Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MWALIMU BORA DUNIANI ATOKA NCHINI KENYA

$
0
0
*Hutoa asilimia 80 ya mshahara wake kusaidia wanafunzi, Rais Kenyatta ampongeza

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MWALIMU  wa hesabu na fizikia  Peter Makaya Tabichi kutoka eneo la Nakuru  nchini Kenya ameshinda tuzo ya mwalimu bora duniani kwa 2019 na kuibuka na kitita cha dola milioni moja.

Tabichi anafundisha katika shule ya sekondari mchanganyiko ya Keriko Pwani vijijini.

Imeelezwa kuwa Tabichi (36)hutoa asilimia 80 ya mshahara wake wa mwezi kwa watu wasiojiweza na  tuzo hiyo imetolewa katika sherehe iliyofanyika Jumamosi huko  Dubai.

Aidha mwalimu huyo  husaidia wanafunzi wake wasiojiweza  kununua sare za shule na vitabu, akizungumza na vyombo vya habari Tabichi amesema;
"Kila siku Afrika tunafungua ukurasa mpya wa maisha. Tuzo hii hainitambui mimi bali inawatambua vijana wa bara hili. Nipo hapa kwa sababu ya kile ambacho wanafunzi wangu wamefanikiwa katika maisha yao,"ameeleza.

Aidha amesema kuwa tuzo hiyo inawapa wanafunzi hao na  imeutangazia  ulimwengu kuwa wanaweza kufanya kitu chochote katika sekta hiyo.

Tabichi aliwabwaga  walimu wengine tisa kutoka sehemu mbalimbali  funiani waliofanikiwa kufika fainali katika kuwania tuzo hiyo ya mwalimu bora huku idadi wa washiriki ikiwa ni 10,000.

Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyata amempongeza mwalimu na kusema kuwa historia yake ni kubwa Afrika na jambo hilo ni kubwa kwao kama taifa na kwake pia.

Mikataba Hoteli za Kitalii za Serikali kupitiwa

$
0
0

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amesema Serikali inapitia mikataba na makubaliano ya wawekezaji waliopewa kuendesha Hoteli za Kitalii zinazomilikiwa na Serikali kwenye maeneo ya Hifadhi. 

Kanyasu alitoa kauli baada ya kutembelea Hoteli ya Ngorongoro Wild Life Lodge iliyomo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni ziara yake iliyoanzia Hifadhi ya Serengeti, Manyara na kwingineko. 

Naibu Waziri Kanyasu mara baada ya kuzungumza na Mejinementi ya NCAA, alisema kwamba hoteli hizo zilibinafsishwa kwa malengo ikiwamo kuona zinaendeshwa kwa faida, kuajiri Watanzania na kulipa kodi. 

“Nitapita kwenye hoteli hizi moja baada ya nyingine kuangalia makubaliano ya kuziendesha ni yale yale au wamekiuka kama wamekiuka basi serikali itaangalia kwanza ushauri lakini kuvunja mkataba,” alisema Naibu Waziri Kanyasu. 

Kaimu Mhifadhi wa NCAA Needpeace Wambuya kwa upande wake alisema moja ya jukumu lao n kuhakikisha ukaguzi wa utoaji huduma zenye viwango vya kimataifa unafanywa ndani ya hoteli zilizopo NCAA.

“Kwenye eneo hili la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tuna hoteli kubwa tano ukijumlisha na nyingine za kawaida zinafikia hoteli 11,” alisema Wambuya. 

RAIS MAGUFULI AMZAWADIA PETER TINO KIWANJA NA PESA SHILINGI MILIONI 5, AFUNGUA AKAUNTI CRDB NA KUZIWEKA

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino leo amekabidhiwa shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambayo ilifuzu kuingia fainali Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON).

Mchezaji Peter Tino ndiye aliyefunga goli lililoiwezesha Tanzania kuingia fainali hizo na tangu mwaka huo wa 1980 Tanzania haikuwahi kufanikiwa tena kuingia hatua hiyo mpaka mwaka 2019 ikiwa ni miaka 39 imepita.

Peter Tino alialikwa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Machi, 2019 wakati Rais Magufuli alipokutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambao jana waliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) na kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadaye mwezi Juni 2019 huko Misri.

Pamoja na kupatiwa shilingi Milioni 5, Peter Tino pia ameunganishwa katika zawadi ya kupatiwa kiwanja Jijini Dodoma kwa kila mchezaji wa Taifa Stars iliyotolewa na Rais Magufuli ambapo naye atapatiwa kiwanja cha kujenga nyumba.

Peter Tino amezeweka pesa hizo katika akaunti yake ya Benki ya CRDB aliyoifungua mara tu baada ya kutoka Ikulu na kukabidhiwa kadi yenye taarifa zake za benki (ATM).

“Hakika Mungu ni mkubwa” amesema Peter Tino baada ya kupokea kadi yake ya Benki kwa Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, Bw. George Yatera, akishuhudiwa na Afisa kutoka kutoka TFF Bw. John Michael Mashaka. “Hela hii sikuiota hata ndotoni na mradi Raisi wetu mpendwa John Pombe Magufuli kanikumbuka hakika sintomwangusha. Yaani nitakwenda kumalizia kibanda changu kule Morogoro, ” aliongezea.

Afisa wa Benki hiyo Bi. Gloria Kaale ndiye aliyemsajili mchezaji huyo ambaye wadogo zake, Gebbo Peter na Emma Peter, nao walitikisa anga za soka nchini kwa nyakati tofauti siku za nyuma kabla ya na wao kustaafu. Familia yao kwa sasa inaishi Morogoro.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, ilikuwa ni Agosti 26,1979 wakati timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars ilipokuwa ikirudiana na timu ya soka ya Taifa ya Zambia katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 1980 zilizofanyika nchini Nigeria.Pambano hilo lilichezwa mjini Ndola.

Mechi hiyo ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa Taifa Stars kwa vile ilikuwa ikihitaji sare ya aina yeyote ili iweke historia ya kufuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza , tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo mwaka 1968. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili nyuma kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars iliishinda Zambia bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na kiungo Mohammed Rishard Adolph.

Ushindi huo ulipatikana kwa mbinde kiasi kwamba mashabiki wengi hawakuwa na imani iwapo Taifa Stars ingeshinda ama kupata sare katika mechi ya marudiano. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwani Wazambia walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika za mapema na kudumu nalo kwa takriban dakika 86.

