Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Miradi inayotekelezwa sio kikwazo cha mishahara kupanda kwa watumishi wa umma- Naibu Katibu Mkuu Dkt Francis

0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

SERIKALI imesema miradi inayoendelea hivi sasa nchini si kikwazo kinachosababisha mishahara ya watumishi kutopanda.

Pia imesema tayari bodi ya watumishi imeshafanya tafiti zake za kuangalia  viwango vya mishahara kwa kila mtumishi na kuondoa utofauti uliopo kwa baada ya kupanda kila mtumishi atafufurahi.

Imesema kinachosubiriwa hivi sasa ni vikao vya pamoja kwa ajili yakujadili kuhusiana na ripoti hiyo na baadae iweze kupelekwa kwa Rais ili iweze kufanyiwa utekelezaji.Hayo yalisemwa jana na Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menegimenti ya Utumishi wa Umma Dkt.Francis Michael katika mkutano wa 25 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA lililofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Amesema Serikali ina lengo zuri la kutekeleza miradi ya maebdeleo ambayo inatija kubwa katika Taifa.Michael amesema miradi hiyo inatekelezwa na fedha za watanzania na miradi hiyo ni faida kwa watanzania ambao fedha zao zinatumika hivi sasa.

"Faida ya miradi ya maendeleo haiwezi kuonekana leo,lakini baada ya miaka kadhaa tutaona faida ya miradi hiyo,ijapokuwa miradi ya barabara tayari ishaanza kuleta faida na wananchi kuweza kufaidika.Katika mkutano huo,Dk.Michael aliupongeza  uongozi wa TPA kwa ufanyaji wake wa kazi kwa kuwa imekuwa ndio chanzo kikuu cha kuongeza mapato nchini.

Amesema shehena ndio kigezo kikuu cha uendelezaji wa Bandari ya Tanzania ambapo hivi sasa imeongezeka kutoka milioni 14hadi milioni 15.Dk Michael alilitaka Baraza hilo kushirikuana na uongozi wa TPA ili kuweza kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Baraza hilo .Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema,TPA inaendelea kujiwekea malengo ambayo yatakuwa endelevu katika kulisaidia taifa na kukuza uchumi wake.Hata hivo Mhandisi Kakoko amesema dhumuni lao kubwa ni kuongeza shehena nyingi zaidi ili kuweza kuongeza mapato kwa taifa.

,,Uboreshaji wa bandari zetu nchini zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza shehena nyingi zaidi kutoka katika nchi mbalimbali kutokana na kupakana na nchi nyingi ambazo zinategemea bandari zetu"amesema Mhandisi Kakoko.

"Kila nchi inayopakana na bandari zetu za hapa nchini tutafanya nao mazungumzo ili mizigo yao wawe wanaipitisha katika bandari hizo na hilo linawezekana kutokana na mikakati waliojiwekea.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akitoa utendaji wa mamlaka hiyo katika Mkutano wa 25 wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo uliofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) Abraham Lukumay akitoa maazimio ya baraza hilo katika mkutano wa 25 uliofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt Francis Michael akifungua mkutano wa 25 wa baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari uliofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Mgeni rasmi katika picha pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Makao Mkuu
 Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la TPA katika Mkutano wa 25 uliofanyika Mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi la TPA wakisikiliza taarifa mbalimbali za baraza


TASWIRA LA KONGAMANO LA TDC GLOBAL LILIVYOFANA NCHINI SWEDEN

0
0


 Wageni rasmi wakiongozwa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dr. Wilbroad Slaa, wakibadilishana mawili matatu kabla ya kuingia kwenye meli ya abiria iliyotumika kufanyia kongamano la Uwekezaji na uzinduzi rasmi waTDC Global.
 Wadau mbalimbali, Diapora na wawekezaji walifika kuhudhuria kongamano wakijiandaa kuingia kwenye meli.

Kwa picha zaidi bofya soma zaidi





CHEZA SASA NA USHINDE MTAJI NA BIKO,MAMILIONEA NA BODA BODA,

CHAMA CHA ADC CHAFANYA MKUTANO MKUU ZANZIBAR

0
0


-Mwenyekiti Taifa wa Chama cha lliance For Democratic Change(Diara ya Mabadiliko-ADC)Hamad Rashid akisisitiza jambo alipokua akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika Hoteli ya Madinatul Bahri Chukwani Zanzibar.
Mwenyekiti Taifa wa Chama cha lliance For Democratic Change(Diara ya Mabadiliko-ADC)Hamad Rashid akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika Hoteli ya Madinatul Bahri Chukwani Zanzibar.
Baadhi ya Wageni Waalikwa wavyama mbalimbali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha ADC uliofanyika Hoteli ya Madinatul Bahri Chukwani Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change(Diara ya Mabadiliko-ADC)waliohudhuria katika Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Madinatul Bahri Chukwani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (Dira ya Mabadiliko-ADC)Queen Althbat Sendiga akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika Hoteli ya Madinatul Bahri Chukwani Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change(Diara ya Mabadiliko-ADC)Doyo Hassan Doyo akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika Hoteli ya Madinatul Bahri Chukwani Zanzibar.
….

