Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

HATUNA UGOMVI NA RAIS MAGUFILI - TUCTA

0
0
Na Emanuel Madafa, Mbeya 
Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi  nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amesema wao kama shirikisho la vyama vya vya wafanyakazi  hawana  ugomvi  na Rais Magufuli  na kwamba ujio wake Mkoani Mbeya katika sherehe Mei Mosi kuna uwezekano wa kutamkwa jambo kubwa ambalo litaleta faraja kwa wafanyakazi Nchini.

Nyamhokya ametoa kauli hiyo jijini Mbeya katika kikao cha maandalizi ya sherehe za wafanyakazi nchini ambapo kitaifa itafanyika mkoani huku mgeni rasmi anatatajiwa kuwa Rais Magufuli.

“Sisi kama TUCTA hatujawahi kuwa na ugomvi na Rais Magufuli , yapo mambo madogomadogo  ambayo kwa upande wetu tumekwosha yaweka sawa “Amesema Nyamhokya.

Amesema yapo Mambo mengi ambayo amewachia wafanyakazi likiwemo suala la kikotoo hivyo kwa ujio wake mkoani Mbeya katika sherehe hizo kuna uwezakano mkubwa akatoa majibu ya maswali ambayo wafanyakazi wengi wamekuwa wakijiuliza.

“Maadhimisho haya yanafanyika Mbeya lakini nchi nzima macho na nasikia yatakuwa hapa wanamuangalia huyu ni Rais wetu “Amesema Tumaini Nyamhokya .

Sherehe hizo za siku ya wafanyakazi Mei Mosi zinatarajiwa kufanya mkoani Mbeya ambapo mgeni rasmi anatajwa kuwa Rais Dkt Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais hiyo wa TUCTA amesema wananchi wa mkoa wa Mbeya wajiandae kwa ajili ya kupokea ugeni huu kwani anaamini yapo mambo mengi ambayo yatanufaisha Mkoa huu .
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini, Tumaini Nyamhokya akizungumza katika kikao cha kwanza kwa ajili ya maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi ambapo Kitaifa zitafanyika Mkoani Mbeya huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Dkt Magufuli.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Mei Mosi wakimsikiliza kwa makini Rais wa TUCTA (hayupo pichani) Tumaini Nyamhokya katika kikao cha kwanza cha maandalizi ya sherehe  za Mei Mosi zitakazo fanyika mkoani Mbeya ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt Magufuli.

Ubalozi wa Uswizi wazindua awamu ya tatu ya progamu ya uwajibikaji wa Kijamii

0
0
UBALOZI wa Uswisi nchini Tanzania kupitia shirika la Maendeleo ya Ushirikiano la Uswisi SDC umezindua awamu ya tatu ya programu ya uwajibikaji wa kijamii (Social Accountability Programme SAP).

ASAP inachangia kuziwezesha asasi za kiraia (AZAKI) zinazofanya kazi ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania na kusaini mkataba huo wa pamoja

  Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli  amesema, nchi yao ina nia ya kuchangia zaidi katika kuimarisha utendaji kazi na uwajibikaji wa mamlka za umma ili zitoe huduma bora kwa wananchi.

Amesema, SDC itachangia bilion 18 kwa kipindi cha miaka minne ijayo kwa asasi kadhaa za kiraia ikiwa ni pamoja na Foundation for Civily Society (FCS), Policy Forum na Twaweza na zitashirikiana na asasi hizi ambazo zinahusika na uanzishwaji na usimamizi wa sera za maendeleo ili kuboresha maisha ya wananchi ya kawaida.

“Uswisi tunaamini kwamba asasi za kiraia ni moja a wadau muhimu kwa nchi ya Tanzania ili kufikia malengo yake ya dira ya maendeleo ya Taifa 2025, na ASAP ni sehemu ya michango katika kuimarisja masuala ya uwajibikaji ikiwa na uhusiano wa muda mrefu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kwenye kuimarisha uwezo wake wa uchunguzi,”amesema 

Kwa upande wa Mkurugenzi Aidan Eyakuze amesema kuwa, mradi huu utazidi kuimarisha uwazi kwa wananchi na taifa  na umuhimu wa kushirikiana na wananchi na kuhakikisha sauti zao zinasikika kwenye kutunga na kuboresha sera zinazowahusu wao.

Ameeleza kuwa, uwajibikaji katika kuleta maendeleo , ubunifu na utekelezaji wa kutathmini maendeleo ya wananchi.

Mweyekiti wa FCS Francis Kiwangwa ameongezea kwa kusema Mradi huu utasaidia katika ufuatiliaji wa rasilimali, kuimarisha mifumo ya udhibiti rasilimali pamoja na uwazi na uwajibikaji.


