Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

DKT. KIJAJI: MZUNGUKO WA FEDHA KATIKA SOKO UKO IMARA

0
0
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa kwa sasa nchi haina tatizo la mzunguko mdogo wa fedha katika soko kutokana na hatua mbalimbali ilizozichukua kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuongeza ukwasi kwenye uchumi.

Hayo yameelezwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Momba Mhe. David Silinde (Chadema), aliyetaka kujua sababu za mzunguko mdogo wa fedha.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, katika kutatua changamoto ya kupungua kwa mzunguko wa fedha katika soko, Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichukua hatua  mbalimbali za kuongeza ukwasi kwenye uchumi ikiwemo kushusha riba ya Benki Kuu (discount rate) kutoka asilimia 16 kwa mwezi Machi, 2017 hadi asilimia 7, Agosti 2018.

“Benki Kuu ilipunguza kiwango cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na mabenki ya biashara(Statutory Minimum Reserve Requirement, (SMR)) kutoka asilimia 10 hadi asilimia 8 mwezi April 2017 pamoja na kuruhusu mabenki kutumia asilimia 10.0 ya sehemu ya SMR kama chanzo kimojawapo cha kusaidia hali ya ukwasi kwenye uchumi”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema Benki Kuu ilianzisha utaratibu wa kutoa mikopo ya muda maalumu kwa mabenki pamoja na kununua fedha za kigeni kutoka kwenye soko la jumla la mabenki ili kuongeza ukwasi kwenye uchumi.

Alifafanua kuwa mzunguko wa fedha katika uchumi unaendana na malengo pamoja na mahitaji halisi ya shughuli za kiuchumi zizopo kwa sasa.

Aidha, Dkt. Kijaji alisema Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania inatekeleza Sera ya Fedha inayolenga kusimamia mzunguko wa fedha unaoendana na mahitaji halisi ya uchumi kwa lengo la kudumisha utulivu wa mfumuko wa bei na hivyo kuweka mazingira mazuri ya ukuaji wa uchumi.

MAJALIWA AKUTANA NA SPIKA WA BUNGE LA MISRI DKT. ALI ABDEL AAL

0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge la Misri, Dkt. Ali Abdel Aal kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge la Misri, Dkt. Ali Abdel Aal, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AIRTEL WATOA NAFASI 100 ZA MASOMO

0
0
Airtel kupitia UFADHILI WA AIRTEL TUNAKUJALI tunatoa nafasi kwa vijana 100 kusoma masomo ya ufundi kutoka chuo ya VETA kupitia simu ya mkononi BURE. Masomo haya yatatolewa kwa njia ya simu ya mkononi kupitia VSOMO App inayopatikana Google Play Store Bure.

Mafunzo ya Vitendo yatatolewa katika vyuo vitatu vya VETA;
1.VETA KIPAWA- Dar es salaam
2.VETA Chang’ombe- Dar es salaam
3.VETA Dodoma- Dodoma

Masomo ya Ufundi yatolewayo ni;
1.Ufundi Umeme wa Majumbani
2.Ufundi Bomba
3.Urembo- Saluni za Kike
4.Upishi wa Vyakula na Kuhudumia Wateja (Catering Service)
5.Uokaji mikate na Vitafunwa

Kujisajili, Pakua Application ya VSOMO kupitia https://goo.gl/Dufimz , bonyeza kitufe cha AIRTEL TUNAKUJALI ili kujisajili.

Kwa maelezo Zaidi; 
Huduma Kwa Wateja: 0699 859 572/ 0699 859 573

Facebook Page: https://play.google.com/store/apps/details?id=com.vsomo&hl=en

Instagram Page: https://www.instagram.com/vsomo_veta/

Website: http://www.vetakipawa.ac.tz/kipvsomo.php

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA PETER MOLLEL BUNGENI

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wabunge wakifurahia katika mazungumzo na Peter Mollel maarufu kwa jina la Pierre Konki Liquid (katikati) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 3, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Mariamu Ditopile, Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima, Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KINYWAJI CHA VIMTO RASMI KUZALISHWA NCHINI NA KAMPUNI YA BAKHRESA

0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Said Salim bakhresa  imeingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Nichol PLC kwa ajili ya uzalishaji wa kinywaji cha Vimto.

Mwakilishi kutoka kampuni ya Nichol PLC, Robert Hammersley amesema ni matumaini kuwa makubaliano hayo yataongeza pato la taifa kupitia uzalishaji wa kinywaji hicho cha Vimto.

Pia ameeleza kuwa ni wakati wa kuburudika na kinywaji hicho kutokana na kuzalishwa hapa nchini kwa sasa.

"Kinywaji cha Vimto kinaburudisha na hakina madhara na kinaweza kutumiwa kwa  rika lolote ," alisema  Hammersley.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Bakhresa, Said Salim    amesema makubaliano hayo ni fursa kubwa kwa nchi pamoja na kampuni ambayo imepata ikiwa ni ishara tosha kwa ubora wa bidhaa unazingatiwa kwa hali ya juu.

Aidha, kinywaji cha vimto kinatambulika ulimwenguni kote kinachopatikana katika vionjo kama vile soda ,juisi na peremende .

