Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE. YAHAYA SIMBA


BREAKING NEWZZZZ: BONDIA HASSAN MWAKINYO AMTWANGA MU-ARGENTINA JIJINI NAIROBI, ALICHOONGEA KABLA YA MPAMBANO

0
0
Fight video courtesy of Bongo 5

TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA VYA MAKURUNGE KITALU "N" BAGAMOYO MJINI

0
0
VIWANJA VYA MATUMIZI MBALIMABALI VINAUZWA ENEO LA MAKURUNGE BAGAMOYO MJINI. VIWANJA  HIVYO VIPO UMBALI WA KILOMITA 3.5 KUTOKA BARABARA KUU YA MSATA-BAGAMOYO INAYOTUMIWA NA MAGARI YAENDAYO MIKOA YA KASKAZINI KUTOKA DAR ES SALAAM. 

PIA VIWANJA VIKO MITA 500 KUTOKA BARABARA YA KUELEKEA PANGANI NA TANGA INAYOENDELEA KUJENGWA  KWA KIWANGO CHA LAMI NA KUWEKEWA MIUNDOMBINU YA MAJI NA UMEME.  

VIWANJA VIPO MPAKANI  MWA ENEO LA RAZABA AMBALO SEHEMU YAKE INA SHAMBA LA MIWA LA  BAKHARESA NA KIWANDA CHA SUKARI KINACHOENDELEA KUJENGWA KM 7 KUTOKA MAHALI VIWANJA VIPO. ENEO LINALOPAKANA NA VIWANJA HIVI LIMEPIMWA NA VIWANJA VYOTE VIMESHAUZWA  NA VIMEISHA. HUDUMA ZOTE ZA JAMII ZIMETENGEWA MAENEO HAYO.

VIWANJA HIVI VINAUZWA KWA GHARAMA ZA MITA ZA MRABA YA SH. 3900 KWA VIWANJA VYA MAKAZI NA T.SHS 4500 KWA VIWANJA VYA BIASHARA  NA SHUGHULI ZINGINE ZA KIUCHUMI IKIJUMUISHA NA HOUSING ESTATES . VIWANJA HIVI VINA UKUBWA WA KATI YA MITA ZA MRABA WA 450 HADI 11000. 

BAADHI YA VIWANJA VINA HATI TAYARI NA VINGINE MNUNUZI ATATENGENEZEWA HATI NA HALMASHAURI KATIKA MKATABA  WA MANUNUZI UTAKAOFANYWA MBELE YA HALMASHAURI.  MALIPO YA KIWANJA YANAWEZA KUFANYWA KWA AWAMU NDANI YA MIEZI SITA. 

 KWA MAHITAJI NA KUCHAGUA KIWANJA PIGA SIMU 
NAMBA 0765851517 AU 0653461126 
AU FIKA OFISI YA AFISA ARDHI MTEULE BAGAMOYO


 Ramani ya site na 
inayoonyesha viwanja


MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 24,2019

HUDUMA ZA MATIBABU YA KIFUA KIKUU ZABORESHWA.

0
0
SERIKALI imeendelea kuboresha huduma za matibabu ya kifua Kikuu kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma za matibabu sambamba na kuongeza vifaa tiba, ikiwa ni jitihada za Serikali kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kifua Kikuu na kutoa tamko kuhusiana na ugonjwa huo katika Hospitali ya Mbagala Jijini Dar es salaam.

"Huduma za matibabu ya Kifua Kikuu (TB) sugu zimesogezwa karibu kwa wananchi, ambapo kwa sasa tunazo hospitali 93 za kutibu Kifua Kikuu sugu ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo, huduma za matibabu zilikuwa zinapatikana katika Hospitali ya Kibong'oto pekee " amesema Waziri Ummy.

Pia, Waziri Ummy amesema katika kila Watanzania 100,000 Watanzania 269 wanahisiwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu, huku watu 70 wanafariki kila siku kutokana ugonjwa wa Kifua Kikuu ambapo ni sawa na watu watatu hufariki kila saa.

"watu 70 kila siku kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, kwahiyo kila saa ni sawa na watu watatu wanafariki kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao unatibika " alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema takribani wagonjwa 154,000 wanaokadiriwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu wanapaswa kufikiwa na kuingizwa katika mpango wa matibabu kila mwaka ili kuutokomeza ugonjwa huu nchini.

Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 Duniani zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa Kifua Kikuu, inakadiriwa kuwa wapo wagonjwa takribani 154,000 ambao huugua ugonjwa wa kifua Kikuu kila mwaka.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Mgonjwa wa Kifua Kikuu ambae hajaanza matibabu anaweza kuambkiza Kati ya watu kumi hadi watu 20 kwa mwaka, hivyo jitihada za makusudi zinatakiwa kuendelea kuchukuliwa ili kutokomeza ugonjwa huu nchini.

"ifahamike kuwa mgonjwa wa kifua Kikuu ambae hajaanza matibabu anaweza kuambukiza kati ya watu kumi hadi watu ishirini kwa mwaka, hivyo tunalojukumu kubwa lakuhakikisha tunawafikia wote wanaougua ili tuweze kuzuia maambukizi mapya ya Kifua Kikuu" alisema Waziri Ummy

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa kitaifa tunakadiliwa kuwa wapo wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu takribani 200 na kati yao, wagonjwa 167 sawa na 84% walianzishiwa matibabu, huku akitoa wito kwa wagonjwa wengine kujitokeza kupata matibabu.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva amemuomba Waziri Ummy kuona ulazima wa kuipanua Hospitali ya Mbagala, ili kurahisisha utoaji huduma za Afya, kwani takribani wanawake 67 mpaka 70 hujifungua kwa siku.

