Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA MICHEZO JUMUIYA YA MADOLA IKULU ZANZIBAR

0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais wa Shirikisho la la Michezo la Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin alipowasili katika ukumbi wa mkutano Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo,11-4-202019
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Shirikisho la Michezo la Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo, 11-4-2019. akiwa na Ujumbe wake.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiuliza Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, alipofiki Ikulu Zanzibar , kuonana na kufanya mazungumzo leo 11-4-2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, kushoto akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.11-4-2019
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Bi. Dame Louis Martin, wakitowa ukumbi wa mkutano baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar 11-4-2019
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake baada ya kumaliza mazungumzo yao Bi. Dame Louis Martin yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

SERIKALI YASAINI MAKUBALIANO UZALISHAJI WA SAMAKI.

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Norad, Norway imesaini mkataba wa uzalishaji samaki aina ya Sato zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mradi huo,  Katibu Mkuu Uvuvi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah amesema,  mradi huo umekuja muda muafaka wakati nchi ina mahitaji makubwa.

Amesema lengo la Serikali ni kuzalisha samaki kwa wingi ambapo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwenye mabwawa.Amesema mradi huo umekuja kwa sababu ya kazi nzuri ya asasi ya NorgesVel, Chama cha Ukuzaji Viumbe Maji Tanzania (AAT) na Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA).

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka 20 sasa Tanzania imekuwa haifanyi vizuri katika sekta ya uvuvi ambapo imekuwa ikizalisha samaki tani 350,000 hadi 380,000 kwa mwaka."Samaki wanaozalishwa hivi sasa kwenye vyanzo vya maji idadi yake imebaki kuwa vilevile haiongezeki kwa kasi hivyo kuna kila haja ya kuongeza kasi ya uzalishaji,"alisema Tamatamah.

Amesema serikali ina nia ya dhati katika kuendeleza ufugaji samaki japokuwa imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa.Tamatamah amesema fursa zilizopo hapa nchini ni pamoja na vyanzo vya vya maji, hali ya hewa na mazingifa lakini wameshindwa kuzalisha tani za kutosha.

Amesema hadi sasa Tanzania imekuwa ikizalisha tani 16,000 wakati Norway inazalisha tani milioni 2.5 kwa mwaka."Hii ni fursa kwetu kwakuwa wenzetu wana ujuzi wa uzalishaji samaki, itasaidia kutuongezea ujuzi na sisi,"alisema Tamatamah.Mradi huo utatekelezwa Kibaha mkoani Pwani ambapo vijana watapata fursa ya elimu pamoja na luzalisha samaki.

Amesema ana amini hakuna uzoefu mbadala kwa mbinu hiyo kwani ni moja ya njia sahihi ya kupata ujuzi.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama mradi huo ni fursa na neema kwa wananchi wa Kibaha.

Alisema anaamini mradi huo utaongeza idadi ya samaki wanaozalishwa nchini pamoja naa kukuza uchumi wa nchi.Naye, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elizabeth Jacobson alisema, ana imani mradi huo utafungua fursa kwa vijana na kukuza uchumi wa nchi.

Alisema mradi huo umeletwa ili kutokomeza changamoto zilizopo za uhaba wa samaki pamoja na kufungua njia za ujasiriamali kwa wananchi.
 Afisa Mtendaji Mkuu FETA Yahaya Mgawe (kushoto) akisaini makubaliano  ya uzalishaji samaki aina ya Sato zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka katika kipindi cha miaka 10 ijayo  katikati ni Mshauri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norgesvel Reinaart Pretorius leo jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu Uvuvi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah akizungumza na katika hafla ya kusani makubalino ya mkataba wa uzalishaji samaki aina ya Sato zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka katika kipindi cha miaka 10 ijayo leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Katibu mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi-Uvuvi Rashid Tamatamah akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini makubaliano ya uzalishaji wa samaki aina ya Sato leo jijini Dar es Salaam.

WAJUMBE WA NEC WASHAURI UBUNIFU WA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU UIGWE

0
0

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga (katikati mbele), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya(wa sita kushoto mbele) wakiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali na wanafunzi wa kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoani Simiyu, wakati wa makabidhiano ya chakula (mchele na maharage), kilichotolewa na Ndg. Emmanuel Gungu Silanga na Wajumbe wenzake wa NEC na baadhi ya viongozi CCM mkoa kwa wanafunzi hao walio katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa .
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni hapo wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga na viongozi wengine walipokabidhi msaada chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kabla ya kukabidhi msaada wa chakula kwa ajili ya wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita walio katika Kambi ya Kitaaluma katika Shule ya Sekondari Maswa, wakifurahia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) na Mkoa wa Simiyu, waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa chakula na kuzungumza na wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kutoka Mkoa wa Geita, Ndg. Idd Kassim Idd akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, alipotembelea shuleni hapo wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga alipokabidhi msaada wa kilo 100 za mchele na kilo 400 za maharage kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya akimpongeza mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kutoa maneno ya shukrani kwa baadhi ya viongozi mbalimbali wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC na Mkoa wa Simiyu waliofika shuleni Aprili 11, 2019 hapo na kutoa msaada wa chakula.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha, Ndg. Anna Agatha Msuya(katikati) akizungumza jambo na baadhi ya viongozi na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, allipotembelea shuleni hapo Aprili 11, 2019.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu, Mariam Manyangu akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika Kambi ya Kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, wakati alipotembelea shuleni hapo wakati Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga alipokabidhi msaada wa kilo 1000 za mchele na kilo 400 za maharage kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.

………………………….

Na Stella Kalinga, Simiyu

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mikoa ya Arusha na Geita wamewapongeza viongozi Mkoani Simiyu kwa ubunifu waliofanya kuanzisha kambi za kitaaluma kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kutoa wito kwa viongozi wengine kuiga ubunifu huu ili waweze kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.

Hayo yamesemwa na Ndg. Anna Agatha Msuya Mjumbe wa NEC (Arusha) na Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita) mara baada ya kutembelea wanafunzi wa Kidato cha Sita mwaka 2019 walio katika kambi ya kitaaluma inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, mara baada ya viongozi hao kuungana na Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga kukabidhi msaada wa chakula kwa wanafunzi hao Aprili 11, 2019.

Akizungumza mara baada ya msaada wa chakula kukabidhiwa Ndg. Anna Agatha Msuya amesema laiti kambi hizi zingekuwa zinafanyika katika maeneo mengi matokeo ya Mitihani hususani ya Taifa yangekuwa mazuri zaidi ya sasa kwani zimeonekana kuusaidia mkoa wa Simiyu kupanda kielimu.

“Nimevutiwa na ubunifu wa Simiyu kuwa na kambi za kitaaluma, tungekuwa na matokeo mazuri kama tungekuwa na viongozi wa Serikali wabunifu kama hapa Simiyu, naomba tulichokiona Simiyu kifanyike na mikoa mingine; mwaka juzi walikuwa wa 26 Kitaifa, mwaka jana wakawa wa 10 na naamini kwa kambi hii hatutaikosa Simiyu katika mikoa mitano bora” alisema Anna Agata Msuya.

Naye Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita) pamoja na kupongeza juhudi za mkoa wa Simiyu katika elimu, ameahidi kuwa amejifunza kupitia kambi hiyo ya kitaaluma na kulichukua wazo hilo kwa jili ya kushauri viongozi wa mkoa wa Geita kuona namna ya kulifanyia kazi ili kuwa na ufaulu mzuri.

Aidha, Mwl. Ezekiel Mollel mwekezaji katika Sekta ya Elimu amesema suala la kambi za kitaaluma ni la kipekee kwa mkoa wa Simiyu, hivyo akatoa wito kwa mikoa mingine kuiga huku akiwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuendelea kuchangia mahitaji mbalimbali ya wanafunzi walio katika kambi ili waweze kujifunza kwa amani wakiwa na mahitaji ya msingi.

Kwa upande wake Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Simiyu, Ndg. Emmanuel Gungu Silanga amesema ametimiza ahadi yake ya kutoa kilo 1000 za mchele na kilo 400 za maharage kwa wanafunzi wa kidato cha Sita na kueleza matarajiao ya wana Simiyu kwa wanafunzi hao kuwa, ni kuwaona wanasoma kwa bidii na hatimaye waifanye Simiyu kuwa ya kwanza Kitaifa mwaka 2019.

Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzao wa kidato cha Sita mwaka 2019 walioko kambini Hidaya Simba(Maswa Girls) na Masanja Ng’hwenu (Meatu) wamewashukuru viongozi hao kwa msaada wa chakula walioutoa na kuahidi kuwa shukrani yao kubwa kwa walimu, viongozi, wazazi na wadau wa elimu wanaowasaidia ni kufanya vizuri na kuifanya Simiyu iwe nambari moja.

Pamoja na kilo 1000 za mchele na kilo 400 za maharage zilizotolewa na Mjumbe wa NEC (Simiyu), Ndg. Emmanuel Gungu Silanga, Ndg. Idd Kassim Idd Mjumbe wa NEC(Geita) ametoa kilo 200 za mchele, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu ametoa kilo 100, Mdau wa Elimu Ezekiel Mollel kilo 50 na Ndg. Anna Agatha Msuya Mjumbe wa NEC (Arusha) ameahidi kutoa zawadi kwa wanafunzi watakaopata daraja la kwanza(divion one)

WANANCHI WANUFAIKA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI (TASAFU) watakiwa kutunza miradi walioibuni.

