Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

TUNAELEKEZA NGUVU KWA TIMU YA VIJANA KUELEKEA AFCON UNDER 17 , MECHI YA TWIGA STARS -MAKONDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda @baba_keagan amemkabidhi Kijana Ikuzi Kicheko muhamasishani Mzalendo Kitita cha Shilingi Milioni 1 Baada ya Kujitolea Kutembea Kwa Mguu Kutoka MANYARA Mpaka DAR Kuja Kuhamasisha Ushindi Kwa Taifa Stars,Lakini Pia Viongozi wa TFF Wameahidi Kumpatia Zawadi zaidi na Kwa Kuanzia Wamempa Nguo Zikiwemo Jezi Original za Taifa Stars na Mpira Ili akirudi Mkoani Manyara Watu Wasimshangae na Kumkataa Tena Njiani.
 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMATI ya Saidia Taifa Stars ishinde imesema baada ya kufanikisha ushindi wa Taifa Stars sasa inaelekeza nguvu zake kuweke mikakati ya ushindi kwa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys inayojiandaa kushiriki kushiriki mashindano ya AFCON Under 17.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuna mashindano makubwa yanakuja ya AFCON Under 17 ambayo yatafanyika nchini Tanzania.

"Tunawaomba Watanzania tuendelee kushikamana na kuonesha umoja wetu kwa kuhakikisha timu yetu ya vijana inashinda michuano ya AFCON na kupata tiketi ya kwenda kushiriki kombe la Dunia la vijana linalotarajia kufanyika nchini Brazil.

"Tuna uhakika kwa umoja wetu na kwa mapenzi ya Mungu tutakwenda Brazil.Kikubwa ni kuwapa hamasa wachezaji wetu wa Seregeti Boys watafanya vema, katika mashindano ya AFCOM under 17 tunahitaji kushinda mechi mbili tu , tuna uhakika tutashinda na Kamati yetu imejipanga na tutaendelea kupeana taarifa kila kinachoendelea,"amesema Makonda.

Pia amesema kuwa Aprili 5, mwaka huu timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' nayo inacheza na ni jukumu la Watanzania kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwa kuinga mkono. "Tuna uhakika Taifa Stars itashinda katika mchezo wa Aprili 5, 2019 kwani katika Uwanja wa Mkapa yoyote atakayekuja atapigwa tu,'amesema Makonda.

YAMETIMIA NI RASMI JENGO LA WIZARA YA ARDHI LAKAMILIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA DODOMA

$
0
0
 Sura ya halisi ya Jengo la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya kukamilika rasmi katika mji wa Serikali Ihumwa mkoani Dodoma. Jengo hilo limejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kampuni yake ya ujenzi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa nje ya jengo la Wizara yake katika mji wa Serikali wa Ihumwa mkoani Dodoma alipotembelea leo tarehe 26 Machi 2019 kufuatia kukamilika ujenzi wake. Kushoto ni Mhandisi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Grace Musita.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa na Mhandisi wa ujenzi wa jengo la Wizara kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Grace Musita (Kushoto) leo tarehe 26 Machi 2019 alipotembelea kufuatia kukamilika ujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiooneshwa moja ya kazi zilizofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika ujenzi wa jengo la Wizara na Mhandisi wa ujenzi Grace Musita alipotembelea kujionea kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo katika mji wa Serikali Ihumwa Dodoma leo tarehe 26 Machi 2019.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiooneshwa eneo la Makatibu Muhtasi wa ofisi ya Waziri na Mhandisi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Ardhi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Grace Musita alipotembelea kujionea kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo kwenye Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma leo tarehe 26 Machi 2019.

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiooneshwa eneo la kunawia maji katika moja ya maliwato ya ofisi ya Waziri na Mhandisi wa Ujenzi wa jengo la Wizara ya Ardhi kutoka Shirika la NHC Grace Musita alipotembelea kujionea kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo katika mji wa Serikali Ihumwa Dodoma leo tarehe 26 Machi 2019.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa jengo la Wizara ya Ardhi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Grace Musita nje ya jengo alipotembelea kujionea kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo katika mji wa Serikali Ihumwa Dodoma leo tarehe 26 Machi 2019.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na akina mama wanaofanya usafi kwenye majengo ya Wizara yaliyopo katika Mji wa Serikali Ihumwa alipotembelea kujionea kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Wizara ya Ardhi katika mji wa Serikali Ihumwa mkoani Dodoma leo tarehe 26 Machi 2019.(PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-WIZARA YA ARDHI)

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu:Vyanzo maji visimamiwe kwa vizazi vya sasa na vijavyo

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa vyanzo vya maji ni lazima visimamiwe kuhakikisha rasilimali hiyo ya maji inapatikana ya kutosha na inakuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Huduma ya upatikanaji wa maji ambayo kupitia watoa huduma hiyo hususani mamlaka za maji, yanatokana na uhifadhi unaofanywa na Bodi za Maji za Mabonde (ambayo ni 9) yaliyopo nchini ambapo yanayotekeleza Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya Mwaka 2009.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde Wami/Ruvu Hamza Sadiki wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Warsha Maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa Usimamizi na Utunzaji wa Rasilimali za Maji iliyoandaliwa na Bodi.

Amesema Bodi hiyo ndio wasimamizi wa vyanzo vyote vya maji vilivyopo kwenye Bonde la Wami/Ruvu ambalo linapita kwenye mikoa 7 ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Manyara, Tanga na…hivyo ni lazima wasambazaji wote wa maji hayo wapate kibali kutoka bonde hilo.

