Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

KADINALI PENGO ASHAURI WATANZANIA KUTUNZA AMANI, UTULIVU ULIOPO NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu wa Mstaafu Mh Mizengo Pinda akisalimiana na wake wa marehemu Sokoine Mara baada ya kuwasili nyumbani kwa hayati Moringe Sokoine Monduli juu kwa ajili ya misa
Waziri Mkuu wa Mstaafu Mh Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili nyumbani kwa hayati moringe Sokoine Monduli juu kwa ajili ya kushiriki misa
Askofu wa mkuu wa jimbo la kuu katoliki mkoani Arusha Isack Aman akiwa analibariki kaburi la hayati waziri mkuu wa zamani Moringe Sokoine
kadinali Polycarp Pengo akiwa anawasili viwanja vya Waziri mkuu wazamani hayati Moringe Sokoine kwa ajili ya kuendesha ibada ya maadhimisho ya miaka 35

Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushiriki ibada ya maadhimisho ya miaka 35 ya Hayati Moringe Sokoine

Wake wa marehemu Hayati Moringe Sokoine wakiweka kwa pamoja shada la maua katika kaburi la marehemu mume wao



Woinde Shizza Globu ya jamii

WATANZANIA wameshauriwa kutokuwa chimbuko la kuleta mafarakano na uvunjifu wa amani hapa nchini Tanzania badala yake wawe chanzo cha chanzo cha amani kwa taifa letu na dunia kwa ujumla

Ushauri huo umetolewa leo Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wakati akiongoza ibada ya maadhimisho ya miaka 35 ya kumbukumbu ya Waziri Mkuu wa zamani hayati Edward Moringe Sokoine ambapo Misa imefanyika nyumbani kwake nyumbani kwake Monduli Juu mkoani Arusha.

Amesema ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha anailinda amani ya nchi yetu na kutokubali kabisa mtu kujaribu kutushawishi kwa njia yote ile kuvuruga amani ambayo iliasisiwa na wazee wetu wa zamani akiwemo Edward Sokoine pamoja na muasisi wa Taifa hili Hayati Julius Nyerere.

Ameongeza kuwa chimbuko la ukosefu wa amani unatokana na ubinafsi wa watu ambao wamepata uwezo lakini wakataka kuendelea kujikusanyia mali hata kama wengine wanakufa na njaa.

Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dk.Augustine Mahiga amewataka wananchi kujijengea tabia ya kuwa na nidhamu katika kufanya kazi.

"Unajua hayati Sokoine alikuwa ni mchapakazi ,alikuwa anafanya kazi kwa bidii ,pia alikuwa ni kiongozi alikuwa anajua umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na pia alikuwa akikupa kazi na usipoifanya vizuri lazima atakupa adhabu hivyo ni muhimu kuyaenzi yale mema yote aliyoyafanya,"amesema Dk.Mahiga.

Kwa upande wake Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amesema kuwa hayati Sokoine kama mzalendo alihakikisha kuwa wananchi wote wanaishi maisha sawa.Pia alitumia nguvu kubwa kukabiliana na mafisadi pamoja na wahujumu uchumi katika nchi yetu.

Akitoa shukrani kwa wote waliouthuria Misa hiyo mtoto wa hayati Soikoine Balozi Josephy Sokoine amesema kuwa baba yao alikuwa na anatabia ya kusaidia wanyonge pamoja na wale wananchi wasiojiweza, hivyo wao kama familia wameamua kutumia siku hii ya Aprili 12 kwa ajili ya kusaidia wananchi wasiojiweza kwa kutoa kadi za bima ya afya kwa familia 100 ambazo azina uwezo.

Pia amesema wanatarajia kugawa kadi 600 za bima ya afya ambazo wamezitoa bure na kuongeza wametumia siku hii ya leo kutoa dawa kwa ajili ya zahanati ya Monduli Juu ,ambapo alisema kuwa dawa hizo zinathamani ya Sh. milioni 2.3.

MADAKTALI BINGWA WASOGEZWA BUGANDO

$
0
0
Madaktari Bingwa wa MOI, Cuba pamoja na Bugando wakifanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Nyimbi akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika hafla ya kufunga kambi ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu iliyofanyika Bugando.


Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akieleza namna MOI ilivyojipanga kusogeza huduma kwa wananchi kwa kufanya kambi za uapasuaji, katika hafla ya kufunga kambi ya Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu iliyofanyika Bugando
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Bugando Profesa Makubi akitoa taarifa ya namna kambi ya upasuaji iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya MOI ,Bugando na Cuba 

 …………………….

Taasisi ya tiba ya Mifupa MOI,Cuba wameungana kwa pamoja na hospitali ya rufaa ya Bugando katika kambi ya upasuaji wa Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu ambayo ilikuwa inafanyika mkoani Mwanza.

Zaidi ya wagonjwa 400 wamehudumiwa kati yao 17 wakifanyiwa upasuaji mkubwa na jopo la madaktari hao bingwa toka tarehe 8/04/2019 hadi 12/04/2019.

Akihitimisha kambi hiyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt Philisi Nyimbi amemshukuru rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuri kwakufanya maboresho makubwa hapa nchini hususani kwenye huduma za afya.

“Kambi hii ya upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu imeweza kutokana na maboresho yaliyofanya na serikali ya awamu ya tano, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndg. John Mongela tunawashukuru wakurugenzi wakuu wa MOI na Bugando pamoja na madaktari bigwa wote, kwa hili wananchi wa kanda ya ziwa wamenufaika sana”. Amesema Dkt Philisi.

Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respicios Boniface amesema hii ni sehemu ya mkakati wa MOI na serikali kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia wananchi wote hususani wa mikoa ya pembezoni.

“Baada ya serikali kufanya uwekezaji mkubwa MOI, rufaa za nje ya nchi zimepungua sana hivi sasa wa MOI na serikali ni kuhakikisha huduma za kibigwa zinawafikia wananchi wote”. Amesema Dkt.Boniface.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya Bugando Profesa Abeli Makubi ameushukuru uongozi wa MOI kwa kukubali kuleta madaktari bingwa mkoani Mwanza ambao wamewahudumia wakazi wa kanda ya ziwa na kuwapunguzia adha ya kusafiri kwenda Dar es Salaam au nje ya nchi.

“Kwa niaba ya bodi pamoja na menejimenti ya hospitali ya Bugando tunawashukuru wenzetu wa MOI,Cuba kwa kuja kushirikiana nasi hapa kwenye kambi yah ii, tunaamini huu ni mwanzo wa ushirikiano baina ya taasisi zetu wakazi wa kanda ya ziwa wataendelea kunufaika”. Amesema Prof. Makubi..

Taasisi ya MOI imekuwa ikitekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kuhakikisha inawaongezea wananchi wa mikoa ya pembezoni huduma za kibigwa ili kuwapunguzia adha ya kusafiri kuzifuata huduma hizo MOI.

DC MURO NA KKKT MERU WATOA NG’OMBE 20 KWA WANANCHI

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro kwa kushirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Meru Wametoa ng’ombe 20 kwa watu waishio katika mazingira magumu. 

Wakikabidhi ng’ombe hizo Askofu wa dayosisi hiyo Elias Kitoi pamoja na Dc Muro wamesema Kanisa pamoja na Serikali wanashirikiana pamoja na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha wanasaidia wananchi kiroho na kimwili katika kuleta maendeleo yanayolenga kuwaondolea umasikini wananchi 

“Fedha za kununua Ng’ombe hizi zilipatakana kwa shida sana kutoka kwa wadau walioko Marekani , kufuatia mahusiano mazuri kati ya kanisa , serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya utoaji wa ng’ombe 20 wenye thamani ya zaidi ya milioni 20 alisema 

Askofu Kitoi Alisema kama dayosisi ya Meru hawakuliangalia jambo hilo kibinadamu zaidi walimuomba Mungu ili waweze kufikisha mradi huo sehemu husika ambapo walishirikiana na wakuu wa majimbo, wachungaji pamoja na wainjilisti ili kuwapata wale wahitaji katika sharika zao jambo alilosema limefanyika kwa uaminifu. 