Zikiwa zimesalia dakika tatu pambano hilo kumalizika, mshambuliaji mrefu mwenye kasi na mashuti makali, Peter Tino alibadili sura ya mchezo na kufanya kile kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo huo nchini.

Ilipigwa kona kwenye lango la Taifa Stars, kipa Juma Pondamali akaupangua mpira kwa ngumi, ukamkuta kiungo Leodegar Tenga, aliyetoa pasi ndefu kwa kiungo mwenzake, Hussein Ngulungu, ambaye naye alitoa pasi ndefu kwa Tino.

Akiwa amezungukwa na mabeki watatu wa Zambia, Tino alilazimika kupiga hesabu za haraka haraka. Aliwachomoka mbio mabeki nao na kukimbia na mpira kwa kasi. Alipofika nje kidogo ya eneo la hatari la Zambia, alifumua shuti kali la mguu wa kulia, lililompita kipa Shileshi wa Zambia na mpira kutinga wavuni.Bao hilo lilipatikana baada ya pasi tatu.

Katika mechi hiyo, Taifa Stars iliwakilishwa na kipa Juma Pondamali,mabeki ni Leopard Tasso, Mohammed Kajole/ Ahmed Amasha, Salim Amir, Jella Mtagwa, viungo ni Leodegar Tenga, Hussein Ngulungu na washambulaji ni Omari Hussein, Peter Tino, Mohamed Salim na Thuweni Ally.

Kikosi hicho kilikuwa chini ya Kocha Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Wazawa Joel Bendera na Ray Gama (ambao kwa sasa wote ni marehemu), ndicho kilichoiwakilisha Tanzania katika fainali za kombe hilo zilizofanyika nchini Nigeria.

Katika fainali hizo, Taifa Stars ilichapwa mabao 3-1 na wenyeji Nigeria katika mechi ya ufunguzi, ilitoka sare ya mabao 2-2 na Ivory Coast kabla ya kuchapwa mabao 2-1 na Misri na kutolewa hatua ya makundi.

Hiyo ilikuwa ni miaka 39 iliyopita ambapo hivi sasa, baada ya kuichapa Uganda mabao 3-0 Jumapili, kila Mtanzania ameweka matumaini kwenye kikosi hicho kipya kilicho chini ya kocha kutoka Nigeria, Emmanuel Amunike.
  Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akikamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 leo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha Tanzania kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON). Wanaoshuhudia ni Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, George Yatera na Afisa kutoka kutoka TFF John Michael Mashaka. Kushoto ni Afisa wa Benki hiyo Bi. Gloria Kaale ambaye ndiye aliyemfungulia akaunti nyota huyo wa zamani.
 Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akielekezwa na Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, Bw. George Yatera namna na kutumia kadi yake ya ATM baada ya kukamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON). Kushoto ni Afisa wa Benki hiyo Gloria Kaale
 Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akikabidhiwa kadi yake ya ATM kutoka kwa Meneja Biashara wa Tawi la CRDB la Azikiwe, Bw. George Yatera baada ya kukamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON). Wanaoshihudia ni Afisa kutoka kutoka TFF Bw. John Michael Mashaka na Afisa wa Benki hiyo Bi. Gloria Kaale ambaye ndiye.
 Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akionesha kadi yake ya ATM baada ya kukamilisha kufungua akaunti ili aweke shilingi Milioni 5 alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON).
Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Peter Tino akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumzawadia shilingi Milioni 5 kwa kutambua mchango wake kwa Timu ya Taifa ya mwaka 1980 ambapo goli lake liliiwezesha Tanzania kufuzu fainali ya Michuano ya Soka Barani Afrika (AFCON) wakati Rais Magufuli alipokutana na kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambao jana waliifunga Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) na kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika baadaye mwezi Juni 2019 huko Misri. Picha na Sultani Kipingo

NAJIVUNIA KUONGOZA ENEO AMBALO ARDHI YAKE ASILIMIA 67 IMEPIMWA,IMESAIDIA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI- DK FAUSTINE, NDUGULILE

$
0
0

Naibu Waziri wa afya na Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine, Ndugulile, amesema anajivunia kuongoza eneo ambalo ardhi yake asilimia 67 imepimwa, jambo ambalo limesaidia kutatua migogoro ya ardhi na kuwa na ardhi inayotambulika.

Naibu waziri huyo wa afya ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akigawa mkataba wa ununuzi wa viwanja kwa wananchi wa Mtaa wa Mwasonga, Kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi nchini.

Ndugulile, amesema kitendo cha KC kupeleka mradi huo ni katika kuendeleza juhudi hizo za Serikali na kuahidi hadi kufika mwaka 2020 wana imani ardhi yote itakuwa imepimwa kwa eneo lilibaki ni asilimia chache.

“Eneo la kisarawe2 ni la kimkakati kwa ajili ya biashara na tayari eka 1,000 zimetengwa kwa ajili ya viwanda, hivyo mlioamua kununua viwanja hapa hamtajuta kwani huko mbele ya Kigamboni inatarajiwa kuwa kitovu cha biashara katika mkoa wa Dar es Salaam ,”amesema Ndugulile.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya KC, Khalid Mwinyi, amesema viwanja hivyo huuzwa kwa mkopo ambapo mteja akishalipa asilimia 20 ya bei ya kiwanja husika, inayobaki analipa kwa miaka miwili.

Mwinyi amebainisha kuwa wamekuja na mkakati huo kama njia ya kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini kumiliki ardhi ambapo ekari 200 zilizopimwa zimechukuliwa na wananchi zaidi ya 900.

“Moja ya changamoto tuliyoipata katika kupata wateja ni pamoja na suala la wananchi kuamini kama kweli watapata viwanja kwa kile walichodai wameshatapeliwa sana huko nyuma, hivyo tunajitahidi kuwaonyesha sisi hatupo hivyo kwa kuweka kila kitu wazi, hivyo tunaomba wananchi watuamini tumekuja kuleta suluhisho la migogoro ya ardhi,” amesema.

Naye Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuna alichojifunza kuhusu umuhimu wa kuwa na maeneo ya kupimwa kutoka Kigamboni, ustaarabu ambao amesema atapeleka elimu hiyo Ilala ili nao waige mfano huo mzuri.