Akisisitiza kuwa wananchi wengi wana uelewa mdogo kuhusiana na uhifadhi wa maji na kusababisha vyanzo hivyo kuingiliwa na shughuli mbalimbali za kibidamu zikiwemo uvuvi, kilimo pamoja na ufugaji.

“Vyanzo vya maji nchini chanzo kikuu ni mvua, hivyo kila mmoja akivuna maji ya mvua. Mwisho wa siku maji hayo yanayohifadhiwa chini ya ardhi na kutumika kama vyanzo vya chini na juu ya ardhi yatakosekana”, amesema Mwenyekiti.
Mwakilishi wa Afisa wa Maji wa Bonde la Wami\Ruvu Mshuda Wilson amesema kuwa visima vinavyochimbwa vinatakiwa kuwa na kibali kuendelea kumiliki kisima hicho ni kosa la kisheria.

Sheria inakataa uchafuzi wa mazingira na inapotokea mtu anachafua maji ikiwemo utiririshaji maji maji katika vyanzo vya maji yatakiwa kuipimwa na ndipo yaweze kurudishwa katika vyanzo hivyo. Amesema shughuli za kibidamu katika ndani ya mita 60 ya vyanzo ya maji zinazuiliwa kufanyika na kuwepo shughuli hizo ni kinyume cha sheria ya maji ya usimamizi wa rasilimali za maji. 

Amesema kuwa maji ya mvua nayo uvunaji wake unaangaliwa kwa kiwango endapo kiwango kitazidi zaidi lita 20,000 lazima uvunaji wa maji hayo yapate kibali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Hamza Sadiki. Akizungumza na waandishi wa Habari wa akifungua warsha ya Bonde la Wami/Ruvu

 Mwakilishi wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Mshuda Wilson akitoa taarifa Bonde la wami/Ruvu katika warsha ya waandishi habari kuhusiana na uhifadhi wa vyanzo vya maji

KESI YA MHASIBU WA TAKUKURU KUMILIKI MALI ISIYOLINGANA NA KIPATO CHAKE YAKWAMA TENA

$
0
0
*Ni baada ya mashahidi kukosa nauli ya kuwafikisha mahakamani 

Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

KWA mara nyingine tena, kesi ya kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake imekwama kuendelea kusikilizwa kwa kuwa mahakama haina fedha ya kuita mashahidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa amedai leo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa wameshindwa kuita mashahidi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu hawana fedha za kuwalipia nauli.

Mbagwa amedai kesi hiyo ilipangwa leo Machi 26, 2019 kwa ajiri ya kusikilizwa shahidi wa upande wa mashtaka lakini wameshindwa kuwaita mashahidi kwa sababu hawana fedha za kuwalipia nauli. 

"Tumeshindwa kupata mashahidi kwa sababu wote wanatoka nje ya Jiji la Dar es Salaam na wamesema hawana uwezo wa kujisafirisha kuja kutoa ushahidi, " amedai Mbagwa.Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa amedai anaomba suala la kuwaita mashahidi lifanyiwe kazi haraka.

Hata hivyo Hakimu Simba amesema, malipo ya mashahidi yana utaratibu wake na kwamba mahakama yake italifanyia kazi na watalitatua suala hilo kwani linazungumzika.Kwa kukumbusha tu ni mara ya pili kwa kesi hiyo imekwama kuendelea kusikilizwa baada ya mwanzoni mwa Oktoba mwaka jana kushindwa kusikilizwa kwa ukosefu wa fedha.

Kesi hiyo itasikilizwa Aprili 8, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu. Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Gugai na mwenzake watatu wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

Inadaiwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh.bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.

SABA KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAPIPA 20 YA MABAKI YA MADINI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii 

WATU saba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la tuhuma za wizi wa mapipa 20 ya mabaki ya madini yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 900. 

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Mbando, Wakili wa Serikali Jenifa Masue amewataja washtakiwa hao ni Jacob Kihombo, Yahaya Masoud, Mbaraka Lipinda, Ramadhani Zombe, Waziri Kibua, Mustapha Mnyika na Richard Sàngana. 

Imedaiwa kati Februari 6 na 7 mwaka huu ndani ni Jiji la Dar es Salaam washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa la kula njama ya wizi wa mali inayosafilishwa. 

Katika shitaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa waliiba mali hiyo ambayo ni mapipa 20 ya mabaki ya madini aina ya Tantalite Concentrates yenye thamani ya Sh.938,339,907 mali ya Kampuni ya Bollore Transport and Logistics. 

Shitaka la tatu linalomkabili mshtakiwa Zombe peke yake ambaye ni mlinzi, anadaiwa siku hiyo akiwa mwajiriwa wa Kampuni ya Bollore, kama mlinzi, alishindwa kuzuia kutendeka kwa kosa la wizi wa mapipa hayo ya madini. 

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka katika taasisi zinazotambulika na serikali watakaosaini bondi ya Sh. milioni 52 kila mmoja. 

Pia mdhamini au mshitakiwa ametakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya milioni 52. Kwa mujibu wa upande wa mashitaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. 

HDIF yakutanisha wadau wa sekta ya afya kujadili fursa na vikwazo katika kutumia tehama kwenye kukuza sekta ya afya

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MFUMO  wa teknolojia kwenye sekta ya afya utasaidia kupunguza matumizi ya makaratasi ambayo huchelewesha wagonjwa kupata huduma.

Hayo yamebainishwa leo Machi 26, 2019 na Mkurugenzi wa Ufundi wa Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya watu (HDIFl) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu yaliyoandaliwa na HDIF kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech).

