Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TUMKUMBUKE SHENAZI SALUM.

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Ni hulka ya sisi wanaadamu kusahau mambo mema yaliyofanywa na mazurikumbushana kwa yale mazuri yaliyojiri katika sakafu hii ya Ulimwengu.

Yawezakana kuna baadhi ya watu wameyasahau majina ya Shenazi Salum, aliyekuwa muigizaji na mchezaji wa muziki wa kujitegemea.

Alikuwa kungwi anayefundisha akina mama jinsi ya kuishi na mume hususan kwenye sherehe za kumuaga bi harusi mtarajiwa ‘Kitchen Paty’.
Wasifu wa mwanamama huyo unaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1972 jijini Dar es Salaam.

Shenazi alijulikana mno na baadhi ya watu kufuatia 'vimbwanga' vyake alivyokuwa akiviporomosha katika shughuli zake hizo.Alikuwa akiingia ukumbini, watu walikuwa wakizizima kwa nderemo na vifijo, wakimshangilia yeye akipita akijimwayamwaya huku maungo yake yaliyokuwa yamejengeka vyema, yakipishana.

Lakini kwa mapenzi yake mungu, Shenazi alifariki dunia Septemba 08, 2007 katika ajali ya basi iliyotokea kijiji cha Majenje, Mbarali, mkoani Mbeya wakati huo.Alikuwa kwenye basi la SABCO aina ya Scania, T443 APF ambalo liligongana na lori pamoja na magari mawili yanayomilikiwa na Halmashauri ya Mbarali.

Ilielezwa kuwa baadhi ya abiria walikuwa wakimshinikiza dereva wa basi hilo kuongeza kasi ya mwendo, ili wawahi ufunguzi wa Uwanja mpya wa Taifa, ambako kulikuwa na pambano kati ya Taifa Stars na Msumbiji.

Kwa mujibu wa mdogo wa mwanamuziki huyo aitwaye Hanifa Salum, Shenazi alifariki, muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo, iliyohusisha magari matatu na kuua abiria wengine 27.

Aliseme kuwa dada yake Shenazi, alikuwa akirejea nyumbani kwake Dar es Salaam, akitokea katika mji wa Tunduma, alikokuwa akifanya shughuli zake za muziki.“Alituaga kwamba anakwenda Mbeya kufanya ‘shoo’, hatukujua kama ndiyo kifo kilikuwa kinamwita, lakini ndiyo hivyo Mungu kamchukua…”…. alisema Hanifa huku akitokwa na machozi.

Shenazi kwa mara ya mwisho alishiriki katika filamu ya "Kitchen Party", akiwa kama kungwi pamoja na rafiki yake wa karibu aiitwaye Mwajuma Thabiti maarufu kama "Rose Jimama".

Filamu hiyo inaonyesha namna ya kuishi vizuri na mume na mambo mengine mengi tu yenye faida kwa walengwa hususani akina mama.Shenazi alikuwa Malkia wa kunengua miondoko ya Taarab na Mduara nchini, Shenazi

Alikuwa kila aingiapo kwenye ukumbi wowote, hakuwa na soni kujimwagamwaga huku akitikisa maungo yake yaliliyokuwa yamejengeka kike.Rafiki wa Shenazi ambaye naye ni mnenguaji maarufu, Mwajuma Thabit ‘Rose Jimama’, alisema kuwa marehemu alikwenda Mbeya na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Tuki.

“Nilipata taarifa kama Shenazi amepata ajali, nikapiga simu yake, ikapokelewa na polisi mmoja huko Mbeya. Nikamuomba kuongea na Shenazi, akanijibu, unataka kuongea na maiti? Nilichanganyikiwa, yule polisi aliniambia rafiki yangu Shenazi amekufa, Tuki hali yake ni mbaya, nilidhani utani, lakini yote ni mipango ya Mungu…” alisema Rose kwa uchungu mkubwa.

Habari zaidi zilisema kuwa rafiki huyo wa Shenazi, Tuki, alivunjika miguu yote na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala, Mbarali.

Mbali na kunengua, malkia Shenazi atakumbukwa kama kungwi maarufu, aliyekuwa akiwafunda watu kabla ya ndoa pia uigizaji wake.

Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.

WATENDAJI MAMLAKA ZA MAJI WATAKIWA KUWAJIBIKA ZAIDI

$
0
0
 Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akiongea na watendaji wa wizara yake wakati wa mkutano wa Mapitio ya Sekta ya Maji (JWSR), ambao pia ulikua ni moja ya matukio ya Wiki ya Maji kwa mwaka 2019, uliokutanisha wadau wa sekta ya maji kwa pamoja.


Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema watendaji wa mamlaka za maji watakaoshindwa kulipa tozo mbalimbali kwa wakati watawajibishwa kwa uzembe katika kazi. 

Profesa Mkumbo amesema hayo wakati akihitisha Wiki ya maji kwa mwaka 2019 na Mkutano wa Mapitio ya Sekta ya Maji (Joint Water Sector Review) jijini Dodoma. Tozo zinatakiwa kulipwa katika bodi za mabonde mbalimbali ambako mamlaka zina vyanzo vya maji na tozo za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). 

Hata hivyo, ameainisha kuwa endapo tozo hizo ni kubwa watendaji wa mamlaka za maji wanatakiwa kusema na kuwataka kulipa tozo kwa wakati kwani ni moja kati ya vigezo vya kupima utendaji kazi katika mikataba iliyosainiwa kati ya Watendaji wa Mamlaka za maji na Wizara ya Maji mapema mwezi Machi, 2019 jijini Dodoma. 

Pamoja na hayo, Prof. Mkumbo amesema miongoni mwa mambo ambayo watendaji wa mamlaka za maji wanayotakiwa kuyapa uzito ni suala la upotevu wa maji (NRW). Amesema jambo hilo ni kero na linapoteza mapato, na pia huduma kwa wananchi inakua ya kusuasua katika baadhi ya maeneo kwasababu maji yanapotea. Eneo jingine la msisitizo ni suala la usafi wa mazingira ambapo mipango mizuri inatakiwa kuwekwa na mamlaka zote kwa kuzingatia mipango ya biashara. 

Prof. Mkumbo kupitia wiki ya maji amewapongeza Washirika wa maendeleo kwa ushirikiano mzuri na Serikali, pamoja na AZAKI ambazo zinapaza sauti kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu huduma ya maji kwa wananchi. Amesema yote wanayoshauri yanachukuliwa na kufanyiwa na Serikali kwasababu wananchi ndio wadau namba moja wa Serikali. 

Kaulimbiu ya wiki ya maji 2019 ilikuwa ni “Hakuna Atakayeachwa: Kuongeza Kasi ya Upatikanaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa Wote katika Dunia inayobadilika kitabia nchi” 

Mwaka 1993 Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira na Maendeleo lilipitisha Azimio rasmi la kuadhimisha Siku ya Maji Duniani kila mwaka ifikapo tarehe 22 Machi. 