NA Rahma Khamis Maelezo Zanzibar

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa Hamad Rashid Mohammed amewataka wanachama wa chama hicho kufuata ilani yao kwa vitendo ili kupambana na vitendo viovu ikiwemo rushwa na wizi uliyomo katika jamii.

Ameyasema hayo huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar katika Ukumbi wa Madinat Al Bahri wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

Amesema msingi wa Mkutano huo unatokana na matakwa ya katiba ya ADC ambao ndio dira ya maendeleo ya wananchi katika kufikia malengo ya kuchagua viongozi ambao wanaweza na hatimae kushika dola.

Aidha amesema kuwa mkutano huo utawezesha kutambua changamoto zinazowakabili wanachama na kutoa mafunzo ya mara kwa mara ili kutatua changamoto hizo zinazowakabili. Mwenyekiti huyo amefahamisha kuwa umakini wa uongozi wa chama ndio msingi unaohitajika kwani ndio unaoleta maendeleo na kuweza kupata wanachama wapya ambao ndio watakaofikisha chama hicho kule wanakokuhitaji.

Akizungumzia suala la kisiasa amesema kuwa Duniani kote wanazingati a hali ya usalama na amani hivyo anazipongeza Serikali zote mbili kwa kudumisha amani na utulivu uliopo Nchini. Pia amefafanua kuwa ADC ina uwezo wa kusimamia hali ya usalama na amani na ndio mana imefanikiwa hadi leo kufikia Mkutano Mkuu wa chama Taifa na kuchagua Viongozi watakaoweza kusimamia na kuleta maendeleo.

Amesema kuwa suala la Bima ya Afya lazima lifanyiwe kazi ili kuwapunguzia wananchi gharama za matibabu sambamba na kufanikiSha afya bora kwa kila mwananchi. Hata hivyo Hamad Rashid anaunga mkono Serikali suala la elimu bure hadi kufikia chuo kikuu lakini kwa upande wao wamsema kuwa ni hatua kawa hatua hadi kufikia lengo hilo.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa chama ADC Queen Alithbert Sendiga amesema kuwa katika uchaguzi mkuu ujao 2020 anatarajia kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia ADC ili kuweza kuwainua wanawake kimaendeleo.

Aidha amefahamishakuwa wanawake wengi ndio wanaokuwa mbele katika kushiriki mambo mbalimbali laikini wanarudi nyuma kutokana na changamoto zinazowakabili ikiwemo mila na taratibu zinazowazuwia kugombea nafasi hizo.

TPDC YAAZIMIA KUKUZA MATUMIZI YA GESI ASILIA NCHINI

0
0
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mhe. Dustan Kitandula, Mbunge wa Mkinga mkoani Tanga, wamekutana na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kupokea taarifa za maendeleo ya miradi mbalimbali katika taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo. 

Akiwasilisha miradi ya kipaumbele ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Mha. Kapuulya Musomba alieleza kwamba TPDC imeweka kipaumbele katika vipengele muhimu ikiwa ni pamoja na; kuunganisha wateja wapya wa viwandani na majumbani, kuwekeza zaidi katika utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi, kushiriki katika mradi wa gesi ya kimiminika (LNG), kuharakisha utekelezaji wa mradi wa mafuta ya kimkakati (SPR), kuwajengea uwezo wataalamu wa Shirika la TPDC pamoja na kuendelea kutoa taarifa sahihi na kwa wakati juu ya maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi. 

Mhandisi Musomba alieleza kwamba katika kukabiliana na changamoto ya mtaji mdogo wa biashara, TPDC imejipanga kushirikiana na sekta binafsi katika mfumo wa PPP (Public Private Partnership) katika kutekeleza miradi ya usambazaji wa gesi asilia hapa nchini. 

“Usambazaji wa gesi asilia hapa nchini unafanywa kulingana na Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia wa mwaka 2016” anaeleza zaidi Mhandisi Musomba. 

Akiongea wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili kwa Kamati hiyo ya Bunge, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (MB) alieleza mabadiliko ya majukumu ya TPDC kama yalivyoainishwa katika sheria ya Petroli ya 2015 [Petroleum Act, 2015) ambapo TPDC imetambulika kama Shirika la Taifa la Mafuta (National Oil Company-NOC). 

Waziri Kalemani alieleza kwamba TPDC sasa ina jukumu la kujiendesha kibiashara na kusimamia maslahi na ushiriki wa kibiashara wa Serikali katika miradi ya utafiti, uendelezaji, uzalishaji na usambazaji wa mafuta na gesi hapa nchini. 

Waziri Kalemani alisema “Sheria mpya ya petroli pamoja na mambo mengine inaitaka TPDC iachane na uendeshaji ule wa zamani na kujiendesha kama shirika la kibiashara linalotengeneza faida na kukuza mtaji”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dustan Kitandula aliipongeza TPDC kwa jitihada za kusambaza gesi majumbani na viwandani na kuwataka kuongeza kasi ya usambazaji gesi na utafutaji masoko ili kutumia vema bomba kubwa la gesi linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam. 