Amesema matumizi ya makaratasi wakati wa uchukuaji taarifa za wagonjwa hutumia muda mrefu kuliko kutoa huduma husika hivyo matumizi ya Tehama yatachochea utoaji wa huduma bora za afya kwa wakati.

"Tumewakutanisha wadau wa afya pamoja na serikali na tulichojifunza ni wadau wa maendeleo kuhakikisha wanajua ni watu gani wa kuwasiliana nao ili kuanzisha mifumo ambayo haikuwahi kuanzishwa ili kusaidia kutoa huduma za afya na sio kila mdau kuwa na miradi  inayofanana nchini ambapo kufanya hivyo kutasaidia hivyo ni muhimu kuwasiliana na serikali kabla
ya kuanzisha miradi," alieleza Kaemdin.

 Kwa upande wake, Ofisa Tehama kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sultana Seif akiwasilisha mada,kuhusu hali ya utumiaji wa Tehama katika sekta ya afya amesema, utumiaji wa Teknolojia  Habari na Mawasiliano (Tehama), katika sekta ya afya  imekuwa na kufikia asilimia 70 ambayo imesaidia kurahisisha utoaji wa huduma bora katika vituo vya afya na hospitali nchini.

Amesema, pia mfumo hwa Tehama wa E-health unasaidia kufuatilia utoaji wa chanjo kwa watoto unaowawezeaha kutambua siku aliyozaliwa, chanjo alizopata na zile ambazo hakuzipata ili kuhamasisha  was a so kuwapeleka watoto wao kliniki kupata chanjo husika kwa ajili ya kuwakinga na magonjwa.

Seif amesema, kuwa mfumo huo ambao umeisha anza kutumika umeleta matokeo chanya kwa kuwa sasa mtu unauwezo wa kufuatilia upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba kwenye hospitali na vituo vya afya mijini na vijijini.

"Mfumo huu ulipoanza kutumika, mwaka 2015, watumishi wengi wa sekta hii ya afya hawakuukubali kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha lakini kutokana na mafunzo mbalimbali, wameukubali na sasa unatumika bila matatizo", amesema.

Amesema malengo makubwa ya mfumo huo wa E-health ni kusaidia taarifa kufikia vituo vya afya vilivyopo vijijini na  kutoa huduma bora kwa wakati.

Ameongeza kuwa, serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa sekta ya afya inatolewa kwa njia ya kidijitali ili kuboresha huduma hizo kwani kila mwananchi ana haki ya kupata huduma bora za  na ndio maana serikaki ikatafuta namna bora ya kuboresha huduma hizo na  kuzingatia usiri na usalama wa taarifa za wateja wetu.

Pia alisema wadau wa maendeleo na taasisi nyingine za serikali zimeshiriki kutengeneza mfumo huo kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa kuandaa mazingira ya usawa na haki.

Alieleza miongozo hiyo inasaidia wadau kufanya kazi kwa kufuata miongozo iliyowekwa kwa sababu kumekuwa na changamoto ya wadau wa maendeleo kuanzisha miradi ya afya na kisha kuiacha bila kuiendeleza hivyo hupoteza rasilimali na haileti manufaa.

Naye,ll Meneja Program wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana kutoka Shirika la  Amref, Dk Serafina Mkua amesema serikali imefanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya afya kwa njia ya kidijiti na sasa  inalekea kuondoka kwenye data ambazo zinakusanywa kupitia makaratasi na kwenda kwenye mfumo huo wa  E-health ambapo sasa watatumia simu na  kompyuta kukusanya taarifa.

"Miongozo ambayo imewekwa ni kitu kizuri ambacho kitasaidia wadau wote katika kutekeleza mikakati ambayo ipo lakini pia  kuleta bunifu zinazofuata miongozo ambayo ipo tayari.  Itasaidia  kuboresha utendaji lakini pia utoaji wa huduma kutokana na mabadiliko hayo," alisema Dk Mkua.
 Mkurugenzi wa Ufundi wa HDIF, Muzafar Kaemdin(kulia) akiongoza mjadala wa umuhimu wa matumizi ya Huduma bora za afya  kwa kutumia Teknohama. Uliohudhuriwa na wataalamu wa maendeleo ya afya wakati Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
 Meneja Program wa Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana kutoka Shirika la  Amref, Dk Serafina Mkua akizungumza na wataalamubwa afya namna serikali ilivyofanya  mabadiliko makubwa kwenye sekta ya afya kwa kitumia njia ya kidijitali wakati wa wiki ya ubunifu iliyoandaliwa na HIDF kwa kushirikiana na COSTECH.
 Ofisa Tehama kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sultana Seif(katikati) akiwasilisha mada kuhusu hali ya utumiaji wa Tehama katika sekta ya afya kwenye Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech).
Mjadala ukiendelea

VICE-PRESIDENT OF TANZANIA TO GRACE 7TH EAST AFRICAN HEALTH AND SCIENTIFIC CONFERENCE & INTERNATIONAL HEALTH EXHIBITION AND TRADE FAIR

$
0
0

EAST AFRICAN HEALTH RESEARCH COMMISSION


East African Health Research Commission, 26th March, 2019, Dar es Salaam, Tanzania: The Vice-President of the United Republic of Tanzania, H.E. Samia Hassan Suluhu, will on Wednesday, 27th March, 2019 to grace the official opening of the 7th East African Health and Scientific Conference (EAHSC) at the Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam, Tanzania.

The biannual event, which is the 7th in the series, is being held under the theme “Technology for health systems transformation and attainment of the UN-Sustainable Development Goals.’’

The EAHSC brings together stakeholders from the health sector within the EAC namely EAC Organs and Institutions, EAC Partner States' Ministries of Health, Finance, Higher Education, Science and Technology, Members of Parliament from National Assemblies, government officials, researchers, scientists, practitioners, civil society, media, donors and development partners and the public at large.

