Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INERNTIONAL) ya mwaka 2018 kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA,  Emilia Monjowa Lifaka, baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka (wa pili kushoto) baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Babati Vijijni, Vrajilal Jitu Son na wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum na Mwakilishi wa CPA tawi la Tanzania, Maria Kangoye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha mandhari ya jiji la Dodoma, Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MRADI WA BORESHA HABARI WAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI REDIO NURU FM IRINGA

$
0
0
Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 
Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo akiwaeleza waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 
Baadhi ya waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa wakimsikiliza mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru fm 93.5 mkoani Iringa wametakiwa kujikita kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ndani ya jamii, ambayo yamekuwa yakifichika na kutopaziwa sauti, jambo ambalo litawasaidia wananchi kutatulia kero ambazo zimekuwa zikiwakabili sababu ya kukosa sehemu pa kuzisemea.

Hayo yamebainishwa na mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru Fm Iringa juu ya kusaidia kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, hususani wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. 

Alisema waandishi wa habari wanamsaada mkubwa sana ndani ya jamii kwa kupaza sauti za wanyonge kupitia kalamu zao, kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi, na hasa kwa kuandika habari za uchunguzi ili jamii ipate kutatuliwa kero zao.

“Naombeni waandishi wa habari mjikite zaidi kuandika habari za uchunguzi kwa kuibua matatizo ambayo yamekuwa yakijificha ndani ya jamii, hususani kwa wale wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini, ambao wamekuwa wakikosa wa kuwapazia sauti na kuendelea kuishi maisha ya shida,”Alisema Mahondo

Mahondo alisema kuwa waandishi wa habari mkijikita kwenye habari hizi mtakuwa mnaisaidia jamii ya wananchi wale wale wanyonge kwa kuwa tayari mtakuwa ninyi ndio sauti yao kwa kipindi chote ambacho mtakuwa mnaandika habari hiz.

“Kuandika habari hizi zinanafasisi kubwa wa kuzifanya kwa kuangalia changamoto na manufaa katika sekta ya Afya,sekta elimu,sekta ya miundombi,sekta ya kilimo na mazingira na utapata uwanda mpana sana wa kufanya habari zenye tija kwa jamii” alisema Mahondo 

Aidha Mahondo alisema,licha ya jamii kuhitaji kupata habari za kiburudani ambazo zimekuwa zikiwaburudisha kwa muda mfupi tu lakini kubwa zile habari ambazo zinasaidia kutatua changamoto za wananchi ndio zinatija hasa kwenye jamii kwa kufanikisha kutatua matatizo yao.

“Hakuna wananchi ambaye hapendi kupata burudani hivyo tunaangalia aina gani ya burudani ambayo inawapa zaidi furaha jamii kwa kipindi kirefu ambayo itawasaidia kufanya shughuli za kimaendeleo ambazo zitawaletea faida wananchi” alisema Mahondo

Naye mwaandishi wa habari na mtangazaji wa kipindi cha Sunrise Power cha Nuru fm Godfrey Mengele aliwatupia lawama wananchi hususani wa maeneo ya vijijini, ambapo wamekuwa waoga kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kwa kushindwa kuzungumza matatizo yanayowakabili.

alisema kuwa waandishi wa habari hawezi kuchunguza habari bila ya kupewa taarifa (Tipu) juu ya tatizo linalo wakabili wananchi, pamoja na kutozungumza na wahusika waliofanyiwa matukio hayo ya ukatili ama ndugu, ambapo wananchi hao hua hawapo tayari kuzungumza na kuwakimbia waandishi.

Mengele aliwataka wananchi kuachana na tabia za uoga pale wanapotaka kusemewa matatizo yanayo wakabili kupitia vyombo vya habari, bali wawe karibu na media ambazo ndio msaada mkubwa kwao.

“Wananchi wamekuwa waoga sana kutupa habari ambazo zinawagusa wao kwa kuhofia kufikishwa polisi,kwenye ofisi za serikali za mitaa hata mahakamani kutoa ushaidi ndio maana waandishi tunapata wakati mgumu pia kuandika habari hizi” alisema Mengele

Lakini alitoa rai kwa waandishi wa habari kujikita kuandika habari za kichunguzi ambazo ndio zimekuwa zikiibua matatizo ya wananchi na kutafutia ufumbuzi wa kutatua changamoto zao.Kwa upande wake mtangazaji wa kipindi Street Bamiza Roger Magoha alisema mafunzo aliyopata yatamsaidia kukuza vipaji halisi vya wasanii wanaopenda kutoa burudani na kujua aina gani ya burudani wasikilizaji wanapenda kusikiliza.

“Sasa nitafanya uchunguzi kujua wasikilizaji wangu wanapenda aina gani ya burudani kwa kuwa nimeshapata mbinu za kufanya uchuzi huo kutoka kwa mkufunzi wa Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo” alisema Magoha

Magoha aliongeza kwa kusema kuwa amejifunza kufanya mahojiano bora na wasanii mbalimbali pamoja na viongozi hivyo mafunzo hayo yamemwogezea kitu kipya kichwani mwake ambacho hapo awali hakuwa nacho.

Tarehe 17 Januari 2018, Serikali ya Marekani kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ilizindua mradi wa kuimarisha asasi za kiraia na vyombo vya habari uitwao Boresha Habari Katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mradi huo ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360, mradi wa Boresha Habari utashirikiana na wabia wa Kitanzania, ikiwa ni pamoja na: Baraza la Habari Tanzania, Tanzania Bora Initiative, na Jamii Media; ili kuboresha weledi miongoni mwa waandishi wa habari na kusaidia kuweka mazingira yaliyo wazi kwa vyombo vya habari. 

“Serikali ya Marekani imedhamiria kwa dhati kusaidia kuinua ujuzi na weledi wa vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali za Kitanzania hususan katika kuwawezesha wanawake na vijana kupaza sauti zao na kueleza dukuduku zao kwa ufanisi,” 

Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, mradi wa Boresha Habari unalenga kufanya kazi na wadau wa vyombo vya habari katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mwanza na Kigoma. 

Aidha, mradi wa Boresha Habari utatoa mafunzo na msaada wa kitaalamu kwa vyombo vya habari vya humu nchini ukivisaidia kuanza kutumia teknolojia za kidijitali na kuimarisha uwezo wao wa kiusimamizi na kifedha. 

Hali kadhalika, mradi huu utatoa mafunzo kwa asasi za kiraia ili ziweze kushirikiana vyema na vyombo vya habari katika kusukuma mbele jitihada zao. Kwa kuzingatia umuhimu wa redio za jamii kama vyanzo maarufu vya habari za maeneo husika, mradi wa Boresha Habari utafanya kazi na vituo mbalimbali vya redio nchini kote ili kuboresha uwezo wao wa kitaalamu na uendelevu katika masuala ya kifedha.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov.