Uswisi imekuwa ikichangia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini tangu mwaka 1960 na inaendelea kutoa takriban bilioni 51 kila mwana kusaidia sekta ya afya, ajira na mapato na utawala bora.
Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli(kulia)  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kutiliana sahihi wa shilingi bilioni 18 kwa asasi za Kiraia(AZAKI) kupitia Shirika la Maendeleo na Ushiriano wa Uswisi (SDC) ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanavyofanya kazi na asasi zaidi ya 150 ya hapa nchini ili kuhimarisha ufuatiliaji wa raslimali wakishiriana na Serikali pamoja na wadau wengine kama Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzania. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze na kulia ni Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli.
Mwenyekiti wa Mtandao Policy Forum, Japhet Makongo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna wananchi wanavyoweza kutoa maoni kwa kuunganisha sauti ya mtu mmoja mmoja au vikundi kupitia mtandao huo wakati wa hafla fupi ya kutiliana sahihi wa shilingi bilioni 18 kwa asasi za Kiraia(AZAKI) kupitia Shirika la Maendeleo na Ushiriano wa Uswisi (SDC). Kulia ni Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania Romana Tedeschi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taasisi hiyo inavyofanya kazi kwa ushirikiano na Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania wakati wa hafla fupi ya kutiliana sahihi wa shilingi bilioni 18 kwa asasi za Kiraia (AZAKI). Kulia ni Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga.
Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli(katikati) akifuatilia utiliaji saini wa awamu ya Tatu ya programu ya uwajibikaji wa Kijamii(Social Accountability Programme- SAP) baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze(kushoto) na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzania Romana Tedeschi(kulia) ili kuziwezesha asasi za kirai(AZAKI) ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania. 
Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli(wa pili kulia) akifuatilia utiliaji saini wa awamu ya Tatu ya programu ya uwajibikaji wa Kijamii(Social Accountability Programme- SAP) baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga(wa pili kushoto) na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzania Romana Tedeschi(kulia) ili kuziwezesha asasi za kirai(AZAKI) ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania.

 Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli(wa pili kulia) akifuatilia utiliaji saini wa awamu ya Tatu ya programu ya uwajibikaji wa Kijamii(Social Accountability Programme- SAP) baina ya Mwezeshaji wa Mtandao Policy Forum, Semkae Kilonzo(wa pili kushoto) na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzania Romana Tedeschi(kulia) ili kuziwezesha asasi za kirai(AZAKI) ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania. wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao Policy Forum, Japhet Makongo.

Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli(katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga(kushoto)  mara baada ya utiliaji saini wa awamu ya Tatu ya programu ya uwajibikaji wa Kijamii(Social Accountability Programme- SAP)  ili kuziwezesha asasi za kirai(AZAKI) ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania. 
Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli(wa pili kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa Mtandao Policy Forum, Japhet Makongo(kushoto)  mara baada ya utiliaji saini wa awamu ya Tatu ya programu ya uwajibikaji wa Kijamii(Social Accountability Programme- SAP)  ili kuziwezesha asasi za kirai(AZAKI) ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania. 

Mkutano ukiendelea

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA JIJINI DODOMA

0
0
 Spika wa Bunge,  Job Ndugai (kushoto) akimkaribisha Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (wa pili kushoto) alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kulia ni Msaidizi wa Gavana, Dkt. Nguling’wa Balele, Meneja Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania, Ndg. Zaria Mbeo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Dodoma, Ndg. Harry Mwansembo.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Dodoma, Ndg. Harry Mwansembo na Meneja Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania, Ndg. Zaria Mbeo
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ulioongozwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (wa pili kushoto) walipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Gavana, Dkt. Nguling’wa Balele, Meneja Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania, Ndg. Zaria Mbeo na Kaimu (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Dodoma, Ndg. Harry Mwansembo.
Spika wa Bunge,  Job Ndugai (kulia) akiagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Vifo vya Wajawazito vimepungua kwa asilimia 40-Waziri Ummy Mwalimu

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Serikali imesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika Sekta  ya afya wameweza kupunguza vifo vya wamama wajawazito kwa asilimia 40.

Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua jengo la Huduma za Afya Binafsi katika Hospitali ya CCBRT, amesema kuwa vifo vya akina mama vilikuwa vingi kutokana na kukosekana kwa baadhi ya huduma lakini sasa Serikali imejenga vituo vya Afya 350 ikiwa pamoja na kuweka huduma za dharula ya kumtoa mtoto tumboni.

Amesema kuwa CCBRT imekuwa ni moja ya Hospitali iliyoweza kupambana na ugonjwa wa Fistula ambao ilikuwa unafanya wanawake kukosa amani. Mwalimu amesema serikali imeondoa kodi katika dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa gharama nafuu. Aidha ameiagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulipa kwa wakati madai ya watoa huduma za afya ili fedha hizo ziweze kuendesha huduma mbalimbali ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi.

Amesema wagonjwa asilimia 60 wanatibiwa kwa msamaha hivyo huduma za wagonjwa binafsi ndio wanaweza kuchangia katika kuziba  sehemu ya huduma kwa wale wasio na uwezo. Amesema kwa CCBRT kujenga jengo kwa ajili ya a wagonjwa binafsi wataongeza huduma mapato pamoja kuendelea kutoa huduma kwa wale wasiojiweza.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi amesema kuwa ilianza kwa kutoa huduma za macho lakini kutokana kuzidi kuimarika walianzisha huduma zingine kufikia kujenga jengo la wagonjwa Binafsi. Amesema kuwa CCBRT mipango yake ni kuhakikisha wanawafikia wananchi wote katika utoaji wa huduma za afya zilizo bora.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi  wa jengo la wagonjwa binafsi katika hospitali ya CCBRT.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy  Mwalimu akipata Maelezo kutoka Kwa Dkt. Luijisyo Mwakalukwa kuhusiana Idara ya Mifupa na Utengamao inavyofanya kazi wakati Waziri huyo akitembelea maonesho katika uzinduzi wa Jengo la Wagonjwa Binafsi.
 Waziri wa Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipata maelezo kutoka kwa  Muuguzi Mwandamizi Idara ya Macho wa CCBRT Neema Manyerere wakati Waziri  huyo akitembelea maonesho katika uzinduzi wa Jengo la  Wagonjwa Binafsi katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Brenda Msangi akitoa  maelezo kuhusiana  na Jengo la Wagonjwa Binafsi katika  katika uzinduzi wa Jengo la  Wagonjwa Binafsi katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa  Afya, Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akizungumza na hadhara ya Hospitali ya CCBRT  mara  baada ya kufungua Jengo la Wagonjwa Binafsi katika hospitali hiyo jijini Dar es  Salaam.
 Vifaa Bandia wanaowekea katika Hospitali ya CCBRT

WANANCHI WATAKIWA KULINDA NA KUVITUNZA VYANZO VYA MAJI ILI VIDUMU

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Kitengo cha Mazingira Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Modester Mushi amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kulinda vyanzo vya maji.

