Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

RMO SIMANJIRO ATOA UTARATIBU MPYA KUINGIA NDANI YA UKUTA WA MAGUFULI

0
0



Ofisa madini mkazi wa kimkoa wa kimadini wa Simanjiro Daudi Ntalima akizungumza juu ya utaratibu wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani (maarufu kama ukuta wa Magufuli).


Wanawake wanaojihusisha na shughuli mbalimbali wakiwa kwenye mstari wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Wanawake wachekechaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifanya kazi yao ya kuchekecha mabaki ya udongo unatolewa migodini.
………………………..
Ofisa madini mkazi wa kimkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima amepiga marufuku uuzwaji wa bia, viatu na wamachinga, pombe haramu ya gongo na vibanda vya uuzwaji baruti, ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani. 

Ntalima aliyasema hayo wakati akizungumzia utaratibu mpya wa kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi hiyo. Alisema utaratibu huo mpya utaanza kutumika April mosi mwaka huu na hakutakuwa na ruhusa ya watu kuingia na kukaa bila kazi maalum ndani ya ukuta huo. 

Alisema migodi yote ndani ya ukuta inatakiwa kuzungushiwa uzio wa bati ndani ya miezi miwili na migodi au leseni ambazo hazifanyiwi kazi zitafutwa.
“Vibanda au makazi yoyote nje ya uzio wa mgodi husika hayaruhusiwi tena na hairuhusiwi kukata mti wowote ndani ya ukuta bila kibali,” alisema Ntalima. Alisema hairuhusiwi mtu yeyote kuonekana maeneo ya machimbo tofauti na maeneo ya masoko bila kibali na vibanda au makazi yoyote nje ya uzio wa mgodi hayaruhusiwi. 

Alisema maeneo mapya ya masoko yaliyotengwa kwa kupewa namba maalum ya kufanya biashara wanapaswa kuwa na kitambulisho cha mjasiriamali. “Watu wote wanaofanya biashara mbalimbali ndani ya ukuta tofauti na uchimbaji madini wanapaswa kufuata utaratibu huu mpya uliotolewa,” alisema Ntalima. 

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Mirerani, walipongeza hatua hiyo kwani siyo vyema kwa kila mtu anapaswa kuingia ndani ya ukuta hadi migodini. Hassan Juma alisema hivi sasa kuna watu wengi kwenye maeneo ya migodini huku huduma za vyoo ikiwa ni tatizo hivyo kuhofia magonjwa ya milipuko pindi mvua zikinyesha. 


Kaanael Minja alisema biashara nyingine ambazo hazina umuhimu wa kuwepo ndani ya ukuta zinapaswa kukomeshwa hasa wamachinga na wanawake wanaojiuza kwa wanaApolo. “Watu ni wengi migodini vumbi la ulanga linatimka na kuhofia ugonjwa wa Silikosis pia baada ya watu kuruhusiwa kuna wanawake wanaojiuza migodini,” alisema Minja.

UMOJA THABITI NA NIA YA PAMOJA KWA WADAU WA HABARI VYATAJWA KAMA HATUA MUHIMU KUZIKABILI CHANGAMOTO KATIKA TASNIA HIYO

0
0
Picha ya pamoja ya washiriki wa semina hiyo


Na Mwandishi Wetu

MISA Tanzania na shirika linalojikita katika kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari ili kupunguza migogoro, kuimarisha demokrasia na kuwezesha uhuru wa kupata taarifa la IMS zimewakutanisha wadau mbali mbali katika semina ya kujadili mazingira yaliyopo na kupendekeza namna ya kuzikabili changamoto zinazodumaza sekta ya habari na uhuru wa kujieleza nchini.
Bw.Rashweat kutoka International Media Support (IMS) akielezea umuhimu wa ushirikishwaji kwa kila mdau katika mchakato wa kukuza sekta ya habari na uhuru wa kujieleza

Semina hiyo ya siku mbili iliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro iliwakutanisha wawakilishi wa wadau mbalimbali wa tasnia ya habari ikiwemo waandishi wa habari,asasi za kiraia,wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu.

Wakijadili,walitaja baadhi ya changamoto zikiwemo za kiuchumi miongoni mwa wanahabari,sheria zisizo rafiki,wadau kutokuwa na uelewa mzuri wa sheria na kanuni washiriki hao wamesema kuwa kutokuwa na umoja thabiti na nia ya pamoja ndio imekuwa chanzo kikuu cha matatizo mengine kunawiri na kupendekeza kuwa kabla ya kutafuta suluhu nyingine,mkazo uwekwe katika kuwa na umoja thabiti na nia ya pamoja miongoni mwa wadau wote wa tasnia ya habari.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bw.Alex Benson (wa kwanza kushoto aliyeketi) akielezea umuhimu wa wanahabari kuwa na uelewa wa kanuni zinazowasimamia ili kuepuka kuzikiuka mara kwa mara
Wakili James Marenga akiwasilisha mada kwa niaba ya kundi la majadiliano katika semina hiyo
Dr.Geofrey Chambua mshauri wa maendeleo na sheria akielezea uzoefu wake katika kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali kutatua changamoto za kimaendeleo
Mwandishi wa habari wa kujitegemea kutoka Zanzibar Bw.Ali Othman akichangia mawazo katika semina hiyo
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St.John (SMC) Bw.Michael Gwimile akichangia mada katika semina hiyo
Bi.Joyce Shebe mhariri Clouds Media akiwasilisha mada kwa niaba ya kundi la majadiliano katika semina hiyo
Kaimu mkurugenzi wa MISA Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akitoa neno la shukrani na kuhitimisha semina hiyo

WAZAZI WASIFICHE WATOTO WENYE USONJI NDANI-JK

0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wazazi na walezi kutowaficha ndani watoto wenye Usonji kwa kuwa wanauwezo wa kufundishika. 

Akizungumza baada ya matembezi hayo Dkt. Kikwete amesema ugonjwa wa usonji umeenea duniani kote kwa wananchi matajiri na masikini, lakini pia unaitaji uvumilivu kwa wazazi na walezi kwa kuwa ugonjwa huo unaitaji uangalizi wa hali ya juu wakati wote.

" Watoto hao wanategemea sana mapenzi ya wazazi na walezi na jamii kwa ujumla, pia wanategemea kulindwa kwasababu wasipolindwa na kuangaliwa wanaweza hata kujiumiza wenyewe"amesema

Aidha ameipongeza Bodi ya shule ya Al Muntazir ambayo imeanzisha shule maalumu ya watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo Usonji ambao wamekuwa wakiwapatia mafunzo mbalimbali ya vitendo pamoja na Elimu.

Dkt. Kikwete ametoa wito kwa wizara husika ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto na makundi mbalimbali kwenye jamii kutambua tatizo hilo na kuchukua hatua ya kutoa elimu kwa jamii,katika kuelimisha malenzi kwa watoto hao na nini kifanyike ili kuweza kuwasaidia watoto wenye maradhi ya Usonji. 

Aidha amesema jitihada hizo ziongezwe mara dufu kwa kuwekeza elimu kwa jamii ili waweze kutambua ugonjwa wa Usonji,pia ameiomba jamii kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na shule ya Amsen ili mradi huo uweze kufanikiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shule za Al Muntazir Imtiaz Halji amesema njia bora ya kuwaonesha watoto wenye mahitaji maalumu ni kuwalinda na kuwapenda na kuacha tabiya ya kuwatenga ili wasishirikiane na wenzao.