"Kwa sasa kinywaji cha Vimto kitazalishwa hapa nchini na kuuzwa kwa bei nafuu ili kuwafikia wanywajwi wote," 

Hata hivyo salim ametoa rai kwa wazalishaji wote wa bidhaa mbalimbali kuboresha bidhaa zao ili waweze kupata mikataba na masoko ya nje ya nchi.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza  jambo wakati akiongoza Kikao cha 2 cha Mkutano wa 15 wa Bunge la 11 leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia mbele) akiteta jambo na Spika wa Bunge la Misri, Mhe. Dkt. Ali Abdel Aal Sayyed Ahmed (katikati mbele) katika jukwaa la Wageni wa Spika Bungeni Jijini Dodoma, Mhe. Dkt. Ali kalitembelea Bunge katika ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Kushoto mbele ni Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverin Ndikuriyo
Mhamasishaji Maarufu wa Timu ya Taifa Stars, Ndg. Peter Mollel alimaarufu kama Pierre Liquid akitambulishwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Spika wa Bunge, Mhe. Job ndugai (hayupo kwenye picha) aliemualika kama mgeni wake.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (mbele) akielezea ukaaji ndani ya Bunge kwa Spika wa Bunge la Misri, Mhe. Dkt. Ali Abdel Aal Sayyed Ahmed (kulia) na Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverin Ndikuriyo (wa pili kulia) pale ugeni kutoka nchi hizo ulipotembelea leo Bungeni Jijini Dodoma. Katika ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizo mbili na Tanzania. Wageni wengine ni maofisa kutoka Bunge la Misri, Burundi na Tanzania
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Spika wa Bunge la Misri, Mhe. Dkt. Ali Abdel Aal Sayyed Ahmed alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Katika ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Katikati ni Mkalimani Ndg. Alaa Salah Abdelwahed.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Misri, Mhe. Dkt. Ali Abdel Aal Sayyed Ahmed alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katika ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizi mbili   
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Misri ulioongozwa na Spika wa Bunge la Misri, Mhe. Dkt. Ali Abdel Aal Sayyed Ahmed (watatu kushoto) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Katika ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimpatia zawadi ya picha yenye Jengo la Bunge Spika wa Bunge la Misri, Mhe. Dkt. Ali Abdel Aal Sayyed Ahmed alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Katika ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Kulia ni Mkalimani Ndg. Alaa Salah Abdelwahed
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiongozana na Spika wa Bunge la Misri, Mhe. Dkt. Ali Abdel Aal Sayyed Ahmed (katikati) alieambatana na ugeni kutoka Bunge la Misri wakielekea katika Ukumbi wa Pius msekwa Kuhutubia Bunge tukio lililofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma, Wageni walikuja katika ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. 


Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge na Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wakiwa katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, wakifuatilia hotuba ya Spika Ndugai pale ugeni kutoka Bunge la Misri, Burundi na Cameroon ulipotembelea Bunge la Tanzania, Kwa ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizo na Tanzania.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Misri, Burundi na Cameroon pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge na Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge katika Ukumbi wa Pius Msekwa leo Bungeni Jijini Dodoma. Ugeni huo ulitembelea Bunge kwa ziara ya kuboresha mahusiano baina ya nchi hizo na Tanzania. (PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

VODACOM, TALA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUISABABISHIA HASARA SERIKALI

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi, Vodacom Tanzania, Hisham Hendi raia wa Misri , wafanyakazi wake wanne, raia wawili wa Kenya na wenzao,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi  ya uhujumu uchumi, likiwemo  shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya bilioni 5.2

Mkurugenzi huyo na wenzake wameunganishwa na washtakiwa Ahmed Issa ambaye ni Meneja uwendeshaji wa biashara wa kampuni ya Inventure Mob Tanzania Ltd, na raia wa Kenya,  Brian Lusiola ambaye ni mtaalami wa IT,  ambao walisomewa mashtaka sita wiki iliyopita.
  Mbali na Hend ambaye ni raia wa Misri, washitakiwa wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mapato wa Vodacom PLC, Joseph Nderitu ambaye ni raia wa Kenya, Mkurugenzi wa Sheria wa kampuni hiyo, Olaf Mumburi Mkazi wa Victoria Kinondoni.

Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa kampuni hiyo, Joseph Muhere, Meneja wa Uhasibu, Ibrahim Bonzo wa Kampuni ya Vodacom iliyopo Ursino Estate barabara ya Bagamoyo.

Akisoma hati ya mashtaka  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Jackline Nyantori amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kuwa, kati ya Januari 2018 na Machi 2019 huko katika jengo la Tanzanite Park, lililopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa Ngasa, Lusiola na kampuni ya Tala Tanzania waliongoza genge la uhalifu  na kuisababishia serikali kupitia TCRA, hasara ya Sh bilioni 5.8.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao hao  wanadaiwa, katika tarehe isiyofahamika kati ya Januari Mosi na Desemba 31, 2018, waliingiza kifaa cha mawasiliano kinachoitwa Proliant MLI GEN 9 Server (PABX Virtual Mashine yenye serial number 76520D88838129_425) bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Washtakiwa wanadaiwa pia kusimika kifaa hicho na kuendesha mtambo huo wa mawasiliano bila kuwa na leseni inayotolewa na TCRA.

