Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA TUNDURU-MATEMANGA –KILIMASERA-NAMTUMBO KM 193 TUNDURU MKOANI RUVUMA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru pamoja na viongozi mbalimbali  wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Tunduru-Matemanga-Kilimasera km 193 katika sherehe zilizofanyika Tunduru mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wanne kutoka kulia Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto wanane kutoka kushoto, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru wa kumi kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Tunduru-Matemanga-Kilimasera km 193 katika sherehe zilizofanyika Tunduru mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Tunduru-Matemanga-Kilimasera km 193 katika sherehe zilizofanyika Tunduru mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Tunduru-Matemanga-Kilimasera km 193 katika sherehe zilizofanyika Tunduru mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Tunduru-Matemanga-Kilimasera km 193 katika sherehe zilizofanyika Tunduru mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto kulia pamoja na Mwakilishi Mkuu wa JICA hapa nchini Naofumi Yamamura mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Tunduru-Matemanga-Kilimasera km 193 katika sherehe zilizofanyika Tunduru mkoani Ruvuma.
 Kwaya ya JKT kutoka Tunduru ikiimba katika sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo Tunduru mkoani Ruvuma.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Tunduru kabla ya kuifungua rasmi barabara ya Tunduru-Matemanga-Kilimasera km 193. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Tunduru mara baada ya kuwahutubia. PICHA NA IKULU



HALMASHAURI ZATAKIWA KUTOBOMOA NYUMBA ZA WANANCHI KWENYE MAKAZI HOLELA

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

WIZARA ya Ardhi ,Nyumba na Kakazi imezitaka halmashauri zote nchini kutokubomoa nyumba za wananchi ambazo zipo kwenye makazi holela,ambayo hayakupimwa na badala yake ziweke utaratibu utakaowezesha kuwapatia hati miliki wa nyumba hizo.

Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Ardhi, nyumba na makazi , William Lukuvi ,alipokuwa kwenye maazimisho ya siku ya nyumba Duniani, ambayo imeandaliwa na benki ya NMB, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo ya nymba inayotolewa na benki ya NMB.

Waziri Lukuvi,amesema serikali inatambua asilimia 70 % ya wananchi wanaishi kwenye makazi holela ambayo hayakupangwa hawatakiwi kubomolewa nyumba zao badala yake imeaanzisha mpango wa kurasimisha makazi yao na hivyo wasibomolewe nyumba zao.

Amesema serikali katika kuhakikisha wananchi waisho kwenye makazi holela hawabomolewi nyumba zao imewezesha wamiliki wa nyumba hizo ambazo hazikupimwa wapate mikopo ya pesa kutoka kwenye benki ili wajinyanyue kiuchumi.

Lukuvi,amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kupima ardhi zao na kulipia kodi ya serikali ambayo imepunguzwa kutoka asilimia 15% hadi kubakia asilimia 1 % tu na kuhakikisha kila anayejenga nyumba anapata hati miliki .

Amesema kuwa amesikia kilio cha wananchi kuhusu tozo inayotozwa ya nyumba ambayo ni shilingi 250,000 ili kuwezesha kupata leseni ya makazi kuwa imekuwa ni kubwa hivyo wizara ya ardhi, makazi na nyumba, itatoa leseni hizo kwa wananch wote ambayo itakuwa ni shilingi 5000, ambayo itadumu kwa kipindi cha miaka mitano tu

Lukuvi,amesema punguzo hilo la tozo ni kuwapunguzia wananchi makali na baada ya miaka hiyo mitano watalazimika kulipa tozo hiyo ya shilingi 250,000 kwa kuwa hiyo itakuwa ni dhamana kwa mwenye nyumba..

Lukuv,amesema hajaridhishwa na benki nchini kutokana na kutotoa mikopo ya nyumba kwa wananchi na badala yake benki hizo zimekuwa zikitoa mikopo ya fedha.Amesema benki zinatakiwa kuwakopesha wananchi nyumba ambazo watazilipia kidogokidogo na hatimae wakimaliza madeni yao watamikilishwa nyumba hizo

Benki ya NMB ni mshirika mwenza wa shirika la nyumba nchini NHC, katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na makazi bora na ambayo ni salama

NYUMBA ZA ASKARI POLISI 20 ZAJENGWA PWANI ILI KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MAKAZI UNAOWAKABILI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, handisi Evarist Ndikilo na Kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa wakikagua ujenzi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, handisi Evarist Ndikilo akijadiliana jambo na kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa.



Mafundi wakiendelea na ujenzi wa nyumba hizo. 

…………………………………………………………………………………………..
 
 
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

ASKARI wa jeshi la polisi mkoani Pwani, wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa makazi ya kuishi, hali inayosababisha kushindwa kuwahi wakati wakihitajika haraka katika dharula za majukumu yao ya kikazi.
Kutokana na hali hiyo, kwasasa jeshi hilo linajenga nyumba 20 za makazi ya askari polisi hao,zitakazogharimu milioni 500 ili kukabiliana na hali hiyo. 

Akizungumza wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa nyumba hizo zinapojengwa Kibaha Mjini, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alitaka ujenzi huo ,ukamilike ifikapo June 30 mwaka huu, kama amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama ,dkt. John Magufuli alivyoelekeza. 

