Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live

SPIKA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAJUMBE KAMATI YA NISHATI NA MADINI

$
0
0


SPIKA 2
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya madini wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, mafunzo hayo yamefanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
SPIKA 5
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa mgeni ramsi katika semina ya wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya madini wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ,kulia kwake ni Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko  na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati  na Madini Mhe, Dunstan Kitandula. Semina hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI

$
0
0


V25A7464
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence Mattli alipomtembelea leo Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
V25A7482
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence Mattli baada ya mazungumzo yaliyofanyika  leo Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. 
V25A7426
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Ndg. Florence Mattli alipomtembelea leo katika Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

DC RUANGWA AWATAKA WACHIMBAJI NAMUNGO KUZINGATIA SHERIA

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (kushoto), akisalimiana na Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kusini, Bw. Eliamini Mkenga (katikati), mara baada ya kuwasili kijijini Namungo kwa ajili ya kufungua mafunzo ya matumizi salama ya kemikali kwa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi wa Namungo. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. Davidi Elias na kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Gemini, Bw. Alfred Michael, ambaye ni mmoja ya viongozi wa kampuni za wachimbaji wanaoshiriki mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Namungo, Mhe. Hashim Mgandilwa (kushoto), akiongea na wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wachimbaji hao yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika katika kijiji cha Namungo kilichopo wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias (kushoto), akiongea kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (wa pili kushoto), kufungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo. Wengine kutoka kulia ni Katibu wa Mkuu wa Wilaya na Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kusini, Bw. Eliamini Mkenga.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (aliyekaa katikati), akiwa pamoja na wawezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Namungo, Bw. Abraham Pasati (wa pili kulia, waliokaa), na washiriki wa mafunzo kutoka mgodi wa Namungo.

……………………….

Na Sylvester Omary – GCLA

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amewataka wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi wa Namungo kuzingatia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali wanapokuwa wanatekeleza shughuli za uchimbaji kwa lengo la kulinda afya zao na mazingira.

Mgandilwa ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Matumizi Salama ya Kemikali kwa wachimbaji hao yanayotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika kwenye kijiji cha Namungo wilayani Ruangwa.

“Nawaomba wachimbaji wa mgodi huu mtumie fursa hii ya mafunzo kujifunza Sheria zinazohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali ili muweze kuzingatia matumizi salama ya kemikali katika shughuli zenu kwa lengo la kulinda afya zenu na mazingira yanayowazunguka kwani natambua uchimbaji wa dhahabu unahusisha matumizi ya kemikali na hakuna kemikali isiyo na madhara duniani, hivyo mafunzo haya yawasaidie kujua namna bora ya kujilinda na madhara bila kuathiri shughuli zenu za uchimbaji”, alisema Mgandilwa.

Alifafanua kuwa sekta ya madini ni sekta muhimu sana katika uchumi na ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano inajitahidi kuwawekea mazingira mazuri wachimbaji ili kuhakikisha wanafaidikia na kazi hizo pia wanalinda afya zao kwa kuwa athari za kemikali nyingine zinaweza kuonekana baada ya miaka mingi.

Aidha, Mkuu wa Wilaya huyo aliwataka wachimbaji hao kujisajili Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kutambulika kama wadau wanaotumia kemikali katika shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

“Pia, niwaombe wachimbaji wa mgodi huu kutumia mafunzo haya kujifunza namna na taratibu sahihi za kujisajili, hivyo mnapaswa kuuliza maswali pale mnapoona mnahitaji ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa wawezeshaji wa mafunzo kwa lengo la kuboresha shughuli zenu na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao hawajaweza kupata elimu hii kwa sasa,” Aliongeza.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias alisema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kuwafikia wadau wake na kuwapa elimu ya matumizi salama ya kemikali kwa lengo la kuongeza uelewa wa masuala ya kemikali ili kuepusha madhara makubwa ya kiafya na kimazingira yanayoweza kusababishwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali. Vile vile alisisitiza kuwa wachimbaji hao ni sehemu ya wadau wengi ambao Mamlaka imejipanga kuwafikia na kuwapatia elimu hiyo.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji ya Gemini, Alfred Michael ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kuamua kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuimarisha shughuli zao za uchimbaji hasa kwenye matumizi ya kemikali.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuona umuhimu wa kuja kutoa mafunzo haya kwetu kwa sababu yatatusaidia katika kujilinda dhidi ya madhara ya kemikali kwenye kazi zetu za uchimbaji, tunaamini mafunzo haya yatakuwa chachu ya kufuata Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali kwa lengo la kuboresha uchimbaji na kulinda afya na mazingira kwa ujumla”, alisema Michael.

Mafunzo hayo yamehusisha jumla ya wachimbaji wadogo wadogo 50 kutoka Kampuni za uchimbaji za Gemini na Majini zinazojihusisha na uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa Namungo uliopo wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi.

MRADI WA MAJI MLANDIZI -MBOGA KUANZA MWEZI WA NNE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI

MBUNGE wa Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ameeleza, imechukua miaka 16 kwa wananchi wa Chalinze kupata majisafi na salama na imani yake kubwa ipo kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA wafanikishe mradi huo.

Aliyasema hayo, wakati alipotembelea, kiwanda cha mabomba cha Tanzania Steel Pipes kinachotengeneza mabomba ya kusafirishia maji kwenye mradi wa maji wa Mlandizi- Chalinze- Mboga.