Aliongeza kwa kuwataka waliopewa ng’ombe hizo kuwa mawakili wema ili kuwasaidia na wahitaji wengine pindi zinapozaliana huku akisema kuwa wamepatiwa bure bila malipo yoyote isipokuwa katika kila uzao wa kwanza kwa kila ng’ombe atapelekwa Kanisani. 

“Tunatamani muendeleze mradi huu ili wengine wanufaike tumeweka utaratibu kuwa kila Mzaliwa wa kwanza wa ndama jike atapelekwa Kanisani ili apatiwe muhitaji mwingine lakini mzaliwa wa kwanza dume ataletwa kanisani kama Limbuko na hii itakuwa manufaa kwa usharika husika”alisema Askofu. 

katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro alisema anatambua mchango mkubwa wa Kanisa katika wananchi wa Arumeru ambapo hapo awali walishakabidhi mbuzi kwa wananchi hao 

Pia Dc Muro aliwataka wanufaika wa mradi huo kutumia fursa hiyo kikamilifu lengo likiwa ni kutokomeza umaskini katika Jamii ambapo alisema yeyote atakayeshindwa kutunza ng’ombe hao ni vema akarudisha Katika Usharika wake ili apatiwe mtu mwingine ambaye ni muhitaji . 

“Nitoe rai kwa wote mliopatiwa zawadi hii kama mkishindwa kuwatunza ng’ombe hawa warudisheni Kanisani ili wapatiwe wengine wenye uhitaji zaidi na watakaothamini hili”Alisema Dc Muro 

Mkuu huyo wa Wilaya aliahidi kutoa ufadhili wa kuchanja ng’ombe wote kama mchango wake na kuunga mkono juhudi za Dayosisi hiyo ambapo alisema pia atawaunganisha na Afisa mifugo wa Halmashauri ya Meru ili ng’ombe hao wapatiwe huduma stahiki.

Halmashauri zisizotoa 10% kwa Vikundi Kukiona

$
0
0

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani S. Jafo(Mb) amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Walemavu kutoka katika asilimia kumi ya mapato ya ndani kama ilivyoelekezwa kwenye Sheria. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake asubuhi ya Leo Mhe. Jafo amesema Halmashauri zitakazoshindwa kutoa mikopo kwa vikundi hivyo watachukuliwa Hatua kali za kisheria kama ilivyoelekezwa katika Kanuni za utoaji wa mikopo ya vikundi. 

Amesema kuwa licha ya uwepo wa Sheria inayoelekeza suala zima la Utoaji wa mikopo kwa vikundi, utekelezaji wake umekua wa kusuasua sana kwa baadhi ya Halmashauri na hadi kufikia Machi 2019 jumla ya fedha zilizotolewa kwa vikundi ni shilingi bilioni 20.7 ya shilingi bilioni 54.08 zinazopaswa kutolewa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 sawa na asilimia 38.27 ya Lengo. 

“Hivi sasa hakuna kisingizio chochote katika utekelezaji wa sheria hii kwani Serikali imeshatoa Kanuni, zinazoongoza utoaji wa mikopo hiyo na Kanuni hizo zimetangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 141 la Tarehe 5 April, 2019 kwa GN. Na. 286 la mwaka 2019 kwa hiyo Mkurugenzi atakayeshindwa kutekeleza kwa ufanisi atachukuliwa hatua” alisema Mhe. Jafo. 

Aliongeza kuwa katika kipindi hiki kuna Halmashauri 23 ambazo zimefanya vibaya zaidi kwa kutoa mikopo chini ya asimili 20 ya malengo. 

Amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni Nsimbo, Nyasa, Busega, Kondoa Dc, Namtumbo, Kasulu Dc, Bariadi Dc, Msalala, Mbulu Tc pamoja na Njombe Dc. 

Halmashauri zingine ni Kongwa Dc, Musoma MC, Sumbawanga Dc, Kondoa Tc, Uvinza Dc, Ilala Mc, Lindi Dc, Mpwapwa Dc, Bahi Dc, Chamwino Dc, Momba Dc, Temeke Mc, Mbulu Dc na Lindi Mc. 

Wakati huo huo Mhe. Jafo alitoa maelekezo kwa Halmashauri zote kuwa zinapaswa kutoa fedha kwa vikundi kwa mujibu wa Sheria na mpaka ifikapo Juni 30,2019 Halmashari ziwe zimetoa mikopo siyo chini ya asilimia 83 ya fedha zote za mikopo kutoka asilimia 10 ya fedha zote za mapato ya ndani. 

Ameoongeza kuwa mpaka ifikapo Julai 20, 2019 Halmashauri zote ziwe zimetoa mikopo yote kwa asilimia 100 ya fedha zote za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2018/2019. 

“Mkurugenzi yeyote atakayeshidwa kutoa fedha kwa Vikundi kama ilivyoanishwa hapaswi kumlaumu mtu yeyote kwa sababu atachukuliwa hatua kama ilivyo elekezwa kwenye Kanuni za utoaji wa mikopo ya vikundi” amesema Mhe. Jafo. 

Ikumbukwe kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya marekebisho katika Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura Na, 290 katika kifungu 37A ambacho kimeelekeza namna ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu kutoka katika asilimia 10 ya mapato ya ndani. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani S. Jafo(Mb)

ZALISHENI MIFUKO MBADALA KWA WINGI MZIBE PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI -DKT. ANNA MGWIRA

$
0
0


Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif akionyesha wateja waliotembelea katika banda hilo.
Mmoja wa mtendakazi katika kampuni hiyo akionyesha aina ya mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira wataanza kuisambaza kwa wananchi kwa bei nafuu.


Na Vero Ignatus, Kilimanjaro

Wazalishaji wa mifuko mbadala wametakiwa kuchangamkia fursa kuzalisha mifuko kwa wongi ya kukidhi mahitaji ambayo ni rafiki wa mazingira kwani tayari mkoa wa Kilimanjaro umeshapiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira alipotembelea maonyesho ya wiki ya elimu katika uwanja wa Mashujaa Wilayani Moshi ,amesema kuwa wajasiriamali wanaotumia vifungashio vya mifuko ya plastiki wanapaswa kujiianda mpaka muda uliopangwa na serikali Mwezi June mwaka huu waweze kuondokana na matumizi ya plastiki.

“Kwa sasa mkoa wa Kilimajaro ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki tumeanza mapema ili watu wajiandae ikifika mwezi wa sita mwaka huu watu wawe kwenye mstari na kuzoea kutumia mifuko mbadala tunashukuru wenzetu wa Harsho Group wameanza kuzalisha mifuko ya kutosha ” Alisema Dkt.Anna

Nae Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro wamejianda vyema kuzalisha mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira na kuisambaza kwa bei nafuu.

Caroline alisema kuwa wanazalisha mifuko laki 5 kwa siku ambayo inatosheleza mahitaji ya mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani pamoja na Tanzania nzima hivyo wamejiandaa kuzi ba pengo la mifuko ya plastiki.Anaeleza kuwa mifuko hiyo inaweza kufuliwa zaidi ya mara tano na iwapo ikitupwa inaweza kuoza na kuwa mbolea katika ardhi.

Mkazi wa Manispaa ya Moshi Roman Mnzava alisema kuwa hatua ya Mkoa wa Killimanjaro kupiga marufuku matumizi ya plastiki utasaidia kuokoa mazingira na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambao ni kitovu cha utalii mkoani hapa.

