Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

TABORA YAGUNDUA WAGONJWA 2,369 KATI YA 2,850 WA TB WALIOKUSUDIWA MWAKA JANA

0
0
MKOA wa Tabora ulilenga kugundua wagonjwa wa kifua kikuu, 2850 kwa mwaka 2018 lakini ulifanikiwa kugundua wagonjwa 2,369 wa kifua kikuu ikiwa sawa na asilimia 83 ya malengo uliojiwekea.

Kauli hiyo imetolewa mjini Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa mwaka 2019 ambapo kimkoa yamefanyika wilayani Nzega.

Alisema sababu ambazo zilisababisha kutoweza kufikia malengo hayo ni pamoja na uelewa mdogo wa jamii kuhusu kifua kikuu na uchache wa vituo vya tiba vinavyoweza kupima na kudhibitisha ugonjwa kifua kikuu.

Mwanri alisema juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisa wanatafuta wagonjwa wote wa kifua kikuu na kuwaweka kwenye matibabu sahihi.

Alisema elimu sahihi juu ya kifua kikuu, uimarishaji wa huduma za kifua kikuu na kubadili tabia vinhitajika kwa kiwango kikubwa, ili wananchi waweze kujua dalili mapema na kutumia huduma za afya.

Mwanri alitoa wito kwa wadau wote wa afya na wasio wa afya kuungana na Serikali katika mapambano dhidi ya kifua kikuu, uhamasishaji unaolenga kubadili tabia pamoja na watoa huduma kuungana pamoja ili kuhakikisha elimu kuhusu kifua kikuu inatolewa na huduma za kifua kikuu zinapatikana kiurahisi.

Naye Mganga wa Mkoa wa Tabora(RMO) Dkt. Honoratha Rutatinisibwa alisema lengo la maadhimisho haya ni kukumbusha, kuelimisha na kushirikisha jamii katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, na hivyo kuongeza uibuaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu, kuwapatia matibabu na hivyo kupunguza na kutokomeza ugonjwa huu wa hatari unao sababisha vifo vya watu wengi.

Alisema Mkoa wa Tabora suala la uibuaji wa wagonjwa Kifua Kikuu unaongezeka kila mwaka ambapo takwimu zinaonesha idadi ya wagonjwa walioibuliwa imeongezeka kutoka 1,751 kwa mwaka 2014 hadi 2,369 kati ya lengo la kwa mwaka 2018.

Dkt. Rutatinisibwa alisema kiwango cha maambukizi ya Kifua Kikuu kwa takwimu za 2018 kwa mkoa wa Tabora ni wagonjwa 269 kwa kila watu laki moja hivyo kuwa na makadirio ya wagonjwa 7000.

Aliongeza kuwa huduma shirikishi za Kifua Kikuu na VVU zinaendelea kutolewa ambapo kwa mwaka 2018 idadi ya wagonjwa wa Kifua Kifuu 2,271 sawa na asilimia 95.9 walipimwa VVU kati ya hao 837 sawa na asilimia 36.9 walikutwa na maambukizi ya VVU na wote walianzishiwa dawa za kufubaza VVU.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kifua kikuu mwaka huu ni wakati ni huu tuunganishe nguvu katika kutokomeza kifua kikuu. Mwisho
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(katikati) na Mganga wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa(kshoto) wakijadiliana wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa mwaka 2019 ambapo kimkoa yamefanyika wilayani Nzega ambayo kauli mbiu inasema wakati ni huu .tuunganishe nguvu katika kutokomeza kifuaa kikuu.
 Mganga wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa akitoa maelezo kuhusu hali ya kifua kikuu mkoani Tabora wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa mwaka 2019 ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Nzega.
 Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifuaa Kikuu na Ukoma(NTLP) Dkt. Liberate Mleo akitoa maelezo kuhusu hali ya kifua kikuu nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa mwaka 2019 ambapo Tabora kimkoa yamefanyika wilayani Nzega.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa mwaka 2019 ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Nzega.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa mwaka 2019 ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Nzega.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Nzega wakiwasikiliza viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani kwa mwaka 2019 ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Nzega. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema wakati ni huu tuunganishe nguvu katika kutokomeza kifuaa kikuu. Picha na Tiganya Vincent

Mama Napono Sokione mtembelea Mama Maria Nyerere

0
0
Mama Maria Nyerere na akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni wake, mjane wa Waziri Mkuu wa zamani, Mama Mama Napono Sokoine aliyemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha (kutoka kushoto) ni msaidizi wa Mama Maria, Wambura; Mbunge wa Viti Maalumu, Namelok Sokoine, Elysia Sokoine; na Ninai Sokoine. Mbuzi anayeonekana ni zawadi ya Mama Sokione aliyopelekea Mama Maria.

NEC YATANGAZA KUANZA UBORESHAJI WA MAJARIBIO

0
0
Na Margareth Chambiri

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kwa majaribio katika Kata mbili za Kibuta iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani na Kihonda katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoani Morogoro.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne Tarehe 26. 03. 2019) imesema Uandikishaji huo wa Majaribio utakaoanza Machi 29, hadi Aprili 04, 2019 utafanyika katika vituo 20 vya kuandikisha Wapiga Kura ikiwa ni vituo 10 katika kila Kata.  

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uandikishaji huo unalenga katika kuvifanyia majaribio vifaa na mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura ili kubaini changamoto kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo.

Imezitaja sifa za watu watakaoandikishwa katika uandikishaji huo kuwa ni raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 au atakayetimiza umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi  Mkuu ujao.

Aidha uandikishaji huo hautawahusu raia walio chini ya kiapo cha utii wa nchi nyingine, aliyebainika kuwa hana akili timamu au yuko kizuizini kama mhalifu mwenye ugonjwa wa akili au yuko kizuizini kwa ridhaa ya Rais.

Taarifa hiyo imeendelea kutaja watu ambao hawatahusika katika majaribio hayo ya uboreshaji kuwa ni mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama au anatumikia kifungo kinachozidi miezi sita pamoja na mtu aliyepoteza sifa za kuandikishwa kuwa Mpiga Kura chini ya Sheria za Uchaguzi au Sheria nyingine yoyote inayohusu makosa ya uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawajulisha wakazi wa Kata hizo zinazofanya Uandikishaji wa Majaribio na ambao walijiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 kuwa wanaweza kutumia fursa hiyo kuhakiki taarifa zao katika vituo walivyojiandikishia.

Wakati huo huo Tume inatoa fursa kwa Vyama vya Siasa kuweka Wakala mmoja  katika kila kituo cha Kuandikishia Wapiga Kura kwa lengo la kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika pamoja na changamoto zitakazojitokeza ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kabla ya zoezi rasmi la Uandikishaji.

Tume imevitaka Vyama vyenye nia ya kuweka Mawakala katika uandikishaji huu wa Majaribio kuwasilisha orodha ya majina ya Mawakala na vituo walivyopangiwa kwa Maafisa Waandikishaji wa Halmashauri za Kisarawe na Manispaa ya Morogoro.

Kadhalika Vyama vimetakiwa kuwasilisha nakala mbili za barua za utambulisho zikiwa na picha mbili na nakala mojawapo kati ya Kitambulisho cha Taifa au Kadi ya Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria au Leseni ya Udereva na kwamba kila Chama kitagharamia Wakala wake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo wakati wa uandikishaji huo wa majaribio Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatumia runinga, redio, mitandao ya kijamii na magari ya matangazo kwa ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo.

Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Kaijage kupitia taarifa hiyo amewaomba wakazi wa Kata za Kibuta na Kihonda kujitokeza kwa wingi katika Uandikishaji huo wa majaribio na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hilo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia ya Taifa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoipa Tume mamlaka ya kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano pamoja na Madiwani kwa Tanzania Bara.

Tume kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja na unaofuata.  

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANDA CHA KISASA CHA UNGA WA MUHOGO NCHINI

0
0
 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua kiwanda cha kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation (CSTC) cha unga wa muhogo wenye kiwango cha juu katika kijiji cha mbalala, kata ya Nyegedi, mkoani Lindi. Wengine kutoka kulia ni Mhe. Omary Mgumba (MB), naibu waziri wizara ya kilimo, mkuu wa wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga, mwenyekiti wa kampuni ya CSTC bwana Gerald Billet, Balozi wa ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier, Mkurugenzi mtendaji wa CSTC bwana Christophe Gallean na mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye.
 Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akivuta pazi pamoja na mwenyekiti wa kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation, Gerald Billet kuashiria ufunguzi wa kiwanda cha unga wa muhogo cha CSTC katika kijiji cha mbalala mkoani Lindi.
 Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kiwasha mashine ya mihogo wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha unga wa muhogo cha kampuni ya CSTC mkoani Lindi.



 Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kipewa maelezo kuhusu taratibu za kiwanda cha unga wa muhogo baada ya kukifunguwa rasmi katika kijiji cha Mbalala, mkoani Lindi.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akiangalia mihogo inavyopita kwenye mashine wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha unga wa muhogo cha kampuni ya CSTC mkoani Lindi.


KIWANDA cha kisasa cha kuzalisha unga wa muhogo wenye kiwango cha juu cha kampuni ya ulimaji na usindikaji muhogo ya Tanzania ijulikanayo kama Cassava Starch of Tanzania Corporation – CSTC kimefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Christophe Galléan.

Kiwanda hicho ambacho ni cha aina ya kipekee katika soko la Tanzania kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 1 ya unga wa Muhogo wenye kiwango cha juu ndani ya saa  moja na kadiri ya tani 6,000 kwa mwaka.

Akifunguwa kiwanda hicho Waziri Mkuu alitoa pongezi kwa kampuni hiyo kwa kuchangia juhudi za serikali katika kuinua uchumi kupitia viwanda. Aliipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji mkubwa waliotekeleza katika mkoa wa Lindi kwa kujenga kiwanda hicho cha kisasa ambacho kitaendeleza kilimo cha muhogo na pia kutoa ajira kwa wakazi wa mkoa huo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CSTC, Christophe Galléan alisema "Tunafurahi kuanzisha rasmi kiwanda cha kwanza cha ubora wa hali ya juu na cha kisasa nchini Tanzania. Tunajivunia sana uwepo wa kiwanda hiki na taswira inayoipa kampuni yetu ya CSTC, mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla. Tunashukuru sana kwa ushirikiano wa serikali chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, na utekelezaji wako Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. "

Cassava Starch of Tanzania Corporation iilianzishwa miaka saba iliyopita ikiwa na makao yake makuu mkoani Lindi ikiwa na lengo kuu la kuuza ndani na nje ya nchi unga wa muhogo wenye ubora wa hali ya juu kabisa. Kiwanda hicho ambacho kipo kimkakati karibu na bandari ya Mtwara kitakuwa na uwezo wa kusafirisha bidha zake katika masoko muhimu duniani yakiwemo ya Afrika ya Mashariki na Kusini, Mashariki ya Kati, Marekani na Ulaya.

Mfumo wa utendaji wa CSTC ni kukuza mazao yenye ubora wa hali ya juu katika mashamba makubwa yenye ufanisi na kusimamiwa na CSTC. Vilevile kusindika mazao yote katika kiwanda kilichopo eneo la karibu, Mfumo huu wa utendaji unaofuatwa na CSTC wa kuzalisha mazao na kuwa na kiwanda cha usindikaji ni wa kipekee katika soko la unga wa muhogo la Afrika. 

CSTC ilianza kufanya kazi mwaka 2012 nchini ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 400 ambao kati yao asilimia 97 ni Watanzania. "Tunaendelea kuongeza wafanyakazi, kutoa mafunzo na kuendelea kutoa fursa kwa vijana wengi za uongozi katika ngazi zote za uendeshaji kuanzia kiwandani, mashambani na katika shughuli za utawala" alisema Mr Galléan.

Kampuni ya CSTC ina mpango wa kujenga kiwanda cha kusindika wanga kutoka kwenye muhogo katika siku za usoni na kiwanda hicho kitategemea kutoa ajira zaidi kwa Watanzania. Mipango hii itanufaisha jamii kwa ajira, miundo mbinu na huduma za kijamii ambazo zinaendelea kutolewa katika vijiji mbali mbali mkoani Lindi. Kwa kuanzia, CSTC imewekeza katika elimu kwa kujenga darasa la shule ya msingi,ujenzi wa barababara na kukarabati miundombinu ya maji katika kijiji cha Lipome.

Hapo baadaye, CSTC itaanzisha mpango wa wakulima wadogo ambao utahusisha utoaji mafunzo kwa wakulima ili wajifunze njia mpya na za kisasa za kilimo, kuanzia maandalizi sahihi ya ardhi kwa ajili ya kuweza kuzalisha mazao bora na kuongeza mavuno ya mazao yao.  Lengo la programu hii pia ni kuwawezesha wakulima wadogo kuweza kuzalisha mazao kwa gharama nafuu na hivyo kuongeza ushindani wao katika soko la muhogo.
 
"Inashurtisha katika usindikaji wa mazao kufanyika ndani ya masaa 24 baada ya mavuno. CSTC inaanzisha  mpango huo wa kutoa mafunzo ya kilimo kwasababu miundombinu katika mavuno ni muhimu sana. Tunatafuta washirika ambao tutatekeleza nao mradi huu na kuweka malengo sahihi ili kuweza kufaidisha sekta ya kilimo katika kanda hii,” alisisitiza Mkurugenzi Christophe Galléan.

Christophe Gallean pia alimalizia kwa kuishukuru serikali kwa ushirikiano wake kwa CSTC na kueleza kuwa ana shauku kubwa kuanza upanuzi wa viwanda na mashamba ya kampuni hiyo hapo baadaye.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA NBC

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 26, Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo amefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha akiwa ameongozana na Meneja mahusiano na Serikali William Kalaghe pamoja na Afisa Masoko wa NBC Bi. Neemarose Singo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi, Afisa  Masoko wa NBC Bi. Neenarose Singo pamoja na Meneja wa Mahusiano na Serikali Ndugu William Kallaghe (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Balozi wa Tanzania nchini Sudan akutana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Kombo Haji, amekutana na kufanya mazungumzo rasmi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (International University of Africa - IUA), Profesa Kamal Muhammed Ubeid, mjini Khartoum, Sudan. Katika mazungumzo baina yao, Prof. Ubeid alimhakikishia Balozi Silima kuwa, chuo hicho kitaendeleza ushirikiano na Tanzania kwa kuendelea kutoa ufadhili wa elimu ya juu kwa wanafunzi wengi zaidi wa Kitanzania kadri hali itakavyoruhusu.

Takribani wanafunzi wa Kitanzania wapatao 517 wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini Sudan ambapo 490 kati yao wanasoma katika chuo hicho kilichopo Khartoum katika fani mbalimbali zikiwemo uhandisi wa mafuta na gesi, uchumi, udaktari na dawa na maabara, sheria, lugha na fani nyinginezo. 
Balozi Silima mara baada ya mazungumzo na Profesa Ubeid. 

