Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

LE MUTUZ SUPER BRAND AHAMASISHA WATANZANIA KUISHANGILIA TAIFA STARS


MSANII WEMA SEPETU AHAMASISHA WATANZANIA KUISHANGILIA TAIFA STARS JUMAPILI

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI YATAKAYOWEZESHA UTEKELEZAJI WA UJUMUISHWAJI WA MASUALA YA KIJINSIA SEHEMU ZA KAZI

$
0
0
Taasisi za umma nchini zimetakiwa kuweka mazingira rafiki sehemu za kazi ili kuwezesha utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa ufanisi na hatimaye kufikia usawa wa kijinsia  utakaokuwa na tija kwa maendeleo ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Leila Mavika wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengo la kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika taasisi za umma.
Leila amesema kuwa, mazingira rafiki ya ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi yanategemea  menejimenti za taasisi za umma kutoa kipaumbele kwa masuala ya anuai za jamii kuwa ni sehemu ya shughuli za uendeshaji wa ofisi za kila siku.

Leila ameainisha kuwa, ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia utafanikiwa iwapo kutakuwa na uelewa wa pamoja wa masuala ya kijinsia kwa watumishi wa umma na menejimenti zao ambao utasaidia kuepuka ubaguzi na unyanyapaa mahala pa kazi na kuongeza kuwa,  taasisi za umma zikijenga majengo jumuishi yenye miundombinu inayofikika kwa urahisi na wadau wote hususan watu wenye ulemavu wa viungo, zitawezesha jinsia zote kupata huduma bora bila kikwazo cha aina yoyote. 

“Ni vema taasisi zikaweka mifumo thabiti itakayoweka mazingira rafiki, wezeshi na mifumo rejeshi inayotoa fursa kwa wananchi kutoa taarifa za masuala ya  unyanyasaji wa kijinsia  na ukiukwaji wa maadili kwa ujumla” amesema Bi. Leila.

Leila amezitaka taasisi zote za umma kuhakikisha kwamba, zinatenga bajeti kwa ajili ya  ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi na kuyafanya masuala ya kijinsia kuwa ajenda ya kudumu katika vikao  vya kitaasisi vya ndani na nje.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hamidi Mbegu amesema kuwa, kikao kazi hicho cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kitakuwa ni chachu ya kuboresha utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika wizara yake na taasisi zote za umma.
Aidha, Bw. Mbegu amesema, kikao hicho kimeazimia kuwepo mwongozo rasmi utakaowezesha utekelezaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi, ambao utasaidia uanzishaji wa madawati ya kijinsia sehemu za kazi ambayo yatarahisisha   utekelezaji na ufuatiliaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi.

Naye, Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Mradi wa SAUTI kutoka Shirika la Jhpiego, 
 Grace Munisi amesema kuwa, serikali imekuwa ikishirikiana na mradi huo katika utekelezaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kupitia udhamini wa warsha mbalimbali zinazosaidia kuwapa uelewa watendaji juu ya mahusiano ya kijinsia yanavyoweza kusababisha  maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kuepuka mila potofu zinazosababisha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI sehemu za kazi na kwenye jamii kwa ujumla.

Kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi katika Taasisi za Umma kilijumuisha Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka katika Wizara, kwa lengo la kujadili fursa na changamoto za masuala ya kijinsia katika utumishi wa umma ili kuweka mikakati endelevu itakayofanikisha uwepo wa Usawa wa Jinsia mahala pa kazi  utakaowezesha maendeleo endelevu.
 Mkurugenzi Msaidizi, Idara wa Utawala, Mahakama ya Tanzania, Wanyenda Kutta akitoa mada kuhusu uzoefu wa taasisi yake katika masuala ya kijinsia kwenye kikao cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Leila Mavika akifunga kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Christina Mangwai akichangia mada wakati wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakijadiliana maazimio wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, BLeila Mavika akitoa maelekezo kuhusu maazimio wakati wa kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.

EAC TO COMMEMORATE 25 YEARS OF THE GENOCIDE AGAINST THE TUTSI

$
0
0
The East African Community Secretariat in collaboration with the Tanzanian Local Authorities in Arusha, the Arusha and Moshi Rwandan Community, the Embassy of Rwanda in Tanzania, the International Residual Mechanism for Criminal Tribunals (IRMCT), the Religious Denominations based here in Arusha, the Representatives of Students from High School and Universities of the Arusha region and EAC staff will commemorate the 25th anniversary of the Genocide against the Tutsi in Rwanda on Sunday 7 April, 2019 at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

Themed “Remember-Unite-Renew”, this year’s commemoration will be an occasion to pay tribute to the more than one million innocent lives lost through the heinous extermination of Tutsis in Rwanda 25 years ago.

Under the above theme, this year’s commemoration will focus mainly on the legacy of strength, resilience, and unity that the new generation is called upon to sustain as well as safeguarding the strides Rwanda has been able to make over the past quarter of the century and carry forward the vision for Rwanda’s transformation.