Wizara ya Maji imekua ikiratibu na kuadhimisha siku hii muhimu kuanzia mwaka 1988. Haya yamefanyika kwa kuwashirikisha wananchi na wadau wa maji. Lengo kuu likiwa kuungana na Mataifa mengine Duniani katika kutathmini utekelezaji, mafanikio, changamoto na kuainisha mikakati ya kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira na kusimamia utunzaji wa rasilimali za maji. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 

23.03.2019

WATER HEALTH YAADHIMISHA SIKU YA MAJI KWA KUWATAKA WANAFUNZI KUWA MABALOZI BORA KATIKA SEKTA HIYO

$
0
0
IKIWA ni kilele cha maadhimisho ya siku ya maji duniani leo Machi 22 muanzilishi wa taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health)Diana Kato ametoa elimu ya maji safi na salama na matumizi yake katika shule tatu za jiji la Dar es salaam ambazo ni shule za msingi Mtambani, Tabata na Tabata Jica.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Kato amewataka wanafunzi huo kuwa mabalozi bora katika kutunza vyanzo vya maji bila kuvichafua wala kuruhusu watu wengine wavichafue vyanzo hivyo kwa namna yoyote ile.

Aidha amesema kuwa kampeni kuhusiana na sekta ya maji ni endelevu kwani umuhimu wake ni mkubwa sana na kueleza kuwa elimu zaidi inahitajika ili kukomesha tabia ya uharibifu wa mazingira unaochangia kuhatarisha sekta hiyo.

Katika maadhimisho hayo elimu ilitolewa kupitia mabango yanayoeleza umuhimu na faida za maji pamoja na kuulizwa maswali na walimu wao kuhusiana na sekta nzima ya maji.

Pia Kati amekabidhi vitabu kwa shule hizo vilivyotolewa na Nyambari Nyangwine Publishers ambavyo vitawasaidia katika kujifunza na kuongeza maarifa zaidi.
 Muanzilishi wa Taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health) Diana Kato akizungumza na wanafunzi wa shule ya shule za msingi Mtambani, Tabata na Tabata Jica wakati wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.

Mwalimu mkuu wa shule za msingi ya Tabata, Khamis Ngoda  akizungumza na wadau wa maji pamoja na wanafunzi wa shule za msingi Mtambani, Tabata na Tabata Jica wakati wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.
 Mmoja wa wafafuzi akitoa shukrani kwa uongozi wa Taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health) baada ya kupokea zawadi ya vitabu wakati wa wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.
  

Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye picha za pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya vitabu kutoka Taasisi ya maji isiyo ya kiserikali (Water Health)  wakati wa maadhimisho ya  maadhimisho ya siku ya maji duniani.

PROFESA KABUDI AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA WIZARA YAKE

$
0
0
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amewataka watumishi waliopo katika wizara hiyo kubadilika na kuboresha utendaji kazi na kutekeleza majukumu yao kwa weledi,kasi na uzalendo usiotiliwa mashaka sema wizara usiotiliwa mashaka kwa kuwa Wizara hiyo ndio kioo cha Taifa.

Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha watumishi wote wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki uliofanyika Dodoma kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuiongoza wizara hiyo,Profesa Kabudi amesema ilani ya chama cha mapinduzi imetoa maelekezo yanayopaswa kutekelezwa na wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia uchumi wa viwanda pamoja na diplomasia ya kiuchumi.

“Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imetoa mambo ambayo yanapaswa kutekelezwa na Wiazara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ambayo yako wazi kabisa ikiwa ni pamoja na kusimamia uchumi wa viwanda pamoja na diplomasia ya uchumi ambayo itaisaidia Tanzania kujenga uchumi imara utakaowezesha kutoa huduma za kijamii na kutoa ustawi kwa watanzania wote”

Ameongeza kuwa ili lengo hilo litimie ni lazima sasa watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kufanya kazi kitimu kwa kushirikiana na wizara nyingine kwa Mslahi mapana ya Taifa.

Amesema kuwa wizara hiyo ni nyeti kwa kuwa ndio sikio,jicho na msemaji wa nchi kimataifa hivyo watumishi hawana budi kujituma na kuongeza kasi na weledi ili kufikia malengoya wizara hiyo na matarajio ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Aidha Profesa Palamagamba John Kabudi mbali na kuwataka watumishi wa wizara hiyo kutekeleza masuala yaliyoahidiwa kupitia ilani ya chama cha mapinduzi,amewataka pia kuzingatia hotuba iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akilizindua Bunge 11, Novemba 20,2015.

Amesema amelazimika kukukutana na watumishi wa wizara hiyo kwa kuwa imekuwa na taswira ambayo haijafikia matarajio yanayotarajiwa na ili iweze kufikia malengo hayo ni budi kuzingatia maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na Hotuba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya uzinduzi wa Bunge la 11 kwa kuwa wizara hiyo italazimika kutoa mrejesho wa kile kilichotekelezwa kupitia maagizo hayo ya Ilani na Hotuba ya Rais.

Amewataka pia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wawe tayari kubadilika na kufanya kazi mahali popote kwa kuwa lengo la serikali ya awamu ya Tano na vipaumbele vyake inaweza kumuhitaji mtumishi yeyote wa uma kwenda kufanya kazi popote kulingana na mahitaji.“Ni imani yangu kuwa wtumishi wa wizara hii wamenielewa na sasa watatekeleza majukumu yao kwa kasi,weledi,uelewa na uaminifu usiotiliwa mashaka ili kufikia matarajio ya watanzania katika wizara hii”
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa wizara yake, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Faraji Kasidi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (wa pili kutoka kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu Bi. Severa Kazaura (wa kwanza kushoto) na wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi Wizarani (TUGHE) Bw. Hassan Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Pro. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Joachim Otaru. Tukio hilo limefanyiaka wakati Profesa Kabudi alipokutana na Kufanya Mkutano na Wafanyakazi wa Wizara yake ikiwa ni kwa mara ya kwanza tokea ameteuliwa na Rais wa Ja,huri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Katikati ni Katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt Faraji Kasidi Mnyepe akishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wizara yake pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mara baada ya kumaliza mkutano kati ya Profesa Palamagamba John Kabudi na Watumishi wote. 

MBUNGE RAZA AZINDUA KIKUNDI CHA KINAMAMA WA UWT JIMBO LA KIEMBESAMAKI CHA GREEN ROSE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Ibrahim Raza akizungumza na Kinamama wa Kikundi cha Green Rose mara baada ya kukizindua kikundi hicho kinachojishuhulisha na utengenezaji wa Mabatiki na Sabuni za aina mbalimbali katika hafla iliyofanyika Tawi la CCM kwa Mchina.
Mjumbe wa NEC Amini Salmin Amour akitoa nasaha zake kwa kinamama wa kikundi cha Green Rose kiliopo Jimbo la Kiembesamaki katika hafla ya uzinduzi wa kikundi hicho uliofanyika Tawi la CCM Mchina Mjini Unguja.
Wakinamama wa Kikundi cha Green Rose (UWT) Jimbo la Kiembesamaki wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) Ibrahi Raza alipokuwa akizungumza nao
Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza (katikati) akiwa na wanakikundi cha Green Rose katika picha ya pamoja. Kushoto ya Mjumbe wa NEC Amini Salmin Amour.Picha na Makame Mshenga.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KAMBI YA STARS

$
0
0
*Kamati yaahidi milioni 10 kwa kila mchezaji, iwapo watavuka 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kambi ya wachezaji wa timu ya Taifa na kuwaeleza kwamba Serikali na wananchi wanamatumaini makubwa kwa timu yao, hivyo wahakikishe wanapata ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa maendeleo makubwa yanayoendelea kupatikana katika soka nchini.