Ridhiwani amefurahishwa na maendeleo ya utengenezaji wa mabomba hayo ambapo takribani mabomba 321 yameanza kusafirishwa kwa ajili ujenzi wa meadi huo unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi April.“Sikuwahi kuona namna wananchi wanatumia maji pamoja na wanyama kama ng’ombe ila kukamilika kwa mradi huu kutawezesha watu kupata majisafi na salama"

Alisema mradi huo utawanufaisha wakazi wa maeneo hayo ikiwa pamoja na wananchi wanaoishi kwenye eneo la mradi.

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi ,Arone Joseph Nae Joseph alisema ,mradi wa maji wa Mlandizi -Mboga unatarajiwa kusafirisha maji lita milioni 9.3 (mita za ujazo 9300) kwa siku kiasi kianchokisiwa kuweza kutosheleza mahitaji ya walengwa kwa sasa na ongezeko la matumizi kwa siku za usoni.

“Hadi sasa, kiasi cha mabomba ya umbali wa km 3.7 yameshazalishwa katika kiwanda cha TSP na yameanza kupelekwa kwenye maeneo ya mradi ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza katika Vijiji vya Mboga na Msoga,” alisema Joseph.

“Katika usanifu wa mradi huo, umetilia maanani ongezeko la watu na mahitaji ya miaka 20 ijayo na kutosheleza idadi ya watu hadi kufikia 120,912 ndani ya eneo la mradi na utakuwa kwa umbali wa Kilomita 58 ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji na utagharimu bilion 14 hadi kukamilika kwake,”anasema Joseph.

Maeneo yatakayohudumiwa na mradi huo ni pamoja na Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.

Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzi reli ya kisasa (SGR)
 Mbunge wa Chalinze ,akielezea kwa umakini ramani ya mradi wa Mlandizi Mboga unaotarajiwa kuanza kujengwa mwezi April ,mwaka huu utakaohudumia wakazi wa jimbo hilo akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph  na Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Lydia Ndibalema.(picha na Mwamvua Mwinyi) 
Mbunge wa Chalinze ,Ridhiwani Kikwete akikagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi -Mboga Chalinze. (picha na Mwamvua Mwinyi) 

RAIS MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) 146 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kabla ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 146 wa kundi la 65 la mwaka 2018 katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania 146 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Wakivalishana vyeo mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika tukio lililofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakila kiapo cha Utii mbele ya Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoka katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
  Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakati wakielekea kwenda kupiga picha za kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Maafisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

UJENZI ZONE & MAFUNDI CONNECT AGENCY WAANDAA BONANZA KUWAKUTANISHA MAFUNDI WA FANI HIYO

$
0
0
Kampuni ya Ujenzi Zone & Mafundi Connect wameandaa Bonanza litakalowakutanisha mafundi na wadau mbalimbali wa fani ya ujenzi, bonanza litakalofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili March 31, 2019.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni hiyo, Jacqueline Mushi amesema lengo lakuandaa bonanza hilo nikuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kufahamiana, kuburudika pamoja na kuandaa mipango na mikakati kabambe ya itakayo rahisisha shughuli nzima za ujenzi. 


Mushi amesema wanakutana kutokana na wadau mbalimbali wa fani hiyo kutegemeana kwenye fani hiyo, Wazalishaji wa Vifaa vya ujenzi wanamtegemea zaidi fundi na fundi anafikisha akielewa bidhaa atafikisha ujumbe kwa wateja. 

Pia Mushi amesema wameanzisha Kampuni hiyo kwa takriban miaka Saba sasa, kutokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakumba katika Ujenzi. Mfano uwepo wa migogoro baina ya Mafundi ya Wateja.


Moja wa Wadhamini, kutoka Kampuni ya Vifaa mbalimbali vya Ujenzi ya Import International Tanzania Limited,  Tumaini Mkojera amesema wamevutiwa na kazi za Ujenzi Zone & Mafundi Connect kutokana na Kampuni hiyo kuvutiwa na kuweka uhusiano mzuri kati ya Mafundi Ujenzi na Wateja. 


Mkojera amesema wameona ni vyema kushiriki Bonanza hilo ili kupata nafasi kukutana na Mafundi nakuwapa mafunzo yatakayowasaidia kwenye baishara zao. 

Bonanza hilo litatumia nafasi hiyo kuwakutanisha wadau hao wa fani ya ujenzi na mafundi ambapo pia litaunda Timu ya Mpira wa Miguu itakayoitwa Ujenzi FC. 
Pia litashirikisha Wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva akiwemo Inspector Haroun 'Babu' na Banana Zoro.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni hiyo, Jacqueline Mushi  akizungumza na waandishi wa hahari juu ya bonanza litakalowakutanisha mafundi na wadau mbalimbali wa fani ya ujenzi,  litakalofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili March 31, 2019.
Picha ya pamoja.

Waziri Kangi Lugola afungua Kongamano la Usalama Barabarani

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola akioneshwa Askari wa Usalama Barabarani Ibrahim Samwix  namna wanavyofanya ukaguzi katika vyombo mbambali vya usafiri wakati wa Kongamano la usalama barabarani lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola akizungumza na waandishi habari katika kungomano la usalama barabarani lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi wa Kituo cha Ukaguzi Cha Usalama Barabarani cha Mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani Ibrahim Samwix akizungumza mbiinu mbalimbali wanazozitumia katika ukaguzi vyombo vya usafiri katika kongamano la usalama barabarani lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola akitoa maelekezo kwa askari wa usalama barabarani katika kongamano la usalama barabarani lililofanyika jijini Dara es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola akitoa maelekezo askari wa usalama Barabarani Ibarahimu Samwix wakati wa kongamano la usalama barabarani lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Serikali yatenga fedha za ndani kupeleka umeme wa Gridi Katavi

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Katavi
Imeelezwa kuwa, Serikali imetenga fedha za ndani, kiasi cha Dola za Marekani milioni 70 kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Katavi ambayo itawezesha Mkoa wa Katavi kuunganishwa na gridi ya Taifa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani mkoani Katavi wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme katika Wilaya ya Mpanda, Nsimbo na Tanganyika ambapo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla.