JUMUIYA YA WAZAZI MOROGORO KUPATIWA MAFUNZO YA UFUGAJI WA NYUKI NA KILIMO CHA MIHOGO

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Morogoro, Francis Heri Hoza akizungumza na kuunga mkono hoja mbalimbali zilizotolewa na jumuiya ya wazazi na wawakilishi wengine katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo mkoa kwa Morogoro na kukipa kipaumbele kilimo cha misitu na ufugaji wa nyuki.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Francis Henry hozza pamoja na Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Shaka Hamidu Shaka na katibu wa siasa, itikadi na uwenezi mkoa wa Morogoro Anthony Muhando wakisikiliza michango mbalimbali inayotolewa na jumuiya ya wazazi Morogoro.

 *Hozza amesema Morogoro ni mkoa kwa kipekee kwa misitu

Na.Khadija Seif, Globu ya jamii

BARAZA  kuu la wazazi mkoa wa Morogoro limefanyika na kuadhimia kuisaidia jamii kwa kutoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki na  kilimo cha mihogo katika mkoa wa Morogoro ili kuchangia ukuaji wa kiuchumi na kuikwamua jamii katika kutokomeza kasi ya umasikini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea hoja
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro Francis Heri Hozza amesema mkoa wa Morogoro umejaaliwa misitu mingi na ardhi yenye rutuba kwahiyo kama jumuiya inahitajika kutumia fursa hiyo kuanzisha miradi ya kiuchumi kama ufugaji wa nyuki kama zao la biashara lakini pia kama njia ya kuzuia wanyama wasiharibu mazao ya wakulima na kilimo hususani cha mihogo.

Na pia kutoa fursa kwa jamii kujifunza na kuwatafutia masoko ili kushiriki katika kuunga mkono jitihada za mhe Rais katika kutoa fursa za wananchi kujiajiri .

"kazi ya jumuiya ya wazazi sambamba na kufanya shughuli za kisiasa lakini pia ni pamoja na kuisaidia jamii kivitendo kwa kuwajengea uwezo wa kutambua fursa na kuzitumia ," alisema hoza

Hata hivyo hozza ameeleza kuwa  wataalamu wataletwa kutoa mafunzo ya kilimo cha mihogo na ufugaji wa nyuki kwa jumuiya ya wazazi pia wataalikwa wananchi, makampuni, mashirika, vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ili viweze kunufaika na mafunzo hayo.

Alikadhalika hozza amefafanua zaidi kuwa mbali ya kutoa mafunzo hayo kwa umoja wa wazazi wilaya zote lakini pia itazialika jumuiya nyingine za chama, makampuni, watu binafsi, vikundi mbalimbali vya ujasiriamali, asasi za kiraia na watu wa makundi maalumu na kadhalika ili kuwapatia fursa hii muhimu ya kupata utaalamu utakaowawezesha kujiajiri.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Shaka Hamidu Shaka ambae amempongeza katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) dk.Bashiru Ally Kwa uchapakazi wake mzuri hususani mkoani Morogoro ambapo mara kwa mara amefika kushughulikia kero mbalimbali za chama na serikali, na kuitaka jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro kushiriki kikamilifu katika tamasha kubwa la uzinduzi wa kauli mbiu ya Morogoro ya kijani litakalofanyika hivi karibuni.

" Nampongeza  mhe Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa ziara nzuri anazozifanya za kukagua utekelezaji wa ilani ambazo zina matokeo chanya na mafanikio makubwa kwa maslahi ya taifa," alisema Shaka.

Ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro kujitokeza kwenye mafunzo ya ujasiliamari pindi wakufunzi watakapowasili .

Nae katibu wa siasa, itikadi na uwenezi mkoa wa Morogoro Anthony Muhando ameipongeza jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro kwa kufanyakazi vizuri na kuitaka iendelee kusimamia na kuwa mfano wa maadili na malezi ndani ya mkoa.


... Mwisho

UZINDUZI WA MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI MWANZA

$
0
0


Warioba Sanya mwakilishi wa RAS Mwanza, ambaye ni mshauri wa miradi ya usafi wa mazingira (WASH ADVISOR) akieleza wadau hali halisi ya usafi wa mazingira katika jiji la Mwanza, mradi wa usafi wa mazingira jijini Mwanza (Pro poor WASH entreprise) utekelezwe kwa mafanikio.
Mhandisi James Mturi Meneja miradi ya WASH kutoka Amref Health Africa-Tanzania akitambulisha mradi wa usafi wa mazingira jijini Mwanza (Pro poor WASH entreprise) kwa wadau wa mazingira jijini humo

Afisa afya wa mkoa wa Mwanza(R.S.O) Fungo S Masalu, akitoa ufafanuzi wa kuhusu madhara yatokanayo na uchafu wa mazingira katika jiji la Mwanza, pamoja na kueleza namna mradi wa usafi wa mazingira jijini Mwanza (Pro poor WASH entreprise) utakavyowanufaisha wakazi wa jiji hilo.
Wadau wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa usafi wa mazingira jijini Mwanza.

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa uzinduzi wa mradi wa usafi wa mazingira jijini Mwanza.



Jiji la Mwanza lililoko mwaloni mwa ziwa Victoria ambalo ni chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa, lina wakazi takribani 819,796 huku ongezeko la watu likiwa ni asilimia 3.2 kwa mwaka. Asilimia 66 ya wakazi wa jiji la Mwanza hawana huduma za usafi wa mazingira, ambapo zaidi ya asilimia 20 hawana vyoo, huku zaidi ya asilimia 90 ya vyoo haviko kwenye mtandao wa maji taka wa MWUWASSA. Jiji la Mwanza huzalisha taka ngumu kwa wastani wa tani 813 kwa siku, ambapo ni asilimia 74 tu ya taka zinazozalishwa ndio hukusanywa na kupelekwa dampo. Hivyo taka ngumu bado ni chanagamoto kutokana na uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji, hivyo kupelekea milipuko ya magonjwa na vifo hasa kwenye jamii masikini.

Amref Tanzania ikishirikiana na ofisi ya RAS Mwanza, kwa msaada wa kifedha toka Manispaa ya jiji la Madrid nchini Hispania, inaanzisha mradi wa kuboresha usafi wa mazingira kwa watu wenye kipato cha chini kibiashara jijini Mwanza. Mradi huu unalenga kusaidia juhudi za Serikali ya Tanzania kuongeza na kuboresha huduma za usafi wa mazingira kupitia kamapeni ya kitaifa NSC-II (2016-2020); Mkakakati wa Kitaifa wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA-2015) na kufikia Malengo Endelevu ya Millenia (SDGs-2030). Lengo mahususi la mradi ni kuchangia utekelezaji wa mpango mkakati wa jiji la Mwanza wa mwaka 2004 wa kusimamia taka ngumu na kuboresha vyoo.
Mradi huu utawalenga akinamama na vijana katika maeneo ya wakazi wenye kipato cha chini kwa kuwezesha fursa za kukua kiuchumi kwa kufanya ujasiriamali kwa kuzalisha bidhaa mbadala kutokana na taka ngumu na vinyesi. Mradi unatarajia kuongeza fursa kwa jamii nzima katika uelewa na mahitaji ya kusimamia na kuondoa taka katika maeneo ya makazi. Mradi utatoa elimu ya ujenzi wa vyoo bora na huduma za kuondoa vinyesi katika ngazi ya kaya, huku ukiijengea Serikali uwezo wa kutoa huduma kwa kushirikiana na taasisi binafisi/wananchi kupitia mbinu za kibiashara. Mradi huu kwa kuanzia utatekelezwa katika Wilaya ya Ilemela na Nyamagana , ambapo unarajia kufikia walengwa 200,000.
Kuhusu Amref Health Africa.