Alisema ,askari wanapaswa kulinda mali ya mwananchi na kulinda usalama wa raia hivyo wanatakiwa waishi kwenye mazingira yaliyo bora. “Kanda maalum ya kipolisi Rufiji imepatiwa milioni 500, pamoja na jeshi la polisi Pwani milioni 500, jumla milioni 100, ambazo zimetolewa na serikali kuhakikisha kila mkoa askari wanajengewa makazi ya kuishi “ “Hivyo ni wajibu wa jamii, wenye viwanda kushirikiana na serikali na jeshi la polisi kujenga mazingira bora ya askari hawa waweze kutulinda kwa moyo na upend “alifafanua Ndikilo. 

Awali akitoa taarifa fupi kwa mkuu wa mkoa huyo juu ya ujenzi unavyoendelea, kamanda wa polisi Pwani, Wankyo Nyigesa alibainisha, kutokana na ufinyu wa bajeti wamepewa milioni 500 na kwa wastani kila nyumba itagharimu milioni 25 mpaka kukamilika kwake. 

Aliwashukuru wadau waliojitokeza kusaidia akiwemo Said Salim Bakhresa, jeshi la wananchi wa Tanzania kupitia kikosi cha usafirishaji (KJ 95) ambao waliwapatia lowbed kwa ajili ya kubeba buldoza kutoka bakhresa sugar company huko Bagamoyo. 

Wengine ni Chila mkurugenzi wa Creative Intertraders ltd ambae ametoa mifuko 100 ya saruji na Twyford Ceramics (KEDA )ya Chalinze na wengine ambapo amewashukuru na kuomba wadau wengine waendelee kuwashika mkono. 


Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa ambayo , Amiri Jeshi wa Majeshi dk. Magufuli akiwa anazindua nyumba za askari polisi mkoani Arusha ,april 7 mwaka 2018, alitoa maelekezo kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) kwamba atapatiwa fedha kwa ajili ya makazi ya askari ,ambapo mkoa huo umeanza utekelezaji baada ya kupokea fungu hilo.

MUONEKANO WA CHUO CHA VETA KILICHOZINDULIWA LEO NA RAIS DKT MAGUFULI WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA.

$
0
0

Mjini Namtumbo, Mhe. Rais Magufuli amezindua Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kilichojengwa na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya shilingi Bilioni 6.5 na ambacho kitakuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi 600 wa kozi ndefu na fupi kwa mwaka. 

Mhe. Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa kwake na gharama kubwa zilizotumika ikilinganishwa na thamani ya majengo yaliyojengwa na ameitaka VETA na viongozi wote wa Serikali kutambua umuhimu wa kubana matumizi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Joyce Ndalichako amesema pamoja na chuo cha VETA Namtumbo, Serikali imejenga vyuo vingine vya VETA katika Mikoa ya Njombe, Rukwa, Geita na Simiyu. Pia imejenga vyuo vya maendeleo ya jamii 20 ambavyo vitaongezeka hadi kufikia 34 ifikapo mwaka 2020.



CCM YAANGUSHA NGOME YA UPINZANI KARATU, MADIWANI WATATU WA CHADEMA WABWAGA MANYANGA, MAELEKEZO MAZITO YA MIRADI YA MAJI YATOLEWA

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Karatu kimepokea Madiwani watatu wa Upinzani kutoka Chadema na mmojawapo akiwa Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu. Madiwani hao wanatoka kata za Ganako, Daa na Mbulumbulu.

Akizungumza katika Mkutano wa kuwapokea Madiwani hao Katibu wa HKT Mwenye dhamana ya Itikadi na Uenezi Ndg. H. Polepole amesema tofauti na nyakati nyingine awamu hii ya tano ya Uongozi wa Chama na Serikali chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli tumejifunza kwamba iko tija kubwa katika kusema na kisha kutenda.

 Ndg. Polepole ameelezea miradi mikubwa ya kimkakati na miradi mikubwa ya kisekta ikiwemo Elimu bure, Huduma za Afya, Barabara, Maboresho makubwa ya Kilimo na Upatikanaji wa maji inatekelezwa kwa haraka na asilimia kubwa ikiwa fedha za ndani.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa Maelekezo kwa Serikali kwamba ifikapo Julai 1, 2019, taasisi ndogo ndogo binafsi zinazojihusisha na utolewaji wa huduma za Maji zitakuwa chini ya Mamlaka ya Serikali ili kuongeza ubora, ufanisi na kushusha viwango vya bei za maji kwa wananchi ikiwemo hapa Karatu kwasababu jambo hili jema na ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM amesema Ndg. Polepole

Shughuli ya kupokea Madiwani Wilayani Karatu imehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg. Loata Sanare, Mjumbe wa HKT Mkoa wa Arusha Ndg. Daniel Awaki na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Karatu.

Huu ni muendelezo wa kazi za ujenzi na uimarishaji wa Chama ndani ya Chama na nje ya Chama ndani ya Jamii ikiwemo kujiridhisha utekelezwaji wa Ilani ya CCM.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

BAADA YA KIMYA KIREFU SASA WASANII AMINI NA LINAH WAMENASA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya mwenye uwezo mkubwa wa kuteka hisia za mashabiki Amini Mwinyimkuu anatarajia kuipua kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Nimenasa akimshiriki mwanadada aliyekwe ubora wake Esterina Peter Sanga a.k.a Linah.

Akipiga stori na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam Amin amesema wimbo huo utauachia wiki ijayo na kwamba ameufanyia Studio ya C9 chini ya mtayarishaji Kichwa Touch Killer.

Kama kawaida yake akiwa anazungumza kwa upole wa hali ya juu ukiambatana na umakini wa kujieleza amesema ni wakati muafaka wa kutoa wimbo huo akiwa amemshirikisha Linah kwani ni mwanamuziki wa kike anayemkubali.

