Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

UTABIRI WA HALI YA HEWA KW SAA 24 ZIJAZO


Taarifa ya Msiba

0
0
Taarifa ya Msiba

Habari za mchana.Taarifa fupi zilizotufikia muda mchache uliopita mtanzania mwenzetu aishie hapa Columbus Ohio *Stanley Mushi* amefariki dunia .

Marehemu hakuwa mwanamfuko hila kama jumuiya tunaombwa kushirikiana wote kwenye jambo hili.

Taratibu zingine na maelezo mengine tutawajulisha . Mungu amlaze mahali pema peponi.Amina!

TCCA

Uongozi.


BALOZI KARUME AWATAKA WATANZANIA KUSHIRIKI UTALII WA NDANI.

0
0
Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume amewataka Watanzania kutembelea sehemu za Vivutio vya Utalii na kuondokana na dhana kwamba utalii unafanywa na wageni tu.

Balozi Karume ameyasema hayo leo Wilayani Mbozi,Mkoa wa Songwe wakati alipotembelea eneo la urithi na uhifadhi ambapo kulidondoka KIMONDO chenye uzito wa tani 12 kinachokifanya KIMONDO hicho kinachopatikana Mkoa wa Songwe kuwa ni cha nane(8) duniani na cha pili Afrika kwa Uzito.

“Nimefurahishwa sana na Historia ya kimondo hichi,ni vyema Watanzania wengi zaidi wakatenga muda kuja kujifunza hapa.Ni jambo la kujivunia kidunia kuwa sehemu ya nchi zanye Vimondo vizito zaidi duniani”Alisema Balozi Karume.

Wakati huo huo Balozi Karume aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jenarali Mwangela,*Naibu Waziri Mavunde* na Naibu waziri wa Vijana SMZ Mh Lulu Mshamu kukagua maandalizi ya mwisho ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge Kitaifa zinazotarajiwa kuzinduliwa tarehe 2.4.2019 Mkoani Songwe.






Tanzania Yang’ara Suala la Amani Duniani, Yaongoza Afrika Mashariki, Yawa 10 Bora Barani Afrika

0
0
Taswira ya Tanzania kimataifa imeendelea kupaa baada ya Taasisi ya Global Peace Index (GPI) kuitangaza Tanzania kushika nafasi ya 51 miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani katika kipindi cha mwaka 2018. 

Tanzania imeshika nafasi hiyo ikiwa ni ya juu zaidi kufikiwa tangu mwaka 2010 na kuzishinda nchi kubwa duniani kama Marekani, China, Uingereza na Ajentina ambapo kwa Afrika ipo katika nafasi 10 bora na kuwa kinara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Tangu Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli iingine madarakani, Tanzania imekuwa ikipanda nafasi kila mwaka ambapo mwaka 2017 ilishika nafasi ya 54, mwaka 2016 nafasi ya 58 na mwaka 2015 nafasi ya 64. 

Kwa mujibu wa GPI, sababu zilizoipaisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani ni pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kupambana na rushwa, mgawanyo sahihi wa rasilimali, upatikanaji huru wa taarifa, mazingira wezeshi ya biashara, uhusiano mzuri na nchi za jirani, kiwango cha rasilimali watu, kuheshimu haki za watu wengine na ufanyaji kazi mzuri wa Serikali. 

“Nchi 71 zilikuwa na amani zaidi mwaka 2018 kuliko mwaka 2017”, inaeleza sehemu ya taarifa ya Global Peace Index na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi hizo 71 baada ya kushika nafasi ya 51 kulinganisha na nafasi ya 54 iliyoshika mwaka 2017. 

Akitoa maoni yake juu ya kupaa kimataifa katika suala la amani, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbasi, kupitia akaunti yake yaTweeter, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuienzi amani ya Tanzania. 

Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali amewapongeza wananchi na wadau wote waliotimiza wajibu wao katika kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani duniani. 

Taarifa hii ya 12 kutolewa na Global Peace Index ambayo huzipima nchi 163 kulingana na hali ya amani katika nchi hizo. Taasisi hii inaongoza na kuheshimika katika masuala ya kwa kupima hali ya amani katika nchi mbalimbali duniani. 

Serikali yatenga fedha za ndani kupeleka umeme wa Gridi Katavi

0
0
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla (wa kwanza kushoto) wakiwa katika Mkutano na wananchi wa Kijiji cha Kapalala (hawapo pichani) wakati walipofika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akizungumza na Bi. Salma Karamba, mkazi wa Kijiji cha Ifukutwa wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi ambaye ameunganisha umeme kwenye nyumba yake kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria kuwashwa rasmi kwa umeme katika Kijiji cha Ifukutwa wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa pili kushoto) akikagua mitambo ya umeme wa mafuta katika kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda wilayani Katavi. Kituo hicho kinazalisha umeme wa kiasi cha megawati 3.5.
Na Teresia Mhagama, Katavi
Imeelezwa kuwa, Serikali imetenga fedha za ndani, kiasi cha Dola za Marekani milioni 70 kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Katavi ambayo itawezesha Mkoa wa Katavi kuunganishwa na gridi ya Taifa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani mkoani Katavi wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme katika Wilaya ya Mpanda, Nsimbo na Tanganyika ambapo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla.

“Serikali imeamua kujenga mradi huu ili Mkoa wa Katavi uachane na kutumia umeme wa mafuta ambao ni ghali kwani shilingi milioni 21 zinatumika kila wiki kuendesha mitambo hii, hivyo gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa tofauti na mapato yanayoingia.” Alisema Dkt. Kalemani.