Aidha  washtakiwa wanadaiwa, kutoka Januari 2 hadi  Machi 11,2019 waliendesha kifaa hicho cha kieletroniki cha mawasiliano kwa kuruhusu simu za kimataifa zilizoingia nchini bila kibali cha TCRA. Pia imedaiwa kati ya Aprili 17, mwaka jana na Machi 11, washtakiwa waliendesha mitambo hiyo kwa kupokea na kusambaza upokeaji wa simu za kimataifa bila kuwa na leseni hiyo.

Katika shtaka la tano, inadaiwa kati ya Aprili 17, mwaka jana na Machi 11, mwaka huu, washtakiwa walikwepa kodi ya kupokea na kusambaza huduma ya upokeaji wa simu za kimataifa kwa kusambaza mawasiliano kwa kutumia mfumo huo.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa Aprili 17, mwaka jana na Machi 11, mwaka huu kinyume na sheria, washtakiwa walitumia vifaa vya mawasiliano kuunganisha  huduma ya kieletroniki ya mawasiliano kwa lengo la kupokea na kusambaza mfumo wa mawasiliano bila kupata kibali cha TCRA.

Imeendelea kudaiwa kuwa, katika tarehe hizo, maeneo ya Tanzanite Park Building Kinondoni, Ngassa, Lusiola na Kampuni ya Tala, walitumia namba 813 za Vodacom ambazo ni namba maalum bila kupewa na TCRA.

Ngassa, Lusiola na Tala, pia wanadaiwa katika tarehe hizo, waliisababishia TCRA hasara ya Sh Milioni 642.2.

Katika shtaka la Tisa, Wakili Wankyo Simon amedai kuwa Hendi, Nderitu, Mumburi, Muhere, Bonzo na Kampuni ya Vodacom, kati ya Aprili 17, mwaka jana na Machi 11, mwaka huu maeneo ya jengo la Vodacom, lililopo Ursino Estate barabara ya Bagamoyo, Dar es Salaam, waliwaruhusu  Ngassa, Lusiola na Tala kutumia namba 813 za Vodacom bila kuzipata kutoka TCRA.

Pia Simon alidai washitakiwa hao kutoka Vodaom katika tarehe hizo, kwa pamoja waliisababishia serikali na TCRA hasara ya Sh 5,250,237,000.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mhakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ispokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi  Aprili 17, 2019 kwa kutajwa

YANGA INAENDELEA KUMKOSA AJIB MCHEZO WA KESHO DHIDI YA NDANDA FC

0
0
KIKOSI cha Yanga kinatarajia kushuka kesho kuwavaa Ndanda Fc katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona  ikiwa ni muendelezo wa mchezo ligi kuu soka Tanzania bara (TPL).

Yanga wataendelea kukosa huduma ya nahodha wao  Ibrahimu Ajib akisalia Dar es Salaam akiendelea kupata matibabu.

Imeripotiwa kuwa Nahonda wa kikosi cha Yanga Ibrahim Ajibu hajasafiri na na timu yake na hatakuwa katika sehemu ya  mchezoni siku hiyo, ikiwa ni mchezo wa pili mfululizo  kukosa kucheza, mwingine ambao aliukosa ni mechi ya  robo fainali kombe la FA dhidi ya Alliance fc kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mwishoni mwa wiki.

Aidha Afisa habari wa Yanga, Dismas Ten ameiambia Yanga Tv kuwa "Nahodha Ibrahim Ajib ataendelea kukosekana kikosini kutokana na majeraha hivyo hatakuwa katika sehemu ya mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Nangwanda sijaona ambapo kikosi chetu kitavaana na Ndanda Fc"

Hata hivyo mchezaji huyo amesema  kuwa  kukosekana kwake kikosini na kukosa mchezo wa pili mfululizo  kunatokana na maumivu ya nyonga ambayo yamekuwa yakimsumbua siku za hivi karibuni

Vilevile kufuatia sakata hilo la Ajib kutosafiri na timu yake  katika mechi hizo baadhi ya magazeti yameripoti kuwa Ajib tayari amemalizana na mabosi wa Simba ambao wamemtengea mkataba wa miaka miwili

kutokana na taarifa zinazotawala katika vyombo vya habari kuwa yuko mbioni kurejea Simba, Ajib amenukuliwa gazeti la mwanasport akisema "ukweli au uongo wa taarifa hizo utafahamika msimu ukimalizika mimi nina mkataba na klabu ya Yanga, nitaendelea kuitumikia timu yangu.”

Mchezaji huyo ameendelea kusema kuwa  "hizo taarifa za mimi kusajiliwa na Simba ukweli au uongo wake utafahamika mwishoni mwa msimu, Mimi ni mchezaji wa Yanga ni vyema nikaulizwa mambo yanayoihusu Yanga, hayo mengine tuwaachie wanaotumia kalamu zao kujinufaisha kwa kuuza magazeti lakini ifahamike mimi ni mchezaji wa Yanga"

Pia  hivi karibuni kaka yake Athumani Ajib ambaye ndiye wakala wake, alikanusha taarifa hizo huku akibainisha kuwa wamefanya mazungumzo ya mkataba mpya na Yanga lakini wamekubaliana ni vyema wakasubiri mpaka mwishoni mwa msimu ndio aweze kusaini mkataba mpya.