0
0
Wananchi wanaonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) wametakiwa kutunza na kuiendeleza miradi waliobuni na kutekelezwa na serikali ili iendelee kuwahudumia na kuwanufaisha mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha miradi hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Shaaban Seif Mohamed alieleza hayo wakati alipokuwa katika ziara maalum iliojumuisha Wilaya ya Magharibi “A”na Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa lengo la kukagua miradi hiyo ya TASAF awamu ya tatu na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi hao ili kuzipatia ufumbuzi.

Katibu Mkuu Shaabani alisema, serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuwaanzishia wananchi wake miradi mbali mbali lakini hujitokeza changamoto ya kuilinda na kuendeleza miradi hiyo pale serikali inapoiwacha mikononi mwa wananchi pindi miradi inapofikia ukingoni.

Akikagua kituo cha Afya kilichopo Kianga na Nyumba ya Madaktari iliopo Matamwe Kijini ambavyo vyote vimesaidiwa kupitia Mradi wa TASAF Katibu Mkuu amesema wananchi wanapaswa kuiendeleza miradi hiyo kwa niaba ya serikali na wasisite kuwachukulia hatua endapo watawaona watu wasiokuwa waaminifu wakiharibu miradi yao.

“Baadhi ya watu hawathamini jitihada za serikali ambazo zinalenga kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo hufanya hujuma za makusudi nawaombeni msisite kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi” Alieleza Katibu Shaaban.

Katika ziara hiyo ametembelea mradi wa Kilimo katika bonde la kizimbani bonde ambalo Mpango wa kunusuru kaya maskini umeliendeleza kwa kuligawa kwa kujenga matuta maalum na kuweka miundombinu ya kupitishia maji kwa vile serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dk. Ali Mohamed Shein itaendeleza jitihada hizo.

Akitolea ufafanuzi suala la baadhi ya watu kutoa upinzani kwa kuwabeza na kuwapuza katika shughuli zao za kilimo alisema serikali italipatia ufumbuzi suala hilo kwa kuendelea kuwaelimisha watu hao ili waachane na vitendo visivyofaa ili lengo la serikali la kuwaletea maendeleo wananchi wake liweze kufikiwa.

Wakulima walionufaika na mradi wa kupunguza Kaya Maskini walimueleza Katibu Mkuu kupitia ziara yake hiyo kuwa, wameishukuru serikali ya mapinduzi kutokana na miradi walioanzishwa imewaletea matunda kwa kupata kipato kinachowasaidia katika kutatua matatizo yanayowakabili.

Pamoja na mambo mengine wananchi hao kupitia katibu mkuu huyo wameiomba serikali kuwapatia vifaa vitakavyowasaidia kuendeleza shughuli zao za kilimo ili waweze kuzalisha za kupata kipato cha ziada.

Akiwa katika kijiji cha Kijini Katibu mkuu Shaaban alipokea changamoto inayolalamikiwa na wananchi hao juu ya kukosekana kwa daktari wa kudumu katika spitali yao licha ya kuchukuwa jitihada ya kujenga nyumba maalum ya kulala daktari pamoja na kuweka miundombinu yote ikiwemo umeme, maji safi na salama.

Wamesema kukosekana kwa daktari wa kulala kijijini hapo kumepelekea wananchi wanapatwa na maradhi nyakati za usiku kupata usumbufu na kupelekea kutafuta huduma masafa marefu.

Nae Mkurugenzi Uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Khalid Bakar Amrani amewaeleza wananchi hao kuwa hivi sasa serikali ipo katika mchakato wa kuwapelekea awamu nyengine ya TASAF. hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupitia kwa masheha katika shehia zao na kutoa taarifa sahihi zitakazoisaidia serikali kupanga mipango yake.

Ziara hiyo ya Katibu mkuu imejumuisha shehia za Kianga, Kizimbani, Donge mbiji, na matemwe kijini ambapo amepata fursa ya kutembelea miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya na Kilimo iliyobuniwa na wanakaya husika.

Kassim Salum Abdi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mashamba ya kilimo cha mpunga cha Kizimbani yanayoendelezwa na Wakulima kupitia Kaya Maskini chini ya Mradi wa Tasaf Awamu ya Tatu.
Wanakaya Maskini wa Kijiji cha Donge Mbiji wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Shaaban Seif hayupo pichani alip[ofanya ziara ya kuangalia changamoto zinazowakabili.
Sheha wa Shehia ya Donge Mbiji Abdulla Machano Haji akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Shaaban Seif alipofika kuangalia changamoto zinazowakabili.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mophamed akizungumza na Wananchi wa Matemwe Kijini kwenye Kituo cha Afya cha kijiji hicho alipokuwa katika zaiara ya kutembelea Miradi ya Tasaf iliyobuniwa kwa Kaya Maskini.Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Uratibu wa shughuli za serikali SMT, SMZ Khalid Bakar Amrani.
Muonekano wa Kituo cha Afya cha Shehia ya Kianga kilichojengwa kupitia Mradi wa Tasaf Awamu ya Tatu kikiwa katika hatua ya mwisho lakini tayari kimeanza kutoa huduma.
Picha na – OMPR – ZNZ.

KUMBUKIZI YA 35 YA KIFO CHA EDWARD MORINGE SOKOINE

0
0
 
1. Usuli:

Ijumaa ya leo, tarehe 12 April 2019, Taifa letu linatimiza miaka 35 toka kipenzi cha watanzania, marehemu EDWARD MORINGE SOKOINE, afariki kwa ajali ya gari tarehe 12 April 1984 eneo la Dakawa, wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

2. Kuzaliwa kwa SOKOINE:

Jumatatu ya tarehe 1 Agosti 1938, katika kitongoji cha Kilasho, kijiji cha Emairete, Monduli Juu, Arusha, huku mvua kubwa ikirindima, alizaliwa mtoto wa kiume aliyekuja kuitwa EDWARD MORINGE SOKOINE. Baba yake aliitwa SOKOINE OLE SEVERE na mama yake aliitwa NAPELEL SINYATI NOOMAYAKI.

3. Elimu:

SOKOINE alisoma Shule ya Msingi Monduli kuanzia mwaka 1949 hadi 1953 na kisha akajiunga na "Monduli Middle School" toka mwaka 1953 hadi 1956. Baada ya hapo alijiunga na Shule ya Sekondari ya Umbwe alikosoma mwaka 1956 hadi 1958.

4. SOKOINE Ajiunga na TANU:

Tarehe 1 Januari 1961,SOKOINE alijiunga na chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ikiwa ni miezi michache kabla ya Tanganyika haijapata uhuru.

5. SOKOINE Agombea Ubunge:

Tarehe 25 Octoba 1965, SOKOINE, akiwa kijana mdogo tu wa miaka 27 lakini mwenye akili na ubunifu mkubwa, aligombea na kushinda ubunge jimbo la Monduli.

6. Mh. SOKOINE Aukwaa Uwaziri Mdogo:

Mwaka 1967, Mh.SOKOINE aliteuliwa na Rais NYERERE kuwa Naibu Waziri, Wizara ya Mawasiliano, Usafirishaji na Kazi.

7. Mh. SOKOINE Aukwaa Uwaziri Kamili:

Mwaka 1970, Rais NYERERE, baada ya kuvutiwa na uchapakazi wake, alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri wa Nchi na mwaka 1972 akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

8. Mh. SOKOINE Awa Mjumbe wa CC ya CCM:

Baada ya CCM kuzaliwa kutokana na TANU na ASP kuungana tarehe 5 Februari 1977, Mh. SOKOINE akawa mjumbe  wa Kamati Kuu ya CCM.

9. Mh. SOKOINE Ateuliwa kuwa Waziri Mkuu:

Tarehe 13 Februari 1977, kutokana na utendaji kazi wake mujarab, Rais NYERERE alimteua Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu.

Hata hivyo, tarehe 7 Novemba 1980, Mh. SOKOINE alijiuzuru na kwenda masomoni Yugoslavia na nafasi yake ikachukuliwa na Mh. CLEOPA DAVID MSUYA.

Baada ya kurejea, Rais NYERERE alimteua tena Mh. SOKOINE kuwa Waziri Mkuu tarehe 24 Februari 1983. Aidha, mwaka huo wa 1983, Mh. SOKOINE alianza kusomea shahada ya "Political Science" Udsm na alikuwa amebakiza sura moja tu umauti ulimpomfika.

10. Mh. SOKOINE "Aliota" kifo chake:

Mh. SOKOINE alihudhuria kikao cha bunge jijini Idodomia mwezi April 1984. Hata hivyo, matendo ya Mh. SOKOINE kabla ya kifo chake yanaashiria huenda alihisi maisha yake duniani yalikuwa yakifikia tamati.

Jumatatu ya tarehe 9 April 1984, Mh. SOKOINE alikwenda kusali kanisa la Mtakatifu PAUL, Idodomia. Usiku wa Jumanne, tarehe 10 April 1984, Mh. SOKIONE aliandaa karamu ya chakula cha jioni kwa Mawaziri na Wakuu wa Mikoa ambapo alionekana kuongea na kila Waziri na kila Mkuu wa Mkoa. Jumatano, tarehe 11 April 1984, aliandaa chakula cha jioni "The Last Supper" kwa Wabunge wote wa mkoani kwake Arusha ambapo aliwasihi wafanye jitihada kuwaondoa wananchi wao kwenye lindi kubwa la ufukara.

11. Mh. SOKOINE Atema Cheche na Kuliaga Bunge:

Mh. SOKOINE, siku ya Jumatano ya tarehe 11 April 1984, akilivunja Bunge, alitiririka:

"Ndugu Spika, ningependa kumalizia kwa kukubaliana na wabunge wote waliosema na ambao hawakusema lakini wana mawazo haya kwamba jambo hili la kutumia fedha bila idhini ya bunge lazima tutafute kila njia ya kulikomesha..... Mungu akipenda tutakutana tena kwenye kikao kijacho cha  bunge. Mimi nasafiri kwa njia ya barabara ili nijionee hali ya mazao ya wakulima...".