Amref Health Africa ni shirika la kimataifa lisilo la Kiserikali lililoanzishwa mwaka 1957 kama Madaktari wa Anga (Flying Doctors) wa Afrika Mashariki kwa lengo la kutoa msaada wa matibabu katika maeneo magumu kufikika ndani ya Afrika Mashariki. Mwaka 1987, Amref Health Africa ilifungua rasmi ofisi yake jijini Dar es Salaam Tanzania, ikiwa na lengo la kuchangia juhudi za Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya kuboresha huduma za afya na maendeleo ya Jamii kupitia sera na miongozo ya afya ya kitaifa. Kwa sasa Amref iko katika nchi 35-barani Africa, Asia, Ulaya na Marekani.

Hivi sasa, Amref Health Africa Tanzania ina miradi zaidi ya 25 katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania (takribani asilimia 45 ya miradi yote inatekelezwa katika mikoa ya kanda ya ziwa). Vile VileAfrica Tanzania ina miradi yenye mtazamo wa Kitaifa kama vile mpango wa elimu kwa njia ya masafa (eLearning) na mradi wa kuimarisha Maabara. ambao unatekelezwa katika mikoa tofauti nchini ikiwemo na Zanzibar. Miradi Amref nchini Tanzania imegawanyika katika maeneo makuu manne ambayo ni: Afya ya uzazi, watoto wachanga na vijana (RMNCAH); Mpango wa Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (DCP) ambao unajumuisha programu za VVU na UKIMWI, Kifua Kikuu (TB), Huduma za Maabara, Fistula ya Uzazi na Malaria; Maji safi, Usafi wa mazingira na mwili (WASH) na Mpango wa Kujenga Uwezo kupitia mafunzo (Capacity Building).


Kupitia miradi hii, Amref Health Africa imeendelea kujibu vipaumbele vya afya ya kitaifa na malengo ya maendeleo endelevu katika kushughulikia mahitaji ya afya ya wanawake na watoto. Amref Health Africa inajitahidi kuongeza ufanisi na uendelevu wa huduma hizi kwa kiuchangia kuimarisha mifumo ya afya, kuboresha upatikanaji wa huduma na kuhamasisha mifumo ya afya ya jamii na sera kwa ujumla. Pamoja na mkakati wake mpya wa 2018-2022, badoAmref Heath Africa ni msaidizi mkubwa wa ajenda ya Huduma ya Afya kwa Wote.
Jifunze zaidi kuhusu Shirika la Amref Health Africa kupitia www.amref.org

Kwa habari zaidi, Tafadhali Wasiliana na ,
Idara ya Mawasiliano ya Amref Health Africa Tanzania ,
Eliminatha.paschal@amref.org

KUKAMILIKA KWA OFISI YA RAIS,MJI WA SERIKALI...WANANCHI DODOMA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge amesema wananchi wa Mkoa wa Dodoma wanamshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuhamisha rasmi shughuli za makao makuu ya Serikali mkoani humo tena kwa vitendo.

Dk.Mahenge amesema baada ya Rais Magufuli kutangaza Serikali kuhamia Dodoma ,wananchi wameshuhudia zikitengwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo mikubwa inayofanyika kwa vitendo na wananchi wanaona utekelezaji unavyoendelea.

Akizungumza leo Aprili 13,2019 wakati wa uzinduzi wa Mji wa Serikali mkoani Dodoma ambapo Dk.Mahenge amesema Rais Magufuli ameandika historia kwa uamuzi wake wa kuamua shughuli za Serikali kuhamia Dodoma rasmi na kutekeleza maagizo yake kwa vitendo.

Amesema ujenzi wa soko kubwa la.kisasa,kituo kikubwa cha mabasi,hospitali,shule na miundombinu mingine inaendelea kutekelezwa na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake na wananchi wamekuwa mashahidi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea ndani ya Dodoma.

"Wananchi wa Dodoma wanashukuru kwani maamuzi yako Rais Dk.Maguful yamesababisha uchumi wa Dodona kukua kwa kasi kubwa na sasa wananchi wanafurahia uwepo wa Serikali.

"Baada ya kuanza kutekelezwa kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo shughuli za ukuaji uchimi nazo zimeshika kasi hapa Dodoma.Tunakushukuru Rais kwa uamuzi wako," amesema Dk.Mahenge.

Amefafanua kuwa wakati leo zikizonduliwa ofisi za wizara na nyumba Serikali tayari jana na juzi baadhi ya mataifa yakiwamo ya China,Ujeruman Na Umoja wa Mataifa(UN)/wamefungua ofisi zao katika Mkoa huo wa Dodoma.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Watanzania kwenda kuwekeza Mkoa wa Dodoma kwani kuna kila kitu na maeneo ya uwekezaji yapo na yamepimwa,hivyo haoni sababu ya wawekezaji kuchelewa kwenda kuwekeza ndani ya mkoa huo.

Awali Waziri Mkuu mstaafu John Malecela amesema Rais Dk.Magufuli jina lake libaki katika mioyo ya wananchi wa wa Mkoa Dodoma na kwamba hivi sasa unaipotaja Dodoma unataja na Magufuli.

Uamuzi wako wa kuhamishia shughuli rasmi Dodoma ,Rais wetu unabaki kwenye mioyo ya wananchi wa Dodoma .Tutakumbuka kwa kizazi hiki na kizazi kijacho kadri dunia itakavyoendelea kuwepo,"amesema Malecelela.

Kwa kukumbusha tu Rais Magufuli Julai 25, 2016 alitoa tamko la kuhamishia Serikali Dodoma kutola Dar es Salaam kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi wote na hatimaye leo hii Serikali imeshahamia Dodoma kwa kukamilika kwa Mji wa Serikali pamoja na ofisi ya Rais iliyoko Chamwino ambayo nayo imekamilika.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge

BENKI YA DUNIA KUIJAZA TANZANIA MKOPO NA MSAADA WA SHILINGI TRILIONI 4 KWA AJILI YA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Washington D.C
BENKI ya Dunia imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu na msaada wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.7 sawa na takriban shilingi trilioni 4 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.
Ahadi hiyo imetolewa mjini Washington D.C nchini Marekani na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.
Bw. Ghanem amemhakikishia Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwamba uhusiano kati ya Serikali na Benki yake bado uko imara na kwamba benki hiyo iko tayari kushirikiana na Tanzania ili iweze kufikia maendeleo yanayo tarajiwa.
Miongoni mwa miradi itakayonufaika na mkopo na msaada huo ni mpango wa elimu ambapo benki hiyo imeongeza ufadhili kutoka dola milioni 300 hadi dola milioni 400 na mradi wa kusaidia kaya masikini kupitia TASAF ambapo benki hiyo imeamua kuongeza kiwango cha fedha kutoka dola milioni 300 hadi kufikia dola milioni 450.
Kiasi kingine cha fedha kitatumika kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta za miundombinu ya barabara, maji, Tehama, Afya, kilimo, hifadhi ya jamiim Nishati, utawala bora, lishe, sekta ya fedha, biashara, mazingira na maliasili pamoja na maji nk.
Akizungumza kwenye kikao hicho Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Benki hiyo namna inavyoisaidia nchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii ambapo mpaka sasa Benki hiyo imefadhili miradi 21 ya maendeleo kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 4.8, sawa na takriban shilingi trilioni 11.
Ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa masuala mbalimbali na kuiomba benki hiyo iendelee kuisaidia nchi ili iweze kufikia maendeleo yaliyokusudiwa ikiwemo kuondoa umasikini wa  wananchi.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, ukimshirikisha pia Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, upo mjini Washington D.C nchini Marekani kuhudhuria mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, taasisi ambazo Serikali ina hisa.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akifurahia jambo lililozungumzwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem (hayuko pichani) wakati wa mkutano wa ujumbe wa Tanzania na uongozi wa Benki hiyo Mjini Washington D.C, Marekani. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi-Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omar na kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga.
 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem, akiihakikishia Tanzania kwamba Benki yake itaipatia dola za marekani bilioni 1.7 ili iweze kutekeleza miradi yake mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha mwaka mmoja ujao wa fedha 2019/2020.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila (kulia) na Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mary Maganga, wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mi[pango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bw. Hafez Ghanem (hawako pichani) mazungumzo yaliyofanyika Mjini Washington D.C, Marekani, ambapo Benki hiyo imeahidi kuipatia Tanzania karibu shilingi trilioni 4 kwa ajili ya kutekeleza miradi yake mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mwaka wa Fedha 2019/2020.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem, Mjini Washington D.C nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Wilson Masilingi (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga (kushoto) kabla ya kuanza kwa mkutano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Hafez Ghanem, Mjini Washington D.C nchini Marekani. (Picha na Benny Mwaipaja, WFM, Washington D.C)