Waziri Mkuu ametembelea kambi hiyo leo (Jumamosi, Machi 23, 2019) jijini Dar es Salaam na amewaeleza kuwa Serikali inaimani nao na kwamba wasiwe na wasiwasi kwa sababu hawana tofauti yoyote na wachezaji wa timu nyingine duniani.

“Macho yote ya Watanzania yameelekezwa katika mechi ya kesho na Serikali inamatumaini makubwa na timu ya Taifa, hivyo waelewe kwamba kesho ni siku muhimu sana. Lengo letu ni kufikia hatua ambayo mataifa mengine yamefikia”.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kamati yake itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON)

Makonda amesema Watanzania wanachokijua kwa sasa ni kwamba AFCON 2019 ni zamu yao, hivyo amewaomba wachezaji wa timu ya Taifa wahakikishe wanawapa furaha kwa kuifunga timu ya Taifa ya Uganda na kwamba wananchi wengi wamehamasika kwenda kuwashangilia.

Nae, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala ameahidi kuwapeleka katika mbuga ya wanyama kwa ajili ya mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda hapo kesho.

Dkt. Kigwangala amesema Serikali ipo pamoja na wanamichezo, ambapo amewataka wachezaji hao wa timu ya Taifa wakapigane kweli kweli kwa ajili ya Taifa lao. “Kesho muingie uwanjani kama askari wa nchi. Mkapiganie ushindi wa Taifa letu”.

Awali, Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samata amesema,”Ninafuraha si kwa sababu ya ukubwa wa mechi ya kesho bali ni kwa sababu naona kesho nakwenda kuongoza nchi. Tupo tayari kuliletea Taifa ushindi”.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wachezaji na viongozi wa Timu ya Taifa ya Soka - Taifa Stars jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala  na kulia ni Mwenyekiti wa TFF, Wallas Karia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa  ya Soka – Taifa Stars baada ya kuzungumza nao  jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. Wa tano kulia (mstari wa mbele), ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala  na wa sita ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.  Wa nne kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Soka, Mbwana Samata  baada ya kuzungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwenye hoteli ya Kunduchi jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019.  Kushoto ni Mwenyekiti wa   TFF, Wallas Karia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa  ya Soka - Taifa Stars, Mbwana Samata  baada ya kuzungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo  jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEWZ ALERT: MEYA WA ILALA KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA ATANGAZA KUJIUZULU NAFASI HIYO.

$
0
0
Meya wa Ilala kupitia chama cha CHADEMA Charles Kuyeko ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli. '' Rais Magufuli ni mtu wa kuigwa, anastahili sifa na kazi ya kutukuka, nawaheshimu Viongozi wa CHADEMA kwa kunipa nafasi, nawashukuru na nitaendelea kuwaheshimu lakini mapenzi yangu ya dhati ni CCM ''.

RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA SKULI YA MSINGI NA MAANDALIZI FUONI PANGAWE WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akikata Utepe kuashiria kuifungua Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B Unguja kushoto Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma na Mwakilishi wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Bi, Shen Qi na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Haji Omar Kheri na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Wananchi wa Jimbo la Fuoni na Pangawe, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B,Unguja. katika viwanja vya Skuli hiyo Fuoni Mambosasa.(Picha na Ikulu).
 KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hijja akitowa maelezo ya Kitaalam ya ujenzi wa majengom ya Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe Wilaya ya Maghareibi B Unguja wakati wa hafla hiyo leo.(Picha na Ikulu)
 MWAKILISHI wa Ubalozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Zanzibar B. Shen Qi, akitowa salamu za Serikali ya China wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli hiyo iliojengwa kupitia msaada kutoka China, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi uliofanyika leo 23-3-2019.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Riziki Pembe Juma, akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B,Unguja iliojengwa kwa msaada na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibare na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea moja ya madarasa ya Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe,baada ya kuifungua akizungumza na wWanafunzi katika darasa hilo kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Dkt. Idrissa Muslim Hijja.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Rizipi Pembe Juma, akitowa maelezo wakati akitembelea chumba cha maabara ya Skuli hiyo baada ya kuifungua leo,23-3-2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea majengo ya Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe, baada ya ufunguzi wa Skuli hiyo akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma kulia na kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Dkt. Idrissa Muslim Hijja.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akielekea katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B,Unguja leo, kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Riziki Pembe Juma na kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheri.(Picha na Ikulu)
 WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Fuoni wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi Fuoniwakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hadhara hiyo.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli ya Fuoniu wakiimba wimbo wa Sisi Sote Tumegomboka wakatin wa hafla ya ufunguzi wa Majengo ya Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B,Unguja leo.(Picha na Ikulu)
 WANANCHI wa Fuoni Pangawe wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katiika hafla hiyo iuliofanyika katika viwanja vya skuli hiyo Fuoni Mambosasa leo,23-3-2019.(Picha na Ikulu)

 BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B, Unguja leo.Picha na Ikulu)
 JENGO jipya la la Skuli ya Msingi na Maandalizi Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B Unguja Ilililojengwa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein, leo,23-3-2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Ubalozi Mdogo wa China Uliopo Zanzibar Bi. Shen Qi , alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi na Maandalizi ya Fuoni Pangawe Wilaya ya Magharibi B Unguja, (Picha na Ikulu)

Waziri Biteko asema wizara iko tayari kuwahudumia watanzania kutokea Ihumwa

$
0
0
*Viongozi Waandamizi Madini watembelea jengo la Wizara, Ihumwa
*Waziri Biteko asema wizara iko tayari kuwahudumia watanzania kutokea Ihumwa
*Mkandarasi aahidi kukamilisha ujenzi ndani ya siku Tano

 Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini, wakiongozwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Machi 23, wametembelea Jengo la Wizara ya Madini lililopo mji wa Serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Akizungumza baada ya kukagua jengo hilo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishia watanzania wote pamoja na wadau wa madini kuwa, wizara iko tayari kuwahudumia kutokea eneo hilo la Ihumwa pindi itakapohamia na kuwataka watumishi kujiandaa kuhamia eneo hilo mara baada ya mkandarasi kukabidhi jengo kwa wizara. Vilevile, Waziri Biteko amezitaka taasisi nyingine zenye uhitaji wa kutumia madini ya mawe yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na mable, kuwa wizara iko tayari kuwasaidia kwa kuwaunganisha na wajeta wake.