“Wakati sasa umefika tuunganishe nia zetu kuelekea lengo moja,kufanya kila kitu kilicho ndani ya uwezo wetu kuunga mkono katika kuelimisha jamii ”amesema
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza Matembezi ya kuchangia Watoto wenye Usonji wanaosoma katika Shule ya Al Muntazar.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wazazi pamoja na Wadau waliofika katika Maadhimisho ya siku ya Usonji 
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Zawadi kutoka kwa Azim Dewji mara baada ya kushiriki Matembezi ya siku ya Usonji
Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete akikabidhi Zawadi ya Picha kwa Mmoja ya Wazazi wa shule hiyo ambao walinunua kama ishara ya kuchangia Watoto wenye Usonji
Rais Mstafu wa awamu ya Nne,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Matembezi ya Wazazi na Wanafunzi wa Shule ya Al Muntazar

KWA HILI TAASISI YA WAJIBU INASTAHILI PONGEZI

0
0

 *Somo la jaji Sammata kwa wanasheria kukomesha kabisa kansa ya rushwa

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

TAASISI ya Wajibu nchini inayoshughulika na fikra ya uwajibikaji kwa umma imeendelea kutoa mafunzo kwa watu wa kada mbalimbali kuhusiana na masuala ya uwajibikaji na uadilifu.

Moja ya midahalo mikubwa ni ile iliyotolewa na jaji mkuu mstaafu na mkuu wa chuo cha Mzumbe Barnabas Sammata katika Chuo kikuu cha Dodoma na Chuo cha sheria nchini kilichopo jijini Dar es salaam na katika midahalo hiyo jaji Sammata alitoa mada kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa kwa kueleza kuwa rushwa ni kansa inayosababisha kutoweka kwa imani ya raia juu ya demokrasia .

Akiwa katika chuo cha sheria jaji Sammata aliaishukuru taasisi ya wajibu  na uongozi wa chuo cha sheria kwa heshima waliyompa hasa kwa kutoa mada na kuwanoa wanasheria hao kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa ambayo imekuwa adui zaidi kwa ustawi wa wananchi wakati wa amani  kuliko wakati wa vita.

Jaji Sammata alieleza kuwa rushwa katika nchi inatakiwa ishughulikiwe kwa karibu sawasawa na inavyoshughulikiwa suala la uhaini na vijana lazima wawe mstari wa mbele katika kupinga rushwa.

Sammata alieleza kuwa ili kukabiliana na kansa ya rushwa lazima ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka na TAKUKURU kuhakikisha nini kifanyike ili kumwokoa mnyonge kutoka kwenyejanga hilo.

"Rushwa si kansa iliyoanza jana au juzi,kwa mujibu wa biblia ilikuwepo tangu wakati wa yesu miaka ipatayo zaidi ya elfu mbili iliyopita, Korani inakemea sana uovu huo" alieleza Sammata huku akisema kuwa sababu za kupokea rushwa ni nyingi ikiwemo kuharakisha kupata huduma, kupata zaidi ya unachostahili pamoja na kupata kile ambacho mtu ana haki nacho.

Vilevile alieleza madhara ya rushwa ambapo  Jaji Sammata alisema kuwa kansa hiyo ni kuwanyang'ganya wananchi haki yao hasa matarajio yao ya baadaye ikiwemo maisha bora na maendeleo waliojiwekea, alisema kuwa rushwa  hujenga chuki kwa kuwa huvunja haki na waathirika huchukua sheria mkononi wakiona vyombo husika havijatenda haki.

Jaji Sammata alitoa maoni yake na kusema kuwa ili kuepuka hayo yote lazima elimu zaidi kwa umma itolewe na kushauri vyama vya siasa hasa chama tawala na vyombo vya dola kukemea vitendo hivyo huku akihimiza taasisi za dini zishiriki katika kupinga kampeni hiyo kwa kutoruhusu mapato ya rushwa kutunisha kampeni hizo.

Aidha katika mdahalo huo aliwataka wanasheria nchini kote kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo hivyo na kuwa waaminifu   bila kujali ukubwa au udogo wa rushwa ambayo zinaathiri maendeleo ya jamii huku akisisitiza watakaokiuka taratibu za kisheria hata wakiwa waandishi wa habari ambao watakutwa na vitendo hivyo katika kazi zao wachukuliwe hatua kali kwa kuwa wao ndio ngao muhimu katika kumulika vitendo hivyo.

Katika mdahalo huo mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU ambaye pia ni  mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)Ludovick Utouh alisema kiwa taasisi hiyo ni changa na kuanzishwa kwake kulisababishwa na kulegalega kwa uwajibikaji na uadilifu na alihaidi kuendelea kuwafikia walengwa kadri watakavyoweza huku wakiwalenga wanafunzi wa vyuo ambao ndio viongozi watarajiwa.

WAZIRI WA MADINI UGANDA, ATEMBELEA TANZANIA

0
0
Kutoka kushoto, Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella wakimsubiri Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris pamoja na ujumbe wake kabla ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza tarehe 01 Aprili, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto mbele) akiwaongoza Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo, Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris pamoja na ujumbe wake kwenye ukumbi wa mikutano.
Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris (wa pili kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo, akielezea mafanikio ya nchi ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa ujumbe wa Uganda.
Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris akifafanua jambo kwenye mkutano huo.

Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris (waliosimama katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka nchini Uganda na Tanzania.





Greyson Mwase na Remija Salvatory, Mwanza 


Waziri wa Madini Nchini Uganda, Peter Lokeris pamoja na ujumbe wake wameanza ziara nchini Tanzania leo tarehe 01 Aprili, 2019 yenye lengo la kujifunza namna sekta ya madini nchini Tanzania inavyoendeshwa. Waziri Lokeris ameongozana na maafisa waandamizi kutoka Serikali ya Uganda pamoja na wawakilishi wa wachimbaji wadogo. Waziri wa Madini Nchini Uganda pamoja na ujumbe wake walipokelewa na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. 

Akizungumzia lengo la ziara hiyo kupitia mahojiano maalum aliyoyafanya na vyombo vya habari, mara baada ya kupokelewa na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo, Waziri Lokeris alisema kuwa lengo la ziara yake ni kujifunza sheria na kanuni za madini nchini Tanzania zinavyosimamiwa vyema pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini nchini Tanzania kwa vitendo kupitia wawekezaji waliowekeza nchini pamoja na wachimbaji wa wadogo wa madini. 

“Tulifanya utafiti na kubaini Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa madini na uzoefu mkubwa kwenye uchimbaji wa madini na tumeona wachimbaji wadogo wakisaidiwa sana na Serikali ya Tanzania,” Alisema Lokeris. 

Aliongeza kuwa, kati ya maeneo wanayotarajia kujifunza ni pamoja na ushirikishwaji wa wazawa kwenye shughuli za uchimbaji wa madini (local content) utoaji wa huduma kwa jamii inayozunguka shughuli za uchimbaji wa madini (corporate social responsibility), usimamizi wa sheria ya madini pamoja na kanuni zake. 

Aliongeza kuwa ushirikiano wa Tanzania na Uganda umekuwa ni wa muda mrefu na kusisitiza kuwa Serikali ya Uganda ipo tayari kujifunza na kubadilishana uzoefu kwenye usimamizi wa sekta ya madini. 