Hayo ameyasema wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyofikia tamati leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Mhandisi Modester amesema mazingira yanatakiwa yalindwe katika nyanja zote kuanzia kwenye vyanzo vya maji, miradi inayojengwa na kupata ushauri kutoka Baraza la Mazingira NEMC na Wizara husika.

Amesema, katika sheria ya mazingira ya 2004 imeweka wazi kuwa kwenye kila mradi uandaliwe tathimini itakayoangalia athari za kijamii na kibinadamu. “Mkandarasi anatakiwa afahamu mazingira anayoenda kufanyia kazi, wafanyakazi kuwa na vifaa vya kufanyia kazi, alama elekezi zitakazomuonyesha mwananchi kazi inayofanyika kwa muda huo,”amesema Modester.

Ameeleza, miradi inapomalizik basi hali ya mazingira inatakiwa irudishwe kama awali au kuboreshwa zaidi ya zamani na hilo linakuja mpaka upande wa uendeshaji wa mfumo wa majitak ikiwemo kuandaa sheria. Akizungumzia upandaji wa miti pembezoni mwa vyanzo vya maji, Mhandisi Modester amesema wameshapanda miti 23,000 aina ya mitomondo katika Chanzo cha Mto Kizinga, pembezoni mwa mto Ruvu kuanzia kwenye Mtambo wa Ruvu Chini na zoezi hilo litaenda mpaka Mgeta chanzo kilipoanzia.

Amesema, upandaji wa miti unapunguza mmomonyoko wa ardhi na kusaidia ardhi kushika na shughuli za kijamii zinazofanyika pembezoni za Mto husababisha udongo kuingia na kiwango cha tope kuwa kingi na kupelekea kina cha mto kupungua na kusababisha mafuriko.

Ameongezea na kuwataka wananchi watunze mazingira ili yawatunze na kuwaomba washirikiane na Maafisa ugani ambao ni wataalamu wa kilimo ili kuweza kutambua ni aina gani ya udongo na mimea inayofaa kupandwa.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mazingira Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Modester Mushi akizungumzia umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kulinda vyanzo vya maji na kurudisha ubora wa maeneo pindi miradi inapomalizika leo kwenye Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

TBS YAKABIDHI LESENI KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA AMBAZO ZIMEKIDHI VIGEZO VYA UBORA

0
0
*Yawashauri kutumia alama ya ubora kupanua soko la bidhaa zao kwa maslahi ya nchi

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa ushauri kwa wazalishaji ambao bidhaa zao  zimekidhi matakwa ya viwango na kukabidhiwa leseni  za kutumia alama ya ubora kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kupanua masoko yao ikiwa pamoja na kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBS Profesa Makenya Maboko wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika (ARSO)  yaliyofanyika makao makuu ya shirika hilo Ubungo  jijini Dar es Salaam. 
Maadhimisho yameenda sambamba na utoaji leseni  za kutumia alama za ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimekidhi matakwa ya viwango. 
"Alama ya ubora ni muhimu katika biashara , kwani inampa mzalishaji uhakika  kuhusiana na ubora na usalama wa bidhaa yake, hivyo kumjengea imani kwa walaji.Pia alama ya ubora humsaidia mzalishaji  kupanua masoko ya bidhaa zake nje ya nchi,"amesema Prof. Maboko Amesisitiza hatua hiyo ni ya kujivunia kwa wazalishaji ambao wamefikia hatua hiyo ya bidhaa ambazo wanazalisha kukidhi viwango vya ubora na kupewa leseni ya kutumia alama hiyo na kwamba kamaTaifa kupanuka kwa masoko  ya kikanda na kimataifa  kutasaidia kuongeza fedha za kigeni, hivyo kusaidia kukuza uchumi.
Amefafanua kuwa hali hiyo  itasaidia kufikiwa kwa azma ya Taifa ya kujenga uchumi wa kati unaotegemea uzalishaji wa viwandani ifikapo mwaka 2025.
 Hata hivyo amewataka wazalishaji  waliopatiwa leseni hizo  kuzingatia masharti yake na kuwa waadilifu katika uzalishaji wao, ili kuhakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa  zinazokidhi matakwa ya viwango wakati wote. 
 Akizungumzia jitihada zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli  katika kupambana na rushwa nchini, Prof.Maboko, ameeleza  wao kama wadau wa viwango ni fursa muhimu  ya kuhakikisha wanatoa mchango wao kwa kueneza uelewa na weledi unaotumika katika kuandaa viwango na pia kuwahamasisha wazalishaji na watoa huduma kuhusu umuhimu wa kuzingatia matakwa ya viwango katika shughuli zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, amesema wao kama taasisi Siku ya Maadhimisho ya  Viwango Afrika ni muhimu, kwani wanapata fursa ya kuwakumbusha wazalishaji, watoa huduma na wananchi wote kuhusu umuhimu wa kuzingatia viwango vya ubora katika maisha yao ya kila siku.
Kwa mujibu wa Dkt. Ngenya , kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ya saba ya Siku ya Viwango Afrika ni ; “Nafasi ya viwango katika kufanikisha mapambano dhidi rushwa kwa mabadiliko endelevu  ya  Afrika.”