Wananchi waliokabidhiwa mikataba akiwemo Eleotheria Namikowi ambaye ni mkazi wa Mwananyamala na Bashiru Mkabala wa Ubungo, wamesema moja ya jambo lililowashawishi kuchukua viwanja hivyo ni pamoja na kukopeshwa vifaa vya ujenzi.
Mbunge wa Kigamboni ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi, ambapo ameiomba kampuni ya KC isiwe chanzo cha migogoro ya ardhi katika hafla ya kugawa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwa wananchi wa Mtaa wa Mwasonga, Kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi jijini Dar es Salaam.
Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi ambapo ameipongeza kampuni ya KC kwa kuwakopesha wananchi viwanja bila riba katika hafla ya kugawa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwananchi wa Mtaa wa Mwasonga, kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya KC, Khalid Mwinyi akisoma hotuba katika hafla kugawa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwananchi wa mtaa wa Mwasonga, kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile (katikati) akizindua utoaji wa mikataba ya ununuzi wa viwanja kwananchi wa Mtaa wa Mwasonga, Kata ya Kisarawe2, vinavyouzwa kwa mkopo na kampuni ya KC inayojishughulisha na upimaji na kuendeleza ardhi jijini Dar es Salaam. Kushoto Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.(kulia) Mkurugenzi wa kampuni ya KC, Khalid Mwinyi.
Mbunge wa Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akisalimina na wananchi wa Kigamboni.( Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Maafisa wa kampuni ya KC wakiwagawia mikataba ya ununuzi wa viwanja wananchi wa Mtaa wa Mwasonga, kata ya Kisarawe2, wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

MEYA UBUNGO AGAWA VYEREHANI 10 KWA AKINA MAMA WAJASIRIAMALI,AWAASA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

$
0
0
Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mh,Boniface Jacob leo amegawa vyerehani kumi (10), Vya kisasa Vinavyogharimu kiasi cha Tsh Millioni 20 Kwa Vikundi viwili (2) Vya Wanawake Manispaa ya Ubungo ambavyo ni MASHUJAA WOMEN GROUP na VICTORIA FOUNDATION GROUP

Katika Hafla hiyo ya ugawaji wa Misaada hiyo ya vyerehani kumi (10),lengo kubwa ikiwa ni Kuwawezesha Wanawake kujikwamua kiuchumi, na kuwapatia Mafunzo ya ushonaji na Ujasiriamali 

Mstahiki Meya ameshirikiana na Kiwanda Cha Ushonaji cha SPESHOZ TANZANIA ambapo Mkurugenzi wake Bw,Jeffrey Jessey amesema Kampuni Yake Itaunga mkono Juhudi za Mstahiki Meya za Kuwawezesha Wanamke kujikwamua Kiuchumi kwa Kutoa Mafunzo ya Miezi mitatu(3) kwa wanawake 48 wa Vikundi vyote viwili Vya wakina Mama Waliopokea Misaada hiyo Kwa awamu hii ya Kwanza.

Aidha Mkurugenzi mwenza wa SPESHOZ TANZANIA Bi Cecilia Mosha, ameahidi kuendelea kutoa Ushirikiano Kwa Mstahiki Meya katika awamu zingine zitakazo fuatia Katika Programu ya Ugawaji Vyerehani kwa ajili ya Kumsaidia Mwanamke Kujikwamua Kiuchumi, Pamoja na kutoa wito kwa Wanawake wengine kuitikia fursa ya Mstahiki Meya na kufanyia kazi kwa Vitendo kauli ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda

Mstahiki Meya ametoa wito kwa wakina Mama wengine ndani ya Manispaa ya Ubungo kuendelea kuandika barua za Maombi na Maandiko ya Mchanganuo ya Miradi ya Ushaonaji ,Kwa ajili ya kupatiwa Misaada Awamu zingine zinazofuata.
Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mh,Boniface Jacob (katikati) akiwakabidhi vyerehani kumi vikundi viwili vya wajasiriamali wanawake vyenye thamani ya Millioni 20 leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Maasaka,MMG)
Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mh,Boniface Jacob (katikati) akizungumza leo jijini Dar es Saam katika hafla ya ugawaji ya vyerehani kumi vyenye thamani ya Millioni 20 kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

AFCON MWAKA 1980: NIGERIA VS TANZANIA JIJINI LAGOS

MBUNGE WA MIKUMI MHE JOSEPH HAULE "PROFESA J" AIZUNGUMZIA TAIFA STARS

KUKOSEKANA ELIMU YA KUTOSHA JUU YA WAJUMBE WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA NGAZI ZA KATA CHANZO MIGOGORO

$
0
0

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Tanga Doris Wilson wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo mabaraza,wenyeviti na wajumbe juu ya ujuaji wa sheria na kufata taratibu na kutoa maamuzi sahihi ili kuweza kutatua migogoro ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) na kufanyika mjini hapa 
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub akizungumza wakati wa warsha hiyo 
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo wakati wa warsha hiyo 
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo 
Sehemu ya wajumbe wa warsha hiyo wakifuatilia 


KUKOSEKANA elimu kwa wajumbe wengi waliopo kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya kata kumeelezwa kuchangia kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa waledi mkubwa na kusababisha migogoro kwa wananchi na manung’uniko.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Tanga Doris Wilson wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo mabaraza,wenyeviti na wajumbe juu ya ujuaji wa sheria na kufata taratibu na kutoa maamuzi sahihi ili kuweza kutatua migogoro ulioandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) na kufanyika mjini hapa.

Alisema elimu hiyo itakuwa chachu kwa wajumbe hao kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwenye mabaraza hayo lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi ambao wanakabiliwa na migogoro mbalimbali kwenye maeneo yao.

“Changamoto kubwa ya mabaraza ya Kata ni elimu wajumbe wengi hawajapata elimu kuhusu mabaraza hayo, muundo, namna ya utendaji, akidi katika kuendesha na utaratibu wa kuendesha mashauri hivyo tunaamini kupitia elimu hii inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye utekelezaji wa shughuli zenu “Alisema Mwenyekiti huyo.

“Lakini pia tunaishukuru Tawla kwani wanapotoa mafunzo ya namna hii wanawapa wajumbe uelewa kuhusu namna ya kuendesha mashauri hayo,kwa kufanya hivyo haki kwa wananchi inaweza kutendeka na kuondoa manung’uniko “Alisema 

Aidha alisema mikakati waliokuwa nayo hivi sasa ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa mabaraza ya ngazi ya kata ili waweze kufanya kazi zao kwa waledi mkubwa katika kutoa haki pindi wanapopelekewa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub alisema lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu kwa ngazi mbalimbali kwa viongozi wa mabaraza,wenyeviti na wajumbe ili waweze kujua sheria na kufuata taratibu na kutoa maamuzi sahihi wakati wakitatua migogoro.