12. Mh. SOKOINE Apata Ajali, Afariki:

Mapema Alhamis, tarehe 12 April 1984, Mh.  SOKOINE aliondoka na msafara wake Idodomia akiwa ndani ya Mercedes Benz ambapo msafara huo uliongozwa na gari la polisi. Magari yote yaliyokuwa yakikutana na msafara huo yalikuwa yakipaki pembeni kuupisha.

Baada ya msafara huo kufika eneo la Dakawa, ghafla kilisikika kishindo kikubwa. Gari la Mh. SOKOINE liligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Landcruiser lililokuwa likiendeshwa na DUMISAN DUBE (23), mpigania uhuru wa chama cha ANC aliyekuwa akiishi Mazimbo, Morogoro. DUBE, licha ya kusimamishwa na polisi, hakusimama kwavile alikuwa kwenye mwendo wa kasi. DUBE, katika Landcruiser hiyo, alikuwa na abiria wawili, Bw. BOYCE MOYE na PERCY GEORGE.

Mh. SOKOINE, ambaye alikuwa amekaa kiti cha nyuma huku hajafunga mkanda, alirushwa na kugonga kioo cha mbele ambapo aliumia sana kifuani na shingoni na kufariki kabla ya kufikishwa hospitali ya serikali mkoani Morogoro ambako madaktari walithibitisha kifo chake.Bw. YUSTO CHUMA, aliyekuwa bodigadi wake aliyekuwa amekaa kiti cha mbele kushoto, aliumizwa vibaya na Bw. ALLY ABDALLAH,ambaye alikuwa ndiye dreva wake, alivunjika mguu.

13. Rais NYERERE Alitangazia Taifa Kifo cha SOKOINE:

Alasiri ya siku hiyo ya alhamis, Radio Tanzania, ikiwa inaendelea na vipindi vyake, ghafla vikasitishwa na wimbo wa Taifa ukapigwa.

Rais NYERERE, baada tu ya wimbo wa Taifa, kwa uchungu mkubwa lakini kwa ujasiri wa hali ya juu, akalitangazia Taifa msiba huo wa kihistoria nchini kama ifuatavyo:

"Ndugu wananchi, leo hii, ndugu yetu, kijana wetu, EDWARD MORINGE SOKOINE, Waziri Mkuu wa Tanzania, alipokuwa akirudi Dar Es Salaam toka Dodoma, gari lake lilipata ajali na amefariki dunia. Ndugu Watanzania, naomba muamini EDWARD amefariki kwa ajali na si kitu kingine".

Mara tu baada ya tangazo hilo, vilio na simanzi vilivyotamalaki nchi nzima "havikuwa vya nchi hii". Aidha, watanzania waliokuwa nje ya nchi nao walibubujikwa na machozi kwa kuondokewa na kipenzi chao. Watanzania kila mahali walikuwa wenye simanzi kubwa. Watu walionekana "dhahir shahir" wamevurugwa!

Kikao cha UWT kilichokuwa kikifanyika Ofisi ya CCM Lumumba kilisambaratika ghafla bila kuahirishwa mara tu Mwenyekiti wake, mama SOPHIA KAWAWA, alipowatangazia wajumbe habari hizo zilizoleta jakamoyo na jitimai kubwa!.

Serikali ikatangaza wiki 2 za maombolezo huku bendera ya Taifa ikipeperushwa nusu mlingoti nchi nzima.

14. Rais NYERERE Aangua Kilio Baada ya Kuuona Mwili wa SOKOINE:

Mwili wa SOKOINE uliwasili Ikulu kutoka Morogoro saa 11 jioni ukiwa umefunikwa bendera ya Taifa. Rais NYERERE, akiongozana na mama MARIA, alijongea kwenye mwili huo na akafunua bendera ya Taifa. Mwalimu akaweka mikono yake miwili kwenye paji la uso wa SOKOINE na yeye na mama MARIA, aliyekuwa na kitambaa cheupe, wakalia kwa uchungu sana hadi kuondolewa na walinzi wao. Kwa wengi, ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Mwalimu akilia hadharani. Kwa hakika, ilikuwa ni siku ya uchungu mkubwa kwa taifa letu kwa jinsi kifo kilivyotokea na hasa kwavile SOKOINE alikuwa akipigiwa chapuo na wengi kuja kuwa Rais wa Tanzania baada ya Mwalimu.

15. JOSEPH NYERERE Azua Kimuhemuhe na Taharuki Ikulu:

JOSEPH NYERERE, mdogo wa Mwalimu, ambaye alijulikana kwa ufyatu wake na kutomun'gunya maneno, ghafla bin vuu, aliingia eneo ulipowekwa mwili huo na kuonekana amefura hasira huku akilia kwa sauti ma kwa uchungu. Ghafla akatamka:
"Mwalimu, huna ulinzi. Waziri Mkuu anakufa barabarani?" . Walinzi wa Ikulu, si tu walimtoa "mkuku" bali pia walihakikisha ameondolewa eneo la Ikulu haraka.!

Mwili wa SOKOINE ukapelekwa hospitali ya Muhimbili kwaajili ya kuhifadhiwa.

16. Jeneza la SOKOINE Latengenezwa Fastafasta Usiku wa Manani:

Shuguli ya kutengeneza jeneza hilo alipewa Bw. GEORGE CHRISTOS (86). Huyu alizaliwa na baba Mgiriki na mama Msukuma aliyeitwa MARIA, aliyekuwa mmoja wa mabinti wa Chifu KIDAHA. Bw. CHRISTOS alikuwa ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu Tanzania.

Saa 12 jioni siku hiyo, yeye na mkewe, Bi. ELIZABETH WALKER, walitinga Muhimbili ili kuangalia mwili na kuchukua vipimo.

Wakati huo, bohari zote mikoani ilikuwa ni lazma ziwe na majeneza 5 ili ikitokea msiba wa kiongozi kusiwe na tatizo.

SOKOINE alikuwa mtu wa miraba minne "aliyekwenda hewani" hivyo majeneza yote kwenye bohari zote hayakumfaa.

Bw. CHRISTOS, mkewe na Bw. PAUL MKANGA, aliyekuwa Katibu Mkuu Ujenzi, baada ya kupata vipimo, walienda kwenye kiwanda cha HEM SINGH-Chang'ombe ambako walimkuta mwenyewe akiwa katika harakati za kufunga. Kazi ya kulitengeneza jeneza ikaanza mara moja na kumalizika usiku wa manani. Kisha, Bi. WALKER akalipamba jeneza hilo na likapelekwa Muhimbili.

17. SOKOINE Aagwa na Wakazi wa Dsm:

Ijumaa, tarehe 13 April 1984, wakazi wa jiji la Dsm na mikoa ya jirani walifurika kuuaga mwili wa SOKOINE. Kwa hakika, umati huo ulikuwa haujawahi kutokea nchini na rekodi hiyo ilikuja kuvunjwa na msiba wa Baba wa Taifa, Octoba 1999.

18. Daladala Zote Zawapeleka Watu Bure "Airport"

Jumamosi ya tarehe 14 April 1984, mwili wa SOKOINE ulipelekwa "airport" kwaajili ya kusafirishwa kuelekea Arusha. Daladala zote jijini ziliacha "kula vichwa" na badala yake zikawasafirisha wananchi bure kwenda "airport" kama mchango wao kwa kipenzi chao. Ikumbukwe kuwa mwaka 1983, baada ya kuona UDA "inambwelambwela", Mh. SOKOINE ndipo alipoanzisha utaratibu wa "DALADALA", jina lililotokana na neno "Dollar" ambapo "Exchange rate" wakati huo ilikuwa shilingi Tano ambayo ndiyo ilikuwa nauli ya Daladala.

19. SOKOINE Azikwa kwa Heshma Zote:

Kaburi la aina yake la marehemu SOKOINE lilijengwa kwa ustadi mkubwa na Jenerali JOHN BUTLER WARDEN "Black Mamba", Mtanzania Chotara, akisaidiwa na askari wa TPDF.

Kutokana na ubunifu huo wa aina yake, Jenerali WARDEN akapewa heshima ya kujenga kaburi la aliyekuwa Rais wa Msumbiji, SAMORA MOSES MACHEL, ambaye alifariki baada ya ndege yake aina ya Tupulov Tu 134, kuanguka tarehe 19 Octoba 1986.

Mazishi ya SOKOINE yalipewa  heshima zote za kitaifa na yalihudhuriwa na maelfu ya wananchi wakiongozwa na Baba wa Taifa na viongozi toka nje ya nchi.

Miongoni mwa waliohudhuria toka nje ni Mh. OLIVER TAMBO, aliyekuwa Rais wa ANC na Mh. ALFRED NZO aliyekuwa Katibu Mkuu wa ANC ambao walieleza kusikitishwa kwao na ajali hiyo iliyosababishwa na raia mwenzao wa Afrika Kusini.

20. SOKOINE Aacha Wake 2 na  Watoto 11:

SOKOINE alikuwa na wake wawili ambao ni mama NAPONO SOKOINE na mama NAKITETO SOKOINE na watoto 11 wakiwemo Mh. Balozi JOSEPH na Mh. Mbunge NAMELOK.

21. DUMISAN DUBE  Afikishwa kwa Pilato, "Apigwa Mvua 3"

Tarehe 17 Mei 1984, DUMISAN DUBE, aliyesababisha kifo cha SOKOINE, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro kwa mara ya kwanza. Kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe 29 Mei 1984.