Amefafanua kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua katika suala la vita dhidi ya rushwa, hivyo na wao katika tasnia ya viwango, wanayo fursa ya kuonesha njia katika kufanikisha mapambano dhidi ya rushwa, hivyo kuhakikisha rasilimali za nchi  zinatumika ipasavyo katika kuondoa wananchi katika umaskini na kuwaletea maendeleo.
Ameongeaza kuwa wanayo fursa ya kuweka kielelezo cha uadilifu kwa kuhakikisha  kuwa michakato ya ukaguzi, upimaji, ugezi, utoaji leseni na udhibiti ubora kwa ujumla inafanyika kwa kuzingatia misingi na taratibu.
Pamoja na mambo mengine maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na utoaji zawadi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu walioshiriki na kushinda shindano la insha  lililojikita katika kauli mbiu ya maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Profesa Makenya Maboko (watatu kutoka kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dkt. Yusuf Ngenya (kulia kwake) akiwa amesimama na wajumbe wa bodi na menejimenti ya shirika kwa ajili ya kuanza kutoa leseni za kutumia alama za ubora kwa wazalishaji ambao bidhaa zao zimekidhi viwango. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya shirika hilo Ubungo jijini Dar es salaam  ambapo imekwenda sambasamba na Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika.
 Mmoja ya wazalishaji wa bidhaa nchini akiwashukuru maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi waliokuwa mezaa kuu kwa kuwapa mkono baada ya kukabidhiwa leseni yake kutokana na bidhaa anazozalisha kukidhi vigezo vya ubora unaotakiwa na shirika hilo.
 Mmoja wa washiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika (ARSO)  akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya shirika hilo Ubungo  jijini Dar es Salaam . 
Baadhi ya washiriki kutoka vyuo vikuu mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Ubungo jijini Dar es Salaam.

KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAJADILI BAJETI YA MKOA WA TABORA

0
0
 Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa wa Tabora kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
 Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa  Hamad Maalim akichangia jambo wakati Kamati hiyo ikipokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa wa Tabora kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa huo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto

0
0
 Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau kwa kushirikiana na madaktari kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefinyiwa upasuaji wa kuziba matundu na hali zoa zinaendelea vizuri
 Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Evarist Nyawawa kwa kushirikiana na madaktari wa Shirika la Open Heart International (0HI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu wakati wa kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watu wazima watano wenye matatizo ya moyo wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku saba na hali zao zinaendelea vizuri.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lilian Peter kwa kushirikina na wenzake wa Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimuhudumia mtoto aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayofanywa katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. Picha na Genofeva Matemu - JKCI

MAMLAKA ZA MAJI ZIIGE MFANO WA DAWASA KUWAUNGANISHIA MAJI WANANCHI KWA MKOPO- NAIBU WAZIRI AWESO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

NAIBU Waziri wa Maji Juma Aweso amezitaka Mamlaka za maji nchini kuiga mfano wa DAWASA wa kuwaunganishia maji wananchi kwa mkopo na kuwakata kidogo kidogo kil mwisho wa mwezi.

Aweso ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam kwenye banda la maonesho la Mamlaka hiyo kupata maelezo mbalimbali kwenye Wiki ya Maji duniani iliyofikia kilele.

Akizungumza baada ya kumaliza kupata maelezo kuhusu huduma wanazozitoa kwenye banda la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA , Naibu Waziri amesema kuwa maji yapo ila changamoto kubwa ni wananchi wanatakiwa kuunganishwa huduma ya maji na kikubwa DAWASA waliona umuhimu na kuwaunganishia maji wananchi na kuwakata kidogo kidogo kila mwisho mwezi.

Aweso amesema, katika wiki hii ya maji watendaji wanatakiwa wajitafakari kuanzia kwenye utendaji, changamoto na mafanikio kwenye sekta ya maji pia tutambue maji ni uhai na uchumi na tutoke maofisini tuingie mtaani kutatua changamoto za maji.

“Mamlaka zote wanahakikishe wanawaunganishia maji wananchi  na waige mfano wa DAWASA wa kutoa vifaa na kuwaunganishia maji wananchi na baadae kuwakata kidogo kidogo kila mwisho wa mwezi,”amesema Aweso.

Ameeleza kuwa bado kuna changamoto za maji katika maeneo ambayo hayana mtandao kwa mkoa wa Dar es Salaam, kuna mradi wa Visima vya Kimbiji na Mpera ambapo vipo katika utekelezaji sasa nataka DAWASA waelekeze nguvu zao zote na kazi ianze mara moja ili wananchi wa Temeke, Ukonga, Kigamboni na maeneo mengine wapate maji safi na salama.

“ kuna miradi 1659 imeshakamilika, na miradi mingine 492 ikiwa ipo katika hatua tofauti za utekelezaji  ninaamini itakamilika kwa wakati na mwananchi anatakiwa apelekewe maji mita zisizozidi 400 kutoka mahala anapokaa,” amesema.

Aweso amezungumzia pia ujenzi wa mabwawa ya maji ambapo amesema hiyo ni fursa kwa Wizara kwani kuna maeneo yana mafuriko ikiwemo Kilosa Mkoani Morogoro na watatumia nafasi ya kujenga mabwawa wanaweza wakayatumia kwa kilimo cha umwagiliaji  pamoja na kutatua kero ya maji Kwene Jiji la Dodoma na Morogoro ikiwemo.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Arone Joseph amesema kuwa wamefurahi kwa Naibu Waziri ambaye ni mzazi kwao kuweza kufika kwenye mabanda yao ambapo ndani ya wiki ya maji wameweza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kusikiliza kero za wananchi.

Joseph amesema, wameweza kusikiliza kero 150 za wananchi na asilimia 70 zikiwa zimefanyiwa kazi na nyingine zikiwa zinaendelea kutatuliwa.

