Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Marekani Yatoa Vifaa vya Kupimia Maji kwa Bodi za Mabonde ya Maji Rufiji na Wami / Ruvu

0
0

Serikali ya Marekani ilikabidhi vifaa vya kupimia maji kwa Bodi za Mabonde ya Maji Rufiji na Wami / Ruvu. Vifaa na huduma za ziada vitasaidia bodi kukusanya na kuchambua takwimu juu ya ubora na kiasi cha maji. Ufuatiliaji wa uboreshaji wa maji utasaidia wilaya kufanya maamuzi sahihi juu ya ugawaji wa maji ili kusimamia na kulinda rasilimali za maji kwa vizazi vijavyo.

Mbali na vifaa vya kupimia maji, Bodi za Maji zilipata boti/mashua, kompyuta, redio, vifaa vya kukadiria umbali, na vifaa vya mtandao kwa shughuli za zinazofanyika katika eneo la mradi na ofisini. Wafanyakazi watafundishwa namna ya kutumia vifaa vya kupimia maji ya mtoni.

Vifaa na huduma, vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 za Kitanzania (dola 980,000 za Kimarekani), zilikabidhiwa na Shirika la WARIDI, na kufadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). WARIDI inaendeleza usimamizi wa rasilimali maji na kuboresha upatikanaji wa huduma za maji.

“Kwa sababu maji yana jukumu muhimu katika kupunguza umasikini, kuboresha afya, na kuongeza uzalishaji, ni lazima yapewe kipaumbele cha juu serikalini na jumuiya ya wafadhili,” alisema Andrew Karas, Kaimu Naibu Balozi wa Ubalozi wa Marekani.

Kupitia WARIDI, Serikali ya Marekani pia ilipatia Wizara ya Maji mwongozo wa matumizi ya kutathmini uwezo wa Jumuiya za Watumia Maji (WUAs), asasi za kijamii zinazohusika na usimamizi wa rasilimali za maji. WUA wana mamlaka ya kisheria ya kupata na kutumia vibali vya matumizi ya maji, kutatua migogoro ya matumizi ya maji, kulinda vyanzo vya maji, kuwakilisha maslahi ya watumiaji katika ngazi ya jamii, na kukusanya tozo za watumiaji wa maji kwa niaba ya Bodi za Mabonde za Maji.
 

 Kifaa kinaweza kutumika kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa WUA na kutambua hatua za kuboresha utendaji. Ilianzishwa kupitia mchakato shirikishi unaohusisha wawakilishi kutoka Bodi ya Maji ya Bonde, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara ya Maji, na washauri wa ndani.

Ili kuomba taarifa zaidi, tafadhali piga simu Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kupitia: +255 22 229-4000 au barua pepe: DPO@state.gov.

UONGOZI WA BUNGE SPORTS CLUB WAITAKIA HERI TIMU YA TAIFA STARS

0
0


NGEREJA 1ANGEREJA 2B
Mwenyekiti wa Timu ya Michezo ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngereja akizungumza na waandishi wa habari kuitakia heri Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) katika mchezo wake wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda inatoyatarajiwa kuchezwa tarehe 24 Machi, 2019 Jijini Dar es Salaam, Mkutano huo ulifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma,
NGEREJA 4D
Mwenyekiti wa Timu ya Michezo ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngereja akizungumza na waandishi wa habari kuitakia heri Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) katika mchezo wake wa kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda inatoyatarajiwa kuchezwa tarehe 24 Machi, 2019 Jijini Dar es Salaam, Mkutano huo ulifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Mhe. Vanance Mwamoto na Katibu Wa Timu, Ndugu Waziri Kizingiti. (Picha na Ofisi ya Bunge)

BEI ZA BIDHAA MBALIMBALI KATIKA SOKO LA MAPINDUZI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Bei za bidhaa mbalimbali katika Soko la Mapinduzi Mwananyamala wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,kama zinavyoonekana katika picha.
Bei ya maharage ya soya kilomoja ni shilingi 2200,2400.
Wafanya biashara wa viazi katika Soko la Mapinduzi Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam wakisubiri wateja wanaotoka sehemu mbalimbali,ambapo fungu moja la viazi limauzwa shilingi 1000 mpaka 2000. Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

MBUNIFU WA MAVAZI KUTOKA TANZANIA APEWA TUZO YA USHAWISHI NA RAIS WA MISRI ABDELFATTAH ELSISI,JIJINI ASWAN MISRI.

0
0
Mbunifu wa mavazi na mwanaharakati wa vijana kutoka Tanzania Rahma Bajun alipokea tuzo ya utambuzi kutoka kwa Rais wa Misri Abdelfattah Elsisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki. 

Tuzo hiyo ilitolewa jijini Aswan nchini Misri kwenye mkutano wa “Arab and African Youth Platform” uliofanyika hivi karibuni Rahma sambamba na vijana wengine 9 kutoka nchi za Afrika na za Kiarabu wanaotoka kwene sekta mbalimbali wamepokea tuzo hizo za heshimwa kwa mchango wanaotoka vijana, nchi zao na Afrika kwa ujumla.
Rais wa Misri Abdelfattah Elsisi(Kushoto) akimkabidhi Mtanzania Bi. Rahma Bajun tuzo ya 'Most inspiring youth in Africa and Arab region' wakati wa mkutano wa Arab and African Youth Platform uliofanyika nchini Misri.
Mbunifu wa mavazi na mwanaharakati wa vijana kutoka Tanzania Rahma Bajun (wa tatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na washiriki wengine kutoka Barani Africa wakati wa mkutano huo.

MAALIM SEIF, ZITTO WATOA YA MOYONI KUHUSU KUTUHUMIWA KUWA WAO NI 'MAMLUKI' WA CCM

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.


KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na mwanachma mwenye kadi namba moja wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad wameendelea kuchanja mbuga ikiwa ni mkakati wa kuzungumza na wanachama wao. 

Maalim Seif aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF)amejiunga na ACT -Wazalendo baada ya kutoridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam baada ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba katika nafasi ya uenyekiti wa CUF.

Wakizungumza kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Maalim Seif na Zitto wamekiri mkakati wa wao wa kuwa pamoja si wa kukurupa bali yamefanyika mazungumzo ya kutosha yaliyokwenda sambamba na kufanyika kwa utafiti kabla ya kufikia uamuzi.

Kwa upande wake Maalim Seif amesema kutokana na mgogoro uliokuwa ndani ya CUF yeye pamoja na viongozi wenzake walianza kuweka mipango mipya ambayo itawawezesha kuendelea na siasa.Moja ya mkakati ulikuwa ni kutafuta Chama ambacho ambacho watajiunga nacho , hivyo wamejirisha kuwa ACT- Wazalendo ndio sehemu sahihi kwao.

"Kujiunga na ACT haikuwa jambo la kukurupuka , tumetafakari, tumefanya uchunguzi na tumejiridhisha tuko sehemu sahihi na mapambano yanaendelea.Wakati tukiendelea na kesi tuliamua kuanza kujiandaa kwa kutafuta Chama sahihi ambacho kitatufaa.Hivyo ujio wetu ACT ni maandalizi ya muda mrefu,"amesema Maalim Seif.

Kuhusu tuhuma za kwamba Maalim Seif ni Mamluki wa CCM, amejibu kuwa tuhuma hizo zimekuwa zikielekezwa kwake kwa muda mrefu lakini hajawahi kuzijibu kwani anajua anachokifanya.

"Ningekuwa mamluki usingetengezwa mgogoro CUF ili kutudhoofisha kisiasa na hakari za kudai demokrasia huru nchini. Sababu za mgogoro ulipo ndani ya CUF ni kupunguza nguvu yangu ya kisiasa. Nipo ACT kuendeleza mapambano ya kisiasa ili kuipata Tanzania mpya,"amesema Maalim Seif.