WAZALISHAJI MIFUKO MBADALA KUZIBA PENGO LA MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud,Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr.Anna Mghwira amewataka Wazalishaji wa mifuko mbadala ambayo ni rafiki wa mazingira kuchangamkia fursa ya kuzalisha kwa wingi mifuko na kukidhi mahitaji ya mifuko kwani tayari mkoa huo umepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

Mghira alisema hayo akitembelea maonyesho ya wiki ya elimu katika uwanja wa Mashujaa Wilayani Moshi ,amesema kuwa wajasiriamali wanaotumia vifungashio vya mifuko ya plastiki wanapaswa kujiianda mpaka muda uliopangwa na serikali Mwezi June mwaka huu waweze kuondokana na matumizi ya plastiki.

“Kwa sasa mkoa wa Kilimajaro ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki tumeanza mapema ili watu wajiandae ikifika mwezi wa sita mwaka huu watu wawe kwenye mstari na kuzoea kutumia mifuko mbadala tunashukuru wenzetu wa Harsho Group wameanza kuzalisha mifuko ya kutosha ” Alisema Dr.Anna

Mratibu wa Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro wamejianda vyema kuzalisha mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira na kuisambaza kwa bei nafuu.

Caroline alisema kuwa wanazalisha mifuko laki 5 kwa siku ambayo inatosheleza mahitaji ya mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani pamoja na Tanzania nzima hivyo wamejiandaa kuzi ba pengo la mifuko ya plastiki.

Anaeleza kuwa mifuko hiyo inaweza kufuliwa zaidi ya mara tano na iwapo ikitupwa inaweza kuoza na kuwa mbolea katika ardhi.

Mkazi wa Manispaa ya Moshi Roman Mnzava alisema kuwa hatua ya Mkoa wa Killimanjaro kupiga marufuku matumizi ya plastiki utasaidia kuokoa mazingira na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambao ni kitovu cha utalii mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr.Anna Mghwira

MNYETI AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza ofisini kwake mjini Babati.
……………………….
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema sekta ya afya ni nyeti isiyopaswa kuingiliwa na wanasiasa ila madaktari na wauguzi wanapaswa kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwemo kuzuia vifo vya mama na mtoto.
Mnyeti aliyasema hayo mjini Babati, wakati akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, madaktari na wauguzi kwenye uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama. 

Alisema kazi ya viongozi ni kusimamia utekelezaji na madaktari na wauguzi wafanye kazi zao kwa vitendo huku wakitumia lugha nzuri pindi wanapotoa huduma kwa wagonjwa. Alisema wataalamu wa afya wanapaswa kutimiza wajibu wao katika uwajibikaji na kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga waweze kuwa watu wazima. 

“Kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anatimiza jukumu lake ikiwemo kupatiwa huduma bora ili kudhibiti vifo vya kina mama na watoto pamoja na kutoa elimu kuanzia ngazi ya jamii,” alisema Mnyeti. Alisema kwa mujibu wa sera za afya nchini, huduma za uzazi hutolewa bure ila kuna baadhi ya maeneo malalamiko ya mama wajawazito kudaiwa fedha yamekuwa yakitolewa. 

“Halmashauri na wengineo kasimamieni hilo inawezekana suala la kuwatoza fedha wajawazito au wa mama waliojifungua halipo kwetu ila lichunguzwe na kufanyiwa kazi,” alisema Mnyeti. Mkazi wa mjini Babati, Aloyce Bura aliiomba serikali kuhakikisha wanaboresha huduma kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) ikiwemo upungufu wa watumishi na dawa. 

Bura alisema wakati huu ambapo serikali inaboresha huduma za afya ikiwemo kujenga vituo vya afya na hospitali za wilaya inapaswa kuongeza watumishi na dawa. Mkazi wa mtaa wa Miyomboni, Mariam Sulle aliwapongeza wauguzi wa hospitali ya Mrara kwa kuwa na lugha nzuri kwa wanawake wajawazito pindi wanapowahudumia tofauti na awali. 


“Mgonjwa anahitaji faraja na lugha nzuri, niwapongeze kwa kutoa huduma zao ipasavyo kwani ukitoa lugha mbaya mgonjwa anaona bora akafie nyumbani kwao kuliko kutukanwa hospitalini,” alisema Sulle.

RAIS MAGUFULI HALALI KWASABABU YA KUHAKIKISHA WATANZANIA WANAPATA MAENDELEO-WAZIRI MKUU MAJALIWA

$
0
0
*Akumbuka simu aliyopigiwa saa nane usiku akipewa maagizo ya ujenzi Mji wa Serikali

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dk.John Magufuli halali kwasababu ya kuwaza kuwaletea maendeleo ya Watanzania wote huku akifafanua amekuwa akipokea simu za Rais hadi saa nane usiku.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Aprili 13,2019 wakati anazungumza kwenye uzinduzi wa Mji wa Serikali Dodoma ambapo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa na maendeleo na kubwa zaidi ni uamuzi wa Rais wa kutoa tamko la kuhamishia Serikali Dodoma na hatimaye ndoto hiyo imetimia.

"Rais wetu unafanya kazi kubwa sana kwa ajili ya nchi yetu,naomba niseme kitu,kuna siku Rais ulinipigia simu saa nane na dakika 25.Nimetaja hizi dakika kwasababu baada ya kuangalia saa nikaona ni saa nane,nikaamua kuangalia dakika ni 25.Ilikuwa usiku wa maneno Rais yuko macho.

" Nilichojifunza ni kwamba Rais wetu halali kwa ajili ya kuwaza maendeleo ya nchi yetu,nakumbuka siku hiyo ulitoa na maelekezo kuhusu ujenzi wa Mji wa Serikali na baada ya hapo tukaanza utekelezaji wake na leo hii unazindua Mji wa Serikali hapa Dodoma .Ahsante Rais na nikuahidi tutaendelea kupokea maagizo yako na tutayatekeleza kwa wakati,"amesma Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesisitiza kila ambacho Rais ataagiza watatekeleza na kutumia nafasi hiyo kuwaomba watumishi kutozima simu zao kwani maagizo na maelekezo yanaweza kutolewa wakati wowote na yanahitaji kufanyiwa utekelezaji wa haraka.

Akizungumzia majengo hayo ya Serikali,Waziri Mkuu amesema majengo 20 tayari yamekamilika na baada ya kuzinduliwa leo na Rais watumishi wataanza kutoa huduma kuanzia kesho na kufafanua watumishi wote walilloko Dodoma watakuwa huko.

Pia amesema kuna baadhi ya majengo ujenzj unaendelea na upo katika hatua.mbalimbali na hiyo imetokana na aina ya ramani ya jengo lakini akafafanua kuwa nayo yatakamilika katika kipindi kifupi kuanzia sasa. 