NHIF Yachangia Mageuzi Sekta ya Afya Nchini

$
0
0
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Umetajwa  kuchochea   mageuzi  katika ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya hapa nchini hali ilichangia kupungua kwa idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kupata matibabu.
Akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF  Bw. Benard Konga amesema kuwa uwekezaji  mkubwa umefanywa na mfuko huo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI),  KCMC, Bugando na Hospitali za Kanda kwa kuchangia kuimarisha huduma za kibingwa na miundombinu kama majengo.
Aliongeza kuwa matibabu ya kibingwa kama ya upandikizaji figo yanafanyika hapa nchini  kwa sasa kutokana na juhudi za  kuimarisha huduma za afya zinazofanywa na Serikali kupitia NHIF.
“ Vituo zaidi ya 7000 vimesajiliwa kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF kote nchini ambapo mafao mbalimbali yameanzishwa ikiwemo linalowawezesha wakulima kupata huduma hizi kupitia vyama vyao vya ushirika na tumenza na wale walio katika uzalishaji wa mazao ya kimkakati kama pamba, kahawa, korosho, chikichi na alizeti,” alisisitiza Konga
Akifafanua, amesema kuwa moja ya mikakati ya NHIF kusogeza huduma kwa wananchi imekuwa kutekeleza programu ya kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni ambayo ina upungufu wa wataalamu hao ambapo wagonjwa 21,375 wamehudumiwa kupitia utaratibu huu na kati yao 1,020 wakifanyiwa upasuaji wa aina mbalimbali.
Aliongeza kuwa mfuko huo kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Ujerumani (KfW) inatekeleza mpango wa tumaini la mama katika mikoa ya Tanga, Lindi, Mtwara, Mbeya  na Songwe ili kusaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga.
“Hadi Juni 2018 vituo takribani 330 vimeshaomba na kuidhinishiwa mikopo ya vifaa tiba kama MRI, CT SCAN ambapo mikopo hiyo imeshaidhinishwa na kuchangia katika kuleta mageuzi sekta ya afya hapa nchini kutokana na kuimarika kwa huduma za afya kwa wananchi,” alisisitiza Konga
Aidha, Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kujenga uchumi wa Viwanda, NHIF  kwa kushirikiana na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na wadau mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mkoa wa Simiyu inatekeleza uwekezaji wa ujenzi wa kiwanda kitakachozalisha bidhaa mbalimbali za hospitali zitokanazo na malighafi pamba.
Watanzania asilimia 32 wananufaika na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kati ya hao asilimia 25 ni wale wanaonufaika kupata matibabu kupitia Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF)  ambapo mpango ni kufikia asilimia 50 ya Watanzania ifikapo mwaka 2020.
Mfuko wa Taifa  wa Bima ya Afya umejidhatiti kuendelea kuchangia katika kuboresha huduma za afya hapa nchini na kusaidia kuchangia katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi ili waweze kushiriki katika ujenzi wa Taifa na uchumi wa viwanda.

TASWA YAKAMILISHA HATUA MUHIMU KUHUSU MAREKEBISHO YA KATIBA

$
0
0
KAMATI ya Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) imekamilisha hatua zote muhimu kuhusu marekebisho ya katiba hiyo na sasa imeitisha mkutano wa wadau wote Aprili 12 mwaka huu kwa ajili ya kuijadili na kuipitisha rasimu hiyo.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Kamati ya Katiba ya TASWA inaamini mkutano huo utakuwa na tija katika kuboresha rasimu hiyo ili taratibu zingine ziendelee ikiwa ni pamoja na kupanga tarehe ya uchaguzi wa TASWA.

Kwa vile Kamati imekamilisha jukumu ililopewa la kuandaa rasimu hiyo, hivyo kilichobaki ni ushirikiano kutoa kwa wadau ili kumaliza jambo hilo.

Pamoja na mambo mengine rasimu hiyo imeandaliwa kwa kuangalia Katiba za vyama mbalimbali duniani vinavyohusiana na waandishi wa habari za michezo na pia kupitia muongozo kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), ambacho TASWA ni mwanachama.

Pia Kamati imechambua Katiba ya sasa ya TASWA na kupokea maoni kutoka kwa waandishi wa habari za michezo kuhusu maeneo yenye upungufu kwa nia ya kuiboresha.

Maeneo mbalimbali yamefanyiwa kazi katika rasimu hiyo baadhi yakiwa ni sifa ya mwanachama, wajibu wa mwanachama, muundo wa uongozi, sifa za viongozi na pia ukomo wa uongozi. Pia kuna mapendekezo katika rasimu hiyo ya kuanzishwa kamati mbalimbali kwa nia ya kuisaidia Kamati ya Utendaji.

Kamati ya Katiba ya TASWA imeundwa kutokana na agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyeitaka BMT isitishe uchaguzi wa TASWA uliokuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana na badala yake BMT ikutane na viongozi wa TASWA pamoja na baadhi ya wanahabari wa michezo kuona namna ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TASWA iendane na wakati.

Kamati ya Katiba inayoongozwa na Mwenyeketi wa zamani wa TASWA, Boniface Wambura ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), viongozi wengine ni Katibu wa Kamati Amir Mhando ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TASWA na mwanahabari, Gift Macha ambaye ni Katibu Msaidizi wa Kamati.

Wajumbe ni Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Abdul Mohammed, Mhazini wa zamani wa TASWA, Nasongelya Kilyinga na wanahabari Thabit Zacharia na Devotha Kihwelu.

Nawasilisha,
Amir Mhando

Katibu wa Kamati ya Katiba/ Katibu Mkuu TASWA

5/04/2019

MAREKEBISHO YA SHERIA VYAMA VYA SIASA YA MWAKA 2019 YAANZA KUTUMIKA.