Pia, amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutokana na msukumo alioutoa kuhakikisha ujenzi wa majengo ya serikali unakamilika kwa wakati. Aidha,  amempongeza Mkandarasi kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd kutokana na kuongeza kasi ya ujenzi ikiwemo kuzingatia ubora nakuongeza kwamba, wizara imeridhika na ujenzi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameeleza kuwa, wizara imepanga kulifanya eneo la ofisi hiyo kuwa kijani kwa kuhakikisha inapanda miti ya aina mbalimbali na kuhakikisha kwamba eneo hilo linawekewa mazingira mazuri ya kuvutia.
Naye, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila Amesema Mkandarasi Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd imeahidi kuikabidhi Wizara jengo hilo ndani ya kipindi cha siku Tano zijazo “awali ujenzi ulianza kwa kusuasua lakini sasa uko katika hatua nzuri na mkandarasi amezingatia ubora,” amesema Prof. Msanjila.
Akizungumzia mahitaji ya ofisi na idadi ya watumishi, amemsema kwa idadi ya watumishi wa wizara Makao Makuu ofisi zilizopo katika jego hilo zinatosheleza mahitaji na kuongeza kuwa, kwa kuanza Idara zote na Vitengo vya Wizara vinatarajia kuhamia katika eneo hilo isipokuwa Idara ya fedha kutokana na masuala ya mfumo wa kifedha. Pia, ameeleza kuwa, wizara imetumia malighafi inayopatikana nchini yakiwemo madini ya mable ambayo yamepatikana kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa kampuni hiyo   Hamisi Msangi ameihakikishia wizara kuwa , ndani ya siku tano zijazo, jengo hilo litakabidhiwa rasmi kwa wizara hiyo.

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa. 
 Waziri wa Madini Doto Biteko, (mwenye koti) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) na Prof. Simon Msanjila (mwenye tisheti nyekundu) wakikagua maeneo maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara
 Waziri wa Madini Doto Biteko ( wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto ) na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila, wakijadiliana jambo wakati wakikagua maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara, eneo la Ihumwa.
Waziri wa Madini Doto Biteko  katikati na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakiangalia kitu wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara, Ihumwa. 

PROF. MBARAWA - NATAKA UFUATILIAJI NA KASI ZAIDI SEKTA YA MAJI

$
0
0
 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa (Mb) akiongea katika Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maji jijini Dodoma. Waziri Mbarawa amewataka wafanyakazi kuongeza kasi, ubunifu na ufuatiliaji wa kazi mbalimbali katika sekta ya maji. Kulia ni Katibu Mkuu Prof. Kitila Mkumbo
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akiongea katika Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maji. Prof. Kitila amesisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Wafanyakazi katika mipango kwani wao ndio watekelezaji wakuu. Baraza hilo limefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Maji jijini Dodoma.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Wizara ya Maji waliohudhuria Baraza la Wafanyakazi wakiwasikiliza viongozi wa wizara wakati wa kikao cha Baraza kilichofanyika jijini Dodoma.

JE, WAJUWA FRANCO MAKIADI ALIZIKWA MARA MBILI MAKABURI TOFAUTI?

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
Rekodi ambayo haiwezi kusahaulika barani Afrika pengine duniani kote, ni ya aliyekuwa mwanamuziki nguli hayati Franco Luambo Luanzo Makiadi, mwili wake kuzikwa mara mbili katika makaburi tofauti.

Tukio lingine ni lile ambalo kamwe halijasikika sehemu nyingine ni lile la mke mmoja aliyeolewa na marais wawili kwa nyakati tofauti.

Graca aliyekuwa mke wa rais wa Msumbiji hayati Samora Machael, baada ya kufariki mumewe, akaja kuolewa na aliyekuwa rais wa nchi ya Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.

Wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na nchi jirani, kila mwaka ifikapo mwezi wa Oktoba hukumbuka kifo cha mwanamuziki huyo.

Franco alipatwa na mauti Oktoba 12, 1989 akiwa katika hospitali mojawapo nchini Ubelgiji alikokuwa amelazwa kwa maradhi ya muda mrefu.

Mwili wake ulisafirishwa ukarejeshwa kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire zamani), kwa mazishi.

Baada ya kufikishwa nchini mwake, jeneza lililokuwa limebeba mwili wake lilipitishwa mitaani kuagwa na wananchi likisindikizwa na ulinzi mkali wa polisi na baadaye serikali ikatangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa.

Siku ya mazishi yake, Leon Kengo wa Dondo,  alikwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa niaba ya serekali.

Mazishi ya mara ya kwanza

Wakati wa misa  ya mazishi yake, Padre alitamka “Luambo alikuwa Mtume wa muziki, hakuna alichokisahau katika utunzi wake, kavichambua vitu kadhalika na watu wa kila rika, hata rais Mobutu hajaachwa nyuma.

Nyimbo zake kadhaa zilipigwa marufuku, hata hivyo ziliendelea kupendwa sana na umma. huku nyimbo zake  nyingine hadi leo huchukuliwa kama nembo ya taifa….”

Katika siku hizo za maombolezo radio ya taifa hilo ilikuwa ikipiga nyimbo za Franco hadi tarehe 17, Oktoba 1989 alipozikwa kwa heshima zote za kitaifa.



Mazishi mara ya pili:

Baadaye serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilieonesha kwa kiasi kikubwa kuwathamini wanamuziki waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Uchumi na Siasa nchini humo.

Mabaki ya mwili wa Franco Luanzo Makiadi yaliyokuwa katika makaburi ya Gombe, yalifukuliwa na kwenda kuzikwa kwa mara ya pili eneo ambako kulijengwa mnara wa sanamu yake karibu lango la kuingilia makaburi hayo yakitazamana na barabara kubwa ya  Bulbati.

Kwa kuthamini mchango wake mkubwa kwa taifa, Waziri Mkuu wa nchi hiyo wakati huo Augustin Matata kwa niaba ya serikali yake, alizindua mnara  huo Oktoba 17, 2015, wakati wa sherehe kubwa ya maadhimisho ya miaka 26 ya kifo chake zilizofanyika katika jiji la Kinshasa.

Katika sherehe hizo ilitamkwa kwamba serikali itaendelea kuwaenzi wasanii wote na kuahidi kujenga minara ya nguli wengine waliotangulia mbele za haki.



Wasifu wa Franco:

Wasifu wa gwiji hilo unaeleza kuwa alizaliwa Julai 06, 1938, katika kijiji cha Sona Bata Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Baba yake Joseph Emogo alikuwa mfanyakazi wa shirika la reli wakati mama yake alikuwa mama wa nyumbani akioka mikate na kuuza sokoni.

Wakati akiwa bado mdogo wazazi wake walihamia katika jiji la Kinshasa.

Franco akiwa na umri mdogo alitengeneza gitaa la kienyeji ambalo alilitumia kupiga na kuwavutia wateja pembeni mwa mama yake wakati akiuza mikate.

Kipaji chake kiligunduliwa na mpiga gitaa Paul Ebengo Dewayon, ambaye alijitolea kumfunza Franco jinsi ya kupiga vyema ala hiyo.

Mwaka 1950, wakati huo akiwa na umri wa miaka 12, alitengeneza jina akiwa katika bendi ya Watam ya Dewayon ambaye alikuwa kiongozi wa bendi hiyo.

Miaka mitatu baadae Franco alirekodi  wimbo wake wa kwanza uliokuwa na jina la Bolingo na ngai na Beatrice. (mpenzi wangu Beatrice).