Aliendelea kusema kuwa, Serikali ya Tanzania inapenda kuona wananchi wake hususan waishio vijijini wananufaika na sekta ya madini kupitia uboreshwaji wa huduma za jamii kama vile elimu huduma za afya, na ili kuhakikisha wananchi wake wananufaika, Serikali imeamua kutuma wataalam wake Tanzania kujifunza kutokana na hatua kubwa iliyopigwa na nchi ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini. 

Akielezea changamoto kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa nchi ya Uganda, Waziri Lokeris alieleza kuwa ni pamoja na kutokuwa na teknolojia ya kutosha kwenye uongezaji thamani wa madini pamoja na utoroshwaji wa madini unaofanywa na wachimbaji wadogo. 

Wakati huohuo Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo alisema kuwa nchi ya Tanzania ipo tayari kutoa uzoefu wake kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa nchi ya Uganda kupitia wataalam wake. 

Alisema katika ziara ya ujumbe huo, mbali na nchi ya Tanzania kutoa uzoefu wake kwenye usimamizi wa sekta ya madini nchini, wanatarajia kuupeleka ujumbe huo kwenye soko la madini mkoani Geita lililozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasim Majaliwa pamoja na baadhi ya mitambo ya kuchenjulia dhahabu. 

Akielezea mikakati ya Serikali ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini, Naibu Waziri Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na uboreshaji wa sheria ya madini pamoja na kanuni zake ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa wachimbaji wadogo wa madini. 
Alieleza mikakati mingine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini katika kila mkoa ili kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini.

BBC KUZINDUA LADHA MPYA YA VIPINDI VYA REDIO

0
0
  Kuanzia siku ya Jumatatu, tarehe 1 mwezi Aprili,wasikilizaji wa vipindi vya Kiswahili vya BBC watasikiliza ladha mpya  ya vipindi vya Dira ya Dunia na Amka na BBC.Mabadiliko haya yatahusisha pia watangazaji wapya na kutambulishwa kwa habari bora kuhusu biashara pamoja na Makala zenye kuleta matokeo chanya.

Matangazo ya barabarani yatafanyika Kenya na Tanzania katika uzinduzi huu.Matangazo hayo yatafanyika katika mji wa Bandari Mombasa, mji wa Kwale, Kitui, Dodoma,Morogoro,Kibaha na Dar es Salaam.Wasikilizaji watasikia matangazo hayo maalumu kwa kipindi cha siku tano, kutoka kwenye maeneo hayo na kusikia sauti za watu mbalimbali katika maeneo tutakayoyafikia.

 -Mahojiano na watu mashuhuri na viongozi:
- Wanamuziki - Venessa Mdee, Susumila and Mwasiti
- Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
- Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho
- Mbunge wa Tanzania, Zitto Kabwe
- Mwanasiasa wa upinzani kutoka visiwani Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamadi
- Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi
- Mkuu wa wilaya, Jokate Mwegelo
- Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Winnie Kiiza
- Mbunge wa Tanzania na mke wa Rais wa awamu ya nne,Salma Kikwete
- Rais wa zamani wa Tanzania , Jakaya Kikwete
- Gavana wa Machakos,Dokta Alfred Mutua

Taarifa motomoto:
-‘’ Wahandisi’’ wanawake wa Zanzibar
- Wanakijiji watengeneza mkate wa wadudu
- Nyumba iliyojengwa katikati ya mpaka wan chi mbili
- Uvutaji wa sehemu za siri za wanawake nchini Rwanda
- The Kenyan community without sweat pores
-Jamii ya Kenya isiyotoa jasho
- Kisiwa chenye uhaba wa Condom

Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeweka utaratibu wa kutembelea Wanafunzi  wa Kidato cha Sita katika Shule za Sekondari ili kutoa elimu ya namna ya kuomba Mikopo katika Bodi hiyo. 

Akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya  Sekondari ya Ubungo Islamic  Afisa Mwandamizi Bodi hiyo Josephat Bwathondi amesema kuwa bodi iko kwa kazi moja ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji kwa ajili ya elimu  ya juu ambapo kukosekana kwa chombo  hicho baadhi ya watanzania wangekosa elimu ya juice kutokana uchumi walio nao. 

Amesema kuwa lengo la kuwafikia Wanafunzi wa shule hiyo ni kwa ajili ya kuwapa namna ya uombaji mikopo  na taarifa  zinazohitajika katika uambaji mikopo.

Aidha amesema taarifa za msingi katika maombi hayo ni vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi, Wazazi, Kama mwanafunzi kafiwa na mzazi kuwepo kwa cheti cha kifo katoka kwa Wakala wa Udhamini, Ufilisi, Usajili wa Vifo na Vizazi (RITA).
Amesema utaratibu  hapo nyuma haukuwepo lakini wameona ni muda mwafaka wa kutoa elimu ya uoambaji Mikopo. 
Nae Afisa wa Urejeshaji Mikopo wa  Bodi hiyo Emmanuel Mtavangu amesema kuwa katika  kuwapa elimu ya uombaji  Mikopo pia lazima watambue kuwa Mikopo hiyo inarejeshwa kwa ajili ya kusomesha wahitaji wengine.
 Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Josephat Bwathondi akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ubungo Islamic wakati walipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi Wasichana wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic wakisikiliza mada za Bodi ya Mikopo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Sekondari hiyo.
 Wanafunzi Wavulana wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic wakisikiliza mada za Bodi ya Mikopo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Sekondari hiyo.
Afisa wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Emmanuel Mtavangu akitoa maelezo ya taratibu za Urejeshaji mikopo baada ya kuhitimu shahada ya kwanza wakati Bodi ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic jijini Dar es Salaam.

MABONDIA HUSSEIN PENDEZA NA JUMA RAMADHAN KUZICHAPA SIKU YA PASAKA

0
0
 Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MABONDIA Hussein Pendeza na Juma Ramadhani 'Choki' wametamba kila mmoja kwa wakati wake kuibuka na ushindi katika mpambano kati yao ambao unatarajia kufanyika Aprili 21 mwaka huu ambayo itakuwa Sikukuu ya Pasaka.

Akizungumzia mpambano huo ambao utafanyika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam Juma Ramadhan 'Choki' amesema ana uhakika wa kushinda kwani hivi sasa yupo fiti mpaka mwenyewe anajiogopa kutokana na mazoezi ambayo ameyafanya kujiandaa na pambano hilo.

"Kwa namna ambavyo nimejiandaa , sio huyo tu Pendeza, yoyote ambaye atakuja mbele yangu atapokea kichapo tena cha mbwa mwizi.Hivyo wakae chonjo vingenevyo nitawararuaraua na sijaona katika uzito wangu wangu wa kilogramu wa kunisumbua kwani najiamini na ninajimini kwa mazoezi ambayo nimeyafanya,"amesema.

Hivyo Choki amewaomba mashabiki wake wa Manzese,Mabibo, Mbagala Kuu na Mtoni Kijichi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kumpa sapoti na anataka kuweka historia ya aina yake kwenye mpambano huo.

 Kwa upande wake bondia Pendeza amesema kuwa atahakikisha anampiga Choki kama begi kwani kwake ni mtoto mdogo sana katika ulimwengu wa masumbwi na kipigo ambacho atampatia atajuta kuzaliwa kwa kipigi ambacho atakipata.Pia ameongeza anawaomba mashabiki wake wote na wapenzi wa ngumi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuangalia jinsi anavyo msambaratisha mpinzani wake.