Mawaziri wa Afrika wakutana Morocco

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Morocco, Mhe. Nasser Bourita, baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano.

Dkt. Mnyepe amemwakilisha Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika kuhusu maamuzi ya Umoja wa Afrika (AU) kuunga mkono jitihada za usuluhishi wa mgogoro wa eneo la Sahara Magharibi kati ya Morocco na Saharawi uliofanyika jijini Marrakech, Morocco tarehe 25 Machi, 2019. 
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe akifuatilia mazungumzo na michango ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakati wa mkutano huo. 
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe wa tatu kutoka kushoto, mstari wa nyuma, akiwa katika picha ya pamoja ya Mawaziri na Wawakilishi wa Mawaziri walioshiriki mkutano huo. 

WIZI WA MITIHANI UNALIVUNJIA TAIFA HESHIMA-MAJALIWA

0
0
*Awaonya Maafisa wanajihusisha na wizi waache mara moja

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa baadhi ya Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wanaoshirikiana na waliamu kujihusisha na wizi, udanganyifu na uvujaji wa mitihani waache mara moja tabia hiyo na mwenendo huo kwa sababu unalivunjia heshima na hadhi Taifa.

“Kamati za Mitihani za Mikoa na Wilaya ziendelee kusimamia sheria, kanuni na taratibu bila ya woga, upendeleo na tusiyumbishwe na hatua za kinidhamu na kiutumishi kwa mujibu wa sheria.Hatua ziendelee kuchukuliwa dhidi ya wote wanaobainika kukiuka sheria, taratibu na miongozo inayotolewa”.

Waziri Mkuuametoa onyo hilo leo (Jumanne, Machi 26, 2019) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya(REDEOA), uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo inasema “Elimu Bora Itatufikisha Katika Uchumi wa Kati Ifikapo 2025”

AmesemaBaraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni chombo ambacho kwa muda mrefu kimejijengea sifa kubwa sana nchini na barani Afrika, ambapo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha rasilimali ili kukifanya chombo hiko kuwa imara na cha kisasa. 

Waziri Mkuu amesema hali hiyo imezifanya nchi mbalimbali kuja nchini kujifunza masuala ya upimaji na uendeshaji wa mitihani. “Nimejulilishwa pia hivi sasa hapa nchini wapo Viongozi wa Mabaraza ya mitihani kutoka nchi za Afrika Mashariki”.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema suala la tatizo la nidhamu mbaya ya wanafunzi ni jukumu la walimu wote, hivyo wanatakiwa watekeleze majukumu yao ya kufundisha, kulea, kuwaongoza na kuwaendeleza wanafunzi kimwili, kiakili na kiroho kwa uadilifu na kuzingatia sheria. 

Waziri Mkuu amesema Serikali imesikitishwa sana na matukio ya hivi karibuni ya athari ya viboko kwa wanafunzi shuleni ikiwemo kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu pamoja na tukio la kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius wa shule ya msingi Kibeta Mkoani Kagera. 

“Ninatambua si kusudio la walimu kuwadhuru wanafunzi lakini tukubaliane kuwa kuna udhaifu katika utaratibu wa utoaji na usimamizi wa adhabu ya viboko shuleni. Maafisa Elimu kawakumbusheni walimu wote nchini wazingatie mwongozo wa kutoa adhabu shuleni chini ya kifungu cha 61 cha sheria ya Elimu sura 353 pamoja na kanuni zake”.

“Adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhamu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Na adhabu hii itatolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi. Nina hakika tukisimamia utaratibu, matukio haya yaliyoanza kuonekana yatakoma”.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya hao kwa sababu wanafanya kazi kubwa ambayo imechangia kupandisha ufaulu wa kidato cha sita na cha nne nchini. Amewasisitiza waendelee kufanya kazi kwa bidii.

Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka maafisa hao wawe wanatoa taarifa sahihi kuhusu idadi ya wanafunzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.

Awali, Mwenyekiti wa REDEOA, Germana Mung’aho amesema umoja wao unatekeleza majukumu yao ya kusimamia elimu kikamilifu nchini, lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli, ambaye anasisitiza watu wafanye kazi.

Amesema umoja huo una wanachama zaidi ya 400 na ulianzishwa ili kusimamia utoaji wa elimu nchini. Katika mkutano huo wanatarajia kujadiliana changamoto mbalimbali za sera ya elimu na namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali iwapatie magari maafisa hao watakayoyatumia kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya elimu kwenye maeneo yao ya kazi, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua   Mkutano Mkuu wa Sita wa Maafisa  Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDOA) kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDOA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kufungua  Mkutano Mkuu wa Sita wa Maafisa Elimu  wa Mikoa na Halmashuri (REDOA) kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa REDOA, Germana Mung'aho. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri  (REDOA), German Mung'aho baada ya kufungua Mkutano  Mkuu wa Sita wa REDOA kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019.  Wa pili kulia ni  Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)


NEC YATANGAZA KUANZA UBORESHAJI WA MAJARIBIO

0
0
Na Margareth Chambiri

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kwa majaribio katika Kata mbili za Kibuta iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani na Kihonda katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoani Morogoro.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne Tarehe 26. 03. 2019) imesema Uandikishaji huo wa Majaribio utakaoanza Machi 29, hadi Aprili 04, 2019 utafanyika katika vituo 20 vya kuandikisha Wapiga Kura ikiwa ni vituo 10 katika kila Kata. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uandikishaji huo unalenga katika kuvifanyia majaribio vifaa na mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura ili kubaini changamoto kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo.

Imezitaja sifa za watu watakaoandikishwa katika uandikishaji huo kuwa ni raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 au atakayetimiza umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Aidha uandikishaji huo hautawahusu raia walio chini ya kiapo cha utii wa nchi nyingine, aliyebainika kuwa hana akili timamu au yuko kizuizini kama mhalifu mwenye ugonjwa wa akili au yuko kizuizini kwa ridhaa ya Rais.

Taarifa hiyo imeendelea kutaja watu ambao hawatahusika katika majaribio hayo ya uboreshaji kuwa ni mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama au anatumikia kifungo kinachozidi miezi sita pamoja na mtu aliyepoteza sifa za kuandikishwa kuwa Mpiga Kura chini ya Sheria za Uchaguzi au Sheria nyingine yoyote inayohusu makosa ya uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawajulisha wakazi wa Kata hizo zinazofanya Uandikishaji wa Majaribio na ambao walijiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 kuwa wanaweza kutumia fursa hiyo kuhakiki taarifa zao katika vituo walivyojiandikishia.

Wakati huo huo Tume inatoa fursa kwa Vyama vya Siasa kuweka Wakala mmoja katika kila kituo cha Kuandikishia Wapiga Kura kwa lengo la kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika pamoja na changamoto zitakazojitokeza ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kabla ya zoezi rasmi la Uandikishaji.

Tume imevitaka Vyama vyenye nia ya kuweka Mawakala katika uandikishaji huu wa Majaribio kuwasilisha orodha ya majina ya Mawakala na vituo walivyopangiwa kwa Maafisa Waandikishaji wa Halmashauri za Kisarawe na Manispaa ya Morogoro.

Kadhalika Vyama vimetakiwa kuwasilisha nakala mbili za barua za utambulisho zikiwa na picha mbili na nakala mojawapo kati ya Kitambulisho cha Taifa au Kadi ya Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria au Leseni ya Udereva na kwamba kila Chama kitagharamia Wakala wake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo wakati wa uandikishaji huo wa majaribio Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatumia runinga, redio, mitandao ya kijamii na magari ya matangazo kwa ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo.

Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Kaijage kupitia taarifa hiyo amewaomba wakazi wa Kata za Kibuta na Kihonda kujitokeza kwa wingi katika Uandikishaji huo wa majaribio na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hilo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia ya Taifa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoipa Tume mamlaka ya kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano pamoja na Madiwani kwa Tanzania Bara.

Tume kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja na unaofuata.

AFISA ELIMU MSINGI AWEKA MIKAKATI MIPYA KWA WALIMU KUONGEZA UFAURU

0
0

KARIM JUMA - CHALINZE

Afisa Elimu Msingi wa Halimshauri ya Wilaya ya Chalinze Bi. Zainabu Makwinya amesema kwamba kwasasa mikakati ya kupandisha elimu kwenye kila shule za msingi za halmashauri kwa kupunguza kabisa kutokuwa na watoto kupata alama ambazo aziwezi kuendelea mbele ,Kikao hiko kilifanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri majira ya saa 8:00 asubuhi huko lugoba ,Chalinze.

Bi. Makwinya amesema kwamba idara ya elimu imeweka fungu maalumu kwa mayitaji ya vifaa vya kuweza kufundisha wanafunzi na ustadi mkubwa na kuweza kuwamasisha walimu kwa kufundisha muda waziada na kupitia mapato ya ndani idara imeona kwa darasa la saba na darasa la nne kuweza kupata masomo ya jioni.

Hata hivyo alisema kwamba niko tayari hata kuweza kutoa mashara wangu kwa darasa au shule wakifauru wote kwa masomo ya sayansi na ufahuru uliokuwa mzuri,Pia mikakati hii tunahitaji nchi iwe na watalamu wengi hapo baadaye wa wasayansi na ukiangaria mabadiliko ya dunia lazima uwitaji watalamu hao.

Pia mkakati moja kuweza kuwafanya walimu kujua umuhimu wao katika shule zote ,pili kutambua changamoto zinazowabakiri kwa wakati ,kupambana na wizara ya elimu kuakikisha upungufu au umalizaji wa madeni sugu kwa walimu wote na kuwaweka walimu na mazingira rafiki kwa maana ya mahitaji wa binadamu.

Bi. Makwinya amesema kwamba atawashauri baraza la madiwani kwa kila kata kufanya uchunguzi kwa walimu na wanafunzi maana wao wapo karibu na izo shule kuweza kutoa taarifa mapema na kuweza kuchukua mahamuzi sahihi.

Bi. Makwinya amesema kilio changu kuona wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu chache chache na sitakubali kusikia au kuambiwa kwamba mwanafunzi furani ameacha shule au mzazi/ mlezi ameshindwa kupeleka shule uyo nitang’ang’aniana naye kama pete na kidole.

MADAWATI YA JINSIA YA JESHI LA POLISI 450 YAANZISHWA KOTE NCHINI

0
0
Serikali inaendelea na utaratibu wa kuanzisha vituo vya mkono kwa mkono kote Nchini kama hatua muhimu ya kuzuia na kupunguza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto na tayari baadhi ya vituo hivyo vimeanza kufanya kazi katika hospitali za Mwananyamala, Ilala pamoja na Tumbi.

Akiongea Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema vituo hivyo kimsingi vinalenga kupunguza mzunguko na mlolongo wa huduma kwa wahanga wa ukatili kwani huduma zote ikiwemo ya matibabu, polisi na unasihi zitapatikana kwa wakati na kwa haraka.

Dkt. Ndugulile ameimbia Kamati hiyo ya Bunge kuwa juhudi nyingine zinazofanywa na Serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ni kuanzishwa kwa takribani Madawati ya Polisi ya Jinsia 450 kote Nchini ambayo yamekuwa msaada mkubwa kwa wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili na kulitaka Jeshi la polisi kuongeza madawati hayo kwa kila kituo cha polisi kote Nchini.

Aidha, Naibu Waziri Ndugulile ameongeza kuwa Serikali inajipanga kuanzisha Dawati la Jinsia katika Shule zote Nchini ili kutoa nafasi kwa watoto ambao wanafanyiwa ukatili na hawana mahali pakutolea taarifa kutumia Dawati la Jinsia la Shule kutoa taarifa za vitendo vya ukatili.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndugulile ameimbia Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuwa Serikali inafuatilia vyema huduma zinazotolewa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuhakikisha Mashirika hayo yanatekeleza shughuli zao kwa kuzingatia Sheria. Ameongeza kuwa Wizara inakamilisha maboresho ya kanzidata ili kuongeza ufanisi katika uratibu wa shughuli za mashirika kwa kutambua kazi zinazofanyika na mchngo unaotolewa katika sekta mbalimbali

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu ameimbia kamati hiyo kuwa Wizara inajukumu la kupitia mitaala ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii na imekuwa ikifanya hivyo kila baada ya miaka mitano na limekuwa likifanyika kufuatia matokeo ya utafiti ili kubaini mahitaji ya soko la ajira.

Dkt. Jingu alisema hayo alipokuwa akijibu swali la Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bw. Peter Selukamba aliyetaka kujua kama mitaala ya vyuo hivyo ufanyiwa mapitio ili wataalamu wanaotolewa na vyuo hivyo waendane na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imekutana leo mjini Dodoma na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuwasilisha rasimu ya Makadilio ya Bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2019/2020.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo wakati Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akiwasilisho hoja Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo wakati Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akiwasilisho hoja Mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.

Tigo yazindua tawi jipya la huduma kwa wateja Iringa mjini

0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduziwa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akikata utepe kuashiri uzinduzi rasmi wa duka hilo litakalokuwa na uweza wa kuwahudumia wateja wengi zaidi. 
 1Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akiwatubia wananchi waliofika katika uzinduzi wa tawi hilo linaloweza kuwahudumia wateja wengi Zaidi kwa wakati mmoja
 Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduziwa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akiwa na Abbas Abrahmani ambaye ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini pamoja na Laverty Khana ambaye ni Meneja Huduma kwa Wateja kanda ya Kusini  muda mfupi kabla ya uzinduzi rasmi wa duka hilo 
 : Mgeni rasmi kwenye tukio la uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililipo mtaa wa Miomboni mjini Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela (wa kwanza kulia) akipata maelekezo kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo namna wanavyohudia wateja.

Waandishi wa habari wakichukua matukio mbali mbali ikiwamo hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela kwenye uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa.



Kampuni ya Tigo leo imezindua duka jipya la huduma kwa wateja lililopo Iringa mjini ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wake wa eneo la Iringa mjini na maeneo ya jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo Mkurungezi wa kanda ya Kusini wa Tigo, Henry Kinabo, amesema tawi hilo jipya lililopo mtaa wa Miyomboni, ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuwafikishia wateja wake huduma zake karibu zaidi.

Kinabo alisema duka hilo litahudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku kwa kuwapa huduma mbalimbali za Tigo ikiwemo huduma ya kuunganishwa na intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma za simu janja.

“Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu imepeleka huduma zetu kuwa karibu zaidi na wao. Pia linapatikana sehemu nzuri inayofikika kirahisi kiasi kwamba litavutia wateja wengi kutoka maeneo jirani. Tumebadilisha pia muonekano wa duka letu kuwa mzuri zaidi, na kuongeza pia nafasi ili kuweza kuwahudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema.