Baada ya kukubalika kuwa mmoja wa wana bendi ya Loningisa Studio, kiongozi wa bendi hiyo Henri Bowane alitoa nadhiri kwamba ataishi na Franco katika maisha yake yote yaliyosalia.

Chini ya Bowne, Franco akawa mpiga gitaa la solo, alikuwa akipigamtindo wa sebene.

Akaanza kutunga na kuimba yeye mwenyewe kwa mtindo wa rumba na za Kiafrika na hata za Kilatini.

Mwaka 1955 pamoja na kwamba alikuwa akipewa kazi nyingi katika studio, Franco aliunda bendi akiwa na Jean Serge Essous iliyokuwa ikipigia katika ukumbi wa baa ya OK.

Mwaka uliofuatia bendi hiyo ilibadilishwa jina na kuwa OK Jazz, baadae ikaitwa T.P.OK. Jazz kuenzi sehemu ilipoanzia bendi hiyo yaani katika baa yenye jila la OK (OK. Bar)

Katika kipindi cha mwaka mmoja bendi ya T.P.OK Jazz ikagundulika kwamba inataka kumpiku Vicky Longomba ambaye alikuwa katika bendi ya African Jazz, illiyokuwa ikiongozwa na Joseph Kabasele ‘Grand Kale’ ambayo ndiyo ilikuwa bendi kubwa nchini humo.

Franco alishadai kwamba bendi yake ya T.P. OK Jazz ilitoa zaidi ya album 150 katika kipindi cha miaka 30. 


Kwa kuwa sheria haina umaarufu, mwaka 1958 Makiadi alifungwa kwa kosa la ajali ya barabarani.

Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Kongo ina historia ndefu katika siasa na muziki. Katika makala haya imekudokezea kwa kifupi maswala mazima ya siasa na muziki yanavyouwiana kwa kiasia kikubwa.

Purukushani za Kisiasa katika nchi yake ya Kongo. Franco alilazimika kuhamia Ubelgiji kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake.

Baada ya nchi kutulia ikiwa chini ya uongozi wa rais Mobutu Seseseko Kuku Ng’endu Wazabanga, ambaye alibadilisha jina la Kongo kuwa Zaire, Franco alirudi nchini mwake na kafanya tamasha kambambe la Festival OK. Jazz African Arts lililofanyika Kinshasa mwaka 1966.

Mobutu alitawala nchi hiyo tangu Novemba 25, 1966 hadi Mei 16, 1997.  Alitanguliwa na rais wa kwanza Joseph Kasavumbu, aliyekuwa rais tangu Julai 01, 1960 hadi Novemba 24, 1965.

Mobutu Seseseko alipinduliwa na Laurent Kabila ambae aliitawala nchi hiyo tangu mei 17, 1997 hadi Januari 16, 2001 alipouawa. Baada ya kuawa Laurent Kabila, nchi ikaongozwa na mwanae Joseph Desire Kabila, hadi alipomuachia kijiti rais aliyepo Tshisekedi.
    
Bendi ya OK. Jazz iliisaidia sana serikali ya Mobutu katika mambo ya kisiasa kupitia nyimbo zake zilizokuwa na mafunzo pamoja na ushawishi mwingi.

Franco katika tungo zake hakuona soni kusifia mazuri wala kuonya mabaya pamoja na kwamba aliwekwa lupango mara nyingi alipokiuka taratibu za nchi.

Mwaka 1970 Luambo alipata pigo kubwa kwa kufiwa na mdogo wake Bavon Marie Marie, ambae kifo chake kilitokana na ajali ya gari alipokuwa akiendesha kwa hasira baada ya kukorofishana na kaka yake Franco juu ya mwanamke wa mdogo wake.

Mwaka 1980 serikali ya Kongo (Zaire) ilimtunukia hadhi ya kuwa babu wa muziki wa DRC, kama heshima kwa juhudi zake za kufufua uchumi uliokuwa ukiyumba nchini humo.

Wakati wa maisha yake aliwahi kuongeza uzito ghafla na kufikia paundi 300 ambazo ni sawa na kilo 136.

Franco Luambo Makiadi alitokea kuwa tajiri sana katika kipindi cha utawala wa rais Mobutu Seseseko.

Mbali na urafiki ambao aliokuwanao na rais huyo, ilifikia wakati fulani serekali ikazipiga marufuku baadhi ya nyimbo zake zilizo kuwa na ujumbe uliokiuka maadili ya umma.

Kutokana na sababu mbali mbali, serikali ya Mobutu ilikuwa makini sana na wanamuziki wake. Kulikuwa watu maalumu wakifanya kazi za kuwazichunguza kila wimbo kubaini ujumbe uliomo.


Sifa kubwa ya Franco ni kwamba takriban nyimbo zake zote zilikuwa ni zenye mafunzo kwa jamii, aidha hakusita kukemea hata serikali yake ilipofanya sivyo ndivyo.

Franco Makiadi kuna kipindi alishutumiwa kuimba nyimbo ambazo zilikuwa zikiigusa serikali ya Mobutu, ambapo ilimfungulia mashitaka akawekwa jela.

Baadae Luambo akiwa na kundi lake wakavuka mto Kongo unaotenganzisha nchi hizo mbili za Kongo Brazzaville na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), kwenda kujihifadhi kwa muda katika jiji la Brazzaville.

Akiwa jijini humo, rais Mobutu alimtumia wajumbe kwa ajili ya kumshawishi arudi Kinshasa, akiahidiwa kuwa maisha yake yasingelikuwa hatarini.

Bila kinyongo Franco aliupokea wito huo japo alikuwa ni mwenye kusita, mwishowe akaamua kurudi kama alivyoombwa na kiongozi wake wa nchi.

Pasipo katarajia Franco alipokanyaga ardhi ya  Kinshasa, kajikuta yuko matatani tena, akikaribishwa na kikosi cha wanajeshi.

Wakamuamuru yeye na kundi lake kupanda kwenya gari lao, akapelekwa hadi jela ya Ndolo.

Huko walikaa kwa muda wa siku mbili, yasemekana walicharazwa bakora za kutosha.

Baada ya kutolewa kwenye jela ya  hiyo,  Franco na kundi lake, wakahamishwa kwenye kambi ya jeshi  ya Tshatshi ambako walishikiliwa kwa siku kadhaa.

Ndipo ikatokea siku ambayo rais Mobutu alikwenda mwenyewe kujadiliana na Luambo Makiadi.

Alimtamkia maneno haya: “ kuanzia leo hii hadi itakapo fikia wakati wa mimi kuondoka madarakani, utakuwa ukiniimbia ukunisifia mimi, unatakiwa kunifanyia kazi zangu zote, tena kwa wakati wowote nitakapo kuhitaji…”

Kuanzia siku hiyo Franco akawa kiungo kikuu hususani katika Kampeni zote za rais.

Kwa ushirikiano huo, Franco alinufaika sana kuwazidi wanamuziki wengine wote wa nchi hiyo katika kipindi hicho cha utawala wa serekali ya Mobutu Seseseko Kuku Ng’wendu Wazabanga.

Mwaka 1978, Luambo akawekwa tena jela kutokana na utunzi wa nyimbo za Helein na Jackie.