"Wakina mama wanaojifungua hapa ni wengi sana, kwa Mfano jana tu wakina mama 67 wamejifungua, siku nyingine wanafika 70 mpaka 80, hivyo tunahitaji ipanuliwe hospitali hiyo " alisema Mhe. Felix Lyaviva

Nae Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mbagala Dkt. Dk Ally Mussa amesema kuwa kutokana na maboresho makubwa ya hospitali kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa hadi kufikia wagonjwa 1700 kwa siku, kumekuwa na maboresho makubwa ya huduma za mama na mtoto, maboresho ya huduma za uchunguzi wa magonjwa (maabara za kisasa)

"kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa baada ya maboresho mengi katika huduma za Afya za hospitali, kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa hadi kufikia wagonjwa 1700 kwa siku" alisema Dkt. Dk Ally Mussa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa (kushooto) akisema jambo na wananchi wa Mbagala alipotembea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam na kutoa tamko la Siku ya Kifua Kikuu duniani.(wapili kushoto),Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akitoa dawa za Kifua Kikuu kwa Bw. Abbas Sudi alipotembelea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam kujionea hali ya utoaji huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na kutoa Tamko la Serikali katikabkuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani amnayo huadhimishwa Tarehe 24 Machi kila Mwaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akitoa dawa za Kifua Kikuu kwa Bi. Aisha Rashid alipotembelea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam kujionea hali ya utoaji huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na kutoa Tamko la Serikali katikabkuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani amnayo huadhimishwa Tarehe 24 Machi kila Mwaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiangalia zawadi ya nguo aliyopewa na Taasisi ya Mukukite inayojishughulisha kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva akizungumza na wanachi wa Mbagala leo jijini Dar es Salaa ambapo amewaomba wananchi wanapoona dalili za (TB) waende mapema Hospitali watatibuwa bure.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva pindi alipofanya ziara na kujionea huduma za matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali ya Mbagala leo jijini Dar Es Salaam.picha zote na (Emmanuel Maasaka,MMG)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva (wa kwanza kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wa afya wakiwasili katika Hospitali ya Mbagala leo jijini Dar Es Salaam.picha zote na (Emmanuel Maasaka,MMG)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam kuhusu uchugnguzi wa ugonjwa wa Kifua Kikuu alipotembelea Hospitali ya Mbagala leo jijini Dar Es Salaam.
Picha ya pamoja.

Mwandishi wa habari Afariki dunia Jijini Arusha ni Muwakilishi wa (DW)

0
0
Charles  Ole Ngereza enzi za uhai wake
Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC) Cloud Gwandu akiwa msibani nyumbani kwa marehemu Charls Ngereza na baadhi ya waandishi kama wanavyoonekana pichani. 
 Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Mkoani Arusha wakiwa msibani nyumbani kwa Marehemu Charles Ngereza eneo linalofahamika kama Kwa Mrefu.
Na. Vero Ignatus, Arusha.

Mwandishi wa habari aliyekuwa muwakilishi wa habari wa ITV na Radio one hatimae idhaa ya Kiswahili DW mkoani na makamu mwenyekiti wa Arusha Press Club Arusha Charles amefariki duania leo alfajiri

Marehemu alianza kuugua mwishoni mwa mwezi December 2018  ambapo alianza kupatiwa  matibabu katika  hospitali ya KCMC, ambapo alihamishiwa nchini India kwa matibabu zaidi na baadae alirudi nyumbani na kuendelea kujiuguza.

Hata hivyo hali yake ilibadilika ghafla hapo jana mchana na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kisha kuhamishiwa Hospitali ya ST Elizabeth Mkoani Arusha na kufariki dunia alifajiri ya leo

Kwa upande wake mwenyekiti wa Arusha Press Club Cloud Gwandu amesema kuwa msiba huo ni mzito kwa wanahabari wa mkoa wa Arusha kwani marehemu alikuwa ni mchapakazi, asiyekuwa mvivu na alikuwa mtu wa viwango na ubora.

Kwahiyo kama kiongozi mwenzetu tumeshirikiana nae katika mambo mengi sana hata hivi  alipoondoka kuna mradi alituunganisha na wadau wake katika APC wazaidi ya milioni 500 ambao utaleta manufaa kwa wanachama wa APC na tunaamini kwamba wadau hao hawatausitisha

Waandishi wahabari kwa pamoja Jijini Arusha wamesikitishwa kuondokewa mwenzao hivyo  ametoa pole kwa wanahabari na wote walioguswa na msiba huu. Alisema Gwandu.

Nayo familia ya Marehemu `  na wanahabari  Mkoani humu wanaendelea na maandalizi ya siku ya mazishi yatakayotangazwa baadaye.

Marehemu ameacha mke mmoja na watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe.

RC,DC WAPAMBANA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI IRINGA

0
0
Mkuu wa Mkoa Iringa Ally Hapi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mh Richard Kasesela. Ziara ya mkuu wa mkoa akishirikiana kwa karibu na Mkuu Wa Wilaya Iringa Mh Richard Kasesela wameendelea kutatua kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi. Ziara hizi zimekuwa na mafanikio makubwa Kwa wanainchi, pia imekuwa ikileta changamoto Kwa watumishi wa serikali ambao hawawatendei haki wanainchi. 
Mkuu wa MKoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza mbele ya Wananchi wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ikiwemo migogoro ya Ardhi,Pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akimsikiliza mmoja wa Wananchi alipokuwa akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa Mh Ally Hapi
Ziara ya mkuu wa mkoa akishirikiana kwa karibu na Mkuu Wa Wilaya Iringa Mh Richard Kasesela wameendelea kutatua kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi. Ziara hizi zimekuwa na mafanikio makubwa Kwa wanainchi, pia imekuwa ikileta changamoto Kwa watumishi wa serikali ambao hawawatendei haki wanainchi

DC CHEMBA AZINDUA USAJILI NA UTOAJI VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO

0
0

Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewaasa wananchi wa Chemba kuacha tabia ya kupuuza wito wa Viongozi wa Serikali  na taarifa mbalimbali zinazowahamasisha juu ya maendeleo kwani zoezi la usajili  na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ni kwa manufaa ya kwao.

Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa akizindua zoezi la usajili na utoaji  wa vyeti vya kuzaliwa vya watoto waliochini ya miaka mitano(5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika  tarehe 19/3/2019 katika viwanja vya Godown.

Odunga  alisema "Ifikie mahali suala la hiari litoke na iwe lazima kwani vyeti vya kuzaliwa kwa watoto ni muhimu sana katika maisha yao ya kila siku,kwani  vyeti  vya kuzaliwa vinatumika kwenye uandikishaji kuanzia darasa la kwanza na  Chuo Kikuu kwenye kuchukua mikopo kwa wanafunzi,tumieni  fursa hiyo kwa kuwa awamu ya kwanza ni bure"

Ningependa zoezi hili Watendaji na Wenyeviti waweze kushirikiana nao bega kwa bega  katika kutoa taarifa hasa kwa wale ambao hawajaandikisha watoto wao na kwa wale wanaogoma hatua kali zichukuliwe,pia nawapongeza wakinamama kwa kuweza kuitika wito wa kuwaandikisha watoto wenu kupata vyeti lakini kumbukeni kasi inahitajika zaidi .

Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba  amesema katika zoezi hilo lilianza na semina kwa Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba iliyofanyika tarehe 7/3/2019 mpaka tarehe 9/3/2019 na Wahudumu wa afya na watendaji walipata semina hiyo kuanzia tarehe 11/3/2019 hadi 13/3/2019

Aidha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti lilianza rasmi tarehe 15/3/2019 na  kuisha tarehe 28/3/2019 na mpaka leo watoto waliosajiliwa taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo wa taarifa kwa njia ya simu .

Vilevile Mratibu wa zoezi hilo kwa wilaya ya Chemba Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya Bi.Euphrezia Anthony amesema zoezi linaenda vizuri pamoja ya kuwa  changamoto hazikosekani.
Ameeleza kuwa Changamoto  wanazokumbana nazo kwenye zoezi hilo ni pamoja na baadhi ya kata kukosekana kwa mtandao,upungufu wa magari 2pamoja na ugeni wa simu za kisasa kwa watendaji na wahudumu wa afya lakini wanajitahidi kuzikabili kwa kuongeza timu ya usajili kwa njia ya simu na kuongeza gari la pili ili kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akikabidhi cheti kwa mmoja wa akina mama aliyeshiriki hafla ya uzinduzi wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliochini ya miaka mitano (5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika Machi 19,2019 katika viwanja vya Godown wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba akifafanua jambo kabla ya uzinduzi wa tukio hilo kufanyika . 
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza mbele ya baadhi ya Wananchi alipokuwa akizindua zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliochini ya miaka mitano (5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika Machi 19,2019 katika viwanja vya Godown wilayani humo.


Waganga wa kienyeji Kufyagiwa Sumbawanga Baada ya Mauaji ya Watoto Wawili

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP Mathias Nyangi kuhakikisha anafanya msako wa waganga wa kienyeji katika mkoa na kuwakamata wale wote wanaofanya uganga wa kienyeji bila ya kuwa na leseni halali za kuwaruhusu kufanya shughuli hizo.

Ametoa agizo hilo baada ya kusikiliza vilio vya wananchi wakati wa mkutano ulifanyika mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite, mjini Sumbawanga, wananchi waliokuwa wakiomboleza vifo vya watoto wawili na mmoja kubaki mahututi katika hospitali ya rufaa ya mkoa baada ya mganga wa kienyeji kuwateka na kuwaficha katika gari lake chakavu tangu watoto hao kupotea tarehe 21.3.2019 na wawili kupatikana wakiwa wamefariki tarehe 23.3.2019 baada ya mmoja aliyepona kutoroka na kuwajulisha wananchi kilichotokea.

Amesema kuwa msako huo wa waganga wa kienyeji ufanyike katika wilaya zote tatu za mkoa ili kuwahakikishia wananchi amani na utulivu ambayo imekuwepo kwa miaka yote na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha wanawafagia waganga hao wanaonyesha dalili za kuvuruga utulivu uliopo katika mkoa.

“RPC fanya Operesheni kali ya waganga wa Kienyeji ndani ya Mkoa huu, wale ambao wana leseni tutajua hukohuko kwamba huyu ana leseni n ani halai au siyo halali na kama sio halali basi huyo ni halali yako, na kama kuna mganga wa kienyeji asiye na leseni, huyo ndio kabisa halali yako zaidi, kuanzia sasa hivi bonde la ziwa Rukwa kule Nkasi, Kalambo, Sumbawanga yenyewe hapa kote, opresheni ipite ya kamatakamata waganga wa kienyeji, tumechoka,” Alisisitiza.

Wakati wakitoa malalamiko yao kwa mkuu huyo wa mkoa, wananchi hao walisema kuwa vifo vya watoto hao vinahusishwa na Imani za kishirikina ambapo kumekuwa na wimbi la vijana wanaoonekana wakila, wakinywa na kuvaa vizuri bila ya kujulikana shughuli zao maalum wanazofanya jambo mbalo limekuwa likiwaumiza kichwa wananchi hao na kukosa majibu.