Mratibu huyo alisema warsha hiyo imehusisha wajumbe, makatibu na wenyeviti wa mabaraza ya ardhi kutoka kwenye kata mbili za Magila na Kilulu kwalengo la kuwajengea uwezo wa kufahamu sheria za ardhi na kuto maamuzi sahihi kwa wananchi.

Hata hivyo alisema watajaribu kuangalia jinsi gani ya kuweza kushirikiana kwa pamoja kupunguza changamoto hizo yakiwemo mashauri mengi yaliwepo kwenye baraza hilo hali itakayowezesha kuondosha migogoro kwa wananchi.

NSSF,Magereza kuanzisha mradi wa kiwanda cha sukari Morogoro,Watembelea shamba la Bakharesa Bagamoyo kujifunza

$
0
0
Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio akiwa na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo,kuhusu maandalizi makubwa yanayotarajiwa kufanywa ndani ya shamba hilo ikiwemo na miundo mbinu mbalimbali namna itakavyojengwa,Uongozi wa NSSF jana Machi 25,2019 umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .

Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna (mwenye kofia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio akiwa na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo,namna ya kuandaa shamba la miwa,upandaji mbegu na utunzaji wake. Uongozi wa NSSF umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .

Muonekano wa shamba la Miwa akianza kuchipua

Operesheni Meneja wa Shamba Narayawan Krishna akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kati) walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya shamba hilo ikiwemo kujionea ujenzi wa miundo mbinu kama vile mabwawa ya maji,mabomba ya maji,barabara yote hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi makubwa yanayotarajiwa kufamywa ndani ya shamba hilo lenye ukubwa wa Ekari elfu 25,000, kushoto ni Mkuu wa Mradi wa shamba hilo,Hosein Sufiani.

Operesheni Meneja wa shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa, Narayawan Krishna (mwenye kofia) akieleza maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji ndani ya shamba hilo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio alieongozana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka shirika hilo. Uongozi wa NSSF umetembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo,ambapo shamba hilo lina ukubwa wa Ekari 25,000 .

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kushoto) akiwa ameongozana na Wasimamizi wa shamba hilo wakitembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa miundombinu katika shamba hilo,lililopo nje kidogo ya mji mkongwe wa Wilaya ya Bagamoyo,mkoani Pwani.


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi Waandamizi wa shirika hilo,walifika Ofisini kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakharesa, Bw. Said Salim Bakharesa (pichani kulia),kumshukuru mara baada ya kumaliza ziara yao walioifanya asubuhi Machi 25,2019 ya kutembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo ya sukari.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,William Erio (pichani kulia ) akimsikiliza Mkuu wa Mradi wa shamba hilo,Hosein Sufiani alipokuwa akieleza namna mbegu za miwa zinavyooteshwa ndani ya Kitalu,jana Machi 25,2019,ambapo Uongozi wa NSSF ulietembelea shamba la sukari la Bagamoyo lenye ukubwa wa Ekari 25,000 linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Said Salim Bakharesa ofisini kwake jana Machi 25,2019 jijini Dar,akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi waandamizi wa shirika hilo (hawapo pichani),walipokwenda kumshukuru mara baada ya kumaliza ziara yao walioifanya leo asubuhi walipotembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo ya sukari.

Serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Jamii, NSSF na Jeshi la Magereza Tanzania, wapo katika hatua za mwisho za uanzishwaji wa mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Morogoro Vijijini, eneo ambalo linamilikiwa na Jeshi la Magereza.NSSF kupitia kampuni yao tanzu ya Mkulazi imeamua kuliendeleza shamba hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha sukari, lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa sukari nchini, pia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni za kuagiza sukari nje ya nchi na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo.
Picha ya Pamoja mara baada ya mazungumzo mafupi.




Na Grace Semfuko-maelezo

Serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Jamii, NSSF na Jeshi la Magereza Tanzania, wapo katika hatua za mwisho za uanzishwaji wa mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Morogoro Vijijini, eneo ambalo linamilikiwa na Jeshi la Magereza

NSSF kupitia kampuni yao tanzu ya Mkulazi imeamua kuliendeleza shamba hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha sukari, lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa sukari nchini, pia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni za kuagiza sukari nje ya nchi na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo.

Akizungumza Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani wakati alipotembelea shamba la sukari la Bagamoyo linalomilikiwa na Kampuni ya Bakharesa kwa lengo la kujifunza kilimo na uzalishaji wa bidhaa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio, alisema mradi huo unalenga kuzalisha tani za sukari zisizopungua laki mbili kwa mwaka.

Alisema pia katika mradi huo watazalisha umeme kwa kutumia mabaki ya miwa kiasi cha megawatt 20 kwa mwaka, kwa ajili ya matumizi ya kiwanda na kuuza TANESCO, kiasi hicho aliongezea kusema kitatokana na uzalisha wa miwa kwa tani milioni mbili kwa mwaka.

“Sisi NSSF tunafahamu mahitaji makubwa ya sukari katika nchi yetu, Mradi huu mkubwa utaongeza sukari sokoni, lengo letu kubwa ni kuongeza ajira na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa sukari nchini Tanzania,” alisema Bw. Erio.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Said Salim Bakhresa, alizipongeza taasisi hizo za Serikali kwa hatua hizo na akawataka kuendelea kujifunza na kuonesha milango kuwa wazi wakati wowote.

“Sisi Makampuni ya Bakhresa tupo wakati wote na tutawapa ushauri wa suala lolote mnalotaka kujifunza kwa kuwa tunajenga Taifa moja kiuchumi, milango ipo wazi” alisema, Bw. Bakhresa.

Bw. Bakhresa ni mwendeshaji wa shamba la miwa ya kufua sukari la Bagamoyo, lenye Hekta elfu kumi lililopo katika eneo la Makurunge, nje kidogo ya mji mkongwe wa Bagamoyo, ambalo lilianza shughuli zake za kilimo cha miwa kwa majaribio mwaka 2018 na kufanikiwa kuvuna tani 864 za miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

Mwezi Oktoba 6, mwaka 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, mara baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Bakhresa,aliipatia kampuni hiyo shamba hilo kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo cha miwa, ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo.

Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 mahitaji ya sukari yalikuwa tani 590,000 na kati ya hizo tani 135,000 zilikuwa ni mahitaji ya viwandani na tani 455,000 mahitaji ya kawaida ya binaadamu, ambapo uzalishaji wa sukari nchini ulikuwa tani 350,846 na kuwepo na upungufu wa tani 259,156; hatua iliyoifanya Serikali kuwezesha sekta binafsi katika kuzalisha bidhaa hiyo, na hivyo kiwanda cha Bakhresa pekee kinatarajia kuzalisha tani laki moja za sukari ifikapo mwaka 2022.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 26,2019

MKAZI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI AJINYAKULIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI TANO KUTOKA BIKO

$
0
0
 Mkulima wa mananasi mwenye maskani yake, Bagamoyo, mkoani Pwani, Ambari Zuberi Kingwamba, amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka Biko, bahati nasibu ya Watanzania inayotoa ushindi mkubwa, ambapo alinyakua sh milioni tano kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake. Kulia ni Mratibu Msaidizi wa Biko, Hassan Ahmed. P
 Mshindi wa sh milioni tano kutoka kwa waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Ambari Zuberi Kingwamba wa Bagamoyo mkoani Pwani, anayejihusisha na ukulima wa mananasi, amekabidhiwa fedha zake leo tayari kwa kuziingiza kwenye matumizi yake ya kila siku ili kuinua uchumi wake. Picha na Mpigapicha Wetu.

TVMC YAENDESHA MAFUNZO YA KUTENGENEZA BATIKI KWA VIKUNDI VYA WAZAZI

$
0
0

Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC) Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO limeendesha mafunzo ye kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.

Mafunzo hayo ya siku nne yalianza Machi 21 na kumalizika Machi 25,2019 katika ukumbi wa SIDO mkoa wa Shinyanga kwa kukutanisha washiriki 25 yakiwa na lengo la kuwakwamua kiuchumi,kuondokana na umaskini ili kuzuia mimba na ndoa za utotoni sambamba na kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia alilipongeza shirika la TVMC kumsaidia Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kutengeneza viwanda.

“TVMC mmeonesha kwa vitendo kuwa mnaunga mkono serikali ya Viwanda,tunawapongeza kwa kufanya kazi nzuri inayofuata matakwa ya serikali,tunaamini kuwa kupitia mafunzo haya,tutapata viwanda vidogo kutoka wajasiamali hawa na tunafurahi mmetoa mafunzo kwa kushirikiana na SIDO”,alieleza Mbia.Aidha alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwainua kiuchumi wananchi huku akiwataka wajasiriamali kuomba mikopo kwenye halmashauri za wilaya ili kuendeleza shughuli zao.

Kwa Upande wake,Mkurugenzi wa Shirika la TVMC, Musa Ngangala alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni unaotekelezwa na TVMC kwa ufadhili wa shirika la Firelight Foundation la nchini Marekani.

“Ili kufanikisha mradi huu,mwaka 2016 tulianzisha vikundi vya ujasiriamali kwa wazazi ili kuhakikisha tunawakwamua kiuchumi ili kuondokana na umaskini ambao huchangia kwa kiasi kikubwa mimba na ndoa za utotoni,na kwa muda wa siku nne tumetoa mafunzo ya kutengeneza batiki”,alieleza Ngangala.

“Ili kuunga mkono kwa vitendo sera ya serikali ya Viwanda kupitia kwa Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli,Tunatarajia kuanzisha vyumba maalum kwa ajili ya shughuli ya utengenezaji batiki na tutatoa vitendea kazi vya kuanzia ili kuhakikisha vikundi hivi vinakuwa vya mfano katika Manispaa ya Shinyanga lakini mkoa kwa ujumla”,alisema Ngangala.

Hata hivyo Ngangala alisema TVMC itaendelea kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ili kuwapa ujuzi wananchi wafanye shughuli za ujasiriamali ikiwa ni katika kuwaletea maendeleo wananchi.Mara baada ya mafunzo ya Utengenezaji Batiki kumalizika,umefanyika uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.

Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga yaliyoendeshwa na SIDO kwa ufadhili wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness Elia,kulia ni Mkurugenzi wa TVMC,Musa Ngangala. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Musa Ngangala akielezea lengo la kutoa mafunzo ya utengenezaji batiki kwa vikundi vya wazazi katika kata ya Chamaguha. Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza batiki kwa vikundi vya wazazi kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakiwa wameshikilia batiki iliyotengenezwa na vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha wakati wa uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Kulia ni Mkurugenzi wa TVMC ,Musa Ngangala akifurahia batiki ya ukweli.

Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC ukiendelea.
Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Pichani ni miongoni mwa batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka Chamaguha.
Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC ukiendelea.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la PACESH, Perpetua Magoke aliyealikwa kushuhudia kazi ya wajasiriamali wa Chamaguha.
Zoezi la utoaji vyeti kushiriki na kufuzu mafunzo ya utengenezaji batiki likiendelea.
Utoaji vyeti ukiendelea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakitengeneza batiki.
Utengenezaji batiki ukiendelea.
Zoezi la kuchanganya rangi likiendelea.
Batiki ikitolewa kwenye rangi.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ya utengenezaji batiki. Picha ya pamoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 25.03.2019

MKUU WA WILAYA TUNDURU AKABIDHI VITI, MEZA KWA SHULE YA SEKONDARI MUHUWESI

$
0
0


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amekabidhi meza na viti 70 kwa shule mpya ya Sekondari ya Muhewesi iliyosajiliwa mwaka 2019 na hiyo kumaliza changamoto hiyo ambayo ilikuwepo shuleni hapo. 

Homera amekabidhi viti na meza hivyo kwa Ofisa Elimu Sekondari katika wilaya hiyo Selestine Kahangwa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru. 

Shule hiyo ipo kwenye kijiji na kata ya Muhuwesi ambapo moja ya changamoto kubwa ilikuwa ni ukosefu wa viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo. 

Akizungumzia vifaa hivyo ,Homera ameiambia Mchuzi Blog kuwa thamani ya vifaa vyote hivyo ni Sh.5,000,000 na kwamba amewashukuru wadau walioshiriki kuchangia meza na viti hivyo.Amewataja baadhi ya wadau hao ni Kampuni ya Jafu Investment iliyochangia meza 40 na viti 40, Jitegemee Ranchi iliyochangia meza 15 na viti 15, Lupondo amechangia meza 5 na viti 5,na Mataka amechangia meza 10 na viti 10. 

Hata hivyo, Homera amesema anatarajia kukabidhi meza 200 na viti 200 vingine kwa ajili ya shule mbalimbali za sekondari wilayani humo huku akisisitiza kuwa "Tukutane site#Tukutane Kazini.