Tamko Kutoka TPSF kuunga mkono Kauli ya Mh. Rais JPM kuhusu kodi

0
0
TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION 


TAMKO LA KUMUUNGA MKONO MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA MSIMAMO WAKE THABITI NA MAELEKEZO KWA WIZARA YA FEDHA NA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA JUU YA UMUHIMU WA KUPANUA WIGO WA WALIPA KODI 

Kwa niaba ya Wadau wa Sekta Binafsi, Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Menejimenti, tunachukua fursa hii kwa mara nyingine tena kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumshukuru kwa Hotuba yake na Maagizo yake aliyoyatoa wakati akizungumza na Wizara ya Fedha na Mipango, Watendaji wa TRA na Taasisi zingine za Umma tarehe 1 Aprili 2019. Tumefarijika sana na juhudi zake binafsi za kuona umuhimu wa kuhakikisha kuwa Nchi yetu ina Mazingira Bora na ya Kuvutia Uwekezaji na Ufanyaji Biashara. 

Mheshimiwa Rais, amezitaja na kukemea Changamoto za Kodi kuwa ni kubwa na nyingi; utitiri wa taasisi za usimamizi na gharama zao ambazo zimekuwa zinatukwaza sana Sekta Binafsi kwa muda mrefu. Mzigo wa kodi ni mkubwa kwa wachache ambao wameandikishwa kwa sekta binafsi na hivyo maagizo yake kwamba zirekebishwe haraka yametupa faraja na hamasa ya kuongeza mchango wetu katika Uchumi wa Nchi Yetu tukielekea katika Uchumi wa kati na wa Viwanda. 

Sekta Binafsi tupo tayari kukaa na Serikali kupendekeza na kufikia muafaka wa njia mbalimbali za kupanua wigo wa walipa kodi, ili kwa pamoja, tufanyie kazi maagizo haya wa Mheshimiwa Rais. Sekta binafsi tutakutana ili kujadili na hatimaye kuwasilisha mapendekezo yetu kwa Mheshimiwa Rais kupitia Waziri wa Fedha na Mipango yatakayosaidia kuongeza wigo na kupunguza mzigo wa kodi kwa wadau. 


Katika kuratibu zoezi hili, TPSF na Sekta Binafsi katika ngazi zote kuanzia mawilayani na mikoani hadi Taifa tutashirikiana na Serikali na Taasisi za Sekta ya Umma ili kwa pamoja tujadiliane na kukubaliana hatua za haraka za kuchukuliwa kurekebisha mapungufu na changamoto alizoziainisha na kuzitolea maagizo Mheshimiwa Rais. Tuna uhakika kuwa tukitekeleza azma yake tutapanua wigo wa kulipa kodi na mapato ya Serikali na Uchumi wetu utaimarika na kuongezeka kwa kasi kubwa. 

Aidha, Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kumteua Naibu Katibu Mkuu (Sera) katika Wizara ya Fedha na Mipango. Sekta Binafsi tyumepokea uteuzi huu kwa mikono miwili na kuuona kama ni mwanzo mzuri wa kujengea uwezo wa Wizara katika kufanyia kazi masuala ya Sera, badala ya kutegemea TRA kama mshauri pekee. Tuna imani kwamba mtizamo wa Wizara ya Fedha na Mipango ni wa kukuza uchumi kupitia Sera ya Kodi lakini Mamlaka ya Mapato mtizamo wake ni wa kukusanya kodi hivyo basi kuna mgongano wa maslahi. Wizara pia itakuwa na uhuru wa kufanyia kazi masuala mtambuka. 

TPSF tunaungana na Mheshimiwa Rais kuhimiza na kuhamasisha Watanzania wote tulipe kodi kwa manufaa ya maendeleo yetu wenyewe. TPSF inamhakikishia Mheshimwa Rais kwamba tupo tayari kushirikiana na Serikali kupanua wigo wa walipa kodi pamoja na kushiriki kikamilifu katika Kamati za ushauri kuhusu masuala ya kodi, kama alivyoelekeza. Tuna uhakika kuwa kodi zikipunguzwa na taratibu za ulipaji zikiboreshwa na kufanywa rafiki zaidi, WaTanzania tutakuwa tayari kulipa kodi halali bila kushurutishwa au kutishwa. 

Tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali na Sekta nzima ya Umma kwa kuwa na majadiliano ya kudumu yenye nia ya kuboresha mazingira ya kuwekeza, kushindana ndani na nje ya nchi na kuhakikisha kuwa WaTanzania, wadau wa Sekta Binafsi, wananufaika kutokana na jitihada hizi na kukuza uchumi wao na Taifa Zima kwa Ujumla. 