Mmoja wa wananchi hao Debora Maenge alisema “ Nasikitika kwa tukio hili lililotokea mtaa wa Vuta, huyu mtu tunaishi nae jirani sana, tunajua ni mtu mwema, kumbe ni mtu ambae sio mwema na hafai kabisa katika jamii, cha kushanga alikuwa na vibali ambavyo alikuwa akijitambulisha kuwa yeye ni mganga wa jadi, vibali hivi vinatolewa serikalini, Je serikali yetu mtaendelea kutoa vibali hivi ili watu waendelee kuuawa kiasi hiki? serikali angalieni mnapotoa vibali je ni waganga Kweli?” Aliuliza.

Mh. Wangabo alitembelea eneo la nyumba ya mganga huyo wa kienyeji ambayo gari alilowafichia watoto ilikuwamo na kukuta nyumba hiyo ikiwa imevunjwa na gari la mganga huyo kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.

Watuhumiwa James Kapyela (52) pamoja na mtoto wake Michael Martin (14) wa tukio hilo la mauaji ya watoto Nicolous Mwambage (7) pamoja na Emanuel Juma (4) hivi sasa wanashikiliwa na polisi huku uchunguzi wa awali ukionyesha watoto hao walifariki kwa kukosa hewa baada ya kufungiwa ndani ya gari chakavu aina ya Chaser Saloon iliyokuwa haitumiki na vioo vya gari hiyo kufungwa. 
 Eneo la Nyumba ya mtuhumiwa ambaye ni Mganga wa Kienyeji wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite mjini Sumbawanga baada ya nyumba hiyo kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kubaini kuwa mganga huyo amesababisha vifo vya watoto wawili na mmoja kuwa mahututi. 
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Vuta Sangu Sokoni juu ya tukio la kupotea kwa watoto watatu na hatimae kupatikana wawili wakiwa wamefariki na mmoja kuwa mahututi akiendelea na matibabu.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akionyesha eneo katika nyumba iliyokuwa haijamalizika ambapo maiti za watoto hao zilipatikana baada ya kutupwa na mtuhumiwa James Kapyela ambae ni mganga wa kienyeji. 
  Diwani wa Kata ya Kizwite ambae pia ni mchungaji Felician Mavazi (alipiga magoti) akiomba muda mfupi kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Mh. Joachim Wangabo kuongea na wananchi wa mtaa huo wa Vuta kata ya Kizwite juu ya tukio la mauaji ya watoto wawili. 
-Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Mh. Joachim Wangabo alipokuwa akiongea na wananchi wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite Sumbawanga mjini. 

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa pole kwa wazazi waliofiwa na watoto wao alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa mara tu baada ya kupata taarifa ya vifo vya watoto wawili na mmoja kuwa mahututi baada ya kupatikana tangu kupotea kwao tarehe 21.3.2019.

Watanzania 52 wachomoza programu ya wajasiriamali TEF

0
0
Na Ripota Wetu -ABUJA, NIGERIA

WATANZANIA 52 ni miongoni mwa waliofanikiwa kushinda katika programu ya wajariamali Afrika, inayoratibiwa na na Taasisi ya Tony Elumelu ya nchini Nigeria.

Kuchaguliwa kwao sasa kunawafanya kuwa miongozi mwa wajariamali 1,000 ambao watanufaika kwa kuwezeshwa zaidi ya Sh milioni 10 ili kuimarisha biashara zao na kuzalisha ajira kwa vijana hususani kwa nchi za Afrika.

Hatua hiyo inatokana na matokeo yaliyotanganzwa mwishoni mwa wiki na Taasisi ya Tony Elumelu (TEF) ambayo ni ya Kiafrika inayoongoza kutoa ushauri na kuwawezesha wajasiriamali kutoka Afrika.

Pamoja na hali hiyo pia ilitangaza wajasiriamali wa Afrika 3,050 kutoka nchi 54 za Afrika ambao wamejiunga kwenye mzunguko wa tano wa dola za Marekani milioni 100 katika programu ya Ujasiriamali wa TEF.

Matokeo hayo yalitangazwa jijini Abuja baada ya washauri wa maendeleo kuwasilisha mchakato wa uteuzi huo, ambapo kwa mwaka huu zaidi ya watu 216,000 waliwasilisha maombi ikiwa ni ongezeko ya watu 151,000 kutoka mwaka jana.

“Takribani maombi 90,000 yaliwasilishwa na wajasiriamali wanawake ikiwa ni ongezeko la asilimia 45, hii ni ishara ya mkakati wa Taasisi hiyo kufikia usawa wa jinisia. Wajasiriamali waliochaguliwa kila moja atapokea dola za Marekani 5,000 za mitaji ambayo haitarudishwa, upatikanaji wa washauri na wiki 12 ya mafunzo ya biashara yanayohusisha moja kwa moja mahitaji ya wajasiriamali kutoka Afrika.

“Julai 26 – 27, 2019, watakusanyika kwenye Mkutano wa Biashara wa TEF, mkusanyiko mkubwa wa kila mwaka wa wajasiriamali wa Kiafrika na mazingira ya ujasiriamali katika Bara hili la Afrika

“Kila mwaka, tunakabiliwa na kazi ngumu – kuchagua wajasiriamali 1,000 kutoka maelfu ya waliyoomba. Wajasiriamali wetu wananjaa ya kuchochoea mabadiliko. Lazima tushirikiana kuwawezesha ili kuchochea mabadiliko tunayotaka katika bara letu,” alisema muasisi wa TEF, Tony Elumelu.

Katika hotuba yake, Mke wa Rais wa Nigeria, Aisha Buhari, alipongeza jitihada za programu na kuwasisitizia wajasiriamali waliochaguliwa kuchangia maandeleo ya bara la Afrika.

