Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 281 | 282 | (Page 283) | 284 | 285 | .... | 3272 | newer

  0 0


                                                                                                              November 30, 2013

  By Virginia Blaser

  Every year on December 1, the global community commemorates World AIDS Day.  It is a day to reflect on lives lost, and lives forever changed, by HIV and AIDS.  It is also an opportunity to acknowledge the more than 34 million people living with HIV worldwide.  Today, we celebrate those lives saved in Tanzania and throughout the world, and we commend Tanzanians for their contributions and achievements in this global struggle.
  As President Obama reinforced during his visit last July, Tanzania remains a key partner of the United States.  The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief, or PEPFAR, is a cornerstone of the United States’ investment in Tanzania.  In 2013 alone, PEPFAR’s care and support programs directly aided more than 990,000 people in Tanzania, including more than 330,000 orphans and vulnerable children.  The American people, in partnership with others, provide life-saving antiretroviral treatment for over 444,000 Tanzanians.  And this year alone, we have together tested and counseled more than five million Tanzanians, almost one and a half million of whom were pregnant Tanzanian women.  Due to our combined efforts, Tanzanians are less likely to be infected with HIV, and those living with HIV and AIDS are more likely to live full and healthy lives.


  Today, an AIDS-free generation is in sight not only in Tanzania, but also around the world.  For example, thanks to global efforts of PEPFAR and its partners to prevent mother-to-child transmission (PMTCT), in 2013 we witnessed the millionth HIV-free baby born to an HIV-positive mother.  Furthermore, through scientific advances and national and individual behavioral changes, we have reached a tipping point in this epidemic.  By rapidly scaling up proven HIV interventions -- including treatment, PMTCT, condoms, testing and counseling, and voluntary medical male circumcision -- we can turn the tide on HIV and AIDS.

  Over the last few years, Tanzania has made progress in the fight against AIDS, and the American people have been proud to play a supporting role.  This month, the U.S. Congress unanimously passed the PEPFAR Stewardship and Oversight Act which renews PEPFAR for an additional five years.  As Secretary of State John Kerry said recently: “A decade ago, PEPFAR created the world’s largest and most successful foreign assistance program ever for a single disease.  And now, a disease that at one time seemed to be unstoppable is actually in retreat.”


  Even with such great progress, we cannot rest on past achievements.  In the coming year, we intend to work with the Government of Tanzania and development partners to increase the sustainability of our shared success.  The road to achieving an AIDS-free generation will not be easy, but strong partnerships like the collaboration between the American and Tanzanian peoples illustrate how we, by joining forces, can ultimately reach the goal of a Tanzania free of HIV.  I applaud the Government of Tanzania for the creation of the AIDS Trust Fund and look forward to working together to build a sustainable program.


  On this World AIDS Day, I strongly reaffirm the partnership between the American and Tanzanian Peoples.  Together we can end this epidemic.


  ______________________________________________________________________________
  Virginia Blaser is the Chargé d'Affaires ad interim of the United States Embassy in Dar es Salaam, Tanzania.


  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Cheti cha ubora Baraka Magure ambaye aliibuka kuwa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika wahitimu wa Shahada katika mahafali ya Chuo cha Biashara yaliyofanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Sigara iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam Novemba 30, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zwadi Revocatus Mavuno ambaye alifanya vizuri kwa wanafunzi wa ngazi ya Stashahada katika mahafali ya Chuo cha Biashara yaliyofanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Sigara iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam Novemba 30, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Almight God of the Second chance, our God loves us unconditionally regardless of our backgrounds. To me is very personal, having hit by the  sudden death of my lovely wife 40 days ago, it's a wake up call not only 
  for me but for everybody else. God wants us to live a holly life and be ready at all times. Responding to this call I have decided to serve Him all my life. Now, it is with great honor to  introduce to you  Kassuwi Gospel Ministry blog with the address http://alexkassuwi.blogspot.com. Everybody is welcomed. KGM Online TV and Radio coming up soon. Stay blessed 