Alipoulizwa anatoa kauli gani baada ya baadhi ya wanachama aliiondoka nao CUF kuonekana wakiwa wameshika vitabu vitakatifu wakati wanapandisha bendereza ACT visiwani Pemba, amejibu hakuna udini wowote.

"Kutaka jina la Mwenyezi Mungu katika shughuli za kila siku kwa jamii ya Watanzania ni mambo ya kawaida.Ndio maana hata Bungeni kabla Bunge kuaza dua inayoambatana na kutajwa kwa jina la Mungu ni jambo la kawaida.Hivyo sioni kosa lilipo,"amesema Maalim Seif.

Hivyo amefafanua hakuna mambo ya udini ila kilichotokea wanachama hao waliamua kusema Alhau Akibarr kwa maana ya Mungu Mkubwa na ni jambo la kawaida.

Kwa upande wake Zitto amesema kitendo cha Maalim Seif kujinga na ACT-Wazalendo kunafungua ukurasa mpya na Maalim Seif ameandika historia mpya huku naye akitumia nafasi hiyo kueleza ujio wake ndani ya chama hicho mchakato wake ulianza muda mrefu.

"Tulikuwa tunaangalia namna ambavyo wenzetu CUF mgogoro wao unavyoendelea, tukaona ACT ni jukumu letu kuhakikisha tunajiandaa ili wenzetu wakikosa nafasi tunaungana nao na kuendelea na mapambano katika medani za kisiasa. Maandalizi ya Maalim Seif kuja kwetu hayakuwa maandalizi ya muda mfupi bali ni ya muda mrefu.Tunawapokea pia watu ambao wanapenda mabadiliko na wamechoka kuburuzwa,"amesema Zitto.

Akizungumzia tuhuma za kwamba Zitto ni mamluki, amejibu kuwa "Kwanza nieleze tu historia ya miaka michache imeonesha dhahiri kuwa maneno ya umamluki si sahihi na Watanzania wanaona namna ambavyo chama ninachokiongoza kilivyokuwa mwiba.

"Pili kiongozi lazima awe na uwezo wa kuunganisha watu, ukiona kiongozi anagawa watu basi uongozi wake una mashaka, hivyo kwake aliona iwapo kuna fursa ya kuunganisha watu. Muhimu ni matendo na huwezi kuzuia watu wasiseme.Wakati nagombana na Chadema nilikuwa na nafasi ya kwenda CCM lakini niliona hakuna sababu hiyo kwani lengo ni kuendeleza mapambano.Siwezi kuwa mamluki,"amesema Zitto.

Wakati huo huo, jana Maalim Seif pamoja na Zitto walikuwa visiwani Zanzibar wakizungumza na wanachama na wapenzi wa ACT na leo wameendelea kuchanja mbuga kwani wapo mkoani Tanga.ACT-Wazalendo wameamua kumtambulisha Maalim Seif kwa wanachama wao huyo ambaye amekwenda huko akiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CUF ambao wanamuunga mkono Maalim.
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akiwa pamoja na Maalim Seif aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF)amejiunga na ACT -Wazalendo 

Dkt. Ndugulile atembelea MOI,akagua maendeleo ya chumba cha tiba mtandao

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametembelea Taasisi ya Tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI)kukagua maendeleo ya chumba maalum cha Tiba mtandao ambacho kinatarajia kukamilika na kufanya kazi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Awali akiwa kwenye taasisi hiyo ya MOI, Dkt. Ndugulile aliweza kupokea maendeleo ya ukamilishwaji wa chumba hicho cha tiba mtandao ambapo pia aliwataka kuhakikisha wanasimamia vizuri  uendeshaji wake  kwani utasaidia Taifa kutoa huduma za kibingwa sehemu kubwa zaidi hapa nchini zikiwemo hospitali za rufaa za mikoa na nyingine

Aidha, Dkt. Ndugulile amewataka kukamilisha hatua zote za chumba hicho na kitakapokamilika  uzinduzi ufanyike kama inavyotarajiwa

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Respicious Boniface amesema kuwa, chumba hicho kinategemea kukamilika na kuanza kufanya kazi mwezi  Juni mwaka huu na kitakapokamilika kitasaidia matibabu kwa kwa njia ya mtandao nchi nzima

“Chumba cha Tiba mtandao hapa MOI kitakapokamilika hospitali zote kubwa za rufaa za mikoa na zingine za  Rufaa, zitatuma picha hapa na watalaam wa MOI wanatoa majibu na kurudisha tiba kule na kutoa ushauri wa jinsi wa kutoa matibabu kwa wagonjwa wakiwa hukohuko” alieleza Dkt. Boniface.

Chumba hicho cha tiba  mtandao kinatarajiwa kuwepo kwenye jengo jipya la MOI ambapo tayari timu ya watalaam wanaendelea na taratibu za kukamilisha uendeshaji wake.

MOI ni miongoni mwa Taasisi za tiba zenye kutoa huduma za kibingwa huku ikiwa na Madaktari wabobezi kwenye tiba ya mifupa, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

 Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (Mb) ametembelea kituo Cha Utafiti na Maabara ya ugonjwa wa Seli Mundu kilichopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wakati akiwa katika ziara hiyo, aliwasisitiza watalaam kuhakikisha maabara hizo zinakuwa na manufaa mapana kwa wananchi  ambao mara nyingi wanachelewa kujua kama wanamatatizo ya Seli Mundu na magonjwa mengine ya kurithi. Aidha, alieleza maabara hiyo ni miongoni mwa maabara chache sana Africa Mashariki hivyo, zitumike vyema  kupata matokeo chanya pamoja na kutumika kujifunza na kufanyia tafiti mbalimbali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.




RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI

0
0
Kufuatia kusuasua kuanza kwa miradi ya kimkakati, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya za Ilala na Kinondoni, Wakurugenzi wa manispaa na wakuu wa idara kuhakikisha hadi kufikia Jumanne ya March 26 miradi yote iwe imeanza utekelezaji ikimaanisha kuwa mikataba imesainiwa na mkandarasi yupo kazini.

RC Makonda amefikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa kuona miradi haijaanza kutekelezwa hadi sasa licha ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa fedha zote za miradi lakini baadhi ya watendaji wamekuwa wakichelewesha kuanza kwa miradi.

Aidha RC Makonda amempa Siku tatu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema na Mkurugenzi wa manispaa hiyo kuhakikisha mkataba wa ujenzi wa machinjio ya kisasa Vingunguti unasainiwa mara moja na mkandarasi anaanza kazi.

Hivyohivyo RC Makonda amempa siku tano Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Mkurugenzi wake kuhakikisha ujenzi na Maboresho ya ufukwe wa kisasa wa Coco unaanza mara moja.

Mhe. Makonda amesema endapo wahusika watashindwa kutekeleza agizo hilo watatafsiriwa kuwa wameshindwa kusimamia fedha na miradi ya serikali.

Itakumbukwa mwaka jana Rais Dkt.John Magufuli alitoa fedha za kutosha kwaajili ya miradi ya kimkakati ya kuwakwamua wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara, hospital, zahanati,vituo vya daladala,maji,umeme,elimu na machinjio ili kupunguza kero za wananchi.