Alieleza kuwa, njia hiyo ya umeme ya kV 132 itakuwa na urefu wa kilometa 284 na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2020 kwani taratibu za ujenzi zimeshaanza.

Akiwa katika kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda, Dkt Kalemani alisema kuwa, mwaka jana kituo hicho kilikuwa na mashine mbili zenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2.6 lakini mwaka huu imeongezwa mashine ya tatu na kufanya kituo hicho kuwa na uwezo wa megawati 3.75, hivyo kukidhi mahitaji ya umeme ya Mkoa wa Katavi kwa sasa.

Aidha, Dkt Kalemani aliwapongeza wafanyakazi wa TANESCO katika Kituo hicho kwa kutumia shilingi milioni 100 tu kwa kazi ya uboreshaji wa kituo pamoja na uhamishaji wa mashine hiyo ya tatu ya kufua umeme ambayo ilikuwa wilayani Loliondo.

“ Nataka niwapongeze watumishi hawa wa TANESCO kwani Mkandarasi kutoka Uholanzi alisema kuwa gharama atakayotumia kwa ajili ya kazi hiyo ya uhamishaji wa mashine ni shilingi bilioni mbili lakini niliagiza wataalam wetu kuwa tuihamishe wenyewe na wametumia shilingi milioni 100 tu.” Alisema Dkt Kalemani.

Katika ziara yake wilayani Nsimbo, Waziri wa Nishati alikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Kapalala ambapo pia aliwasha umeme katika Kijiji hicho na kumuagiza mkandarasi kampuni ya CRCC kupeleka umeme katika vitongoji vyote vya Kijiji hicho.

Vilevile, katika ziara yake wilayani Tanganyika, Dkt Kalemani alikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Mchakamchaka na Ifukutwa na kuwasha rasmi umeme katika Vijiji hivyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Asaini Kitabu Cha Maombolezi

0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia saini Kitabu cha Maombolozo kwenye Ubalozi Mdogo wa Jamuhuri ya Msumbiji uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar kufuatia maafa yaliyotokea Nchini Msumbiji yaliyotokana na kimbunga kikali kilichosababisha Mafuriko.Kulia ya Balozi Seif aliyesimama ni Balozi Mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bwana Jorge Augusto Menezez.
Balozi Mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bwana Jorge Augusto Menezez Kushoto akimsindikiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kuweka saini Kitabu cha Maombolezo. Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema maafa yaliyowakumba Wananchi wa Msumbiji baada ya kukumbwa na kimbuka kikali kilichotokea Nchini humo Wiki iliyopita yamewagusa pia Watanzania walio wengi kufuatia uhusiano wa ujirani mwema uliopo kati ya Nchi hizo mbili.
Alisema ameshtushwa na tukio hilo lililoleta huzuni na simanzi kubwa kwa Familia kadhaa ya Wana Msumbiji waliopoteza roho zao kupitia vyombo vya Habari mbali mbali Duniani wakati akiwa safarini nje ya Nchi.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo alipofika Ofisi ya Ubalozi Mdogo wa Msumbiji iliyopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar kutia saini Kitabu cha Maombolezo kufuatia vifo vya Wananchi wa Msumbiji zaidi ya 500 vilivyotokana na Maafa yaliyosababishwa na Kimbunga hicho.
Alisema maafa hayo yaliyozigusa pia Nchi za Malawi na Zimbabwe yameleta hali ya kusikitisha iliyowaacha Wananchi wengi wa Msumbiji hasa wale walioko kwenye Mji wa Beira katika mazingita hatarishi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Balozi Mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar alizitaka Familia za Wananchi waliopatwa na misiba Nchini Msumbiji kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu cha maafa na maombolezo.
Akitoa shukrani zake Balozi Mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bwana Jorge Augusto Menezez ameendelea kuishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua yake ya mara moja iliyochukuwa katika kuipatia msaada wa dharura wa Kibinaadamu Nchi yake.
Balozi Jorge alisema Serikali ya Msumbiji kwa sasa iko katika harakati za awali za kurejesha miundombinu iliyoharibika kutokana na kimbunga hicho huku ikikaribisha kupokea misaada mbali mbali kutoka kwa washirika wao itakayotoa afueni kwa Jamii za Watu walioathirika kutokana na Maafa hayo.
Alisema katika kipindi hichi cha mpito jitihada zinaendelea kuchukuliwa katika kujiweka tayari kukabiliana na miripuko ya maradhi ya kuambukiza iwapo yatachomoza ambayo mara nyingi huibuka wakati yanapotokea maafa kama hayo.
Balozi Jorge alifahamisha kwamba idadi ya vifo vilivyoripotiwa kwa sasa inaeleza kufikia zaidi ya Watu Mia 500 ambayo Takwimu halisi kutokana na zilizaha hiyo inakisiwa kufikia zaidi ya Watu 1,000.
Alisema Mji wa Beira umeteketea kutokana na Kimbunga hicho kilichowaacha Watu zaidi ya Milioni Moja kukosa Makaazi baada ya Nyumba zao kukumbwa kabisa na Mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga hicho.
Balozi Jorge alieleza kwamba idadi ya Majengo ya Skuli yaliyoathirika kwa sasa yanakadiriwa kufikia Elfu 3,000, Wanafunzi Elfu 4,000 hivi sasa wamekosa Majengo ya kusomea, Hospitali 45 zimebomoka na Mashamba ya Kilimo yapatao Laki 450,000 yameharibika kabisa.

WAZIRI WA KILIMO AFUNGUA MKUTANO MKUU TFA

0
0
Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga akizungumza katika mkutano mkuu wa TFA uliofanyika jijini Arusha

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanganyika Peter Sirikwa akizungumza katika mkutano mkuu wa TFA


Viongozi wa TFA wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga



Na Vero Ignatus,Arusha.

Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga amefungua mkutano mkuu wa wanahisa wa Chama cha Wakulima la Tanganyika (TFA) kilichowakutanisha wadau wa kilimo na wanahisa kwa pamoja ili kujadili maendeleo ya kilimo

Hasunga ameipongeza TFA kwa juhudi wanazozifanya katika kukuza sekta ya kilimo nchini ambayo ni kiinua mgongo na imeajiri watu wengi zaidi ya asilimia 80% ya Watanzania.

Akizungumza katika mkutano huo ambao uliambatana na utoaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wakulima hao .Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na TFA katika kutatua changamoto za wakulima ili kuboresha sekta ya kilimo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima TFA Peter Sirikwa amesema kuwa TFA iko mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini na kuwanganisha wadau wa kilimo kwa pamoja .

SGR KIPANDE MORO-MAKUTUPORA WAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 7, TAZAMA HANDAKI TRENI ITAKAPO PITA


WASAIDIZI WA KISHERIA WAPEWA MAFUNZO YA SHERIA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE MASOKO

0
0
Jumla ya Wasaidizi wa Kisheria 36 katika Masoko ya Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya sheria na Shirika la Agape AIDS Control Programme ili wakasaidie kutoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara kwa lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake wafanyabiashara sokoni. 
Mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu katika Ukumbi wa Katemi Hoteli Mjini Shinyanga yamefungwa leo Jumapili Machi 31,2019 na Mkurugenzi wa shirika la Agape,John Myola. 
Myola amesema katika mafunzo hayo,Wasaidizi wa Kisheria wamepewa elimu kuhusu sheria mbalimbali na kutambua haki za binadamu,haki za kiuchumi,jinsi ya kufanya biashara,ukatili wa kijinsia na mahali sahihi pa kutoa taarifa za vitendo vya kikatili. 
Amesema mafunzo hayo ni Mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” kwa lengo la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabishara katika masoko unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 
“Naomba mafunzo haya mliyopata yatakuwa msaada kwenu binafsi lakini pia nendeni mkawasaidie wananchi,katoeni huduma bila upendeleo na bila kuonea mtu ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anapata haki sokoni”,alisema Myola. 
“Nawashauri pia kutunza siri za watu,msiwe waoga kutatua migogoro inayotokea sokoni,naamini mtakuwa mstari wa mbele kupiga vita dhuluma mbalimbali ikiwemo rushwa ya ngono na kuwapigania akina mama na wasichana ambao wana maumivu ya kutendewa vitendo vya kikatili”,aliongeza Myola. 
Aliyataja masoko ambako mradi huo unatekelezwa katika manispaa ya Shinyanga kuwa ni soko Kuu Mjini Shinyanga,Kambarage,Nguzo Nane,Ibinzamata,Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Sheria ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria ili wakataokwenda kutoa elimu kwa wafanyabiashara kwenye masoko yaliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ili kukabiliana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akiwasisitiza Wasaidizi wa kisheria kutumia mafunzo waliyopata kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko.
Wasaidizi wa Kisheria kwenye masoko wakimsikiliza Myola.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Awali Afisa Masoko Manispaa ya Shinyanga,Alex Hinda akitoa mada kuhusu namna bora ya kufanya biashara na kuwataka wafanyabiashara kujitahidi kutunza taarifa zao za fedha.
Afisa Masoko Manispaa ya Shinyanga,Alex Hinda akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa ukumbini.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa ukumbini.
Wasaidizi wa Kisheria wakifanya Mtihani wa kipimo cha uelewa wa mafunzo waliyopatiwa kwa kipindi cha siku tatu kuhusu masuala mbalimbali ya sheria ili kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wasaidizi wa Kisheria wakifanya mtihani.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo kufungwa.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo kufungwa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Nyongo (pichani) aamuru kuanzishwa kwa soko la madini Kahama, Chunya, Musoma na Singida kudhibiti utoroshwaji madini

0
0
Na Greyson Mwase, Kahama
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (pichani) ameelekeza soko la madini katika mkoa wa kimadini wa Kahama ikiwa ni pamoja na maeneo mengine ya Chunya, Musoma, Singida kuanzishwa mara moja ili kudhibiti utoroshwaji wa madini unaopelekea Serikali kukosa mapato yake.
Naibu Waziri Nyongo ameyasema hayo leo tarehe 31 Machi, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mjini Kahama. Wengine waliokuwepo katika mkutano huo ni pamoja na Kamishna Msaidizi, Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini,  Ali Saidi Ali, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Andrea Fabian pamoja na wataalam kutoka Tume ya Madini.

Alisema kuwa, mara baada ya kufanya ziara yake ya siku moja katika Wilaya ya Kahama, alibaini kumekuwepo na udanganyifu mkubwa katika shughuli za uchenjuaji wa madini huku akitolea mfano wa kampuni ya Busami inayojihusisha na uchenjuaji wa madini ya dhahabu.
Alisisitiza kuwa, alibaini kumekuwepo na udanganyifu kwenye uzito na kiwango halisi cha dhahabu kwenye madini yaliyopatikana hali inayopelekea Serikali kukosa mapato yake stahiki.
“Kwa mfano katika mtambo wa kuchenjua dhahabu unaomilikiwa na kampuni ya Busami tumebaini kuna udanganyifu kwenye uchenjuaji, jana baada ya kufika na kuona namna uchenjuaji wa madini unavyofanyika na kuelekeza wataalam wa madini kuchenjua upya mchanga uliokuwepo kwenye maji yaliyohifadhiwa, tulibaini kuna madini," alisema Nyongo