Ujue iko hivi Amini na Linah huko nyuma walikuw na uhusiano ule wa kibaba na mama lakini safari hii wameamua kukutana kwa ajili ya kufanya kazi moja tu ya kutoa wimbo kwa ajili ya mashabiki wao.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi kama wameruadia au laa, Amini akizungumza kwa kujiamini kama jina lake kuwa hakuna uhusiano huo zaidi ya ule wa kufanya kazi kama wasanii.

"Hatuna uhusiano ila nimeamua tu safari hii katika wimbo wangu mpya nishirikiane na dada Linah."Swali likawa tena kwanini Amini anamuita dada Linah ,eti akajibu hivi "Wanawake ndio mama zetu, na akiwa mdogo kwangu atakuwa dada,ndio maana nasema ni dada Linah."

Kwanini ameamua kumshirikisha Linah katika kibao hicho cha Nimenasa, amejibu anavutiwa na uwezo na kipaji cha mwanadada huyo na kwamba Linah hata akiamshwa kutoka usingizi ubora wa sauti na uwezo wa kuimba uko palepale.
"Linah anao uwezo mkubwa sana wa kuimba na ndio maana nimeamua kumshirikisha,pia na hata pale unapokuwa umetunga mashairi ya wimbo ukimpa anaweza kukariri kwa muda mfupi," amesema Amini.

Alipoulizwa kama Caple yao yaani Amini na Linah inaendana ,amejibu ukweli ni kwamba mashabiki wanaofuatilia muziki wao wamekuwa wakisema wanafurahia Caple yao na wanatamani wafanye kazi pamoja.Mbona raha.Acha tusubiri tuone kama kweli wanaweza kuishia kwenye kuimba tu au watarudi kuleee kwenye mahusiano ya michezo ya kibaba na kimama.

Kwa kukumbusha tu msanii Amini umaarufu katika muziki umetokana na nyimbo zake mbalimbali zikiwemo Ni wewe,Mtima wangu, Robo Saa, Unikimbie, Nyota,Yameteka dunia na Novemba or Desemba.

NUKUU ZA NDG. HUMPHREY POLEPOLE KWENYE DARASA LA ITIKADI - CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI KATA YA MABIBO

$
0
0

1. " Ukiwa Mwanachama wa CCM lazima usome na uelewe kuhusu Chama chetu tunataka kuendesha Chama chetu kisayansi, tunataka kuendesha Chama chetu kisasa ili tutimize shabaha ya kuwatumikia watanzania kwa uaminifu, uadilifu na  kwa kasi zaidi" Ndg. Polepole

2. "Mageuzi ya Chama chetu yanakwenda sambamba na kuhakikisha kuwa tunakuwa na Viongozi  waaminifu, wachapakazi, wanachukizwa na rushwa na wanaokubalika ndani ya Chama na nje ya Chama ndani ya Jamii" Ndg. Polepole

3. "Wapo watu wamechagua kutubeza, kumbeza Rais wetu na kubeza maendeleo ya wananchi, wanaCCM tusimame imara na tukitetee Chama chetu na Serikali yetu wakati wote" Ndg. Polepole

4. "Siku hizi hapa Tanzania CCM ndio habari ya mjini, watu wote tunaojitambua tupo CCM upende usipende huo ndio uhalisia" Ndg. Polepole

5. "Mwaka jana 2018 Rais wetu amefanya kitendo ambacho Afrika nzima hakuna nchi imewahi kufanya, alipoona wanunuzi wakorosho wanawalangua wakulima Serikali ilifanya uamuzi  wa kununua Korosho yote sio ipate faida bali  istiri jasho la mkulima" Ndg. Polepole

6. "Tunatoa wito ifike wakati Serikali itunge sheria ya kuwaratibu madalali hawa wana wanyonya sana wakulima" Ndg. Polepole

7. "Tukapojua wapi  kuna shida za watu tukazitatua tutakuwa na nafasi nzuri sana kwenye chaguzi" Ndg. Polepole

8. "Chama tunampango uliyotukuka wa kuwatumikia watanzania kwa vizazi vitatu, kizazi cha kwanza 2025 - 2050, kizazi cha pili 2050 - 2075 na kizazi cha tatu 2075 - 2100 na hapa Tanzania itakuwa zaidi ya ulaya" Ndg. Polepole 

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI


RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN, AFUNGUA MSIKITI KIJIJI CHA MTENDE WILAYA YA KUSINI UNGUJA LEO

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Alim Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid Maryan Mtende Wilaya ya Kusini Unguja kushoto Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar Ndh Said Salim Bakhressa, hafla hiuyo imefanyika katika Kijiji hicho leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekitin wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Waumini wa Dini ya Kiislam wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa hafla hiyo ya Ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende, uzinduzi huo umefanyika leo 5-4-2019
MWANAMCHI wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja Sheikh Khamis Ramadhan Mbarak. akisoma risara ya Wananchi wa Kijiji cha Mtende wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Msikiti wao Mpya uliojengwa kwa Ufadhili wa Bw. Said Salim Bakhressa.
BAADHI ya Wananchi wa Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakifuatilia hutuba ya ufunguzi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Mkoa wa Kusini Unguja leo 5-4-2019
MIFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Wilaya ya Kusinu Unguja, kushoto Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Mfanya Biashara Maarafu Tanzania Bw. Said Salim Bakhressa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Khamis Maalim Juma na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan, wakiitikia dua wakati wa hafla hiyo
MKURUGENZI wa Mashtaka Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee mwenye miwani akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakiitikia dua wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende leo
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduzi Mhe. Haroun Ali Suleiman akitowa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Wilaya ya Kusini Unguja leo, baada ya uzinduzi wake leo.(Picha Ikulu).