Nyimbo hizo zilikuwa na maneno machafu yasiyo na maadili kwa umma. Sheria ikachukuliwa kuzipiga marufuku zisipitishwe kwenye radio na TV ya taifa.

Franco mwenyewe alijitetea akisema kuwa nyimbo hizo zilikuwa bado hazijaingia sokoni, bali zilikuwa zikiiandaliwa kwenye CD. Japo watu walikuwa wakizisikiliza wakati wa maonesho yao kwenye ukumbi wake wa 1.2.3 Kinshasa.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kipindi hicho  Bwana Leon Kengo wa Dondo, alisimamia swala hilo akaamuru Franco awekwe jela.

Alipelekwa kwenye jela ya Luzubu, iliyopo mkoa wa Bas Kongo, ambao ndiko alikozaliwa Franco.

Akiwa jela, Makiadi akawa ni mwenye masikitiko, akijiuliza kisa cha rais Mobutu kushindwa kumsaidia. Msongo huo wa mawazo ulipelekea kuathirika na ugonjwa wa Hemorrhoid, uliomsumbua sana.

Miaka michache baadae, palitokea na mabadiliko kwenye baraza la mawaziri, ambapo mwanasheria mkuu wa serikali Leon Kengo wa Dondo, alienguliwa wadhifa huo, na akapelekwa kuwa balozi nchini Ubelgiji.

Franco baada ya kuskia hivyo, furaha ilimjaa na bila kukawia akamtungia wimbo  “Tailleur”, wenye tafsiri ya “Utabiri wangu umetokea kuwa kweli, mdomo wangu kama mganga wa jadi”

Luambo baadae mwaka 1985, alifyatua wimbo mkali uliotikisa nchi, uliopewa jina la ‘Mario’.

Lakini mwaka 1987 fununu zikaanza kuzagaa kwamba Franco yu mgonjwa.

Wimbo aliotengeneza mwaka huo kabla ya kifo chake ulikuwa wa ‘Attention na SIDA ’(jihadhari kwa ukimwi/ aids)

Mwaka huu Oktoba 12, itatimia miongo mitatu tangu aiage dunia.

Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina,

ALPHA NA OMEGA YA SHAABAN DEDE

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
Mwaka 2018 tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini,  ilipata pigo la kuondokewa na wanamuziki wakubwa, Halila Tongolanga aliyefariki dunia Julai 04, 2017 na Shaaban Dede Julai 06, 2017.

Nguli hawa walipishana kwa siku mbili kuiaga dunia wakiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili walikopelekwa kwa nyakati tofauti kwa ajili ya matibabu.

Shaaban Dede baada ya kifo chake, taratibu za maziko yalifanyika, hadi kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Dede alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kisukari pamoja na Figo, wakati huohuo Tongolanga alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Figo kwa wiki kadhaa. Halila Tongolanga atakumbukwa zaidi kwa wimbo wake wa “Kila Munu Ave na Kwao”

Katika makala hii imeandikwa historia ya mwanzo wa hadi mwisho wa maisha ya marehemu Shaaban Dede.

Wasifu wake unaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1959, katika kijiji cha Kanyigo, mkoa wa Ziwa Magharibi wakati huo.

Yawezekana kabisa vijana wa kizazi hiki hawafahamu Mkoa wa Kagera ulipewa jina hilo baada ya vita vya Tanzania na Uganda.

Kabla ya hapo, mkoa huo ulikuwa na majina ya Ziwa Magharibi. Lakini hata kwa lugha ya Kimombo, ulifahamika kama West Lake Region.

Kazi aliyoifanya katika kipindi chote cha maisha yake ilikuwa ni muziki, bendi yake ya kwanza kuifanyia kazi ilikuwa TANU Jazz ya mjini Biharamulo mkoani humo.

Marehemu Shaaban Dede alikuwa na vipaji vingi vikiwemo vya utunzi na uimbaji pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza wenzake.

Aliingia mjini Tabora mwaka 1977, akitokea Bujumbura nchini Burundi, ambako baba yake mzazi ndiko alikokuwa akiishi.

Dede akaenda kuomba kufanya kazi katika bendi ya Tabora Jazz, lakini hakufanikiwa baada ya kutengenezewa ‘zengwe’ dhidi yake.

Wakati huo ilikuwepo bendi ya Milambo Jazz “Wana Sona Sona’ iliyokuwa ikiongozwa na mwanamuziki Hassani Athumani.

Shaaban Dede alikwenda kuomba kujiunga katika bendi hiyo, akafanikiwa.

Alishirikiana na wanamuziki wengine aliowakuta katika bendi hiyo, akina Kawelee Mutimanwa, Pulukulu Wabandoki Motto, Roga, Kassim Rashid ‘Kizunga’, Hassan Kimbunga, aliyekuwa akicharaza gita la rhythm, Juma Ogan na wengine.

Baada ya kuonesha uwezo wake wa kutunga na kuimba katika bendi hiyo, uongozi wa bendi ya Tabora Jazz, uliombeza mwanzoni, ukamhitaji ajiunge nao.

Uongozi wa Milambo Jazz, ulikubali kwa sharti la kulipa deni la baiskeli aliyokuwa ameibiwa Shabani Dede ikiwa ni mali ya bendi.

Tabora Jazz walilipa deni hilo, Dede akajiunga na bendi hiyo. Hata hivyo  alipiga muziki kwa kipindi kifupi kabla ya kutimkia mjini Dodoma, akajiunga na bendi ya Dodoma International.

Akiwa na bendi hiyo aliweza kutunga nyimbo zikiwemo za ‘Fatuma’ na ‘Mtu ni tabia njema’

Baadae Shaaban Dede ‘alinyakuliwa’ na kiongozi na mpiga solo maarufu katika bendi ya JUWATA, Saidi Mabera, akampeleka katika bendi yake.

Madhumuni yalikuwa ni kuziba pengo lililoachwa wazi na Hassan Rehani Bichuka, aliyetimkia katika bendi ya DDC Mlimani Pack Orchestra mwaka 1990.

Uongozi wa JUWATA uliona sauti yake inashabihiana sana na ya Hassan Rehani Bichuka.

Dede akiwa katika bendi hiyo, alijipatia umaarufu mkubwa kupitia vibao vyake vya ‘Fatuma’, ‘Jenny’, ‘Sauda’,  ‘Mkono wa Birika’ na nyinginezo.

Aliimba nyimbo hizo akishirikiana na Joseph Lusungu, Juma Akida, TX Moshi William na Suleiman Mbwembwe (wote ni marehemu).


Licha ya kujipatia sifa na umaarufu kwa kipindi kifupi, Dede aliamua kuiacha bendi hiyo ya JUWATA akaenda kujiunga bendi ya DDC Mlimani Park Orchestra ‘Wana Sikinde’ ambako ilizidi kujimtambulisha zaidi kimuziki.


Akiwa katika bendi hiyo, alipewa nafasi ya kuwa mmoja wa viongozi  kwa vipindi vinne tofauti.

Dede alitunga nyimbo lukuki, ambazo ziliipatia umaarufu mkubwa bendi hiyo ya DDC Mlimani Park Orchestra.