TMA YATOA MREJEO WA MUELEKEO WA MVUA KIPINDI CHA MACHI - MEI 2019

$
0
0
Taarifa hiyo imeelezea uwepo wa migandamizo midogo ya hewa kuanzia tarehe 5 Machi, umepelekea kutokea kwa kimbunga (Idai) kuanzia tarehe 10 hadi 15 Machi, 2019 katika rasi ya Msumbiji na kusababisha upepo wenye unyevunyevu kusukumwa kusini mwa Afrika na hivyo kupelekea upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi hususan ukanda wa kaskazini. Migandamizo midogo ya hewa inaendelea kujitokeza katika maeneo ya kaskazini mwa Madagascar, ambapo kwa sasa moja ya migandamizo hiyo imeimarika na kuwa kimbunga Savannah. Migandamizo na vimbunga hivi vinatarajiwa kusababisha mvua kuelekea zaidi katika maeneo ya bahari ya Hindi na upungufu katika maeneo mengi ya nchi, kutokana na mahali mwelekeo unaotarajiwa.

Kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na jinsi inavyotarajiwa kuwa kwa kipindi cha Machi – Mei 2019 (kama ilivyoelezwa katika kipengele II cha taarifa hii);

Uwezekano mkubwa wa upungufu wa mvua katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Tanga, maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na vipindi vichache vya upungufu wa mvua katika maeneo machache ya mikoa ya Kilimanjaro na Manyara.
Mwelekeo wa mvua za Masika uliotolewa ulionesha kuwa mvua zinatarajiwa kuwa za muda mfupi na kuisha mapema kati ya wiki ya nne ya mwezi Aprili na wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2019. Hata hivyo, hali iliyopo sasa inaonesha uwezekano wa mvua za Masika kuisha mapema zaidi katika baadhi ya maeneo wiki ya pili ya mwezi Aprili, 2019.
Mvua za msimu (Novemba-Aprili) zinatarajiwa kuendelea kama zilivyotabiriwa. “Mvua za Msimu ambazo zilianza mwezi Novemba, 2018 zinatarajiwa kuendelea hadi mwishoni mwa mwezi April 2019. Katika kipindi hicho mvua hizo za Msimu zinatarajiwa kuwa za wastani katika maeneo mengi. Hata hivyo, mvua za chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo machache ya kanda ya Kusini (Ruvuma), pamoja na mikoa ya Dodoma na Singida”.
I. MREJEO WA MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA KIPINDI CHA MACHI - MEI 2019

Msimu wa mvua za Masika ni mahususi katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki, pwani ya Kaskazini na visiwa vya Unguja na Pemba, ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Ufuatao ni mwelekeo wa mvua za Masika kwa kipindi kilichosalia;

a) Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara na Simiyu): Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani kwa ujumla katika maeneo ya mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Mara. Hata hivyo, maeneo machache ya mkoa wa Kagera na wilaya ya Kibondo yanatarajiwa kuwa na upungufu wa mvua. Mvua zinatarajiwa kuisha mapema katika wiki ya tatu ya mwezi Aprili, 2019.

b) Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro):

Katika kipindi cha msimu kilichosalia, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro. Aidha, mvua za wastani kwa ujumla zinatarajiwa katika maeneo mengi ya visiwa vya Unguja na Pemba. Pamoja na mvua za juu ya wastani kujitokeza katika maeneo machache ya visiwa vya Unguja na Pemba, mvua zinatarajiwa kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Aprili, 2019. Mvua katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro zinatarajiwa kuisha katika wiki ya pili ya mwezi Aprili, 2019.

c) Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):

Kwa ujumla, mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi. Hata hivyo, mvua za juu ya wastani zinatarajiwa kujitokeza katika maeneo machache ya mkoa wa Arusha. Mvua zinatarajiwa kuisha mapema katika wiki ya tatu ya mwezi Aprili, 2019.

II. MIFUMO YA HALI YA HEWA

Hali ya joto la bahari pamoja na mifumo ya hali ya hewa inaonesha upungufu wa mvua katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Katika kipindi cha msimu kilichosalia, joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika maeneo ya kati na kusini magharibi mwa bahari ya Hindi, hali ambayo inatarajiwa kupelekea kuvuma kwa upepo hafifu kutoka mashariki na kusababisha upungufu wa mvua katika maeneo mengi nchini. Halikadhalika, joto la bahari la wastani hadi juu kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo la kusini mashariki mwa bahari ya Atlantic karibu na pwani ya Angola. Hali hii inatarajiwa kupunguza msukumo wa upepo kutoka magharibi na hivyo kupunguza uwepo wa unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo.

III. USHAURI

Mamlaka ya Hali ya Hewa inawashauri watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima, wafugaji, Mamlaka za Wanyamapori, Mamlaka za Maji na Afya waendelee kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalamu katika sekta husika.

Mwelekeo wa mvua uliotolewa hapa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia utabiri wa saa 24, siku 10 pamoja na mwezi kama unavyotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini

Dkt. Kalemani akagua REA III wilayani Kasulu, Buhigwe na Kigoma Vijijini

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Kigoma
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kasulu, Kigoma Vijijini na Buhigwe mkoani Kigoma kwa lengo la kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) ambapo pia aliwasha umeme katika baadhi ya Vijiji.

Akiwa wilayani Kasulu, Dkt Kalemani alikagua kazi zinazofanywa na mkandarasi katika Kijiji cha Ruhita ambapo alikuta Kijiji hicho bado hakijaunganishwa umeme na kumuagiza Mkandarasi, kampuni ya CCCE Etern kufikisha umeme kijijini hapo baada ya siku 15.

Aidha, alimtaka Meneja wa TANESCO, Wilaya ya Kasulu kuhakikisha kuwa, anasimamia suala ya uchoraji wa ramani za kuingiza umeme ndani ya nyumba za wananchi kwani kuna baadhi ya watu binafsi wanaofanya kazi hizo wamekuwa wakiwatoza wananchi gharama kubwa bila kujali tofauti ya ukubwa au udogo wa kazi.

Vilevile, Dkt Kalemani alimtaka Meneja huyo kuhakikisha kuwa watu wanaofanya kazi za kufunga nyaya za umeme ndani ya nyumba za wananchi wanatambulika na TANESCO ili kuepusha utapeli na kufanya kazi chini ya viwango vinavyotakiwa.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange alimweleza Dkt Kalemani kuwa, wananchi wa Kijiji hicho wamesubiri umeme kwa muda mrefu baada ya kupata ahadi ya kupelekewa nishati hiyo, hivyo wanaomba Mkandarasi akamilishe kazi hiyo mapema ili waweze kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.

