Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

MHESHIMIWA KAIRUKI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO WA KUWASIADIA WANAWAKE WALIOFANYIWA UKATILI

0
0
Mheshimiwa Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akisoma hotuba yake kwa wadau mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa kijitabu cha MWONGOZO WA KUWASIADIA WANAWAKE WALIOFANYIWA UKATILI kilichoandaliwa na Chama cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC). Hii ni katika mwendelezo wa Kampeni ya Siku 16 za Kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto aliyoizindua hivi Karibuni. Katika picha aliyekaa kushoto kwa Mhe. Kairuki ni Mama Nakazaeli Tenga, Mwenyekiti wa Bodi ya WLAC.
Mama Mama Nakazaeli Tenga, Mwenyekiti wa Bodi ya WLAC akitoa maelezo ya awali kuhusu kijitabu cha MWONGOZO WA KUWASIADIA WANAWAKE WALIOFANYIWA UKATILI huku Mheshimiwa Kairuki (aliyekaa) akifuatilia kwa makini.
Mheshimiwa Kairuki akiwaongoza viongozi wa WLAC na wadau wake katika kuinua kijitabu cha MWONGOZO WA KUWASIADIA WANAWAKE WALIOFANYIWA UKATILI kuashiria uzinduzi rasmi wa kijitabu hicho.

Rais Kikwete alipokeam kombe la Dunia jijini Mwanza leo

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilifunua na kulinyanyua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo wa CCM Kirumba mjini Mwanza leo jioni(picha na Freddy Maro)

Balozi Kamala amtembelea Balozi wa Sweden Tanzania

0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Mhe Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Sweden Tanzania Mhe Lennarth Hjelmaker ofisini kwake Dar es salaam,wakati walipokutana kwa mazungumzo.

KIKAO MAALUM CHA KUPITIA RASIMU YA MABORESHO YA JESHI LA MAGEREZA CHA FUNGWA RASMI MKOANI MOROGORO

0
0
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile akitoa hotuba fupi ya ufungaji wa Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza leo Novemba 29, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba ya Ufungaji wa Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza iliyotolewa na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile( hayupo pichani) kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini.
Afisa Mkuu wa Mipango wa Jeshi la Magereza, Bw. Boniface Mkumbo( wa tatu kushoto) akiteta jambo na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza mara baada ya kufungwa rasmi Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza leo Novemba 29, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Morogoro.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kikao Maalum cha kupitia rasimu ya Maboresho ya Jeshi la Magereza mara baada ya kufunga rasmi Kikao hicho leo Novemba 29, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Morogoro( wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Haji Janabi(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine( wa kwanza kulia) ni Mchambuzi Kazi Mkuu toka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

KAMATI ZA MAADILI ZAWATAKA WANACHAMA WA TFF KUBADILI KATIBA ZAO

0
0
Wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wanatakiwa kufanyia marekebisho katika katiba zao kwa kuingiza ibara ya Kamati za Maadili.

Maagizo hayo yanatokana na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyoketi Novemba 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jamal Malinzi ambapo pamoja na mambo mengine ilijadili umuhimu wa wanachama wake kuunda kamati hizo.

Wanachama wa TFF ambao muda wao wa uchaguzi umekaribia, wanatakiwa kufanya marekebisho hayo kwanza kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi.

TFF ina aina tatu za wanachama. Wanachama hao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na Klabu za ligi Kuu.

FAINALI YA KOMBE LA UHAI CHAMAZI
Mechi ya Fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu itachezwa keshokutwa (Jumapili) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Coastal Union ndiyo itakayocheza fainali hiyo kuanzia saa 9.30 alasiri dhidi ya mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili kati ya Yanga na Mtibwa Sugar inayotarajia kuchezwa baadaye leo.

Mechi ya fainali itatanguliwa na ile ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Azam na timu itakayoshindwa katika mechi ya pili ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu iliyoanza katika viwanja vya Karume na DUCE kabla ya kuhamia Chamazi.