“Nina imani hawa wajasiriamali wa Tony Elumelu watakuwa na msaada mkubwa sio tu Nigeria lakini bara nzima,” alisema.

Akizungumza kuhusu mchakato huo Ofisa Mtendaji Mkuu ajaye Ifeyinwa Ugochukwu, alisema “Programu ya Ujasiriamali wa Taasisi ya Tony Elumelu, imewawezesha kwa mafanikio wajasiriamali 7,520 katika miaka yake mitano ya kwanza kati ya miaka 10 ya programu. Ikitimiza miaka mitano kati ya miaka 10 ya programu, uteuzi wa mwaka huu umehusisha wajasiriamali 2,050 wakisaidiwa na washirika wa Taasisi.

“Mwaka jana, tulizindua TEFConnect - jukwaa la mitandao ya digital kwa wajasiriamali wa Kiafrika na kufunguliwa kwa wote - kuendeleza demokrasia ufikiaji wa fursa kwa maelfu ya wajasiriamali ambao hawawezi kufaidika moja kwa moja na Programu ya Wajasiriamali. Hii inaonyesha zaidi dhamira yetu ya kuwawezesha wajasiriamali wetu na imani yetu kuwa ujasiriamali una ufunguo wa kufuta uwezo wa kweli wa bara la Afrika,” alisema. 
 
Alisema washirika wa taasisi hiyo kwa sasa wanazidi kuongezeka ni Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), United Nations Development Programme (UNDP), Serikali ya Benin (Seme City), Anambra State Government, Indorama, Serikali ya Botswana na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB).
Mwanzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu, Tony Elumelu (Kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na na mke wa Rais wa Nigeria, Aisha Buhari (katikati) na kulia ni Mwasisi Msaidizi Dk. Awele Elumelu. Hafla ya kutangaza majina ya wajariamali 1,000 wa Afrika wataowezeshwa na Taasisi ya TEF ilifanyika jana jijini Abuja nchini Nigeria
Kutokana kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tony Elumelu anayeingia, Ifeyinwa Ugochukwu, Mkurugenzi anayemaliza muda wake Parminder Vir, Balozi WA Israel nchini Nigeria, Shimon Ben-Shoshan, Mwasisi wa Taasisi ya Tony Elumelu, Mke wa Rais wa Nigeria Aisha Buhari, Mwasisi Msaidizi wa TEF, Dk. Awele Elumelu, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa kwa majina ya wajasiriamali 1,000 watakaonufaika kwa kuwezeshwa na taasisi hiyo.

WAZIRI LUGOLA ATAKA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU IDHIBITIWE, KUFUNGUA MKUTANO MKUBWA WA WADAU WA KUZUIA BIASHARA HIYO, MJINI UNGUJA, ZANZIBAR KESHO

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Zanzibar. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameitaka Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu nchini, iongeze kasi ya kupambana na biashara hiyo ili iweze kudhibitiwa kwa kuwa inaichafua nchi. 

Waziri Lugola, ambaye kesho anatarajia kufungua mkutano mkubwa wa mafunzo kwa watekelezaji wa sheria ya kuzuia biashara hiyo haramu, katika hoteli ya Ngalawa, mjini Unguja, Zanzibar, alisema wakati akijiandaa kufungua mafunzo hayo, lakini wahusika waweke mikakati thabiti ya kuidhibiti biashara hiyo. 

Mafunzo hayo ambayo ni ya siku tano, yatatolewa kwa wadau wanaotekeleza sheria ya kuzuia na kupambana na Biashara hiyo, Maafisa Polisi, Uhamiaji, waendesha mashtaka, Mahakimu, Maafisa Ustawi Jamii na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO's) yaliyopo Zanzibar. 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, Waziri Lugola alisema Mkutano huo ni muhimu kwa wadau hao kupata mafunzo ya kukabiliana na mapambano ya biashara hiyo haramu ambayo Wizara yake itaendelea kuidhibiti. 

“Nimealikwa kufungua mkutano huo, baada ya mafunzo hayo ya kitaalamu ambayo nimeambiwa yatakuwa ya siku tano, naamini maafisa watakaopewa mafunzo hayo kutoka Wizara yangu na maafisa wengine wa Serikali kutoka sehemu mbalimbali nchini, pamoja na NGO’s za hapa Zanzibar watakuwa wamepikwa na kuiva na hatimaye watatusaidia katika kutekeleza sheria ya kuzuia biashara hii haramu ya usafirishaji wa binadamu,” alisema Lugola. 

Kwa upande wake, Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo Haramu kutoka Wizara hiyo, Separatus Fella, alisema zaidi ya washiriki 80 watapewa mafunzo hayo na anamatarajio makubwa elimu watakayopewa itazaa matunda. 

Fella alisema washiriki watapewa mafunzo mbalimbali katika semina hiyo itakayofanyika Kesho Machi 25, 2019, ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa zikiwemo, washiriki kujua kutofautisha makosa ya biashara haramu ya usafirishaji binadamu na mengine, na namna ya kupeleleza na kuendesha mashtaka. 

“Pia washiriki watajifunza namna ya kuwalinda na kuwasaidia wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu, namna ya kuhoji watuhumiwa na mashahidi kwenye kesi za biashara haramu ya usafirishaji Binadamu,” alisema Fella. 

Aidha, katika ufunguzi wa mafunzo hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Lugola, Fella alisema pia maafisa mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar watashiriki kwenye hafla ya ufunguzi huo. 

Aliongeza kuwa, mafunzo hayo ni kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Marekani linalojihusisha na Masuala ya Utafiti (RTI).