Waziri Biteko akutana na kufanya mazungumzo na Wadau mbalimbali wa Madini

$
0
0
Na Issa Mtuwa, Dodoma
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na makundi mbalimbali ya wadau wa madini    Aprili 3, 2019, Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Miongoni mwa aliokutana nao ni pamoja na Kampuni ya MAGAL Security System inayojihusisha na ufungaji wa mitambo ya usalama (security system) katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya migodini.
Mkurugenzi wa Biashara na Uendelezaji wa Masoko wa kampuni hiyo, Michael Gur Arie, amemweleza Waziri kuwa, kampuni yake inataka kufanya kazi na Wizara ya madini katika masuala ya ufungaji wa mitambo ya usalama kwenye migodi hususani Mirerani.
Amesema kuwa, kampuni hiyo ina uwezo wa kufunga mitambo Mirerani na wizara ikawa na uwezo wa kufuatilia kinacho fanyika kwenye eneo lote la mgodi huku shughuli nyingine za ofisi zikiendelea.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko ameishukuru kampuni ya MAGAL kwa kumtembelea na kuzungumza nae kuhusu suala la usalama hususani Mirerani. Amesema suala la usalama mirerani linapewa kipaumbele na uzito mkubwa katika kulinda raslimali hiyo ili iwanufaishe Watanzania wote.
Ameongeza kuwa, serikali imelipa kipaumbele suala la usalama katika eneo la Mirerani na Wizara imekuwa na mpango wa awamu mbili katika kutekeleza suala hilo. Amesema, Awamu ya kwanza ilikuwa ni kujenga ukuta kuzunguka eneo lote la migodi ya Mirerani na kufunga kamera na awamu ya pili inasubiri ushauri wa namna ya kutekeleza huku utekelezaaji wake ukitarajiwa kutafanyika baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia, waziri Biteko amekutana na Viongozi wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Nchini (FEMATA) wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo, John Bina.
Bina na ujumbe wake wamemtembelea Waziri Biteko kwa lengo la kukutana na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu shirikisho hilo ukizingatia kwamba, tangu ateuliwe kushika wadhifa huo hawajawahi kukutana na kufanya mazungumzo rasmi zaidi ya kukutana kwenye ziara mbalimbali.
Pamoja na mambo mengine, Bina amemweleza Waziri kuwa, Shirikisho lina laani vikali tukio la udanganyifu uliotokea hivi majuzi huko Chunya na kuongeza kwamba, FEMATA haikubaliana na udanganyifu unaofanywa na wachimbaji kwa kushirikiana na baadhi watendaji wa serikali waliopewa dhamana na kwamba halipo tayari kuwalinda wala kuwateteta.
Pia, Bina amezungumzia kuhusu Mgodi wa Buhemba uliofungwa na serikali akimuomba waziri kuufugua mgodi huo kwani  wanachi wengi walio katika eneo hilo wanategemea maisha yao  kutokana na uwepo wa mgodi huo.
Aidha, amemwomba Waziri maeneo mbalimbali yanayochukuliwa na serikali, afikirie kuwapatia wawekezaji wazawa ili wayaendeleze kwa  shughuli za uchimbaji. Bina ameongeza kuwa, FEMATA ina mpango wa kuanzisha Benki ya Wachimbaji (Miners Bank) kwa ajili ya kuwahudumia wachimbaji nchini.
Kwa upande wake, Waziri Biteko amemshukuru Rais wa FEMATA na ujumbe wake kwa kumtembelea. Amesema FEMATA na Wizara ya Madini huwezi kutenganisha kwa kupiga mstari kwa kuwa watu wa FEMATA ndio wadau wa wizara na kwamba hawajawahi kutofautiana na  kuomba ushirikiano huo uendelee.
Vilevile, Biteko amewashukuru FEMATA kwa kuunga mkono na kulaani kitendo cha udanganyifu uliofanywa na wachimbaji kwa kushirikiana na watendaji wa wizara huko Chunya kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu uzalishaji wa madini.
Kuhusu kufunguliwa kwa mgodi wa Buhemba, Biteko amesema Wizara ina thamini maisha ya watu kuliko shuguli za uchimbaji na kuongeza kwamba hivi sasa kuna timu ya wataalamu ambao wamekwenda  Buhemba kufuatilia utekelezaji wa  waliyokubaliana katika kikao cha tarehe  6 Machi, 2019, na ripoti  hiyo inategemewa kuwa mwongozo wa iwapo mgodi huo ufunguliwe au ufungwe.
Akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa Benki ya Wachimbaji amesema ni jambo zuri na kushauri kuanza na SACCOS ili kupima imani ya uaminifu wa wanchama wake katika kurejesha amana watakazo kuwa wanakopa.
Waziri Biteko amewahakikishia FEMATA kuwa wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yake.
 Waziri Doto Biteko akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa Michael Gur Arie, Mkurugenzi wa Biashara na Uendelezaji wa Masoko  wa Kampuni ya MAGUL Security System wa kwanza kushoto kwa Waziri alie ambatana na Idan   Segev wa kwanza kulia walipo mtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma kwa mazungumzo.
 Waziri Doto Biteko katikati akiwa katika picha ya pamoja na Michael Gur Arie, Mkurugenzi wa Biashara na Uendelezaji wa Masoko  wa Kampuni ya MAGUL Security System kulia na kushoto ni Idan   Segev  afisa masuala ya Biashara na Mauzo wa kampuni hiyo.
 Waziri Doto Biteko akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Wachimbaji nchini (FEMATA), John Bina kulia wakati wa mazungumzo yao ofisini kwake Dodoma. Kushoto ni Mtendaji mkuu wa Shrikisho hilo amabe pia ni Kamishna wa Tume ya Madini Haroun Kinega.
 Waziri Doto Biteko akiongea na Viongozi wakuu wa Shirikisho la Wachimbaji nchini (FEMATA) wakati wa mazungumzo yao ofisini kwake Dodoma. Kulia  ni Rais wa Shirikisho hilo John Bina na kushoto ni Mtendaji mkuu wa Shrikisho amabe pia ni Kamishna wa Tume ya Madini Haroun Kinega.
Waziri Doto Biteko katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Wachimbaji nchini (FEMATA) walipo mtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma kwa mazungumzo. Kulia  kwake ni Rais wa Shirikisho hilo John Bina na kushoto ni Mtendaji mkuu wa Shrikisho hilo amabe pia ni Kamishna wa Tume ya Madini Haroun Kinega.

SPIKA WA BUNGE LA BURUNDI AKUTANA NA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA

$
0
0
 Rais wa Seneti ya Burundi, Reverin Ndikuriyo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mussa Zungu.
 Rais wa Seneti ya Burundi, Reverin Ndikuriyo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mussa Zungu.
 Rais wa Seneti ya Burundi, Reverin Ndikuriyo akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu wakati Rais huyo pamoja na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mussa Zungu.
 Rais wa Seneti ya Burundi, Reverin Ndikuriyo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mussa Zungu.
Rais wa Seneti ya Burundi, Reverin Ndikuriyo akiagana na Mbunge wa Bunge, Charles Tizeba wakati Rais huyo pamoja na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Tanzania na kukutana na kamati Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. PICHA NA OFISI YA BUNGE

AGAPE YAFADHILI WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI KUSOMA CHUO CHA VETA.. DAS AKABIDHI BAISKELI 10

$
0
0
Shirika la Agape AIDS Control Programme limetoa msaada wa baiskeli kwa Watoto Wafanyakazi 10 wa nyumbani katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwafadhili kusoma fani mbalimbali katika Chuo Cha Ufundi Stadi – VETA mkoa wa Shinyanga. 