Mpambano huo umeandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo amefafanua maandalizi yote muhimu yameshafanyika ."Pambano litafanyika Siku ya Sikukuu ya Pasaka,"amesema Super D.

Pia amesema bondia mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anayefanya shughuli zake nchini Australia  ndiyo aliyosababisha mabondia hao wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio maana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyike

Super D ameongeza mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia  Idd Mkwera ataoneshana umwamba na Rojas Masamu wakati Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede.

Wakati Ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atapambana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala

Mapambano yote hayo yanaletwa yanafanyika chini ya kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinua vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini. 

Ubalozi wa Kenya wapanda miti kumsherehekea Wangari Maathai

0
0
Dk Reginald Mengi (mwenye tai nyekundu) akipanda mti kama ishara ya kumsherehekea Profesa Wangari Maathai, mwanaharakati wa mazingira kutoka Africa mashariki. Tukio hili limefanyika leo wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa nchi za Africa, wawakilishi kutoka sekta binafsi na Umoja wa Mataifa. Wa tatu kulia ni Balozi wa Kenya, Mh Dan Kazungu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Sanjay Rughani (kulia) na wafanyakazi wa ubalozi huo. 
Wawakilishi kutoka Ubalozi wa Norway na UNDP, Nancy Shedrack na Helge Flaard wakimwagilia mti kama ishara ya kumsherehekea Profesa Wangari Maathai, mwanaharakati wa mazingira kutoka Africa mashariki. Tukio hili limefanyika leo wakati wa tafriji fupi iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa nchi za Africa, wawakilishi kutoka sekta binafsi na Umoja wa Mataifa. Katikati ni Balozi wa Kenya, Mh Dan Kazungu. 
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mh Dan Kazungu akipanda mti kama ishara ya kumsherehekea Profesa Wangari Maathai, mwanaharakati wa mazingira kutoka Africa mashariki. Tukio hili limefanyika leo wakati wa tafriji fupi iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa nchi za Africa, wawakilishi kutoka sekta binafsi na Umoja wa Mataifa. 
Balozi wa Kenya nchini Tanzania (3 kushoto) na wafanyakazi wa ubalozi huo wakipanda mti kama ishara ya kumsherehekea Profesa Wangari Maathai, mwanaharakati wa mazingira kutoka Africa Mashariki. Tukio hili limefanyika leo wakati wa tafriji fupi iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa nchi za Africa, wawakilishi kutoka sekta binafsi na Umoja wa Mataifa.

DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI

0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpongeza mwenyekiti wa halmshuri ya wilaya ya Iringa Vijijini Stephen Mhapa kumpa tuzo ya ngao kwa kufanya vizuri katika utunzaji wa mazingira pamoja na kuwa na vyoo safi na bora.
Baadhi ya washiriki waliofika katika kikao hicho cha utoaji tuzo kwa utunzaji bora wa mazingira na kuwa na vyoo bora.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa sambamba na mkurugeni wa halmashauri ya Iringa vijijini Robert Masunya wakinywa maziwa ya Asas



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wananchi,viongozi,taasisi na jumuiya mbalimbali kwa kutekeleza vizuri kampeni ya kuwa na vyoo bora ambavyo vimeipa ushindi halmasahuri ya Iringa Vijijini kwa kupata tuzo ya usafi hapa nchini.

Kasesela alisema kuwa ofisi ya afya katika halmasahuri ya Iringa Vijijini wamekuwa wakisimamia vizuri swala la afya na kuwa na vyoo bora ambapo wanataraji kuwa halmashauri ya kwanza kwa kuwa na vyoo bora kuliko halmashuri zote za mkoa wa Iringa hadi taifa.

“Nampengeza bibi afya wa hapa amekuwa mkali kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kukwamisha zoezi lolote la kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha afya za wananchi wa wilaya hii wanakuwa na afya njema” alisema Kasesela

Aidha Kasesela amepiga marufuku wa wazazi kujifungulia majumbani kwa kuwa sio sehemu salama kwa uzazi wa mtoto wakati serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ambayo ndio kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano. 

“Jukumu la kwanza kwa baba ni kuhakikisha amempeleka mama kliniki kupata huduma ili kuwa na malezi mazuri ya mtoto,hivyo tutaondoa ile njia ya akinamama kujifungulia majumbani kwa kuwa tayari baba atakuwa anajua wajibu wake” alisema Kasesela

Kasesela amewataka watendaji wa kata,vijiji na maafisa tarafa kuhakikisha hakuna mama anajifungulia nyumbani na nitamshughulikia mtendaji yeyeto Yule ambaye hata wachukulia hatua akibaba watakao fanikisha mama kujifungulia numbani.

Awali akitoa hutuba kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa halmasahuri ya Iringa Vijijini Robert Masunya aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wameendeleza juhudi hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na vyoo bora ili kupunguza na kumaliza tatizo la milipuko ya magonjwa.

“Niwaombeni tena tuendelee kushirikiana vyema katika kuhakikisha halmasahuri ya Iringa Vijijini inaongoza kwa kuwa na mazingira bora na safi kuliko halmashuri zote hapa nchini kwa kuwa tuna mikakati ambayo ni bora sana” alisema Masunya

DKT ANNA MGHWIRA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILIYOAMBATANA NA UPEPO KILIMANJARO.

0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakitembelea maeneo yaliyoathirika na mvua iliyonyesha juzi ikiambatana na upepo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akizungumza na mmoja wa maafisa wa Magereza waliokuwa katika uismamizi wa wafungwa wakati wa kukata miti mikubwa iliyofunga barabara baada ya kuanguka. 
Moja ya miti mikubwa iliyoanguka katika ya barabara ukiwa umekatwa. 
Kukatika kwa miti hiyo kulikuwa ni fursa kwa watu wengine waliojitokeza kuokota kuni. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akitizama mafundi wa shirika la umeme Tanesco wakati wakijaribu kurejesha miundo mbinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua iliyoambatana na upepo. 
Mafundi wa TANESCO wakijaribu kurejesha nyaya zilizokatika . 
Sehemu ya nyaya zilizokatika kufuatia mvua hiyo. 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakitembelea Kiwanda cha kuzalisha vifaranga vya kuku ambacho kuta zake zilianguka pamoja na mti mkubwa kukatika. 
Mti ulikuwa jirani kabisa na jengo lililokuwa na mashine za kuangulia vifaranga na kuharibu mashine mbili pamoja na kuahribu mayai zaidi ya 15,000. 
Mafundi wakijaribu kuondoa sehemu ya mti ulioangukia jengo hilo. 
Sehemu ya mashine hizo. 
Mayai yakiwa kwenye mashine tayari kwa ajili ya kuanguliwa. 
Vifaranga vya kuku vikiwa katika mashine baada ya kuanguliwa. 
Kuku wakubwa wakiwa katika kiwanda hicho kwa ajili ya mayai. 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira akitizama moja ya nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari ya Old Moshi ambaye paa la nyumba hiyo liliezuliwa kutokana na upepo. 
Nyumba nyingine katika shule ya sekondari ya Old Moshi ikiwa imeezuliwa na upepo. 
Moja ya miti iliyoanguka katika shule ya sekondari ya Old Moshi ,mti huu uliangukia bweni la wananfunzi bahati nzuri haukuweza kusababisha madhara. 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Annag Mghwira akitoa pole kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Old Moshi alipowatembelea kuwajulia hali baada ya mvua iliyoaambatana na upepo kuharibu baadhi ya miundo mbinu zikwemo nyumba za walimu. 
Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Old Moshi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira (hayupo pichani).
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

NAIBU MEYA JOSEPH LYATA AWATAKA WANAFUNZI KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

0
0
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata amewataka wanafunzi wa manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani
Mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.
Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiongea na wanafunzi walijitokeza kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa



NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

NAIBU MEYA wa manispaa ya Iringa amewataka wanafunzi wa manispaa ya Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani.

Akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mwembetogwa,Lugalo,Tagamenda na Mawelewele naibu meya Joseph Lyata aliwataka wanafunzi hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha pekee ya kuhakikisha tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.

Kuthamini vitu vilivyopo katika nchi yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za nchi na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo” alisema Lyata

Lyata alisaema kuwa nchi nyingi ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana uongozi bila kutumia mabavu,hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.

“Angalieni nchi kama Somalia tu hapo jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo wa wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu” alisema Lyata

Lyata aliongeza kwa kusema kuwa uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa wazalendo na nchi yao.

“Lazima tuambizane ukweli kabisa maana sisi kama manispaa tunahakikisha manispaa inaendelea kuongoza kwenye usafi,kuhakikisha wanafunzi mnasoma vizuri bila kuwa na woga na kuhakikisha tunailinda mipaka ya nchi yetu huo ndio uzalendo wa nchi yetu” alisema Lyata

Lyata aliwata wanafunzi kuanza kuwa na uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda nchi hii kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa watakuwa na lengo la kulinda amani ya nchi.

“Uzalendo pia huanzia pale unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara kuna mambo ya msingi utajifunza tu” alisema Lyata

Naye mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa (UVCCM) Salvatory Ngerera aliwataka wanafunzi kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.

“Wananchi wanasababisha umasikini wenyewe kutokana na kuchagua viongozi ambao hawana uwezo ndio hupelekea umaskini katika kwa wananchi waliomchagua kiongozi waliyekuwa na imani naye,hivyo kukosea kuchagua kiongozi bora ni kujitafutia matatizo wenyewe” alisema Ngerera

Ngerera aliongeza kwa kuwaambia wanafunzi hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri huo waliona wanafunzi kwa kuwa ndio kipendi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa wa maisha ni nini.

“Jamani lazima mjifunze mnapotaka kumlaumu kiongozi mlimchagua wenyewe ni lazima mjipie wenyewe kwanza mlikosea wapi na sasa mnatakiwa mfanye nini ili kuhakikisha mfanya kazi huku mkiwa mmetawaliwa na uzalendo wenu” alisema Ngerera

NMB YATOA MSAADA WA MABATI,VITANDA NA MADAWATI CHUO CHA VETA KALAMBO MKOANI RUKWA

0
0
Naibu Waziri Tamisemi Mh Josephat Kandege akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa Msaada wa Mabati 802 ,Vitanda 8 vya Hospital pamoja na Madawati 50 vyenye Jumla ya Thamani ya shilingi Mil 35 Kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ,Straton Chilongola Mwenye Suti nyeusi (kulia) hafla ambayo imefanyika katika Soko la Wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.March 30,2019.
Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Straton Chilongola(Kulia) akimkabidhi Naibu Waziri wa Tamisemi Mh Josephat Kandege msaada wa Vitanda 8 vilivyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Chuo cha Veta Kalambo Mkoani Rukwa,Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangambo na Juliet Benyura Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ,hafla ambayo imefanyika katika Soko la wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo March 30,2019.
Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Straton Chilongola(Kulia) akimkabidhi Madawati 50 Naibu Waziri wa Tamisemi Mh Josephat Kandege (MB) kwa ajili ya Chuo cha Veta Kalambo Mkoani Rukwa,Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangambo , Vitu vingine vilivyotolewa na Benki hiyo ya NMB kwa ajili ya Chuo hicho ni pamoja na Vitanda 8 vya hospital,Mabati 802 ,hafla ambayo imefanyika katika Soko la wakulima Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo March 



MASOKO MAKUBWA NA MAARUFU ZAIDI DUNIANI HAYA HAPA

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MASOKO makubwa zaidi  duniani yamepata nafasi ya kuwa vivutio kwa watalii na hiyo ni kutokana na bidhaa zinazouzwa katika masoko hayo pamoja na maonesho ya tamaduni mbalimbali, masoko makubwa na maarufu zaidi duniani ni pamoja na:

1. Soko la Tsukiji
Soko hili linapatikana Tokyo nchini Japan, ni soko kubwa la samaki duniani ni sehemu ambayo unaweza kupata vyakula freshi vya baharini pamoja na vinywaji.

Lilianza rasmi Februari 11, 1935 na huuza vyakula vya baharini zaidi ya 480 huku likiwa na migahawa na linafahamika zaidi kwa kuwa kivutio kwa wazawa na wageni.

2. Soko la Bazaar
Hili linapatikana  Instanbul nchini Uturuki, ni moja kati ya soko kubwa na kongwe zaidi duniani lililoanzishwa mwaka 1461. Ni kivutio kwa watalii na ni sehemu ambayo bidhaa za nguo,viungo na manukato hupatikana huku ikielezwa kuwa bidhaa zao ni bora zaidi.

Mwanzo soko hilo lilikiwa kituo cha biashara kwa ngome ya Ottoman ambapo soko hilo lilikuwa chini ya usimamzi wa wanajeshi wa nchi hiyo.

3. Soko la Chatuchak
Soko hili linapatikana Bangkong nchini Thailand likiwa ni soko kubwa zaidi nchini humo hasa kwa siku za mapumziko, soko hilo limechukua jumla ya hekari 35 pamoja ma stoo 15000 huku likiwa na sehemu za kuuza vyakula,nguo na mapambo. Hufunguliwa kila siku ila katika siku za mapumziko bidhaa hupatikana kwa wingi.

4. Soko la Marrackech Sooks
Hili hupatikana huko Marrakech nchini Moroccco, linapatikana katikati ya mji na limekuwa kitovu cha biashara pamoja masuala ya uchumi na tamaduni nchini humo.
Ni soko la kitamaduni na maarufu kwa kuuza bidhaa za ngozi, viungo na nguo na nyakati za jioni huwa soko la usiku ambapo vyakula mbalimbali kama kababu na vyakula vingine vya mtaani hupatikana na inaelezwa kuwa sehemu hiyo ni nzuri ya kufurahia usiku ukiwa nchini Morocco.

5. Soko la Viennese Krismasi
Soko hili linapatikana Vienna nchini Australia likiwa maarufu zaidi kwa kuuza bidhaa na mapambo ya krismasi, mishumaa, mapambo, vyakula na vinywaji hasa mvinyo.
Tamaduni za watu mbalimbali huoneshwa katika viwanja vya soko hilo zikiwemo kwaya za Krismasi huku likiwa na masoko makubwa zaidi ya 20.