WAVAMIZI SHAMBA LA MITI BIHARAMULO WAPEWA MIEZI 3

0
0
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati)  akizungumza   na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe.  Mtemi Simeoni (kushoto)   wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa  ukubwa  wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita., Kulia ni Meneja wa shamba hilo, Edward Nyondo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Chato,  Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto)  alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo  kwa  ukubwa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine ni watumishi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  akizungumza na  wananchi pamoja na watumishi wa shamba la miti la Biharamulo ambalo mara baada ya kukamilika kwa kupandwa miti katika eneo lote litakuwa ndio  shamba la pili kwa ukubwa kati ya mashamba  20 yanayomilikiwa na Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania lililopo wilayani Chato mkoani Kagera.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipanda mti wakati alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa  hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
 Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni akipanda mti wakati alipoambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa  hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya na watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Baadhi ya watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika shamaba hilo hukuakiwasisitizan umuhimu wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wanaoishi karibu na shamba hilo. 
(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Ametoa muda huo ili wananchi  waliolima   mazao mbalimbali yakiwemo  mahindi na pamba  waweze kuvuna mazao yao  kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.

Mhe.Kanyasu  ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya   kutembelea shamba la miti Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.

Amesema Oparesheni hiyo haitasubiri taarifa ya Wizara tano inayoendelea kufanyiwa kazi kwa kuwa eneo hilo halihusiani na vile vijiji 366  vilivyokutwa ndani ya Hifadhi.

Amesema  haiwezekani wananchi waliovamia eneo hilo waendelee kuachwa kwa kisingizio cha Kauli ya Rais aliyoitoa Januari 15 mwaka huu kuhusiana na vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya maeneo ya Hifadhi.

Amebainisha kuwa wananchi waliovamia eneo hilo wameitafsiri visivyo Kauli hiyo na kuongeza kuwa baada tu ya tamko la Mhe. Rais , baadhi ya wananchi hata wale waliokuwa wakiishi  katika maeneo mengine nje ya hifadhi waliendelea  kuvamia na kuanza kujimilikishia  maeneo makubwa  wakidai kuhalalishwa na tamko la Rais.

Amefafanua kuwa taarifa inayoendelea kufanyiwa kazi  na timu ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Wizara tano imebainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya vijiji 700 vimekutwa ndani ya Hifadhi badala 366 vilivyoripotiwa awali.

Kufuatia hali hiyo amesema baadhi ya wavamizi wa Hifadhi katika maeneo mbalimbali wataendelea kuondolewa bila kusubili kukamilika kwa zoezi linaloendelea kwa kuwa walieendelea kuvamia maeneo ya Hifadhi kwa kisingizio cha tamko la Rais huku maeneo hayo yakizidi kuharibiwa kwa miti kukatwa na shughuli nyingi za kibinadamu

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kutenga Bajeti ya kugharamia operesheni ya kuwaondoa  wavamizi ndani ya Shamba hilo.

Ameitaka TFS kuendesha oparesheni za mara kwa mara ili wavamizi hao wajue Serikali ipo kazini kulinda rasilimali za Taifa muda wote.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Chato,  Mtemi Simeoni akizungumza katika ziara hiyo  alisema kuwa  baadhi ya wananchi kutoka nje ya wilaya hiyo wamekua wakivamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba hilo, suala ambalo ni kinyume cha sheria.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa wananchi katika maenro hayo wana mahitaji makubwa ardhi na kuiomba Wizara iangalie  namna ya kuwasaidia  hekari 5000 ili wapate maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba hilo Bw. Thadeus Shirima  amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa hadi sasa zaidi ya hekari 900 zimepandwa miti licha ya Shamba hilo  kukabiliwa  na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendea kazi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki azungumza na Watumishi wa Wizara

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mahsariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Ukumbi wa Mikutano la Informatics lililopo Chuo Kikuu cha Dodoma kwa ajili ya kukutana kwa mara ya kwanza na Watumishi wa Wizara tarehe 23 Machi 2019
Mhe. Prof. Kabudi akizungumza na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) alipokutana nao kwa mara ya kwanza  baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nafasi hiyo tarehe 3 Machi 2019. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Prof. Kabudi aliwataka Watumishi wa Wizara kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu miongozo na maelekezo mbalimbali pamoja na kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa kushirikiana na  kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi ambaye haonekani pichani alipozungumza nao

Sehemu nyingine ya Watumishi wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani)

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye mkutano wao na Mhe. Waziri

Mkutano ukiendelea huku Watumishi wa Wizara wakifuatilia

Sehemu nyingine ya Watumishi

Mhe. Prof. Kabudi alitumia fursa ya mkutano wake na Watumishi wa Wizara kugawa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 kwa Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara na kuwaagiza kuitekeleza kwani ni miongoni mwa miongozo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Pichani Mhe. Waziri akimkabidhi Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza Ilani hiyo
Mhe. Waziri akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Ilani ya Chama cha Mapinduzi
Mhe. Prof. Kabudi akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Joachim Otaru
Mhe. Prof. Kabudi akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Bw. Wilbroad Kayombo
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Watumishi na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri
Mhe. Waziri (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa meza kuu. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizzi wa Rasilimali Watu, Bibi Savera Kazaura na kulia ni Bw. Hassan Mnondwa, Mwenyekiti wa TUGHE Wizarani .

Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo

WANAFUNZI WA NYANGAO HIGH SCHOOL WAWEKA HISTORIA UJENZI WA SGR, WAMPA TANO JPM KWA KUJENGA RELI HIYO

EAC TECHNICAL WORKING GROUP MEETING ON PILOT TESTING OF HARMONIZED PESTICIDES GUIDELINES FOR EFFICACY TRIALS

0
0
cid:image003.jpg@01D4D5C8.6F6284D0

EAC Secretariat
 The EAC Deputy Secretary General in-charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo has called upon pest control product companies to take advantage of EAC harmonized system for testing and registration of pesticides.