Baadhi ya nyimbo hizo ni ‘Talaka rejea’, ‘Amua’, ‘Ndugu wagombanapo’, ‘Kumbuka fadhila’, ‘Binamu’, ‘Uchungu wa mwana’, ‘Chozi la huba’, ‘Fumanizi’, ‘Maneno maneno’ na nyinginezo.

Mashirika ya Umma hapa nchini yalianzisha vikundi vya burudani zikiwemo bendi za muziki.

Shirika la Bima Taifa lilikuwa na bendi ya Orchestra Bima Lee. Uongozi wa bendi hiyo uliamua kuongeza wanamuziki wengine mahiri toka bendi ya zingine kuimarisha nguvu.

Shabani Dede alikuwa miongoni mwa waliosombwa mwaka 1983, akiambatana na mpiga gitaa la solo Joseph Mulenga ‘King Spoiler’, Mafumu Bilali, Abdallah Gama na Jerry Nashoni ‘Dudumizi’.

Wanamuziki wengine walioijenga Bima Lee walikuwa akina Athumani Momba, Dancun Njilima na Suleiman Mwanyiro  ‘Compyuta’

Baadhi ya nyimbo alizotoka nazo ni za Aziza, Kununanuna, Dunia duara, Shangwe ya harusi, Bilionea wa mapenzi, Kipepeo na nyingine nyingine nyingi.

Mashabiki wa bendi hiyo walimpachika Shaaban Dede jina la ‘Mzee Tingisha’.

Mkataba ulipomalizika, Dede alirejea katika bendi ya DDC Mlimani Park.

Super Motisha Dede baada ya kuitumika bendi hiyo kwa kipindi kirefu kidogo, alirejea tena kwenye bendi yake Msondo iliyomkaribisha wakati alipokuwa akitokea Dodoma.


Shaaban Dede aliamua kurejea Msondo Ngoma baada ya kuikumbuka na kuwakosa mashabiki wake kwa muda mrefu.

Alikaririwa akisema hakuodoka katika bendi ya DDC Mlimani Park Orchestra ‘Wana Sikinde’ kwa sababu ya kushawishiwa kwa pesa, mtu ama kiongozi yeyote wa Msondo Ngoma, huo ulikuwa uamuzi wake binafsi.

Dede ambaye alipachikwa jina la ‘Kamchape’ na mashabiki wake, alikuwa hodari wa kutunga na kuimba nyimbo za maudhui na ujumbe mzuri katika jamii.

Katika historia yake katika muziki, bendi aliyodumu nayo kwa kipindi kirefu katika maisha yake ni Msondo Ngoma.

Dede alipokuwa katika bendi hiyo alishirikiana kuimba na waimbaji akina Juma Katundu, Twaha Mohamed, Hassan Moshi William ‘TX Junior’ na Hussein Kalembo.

Sauti zao zilikuwa zikienda sambamba na wakung’utaji magitaa ya solo na rhythm ambao ni Ridhiwani Pangamawe na Huruka Uvuruge, Ramadhani Zahoro Bangwe na Mustafa Hamis ‘Pishuu’.

Dede alipokuwa akiimba sauti yake ilipambwa na gitaa zito la besi la akina Ally Lindunga na Saad Ally ‘Sure Boy’.

Kwenye drums alikuwa zikichanganywa na Saad Ally ‘Mashine’ na Arnold Kang’ombe, tarumbeta alikuwa akipulizwa na Roman Mng’ande ‘Romarii’ na Hamis Mnyupe. Tumba zikipigwa na Amiri Said Dongo pamoja na Dorice George.

Dorice ni mwanamuziki mpya wa kike mwenye vipaji vingi, ambaye ni tunda la Chuo cha Sanaa Bagamoyo, bado yupo kwenye majaribio.

Dede aliwahi kufanya kazi na baadhi ya wanamuziki ambao wamekwisha tangulia mbele za haki akiwemo Mjomba Muhidin Maalim Gurumo.

Wengine ni TX Moshi William, Nicko Zengekala, Selemani Mbwembwe, Mnenge Ramadhan, Joseph Maina, Mustafa John Ngosha, Suleimani Mwanyiro, Tino Maselenge ‘Arawa’ na Athuman Momba.

Kwa upande wa upulizaji wa saxophoni alikuwepo Alli Rashidi, aliyefariki dunia siku ambayo bendi hiyo ikitimiza miaka 50, Oktoba 10, 2014.

Kamchape atakumbukwa kwa jinsi alivyokuwa akiipenda bendi hiyo ya Msondo, licha ya kuihama na kwenda kwa wahasimu wao Mlimani Park Ochestra ‘Sikinde’.

Aliporejea katika bendi hiyo ya Msondo Ngoma, alipewa nafasi ya uongozi, wala hakuhama tena hadi kifo kilipomchukua.

Bendi hizi za Mlimani Park na Msondo Ngoma, unaweza zinamashabiki kama ilivyo kwenye klabu za Simba na Yanga.

Marehemu Dede alikuwa na tabia ya kuwapiga madogo mahasimu wake wa Sikinde, ikipanda jukwani.

Bendi hizo zilikuwa na utaratibu wa kupiga muziki pamoja kwenye viwanja vya Sigara TTC Chang’ombe ama viwanja vya Leaders Club.

Katika onesho lao na Sikinde, katika viwanja vya Leaders Club, moja ya nyimbo za Msondo Ngoma, Shaaban Dede na Juma Katundu wakawa wanachomekea vionjo vikiwakejeli mahasimu wao Sikinde.

Alijulikana kwa uimbaji wenye kiwango cha juu kutokana na tungo zake murua, ambazo baadhi zilitokea kuwa gumzo ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa nyimbo za Dede, ambazo zinapendwa na wadau wa muziki wa dansi ni Fumanizi, Kelele za paka hazimzuii mwenye nyumba kulala, Mshenga, Baba mkwe, Amina, Talaka rejea na Kizabinazabina.

Nyimbo hizo na nyinginezo kadhaa, alizitunga wakati akiwa katika bendi ya DDC Mlimani Park kwa muda wa miaka 27, kabla hajarudi katika bendi yake ya zamani ya Msondo Ngoma, mwaka 2014.


‘Kamchape’ atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kwa sauti yake tamu kupitia nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali, zikiwemo za Bima Lee, Mlimani Park na Msondo Ngoma Music.

Shaaban Dede baada ya kifo chake, taratibu za maziko yalifanyika, hadi kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milile kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Mazishi hayo yaliweka rekodi ya kuhudhuriwa na mamia ya watu, wakiwemo wanamuziki wakongwe, wa kizazi cha sasa na wadau wa tasnia ya muziki.


Baadhi ya watu waliofanyakazi naye, walimuelezea Dede kwa namna walivyokuwa wakimfahamu.


“Nilimfahamu Dede kwa kipindi kirefu kwani alikuwa mtunzi mzuri na mtu mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya muziki. Nimesikitishwa sana na kifo chake na pengo lake halitazibika kwa urahisi” alisema Hassan Rehani Bichuka.


Kiongozi wa sasa wa Mlimani Park, Abdalah Hemba, alikiri kuwa Shaaban Dede ndiye aliyeibua kipaji chake, ambacho kwa sasa kimemfanya awe mwimbaji mahiri na kiongozi wa bendi hiyo kongwe nchini.