Addressing Journalists in a media briefing ahead of the conference, the Executive Secretary of the East African Health Research Commission, Prof. Gibson Sammy Kibiki, said the EAHSC contributes towards strengthening regional cooperation in health in line with Article 118 of the Treaty for the Establishment of EAC as well as other relevant provisions of the EAC Common Market Protocol.

“It enhances the ideals of the EAC, which is free movement of People, Services, and Goods,” said Prof. Kibiki.

During the conference several EAHRC initiatives will be launched including Digital REACH Strategic Plan, EA Web Portal, Young East African Health Research Scientists Forum (YEARS), East African Government Leaders, Legislators, and Legal Executives’ Forum (EAGLES), 6th EAHSC Report, and the book of abstracts on Digital Health in East Africa, among other activities. 

At the end of the conference, participants are expected to get to know new health projects, build networks for future collaboration, find out what's new in the region and future research trends in East Africa.

Exhibition 
Alongside the conference, there will be an international health exhibition. Research institutions, health care facilities, medical/health academic institutions, medical and pharma industries, NGO's, CSO's, Ministries, EAC Organs and Institutions, International organizations, UN agencies (WHO, UNICEF, UNFPA, UNESCO, etc.) will showcase their services and products.
The exhibition will allow participants to showcase products from research, academia, healthcare services and the health sector in general.

Media Accreditation
All Local (Tanzanian) Journalists intending to cover the 7th East African Health and Scientific Conference (EAHSC) are alerted that registration for accreditation will be done through:

MS GAUDENSIA SIMWANZA

MANAGER, COMMUNICATION AND PUBLIC EDUCATION
TFDA 


All Foreign Journalists seeking accreditation must register through: 

FLORIAN MUTABAZI 

MEDIA COORDINATOR 
EAC SECRETARIAT


For more information on 7th East African Health and Scientific Conference (EAHSC) please visit:http://conferences.eahealth.org


Corporate Communications and Public Affairs Department

EAC Secretariat

Arusha, Tanzania



TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOA WA MBEYA

$
0
0


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu ishirini na moja [21] kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za uganga bila kibali.


KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO YA WIZI.


Mnamo tarehe 23.03.2019 saa 14:39 mchana huko eneo na Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata JOSEPH MGAYA [27] Mkazi wa Ilomba akiwa na Pikipiki MC 395 BYN aina ya Kinglion ambayo mtuhumiwa amekiri kuiiba Pikipiki hiyo huko Kijiji cha Lupatingatinga Wilaya ya Chunya. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.


KUFANYA SHUGHULI ZA UGANGA BILA KIBALI.


Mnamo tarehe 25.03.2019 saa 00:10 usiku huko katika Kitongoji cha Mapinduzi 'B' kilichopo katika Kijiji cha Idunda, Kata ya Itewe, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata PASCHAL PATRICE [30] Mkazi wa Kijiji cha Idunda na wenzake 19 wakifanya shughuli ya uganga bila kibali.


Watuhumiwa wote wakiwemo wanawake 03 walikutwa wakiwa kwenye nyumba ya mtu aliyefahamika kwa jina moja la MWARABU mkazi wa Dar es salaam. Pia katika nyumba hiyo wamekutwa watu watatu wote wanaume waliokuwa wamekwenda kutibiwa hapo. 

Upekuzi umefanywa ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kupata begi ambalo ndani yake likiwa na kibuyu kimoja, chupa mbili za plastiki zenye unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kienyeji, kikopo cha plastiki cha njano chenye unga unaodhaniwa kuwa dawa za kienyeji zinazotumiwa na waganga kutolea tiba pamoja na ngoma moja. Upelelezi unaendelea.


 

 

KUSAFIRISHA BIDHAA NJE YA NCHI BILA KIBALI.


Mnamo tarehe 24.03.2019 saa 12:15 mchana huko Kitongoji cha Mwambuluko, Kijiji cha Isaki, Kata ya Katumbasongwe, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa mbeya. Askari Polisi walikamata gari moja lenye namba T. 268 BNH aina ya Mitsubishi Fuso truck likiwa limebeba magunia yenye nafaka mahindi makavu yapatao magunia 88 mali ya mtu mmoja aitwaye DORIN KAONGA [35] Mmalawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Kalonga - Malawi na GLORY KAFWILA [32] Mmalawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Kalonga - Malawi.


Dereva wa gari hilo alikimbia kusikojulikana na msako mkali wa kumtafuta unaendelea. Gari hilo lilikua likielekea kivuko haramu cha Nyasa katika mto Songwe mpakani mwa nchi ya Tanzania na Malawi kwa ajili ya kuyavusha magunia hayo ya mahindi kwa mitumbwi kuelekea nchi hiyo jirani ya Malawi.


Gari hilo lililotumika kubeba magunia hayo ya mahindi ni mali ya mtu mmoja aitwaye SHABAN ADIL KAJUNI wa huko Wilaya ya Rungwe. Vielelezo gari hilo na magunia hayo ya mahindi vimekabidhiwa mamlaka ya mapato idara ya forodha Kasumulu na hatua zaidi za kisheria. Upelelezi unaendelea.


Imetolewa na:

 [ULRICH O. MATEI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 

Vifaa vya Uganga vilivyokamatwa 
Kivuko haramu kinacjotumiwa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kupitisha bidhaa kwenda nje ya nchi. 
 Magunia ya Mahindi yaliyokamatwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani ya Malawi bila kufuata utaratibu.