TANZANIA YAPIGA HATUA MATUMIZI YA VYANDARUA VYENYE DAWA

0
0



 Mratibu wa Malaria wa Halmashauri ya Kigoma/Ujiji Dkt. Abigael Kasumani (kushoto) akitoa salamu leo za washiriki wa semina za siku moja kuhusu usambazaji wa matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2017 kwa Kanda ya Magharibi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Waratibu wa Malaria Mkoa, Halamashauri ,Mameneja Takwimu wa Mikoa na  Wawakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS). wengine ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Hamis Mkunga(katikati) na Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tabora kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Gabriel Gewe(kulia).
2
Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tabora kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Gabriel Gewe(kulia) akitoa maneno ya utangulizi wakati wa  semina za siku moja kuhusu usambazaji wa matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2017 kwa Kanda ya Magharibi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Waratibu wa Malaria Mkoa, Halamashauri ,Mameneja Takwimu wa Mikoa na  Wawakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS). wengine ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Hamis Mkunga(katikati) na Mratibu wa Malaria wa Halmashauri ya Kigoma/Ujiji Dkt. Abigael Kasumani (kushoto) .
3
Baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja  kuhusu usambazaji wa matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2017 kwa Kanda ya Magharibi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Waratibu wa Malaria Mkoa, Halamashauri ,Mameneja Takwimu wa Mikoa na  Wawakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).
44a
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Hamis Mkunga(katikati) akifungua semina leo mjini Tabora ya siku moja kuhusu usambazaji wa matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2017 kwa Kanda ya Magharibi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Waratibu wa Malaria Mkoa, Halamashauri ,Mameneja Takwimu wa Mikoa na  Wawakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).  wengine ni  Mratibu wa Malaria wa Halmashauri ya Kigoma/Ujiji Dkt. Abigael Kasumani (kushoto) na Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tabora kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Gabriel Gewe(kulia)
5
Washiriki wa semina ya siku moja  kuhusu usambazaji wa matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2017 kwa Kanda ya Magharibi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Waratibu wa Malaria Mkoa, Halamashauri ,Mameneja Takwimu wa Mikoa na  Wawakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa semina hiyo leo mjini Tabora.Picha na Tiganya Vincent
………………………….
 
NA TIGANYA VINCENT,TABORA    
                                         
MATOKEO ya utafiti uliofanywa mwaka 2017 na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine umeonyesha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika juhudi za kuzuia na kupambana na ugonjwa wa malaria kupitia matumizi ya vyandarua vyenye dawa katika ngazi ya kaya.
 
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Tabora na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Hamis Mkunga wakati akifungua semina za siku moja kuhusu usambazaji wa matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa Mwaka 2017 kwa Kanda ya Magharibi kwa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Waratibu wa Malaria Mkoa, HalmashauriMameneja Takwimu wa Mikoa na  Wawakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).

Alisema utafiti huo umeonyesha jumla ya asilimia 78 ya kaya zote nchini zinamiliki walau chandarua kimoja chenye dawa ambapo kaya za mjini zina uwezo mkubwa wa kumiliki vyandarua kwa asilimia 81 ukilinganisha wa vijijini ambapo ni asilimia 77.

Mkunga alisema katika utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2015/16, ni asilimia 66 tu za kaya zilikuwa zinamiliki angalau chandarua kimoja chenye dawa.

Aliongeza kuwa kwa upande wa Tanzania Bara, Mkoa wa Pwani ndio unaoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha umiliki wa vyandarua vyenye dawa kwa asilimia 89 na Mkoa wa Njombe una kiwango kidogo cha umiliki wa vyandarua vyenye dawa asilimia 58 ikilinganishwa na mikoa mingine.

Aidha, Mkunga alisema matokeo ya utafiti huu yameonesha kiwango cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini kimeshuka kwa zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3 mwaka 2017.

Aliitaja miongoni mwa mikoa ya Tanzania Bara ambayo imeonyesha kuwa kiwango kikubwa cha watoto wenye malaria ni Kigoma  kwa asilimia 24.4 ikifuatiwa na Geita yenye asilimia 17.3, Kagera asilimia 15.4 na Mtwara asilimia 14.8 ambapo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe, Dodoma na Mikoa yote mitano (5)ya Zanzibar ina kiwango kidogo cha maambukizi ya malaria ya chini ya asilimia moja.

Alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza kiwango cha malaria, bado wanajamii wanatakiwa kutumia vyandarua ipasavyo katika kujikinga na ugonjwa wa malaria, kuondoa mitazamo potofu kama vile viuatilifu vinaleta kunguni na viroboto na kuwa vyandarua vinapunguza nguvu za kiume.
Utafiti huo umefanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wengine

WATU ELFU 15 WAJINYAKULIA ZAWADI KATIKA PROMOSHENI YA COKE STUDIO KUNYWA NA USHINDE

0
0
Washindi wa Televisheni katika Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde wakiwa na zawadi zao muda mfupi mra baada ya kukabidhiwa wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite Bottlers mjini Moshi
Washindi wa Televisheni katika Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho kujionea uzalishaji unavyofanyika.
 Sehemu ya kiwanda cha kuzalisha vinywaji baridi jamii ya Cocacola ,kiwanda cha Bonite Ltd mjini Moshi.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers mkoa wa Arusha,Boniface Mwase akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde walijinyakulia Televeisheni . 
Baadhi ya Washindi wa Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde wakimsikiliza Meneja Mauzo wa Kampuni ya vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers mkoa wa Arusha,Boniface Mwase wakati akitangaza majina ya washindi wa Televeisheni wakat wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo iliyofanyika katika kiwanda cha Bonite.
Mratibu wa Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers ,Leonard Makuka akikabidhi zawadi ya Televeisheni kwa Hadija Mmbughu ,mshindi katika promsheni ya Coke Studio kunywa na ushinde.
Mtathimini wa Biashara katika kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite Bottlers ,Japin Solank akikabidhi zawadi ya Televisheni kwa Mshindi katika Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde ,Mohamed Hussein ,mkazi wa Pasu mjini Moshi.
Mratibu wa Mauzo katika kampuni ya Vinywaji Baridi ya Bonite Bottlers ,Godfrey Amani akikabidhi zawadi ya Televisheni kwa mshindi wa Promosheni ya Coke Studio kunywa na ushinde ,Laurant Mlingi mkazi wa Arusha.
Baadhi ya zawadi za Televeisheini zilizotolewa kwa washindi.

 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

ZAIDI ya wateja 15,000 wa vinywaji baridi vinavyozalishwa na kampuni  ya  Bonite Bottlers Ltd ya mjini Moshi wamejishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya “Coke Studio kunywa na Ushinde “ inayoendelea .

Wateja hao wamejishindia zawadi baada ya kununua soda jamii ya Cocacola ,Fanta  na Sprite zikiwa katika ujazo wa mililita 350 na mililita 500 huku wengine 22 wakikabidhiziwa zawadi zao za Televisheni za kisasa za ukubwa wa inchi 32.

Hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao kutoka mikoa ya ,Arusha,Kilimanjaro na Manyara imefanyika katika viunga vya Kiwanda cha Bonite Bottlers Ltd na baadae washindi wote walipata nafasi ya kutembelea na kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za Bonite.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ,Boniface Mwase alisema wateja wa bidhaa zinazozalishwa na Bonite kila mmoja yupo kwenye nafasi ya kujishindia zawadi kwa kutumia kiasi cha Sh 500 na sh  1000.

“Zawadi ambazo tumezitoa leo (Jana)  ni televisheni 22 kwa washindi ambao wamejitokeza ,zipo zawadi za soda za bure ,zipo zawadi za fedha kiasi cha sh 5000 hadi 10,000,hizi zinatolewa pamoja hapo mteja anapokunywa soda anashinda papo hapo “alisema Mwase.

Alisema kumekuwa na hamasa kubwa kwenye shindano la Coke Studio kunywa na ushinde na washindi wameendelea  kupatikana kutoka maeneo yote ambayo bidhaa za  Bonite zinapatikana na kwamba kila atakayeshinda atafikishiwa zawadi yake kwa wakati.

Mwase alisema  Bonite imekuwa na utaratibu wa kufanya Promosheni kila mara lengo likiwa ni kurejesha seheu ya faida inayopata kwa wateja ambao wamekuwa wakiunga mkono kampuni hiyo kwa kutumia bidhaa zake.
“Nitoe wito kwa wateja wetu waendelee kutumia soda za jamii ya Coca Cola kwa sababu zawadi bado ni nyingi na kila mmoja ana nafasi ya kushinda.”alisema Mwase.