6. Khan Al-Khalili
Hili linapatikana Cairo nchini Misri na lilianza karne ya 14 na lilianza kama kituo cha kuuzia dhahabu, viungo na madini mengine ya thamani na kwa sasa vito vya kila aina vinapatikana katika soko hilo pamoja na nakshi na mapambo ya kila aina. Soko hilo lina maduka  zaidi ya 900.
Ni soko ambalo limepakana na mji mkuu na ni moja ya soko kubwa na kongwe zaidi huku likiwa na sehemu ya kupumzika maarufu zaidi iitwayo Fishawi's Coffee iliyoanza kutoa huduma mwaka 1773.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI WAWILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Msafiri Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Adolf Ndunguru akiwa pamoja na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wakila Kiapo cha Uadilifu  Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza salamu mbalimbali zilizokuwa zikitolewa Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumuapisha Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) pamoja na Msafiri Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi wa John Kijazi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji wakwanza kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera) Adolf Ndunguru  wapili kutoka kulia Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo wapili kutoka kushoto mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA POLE KWA MBUNGE WA IRINGA MJINI MCHUNGAJI PETER MSIGWA ALIYEFIWA NA DADA YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili Kimara kwa ajili ya kutoa heshma za Mwisho kwa mwili wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza la marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Msibani pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakwanza kulia, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa wakwanza kushoto aliyekaa pamoja na ndugu zake kufatia kifo cha Dada yake marehemu Tryphosa Simon Sanga kilichotokea juzi jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili Kimara msibani huku akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa ambaye alifiwa na Dada yake marehemu Tryphosa Simon Sanga.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakati akitoka kutoa heshma za mwisho kwenye msiba  wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka eneo la msibani Kimara mara baada ya kutoa heshma za mwisho kufatia kifo cha wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

SERIKALI HAIJAZUIA BIASHARA YA MADUKA YA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI

0
0
 Katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Fedha inachangia ipasavyo utulivu na ukuaji wa uchumi nchini, Benki Kuu ya Tanzania ilibaini uwepo wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo yalikuwa yakiendeshwa pasipo kuzingatia Sheria ya Foreign Exchange Act 1992, Kanuni za The Foreign Exchange (Bureau de Change) Regulations 2015 na marekebisho ya mwaka 2017 na Taratibu za utoaji wa huduma za ubadilishaji wa fedha za kigeni. Kufuatia hali hiyo, zoezi maalum la ukaguzi wa kina kwa maduka hayo lilifanyika Arusha Novemba 2018 na kwa Dar es Salaam siku ya tarehe 27 Februari 2019, 1 na 8 Machi 2019 kwa kuhusisha vyombo vya Dola na kubaini ukwepaji mkubwa wa kodi na uvunjaji wa Sheria.

Zoezi hili limebaini pia uondoshwaji wa fedha katika mfumo rasmi wa fedha na kuelekezwa kwenye mifumo ya utakasishaji wa fedha haramu, kupokea Amana kutoka kwa wafanyabiashara kinyume cha matakwa ya leseni za biashara husika, kudhoofisha thamani ya shilingi, pamoja na mambo mengine ambayo yalianza kuathiri usalama wa nchi kwa ujumla. Kwa mfano, baadhi ya maduka yaligundulika kutumia fedha nyingi za Tanzania kununua fedha za kigeni lakini fedha kidogo za kigeni ziliuzwa na hakuna taarifa ya matumizi ya fedha za kigeni zilizobaki.

Ni vizuri ieleweke kuwa, zoezi la ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni lilitekelezwa kwa kuzingatia Sheria za nchi tofauti na malalamiko na tuhuma mbalimbali zilizotolewa za kudai uwepo wa ukiukwaji wa Sheria na haki kwa wamiliki wa maduka hayo. Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna mmiliki yeyote wa duka aliyewasilisha malalamiko kuhusiana na zoezi hili kwenye mamlaka husika. Hata hivyo, Benki Kuu ya Tanzania na Mamlaka nyingine za Serikali zinafuatilia kwa umakini ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zinazotolewa.

Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza majukumu yake kwa umakini. Hivyo, Serikali inauthibitishia umma wa Watanzania kuwa katika zoezi la ukaguzi wa Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni hakuna fedha au mali yeyote iliyotaifishwa. Taratibu za kisheria zilifuatwa wakati wa kuchukua vielelezo mbalimbali zikiwemo fedha, kompyuta, simu za viganjani, mashine maalum za kuhifadhi taarifa na taarifa mbalimbali ili kusaidia uchunguzi. Aidha, lengo la zoezi hili sio kufuta biashara ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kwa watu binafsi, bali ni kudhibiti ukiukwaji wa sheria uliokithiri, ukwepaji wa kodi na utakatishaji wa fedha haramu. Maduka machache ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo yalizingatia Sheria na Kanuni za Foreign Exchange na masharti ya biashara hiyo yaliachwa kuendelea na utoaji wa huduma hiyo.

Hivi sasa Serikali imeandaa Kanuni mpya kwa ajili ya biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambazo zitaelekeza jinsi ya kuomba leseni za uendeshaji wa maduka hayo kwa mtu binafsi au taasisi yeyote na masharti ya kuzingatiwa wakati wa shughuli hizo.

Kanuni hizo zinalenga kuweka mazingira mazuri ya biashara ambayo hayatatoa athari kwa sekta ya fedha na uchumi jumla, na inakuwa yenye manufaa kwa nchi. Kwa kuzingatia maduka mengi yaliyokaguliwa yamefungwa, Benki Kuu ya Tanzania imechukua tahadhari ya kuhakikisha huduma ya ubadilishaji fedha za kigeni inaendelea nchini kwa kutolewa na benki zote pamoja na Shirika la Posta. Benki Kuu ya Tanzania itakuwa inatoa taarifa kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo na kuzihimiza benki za biashara na Shirika la Posta kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na huduma katika maduka yaliyofunguliwa na benki hizo na Ofisi ya Posta.

Kwa kipindi kifupi cha utekelezaji wa zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha za kigeni, thamani ya shilingi imeimarika na upatikanaji wa fedha za kigeni katika benki za biashara umekuwa mzuri. Kabla ya zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha ya kigeni dola ya Marekani ilikuwa inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,450 na baada ya utekelezaji wa zoezi hivi sasa dola ya Marekani inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,300. Aidha, Benki za biashara kwa wastani hivi sasa zinakusanya jumla ya dola za Marekani milioni 15 kwa siku. Ni matarajio ya Serikali kuwa udhibiti huu utaziwezesha Benki za biashara na taasisi nyingine kuuza fedha za kigeni kwa wingi kwenye soko la fedha za kigeni na hatimaye kuongeza akiba ya fedha za kigeni.

Serikali inatoa tahadhari kwa wananchi kutoshiriki kwenye biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa njia zisizo halali. Hivi sasa kuna taarifa kwa baadhi ya maeneo ya mipakani na majiji ya Dar es Salaam na Arusha wamejitokeza watu wanaofanya biashara haramu ya kubadilisha fedha za kigeni ambao wamewaathiri baadhi ya wananchi kwa wizi. Vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi vimeongeza nguvu katika kuhakikisha biashara hii haramu (Black Market) inatokomezwa na hivi sasa wahalifu saba wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Serikali inapenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa inayo akiba ya fedha za kigeni ya kutosha zipatazo dola za Marekani bilioni 4.67 hadi tarehe 30 Machi 2019 zenye uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisicho pungua miezi 4.8. Hivyo, wasiwasi kuwa Serikali imechukua hatua ya kufunga baadhi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kwa sababu haina akiba ya fedha za kigeni si ya kweli hata kidogo. Aidha, hofu kwamba nchi inarejea katika kipindi cha nyuma ambapo fedha za kigeni zilikuwa zinatolewa kwa vibali (rationing) ili kukidhi mahitaji ya fedha hizo kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, nazo hazina msingi.