"Kuanzia kesho watumishi wote watatoke Ihumwa katika Mji wa Serikali kwani walikuwa wanasubiri kufanyika kwa uzinduzi na huduma zote muhimu zipo ikiwemo maji ,umeme,barabara za lami na kinachoendelea ni mtandao wa mawasiliano," amesema Waziri Mkuu.

Akifafanua zaidi kuhusu kuhamishiwa Serikali Dodoma amesema inatokana na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 ambayo imezungumzia kufanyika mchakato wa Serikali kuhamia Dodoma na kisha Rais Magufuli katika kutekeleza hilo alitangaza rasmi kuanza utekelezaji ambao sasa umetimia.

Pia amesema kutajengwa kituo cha afya katika eneo hilo la Mji wa Serikali ambacho kitatoa huduma kwa watumishi wa umma waliko maeneo hayo na wananchi kwa ujumla.Amefafanua kuwa kukamilika kwa Mji wa Serikali Dodoma kunakwenda kufungua fursa nzuri za ajira kwa wananchi ambapo zaidi ya wananchi 1000 wa mkoa huo wamepata ajira.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akiteta jambo na Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, kwenye uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma Aprili 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akitoa taarifa ya Serikali kuhamia Dodom, kwenye uzinduzi wa mji wa Serikali eneo la Mtumba, jijini Dodoma Aprili 13, 2019. Mgeni rasmi alikua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO NCHINI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira mazuri Kwa watoto nchini Kwa lengo la kuondoa changamoto wanazokumbana nazo.

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa ya Themi wakati wa maazimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto yaliofanyika jijini Arusha na kusema kuwa ndio maana serikali ikaanzisha huduma bure ya elimu nchini.

Ameeleza kuwa kumekuwepo na mikakati mbali mbali iliyoandaliwa na serikali Kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na wanaofanyakazi mitaani ikiwa ni lengo la kuwaunganisha na familia zao na jamii kuweza kufikia malengo yao ikiwemo kusoma na kupata matibabu sanjari na makazi.

Awali akimkaribisha mgeni Rasmi Afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha Martha George alisema jiji la Arusha limeweza kuwaunganisha watoto waishio mitaani na mazingira hatarishi katika vituo vya kulea watoto hao na wengine kuwarudisha katika familia zao.

Amesema kuwa malengo ya maadhimisho hayo ya kila mwaka yamejikita kuhakikisha kuona umuhimu wa kuisogeza jamii kuwalea watoto wenye uhitaji na wanaoishi na kufanyakazi mitaani.

Kwa upande wao watoto hao kwenye Risala yao wamesema kuwa wanakumbana na changamoto mbali mbali ikiwemo kutopata elimu sanjari na malezi Bora na kuiomba serikali kuona umuhimu wa kuwaunganisha na familia zao.

Wameeleza kuwa changamoto hizo ni pamoja na jamii kuwanyanyapaa na kuwaona sio sehemu yao Kwa kuwaita majina mbali mbali hivyo kuiomba jamii kuwaona ni sehemu ya maisha yao.

Jumla ya watoto 6,393 Sawa na asilimia 76 wanaishi katika mazingira hatarishi kwenye majiji sita hapa nchini hii imebainishwa na ripoti ya wizara ya afya kwenye mpango wa kizazi kipya Kwa ushirikiano na USAID.

Ambapo watoto wenye umri Kati ya miaka 15-18 Sawa na asilimia 51 huku watoto wenye umri wa miaka 11-14 wakiwa Sawa na asilimia 35 huku ikionyesha watoto wenye umri 0-10 Sawa na asilimia 14 huku watoto wakike wakiwa Sawa na asilimia 86 kwenye umri unaonzia miaka 15-18 

Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi yaliofanyika jijini Arusha yenye kauli mbiu ya "hakikisha usawa Kwa watoto wote" Kwa kuwapatia ulinzi na mahitaji yote Kwa watoto wenye kuishi katika mazingira hatarishi.

Ugumu wa kurudi shuleni uksefu wahali ya upendo vipigo bajeti za watoto wenye kuishi mtaani Kwa kurowabaguza kwani sikuhiini muhimu Kwa kuikumbusha serikali umuhimu wa matunzo ya watotowanaoishi katika mazingira hatarishi.

Jiji la Arusha Lina jumla ya watoto 544 wanaofanyakazi katika kada mbali mbali kama ripori ya serikali inavyoonyesha ambapo watoto hao wanatoa wito Kwa wadau kuwaona kama jamii na kuwasaidia ili nao waje kuwa mfano katika jamii.

Rais magufuli Atekeleza Ndoto ya Baba wa Taifa kwa Kuzindua Mji wa Serikali Dodoma

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi wengine mara baada ya kufunga jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya kukata utepe kwenye jengo la Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kuashiria uzinduzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhadisi Balozi John Kijazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Mzee Samwel Malecela, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Salma Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Majeshi na Ulinzi, CDF, Venance Mabeyo akimbadilishia cheo kutoka Kanali hadi kuwa Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), Brigedia Jenerali Charles Mbuge wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo. Wengine wanaoshuhudia zoezi hilo ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro. Brigedia huyo amepewa cheo hicho na Mhe. Rais kufuatia uchapakazi wake katika kusimamia miradi ya ujenzi mbalimbali inayotekelezwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na JKT. Baadhi ya wananchi na wabunge wakifuatila hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serkali uliojengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodo leo. Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adeladius Kilangi, Waziri wa Madini, Doto Biteko, na Waziri wa Nishati, Selemani Jaffo walipokutana katika hafla ya hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kikosi Kazi kilichoratibu zoezi la Serikali Kuhania Dodoma mara baada ya uzinduzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma. .(Picha na Frank Shija - MAELEZO).

JPM:Nataka yote Tuliyoyaahidi Tuyatimize

$
0
0
Na Immaculate Makilika- MAELEZO 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ni lazima kutekeleza masuala mbalimbali aliyoyaahidi Watanzania wakati akiingia madarakani mwaka 2015, ambayo yanalenga kuwaletea wananchi maendeleo. 

wakati alipokuwa akizindua mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema kuwa aliamua kutimiza ahadi ya Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1973 ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi. 

Rais Magufuli alisema “Nataka yote tuliyoyaahidi tuyatekeleze, nataka ofisi hizi nzuri tulizojenga ziwe na watu, na zianze kutoa huduma kwa wananchi” 

Alisisitiza, “ jukumu langu lilikuwa kutekeleza ahadi ya Mwalimu Nyerere, na nilipata nguvu baada ya kukumbuka kuwa ziko nchi nyingi tu duniani ikiwemo nchi za Afrika kama Nigeria na Cote d’Ivoire ambazo zilihamisha makao makuu ya nchi yao katika kipindi kifupi, nataka kuwahakikishia na mimi nakuja Dodoma kwa sababu hakuna kinachonichelewesha” 

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali inaendelea kukamilisha mifumo na ujenzi wa miradi mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wa umma ambao watahamia na kufanya kazi katika majengo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaofika katika mji huo wa Serikali, ikiwa ni sambamba na kuboresha jiji la Dodoma. 

Alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara itakayogharimu bilioni 500 kwa mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayojengwa kutokea Mtumba, Veyula na Nala ambayo ina urefu wa kilomita 4. 

Vile vile amesema, serikali inaendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa na wa kimataifa unaogharimu bilioni 400 pia inafanya maandalizi ya ujenzi wa Bandari kavu kwa vile jiji la Dodoma lina kituo kikuu cha reli ya kisasa (SGR). 

