Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live

WAZIRI KANGI LUGOLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKZI NDANI YA JESHI LA POLISI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola akiwa pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakiingia katika ukumbi wa maafisa wa Polisi Oysterbay leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la wafanyakazi ndani ya Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola (KUSHOTO) akiwa pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (KATIKATI) na Mwenyekiti wa TUGHE makao Makuu ya Polisi, Dominic Nyoni wakiimba wimbo wa “Solidarity Forever” katika ukumbi wa maafisa wa Polisi Oysterbay leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la wafanyakazi ndani ya Jeshi la Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.


NEC YAWATAKA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUFANYA KAZI KWA WELEDI

$
0
0
Wasimamizi wa Uchaguzi kwenye Uchaguzi Mdogo wa Arumeru Mashariki na Kata Sita (6) za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika Tarehe 19 Mei mwaka huu wametakiwa kuwa na weledi ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki.

Akifungua mafuzo kwa wasimamizi hao Jijini Dodoma leo (Ijumaa Tarehe 12.04.2019), Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (Rufaa), Mbarouk Salum Mbarouk amewaambia wasimamizi hao kwamba weledi utapatikana kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo ya Tume.

Jajji Mbarouk amewakumbusha kuwa Tume ndiyo yenye jukumu la kusimamia, kuendesha na kuratibu Uchaguzi, lakini watakaosimamia jukumu hilo kwa karibu ni wao (wasimaizi) kwa sababu wanabeba dhamana katika Jimbo hilo na Kata hizo sita.

Aidha, kiongozi huyo aliwaambia kuwa wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazingatia maelekezo watakayopewa na Tume, kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria zinazosimamia Uchaguzi badala ya kufanya kwa mazoea.

Pamoja na hayo, Jaji aliwaeleza Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi hao kuwa wanapaswa kujiamini na kujitambua kwa sababu wameaminiwa na Tume na wahakikishe kwamba wanayajua maeneo yao ya uchaguzi vyema.

Amesema chaguzi hizo ndogo zitajumuisha wapiga kura 211,741 waliojiandikisha Katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika vituo 567 vya kupigia kura.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bi. Givenes Aswile aliwakumbusha washiriki hao wa mafunzo kuwa wanapaswa kuhakikisha kwamba chaguzi hizo zinafanyika bila kuwa na dosari ili kupunguza malalamiko na mashauri mahakamani.

Kaimu Mkurugenzi aliwakumbusha pia Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi hao kuwa wanatakiwa kuwepo maeneo ya kazi muda wote katika kipindi cha kutoa fomu za uteuzi, siku ya uteuzi, wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura, kuhesabu na kujumlisha kura hadi kutangaza matokeo ya Uchaguzi.

Bi. Aswile aliwaambia kuwa wajiepushe na migogoro ya Vyama vya siasa kwa kutotoa fomu za uteuzi kwa wagombea wawili wa Chama kimoja cha Siasa. Kila Chama kinatakiwa kumdhamini Mgombea mmoja tu.

Wakati wa Kampeni, Kaimu Mkurugenzi aliwakumbusha kwamba wanatakiwa kuunda Kamati za Maadili Ngazi ya Jimbo kwa Ubunge na Kamati ya Maadili Ngazi ya Kata kwa Udiwani ili kushughulikia kwa haraka malalamiko kama yatakuwepo.

Kata zenye uchaguzi ni pamoja na Uwanja wa Ndege iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Kitobo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Kyela iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, Mikocheni iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam, Mvuleni iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi na Manda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
 Wajumbe wa Tume na Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Arumeru Mashariki na Kata Sita (6) za Tanzania Bara utakaofanyika Tarehe 19 Mei mwaka huu wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa. Mafunzo kwa wasimamizi hao yamefanyika Jijini Dodoma leo (Ijumaa Tarehe 12.04.2019) chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). (Picha kwa Hisani ya NEC)
Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Arumeru Mashariki na Kata Sita (6) za Tanzania Bara utakaofanyika Tarehe 19 Mei mwaka huu wakila kiapo wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jijini Dodoma leo (Ijumaa Tarehe 12.04.2019). (Picha kwa Hisani ya NEC)

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA WAJUMBE MBALIMBALI KUTOKA TAASISI KUTEKELEZA AGIZO LA KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ambao kwa pamoja wanaunda kikosi kazi cha kusimamia utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki hapa nchini. Wajumbe hao ni kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Mapato Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kikao hicho kimefanyika hii leo katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango – Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wanaounda kikosi kazi cha kusimamia utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki hapa nchini wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika hii leo katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango.

PSSSF YATOA ELIMU KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WAKALA WA UFUNDI NA UMEME TEMESA

$
0
0
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), umeendesha semina fupi kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuhusu shughuli za Mfuko ikiwa ni miezi nane tangu kuanzishwa kwake.

PSSSF imeundwa kwa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 2 iliyopitishwa na Bunge Januari 31, 2018 ambayo inaunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, LAPF, PPF na PSPF.

Katika semina hiyo iliyofanyika Aprili 12, 2019, wajumbe walielimishwa kuhusu majukumu ya Mfuko, Wanachama wa Mfuko na Mafao yatolewayo na Mfuko.
Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Mordgard Maten, (kulia), akitoa elimu kuhusu shughuli za Mfuko huo kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019. Wakwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Japhet Maselle.
Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw. Mordgard Maten (kulia), akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019.
Afisa Mtekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bw.Msafiri S. Mugaka (kulia), akiwa na Afisa Mkuu wa Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. Mordgard Maten kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam Aprili 12, 2019.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (kulia), akiwa na baadhi ya viongozi wa baraza hilo wakisikilzia mada zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa PSSSF.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
Afisa Uhsiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akizunumza wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya wajumbe wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF.
Maafisa wa PSSSF kutoka kushoto, Bw.Msafiri S. Mugaka, Bw. Abdul Njaidi na Bw.Donald Peter.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (kulia), akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle (watatu kulia), na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA, na maafisa waandiamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko kwa wajumbe wa Baraza hilo.

KATIBU MKUU CCM ASEMA ILI TAIFA LIWE NA MAENDELEO LAZIMA WALIOPEWA NAFASI WATENDE HAKI KWA USAWA

$
0
0
Na Hussein Stambuli-Morogoro.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally amesema ili Taifa lifikie malengo ya maendeleo na amani idumu inapaswa viongozi waliopewa nyadhfa mbalimbali katika jamii kutenda haki na usawa na kuachana na wizi wa mali za umma, unyonyaji kwa wanyonge, rushwa pamoja na ufisadi.

Dk.Bashiru ameyasema hayo leo Aprili 12, 2019, wakati akizungumza na wakulima kwenye mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya Waziri Mkuu wa zamani nchini Hayati Edward Moringe Sokoine kwa kuangalia mtazamo wake kuhusu maendeleo vijijini na mchango wa wakulima wadogo katika ujenzi wa uchumi wa kitaifa ambapo akataka kiongozi huyo kuenziwa kivitendo.