Akizungumzia suala hilo, Dkt Kalemani alisema kuwa, Mkandarasi ambaye ni kampuni ya CCCE Etern ameanza kazi mwezi Januari mwaka huu tofauti na wanandarasi wa umeme katika maeneo mengine nchini ambao walianza kazi mwaka jana, hii ni kwa sababu ya masuala ya kisheria yaliyojitokeza hapo awali lakini sasa Mkandarasi huyo anaendelea na kazi.

Akiwa wilayani Buhigwe, Dkt Kalemani alikagua miundombinu ya umeme katika Kijiji cha Bulimanyi ambacho tayari kimeshafikishiwa umeme na kaya zaidi ya Kumi zimeshaunganishwa na nishati hiyo na kumuagiza Mkandarasi kupeleka umeme katika Vijiji vyote vya Wilaya hiyo.

Dkt. Kalemani pia alikagua miundombinu ya umeme katika Kijiji cha Mkigo wilayani Kigoma Vijijini, ambapo pamoja na kuzungumza na wananchi, aliwasha umeme katika Kijiji hicho.
 Moja Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mpigo wilayani Kigoma Vijijini mkoa wa Kigoma kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho.
Wananchi katika Kijiji cha Bulimanyi wilayani Buhigwe, Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati alipofika kijijini hapo kukagua miundombinu ya usambazaji umeme.

KUMBUKIZI: MASHUJAA WA RIADHA WENYE HISTORIA NZITO ZA MICHEZO KULIKO ZOTE TANZANIA

$
0
0

Pichani ni Jenerali Mirisho Hagai Sarakikya (kati) akiwa na wanariadha mabingwa wa dunia wa zamani, Filbert Bayi (kushoto) na Juma Ikangaa.  Hawa ni watu watatu ambao mjina yao yanastahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu katika vitabu vya kumbukumbu  ya historia ya riadha na michezo nchini Tanzania. Hilo halina ubishi...

Tukianza na Jenerali Sarakikya, yeye ndiye alikuwa Mkuu wa Majeshi wa kwanza mara tu bada ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1964 na akatumikia wadhifa huo kwa miaka kumi yaani toka hiyo 1964 hadi alipostaafu mwaka 1974. 
Wakati anapata cheo kuwa CDF Jenerali Sarakiya pia alikuwa ndiye mwenyekiti wa chama cha riadha cha Tanzania (TAA) kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1972.
Ikiwa hiyo haitoshi mara baada ya kustaafu jeshini mwaka huo huo wa 1974, Mwalimu Nyerere alimteua Jenerali  Sarakikya kuwa Waziri wa Michezo, Vijana na Utamaduni.
Ukiangalia katikati ya mistari utamaizi kwamba historia ya mafanikio ya riadha na michezo kwa ujumla nchini Tanzania yalikuwa katika miaka hiyo ambayo Jenerali Sarakikya alikuwa mwenyekiti wa TAA, Mkuu wa Majeshi na baadaye Waziri wa michezo, vijana na utamaduni.
Huo ndio wakati wanariadha Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Suleiman Nyambui, Gidamis Shaganga, Mwinga Mwanjala, Nzaeli Kyomo na wengi wengine walikuwa wanang’ara kwenye medani za kimataifa.
Kwa hiyo picha hii ni kubwa na yenye historia nzito kwa kadri mafanikio katika michezo kwa nchi hii yanahusika.
Wote watatu ni wanajeshi wastaafu, kwani Filbert Bayi  baada ya ushindi wake alipandishwa cheo hadi kuwa Luteni, na baada ya kuhudhuria mafunzo ya afisa kadet huko Monduli mwaka 1977 alipanda kuwa Kepteni. Hadi anastaafu mwaka 2001 alikuwa na cheo cha Meja kitengo cha ufundi wa ndege jeshini.

Kwa upande wa Ikangaa, yeye alikuwa Mkurugenzi wa michezo makao makuu ya jeshi hadi alipostaafu kwa mujibu wa sheria akiwa na cheo cha Kanali. 
Filbert Bayi Sanka ni mwanariadha aliyeiandikia Tanzania historia isiyoweza kusahaulika. Filbert Bayi ndie mwanariadha wa Pili ambae anakamilisha medali ya pili ya Tanzania kwenye Mashindano ya Olympic.
Tanzania Imewahi kupata Medali mbili tu katika Mashindano ya Olympic mpaka sasa. Filbert Bayi alipata Medali ya Silver katika mbio za mita 3000 katika mashindano ya Olympic yaliyofanyika mwaka 1980 MOSCOW Mwaka 1978(mita 1500) na Mwaka 1973 (mita 1500) katika mashindano ya All African Games Fibert Bayi alishinda Medali za Dhahabu kwa kuibuka namba moja katika mashindano yote mawili.
Ushindi huu ulitengeneza historia kubwa Tanzania. Mwaka 1974 katika mashindano ya Commonwealth Games yaliyofanyika Christchurch “New Zealand” Filbert Bayi aliweka rekodi ya kukimbia mita 1500 kwa dakika 3 na sekunde 32.2 mbele ya mwanariadha kutoka New Zealand John Walker na Mkenya Ben Jipcho, hivyo kuiwezesha Tanzania kupata medali ya Dhahabu katika mashindano hayo. 

MAFUNZO YA MADAKTARI WA WATOTO WACHANGA KUTOKA AFRIKA MASHARIKI NA KATI YAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Na Ramadhani Ali - Maelezo Zanzibar

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Fadhil Mohd Abdalla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi mmoja vinavyotokana na maambukizi.

Aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha huduma za maradhi ya maambukizi yanayowasumbua watoto ndani ya wiki ya kwanza tokea kuzaliwa zinatolewa katika vituo vyote vya afya badala Hospitali kuu pekee.

Dk. Fadhil alitoa kauli hiyo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya madaktari wakufunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi.

Alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi mitatu lakini vifo vya watoto wachanga wa siku saba za mwanzo tokea kuzaliwa bado imekuwa ni changamoto.

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya alisema Wizara itaendelea kufundisha Madaktari wa vituo vya ya afya msingi ili kuhakikisha kila kituo kinaweza kutoa tiba ya maambukizi.