Baiskeli hizo 10 zilizotolewa na Shirika la Agape kupitia Mtandao wa Kusaidia Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani (Tanzania Child Domestic Workers Coalition – TCDWC) zitasaidia kuwarahisishia usafiri watoto hao kutoka nyumbani kwa waajiri wao hadi chuoni. 

Akizungumza leo Ijumaa Aprili 5,2019 wakati wa kukabidhi baiskeli hizo mbele ya Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi,Mkurugenzi wa shirika la Agape John Myola alisema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji. 

“Pamoja na kuwapatia baiskeli hizi zenye thamani ya shilingi 110,000/= kila moja,pia tumeshawalipia gharama zote za masomo ya Kozi mwaka mmoja katika fani za udereva,ushonaji,saluni na umeme katika chuo cha VETA kiasi cha shilingi Milioni 1.1 kila mmoja”,alieleza Myola. 

“Agape inapenda kila mtoto hasa watoto wa kike anapata haki ya elimu,tumeona ni vyema kuwapa ujuzi wa kujiendeleza kwenye maisha yao,tunaomba waajiri wawape muda watoto hawa wasome”,aliongeza Myola. 

Kwa upande wake,mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi baiskeli hizo,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi alilipongeza shirika la Agape kwa kuendelea kuwa wadau muhimu katika kuwaletea maendeleo wananchi kwani wamekuwa wakiunga kwa vitendo jitihada za serikali katika kuwasaidia wananchi. 

“Agape mmekuwa mfano bora,mnajipambanua kwa vitendo kusaidiana na serikali kuwaletea maendeleo wananchi,naomba ‘NGO’s/mashirika mengine pia yafanye kazi za kuonekana badala ya kujinufaisha wenyewe”,alisema Chambi. Aidha aliwaasa vijana hao kutunza baiskeli hizo na kuzingatia masomo yao huku akiwataka waajiri kuwapenda wafanyakazi wao wa ndani kwani ni watu muhimu kwa ustawi wa familia hivyo wawape nafasi ya kusoma na kutowanyanyasa. 

Naye Msimamizi wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa shirika la Agape, Joyce John alisema lengo la mradi huo ni kuhakikisha mtoto mfanyakazi nyumbani anawezeshwa kijamii na kiuchumi ili aweze kujikwamua kimaisha. 

“Mradi huu wa miaka mitatu (2016-2019) umejikita katika eneo la kuwapatia mafunzo ya ufundi na idadi ya watoto tuliowafikia hadi sasa ni 75,wengi wao tumewapatia elimu ya ushonaji,ujasiriamali na vitendea kazi ikiwemo cherehani”,alisema John. 

Kwa upande wao, watoto waliopata baiskeli na kufadhiliwa kusoma katika chuo cha Veta walilishukuru shirika la Agape na kuahidi kusoma kwa bidii ili kujikwamua kielimu,kijamii na kiuchumi.
Mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi baiskeli hizo,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza kabla ya kukabidhi baiskeli 10 kwa watoto wafanyakazi 10 wa nyumbani waliofadhiliwa na shirika la Agape kusoma fani mbalimbali katika chuo cha VETA - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape John Myola akielezea namna shirika hilo linavyounga mkono serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea maendeleo wananchi.Kulia ni Msimamizi wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa shirika la Agape, Joyce John,kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi.
Watoto wafanyakazi majumbani wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape John Myola.
Baadhi ya Waajiri wa Watoto wafanyakazi majumbani waliokubali watoto wao wafadhiliwe na shirika la Agape John Myola kupata elimu ya fani mbalimbali katika chuo cha VETA.
Msimamizi wa mradi wa Kumlinda Mtoto Mfanyakazi wa Ndani Dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa shirika la Agape, Joyce John akitoa taarifa ya mradi huo huku akitaja changamoto iliyopo kuwa ni ukosefu wa elimu ya haki na wajibu wa watoto wafanyakazi wa nyumbani kwa waajiri na jamii kwa ujumla.
Baiskeli zilizotolewa na shirika la Agape kwa ajili ya watoto wafanyakazi wa nyumbani waliofadhiliwa na Agape kusoma katika chuo cha VETA.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akikabidhi baiskeli kwa mmoja wa watoto wafanyakazi wa nyumbani.
Zoezi la kukabidhi baiskeli likiendelea.
Mtoto akifurahia baiskeli huku akisindikizwa na mwajiri wake.
Mkurugenzi wa shirika la Agape,John Myola akishikana mkono na mtoto anayekwenda kusoma udereva katika chuo cha VETA.
Mfanyakazi wa nyumbani wa kiume akisindikizwa na mwajiri wake wa kike ) anayeshikana mkono na Mkurugenzi wa Agape,John Myola)akipokea baiskeli.
Watoto wakiwa na baiskeli zao.
Afisa Miradi wa Shirika la Agape, Mustapha Isabuda akiwashauri wazazi na walezi kuwapenda wafanyakazi wa nyumbani na kuepuka kuwanyanyasa kwani hakuna ajuaye kesho nani anaweza kuwa nani.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU SPIKA BUNGE LA CAMEROON BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0

 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INTERNATIONAL),  Emilia Monjowa Lifaka (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum na Mwakilishi wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania, Maria Kangoye
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa taarifa za shughuli Mbali mbali zilizofanywa kwa mwaka 2018 na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimpatia zawadi ya Shuka la Kimasai Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum na Mwakilishi wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania, Maria Kangoye, baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. (PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

Waziri Kabudi aongoza kumbukumbu za Wataalam wa Kichina waliokufa wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), akiweka shada la Ua kwenye mnara uliopo kwenye makaburi ya wataalam 70 kutoka China waliokufa wakati wa ujenzi wa Reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya utamaduni wa Wachina na kuwakumbuka wataalam hao yaliyofanyika kwenye eneo la makaburi walikozikwa wataalam hao lililopo Gongo la mboto, Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Msemaji wa Serikali Mhe. Dkt. Abbas, Kailua Kurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Caesar C. Waitara na viongozi mbalimbali wa serikali
Prof. Palamagamba Kabudi pamoja na Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakitoa heshima zao kwa kuinamisha vichwa kama ishara ya kuwakumbuka wataalam hao kutoka China. 
Prof. Palamagamba pamoja na Mhe. Wang Ke wakiweka maua katika moja ya kaburi la wataalam hao.
Bw. Caesar Waitara akiweka Ua katika moja ya kaburi la wataalam hao.
Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.), akihutubia katika hafla hiyo mara baada ya kumaliza zoezi la kuweka maua kwenye makaburi ya wataalam wa kichina waliokufa wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara. Katika Hotuba hiyo waziri Kabudi aliendelea kuusifu ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta mbalimbali ambapo Ujenzi wa reli ya Tazara ulipelekea kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali.