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo alisimamisha shughuli za uchenjuaji katika kampuni ya Busami na kutaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mmiliki wake.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Nyongo alielekeza wamiliki wote wa mitambo  ya kuchenjulia madini ya dhahabu nchini kuhakikisha wanakuwa na mizani na mashine maalum za kupimia madini ya dhahabu zilizoidhinishwa na Wakala wa Vipimo Tanzania, na biashara ya madini kufanyika katika masoko ya madini yaliyoanzishwa na kusisitiza kuwa lazima madini yajulikane yanapopelekwa na Ofisi za Madini Nchini kuhakikisha zinatuza kumbukumbu sahihi.
Wakati huo huo Naibu Waziri Nyongo aliagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya kufuatilia iwapo hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya kampuni inayojihusisha na uchenjuaji wa madini ya dhahabu Wilayani Kahama ya Jema baada ya kukamatwa ikifanya udanganyifu hivi karibuni.

DC KIBONDO AWAONYA WANA CCM WATAKAPOKEA RUSHWA KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilayani Kibondo mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kupokea rushwa kwa baadhi ya viongozi wanaotaka kwenda kugombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Rai hiyo ilitolewa juzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa Chama hicho kwa ngazi ya tawi, kata na jumuiya hasa namna gani ya kuongoza ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Louis Bura  aliwataka kuwaacha wananchi kuchagua kiongozi aliebora na si kumpendekeza kiongozi ambae amepita na kuwagawia rushwa katika kata zao.

Alisema Katika kuelekea uchaguzi mwaka huu na mwaka 2020 ni lazima viongozi wa chama wanakuwa makini na viongozi wanaotaka Kugombea kwa kuwa watapita mitaani kuwashawishi kwa kuwa wao ndio wapiga kura wa kwanza , na kuwataka viongozi hao kuacha kuchochea kiongozi furani apitishwe kwakuwa katoa hela kiongozi mtoa rushwa hafai katika uchaguzi huu kwa kuwa anakuwa ana lengo lq kuja kujitengenezea masilah yake binafsi.

"Tunafahamu wapo baadhi ya watu wanaotaka kugombea wanapita wanawashawishi muwachague niseme tu kwa yeyote tutakae mkamata hatutasita kumuadhibu na ikiwezekana tutashirikiana na viongozi wa chama kumfuta kabisa katika watu wanaogombea hatutaki viongozi wanaotoa rushwa kiongozi apite kwa kujiamini mwenyewe na kuaminiwa na Wananchi", alisema Bura.

Akiwakaribisha watoa mada walioandaliwa Katibu Wa CCM Wilaya ya Kibondo Stanley Mkandawile aliwataka viongozi wa matawi na kata kuwa wakweli kutoa tathimini za kweli ni mgombea gani anakubalika na  Wananchi ilikuhakikisha  wanakipatia ushindi wa kutosha chama.

Alisema viongozi wanaotoa fedha kuwashawishi wapiga kura kuwachagua hawafai na viongozi ambao hawakubaliki kwa Wananchi hawafai lazima viongozi wa chama wa kata na matawi, kupita kwa Wananchi kujua ni kata gani Chama kina mgombea ambae anakubalika na kata gani ambako kunachangamoto kiongozi aliepo hakubaliki.

Aidha Mkandawile alisema lengo la chama ni kuhakikisha kata 19 na vijiji vyote vya kata hizo wanapata ushindi pamoja ilikufanikisha hilo ni lazima  viongozi kupata idadi ya Wanachama waliopo katika kata zao na kutatua kero zote ambazo zinaweza kusababusha Chama kukosa ushindi.

Katibu Kata ya Misezero Benjamini  Mlinjie  alisema Semina ya kuwajengea uwezo imeweza kuwafungua  fikira za uongozi na mpaka sasa wamejipanga kushirikiana na TAKUKURU  kuwafichua wale wote wasiojiamini na wanataka kutoa rushwa iliwapitishwe.

Alisema wapo baadhi wanatabia hizo na kwa sasa Watahakikisha viongozi wote wanaopita wanauwezo wa kuongoza na Wanapita kutokana na Wananchi wanavyo wakubali na sio kwasababu ya kutoa rushwa.

Alisem wako tayari kumuunga Mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa kuhakikisha chama kinapata viongozi waadilifu na wanaokubalika na Wananchi kwa kuwa chama kinahazina ya kutosha.
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Louis Bura akizungumza na Viongozi wa CCM Wa Wilaya ya Kibondo
 Katibu Wa CCM Wilaya ya Kibondo Stanley Mkandawile akiwakaribisha watoa mada walioandaliwa huku akiwataka viongozi wa matawi na kata kuwa wakweli kutoa tathimini za kweli ni mgombea gani anakubalika na  Wananchi ili kuhakikisha  wanakipatia ushindi wa kutosha chama chao.
 Baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Kibondo Wakiwa katika Semina ya kujengewa uwezo wa uongozi

MAHAFALI YA 35 CHUO KIKUU HURIA YAFANYIKA KITUO CHA ARUSHA

0
0
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro akizungumza kwenye mahafali ya 35 katika chuo Kikuu Huria Jijini Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro akizungumza kwenye mahafali ya 35 katika chuo Kikuu Huria Jijini Arusha, kushoto kwake ni makamu mkuu wa chuo hicho kwa tawi la Arusha Marcel Masalu
Naadhibya wahitimu wa Chuo Kikuu huria Kituo cha Arusha kama wakiwa kwenye magafali
Bi Joyce Bendera akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Daqqaro mara baada ya kuhitimu masomo yake kagika chuo kikuu huria kituo cha Arusha. 
 Ndugu Godfrey Mmassy Kipokea cheti mara baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu yake ya Master of monitoring and Evaluation (M&E) katika chuo kikuu huria kituo cha Arusha. 
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 35 ya Chuo kikuu huria Kituo cha Arusha, mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro, viongozi wa juu wa chuo kikuu huria, na viongozi wa serikali ya wanafunzi, pamoja na mwenyekiti wa chama ctawala mkoa wa Arusha Aloota Sanare. 