“Lengo ni kuhakikisha dawa za maambukizi zilizokuwa zikitolewa Hospitali kuu sasa zinasambazwa katika vituo vya afya ili kupunguza vifo vya watoto wachanga” alisisitiza Dk. Fadhil.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Ofisi ya Brazzaville Congo, ambae ni mtaalamu wa afya ya watoto wachanga Dk. Assumpta Muriizhi, alisema akinamama wanapitia kipindi kigumu katika kipindi cha miaka miwili baada ya kujifungua kutokana na kupambana na afya ya mtoto ambae hawezi kujieleza.

Alisema wapo baadhi ya wazazi hawaoni umuhimu wa kuwapeleka watoto wao Hospitali wanapopata maambukizi jambo linapelekea kuathirika zaidi na hatimae kupoteza maisha.

Aliwashauri akinamama wanapogundua watoto wao wachanga wanasumbuliwa na maradhi kuwawahisha mapema vituo vya afya vya karibu kupata huduma ya awali kabla ya kuwapelekwe Hospitali kuu iwapo matatizo yataongezeka.

Alisema hakuna umuhimu mkubwa kwa watoto wachanga kuwaanzisha huduma za afya katika Hospitali kuu hasa kwa Zanzibar ambapo vituo vya afya vinapatikana kila sehemu.

Mkutano huo unahudhuriwa na Madaktari Wataalamu wa watoto wachanga kutoka Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Kenya, Uganda, Tanzani Bara, Zanzibar na Maafisa

Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa ya WHO na UNICEF. 
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Ofisi ya Brazzaville Congo Dk. Assumpta Muriizhi akizungumza na washiriki wa mafunzo ya madaktari wa watoto katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Fadhil Mohd Abdalla akifungua Mafunzo ya siku tano ya madaktari wa watoto wachanga kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya madaktari wa watoto wachanga kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati wakimskiliza Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Fadhil Mohd Abdalla (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo hayo.
 Mshauri wa afya ya watoto wachanga Dk. Samira Aboubakar akijadiliana na baadhi ya washiri wa mafunzo ya watoto wachanga katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja. 
 Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ya siku tano ya madaktari wakufunzi wa watotot wachanga kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati na mgeni rasmin. Picha na Makame Mshenga.

NAIBU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AKEMEA VITENDO VYA UVUNJIVU WA SHERIA ZANZIBAR

$
0
0
Na Khadja Khamis - Maelezo Zanzibar
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Mohamed Ali Ahmed amekemea vitendo vya uvunjifu wa sheria vinavyofanya na baadhi ya wanachama wa ACT Wazalendo na waliokuwa wafuasi wa CUF wanaomuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharifu Hamad .

Mohamed aliyasema hayo Ofisini kwake Mbweni wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu vitendo visivyo vya kiungwana baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa hukumu ya Mgogoro wa viongozi kwa CUF ambapo ilimthibitisha Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa Chama hicho.

Alisema Ofisi ya Vyama vya Siasa haitovumilia uvunjifu wa sheria na kutumia dini katika masuala ya vyama vya siasa vinavyofanywa na mashabiki wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa Maalim Seif Sharifu Hamad.

Aliwataka wanachama na wafuasi hao kuacha kufanya vitendo vya kuchoma bendera za chama pamoja na kuhujumu mali za CUF kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za vyama vya siasa nchini.

Aidha alisema Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa haitomvumilia chama chochote cha siasa kinachokiuka sheria ikiwemo matumizi ya dini kwa lengo la kujinufaisha kisiasa.

“Suala la kutumia dini katika harakati za kisiasa halitapewa nafasi katika zama hizi na atakayejishughulisha na vitendo hivyo atapambana na mkondo wa sheria,” alisisitiza Naibu Msajili wa vyama vya siasa.

Alisema Sheria ya vyama vya siasa inatekeleza majukumu yake ya kuhakikisha vyama vinaendeshwa katika misingi ya kistaarabu kwa lengo la kuleta maendeleo ya wananchi.

Naibu Msajili wa vyama vya siasa alitoa wito kwa wananchi na wafuasi wa vyama vya siasa kutii sheria za nchi na kutokubali kurubuniwa na wanasiasa na hatimae kujiingiza katika matatizo ambayo hayaleti tija yoyote kwa upande wao.
 Naibu Msajili wa vyama Vya siasa Tanzania Mohamed Ali Ahmed akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu vitendo vya uvunjifu wa Sheria vinavyofanywa na mashabiki wa vyama vya Upinzani Zanzibar Ofisini kwake Mbweni Wilaya ya Magharibi B.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia maelezo ya Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania Mohamed Ali Ahmed alipokuwa akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Msajili ya Vyama vya siasa Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar.

Wauguzi Muhimbili watakiwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi

$
0
0
Wauguzi na wakunga Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa mbalimbali wanaotibiwa katika hospitali hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Muuguzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC), Gustav Moyo kwenye kongamano la siku moja linalofanyika katika Hospitali ya Muhimbili.

Moyo aliwataka wauguzi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia taaluma ya uuguzi na ukunga inayoitwa “The Nursing and Midwifery Act. 2010” pamoja na kanuni zake.

Pia, aliwataka wauguzi na wakunga kutowatelekeza wagonjwa wakati wanapohitaji huduma kwa kuwa kumtelekeza mgonjwa ni kosa kwa mujibu wa sheria na hivyo amewataka kuzingatia sheria na kanuni za kazi ili kuboresha huduma mahali pa kazi.

“Wauguzi na wakunga mnapaswa kuzingatia upendo na huruma kwa wagonjwa, ndugu na jamaa wa wagonjwa. Jambo muhimu mnatakiwa kuboresha mawasiliano na kuzingatia maandili na kuwaona ndugu wa wagonjwa ni wadau,” amesema Moyo.

Naye  Happy Masenga katika kongamano hilo alisisitiza umuhimu wa wauguzi na wakunga kujiendeleza katika mafunzo mbalimbali ili kuendana na sayansi na teknolojia wakati wa kutoa huduma.

Katika mafunzo hayo pia wamefundishwa jinsi ya kujaza kitabu maalamu (Log Book) ambacho kinasaidia upatikanaji wa leseni kwa wauguzi. Watoa mada katika kongamano hilo ni Gustav Moyo, Happy Masenga na Asha Gembe.
 Afisa Muuguzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC),  Gustav Moyo akitoa mada kwenye kongamano la siku moja kuhusu sheria na kanuni za kazi kwa wauguzi na wakunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Baadhi ya wauguzi na wakunga wabobezi wakiwa kwenye kongamano la siku moja kuhusu sheria na kanuni za kazi kwa wauguzi na wakunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images