Ameongeza, Katika moja ya mikakati yao ndani ya wiki ya maji duniani ilikuwa ni kuhakikisha wanamaliza miradi mbalimbali na wananchi waanze kupata maji na hilo limefanikiwa kwenye maeneo ya Bonyokwa, Kiwalani, Saranga, Kinzudi, Kwa Msuguri na Bagamoyo.

“Kuna miradi mingine mikubwa bado inaendelea kutekelezwa ila malengo ni kufikia asilimia 95 ya wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanapata majisafi na Salama,” amesema Joseph.

Wiki ya Maji imefikia kilele leo ambapo kitaifa imefanyika Jijini Dodoma na malengo yakiwa ni kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa kwenye kupata huduma ya majisafi na kumtua mama ndoo kichwani.
 Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutembelea na kupata maelezo kwenye  banda la maonesho la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA leo katika Kilele cha Wiki ya Maji kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza na wananchi waliofika kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA leo katika Kilele cha Wiki ya Maji kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam

WATEJA WA MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR, ZAWA KULIPIA BILI KWA T-PESA

0
0

Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (katikati) akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za maji kupitia T-Pesa. Tukio hilo limefanyika sambamba na Maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Maji, yenye kauli mbiu 'Hakuna Atakae Achwa'. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (kushoto) kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za maji Zanzibar kupitia T-Pesa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimwelekeza Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (kushoto) namna ya kufanya malipo ya bili ya maji Zanzibar kupitia T-Pesa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za maji kupitia T-Pesa.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Kazija Mussa Msheba (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za ZAWA kupitia T-Pesa. Kwa makubaliano hayo sasa wateja wa ZAWA watakuwa wakilipa bili zao kupitia mtandao wa T-Pesa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (katikati) akionesha simu ya mkononi aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kuliye aliyeshika kipaza sauti) kama zawadi.
Baadhi ya washiriki kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za Mamlaka ya Maji Zanzibar kupitia T-Pesa wakifuatilia matukio anuai. Kwa sasa wateja wa ZAWA watakuwa wakilipa bili zao kupitia T-PESA.
Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kushoto) wakiwaelekeza washiriki namna ya kulipia huduma za ZAWA kupitia T-Pesa.
Wateja wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) wakipata maelekezo namna ya kulipia bili kwa T-PESA.
Picha ya pamoja na meza kuu mara baada ya hafla hiyo.

WIKI YA MAJI YAISHA KWA KISHINDO: WAKAZI WA SARANGA KUTEMBEA KIFUA MBELE KWA MAJI YA DAWASA

0
0
Hitimisho la Wiki ya Maji Duniani, Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) wamewapa furaha wakazi wa Saranga na maeneo jirani kwa kuwapatia maji safi na salama. Akizungua wakati wa kuzindua mradi wa kuwasambazia maji wakazi wa Saranga Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori amesema kuwa amefurahishwa jinsi DAWASA walivyoweza kuwapa furaha wakazi hao wa Saranga kwa kuwapatia maji ambayo watakuwa wakiyapata masaa 24. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es S  alaam Kisare Makori (kushoto) akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema kwa kuweza kufanikisha uwekaji wa bomba eneo la Saranga jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (kushoto) akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema kwa kuweza kufanikisha uwekaji wa bomba eneo la Saranga. Wengine wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (kushoto) akizungumza na wakazi wa Saranga (picha ya chini) Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema akizungumza na wakazi wa Saranga jijini Dar es Salaam kuwaelezea jinsi walivyoweza kufanikisha kufikisha mradi huo.
Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka akielezea jinsi mradi ulivyoweza kukamilika wakati wa hitimisho la wiki ya Maji Duniani iliyoanza Machi 16-22, 2019.
Diwani wa kata ya Saranga Mhe. Haruni Mdoe akizungumza na wakazi wa Kimara Tembeni kata ya Saranga jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (wa tatu kutoka kushoto) akikata utepe na Diwani wa kata ya Saranga Mhe. Haruni Mdoe kuzindua huduma hiyo.
Tukio Lingine alilolifanya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Makori ni kuzindua eneo la Bomba la Kwanza lililowekwa kwa mkazi mmoja wa Saranga ili kuonyesha ishara ya usambazaji wa maji kwa wakazi hao.
Wakazi wa Saranga wakijiandikisha mbele ya wenyekiti wa Serikali za mtaa ili waweze kupatiwa maji na DAWASA.
Meneja wa huduma kwa wateja wa DAWASA Doreen Kiwango akiangalia zoezi la uandikishaji wateja wapya wakazi wa Saranga linavyoendelea.

PROF. KABUDI AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Taarifa kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) (hawapo pichani) wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara kilichofanyika kwenye Ofisi za Bunge, Dodoma tarehe 22 Machi, 2019. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan M. Mwinyi. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Mussa Azan Zungu akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) (hayupo pichani), wakati akiwasilisha taarifa kuhusu bajeti ya Wizara yake wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara kilichofanyika Ofisi za Bunge, Dodoma tarehe 22 Machi, 2019. Wakati wa kikao hicho, Mhe. Zungu alitumia fursa hiyo kwa niaba ya Kamati, kumpongeza Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua ya kupeleka haraka misaada ya chakula na dawa kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe baada ya kupatwa na maafa yaliyosababishwa na kimbunga kikali kilichozikumba nchi hizo. 
Kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikiendelea 
Sehemu ya Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati hiyo wakifuatilia kikao 
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao na Kamati ya Bunge ya NUU 
Wajumbe wa Kamati wakimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani) 
Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao 