Mhe. Kitandula aliongeza kwamba kuna fursa kubwa ya matumizi ya gesi asilia hapa nchini na TPDC iziangalie kwa jicho la tatu ili kuweza kufaidika nazo. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ndio yenye jukumu la kuishauri bunge juu ya masuala yahusuyo sekta ya nishati na madini. 

Semina hiyo ya siku mbili ililenga kuangazia maendeleo katika sekta ya nishati na madini pamoja na changamoto zinazohitaji kutatuliwa ili sekta iweze kutoa matokeo chanya zaidi katika uchumi wa Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba akitoa mada mbele ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani) wakati wa semina ya siku mbili kwa wajumbe hao kutoka kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (MB) akikubaliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Mhe. Dustan Kitandula (kulia) wakati wa semina ya siku mbili kwa wajumbe hao kutoka kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa taarifa za maendeleo ya miradi ya nishati katika semina ya siku mbili kwa wajumbe hao kutoka kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati. 

RC NDIKILO AMKABIDHI BAJAJ YA MILION 7.9 ,MLEMAVU WA MIGUU MIWILI

0
0


NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemkabidhi bajaj iliyogharamiwa kiasi cha sh.milioni 7.9 ,mlemavu aliyekatwa miguu miwili kutokana na kuugua ,Domitian Magomba .

Bajaj hiyo ni msaada kutoka kwa mfanyabiashara ,Reginald Mengi,ambae ofisi ya mkoa huo ilimuomba msaada ili amsaidie mzee huyo.

Akikabidhi bajaj hiyo, mhandisi Ndikilo amesema kabla hujafa hujaumbika kwani Magomba alizaliwa mzima na akiwa shule ya sekondari alikuwa mchezaji mpira. 

Alieleza,mzee huyo hakutaka kuendelea kupewa misaada ya fedha kila siku kwakuwa anahudumia familia ndipo alipokwenda ofisini kwake kumuomba msaada huo. 

"Hakukata tamaa kwakuwa anafamilia alikuwa akijakuomba msaada kwangu na baadae akaona aombe msaada wa kimaendeleo, apewe mtaji, nikaongea na mdau Reginald Mengi na nashukuru alikubali ombi hili na kuamua kutoa fedha hizo "alisema Ndikilo. 

Hata hivyo Ndikilo alimkabidhi sh. 150,000 mzee huyo ili imsaidie katika mwanzo wa biashara yake kama kuweka mafuta. Akikabidhiwa msaada huo, Magomba aliishukuru serikali ya mkoa wa Pwani kwa kusikiliza shida za watu wenye mahitaji maalum pamoja na kumshukuru Mengi kwa kusaidia. 




INTRODUCING "UWOYA" BY KAYUMBA

INTRODUCING WIMBO MPYA "LIKES NYINGI" KUTOKA KWA "FREGE & BAD"


INTRODUCING "NILEGEZE" BY LULU DIVA

INTRODUCING "MAPOPO" BY LULU DIVA FT. COUNTRY BOY

Zoezi la Kuunga Reli kwa Umeme, Kichwa cha Treni ya SGR kufanyiwa Majaribio Mwezi wa Saba

Benki ya CRDB yatangaza ufanisi mwaka 2018 huku faida yake ikiongezeka maradufu

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa Benki hiyo ikitangaza faida nono ya TZS 64.1 bilioni ambayo ni ongezeko la asilimia 77% kutoka TZS 36.2 bilioni iliyoipata mwaka 2017, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Benki ya CRDB imetangaza faida nono ya TZS 64.1 bilioni ambayo ni ongezeko la asilimia 77% kutoka TZS 36.2 bilioni iliyoipata mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ongezeko la faida hiyo limetokana na kuimarika kwa mazingira ya biashara na jitihada binafsi za benki kutoa huduma zinazokidhi mahitaji na matarajio ya wateja.

“Mwaka 2018 ulikuwa wa mafanikio kwa Benki ya CRDB. Mapato na faida yetu viliongezeka kutokana na kuimarika kwa mapato halisi ya riba na mapato halisi yasiyo ya riba. Tulifanikiwa pia kuongeza kiwango cha mikopo huku tukishusha uwiano wa mikopo chechefu.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo akifafanua jambo kwa wadau na wanahabari wakati Benki hiyo ikitangaza faida nono ya TZS 64.1 bilioni ambayo ni ongezeko la asilimia 77% kutoka TZS 36.2 bilioni iliyoipata mwaka 2017, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Mikopo tuliyotoa kwa wateja iliongezeka sambamba na amana za wateja huku tukiwafikia wateja wapya kupitia huduma za kidijitali kama vile SimBanking, SIMAccount, mawakala wetu wa CRDB Wakala na kuanzisha mfumo mpya wa baadhi ya matawi yetu madogo kuendeshwa na mawakala binafsi. Tukiwa na mtaji wa kutosha pamoja na ukwasi unaokidhi mahitaji ya uendeshaji, tumeuanza mwaka 2019 tukiwa na uwezo wa kuwapa wateja wetu huduma bora zaidi na kuongeza thamani kwa wadau wetu,” amesema Nsekela.