Zainaabu Lusoke ,mkazi wa Arusha ni mmoja wa washindi wa Televisheni katika promoshen ya Coke Studio kunywa na ushinde amesema zawadi hiyo inatokana na Mama yake mdogo aliyemtaka kuokota kizibo alichotupa pindi aliponunua Soda aina ya Fanta.

“Katika shindano hili sikutegemea kama nitashinda ,nilinunua soda nikatupa kile kizibo ,ma mdogo akaniambia kwa nini  unatupa ,nikamwambia hivi vizibo vya Bonite vimeandikwa Jaribu tena ,akaniambia kachukue kile kizibo ,ndipo nilipotizama nikakuta nimeshinda TV”alisema Zainabu.

Washindi waliojinyakulia zawadi za Televisheni ni pamoja na Mariam Mkara,Saumu Rashid ,Hadija Mmbughu,Emanuel Magige,Lightnes Lusega,Mwanahawa Miraji,Mohamed Hussein na Fadhili Lyimo.

Wengine ni Hilda Silayo,Judith Assey ,Haruna Mohamed,Nasibu Juma,Happy Kombe,Fii Mkwanda,Emanuel John,Nembris Simon,Godfrey Wilson ,Zainabu Salim,Rajabu Miraji,Said Massatu na Laurant Mlingi.

Mwisho.

WIKI YA MAJI,DC TUNDURU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI

0
0
 Mhandisi wa maji wa wilaya ya Tunduru Batholomeo Matwinga kushoto,akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa na Serikali katika kijiji cha Milonde kata ya Matemanga wilayani humo kwa Mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera aliyevaa suti   wakati wa kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Maji Nchini,
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akipanda ngazi kukagua ujenzi wa Tenki la kuhiafdhia maji katika kijiji cha Milonde wialayni humo wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji Nchini.
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Tenki la maji   katika mradi wa Maji kijiji cha Milonde kata ya Nakapanya wilayani humo,kulia aliyevaa kofia Mwenyeki wa Halmashauri ya wilaya Mbwana Mkwanda Sudi,na kushoto anayemsaidia Mhandisi wa Maji wa Wilaya Batholomeo Matwiga.picha na Muhidin Amri

NAIBU WAZIRI ULEGA ASISITIZA UKUAJI WA SEKTA YA MAZIWA MKOANI TANGA

0
0
Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amefanya ziara ya siku moja Mkoani Tanga na kukutana na mkuu wa mkoa huo Mh.Martine Shigella pamoja na kuzungumza na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU).

Mara baada ya kufika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga, Mhe. Ulega alipokea taarifa ya mkoa iliyoainisha pia changamoto zilizopo katika sekta ya mifugo na uvuvi mkoani humo, ambapo Bw. Shigella ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuzidi kutoa elimu kuhusu operesheni mbalimbali ambazo zinafanywa na wizara hiyo ili kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza kwa wananchi hususan kwa wanaofanya shughuli za uvuvi katika mwambao wa Bahari ya Hindi.

“Niiombe Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia kwako mhe. Naibu Waziri kumekuwa na operesheni ambazo zinafanyika mara kwa mara na wakati mwingine watu kulalamika kuonewa, ni vyema operesheni hizi zikaenda sambamba na utoaji wa elimu ili kuondoa malalamiko ya wananchi.” Alisema Bw. Shigella

Aidha Bw. Shigella amemfahamisha Naibu Waziri Ulega ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ni fursa kubwa ya kuwezesha uzalishaji wa maziwa katika Mkoa wa Tanga kupitia matumizi ya bandari na ubia na kiwanda cha Tanga Fresh, hivyo wizara haina budi kuwawezesha wafugaji kupata ng’ombe wa kisasa ili kuzalisha maziwa kwa wingi na kufaidika na ushirikiano huo.

Akibainisha hatua mbalimbali za Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuboresha sekta ya maziwa kwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Naibu Waziri Mhe. Abdallah Ulega amesema fursa mbalimbali zinazojitokeza mkoani Tanga ikiwemo ujumbe kutoka Rwanda kutumia bandari ya Tanga na kuweka ubia na kiwanda cha Tanga Fresh kutasaidia kukuza sekta ya maziwa mkoani humo.

“Kupitia uwekezaji huu uzalishaji wa maziwa utaongezeka na hivyo kuimarisha uchumi na kipato cha mwananchi kwa kuwa mahitaji ya maziwa yataongezeka hivyo lazima kuhamasisha zaidi ufugaji wa kisasa na wenye tija.” Alisema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega amesema kuhusu operesheni mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kulalamikiwa na baadhi ya watu kuonewa, amesema masuala ya operesheni yanafanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo yanajitokeza katika operesheni hizo hivyo yanafanyiwa utafiti ili kuainisha yale ambayo yataonekana hayaendani na hali halisi ya wakati huu.

Katika hatua nyingine, mara baada ya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella, Naibu Waziri Ulega alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh na baadae kuzungumza na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU).

Akizungumza na wanachama hao Mhe. Ulega amebainisha kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Dawati la Sekta Binafsi imeiuanganisha Benki ya Kilimo (TADB) na TDCU kutoa mikopo ya ng’ombe takriban 300 kwa wafugaji wa Mkoa wa Tanga ili kukuza uzalishaji wa maziwa katika mkoa huo.

“Tuna nia ya kuwawezesha zaidi wafugaji na sisi kupitia Dawati la Sekta Binafsi lililoanzishwa mwezi Oktoba mwaka jana, tuliwapatia lengo la kuhahakisha tunazalisha kiwango cha upatikanaji wa maziwa katika taifa letu na kufanikisha mkopo kati ya TADB na TDCU ambapo sasa mnakwenda kupata ng’ombe bora kabisa takriban 300.”

Aidha Mhe. Ulega amewataka wafugaji kuhakikisha wanatunza mifugo yao vyema na kuwapatia chanjo ili waweze kupata maziwa bora ambayo ndiyo yatawezesha kiwanda cha Tanga Fresh kuzidi kukua na kutoa bidhaa bora zaidi zitokanazo na maziwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) Bw. Hamisi Mzee amemwambia Naibu Waziri Ulega kuwa chama kinahakikisha kiwanda cha Tanga Fresh kinazidi kuimarika kwa kufuata kanuni za ubora wa maziwa tangu yanapotoka kwa ng’ombe hadi kufika kiwandani hapo.

Amesema uwepo wa kiwanda hicho ni fursa pekee kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga na maziwa hayo yamekuwa sehemu ya vitambulisho vikuu vya mkoa huo katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akishuhudia ng'ombe wa kisasa kwa mmoja wa wafugaji katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga, huku akishuhudiwa na mkuu wa mkoa huo Bw. Martine Shigella (katikati)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akishuhudia moja ya bidhaa zinazotegenezwa katika kiwanda cha Tanga Fresh

WAZIRI MKUU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ZAMBIA, ITALIA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Hassan Simba Yahya ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Italia Nchini, Mhe. Roberto Mengoni, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Mhe. Hassan Simba Yahya kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019.



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mheshimiwa Balozi Hassan Simba Yahya, ambapo amemtaka akaimarishe mahusiano baina ya nchi zote mbili.

Amekutana na Balozi Yahya leo (Jumamosi, Machi 23, 2019) katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za Kidiplomasia kati ya Tanzania na Zambia.

Pia, Waziri Mkuu amemtaka akakutane na wafanyabiasha wa Zambia na awahamasishe waje wawekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda. Amesema Balozi huyo anaweza kuandaa kongamano la biashara na uwekezaji kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Zambia ili kuboresha uchumi.

Kwa upande wake, Balozi Yahya amesema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Italia waje wawekeze nchini na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha. Ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Balozi Roberto Mengoni.