“Serikali imeamua kujenga mradi huu ili Mkoa wa Katavi uachane na kutumia umeme wa mafuta ambao ni ghali kwani shilingi milioni 21 zinatumika kila wiki kuendesha mitambo hii, hivyo gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa tofauti na mapato yanayoingia.” Alisema Dkt. Kalemani.

Alieleza kuwa, njia hiyo ya umeme ya kV 132 itakuwa na urefu wa kilometa 284 na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2020 kwani taratibu za ujenzi zimeshaanza.

Akiwa katika kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda, Dkt Kalemani alisema kuwa, mwaka jana kituo hicho kilikuwa na mashine mbili zenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2.6 lakini mwaka huu imeongezwa mashine ya tatu na kufanya kituo hicho kuwa na uwezo wa megawati 3.75, hivyo kukidhi mahitaji ya umeme ya Mkoa wa Katavi kwa sasa.

Aidha, Dkt Kalemani aliwapongeza wafanyakazi wa TANESCO katika Kituo hicho kwa kutumia shilingi milioni 100 tu kwa kazi ya uboreshaji wa kituo pamoja na uhamishaji wa mashine hiyo ya tatu ya kufua umeme ambayo ilikuwa wilayani Loliondo.

“ Nataka niwapongeze watumishi hawa wa TANESCO kwani Mkandarasi kutoka Uholanzi alisema kuwa gharama atakayotumia kwa ajili ya kazi hiyo ya uhamishaji wa mashine ni shilingi bilioni mbili lakini niliagiza wataalam wetu kuwa tuihamishe wenyewe na wametumia shilingi milioni 100 tu.” Alisema Dkt Kalemani.

Katika ziara yake wilayani Nsimbo, Waziri wa Nishati alikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Kapalala ambapo pia aliwasha umeme katika Kijiji hicho na kumuagiza mkandarasi kampuni ya CRCC kupeleka umeme katika vitongoji vyote vya Kijiji hicho.

Vilevile, katika ziara yake wilayani Tanganyika, Dkt Kalemani alikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Mchakamchaka na Ifukutwa na kuwasha rasmi umeme katika Vijiji hivyo.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla (wa kwanza kushoto) wakiwa katika Mkutano na wananchi wa Kijiji cha Kapalala (hawapo pichani) wakati walipofika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akizungumza na Bi. Salma Karamba, mkazi wa Kijiji cha Ifukutwa wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi ambaye ameunganisha umeme kwenye nyumba yake kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria kuwashwa rasmi kwa umeme katika Kijiji cha Ifukutwa wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa pili kushoto) akikagua mitambo ya umeme wa mafuta katika kituo cha kuzalisha umeme cha Mpanda wilayani Katavi. Kituo hicho kinazalisha umeme wa kiasi cha megawati 3.5.

WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,

$
0
0
WAKATI Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA)ikitangaza uwepo wa mvua nchini,wakazi wa Mbagala Kiuzuiani Mtaa wa Juhudi wameiomba Halmashauri ya Temeke na Mkoa wa Dar es Salaam kuwawekea mifereji au mitaro ya kupitisha maji ili kunusuru makazi yao na watu wa maeneo hayo.

Wamesema katika eneo la Juhudi changamoto kubwa ni maji kujaa katika makazi ya watu ambayo msingi wake mkubwa ni kukosekana kwa mifereji ya kupitisha maji ya mvua,hivyo yanalazimika kupata katika barabara  na matokeo yake yanakwenda kutuama katika makazi ya watu.

Wakizungumza leo wakazi wa mtaa huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi Athuman Namna, wamesema ombi lao kubwa ni eneo hilo kuwekwa mifereji kwani wanaamini ndio ufumbuzi wa kero ya maji kutuama ambayo ni ya muda mrefu huku wakieleza matumaini yao kwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejikita kuwasiliza wanyonge na kutatua kero zao.

Wakati mvua za masika zikianza kushika kasi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo  mkoa wa Dar es Salaam wakazi wa mtaa wa Juhudi kata ya Kiburugwa wameeleza hofu yao kufuatia mvua hizo.

Wamesema kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji makazi yao  yamekuwa njia ya maji taka na inapofika msimu wa mvua maisha yao wanakuwa hatarini pamoja na uwepo wa magonjwa ya mlipuko yakiwamo ya kipindupindu.

Mkazi wa eneo hilo Hawa Kombo amesema mvua zinaponyesha wakazi wa mtaa huo wanakuwa hatarini kutokana na maji mengi kuelekezwa kwenye nyumba zao.

Amesisitiza wapo roho juu, kwani wakiona dalili ya mvua au manyunyu  wanakosa raha huku akifafanua mvua ikinyesha maji yote ya juu yanakuja kwenye nyumba zao na barabarani nako maji yanajaa na kusababisha njia kutopitika kabisa

“Sasa wapo ambao wanatumia mwanya huo kufungulia vyoo vyao basi hapo ndio hatari inapozidi kuwa kubwa magonjwa kama kipindupindu yanakuwa sehemu ya maisha yetu mvua zikianza,”

Wakati huo huo mkazi mwingine wa eneo hilo Rashid Mgaza amesema kuwa hali ya kufurika maji wakati mwingine inasababisha watoto kushindwa kwenda shuleni kwani kuna wakati maji yanakuwa mengi kiasi cha kufika usawa wa madirisha ya nyumba.