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio hayo, Nsekela alisema: “Tunajivunia ukweli kwamba tupo kwenye uelekeo mzuri kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea. Lengo si kutyafikia tu, bali Tunakusudia kuyavuka. Tutaongeza kasi zaidi ya utendaji hususani katika ubunifu na utoaji wa huduma za kidijiti zenye ubora wa juu. Tutaendelea kuimarisha na kupitia mara kwa mara mifumo yetu ya utoaji huduma kwa wateja ili kuhakikisha kuwa tunakidhi mahitaji ya soko.”
Mwaka 2018, mapato halisi ya riba ya Benki ya CRDB yaliongezeka kwa TZS 33.1 bilioni na kufika TZS 442.8 bilioni kutoka TZS 409.7 bilioni za mwaka 2017 ambalo ni ongezeko la asimia 8.1 lililotokana na kuimarika kwa mapato ya riba sambamba na kupungua kwa gharama za riba.

“Tumejipanga kutoa huduma kwa namna inayohamasisha uwajibikaji miongoni mwa mteja wetu ndio maana tunajielekeza zaidi kuwapa elimu ya fedha ili kurahisisha jinsi wanavyoweza kukopa na kurejesha kwa wakati,” amesema Bwana Nsekela.

Katika mwaka huo, uwiano wa jumla ya mikopo na mikopo Benki isiyolipika au chechefu ulipungua kwa asilimia 4.1 na kufika asilimia 8.5 kutoka asilimia 13.6 uliokuwapo mwaka2017. “Tumepunguza uwiano huo mpaka wastani wa asilimia 8 na tunataka ushuke mpaka chini ya asilimia 5 mwakani. Hili litawezekana kwa kunyumbua utaratibu wa marejesho ya wateja na kusimamia kw aukaribu mikopo tunayoitoa,” amesema mkurugenzi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akitoa muongozo katika hafla hiyo.

Bwana Nsekela alifafanua kwamba kupungua kwa uwiano wa mikopo isiyolipika ni ishara dhahiri ya kuimarika kwa utoaji na ukusanyaji wa mikopo kulikowezeshwa kwa kiasi kikubwa na kuanzishwa kwa dawati la Usimamizi wa Mali na matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kukusanya marejesho (e-collect) ambao unaratibu na kufuatilia taarifa za wateja.

“Mfumo wa kielektroniki wa kukusanya marejesho unaturahisishia kufuatilia mwenendo wakopaji wetu hivyo kutuweka jirani zaidi na wateja wetu jambo linalomaanisha tunaweza kushauri wakati wowote inapoonekana una dalili ya kufanya vibaya kuepuka mikopo isiyolipika,” amesema.

Ndani ya mwaka huo vilevile, mali za Benki ziliongezeka kwa asilimia 2.3 kutoka TZS 5.9 trilioni Desemba 2017 hadi TZS 6 trilioni mwaka 2018. Ongezeko hilo, tunaamini limetokana na mpango mkakati wa Benki kuongeza kiasi cha mikopo inachotoa ili kuimarisha mapato yatokanayo na riba.

Maeneo muhimu ya ufanisi wa mwaka 2018

· Amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 7.8 na kufika TZS 4.66 trilioni kutoka TZS 4.33 trilioni za mwaka 2017.

· Thamani ya mali za benki ilikua kwa asilimia 2.3 na kufika TZS 6 trilioni kutoka TZS 5.9 trilioni za mwaka 2017.

· Mapato ya riba yaliongezeka kwa asilimia 4.6 hadi TZS 586.3 bilioni kutoka TZS 560.3 bilioni za mwaka 2017.

· Mapato halisi ya riba yaliongezeka kwa asilimia 8.1 na kufika TZS 442.8 bilioni kutoka TZS 409.7 bilioni za mwaka 2017.

· Faida ghafi iliongezeka kwa asilimia 85 na kufika TZS 99.1 bilioni kutoka TZS 53.6 bilioni ya mwaka 2017.

· Faida halisi (baada ya kodi) ilikua kwa asilimia 77 ikifika TZS 64.1 bilioni ikilinganishwa na TZS 36.2 bilioni za mwaka 2017.

· Mikopo iliyotolewa kwa wateja wetu iliongezeka kwa asilimia 8 na kufika TZS 3.1 trilioni ikilinganishwa na TZS 2.9 trilioni iliyotolewa mwaka 2017.







ALL YOU NEEDED TO KNOW ABOUT DENGUE FEVER

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 15,2019.

CREDIT SUISSE BANK: TUTAENDELEA KUIKOPESHA TANZANIA KWA KUWA INAKOPESHEKA NA MAHILI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Washington DC

Benki ya Credit Suisse ya Uingereza imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuikopesha Tanzania ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo baada kuridhishwa na uaminifu wa urejeshaji mikopo kwa wakati pamoja na ubora wa viwango vya miradi inayotekelezwa nchini.