ANC Tawi la Mazimbo lilimchukua wakili nguli, MOHAMED ISMAIL, kumtetea DUBE. Hata hivyo, ANC HQ Lusaka ilipanga kumtafuta wakili mwingine guru ili kumtetea mpigania uhuru huyo.

Tarehe 12 Juni 1984, upande wa Mashtaka ukiwa "Kamili-Gado" ukiongozwa na  JOHNSON MWANYIKA (SSA) aliyekuwa na mashahidi 21 akiwemo mkulima aliyeshuhudia ajali hiyo,  DUBE aliposomewa tu mashtaka 7 akakiri na Pilato wa wakati huo, Mh. SIMON KAJI (PRM) "akamtwanga mvua 3".

22. SOKOINE Alikuwa Kipenzi Kikubwa cha NYERERE:

Baba wa Taifa alimpenda sana SOKOINE kutokana na uadilifu wake, uchapakazi wake usio wa kawaida, uchamungu wake na ubunifu wake kuntu.

23. Mambo Yaliyofanya SOKOINE Kuwa Kiongozi wa Kipekee na Kupendwa Sana na Watanzania:

23.1 SOKOINE alichukia sana wazembe. "Ole wake Kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta. Viongozi wazembe na wabadhilifu wahesabu siku zao". 26 Machi 1983.

23.2 SOKOINE alitaka wazazi wawajibike kwa watoto  wao- "Vijana wengi leo wana mali kuliko wazee wao waliofanyakazi kwa miaka 40 lakini wazee hao wanataka serikali ndio iwaulize vijana mali wameipata wapi! Hivi kwanini mzazi usimuulize mwanao -"Hii mali umepata wapi"?.

23.3 SOKOINE alihimiza majeshi yawe kwa faida ya wote -  "Katika nchi inayojali haki na usawa, Majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya wengi. Kamwe hayaruhusiwi kuwa chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao"
1 Februari 1977.

23. 4 SOKOINE alipenda Uzalendo na alikuwa Mzalendo wa kweli kwa nchi yake. "Viongozi wanaoteuliwa lazma wawe Wazalendo. Naskia huko mikoani baadhi ya viongozi wanagombania magari na nyumba. Mambo hayo si muhimu. Viongozi wanatakiwa kugombania juu ya maendeleo ya wanavijiji. Huu ni ugomvi mtakatifu."
11 Desemba 1982.

23.5 SOKOINE alichukia upuuzi. Mwezi Machi 1983, SOKOINE alifanya ziara Singida. Mmoja wa viongozi mkoani humo akamfuata Bw. ACCADOGA CHILEDI aliyekuwa "Press Secretary" wa SOKOINE na kumwambia - "Mzee tumeishamtayarishia Blanketi Chapa ya Binadamu"(akimaanisha Kimada). Bw. CHILEDI akamuuliza Kiongozi huyo- "SOKOINE unamjua au unamsikia? Hilo Blanketi ondoka nalo na toweka hapa haraka, nikimwambia ujue unapoteza kazi yako sasa hivi".

23.6 SOKOINE alikuwa mchapakazi hodari. Daima alifanya kazi hadi usiku na mara nyingine hadi usiku wa manani. Aliwachagua vijana 2 hodari; PHILEMON LUHANJO na MARTENS LUMBANGA waliokuwa chini ya Katibu Mkuu, HORACE KOLIMBA. Hawa watatu walibatizwa jina la "WAFUASI WA SOKOINE" kwani walizunguka nae kote alikoenda na kufuatilia maagizo yote "Bampa tu Bampa".

23. 7 SOKOINE hakupenda utajiri. Maisha yake yalielezewa kwa ufasaha na Mwalimu msibani : "EDWARD hakuwa na mali yoyote ukiachilia mbali ng'ombe wake wa urithi. Alikuwa na suti tatu na viatu pea mbili".

23.8 SOKOINE alikuwa ni mbunifu sana. Alianzisha "PRESIDENTIAL TRUST FUND" Ikulu ambapo alikuwa akiweka sehemu ya mshahara wake ili kuwasaidia akina mama kuweza kukopa!.

23. 9 SOKOINE alikuwa Mchamungu sana. Alikuwa Mkristu mkatoliki na mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisca.

24. NUKUU MUJARAB ZA MH. JPM NA PM KUHUSU SOKOINE:

24.1 "Tarehe 12 April 1984, aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. SOKOINE alipofariki ilikuwa siku ya huzuni kubwa. Mimi nilikuwa JKT Mpwapwa "Operesheni ya Nguvukazi". SOKOINE hatasahaulika Tanzania kwani alipiga vita rushwa, wizi na unyonyaji. Alikuwa Mzakendo wa kweli. Ni wito wangu Watanzania tumuige na tumuishi.."
Mh. JPM, 12 April 2018.

24. 2 "SOKOINE alikuwa Kiongozi bora aliyechukia rushwa na ulanguzi. Hakuwa na ubinafsi, kinyongo wala tamaa ya mali. Namuomba Mungu niwe kama SOKOINE"
Mh. K.MAJALIWA, 12 April 2018.

25. Tafakuri Jadidi:

Je, wewe kama Kiongozi (wa ngazi yoyote ile iwe Kata, darasani au serikalini) unamuenzi na kumuishi marehemu SOKOINE kama alivyotuasa Mh. Rais MAGUFULI?
Jitafakari.

NB: NYIE WOTE MNAOFOWADI ATIKALI ZANGU BAADA YA KUONDOA CHATA LA "ALLEZ LIVERPOOL FC👇 DAWA YENU IPO JIKONI!!.

ALLEZ ALLEZ ALLEZ LIVERPOOL FC!!!🔥🔥🔥KUMBUKIZI YA 35 YA KIFO CHA EDWARD MORINGE SOKOINE

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MAFINGA AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI IRINGA

0
0
 1

2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mafinga mara baada ya kuwasili wakati akitokea Makambako mkoani Njombe. 
4
6
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kijana Baraka Mwakipesile (Anko Magu) wa Mafinga ambaye anaigiza sauti ya Rais Dkt. Magufuli mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza.
3
7
8
9
 Umati wa Wananchi wa Mafinga  wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza nao.
11
Baraka Mwakipesile (Anko Magu) Kijana anayeigiza sauti ya Rais Dkt. Magufuli akipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia. Picha na IKULU

TIMU YA WANASHERIA YATEMBELEA MAGEREZA YA MTWARA, NEWALA NA MASASI KUTATUA KERO ZA KISHERIA ZINAZOWAKABILI WAFUNGWA NA MAHABUSU

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akiwa na Mkurugenz wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo mganga na wanasheria wengine nje ya Gereza Kuu Lilungu la Mtwara baada ya kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo mjini Mtwara. 

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Ngwembe akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju (mwenye miwani), Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Bw. Biswalo Mganga (wa kwanza kushoto), Naibu DPP Dkt. Edson Makallo (wa kwanza kulia) walipomtembelea Ofisini kwake mjini Mtwara wakati timu ya wanasheria wakiongozwa na Bw. Mpanju walipokuwa mjini Mtwara kutembelea gereza kuu la Lilungu.

Naibu DPP Dkt. Edson Makallo (wa kwanza kushoto) akizungumza kitu na Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Newala wakati timu ya wanasheria ilipokuwa wilayani humo kutembelea gereza la wilaya hiyo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu na kutatua kero za kisheria wanazokabiliana nazo.
Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Newala (katikati) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju (kushoto) na Naibu DPP Dkt. Edson Makallo (kulia) walipomtembelea Ofisini kwake mjini Newala wakati timu ya wanasheria wakiongozwa na Bw. Mpanju walipotembelea gereza la wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju na timu ya wanasheria wakiwa nje ya Gereza la Wilaya ya Newala baada ya kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo mjini Newala.
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Newala Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Juma Mgunda aliyeshika karatasi akijiandaa kusoma taarifa ya gereza kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju wa kwanza kulia alipofika katika gereza la Wilaya ya Masasi kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na Mahabusu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju na timu ya wanasheria wakiwa nje ya Gereza la Wilaya ya Masasi baada ya kulitembelea na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo mjini Masasi.

………………..

Timu ya Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Mahakama, Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza mkoa wa Mtwara wamefanya ukaguzi katika Magereza mkoani Mtwara kusikiliza na kujionea changamoto za kisheria zinazowakabili wafungwa na mahabusu walioko ndani ya magereza mkoani humo.

Timu hiyo inayoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Amon Mpanju na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Edson Makallo imetembelea gereza Kuu la Lilungu lililoko Mtwara mjini, gereza la wilaya ya Newala na gereza la wilaya ya Masasi.

Timu hiyo imefanya ukaguzi wa maeneo yanayotumiwa na wafungwa na mahabusu ndani ya magereza hayo na kuzungumza nao ili kujua changamoto za kisheria na kijamii zinazowakabili na kuchukua hatua stahiki.

Katika ziara hiyo Timu ya wataalamu hao imechukua majina ya mahabusu ambao kesi zao ni ndogo ndogo na waliokiri kufanya makosa husika na kujutia, wenye watu wa kuwawekea dhamana, walio tayari kulipa fedha za vitu walivyoiba, au kurudisha vitu walivyoiba, kupigana, kutukanana na wako tauari kuombana msamaha, kujeruhiana na walioafikiana kumaliza kesi zao nje ya mahakama ili ziweze kufutwa na hivyo kuachiwa huru baada ya DPP kujiridhisha nayo.

Timu pia kwa kushirikiana na Mahakimu wa Mkoa na Wilaya husika wamekubaliana kufanya mapitio ya adhabu za wafungwa wa chini ya miaka mitatu ili wabadilishiwe adhabu kwa kufanya kazi za jamii au vifungo vya nje ambapo wakimaliza watakuwa raia huru.