The 38th Extra-Ordinary Council of Ministers held on 30th January, 2019 approved the EAC pesticides management guidelines on efficacy trials, residue trials and registration requirements.  The Council further directed Partner States to domesticate them by 30th May 2020. 

The EAC harmonized system comes with a number of benefits that will translate to reduced time and costs associated with testing and registration of pest control products across EAC Partner States.  It is expected that farmers in the region will have increased access to quality, safe and affordable pesticides.

Hon. Bazivamo informed the companies that involvement of the Private Sector is pivotal for successful implementation of the guidelines. He further said that EAC appreciates and recognizes the contribution that the private sector makes in the EAC integration agenda.

Hon. Bazivamo made the remarks during the Technical Working Group meeting on pilot testing of EAC harmonized pesticides registration guidelines held at the Mt. Meru Hotel in Arusha, Tanzania from 18th to 21st March, 2019. 

The meeting was convened by the EAC Secretariat with support from USAID Kenya & East Africa, the United States Department of Agriculture and Africa Lead II. The main objective of the meeting was to finalize roadmap and discuss modalities of pilot testing of EAC harmonized guidelines for testing and registration of pesticides.

The meeting was attended by members of the EAC Technical Working Group on Pesticides harmonization, Agriculture Desk officers from Ministries responsible for EAC Affairs, pest control product companies (Bayer, Syngenta, AgBiTech,  REAL IPM, Corteva, Triachem, Provivi and Arysta Life Science), CropLife Africa Middle East, the African Agricultural Technology Foundation,  Africa Lead, the Alliance for a Green Revolution and the EAC Secretariat.

Addressing the meeting, Hon. Christophe Bazivamo, mentioned that area of agrochemicals and pest control products is a key priority in the EAC agricultural sector. Article 108 of the EAC Treaty focuses on the need for EAC Partner States to adopt common mechanism to ensure safety, efficacy and potency of agricultural inputs including chemicals, drugs and vaccines.

Hon. Bazivamo informed the meeting that 11th Sectoral Council on Agriculture and Food Security held in June 2018 adopted the EAC pesticides management guidelines and urged Partner States to pilot implementation of the pesticide efficacy guidelines for the first three years in order to pave way for operationalization of full mutual recognition.

The Sectoral Council also urged Partner States to prioritize joint testing of pesticides and to share information on products that can control the Fall Army Worm which has posed a major threat to food security in the region. 

Since 2016 the Fall Army Worm has been spreading across much of sub-Saharan Africa. Currently, over 45 countries out of 55 countries in Sub-Saharan Africa have been affected.  It is estimated that Fall Army Worm has the potential to cause maize yield losses in the range of US$ 2 to 6 billion in Africa’s maize producing countries. 

During the meeting, representatives of Bayer, Syngenta, AgBiTech,  REAL IPM, Corteva, Provivi and Arysta Life Science made presentations about products developed by their respective companies to control the Fall Army Worm. The presentations also outlined the efficacy and safety of the products and EAC Partner States where the companies intend to conduct pilot trials of their products. 




Timu zilizofuzu AFCON 2019 hizi hapa .

KISHINDO TANZANIA...TAIFA STARS SAFARI YA MISRI IMETIMIA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAGOLI matatu ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda ' The Cranes' yametosha kuwapelekeaWatanzania nchini Misri kwenye michuano ya AFCON mwaka 2019.

Mbele ya mashabiki  zaidi ya 60,000 ambao walikuwa na jukumu la kuhakikisha wanaishangalia Taifa Stars yalikuwa chachu tosha kwa wachezaji ambapo waliokuwa wanacheza kwa uwezo wa hali ya juu.

Taifa Stars ilipata goli la kwanza kupitia kwa Mshambuliaji wake Simon Msuva ambalo liliduma hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza, hadi wanakwenda mapumziko Taifa Stars ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0 dhidi ya The Crains.

Wakati wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakicheza kwa jihadi huku wakitambua kaulimbiu inayosema ' Ni zamu yetu', kipindi cha pili walirudi uwanjani wakiwa na nguvu zaidi na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara golini kwa 'The Cranes'.

Mashambulizi ya Taifa Stars yalisababisha kupatikana kwa penalti kwa upande wa Tanzania ambapo mchezaji aliyekuonesha umahiri wa hali ya juu kumiliki mpira Erasto Nyoni aliifunga goli la pili.

Kasi ya Taifa Stars ilisababisha kupatikana kwa goli la tatu kupitia kwa mchezaji Agrey Morris.

Hata hivyo wachezaji wa Uganda walionekana kusuka mipango ya kutafuta bao lakini Taifa Stars waliziba njia zote na kuharibu mipango na kuifanya kushindwa kupata goli.

Watanzani waliokuwa uwanjani wakiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walikuwa na furaha isiyo kifani huku wachezaji wa Taifa Stars wakionesha kuwa kichwani wanaiwaza AFCON na sio kitu tofauti na hicho.

Magoli ya Taifa Stars yalisababisha mashabiki kushindwa kukaa kwenye viti ambapo karibu muda wote wa mchezo walikuwa wakishangilia.

Hata hivyo wakati Taifa Stars na Uganda wakiendelea kuchezaji,mashabiki walitangaziwa kuwa mechi kati ya Lesotho na Cape Verde yalikuwa ni sare .Matokeo hayo yameipeleka Taifa Stars na Uganda Misri hasa kwa kuzingatia Uganda walishafuzu kwa kuwa na alama 13 kabla ya mchezo wa leo.