Imetolewa na Salum Shamte 
Mwenyekiti - Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) 
April 3, 2019 

MAJALIWA AKUTANA NA RAIS WA SENETI YA BURUNDI, REVERIEN NDIKURIYO

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverien Ndikuriyo kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Aprili 3, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Seneti ya Burundi, Mhe. Reverien Ndikuriyo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi

0
0
Na. Paschal Dotto-MAELEZO

 Rais Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Nanyamba, Tandahimba, na Newala Mkoani Mtwara kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya uhakika ili kuunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi na wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuweza kujiletea maendeleo yao.

Akizungumza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, Rais Magufuli amesema Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Nanyamba yenye urefu wa kilometa 50 itakayogharimu kiasi cha Tsh.bilioni 86 na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe kutangaza zabuni ya ujenzi wa kilometa zingine na kufikia kilometa 100 na hivyo kuunganisha kwa urahisi nyanda za kiuchumi katika mikoa ya kusini.

“Barabara hii itakuwa ni kiunganishi cha uchumi mikoa ya kusini, hatuwezi kushindwa kujenga kilometa 100, lengo letu kuu ni kuiunganisha Bandari yetu ya Mtwara na mizigo inayotoa Malawi,” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema kuwa katika kuwainua wakulima wa Mkoa wa Mtwara, ambapo Serikali imetekeleza ununuzi wa korosho kutoka kwa wananchi wenye korosho zaidi ya kilo 1500, na Tsh Bilioni 50 tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao, na kwa upande wa wakulima wa korosho wenye kilo chini ya 1500 wamelipwa kiasi cha Tsh Bilioni 578.

Rais Magufuli amewahiza wafanyabiashara walanguzi wa zao la korosho ‘Kagomba’ kuacha kuwadhulumu wakulima wadogo kwa kuwapa bei ambayo hailidhishi huku wakijua wametumia gharama kubwa katika kuendeleza zao hilo, na kusema serikali ya Awamu ya tano haitarudi nyuma kuwatetea wakulima hao.

“Utakuta mtu amelima korosho zake, amenunua madawa, ametumia gharama kuzivuna unakuja kumpa bei ya 1500, kwa Serikali ya Awamu ya Tano hili halikubaliki”, alisema Rais Magufuli.

Akiongelea miradi mingine inayotekelezwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa ni pamoja na upanuzi wa bandari ya Mtwara, , upanuzi wa uwanja wa Ndege na ukarabari wa mradi wa maji wa makonde ambao utagharimu kiasi cha Tsh.bilioni 160 zikiwa ni fedha za mikopo kutoka Serikali ya India unaowezesha ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 nchini.

Watoa huduma msaada wa kisheria waaswa kutumia weledi wao wa Kazi

0
0
Na Woinde Shizza Globu ya jamii 

Watoa huduma za msaada wa kisheria nchini wametakiwa kutotumia nafasi yao ya kutoa msaada wa kisheria kufanya mambo kinyume na taaluma yao na maadili yao ya kikazi.

Hayo yamebainishwa Leo na Katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria prof  Sifuni Mchome wakati akiongea katika kongamano la Watoa huduma za msaada wa kisheria uliofanyika jijini Arusha ambapo alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha Watoa huduma hao kufuata maadili ya Kazi yao.

Alisema kuwa kwakuwa Watoa huduma wa msaada wa kisheria wanafanya Kazi kwa kujitolea hivyo ni wajibu wao kuzingatia maadili ,yanayoendana na Katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kulinda tamaduni njema za kitanzania.

"Napenda kusisitiza msitumie mlango wa usaidizi wa kisheria kutumika kama vibaraka " alisema mchome.

Kwa upande wake Waziri wa katiba na sheria Balozi dkt Augustine Mahiga aliwataka Watoa huduma hii ya kisheria kutumia kikamilifu makubaliano yaliowekwa na utekelezaji wake usibaki katika karatasi bali wayafanyie Kazi kikamilifu ili wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria waweze kufaidika nayo.

Aliongeza kuwa itakuwa haina maana kama sheria ,kanuni miongoni na makubaliano yaliopo hayata mnufaisha Mwananchi mhitaji wa huduma hii pia libainisha kuwa wakati pia serikali inaendelea kuimarisha mifumo ni vyema pia wahakikishe wanawafikia wananchi walio wanyonge katika maeneo yao.

Mahiga alisema kuwa serikali iko mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wananchi wanyonge wanathaminiwa nakupewa hadhi sawa na wengine ,na kwakutilia mkazo serikali imepitisha sheria ya msaada wa kisheria na itaendelea kuimarisha nifumo ya upatikanaji haki nchini ili huduma hii itolewekatika utaratibu na mfumo mzuri utakao wezesha kuwafikia wananchi kwa wakati na kwa ubora unaostaili.

Aidha aliwataka wasaidizi hawa wa kisheria kuendelea kusimamia misingi imara ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inayotambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kulinda tamaduni njema za kitanzania ambazo ndiyo tunu yetu tunayojivunia katika kulinda utu na heshima ya mtanzania .
 Waziri wa katiba na sheria Balozi Dkt  Augustine Mahiga akizungumza na  waandishi wa habari Mara baada ya kufungua kongamano
Msaili wa Watoa  huduma za msaada wa kisheria nchi bi.Felistas Mushi akizungumza na Waandishi mara baada ya ufunguzi.