Katika jitihada za Serikali za kuliboresha jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya nchi, Serikali imepanga kujenga shule ya sekondari ya kisasa itakayogharimu shilingi bilioni 13na Chuo cha mafuzo (VETA) kitakachogharimu shilingi bilioni 18. Ikiwa ni pamoja na kuendelea kuimarisha hospitali ya Benjamini Mkapa ambayo imeanza kutoa matibabu ya kibingwa. 

Aidha, Rais Magufuli alilipongeza Jeshi la Wananchi kwa kujenga majengo hayo ya mji wa Serikali, pamoja na kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo ukuta wa Mererani uliopo Arusha, ambapo amempandisha cheo msimamizi wa miradi hiyo ya ujenzi Kanali Charles Mbuge pamoja na kutoa ajira kwa vijana walioshiriki katika ujenzi huo. 

Rais Magufuli, “Kanali Mbuge atakuwa Brigedia kuanzia leo, nataka ufanyike utaratibu wa kumuongezea vyeo ufanyike na aendelee na hii kazi. Tuwe na kikosi cha ujenzi na kiongozwe na Mbuge ili kusaidia kufanya maajabu katika nchi hii, nawapongeza Jeshi la Wananchi, kwani mnafanyakazi nzuri” 

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempongeza RaisMagufuli kwa uamuzi wake wa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma kwani uamuzi huo utasaidia kusogeza huduma kwa wananchi, pamoja na kusaidia ukuaji wa uchumi katika mikoa iliyopo katikati ya nchi. 

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama, alisema kuwa katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano miradi mbalimbali imetekelezwa katika jiji la Dodoma ikiwemo uzalishaji umeme megawati 48, huku mahitaji halisi yakiwa megawati 28. 

Akitaja baadhi ya miradi mingine inayoendelea kutekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za mzunguko ndani ya Dodoma yenye urefuwa kilomita 39 pamoja na kituo cha afya katika mji wa Serikali kitakachogharimu bilioni 4.5. 

Awali Rais Magufuli alizindua jengo la ofisi zake, pamoja na nyumba 41 za wafanyakazi wa Ikulu vilivyopo Chamwino jijini Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.

DC MURO AHIMIZA UCHANGIAJI WA TAASISI ZA DINI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro amehimiza uchangiaji wa ujenzi wa majengo ya taasisi za dini na kuacha kutegemea wahisani ambao wamekuwa na masharti magumu.

Muro ametoa rai hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti Mdogo wa Kati uliopo Ngarenaro unaogharimu kiasi cha zaidi ya milioni 800.

Amesema ipo Haja kwa waumini kuimarisha juhudi zao wenyewe katika uchangiaji jambo ambalo litafanikisha kukamilisha ujenzi kuliko kutegemea michango ya wahisani ambayo imekuwa haifiki kwa wakati.

Muro ambaye amekubali kuwa mwanakamati wa ujenzi wa msikiti huo, ametoa kiasi cha sh,milioni 1,huku akiahidi kutoa fulana 100 kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji na ameahidi kumsomesha hadi chuo kikuu mtoto wa miaka 7, Abdulkarim Hasan baada ya kuvutiwa na uwezo wake mkubwa katika kuielewa wa dini ya kiislam.

Awali imamu wa msikiti huo,Hasan Kileo,amesema ujenzi wa msikiti huo utasaidia kuingiza idadi kubwa ya waumini tofauti na ule wanaosalia kwa sasa na utagharimu kiasi cha sh,milioni 800 nakwamba hadi sasa wamefanikiwa kupata sh,milioni 18 ambayo imetumika katika ujenzi wa msingi.

Naye sheikh Haruna Husen pamoja na kumshukuru mgeni rasm Jeri Muro kwa kuchangia ujenzi huo wa msikiti lakini aliwataka waumini wa kiislamu kuwa mstari wa mbele kujitoa katika ujenzi wa nyumba za Mungu.
Aliwataka waumini kujivunia kila walichokijenga wao kuliko kujengewa na mtu mwingine .pamoja na harambee hiyo watoto zaidia ya 50 wamehitimu elimu ya madrasa na kutakiw kufuata mema waliofundishwa
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akiwa ameketi katikati ya watoto wa madrasa wakimsomea  huku wakimsomea dua. 
 Wanafunzi waliomaliza madrasa wakiwa wanasikiliza kwa makini hutuba ya mkuu wa wilaya
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwa anahutubia katika harambee ya kuchangia msikiti wa  Ngarenaro uliopo jijini Arusha

 picha ikionyesha wa kwanza kushoto sheikh Haruna Husen akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jerry Muro wa tatu ni imamu wa msikiti wa Ngarenaro ,Hasan Kileo, wakiwa wanafatilia harambee hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiwa na mtoto Abdulkarim Hassan ,ambapo mkuu wa wilaya amejitolea kumsomesha mtoto huyu 

TANESCO YAFANYA BONANZA KUBWA LA MICHEZO JIJINI ARUSHA

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akikabidhi kikombe kwa Mshindi wa kuvuta kamba kitengo cha Mita Tanesco katika bonanza la michezo liloandaliwa na shirika hilo na kufanyika katika viwanja vya General Tyre ,kulia ni Nahodha wa timu hiyo Innocent Pascal.
Nahodha wa Timu ya Mpira wa pete ya RAS ,Grace Kija akipokea zawadi wa kombe kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro.
Nahodha wa Timu ya mpira ya Ras akipokea zawadi ya kikombe ,baada ya kuifunga timu ya Tanesco goli 2 kwa 1.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya RAS wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa mpira wa pete baada ya kukabidhiwa zawadiWachezaji wakisakata kabumbu kati ya Timu ya TANESCO na timu ya RAS
Mashindano ya kuvuta kamba kati ya Timu ya Tanesco na RAS ambapo TANESCO iliibuka na ushindi katika viwanja vya General tyre Njiro Jijini Arusha
Michezo ikiendelea hapa timu zote wakivuta kamba katika viwanja vya General tyre Njiro Jijini Arusha


Na Vero Ignatus, Arusha.


Shirika la Umeme Tanesco mkoani Arusha limefanya bonanza kubwa la michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na kukimbiza kuku huku wadau wengi wakijitokeza kwenye viwanja vya General tyre kushughudia michezo hiyo.

Akifungua Bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amesema kuwa michezo ni afya ,ajira na furaha katika jamii hivyo bonanza hilo la Tanesco linalenga kuhamasisha wananchi kuunga mkono timu ya Vijana ya Taifa ya Serengeti ambayo inashiriki katika michuano ya Afcon.

Daqqaro amesisitiza kuwa michezo inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza kama presha,kisukari na saratani ambayo husababishwa na aina ya maisha isiyozingatia mazoezi na lishe.

Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Arusha Donasiano Shamba amesema kuwa bonanza hilo linahusisha michuano mikali kati ya timu ya Tanesco na RAS arusha ambao walichuana katika mpira wa miguu na mpira wa pete.

Shamba amesema kuwa michezo hilo inalenga na kujenga na kudumisha ushirikiano kati ya wadau mbalimbali ili kuleta maendeleo na pia kuunga mkono juhudi za Timu zinazoiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa ikiwemo Serengeti.

Mmoja kati ya washiriki wa Bonanza hilo Innocent Pascal ameshauri waandaaji kuandaa michezo hiyo mara kwa mara ili kuibua vipaji vya michezo ambavyo vinaweza kuleta medani za heshima za kitaifa na kimataifa.

CCM YATOA MWEZI MMOJA KUMALIZA CHANGAMOTO ZA WAJASIRIAMALI WA SOKO LA MABIBO MAHAKAMA YA NDIZI

$
0
0
Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mahakama ya ndizi Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema CCM inatoa muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kushughulika na changamoto za wafanyabiashara wa soko la Mahakama ya ndizi.