Mapato ya Nchi yanayotokana na vyanzo vya fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi yalikuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 8,554.5 kwa mwaka unaishia Februari 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.4 ikilinganishwa na fedha za kigeni zilizopatika mwaka unaishia Februari 2018. Ongezeko hilo la mapato ya fedha za kigeni kwa Nchi yamechangiwa zaidi na uuzaji wa bidhaa zisizo asilia nje ya nchi zikiwa na thamani ya dola za Marekani milioni 3,878.5 sawa na asilimia 10.3 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Vile vile, huduma zilizotolewa nje ya nchi kama vile usafiri na usafirishaji na utalii ziliingiza jumla ya dola za Marekani milioni 4,074.1 sawa na ongezeko la asilimia 6.1 ikilinganishwa kiasi kilichopatikana mwaka ulitangulia.

Aidha, Serikali inachukua fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa nchi yetu ina akiba ya chakula cha kutosha ambacho kina utoshelevu wa asilimia 124 kwa mwaka huu wa fedha 2018/19. Hivyo, Serikali haitarajii kutumia fedha za kigeni kuagiza chakula kutoka nje ya nchi isipokuwa tu kama ikitokea hali ya ukame ikawa mbaya katika siku zijazo.

Serikali, kupitia Benki Kuu ya Tanzania, inawataka wafanyabiashara ya huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kuzingatia na kutii Sheria ya Foreign Exchange 1992, Kanuni ya Foreign Exchange (Bureau de Change) Regulations 2015 na marekebisho ya mwaka 2017, Masharti ya biashara ya huduma ya kubadilisha fedha za kigeni na Maelekezo ya Msimamizi (BOT) wa Sekta ya Fedha Nchi. Mwisho Serikali inawapongeza wananchi wa Tanzania kwa kuwa waelewa na watulivu wakati wote zoezi la ukaguzi likiendelea, licha ya kujitokeza kwa taarifa za upotoshwaji wa zoezi hili.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu Ukaguzi wa Maduka ya kubadilisha Fedha za Kigeni ambapo alisema lengo lake sio kufuta biashara ya maduka hayo bali ni kudhibiti ukiukwaji washeria uliokithiri na utakasishaji wa Fedha haramu.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, akieleza kuwa jumla ya maduka 87 yamefanyiwa ukaguzi Jijini Dar es Salaam na ni maduka matano pekee ndio yamebainika kutokiuka sheria, wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (kushoto), wakiwa katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ambapo Waziri huyo alisema hakuna mmliki wa Duka la Kubadilisha Fedha ambaye amewasilisha malalamiko yoyote kwa mamlaka husika kuhusu zoezi la ukaguzi wa maduka hayo.
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, Sharon Sauwa, akiuliza swali kuhusu kufungwa kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni wakati wa Mkutano kati ya waandishi wa habari na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani) kuhusu ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akifafanua jambo wakati wa mkutano kati yake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu na Kamishna wa Sera wa Wizara hiyo Bw. Mgonya Benedicto .
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma. (Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

PRECISION AIR WAZINDUA SAFARI ZA NDEGE KUELEKEA DODOMA, KATAMBI AWAMWAGIA SIFA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma amezindua safari za ndege za Shirika la Ndege la Precision Air kutokea Dar es Salaam kwenda Dodoma leo April Mosi. 

Akizungumza baada ya Ndege aina ya PW 466 katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amesema sekta ya anga ni muhimu sana kwa maendeleo ya Jiji la Dodoma na kuja kwa shirika la Ndege la Precision Air kutaongeza zaidi fursa kwa watalii kuja kutembelea maeneo yaliyopo ndani ya Jiji na maeneo yaliyo karibu ikiwemo Kondoa.

Katambi amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli imetoa fursa ya ushindani kwa sekta binafsi na Precision Air ni moja ya wabia wakubwa wa maendeleo hususani kwenye masuala ya usafiri na imekuwa ikifanya kazi zake kwa muda mrefu na uaminifu mkubwa.

“Kwanza napenda kuwapongeza Shirika la ndege la Precision Air kwa uamuzi wa kuleta safari za kutokea Dar es salaam na kuja Dodoma na pia kutoka Dodoma kuelekea Kilimanjaro, hii kwetu ni fursa kubwa sana kwa maendeeo ya Jiji letu hususani kwenye sekta ya utalii kwani lengo letu ni kuhakikisha tunafikia malengo ya kuwa moja ya Jiji kubwa ndani ya Afrika Mashariki na Kati,”amesema 

“Tayari kuna ujenzi wa Uwanja mkubwa wa kimataifa  utakaokuwa unashuka ndege kubwa, Rais ameshatoa fedha na utajengwa Msalato sisi tumeshaleta Dreamliner na Airbus kwahiyo hata kama na nyinyi Precision Air mna ndege kubwa mnakaribishwa kuzileta,”amesema Katambi.

Amesema, angependa kuona Precision Air wakiboresha zaidi huduma zao kwa kuongeza safari za kuelekea maeneo tofauti ya Utalii kama Kigoma, Mwanza kwani fursa ya safari hizo zipo kutokana na Dodoma kuwa Jiji kwa sasa na watu wamekuwa na uhitaji wa safari hizo.

“Ndani ya Jiji la Dodoma kumekuwa na safari za Shirika la Ndege la Air Tanzania ila kwa sasa na nyie Precision mmekuja ninafurahi kwakuwa mmeweza kuongeza chachu ya maendeleo, mmerahisisha safari za wafanyakazi wetu pamoja na wageni wanaokuja kwenye ofisi za Serikali,”amesema Katambi.

Akizungumzia uzinduzi wa safari hizo Kaimu Mkurugenzi wa Precision Air, Patrick Mwanri amesema wanayo furaha kubwa kuchangia juhuhudi za Raisi wa awamu ya tano Dkt.John Joseph Pombe Magufuli na serekali yake katika kuundeleza na kuufungua mjii mkuu Dodoma pamoja na kuendeleza sekta ya anga.

“Kwa miaka 25 tumekuwa tukitekeleza jukumu la kuiiunganisha Tanzania na kuhakikisha abiria wanasafari kwa urahisi ndani na nje ya nchi. Safari zetu za Dodoma zitarahisisha shughuli za utawala na biashara kati ya Dodoma na Mikoa mengine na zaidi,”amesema Mwanri.

Pia tuanayo furaha kwa kuweza kuwapa abiria wetu uchaguzi mzuri wa muda wa kusafiri, kwa kuzingatia aina ya soko ni ukweli ulio wazi kwamba abiria wanahitaji uhuru katika kuchagua muda wa kusafiri na ndo maana tuna Ndege ya za Asubuhi na Mchana zikiwemo safari za saa 1:00 Asubuhi, Saa 3:25 Asubuhi na Saa 7:50 Mchana kwa safari za kutokea Dar es Salaam na Safari za saa 2:25 Asubuhi, saa 4:55 Asubuhi na saa 10:55 Alasiri kwa safari za Kutokea Dodoma. Aliongeza Bw. Mwanri

Mwanri amefafanua zaidi kuwa Precision Air itakua ikifanya safari zake moja kwa moja kwenda Dodoma kila Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Jumamosi, huku Kwa siku ya Alhamisi na Ijumaa safari hizo zitakua zikipitia Kilimanjaro.