"Usawa ni kila binadaam anastahili heshima ya kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake sio usawa wa rangi wala kimo au umaarufu au uduni wao lakini woote ni binaadam ambao utu wao unastahili kuheshimiwa, na mtu anaeamini katika usawa wa binaadam lazma pia akubali katika jamii ile ile watokee watu ambao wanakula na kusaza na kutupa wakati wengine wanakufa na njaa,"amesema Dk.Bashiru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kavazi la Mwalimu Julias Nyerere, Profesa Issa Shivji amesema wananchi hawawezi kujikomboa bila mapambano, hivyo ni muhimu kuwa na umoja na kukemea uovu wowote unaofanywa kwa kwenda kinyume na sharia na taratibu za nchi. "Lazima tuwe na chombo chetu kama wakulima chombo cha kutuelimisha, kutulinda hasa wananchi wa vijijini jambo litakalowasaidia kufahamu haki zao,"amesema Shivji.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa MVIWATA Steve Ruvuga amesema lengo kuu la mdahalo huo ni kujadili na kufikisha maoni kwenye ngazi mbalimbali ili uzalishaji uwe na tija zaidi kwa wakulima nchini."Naamini tunayoyazungumzia hapa yanahusu masuala mapana ya kilimo yanayohusu masuala mapana ya kilimo pamoja nauzalishaji wa kilimo chenyewe hasa kwa wakulima wadogo kwahiyo tunaamini tafakari ya leo itatufanya tufaham namna bora ya uzalishaji na kukuza uzalishaji."
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) taifa dr bashiru ally akizungumza na wakulima wadogo katika maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe sokoine
 2. wakulima waliojitokeza katika  mdahalo ulioandaliwa na  mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania mviwata ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe so
 Mwenyekiti wa kavazi la mwalimu julias kambarage nyerere prof issa shivji akizungumza na wakulima wadogo katika maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani wa tanzania  hayati edward moringe so
 5.katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) taifa dr bashiru ally katikati, kulia Mwenyekiti wa kavazi la mwalimu julias kambarage nyerere prof issa shivji na kuliadk.ng’wanza kamata, mhadhiri kutoka chuo kikuu ch
 Mkurugenzi mtendaji wa mviwata steven ruvuga akifafanua jambo katika mdahalo ulioandaliwa na  mtandao wa vikundi vya wakulima tanzania mviwata ikiwa ni maadhimisho ya kutafakari maisha ya waziri mkuu wa zamani .

UNDER THE SAME SUN KUTOA ELIMU KWA WABUNGE KUHUSU UALBINO

$
0
0
 Viongozi, Wafanyakazi na Wanachama wa Shirika la Under The Same Sun wakiwa katika picha ya Pamoja bungeni Jijini Dodoma leo.
  Viongozi, Wafanyakazi na Wanachama wa Shirika la Under The Same Sun wakiwa ndani ya Ukumbi  Bunge Jijini Dodoma leo.
  Viongozi, Wafanyakazi na Wanachama wa Shirika la Under The Same Sun wakiwa ndani ya Ukumbi  Bunge Jijini Dodoma leo.
Shirika la Under The Same Sun lenye kuhudumia na kutetea maslahi ya watu wenye ualbino nchini, linakusudia kufanya semina ya siku moja kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania. 

Semina hiyo yenye lengo la kuwapatia uelewa kuhusu  ualbino, waheshimiwa wabunge inatarajiwa kufanyika jijini Dodoma kwenye Ukumbi wa Msekwa siku ja jumapili April 14. 

Under The Same Sun iliyoanzishwa miaka kumi iliyopita imekuwa ikitoa elimu kwa jamii juu ya ualbino na watu wenye ualbino kwa njia ya mikutano, semina na mafunzo mbalimbali pamoja na kutoa ufadhili wa elimu kwa watu wenye ualbino kuanzia ngazi ya awali, msingi, sekondari hadi chuo kikuu.

Mwenge wa Uhuru waacha maumivu kwa Ma-DC – Rukwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku tatu kwa wakuu wa wilaya wanaosimamia halmashauri ambazo Mwenge wa Uhuru umekataa kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyopitiwa na Mwenge huo kutoa maelezezo ya kina juu ya sababu ya kukataliwa kwa miradi hiyo yenye tamani ya shilingi 1,248,489,871.

“Napenda nitoe maelekezo kwa Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wenye miradi iliyokataliwa kunipa taarifa ya kwanini miradi yao haikuzinduliwa/kuwekewa mawe ya msingi. Maelezo hayo niyapate ndani ya siku tatu kuanzia tarehe ya leo hadi tarehe 14, April, 2019,” Alisisitiza.

Ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Amos Makalla huku Mwenge huo ukiwa umekimbizwa katika halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa zikichukua umbali wa kilemeta 832.5 na kutembelea miradi 35 na vikundi 11 ikiwa na tamani ya shilingi 45,404,104,489.59

Aidha, kutokana na mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kubeba kauli mbiu isemayo “Maji ni haki ya Kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa,” hivyo alitoa wito kwa wananachi kuendela kutunza vyanzo vya maji, kuimarisha jumuia za watumia maji pamoja na kufanya maandalizi thabiti ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo.

Kwa upande wake Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kumpa ushirikiano wa Kutosha tangu wanawasili katika mkoa huo hadi kuondoka na kuelekea katika mkoa wa Katavi na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kufikisha asilimia 55 ya wananchi wa Mkoa huo kupata maji safi na salam.

“Mimi nikupe hongera kwasababu takwimu zinaonyesha katika mkoa wako wa Rukwa umejitahidi kwa asilimia 55 kuhakikisha wananchi woyte wanapata maji ya uhakika na salama sambamba na hilo katika kupambana na Rushwa katika TAKUKURU kuna malalamiko 64 na kesi 59 wanazifanyia kazi, endeleeni kufanya kazi na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote,” Alisema.

Kutokana na mapungufu yaliyobainika Mwenge wa Uhuru haukuzindua amakuweka mawe ya msingi kwenye miradi mitatu, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mradi mmoja vyumba vitano vya madarasa wenye thamani ya shilingi 76,250,000, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mradi mmoja wa ujenzi wa nyumba ya waalimu “6 in 1” wenye thamani ya shilingi 174,977,775 na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mradi mmoja wa maji wenye thamani ya shilingi 997,262,096.
Mkuu wa Mko a wa Katavi Mh. Amos Makalla (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) katika viwanja vya shule ya msingi Milumba Mkoani Katavi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Mzee Mkongea Ali (kushoto) akitoa pongezi kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mh. Joachim Wangabo (kulia) muda mfupi kabla ya Mwenge wa Uhuru kuelekea Mkoani Katavi tarehe 11.4.2019. 

Waziri Kigwangalla kutua Longido kumaliza mgogoro baina ya vijiji na Kampuni ya uwindaji ya Green Miles Safari.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla (pichani) anatarajia kutua wilayani Longido, hivi karibuni, kutatua mgogoro baina ya Kampuni ya Uwindaji ya Green Miles Safari Ltd inayomiliki kitalu cha Lake Natron wilayani Longido na vijiji 23 vinavyozunguka kitalu hicho.

Vijiji hivyo, vinaidai kampuni hiyo, kiasi cha sh 329 milioni kutokana na makubaliano ambayo wamefikiwa ambapo licha ya suala hilo kufikishwa ngazi ya halmashauri, wilaya na mkoa kampuni hiyo inadaiwa kumegoma kulipa.

Akizungumza jiji hapa, Waziri Kigwangalla alisema, baada ya kupokea ujumbe wa viongozi wa wilaya ya Longido kutaka wizara hiyo kutatua mgogoro huo, wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Frank Mwaisumbe, Mkurugenzi a halmashauri, Jumaa Mhina na madiwani, atakwenda Longido.