Aliongeza, “Kupitia duka letu hili lililoboreshwa, wateja watapata pia promosheni zetu mbali mbali kama; 4G+, App ya Tigo Pesa, promosheni ya CASH IN kwa mawakala, pamoja na simu mpya za S10 na S10+.” 

Duka hili limetenga pia sehemu maalum ya uuzaji wa bidhaa mbalimbali kama simu janja ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribu kabla ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi kabla ya kununua, hivyo huchagua na kununua aina ya simu inayokidhi mahitaji yake.”

RC GAMBO ATOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MWANDISHI WA DW

0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Charles Ngereza mwandishi wa idhaa ya kiswahili ya Sauti ya ujerumani aliyefariki siku ya jumamosi tarehe 23 na anatarajiwa kuzikwa kesho 27 eneo la baraa jijini Arusha picha na Pamela mollel

UKIWA UNAONGEA KILE UNACHOANDIKA NA UNA MWANDIKO MBAYA SOMA HAPA

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BAADHI ya watu wana matatizo au hali za chini katika kuelewa lugha hasa katika maandishi na kuongea, wataalamu wengi wamefanya tafiti nyingi ya kutambua matatizo hayo likiwemo la Disigrafia.

Imeelezwa kuwa disgrafia ni tatizo linalompata mtu ambapo hushindwa kuandika na kuelewa maandishi na michoro, mtu mwenye tatizo  hili hushindwa kuumba herufi na anakuwa na mwandiko mbaya.  Aidha mtu mwenye disigrafia hushindwa kuwasilisha mantiki katika karatasi.

Watu wengi huwa na matatizo katika kuandika ila disigrafia ni zaidi ya hapo kwani tatizo hilo hugusa mifumo ya fahamu na hujitokeza wakati mtoto anapoanza kujifunza kuandika, mfano: katika daftari lenye mistari anaweza kuandika sentensi moja katika mistari minne huku akichanganya herufi kubwa na ndogo na zenye ukubwa tofauti tofauti.

Tatizo hili humfanya mtu kushindwa kubadili sauti za lugha kuwa herufi za maandishi, kushindwa kutambua herufi au kuandika kinyume mfano: d kuwa b au z kuwa 3.

Dalili za mtu mwenye tatizo hili ni pamoja na; kugeuza herufi, maandishi yasiyolingana ukubwa, kuchanganya herufi na namba na kuchanganya herufi kubwa na ndogo.

Pia mwenye tatizo hili anaweza kuandika maneno yasiyokamili mfano; Mama anapk,  kushika vibaya viandikio kama kalamu na peni. Aidha mtu mwenye tatizo hili huandika mwili ukiwa unacheza, kuzungumza kila anachoandika na kupata ugumu wa kuunganisha mawazo.

Na inasemekana kuwa watu wenye tatizo hili huzungumza vizuri kuliko kuandika.

KTO YATOA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAKUFUNZI WA VYUO KUMI VYA MAENDELEO YA WANANCHI NCHINI

0
0
Na Francis Daudi, Blogu ya Jamii
WARSHA wa Mafunzo ya Siku Mbili katika kuwajengea Uwezo wakufunzi kutoka Vyuo kumi vya Maendeleo ya Wananchi vilivyoingizwa kwenye mradi wa Elimu Haina Mwisho unaohusisha vyuo  20 vya Maendeleo ya Wananchi kati ya 54 vilivyopo nchini. 

Mafunzo hayo yaliandaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) yamehitimishwa Leo huku wawezeshwaji wakishukuru kwa kupata fursa hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo,  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa ameeleza kuwa hiyo ni moja ya jitihada ya kuunga mkono juhudi za Serikali hasa katika kuwajengea Maarifa Wakufunzi na kwamba miradi ya namna hiyo ni sehemu ya mipango ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi kwa kuwa Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vina nafasi kubwa katika kulipeleka taifa katika uchumi wa viwanda.

Aidha, Ameongeza kwamba, Mfumo usio rasmi utawanufaisha Wanawake Vijana waliokatizwa masomo kutokana na sababu mbalimbali kama vile Kukimbia Ndoa za Utotoni, Ukeketaji na Ujauzito. Na hivyo basi mradi huo una malengo ya kuchangia katika jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwenye kuviimarisha Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi ili viwe na  tija kubwa kwa Wanawake vijana wengi wenye kutokea kwenye familia za  watanzania wenye vipato duni.  

Baadhi ya miradi ambayo taasisi ya KTO inashirikiana na wizara ni pamoja na ‘Elimu Haina Mwisho’ ambayo ni programu ya kuwapatia maarifa na ujuzi wanawake vijana waliokosa fursa  hiyo  kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni, ukeketaji na kupata ujauzito wakiwa shuleni. Vilevile, KTO inaendesha programu ya ‘ Mpira Fursa’ inayohusika na kuendeleza mpira kwa wanawake na hapa nchini mafunzo hutolewa katika Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi na Wanawake vijana wanaopata programu ya Mpira Fursa ambao hawajifunzi kucheza mpira pekee, bali pia kupata mafunzo na ujuzi mwingine.

Kwa muda mrefu KTO imekuwa kiungo muhimu katika Vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi nchini na Wizara pamoja na wahisani wa Kimaendeleo kama SIDA,( Sweden) HDIF ( Uingereza) na Mastercard Foundation ( Canada) na wengineo wamekuwa bega kwa bega na KTO pamoja na kushiriki katika kuboresha utolewaji wa Mafunzo ndani ya Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi.


Akifunga Mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KTO,  Aidan Mchawa, Ameishukuru Serikali kwa kutoa nafasi ya kufanyika kwa Mafunzo hayo, amewasihi wakufunzi toka vyuo kumi vilivyoshiriki kutumia maarifa  waliyoyapata, ili yawe sehemu muhimu katika kuandaa Wanawake Vijana ambao kwa miaka ijayo ndio hasa watakuwa nguvu kazi ya Taifa.

Pia amelishukuru Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kuwezesha Warsha Mafunzo hii ya siku mbili.

Mafunzo hayo ya siku mbili, yalitanguliwa na Mafunzo ya siku kumi yaliohusisha vyuo 20, wakati huo taasisi ilitoa vifaa ambavyo vitawasaidia wawezeshwaji katika kutekeleza majukumu yao. Vifaa  hivyo ni pamoja na kompyuta 10 zenye thamani ya shilingi milioni 7, External hard driver 10 ambazo zina programu za kufundishia watoto kama vile Ubongo kids zenye thamani ya shilingi milioni 2.8, projector 20 zenye thamani ya shilingi milioni 18  pamoja na vitabu vya elimu ya awali vyenye thamni ya shilingi milioni 5.2.

Mafunzo hayo pia  yaliambatana pia na utolewaji wa Komputa  30 na Projekta 10 kwa Vyuo 10(Komputa 3 na Projekta 1 kila Chuo) vilivyotoa ushiriki wao katika Warsha hii ili vikasaidie utekelezaji wa mradi kwa Ufanisi.
Baadhi ya washiriki wa warsha huo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kupata mafunzo hayo, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya KTO Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa utolewaji wa mafunzo hayo ambapo amewataka wawezeshwaji kutumia maarifa waliyoyapata katika kuleta matokeo chanja katika jamii, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi KTO Aidan Mchawa akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ambapo ameishukuru serikali kwa ushirikiano na kuhaidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuendeleza taifa.