Akizungumza na Balozi huyo Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es salam, Waziri Mkuu amesema Tanzania ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye nchi hiyo. “Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini ili kukuza uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo tunawakaribisha wafanyabiashara waje wawekeze”.

Amesema Tanzania iko tayari wakati wote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wawekezaji watakaojitokeza kuwekeza nchini wanafanikiwa ili mataifa yote yaweze kufaidika, ambapo Ofisi yake kupitia Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji, Bibi Angela Kairuki yuko tayari kuwasikiliza na kuwasaidia wawekezaji wote wanaokusudia kuwekeza nchini.

Naye, Balozi Mengoniameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Italia, hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza na amesema wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa. 

WAZIRI MKUU AKIHAMASISHA WATANZANIA KUISHANGILIA TAIFA STARS HAPO KESHO UWANJA WA TAIFA

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAANDIKA HISTORIA YA KUWA TAASISI YA KWANZA KUZINDUA HUDUMA ZAKE KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikata utepe kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Mkuu-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro wameshiriki tukio hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakifurahia uzinduzi wa ofisi yao iliyojengwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma, mara baada ya Mhe. Mkuchika kuzindua ofisi hiyo.
Mwonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya TBA kulikabidhi jengo hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa kwenye ofisi yake iliyopo kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma mara baada ya kuizindua.
Mkurugenzi wa Ujenzi, Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Hamphrey Kilo akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) mara baada ya kumkadhi waziri huyo jengo hilo lililopo kwenye mji wa serikali jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akimkabidhi hati ya kiwanja mtumishi wake Bi. Zena Makaye, mara baada ya waziri huyo kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akimkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi yake Bw. Peter Mhimba, mara baada ya waziri huyo kuzindua rasmi ofisi yake iliyojengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi yake mbele ya ofisi aliyoizindua ambayo imejengwa kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma. Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Mkuu-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ni miongoni mwa waliojumuika katika picha hiyo.



Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeandika historia nchini ya kuwa taasisi ya kwanza kukabidhiwa jengo la ofisi yake na Wakala ya Majengo Tanzania (TBA) kwenye mji wa Serikali uliopo Mtumba jijini Dodoma, na jengo hilo kuzinduliwa rasmi na Waziri mwenye dhamana ya utumishi wa umma na utawala bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) kwa ajili ya kuanza kutoa huduma rasmi kwa wananchi na wadau wa masuala ya kiutumishi na utawala bora. 

Historia hiyo imeandikwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mara baada ya Mhe. Mkuchika kukabidhiwa rasmi jengo hilo na kukata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma zitakazoanza kutolewa na ofisi yake kuanzia tarehe 02 Aprili, 2019 katika jengo hilo lililopo kwenye mji wa Serikali jijini Dodoma. 

Mhe. Mkuchika amesema ofisi yake imetekeleza kwa vitendo agizo la ujenzi wa ofisi katika mji wa serikali, na hatimaye kuandika historia ya kuwa taasisi ya kwanza kukamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza na kuongeza kuwa, anaamini kwamba, ofisi yake ndio itakuwa ya kwanza kutoa huduma kwenye ofisi za wizara zinazojengwa katika mji huo wa Serikali. 

Mhe. Mkuchika amesisitiza kuwa, kuanzia tarehe 02 Aprili, 2019 yeye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kurugenzi za Utawala Serikalini, Uendelezaji Sera na Taarifa za Utumishi na Mishahara kwa pamoja wataanza kutoa huduma katika ofisi hizo. 

‘Kuanzia Aprili 2, mtumishi au mwananchi mwenye uhitaji wa kumuona Waziri, Naibu Waziri,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu afike katika ofisi za Utumishi mtumba ili aweze kuhudumiwa’, amefafanua Mhe. Mkuchika. 

Mhe. Mkuchika ameeleza kuwa, baada ya ofisi yake kuhamia, anaamini kwamba, ndani ya mwezi mmoja ujao wizara nyingi zitakuwa zimehamia rasmi na hatimaye wananchi na watumishi kutoka katika maeneo mbalimbali nchini watahitaji huduma ya usafiri kuja kwenye mji wa serikali ili kupata huduma, hivyo ametoa wito kwa mara nyingine tena kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri jijini Dodoma kuchangamkia fursa hiyo. 

Aidha, katika kuwawezesha watumishi wa ofisi yake kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa karibu na ofisi iliyojengwa, Mhe. Mkuchika alitumia fursa hiyo kuwapatia hati za viwanja watumishi ambao ofisi imewarahisishia mchakato wa kununua viwanja vya serikali vilivyopo mtumba katika mji wa serikali ili watumishi hao wawe na makazi bora yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu. 

Mhe. Mkuchika ametoa rai kwa watumishi wote wa umma waliohamia jijini Dodoma, kuhakikisha wanajipatia viwanja vilivyopimwa na serikali na kujenga nyumba bora ili kuishi kwa staha na kulinda hadhi ya kuwa watumishi wa umma. 

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameishukuru Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kukamilisha ujenzi kwa wakati na kwa kiwango bora na hatimaye kukabidhi ofisi rasmi ili ziweze kutoa huduma kwa wananchi. 

Dkt. Mwanjelwa amewashukuru na kuwapongeza watumishi wote wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ushirikiano waliouonesha kwa menejimenti tangu mwanzo wa ujenzi mpaka ofisi imekamilika na kuwataka kuendelea na utamaduni huo wa ushirikiano. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewashukuru watumishi wote wa ofisi yake kwa kushiriki kikamilifu katika kufanikisha ujenzi huo na amewapongeza watumishi hao kwa kutenga muda wao ili kushiriki katika zoezi la upandaji miti kwenye ofisi hiyo lililofanyika wakati ujenzi ukiendelea. 

Awali, akiwasilisha taarifa fupi ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya Utumishi, Mkurugenzi wa Ujenzi, Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Hamphrey Kilo amesema, ujenzi ulianza rasmi mnamo tarehe 26 Disemba, 2018 na kutarajiwa kukamilika tarehe 22 Machi 2019, tarehe ambayo ndio wamekabidhi jengo ambalo kwa mujibu wa mkataba, kazi zote zilizoanishwa zimekamilika kwa kiwango bora. 