"Nitakwenda Longido kutoa maamuzi ya serikali baada ya kuzisikiliza pande zote"alisema Kigwangalla

Kampuni ya Green Miles ambayo tayari imesitishiwa huduma na Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori(TAWA) kutokana na kushindwa kutimiza kanuni za umiliki wa vitalu,imekuwa na mgogoro na wananchi wa vijiji vya Longido na serikali mkoani Arusha.

Naibu Kamishna wa Utalii na Biashara wa TAWA, Imani Nkuwi alisema kampuni hiyo, imeshindwa kulipa ada za kutotumia zaidi ya asilimia 40 ya mgao wa kuwinda katika vitalu."kampuni hii tumeinyia huduma za kuwinda katika vitalu vyake vyote wakati suala lao likifanyiwa kazi"alisema.

Kampuni hiyo, inamiliki vitalu wilayani Longido na katika pori la akiba la Selous na katika siku za karibuni, imekuwa na migogoro na vijiji ilipowekeza wilayani Longido.

Hivi karibuni, Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe alitoa agizo , kukamatwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Green Miles Salim Abdalah Awadhi, kutokana na kushindwa kulipa madeni ya vijiji na halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha.

Mwaisumbe alisema vijiji 23 vya wilaya hiyo, vinaidai kampuni hiyo, kiasi cha sh 329 milioni kutokana na makubaliano walioingia tangu mwaka 2017/18.Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido, Wakili Jumaa Mhina, alisema ofisini yake imekuwa ikiitaka kampuni hiyo kulipa fedha za vijiji na halmashauri bila ya mafanikio.

"mimi nimekuwa nikimtaka aje kulipa ni dawa ya migogoro kwani ndugu zangu hawa masai ni watu waelewa lakini imeshindikana"alisema
Hata hivyo,Mkurugenzi wa Green Miles Safari Ltd, Salim Abdalah Awadhi amekuwa akikanusha tuhuma mbali mbali dhidi ya kampuni yake,ikiwepo kudaiwa na vijiji fedha. 

Wakati Mgogoro huo wa madai ukiendelea, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameunda kamati ya vyombo vya ulinzi na usalama na uhifadhi, kuchunguza kwa kina chanzo cha kuuawa na Majangili Twiga 25 wilayani Longido na 16 kati yao katika kitalu cha kampuni hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka watendaji wa kampuni hiyo, kujitokeza kutoa maelezo kwa kamati yake, kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa..

TANZANIA YARIDHIA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KUONGEZEWA MTAJI

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Washington DC

TANZANIA imeunga mkono uamuzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB wa kutaka kuongezewa mtaji ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa mikopo kwa nchi wanachama wa benki hiyo kwa lengo la kuchochea zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wa 7 wa magavana wa ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54 wanachama wa Benki hiyo, Mjini Washington DC, Marekani, Waziri wa Fedfha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameeleza kuwa AfDB imefanya mambo makubwa nchini Tanzania ndio sababu inaunga mkono kusudio hilo.

Amesema kuwa Benki hiyo imeipatia Tanzania mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, kilimo, nishati na maji.

Benki inataka kuongezewa mtaji kwa asilimia 200 kutoka wastani wa UA bilioni 67.69 hadi UA 191.89 (kutoka dola za Marekani 94.76 hadi dola bilioni 268.6 ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii ya nchi wanachama hususan katika ujenzi wa reli, barabara, usafiri wa anga, tehama, bandari, uzalishaji na usambazaji wa nishati.

"Wakati umefika ili twende haraka zaidi, mitaji sehemu nyingine imepungua, pendekezo la kuongeza mtaji wa benki hii ni jema na matokeo ya miradi inayofadhiliwa na Benki hii yanaonekana katika nchi zetu za kiafrika kwa sababu benki hii iko Afrika na inaijua Afrika tofauti na benki nyingine" alisisitiza Dkt. Mpango

Uamuzi wa nchi za Kiafrika zenye hisa katika Benki ya Maendeleo ya Afrika ya kutaka Benki hiyo iongezewe mtaji ulitolewa wakati wa mkutano wa Magavana wa Benki hiyo mjini Rome, Italia, baada ya mahitaji ya nchi wanachama ya kutafuta mikopo kwenye taasisi hiyo kuongezeka.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina, Mjini Washington DC, Marekani, kabla ya mkutano wa magavana wa Benki hiyo ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54 zenye hisa kwenye benki uliofanyika katika ukumbi wa Willard Continental kujadili namna ya benki hiyo kuongezewa mtaji ili iweze kutoa mikopo kwenye nchi hizo kwa ufanisi zaidi
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC, Marekani, ambapo Tanzania imeridhia hatua hiyo.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC, Marekani, ambapo Tanzania imeridhia hatua hiyo.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Washington DC

Halmashauri zaaswa kutekeleza sera na mipango ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani-Railway Children

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Shirika la Railway Children limesema kuwa serikali imefanya mikakati mbalimbali yanayohusu watoto kilichobaki ni utekelezaji wa kwa halmashauri katika kuingiza mipango ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani lisiwepo.

Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo Mussa Mugatta wakati akitangaza maadhimisho ya Siku ya Watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani ambayo hufanyika kila Aprili 12 ya mwaka, amesema ipo haja kwa mamlaka za serikali za mtaa kuingiza mipango ya watoto kutokana na serikali kuu imeweza kufanya kila kitu hivyo serikali za mitaa zinawajibu wa kugusa eneo watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani.

Amesema Railway Children inafanya kazi na majiji sita nchini katika kuhakikisha watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani linasimamiwa ili kuleta ustawi kwa watoto hao.

Mugatta amesema makundi yw watoto yapo 13 katika utekelezaji wa masuala ya watoto wanaoishi na kufanya kazi ni pamoja nchi kuridhia mkataba wa kimataifa wa umoja wa mataifa katika eneo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Aidha amesema kuwa watoto wanaoishi kazi wanatoka mkoa moja kwenda mwingine hivyo kwa Halmashauri lazima wafatilie kwa watoto wanaosafiri kujua wanakwenda wapi kwani baadhi wanatakiwa kuwa shule.

Mugatta amesema wananchi katika kukabiliana na watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani kila mmoja katika nafasi yaka anachukua hatua ya kuokoa kundi hilo.Amesema kama shirika linaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kuhakikisha watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wanalindwa kutokuwepo.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Railway Children Mussa Mugatta akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza wiki ya maadhimisho Siku Watoto wanaoishi na kufanya kazi ambayo huadhimishwa kila Aprili 12 ya kila mwaka.

NMB YATOA MSAADA WA MADAWATI 100 KILOMBERO

$
0
0
NGabariel Leshabari, Kilombero

SHULE za sekondari Kiberege na Mchombe Wilayani Kilombero zapokea msaaada wa Viti na meza 100 kutoka banki ya NMB mkoani morogoro, vyote vikiwa na Thamani y ash milioni kumi(10) vikiwa na malengo ya kutatua changamoto ya Elimu na Afya.

Akikabidhi msaada huo meneja kanda ya mashariki banki ya NMB morogoro Bw. Baraka Ladislaus alisema kuwa NMB ilipo pasta barua toka ofisi ya mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero alifarijika sana na kuwa pamoja nao na kuweza kutekeleza hatua hiyo maramoja.

Hata hivyo meneja wa NMB Bw Ladislaus alikabdhi tamani hizo kwa mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kilombero amba alikuwa kaimu mkurugenzi afisa Elimu sekondari Dr Janeth barongo alimwakilisha mkurugenzi akiongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Devd Ligazio.