RAIS DKT MAGUFULI KESHO KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI RUVUMA

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOWANYANYASA WATOTO

0
0



Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma. 

Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua watu wanaowanyanyasa watoto kwa kukiuka Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009. 

Hayo yamesemwa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Mgebi Jadi Kadika juu ya mikakati ya Serikali ya kuondoa tatizo la kuwakosesha watoto haki za msingi na malezi bora kwa kuwatumia katika kutoa huduma ya kubeba mizigo na kupewa ujira mdogo. 

“Huduma za ulinzi wa mtoto zinatekelezwa kupitia Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009. Katika kusimamia utekelezaji wa Sheria hiyo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ulioanza kutekelezwa kuanzia mwaka wa Fedha 2017/18 hadi 2021/22,” amesema Kandege. 

Ameendelea kusema, tathmini imebaini kuwa watoto wengi wanaojihusisha na kazi za kubeba mizigo masokoni ni matokeo ya umaskini uliokithiri kwa baadhi ya Kaya, kuondokewa na wazazi wao kwa maambukizi ya UKIMWI, migogoro ya ndoa na ukatili dhidi ya watoto. 

Amesema, mkakati unaotekelezwa na Serikali ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki za msingi za mtoto kupata elimu na malezi bora. Aidha, utoaji wa elimu msingi bila malipo umetoa fursa kwa watoto wengi wenye umri wa kwenda shule kuandikishwa kuanza elimu ya awali kupitia mfumo rasmi na mfumo usio rasmi. 

Aidha ametoa wito kwa wazazi kutimiza wajibu wao wa kuwalea, kuwatunza na kuwalinda watoto ambao ni Taifa la kesho kwa kutowatumikisha katika kazi ambazo haziendani na umri wao.

SERIKALI: WAZABUNI WATIA KIBINDONI SHILINGI BILIONI 199

0
0

Na Farida Ramadhani na Josephine Majura, WFM, Dodoma

Serikali imeleeza kuwa imeshawalipa Wazabuni 2048 kiasi cha Shilingi 199 tangu kutolewa kwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 3 Januari, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam la kutaka Wazabuni wote wanaoidai Serikali walipwe.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Ritta Kabati, aliyetaka kujua baada ya tamko la Mhe. Rais kuhusu Wazabuni wote wanaoidai Serikali walipwe ni Wazabuni wangapi wameshalipwa.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa kati ya Wazabuni 2048 waliolipwa na Serikali, Wazabuni 1,277 walihudumia Sekretarieti za Mikoa na 771 walihudumia Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali. Dkt. Kijaji alifafanua kuwa Shilingi 3,729,605,175 zimetumika kulipa Wazabuni waliotoa huduma kwa Sektretarieti za Mikoa na Shilingi 195,334,409,791.64 zimetumika kulipa Wazabuni wa Wizara, Taasisi na Wakala za Serikali.

“Ikumbukwe kuwa madeni yote haya yalilipwa baada ya uhakiki kufanyika”, alisisitiza Dkt. Kijaji. Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kulipa madai mbalibmali ya wazabuni kulingana na upatikanaji wa fedha, sambamba na uhakika wa madai husika. Dkt. Kijaji amesema kuwa ili kukamilisha zoezi la uhakiki kwa wakati, wazabuni wote wanatakiwa kutoa ushirkiano, hususan kuwasilisha taarifa na vielelezo sahihi vya madai yao pindi wanapotakiwa kufanya hivyo.

Katika swali la nyongeza Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Kabati alitaka kujua vigezo vilivyotumika kuwalipa wazabuni hao.

Akijibu swali hilo la nyongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa vipo vigezo vingi ambavyo Serikali imevitumia kulipa madeni hayo moja ikiwa umri wa deni, madeni ambayo yamekaa kwa muda mrefu na ambayo tayari yamehakikiwa ndiyo yanapewa kipaumbele katika malipo.

Aliongeza kuwa kigezo cha pili ni riba Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa madeni ambayo riba yake inakuwa kulingana na muda, ili Serikali isiendelee kuumia wala mwananchi asiendelee kuumia.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji

WATU WAWILI WANASWA NA JESHI LA POLISI MBEYA KWA KUHARIBU MIUNDOMBINU YA UMEME

0
0


KUHARIBU MIUNDOMBINU YA UMEME.

Mnamo tarehe 01.04.2019 saa 23:00 usiku huko Kitongoji cha Mwaisongoli, Kijiji cha Mpunguti, Kata ya Ikama, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliwakamata watu wawili waliofahamika kwa majina ya 1. ELIA CHARLES [24] na 2. AMIR OMAR [27] wote vibarua wa Kampuni ya Umeme wa REA – STEG International Service na wakazi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe kwa kuharibu miundombinu ya umeme.

Watuhumiwa walikamatwa wakiwa wanakata nyaya za umeme za kampuni ya REA – STEG International Service kwa kutumia plaizi kwa lengo la kwenda kuuza ili wajipatie fedha. Thamani halisi ya uharibifu huo bado kufahamika. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

MAUAJI – MBEYA MJINI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawasaka watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la AIDAN PAUL CHONGOLA [27] Mkazi wa Hayanga, Dereva Bodaboda.