IMETOLEWA NA; 
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI 
OFISI YA RAIS (UTUMISHI) 
TAREHE 23 MACHI, 2019

NCHI YA CUBA KUENDELEA KUIMAIRISHA USHIRIKIANO WAKE WA KIDIPLOMASIA NA TANZANIA

0
0
Cuba itaendelea kudumisha ushirikiano wake wa Kidiplomasia na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika mafungamano ya kustawisha Wananchi wake licha ya Taifa hilo la Caribean kipindi hichi kupita katika mabadiliko ya Kisiasa, Uchumi na Utamaduni.
Rais wa Bunge la Cuba Mheshimiwa Esteban Lazo Harnandez alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  aliyefika kusalimiana nae pamoja na  kumpongeza baada ya kuchaguliwa tena kuliongoza Bunge hilo hapo katika Ofisi ya Bunge hilo Mjini Havana Nchini Cuba.
Mhe.Esteban Lazo Harnandez alisema kutokana na mabadiliko ya mfumo wa Dunia uliopo hivi sasa katika masuala ya Uchumi, Siasa na Utamaduni Jamuhuri ya Cuba imelazimika kufanya mabadiliko ya Katiba yake ili yalingane na mfumo huo wa Dunia inayozunguuka katika mazingira ya Kijiji.
Alisema Bunge ya Cuba tayari limeshafanya marekebisho katika Katiba yake kutoa nafasi kwa Wananchi wake kuwa na Uwezo na Uhuru wa Kumiliki Nyumba Ardhi pamoja na uwepo wa Waziri Mkuu atakayekuwa na Mamlaka ya kusimamia utendaji wa Serikali.
Mheshimiwa Esteban alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba wakati Vikao vya Bunge hilo vinatarajiwa kuanza Wiki ijayo baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Wabunge wake, Serikali ya Nchi hiyo imeanza kupiga hatua kubwa zaidi ya Maendeleo kutokana na Mabadiliko hayo.
Rais huyo wa Bunge la Cuba alisisitiza kwamba Taasisi za Kifedha zitalazimika kuzingatia ukusanyaji bora zaidi wa Mapato katika maeneo yote ya Uchumi ili ushiriki wa Wananchi waliowengi katika katika mfumo huo wa kifedha upatikane vyema.
Mheshimiwa Esteban alimuhakikishia Balozi Seif  kwamba ule uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili utaendelea kuimarishwa na kukuzwa katika muda wote.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema Zanzibar na Tanzania kwa ujumla zitaendelea kufuatilia Mabadiliko ya Cuba na kuangalia hatua inayoweza kuiga mabadiliko hayo katika azma ya kuimarisha Uchumi na Ustawi wa Wananchi walio wengi.
Balozi Seif  katika mazungumzo hayo alimpongeza Rais wa Bunge hilo la Cuba Mheshimiwa Esteban Lazo Harnandez kwa kuchaguliwa tena kushika wadhifa huo ikionyeshawazi  ishara halisi ya kukubalika vyema na Wananchi wa Nchi hiyo kupitia Viongozi wake.
Balozi Seif na Ujumbe wake alimalizia ziara yake Nchini Cuba kwa kufanya mazungumzo na Uongozi wa Waziri wa Afya wa Nchi Hiyo ukiongozwa na Naibu Waziri wake Bibi Marcia Cobas hapo Makao Makuu ya Wizara ya Afya Mjini Havana Nchini Cuba.
Katika mazungumzo yao ya ushirikiano wa Kidugu Balozi Seif alisema matunda ya Darasa la Madaktari Wazalendo waliosimamiwa na Wataalamu pamoja na Wahadhiri wa Nchi ya Cuba yameanza kutoa Matumaini.
Balozi Seif alisema  Kitendo cha Serikali ya Cuba kukubali kupunguza gharama kubwa ya kuwaendeleza Madaktari hao Wazalendo wapatao 15 katika Shahada ya juu ya Udaktari wa Uzamili Nchini humo kinaendelea kuleta faraja kubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Watu wake.
Alisema wakati Zanzibar ikiendelea kutekeleza Sera ya Afya ya kuwa na miuondombinu ya huduma za Afya katika umbali usiozidi Kilomita Tano kundi hilo na Madaktari linaloendelea kuongezeka kila Mwaka litakuwa Mkombozi wa utekelezaji wa Sera hiyo muhimu.
Naye Kaibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Asha Ali Abdullah aliueleza Uongozi huo wa Wizara ya Afya Cuba kwamba Zanzibar hivi sasa inapita katika kipindi cha kujiimarisha kwenye mapambano yake dhidi ya Maradhi yasiyoambukiza.
Bibi Asha alisema maradhi yasiyoambakiza kama Kisukari pamoja na shindikizo la Damu hivi sasa yamekuwa yakiathiri Wananchi walio wengi na kuleta vifo vingi jambo ambalo jitihada zinachukuliwa katika kuona kasi hiyo ya athari inapungua au kuondoka kabisa.
Alisema kwa upande wa maradhi ya Malaria hivi  sasa yamepungua kutokana na Kampeni kubwa iliyochukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na Taasisi na Mataifa wahisani katika kuangamiza vilui lui vya maradhi hayo.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar alimuhakikishia Naibu Waziri wa Afya wa Cuba kwamba ushauri wote walioupata katika ziara yao kwenye Taasisi za Afya Nchini Cuba likiwemo suala la Upatikanaji wa Dawa litazingatiwa na iwapo linaweza kuleta fueni ya gharama kwa Zanzibar watalichukulia hatua mara moja.
 Rais wa Bunge la Cuba Mheshimiwa Esteban Lazo Harnandez kulia mwenye shati nyeupe akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Ofisi yake kufanya mazungumzo ya Ushirikiano.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Rais wa Bunge la Cuba Mheshimiwa Esteban Lazo Harnandez Mjini Havana Nchini Cuba.
 Mheshimiwa Esteban Lazo Harnandez kulia akipokea zawadi ya Mlango wa Zanzibar kutoka kwa Balozi Seif kama ishara ya kufunguliwa milango ya kutembelea Zanzibar.
 Mheshimiwa Esteban Lazo Harnandez akimtembeza Balozi Seif sehemu mbali mbali za Jengo la Bunge ya Cuba lenye Historia ya muda mrefu ambazo zimewekwa kama kumbu kumbu ya Taifa hilo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Pili kutoka kulia na Ujumbe wake akifanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Afya Mjini Havana Nchini Cuba.Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mkuu wa Utafiti Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Mayasa, Kulia ya Balozi Seif ni Katibu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Asha Ali Abdullah na Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Dr. Juma Salum Mbwana {Mambi}.Wa Kwanza kutoka Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya wa Cuba Bibi Marcia Cobas.
Naibu Waziri wa Afya wa Cuba Bibi Marcia Cobas akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara  baada ya kumaliza mazungumzo yao mwisho mwa ziara ya Ujumbe wa Zanzibar Nchini Cuba.Picha na – OMPR – ZNZ.

Mradi wa majitaka Mwanza wavutia wageni kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.

0
0
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) imepokea ugeni kutoka Asasi zisizo za Kiserikali kutoka Brazil, Afrika Kusini, Kenya na Uganda ambao umevutiwa na ubunifu uliyotumika katika ujenzi wa mradi wa Mfumo rahisi wa uondoshaji majitaka kwenye maeneo ya milimani unaofahamika kitaalam kama 'Simplified Sewerage System'.

Hayo yamebainishwa Machi 22, 2019 na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Dkt. Tim Ndezi ambaye alikuwa mwenyeji wa ugeni huo kwa hapa nchini.

Dkt. Ndezi alisema mradi wa majitaka wa simplified sewerage umeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa mataifa mbalimbali kote ulimwenguni.

Alisema taasisi zinazojishugulisha na masuala ya usafi wa mazingira kutoka nchi mbalimbali baada ya kupata sifa za mradi huo wa Mwanza zimevutika kujifunza zaidi ubunifu uliotumika katika utekelezaji wake ili pia kuutumia katika nchi wanazotoka. "Wageni hawa wamekuja kujifunza namna ambavyo mradi huu umejengwa ili nao wakaandae mradi wa namna hii kwenye nchi zao," alisema Dkt. Ndezi.

Mradi huo wa Simplified Sewerage umeendelea kutembelewa na wageni kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo la kujifunza namna ukivyotekelezwa na namna ambavyo unaendeshwa.Kwa mujibu wa Dkt. Ndezi ni kwamna ugeni huo vilevile ulilenga kuzungumza na wanufaika wa mradi huo ili kufahamu wajibu wao na namna ambavyo waliupokea na njia wanazotumia kuutunza. 

Hii ni mara ya pili kwa mwaka huu 2019 mradi huo kutembelewa na ugeni kutoka nje ya nchi kwani hivi karibuni MWAUWASA ilipokea ugeni kutoka Kenya ambao ulifika kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kutekeleza mradi wa majitaka hususan kwa maeneo yasiyo rasmi. 

Ugeni huo wa awali kutoka Nchini Kenya ulieleza namna ulivyovutiwa na ubunifu mkubwa uliyotumika katika ujenzi wa mradi wa majitaka kwenye maeneo ya milimani na kuahidi kurejea tena na wataalam wa mamlaka zinazohusika ili kujenga miradi ya namna hiyo nchini mwao. 

Akizungumza mmoja ya wageni hao kutoka Uganda, Mundamba Omar alisema nchini humo ipo changamoto ya wananchi hususan wa kipato duni kukosa mfumo bora na rasmi wa uondoaji wa majitaka na kwamba ziara hiyo waliyoifanya Jijini Mwanza imewapatia uzoefu na ujuzi wa namna ya kujenga na kusimamia mradi mzuri wa majitaka. 