Aidha katika makabidhiano hayo walikuwepo walimu wakuu wa shule zote mbili za Kiberge mwalimu Mohamed Ally Mmandika na mwalimu mkuu wa Mchombe Good MelkiorChami wakiwemo baadhi ya wananchi wa kata ya kiberege ambao walifika kwa ajili ya kuwa mashuhuda wa tukio hilo la NMB kuchangia thamani hizo pamoja na wanafunzi ambao ni walengwa wenyewe.

Pamoja na hayo meneja wa NMB alisema kuwa hivi sasa banki yake imekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia serikali kupambana na mambo makuu mawilia ambayo ni Elimu na Afya, ambapo thamani ya zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 400 kwa kipindi cha mwaka 2019.

Fedha hizo zimetumika katika kujikita zaidi kwenye miradi ya Elimu(madawati, vifaa vya kuezeka) , Afya katika Vitanda na magodoro yake kwa ujumla na kusaidia majanga zaidi yanayo ipata nchi yetu kwa jamii, zaidi ya miaka saba mfululizo NMB imekuwa ikichangia kwa asilimia moja.

Sambamba na hayo kwa kipindi cha mwaka 2019 NMB imeamua kushirikiana na shule za kiberege kwa kutoa viti na meza 50 na shule ya sekondari mchombe pia imepata viti na meza 50 vyote vikiwa na thamani ya milioni 10, NMB kwa kipindi cha mwaka 2019 imetenga zaidi ya biloni moja(1) Kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamiiikiwemo kusaidia sekta ya Elimu na Afya kwa kiasi hicho kinaifanya kuwa banki ya kwanza katuika kuchangia maendeleo kuliko banki yoyote hapa nchini.

Meneja wa NMB Ladisalus alisema kuwa hivi sasa bank hiyo imekuwa na matawi mengi zaidi 228, ATM zaidi ya 800nchi nzima,NMB mawakala zaidi ya 7,000 pamoja na wateja zaidi ya milioni tatu(3) idadi ambayo ni hazina kubwa ukilinganisha na banki zingine hapanchini.

Hata hivyo meneja aliwataka wanafunzi wa shule hizo za Kiberege na mchombe kuhakikisha wanatunza thamani hizo na kuhakiksha wanasoma na kufaulu ili NMB iweze kuwa na moyo wa kuwachangia zaidi katika maendeleo ya Elimu kwa ujumla Wilayani humo na sehemu zinguinezo.

Naye kaimu mkurugenzi ambaye ni Afisa Elimu sekondari Dr janeth Barongo aliipongez banki ya NMB kwa kujitolea kwa kuona changamoto ilipo Wilayani kilombero hususani sehamu ya Elimu kuwa kuna change moto ya madawati pamoja na majengo ya kwa wanafunzi Wilayani humo, pia aliomba kuwa isiwe mwisho wa kuotoa michango katika shule zilizopo Wilayani humo, kwa kufanya wanafunzi waweze kusoma kwa wakati na kujengea ufaulu wao.

Dr Barongo aliendelea kusema kuwa hali hiyo imewafanyas wananchi kuona kuwa banki ya NMB ipo karibu yao kama usemi wao husema kuwa NMB karibu yako, kwa maendeleo zaidi hususani kwa motto na watu wazima kuifungulia akaunti kwao NMB.

Walimu wa shule hizo za Sekondari za kiberge na Mchombe Mwali MohamdAlly Mmandika na Good Melikior Chami walisema kuwa wapo pamoja na o katika kutoa elimu kwa wanafunzi wao na iliyo bora na siyo Elimu na kuhakikisha alama sifuri inatoweka hata kikiwezekana hata alama nne inahama kwao

Pia wanafunzi wa shule hizo waliipongeza NMB kwa kuona shida aliyokuwa nayo na kuweza kuwasaidia tamani ya meza na viti, na kuomba kuwa watakuwa makini kwa kuvitunza na kusema kuwa watakuwa wana tunza na kusoma na kuondao alama sifuri shuleni humo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Kilombero mhe Devdi Ligazio alisema kuwa niaba ya wananchi wa Kilombero kuwa hali aliyo iyona kwa Banki ya NMB kujitolea katika kuchangia thamani hizo kwake imekuwa ni faraja kubwa na kuona kuwa taasisi za kifedha kuwa ina wajali wanan jamii iliyo wazunguka na kuona faida yake.

Mhe Ligazio aliwaomba mameneja wa NMB MOrogoro Baraka Ladislaus na Abdalah Chakachaka NMB tawila Ifakara kuhakisha kutokata tama kwa kuona jamii inayo wazunguka ina endelea vuizuri na ndivyo itakavyo pata wateja wazuri na kuwapamoja hususani kauli ya Chakachaka kuwa eleza wana jamii kufungua akanti ya motto katika kukuza elimu
 MENEJA WA NMB BARAKA LADISALUS AKIKABITHIANA MEZA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI DEVDI LIGAZIO.
 MWNYEKITI HALMASHAURI DEVID LIGAZIO AKIMKABDHI DAWATI DR JANETH BARONGO KAMU MKURUGENZIKATIKATI NI MENEJA NMB BARAKA LADISLAUS.
 BAADHI YA MAAFISA WA NMB  NA UWONGOZI WA HALAMASHAURI  WILAYA NA MWENYEKITI BOODI YA SHULE NA WALIMU WAKUU WOTE WAWILI KUTOKA KULIA NA WALIYOVALIA SUTI NI MAMANEJA NMB MOROGORO NA IFAKARA ALIYE SIMAMA
 KUTOKA KULIA MWENYE MIWANI NI MKUU WA SHULE YA SEKONDARI MCHOMBE  AKIFWATIWA NA MENEJA NMB IFAKARA  ABDALAHA CHAKA CHA NA AFISA UHUSIANAO NMB
 WALIYO SIMAMA WATATU NI MENEJA NMB BARAKA  AKIWAPUNGIA WANAFUNZI BAADA YA MAKABIDHIANO .

CAG MSTAAFU UTOUH AWASHAURI WANAWAKE WAHASIBU KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI KWA MAENDELEO YA NCHI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Ludovick Utouh amewashauri wanachama wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA) kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu hasa kwa kutambua wanawake wakiamua naweza. 

Pia amewahamasisha wanawake wenye taaluma mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi kwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwakani ili kupata nafasi ya kuingia kwenye vyombo vya maamuzi pamoja na kutunga sera kwa maslahi ya wananchi wote. 

Utouh amesema hayo leo Aprili 12, 2019 wakati anafungua mkutano wa pili wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini ambao utafanyika kwa siku mbili ambapo wakati anazungumza kwenye mkutano huo amesema anaamini wanawake wanaweza na hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuungana kuleta maendeleo. 

Amesema anatambua nguvu ya wanawake huku akitoa mfano kuwa hata kupinduliwa kwa Rais wa Sudan kumetokana na nguvu ya wanawake baada ya kuamua kupaza sauti zao kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula katika masoko ya nchi hiyo. 

"Nina uhakika wanawake mnaweza, na kwa kuwa leo mnajadili kuhusu nafasi ya mwanamke katika uongozi kuna sifa za msingi ambao kiongozi mzuri anatakiwa kuwa nazo.Baadhi ya sifa hizo ni kwamba kiongozi mzuri ni yule anayekuwa na maono kwa ajili ya wale anaowangoza, uthubutu katika kufanya maamuzi na kuweka ajenda zenye tija kwa jamii unayoiongoza. 