Akizungumza ndani ya magereza hayo Naibu Katibu Mkuu Bw. Mpanju amesema ukaguzi huo ndani ya magereza hayo ni jukumu la kisheria la Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zinazohusika na utoaji haki nchini.

“Sisi kama Wizara na taasisi zote zilizo katika mfumo wa utoaji haki nchini ni jukumu letu kisheria kuangalia jinsi mambo yanavyoendeshwa humu ndani na wadau wetu, kutembelea huku kunatuwezesha kuona kama mwanachi anapata haki yake kwa mujibu wa Sheria, na ikiwa kuna tatizo ni wajibu wetu kumuondolea kero za kisheria akiwa humu ndani,ndio maana tunafanya ukaguzi huu na kuzungumza nanyi ili tuwasikie na kuondoa kero au malalamiko mtakayotuambia,” alisema Bw.Mpanju.

Akizungumza baada ya kubaini mahabusu na wafungwa watakaonufaika na ziara ya wataalamu hao Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Dkt.Edson Makallo amewataka wananchi hao ambao watafutiwa Mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili na wafungwa watakaopata adhabu mbadala kuwa raia wema na kubadili mienendo yao ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa Taifa.

MMILIKI SHULE YA SCHOLASTICA AGUSWA KATIKA MAELEZO YA UNGAMO ,NI KATIKA KESI YA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCHOLASTICA.

0
0
Washtakiwa wa Mauaji ya kukusudia , Mlinzi wa shule ya sekondari ya Scholasica ,Hamis Chacha (aliyebeba maji) , Mwalimu wa Nidhmu katika shule ya Scholastica,Laban Nabiswa (mwenye shati nyeupe) na nyuma yao ni Mmiliki wa shule ya sekondari ya Scholastica ,Edward Shayo ,mshtakiwa wa pili katika shauri hilo 
Mshitakiwa wa Pili katika shauri la Mauji ya kukusudia ,Edward Shayo anayetajwa kama mmiliki wa shule ya sekndari ya Scholastica aliyokuwa akisoma Marehemu Humphrey Shayo akiingia katika chumba cha Mahakama. 
 Baadhi ya wafuatiliaji wa shauri hilo wakiwa ndani ya Chumba cha Mahakama. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

SHAHIDI Irene Mushi (35) ambaye ni wa kwanza kwenye kesi ndani ya kesi ya Msingi ya Mauaji ya kukusudia namba CC 48/2018 ya Mwanafunzi Humphrey Makundi amewasilisha Nyaraka ya Maelezo ya Ungamo ya Mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo ,Hamis Chacha alivyo tekeleza agizo la Mshtakiwa wa pili ,Edward Shayo la kwenda kutupa Mtoni mwili wa mtu aliyeuawa .

Hatua ya Mahakama kujielekeza katika usikilizwaji wa kesi ndani ya kesi unatokana na mabishano ya kisheria baina ya upande wa utetezi dhidi ya upande wa Jamhuri baada ya Upande wa utetezi kuwasilisha hoja ya kupinga kupokelewa kwa maelezo ya Ungamo katika kesi ya Msingi.

Maelezo ya Ungamo ya Mshtakiwa wa kwanza katika shauri hilo Hamis Chacha Wisare yalitolewa mbele ya Shahidi wa 14 katika kesi ya Mauaji ya kukusudia , Irene Mushi ,Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ,Moshi mjini ambaye pia ni mlinzi wa Amani .

Shauri hili linaloendelea Mahakama Kuu Kanda ya Moshi ,mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ,Divisheni ya Rushwa na uhujumu Uchumi,Dar es Salaam ,Firmin Maatogoro linawakabili washtakiwa watatu ambao ni Hamisi Chacha ,mlinzi wa shule ya Sekondari ya Scholastica,Edward Shayo,mmiliki wa shule na Laban Nabiswa ,Mwalimu wa nidhamu shule ya sekondari ya Schoalastica.

Akiwasilisha kusudio la upande wa utetezi ,Wakili wa kujitegemea ,Gwakisa Sambo aliieleza mahakama kuwa upande wa utetezi unapinga maelezo ya mtuhumiwa na kwamba yalichukuliwa bila ridhaa yake ndipo Mahakama ikajielekeza katika usikilizwaji wa kesi ndani ya kesi.

Akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali,Joseph Pande,shahidi Irene Mushi aliieleza Mahakama akiwa na Jukumu la Mlinzi wa Amani alipokea taarifa kutoka kwa Mfawidhi, akimueleza kwamba kuna mshtakiwa anapelekwa mbele yake kwa ajili ya kuandika maelezo ya Ungamo.

Alieleza kuwa alifuata taratubu zote na uchukuaji maelezo ya Mtuhumiwa ikiwa ni pamoja kujibu maswali tofauti ikiwemo kwa nini yupo mbele ya mlinzi wa amani na endapo maelezo atakayotoa yataenda kutumika kama sehemu ya ushahidi endapo atafikishwa Mahakamani huku majibu yake yakiwa anafahamu.

Alieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa katika Afya nzuri na kwamba aliimuliza endapo kama alipigwa ama kutishiwa alimjibu alipigwa tarehe 17/11/2017 na askari Polisi baada ya maelezo yake kutofautiana na y a mlinzi mwenzake.

Baada ya maelezo hayo Wakili Mkuu wa Seriali ,Joseph Pande alimuonesha karatasi ya maelezo ya mshtakiwa na kuuliza kama anaitambua alijibu ndio na kuiomba mahakama kuitumia kama kielelezo katika ushahidi wake na kupokelewa baada ya kuridhiwa na pande zote mbili.

Baada ya kielelezo hicho kupokelewa Shahidi Irene akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali anaye wakilisha upande wa Jamhuri katika Shauri hilo alielekezwa kusoma maelezo yaliyoandikwa katika nyaraka ya maelezo ya ungamo katika mahakama ya mwanzo Moshi mjini.

Katika sehemu ya maelezo ya Shahidi huyo wakati akisoma maelezo ya Ungamo ya Mshtakiwa Hamisi Chacha ,Shahidi huyo alieleza kwamba Chacha akiwa eneo lake la kazi alisikia kishindo cha mtu ndipo alipoamua kupiga tochi na kufuatilia baada ya kubaini kuwa kuna mtu .

Ameileza mahaka kuwa Mtuhumiwa alimueleza kuwa alimpiga mtu huyo na bapa la Panga na akaumia kenye paji la uso na baadae akampiga bapa la pili na mtu alifariki pale pale ndipo alipompigia simu Mwalimu Laban aliyefika eneo hilo na kusema huenda mtu huyo amezirai.

Alieleza Labani aliiuliza kama ameshafanya mawasiliano na Mzee Shayo na baadae alipigiwa Shayo ambaye anatajwa kama mmiliki wa shule hiyo aliyefika eneo la tukio na kutoa maelekezo ya mtu huyo kwenda kutupwa mtoni kama hafahamiki na kwamba huenda ni Kibaka.

Irene ameeleza baada ya hapo yeye Chacha na Mwalimu Labani wakauchukua ule mwili wa marehemu wakaenda kuutupa mtoni na kurudi shuleni na kuitisha Row call kwa ajili ya kujua endapo kama ni mwanafunzi hayupo shuleni .

Shahidi alieleza Mlinzi Chacha alielekea kwenye Mabweni na kukuta kitanda kimoja hakina mwanafunzi na Mwalimu Laban aliuliza ni mwanafunzi gani hayupo ,baade ilibainika kuwa mwanafunzi Humphrey Makundi wa kidato cha pili ndio hayupo.

Upande wa Jamhuri unaaongozwa na Wakili Mkuu w Serikali ,Joseph Pande ,Wakili wa serikali Mwandamizi,Abdalah Chavula,Wakili wa Serikali ,Omari Kibwana na Wakili wa serikali ,Lucy Kiusa waliieleza mahakama kuwasilisha mashahidi wa nne.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wa kujitegemea ,Elikunda Kipoko anaye mtetea Mshtakiwa wa pili ,Edward Shayo akisaidiana na Wakili wa kujitegemea Gwakisa Sambo, Wakili wa kujitegemea David Shilatu anaye mtetea Mshitakiwa wa kwanza ,Hamis Chacha na Wakili wa kujitegemea Patrick Paul walieleza mahakama watawaasilisha shahidi mmoja ambaye ni Hamisi Chacha.

INTRODUCING: Jaco Geezy ft P the Mc MINYAMA Official video

MWAKILISHI WA BAROZI WA CHINA AKABIDHI MAJENGO SABA KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI MOSHI

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akisalimiana na mwakilishi wa Barozi wa China hapa nchini Mr Xu Chen baada ya kuwasili katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi katika hafla fupi ya kupokea majengo saba yaliojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya China.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Jenerali Jacob G. Kingu akipokea mfano wa funguo kutoka kwa mwakilishi wa Barozi wa China  Mr Xu Chen baada ya kumaliza kukabidhiwa majengo saba yatakayo tumika kwa ajili ya  ukufunzi wa Maafisa na Askari katika chuo cha Polisi Moshi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Jenerali Jacob G. Kingu baada kupokea majengo saba yaliojengwa kwa ufadhili wa serikali ya China. (Picha na Jeshi la Polisi)

DAWASA YAANZA KUPELEKA MABOMBA YA MAJI MKURANGA,WANANCHI WAHIDIWA KUPATA MAJI DESEMBA MWAKA HUU

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KATIKA kuhakikisha wananchi wa pembezoni mwa mji wanapata maji safi na salama, Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imedhamiria kuwapelekea maji wananchi wa Mkuranga ifikapo Desemba mwaka huu.