Aidha, alieleza kuwa kutoka na Ushirikiano ulipo Tanzania inatarajia kufungua ubalozi mdogo katika mji wa Guanzou pamoja na kuanzisha Safari ya Ndege za Shirika la Tanzania (ATCL) kuelekea moja kwa moja Guanzou ambapo utapelekea kuongeza watalii kutoka China kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini Tanzania.
Balozi Wang Ke naye akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba zilizo kuwa zikiendelea kutolewa na Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Wang Ke (hawapo pichani) 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya vifo vya wataalam hao.

Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza hafla hiyo.
Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi Wang Ke wakiwa katika picha ya pamoja na wageni engine waliohudhuria tulip hilo.

RAIS MAGUFULI: HATUNA MPANGO WA KUONGEZA MIKOA MPIYA

$
0
0
MAELEZO,DAR ES SALAAM

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo ya utawala ikiwemo kuanzisha mikoa mipya na badala yake imejipanga kuimarisha huduma na mahitaji ya miundombinu iliyopo ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru yenye urefu wa kilometa 193 leo (Ijumaa April 5, 2019), Rais Magufuli alisema Serikali imekusudia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, maji, elimu n.k katika maeneo waliopo.
Aliongeza kuwa katika awamu yake yake ya Uongozi, suala la kuongeza maeneo ya utawala halipo na badala yake kuwataka Viongozi wa maeneo hayo wajipange katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya fedha zilizopo kwenda katika kujenga ofisi mpya za Wakuu wa Mikoa mipya na kuwalipa mishahara viongozi hao.
“Tumepanga kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wetu, tumechelewa kuleta Maendeleo hususani kwa wananchi wetu wa mikoa ya kusini, Serikali ninayoiongoza haina mpango wa kuanzisha mikoa mipya , badala yake pesa hizo tutazielekeza katika ununuzi wa madawa na kuboresha miundombinu ya barabara, elimu na nishati’ alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli alisema bado yapo baadhi ya maeneo mengi nchini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo barabara za lami, hivyo Serikali haitoweza kuleta Maendeleo katika sehemu moja kwa kuwa fedha hizo hazipo kwa kuwa ina na mahitaji makubwa katika kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa huduma muhimu na za msingi kwa Maendeleo ya wananchi zinapewa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati, kwa kuwa kukamilika kwake kutasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo katika miaka ya nyuma vimekuwa vikisababisha vifo vya makundi hayo ya kijamii.
Akizumgumzia kuhusu Sekta ya Maji, Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa kuwasimamia wakandarasi wa miradi ya maji nchini, kwani Serikali imekuwa ikitenga kiasi kikubwa cha cha fedha katika miradi ya Maendeleo pasipo na kupata matokeo yaliyotarajiwa, na hivyo kuisababishia hasara Serikali.
“Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Fedha na Mipango, miradi mingi ya maji imekuwa ikitumia fedha nyingi pasipo na kupata matokeo yoyote na wataalamu wetu hasa wakandarasi wamekuwa wazito kutoa tafsiri za nadharia za utaalamu na kuzileta katika nadharia halisi, na mataifa ya nje yanashangwa tunaposhindwa kuvitumia vyanzo tulivyonazo ili kuweza kuzalisha maji ya kutosha’ alisema Rais Magufuli.
Awali akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema kujengwa kwa barabara hiyo kutaimarisha mawasiliano katika ukanda wa kusini unaojumuisha Mtwara, Mingoyo, Masasi, Mangaka, Tunduru hadi Mbamba Bay na hivyo kuzidi kufungua fursa za kiuchumi nanchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Alisema hadi kukamilika kwake barabara hiyo imegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 173, ambapo Shirika la Misaada la Japan limetoa asilima 23.24, Benki ya Maendeleo ya Afrika asilimia63.32 na Serikali ya Tanzania asilimia 13.35 ikiwemo kodi na kulipa fidia kwa wananchi wanaostahili kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 2007.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania, Shinichi Goto alisema Serikali ya Japan imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara ya Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru na itaendelea kusaidia miradi mingine ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa umaskini kwa wananchi wake yanafikiwa.

MENEJIMENTI YA TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.

$
0
0
Na Estom Sanga-DSM 

Menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umekutana na Wadau wa Maendeleo kutoka mashirika ya kimataifa yanayochangia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko huo. 

Katika kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Mfuko huo jijini Dar es salaam,Wadau hao wa Maendeleo na Menejimenti ya TASAF wamepongeza hatua ya serikali ya kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja nchini kote . 

Wamesema utekelezaji wa Mpango huo umekuwa wa manufaa na mafanikio makubwa na hivyo kuvutia mataifa mengine kuja nchini kujifunza namna Serikali kupitia TASAF ilivyotekeleza mpango huo na kuzaa matunda katika kipindi kifupi tangu kuanza kutekelezwa. 

Aidha kikao kazi hicho kimeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini inakamilika kwa ufanisi na kufanya maandalizi thabiti ya awamu ya pili inayotarajiwa kuanza katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha. 

Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mkazo mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika awamu ya pili itakuwa ni kuwashirikisha walengwa wa Mpango kushiriki katika kazi kwenye miradi itakayoibuliwa kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ili kuinua kipato chao. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia hapa nchini Bwana Mohamed Muderis amesema kwa ujumla Benki ya Dunia na Washirika wengine wa Maendeleo wameridhishwa na namna Serikali ya Tanzania kupitia TASAF ilivyoonyesha dhamira ya dhati katika kutekeleza Mpango wa kunusuru Kaya maskini kwa lengo la kuboresha hali za maisha ya wananchi ambao wamekuwa wakiishi katika hali ya umaskini . 

Menejimenti ya TASAF na wadau wa maendeleo hukutana mara moja kila mwezi kufanya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa lengo la kuhakikisha kuwa utekelezaji huo unakuwa wa manufaa kwa Walengwa .

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bw. Ladislaus Mwamanga (mbele) akiongoza kikao kazi cha menejimenti na Wadau wa Maendeleo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia nchini Bw. Mohamed Muders (aliyesimama akizungumza kwenye kikao kazi kati ya menejimenti ya TASAF na Wadau wa Maendeleo) kushoto kwake ni mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga .

Baadhi ya Wadau wa maendeleo na menejimenti ta TASAF (picha ya juu na chini ) wakiwa katika kikao kazi kilichojadili utekelezaji wa shughuli za TASAF.




Sekta ya ‘Mauzo ya Moja kwa Moja’ kufafanuliwa – QNET

$
0
0
· Dhana potofu zilizosambaa kuhusu sekta ya mauzo ya moja kwa moja 

Biashara ya masoko ya mtandao inakuwa kwa kasi nchini na katika kanda hii kwa ujumla ambayo ni matokeo ya ongezeko la idadi ya watu na vijana wenye umahiri. Hata hivyo bado kuna dhana zisizo sahihi kwamba hii sio biashara halali. 

Dhana hii potofu inaendelea kuwepo licha ya kwamba biashara ya masoko ya mtandao ya kitaalamu ni sekta yenye thamani ya dola za kimarekani billioni 190 ikiwa na zaidi ya wasambazaji milioni 96 duniani kote. Kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ya QNET ni sehemu ya sekta hii ambayo imedhibitiwa na sheria, maadili na taratibu za utendaji zile zinazosimamia taasisi halali. 

Meneja Mkuu wa kanda wa QNET Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika wakati alipotembelea jijini Dar es salaam hivi karibuni, Biram Fall alikanusha dhana potofu kwa kusema kwamba kampuni ya QNET inaendesha biashara halali katika nchini nyingi na duniani kote na wanatoa bidhaa na huduma halisi. 

Bwana Fall alikuwa nchini wakati kampuni ilipoendesha maonesho ya Expo kuonyesha bidhaa na huduma kwa wateja, ambapo alibainisha kwamba wamekuwa wakiendesha shughuli biashara hii kwa zaidi ya miongo miwili na iwapo ingekuwa sio biashara halali haingeweza kudumu kwa muda mrefu kama hivyo. 

“Mifumo ya Piramidi huwa haidumu kwa muda mrefu kama ilivyodumu kampuni hii ambayo imekuwa inafanya kazi tangu 1998, matapeli kama hao huwa hawawezi kustahimili” alisema bwana Fall. 

Aliongeza zaidi kwamba kampuni hii ina nembo yenye sifa nzuri na inayojulikana duniani ambayo iko tayari kuilinda na hivyo haiwezi kujihusisha na utapeli wa aina yoyote. 

“Watu wabaya watakuwepo siku zote hapa na pale, hii ni changamoto. Lakini kwa suala la kanuni tunawahakikishia kuwa biashara katika QNET inaendeshwa kimaadili na kwa sababu hatuko hapa kuwadanganya watu ninawahakikishia kuwa QNET itaendelea kuwa hapa kwa muda mrefu” alisema bwana Fall. 

Tofauti kabisa na dhana hiyo kampuni ya QNET imekuja kuwawezesha watu, hasa vijana, alisema akiongeza kwamba kwa mujibu wa Tathmini ya Idadi ya Vijana Afrika iliyofanywa na Taasisi ya Maendeleo ya Afrika (African Institute for Development), kwa sasa Afrika ina zaidi ya asilimia 45% kati ya watu milioni 150 walioko Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda. 

Wengi wa vijana hawa wana elimu, wengi wana ufahamu wa teknolojia, wanauwezo wa kuendana na mifumo mipya kwa haraka, wanahamasa ya kuweka juhudi na wana fikra za ujasiriamali – sifa ambazo ni za msingi zinazohitajika kwaajili ya mafanikio endelevu katika biashara ya mauzo ya moja kwa moja. 

Biashara ya Masoko ya Mtandao au Mauzo ya Moja kwa moja ni dhana ya biashara ya kimataifa na inaelezewa kama ‘uuzaji wa bidhaa au huduma kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, mbali na maduka halisi ya kawaida.’ Mtindo huu wa mauzo una umri wa zaidi ya miaka 100 na ulianzishwa mwanzoni huko nchi USA. 

Leo, kuna takribani watu milioni 117 wanaohusika katika biashara hii. Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka ya Shirikisho la Vyama vya Mauzo ya Moja kwa Moja Duniani (World Federation of Direct Selling Association) (WFDSA) ya mwaka 2018, biashara ya mauzo ya moja kwa moja ilizalisha dola bilioni $190 za marekani na takribani nusu ya mauzo yote yametokea katika masoko yanayochipukia. 

Afrika imechangia chini ya asilimia 1% ya jumla ya mauzo ya WFDSA lakini wataalamu wanatabiri kwamba soko la Afrika Mashariki linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wenye ari na hata kwa wale wenye kazi za kudumu na wanania ya kujipatia kipato cha ziada kupitia mauzo ya moja kwa moja. 

Katika kanda ambayo matakwa ya ajira rasmi yanazidi kuwa na ushindani na kazi za kudumu kuendelea kuwa kidogo sana, biashara ya mauzo ya moja kwa moja inatoa njia mbadala wa ajira za kawaida kwa wale wanaohitaji kipato cha ziada kuongeza kipato kwaajili kwa mahitaji ya nyumbani, au kwa wale ambao mazingira hayawaruhusu kujipatia ajira rasmi. 

Wakati ambapo mtindo huu wa biashara inakabiliwa na changamoto, changamoto kubwa zaidi ni kuenea kwa mifumo isiyo halali ya piramidi ambayo inajiwasilisha kama kampuni halali ya biashara ya mauzo ya moja kwa moja, ambayo inawaahidi wawekezaji wanaotaka kuwekeza kuwa watapata faida kubwa iwapo watawaandikisha watu wengine. 

Hoja ni kwamba ‘matapeli’ hawa wanajenga dhana potofu kwenye sekta ya Mauzo ya moja kwa moja, jambo ambapo linaleta vikwazo kwa kampuni halali kusajili mawakala wa mauzo na kuendesha biashara zao halisi na halali. 

Matokeo yake, kampuni inatatua tatizo hilo kwa kuwaelimisha umma kuwa makini na ‘matapeli’ kama hao na kuwahamasisha kuthibitisha uhalali wa kampuni yoyote kulingana na inavyotekeleza na kutii kanuni, sheria na taratinbu zilizowekwa na bodi zinazosimamia na mamlaka zinazohusika. 

Katika kuimarisha uwepo wake nchini, kampuni ilifanya maonesho ya bidhaa jijini Dar es salaam ambayo yalibarikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Paul Makonda, ambaye aliwapa changamoto vijana wanaotafuta fursa kupitia katika kampuni hii kuwa na ujasiri wanapofanyia kazi ndoto zao ili waweze kuwa na mafanikio. 

Makonda alisema kwamba historia ya maisha yake binafsi ni ushahidi wa kutosha kwamba kufanyakazi kwa bidii na ujasiri hatimae huleta mafanikio na kuwaasa vijana wadogo kutokutosheka na mafanikio madogo. 