"Hivyo mwaka huu na mwakani ni mwaka uchaguzi, nitoe rai kwenu hakikisheni mnajitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi .Utakapokuwa kwenye vyombo vya maamuzi kwa kutumia taaluma zenu mtakuwa na nafasi nzuri ya kushauri na kutoa muelekeo katika kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu,"amesema Utouh. 

Amefafanua tena kwa wanawake hao wanakila sababu ya kupambana kwa nguvu zao badala ya kusubiri nafasi za kupewa kwani kusubiri kupewa kunakwenda sambamba na kujipendekeza na kwake hayuko tayari kuona wanawake wanajipenda kwani wanaweza kufanya mambo makubwa bila kusukumwa na mtu mwingine. 

Kuhusu nafasi ya wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi, amesem utafiti uliofanyika duniani unaonesha wanawake ndio wanaoongoza kwa kuwa waamini katika kulinda raslimali za nchi ukilingana na wanaume, hivyo ameshauri kwa Serikali kutosita kuwapa nafasi wanawake katika nafasi za uongozi. 

Amesema kufika kwake kwenye mkutano huo imetokana na heshima ambayo amepewa na TAWCA hasa kwa kutambua wazo la kuanzishwa kwake limetokana na yeye akiwa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) ambapo alishauri kuanza kwa taasisi hiyo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA) Neema Kiure-Mssusa amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuwainua wanawake nchini na hasa wanachama wa TAWCA.Pia kuangalia changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi wake. 

"Katika mkutano huu tupo zaidi ya wahasibu wanawake 300, hivyo tutajadili kwa kina kuhusu changamoto zilizopo na namna ya kuzitatua maana tunaamini kwa umoja wetu tunaweza. Tutajadili kwa kina namna gani tunaweza kupiga hatua kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.Ujumbe wangu kwa wanawake nchini tuthubutu kwani tunaweza kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo,"amesema Kihure. 

Akizungumzia nafasi ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo Renata Ndege ambaye ni Meneja Mkuu Fedha TANESCO amesema wanatambua umuhimu wa mkutano huo na hivyo wakaona ni vema wakawa sahemu ya kuufanikisha. 

"Tumeona ipo sababu ya TANESCO kushiriki kikamilifu kwa kudhamini mkutano huu wa Wahasibu Wanawake.Kupitia mkutano huu wa siku mbili wahasibu hao watapata nafasi ya kubadilishana mawazo na kutatua changamoto zilizopo na kwetu TANESCO kuna wahasibu wengi wanawake, hivyo kwetu mkutano huu ni muhimu kwani unakwenda kuwajenga wahasibu wanawake na kutoka na ari mpya ya kulitumikia Taifa,"amesema Ndege. 

Kuhusu nafasi ya mwanamke, amesema kikubwa ni kujiamini na kuthubutu kwani kwake anamini hakuna unyanyasaji wowote iwapo mwanamke atasimama imara na kujiamini kwa kile ambacho anakifanya. 

"Katika mkutano wanawake wahasibu waliohudhiria leo hii ni 300 na wote huko ambako wanatoka ni viongozi.Hivyo ni kujiamini tu badala ya kusema huwezi.Nipo TANESCO nafanya kazi vizuri, sioni kunyanyaswa na mtu , kikubwa ni kuhakikisha unakuwa na sifa zinazohitajika kufanya kazi katika eneo ambalo umepewa kulitumikia.Wanawake tujiendeleze katika elimu na bahati nzuri kwa sasa wanawake wanajitahidi kusoma,"amesema Ndege. 

 Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Ludovick Utouh (kulia) akiwa ameshikana mkono na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA) Neema Kiure-Mssusa baada ya kufungua mkutano wa pili wa TAWCA ulioanza leo jijini Dar es Salaam.Utouh alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo
 Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Ludovick Utouh (kulia) akioesha tunzo aliyopewa na w Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA) Neema Kiure-Mssusa kama ishara ya kutambua mchango wake katika kuanzishwa kwa taasisi hiyo na kufungua mkutano wao wa pili uliofanyika leo Aprili 12,2019 jijini Dar es Salaam
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) mstaafu Ludovick Utouh akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu nchini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Meneja Mkuu Fedha -TANESCO ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo Renata Ndege akizungumzia sababu za Shirika la Umeme Tanzania kuamua kudhamini mkutano huo wa siku mbili ulioanza leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahasibu Wanawake Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili ulioanza leo
Sehemu ya wanawachama wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mdhibti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mstaafu Ludovick Utouh wakati anafungua mkutan o wa taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam

Dkt.Mwakyembe Awataka Watumishi Wa Wizara Kutimiza Wajibu Wao Kuwatumikia Wananchi

$
0
0


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizindua Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu Mkuu Bibi Susan Mlawi ( wa pili kushoto) ,Naibu Katibu Mkuu Bw.Nicholas William (wa pili kulia),Katibu wa Baraza hilo Bw.Bernad Lubogo (wa kwanza kulia) pamoja na Mwenyekiti wa TUGHE Tawi Bibi.Magreth Mtaki ( wa kwanza kushoto). 

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuzindua Mkataba wa Baraza hilo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma.

………………………..

Na Shamimu Nyaki-WHUSM,DODOMA.

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watumishi wa wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika kutekeleza majukumu ya kila siku ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero na kujibu hoja za wananchi kwa ufanisi na haraka.

Hayo ameyasema leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Baraza Jipya la Wafanyakazi wa wizara hiyo ambalo hukutana mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utendaji na maslahi ya watumishi.

“Napenda kusisitiza kuwa vikao vya baraza la wafanyakazi vitumike kujadili malengo na mipango ya wizara ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi ” Dkt. Harrison Mwakyembe

Ameongeza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yapo kwa ajili ya kujadili utendaji wa kila siku na jinsi ya kuboresha zaidi utendaji huo unaolenga kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Aidha Dkt. Mwakyembe amewaagiza Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia kwa dhati suala la maadili katika sehemu za kazi kwa kuhakikisha watumishi wanatumia muda wa kazi vizuri kuwahudumia wananchi.

Kwa Upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi amewakumbusha watumishi kushiriki kikamilifu na kuwa mstari wa mbele katika kupambana na VVU/UKIMWI.

“Ugonjwa wa UKIMWI unagharimu Taifa hivyo nasisitiza kuwa kiini cha ufanisi katika vita hii ni kwa kila mmoja wetu kubadili tabia” Katibu Mkuu Bibi. Susan Mlawi.

Pia amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa weledi ,bidii na tija kwa kuwa hakuna haki bila wajibu.

Naye Mwenyekiti wa TUGHE Tawi Bibi Magreth Mtaki amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi linasaidia wafanyakazi kujadili na kuboresha utendaji kazi wa Wizara ili kuleta maendeleo ya Taifa.

LUDOVICK UTOUH ASEMA CAG NDIO JICHO LA WANANCHI AACHWE AFANYE KAZI YAKE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

HATIMAYE Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) mstaafu Ludovick Utouh amevunja ukimya baada ya kueleza kuwa CAG ndio jicho la wananchi katika kuangalia mali za umma, hivyo haoni sababu ya kuibuka kwa mjadala bungeni kuhusu CAG. 