  0 0

  Taasisi inayosimima uhifadhi na matengenezo ya nyumba za Serikali imeshauriwa kuifanyia marekebisho yaliyosalia Ikulu ndogo ya Kibweni ili itumike vyema katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. 
  Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofanya ziara fupi ya kuikagua nyumba hiyo iliyopo pembezoni mwa Makao Makuu ya Kikosi cha kuzuia Magendo Zanzibar { KMKM } Kibweni Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi. 
  Balozi Seif ambaye ameridhika kiasi na hali halisi ya mazingira ya Ikulu hiyo alisema ni vyema nyumba hiyo ya Serikali ikapangiwa taratibu za kutumika badala ya kuachwa ikikaa bure . Alisema Serikali katika kipindi kirefu imekuwa ikipokea wageni wa Kitaifa na Kimataifa wenye hadhi ya kuishi kwenye nyumba hiyo lakini wengi kati yao wanaishia kuwekwa katika Hoteli za Kitalii jambo ambalo linaweza kuepukwa. 
  Aliwataka wahusika wa matengenezo ya nyumba za Serikali kuhakikisha kwamba nyumba hiyo { Ikulu } inakamilishwa hitilafu ndogo ndogo zilizobakia ili iweze kuhudumia wageni watakaoalikwa kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi kutimia Nusu Karne. 
  “ Tunatarajia kupokea wageni wengi wa Kitaifa na Kimataifa katika sherehe zetu za mwaka ujao . Hivyo kwa hadhi ya nyumba hii tunaweza baadhi yao kuwapangia wakampumzika kwa kutwa moja kabla na baada ya sherehe zetu kabla hawajarejea nyumbani “. Alisisitiza Balozi Seif. Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wasimamizi wa Ikulu hiyo ya Kibweni kwa hatua wanazozichukuwa katika kuihudumia nyumba hiyo kongwe. 
  Alisema mazingira bora yaliyopo hivi sasa kwenye nyumba hiyo yanaruhusu kwa baadhi ya Mikutano na Kazi za Viongozi Wakuu wa Serikali kuzifanyiwa katika eneo hilo. 
  Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Nd. Salum Maulid alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba tatizo liliopo hivi sasa katika nyumba hiyo ni marekebisho ya jiko la kupikia pamoja na huduma ya maji ambayo haipatikani kikawaida. 
  Nd. Salum alisema huduma hiyo ya maji safi hupatikana kwa nadra katika kipindi kirefu tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa utafiti wa kina na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.
    Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Nd. Salum Maulid akimtembeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika baadhi ya sehemu za nyumba ya Ikulu ndogo iliyopo Kibweni Wilaya ya Magharibi.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwaagiza wahudumu wa Ikulu ndogo ya Kibweni kuhakikisha kwamba mazingira ya nyumba hiyo yanaendelea kuwa mazuri.
  Jengo la Ikulu ndogo iliyopo Kiwebi Wilaya ya Magharibi ambalo linatarajiwa kuhudumia baadhi ya wageni watakaoalikwa hudushuria sherehe za Maadhimisho ya Kutimia Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .

  0 0

  Mchezo wa wanakandanda ambao ni Mashabiki wa Yanga na Simba uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Muhimbili, ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 5, huku wapinzani wake watani wa jadi Simba wakishinda bao 3 tu!

  Mchezo huo ambao ulitanguliwa na Kuwakumbuka wanakandanda ambao wamefariki wakiwa members wa KandandaFB, Kwa muda wa Saa moja hakuna mwanakandana alieposti katika KandandaFB wakati wa kuinamisha vichwa huko.


  0 0


  0 0


  0 0


  KAMPUNI ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha la Krismas wametangaza viingilio vya tamasha hilo ambavyo kima cha chini ni shilingi 5000.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama viingilio vingine viti vya kawaida, 10000 VIP B na VIP A 20000.