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Washington D.C nchini Marekani na Mkurugenzi wa Masoko ya Kimataifa wa Benki hiyo Bi. Elizabeth Muchemi, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha na Kimataifa inayoendelea Mjini, Washington D.C.

Bi. Elizabeth Muchemi amesema uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya nchi zinazochukua mikopo hazitekelezi ipasavyo miradi iliyoombewa fedha jambo ambalo ni tofauti kwa Tanzania ambayo miradi iliyoombewa mkopo inatekelezwa vizuri na kwa viwango.

Hivi karibuni benki hiyo iliikopesha Tanzania mkopo wa dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi mabalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta miundombinu ya barabara na reli.

"Tuko tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kadri Serikali itakavyoona kwa sababu ya mipango mizuri ya Serikali pamoja na kulipa madeni kwa wakati. Benki ya Credit Suisse haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania katika urejeshaji wa mikopo jambo linaloongeza imani kwa Tanzania" alisema Bi. Elizabth Muchemi.

Akizungumza na Mwakilishi huyo wa Benki ya Credit Suisse katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, katika kikao kilichohudhuriwa pia na Gavana wa Benki Kuu Prof. Florens Luoga, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameishukuru Benki hiyo kwa utayari wake wa kuendelee kushirikiana na Serikali katika ugharamiaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema kuwa Taifa limejipanga kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli, barabara, umeme, maji, elimu, afya, mradi wa gesi kimiminika (LNG), usafiri wa anga na majini, bandari, elimu, ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, mradi ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa wa rasilimali fedha.

Dkt. Mpango amesema Tanzania inataka kutumia uwepo wa nchi zisizopakana na bahari kama vile Burundi, Uganda, Rwanda, na Jamhuri ya Congo kujenga mtandao wa reli ya kisasa na barabara utakao saidia kuchochea biashara na kukuza uchumi wa nchi na ukanda huo kwa ujumla.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko ya Kimataifa wa Benki ya Credit Suisse ya Uingereza Bi. Elizabeth Muchemi, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ubalozi wa Tanzania Mjini Washington ambapo Credit Suisse Bank imeahidi kuongeza mikopo kwa Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati ya Serikali.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko ya Kimataifa wa Benki ya Credit Suisse ya Uingereza Bi. Elizabeth Muchemi, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ubalozi wa Tanzania Mjini Washington ambapo Credit Suisse Bank imeahidi kuongeza mikopo kwa Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati ya Serikali.

Mauaji ya watu saba Yaitikisa Tabora

0
0
Na. Editha Edward

Kamishina msaidizi wa polisi mkoa wa Tabora ACP Emmanuel Nley kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya nzega wanawashikilia watu watano kwa uchunguzi zaidi kutokana na mauaji yaliyofanyika mapema hii leo katika kijiji cha Luzulo kata ya mizibaziba wilaya ya nzega mkoani Tabora .

Tukio la watu hao wamekamatwa na jeshi la polisi Baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa Jina la Nana Maganga (35) kujichukulia sheria mkononi ya kuwauwa watoto sita akiwemo mtoto mmoja wa kaka yake na watoto watano wa kuzaa mwenyewe 

watoto hao waliouawa ni pamoja na pala masanja (3) Shija Dotto(2) Nyawele Dotto (2) Sida Dotto (5) Kulwa Dotto (4) na Dotto Dotto (4)

Kwa upande wa mashuhuda wa Tukio hilo wameileza Michuzi Blog kuwa wamepokea taarifa za mauaji hayo kwa masikituko maana watoto hao walitegemewa kuwa viongozi wa taifa la kesho 

Aidha Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya nzega Bw. Godfrey Ngupula amewataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi za kutekeleza mauaji ya binadamu yeyote maana ni kinyume cha sheria na taratibu za Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya sheria na vyanzo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutafuta muafaka na njia sahihi.
Baadhi ya Wanakijiji wakiwa wamekusanyika kwa huzuni kwenye moja ya nyumba 

 Kamishina msaidizi wa polisi mkoa wa Tabora ACP Emmanuel Nley pamoja na Mkuu wa wilaya ya nzega Bw. Godfrey Ngupula  wakiwa katika eneo la tukio
 Kamishina msaidizi wa polisi mkoa wa Tabora ACP Emmanuel Nley pamoja na Mkuu wa wilaya ya nzega Bw. Godfrey Ngupula  wakiwa katika eneo la tukio 
 Moja ya kifaa kinachodaiwa kutumika kufanyia mauaji hayo

DC KASESELA AWATAKA KKKT KUWA NA UMOJA ILI KUOKOA VYUO VYAO

0
0
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na wanafunzi na viongozi wa chuo kikuu cha Iringa waliokuwa kwenye mkesha wa kuabudu na kuomba na kuwataka waamini wote kujiandaa kabla hawajaanza kusali ili kuweza kuyafikisha maombi yao vilivyo kwa mwenyezi mungu. 
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na moja ya kwaya iliyota burudani siku hiyo ya mkesha wa kuabudu na kuomba
Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuku cha Iringa wakiwa kwenye mkesha huo.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka waamini wote kujiandaa kabla hawajaanza kusali ili kuweza kuyafikisha maombi yao vilivyo kwa mwenyezi mungu.