“Mvua zikinyesha wakazi wa Juhudi hatuna amani kwanza hata mtoto akienda shule unakuwa roho juu hayo maji yanayotiririka hata mtu mzima ni hatari kupita sasa ndio apite mtoto.Ombi letu kwa Serikali itusikie huku nako tunaoishi ni watu na kwa kuwa serikali yetu ni ya wanyonge basi itusikie na kutupatia ufumbuzi wa changamoto hii,” amesema Mgaza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi Athuman Namna amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa imesababishwa na maji yanayotoka maeneo ya juu kukosa mwelekeo na matokeo yake yanashuka chini kwenye makazi ya watu.

Ameongeza kwa nafasi yake na kwa kushirikiana na wananchi wamechukua hatua mbalimbali za kuwasilina na viongozi wa Manispaa ya Temeke lakini bado hawajapata ufumbuzi wa tatizo hilo.

“Tukisikia mvua amani inatoweka huku kwetu na kama hii iliyotangazwa watu wanalazimika kuacha nyumba zao lakini ikitengenezwa mifereji hili tatizo litakuwa historia,”

“Niwaombe viongozi wangu wasikae ofisini waje kuona hali ilivyo maana kwa kuambiwa unaweza usielewe ila ukweli ni kwamba tuna wakati mgumu sana kuelekea hiki kipindi cha mvua,”amesema Namna

Wakazi wengine wamesema hawana tatizo na Serikali kwani wanaimani na ndio maana haja ya kutoa kilio cha hasa kipindi hiki ambacho mvua hazijashika kasi kwani kuna hatari zaidi kama hakutafanyika jitihada za kuwekwa mitaro hivi sasa."

Michuzi Blog ambayo ilifika eneo hilo,imeshuhudia baadhi ya wakazi wakiwa wameacha nyumba zao na kwenda kutafuta maeneo ya kujisitiri wakiohofia mvua ambazo zimeanza kunyesha zinaweza kusababisha madhara .
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi uliko Mbagala Kizuiani Athuman Namna akionesha uharibifu wa makazi ya watu ambao umetokana na maji kutuama eneo hilo kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji ya mvua katika mtaa huo.
 Moja ya nyumba ambayo iko hatarini kudondoka kutokana na mvua kuharibu miundombinu ya barabara ambayo inaelezwa ni kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji ya mvua na hivyo kusambaa barabarani
 Watoto wakiwa katika barabara ya Mtaa wa Juhudi katika eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo barabara hiyo ambayo inatagemewa imeharibiwa na maji ya mvua kwani haina mitaro ya kupitisha maji
 Gari ikiwa imesimama baada ya dereva kukwama katika eneo hilo la Mtaa wa Juhudi lililopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.Barabara hiyo pamoja na maeneo hayo yameharibiwa na mvua na kusababisha kero kwa wananchi walio wengi

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KAMISHENI YA UTALII NA WIZARA IKULU LEO

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akionesha Mchoro wa Majengo inayotarajiwa kujengwa katika eneo la Bungi Kwa Bihole sehemu ya historia,Wilaya ya Kati Unguja, wakati wa mkutano wake na Viongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Uongozi wa Kamisheni ya Utalii na Makamishna ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo,30-3-2019.
MWANASHERIA Mkuu Mhe. Said Hassan Said na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis Mussa wakiwa na Makamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
MAKAMISHNA wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano huo uliofanyika leo 30-3-2019,Ikulu Zanzibar kuzungumzia masuala ya Utalii Zanzibar.
RAIS wa Zanzibare na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Uongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar,Uongozi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis Mussa akizungumza wakati wa mkutano huo, kulia Mwanasheria Mkuu Mhe. Said Hassan Said na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Zanzibar Ndg Salum Maulid, wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Ikulu leo
KATIBU Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Abdallah Mohammed Juma, akizungumza wakati wa mkutano huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika Ikulu Zanzibar, kulia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dkt, Amina Ameir Issa na Katibu Mkuu Bi. Khadija Bakari wakifuatilia mkutano huo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, akichangia Mada wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu Zanzibar kulia Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bi. Sabaah Saleh na kulia Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Mwenasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Makamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Shirika la AGPAHI latoa mafunzo ya saikolojia kwa watumishi wa afya Mwanza

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka Vituo vya Afya mkoani Mwanza, yanayolenga kuwajengea uwezo katika kutoa msaada na huduma za kisaikolojia kwa watoto na vijana wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).


Mafunzo hayo ya siku tano yalianza jumatatu Machi 25, 2019 hadi Ijumaa Machi 30, 2019 katika ukumbi wa “Isamilo Lodge” Jijini Mwanza ambapo yamewashirikisha wataalam wa afya zaidi ya 60 kutoka Halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo Nyamagana, Ilemela, Misungwi, Magu, Ukerewe na Buchosa.


Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona amesema mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma za afya katika vituo vya tiba na matunzo kutambua namna bora ya kuwahudumia wateja wao hususani watoto na vijana.


Amesema mafunzo hayo yatawasaidia pia kuwatambua watoto na vijana wenye changamoto kisaiklojia na namna ya kuwasaidia huku wakizingatia upatikanaji wa huduma bora na rafiki kwa wateja kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo michezo.


“Tunatarajia pia wataenda kuanzisha vikundi vya akina mama wanaoishi na maambukizi ya VVU ambao wako kwenye kitengo cha kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili nao waweze kujifunza kupitia uzoefu wao huku vikundi vilivyopo vikiimarishwa zaidi”. Amesema Yona.

Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walikuwa wakikumbana na changamoto ya kutambua mazingira halisi yanayowakabili watoto na vijana kupitia klabu zao.


Shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia taasisi ya Centres for Disease Control (CDC), linashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutekeleza afua mbalimbali za kupambana na maambukizi ya VVU pamoja na kuwahudumia watu wanaoishi na maambukizi hayo.

Mmoja wa Wawezeshaji, Margaret Safe kutoka Kibaha mkoani Pwani akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji, Margaret Safe akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Afisa Miradi, Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI, Cecilia Yona.
Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti akiendelea kutoa mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Mwezeshaji, Dkt. Nikodemas Kikoti kutoka mkoani Iringa.
Wataalam wa afya walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa umakini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Timu ya wakufunzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo pia walipewa mtihani na hapa wakiwa kwenye chumba cha mtihani ili kupima uelewa wa kile walichofundishwa.
Washiriki wakijibu mtihani kuhusu walichofundishwa.
Baada ya mafunzo ya nadharia darasani yaliyofanyika Isamilo Lodge, washiriki walielekea Lesa Garden kukutana na baadhi ya watoto na vijana kutoka klabu za elimu na makuzi kwa ajili ya kucheza na kufurahi pamoja ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwasili Lesa Garden iliyopo Luchelele Jijini Mwanza.
Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
Inaelezwa vijana hujifunza na kuelewa vyema kupitia michezo na hapa michezo imepamba moto.
Michezo mbalimbali ikiendela.
Mafunzo kwa vitendo kupitia michezo.
Washiriki wa mafunzo wakifurahi pamoja na vijana.
Michezo ikiendelea Lesa Garden.
Watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo kufikisha elimu kwa watoto na vijana.
Inaelezwa michezo husaidia watoto na vijana kuelewa vyema yale wanayofundishwa hivyo watoa huduma za afya wamehimizwa kutumia michezo pia kuwaelimisha vijana na watoto.
Washiriki wakifurahia pamoja na vijana.
Pia kulikuwa na burudani ya muziki ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo ambapo husaidia watoto na vijana kuwa huru kwa watoa huduma za afya.
Burudani ya muziki.
Washiriki wa mafunzo wakifurahia muziki pamoja na watoto/ vijana.
Michezo na burudani ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

MFUKO MAWASILIANO KWA WOTE YATEMBELEA MINARA INAYOJENGWA ROMBO

$
0
0
Katibu Tawala Wilaya ya Rombo (DAS)Bw. Abubakar Asenga akimuongoza  Dkt. Jimmy Yonazi  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, alipotembelea Minara inayojengwa Rombo na maeneo yenye uhaba wa mawasiliano  ili kuongeza usikivu wa Radio na upatikanaji wa Mawasiliano ya Simu .

Ziara hii inalengo la kumaliza Changamoto ya maingiliano ya Simu na Radio toka nchi Jirani ya Kenya.

Naibu katibu Mkuu Dkt Yonaz aliambatana na viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ili nao waweze kuongeza nguvu zaidi katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ilioahidi kuendelea kuboresha Mawasiliano kwa Wananchi.



 Katibu Tawala Wilaya ya Rombo (DAS), Abubakar Asenga akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano,Dkt Jimmy  Yonaz alipotembelea Minara inayojengwa Rombo na maeneo yenye uhaba wa mawasiliano  ili kuongeza usikivu wa Radio na upatikanaji wa Mawasiliano ya Simu .


TASWIRA MBALIMBALI KATIKA CRDB BIMA MARATHON 2019 JIJINI DAR LEO

MSINGI WA MAENDELEO YA NCHI NI MAENDELEO YA KWELI KWA WANYONGE ASEMA KIKWETE.

$
0
0
Mkakati wa kuhakikisha maendeleo yanawafikia watu wa Hali ya Chini ndiyo msingi utaowafanya Wananchi waendelee kuipenda na kuichagua Ccm. Maneno hayo ameyasema leo Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaweza jiwe la Msingi la Zahanati ya Kitongoji Cha Chahua huko mjini Chalinze mapema hivi leo.

Akiweka jiwe la Msingi ,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alieleza furaha yake juu ya mafanikio ambao Halmashauri yake imepata kwa upande wa Afya,Elimu,Maendeleo ya Jamii na kusisitiza kuwa haya yanatokana na msimamo ambao Chama Cha Mapinduzi kinasimamia inapofika katika utekelezaji wa ilani yake ambayo inawalenga kuwapelekea Mabadiliko ya Kweli wananchi wa hali za chini kabisa.Mheshimiwa Mbunge Ridhiwani hakusita kueleza jinsi Raisi Magufuli anavyoendelea kupambana kuwasaidia Watanzania hasa katika kuwapatia huduma bora hasa kwa Upande wa Afya.

"Katika Halmashauri ya Chalinze tumejenga zaidi ya Zahanati 86 katika vitongoji na Vijiji ,Vituo vya Afya zaidi ya 13 na Sasa tunakamilisha Hospitali ya Wilaya ambayo fedha Kiasi cha Shilingi Milioni 500 zinatarajiwa kuletwa kumalizia Ujenzi pamoja na kununua vifaa tiba. Tunachopaswa wana Chalinze wenzangu ni kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ambazo Raisi Magufuli anafanya akishirikiana nami Mbunge wenu,Diwani wetu na Mwenyekiti wetu wa Kitongoji." Mbunge Ridhiwani Kikwete alisisitiza.