Alisema, “Historia ya maisha yangu ni ushahidi kwamba kwa kufanyakazi kwa bidii na kuwa na ujasiri kila wakati unaweza kupata mafanikio unayoyatafuta. Usiridhike kwa mafanikio au vitu vidogo vidogo kuliko ndoto zako”. 

Maonyesho ya bidhaa ya Expo yaliyobeba jina la Kuishi Kikamilifi ‘Absolute Living’ inayoendana na falsafa ya msingi ya kampuni , maonyesho haya huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi tofauti duniani kote kwa lengo la kuonyesha bidhaa na huduma zake zinazotolewa sokoni. 

Pia inakuwa kama jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kuelewa kuhusu kampuni na mtindo wake wa biashara. Dhana hii ni taswira ya juhudi za kampuni kuhamashisha mwenendo wa kiafya, na mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, kwa kutilia mkazo katika afya, ustawi na Elimu. 

“Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao, (online course) mpaka katika kozi za vifurushi vya sikukuu, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu, vyakula vya nyongeza na saa, tuna aina nyingi mbalimbali zinazoweza kutuwezesha kutoa huduma kwa mahitaji mbalimbali. Katika msingi wa yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya ‘kuishi kikamilifu”, alisema bwana Fall. 

Kampuni pia inatoa fursa za biashara kwa gharama nafuu kwa watu wanaotaka kuifanya, bila kujali kiwango chao cha elimu. 

“Tanzania ni moja kati ya masoko yetu ya kitaalamu katika QNET na kwa kuwezesha kufanyika kwa onyesho la Expo jijini Dar es salaam ni njia ya kurudisha kwa viongozi wetu hapa na kuwa karibu zaidi nao.“ aliongeza. 

Kama taasisi kampuni inaamini kwamba hakuna kinachompa nguvu zaidi mtu kama uhuru wa kifedha ambao unatokana na kufanyakazi katika sekta ya mauzo ya moja kwa moja na inaweza kuwa kazi ya kujitosheleza kwa wale watakaoamua kuifanya fursa hii muda wote au katika muda wa ziada. 

Tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo zinahitaji mtaji mkubwa wa kuanzisha, rasilimali na hata uzoefu, Biashara ya Mauzo ya Moja kwa moja inatoa biashara hii kwa gharama nafuu kwa kila mmoja anayeta kuanza kuifanya bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu. 

Manufaa makubwa ya biashara ya moja kwa moja katika masoko yanayochipukia kama Afrika Mashariki ni kwamba mtindo huu wa biashara una athari kubwa zaidi kuliko katika masoko yaliyoendelea kwa sababu ya athari za kifedha inayoweza kuleta kwenye maisha ya watu, kutoa fursa za ujasiriamali kwa wote, bila kujali sifa au uzoefu, hatimae kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wawakilishi, wafanyakazi na waalikwa wa QNET kuhusu maadili ya kazi kwenye uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za QNET jijini Dar Es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda (katikati) na Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika Biram Fall (kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya bidhaa za QNET 2019 yaliyofanyika hivi karibuni . Kulia ni Mshauri wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.

MWILI WA ALIYEKUWA MTUMISHI WA NEC UMEAGWA LEO KWAKE KIBAHA

$
0
0
Na Idara ya Habari-NEC

Mwili wa aliyekuwa Mtumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwandishi wa Habari mkongwe Bwana CLARENCE SABAYA NANYARO umeagwa jijini Dar es salaam na nyumbani kwake Kongowe-Kibaha mkoani Pwani leo Ijumaa tarehe 05 April, 2019.

Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Kijiji cha Nkoamara Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho jumamosi April 06.

Ibada ya kumuaga Marehemu Clarence Sabaya Nanyaro aliyefariki dunia Siku ya Jumanne April 03, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu imefanyika mapema leo asubuhi katika kanisa la Kilutheri lililopo Hospitalini hapo na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanatasnia ya Habari.

Akiwasilisha salamu kwa niaba ya Uongozi na Wafanyakazi wa Tume Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile amemwelezea Marehemu kuwa alikuwa mfanyakazi aliyeitumikia taasisi yake kwa kujitoa kwa hali na mali pamoja na kujiwekea mipango kadhaa ya kuendeleza taasisi na Taifa kwa ujumla.

Nanyaro ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Habari katika Idara ya Habari ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia alikuwa akiendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu katika Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino kampass ya Dar es salaam.

Miongoni mwa taasisi alizofanya kazi wakati wa uhai wake ni pamoja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambako alifanya kazi hadi mauti yalipomkuta.

Marehemu Clarence Sabaya Nanyaro ambaye alizaliwa April 01 Mwaka 1969 huko katika Kijiji cha Nkoamara Wilayani Arumeru mkoa wa Arusha ameacha mke na watoto wanne (4).

NYUMBA ZA ASKARI POLISI 20 ZAJENGWA PWANI ILI KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MAKAZI UNAOWAKABILI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
ASKARI wa jeshi la polisi mkoani Pwani, wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa makazi ya kuishi, hali inayosababisha kushindwa kuwahi wakati wakihitajika haraka katika dharula za majukumu yao ya kikazi.

Kutokana na hali hiyo, kwasasa jeshi hilo linajenga nyumba 20 za makazi ya askari polisi hao,zitakazogharimu milioni 500 ili kukabiliana na hali hiyo.

Akizungumza wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa nyumba hizo zinapojengwa Kibaha Mjini, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alitaka ujenzi huo ,ukamilike ifikapo June 30 mwaka huu, kama amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama ,dkt. John Magufuli alivyoelekeza.

Alisema ,askari wanapaswa kulinda mali ya mwananchi na kulinda usalama wa raia hivyo wanatakiwa waishi kwenye mazingira yaliyo bora.

"Kanda maalum ya kipolisi Rufiji imepatiwa milioni 500, pamoja na jeshi la polisi Pwani milioni 500, jumla milioni 100, ambazo zimetolewa na serikali kuhakikisha kila mkoa askari wanajengewa makazi ya kuishi "

"Hivyo ni wajibu wa jamii, wenye viwanda kushirikiana na serikali na jeshi la polisi kujenga mazingira bora ya askari hawa waweze kutulinda kwa moyo na upend "alifafanua Ndikilo.

Awali akitoa taarifa fupi kwa mkuu wa mkoa huyo juu ya ujenzi unavyoendelea, kamanda wa polisi Pwani, Wankyo Nyigesa alibainisha, kutokana na ufinyu wa bajeti wamepewa milioni 500 na kwa wastani kila nyumba itagharimu milioni 25 mpaka kukamilika kwake.