Na. Vero Ignatus, Arusha. 

Katika kufanikisha ujenzi wa Tanzania ya viwanda wasomi wametakiwa kutumia elimu yao kuweza vizuri kwa kuweza kujiajiri na kutoa fursa kwa watu wengine kuliko kutegemea kuajiliwa hali inayosababisha kuendelea kuzorota kwa uchumi wa nchi 

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro kwenye mahafali ya Chuo Kikuu Huria Tanzania tawi la arusha ambapo amewasisitiza wahitimu hao kuweza kuenda kulitumikia taifa lao kwa weredi utakao lisogeza taifa katika uchumi wa kati

Pamoja na hayo makamu mkuu wa chuo hicho kwa tawi la Arusha Marcel Masalu amesema wanafunzi waliohitimu masomo yao mwaka 2017/18 ni 145 kwa Arusha peke yake. 

 Masalu amesema Chuo hicho ndicho pekee cha Elimu ya juu Tanzania kinachotoa kozi kwa njia ya Cheti, Estashahada, Stashahada, Shahada za uzamili (Masters) na Uzamili PHD kwa njia ya masafa. 

Aidha mewataka wahitimu hao kuweza kukitangaza chuo hicho huko wanapokwenda kwa kufanya kazi zao kwa ufasaha 

Kwa upande wawanafunzi hao waliohitimu wameeleza changamoto wanazozipata ikiwa nipamoja na upungufu wa madarasa pamoja na majengo ya walimu hali inayosababisha mrundikano wawanafunzi wengi.

Nae Ndugu Godfrey Mmassy aliyehitimu  elimu yake ya Master of monitoring and Evaluation (M&E) amesema mtu yeyote akiamua kusoma akiwa kazini inawezekana kabisa ni maamuzi ya mtu binafsi. 

Smart Lab, XPRIZE, WFP, and DTBi partner to host “Education in 2030” workshop

0
0
The Chief Executive Officer of XPRIZE, Anousheh Ansari speaking during a Corporate to Founder panel discussion at the the "Education in 2030" workshop, The CEO of Smart Codes/Smart lab, Edwin Bruno (right) and left are Dr. George Mulamula (CEO DTBi), Iku Lazaro (Founder & General Manager, Shule Direct. 
The Chief Executive Officer of Smart Codes/Smart lab, Edwin Bruno speaking during the workshop, from right are Anousheh Ansari (CEO XPRIZE) , Dr. George Mulamula (CEO DTBi), Iku Lazaro (Founder & General Manager, Shule Direct, Christine Lucas (Vodacom Tanzania Foundation, and Sharon Nsule, Program Manager SmartLab during a Corporate to Founder panel discussion at the the "Education in 2030" workshop 

BY STAFF REPORTER

Smart Lab in partnership with XPRIZE, World Food Program (WFP), and Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) hosted a workshop themed “Education in 2030” in order to mobilize different stakeholders in education to generate a business model out of Global Learning XPRIZE. 


The workshop hosted March 29, 2019, was one of the concluding events for the innovation week organized by HDIF in Dar es Salaam.

Speaking after the event, Chief Executive of Smart Codes/ Smart Lab said Tanzania said the aim of the workshop also was to find inspiration from other different educational technologies that are already operating in Tanzania.

“The workshop followed the Global Learning XPRIZE 15-month pilot, which has tested 5 different offline software applications on tablets with 2700 children in Tanga region, Tanzania to identify which of the applications best allows out-of-school children to teach themselves basic reading, writing and arithmetic skills and it fell in line with Smart Lab’s series Corporate to Founders that aims at bringing different stakeholders in the corporate world and innovation ecosystem to see the potential of working together and deploying innovative solutions that will impact the community,” he said.

The Chief Executive of (DTBi), Dr. George Mulamula which were the facilitators of the workshop also added that the workshop brought together award-winning ed-tech startups from Tanzania, who presented their solutions.

“We have shared their vision to create an inclusive, innovative and equitable education system, joined by Telecom companies including Vodacom Tanzania, government representatives, development partners and education and research institutions who collectively envisioned how the education system in 2030 in Tanzania should be designed to promote SDG4, inclusive and quality education for all.

“Anousheh Ansari (CEO XPRIZE) and Dr. George Mulamula (CEO DTBi) were the facilitators of the workshop and led the visioning, strategizing and goal-setting, while Edwin Bruno (CEO, Smart Codes/Smart lab), Christine Lucas (Vodacom Tanzania Foundation), Iku Lazaro (Founder & General Manager, Shule Direct) together with Anousheh,” he added.

Speaking during the event the representatives from the main organizers Smart lab, XPRIZE, World Food Program (WFP), and DTBi, Dr. George said that they were excited and glad to be a part of envisioning forward-thinking, scalable solutions to achieving SDG4 by 2030 in Tanzania, leading the way for the rest of the world to adopt their own models.