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA MGENI RASMI HARAMBEE YA KUICHANGIA LIPULI FC JUMAPILI HII

$
0
0
Kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo akiwa mbele ya waandishi wa habari akielezea lengo la kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo ili kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu Tanzania bara.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa wakiwasikiliza viongozi wa timu ya Lipuli fc juu ya mipango na mikakati ya Harambee ya kuichangia timu hiyo.




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


UONGOZI wa timu ya mpira wa migu inayoshiliki ligi kuu Tanzania bara Lipuli Fc ya mkoani Iringa umepanga kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo kwa lengo la kuimarisha uchumi kutatua changamoto za mishahara pamoja ada za wachezaji ambazo hadi hii leo bado wanadaiwa na wachezaji wa klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoa Iringa kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo alisema kuwa lengo la kuitisha harambee hiyo ni kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu Tanzania bara.

“Ni kweli hatujalipa wachezaji miezi miwili hadi hivi sasa nab ado tunadaiwa pesa za usajili kwa wachezaji wetu hiyo tumeamua kufanya hivyo kwa lengo la kuinusu timu kwa msimu ujao kuondokewa na wachezaji wetu ambao ni wazuri kweli kweli na wanaujua mpira sana” alisema Kihwelo

Kihwelo aliongeza kuwa harambee hiyo itafanyika siku ya jumapili tarehe 7 / 4 / 2019 siku ya jumapili katika ukumbi wa kichangani uliopo manispaa ya Iringa ambapo wanatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda kuwa mgeni Rasmi

Siku ya harambee hii tunatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda kuwa mgeni Rasmi akiambatana na wadau mbalimbali akiwepo mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huu ambao tunategemea watachangia timu yao ambayo inafanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara” alisema Kihwelo

Kihwelo alisema wanatarajia kupata zaidi ya shilingi milioni miatatu kwenye Harambee hiyo ambazo zitasaidia kuendesha timu bila kuwa na deni lolote kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo na kuweza kupata usajili mpya wa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara

“Tunalipa zaidi ya milioni ishirini na nne kila mwezi kwa ajili ya mishahara tu ya wachezaji wa timu na tunagharamia zaidi ya laki tatu kwa siku kwa ajili ya kambi ya timu hivyo utaona kwa namna gani timu inavyogharimu kiasi kikubwa cha fedha na timu hadi hivi sasa haina mdhamini yeyeote yule” alisema Kihwelo

Aliezea kuwa mikakati ya msimu ujao ni kuhakikisha timu inapata mdhamini wa kudumu kwa kuwa timu yetu ya Lipuli imekuwa ikipata matokeo mazuri kila msimu hivyo itatusaidia kupata mdhamini ambaye ataamini kuwa timu hiyo inauwezo wa kuitangazia bidhaa yake.

Kwa upande wake katibu mkuu wa klabu hiyo ya Lipuli Julius Leo ameomba wananchi,wadau wa soka na wapenzi wa klabu ya Lipuli kuichangia timu hiyo kwa kutumia akaunti ya benk ya CRDB 01J2072252000 na kwenye namba ya simu ya MPESA ya timu hiyo ambayo ni 0744 16 24 46 inayojulikana kwa jina la LIPULI FC

TFDA YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI 538 WALIO KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU

$
0
0


Baadhi ya wanafunzi wa kikewa kidato cha Sita mwaka 2019 mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (katikati), mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike zilizotolewa kwa ajili yao na mamlaka hiyo, katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kushoto)akiwa na baadhi ya wanafunzi wa kike wa kidato cha sita mkoani humo, wakipokea sehemu ya msaada wa taulo za kike zilizotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kuwasilishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (wa tatu kulia), katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya wanafunzi sehemu ya maboksi ya taulo za kike ambazo zimetolewa msaada kwa wanafunzi kike walio kwenye kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Mwanafunzi Winfrida Nasoro kutoka Shule ya Sekondari Dutwa, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya Kitaaluma ya Kidato cha Sita inayoendelea wilayani Maswa.
Sehemu ya katoni za taulo za kike zilizotolewa msaada Aprili 05, 2019 na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya Kitaaluma ya Kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoani Simiyu inayoendelea wilayani Maswa.
Baadhi ya wanafunzi wa kikewa kidato cha Sita mwaka 2019 mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama (katikati), mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike zilizotolewa kwa ajili yao na mamlaka hiyo, katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.

…………………………

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) imetoa msaada wa katoni 111 za taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni tano, kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019, inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya wasichana Maswa Mkoani hapa.

Akikabidhi msaada huo Aprili 05, 2019 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama, amesema Mamlaka hiyo imetoa msaada huo kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua elimu mkoani Simiyu, ili kuwasaidia watoto wa kike wasome kwa uhuru na utulivu kambini hapo hususani wakati wa hedhi.

Amesema TFDA kama wadau wa mkoa wataendelea kushirikiana na Serikali mkoani Simiyu katika sekta ya elimu na masuala mengine ya Maendeleo, huku akiwasisitiza wanafunzi walio kambini kusoma kwa bidii na kutumia vizuri muda walionao ili waweze kufikia malengo yao.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Mamlaka hiyo kwa msaada uliotolewa kwa wanafunzi wa kike, huku akiwasisitiza wanafunzi wote walio katika kambi ya kitaaluma kusoma kwa bidii.