3 RD EAC MEDIA AWARDS WINNERS CROWNED

BALOZI MODEST MERO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA MKUU WA SHIRIKA LA BIASHARA YA KIMATAIFA DUNIANI

0
0
Mheshimiwa Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva amewasilisha hati za utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.

Katika mazungumzo, Mkurugenzi Mkuu amemfahamisha Mh. Balozi kuwa Shirika la Biashara Duniani liko katika hatua za mwisho kukamilisha majadiliano ya mikataba ya Biashara ya Kimataifa katika maeneo matatu kwa pamoja ikiwa ni masuala ya Kilimo, Maendeleo na Uwezeshaji Biashara.

Aidha, Mkurungenzi Mkuu alielezea mahusiano mazuri aliyonayo na nchi yetu kwa kipindi kifupi akiwa kama Mkurugenzi Mkuu, na kuwa aliliona hilo wakati wa kampeini yake alipokuja nchini kuomba kura yetu.

Ni kwa mantiki hiyo na imani aliyo nayo kwa Tanzania, Mkurugenzi huyo ameomba Tanzania itumie ushawishi wake ili kufanikisha mkutano wa Mawaziri wa Biashara utakaofanyika mjini Bali Indonesia kuanzia tarehe 3-6 December 2013, ili kupitisha mikataba ya Biashara katika maeneo matatu yaliyotajwa hapa juu.
Balozi akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo.
Balozi Mero na Bw. Azevedo katika mazungumzo.
Picha ya pamoja Balozi Mero, Mama Mero na Bw. Azevedo.

Rais Kikwete awasili Jijini Kampala Kuhudhuria Mkutano wa EAC

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Wakuu wan chi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(Photos by Freddy Maro)

DKT.BILAL AENDESHA ZOEZI LA HARAMBEE YA KUCHANGIA MADAWATI MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU JIMBO LA NKENGE

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi chaeti, Mkurugeniz wa Kagera Sugar, Bw. Hamadi Yahaya, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuchangia maendeleo ya Elimu ya Jimbo la Nkenge mkoa wa Kagera,wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali (mst) Fabian Masawe. Jumla ya Shilingi milioni 114, pesa taslimu milioni 65.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe. 
 - Sehemu ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
 Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
 Meza Kuu wakijumuika kuimba wimbo maalumu wa mkoa wa Kagera wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo, hususan katika suala la elimu na kuchangia madawati.
Msanii Saida Karoli na kundi lake wakiburudisha wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Picha na OMR.

1331 WAHITIMU FANI MBALIMBALI KATIKA CHUO CHA SERILALI ZA MITAA HOMBOLO DODOMA

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kulia ) mwenyekiti wa bodi ya chuo cha serikali za mitaa Hombolo Ndg. Ramadhani  Khalfan (kulia ) , meza kuu na halaiki yote iliohudhuria mahafali ya tano chuoni hapo wakiimba wimbo wa taifa tayari kuanza mahafali.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi kwa mamlaka aliyopewa akitunuku astashahada na stashahada kwa jumla ya wahitimu 1331 walihitimu fani za utawala,  usimamizi rasilimaliwatu, uhasibu na fedha na maendeleo ya jamii katika mamlaka ZA serikali za mitaa, katika chuo CHA serikali za mitaa hombolo jana,  Mkuu wa Mkoa alifanya kazi hiyo kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI.
 Baadhi ya wahitimu  wakipongezana kwa furaha baada ya kumalizika kwa mahafali ya tano ya chuo CHA serikali za mitaa Hombolo. 
PICHA ya pamoja Mkuu wa Mkoa, bodi ya chuo, uongozi wa chuo, wanataaluma na wwfanyakazi wa chuo CHA serikali za mitaa hombolo mud mfupi baada ya kumalizika kwa mahafali ya tano chuoni hapo. 
Picha na Jeremiah Mwayoma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.

TAMKO LA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA LINDI NA KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIET

Mhe Angela Kairuki afungua mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume

0
0
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Angelah Kairuki akifungua Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume
 Mwenyekiti wa Tume Mhe Jaji Aloysius Mujulizi akisoma taarifa yake wakati wa kufungua mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya Tume
  Baadhi ya Wastaafu wa Tume wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 30 ya Tume. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

HOTUBA YA RAIS WA TFF KUPOKEA KOMBE LA DUNIA

Rais azungumza na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Daniel Ole Njooley.