Mjumbe wa Kamati akichangia hoja wakati wa kikao hicho 
Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara wakiwa kwenye kikao na Kamati ya Bunge ya NUU 
Mjumbe wa Kamati akichangia jambo wakati wa kikao na Wizara 
Mjumbe mwingine wa Kamati ya Bunge ya NUU akichangia hoja wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara 
Mhe. Mbunge akichangia hoja 

ASKARI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

0
0
 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu Kennedy Komba akizungumza wakati akifungua kikao kazi leo Jijini Tanga kulia ni Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Tanga Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Goodluck Zelote
 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Tanga Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Goodluck Zelote akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni  Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu Kenedy Komb
 Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Tanga Yusuph Msuya akijitambulisha wakati wa kikao hicho
 Sehemu ya wakaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini wakifuatilia kikao hicho
meza kuu wakifuatilia hoja  mbalimbali kwenye kikao hicho
 Sehemu ya Askari wa Jeshi la Zimamoto wakifuatilia kikao hicho

ASKARI wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mikoa ya Kanda ya Kaskazini wametakiwa kufanya kazi kwa waledi,uaminifu na juhudi kubwa wanapokwenda kuzima moto kwa wananchi ili kuweza kuokoa mali zao na maisha hivyo kuleta matumaini mapana kwao na jamii zinazowazunguka.

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu Kenedy Komba kwa Makamanda wa Jeshi hilo mikoa ya kanda ya Kaskazini kilichokuwa na lengo la kubadilisha uzoefu na kuona namna ya kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi mkubwa katika kutoa huduma kwa wananchi wa mikoa hiyo.

Alisema anamina baada ya kumalizika kwa kikao hicho kila Kamanda na mkuu wa kitengo atakuwa amepata faida na kuleta matokeo yaliyomema na kutukuka kwenye kutoa huduma kwa watanzania mikoa wanayotoka na Taifa kwa ujumla.

Alisema dhamira kubwa hivi sasa kwao ni kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi waweze kujua kazi wanayoifanyika hususani wanapokwenda kuzima moto hivyo wategemee maokozi yatafanyika kwa juhudi kubwa yawe ya mali au wananchi ili kuleta matumaini mapana kwa wananchi.

Komba alisema katika kila kazi inapoifanya kwenye sehemu ya kazi kunapaswa kufanya kazi kwa uaminifu na waledi ili kuwafanya waananchi wawweze kuwaamini katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku kupambana na majanga ya moto

“Suala kubwa ni uaminifu na ueledi kwenye kutekeleza majukumu yetu na tusipofanya hivyo tutapoteza imani kwa weananchi ...tujenge mahusiano mema na wananchi lakini kubwa zaidi kutekeleza majukumu kwa ufanisi mkubwa ambao utasaidia kupata wadau walio wema wenye hiari ya kutusaidia kutupa mawazo kwa sababu ya waledi tunaoufanya “Alisema

“Kila mkoa kuchukua yale mazuri yatakayowasilishwa kwenye kikao hicho kwenda kuyafanyia kazi ili kikao kijacho kila mkoa uweze kuleta mafanikiona sio malalamiko kwa kufanya hivyo Jeshi litakuwa la mfano na kuleta matokeo changa kwa mkoa na Taifa kwa ujumla”Alisema

Alisema hatua hiyo ya kukatana na kubadilisha uwezo wa kazi zao wanazofanya italeta matokeo changa kwa wananchi wanao wahudumia kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Naye kwa upande wake Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Tanga Yusuph Msuya alisema dhani ya idara ya ukaguzi ni kupunguza majanga kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye majengo, magari ili kuwawezesha watumiaji kuepukana nayo.

Alisema mpaka sasa wamekwisha kufanya kwa vyombo vya moto vipatavyo 384 ambapo kati ya hivyo mabasi 235 hali zao ni nzuri na yaliyosalia tumewapa ushauri namna ya kufanya ili waweze kuondokana na mapungufu yaliyobainika.

“Ukaguzi tulioufanya kuanzia mwezi Desemba mpaka sasa kwa vyombo 384 kati ya hivyo mabasi 235 hali zao ni nzuri na yasiyosali tumewapa ushauri ili waweze kuondoa mapungufu yaliyobainika”Alisema

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOANI MBEYA

0
0



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu kwa tuhuma mbalimbali.

KUINGIA NCHINI BILA KIBALI,
Mnamo tarehe 21.03.2019 saa 16:30 jioni huko eneo na Kata ya Lupa Tingatinga, Tarafa ya Kipambawe. Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Polisi walimkamata OMARY JUMA @MWAMI [21] raia wa nchi ya Burundi akiwa ameingia nchini bila kibali na kufanya shughuli za kilimo cha Tumbaku. Upelelezi unaendelea.

UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU
Mnamo tarehe 21.03.2019 saa 00:30 usiku huko maeneo ya Veta Kata ya Ilemi, Tarafa ya Iyunga ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya. IMAN ANDISON [20] Dereva bodaboda na mkazi wa Simike alinyang’anywa pikipiki yake yenye namba za usajili MC 833 BVS aina ya Kinglion na watu watatu wasiofahamika.
Mbinu iliyotumika ni kwamba muhanga akiwa amepaki pikipiki yake maeneo ya Kiwira Motel alitokea abiria mmoja na kutaka apelekwe Veta na ndipo alipomfikisha maeneo hayo walijitokeza watu wengine wawili na kumvamia kisha kumjeruhi kichwani na watu hao kutokomea na pikipiki hiyo. Majeruhi amelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Uchunguzi/upelelezi unaendelea kuwabaini waliohusika katika tukio hilo.