Ni kwamba mnamo tarehe 03.04.2019 saa 02:00 usiku huko maeneo ya Ilomba, Jijini Mbeya, marehemu akiwa katika kituo chake cha kazi akiwa na Pikipiki yake yenye namba za usajili MC 557 BBT aina ya Kinglion rangi nyeusi alikodishwa na watu wawili wanaume wasiofahamika ili awapeleke Ituha lakini walipofika maeneo ya Ituha Relini watu hao walimchoma kitu chenye ncha kali upande wa kulia tumboni na kusababisha kifo chake na kasha kuondoka na Pikipiki hiyo.

Mwili wa marehemu ulikutwa kando kando ya reli ya Tazara, Mtaa wa Tonya April, 03, 2019 saa 07:00 asubuhi ukiwa na jeraha tumboni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu. Aidha msako mkali wa kuwatafuta waliohusika katika tukio hili kwa hatua zaidi za kisheria.

TBS YAHIMIZA WANAFUNZI KUWA MABALOZI – KILOMBERO

0
0
Bi. Neema Mtemvu, Afisa Uhusiano (TBS), akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibaoni wakati TBS ilipotembela shuleni hapo kutoa elimu juu bidhaa hafifu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwashungu, wakisikiliza elimu juu ya masuala yahusuyo viwango vya ubora, kutoka kwa maafisa Wa TBS.
Bi.Amina Yasin, Afisa Udhibiti ubora Mwandamizi (TBS), akizungumza na wajasiriamali wilayani kilombero kuhusiana na utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.
Bi Amina Yasin, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi(TBS) akizungumza na wananchi wa soko kuu la Ifakara, wilayani Kilombero, juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS.

……………………………..

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetembelea shule ya sekondari Kibaoni pamoja na Shule ya sekondari ya Kwashungu wakati wa Kampeni yake ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizo na ubora katika Wilaya ya Kilombero. 

Bi. Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS) akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu, amefafanua umuhimu wa viwango katika maisha yao ya kila siku vilevile kuwafahamisha fursa ya huduma bure kwa wajasiriamali wadogo.

Bi Gradness amesisitiza kuwa jukumu la kupiga vita bidhaa hafifu katika Taifa ni la kila mtu, hivyo aliwaasa wawe mabalozi wazuri wa kuhamasisha ubora katika jamii wanazoishi.

Kwa upande wake, Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaoni, Bw. Kalinga aliwapongeza TBS kwa kufika shuleni hapo kwani ni mkakati mzuri ukizingatia shule huwa na wanafunzi wengi na wanaoishi maeneo mbalimbali hivyo ikiwa kila mmoja atasambaza ujumbe huo kwa ndugu jamaa na marafiki utakuwa umewafikia watu wengi kwa muda mfupi. Mwalimu Kalinga pia hakuacha kutoa wito kwa TBS kuendelea na zoezi hilo kwani linajenga msingi mzuri kwa vizazi vijavyo na kutengeneza jamii yenye tamaduni ya kujali ubora.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma pia ilifanyika katika Soko kuu la Ifakara lenye viunga 515 na maduka 105, pamoja na maeneo ya madukani Ifakara mjini, huku jumla ya wanafunzi 2,089 na walimu 78 wakipata elimu juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Ubora .


Sambamba na hayo, TBS ilitoa semina kwa wajasiriamali wapatao 23 katika ukumbi wa halmashauri ya mji Ifakara, ambapo Bi.Amina Yasin, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi (TBS), aliwasisitiza wajasiriamali kufuata utaratibu waliolekezwa ili kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure bila gharama yoyote, kwani ni fursa ambayo inamlenga kumwinua mzalishaji kuweza kushindana na kuuza ndani na nje ya nchi . Vilevile wasisite kutuma maombi TBS kwa ajili ya kupata mafunzo maalum yatolewayo kwa wajasiriamali.

NYANZA BOTTLERS YAENDELEA KUMWAGA ZAWADI KIBAO ZA KAMPENI YA 'KUNYWAAAH NA USHINDE'

0
0


Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= kwa Mkazi wa Mwanza, Carolyne Ngowi wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika jana jijini humo. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’, Marco Msaba (kushoto) na Carolyne Ngowi (kulia) ambao wote ni wakazi wa Mwanza. Hafla ya makabidhiano ya zawadi hiyo ilifanyika jana jijini humo. Kunywaah na Ushinde ni Promosheni ya miezi mitatu inayoenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambao wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo TV na fedha taslim wote wakiwa ni wakazi wa Mwanza. Hafla ya makabidhiano ya zawadi hiyo ilifanyika jana jijini humo. Kunywaah na Ushinde ni Promosheni ya miezi mitatu inayoenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (kushoto) akikabidhi zawadi ya Runinga kwa Mkazi wa Mwanza, Shaban Ismail wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni hiyo inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika jana jijini humo. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambayo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

WADAU WA AFYA WAASWA KUPIKA CHUNGU KIMOJA PASIPO KUSIGANA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WADAU wa sekta ya afya wameaswa kuimarisha ubia baina ya sekta ya umma na binafsi (PPP) mkoani Pwani, badala ya kusigana kwenye baadhi ya mambo ili kujiepusha kuweka rehani maisha ya wananchi ambao wanahitaji huduma bora ya afya .