Utouh amesema hayo leo Aprili 12,2019 jijini Dar es Salaam baada ya kufungua Mkutano wa Pili wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania(TAWCA) ambapo waandishi wa habari walitaka kupata kauli yake kuhusu kinachoendelea kati ya Bunge na CAG Proesa Mussa Assad. 

"Mali za umma ni mali za wananchi, hivyo CAG ndio jicho lao katika kuhakikisha mali zao ziko salama na aachwe afanye kazi yake ,na ripoti kwenda bungeni maana yake ni kwamba kule ndiko waliko wawakilishi wa wananchi.Sioni sababu ya kuwepo kwa mjadala wa kibunge dhidi ya CAG ambao hauna tija yoyote,"amesema Utouh. 

Hata hivyo, amesema ipo haja kwa Wahasibu wengi wakiwamo Wanawake Wahasibu kuhakikisha wanashiriki katika kuwania nafasi za uongozi ikiwemo bungeni ili wakiwa huko watasaidia kuweka mambo sawa ."Kama kutakuwa na wahasibu wengi bungeni maana haya mambo yanayoendelea sasa hayawezi kuwepo kwasababu watakuwa wanajua kuhusu ripoti ya CAG,amesema Utouh wakati anazungumza na Wanawake Wahasibu nchini. 

Kwa kukumbusha tu Profesa Assad ameingia kweye mgogoro kati yake na Bunge baada ya kudai Bunge ni dhaifu kwa kushindwa kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya CAG.Baada ya kutolewa kwa kauli hiyo Bunge kupitia kwa Spika Job Ndugai liliamua kumjia juu kwa kumtaka kuomba radhi. 

Siku za hivi karibuni Bunge lilitoa azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa madai ameshindwa kuomba radhi huku Spika Ndugai akisema kuwa watafanya kazi na ofisi ya CAG na sio Profesa. 

JKCI KINARA HUDUMA BORA ZA MAGONJWA YA MOYO AFRIKA MASHARIKI NA KATI

$
0
0

Na Frank Mvungi- MAELEZO 

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetajwa kutoa huduma katika viwango vya kimataifa na hivyo kupokea wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo ya Afrika Mashariki na Kati. 

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa kwa sasa taasisi hiyo ina vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ikiwemo mtambo wa kufanyia upasuaji kwa njia ya tundu dogo bila kufungua kifua cha mgonjwa kama ilivyo katika nchi zilizoendelea. 

“Kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali katika taasisi yetu kwa mwaka 2018 tuliweza kuwafanyia upasuaji wagonjwa zaidi ya 1400 ambao pengine wangetakiwa kupelekwa nje ya nchi hivyo tumeasaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi wenye magonjwa ya moyo” alisisitiza Prof. Janabi. 

Akifafanua amesema kuwa jukumu lao kama taasisi ni kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa wananchi na kwa sasa wagonjwa takribani 300 wanahudumiwa katika taasisi hiyo kila siku. 

Aliongeza kuwa kwa sasa taasisi hiyo inafanya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya asilimia 85 wanaofika kupata matibabu, lengo likiwa kufikia asilimia 90 kutokana na uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya tano. 

“Bilioni 5 zimetumika kununua na kusimika mtambo wa kusaidia kufanya upusuajia kwa njia ya tundu dogo” alisisitiza Prof. Janabi .Pia wameanzisha kitengo maalum cha kuhudumia watoto wenye matatizo ya moyo na kufanya uchunguzi kwa watoto wakiwa bado hawajazaliwa ili kuona kama wana tatizo lolote katika moyo. 

Katika kuimarisha huduma zake JKCI imekuwa na utaratibu wa kualika madaktari bingwa wa moyo kutoka hospitali rafiki kwa ajili ya kushirikiana kufanya upasuaji na kukuza ujuzi kwa madaktari bingwa wazalendo. 

Baadhi ya huduma mpya zilizoanzishwa ni pamoja na huduma ya kuweka betri kwenye moyo, kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo ambapo wagonjwa 7 hadi 10 wanafanyiwa upasuaji kwa njia ya tundu dogo na wagonjwa 2 hadi 4 upasuaji kwa njia ya kufungua kifua kila siku. 

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kitwete imejengwa kwa gharama ya Bilioni 26 na imekuwa ikiboresha huduma zake mwaka hadi mwaka ili kukidhi mnahitaji na kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kupata matibabu ya moyo ambapo tayari inahudumia asilimia 85 ya wagonjwa wote wanaofikishwa katika taasisi hiyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MIGORI WAKATI AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI DODOMA

$
0
0


35
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Migori katika jimbo la Isimani mkoani Iringa wakati akielekea mkoani Dodoma.
678
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Migori katika jimbo la Isimani mkoani Iringa wakati akielekea mkoani Dodoma.
9A10A
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi pamoja na Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuagiza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Shilingi milioni 400 katika eneo la Migori mkoani Iringa.
11
Wananchi wa Migori wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuagiza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Shilingi milioni 400 katika eneo la Migori mkoani Iringa.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Iringa kuwashukuru wakati kabla ya kuelekea mkoani Dodoma.
13A
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na machhifu wa Kimila wa mkoa wa Iringa mara baada ya kuwashukuru viongozi mbalimbali wa mkoa wa Iringa.
1415
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza huku akiwa ameshika Kitambulisho cha Mjasiriamali mdogo  (Mmachinga) ambae amedai kuwa bado wanatozwa ushuru. Rais Dkt. Magufuli amepiga marufuku kudai ushuru kwa wafanyabiashara wote wenye vitambulisho hivyo ambao mtaji wao hauzidi Shilingi milioni 4. PICHA NA IKULU


DAWASA KUFUFUA VISIMA VYA PEMBEZONI KWA MJI DAR ES SALAAM NA PWANI

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akimsikiliza Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa wakati akimuonyesha ramani ya mtandao wa maji utakavyokuwa wakisambaziwa wananchi na Gezaulole.
Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Neli Msuya (mwenye kofia) akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa kwanza kushoto) mara baada ya kutembelea mradi wa Kisima cha Maji cha Gezaulole kichojengwa kwa muda mrefu na kimekuwa kikitoa huduma kwa watu wachache tu. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akimsikiliza Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa wakati akimuonyesha genereta inayotumika kufua umeme kwa ajili ya kusambazia wakazi wa Gezaulole.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasha mashine.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akionyeshwa mashine zilizokuwa zikitumika kuvuta maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akimsikiliza Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa wakati akimuonyesha kisima cha maji kinachotumika kusambazia wakazi wa Vijibweni, Kigamboni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelekezo kwa msimamizi wa mradi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja  akitoa maelekezo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

 Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imeanza mchakato wa kuvifufua na kuvirejesha visima vilivyojengwa na Serikali na kuachwa kwa muda mrefu bila kutumika kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa pembezoni mwa mji. 

 Akizungumzia mchakato huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuna maeneo ambayo hayana mtandao wa maji ya bomba kwahiyo wameamua kuvifufua visima vilivyojengwa muda mrefu na serikali au wahisani ili viweze kuhudumia wananchi wa maeneo hayo na yaliyokaribu. Amesema, kuna kisima kilichopo Gezaulole na Vijibweni tayari wameshaanza kuvifanyia tathmini na vinatarajia kuanza kutoa maji kwa wananchi wa maeneo hayo na yaliyokaribu nao. 

 “Visima hivi vilijengwa kwa muda mrefu sana, katika maeneo ambayo hayana mtandao wa DAWASA tumeamua kuwapelekea huduma ya maji kwa kutumia visima hivi ambavyo maji yake ni safi na salama,”amesema Luhemeja.