KUINGIZA NCHINI BIDHAA BILA KULIPIA USHURU.
Mnamo tarehe 22.03.2019 saa 07:00 asubuhi huko Uwanja wa Siasa uliopo Kata ya Mbugani, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Polisi wakiwa Doria walimkatama mtu mmoja aitwaye ZACHARIA MWANGUKULU [28] Mkazi wa Mbugani akiwa ameingiza nchini bidhaa mbalimbali bila kulipia ushuru.

Bidhaa alizokamatwa nazo mtuhumiwa ni:-
Mipira ya kiume [Condoms] aina ya Chishango Boksi 45.
Juisi aina ya BAK’S Boksi 27
Mafuta ya Kula aina ya Cook Well ndoo moja yenye ujazo wa lita 10
Mifuko ya Plastiki aina ya Soft vifurushi 03
Bidhaa hizo zilikuwa zikisafirishwa kwenye gari lenye namba za usajili T.532 CGU aina ya Toyota Noah iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye ABRAHAM MWARABU [32] Mkazi wa Njisi Kasumulu Kyela ambaye naye amekamatwa.
Bidhaa hizo zimeingizwa nchini zikitokea nchi jirani ya Malawi kwa kutumia njia na vivuko visivyo halali. Taratibu za kuzikabidhi bidhaa hizo Mamlaka ya Mapato Tanzania zinafanyika.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


Gari lililokuwa likisafirisha mzigo hiyo

KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAJADILI BAJETI YA MKOA WA TABORA

0
0


Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa wa Tabora kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Hamad Maalim akichangia jambo wakati Kamati hiyo ikipokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa wa Tabora kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Agrey Mwanri akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa huo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

WAVAMIZI SHAMBA LA MITI BIHARAMULO WAPEWA MIEZI 3

0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita., Kulia ni Meneja wa shamba hilo, Edward Nyondo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto) alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa ukubwa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine ni watumishi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa shamba la miti la Biharamulo ambalo mara baada ya kukamilika kwa kupandwa miti katika eneo lote litakuwa ndio shamba la pili kwa ukubwa kati ya mashamba 20 yanayomilikiwa na Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania lililopo wilayani Chato mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipanda mti wakati alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita

Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni akipanda mti wakati alipoambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya na watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Baadhi ya watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika shamaba hilo hukuakiwasisitizan umuhimu wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wanaoishi karibu na shamba hilo.
(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
…………………………. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu. 

Ametoa muda huo ili wananchi waliolima mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na pamba waweze kuvuna mazao yao kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo. 

Mhe.Kanyasu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea shamba la miti Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Amesema Oparesheni hiyo haitasubiri taarifa ya Wizara tano inayoendelea kufanyiwa kazi kwa kuwa eneo hilo halihusiani na vile vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya Hifadhi. 

Amesema haiwezekani wananchi waliovamia eneo hilo waendelee kuachwa kwa kisingizio cha Kauli ya Rais aliyoitoa Januari 15 mwaka huu kuhusiana na vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya maeneo ya Hifadhi. 

Amebainisha kuwa wananchi waliovamia eneo hilo wameitafsiri visivyo Kauli hiyo na kuongeza kuwa baada tu ya tamko la Mhe. Rais , baadhi ya wananchi hata wale waliokuwa wakiishi katika maeneo mengine nje ya hifadhi waliendelea kuvamia na kuanza kujimilikishia maeneo makubwa wakidai kuhalalishwa na tamko la Rais. 

Amefafanua kuwa taarifa inayoendelea kufanyiwa kazi na timu ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Wizara tano imebainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya vijiji 700 vimekutwa ndani ya Hifadhi badala 366 vilivyoripotiwa awali. 

Kufuatia hali hiyo amesema baadhi ya wavamizi wa Hifadhi katika maeneo mbalimbali wataendelea kuondolewa bila kusubili kukamilika kwa zoezi linaloendelea kwa kuwa walieendelea kuvamia maeneo ya Hifadhi kwa kisingizio cha tamko la Rais huku maeneo hayo yakizidi kuharibiwa kwa miti kukatwa na shughuli nyingi za kibinadamu 

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kutenga Bajeti ya kugharamia operesheni ya kuwaondoa wavamizi ndani ya Shamba hilo. Ameitaka TFS kuendesha oparesheni za mara kwa mara ili wavamizi hao wajue Serikali ipo kazini kulinda rasilimali za Taifa muda wote. 

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mtemi Simeoni akizungumza katika ziara hiyo alisema kuwa baadhi ya wananchi kutoka nje ya wilaya hiyo wamekua wakivamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba hilo, suala ambalo ni kinyume cha sheria. 


Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa wananchi katika maenro hayo wana mahitaji makubwa ardhi na kuiomba Wizara iangalie namna ya kuwasaidia hekari 5000 ili wapate maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao.
Kwa upande wake Meneja wa Shamba hilo Bw. Thadeus Shirima amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa hadi sasa zaidi ya hekari 900 zimepandwa miti licha ya Shamba hilo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendea kazi.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA JIJINI DODOMA.