Kwa upande wa Shirika la Ndege la Precision Air,  amesema amefurahi kwa mapokezi makubwa waliyoyapata ndani ya Mkoa wa Dodoma na kupewa heshima kubwa. Ndege hiyo ya Precision Air ilikuwa ikiendeshwa na Rubani Kapteni  Peter Fues akisaidiwa na Khalid Othman.

Shirika la Ndege la Precision Air lilianzishwa mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi, likifanya safari zake kusafirisha watalii katika vivutio vya utalii kama Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro pamoja na Visiwa vya Zanzibar. Sasa Shirika hilo lenye makoa yake makuu katika Jiji la Dar es Salaam limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika yanayo heshimika katika ukanda wa Africa Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas  Katambi (Wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Wa Shirika la Ndee la Precision Air Patrick Mwanri na wafanyakazi wa Shirika hilo waliokuja na ndege kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma baada ya uzinduzi wa safari hizo leo April Mosi
  kwenye Uwanja  wa Ndege wa Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi akipata maelekezo kutoka kwa Rubani Kapteni Peter Fues namna wanavyoendesha ndege mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege la Precision Air kutoka  Dar es Salaam kuelekea Makao Makuu ya nchi Dodoma leo kwenye Uwanja  wa Ndege wa Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi akisalimiana na Rubani Kapteni Peter Fues baada ya kutua kwenye Jiji la Dodoma wakati wa uzinduzi wa safari za shirika hilo kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma leo kwenye Uwanja  wa Ndege wa Dodoma..

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma akishuka kutoka kwenye Ndege ya Precision baada ya kuzindua safari za kutokea Dar es Salaam kuelekea Dodomaleo April Mosi leo kwenye Uwanja  wa Ndege wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Precision Air Patrick Mwanri akizungumzia uzinduzi wa safari za ndege kutokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma zitakazokuwa kuanzia siku ya Jumatatu hadi Jumamosi leo April Mosi  kwenye Uwanja  wa Ndege wa Dodoma., kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi.

WAZIRI BITEKO AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA MADINI OFISI YA MADINI CHUNYA

0
0
Na Emanuel Madafa, Mbeya
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko, ameagiza kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi wote ofisi ya madini Wilayani Chunya na kuagiza  kuwafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na kwa tuhuma za kushirikiana na wachenjuaji wa madini.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya , wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika ukumbi wa halmashauri ya Chunya.

Amesema, baada ya serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha inadhibiti mapato yake, utafiti umebaini kwamba Wilaya ya Chunya inashika namba moja kwa wizi na utoroshaji wa madini aina ya dhahabu ikifuatiwa na Kahama.

“Baada ya kufanya utafiti tumeabaini kunawizi mkubwa na usio na aibu ambapo unakuta mtu amepata kilo 1 na gramu 1620 lakini serikali inapata  gramu 208, lakini kuna mahali mtu anapata kilo nne anawasilisha taarifa za gramu 155,sasa wizi namna hii tukiendelea kunyamaza nchi haiwezi kuwa na afya.,”alisema.

Kutokana na hali hiyo Waziri Biteko  amewataka watendaji na viongozi husika kubadilika na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

“Ukiangalia sasa, wazalishaji wengi wanakimbilia Chunya na hii ni kwa sababu ya utaratibu wa eneo husika kushindwa kubaini wizi huu unaofanyika kupitia taarifa za kiwango cha uzalishaji ambacho ndicho kinachohalalisha mapato kwa serikali kupitia mrahaba wa Madini “Amesema Waziri Biteko

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, alimueleza Biteko kuwa Wilaya ya Chunya inahitaji msaada hasa wa kielimu na utaalamu wa madini na kuomba watendaji wasafi wapatikane kwenye sekta hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa sasa wanataka kuzungumza na uongozi wa Mkoa  wa Songwe  ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuimalisha Ulinzi katika maeneo hayo ili kuepusha wizi wa Madini.
Waziri wa Madini Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kabla ya kuanza ziara Wilayani Chunya Mkoani Mbeya. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila.



Balozi Seif aongoza mazishi ya mwakilishi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

0
0
Mamia ya Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Kisiwa cha Unguja Mjini na Vijijini leo wamehudhuria mazishi ya Mwakilishi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Marehemu Mbarouk Wadi Mtando yaliyofanyika kijijini kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Marehemu Mtando aliyewahi kuwa Mwakilishi wa lililokuwa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini “A”katika kipindi cha Mwaka 2005 hadi 2010 alifariki Dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbiji Mjini Da es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mazishi hayo yaliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulidi, Spika Mstaafu  Pandu Ameir Kificho, Naibu Katibu wa CCM Zanzibar Dr. Juma Abdullah Saadala {Mabodi}, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Viongozi Waandamizi wa Serikali pamoja na wale wa Vyama vya Kisiasa.

Marehemu Mbarouk Wadi Mtando ambae alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya Kisukari kwa kipindi kirefu amewahi kupatiwa matibabu Nchini India, akianzia tiba ya Maradhi yake katika Hospitali mbali mbali hapa Nchini.

Kama ilivyo kawaida ya mazingira ya Watoto wa Kitanzania Marehemu Mbarouk Wadi Mtando alipata mafunzo ya Elimu ya Dini na Dunia Kijiji kwao Mwajuni na baadae kujishughulisha na mambo ya Kibiashara na hatimae masuala ya Kisiasa yaliyompelekea kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni kwa kipindi kimoja.

Jamii itaendelea kumkumbuka Mwakilishi huyo wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni kutokana na ukarimu wake kwa Jamii uliompelekea kuwa Maarufu kutokana na moyo wake wa kisaidia bila ya kujali Rangi, Umri, Dini au Itikadi za Kisiasa.

Marehemu Mbarouk Wadi Mtando ametangulia mbele ya Haki baada ya kuitwa na Mwenyezi Mungu Subuhanahu - Wataalah kama walivyoitwa waliomtangulia na kuacha Wamilia ya Watoto kadhaa.

Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Marehemu Mbarouk Wadi Mtando mahali pema peponi. Amin.
 Viongozi wa Serikali, Siasa na Wananchi wakimsalia Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni Marehemu Mbarouk Wadi Mtando aliyefariki Hospitali ya Muhimbili Dar na kuzikwa Kijijini kwao Mkwajuni.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiteta na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulidi wakatiu wa mazishi ya Mwakilishi wa Zamani wa Jimbo la Mkwajuni Mbarouk Wadi Mtando Kijijini kwao Mkwajuni Mkoa Kaskazini Unguja. Wa Tatu Kushoto ya Balozi ni Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dr. Juma Abdullah Saadala { Mabodi }.
 Harakati za mazishi zikiendelea kwenye Viunga vya Kijiji cha Mkwajuni kuuhifadhi Mwili wa Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni Marehemu Mtando kwenye malazi yake ya kudumu.
 Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akimwaga dongo kwenye Kaburi alilozikwa Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni Marehemu Mbarouk Wadi Mtando.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifariji Familia ya Mwakilishi wa zamani wa Jimbo la Mkwajuni Marehemu Mbarouk Wadi Mtando mara baada ya mazishi yake Kijijini kwao Mkwajuni. Picha na – OMPR – ZNZ.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images