Hata hivyo mashabiki wa Uganda waliokuwa uwanjani hapo walionekana nao wakishangilia ushindi wa Taifa Stars.Kabla ya kuanza kwa mechi ya leo iliyofanyika Uwanja Mkuu wa Taifa mashabiki wa Uganda walikuwa na matumaini ya kushinda.



CHADEMA YAIPONGEZA TAIFA STARS BAADA YA KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFCON 2019

0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatoa pongezi kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu, Taifa Stars, pamoja na makocha wao wakiongozwa na Ndugu Emmanuel Amunike, kwa ushindi mnono wa magoli 3 dhidi ya Uganda katika mechi iliyochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo ambayo sasa yanamaanisha kuwa Tanzania imefuzu na itashiriki Mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AfCON 2019) huko Misri, Taifa Stars imetutoa Watanzania wote kimasomaso na kumaliza kiu na hamu ya muda mrefu ya wapenzi wa soka, baada ya kusubiri kwa miaka 39 kupata nafasi hii tena baada ya kushiriki mashindano hayo mwaka 1980 huko Nigeria.

Ni matumaini yetu kuwa Wachezaji wa Taifa Stars na makocha wao watazichukulia pongezi hizi pamoja na furaha kubwa isiyo kifani waliyonayo Watanzania kama chachu kubwa ya hamasa itakayowapatia ari na mori wa kushindana na timu za mataifa mengine huko Misri baadae mwaka huu na kurejea na matokeo mazuri yatakayowatangaza na kuwauza wao kimataifa na kuinufaisha nchi yetu Tanzania kwa ujumla.

Hongera Taifa Stars, hongera Watanzania. Kila la heri Taifa Stars AfCON 2019.

Imetolewa leo Jumapili, Machi 24, 2019 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema

KAULI YA RAIS MAGUFULI BAADA YA TAIFA STARS KUIFUNGA TIMU YA TAIFA YA UGANDA...RIDHIWANI ATUMA MAOMBI MAALUM

0
0
 Na Said Mwishehe,Globu ua jamii

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amemetuma maombi maalumu kwa Rais Dk.John Magufuli baada ya kumshauri aseme chochote kutokana na ushindi ambao wa mabao 3-0 ambao timu ya Tanzania ' Taifa Stars'  dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.

Wakati Ridhiwani akimuomba Rais Magufuli kusema chochote,akizungumza kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mpira kumalizika Rais amesema ushindi wa Taifa Stars ni heshima kwa Tanzania na kwamba leo ameona mpira.

"Kwa ushindi ambao wameupata vijana wetu wa timu ya Taifa kuna kila sababu mtani wangu Rais Dk.Magufuli kusema chochote ili wapiga kura roho zetu zipoe.Ni ushindi mkubwa na tumeandika histori na kubwa zaidi heshima kwa nchi yetu," amesema Ridhiwani.

Hata hivyo Rais Magufuli amezungumzia mchezo huo na kubwa zaidi ametoa pongezi kwa wachezaji kwa mpira ambao wameuonesha na hakika amefurahi sana kwani mpira aliokuwa akitamani kuuona leo ameuona.

"Ni heshima kubwa kwa nchi yetu,hongereni wachezaji,hongereni wote ambao mmefanikisha ushindi .Kwanu nimefurahi sana na leo nilisema sitaenda uwanjani ili niuone hapa hapa Ikulu.

"Ni heshima kubwa kwa nchi yetu," amesema Rais Magufuli huku akieleza matokeo ya Lesotho na Cape Verde nayo yamemfurahisha kwani yameivusha Tanzania kwenda Misri,"amesema Rais Magufuli.

RAIS WA MSUMBIJI AISHUKURU TANZANIA KWA MISAADA YA DAWA NA CHAKULA

0
0




Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi na Wananchi wake wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Wananchi wa Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kutoa misaada ya Madawa, Magodoro na vyakula kwa watu wa Msumbiji walioathirika na kimbunga.

Kimbunga kilichopita katikati ya Jamhuri ya Msumbiji kilicho anza tarehe 14 Machi 2019, kimesababisha madhara makubwa katika mji wa Beira ambao ni wa tatu kwa ukubwa na wa pili kibiashara baada ya Maputo.

Upepo uliambatana na mvua uling'oa miti, mapaa ya nyumba za mabati na vigae na kuvunja madirisha ya vioo bila huruma katika mji huo.

Kufuatia janga hilo ambalo limezikumba pia nchi za Malawi na Zimbabwe, Rais Magufuli alitangaza kutoa msaada wa haraka ambapo ndege kubwa za JWTZ zilipeleka misaada hiyo kama inavyoonekana katika picha.

Mjini wa Beira na wilaya za jirani ziko kwenye uwanda wa tambarale. Mji huo pia una mito miwili mikubwa inayoingia katika bahari ya Hindi na hiyo ndiyo sababu ya mara kwa mara unakabiliwa na mafuriko.

Tanzania inaomba Mungu mvua zipungue kwa majirani hao ili waweze kuidhibiti hali hii ya mafuriko inayoendelea sasa baada ya Kimbunga kupita.

Mji wa Beira umeharibika vibaya ambapo asilimia 97 ya majengo, miundombinu, na mali za wananchi zimeathiriwa na kimbunga hicho.

Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Rajab Luhwavi ambaye alipokea shukrani hizo kwa niaba ya Serikali ameihakikishia Msumbiji kuwa, Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo kwa hali na mali.

Aidha, Mhe. Balozi ametoa pongezi kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wadau wengine kwa kufanikisha msaada huo.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma, Tarehe 24 Machi 2019

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images