“Katika Kata yetu ya Bwilingu, mambo mengi ya kimaendeleo tunayatekeleza ikiwa ni pamoja na kumalizia ahadi za Mheshimiwa Raisi alizozitoa kipindi cha kampeni. Katika Upande wa Elimu ,tunapambana kupunguza wingi wa Wanafunzi pale Shule ya sekondari ya Chalinze kwa kumalizia shule ya sekondari ya pera na mkakati mwengine wa kuanzisha ujenzi wa Shule ya sekondari ya Chahua." Mheshimiwa Mbunge pia aligusia juu ya Ujenzi wa Maabara ya Kisasa katika kituo cha Afya Chalinze ili kusaidia vipimo vya ziada vya Kiafya.

Akizungumza kabla ya Mbunge kuweka jiwe la Msingi Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Sadallah Maisha alimshukuru Mbunge kwa Msaada anaowasaidia Watu wa Chahua hasa katika maendeleo ya Jamanii. " Mheshimiwa Mbunge tunakushukuru kwa Kutupatia Nondo 80 na fedha taslimu Shilingi Milioni Mbili,LAki Mbili na Nusu. Pamoja nawe Halmashauri na Nguvu zetu Wananchi."

Mbunge wa Chalinze anaendelea na Ziara ya kuangalia Shughuli za Maendeleo na Utekelezaji wa Ilani katika Vijiji,Kata na Vitomgoji mbalimbali Vya Halmashauri hiyo. Katika Hali nyengine Mvua kubwa iliyonyesha kuanzia Alhamisi imeharibu Miundo mbinu katika Mji wa Chalinze na pera na Vitongoji mbalimbali.
 

 

MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa Gwakisa ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha eneo lililotengwa kwa ajili ya wajasiriamali linaanza kufanyiwa maandalizi ya awali ili kuondoa changamoto ya eneo la kuzalisha kwa mjasiriamali mdogo. 

Alitoa maagizo hayo wakati akifungua mafunzo ya TBS kwa wajasiriamali wadogo, yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Korogwe, ambapo wajasiriamali 104 walihudhuria.

Mh.Gwakisa alisema eneo la uzalishaji ni kilio cha wazalishaji wadogo wengi, na hivyo hatua hiyo itawasaidia wajasiriamali hao kupata alama ya ubora kwa bidhaa wanazozalisha.

Kwa upande wake, Afisa masoko mwandamizi wa TBS, Bi. Gladness Kaseka, alitoa shukrani kwa Mkuu wa wilaya kwa kuwajali wajasiriamali hao kwani itawasaidia kupata leseni ya kutumia alama ya ubora na vilevile huduma hiyo kwa mjasiriamali mdogo ni bure. 

Kaseka aliwakumbusha kuomba mafunzo maalum TBS, ambapo TBS hufanya kwa kushirikiana na SIDO na TFDA, bila gharama yoyote. 

Wajasiriamali waliopata elimu hiyo, wamefurahishwa na Shirika hilo kuwafikia na kuwaongezea uelewa wa Viwango na kuwajulisha juu ya fursa ya bure kwao, kupata leseni ya TBS itawasaidia kuuza bidhaa zao popote na ushindani halali sokoni.

Sambamba na mafunzo hayo Shirika pia lilitoa elimu ya viwango kwa wananchi katika maeneo ya stendi ya zamani ya manundu, stendi mpya, soko la manundu na sabasaba, pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nyerere yenye jumla ya wanafunzi na walimu 746.
 Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mhe. Kissa Gwakisa, akifungua semina kwa wajasiriamali wadogo juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS, katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Korogwe.
 Wajasiriamali wakisikiliza mafunzo juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS na fursa ya huduma ya bure  kutoka kwa maafisa wa TBS
 Wananchi wilayani Korogwe wakipata elimu ya viwango kutoka kwa Maafisa Udhibiti Ubora waTBS,  Bi. Amina Yassin na Bi. Janeth Kakuru.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyerere,wilayani Korogwe wakipata elimu kutoka kwa Afisa Masoko Mwandamizi(TBS), Bi. Gladness Kaseka

Wanafunzi waaswa kujaza fomu za maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa usahihi

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 Wanafunzi wameaswa kuwa makini katika ujazaji wa maombi ya mkopo wa elimu ya juu katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa  Elimu ya Juu (HESLB).

Akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Daud Elisha amesema bodi iko kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wale wanaohitaji.
Daud amesema kuwa wale ambao wataomba baada ya kuchaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) wanapeleka majina bodi ambao ndio wanaanza kuchakata mikopo kwa wahitaji wa mikopo hiyo.

Aidha amesema kuwa waombaji wote lazima wazingatie vigezo vilivyoanishwa kwani bodi haina uwezo kutoa mkopo kutokana na kukosekana kwa taarifa za huo mkopo. Nae Afisa Bodi hiyo Esther Luvanda amesema mkopo wa kutoka bodi lazima ulipwe ili kuweza kusomesha wengine.

Amesema kuwa wanafunzi wahakikishe wanaambatanisha taarifa zinzohitajika zilizo sahihi.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari Benjamini Charles Mwamwenda amesema bodi wamefika wakati mwafaka kwani wanajuaga changamoto ya wanafunzi waliopita hivyo elimu hiyo itawasaidia kufanya vizuri.
 Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Esther Luvanda akitoa maelezo kuhusiana mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na namna ya kuresha mkopo walipokwenda kutoa elimu ya masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Benjamini Mkapa.
 Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Daud Elisha akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Benjamini Mkapa walipokwenda kutoa elimu ya masuala ya mikopo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa wakiwasikiliza maafisa wa Bodi.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa Charles Mwamwenda akizungumza na waandishi habari namna walivyopokea ujio wa bodi.

CHUO CHA DUCE CHATOA MSAADA KWA KITUO CHA FADHILLAH ORPHANAGE GROUP

$
0
0
UONGOZI wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiambatana na Serikali ya wanafunzi wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Fadhillah kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Mshauri Upendo  Mlungusye amesema wamekuwa na utaratibu wa kutembelea vituo mbalimbali vya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kila mwaka mwaka.