  Msama  alisema watoto katika tamasha hilo watachangia shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa jamii kujipanga kwa ajili ya tamasha hilo. Aidha Msama alisema viingilio katika mikoa yote litakakofanyika ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000na kuendelea kueleza kwamba wadau wajipange vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo. 

  “Tunafanya taratibu za tiketi za tamasha hilo ambazo tumepanga zitoke Uingereza, ili kukwepa wizi utakaofanywa na baadhi ya wasiolitakia mema,” alisema Msama. Msama alisema wanajipanga vilivyo kuhakikisha wanakomesha ujanja unaotarajia kufanywa na wasiolitakia mema tamasha hilo ambalo dhamira yake ni kusaidia wanaoishi katika mazingirahatarishi wakiwemo yatima, wajane na walemavu.

   Waimbaji katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu na New Life Band (Tanzania) na waimbaji kutoka nje ya Tanzania ni pamoja na Solly Mahlangu, Liliane Kabaganza, Solomon Mukubwa na Eiphraim Sekeleti.   

  0 0


  Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
  Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu. Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake. Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.
  Ungana na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya waTanzania wengi.  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete together with his East African Heads Of States  Counterparts shortly after they signed the Protocol on the Establishment of the East African Monetary Union at Speke’s Bay Resort Munyonyo in Kampala this afternoon.Others from Left Presidents Pierre Nkurunzinza of Burundi, Yoweri Kaguta Museveni of Uganda, The new EAC chairman Uhuru Kenyatta of Kenya, and Paul Kagame of Rwanda.(photos by Freddy Maro.   

  0 0

   Katibu wa chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya,Bwa Bryson Mwasimba akionesha kadi yake ya chama hicho akiirejesha kwa chama cha CCM,mara baada ya kuachia ngazi,kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga,Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko mkoani Mbeya kwenye ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama,kukagua miradi mbalimbali ya chama na wananchi sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na namna ya kuyatafutia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya chama cha CCM,Katibu wa chama cha CHADEMA Wilayani Chunya,Bwa.Bryson Mwasimba aliyeamua kujiuzuru wadhifa wake mapema leo na kurejea CCM,huku umati mkubwa wa watu uliofika kwenye mkutano wa hadhara ukishangilia kwa mayowe na miluzi,uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga,Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
   Bwa.Bryson Mwasimba akionesha kadi ya CCM mara baada ya kutangaza kuachia ngazi CHADEMA.
   Bwa.Bryson Mwasimba akizungumza mbele ya wananchi na wanachama wa CCM kuhusiana na kuachia ngazi kwake na kurejea chama cha CCM mapema leo.  0 0

   Sehemu ya ujenzi wa barabara ya Mbeya mpaka Chunya ukiendelea
   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro akwaelekeza jambo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro,walipokuwa wakielekea wilayani Chunya mapema leo.Kwa mujibu wa Barabara hiyo inajengwa na kampuni ya China (China Communications Construction Company),yenye urefu wa Km 36 kwa gharama ya shilingi Bilioni 53.
   Ujenzi ukiendelea kwa nguvu
   Sehemu ya ujenzi wa daraja barabara ya Mbeya kuelekea Chunya kama ionekanavyo pichani
   Mmoja wa wakazi wa Chunya akikatiza kwenye kipande cha sehemu ya barabara iliotiwa lami
  Barabara ya Mbeya kuelekea Chunya ikiendelea kujengwa.

  0 0
 • 11/30/13--20:58: Article 24


 • 0 0

     Ustaadh Ally Abrahaman Muki, ambaye ni Mwl Katika Kituo Cha Madrassa Mukkarramah & Nursery School akitunukiwa cheti pamoja na vifaa vya Kufundishia na Mgeni Rasmi Sheikh Suleiman Amran Kilemile vilivyotolewa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kituo hicho Jana.

