ofisi ya kijiji.

Nae kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Suzan Raymond alitoa wito kwa wananchi wote popote walipo kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa, badala yake watumie nafasi walizo nazo katika mapambano dhidi ya rushwa.

Vile vile aliwaasa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa njia ya simu ya bure namba 113 (maarufu kwa jina la Longa Nasi) au kwa kufika ofisini pindi wanapobaini uwepo wa vitendo vya rushwa.

CUF YAANZA KUIMARISHA CHAMA KUWEZA KUSHINDA CHAGUZI ZIJAZO MWAKA HUU NA MWAKANI

0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha 

Chama cha wananchi. CUF kinajipanga kuhakikisha kinashiriki kikamilifu katika Chaguzi mbali mbali hapa nchini ikiwemo Chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020 Kwa kuimarisha chama maeneo mbali mbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Taifa ulinzi wa chama hicho Masoud wakati alipofanya mahojiano na waandishi wa habari jijini Arusha baada ya kutembelea mikoa ya Dodoma Manyara na Arusha kwenye ziara yake ya kuimarisha chama hicho kwenye mikoa mbali mbali nchini.

Amesema kuwa chama cha wananchi CUF kinajipanga Sawa kuweza kutoa ushindani katika Chaguzi hizo baada ya kutoka katika mgogoro wa viongozi waliondoka na kukimbilia ACT hivyo kimeweka mikakati ya kuimarisha chama hicho kujianda na Chaguzi

"Tumejipanga kukiimarisha chama kushiriki Chaguzi Kwa mafanikio ndio maana tumapita kote kuona chama kinahakikisha kinashinda kwenye Chaguzi zilizo mbele yetu"

Amesema kuwa msingi mkubwa wa chama hicho ni UMOJA Kati ya wanachama na kuimarisha misingi ya chama Kwa kuweza kupata viongozi Bora watakaosaidia jamii kutoka kwenye Lindi la umaskini kuelekea kwa kutekeleza Sera ya utajirisho Kwa watanzania.

Awali akimkaribisha mkurugenzi huyo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Arusha Omary Selusingo aliwataka viongozi wa chama hicho kuwa kitu kimoja kujenga.chama Kwa misingi ya umoja na mshikamano ili kuweza kufikia lengo.

Amesema kuwa mikakati ya chama hicho ni kuona changamoto mbali mbali zikitatuliwa ikiwemo chama mkoani hapa kuwa na ofisi zake kila wilaya sanjari na vitendeakazi vitakavyosaidia kukiimarisha chama mkoani hapa.

"Chama mkoani hapa kinakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na ofisi ila tumeweka mikakati ya kuhakikisha kata tano ndani ya Jiji la Arusha chama kinashinda Kwa kuanzia na Chaguzi za serikali za mitaa"
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images