Akitoa rai hiyo, wakati wa kikao kilichowakutanisha pande hizo mbili mjini Kibaha, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliwaambia afya ni kitu muhimu kwenye maisha ya binadamu ili aweze kushiriki katika shughuli za kimaendeleo hivyo waondoe tofauti, kila mmoja kwa nafasi yake awe sehemu yake ili kutoa huduma.

Alieleza ,mkoa huo una jumla ya vituo vya kutolea huduma ya afya 342 ,kati ya hivyo 275 ni vya umma, 33 binafsi na 34 vya mashirika ya dini lakini ni vituo 20 vyenye malengo ya kuingia mkataba wa utoaji huduma ambapo sita pekee ndio vilivyoingia mkataba. 

"Kutokana na hali hii, manake kuna baadhi ya maeneo yanaathirika kwenye utoaji huduma kutokana na kutokuwa na makubaliano ya sekta ya umma na binafsi "anasema. Ndikilo alifafanua, asilimia 20 ni vituo vya binafsi mkoani humo na asilimia 80 ni vya umma hivyo bado kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuboresha huduma hizo. 

Aidha aliwataka wadau hao, kukutana kila mwaka ili kutathmini, kusimamia utekelezaji na mwenendo wa ubia baina ya sekta hizo. 

Nae mratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi Pwani, Dk. Hussein Athuman alibainisha lengo la kukutana ni kujenga mahusiano baina ya pande hizo, kubadilishana uzoefu na kujiwekea mikakati itakayosaidia kuleta chachu ya mabadiliko chanya kwenye sekta ya afya. 

Awali Dk. Mariam Ongara kutoka wizara ya afya alielezea, vituo vya kutolea huduma ya afya binafsi na mashirika ya dini vina mchango mkubwa kwa jamii. Mariam alisisitiza serikali inatambua mchango unaotolewa na sekta binafsi kwani ina mchango mkubwa kwa watanzania.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo

ULEGA AWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MVUA NA KUSABABISA NYUMBA ZAO KUBOMOKA

0
0
Na Shushu Joel,Mkuranga.

NAIBU waziri wa mifugo na  uvuvi na mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani AbdAllah Ulega amewatembelea wahanga  waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.

Akizungumza na wananchi hao  Ulega aliwapa pole na kuwaomba kuendelea kuwa na subra wakati serikali  ya awamu ya tano ikifanya tathimini ili kubaini kaya zote zilizokumbwa na majanga hayo.

Aliongeza  kuwa majanga kama haya si  ya kisiasa bali yanapangwa na Mungu hivyo katika kipindi hiki  kigumu kwa wananchi wa vikindu ambao ndio waathirika wakubwa wanapaswa kuendelea kuwa watulivu.

Aidha alisema kuwa taarifa za awali alizozipata kuhusu kaya zilizokumbwa na majanga hayo zilikuwa ni 100 lakini kufikia jioni ziliongezeka mpaka kufikia kaya 178 ,ni kaya nyingi kwa kweli kwani wananchi hao wanapata changamoto  kwa sasa.

Pia Naibu waziri huyo amewapatia pole wananchi hao zilizotolewa na Rais wa jamhuri  ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kusema anatambua kilichotokea katika jimbo la Mkuranga na kuwataka  kuzidisha maombi ili Mungu awaondolee majanga.

Aidha katika ziara hiyo ya kuwatembelea wahanga hao Ulega ametembelea familia iliyopoteza mama na mtoto  kwa kuuwawa kwa radi.
"Ofisi ya mbunge imetoa kiasi cha zaidi ya milioni 3 ili kusaidia baadhi ya wahanga wa nyumba zilizoezuliwa na  upepo mkali na itaendelea kuwasaidia  ili kuhakikisha kila  mmoja anarudi kwenye nyumba yake na kuendelea na shughuli zake za uzalishaji"Alisema Ulega.

Kwa upande  wake shuhuda wa tukio hilo,Juma Said  alisema  kuwa radi iliposhuka katika maeneo hayo hali ya hewa kama ilibadirika yote mama wa familia hiyo alikuwa nje ghafla alianguka na huku vijana waliokuwa ndani walipiga kelele ndio tuliwai kutoa msaada kwa mama huyo kimkimbiza hospital ila kijana alikuwa ameshakwisha kufariki.
Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega   akiwapa pole wanafamilia  waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.
Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega   akiwapa pole wanafamilia  waliokumbwa na majanga ya kubomoka kwa nyumba zao na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.
Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega   kulia akiwa amekaa na wafiwa katika msiba , ambapo aliwafariki na kuwaomba kuendelea kuwa na subra  katika kipindi hiki  kigumu ,Wananchi wa vikindu ambao ndio waathirika wakubwa wanapaswa kuendelea kuwa watulivu.


Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi  mbunge  wa Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega akimsikiliza mmoja wa wananchi ambae nyumba yake ilikumbwa na majanga ya kubomoka na kupelekea kupata hifadhi kwa wasamalia wema.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images