Akizunguza wakatika wa mkesha na kuambudu kwa wanafunzi wa chu kikuu cha Iringa mkoani Iringa Kasesela alisema kuwa wa kila jambo ambalo unatarajia kulifanya ni lazima ujiandae kwanza.

“Mimi katika maisha yangu kabla sijafanya jambo huwa natafuta muda wa kulifikiria jambo hilo ndio nalifanyia kazi ndio maana mara nyingi nimekuwa na maamuzi sahihi katika kufanya kazi zangu kila wakati” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wanafunzi hao kufanya maombi ya kukiombea chuo hicho ili kuendelea kuwa chuo bora hapa nchini na nje ya nchi na kuendelea kuutangaza mkoa wa Iringa kwa kuwa jina la chuo hicho limebeba jina la mkoa wa Iringa.

“Chuo hiki kilitaka kufungwa kwa ajili ya mambo ambayo hayana miguu wa kichwa hivyo naowaomba mkiombee chuo hiki ili kisije kikafungwa au kufikiriwa kufungwa tena maana kimekuwa kikitoa elimu iliyo bora sana” alisema Kasesela

Aidh Kasesela alisema kwanini kanisa la KKKT limekuwa kanisa ambalo limegawanyika katika kanda mbalimbali ambapo kila ukanda unafanya mambo bila kuwa na ushirikiano wowote ule na dayosisi nyingine.“Ukiangalia maisha ya viongozi wanaofanya kwenye kanda mbalimbali wanatofautiana kuanzia mishahara na maisha yao yamekuwa yanatofauti kubwa sana sasa nawaomba leo hii mliombee pia hili ili kanisa liwe na umoja” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa mgawanyiko huo utasabisha vyou vingi vya KKKT kufa kutokana na kutokuwa na ushirikiano kama ilivyokuwa na vyuo vingine hapa.Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa,Blaston Gavile aliwataka wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa kukesha na kukiombea chuo hicho mara kwa mara.Ombeni nanyi mtapewa kwa kuwa mnaomna kwa nia njemba na mungu nimoto ambao unaweza kuwabariki kila mmoja wetu hapa hivyo nawaomba tena kuendelea kuomba” alisema Askofu Gavile

Askofu Gavile alimushukuru na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa utendaji wake wa kazi kwa wananchi wote kwa kuwa anaitendea haki nafasi hiyo anayoteuliwa na Rais.

SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AWAFUNDA TAWCA,AKUMBUSHA UTHUBUTU ,KUJIAMINI

0
0
 Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanawake Wahasibu nchini baada ya kufunga Mkutano wa Pili wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu(TAWCA)
Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akikabidhiwa vipeperushi vya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) baada ya kufunga mkutano wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini(TAWCA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.TANESCO ndio waliofanikisha kufanyika kwa mkutano huo kwa kuamini utaleta tija katika maendeleo ya nchi hasa kwa kuzingatia ulilenga kuwajengea uwezo wanawake wahasibu
 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SPIKA wa Bunge mstaafu Anne Makinda amewataka Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini( TAWCA)kujiamini,kuthubutu na kuwa na mtandao katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendelo nchini.

Pia amewakumbusha TAWCA wahakikishe wanawajali wanawake wa hali chini kwa kuwajali na kuwasaidia kufanikisha ndoto zao pamoja na kuwaonesha upendo.

Makinda ameyasema hayo wakati anafunga Mkutano wa Pili wa TAWCA ambapo mkutano huo umefanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam .Wahasibu wanawake wa TAWCA wameshiriki mkutano huo.

"Niwapongeze sana TAWCA kwa namna ambavyo mmejadili mambo yenu na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo mlipokuwa kwenye mkutano wenu kupitia mada ambazo zimetolewa.Kwa namna ambavyo mmejipanga na kwa mikakati yenu mtafika mbali sana.Ni wanawake wenye utalaam wenu ambao mnapanga mambo yenu na yanapangika.Hongereni sana," amesema.

Makinda ametumia nafasi hiyo kueleza wanachama wa TAWCA wana kilasababu ya kujiamini katika kufanya mambo ya maendeleo katika jamii yetu na kwamba pamoja na mambo mengine watambue kupanga muda katika kufanya jambo lolote ni jambo la msingi na lenya maana.

"Hakikisheni suala la muda mnalipa kipaumbele kinyume na hapo mambo hayatakwenda sawasawa.Muda ni muhimu katika kupanga maendeleo,pia tengenezeni mtandao ambao nao ni muhimu kwani huwezi kufanya maendeleo peke yako," amesema Makinda.