Ndg. Polepole ameyasema haya baada ya kupokea Malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wa soko hilo ya kukosekana kwa miundombinu rafiki katika soko, uchakavu wa vibanda vya kufanyia biashara, vyoo vichache, dhulma kutoka kwa baadhi ya madalali na vitisho kutoka kwa wamiliki wa kiwanda cha urafiki.

Ndg. Mkurugenzi tengenezeni mpango kazi hapa ni aibu soko la mahakama ya ndizi kuwa hivi, mnaweza kuwa na mabanda mazuri hapa, miundombinu mizuri hapa na wafanyabiashara wapo tayari kuchangia serikali vizuri bila matatizo yoyote” Ndg. Polepole

Aidha Ndg. Polepole amewahakikishia wafanyabiashara katika soko la Mahakama ya ndizi kuwa changamoto zingine za vifungashio, tuhuma za rushwa kwenye mizani ya uloye, tanangozi na kibaha na mabadiliko katika matumizi ya ardhi katika soko hilo Chama kimepokea, kitazingatia na kuleta majibu ndani ya mwezi mmoja.

Huu ni muendelezo wa ziara za kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020.

AGAPE YAIBUKIA MNADANI..YATOA ELIMU YA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NGOKOLO MITUMBANI

$
0
0
Shirika la Agape ACP limetoa elimu ya kutambua haki za binadamu ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ngokolo Mitumbani Manispaa ya Shinyanga. 

Elimu hiyo imetolewa leo Jumamosi Aprili 13,2019 wakati Mnada wa Jumamosi katika Soko la Ngokolo Mitumbani ukiendelea hivyo kufanikiwa kuwafikia watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wananchi waliofika mnadani hapo kujipatia mahitaji yao. 

Agape ACP wanatoa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

Akitoa elimu, Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda aliwataka wanawake na wasichana wanaofanyiwa vitendo vya kikatili kwenye masoko na katika jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kuwa wakimya na badala yake watoe taarifa kwa viongozi mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia katika kituo cha polisi. 

“Acheni kukaa kimya mnapofanyiwa ukatili,msikubali kukaa na makovu ya ukatili kwenye masoko,pazeni sauti zetu,nanyi wanaume acheni kunyanyasa wanawake,msiwatukane na msiwadhulumu mama lishe,wapeni riziki si matusi”,alieleza Isabuda. 

Isabuda alitumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kuthamini wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni huku akiwatahadhalisha wanaume kuwa waaminifu katika ndoa zao na kuacha tabia ya kutongoza na kufanya mapenzi na wanafunzi kwani matokeo yake ni kufungwa jela miaka 30. 

Naye Afisa Mradi wa 'Mpe Riziki Si Matusi' kutoka Agape,Helena Daudi alisema Agape imeendelea kutoa elimu katika masoko mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga ikiwemo Soko Kuu,Kambarage,Nguzo Nane Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya ili jamii iachane na tabia ya kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara 

Alisema tayari wamewajengea uwezo wasimamizi wa sheria ili wakaosaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotokea kwenye masoko. 

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard alisema wafanyabiashara wanaofanyiwa zaidi ukatili sokoni akina mama hususani mama lishe ambao wanatolewa lugha chafu,wanadhulumiwa na kufanyiwa mashambulio ya aibu ikiwemo kushikwa shikwa bila idhini yao. 

Alizitaja hatua ambazo wamekuwa wakizichukua pindi panapotokea ukatili sokoni kuwa ni kusuluhisha,kuwapiga faini ya shilingi 5000 wanaotukana na kama ni mfanyabiashara basi akirudia kutukana basi hufungiwa biashara yake kwa muda wa wiki mbili.
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akitoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara katika soko la Ngokolo Mitumbani leo - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akielezea madhara ya kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wananchi wakimsikiliza Isabuda.
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwasisitiza wanaume na wanawake kuacha kuwafanyia ukatili wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wananchi wakimsikiliza Isabuda.
Afisa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi kutoka Agape,Helena Daudi akiwahamasisha wananchi kuwapenda wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni badala ya kuwanyanyasa na kuwanyima haki zao.
Afisa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi kutoka Agape,Helena Daudi akiwataka wanawake kutoa taarifa pale wanapofanyiwa ukatili.
Wananchi wakisoma vipeperushi mbalimbali vya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Kikundi cha burudani cha 'Shinyanga Arts Group' kinachoongoza na Msanii ChapChap kikitoa burudani.
Burudani inaendelea.
Wasaidizi wa Kisheria kwenye masoko waliopewa mafunzo na Agape ACP wakitoa eimu ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara kwenye masoko. Aliyeshikilia kipaza sauti kulia ni Shangwe Omary.
Msaidizi wa Kisheria sokoni, Asha Jumanne akitoa elimu kwa jamii namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye masoko.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard akielezea jinsi wanavyokabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni ambapo wamekuwa wakipiga faini ya shilingi 5000 wanaotukana na kufunga biashara za wafanyabiashara wanaofanya ukatili sokoni.
Katibu wa Wafanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Tracy Leonard akielezea namna wanavyowatetea akina mama wanaofanyiwa ukatili sokoni.
Mfanyabiashara Soko la Ngokolo Mitumbani,Zuhura Athuman akielezea changamoto wanazokutana nazo sokoni ikiwemo kutolewa lugha chafu.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

TRENI YA MIZIGO YAACHA NJIA MOROGORO

$
0
0

Na Hussein Stambuli, Morogoro 

Mabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha shehena ya ngano kupitia reli ya kati kutoka jijini dar-es-salaam kuelekea jijini mwanza yameanguka eneo la kola manispaa ya morogoro na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya reli eneo hilo huku baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutumia njia hiyo kukwama kwa muda. 

Akizungumzia tukio hilo mkuu wa stesheni ya morogoro salvatory kimaro amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya saa mbili usiku na hadi sasa chanzo chake hakijfahamika na tayari wataalamu wanaendelea na kazi za kurejesha mawasiliano ya njia hiyo..

“taratibu nyingine ikiwemo mafundi wameshafika eneo la tukio kuweza kufanya tathmini za ujenzi na tunasafisha njia kwa kwa kutengeneza tuta ili zitakapo fika reli tuta liwelimeshaimarika na kumalizika kwa kazi hiyo kutatarajia mwenendo wa kazi za mafundi na tunatarajia kazi itafanyika haraka na kwa uhakika kupunguza usumbufu zaidi” amesema kimaro.

Aidha kimaro amefafanua kuwa kuhusu treni za abiria zilizokuwa zikitokea dar es salaam kuelekea kigoma, mpanda na mwanza zilifika mapema morogoro jambo ambalo limesaidia kubadilishwa kwa abiria waliotoka dar wakaingia iliyokuwa inatoka mwanza na wale wa mwanza wameeendelea kwenye treni iliyokuwa ikitokea dar es salaam kuelekea mwanza.

wananchi wanoishi jirani na eneo hilo wameiomba serikali kutafuta njia mbadala ya kudhibiti ajali katika eneo hilo ambalo linaonekana kuwa na kona kali na mara kwa mara limekuwa likisababisha ajali.

“leo hii imetokea ajali ya treni ya mizigo ni vyema eneo hili likatazamwa vyema kabla haijatokea ajali ya treni yenye watu itakuwa hatari Zaidi” amesema Jackson isack mwananchi 
Mmabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha  shehena ya ngano  kupitia reli ya kati  kutoka jijini dar-es-salaam  kuelekea  jijini  mwanza yakiwa yameanguka eneo la kola  manispaa ya morogoro ....
 Mabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha  shehena ya ngano  kupitia reli ya kati  kutoka jijini dar-es-salaam  kuelekea  jijini  mwanza yakiwa yameanguka eneo la kola  manispaa ya morogoro
Reli ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya mabehewa kuacha njia

Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images