Amesema, jamii ya chuo chao cha DUCE ni utaratibu wao ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma kwa jamii inayowazunguka na kwa mwaka huu wamechagua kutoa msaada huo kwa kituo cha Fadhillah Orphanage Group kilichopi Misugusugu Kibaha.

Upendo ameeleza kuwa kituo hicho kimekuwa na uhitaji mkubwa wa mahitaji kulingana na wingi wa watoto wanaoishi kwenye nyumba hiyo yenye takribani 140 kuanzia umri wa mwaka 0-14.

Mlezi wa Watoto hao, Sulekha amesema wanashukuru kwa msaada wa mahitaji mbalimbali kutoka kwa Chuo cha DUCE  na wamefurahi baada ya kuwambuka watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Sulekha amesema, wana watoto wadogo kuanzia mwaka 0 hadi miaka 14 na wamekuwa wanaishi nao vizuri na yeye binafsi anapenda anachokifanya cha kuwalra watoto hao.

Katibu wa Taasisi ya Fadhillah Orphanage Group Fadhil Rajab amesema wanashukuru kwa msaada huo na Kituo chao kilianza mwaka 2006 na kina jumla ya watoto 140 na wapo ambao wanasoma shule za Msingi na wengine Sekondari.

Mahitaji yaliyopelekwa kwenye kituo hicho ni mchele kg 200, Unga wa mahindi kg 120, Mafuta ya kula lt 60, Maharage kg 60, Mavazi ya aina mbalimbali, Sabuni, Madaftari na peni pamoja na Vinywaji baridi na vitafunwa mbalimbali
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE Upendo Mlungusye(wa tatu kushoto) akikabidhi mahitaji kwa Mlezi wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group Sulekha pamoja na Katibu wa Kituo hicho Fadhil Rajab walipotembelea Kituo hicho kwa ajili ya kutoa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiongozwa na Rais wa Wanafunzi Edward Ngelewa wakikabidhi baada ya mahitaji kwa watoto wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kutembelea kwa ajili ya kutoa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Uongozi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiwa kwenye picha ya pamoja na Walezi wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kutembelea kwa ajili ya kutoa mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kukabidhi mahitaji mbalimbali.
Uongozi wa Serikai ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha Fadhillah Orphanage Group baada ya kuwakabidhi mahitaji mbalimbali kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani

LUGOLA ATANGAZA VITA DHIDI YA MATRAFIKI WALA RUSHWA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Askari Polisi Kikosi cha Usalama barabarani nchini, kusimamia sheria kikamilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia ambao hufariki, kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali.

Akizungumza kabla ya kulizindua kongamano la kitaifa la wadau wa usalama barabarani nchini, Lugola ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alisema wasimamizi wa Sheria wakisimamia sheria kikamilifu na elimu ikaendelea kutolewa kwa watumiaji wengine wa barabarani na wakabadili tabia zao, uwezekano wa kupunguza ajali zaidi ni mkubwa.
“Usalama Barabarani unaanza na kila mmoja wetu, nawaomba sana tutumie fursa hii kikamilifu kwa kutoa mawazo na maoni yetu katika kongamano hili kwa manufaa na mustakabali wa Usalama wetu hivi sasa na vizazi vijavyo,” alisema Lugola.
Pia aliwataka wadau hao, watumie fursa ya kongamano hilo kuzungumza kwa uwazi, kutoa mawazo yao ambayo yanalenga kuboresha utendaji wa Baraza Usalama Barabarani na vyombo vingine ambavyo vinasimamia Sheria ya Usalama Barabarani. 
Lugola alisema Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni kutokomeza ajali za barabarani nchini, hivyo aliwataka wadau wa usalama barabarani wajipange kikamilifu kwa kiuweka mikakati thabiti kwa lengo la kutokomeza ajalin nchini. 
“Ni wazi kwamba wasimamizi wa Sheria wakisimamia sheria kikamilifu na elimu ikaendelea kutolewa kwa watumiaji wengine wa barabarani na wakabadili tabia zao, uwezekano wa kupunguza ajali zaidi ni mkubwa,” alisema Lugola. 
Pia Waziri Lugola alilitaka Baraza la Usalama barabarani kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Baraza Awamu ya Nne, ambao umezinduliwa Waziri huyo ameuzindua na Muongozo wa Utendaji na Utekelezaji wa majukumu ya Kamati za Usalama Barabarani za Mikoa na Wilaya ili kudhibiti ajali za Barabarani na Kuimarisha Utendaji wa Kamati.
Lugola pia aliwataka kusimamia ukaguzi wa magari ili Kuhakikisha Magari mabovu yanaondoka barabarani, na Baraza likamilishe Uundwaji wa Kamati za Usalama Barabarani za Mikoa na Wilaya haraka ili Kamati hizo zianze kazi ili kwenda na Mabadiliko yanayofanyika ndani ya Baraza. 
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masuani alisema takwimu za usalama barabarani zimepungua nchini kutokana na Baraza lake kuweka mikakati za kupambana na ajali nchini.
Kongamano hilo ni mbadala wa Wiki ya Nenda kwa usalama barabarani ambayo kila mwaka ufanyika katika mkoa ambao uchaguliwa na wajumbe wa Baraza hilo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wadau katika kongamano taifa la usalama barabarani lililofanyika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam, akiwataka Askari Polisi Kikosi cha Usalama barabarani nchini, kusimamia sheria kikamilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia ambao hufariki, kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masuani akizungumza na wadau (hawapo pichani) katika kongamano taifa la usalama barabarani lililofanyika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam, , akisema takwimu za usalama barabarani zimepungua nchini kutokana na Baraza lake kuweka mikakati za kupambana na ajali nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.     
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabrani kwa upande wa watu wenye ulemavu, Jutoram Kabatale, alipokuwa anatoa maelezo ya alama za barabarani wakati Waziri huyo alipokua anakagua mabanda mbalimbali katika Kongamano la Taifa la Usalama Barabarani lililofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam,. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akimuuliza swali Mshauri Mtaalamu wa Kiwanda cha Kutengeneza Kofia Ngumu (Helmet) Alpherio Nchimbi (kulia) kuhusu ubora wa kofia ngumu wakati Waziri huyo alipokua anakagua mabanda mbalimbali katika Kongamano la Taifa la Usalama Barabarani lililofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilim.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   