He said by the end of the Global Learning XPRIZE project, the winning technology will be an open source, global, and multilingual software envisioned as a resource for Tanzania (and the world) to build upon

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL MOSI,2019

NAIBU WAZIRI NYONGO AFUNGA MITAMBO YOTE YA KUCHENJULIA MADINI KAHAMA

0
0

Kutoka kulia, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha wakiangalia steel wire iliyokuwa na mabaki ya kaboni yaliyonasa, kwenye ziara yake ya kushtukiza katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group tarehe 31 Machi, 2019.
Kutoka kushoto Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha wakishuhudia kaboni ikichomwa ili kupata dhahabu katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group tarehe 31 Machi, 2019.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na vyombo vya habari juu ya maamuzi ya Serikali kuhusiana na udanganyifu uliofanywa na kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group



Na Greyson Mwase, Kahama

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amefunga mitambo yote ya kuchenjulia madini ya dhahabu Wilayani Kahama baada ya kubaini udanganyifu mkubwa kwenye uchenjuaji wa madini.

Naibu Waziri Nyongo amechukua hatua hiyo kwenye ziara yake aliyoifanya mapema leo tarehe 31 Machi, 2019 Wilayani Kahama yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Kamishna Msaidizi, Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Saidi Ali, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Andrea Fabian, wataalam kutoka Tume ya Madini, wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari.

Akiwa katika ziara hiyo, alifanya ziara ya kushtukiza katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group inayomilikiwa na Theogenes Zacharia pamoja na mwenzake aliyejulikana kwa jina la Antidius na kubaini kampuni hiyo imekuwa ikiwaibia wateja wake kupitia mfumo wa uchenjuaji wa madini ya dhahabu.

Akiwa ameambatana na msafara wake mara baada ya kuwasili katika kampuni hiyo alioneshwa na wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini waliopewa kazi maalum ya kuchunguza mfumo wa uchenjuaji wa dhahabu wa kampuni hiyo, sehemu ya mabomba ya mfumo iliyoharibiwa kwa makusudi kwa lengo la kunasa kiasi cha dhahabu kabla ya kufikishwa katika chombo maalum cha kupokelea kwa ajili ya mteja.

Alisema kuwa, kiasi cha kaboni iliyokuwa na dhahabu iliyokamatwa ilipelekwa kwa ajili ya kuchenjuliwa ili kubaini kiasi cha adhabu kilichokuwa kimeibiwa na kusisitiza kuwa baada ya kuchenjuliwa kiasi cha gramu 102 kiligundulika kutaka kuibwa.

Katika hatua nyingine mbali na kufunga mitambo ya kuchenjua madini ya dhahabu katika Wilaya ya Kahama, Naibu Waziri Nyongo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya ya Kahama kuhakikisha watuhumiwa wote wa kampuni ya Ng’ana Group wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama na uchunguzi kuanza mara moja.

Katika hatua nyingine, Nyongo alisema kuwa maafisa madini wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama wataanza kufungua mtambo mmoja mmoja wa kuchenjua madini ya dhahabu mara baada ya kujiridhisha na uendeshaji wake.

Awali akielezea siri ya wizi unaofanywa na kampuni ya Ng’ana Group, mmoja wa wateja kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Joseph Magunila & Partners, aliyepeleka kaboni kwa ajili ya kuchenjuliwa ili kupata madini ya dhahabu, Wema Shibitali alisema kuwa, wakati zoezi la uchanjuaji likiendelea alishangaa kupata kiasi kidogo cha dhahabu tofauti na kaboni iliyokuwa imewekwa.

Alisimulia kuwa aliomba maafisa kutoka vyombo vya dola kufungua mfumo ili kubaini kama kuna madini yamebaki na kuongeza kuwa mara baada ya mfumo kufunguliwa walibaini kiasi kikubwa cha kaboni kilichokuwa kimebaki kwenye mfumo.

Aidha Shabitali aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuwatetea wachimbaji wadogo kwa kuwa wamekuwa wakiibiwa na wachenjuaji wa madini ya dhahabu kwa muda mrefu.

Wakati huo huo akizungumza katika msafara huo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha mbali na kumpogeza Naibu Waziri Nyongo kwa kutembelea Wilaya yake na kushughulikia changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Madini, alisema kuwa ziara hiyo imewapa mwanga zaidi wa mbinu zinazotumiwa na wachenjuaji wa madini na kusisitiza kuwa ataendelea kusimamia kwa karibu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aliwataka wachimbaji na wachenjuaji wa madini nchini kuunga juhudi zinazofanywa na Rais wa Awamu ya Tano pamoja na Serikali yake, Dkt. John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za madini kwa kuwa waaminifu kwenye ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.

WAKULIMA WA TUMBAKU WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWALETEA FAO LA MATIBABU

0
0


Mmoja wa wakulima wa tumbaku katika kijiji cha kasokola akichambua zao hilo
Baadhi ya wakulima wa kasokola wakisiliza elimu ya Bima ya Afya kutoka kwa wataalamu wa mfuko huo
Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Juma Michael akitoa elimu juu ya mpango wa ushirika afya kwa wakulima wa chama cha ushirika kasokola
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Katavi Luhigiza Sesemkwa akizungumza na wakulima katika kijiji cha Kasokola

……………………………..