"Tunaipongeza MWAUWASA, kazi iliyofanyika hapa ni ya kipekee hatuna budi nasi kuiga," alisema Omar. Itakumbukwa kuwa Mradi huo wa Simplified Sewerage ulikuwa miongoni mwa miradi miwili bora zaidi kuwahi kutekelezwa Barani Afrika chini ya ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendeji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga ujenzi wa mradi huo ulianza Mwaka 2016 na umenufaisha Kaya zipatazo 415.Mhandisi Sanga alisema mradi huo wa Simplified Sewerage ulijengwa kwa majaribio kwenye maeneo matatu ambayo ni Kilimahewa, Mabatini na Igogo. 

Katika maeneo hayo matatu, Mhandisi Sanga alisema mwitikio ulikua mzuri na alitolea mfano kwa Kilimahewa ambapo MWAUWASA ilipanga kuunganisha Kaya 68 lakini kutokana na mwitikio kuwa mkubwa Kaya 117 ziliunganishwa na kwa upande wa Mabatini mpango ulikua ni kuungnisha Kaya 88 hata hivyo zaidi ya Kaya 178 ziliunganishwa na kufikia jumla ya Kaya 415 kwenye maeneo yote matatu.

Hata hivyo Mhandisi Sanga anabainisha kwamba awamu ya pili ya ujenzi wa mradi huo itahusisha maeneo mengi zidi ambayo ni Kabuhoro, Ibungilo, Kawekamo na Isamilo. 

"Maeneo ambayo tulianza nayo kwenye awamu ya kwanza nayo hatujamaliza, kwahiyo haya ni maeneo mapya lakini pia tutarudi kwenye hayo maeneo ya awali tukaunganishe Kaya zilizosalia," alibainisha Mhandisi Sanga. Akielezea sababu za mradi huo kuitwa simplified, Mhandisi Sanga alisema kwamba mradi ulipunguza baadhi ya vigezo kwenye miongozo ya usanifu miradi kutoka Wizara ya Maji. 

"Ukivifuata vigezo vyote kama vilivyo kwenye miongozo inakua ngumu kutekeleza mradi kwenye maeneo ya namna hiyo," alisema Mhandisi Sanga. 
Aliongeza kwamba changamoto iliyopo kwenye Jiji la Mwanza ni kwamba zaidi ya asilimia 70 ya maeneo hususan ya milimani hayajapimwa na hivyo kusababisha ujenzi wa miradi kuwa mgumu. 

Alibainisha kwamba kwa Tanzania, Jiji la Mwanza ni la kwanza kutekeleza miradi ya namna hiyo na kwamba kwa duniani miradi ya namna hiyo inapatikana Nchini Brazili. Mhandisi Sanga alisema lengo mahsusi la mradi huo ni kuondosha majitaka kwa njia rahisi kutoka kwenye maeneo ya milimani ili kuwaepusha wakazi na maradhi yanayoweza kutokea kutokana na mfumo usio rasmi wa uondoshaji wake. 

"Lazima tuhakikishe majitaka yanatolewa na yanatibiwa kwakuwa haya yanaweza kuwa ni hatari kwani mara nyingine hua ni chanzo kikuu cha maradhi," alisema. Alimalizia kwamba hapo awali uondoshaji wa majitaka kwenye maeneo ya milimani Jijini Mwanza ulionekana kuwa mgumu na kutowezekana." Ni lazima tuwe na majawabu kwenye maeneo ambayo hapo zamani ilionekana hayawezekani kabisa," alisema Mhandisi Sanga.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mbugani, Athumani Jama alisema hapo zamani kabla ya mradi hali ilikuwa ni chafu hasa ikizingatiwa hali halisi ya kijiografia ya maeneo hayo ya milimani. “Walikuwa wakichimba vyoo vifupi na wakati wa mvua hali inakuwa tete sana, maji yalikuwa yanatiririka ovyo na magonjwa ya mlipuko yalikuwa ya kufikia tu,” alisema Jama. 

Wananchi waliozungumza wakati wa ziara ya ugeni huo waliiomba MWAUWASA kuharakisha ujenzi wa mradi mpya ili Kaya nyingi zaidi zinufaike.

 Ugeni kutoka Brazili, Afrika Kusini, Kenya na Uganda ukiwa katika moja ya eneo lenye mradi wa majitaka wa simplified sewerage Jijini Mwanza. Huu ni ugeni wa pili kutoka nje ya Tanzania uliyotembelea mradi huo kwa Mwaka huu 2019.

KAMANDA SHANA AANZA NA 'MATAPELI WA DOLLAR' BANDIA

0
0
Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa Machi 21,2019 lilifanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni Ladislaus Peter Mkimu na William Ngalivuva wote wakazi wa jiji la Arusha kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi (ACP) Jonathan Shana, alisema kwamba tukio hilo lilitokea muda wa saa 4:00 Asubuhi katika eneo la Mjini Kati jirani na hospitali ya Saint Thomas.

“Mara baada ya kupata taarifa toka kwa msiri, askari wetu walianza kufuatilia na walipogundua waliweka mtego uliofanikisha kuwakamata watuhumiwa hao, ambao awali walikutwa na kiasi kidogo cha noti hizo na katika mahojiano watuhumiwa hao walikiri kuwa na noti nyingine kwenye makazi yao eneo la Lemara ambapo zilipatikana noti 1,697’’. Alisema Kamanda Shana.

“Jumla ya noti hizo bandia zilizopatikana ni Dola 16,200 zenye thamani ya fedha za kitanzania Shilingi 37,260,000 na zingeweza kuleta athari kubwa katika uchumi wa nchi yetu”. Aliongeza Kamanda Shana.

Aidha alitoa onyo kwa wahalifu wa aina hii kwamba Jeshi la Polisi lipo macho saa Ishirini na Nne na litaendelea kufanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kuwakamata wahusika pamoja na mitambo yao.

Mimi kama Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha nitahakikisha kabla ya wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na Watalii hawajaingiwa hofu juu ya watu wa namna hii sisi tutakuwa tumeshawachukulia hatua”.
“Wale wanaopenda kuvuna pasipo kupanda, wanaopenda kutawanya pasipo kukusanya mwisho wao umefika”. Alionya Kamanda Shana.
 Dola bandia zilizokamatwa jijini Arusha, baada ya Askari Polisi kuweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana akiwaonyesha waandishi wa habari noti bandia ambazo zilikamatwa juzi eneo la Mjini Kati jijini Arusha.

Wafungwa Gereza Songwe Walima Ekari 750 za Mahindi

0
0
Jumla ya ekari 750 za mahindi zimelimwa katika Gereza la Kilimo Songwe ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka magereza yatumike kwa shughuli za uzalishaji ikiwemo kilimo kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa waliopo magerezani.

Akisoma taarifa mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Gereza hilo ,Mrakibu Mwandamizi, Peter Anatory alisema kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa jumla ya ekari 750 za mahindi zimelimwa ikiwa ni kwa matumizi ya chakula kwa wafungwa ambapo wanatarajia kulisha na magereza mengine.