MAJIBU YA ZITTO KABWE KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

0
0

*Ni baada ya Ofisi ya Msajili kutoa barua ya kusudio la kukifuta Chama hicho
*ACT Wazalendo wajitetea kwa kukiri kupeleka hesabu kwa CAG,wagusia udini

Na Said Mwishehe,Globu ya jmii

CHAMA cha ACT Wazalendo kupitia Kiongozi wake Zitto Kabwe kimefafanua na kuweka wazi kuhusu tishio la Msajili wa Vyama vya Siasa kutaka kukifuta chama hicho ambapo pamoja na mambo mengine wamejibu hoja moja baada ya nyingine.

Kauli ya Zitto inakuja baada ya jana Machi 25,2019,Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwaandikia barua ACT-Wazalendo ambayo kwa sehemu kubwa ilijikita katika mambo matatu na kisha kutoa kusudio la kutaka kukifuta.

Kwa mujibu wa barua hiyo ya Msajili wa Vyama vya Siasa jambo la kwanza ni hoja zinazohusu ukaguzi wa hesabu ,pili ni vitendo vya kuchomwa hadharani kwa bendera na kadi za chama cha CUF na tatu ni matumizi ya neno Takbiri kama yalivyoonekana katika baadhi ya video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo Machi 26,2019 akiwa katika Makao Makuu ya ACT-Wazalendo Zitto amesema kuhusu ukaguzi ni kwamba barua ya Msajili wa vyama vya siasa inadai ACT imekiuka sheria ya vyama vya siasa kwa kutopeleka kwake hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 kama sheria inavyotoka.

Amesema tuhama hizo hazina ukweli wowote kwasababu wajibu wa Chama cha siasa ni kuwasilisha hesabu zake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) na kwamba hesabu za mwaka 2013/2014 ziliwasilishwa kwa CAG na kufafanua Chama hicho kilianzishwa kwa kupata usajili wa kudumu Mei 5 ,2014 miezi miwil kabla ya mwaka wa fedha wa Juni 30,2014. 

"Kwa kutumia kanuni za kimataifa za kihesabu na kwa ushauri wa CAG ,Chama chetu kilielekezwa kinaweza kuunganisha hesabu za mwaka 2013/2014 na 2014/2015 katika ripoti moja.Na hili ni jambo la kawaida kabisa katika kanuni za uhasibu kwani inaruhusu kuunganishwa hadi miezi 18 .ACT ilikuwa na miezi 14 tu.

" Kabla ya kuchukua uamuzi huu wa kuunganishwa hesabu,Chama chetu kilimwandikia Msajili wa vyama vya siasa kwa barua mbili zenye kumbukumbu namba AC/HQ/ MSJ/ 2015/006 na AC/ HQ/ MSJ/ 2015/008 za tarehe 22 na 29 Januari 2015.Naye alijibu na kuridhia hesabu za miezi miwili za mwaka 2013/2014 kuunganishwa kwenye mwaka wa fedha 2014/2015,"amesema.

Zitto ameongeza taarifa zote hizo ziko wazi kwa CAG na kama Msajili wa vyama vya siasa angekuwa na nia njema angeweza tu kuuliza na angepewa taarifa sahihi.Kazi ya Chama cha siasa ni kuwasilisha hesabu zake kwa CAG na sio kwa kukagua hesabu zake chenyewe.

"Tulitimiza wajibu wetu huo, CAG naye alitimiza wajibu wake kwa kutukagua ,hivyo basi Chama chetu kwa sasa hakuna mwaka ambao hakijawasilisha hesabu zake.Kwa mwaka 2015/2016 na 2016/2017 chama kina hati safi na mezani kwake.

" Mambo haya ya ukaguzi yako nje ya wigo wa uelewa wa Msajili na ndio maana sheria za nchi zinampa CAG wajibu wa kufanya mambo haya na ukaguzi wa msajili kuwa mlezi wa vyama vya siasa.Msajili afanye mambo anayoyajua,asiyoyajua aachane nayo,"amesema Zitto.

Kuhusu kuchoma bendera na kadi, Zitto amesema barua yenyewe ya Msajili iliyowafikia inasema kuwa hana uhakika kama kweli wahusika ni wanachama wa ACT Wazalendo wakichoma bendera na kadi za chama cha CUF.

"Katika hili Msajili mwenyewe anaonesha hana uhakika kama kweli wahusika ni wanachama wa ACT.Inashangaza anafika uamuzi wa kuandika barua ya kutishia kutufuta kama chama cha siasa kwa tuhuma ambazo hata yeye mwenywe hana uhakika nazo," amefafanua.

Kuhusu Takbir ,Zitto amesema barua ya Msajili wa vyama vya siasa inaeleza chama chao kimevunja sheria ya vyama vya kwasababu wanaodaiwa kuwa wanachama wao wametumia maneno ya takbiri kwenye shughuli za kichama na kwamba maneno hayo ni udini.

"Jambo hili limetushangaza na kutuudhi kwa wakati mmoja.ACT ni chama cha watu wa dini zote na hata wale wasio a dini.Katiba yetu ya Chama tumeonesha wazi hatufungamani na dini yoyote na ndio sababu tumeruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa.Hata hivyo tunafahamu watanzania wana dini zao na wana maneno yao ambayo ni ya kawaida kutumia na hayana uduni wowote.

"ACT haitaki kuamini kusema Takbir kwa muumini wa dini ya Kiislam au hata kwa Mkristo ni udini .Jambo hili tunaachia wanazuoni na waumini wa dini ya Kiislamu walieleze vizuri na kumfahamisha Msajili kwamba hakuna udini wowote katika neno hilo la kuitiana hamasa kwa wahusika,"amesema Zitto.

Amefafanua barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa haina nia njema kwa ACT Wazalendo na wapenda demokrasia wote hapa nchini huku akiitumia nafasi hiyo kuomba Msajili kuangalia na kutafakari kwa upana kuhusu hiyo barua yake na ikiwezekana aifute mara moja kwani inaonesha namna ambavyo nia yake sio nzuri kwa Chama hicho. Hata hivyo amesema barua ya Msajili haiwatishi na wala hawatatishika na kusisitiza kuwa ACT inafanya shughuli zake za kisiasa kwa misingi ya kuheshimu na kuifuata Katiba ya nchini na kwamba wanachama wao kokote waliko wahakikishe wanaheshimu Katiba.
 Waandishi wa habari wakifautilia mkutano wa CHAMA cha ACT Wazalendo kupitia Kiongozi wake Zitto Kabwe alipokuwa akifanunua mambo mbalimbali kuhusiana na tishio la Msajili wa Vyama vya Siasa kutaka kukifuta chama hicho ambapo pamoja na mambo mengine wamejibu hoja moja baada ya nyingine.

 

Mama Napono Sokione mtembelea Mama Maria Nyerere

0
0
Mama Maria Nyerere akiwa na mgeni wake, mjane wa Waziri Mkuu wa zamani, Mama Mama Napono Sokoine aliyemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam, jana. Wengine katika picha (kutoka kushoto) ni msaidizi wa Mama Maria, Wambura; Mbunge wa Viti Maalumu, Namelok Sokoine, Elysia Sokoine na Ninai Sokoine. Mbuzi anayeonekana ni zawadi ya Mama Sokione aliyopelekea Mama Maria. 

NHIF TANGA YAJIPANGA KUTOA ELIMU YA KUTOSHA KWA WANANCHI KUHUSU BIMA YA AFYA ILIYOBORESHWA

0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga NHIF umejipanga kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na Bima ya afya iliyoboreshwa .

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Mfuko huo  Mkoani Tanga, Ally Mwakababu wakati akizungumza na MTANDAO huu kuhusu walivyojipanga kuhakikisha wanaongeza wananchi na kuboresha huduma zao.