 

Kibuyu na vifaa vingine vilivyokamatwa. 

 Gari aina ya FUSO lililokuwa likisafirisha magunia ya Mahindi kwenda nchini Malawi kwa njia ya magendo.

Wanakamati wa Afya kutunukiwa cheti cha Uzalendo Kijiji cha Kirando

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mwenye kapolo) akimsalimia mmoja wa mama waliojifungua katika kituo cha afya Kirando ambacho kimekamila upanuzi wake na kuanza kutumika (kushoto) Daktari mfawidhi wa Kituo hicho Dkt. hashim Mvogogo.

…………………………..

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuhakikisha anawapatia wanakamati ya upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya Kirando cheti cha uzalendo pamoja na kifuta jasho baada ya wanakamati hao kuonesha uvumilivu na kushirikiana na serikali katika upanuzi wa kituo hicho bila ya kudai posho ya aina yeyote.

Amesema kuwa pamoja na wanakamati wengine kukimbia kutokana na kukosa malipo ya aina yeyote wakati wakiendelea na usimamizi wa upanuzi wa kituo hicho cha Afya wao waliendelea kusimama imara ili kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo na hatimae wananchi wa Kijiji, Kata na Tarafa ya Kirando waweze kufaidika na juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya afya katika Mkoa wa Rukwa.

“Na mtayarishe Mkurugenzi cheti cha Uvumilivu, na mkono mtupu haurambwi mtayarishe na hata senti Fulani mle ndani iwe posho yao kwasababu hawajapata posho hata sumuni, kwahiyo muangalie mtajibana wapi ili cheti kiambatane na kifuta jasho tutakuwa tumewatendea haki na wengine wataiga,”Alisema.

Wakati akielezea siri ya kusimama imara Mwenyekiti wa kamati kituo cha afya Kirando ambae alikuwa mjumbe katika kamati ya ujenzi kwaajili ya upanuzi wa kituo hicho Seetbert Kapalata alisema kuwa anamshukuru mheshimiwa Rais kwa kuwafikiria watu wa Kijiji cha kirando na kuwapelekea mradi huo.

“Kweli tunamsukuru mheshimiwa Rais kwani ni jambo la kipekee sana ilikuwa sio rahisi kufikiria kwamba tunaweza kuapata kitu kama hiki miaka imepita mingi lakini hatujapata jambo kama hili kwahiyo ilikuwa ni lazi sisi tuunge mkono jitihada hizo, inawezekana akaja mwingine asifikieriea vituo vya afya akafikiria mambo mengine lakini bila ya afya hakuna kingine katika maisha,” Alisema.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Kituo hicho ambae nae alikuwa katibu wa Kamati Dkt. Hashim Mvogogo wakati akitoa taarifa ya Kituo hicho cha afya alisema kuwa upanuzi huo umesaidia kuboresha huduma za upasuaji na maabara, jengo la wodi ya wajawazito pamoja na nyumba ya daktarin.

“Wodi ya akinamama imeboreshwa na hadi sasa jengo hilo lina uwezo wa kulaza kina mama 25 kwa wakati mmoja, vilevile chumba cha kujifungulia kina uwezo wa kubeba wajawazito wanne kwa wakati mmoja, hivyo tunaishukuru serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna alivyoweza kutuboreshea huduma katika kituo chetu,” Alimaliza.

Ujenzi wa Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Kirando ulianza mwezi Februari mwaka 2018 na kumalizika mwezo Oktoba mwaka 2018 na kugharimu shilingi milioni 412 kwaajili ya ujenzi wa jengo la maabara, wodi ya wajawazito, jengo la upasuaji na nyumba ya daktari.

Waziri Biteko afanya mazungumzo na Kampuni ya PRNG Minerals ya Marekani

$
0
0
Waziri wa Madini  Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd, ya  Marekani, Rocky Smith na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield ofisini kwake Jijini Dodoma. 
Watendaji hao wapo nchini kwa ziara ya kawaida ya kikazi ya siku tano  ambapo waliomba kukutana na Waziri wa Madini.
 Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo inakusudia kuwasilisha taarifa juu ya hali na Maendeleo ya soko la dunia kwa Madini ya Rare Earth Elements na kuzungumzia hatua iliyofikiwa kwa ombi la leseni ya  uchimbaji  Mkubwa wa madini hayo. 
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko  amesema wizara iko tayari kuipokea kampuni husika nchini baada ya kukamilika kwa taratibu kwa mujibu wa sheria. 
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu Rocky Smith, amesema kuwa, amefurahishwa na  ushirikiano unaooneshwa na wizara na kuahidi kuanza shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa taratibu.
 Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd kutoka Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo akiwa ameambatana na Mkurungenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield wa kwanza kulia, na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za sheria Wizara ya Madini Edwin Igenge.
Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd kutoka Marekani Rocky Smith kushoto kwa Waziri. Smith alimtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma kwa mazungumzo, wa kwanza kushoto ni Ali Ali, Kamishna Msaidizi Uendelezaji Migodi na Madini Wizara ya

IFM KUJENGA TAWI JIPYA SIMIYU

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), walipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta alipomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne A. Sagini (wa pili kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati), baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Simiyu (watatu wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tano kulia) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta(kulia) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto), akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Mwenyekiti wa RAAWU Taifa, Dkt. Micahel Mawondo akizungumza jambo wakati Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kushoto) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi , kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne A. Sagini (katikati), baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Simiyu (watatu wa mwanzo kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta( wa tatu kulia mbele) na watumishi wengine wa chuo hicho walimpomtembelea ofisini kwake Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea na kuona eneo lililotolewa bure na Mkoa wa Simiyu katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi, kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la Chuo hicho mkoani hapa.
.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinatarajia kujenga Tawi jipya katika Kata ya Sapiwi Tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Viongozi wa chuo hicho wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tadeo Andrew Satta wametembelea eneo hilo Machi 26, 2019 na baadaye kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Mkoa wa Simiyu ambapo wamekubaliana kushirikiana katika hatua zote kuanzia upimaji wa eneo mpaka ujenzi wa majengo ya chuo.

Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Andrew Satta amewashukuru viongozi hao kwa kutoa eneo la ekari ishirini bure akaahidi kushirikiana na Serikali mkoani hapa kuhakikisha tawi hilo linajengwa mkoani Simiyu ili kusogeza karibu huduma kwa wananchi wa Simiyu.

Awali akizungumza na viongozi hao Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo iko tayari kushirikiana na viongozi wa Chuo hicho kwa kutoa wataalam watakaosaidia katika Usimamizi wa upimaji na akashauri ujenzi wa majengo ya chuo hicho ufanyike kwa kutumia mfumo wa ‘Force Account’ ili kupunguza gharama.

Amesema mfumo huu utapunguza gharama kwa kuwa hautumii wakandarasi badala yake ujenzi utafanywa na mafundi wa kawaida wakisimamiwa na wahandisi wa ujenzi Mkoa na Halmashauri mkoani Simiyu huku vifaa vyote vya ujenzi vikinunuliwa kwa pamoja na chuo hicho.

Aidha, amemhakikishia upatikanaji wa wanafunzi kwa kuwa hadi sasa Mkoa wa Simiyu bado una Vyuo vichache vya elimu ya juu, huku akibainisha kuwa tayari Serikali mkoani hapa imeshatoa ardhi bure kwa ajili ujenzi wa Matawi ya Vyuo mbalimbali vya elimu ya juu ikiwemo Chuo cha Mipango, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo cha Mahakama.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema wanaendelea kushawishi Taasisi nyingi za Elimu ya Juu kujenga matawi yake Mkoani hapa, ili kutoa nafasi kwa Wanasimiyu kupata elimu ya juu itakayochangia kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii

SERIKALI YA MAREKANI KUFADHILI MAFUNZO YA KILIMO KINACHOENDANA NA HALI YA HEWA KWA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MITAA NCHINI TANZANIA

$
0
0


Morogoro.

Viongozi na wadau kutoka baadhi ya mikoa na wilaya nchini Tanzania wamekutana Morogoro, Machi 25-29, kwa mafunzo ya Serikali yaliyofadhiliwa na Serikali ya Marekani kuhusu namna ya kupanga mikakati na kusaidia wakulima wadogo ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutekeleza kilimo kinachoendana na hali ya hewa. Mafunzo kama haya yatafanyika Unguja, Zanzibar, Aprili 1-5.

Programu ya mafunzo, “Landscape Climate-Smart Agriculture Pilot Course,” inafanywa na timu ya wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha California, Davis; Idara ya Kilimo ya Marekani (USDA); Chuo kikuu cha Cornell; kampuni ya EcoAgriculture; na Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo (IITA) na fedha kutoka Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Mafunzo haya ni sehemu ya Mradi wa kujenga uwezo wa upatikanaji wa Chakula, ambao ni mpango wa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na USDA na USAID. Mradi huu unaainisha mapungufu ya uwezo wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri kilimo. Mradi huu unatekelezwa na IITA, FAO, na World Agroforestry Center.

Kilimo kinachoendana na hali ya hewa kinafafanuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kama kilimo ambacho huongeza uzalishaji wa chakula na mapato ya wakulima, hupunguza uzalishaji wa gesi zinazochangia ongezeko la joto, na hukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Mbinu hii inasaidia sekta ya kilimo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwenye hali ya hewa kama ukame, mvua finyu na mafuriko, pamoja na kukidhi ongezeko la mahitaji ya chakula.

Ili kuomba taarifa zaidi, tafadhali piga simu Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kupitia: +255 22 229-4000 au barua pepe: DPO@state.gov.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF

$
0
0
RAIS WA TFF WALLACE KARIA AWASHUKURU WATANZANIA KUIUNGA MKONO TAIFA STARS 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) ametoa shukrani za dhati kwa Serikali,Taasisi Mbalimbali,Vyombo vya Habari,Vyombo vya Usalama na kila Mtanzania kwa kuiunga mkono Timu ya Taifa “Taifa Stars”.

Amesema TFF inaamini kila mmoja alihamasika kuiunga mkono Taifa Stars hasa kutokana na kiu ya kila mmoja kuona  inacheza AFCON.

“Hakika ilikuwa hamasa kubwa na Uzalendo wa hali ya juu ambao unapaswa kupongezwa kwa namna ambavyo kila mmoja alijitoa kwa nafasi yake kwaajili ya timu yake ya Taifa” Amesema Rais wa TFF Ndugu Karia.

Uungwaji mkono uliofanyika kwa Taifa Stars ni sehemu kubwa ya morali kwa wachezaji na TFF inaamini Watanzania wataendelea kuziunga mkono timu za Taifa na Wawakilishi wa Tanzania wanaokabiliwa na mashindano ya Kimataifa.

Kwasasa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” ipo Kambini ikijiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Olympic dhidi ya DR Congo utakaochezwa April 5,2019,Pia timu ya Vijana U17 “Serengeti Boys” ipo Kambini ikijiandaa na mashindano ya AFCON ya Vijana U17 yatakayofanyika Tanzania April 14-28,2019.