 “Ninapoongelea asilimia 85 ya wananchi wanaotumia maji safi na salama ndani ya mkoa wa Dar es Saalaam namaanisha na huduma hii ya visima, na lengo letu ni kuhakikisha kuwa ifikapo Juni 2020 tunataka Watu wote wawe wanapata maji,” Msimamizi wa Miradi ya Pembezoni Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa amesema bado wanaendelea na tathmini ya kufahamu visima hivyo vina uwezo wa kuhudumia wananchi wa ngapi pamoja na kujenga tenki la kuhifadhi la maji. 

 Nao Wananchi wa eneo la Gezaulole wamefurahi kuona wanatarajia kupata maji safi na salama kwakuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wanatumia maji ya visima ambapo ni vifupi na kuhatarisha maisha yao kiafya hususani ifikapo kipindi cha mvua, visima huchafuka na kuchanganyika na udongo. Kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam unapata maji Lita Milion 502 kutoka kwenye vyanzo vya Ruvu juu, Ruvu Chini na Mto Kizinga. 

 Ziara hiyo itaendelea tena kesho kwa kutembelea miradi mingine ikiwemo maunganisho mapya ya wateja, mradi wa Maji Chalinze na Miradi mingine inayoendelea kujengwa kwa kutumia fedha za ndani za DAWASA ambapo takribani Bilion 3 zinatumika kila mwezi.

52%Ya uharibifu wa mazingira wa miti unafanyika katika halmashauri nyingi hapa chini

$
0
0


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Kinyerembe Lwota akizungumza katika Mkutano wa Mabadilikobya Tabianchi Jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Bajeti na mbunge wa Kibakwe George Simbachawene akichangia jambo katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Forumcc Rebbecca Munna akichangia jambo katika mkutano waliouandaa wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dodoma katika hotel ya Morena
Mbunge wa Babati vijijini Mhe. Jitu Soni akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa mabaliko ya tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shahibu akitoa ufafanuzi wa kile wanachokifanya katika halmashauri hiyo katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dododma
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Singida Rehema akieleza namna ambavyo wanakabiliana na kutunza mazingira


Dkt. Ronald Ndesajo kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha matokeo ya Tathmini ya Kijinsia na Madhara ya Mabadiliko ya Tabianchi.


Na.Vero Ignatus. Dodoma


Serikali za mitaa nchini zimetakiwa kubuni miradi ya kupunguza hewa ya ukaa ,kilimo,misitu,na kutengeneza ajira kupitia shughuli hizo ambazo zina wajibu wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi maana wao ni watekelezaji wa sera.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Kinyerembe Lwota ambapo 52%ya uharibifu wa mazingira wa miti unafanyika katika halmashauri nyingi nchini amesema asilimia 90 ya watanzania wanatumia mkaa majumbani kwao ni zaidi na huo ni uharibifu mkubwa zaidi ya hekari laki 4 kwa mwezi

Amesema upandaji wa miti unaofanyika kwa sasa haulingani na uharibifu uliofanyika amesema upandaji wa miti unahitajika ufanyike kwa wingi kulingana na matumizi yaliyofanyika amesema wao kama kamati ya bunge wanaomba gesi ipungue bei ili wanancgi waweze kutumia hiyo swala la miti na mikaa itapungua kwa kiasi kikubwa

“Kamati ya bunge ya Ardhi,maliasili,utalii tulifanya ziara katika ziwa manyara hali ya lile ziwa ni mbaya kabisa ukiangalia tunakoelekea ziwa lile linakwenda kukauka kabisa ,baada ya hapo tulitoa ushauri na tumeona hatua zinachukuliwa kwaajili ya kulinusuru kwasababu utalii wetu ni wawanyama na wanyama wanapata maji na malisho katika ziwa hilo”.Alisema Kinyerembe

Amesema jambo lingine walilolifanya kama kamati ni kuishauri serikali TFS kuwa Mamlaka kamili kwani kwa sasa haina mamlaka ya kufanya shughuli hizo kwa mapana zaidi kwani uwajibikaji wa moja kwa moja haupo ila itakapokuwa mamlaka ni rahisi kuwabana

Kwa upande wake mkurugenzi wa FORUMCC amesema kuwa swala la upatikanaji wa taarifa sahihi wa mabadiliko ya tabianchi haswa maeneo ya vijijini wana elimu duni juu ya mabadiliko ya tabianchi ,amewataka wanahabari kuhakikisha wanaandika taarifa amabazo zitawafikia watu wa vijijini

Amesema ukulima isiwe ndiyo sababu ya uharibifu wa mazingira tufanye kilimo chenye tija na maslahi kwetu na vizazi vijavyo vije kufaidika kwa kukuta mazingira mazuri nah ii lazima tutunze mazingira yetu.alisema Rebecca.

Nawapa changamoto ya kila mmoja kutokuwa muhudhuriaji tu wa semina lakini pia wawe watendaji. Nashukuru sana wote tulioshirikiana nao wakiwamo OxfamTz na timu nzima ya vijana wa mitandao ya kijamii. Mhe. JMakamba amekuwa anatoa sana sapoti katika posti zetu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shahibu amesema kuwa kwenye eneo la mazingira wametoa elimu katika shule za msingi ambapo wanafunzi wanaelewa namana ya kulinda na kutunza mazingira ,amabapo amesema kuwa wamepiga kelele kuhusiana na utupaji wa taka hovyo na kwa sasa wanaelekea kwenye shule za sekondari.

Amesema Halmashauri hiyo imefanya kazi ya kuwajengea uwezo madiwani ili kuhakikisha kuwa wanatengeneza sharia mbadala kwenye serikali za mitaa ili kulinda mazingira mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa sasa mabadiliko hayo yanaathiri watu wengi

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Ufugani na Maji na mbunge wa Babati vijijini Mhe. Jitu Soni amesema kuwa anatamani Halamashauri zote, vijiji, tarafa, wilaya hata mikoa iwe na mashindano ya kutunza mazingira.

Amesema hiyo italeta motisha mkubwa katika jamii na eneo husika hakuna atakayekubali kuwa wa mwisho katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama  Kaya moja ikiwa inatumia kuni na mkaa kwa miaka 10 wanakuwa wameteketeza ekari zaidi ya 30 Je Ni Watanzania wangapi wanapanda miti ya kutosha? Tunalikaribisha jangwa ~ Frank Luvanda kutoka SUHOLE foundation Morogoro


Dr Ronald Ndesajo kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha matokeo ya Tathmini ya Kijinsia na Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na Uwezo wa Kukabiliana Nayo kwa Miradi ya Ardhi Yetu Programme(AYP II) na HELP Katika hali ya kawaida, Kilimo kimepatwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi

Ndesanjo amesema kutokana na changamoto hiyo, kwa asilimia kubwa Wanawake wamepatwa na changamoto kwa kiasi kikubwa,Pili Wanawake ndio wanaoshughulika na shughuli za kila siku nyumbani ; Upatikanaji wa maji tabu sana




















Hasunga Atoa Agizo kwa Bodi za Mazao Kukamilisha Kanzi Data za Wakulima Ifikapo Juni 30

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Serikali imetoa agizo kwa Wakurugenzi wa Bodi za Mazao ya Kilimo nchini kukamilisha Kanzi Data ya wakulima wote itakayowawezesha wakulima hao kutambulika kwa urahisi.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati alipokuwa akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) kupitia mradi wa RARIS. 