Alisema kuwa iwapo wananchi wataweza kupata uwelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa kuwa na kinga ya matibabu kabla ya kuugua wataweza kuwakomboa wananchi wengi.

“Hakuna mtu au kiongozi ambaye atakuwa tayari kuongoza wananchi ambao ni goigoi wa maradhi hivyo Bima ya afya tumejipanga kuhakikisha kwanza tunaongeza idadi ya wanachama lakini kupitia wao  tutaweza kuboresha huduma katika vituo vya afya”alisema Mwakababu.

Hata hivyo Mwakababu alisema kuwa licha ya mkoa wa Tanga kuwa wapili kwa uandikishaji wa bima ya afya ya jamii CHF  lakini bado eneo hilo hawakuweza kufanya vizuri zaidi hivyo kwa mwaka huu wamejikita katika kuongeza uhamasishaji zaidi.

Alisema kuwa wamejipanga kufanya hamasa kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji kwa kushirikisha viongozi wa kiserikali na kisiasa kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi ndani ya Tanga anaona umuhimu wa kuwa na kadi ya Bima.

Vile vile akiongelea kadi ya Bima ya Toto afya Mwakababu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2017/18 waliweka lengo la kuandikisha watoto waliochini ya umri wa miaka 18 ,3000 badala yake waliandikisha 913.

Huku kwa walioko katika ngazi ya sekondari na vyuo ambao wanatumia huduma ya Toto afya kadi waliweza kuandikisha 1435 kati ya malengo waliyojiwekea ya kuandikisha wanachama 3000.

“Tatizo kubwa ni mwamko mdogo wa wananchi kuona umuhimu wa kuwa na bima ya afya  wao wanasubiri mpaka ugonjwa uwe mkubwa  na kushindwa gharama za matibabu lakini kumbe kama wangeweza kujiunga mapema wasiweza kupata huduma bora”alisema Meneja huyo.

KAMATI YA USHINDI YATOA SHUKRANI KWA WATANZANIA WOTE...MAKONDA AWEKA WAZI

0
0



*Asema ushindi wa Taifa Stars ni wa Watanzania wote

*Asisitiza sasa timu yoyote itakayokuja nchini itapigwa tu



Na Said Mwishehe,Globu ya jamii



KAMATI ya Saidia Taifa Stars ishinde yenye wajumbe 14 wakiongozwa na Mwenyekiti wao Paul Makonda imetoa shukrani kwa Watanzania wote kwa kufanikisha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kushinda mechi yake dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda.




Taifa Stars waliifunga Uganda mabao 3-0 na hivyo kufanikiwa kuipeleka Tanzania nchini Misri kwenye michuano ya AFCON mwaka 2019.Ushidni wa Taifa Stars umeifanya nchi yetu kuandika historia ya aina yake baada ya miaka 39.



Akizungumza leo Machi 26,2019 jijini Dar es Salaam Makonda amesema  Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde inatoa shukrani kwa makundi mbalimbali kwa kufanikisha ushindi huo ambao ni Watanzania wote.



"Nitoe shukrani kwa  wapenzi ,wakereketwa na wadau wote wa michezo. Walihakikisha Taifa Stars inashinda kwa kushiriki kwenye dua na sala.Kamati yetu ilikuwa na kazi kubwa mbili , kwanza ni kuhakikisha Taifa Stars inashinda na mbili kufuatilia mchezo mwingine wa Lethoto na Cape Verde.



"Baada ya Rais wa TFF kuteua kamati hii tulihakikisha  hatukuangushi na tunafahamu tulipoteza mechi yetu dhidi ya Lethoto ambako kwa sehemu fulani kulikatisha tamaa.Tuliwepa kazi ngumu,"amesema Makonda.



Amefafanua ili kuhakikisha kamati inatimiza majukumu yake ilichukua jukumu la kuunda makundi mbalimbali yakiwamo ya watu mashuhuri, mastaa katika tasnia ya sanaa nchini, wanamichezo wa zamani, wenye mahoteli, wenye baa,vyombo vya habari na wenye vyombo vya usafiri.



Amefafanua katika nchi yetu klabu za Simba na Yanga ndivyo vyenye mashabiki wengi wa soka, hivyo aliona haja ya kuwachukua Haji Manara na Jerry Muro ambao nao aliwaita kwenye kamati hiyo na hakika wametoa mchango mkubwa katika kusaidia kuunganisha mashabiki wa vilabu hivyo.



Makonda ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema pamoja na kazi hiyo Kamati yao ilihakikisha inairudisha timu ya Taifa Stars kwa Watanzania na kazi hiyo imefanikiwa kwani hapo awali ilionekana kama vile haina mwenyewe na baada ya hapo ndipo likaja wazo la kutafuta watu mashuhuri.



"Kazi ya pili ilikuwa kuzungumza na vyombo vya habari kusaidia kuhamasisha. Jambo la tatu ni kuhamasisha kwenye maeneo yenye watu wengi kama baa, hoteli na vyombo vya usafiri ili nao wato ruhusa ya kujadili kwa mchezo wa Uganda na Tanzania kama sehemu ya kuhamasisha.Kazi ambayo imefanikiwa na wote tumeona,"amesema Makonda.



Amefafanua ushiriki wa makundi hayo ya kufanya kazi ya kuhamasisha, Uwanja wa Taifa ulizidiwa kwa idadi ya watu ambapo ametumia nafasi hiyo kuomba radhi kwa wote waliokuwa na tiketi zao lakini hawakuingia uwanjani na kwamba wamejifunza , hivyo watajipanga isitokee tena.



"Kwa namna ambavyo walijitokeza kwa wingi uwanjani maana yake Watanzania wanapenda mpira na michezo mingine yote. Tutaendelea kushauri ikiwemo ya tiketi kukatwa mapema na pale ambapo uwanja utakuwa umejaa basi watu wambiwe mapema,"amesema Makonda.



Pia amempongeza Kocha wa Taifa Stars kwa kupanga kikosi kizuri cha ushindi na kufafanua zawadi ya viwanja ambayo imetolewa na Rais Dk.John Magufuli wataweka uratatibu utakaosaidia hata wale wachezaji ambao walikuwemo kwenye ile michezo ya awali nao wanapewa.



"Kwa namna ambavyo Watanzania wamehamasisha na timu yetu ya Taifa, nina uhakika timu yoyote itakayokuja Uwanja wa Mkapa lazima itapigwa tu.Mashabiki ni mchezaji wa 12 na sasa tunao , hatuna wasiwasi na timu yetu,"amesema Makonda.


KAMATI ya Saidia Taifa Stars ishinde yenye wajumbe 14 wakiongozwa na Mwenyekiti wao Paul Makonda ikitoa shukrani kwa Watanzania wote kwa kufanikisha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kushinda mechi yake dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda.