Karia amewaomba Watanzania waziunge mkono timu hizo kwa kujitokeza kwa wingi ili kuwa sehemu ya hamasa ya kufanya vizuri kwa timu zetu.

TFF itaendelea kuhakikisha timu hizi zinapata maandalizi mazuri ili kupata matokeo chanya katika mashindano yanayowakabili.

Ni Imani ya TFF kuwa Watanzania wataendelea kujitokeza kwa wingi Uwanjani kuziunga mkono timu zetu kama ilivyokua kwa Taifa Stars.

Vyombo vya Habari ambao ni moja ya Wadau wakubwa tunaamini tutaendelea kushirikiana katika kuhamasisha pia kwa timu zilizopo Kambini.


TFF YAFAFANUA NAMNA YA UUZAJI TIKETI 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),limetoa ufafanuzi wa namna ya uuzaji tiketi katika Viwanja vya Mikoani na  Dar es Salaam.
Katika tiketi zote ambazo zinakatwa katika michezo ya Mikoani zinasimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEM) na kwa Viwanja vya Dar es Salaam, zoezi hilo linasimamiwa na wamiliki wa Viwanja.
TFF katika zoezi hilo imekua ikitaja bei ya tiketi na madaraja yake na kuacha kazi kwa mamlaka husika za TAMISEMI na Uwanja kupanga namna ya ukusanyaji wa mapato kupitia tiketi.
Hivyo TFF haina dhamana ya kuuza tiketi.

RAIS WA TFF WALLACE KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA KIJANA ALIYEFIA UWANJA WA TAIFA 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Familia ya kijana Ibrahim Hassan (7) aliyefariki nje ya uwanja wa Taifa Jumapili Machi 24,2019 katika mchezo wa kutafuta tiketi ya Afcon Tanzania dhidi ya Uganda.

Rais wa TFF Ndugu Karia,amesema amepokea kwa huzuni taarifa za kijana huyo  ambaye alikuwa na kiu ya kushuhudia mchezo huo.

Amesema Shirikisho limeumizwa na tukio lililotokea na kusababisha mauti ya kijana huyo. Kwa niaba ya TFF  ametoa pole kwa familia,jamaa,marafiki na wapenzi wa soka.

TFF inatoa ubani wa kiasi cha Shilingi 500,000 kwa familia ya kijana huyo.

DC KASESELA: WANAUME KUWALIPA MISHAHARA WAKE ZAO WAKIWAKATAKAZA KUFANYA BIASHARA.

$
0
0
NA FREDY MGUNDA,IRINGA. 
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wanaume kulipa mshahara kila mwezi wake zao endepo watawakataza wake zao kufanyabiashara la sivyo wawaache wake hao wafanyebiashara kwa uhuru. 
 Akizungumza na wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye shule zaidi ya saba za wilaya ya Iringa,Kasesela alisema hivyo kutokana na maswali ya wanafunzi hao waliouliza “kwanini wanaume wamekuwa wakiwakataza wake zao kufanya biashara?” 
 Kasesela alisema kuwa wanawake wamekuwa wafanyabiashara wazuri na wenye bahati ya kupata faida na kuweza kuendesha family pamoja na kuongeza kipato cha familia,kumkata wanamke kufanya biashara kunadumisha uchumi wa familia na nchi kwa ujumla. “Naomba niwaambie wanafunzi kuwa mama zenu ndio wamekuwa msingi mkubwa wa kuijenga familia na kuleta maendeleo ya familia pale panapokuwa na maendeleo baina ya baba na mama hapo ndio familia hizo utaona zinavyokuwa na maendeleo” alisema Kasesela 
 Hata hivyo Kasesela alisema,Wanawake wamekuwa waaminifu,watumiaji wazuri wa mikopo,wanajua kupanga bajeti za familia hivyo ukimwacha mwanamke afanye biashara kwa uhuru lazima familia itapata faida kubwa tofauti na ukimyima mwanamke fursa ya kufanya biashara. “Wanaume ndio tumekuwa tukilazimisha kuchukua pesa za mwanamke na kuzitumia vibaya na kuwasababishia hasara wanawake lakini ukiwaacha wafanye biashara utaona wanavyofanya maendeleo kwa kasi kubwa” alisema Kasesela 
 Kasesela aliwapongeza lyra in Africa kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike juu ya kuvunja mila potofu za kimila kwa wanawake ili kuwawezesha wanawake kushika nafasi mbalimbali ya uongozi na kujikomboa kiuchumi. 
 “Lyra in Africa mmekuwa mkiisaidia sana serikali ya wilaya ya Iringa kwa kuwajenga uwezo wanafunzi wa kike kwa kuwa kufanya hivyo kunasaidia kuikomboa jamii kwa ujumla hivyo juhudi zetu zinaonekana na mimi kama mkuu wa wilaya nafurahi uwepo wenu” alisema Kasesela 
 Kasesela alisema,lyra in Africa wamekuwa wakiboresha mazingira ya wanafunzi wa kike kwa kuwajengea mabweni kwenye baadhi ya shule za sekondari zilizopo hapa katika wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivyo ni lazima kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya.
 Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Lyra in Africa mkoa wa Iringa Roserine Malike aliwataka wanafunzi wa kike kusimamia vilivyo ndoto zao katika maisha iliwayumbishwe na wanaume yoyote yule kwa lengo la kutengeneza maisha yao hapo baadae. “Nyie wanafunzi wa kike mnatakiwa kuwa na msimamo katika maisha yenu kwa kipicho cha maisha ili kujenga maisha yaliyo bora na kuwa mfano kwa wanafunzi wengine wa kike kwa lengo la kuikomboa wanafunzi wengine wa kike hapa nchini” alisema Malike 
 Malike aliwataka wanafunzi hao wakike kucha tabia ya kufanya ngono wakiwa bado wanafunzi na kuwasababisha kuharibu ndoto zao wakiwa na umri mdogo na kuongeza kuwa na vijana wengi mtaani wasio na ajira. 
 “Nafikiri mmeona wasichana wengi walipota mimba wakiwa mashuleni wanavyohangaika mtaani kwa kuwa walipoteza ndoto zao wakiwa bado wadogo hivyo mnatakiwa kuwa makini na kudanganywa na wanaume kwenye umri mlionao kwa kuwa starehi hizi zipo tu kila siku” alisema Malike 
 Nao baadhi ya wanafunzi hao wa kike walimweleza mkuu wa wialaya changamoto ya mfumo wa elimu ulivyojikita wanafunzi kutegemea kuajiliwa pindi wamalizapo chuo au elimu yote hivyo wamemuomba kufikisha kilio hicho serikalini ili waangalie mfumo huo upya.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa ushauri kwa baadhi ya wanafunzi wa kike juu kujikinga na mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikiharibu ndoto za wanafunzi wengi wa kike.
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akibadilisha mawazo na wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye shule za sekondari zaidi ya saba kwenye wilaya ya Iringa pamoja na viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa
Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kutoka wa mmoja ya viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye shule za sekondari zaidi ya saba kwenye wilaya ya Iringa pamoja na viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 26.03.2019


RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

SPIKA JOB NDUGAI ATEMBELEA OFISI YA CCM MKOA WA KASKAZINI UNGUJA MJINI ZANZIBAR

$
0
0


Spika wa Bunge, Mlezi wa CCM Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Job Ndugai (kulia) akigawa kadi kwa mwanachama mpya wa Umoja wa Vijana CCM wakati wa zoezi la kugawa kadi kwa wanachama wapya wa CCM tukio lililofanyika jana Machi 26, 2019 Jimbo la Kiwengwa Muembe Majogoo Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjini Zanzibar. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Spika wa Bunge, Mlezi wa CCM Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Job Ndugai akiweka jiwe la msingi Tawi la CCM Muembe Majogoo kabla ya kuzungumza na viongozi wa Matawi, Wadi na Jimbo jana Machi  26 , 2019 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjini Zanzibar.
Spika wa Bunge, Mlezi wa CCM Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Job Ndugai (kulia)akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani, Ndg. Nadir Abdulatif wakati alipowasili na kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja na Wajumbe wa Baraza Kuu ya Jumuiya za Chama Mkoa na Wilaya zake katika kikao kilichofanyika 
jana Machi  26 , 2019  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjini Zanzibar.
Spika wa Bunge, Mlezi wa CCM Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Job Ndugai akicheza Ngoma za Utamaduni wa Watu wa Mkoa wa Unguja wakati akikagua Ngoma hizo katika Ofisi ya CCM Mkoa wa kaskazini Unguja tukio lililotokea 
jana Machi  26 , 2019  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjini Zanzibar.
Spika wa Bunge, Mlezi wa CCM Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja na Wajumbe wa Baraza Kuu ya Jumuiya za Chama Mkoa na Wilaya zake alipowatembelea 
jana Machi  26 , 2019 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja, Wajumbe wa Baraza Kuu ya Jumuiya za Chama Mkoa na Wilaya zake wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) katika kikao kilichofanyika 
jana Machi  26 , 2019  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjini Zanzibar.
Spika wa Bunge, Mlezi wa CCM Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Chaani, Ndg. Nadir Abdulatif akielezea changamoto mbali mbali ambazo wanakumbana nazo Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja na Wajumbe wa Baraza Kuu ya Jumuiya za Chama Mkoa na Wilaya zake katika kikao kilichofanyika 
jana Machi  26 , 2019  katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mjini Zanzibar.

Mawaziri wa Afrika wakutana Morocco

$
0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Mhe. Nasser Bourita,  baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano.

Dkt. Mnyepe amemwakilisha Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika kuhusu maamuzi ya Umoja wa Afrika (AU) kuunga mkono jitihada za usuluhishi wa mgogoro wa eneo la Sahara Magharibi kati ya Morocco na Saharawi uliofanyika jijini Marrakech, Morocco tarehe 25 Machi, 2019.
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe akifuatilia mazungumzo na michango ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe wa tatu kutoka kushoto, mstari wa nyuma, akiwa katika picha ya pamoja ya Mawaziri na Wawakilishi wa Mawaziri walioshiriki mkutano huo.

Mtanzania ateuliwa kuongoza Taasisi ya Kimataifa nchini China

$
0
0


Balozi Mstaafu, Mhe. Ali Mchumo (Pichani) kutoka Tanzania ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya International Network for Bamboo and Rattan (INBAR) yenye makao yake makuu mjini Beijing, China. 
Taarifa ya uteuzi wake imetangazwa tarehe 25 Machi 2019 katika tovuti ya taasisi ya INBAR. Taasisi ya INBAR ilianzishwa mwaka 1997 kwa madhumuni ya kukuza matumizi ya mianzi (Bamboo) kama njia endelevu ya utunzaji wa mazingira . 

Taasisi hiyo inaundwa na nchi wanachama 45 na ina ofisi zake za kanda nchini  Ethiopia, Ghana na Equador. Tanzania ni mojawapo ya nchi mwanachama mwanzilishi wa taasisi hiyo na imenufaika na uwepo wa taasisi hiyo kupitia miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na INBAR pamoja na mafunzo kwa wataalam wa zao la mianzi. 

HABARI ZA UN KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images