Aidha, Mtaka amewashukuru wadau mbalimbali ambao wameendelea kutoa michango kwa ajili ya kufaninisha kambi ya kitaaluma inayoendelea mkoani humo, huku akiahidi kuwa wadau wote waliochangia watatambuliwa na kupewa vyeti.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa ufafanuzi kwa wadau na wananchi kuhusu utaratibu wa kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, kwamba kambi hizi hufanyika katika ngazi za shule na baadaye huundwa kambi moja ya mkoa kuwakutanisha wanafunzi kwa ajili ya kambi ya mkoa.

“Kambi za Kitaaluma kwenye mkoa zilianza muda mrefu lakini kama mkoa tumeweka utaratibu wa kuwa na kambi moja ya kimkoa inayounganisha shule zote za kidato cha sita; kambi za kidato cha nne nazo zinaendelea kwa hiyo tutakapofika mwezi wa saba tutaanza kuunganisha shule, kama tulivyofanya mwaka jana tuliunganisha shule 24 pale Simiyu Sekondari” alisema.

Nao wanafunzi wa kike wa Kidato cha Sita walio katika Kambi hiyo ya Kitaaluma wameishukuru Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa msaada huo ambao wamesema utawasaidia sana kusoma kwa uhuru na kujiamini zaidi wakati wa hedhi.

“Tulikuwa tunakumbana na changamoto ya kutokuwa na amani na kushindwa kujiamini wakati wa hedhi kwa hiyo hata kusoma tulikuwa tunasoma lakini tunakuwa na wasiwasi, kupitia msaada huu ‘tutakuwa comfortable ‘ (tutakuwa na amani) kabisa tunaishukuru sana TFDA”Mwanaidi Halfan.

“Huu msaada tuliopata utanisaidia kufikia ndoto zangu maana wasichana wengi wanapokosa taulo hizi za kike wanashindwa kusoma, wanakuwa na hofu wengine hata darasani hawaendi, lakini kwa kuwa wote tumepata msaada huu najua muda tutakao kuwa hapa tutakuwa huru kujisomea hatutaogopa tena maana zinatuhakikishia usalama tunapokuwa hedhi” alisema Hidaya Simba

Jumla ya wanafunzi 1166 wa kidato cha Sita mwaka 2019 kutoka shule 12 mkoani Simiyu wako katika kambi ya kitaaluma kwa siku 28 katika shule ya sekondari Maswa, kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika mwezi Mei, 2019.

TAARIFA MUHIMU KUTOKA NIDA

KAMPENI YA USINYWE NA KUENDESHA CHOMBO CHA MOTO YAZINDULIWA JIJINI ARUSHA

$
0
0


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe akizungumza na madereva wa magari ya abairia, binafsi na madereva bodaboda katika uzinduzi wa kampeni ya kunywa kistaarabu iliyozinduliwa leo jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha akizungumzia kampeni ya kunywa kistaarabu maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’
Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha akizungumza na madereva bodaboda katika stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe akimvisha kizibao cha kisibqo chakung'aa mmoja wa madereva bodaboda katika stendi kuu ya mabasi jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.

Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi akimvisha mmoja wa dereva bodaboda kizibao cha kung'aa (reflector) katika kampeni iliyozinduliwa Jijini Arusha ya kunywa kistaarabu na kampuni ya Serengeti.Picha na Vero Ignatus.
Mwenyekiti wa bodaboda akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya kunywa kistaarabu stendi kuu ya mabasi Jijini Arusha.


Na. Vero Ignatus, Arusha


Madereva wa vyombo vya moto Mkoani Arusha watakiwa kutotumia vilevi wakati wawapo barabarani

Arusha, Aprili 5, 2019, Kampeni ya unywaji wa kistarabu inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imezinduliwa rasmi Mkoani Arusha ambapo madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani na kutotumia vilevi wakati wa kazi.

Kampeni hiyo maarufu kama ‘Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto’ imeenda sambamba na ugawaji wa makoti ya usalama (Reflectors) kwa madereva bodaboda mkoani humo ikiwa ni mkakati wa kuhimiza matumizi ya vifaa hivyo kwa usalama wa watumiaji wa barabara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Traffic jijini hapa, Mkurugenzi wa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha amesema kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa wateja wake nchini ili kupunguza matukio yanayoepukika kama ajali zitokanazo na unywaji wa pombe kupindukia.

“Pombe isipotumika kiistarabu inaweza kuleta madhara katika jamii na mojawapo ya madhara ni pale mtu anapokunywa pombe na akaendesha chombo cha moto ikasababisha ajali jambo ambalo ni hatari kwa madereva na pia ni hasara kwa Taifa,” alisema

Kampeni hiyo inashirikisha wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi-Kikosi cha usalama barabarani, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), madereva bodaboda pamoja na jamii kwa ujumla ikilenga katika kupunguza ajali zitokanazo na ulevi wa kupindukia nchini.

Kwa upande wake,Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO) Joseph Bukombe alisema kampeni hiyo itasaidia katika kupunguza ajali zinazosababishwa na ulevi huku akiwataka madereva kuzingatia kuacha kutumia vilevi ili kujihakikishia usalama wawapo barabarani.

Madereva bodaboda atakayekamatwa anaendesha hana leseni pikipiki itazuiliwa atalipia shilingi 25,000 ataingia darasani kusoma akimaliza kusoma atapewa cheti chake halafu anaanza kushughulikia leseni yake. Alisema RTO.