Na Ripota Wetu… Katavi


Wakulima wa zao la tumbaku katika kijiji cha Kasokola katika halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameishukuru serikali kwa kuwaanzishia mpango wa Ushirika Afya; unaosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya; utakaowawezesha kupata matibabu kwa urahisi bila malipo kwa kipindi cha mwaka mzima; na hivyo kuwezesha familia zao kupata matibabu na kuondokana na adha ya kutegemea dawa za kienyeji pindi wanapougua kutokana na kukosa fedha za matibabu

wakulima hao wametoa shukurani hizo katika mkutano mkuu wa sita wa chama cha msingi cha ushirika cha kasokola ambapo walisema mpango huo utaondoa adha ya kushindwa kutibiwa kwa kukosa fedha hasa katika msimu ambao sio wa mavuno

Bwana Hussein Mobi ni mmoja wa wakulima wa tumbaku katika kijiji hicho, alisema mwaka uliopita alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tumbo na alitumia gharama kubwa lakini ujio wa mpango huo utakuwa mkombozi kwa wakulima walio wengi

Aidha wakulima hao walikitaka chama hicho kuandaa utaratibu wa kuwakata fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kuchangia mfuko wa bima ya afya

Akizungumzia mpango huo uliozinduliwa rasmi na waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa Julai mwaka jana; Mrajis Msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Katavi bwana Luhigiza Sesemkwa amesema serikali imeona iko haja ya kuwajumuisha wakulima katika fao la matibabu

Naye afisa masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya bwana Juma Michael alitaja baadhi ya faida za mfuko huo kuwa ni pamoja na kuwa na hakika ya kupata matibabu wakati wowote kwa zaidi ya vituo 7000 vya afya hapa nchini na hospitali mbalimbali

Aliongeza kuwa kwa sasa shirika linafanya zoezi la kutoa hamasa kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchi nzima ili wapate kuelewa umuhimu wa mfuko huo na kujiunga nao

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Katavi Bwana Said Juma alisema wakulima wa mazao matano ya kimkakati ikiwemo pamba, kahawa, korosho, chai na tumbaku wanahusishwa na mpango huo kuipitia vyama vya ushirika

Ametoa wito kwa wakulima kujiunga na mfuko ili kuondoa mashaka ya kupata matibabu pale wanapougua wakati familia hazina fedha hasa ukizingatia kuwa wakulima wanapata fedha kwa msimu wa mauzo ya mazao yao

WASAIDIZI WA KISHERIA WAPEWA MAFUNZO YA SHERIA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE MASOKO

0
0
Jumla ya Wasaidizi wa Kisheria 36 katika Masoko ya Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya sheria na Shirika la Agape AIDS Control Programme ili wakasaidie kutoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara kwa lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake wafanyabiashara sokoni. 

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu katika Ukumbi wa Katemi Hoteli Mjini Shinyanga yamefungwa leo Jumapili Machi 31,2019 na Mkurugenzi wa shirika la Agape,John Myola. 

Myola amesema katika mafunzo hayo,Wasaidizi wa Kisheria wamepewa elimu kuhusu sheria mbalimbali na kutambua haki za binadamu,haki za kiuchumi,jinsi ya kufanya biashara,ukatili wa kijinsia na mahali sahihi pa kutoa taarifa za vitendo vya kikatili. 

Amesema mafunzo hayo ni Mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” kwa lengo la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabishara katika masoko unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

“Naomba mafunzo haya mliyopata yatakuwa msaada kwenu binafsi lakini pia nendeni mkawasaidie wananchi,katoeni huduma bila upendeleo na bila kuonea mtu ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anapata haki sokoni”,alisema Myola. 

“Nawashauri pia kutunza siri za watu,msiwe waoga kutatua migogoro inayotokea sokoni,naamini mtakuwa mstari wa mbele kupiga vita dhuluma mbalimbali ikiwemo rushwa ya ngono na kuwapigania akina mama na wasichana ambao wana maumivu ya kutendewa vitendo vya kikatili”,aliongeza Myola. 

Aliyataja masoko ambako mradi huo unatekelezwa katika manispaa ya Shinyanga kuwa ni soko Kuu Mjini Shinyanga,Kambarage,Nguzo Nane,Ibinzamata,Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Sheria ya siku tatu kwa Wasaidizi wa Kisheria ili wakataokwenda kutoa elimu kwa wafanyabiashara kwenye masoko yaliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ili kukabiliana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akiwasisitiza Wasaidizi wa kisheria kutumia mafunzo waliyopata kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko.
Wasaidizi wa Kisheria kwenye masoko wakimsikiliza Myola.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape,John Myola akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Awali Afisa Masoko Manispaa ya Shinyanga,Alex Hinda akitoa mada kuhusu namna bora ya kufanya biashara na kuwataka wafanyabiashara kujitahidi kutunza taarifa zao za fedha.
Afisa Masoko Manispaa ya Shinyanga,Alex Hinda akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa ukumbini.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa ukumbini.
Wasaidizi wa Kisheria wakifanya Mtihani wa kipimo cha uelewa wa mafunzo waliyopatiwa kwa kipindi cha siku tatu kuhusu masuala mbalimbali ya sheria ili kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni.
Wasaidizi wa Kisheria wakifanya mtihani.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo kufungwa.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo kufungwa.icha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KILIMANJARO SAR WATIMIZA MWAKA MMOJA,WATANGAZA KUTOA HUDUMA BURE YA UOKOAJI KWA WAONGOZA WATALII MLIMA KILIMANJARO

0
0
Kikosi cha uokoaji kwa kutumia Helkopita kikiwa katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa msaada kwa wageni .
Ndege aina ya Helkopta inayotumiwa na Shirika la Kilimanjaro SAR katika kufanya shughuli za uokoaji katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shrika la Kilimanjaro SAR,Ivan Brown akitoa taarifa za shirika hilo kwa  wanahabari (hawapo pichani) kuhusu shughuli mbalimbali za uokoaji ilizofanya katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu katika shirika la Kilimanjaro SAR,Amour Abdalah akizungumza na wanahabari (hawapo pichani kuhusu mwaka mmoja wa operesheni ya shirika hilo.