MRADI MKUBWA WA MAJI KUMALIZA KERO YA MAJI JIJINI ARUSHA

0
0
Mkurugenzi mtendaji wa AUWSA Mhandisi Ruth Koya akitoa ufafanuzi kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji walipotembelea moja ya Kisima cha majimoto ambapo mradi mkubwa wa maji unatekelezwa kilichopo Rundugai wilaya ya Hai
 Mkurugenzi mtendaji AUWASA Mhandisi Ruth Koya (mwenye shati light blue) akiwa sambamba na Kamati ya Kudumu ya Bunge walipotembelea mradi huo uliopo Murieti/Terati Jijini Arusha.
 Meneja wa Mradi wa Kutibu majitaka uliopo Muriet /Terati ndugu Niny Yunfeng kutoka kampuni ya China Civil Enginearing Construction akizungumza na waandishi wa habari katika eneo ambalo mradi upo na kuelezea naendeleo ya mradi kwa ujumla.
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari kubusiana na mradi mkubwa wa. Maji unaotekelezwa Jijini Arusha sambamba na kuishukuru kamati ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji
Mshauri na muelekezi wa mradi wa Maji moto uliopo hai mkoani Kilimajaro,jiologisti Profesa Mkulo akitoa ufafanuzi kwa Kamatibya bunge namna mradi huo unavyotekelezwa. 
 Injinia Jailos chilewa ambae ni Mshauri muelekezi wa mradi  ujenzi wa tank la maji Ngaramtoni mkoani Arusha akiwaonyesha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji walipotembelea kukagua mradi huo umefikia kiwago gani.
 Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akiwa pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakionyeshwa mchoro wa ujenzi wa Matenki yakubw ya maji yanayojengwa Ngaramtoni.
 Baadhi ya wakandarasi wa Miradi hiyo mkubwa wa majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha na baadhibya maeneo ya wilaya ya Arumeru unaotekelezwa na AUWSA, Seed farm, SewerNetwork outside CBD, WSP.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge akisoma ramani kwa makini ya mradi wa kutibu majitaka uliopo Murieti/Terati.

Na. Vero Ignatus, Arusha



Serikali imefanikiwa kupata mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Afrika (AfDB) kwa jumla ya shilingi Bilioni 514 (233.9mil.USD) kwaajili ya kuboresha huduma ya majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru



Mhandisi Ruth Koya ni  Mkurugenzi mtendaji AUWSA anasema Mradi huo mkubwa wa maji utaondoa kero ya upungufu wa maji kwani uboreshaji wa huduma utaongezeka kutoka wastani wa lita 40,000,000 hadi lita

200,000,000,kuongezeka kwa wakazi wanaopata maji toka wastani wawatu 325,000 hadi kufikia 600,000 wakiwemo wastani wa watu 250,000 wanaoingia na kutoka Jijini kila siku


''Hii Itapunguza maji yanayopotea kutoka wastani wa 40%hadi25% kuongeza mtandao wa bomba za majisafi kutoka 44%hadi 100%



Mhandisi Koya anasema lengo la mradi ni uboreshaji wa huduma ya usafi wa mazingira na miundombinu yake kuongeza mtandao wa ukusanyaji wa maji taka kutoka 7.66% hadi 30%,kujenga mabwawa ya majitaka, kupunguza kero ya uzibaji wa mabomba, kutoa elimu ya usafi wa mazingira. 



Utafiti wa vyanzo vya maji uliofanywa na kampuni ya Engis kutoka Ufaransa umebaini kwamba chanzo kikuu cha maji kwasasa katika jiji la Arusha ni visima virefu, ambapo umebainisha maeneo ya uchimbaji eneo la Magereza-seed-Farm, Tengeru-Makumira, Usariver, Valeska - Mbuguni  na Majimoto iliyopo Hai mkoani Kilimanjaro. 



Mkuu wa wilaya ya Arusha  Gabriel Daqqaro amesema wanamshukuru mhe. Magufuli 2018 alivyokuja kuzindua mradi huo wa maji, amesema yapo maeneo mengi ambayo yana shida ya maji ila serikali yake imeona Arusha ndiyo jiji linalohitaji mradi mkubwa    kufuatia na ule wa Tabora



Amesema kupitia mradi huu wananchi wa Arusha watakwenda kupata maji kwa 100% tofauti na 44%ya sasa kwamba wanapata milioni 60 wa siku  kwa kipindi cha kiangazi lakini lita zinazo hitajika kwa siku ni lita milioni 94 mradi huu unatuhakikishia kwamba upatikanaji wa maji kwa jumla ya lita milioni 200 kwa siku hivyo tutakuwana akiba ya maji ya kutosha kwa kipindi kirefu.



Tunaihakikishia serikali sisi kama wilaya tutaendekea kuisimamia hii miradi tutailinda, na kuitunza na kuhakikisha miradi hii haihujumiwi na mtu yeyoye na kwenye  vyanzo vyetu vya maji vingine vipo nje ya wilaya vingine ndani tutahakikisha tunashirikiana na serikali za kule kuhakikisha vipo salama.



Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo, mifugo na maji Mahamood Mgimwa Mb (Mufindi Kaskazini) amesema wanaiomba serikali kutupia macho eneo  la TRA kutokuachia mabaomba ambayo yapo kwao kwa takribani miezi 2 yanayochelewesha watu kupatiwa maji



'' Mradi mkubwa wa maji ameuzindua Rais  yeye mwenyewe unacheleweshwa bila kuwa na sababu za msingi huo ucheleweahaji usingelikuwepo leo watu wangelikuwa wanapatiwa maji baadhi ya maeneo''alisema



Ameyataka makampuni yaliyopewa tenda kwenye hiyo miradi yafanye  kazi kwa ufanisi na kwa haraka amewataka kutokuwaingiza kwenye matatizo kwani mwaka 2021 pesa zinatakiwa zianzwe kulipwa zilipokopwa



Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa wizara ya maji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema utekelezaji wa mradi huo wa maji unatekelezwa na wakandarasi 10 na wote wanahitaji msamaha wa kodi ambapo maombi yote yaliwasilishwa serikalini na yamefanyiwa kazi na hadi sasa misamaha 4 imeshapatikana kulingana na jinsi wanavyowasilisha na mingine inatendewa kazi na wakati wowote misamaha hiyo itapatikana



'' Vitu amabavyo vinachanganya katika upatikanaji wa misamaha ya kodi ni ukamilifu wa maombi yeyewe ambayo hayajakidhi vigezo vyenyewe kwasababu maombi mengine tamekuwa yakija yanarudi kwasababu hajajakidhi vigezo vyote, lakini mwombaji yeye kwasababu ameshawasilisha anaona kwamba amechelewa haesabu ule muda kwamba alirudishiwa ili afanya masahihisho.



Amesema serikali imeshaweka utaratibu mzuri wa kushughulikia misamaha kwa miradi yote mikubwa ambayo imeshaainishwa kwamba inahitaji kupata msamaha na kama Wizara wanaendekea kufuatilia kwa karibu maombi yanayowasilishwa



Amesema ameneo yote ambayo maji yatapitia wataachiwa maji kama sera ya maji inavyosema lakini pia bomba linapopita kama sera ya wizara isemavyo kilometa 12 kushoto na kulia watu wale lazima wapate maji



Mwenyekiti wa Bodi ya majisafi na Usafi wa mazingira Jijini Arusha Mhandisi Dkt. Richard Masika amesema kuwa mradi huo utaongeza uzalishaji wa maji kutoka milioni 93 hadi lita milioni 200 itaondoa kabisa tatizo la maji katika jiji la Arusha pamoja na baadhi ya maeneo ya Arumeru



Amewaomba wananchi  waendelee kupata ushirikiano katika maeneo ambayo kazi zinaendelea wawe na uvumilivu kwasababu kila kazi inataratibu zake



Nae Meya wa Jiji la. ARUSHA Kalisti Lazaro ameishukuru Serikali kwa kuona Jiji la Arusha wanastahili kupata mradi huo mkubwa wa maji amesema kwao  ni heshima kubwa kwao



Amesema kwajinsi hali inavyoelekea historia ya tatizo la  maji katika jiji la Arusha itakuwa imesahaulika.



Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images