Aliwashukuru wadau waliojitokeza kusaidia akiwemo Said Salim Bakhresa, jeshi la wananchi wa Tanzania kupitia kikosi cha usafirishaji (KJ 95) ambao waliwapatia lowbed kwa ajili ya kubeba buldoza kutoka bakhresa sugar company huko Bagamoyo.

Wengine ni Chila mkurugenzi wa Creative Intertraders ltd ambae ametoa mifuko 100 ya saruji na Twyford Ceramics (KEDA )ya Chalinze na wengine ambapo amewashukuru na kuomba wadau wengine waendelee kuwashika mkono.

Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa ambayo , Amiri Jeshi wa Majeshi dk. Magufuli akiwa anazindua nyumba za askari polisi mkoani Arusha ,april 7 mwaka 2018, alitoa maelekezo kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) kwamba atapatiwa fedha kwa ajili ya makazi ya askari ,ambapo mkoa huo umeanza utekelezaji baada ya kupokea fungu hilo.

WACHINA, WATANZANIA NA WAZAMBIA WAADHIMISHA MIAKA 45 YA TAZARA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi akihutubia katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, wakati wa zoezi la kuweka mashada ya maua iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019), katika makuburi ya mashujaa hao yaliyoko Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam, waliosimama kulia ni Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akiwa pamoja na  viongozi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi (kulia), akipata maelezo kuhusu Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa hao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa April 5, 2019), kushoto ni Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akiwa pamoja na  viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi (kulia) na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke (kushoto) wakiweka mashada ya maua katika moja ya makaburi ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hao iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019) Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akiweka maua kwatika  moja ya makaburi ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hao iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019) Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi (kulia) na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, wakiweka mashada ya maua katika mnara wa makaburi ya Mashujaa waliojenga Reli ya TAZARA, katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hao iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019) Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi (kulia) na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, wakitoa heshima mbele ya mnara wa makabuli ya Mashujaa waliojenga Reli ya TAZARA, katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hao iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019) Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi, akionyesha maneno aliyoyaandika kuhusu maadhimisho ya siku ya mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, katika siku ya kumbukizi iliyofanyika ijumaa hii katika makaburi ya mashujaa hao yaliyoko Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam, aliyesimama wa nne kushoto ni Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akiwa pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania.
 Mnara wa Makabuli ya Mahujaa waliojenga Reli ya TAZARA yaliyoko Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam, kama unavyoonekana kwenye picha.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda, bungeni jijini Dodoma, Aprili 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa viti maalum Vicky Kamata, bungeni jijini Dodoma, Aprili 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DEWJI AWASIHI MASHABIKI WA SIMBA KUSHANGILIA MWAZO MWISHO MECHI YA KESHO DHIDI YA TP MAZEMBE

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

MWENYEKITI wa klabu ya Simba Mohammed Dewji amewasihi mashabiki wa klabu hiyo kuwa  washangilie mwanzo mwisho siyo kushangilia mpaka wapate goli katika mechi inayotarajiwa kuchezwa kesho majira ya saa kumi jioni katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo klabu ya  Simba SC itaminyana na klabu ya TP Mazembe katika mchezo wa  robo Finali ya kuwania kombe la ubingwa barani Afrika. 

Dewji amezungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam  ambapo amewaomba sana mashabiki hao kuwa ikitokea bahati mbaya wamefungwa basi  waendelee kushabikia sio tu mpaka wakipata goli pia amewasihi  wabadilike kwenye hilo,  washangilie Simba  mwanzo hadi  dakika 90 za mpira zitakapomalizika. 

Hata hivyo Kufuatia mechi hiyo Mo amewawaomba mashabiki wa Simba na Watanzania kijitokeze kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ili wachezaji wapate nguvu na maroli ya kufanya vizuri. 
.
"Kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, moja unawaongezea nguvu wachezaji wetu na wao wanaona kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inawaogopesha wapinzani wetu" amesema Mo Dewji.

"Hapa hatushiriki tu, tunajiamini kwamba tunaweza na tunataka kwenda mbali zaidi ya hapa"amesema Mo. 

Ameongezea kwa kusema kuwa "Shabaha yetu sio tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu"amesema Dewji.

TAKUKURU MOROGORO YABAINI UPOTEVU WA BILIONI 2.5 KATIKA HALMASHAURI ZA MKOA HUO.

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro (TAKUKURU),imefanya uchunguzi wa mfumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Point of sale (POS) na kubaini baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kutokuwa Waaminifu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro, Janeth Machulya,amesema kufuatia kufanyika kwa uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya point of sale (pos) wamebaini baadhi ya Halmashauri mkoani Morogoro kuwa na watumishi wasio waadilifu,ambapo katika kipindi cha robo mwaka 2019 januari hadi machi jumla ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zimefuatiliwa na shilingi milioni 370.2 zikirejeshwa kutoka halmashauri nne za mkoani Morogoro.
 
Amesema Halmashauri zilizorejesha fedha hizo ni pamoja na Kilombero imerejesha milioni 355,950,600/= ikifuatiwa na Kilosa milioni 5,952,00/= huku Mvomero wakirejesha milioni 8,731,850/= na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ikirejesha milioni 5,000,000/=, jumla kwa Halmashauri zote nne zikiwa zimerejesha milioni 370,277,650 na kufanya kiasi cha bilioni 2.5 zilizofuatiliwa kupungua na kubaki bilioni 2.1 ambapo Takukuru Morogoro imeahidi kuzifuatilia na watakaoshindwa kurejesha fedha hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Kufuatia zoezi hilo takukuru morogoro imeanza kuchukua hatua kwa kuanzisha uchunguzi ambapo mpaka sasa jumla ya majalada 10 yamefunguliwa.

“Ningependa kuwakumbusha watumishi wa serikali waliopewa dhamana ya kukusanya mapato na mawakala wote wa Halmashauri za wilaya katika mkoa wa morogoro kuhakikisha kuwa wanawawasilisha benki kwa wakati fedha zote za makusanyo zilizobaki mikononi mwao na maafisa masuhuli kuacha kupanga matumizi ya fedha kabla utaratibu wa kuidhinishwa fedha hizo haujafanywa na mamlaka zinazohusika ” alisema Janeth Machulya.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Morogoro, Janeth Machulya akizungumza na Waandishi wa habari leo kuhusu
uchunguzi wa mfumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Point of sale (POS) na kubaini baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo kutokuwa Waaminifu.

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA CHUO CHA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI CHA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako kuzindua chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kuzindua chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya kuzindua chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
Sehemu ya Wananchi wa Namtumbo waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma. PICHA NA IKULU

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images