DAWASA kwa kutumia fedha za ndani takribani bilion 5.6 wameanza mchakato wa kupeleka mabomba na kuyalaza kwa urefu wa Km 15 kuanzia kwenye mradi huo na kuepelekwa maeneo ya karibu ya Mkuranga..

Akielezea mikakati hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa mkandarasi ataingia kazini mwezi Mei mwaka huu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundo mbinu itakayowezesha kusambaza maji kwa wananchi wa Mkuranga na maeneo ya karibu.

"Mkandarasi ataingia kazini Mwezi Mei mwaka huu, na kuanzia kesho April 12 tutaanza kazi ya ulazaji wa mabomba  yatakayokuwa na urefu kwa Km 15,"amesema Luhemeja.

Luhemeja amesema, mpaka sasa wananchi 2500 ndio wanaopata maji kati ya wananchi 25,500 na wamechimba kisima chenye urefu wa Mita 600 na kutajengwa tenki litakalokuwa na uwezo wa lkuhifadhi maji Lita Milion 1.5 kwa siku.

Amesema, hii ni mikakati ya kufungua maeneo ya pembezoni na mradi huu ukikamilika wananchi wa Mkuranga, Vikindu hadi Mbagala watanufaika kwa kupata maji safi na salama.

Mhandisi Luhemeja amewaomba wananchi kuvumilia mpaka Disemba wataanza kupata maji safi na salama ambapo yataondoa kero ya miaka mingi ya kutokuwa na huduma hiyo.

Balozi Seif akutana na Profesa Kabudi Zanzibar

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alisema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwa na Taifa linaloendelea kudumu muda wote kutokana na misingi imara iliyowekwa na Waasisi wa Taifa hilo.

Alisema yapo Makabila mengi katika Mikoa na Wilaya mbali mbali Nchini Tanzania lakini muungano wa sauti moja inayozungumnzwa na Wananchi wake Bara na Zanzibar imekuwa mfano kwa Mataifa mengine Duniani.

Profesa Palamagamba Kabudi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar alipofika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.

Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yaliyowahi kuunganisha Nchi zao akaitolea Mfano iliyokuwa Yugoslavia na sasa imesambaratika Senegal na Gambia kwa Afrika lakini zimeshindwa kuendeleza Miungano hiyo.

Waziri Palamagamba alisema wakati Serikali zote mbili Nchini Tanzania zinaendelea kuheshimu kwa kuweka Kumbukumbu za Waasisi hao Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Vizazi vya sasa vinapaswa kujifunza tabia ya Viongozi hao walioacha msingi imara wa Umoja ndani ya Ardhi ya Tanzania.

Akigusia suala la Diploma ya Uchumi ambayo kwa sasa Tanzania imeelezekeza nguvu zake kupitia Balozi zake zilizoko nje ya mipaka ya Nchi Profesa Palamagamba alisema Serikali inaendeleza mfumo wa kushawishi Wawekezaji ili kuunga mkono jitihada za Taifa za kuwa na Tanzania ya Viwanda ifikapo Mwaka 2025.

Alieleza kwamba jitihada zinafanywa za kutangaza uimarishaji wa fursa za Kiuchumi zinazopatikana kutokana na rasilami nyingi zilizopo Nchini ambazo uwekezaji wake unaweza kusaidia soko la ajira na mapato ya Taifa.

Alielezea umuhimu wa mkakati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Kuimarisha Uchumi wake unaopaswa kuendelea kuungwa mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika muelekeo wa kuelekea kwenye Maendeleo ya haraka.

Akigusia Sekta ya Utalii inyoonekana Zanzibar kufanya vyema, Waziri Palamagamba alisema Sekta hii muhimu hivi sasa kwa mapato ya Taifa lazima iwekewe utaratibu wa pamoja utakaosaidia kuuza haiba ya pande zote mbili za Muungano.

Alisema vipo vivitio vinavyopaswa kutangazwa kwa pamoja Bara na Zanzibar ambavyo vinaweza kutoa nguvu ya ushawishi wa Watalii kufanya ziara ya makusudi ya kutembelea sehemu zote mbili kwa wakati mmoja.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielezea faraja yake kutokana na Zanzibar kupiga hata kubwa katika kuimarisha Sekta ya Utalii inayoonekana kutoa ajhira kubwa hasa kwa kundi kubwa la Vijana.

Alifahamisha kwamba ongezeko kubwa la idadi ya Watalii wanaotembelea Zanzibar inayopanda kila kukicha imethibitisha uwepo wa mafanikio katika kuendeleza Sekta hiyo muhimu.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ushawishi wa Uwekezaji ndani ya Visiwa vya Zanzibar unapaswa kuungwa mkono na Ofisi zote za Kibalozi za Tanzania zilizopo Mataifa mbali mbali Duniani.

Alisema Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ushawishi wake kwa Wawekezaji na Mataifa ya kigeni unawajibika kusimamiwa na Mabalozi wa Tanzania kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi Seif alimueleza Profesa Palamagamba kwamba Zanzibar kupitia Viongozi wake wote waliopita na waliopo hivi sasa bado wanaendeleza sera na Mikakati iliyoacha na Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Alisema uimarishaji wa Miundombinu ya Mawasiliano, Ujenzi wa Nyumba za Kisasa za Maendeleo, Afya, Elimu pamoja na huduma za Maji safi na salama ni miongoni mwa Sekta zinazoendelea kuimarishwa na Viongozi wote.

Balozi Seif Miradi iliyobuniwa na Serikali ya Mapinduzi ya ujenzi wa Miji Mipya kama ule wa Ng’ambo tuitakayo katika eneo la Kwahani na Mtaa wa Chumbuni imelenga kustawisha maisha ya Wananchi wake ili kuachana na matumizi mabaya ya Ardhi ndogo iliyopo.
 Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipofika kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
 Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wa Pili kutoka Kushoto akielezea msimamo wa Wizara yake katika kuzitangaza fursa za Uwekezaji zilizopo Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Muombwa.
 Profesa Palamagamba Kabudi(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kwanza kulia akimpongeza Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Balozi Seif kulia na Profesa Palamagamba Kabudi wakibadilishana mawazo mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Vuga Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

HAFLA YA KUWAAPISHA WAJUMBE WAPYA WA MABARAZA YA ARDHI YA WILAYA - KAGERA

0
0
Anaandika Abdullatif Yunus - Bukoba.

Mkuu Wa Mkoa Wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amewaapisha Wajumbe wapya wanne Wa Mabaraza ya Ardhi kutoka katika Wilaya za Ngara na Karagwe, katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi mdogo Wa Mikutano Ofisi za Mkuu wa Mkoa mapema Aprili 12, 2019.

Mh. Gaguti amewataka Wajumbe hao kwenda kusimamia Sheria katika misingi ya Haki, huku akisisitiza kuwa Asilimia kubwa ya Migogoro, kesi na kero nyingi ambazo zimemfikia ofisini kwake zinahusiana na masuala ya Ardhi. Hivyo kupitia uteuzi wao ni vyema kuzingatia Maadili ya kazi yao, na kujiepusha masuala yanayoweza kupindisha haki ikiwemo Rushwa.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Bukoba Lucia Kairo, amewataka wajumbe hao kuwa waaminifu, na kutumia weledi katika kazi zao za kuyasaidia mabaraza ya Ardhi.

Wajumbe hao wapya walioapishwa ni Ndg. Longino Frederick (Wilaya Karagwe), Lucletia Shubilo (Wilaya Karagwe), Christina Mugasha (Wilaya Ngara), na Charles Mbeikya (Wilaya Ngara).

Kupitia Hafla hiyo pia Mkuu wa Mkoa Mh. Gaguti amewatambulisha Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Kanda Bukoba, ambao wameongezwa katika mahakama hiyo.
Pichani ni Ndg. Longino Mbeikya Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya Karagwe akila kiapo Mbele ya Mkuu wa Mkoa Kagera Mh. Gaguti.
Pichani ni Bi. Christina Mugasha Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Ngara akila kiapo Mbele ya Mh. Gaguti, Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika hafla ya Kuwaapisha Wajumbe hao.
Pichani ni Ndg. Lucletia Shubilo Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Karagwe akila kiapo Mbele ya Mh. Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Pichani ni Ndg. Charles Mbeikya Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Ngara, Mara baada ya kula kiapo, akiwa amesimama Mbele ya Mh. Gaguti, Mkuu wa Mkoa Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Wajumbe wapya wa Mabaraza ya Wilaya (hawapo pichani) pamoja na wananchi Mara baada ya Kuwaapisha.
Sheikh wa Mkoa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta akitoa neno na Dua katika hafla ya Kuwaapisha Wajumbe wapya wa Mabaraza ya ardhi ya Wilaya
Mchungaji King James wa Hema la Ukombozi akitoa maombi yake katika hafla ya Kuwaapisha Wajumbe wa Mabaraza la Ardhi ya Wilaya za Karagwe na Ngara.
Sehemu ya Wajumbe na wageni waalikwa wa Hafla fupi ya Kuwaapisha Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya za Ngara na Karagwe katika ukumbi mdogo wa Mikutano Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera.
Picha ya Pamoja Mara baada ya hafla ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Mabaraza ya Ardhi ya Ngara na Karagwe.