Kuhusu TAWCA kuwajali wanawake wengine na hasa wale wanaonekana wa hali chini,Mama Makinda amesema ni muhimu wanawake wa chini wakaoneshwa upendo kwani humsaidia kumpa faraja na kubwa zaidi kuhakikisha wanabeba ndoto zao na kuzifanyia kazi.

Wakati anazungumzia wanawake wa hali ya chini,ametoa mfano kwa wadada wanaofanya kazi za ndani ambapo amesema ni muhimu wakathaminiwa badala ya kuzarauliwa na wenye nyumba kisa tu anafanyakazi katika nyumba yako.

"Tuishi vizuri na hawa wanawake(wadada wa kazi) ambao tunaishi nao majumbani.Kwangu mimi huwa nashindwa kumuita dada wa kazi maana naona sitatenda haki.Hivyo Wanawake wahasibu na wanawake wengine kwa ujumla tambue thamani ya hao wadada.

" Wapendeni na kubwa zaidi hakikisheni mnatimiza ndoto zao kwani pamoja na kuwa wanafanya kazi za ndani nao kuna ndoto wanazo.Ukipenda dada wa kazi na kumjali hata ulinzi wa nyumbani mnaongezeka.Unaporudi nyumbani rudi na zawadi ya dada ,atakupenda na atafanya kazi zake kwa bidii,"amesema Makinda.

Kuhusu TAWCA ,Makinda amewema amefurahishwa na namna ambavyo wanawake wahasibu ambavyo wamejipanga kuhakikisha wanatimiza malengo yao na kwa mtazamo wake watafika mbali kikubwa ni kuyasimamia yale ambayo wanakubaliana na kuyaamua kupitia vikao vyao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA) Neema Kiure-Mssusa amesema kikao chao cha siku mbili kimekuwa na mafanikio nakubwa,hivyo kikubwa ni kuyatekeleza kwa vitendo yote ambayo wamekubaliana kama maazimio.

"Kikao chetu kimepata mafanikio makubwa,ndugu washiriki tukayafanyie kazi ambayo tumekubaliana.Pia tuwahakikishie tutaandaa notisi na kisha kuzisambaza kwa wanachama wetu kwa lengo la kukumbusha ambayo tumejadiliana.

" Niwahakikishie yale ambayo yanahitajika kutekelezwa lazima yatekelezwe kwa wakati. Na niwaombe huu ni wakati wa kuendelea kusoma,lazima tusome kwa bidii ili kuongeza maarifa.Kwa kuwa hatusomi hata watoto wetu wakiulizwa wanasema mama hasomi ila afanya kazi.Anajibu hivyo kwasababu hawatuoni tukisoma,hivyo tusome,"amesema.

Ameongeza wanatambua TAWCA wana maono yao mengi lakini moja ya maoni ni kuwa na benki ambayo itakuwa inatokana na Wanawake Wahasibu nchini na hilo watalitimiza.

WANAWAKE WAHASIBU NCHINI TANZANIA SASA WAJIPANGA KUANZISHA BENKI YAO

0
0


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

TAASISI ya Wanawake Wahasibu nchini( TAWCA)imesema moja ya malengo yao makuu ni kuhakikisha wanaanzisha benki yao siku za karibuni na wanaamini hakuna kitakachowakwamisha katika kufanikisha lengo hilo.

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa Pili wa TAWCA uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TAWCA Neema Kiure-Mssusa amewaeleza washiriki zaidi ya 300 waliohudhuria mkutano huo kuwa lengo la kuanzishwa kwa benki litafanikiwa na mikakati waliyoiweka inakwenda vizuri.

"Kutokana na wingi wetu, tuliamua kuanzisha VICOBA na baada ya kuona mafanikio ni makubwa , tukahamia kwenye SACOSS na kwa namna tunavyokwenda ndoto yetu ni kwenda kuanzisha benki. Kikubwa ni kuendelea kushirikiana na kuhakikisha wote tunajiunga kwenye SACOSS ili kufikia lengo la kufungua benki,"amesema.

Kwa upande wake Katibu wa TAWCA Prisca Ndali amefafanua waliamua kuanzisha VICOBA ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wanachama wao kuwa na sehemu ya kutunza fedha na baada ya kuona ni nyingi walamua kuanzisha SACCOS na ndani ya miezi sita wakajikuta wamepata Sh.milioni 70.

"Kutokana na mafanikio ambayo tumeyapata, tukaamua sasa muelekeo wetu ni kuwa na benki yetu ya Wanawake Wahasibu.Kama tulianza na VICOBA na ndani ya muda mfupi tukawa na SACCOS, hivyo hivyo katika muda mfupi ujao unakwenda kuanzisha benki yetu na tukianzisha benki kuna faida nyingi ikiwemo ya kutoa ajira kwa wanawake wengine, katika mkutano wetu wa siku mbili tumezungumza namna ya kuwainua wanawake wengine, hivyo benki hii itasaidia kuwainua wengine,"amesema Ndali.

Amesisitiza kinachowapa matumaini ya kufanikisha lengo la kuwa na benki ni kwamba wamejipanga na wana kila kitu na hata benki itakapoanza hawatakuwa na tatizo katika kuiendesha na kuisimamia kwani wanao watalaamu waliobobea kwenye mambo ya fedha na uhasibu.