Hemba alisema “Dede ndiye alinisaidia kuingia katika bendi hii, hata nimejulikana kupitia sanaa ya muziki. Alikuwa mtambuzi mzuri wa vipaji vya wanamuziki baada ya kuwa nao kwa muda mfupi” alisema Hemba.

Shaaban Dede alikuwa mmoja wa watunzi mahiri wa nyimbo, hasa alipokuwa bendi ya Mlimani Park, ambapo inasemekana alitunga nyimbo zaidi ya 100, akiwa anashika nafasi ya pili nyuma ya Hassan Rehani Bitchuka.

Pia, alikuwa chachu ya ushindani wa kimuziki uliokuwepo kati ya Msondo Ngoma na Mlimani Park, ambapo alikuwa ‘Karata’ muhimu ya ushindi katika kila bendi.

Dede alikuwa anajua nini cha kufanya ili kuwafurahisha mashabiki na kuwapa ile burudani wanayoihitaji.

Nguli huyu ametunga na kuimba ni nyingi zikiwemo za Kilio Cha Mtu Mzima, Kaza Moyo (Msondo), Diana, Tui la Nazi  na Amina (Sikinde) ambazo zinaonesha uhalisia wa maisha ya watu.

Nyimbo hizo na zingine zilijizolea umaarufu katika kumbi mbali mbali za muziki na kuvuta mashabiki wa rika zote.

Ni wazi kuwa Dede ameacha mengi ya kujifunza kwa wanamuziki wa sasa. Nayo ni uvumilivu wa kudumu kwenye bendi kwa miaka mingi, kutunga nyimbo zinazogusa hisia na kuimba kwa sauti yenye mvuto.

Mashabiki wa muziki walikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.

Kazi uliyoifanya hapa duniani imetosha, itabaki kuwa kumbukumbu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo kwa miaka mingi.


Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.

BREAKING NEWS: BONDIA KUTOKA ARGENTINA ACHEZEA KICHAPO KWA BONDIA MTANZANIA NCHINI KENYA

$
0
0
 Bondia kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo amemtwanga Bondia kutoka Argentina, Sergio Gonzalez kwa K.O, Raundi ya 5 katika pambano la Nairobi Night Fight lililofanyika nchini Kenya usiku huu.

 Bondia kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo(kushoto) akimrushia konde Bondia kutoka Argentina, Sergio Gonzalez(kulia)  katika pambano la Nairobi Night Fight lililofanyika nchini Kenya
Bondia kutoka Argentina, Sergio Gonzalez  akiwa cchini mara baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa Bondia kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo
kwa K.O, Raundi ya 5 katika pambano la Nairobi Night Fight lililofanyika nchini Kenya.



MASAUNI ATEMBELEA SHAMBA LA MAHINDI GEREZA LA SONGWE

WANA CCM MBEYA WAANDAMANA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI


QUEEN DARLEEN AONGEA NA MICHUZI TV KUHUSU "MUHOGO" WAKE

Wadau wa mitandao ya kijamii wanogesha Wiki ya Lugha ya Kifaransa

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIKA kushereheka wiki ya Lugha ya Kifaransa ubalozi  wa Uswizi nchini Tanzania umefanya mdahalo na wadau wa mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufahamu changamoto wanazokutana nazo pamoja na sheria za makosa  ya Kimtandao inavyotumika.

Mdahalo huo ulifanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliweza kuwakutanisha wadau mbalimbali akiwemo Wanasaikolojia, mawakili, wamiliki wa mitandao ya kijamii na jamii husika inayotumia mitandao hiyo.

Kabla ya kuanza kwa mdahalo huo, iliwekwa Filamu ya ‘The Cleaners’  iliyofanikiwa kupata tuzo ya The Geneva International Film na Forum on Human Rights kwa mwaka 2018 nchini Uswizi ambayo imekuwa inazungumzia namna mitandao ya kijamii inavyotumiwa vibaya na wale wanaohusika na kusafisha picha au video chafu wanakuwa  kwenye mazingira ya aina gani.

Balozi wa Uswizi nchini Florence Tinguely Mattli  amesema kuwa, filamu ya The Cleaners imeweka wazi namna watu walionyuma ya mitandao ya kijamii wanavyofanya kazi kubwa ya kuweza kusafisha yale yote ambayo hayafai kuonekana  kwa jamii kimaadili au kitaaluma.

Amesema, wadau wanapokutana katika midahalo ya wazi itasaidia kwenye kubadilisha njia ya mawasiliano ikiwemo na kufahamu haki za binadamu na jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kubadilisha maisha ya watu ikiwemo Kutoa elimu kwa nchi ya Tanzania.

“Kuna kazi kubwa inafanywa na wasafishaji walio nyuma ya maudhui mbalimbali ya Mitandao ya Kijamii na wanakutana na picha za aina tofauti kwa siku na wanazifuta na hilo linasaidia kulinda maadili ndani ya jamii”, amesema Mattli.

Mmiliki na Mwanzilishi wa Jamii Forum Maxence Melo amesema kuwa watu wamekuwa wanatumia mitandao ya kijamii vibaya na  hata kwa nchini kwetu namna wanavyopambana kulinda maudhui ya Kiswahili  kama kinachofanyika kwenye filamu ya The Cleaners.

Maxence amesema, watumiaji wa zamani wa mitandao walikuwa ni wasomi na kabla ya kuiweka mtandaoni wanafikiria maudhui ila kwa sasa hivi watumiaji wa mktandao ya kijamii wamekuwa wengi na kila mmoja anaweka kile anachojisikia kwa muda huo.

Mwanasaikilojia Araika Mkulo amesema, filamu ya the Cleaners imeonesha kiasi gani walio nyuma ya mitandao ya kijamii wanapata changamoto kubwa sana ukilinganisha na namna watu wanavyofikiria. “Takribani kwa siku mtu anakutana na picha zisizo na maadili 25,000 na kujiuliza je wanapata stahiki zao kama inavyotakiwa kwani wamekuwa wanakutana na changamoto za kisaikilojia kutokana na kuona picha chafu na zisizo na maadili  mara kwa mara,”amesema .

Wakili wa kujitegemeaBenedict Ishabakaki amesema kwa serikali ya Tanzania imeweka sheria ya makosa ya kimtandao Kipengele cha 12 kikielezea adhabu ya mtu atakayeweka picha au taarifa isiyo na maadili kwenye mtandao wa kijamii ambapo anaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja au faini isiyopungua Milion 5 au vyote kwa pamoja.

Filamu ya The Cleaners inaonesha namna jamii inavyotumia mitandao ya kijamii pasi na kufuata maudhui au maadili na watu walionyuma ya mitandao hiyo wakiwa wanafanya jitihada za kusafisha picha chafu na zisizo kwa dunia nzima.



JK COMEDY AHAMASISHA TAIFA STARS

MONALISA ATAMBULISHA TUZO ZA FILAMU ZA WANAWAKE

MALKIA WA MIPASHO KHADIJA KOPA AFUNGUKA KUHUSU MUZIKI WA TAARABU

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images