     Kiongozi wa Kikundi cha Kinamama cha Ahbaabur Rasuul, Ukhty Samia akipokea zawadi ya Jola ya Kitambaa kama sehemu ya Uwezeshwaji kiuchumi kwa akina Mama uliotolewa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation kwa ajiri ya unifomu za Wanafunzi wa Kituo Hicho.

   Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation walipokuwa katika picha ya Pamoja na wanafunzi wa Kituo cha Madrassa Mukarramah & Nursery School kilichopo Kipala Mpakani – Mkuranga, Pwani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 11/30/13--22:26: Article 22
 • 0 0

   Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu A.O. Chitanda, huku pia waandishi
  wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na
  Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;

  Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama,
  Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, mjadala wake kwa upande wa chama
  umeshafungwa, huku taratibu za kikatiba za ndani ya chama zikiendelea.

  Pili suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa
  taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya;
   
   *1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
  *2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).*
  *3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
  *4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
  *5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.


  Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake
  ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter
  Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.
  Kupata taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa  Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
    Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva katika mazungumzo. Kushoto ni mkewe, Mama Mero
  Picha ya pamoja Balozi Mero, Mama Mero na Bw. Azevedo.
  -----
  Mheshimiwa Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, amewasilisha hati za utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
   Katika mazungumzo,  Mkurugenzi Mkuu amemfahamisha Mh. Balozi  kuwa Shirika la Biashara Duniani liko katika hatua za mwisho ukamilisha majadiliano ya mikataba ya  Biashara ya Kimataifa katika maeneo matatu kwa pamoja  ikiwa ni masuala ya  Kilimo,  Maendeleo na  Uwezeshaji Biashara.
    Aidha,  Mkurungenzi Mkuu alielezea  mahusiano mazuri aliyonayo na nchi yetu kwa kipindi  kifupi akiwa kama Mkurugenzi Mkuu,  na  kuwa aliliona hilo wakati wa kampeini yake alipokuja nchini kuomba kura yetu. Ni kwa mantiki hiyo na imani aliyonayo kwa Tanzania, Mkurugenzi huyo ameomba Tanzania itumie ushawishi wake ili kufanikisha mkutano wa Mawaziri wa Biashara utakaofanyika mjini Bali, Indonesia, kuanzia tarehe 3-6 December 2013, ili kupitisha mikataba ya Biashara katika maeneo  matatu yaliyotajwa hapa juu.

  0 0

  Waziri  wa Nchi  Ofisi ya wa Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu wa pili  kulia akizindua ripoti ya Uwekezaji Tanzania  mwaka 2012, iliyokuwa ikionyesha hali ya uwekezaji wa mitaji binafsi kutoka nje na mtanzamo wa wawekezaji Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC),Bi. Juliet Kairuki, kushoto ni Naibu Gavana wa   Benki Kuu  (BoT), Dkt. Natu Mwamba.
  ---------------------------------------------------------------------------------