Ametumia nafasi hiyo kuendelea kuwahamasisha wana-TAWCA ambao hawajajiunga na SACCOS yao kujiunga kwani kadri wanavyoendelea kujitafakari ndivyo ambavyo wanajichelewesha kunufaika."Katika benki tunaamini haitapita miaka miwili tutakuwa na benki tayari, hivyo ambao hamjajiunga na SACCOS huu ni wakati wenu , jazeni fomu."
Washiriki wa Mkutano wa Pili wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini(TAWCA)wakiwa katika mkutano wao ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia kuanzishwa kwa benki ya wanawake wahasibu

 Mmoja wa washiriki wa Mkutano wa Pili wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini(TAWCA) akifuatilia kwa makini hotuba ya Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda aliyekuwa amealiakwa kufunga mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam

TUCTA IWASHUGHULIKIE VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI WANAOKIUKA KATIBA- DKT FRANCIS MICHAEL

0
0


Na Hussein Stambuli, Morogoro..


Naibu katibu mkuu ofisi ya rais utumishi na utawala bora dr francis Michel amewataka viongozi wa umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuhakikisha wanawaondoa viongozi wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi ambao wanakiuka katiba, miongozo na kanuni za vyama vyao badala yake wanaweka vipaumbele katika marumbano na migongano huku wakiacha kujadili mambo ya msingi kwaajili ya maendeleo ya wafanyakazi..

Akizungumza na kamati tendaji ya baraza kuu la shirikisho hilo katika kikao kilichokuwa na lengo la kujadili na kuchambua jinsi ya kuboresha shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta, dr francis amesema viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanatakiwa kutambua wanajukumu la kutetea maslahi ya wafanyakazi ambao wamewachagua na si masuala binafsi jambo ambalo litawafanya kupoteza wanachama wa vyama hivyo.

“ili kuachana na maslahi binafsi hakuna budi kwa viongozi kufuata katiba, miongozo na kanuni, sasa viko vyama ambavyo viongozi wao wanafanya vitu kwa maamuzi yao binafsi wakilala wakiamka anasema chama kitafanya hivi mara hii katiba haifai tubadili, mfumo huu unavuruga vyama watu wataondoka na chama kikikosa watu hakiendi na nikuombe rais na katibu mkuu tucta mnakazi kubwa si kuongoza tucta tu na kuongoza vyama kama kuna viongozi hawafai muwaondoe” amesema dr francis.

Aidha Rais wa umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamuhoka amesema licha ya serikali kuwa sikivu juu ya masuala mbalimbali ya wafanyakazi bado kuna wafanyakazi wa darasa la saba walioajiriwa tarehe 20 mei mwaka 2004 kwa baadhi ya maeneo wanakabiliwa na changamoto ya kutokurejeshwa kazini licha ya serikali kutoa tamko la kurejeshwa..

“baadhi ya maeneo watumishi hawa hawajarudi kazini na inatokana na tofauti kubwa iliyopo kati ya muajiri mmoja hadi mwingine, maeneo ambayo kunawatumishi waliojaza form za opras na wakajaza wamemaliza kidato cha nne na hawakujaza kwa mapenzi yao walijaza kwa kuelekezwa na maafisa utumishi kwasababu usipojaza kidato cha nne mfumo unakukataa kwasababu mfumo wa ajira serikalini unamtambua mtu mwenye elimu ya kidato cha nne na kukendelea kwahiyo baada ya kujaza fom hizo zimekuja kuwageuka leo wanaambiwa walidanganya baadhi ya halmashauri wamewakubali na baadhi wamewakataa” amesema rais tucta nyamuhoka.

Mwenekiti kamati ya wanawake tucta rehema ludanga amesema wanaishukuru serikali kwa kuwa sikivu hasa kwenye suala la vikokotoo na kuwaomba wafanyakazi nchini wanatakiwa kutambua shirikisho la tucta lipo kwa sababu yao na linafanyakazi kuwawakilisha wao.

“ningependa kuwaomba wafanyakazi nchini kutambua kuwa shirikisho linafanya kazi kwaajili yao na tunawaomba watuamini na tunaendelea kuwatendea kazi na tunashukuru kwa ushirikiano tunaoupata kutoka serikalini inaturahisishia kufanyakazi hasa mfano katika suala la kikokotoo ninaamini na mambo mengine yote yatakwenda vizuri” amesema rehema.
 Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Dkt Francis Michael akizungumza jambo kwenye mkutano huo
 Rais wa umoja wa shirikisho la vyama  huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamuhoka akizungumza na kamati tendaji ya baraza kuu la shirikisho hilo
 Umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika kikao kilichokuwa na lengo la kujadili na kuchambua jinsi ya kuboresha shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta,
Umoja wa shirikisho la vyama vya huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika kikao kilichokuwa na lengo la kujadili na kuchambua jinsi ya kuboresha shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta,_1

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images