“Tunaendelea vizuri na kilimo na kama maelekezo ya Mheshimiwa Rais yalivyotufikia ni kweli tunatumia wafungwa ambao tumewapangia zamu katika shughuli hizi za kilimo,tunategemea kulisha magereza saba baada ya mavuno huku jumla ya ekari 750 zimelimwa mahindi hapa” alisema SSP Anatory

Pia aliitaka serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya zana za kilimo ikiwepo matrekta ili kukamilisha ekari 250 zilizobaki ili kuweza kukamilisha ekari 1000 zilizopo katika gereza hilo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema Gereza la Songwe ni moja kati ya magereza kumi nchini yaliyoteuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano kuendeleza kilimo cha mkakati lengo ni kuwezesha magereza yote nchini kuzalisha vyakula kwa ajili ya kulisha wafungwa na mazao yanayoweza kuwaletea kipato badala ya kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

“Agizo la Rais Dkt.Magufuli ni kuona magereza yanajitosheleza kwa chakula kupitia wafungwa, nawapongeza kwa ekari mlizolima mahindi na kama wizara tunaahidi kulishughulikia suala la zana za kilimo ikiwemo matrekta, na gereza lenu ni moja kati ya magereza kumi ya kimkakati na mnaendelea vizuri” alisema Masauni

Mbali ya kilimo Gereza la Songwe pia linajishughulisha na ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, sungura na simbilisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akielekea kukagua mahindi yanayolimwa na wafungwa katika Gereza la Kilimo Songwe kwa ajili ya chakula cha wafungwa nchini. Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi, Peter Anatory. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akizungumza na Mkuu wa Gereza la Kilimo Songwe, Mrakibu Mwandamizi, Peter Anatory (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua shamba katika gereza hilo kwa ajili ya chakula cha wafungwa nchini. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Mbeya.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MWANAHARAKATI FLORA LAUWO APOKELEWA KWA SHANGWE JIJINI MWANZA BAADA YA KUREJEA KUTOKA OMAN

0
0
 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee Foundation ya Jijini Mwanza, Flora Lauwo asubuhi ya leo Machi 23, 2019 amepokelewa kwa shangwe katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea nchini Oman alikokuwa amealikwa kutokana na mchango wake mkubwa wa kusaidia watu mbalimbali wenye uhitaji katika jamii kupitia taasisi yake.

Mwezi mmoja uliopita, Lauwo kupitia Ubalozi wa Tanzania alialikwa nchini Oman ambapo Machi 08, 2019 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani alipatiwa tuzo mbili za kama ishara ya kutambua mchango wake wa kuwasaidia wenye uhitaji katika jamii.

Pia kwenye maadhimisho hayo (Siku ya Wanawake Duniani 2019), Lauwo alipewa tuzo kupitia tamasha la Binti Filamu lililofanyika Jijini Mwanza na hivyo kufanya idadi ya tuzo alizopokea mwaka huu kuwa tatu. Lauwo pia amewahi kushinda tuzo ya Malikia wa Nguvu inayotolewa na Clouds Media Group.

TANZANIA YAENDELEA KUSHIKILIA CHETI CHA UBORA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA USAFIRI WA ANGA KUPITIA TMA

0
0
Na Karama Kenyunko. Globu ya Jamii
WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi  na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe amesema utabiri sahihi wa hali ya hewa nchini Tanzania unaofanywa na mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), umeiwezesha  Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ya tatu barani kutunukiwa  cheti cha ubora wa huduma za hali ya hewa katika usafiri wa anga. (ISO 9001:2015)na hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Viwango Duniani(ISO.)

Akizungumza leo Machi 23 mwaka huu wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani,  Mhandisi Kamwelwe amesema, ili kuhakikisha wananchi wanaelewa umuhimu wa hali ya hewa serikali imeendelea kuwekeza katika kuboresha huduma za hali ya hewa kwa matumizi ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya anga, Kilimo na miundombinu ya uangazi.
 Amesema, kwa kuhakikisha hilo  serikali imenunua Radar mbili za hali ya hewa ambazo zimewekwa Dar es Salaam na Mwanza huku Radar nyingine tatu ambazo ziko katika hatua ya ununuzi zinatarajiwa kuwekwa katika mikoa ya Mtwara, Mbeya na Kigoma.

"Siku ya hali ya hewa Duniani ni muhimu sana kwani inatupa nafasi ya kutafakari mchango wa Tanzania kama mwanachama wa WMO katika utoaji wa huduma za hali ya hewa hapa Tanzania na ulimwenguni kote" amesema Kamwele.

Kamwelwe amesema katika sekta ya usafiri wa anga mwaka huu Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi tatu barani Afrika zilizopata cheti hicho.

"Kauli mbiu ya mwaka huu ya ‘Jua, Dunia na hali ya hewa imelenga  kutoa elimu kwa jamii na kuongeza uelewa wa sayansi ya hali ya hewa hususani maandalizi, usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa,”amesema Kamwelwe.

Amesema ni dhahiri kwamba huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) zimeendelea kuongeza viwango vya ubora ikiwa ni pamoja na usahihi wa utabiri na zinafaa kutumika katika sekta mbalimbali za maendeleo hapa nchini.

“Katika maadhimisho haya ya 69 ya hali ya hewa duniani ya kauli mbiu ya mwaka huu ‘JUA,Dunia na hali ya hewa’ ambayo imelenga kutoa elimu kwa jamii na kuongeza uelewa wa sayansi ya hali ya hewa hususani maandalizi, usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa,”amesema Kamwelwe.

Ameongeza kuwa, pamoja na mafanikio hayo bado kuna changamoto nyingi zikiwemo  gharama kubwa za vifaa vya hali ya hewa, kuendana na mabadiliko ya kukua kwa teknolojia katika tasnia ya hali ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi ambapo utatuzi wa changamoto hizo unahitaji jitihada za pamoja za wadau.

 Mkurugenzi Mkuu wa TMA,Dk Agness Kijazi amesema TMA  imepata mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kuendelea kumiliki cheti cha Ubora ISO 900;2015 ambapo Tanzania imekuwa nchi ya tatu barani Afrika kufikia viwango vya ubora hiyo ni mpya iliyotolewa na Shirika la Viwango Duniani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari amesema,  Huduma za hali ya hewa zimekuwa ni msaada mkubwa sana katika sekta ya anga hasa kwa kuepusha majanga hasa safarini na kufanya ajali katika sekta hii kuwa chache, "kwa rubani kabla hajaanza safari lazima tupate huduma za hali ya hewa katika njia ambayo atapaswa kupita ili wafike salama na iwapo hali ya hewa ikiwa mbaya basi rubani hataruhusiwa kisafiri" ameeleza Johari

Pia  Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini, (TAA), Elias Mwashiuya amesema, mpaka sasa kuna viwanja 58 na katika viwanja hivyo msingi mkuu ni hali ya hewa. "Tunaangalia kulingana na hali ya hewa pia wanazingatia takwimu za hali ya hewa kulingana na aina ya ndege. Pia tunapata taarifa za kila baada ya saa sita ili kuweza kujua hali ya anga zitakazomuwezesha rubani kutua au kuruka" amesema.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la uwakala wa meli Tanzania, Eng.Japhet L Loisimaye (OLe) amesema utabiri wa Hali ya hewa unaofanywa na TMA umekuwa ukisaidia sana vyombo vya majini kwani haviruhusiwi kuanza safari kabla havijapata utabiri wa hali ya hewa. Kwani wamekuwa wakisimamisha safari za vyombo vya baharini bila kujali hasara watakayoipata bali wanahakikisha na  kuangalia usalama wa wananchi kwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (kushoto) akizungumza na wadau wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto) akizungumza na wadau wa TMA katika maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Kulia ni wadau wa TMA wakiwa kwenye maadhimisho hayo.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Eng. Japhet Loisimaye akielezea namna taarifa zinazotolewa na TMA zinavyowasaidia wadau wa mamlaka hiyo kutekeleza majukumu yao, kwenye hafla ya maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na TMA jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Elias Mwashiuya (kulia).
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari (katikati) akielezea jinsi taarifa zinazotolewa na TMA zinavyowasaidia wadau wa usafiri wa anga kutekeleza majukumu yao, kwenye hafla ya maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na TMA jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Eng. Japhet Loisimaye (kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Dk. Buruhani Nyenzi (kushoto) akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (katikati) mara baada ya kuwahutubia wadau wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Dk. Kijazi akifuatilia.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images