  TANZANIA imeendelea kufanya vizuri katika sekta mbalimbali za uwekezaji na kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa na ajira kwa watanzania hapa nchini. 
  Ripoti ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa uwekezaji katika sekta nyingi za uchumi zimefanya vizuri sana isipokuwa sekta ya kilimo bado haijafanya vizuri. 
  Akizindua ripoti hiyo mwishoni mwa wiki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dkt. Mary Nagu (pichani) alisema serikali bado inaendelea kufanyia kazi maeneo mbalimbali ili kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji nchini.
  “Kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kuongeza kasi ya uwekezaji katika sekta za madini na gesi ili kuisaidia nchi kupata faida zaidi na kutumia fursa hiyo kujenga miundombinu katika sekta ya ya Kilimo ili nayo iweze kuvutia uwekezaji zaidi,” aliongeza Dkt. Nagu. 
  Alisema ripoti hiyo imeonyesha uwekezaji wa mitaji binafsi kutokana nje na mtanzamo wa wawekezaji na hii imeweza kuonyesha mazingira ya uwekezaji nchini ni mazuri na yanavutia wawekezaji kuja kuwekeza. 
  “Ripoti inaonyesha kuwa Tanzania imeweza kufanikiwa kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, kutoka dola za Kimarekani milioni 6,941.5 mwaka 2008 hadi kufikia dola za Kimarekani milioni 9,278.1 mwaka 2011,” alisema. 
  Dkt. Nagu alisema Katika mazingira hayo serikali ingependa kuona ongezeko hilo la uwekezaji linaenda sambambana na maendeleo ya uchumi wa watanzania wa kawaida. “Lengo letu haswa, tunapenda watanzania walio wengi waweze kushiriki katika uchumi wao, wawezeshwe kwa maendeleo endelevu na kuchangia zaidi pato la taifa,” alisisitiza waziri huyo mwenye dhamana ya uwekezaji. 
  Ripoti hiyo imekuja baada ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Benki Kuu ya Tanzania (BoT)na Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS), kushirikiana kwa pamoja kufanya utafiti ambao umekuja na majibu yaliyolenga kuonyeha hali halisi na changamoto zilizopo ili kupata fursa ya kufanya maboresha mazingira ya uwekezaji hapa nchini. 
  “ Viongozi na wadau mbalimbali wanawajibika kutumia tafiti hiyo katika shughuli za maendeleo ili kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri kiuwekezaji na kuchangia maendeleo ya nchi,” alisema. Dkt.Nagu alisema kuwa serikali itatumia ripoti hiyo na kuhakikisha inakuwa ni sehemu ya kufanyia maboresho ya sera ya uwekezaji ambayo itaweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji nchini.
   Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki alisema utafiti huo ulihusisha Kampuni zilizowekeza Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ambapo utatumika katika kupanga mikakati zaidi ya kuongeza uwekezaji. 
  “Kazi kubwa ya kituo chetu ni kuhakikisha Tanzania inapata wawekezaji na tafiti hii ndiyo itatumika katika utendaji wa kila siku na kuupatia kipaumbele kufikia malengo yanayokusudiwa na taifa katika kuhamasisha na kuvutia wawekezaji,” alisema. 
  Bi. Kairuki alisema kuanzia mwaka 1996 hadi 2013 kituo kimeweza kusajiri miradi ya uwekezaji 8,487 kati ya hiyo miradi 4,230 ni ya watanzania, 2,119 ni ya wawekezaji kutoka nje ya nchi na 2,137 ni ya ubia.
   “ Miradi hiyo inatarajia kuajiri watu 1,223,122 na uwekezaji huo una thamani ya Dola za Kimarekani milioni 70,219.65 na pia kituo chake kimefanya utafiti na kubaini asilimia 80 ya miradi iliyosajiriwa na kituo inaendelea vizuri,” alisisitiza mkurugenzi huyo wa kituo. 
  Bi. Kairuki alisema kituo chake kinatafuta fedha kwa ajili ya kuangalia uwezo wa wawekezaji wa ndani sababu hadi sasa hakuna taarifa na picha stahiki juu ya uwekezaji huo. 
  Naye Mkurugenzi wa Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Dkt. Albina Chuwa alisema utafiti huo umefanyika kwa kufuta vigezo vya Ofisi ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa na iliweza kuwashirikisha watumiani katika ngazi zote za utekelezaji kukidhi mahitaji ya kutathimini na kufuatilia sera ya uwekezaji nchini. 
  “ Utafiti umehusu kampuni zote zenye mitaji kutoka nje, taarifa zao zilizokusanywa ni pamoja na vyanzo vya mitaji, aina ya uwekezaji na mchanganuo wake na pia kampuni hizo zilitoa mwitikio mzuri,”Dkt. Chuwa alisema. Alisema ofisi yake inahamasisha watunga sera, wanasiasa kutumia takwimu hizo kuboresha na kuongeza kasi ya uwekezaji hapa nchini.

older | 1 | .... | 281 | 282 | (Page 283) | 284 | 285 | .... | 3272 | newer