JAJI KIONGOZI AHITIMISHA ZIARA YAKE MAHAKAMA-KANDA YA MBEYA: ASISITIZA UONDOSHAJI MASHAURI KWA WAKATI

0
0
Na Mary Gwera, Mahakama –Mbeya
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania,  Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amehitimisha ziara yake ya kikazi katika Mahakama Kanda ya Mbeya huku akitoa wito kwa Uongozi wa Kanda hiyo kutoruhusu mlundikano wa mashauri.
Akizungumza na Viongozi na baadhi ya Maafisa wa Mahakama katika kikao chake cha majumuisho ya ziara yake kilichofanyika Aprili 10, 2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Mahakama Kuu-Mbeya, Jaji Dkt. Feleshi aliwaelekeza Viongozi hao kuainisha mashauri yote yenye umri wa miaka mine (4) lengo likiwa ni kutoruhusu mashauri hayo kuvuka miaka mitano (5).
“Nimeridhika na suala la usikilizwaji na umalizwaji wa mashauri katika Kanda hii kupitia taarifa mbalimbali zilizotolewa, hivyo ni rai yangu kuwa mashauri yote yaliyo na umri kuanzia miaka mitatu na minne (4) yaainishwe na kufanyiwa kazi kabla hayajafikia umri wa miaka mitano (5) Mahakamani,” alieleza  Jaji Kiongozi.
Jaji Kiongozi alisema kuwa lengo la Mahakama ya Tanzania ni kutokuwa na mashauri yanayokaa kwa muda mrefu kuanzia miaka mitano (5) na kuendelea huku akisema kuwa nia iliyopo mashauri yasikae zaidi ya miaka miwili (2) Mahakamani kabla ya kumalizika.
Mbali na agizo hilo, Jaji Kiongozi aliwasisitiza Wahe. Majaji, Wasajili, pamoja na Mahakimu kuheshimu nyaraka mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wa Mhimili huo kwa ustawi bora wa uondoshwaji wa mashauri.
Aidha;  Jaji Kiongozi alionyesha kufurahishwa kwake na juhudi za Majaji na Mahakimu wanaochapa nakala zao za hukumu na kuwapatia Wadaawa kwa wakati.
“Katika Kanda hii nimefurahishwa na jitihada za baadhi ya Mahakimu wanaochapa nakala zao za hukumu, hivyo nitoe wito kwa Majaji na Mahakimu ambao hawajaanza kuiga mfano huu ili kutopelekea ucheleweshaji wa upatikanaji wa nakala za hukumu na mienendo ya mashauri,” alieleza Jaji Kiongozi.
Kwa upande mwingine, Jaji Dkt. Feleshi aliagiza Mahakama katika Kanda hiyo kuhamasisha wanafunzi katika shule za Sekondari kusoma masomo ya sheria ili kuwajengea upendo wa fani ya uanasheria/uhakimu. 
Kabla ya kuhitimisha rasmi ziara yake katika Kanda hiyo, Jaji Kiongozi alitembelea na kupata taarifa za utendaji za Mahakama ya Watoto, Mahakama ya Mwanzo Uyole, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya Mbeya ambapo sehemu zote Jaji Kiongozi alionyesha kuridhishwa na kasi ya uondoshaji wa mashauri na kusisitiza kuendelea na kasi hiyo.
Jaji Kiongozi amefanya ziara ya kikazi katika Mahakama Kanda ya Iringa na Mbeya lengo likiwa ni kujua  hali ya maendeleo ya utekelezaji wa maboresho ya huduma mbalimbali za  Mahakama na vilevile kuwakumbusha Watumishi wa Mhimili huu kuendelea kutekeleza jukumu la msingi la utoaji haki nchini kwa ubora wa hali ya juu kwa manufaa ya wananchi. 

 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania,  Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (aliyesimama) akizungumza na Wahe. Majaji wa Mahakama Kanda ya Mbeya (pichani) pamoja na baadhi ya Viongozi na Maafisa wa Kanda hiyo (hawapo pichani) alipokuwa katika kikao cha Majumuisho ya ziara yake katika Kanda hiyo. Wa tatu kushoto ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Jaji Robert Makaramba, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Jaji Dunstan Ndunguru na wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya,  Jaji Dkt. Lilian Mihayo Mongella.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Mwanzo Uyole, Zawald Nyekelela akimkabidhi Jaji Kiongozi taarifa ya hali ya Utendaji wa Mahakama hiyo pindi Jaji Dkt. Feleshi alipotembelea katika Mahakama hiyo.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
 Jaji Dkt. Feleshi (katikati) akizungumza na wateja wa Mahakama (hawapo pichani), kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Jaji Robert Makaramba na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete.
 Wateja waliofika kupata huduma ya Mahakama Kanda ya Mbeya wakimsikiliza Jaji Kiongozi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao, amewasihi wananchi kuendelea kuwa na imani na Mahakama kwani ipo kwa ajili ya kuhudumia wananchi.

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania,  Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji pamoja na Maafisa wa Mahakama Kanda ya Mbeya na baadhi ya Maafisa alioambatana nao katika ziara yake ya kikazi.
 Jaji Kiongozi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Watoto iliyopo mkoani Mbeya na Maafisa wengine wa Mahakama Makao Makuu na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, wa tatu kulia ni Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Zawadi Laiser.

Halmashauri zisizotoa 10% kwa Vikundi Kukiona

0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani S. Jafo(Mb) amewataka  Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Walemavu kutoka katika asilimia kumi ya mapato ya ndani kama ilivyoelekezwa kwenye Sheria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake asubuhi ya Leo Mhe. Jafo amesema Halmashauri zitakazoshindwa kutoa mikopo kwa vikundi hivyo watachukuliwa Hatua kali za kisheria kama ilivyoelekezwa katika Kanuni za utoaji wa mikopo ya vikundi.
Amesema kuwa licha ya uwepo wa Sheria  inayoelekeza suala zima la Utoaji wa mikopo kwa vikundi, utekelezaji wake  umekua wa kusuasua sana kwa baadhi ya Halmashauri na hadi kufikia Machi 2019 jumla ya fedha zilizotolewa kwa vikundi ni shilingi bilioni 20.7 ya shilingi bilioni 54.08 zinazopaswa kutolewa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 sawa na asilimia 38.27 ya Lengo.
“Hivi sasa hakuna kisingizio chochote katika utekelezaji wa sheria hii kwani Serikali imeshatoa Kanuni, zinazoongoza utoaji wa mikopo hiyo na Kanuni hizo zimetangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 141 la Tarehe 5 April, 2019 kwa GN. Na. 286 la mwaka 2019 kwa hiyo Mkurugenzi atakayeshindwa kutekeleza kwa ufanisi atachukuliwa hatua” alisema Mhe. Jafo.
Aliongeza kuwa katika kipindi hiki kuna Halmashauri 23 ambazo zimefanya vibaya zaidi kwa kutoa mikopo chini ya asimili 20 ya malengo.
Amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni Nsimbo, Nyasa, Busega, Kondoa Dc, Namtumbo, Kasulu Dc, Bariadi Dc, Msalala, Mbulu Tc pamoja na Njombe Dc.
Halmashauri zingine ni  Kongwa Dc, Musoma MC, Sumbawanga Dc, Kondoa Tc, Uvinza Dc, Ilala Mc, Lindi Dc, Mpwapwa Dc, Bahi Dc, Chamwino Dc, Momba Dc, Temeke Mc, Mbulu Dc na Lindi Mc.
Wakati huo huo Mhe. Jafo alitoa maelekezo kwa Halmashauri zote kuwa zinapaswa kutoa fedha kwa vikundi kwa mujibu wa Sheria na mpaka  ifikapo Juni 30,2019 Halmashari  ziwe zimetoa mikopo siyo chini ya asilimia 83 ya fedha zote za mikopo kutoka asilimia 10 ya fedha zote za mapato ya ndani.
Ameoongeza kuwa mpaka ifikapo Julai 20, 2019 Halmashauri zote ziwe zimetoa mikopo yote kwa asilimia 100 ya  fedha zote za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
“Mkurugenzi yeyote atakayeshidwa kutoa fedha kwa Vikundi kama ilivyoanishwa hapaswi kumlaumu mtu yeyote kwa sababu atachukuliwa hatua kama ilivyo elekezwa kwenye Kanuni za utoaji wa mikopo ya vikundi” amesema Mhe. Jafo.
Ikumbukwe kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya marekebisho katika Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura Na, 290 katika kifungu 37A ambacho kimeelekeza namna ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu kutoka katika asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Klabu 10 kuwania ubingwa wa taifa wa kuogelea kesho Jumamosi

0
0
Dar es Salaam. Jumla ya klabu 10 zimethibitisha kushindana katika mashindano ya klabu bingwa ya mchezo wa kuogelea yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Jumamosi.

Klabu ambazo zitashiriki katika mashindano hayo ni i Bluefins, Champion Rise, Mis Piranhas, klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC), FK Blue na Wahoo ya Zanzibar.

Nyingine kuwa ni ISM-Moshi, ISM-Arusha,FK Blue Marlins, Talis-IST na mabingwa watetezi, Dar es Salaam Swim Club (DSC).

Mashindano hayo ambayo yatamalizika kesho Jumapili, yamedhaminiwa na IST, Azam, Pepsi, Asas, Samsung, DTB Bank, Kaka’s, Food Lovers na Snow Cream.

Wadhamini wengine ni Kastipharn Ltd, Ruru Logistics, Knight Support, Oppotune Travel ltd, Pyramid Consumers, Print Galore, ITV Media, Clouds FM, Subway, NMB Bank and Umoja Grand Belt na Road Restaurant.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe alisema kuwa waogeleaji wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi wamewasili kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo.

Waogeleaji hao ni Sonia Tumiotto, Maia Tumiotto , Collins Saliboko, Dennis Mhini, Chichi Zengeni, Natalia Sanford, Smriti Gorkarn na Delvin Barick ambao wote wanasoma shule ya from St Felix , Uingereza.