0
0


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (wa pili kushoto) alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kulia ni Msaidizi wa Gavana, Dkt. Nguling’wa Balele, Meneja Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania, Ndg. Zaria Mbeo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Dodoma, Ndg. Harry Mwansembo
V25A2813
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (wa pili kushoto) alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kulia ni Msaidizi wa Gavana, Dkt. Nguling’wa Balele, Meneja Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania, Ndg. Zaria Mbeo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Dodoma, Ndg. Harry Mwansembo
V25A2867
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
V25A2901
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Dodoma, Ndg. Harry Mwansembo na Meneja Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania, Ndg. Zaria Mbe.
V25A2877
pika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ulioongozwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (wa pili kushoto) walipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Gavana, Dkt. Nguling’wa Balele, Meneja Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania, Ndg. Zaria Mbeo na Kaimu (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Dodoma, Ndg. Harry Mwansembo 
V25A2750
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimkaribisha Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga alipomtembelea leo tarehe 22 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Madaktari bingwa waendesha kambi maalum ya matibabu ya moyo JKCI

0
0


Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau kwa kushirikiana na madaktari kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefinyiwa upasuaji wa kuziba matundu na hali zoa zinaendelea vizuri
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Evarist Nyawawa kwa kushirikiana na madaktari wa Shirika la Open Heart International (0HI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu wakati wa kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watu wazima watano wenye matatizo ya moyo wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku saba na hali zao zinaendelea vizuri.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lilian Peter kwa kushirikina na wenzake wa Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimuhudumia mtoto aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayofanywa katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.

Picha na: Genofeva Matemu – JKCI

Zainabu Katimba: Vijana tuchangamkie fursa za kiuchumi

0
0








Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana bungeni, Zainabu Katimba, kulia, akizungumza na baadhi ya vijana wanaowakilisha makundi mbalimbali jijini Dar es Salaam, katika kongamano aliloandaa lenye dhamira ya kuangalia fursa za kiuchumi zinazoweza kufanyia na vijana kwa ajili ya kukuza uchumi wao. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), Andreas Quasten, ambayo wameshirikiana na Mbunge kuwezesha Kongamano hilo. Picha na Mpigapicha Wetu.

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana bungeni, Zainabu Katimba, akizumgumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika kongamano aliloandaa lenye dhamira ya kumuwezesha kijana katika hali ya kufanyia kazi changamoto zinazowakabili vijana nchini Tanzania. Kongamano hilo pia limeandaliwa kwa ushirikiano mkubwa wa taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES). Picha na Mpigapicha Wetu. 


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

VIJANA mbalimbali nchini Tanzania, wameaswa kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwamo namna bora ya kuungana vikundi ili kuomba fedha za Halmashauri ambazo zimekuwa zikikosa waombaji katika maeneo mengi, huku sababu kubwa ni uelewa mdogo juu ya upatikani wa fedha hizo zinazotolewa maalum ili kuwakomboa vijana kiuchumi. 

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum, akiwakilisha vijana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zainabu Katimba, katika kongamano la vijana aliloandaa kwa kushirikiana na taasisi yake ya WEZESHA, akishirikiana pia na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung, ikikutanisha viongozi wa makundi mbalimbali jijini Dar es Salaam, nchini hapa. 

Akizumgumzia changamoto hizo, mheshimiwa Katimba alisema kuwa wapo watu wanaoamini kuwa fedha hizo hazipo au zinatoka kwa watu maalum, bila kujua kwamba fedha hazitoki kwa watu mmoja mmoja na kinachotakiwa ni kuungana katika makundi na kuanisha vipengele vya kimkakati, jambo ambalo limekuwa halifanyiki. 

“Mimi nawakilisha vijana kule bungeni, lakini pia tunaelekea kwenye bajeti mpya, hivyo naamini pamoja na mambo mengine, tukitoka kwenye kongamano hili la kuwezesha a, kuelimishana sambamba na kufungua milango ya kuiona fursa, naamini tutakuwa katika nafasi nzuri, zaidi uwezo wa vijana kuzichangamkia pia fedha za serikali katika Halmashauri zetu. 

“Nimekuwa nikifanya makongamano haya kwa muda mrefu na dhamira yetu kubwa ni sisi vijana wenyewe kujitambua, kwa sababu tunapoweza kutumia fursa tunazokutana nazo mtaani, walau tunaweza kujikwamua kiuchumi na kulikomboa pia Taifa letu ambalo sera ya viwanda imeshika kasi na sisi vijana wenyewe ndio nguvu kazi ya Taifa kwa namna moja ama nyingine,”Alisema Katimba, ambaye pia ni mwasisi wa taasisi ya Wezesha. 

Akizumgumzia kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), Andreas Quasten, alimpongeza Mbunge wa Viti Maalum, Zainabu, kwakuwa karibu na vijana akisema anawawakilisha vizuri bungeni.
“FES tunampongeza bi Zainabu kwa kufanya mambo mengi yanayohusu vijana, ambapo tunaamini kwa uwapo wake bungeni, unasaidia kuwezesha vijana, katika kipindi hiki ambacho idadi kubwa ya watu Tanzania ni vijana, huku wakiwa na changamoto nyingi ikiwamo ajira, ushiriki katika mambo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. 

“Sisi FES tutaendelea kushirikiana na makundi yote sambamba na serikali Kuu ili kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinakwisha ili kuwafanya vijana na Watanzania wote wanaishi maisha vizuri, sanjari na uelewa mpana wa kutumia fursa endelevu za kiuchumi,”Alisema. 


Katika kongamano hilo la siku moja lililofanyika katika ofisi Kuu za FES zilizopo Kinondoni, Morocco, jijini Dar es Salaam, vijana mbalimbali walichambua changamoto wanazokutana nazo mitaani, bila kusahau mwelekeo unaoatakiwa kufuatwa katika Bajeti Kuu ya Serikali itakayosomwa baadaye mwaka huu bungeni, jijini Dodoma.

RAIS WA ZANZIBAR.DK.SHEIN, AZUNGUMZA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA IKULU ZANZIBAR

0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi Tanzania Nchini Zambia Mhe.Balozi Hassan Simba Yahya, alipofika Ikulu Zanzibar leo 22-3-2019, kwa mazungumzo na Rais.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Mhe. Hassan Simba Yahya, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 22-3-2019(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo,22-3-2019.(Picha na Ikulu)
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images