Hasunga amesema kuwa muda umefika ambapo ni lazima nchi iwe na Kanzi Data ambayo itaonyesha taarifa zote za wakulima zikiwemo za kutambua idadi ya wakulima, eneo wanalofanyia kilimo,aina ya mazao yanayolimwa pamoja na kufahamu wakulima wakubwa, wakati na wadogo pia itasaidia kuweka mipango endelevu na kufanya maamuzi sahihi kwa wakulima hao.

"Imefikia wakati wakulima nao watambulike na kupewa vitambulisho, tulishakaa vikao na Bodi zote za mazao kujadili suala hilo hivyo natoa agizo kuwa ifikapo Juni 30 mwaka huu Bodi zote ziwe na Kanzi Data za wakulima isipokuwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo Kanzi Data yake itachukua muda kidogo kukamilika kwa sababu ya kuwepo kwa mazao mchanganyiko." alisema Hasunga.

Hasunga ameongeza kuwa hadi kufikia muda huu, uandikishaji wa wakulima hao unaridhisha kwani kufikia Machi, 31 mwaka huu, uandikishaji huo umefikia takribani asilimia 72 ambapo jumla ya wakulima 1,274,337 kati ya lengo la makadirio ya wakulima 1,700,000 wamefikiwa.

Aidha, Hasunga amefafanua kuwa ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, lazima kuhakikisha tunaanzisha Bima ya Mazao ambayo itasaidia kilimo nchini kuwa na ulinzi hata ikitokea changamoto yoyote kwa wakulima lazima walipwe fidia kama biashara zingine zinazofanyika.

Akielezea kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mratibu wa Mradi, Osward Mashindano amesema kuwa mradi huo ulianza mnamo Oktoba, 2018 na unatekelezwa kila baada ya miezi mitatu ambapo kwa sasa wanaandaa utekelezaji kwa mara ya tatu.

"Kupitia mradi huu Shirika la UNDP na ESRF wametoa msaada wa vifaa kwa ajili kurahisisha utendaji kazi wa wizara hiyo vikiwemo vya vishikwambi 50, Kompyuta mpakato tatu, printa mbili pamoja na vifaa viwili vya kurekodia", alisema Mashindano.

Kilimo ndio msingi wa maendeleo, takwimu zinaeleza wazi kuwa kilimo kinatoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi ambapo kinachangia asilimia 28.1 ya Pato la Taifa, asilimia 30 ya fedha za kigeni. asilimia 65.5 ya ajira zote zilizopo hapa nchini, asilimia 66 za malighafi zinazohitajika viwandani pamoja na asilimia 100 ya chakula.

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kupotea msaada wa Tablets na vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Mradi RARIS kwa kupitia UNDP na ESRF, leo Jijini Dodoma, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na kwa upande wa kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Natalie Boucly.
Mratibu wa Mradi wa RARIS kutoka ESRF Dkt.Osward Mashindano akitoa taarifa ya namna Mradi wa Kilimo wa RARIS utakavyorahisha upatikanaji wa taarifa muhimu za wakulima kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (hayupo pichani) katika hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa kupitia mradi huo unaofadhili na UNDP pamoja na ESRF leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga (wasita kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Bodi mbalimbali ya mazao ya Kilimo mara baada ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitolewa na UNDP/ESRF kupitia mradi wa RARIS uliyodhaminiwa na Shirika la Maendeleo ya UNDP, ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Natalie Boucly (wasaba kulia) na Katibu Mkuu Wizara Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (wasita kulia) leo jijini Dodoma. 

Rais Magufuli ataka wajasiriamali wasibughudhiwe

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kuhakikisha Wajasiriamali wenye vitambulisho hawatozwi ushuru wala tozo nyingine yoyote inayohusiana na biashara wanazofanya na kwamba kama kuna sheria ndogo zilizokuwa zikihalalisha utozaji huo zibadilishwe.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 12 Aprili, 2019 baada ya wananchi wa Migori Wilayani Iringa na Mtera Wilayani Mpwapwa kuusimamisha msafara wake uliokuwa ukielekea Dodoma na kumueleza kuwa wamekuwa wakitozwa kiwango kikubwa cha ushuru licha ya kuwa na vitambulisho vya Wajasiriamali.

Akiwa Migori wauzaji wadogo wa samaki wamedai Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imemweka mzabuni ambaye amekuwa akiwatoza ushuru wa zaidi ya shilingi 5,000 kwa kila tenga la samaki lenye uzito wa kilo 10, na kufuatia malalamiko ya Wajasiriamali hao (wengi wao wakiwa akina Mama) ameiagiza Halmashauri hiyo kuvunja mkataba na mzabuni aliyepewa kazi ya kukusanya ushuru wa halmashauri hiyo na kuhakikisha sheria ndogo inayotumiwa kukusanya ushuru huo inarekebishwa.

Akiwa Mtera, Mhe. Rais Magufuli amemtaka mzabuni anayekusanya ushuru kwa niaba ya halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kumrejeshea fedha zake kiasi cha shilingi 4,000 Mjasiriamali Leticia Mgonafivi baada ya Mjasiriamali huyo kudai ametozwa ushuru huo hapo jana licha ya kuvaa kitambulisho cha Mjasiriamali alichokilipia shilingi 20,000/-.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero nyingine za wananchi waliosimamisha msafara wake ambapo akiwa Migori Wilayani Iringa ameahidi kuwa Serikali itatoa shilingi Milioni 400 kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya cha Migori ili kutatua changamoto ya matibabu inayoikabili kata ya Migori yenye wakazi 18,000.

Mbunge wa Jimbo la Ismani Mhe. William Lukuvi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa Serikali kutatua tatizo la maji katika eneo la Migori baada ya kutekeleza mradi uliogharimu shilingi Bilioni 1 na Milioni 383 na pia ameshukuru kwa Serikali kutoa shilingi Bilioni 1 na Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Migori kwa kuacha uvuvi haramu na pia amewashauri wakulima wa eneo hilo na maeneo jirani kulima mazao yanayostahimili ukame badala ya kung’ang’ania kulima mahindi ambayo yamekauka kabla ya kukomaa kutokana na uchache wa mvua.

Mhe. Rais Magufuli amechangia shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la maabara la Shule ya Msingi Chipogolo na ameagiza shule hiyo ipelekewe umeme.

Pia amemuagiza Diwani wa kata ya Mtera Mhe. Amoni Kodi kuandika kibao cha kuyatambulisha majengo yaliyoachwa na mkandarasi wa barabara ya Iringa –Dodoma kuwa Kituo cha Afya cha Mtera na amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo kuhakikisha kituo hicho kinapelekewa watumishi na kinaanza kutoa huduma.

Mapema kabla ya kuondoka Mjini Iringa kuelekea Dodoma Mhe. Rais Magufuli amewaalika katika chai ya asubuhi viongozi wa Mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Ali Hapi, na katika salamu zake amewapongeza kwa umoja walionao katika kushughulikia kero za wananchi na kuhimiza maendeleo.

Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mhe. Ali Hapi kukifuatilia kiwanda cha karatasi cha SPM Mgololo kama kinafanya kazi kama ilivyotarajiwa ikiwemo jukumu kuu la kuzalisha karatasi.

Mhe. Rais Magufuli amewasili Mkoani Dodoma baada ya kumaliza ziara yake katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa iliyoanza tarehe 10 Aprili, 2019.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
12 Aprili, 2019
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live




Latest Images