Wengine ni Christian Shirima anayetokea nchi ya Ukraine, Isam Sepetu (Afrika Kusini), Hilal Hemed Hilal na Kangeta wanaotokea klabu ya Hamilton Aquatic ya Dubai.

Alisema kuwa mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi siku ya Jumamosi na waogeleaji watashindana katika staili tano ambazo ni Freestyle, Breaststroke, Butterfly, Backstroke na Individual Medley.

Kwa mujibu wa Hadija, waogeleaji hao pia watashindana katika relay katika mashindano ambayo yamepitishwa na Shirikisho la Mchezo wa kuogelea Duniani (Fina) kuwa ya kutafuta alama za kufuzu mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika nchini Korea mwezi Julai.

“Tunatarajia kuona ushindania mkali kwa waogeleaji wetu ili kutafuta nafasi ya kufuzu mashindano ya dunia. Waogeleaji wengi wapo katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo, bado tunahitaji wadhamini wa mashindano haya,” alisema Hadija.

Kwa mujibu wa Hadija, kutakuwa na jumla ya vipengele vya mashindano 108 na kila klabu imetakiwa kuwakilishwa na waogeleaji wawili katika kila kipengele cha mashindano ambavyo pia vimepangwa kutokana na umri.

ZOEZI LA UCHIMBAJI WA VISIMA WAANZA KATA YA NAMIUGO WILAYANI TUNDURU

0
0
 Wakazi wa Kijiji na Kata ya Namiungo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma hivi karibuni wakishughudia kuanza kwa zoezi la uchimbaji wa visima vya maji kijijini hapo kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la Safe Water for Life and Diginity (SWLD) kutoka nchini Marekani.
Zoezi la uchimbaji wa visima vya maji likiendelea katika Kijiji na Kata ya Namiungo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la Safe Water for Life and Diginity (SWLD) kutoka nchini Marekani wengine ni wakazi wa kijiji hicho hivi karibuni wakishuhudia zoezi hilo.

Mkazi wa Kijiji na Kata ya Namiungo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Rehema Mohamedi hivi karibuni akizungumzia changamoto ya maji inayowakabili wakazi hao baada ya waandishi wa habari kutembelea kijijii hapo hivi karibuni. (FATNA MWINYIMKUU)

Tigo yatoa zawadi za mamilioni kwa Mawakala wa Tigo Pesa

0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni mbili, Mshindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’, Said Khatibu kutoka Zanzibar, jijini Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni mbili, Mshindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’, Mojelwa Mlinga kutoka Dar es Salaam kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Tigo, jijini Dar es Salaam jana
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(katikati) akiwapongeza kwa kuwanyanua mikono juu washindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’. Kulia ni Mojelwa Mlinga kutoka Dar es Salaam na kushoto Said Khatibu kutoka Zanzibar

Washindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa ikijulikana kama ‘Cash In Promotion’.Said Khatibu (kushoto) kutoka Zanzibar na Mojelwa Mlinga kutoka Dar es Salaam na (kulia) wakifurahia mfano wa hundi walizabidhiwa baada ya kuibuka washindi katika promosheni hiyo. 

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari(katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kukabiudhi zawadi kwa washindi wa Promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa iliyokuwa inajulikana kama ‘Cash In Promotion’,Kulia ni Mojelwa Mlinga, mshindi kutoka Dar es Salaam na kushoto Said Khatibu kutoka Zanzibar.

Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imetoa zawadi za mamilioni ya shilingi kwa mawakala wake wa huduma ya Tigo Pesa kupitia promosheni iliyomalizika hivi karibuni ya ‘Wakala Cash In Promotion’. 

Promosheni hiyo ya nchi nzima ilianza Machi 1 na kumalizika Machi 31 ikilenga kuwahamasisha mawakala wa Tigo Pesa kufanya miamala zaidi na wateja ili kujishindia zawadi za fedha taslimu. 

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa baadhi ya washindi jijijni Dar es Salaam jana,mkuu wa kitengo cha bidhaa wa Tigo Pesa James Sumari alisema jumla ya Mawakala 97,000 walishiriki katika promosheni hiyo ya mwezi mmoja. 

“Promosheni hii ya aina yake, ni ya saba kwa Mawakala wetu. Tangu tulipoanza hadi kufikia hivi sasa, tumewazawadia mawakala 12,000 zaidi ya fedha taslimu shilingi bilioni 1. Washindi hawa wametoka kila kanda hapa nchini na tumeendelea kuona mwitikio mkubwa wa Mawakala kupitia promosheni hii na ni mpango wetu kuendelea kuwarushia tunachokipata kupitia wao wakati tukiendela na safari ya kufikisha huduma jumuifu za kifedha nchi nzima,” alisema Sumari 

Kwa mujibu wa Sumari, Promosheni ya mwaka huu, ilishuhudia washindi wakubwa 8 kutoka sehemu mbali mbali za nchi ambao waliweza kujishindia fedha zaidi kutokana kuwa washindi wa jumla kwenye promosheni. 

“Tumechagua Mawakala wawili waliofanya vizuri kuliko wengine katika kanda zote nne na kuwazawadia kutokana na jitihada zao za kufanya miamala mingi zaidi na wateja. Leo pia tunawashindi ambao watapata zawadi zaidi za fedha taslimu. 

Washindi wakubwa ambao leo wanakabidhiwa zawadi zao wanatokea kanda ya Pwani ambao ni pamoja na Said Khatib kutoka Zanzibar ambaye atakabidhiwa shilingi milioni 2 na Mojelwa Mlinga Mojelwa kutoka Dar es Salaam ambaye amejinyakulia Shilingi milioni 1. 

Tunayo furaha kuhitimisha promosheni yetu kwa kishindo.Tunaamini fedha tulizowazawadia Mawakala wetu zitawasaidia kukuza biashara zao pamoja na kukidhi mahitaji yao mengine. Napenda kumalizia kwa kumpongeza bwana Khatib na Mojewa pamoja na maelfu ya washindi wengine. Mchango wao unatusaidia kuweza kufikisha huduma jumuifu za kifedha hapa Tanzania kupitia Tigo Pesa,” alifafanua Sumari. 

Sumari aliongeza kuwa, makabidhiano ya zawadi kwa washindi wa jumla katika kanda za Kaskazini, Kusini na Kanda ya Ziwa yatafanyika baadaye mwezi huu. 

NAIBU WAZIRI UJENZI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI TEMESA

0
0
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akimkaribisha Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa kushoto alipowasili kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikua Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Elias Kwandikwa kushoto.
 Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akisoma hotuba wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa nne kulia) wakiimba wimbo maalumu wa wafanyakazi wa Mshikamano daima pamoja na viongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya mameneja wa mikoa wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada ya kumaliza kikao cha Baraza la wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

OFISA WA JESHI LA POLISI KIZIMBANI KWA TUHUMA YA MASHTAKA 22

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

OFISA wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Lydia Ngua (43) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka 22 ya kujipatia fedha Sh. 489, 615,000 za upatu kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo maofisa wa jeshi hilo.

Akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali, Ester Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mbando kuwa, jijini Dar es Salaam,  mshitakiwa  alijipatia Sh milioni 15.3 kutoka kwa Happy Mhando kwa nia ya kwenda kuziwekeza fedha hizo kwenye vikoba huku akijua kuwa anaenda kuzitumia kwa matumizi yake binafsi .

Imndai kuwa, Septemba 13, mwaka jana jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Ngua alijipatia Sh milioni 13.2 kutoka kwa Elisia Kisoma. Pia katika tarehe na mahali kusikofahamika, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa huyo alijipatia  Sh milioni 7.8.

Katika mashitaka mengine mshtakiwa Ngua alijipatia Sh  milioni 12.3 kutoka kwa Mariam Yohana.  zingine ni sh. Sh milioni 3.4 kutoka kwa Jenifa Fokanya. Sh. milioni 15 kutoka kwa Jane Martin, pia alijipatia Sh milioni 20.8 kutoka kwa WP Mary.

Fedha zingine alijipatia Shilingi milioni 10.9 kutoka kwa maofisa wa jeshi hilo ambao ni ASP, Imelda Twelve, Sh 9.040.000 kutoka kwa ASP Sarah Komba, Sh milioni 67 kutoka kwa Inspekta wa polisi, Richard Ninja na Sh milioni 27 kutoka kwa Shukuru Makaranga, Sh 115,897,000 kutoka kwa Henry Lwiza na Sh milioni 75 kutoka kwa Edna Mbeto

Ofisa huyo pia anadaiwa kujipatia Sh milioni 11 kutoka kwa Sabrina Mwakitalu, Sh milioni 23.3 kutoka kwa Lusiana Mwakitalu,  Sh.milioni sita kutoka kwa Mwanahamisi Issa, Sh milioni 3.78 kutoka kwa Mkemimi Abdulkarim, Sh milioni 191.4 kutoka kwa Zidadu Hassan,  sh milioni  4.322 kutoka kwa Innocent Nunuo, Sh milioni nane kutoka kwa WP Happy, na Sh milioni 37.7 kutoka kwa Halima Nabalanganya.

Imedaiwa kuwa mshitakiwa alijipatia fedha hizo kwa nia ya kwenda kuziwekeza kwenye vikoba huku akijua kuwa anaenda kuzitumia kwa matumizi yake binafsi.

Hata hivo, mshitakiwa amekana hayo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza msharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka mshitakiwa kuwasilisha mahakamani hapo nusu ya fedha anazodaiwa au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Pia ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika na wawe na vitambulisho na wadhamini hao pia wametakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika ye kiasi hicho cha pesa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

Latest Images