0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Daniel Ole Njooley,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana  na  Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Daniel Ole Njooley,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar  leo. 
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Maalim seif ahudhuria mahafali katika skuli ya Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam, ahani msiba wa Mhe Philip Mangula leo.

0
0
  Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne katika skuli ya Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam.
 Baadhi ya wahitimu wa maandalizi katika skuli ya  Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne katika skuli ya Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam.

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ya pamoja na uongozi wa skuli pamoja na baadhi ya wahitimu wa skuli ya Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akitia saini kitabu cha maombolezi kufuatia kifo cha mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)  Peter Philip Mangula.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimpa pole Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)  Bw. Philip Mangula, alipofika nyumbani kwake Ostabey Dar es Salaam, kufuatia kifo cha mtoto wake Peter Philip Mangula. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Joe Makini atumbuiza katika ujio wa kombe la dunia dar

0
0
  Mkali wa muziki wa Hip Hop nchini Joe Makini akitumbuiza mashabiki wa soka waliojitokeza uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia kombe la FIFA la Dunia leo.

jihadhari na kanyaboya hii inayotumwa baada ya wapopo kuiba email ya ann mboya

0
0

I really hope you get this fast. I could not inform anyone about our
trip, because it was impromptu. we had to be in LAGOS for a program.
The program was successful, but our journey has turned sour. we
misplaced our wallet and cell phone on our way back to the hotel we
lodge in after we went for sight seeing. The wallet contained all the
valuables we had I am sorry if i am inconveniencing you, but i have
only very few people to run to now. i will be indeed very grateful if
i can get a loan of $1,200 or whatever you can afford to spare me from
you. this will enable me sort our hotel bills and get my sorry self
back home. I will really appreciate whatever you can afford in
assisting me with. I promise to refund it in full as soon as I return.
let me know if you can be of any assistance. here the hotel phone

Please let me know soonest.

Thanks so much.

JK ahudhuria Mkutano wa wa wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki leo jijini kampala

0
0
 .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati wa nmkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki unaofanyika jijini Kampala Uganda leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi,Rais Yoweri Museveni wa Uganda,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa katika mkutano katika hoteli ya Munyonyo jijini Kampala wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo. Picha na Freddy Maro

mkongwe wa muziki tabu ley afariki dunia leo huko ubelgiji

0
0
Mkongwe wa muziki nchini Congo (DRC) Tabu Ley Rochereau (pichani akiwa amelazwa hospitali) amefariki dunia. Habari zinasema amefariki mapema leo asubuhi huko Ubelgiji alikokuwa amelazwa hospitali akiugua kiharusi.
 Tabuley, aliyezaliwa November 13, 1940, alikuwa kiongozi wa kundi la Orchestre Afrisa International na mmoja wa wasanii wakubwa katika bara la Afrika katika uimbaji na utunzi wa nyimbo. 
Akiwa na mpiga gitaa hodari Dkt Nico Kasanda, Marehemu Tabu Ley alikuwa mwanzilishi wa mtindo wa Soukous, na kuufanya ukubalike kimataifa kwa kuchanganya midundo ya Cuba na Rhumba la Latin Amerika. Tumkumbuke kwa kibao chake "Mokolo Nakokufa"

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ashiriki ziara ya Kombe la Dunia

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga akiwa pembeni ya Kombe la Dunia lililopo nchini katika ziara zake leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo akiwa pembeni ya Kombe la Dunia lililopo nchini katika ziara zake leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu     Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga (katikati) akielekea katika banda lilipo Kombe la Duni wakati wa ziara ya Kombe hilo hapa nchini leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo na Kushoto ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Moses Urio.
 Baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu waliofurika uwanja wa Taifa kushiriki ziara ya Kombe la Dunia wakiwa katika foleni ya kuelekea eneo lilipo Kombe hilo leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija - WHVUM
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images