SOKO LA MADINI KUFUNGULIWA WILAYANI KAHAMA

$
0
0

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akikagua mashine ya kupima dhahabu katika kampuni ya Busami iliyopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo ya kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 30 Machi, 2019.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akijadiliana jambo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali (katikati) katika kampuni ya Busami iliyopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Kutoka kulia Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali wakisikiliza kero za wamiliki wa mitambo ya kuchenjulia dhahabu (hawapo pichani) kupitia mkutano maalum uliofanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

………………………..

Na Greyson Mwase, Kahama

Ofisi ya Afisa Madini Mkazi, Mkoa wa Kimadini wa Kahama inatarajia kuanzisha soko la madini mapema ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini katika kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliyoifanya mapema leo tarehe 30 Machi, 2019 katika Wilaya ya Kahama lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliambatana na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali wataalam kutoka Tume ya Madini pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mara baada ya kufanya ziara katika baadhi ya mitambo ya kuchenjua dhahabu, Nyongo alifanya kikao na wamiliki wa mitambo hiyo na kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuzitatua.

Mara baada ya kusikiliza kero husika ikiwa ni pamoja na ya kutokuwepo kwa soko la madini katika Wilaya ya Kahama, Naibu Waziri Nyongo alimwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Adrea Fabian kuhakikisha sehemu ya ofisi yake inatumika kama soko la madini ya dhahabu ambapo wauzaji na wanunuzi watakuwa wanafanya biashara huku serikali ikipata mapato yake, kauli ambayo ilipokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa madini ya dhahabu.

Aliendelea kusema kuwa kutokuwepo kwa soko la madini katika Wilaya ya Kahama, kunachochea utoroshwaji wa madini ya dhahabu kwakuwa inakuwa vigumu kwa wauzaji wa madini hayo kusafiri umbali mrefu hadi Geita kwa ajili ya kwenda kuuza madini hayo.

“Hapa tunataka kuhakikisha biashara ya madini inafanyika hapa hapa ili kuwarahisishia wafanyabiashara wa madini ya dhahabu huku Serikali ikipata mapato yake,” alisisitiza Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine, Nyongo aliutaka uongozi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama kushirikisha mamlaka nyingine za Serikali kama vile Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mabenki na soko kuanza mara moja.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wamiliki wa mitambo ya kuchenjua dhahabu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za madini kwa kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Madini.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wamiliki wa mitambo ya kuchenjulia dhahabu walioshiriki katika kikao hicho mbali na kumpongeza Naibu Waziri Nyongo wamesema kuwa uwepo wa soko hilo utawarahisishia sana biashara ya madini kutokana na kuepukana na matapeli huku serikali ikipata mapato yake stahiki.

Walisema kabla ya uamuzi huo wamekuwa wakisafirisha madini hadi Geita kwa ajili ya kuuza hali inayopelekea baadhi yao kuuza kwa watu wasio waaminifu.

DC KISARAWE AMPA 'SHAVU' PIERE LIQUID

$
0
0

"Hakuna maneno Muhimu na Machache katika ustawi wa maisha ya Binadamu kama Tafadhali, Asante na Samahani.
Katika Dhifa niliyoiandaa jana, nilialika watu wengi, Wanasiasa, Taasisi za Kiserikali, Mabalozi, Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Wasanii, Wadau wa Burudani N.k.
Na Makusudio ya yote hayo wote tunayajua, ni kutafuta MOTISHA juu ya ELIMU ya Mtoto wa kike, Kisarawe na kote nchini.
Na kwangu mimi na Wilaya nzima ya Kisarawe wote waliofika jana ni muhimu sana sana kwangu na kwetu.
Kipekee kabisa nimshukuru @officialpiere_liquid wako watu maarufu wengi mno tuliowaalika lakini hawakufika. Ila wewe ulichukua muda wako kuhamamisha na kufika na zaidi ya hapo ukatoa mchango wa TSH LAKI MOJA!!! Hukuja kuuza sura tu!! Nasema ASANTE SANA. Wana Kisarawe tunakupenda na tunakukaribisha kuwekeza Kisarawe uanzishe hata mgahawa tutakusaidia kupata eneo. Lakini pia nimesikia ni mtengeneza mzuri sana wa furniture. Hii Shule tunayoenda kujenga inahitaji madawati Naomba tufanye kazi nawewe katika hii fursa. Tuangalie namna japo kidogo tukuwezeshe.
Tunasema Karibu Kisarawe Ukae. Kisarawe Kunogile. Tunasema Samahani kwa kukwazika lakini zaidi Asante Sana kwa kushiriki kwenye #TokomezaZeroKisarawe #ElimuItabakiKuwaJuuKileleni #KisaraweMpya
Ubarikiwe!!!" - DC Jokate Mwegelo
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live




Latest Images