“Unywaji wa pombe kiistarabu ni suala la muhimu sana kwa madereva kwasababu madereva wakiwa kwenye hali ya ulevi ni moja ya chanzo cha ajali za barabarani hivyo tunaipa kipaumbele kampeni hii hapa mkoani Arusha na tutaendelea kutilia mkazo suala hili,” alisema

Bukombe amewakumbusha madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa Stika za usalama barabarani zimeshatoka hivyo wapeleke pikipiki zao kukaguliwa kwa shilinhi 1000,magari ya watu binafsi 3000,magari ya biashara 5000

Aliipongeza SBL kwa kuona umuhimu wa kuwalinda watumiaji wa barabara kwa kutoa elimu hiyo kwa madereva na umma kwa ujumla. “Pamoja na kuwa wao (Serengeti) ni watengenezaji wa pombe lakini wameona wajibu wao wa kumlinda na kuleta usalama wa madereva na watumiaji wengine wa barabara,” alisema

Kwa upande wake mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani (RSA) Bakari Msangi amewataka madereva waendesha bodaboda na magari ya Abiria kuwa makini wawapo barabarani na wafuate sheria kama inavyotakiwa

Tunachowasii na kusisitiza ni kutii sheria mnapokuwa kwenye vyombo vya moto, wacheni ulevi mkiwa kazini, kunywa wakati umeshamaliza kazi, tuhqkikishe tunaondoa ajali zote zinazo epukika

INTRODUCING: YANTE BY DOGO JANJA

DKT. KEBWE AWATAKA WAKINA MAMA WAJAWAZITO KUZINGATIA CHANJO

$
0
0
Mratibu wa afya ya mama na mtoto mkoa wa Morogoro Santiel Kinyongoakizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Morogoro


Na. Vero Ignatus.

Dkt. Mkuu wa mkoa wa Morogoro, daktari Kebwe Steven Kebwe amewataka akina mama wajawazito mkoani humo kuzingatia chanjo zote muhimu wakati wa ujauzito ili wajifungue salama.

Daktari Kebwe pia amewataka akina mama hao kuhakikisha watoto wanaowazaa wanapata chanjo zote muhimu katika vituo vya Afya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya " Jiongeze Tuwavushe Salama " ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hiyo ya kitaifa Kwa ngazi ya mkoa, Daktari Kebwe amesema chanjo zinawalinda mama na mtoto atakayemzaa na maradhi mbalimbali yakiwemo pepopunda.

Kuzinduliwa kwa kampeni hiyo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ukiwemo wa Morogoro ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali kuu kwa wakuu wote wa mikoa nchini kuzindua na kutekeleza ajenda ya kuhakikisha vifo vya wajawazito na watoto wachanga vinapungua.

Daktari Kebwe amesema serikali imewekeza vya kutosha katika sekta ya afya kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana.Amewataka wanawake wajawazito wa mkoa wake kuhudhuria kliniki wakiwa na wenza wao na kuhakikisha chanjo wanazipata Kwa sababu zinatolewa bure.

Amesema mama mjamzito anayehudhuria kliniki atajua mapema changamoto za uzazi atakazopitia ili kuepuka uzazi pingamizi, ambao ni moja ya vyanzo vya kifo kwa akina mama, ikiwemo kutokwa damu nyingi wakati na baada ya kujifungua.

Amewataka watendaji wa mkoa, wakiwemo wakuu wa wilaya wote, wakurugenzi, waganga wakuu, wananchi na wanaohusika katika kutoa huduma kuhakikisha vifo vinapungua.Pia ametia sahihi ya makubaliano ya uwajibikaji wa "kasi" Kwa wakuu wa wilaya zote kuhakikisha maazimio ya kimkoa ya kupunguza vifo yanafikiwa.

" Tunatengeneza utaratibu wa kuwapima ( score card) kuona nani ametimiza wajibu wake ambao kila baada ya miezi 6 utafanyika ," amesema daktari Kebwe.Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama ilizinduliwa na makamu wa Rais, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mwezi November mwaka juzi mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wakuu wote wa mikoa, utekelezaji wake ukiwa chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto wa mkoa wa Morogoro , Santiel Kinyongo amesema mkoa unafanya jitihada kupunguza vifo vya mama na mtoto, ingawa bado kuna changamoto ndogo ndogo.Amesema kwa mfano kuna upungufu Wa wakunga katika vituo vya vingi vya mkoa wa Morogoro, isipokuwa Wilaya ya Ifakara na Manispaa ya Morogoro hali inaridhisha.

Pia ameongelea umuhimu wa mama mjamzito kuhakikisha anahudhuria kliniki si chini ya mara 4 wakati wa ujauzito wake ili apate chanjo za kumlinda yeye.Ameshauri pia mama mjamzito kumpeleka Mtoto atakayemzaa kliniki ili aweze kupewa chanjo zote muhimu.

Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama inatekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo UNICEF
Picha mbalimbali za matukio ya uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama iliyofanyika mkoani Morogoro.

AGAPE YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KWA VIJANA KWA NJIA YA MICHEZO

$
0
0
Shirika la Agape AIDS Control Programme limetoa elimu ya afya uzazi na ujinsia kwa vijana kwa njia ya michezo katika kijiji cha Manyada kata ya Usanda Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI,mimba na ndoa za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia. 

Elimu hiyo imetolewa Ijumaa Aprili 5,2019 katika Uwanja wa Kitongoji cha Mwagala ambapo michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,kukimbiza kuku na mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake imefanyika ikihusisha vijana walio nje ya shule. 

Washindi katika michezo hiyo kutoka vitongoji vya Buchamike,Mwagala,Uswahilini,Sagabahi na Munge wameondoka na zawadi ikiwemo kuku na mbuzi huku wakipata ujumbe wa aina mbalimbali kuhusu namna ya kulinda afya zao lakini pia kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake katika jamii. 

Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga alisema elimu hiyo inatolewa kwenye maeneo ya pembezoni ‘Hard to reach communities’ katika kata ya Usanda ili jamii ichukue tahadhari kuhusu maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. 

“Michezo hii imeshirikisha vijana ambao wapo nje ya shule,tunaamini elimu hii itawasaidia vijana ikizingatiwa kuwa vijana ndiyo wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya VVU na vijana hawa ndiyo wamekuwa wakiwatia mimba watoto na kuwakatisha masomo shuleni”,alieleza Maganga. 

Akitoa elimu ya afya,Muuguzi kutoka Kituo cha Afya Usanda,Jesca Mabula aliwahamasisha vijana kufanyiwa tohara kwani inakinga kwa asilimia 60 dhidi ya maambukizi ya VVU na kutumia kondomu huku akiwashauri kupima afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya VVU au la. 

Pia aliwataka wanaume kuachana na tabia ya kuchepuka pindi wake zao wanapojifungua kwani kitendo hicho kinachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa. 

“Wanaume tunzeni wake zenu,acheni kuchepuka na kuuza vyakula kwa ajili ya kuwahonga na hata kuoa wanawake wengine,pia muwaruhusu wake zenu kupanga uzazi wa mpango na muwe na tabia ya kutembelea vituo vya afya kwa ajili ya ushauri kuhusu masuala ya afya”,alieleza. 

Muuguzi huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi juu ya umuhimu wa kukaa karibu na watoto wao wa kike na kuwaeleza kuhusu mabadiliko ya mwili na kuhakikisha wanawapeleka shule badala ya kuwaozesha wangali wapo katika umri chini ya miaka 18. 

Shirika la Agape la mkoani Shinyanga linatekeleza mradi wa afya ya uzazi na ujinsia katika kata ya Usanda kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la Sida nchini Sweden kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni,maambukizi ya VVU na ukatili wa kijinsia. 
Mgeni rasmi, Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu akizungumza wakati Shirika la Agape likitoa elimu ya afya uzazi na ujinsia kwa vijana kwa njia ya michezo katika kijiji cha Manyada kata ya Usanda Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga akiwahamasisha wananchi kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kukabiliana na maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa,kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia. 
Muuguzi kutoka Kituo cha Afya Usanda,Jesca Mabula akitoa elimu ya afya ya uzazi na kuwashauri vijana kujitokeza kufanyia tohara na kuwahamamisha kutumia kondomu na kuachana na michepuko watunze wake zao.
Muuguzi kutoka Kituo cha Afya Usanda,Jesca Mabula akiwataka akina mama kuacha tabia ya kupeleka watoto wao wa kike kwa waganga wa jadi kutafuta dawa ya kupendwa 'samba' ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni pamoja na maambukizi ya VVU.
Afisa Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwasisitiza vijana wafanyiwe tohara na kuacha kutamani watoto wa shule kuhusu akiwashauri wanaume wanaopenda watoto wa shule wawashonee sketi za shule wake zao ili tamaa ya kutamani watoto wa shule.
Washiriki wa mbio za baiskeli wakichuana vikali katika round 20 kuzunguka uwanja ambapo mshindi wa kwanza alipata zawadi ya mbuzi mmoja.
Ni burudani tu!! Vijana wa kike hawakuwa nyuma katika mbio za baiskeli wakichuana vikali...Hapa wanaoneshana nani mkali katika round 5 kuzunguka uwanja.
Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea ambapo aliyefanikiwa kukamata kuku,ndiyo ilikuwa zawadi yake...kama atakwenda kumfanya kitoweo ama kumfuga basi kazi kwake!!
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu Mwagala kikiwa tayari kabisa kukabiliana na timu ya Buchamike katika uwanja wa Mwagala.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu Buchamike kikiwa tayari kabisa kuwavaa Mwagala.
Mchezo kati ya Mwagala na Buchamike ukiendelea.
Mchezo unaendelea....Hata hivyo Buchamike waliibuka washindi kwa kuwachapa Mwagala bao 1 - 0.
Mashabiki wa timu ya Mwagala wakiwa uwanjani.
Mashabiki wa timu ya Buchamike wakishangilia baada ya timu yao kuwachapa Mwagala bao 1 - 0
Mgeni rasmi, Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu (kushoto) akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa kwanza shindano la mbio za baiskeli upande wa wanaume Jeremiah Dotto.
Mgeni rasmi, Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa kwanza shindano la mbio za baiskeli upande wa wanawake Juke Jackson (aliyebeba mtoto).
Washindi wa pili shindano la mbio za baiskeli (Emmanuel Malale upande wa wanaume na Mariam Segese upande wa wanawake) wakiwa wamebeba zawadi ya kuku baada ya kukabidhiwa.
Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu (kushoto) akikabidhi zawadi ya mbuzi wawili kwa washindi wa kwanza shindano la mpira wa miguu (Buchamike).
Golikipa wa timu ya Buchamike Ntalike Juma(kushoto) na Kapteni wa timu hiyo Jimogela Mwita wakibeba zawadi ya mbuzi wawili.
Golikipa wa timu ya Buchamike Ntalike Juma(kushoto) na Kapteni wa timu hiyo Jimogela Mwita wakiondoka na zawadi ya mbuzi wawili.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Rais Magufuli Atoa Milioni 200 Kusaidi Ukamilishaji Kituo cha Afya Tunduru

$
0
0
NaTheresia Mallya - Afisa Habari Tunduru DC




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametoa maagizo kwa waziri wa Tamisemi Mhe.Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 200 za kukamilisha ujenzi na upanuzi wa  kituo cha afya Juma Homera kilichopo Nakayaya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Maagizo hayo ameyatoa wakati akitoa hotuba kwa wananchi wa wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchele –Nakayaya akiwa katika ziara ya kikazi siku ya pili mkoani Ruvuma.

Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kuguswa na michango ya wananchi waliotoa katika kuchangia ujenzi wa kituo cha afya Juma Homera ya shilingi Milioni 189 ili kujenga kituo hicho kitakachosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya
Tunduru.

“Waziri wa Tamisemi nakuagiza ulete shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufanya upanuzi wa kituo cha afya Juma Homera ili kitoe huduma za upasuaji,mionzi,kuongeza wodi za kutosha ili kurahisha huduma za afya kwa wananchi wa Tunduru”

aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli Alimuagiza waziri wa Tamisemi Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 500 za ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Namiungo ambayo haina zahanati wala kituo cha Afya katika vijiji saba vya kata hiyo.

Magufuli alilazimika kusimamisha msafara na kuwasikiliza wananchi waliokuwa wamefunga barabara ambapo alisema kuna kila sababu ya kata hiyo kuwa na kituo bora na cha kisasa ili kupunguza vifo vya kinamama na wajawazito na watoto vinavyosababishwa na kusafiri umbali mrefu
kufuata huduma za afya.

Hata hivyo alimaliza kwa kuwataka wananchi kufanya kazi na kushikamana katika kuijenga Tunduru na kuepuka chuki za kisiasa kwani  maendeleo hayana chama, niwatake wanatunduru muungane kwa pamoja katika kuleta maendeleo chanya.

LIVE SHEREHE YA UTOAJI TUZO ZA MALKIA WA NGUVU

TAARIFA KUHUSU FURSA YA KUNUNUA KOROSHO ZA TANZANIA

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA KUSAFIRISHA UMEME KV 220 KUTOKA MAKAMBAKO HADI SONGEA MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakiminya kitufe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu wa umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakiangalia mradi huo wa umeme utakavyosambaza umeme katika maeneo mbalimbali kutoka kutoka Makambako hadi Songea
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg, Waziri wa Nishati Medard Kalemani wakielekea eneo la uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa usafirishaji wa umeme.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakipungia mikono wananchi waliohudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mradi wa umeme.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.
 Moja ya kituo cha kupooza umeme cha Songea.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua kituo Kikuu cha Mabasi cha Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo Kikuu cha Mabasi cha Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
 Sehemu ya wananchi wa Songea mkoani Ruvuma wakiwa ndani ya Uwanja wa mpira wa Majimaji kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. PICHA NA IKULU

It’s Time to End Gender-Based Violence, Together

$
0
0
Tausi Suedi speaking at a White Ribbon Alliance for Safe Motherhood meeting in Dar es Salaam, Tanzania 

When it comes to human rights violations, those directed against women and girls, and in some cases young boys, are especially glaring. What’s worse, these crimes are often committed in common, familiar environments: at home, at school, or at a place of worship. The cycle of violence against women and girls is hard to break because the perpetrators are often related to or work closely with the victims, they have more power, and they are sometimes regarded as untouchable by the law. How, then, do we end gender-based violence collectively?

Gender-based violence is learned in the home, where girls are taught to be silent when abused and boys learn to mistreat women, creating a dangerous framework around gender, entitlement, and expectations. Gender-based violence, then, is a language and tradition learned in early childhood, one that stays with men into adulthood, motivating them to harm women, girls, and young boys.

Some common forms of gender-based violence across the African continent include rape culture, domestic violence, forced prostitution, physical violence, human trafficking, female genital mutilation, political violence, forced marriage, acid attacks, and child maltreatment in the home and as well as in public settings. In many societies, gender-based violence is a norm met with silence, and abusers are rarely held accountable, creating risky, unsafe living environments and traumatizing life experiences for victims. The physical, economic, and social costs associated with gender-based violence correlate with high maternal death rates, disabilities, the spread of HIV and sexually transmitted diseases, poverty, undernutrition, and low school-attendance rates.

Among the 2030 Sustainable Development Goals, the fifth, to “achieve gender equality and empower all women and girls,” is particularly important. To end gender-based violence across Africa and create the Africa4Her we all envision requires a focus on the household to help families unlearn those practices, beliefs, and behaviors that give abusers the power to abuse. It also requires extensive and comprehensive coordination of social support services for individuals who have experienced childhood trauma. Now is the time for YALI Fellows and people across Africa to contribute to these ongoing efforts to end violence against women and girls.

Africa4Her benefits everyone because when women and girls are educated and healthy, with access to opportunities, everyone benefits: families are happier and healthier, communities are safe and strengthened, national economies grow exponentially, and the global landscape shifts to achieve a balanced future.

One of my favorite books on gender-based violence is Half The Sky: Turning Oppression into Opportunity for Women Worldwide by New York Times journalist Nicholas Kristoff and his wife, Sheryl WuDunn. I recommend this book because it provides in-depth encounters on the daily acts of violence that women and girls face and offers successful and evidence-based solutions to reverse this violence, underlining the need for multisector, grassroots initiatives to shift norms in societies where gender-based violence persists.

It’s possible to end gender-based violence, and I encourage YALI Network members and others to take active leadership roles, starting with those closest to them: their families and communities.

The views and opinions expressed here belong to the author and do not necessarily reflect those of the YALI Network or the U.S. government. YALI Voices is a series of podcasts, videos and blogs contributed by members of the YALI Network.

Source : Yali
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images