Na Dixon Busagaga wa globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


SHIRIKA la Kilimanjaro SAR linayojishughulisha na utoaji wa huduma ya utafutaji na uokoaji wa watalii wanaopata matatizo ya kiafya katika maeneo yenye muinuko ikiwemo  Mlima Kilimanjaro limetangaza kutoa bure huduma zake kwa  waongoza watalii  pamoja na wapagazi .

Hatua hiyo imefikiwa baada ya  baadhi ya watu wanaojishughulisha na shughuli za kusaidia wageni katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kupata matatizo ya kiafya na kushindwa kupata huduma huku kundi kubwa la watu hao kukosa  Bima za Afya ,wengine wakikosa kabisa kipato cha uhakika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Kilimajaro SAR,Ivan Brown alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya shughuli zilizofanywa na kampuni hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza operesheni za uokoaji kwa kutumia njia ya Helkopta.

“Sisi ni wa kwanza na pekee katika Dunia hii tunaotoa huduma ya uokoaji Bure kwa wote wanaofanya shughuli za mlima ,tunafahamu Wapagazi,Waongoza watalii hawana bima, hawana njia zozote za kujipatia kipato ambazo zingesaidia katika uokoaji”alisema Brown .

“Watakaopata matatizo ya kiafya au ajali wawapo  mlimani wanaweza kuwasiliana nasi ,tutaaenda juu na kumuokoa bila ya gharama zozote kwa sababu mipango yetu ni kuokoa maisha ,ndio sababu tunasema kwa waongoza watalii au wapagazi , uhai ndio kipaumbele cha kwanza”aliongeza Brown .

Alisema shirika hilo likiwa linaadhimisha mwaka mmoja wa utoaji huduma katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tayari imetoa matibabu kwa zaidi ya watu 250 huku akieleza kuweka rekodi ya kwanza Afrika kwa kumuokoa mgonjwa aliyekuwa katika hali mbaya ,umbali wa Mita 5000.

 “ Tayari tumetoa huduma kwa zaidi ya wagonjwa 250 na miongoni mwao aliingia kwenye historia Afrika ya kuwa mtu wa kwanza kuokolewa kwa na Helkopta katika eneo lenye urefu wa Mita 4800 ,katika kambi ya Cosovo Mlima Kilimanjaro June 22 mwaka jana”alisema Borown .


“Tumeokoa waongoza watalii na wapgazi 50 bila malipo ,bado tunashukuru kwa ushirikiano na msaada  kutoka kwa taasisi mbalimbali kwa kuruhusu mazingira kwa shirika letu kuweza kufanya shughulizaek za uokoaji maisha kwa urahisi.

Mbali na shughuli ya utafutaji na uokoaji ,Kampuni ya Kiliamanjaro SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph kwa kuanzisha Kliniki ya kisasa  “Kilimanjaro SAR High Altitude Medicine Clinic” kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu kwa magonjwa yatokanayo na muinuko .

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa shirika hilo ,Amour Abdalah alisema kliniki hiyo ya kwanza Afrika imeanzishwa baada ya kubaini kwamba mgonjwa anapookolewa kutoka mlimani anahitaji pia kupata huduma stahiki za matibabu .

“Magonjwa ya mlimani yanahitaji ,matibabu maalumu ,na ndio sababu tukaanza na operesheni ya kutoa huduma kwa kutumia Helkopta ikiwa ni huduma ya kwanza kwa afrika na baadae mgonjwa huyu hufikishwa katika kliniki yetu na kupatiwa matibabu”alisema Abdalah.

Alisema wazo la kuanzishwa huduma hizo lilianza mwaka 2013  baada ya kuona kwamba utoaji wa huduma sahihi ya uokoaji na vifaa vya kitabibu vilihitajika na si pekee kwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro bali pia kwa Sekta ya Utalii Tanzania.

Abdalaha alisema kwa sasa kampuni ya Kilimanjaro SAR imepanua wigo wa utoaji wa huduma za utafutaji na uokoaji katika maeneo mengine zikiwemo hifadhi za taifa za Serengeti,Arusha,Manyara,Ruaha na Mikumi.

 “Mlima Kilimanjaro umekuwa na wageni wengi wakifanya shughuli za utalii ,na wengi wao baada ya kuapanda mlima Kilimanjaro wanaendelea na safari nyingine kutizama vivutio vya utalii,jambo kubwa tunalofanya katika sekta ya utalii ,tumewahakikishia usalama wageni wanaokuja Tanzania kupanda Mlima Kilimanjaro “alisema Amour.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Shirika la uokoaji ya Kilimanjaro SAR tayari imejinyakulia tuzo tano za uongozi moja ikiwa ni ya Tanzania ambazo ni “C.E.O of the Year 2018 Afrika “ ,“ H.R of the Year 2018 Afrika” ,“Dream Company to work for “ , “Employer Brand Afrika “  ,” Shirika Bora la kati Tanzania “ tuzo iliyotolewa na ATE .

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO KATI YA KAMATI YA UONGOZI NA KAMATI YA BAJETI BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aongoza Kikao cha Mashauriano kati ya Kamati ya uongozi na Kamati ya Bajeti kuhusu Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta, Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, 31 Machi, 2019. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Mawaziri wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia kwa Spika)

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI NA KAMATI YA BAJETI

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Machi 31, 2019 kushiriki katika Kikao cha Mashauriano kati ya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti kuhusu mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara kilichofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na katikati ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, William Tate Ole Nasha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Machi 31, 2019 alishiriki katika Kikao cha Mashauriano kati ya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti kuhusu mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara kilichofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza katika Kikao hicho.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images