Since the 20th commemoration, EAC has taken a commendable route to supporting genocide survivors and recognizing genocide against the Tutsi in Rwanda as a crime against humanity, first by building a genocide monument in the EAC gardens and further by setting apart the 7th of April every year on the EAC calendar as a special day to commemorate the 1994 genocide against Tutsi in Rwanda.

The EAC has taken full ownership of the event and takes this opportunity to invite everyone to join the Government and people of Rwanda to commemorate the 25th anniversary of the Genocide against the Tutsi by standing against genocide denial and its ideology and recognizing the incredible bravery of those who rescued others during the genocide at great risk to themselves and their families

MIGOGORO MIKUBWA 14 KATI YA 29 YATATULIWA NA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
Na Edward Kondela
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Abdallah Ulega amesema wizara kupitia timu yake maalum ya kushughulikia migogoro, hadi sasa imetatua migogoro mikubwa 14 kati ya 29 inayohusisha wakulima na wafugaji pamoja na hifadhi na wawekezaji.

Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Mhe. Lengai Ole Sabaya pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo, mara baada ya kuarifiwa kuwepo kwa mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Hai na kubainisha kuwa ni hatari kwa jamii inayoishi pamoja kuwa na mgogoro wa aina hiyo.

“Nitamsisitiza katibu mkuu mifugo aliangalie kwa karibu sana hili kwa sababu ni hatari sana kwa jamii inayoishi pamoja kutokuwa na maelewano ya kuachiana maeneo kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi.” Alisema Mhe. Ulega

Ulega ametoa kauli hiyo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya kumuarifu kuwa baadhi ya maeneo yenye migogoro ni Kata ya KIA ambapo wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika maeneo ya uwanja wa ndege wa KIA, pamoja na wakulima wilayani humo kutotaka kuwaachia wafugaji maeneo wasiyoyatumia kwa kilimo hususan yenye magadi kwa ajili ya malisho kwa wafugaji hivyo kutengeneza chuki dhidi yao.

Naibu Waziri Ulega amemshauri pia mkuu huyo wa wilaya kutumia Chuo cha Mifugo Tengeru na Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa (NAIC) vilivyopo Mkoani Arusha ili kuleta mabadiliko kwa wafugaji katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro kwa kuwa na ng’ombe wachache na wenye tija ukizingatia ukanda huo kuna kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh ambacho kinahitaji maziwa kwa wingi katika uzalishaji wao.

“Ukanda huu kuna kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh ambacho kinahitaji lita laki moja ya maziwa kwa siku na bado hayatoshelezi hadi inawalazimu kuchukua maziwa kutoka mikoa ya Iringa na Njombe ni vyema mkashirikiana na wizara kutoa elimu ili wafugaji wa wilaya hii wabadilike kwa kufuga kisasa hususan ng’ombe wa maziwa badala ya kuwa na ng’ombe wengi wasio na tija kiuchumi.” Alisema Mhe. Ulega

Naibu Waziri Ulega amemshauri pia mkuu wa wilaya Mhe. Sabaya kuwa na kampeni maalum ya kutoa elimu kwa wafugaji pamoja na kushirikiana na wataalam ili wilaya hiyo iwe ya mfano katika kubadilisha fikra za wafugaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Hai Lengai Ole Sabaya amesema changamoto kubwa zilizopo wilayani hapo ni mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ambao tayari upo katika hatua mbalimbali za kutatuliwa pamoja na wafugaji kutokuwa tayari kubadilika kutoka kwenye ufugaji wa zamani wa kuwa na makundi makubwa ya mifugo isiyo na tija.

Kufuatia mazungumzo baina yake na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ulega, mkuu huyo wa wilaya amesema atazidi kushirikiana na wizara hiyo ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatulika na kuifanya wilaya hiyo kuzidi kunufaika na mifugo iliyopo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akifafanua jambo kwa viongozi wa Wilaya ya Hai (hawapo pichani) namna ya kuiboresha sekta ya mifugo wilayani humo
Baadhi ya viongozi wa Wialaya ya Hai, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya wakiwasilisha hoja mbalimbali kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega

MAMBA WAGEUKA KERO KWA WANANCHI WA KILANGALANGA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI 

WIMBI la mamba katika ukanda wa mto Ruvu, kata ya Kilangalanga, Kibaha Vijijini mkoani Pwani linadaiwa kuwa wengi hali inayojenga hofu kwa wananchi ambapo hadi sasa watu wawili wameshajeruhiwa na mamba hao. 

Aidha  wanyama waitwao Kiboko wanadaiwa kuvamia baadhi ya mashamba ya watu na kuharibu mazao ikiwemo mpunga. 

Akielezea tukio hilo, diwani wa kata ya Kilangalanga, Mwajuma Denge aliomba idara husika isikie kilio chao kwa kuvuna mamba badala ya kuwatega. 

"Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana mmama mmoja alijeruhiwa mkono na mamba na alifikishwa Tumbi hospital ambako anatakiwa kiasi cha sh. 500,000 hadi sasa ili aweze kufanyiwa operesheni na matibabu zaidi "

"Wiki mbili zilizopita pia mama mwingine amejeruhiwa makalio na alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi na alitibiwa kisha amehamishiwa hospital ya Tumbi anaendelea na matibabu hadi sasa. "alielezea Mwajuma. 

Mwajuma alisema kuwa, viboko nao ni kero nyingine wanaomba idara ya wanyamapori waende wakaangalie namna ya kuwadhibiti kwani hawajui wanapotokea. 

"Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa alichukua hatua na kufanya juhudi binafsi kupeleka watu wa maliasili ambao wanaendelea na jitihada zaidi." 

"Kutokana na mto kujaa na kuweka maji ya rangi ya tope wameshindwa kuwapata mamba hao, na wameacha zoezi hilo, watarudi baada ya wiki moja. "alielezea. 

Nae,  makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,ambae pia ni diwani wa Kikongo Fatma Ngozi alisema tatizo hilo, lipo na kata zilizopita mto huo ikiwa ni sanjali na Dutumi, Mtongani, Kwala,na Kikongo .

Alifafanua, mamba waliwahi kuvunwa tangu miaka ya 90 hivyo wamejaa inabidi wapunguzwe. 

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA IKULU ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi Tanzania Nchini Zambia Balozi Hassan Simba Yahya, alipofika Ikulu Zanzibar  leo 22-3-2019, kwa mazungumzo na Rais.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Hassan Simba Yahya, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 22-3-2019(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Balozi Hassan Simba Yahya, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo, 22-3-2019.(Picha na Ikulu)

KATIBU MKUU WA YANGA OMAR KAYA NA GODSON KARIGO WAHAMASISHA WATANZANIA KUSHAINGILIA TAIFA STARS


RC PAUL MAKONDA AAHIDI MENGI ENDAPO TAIFA STARS ITASHINDA JUMAPILI DHIDI YA UGANDA CRANES

UONGOZI WA BUNGE SPORTS CLUB WAITAKIA HERI TIMU YA TAIFA STARS

$
0
0
Mwenyekiti wa Timu ya Michezo ya Bunge (Bunge Sports Club), William Ngereja akizungumza na waandishi wa habari kuitakia heri Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) katika mchezo wake wa kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda inatoyatarajiwa kuchezwa tarehe 24 Machi, 2019 Jijini Dar es Salaam, Mkutano huo ulifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Mhe. Vanance Mwamoto na Katibu Wa Timu, Ndugu Waziri Kizingiti. (Picha na Ofisi ya Bunge
 Mwenyekiti wa Timu ya Michezo ya Bunge (Bunge Sports Club), William Ngereja akizungumza na waandishi wa habari kuitakia heri Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars) katika mchezo wake wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda inatoyatarajiwa kuchezwa tarehe 24 Machi, 2019 Jijini Dar es Salaam, Mkutano huo ulifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, (Picha na Ofisi ya Bunge)

WAVAMIZI SHAMBA LA MITI BIHARAMULO WAPEWA MIEZI 3

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Ametoa muda huo ili wananchi  waliolima   mazao mbalimbali yakiwemo  mahindi na pamba  waweze kuvuna mazao yao  kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.

Mhe.Kanyasu  ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya   kutembelea shamba la miti Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.

Amesema Oparesheni hiyo haitasubiri taarifa ya Wizara tano inayoendelea kufanyiwa kazi kwa kuwa eneo hilo halihusiani na vile vijiji 366  vilivyokutwa ndani ya Hifadhi.

Amesema  haiwezekani wananchi waliovamia eneo hilo waendelee kuachwa kwa kisingizio cha Kauli ya Rais aliyoitoa Januari 15 mwaka huu kuhusiana na vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya maeneo ya Hifadhi.

Amebainisha kuwa wananchi waliovamia eneo hilo wameitafsiri visivyo Kauli hiyo na kuongeza kuwa baada tu ya tamko la Mhe. Rais , baadhi ya wananchi hata wale waliokuwa wakiishi  katika maeneo mengine nje ya hifadhi waliendelea  kuvamia na kuanza kujimilikishia  maeneo makubwa  wakidai kuhalalishwa na tamko la Rais.

Amefafanua kuwa taarifa inayoendelea kufanyiwa kazi  na timu ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Wizara tano imebainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya vijiji 700 vimekutwa ndani ya Hifadhi badala 366 vilivyoripotiwa awali.

Kufuatia hali hiyo amesema baadhi ya wavamizi wa Hifadhi katika maeneo mbalimbali wataendelea kuondolewa bila kusubili kukamilika kwa zoezi linaloendelea kwa kuwa walieendelea kuvamia maeneo ya Hifadhi kwa kisingizio cha tamko la Rais huku maeneo hayo yakizidi kuharibiwa kwa miti kukatwa na shughuli nyingi za kibinadamu

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kutenga Bajeti ya kugharamia operesheni ya kuwaondoa  wavamizi ndani ya Shamba hilo.

Ameitaka TFS kuendesha oparesheni za mara kwa mara ili wavamizi hao wajue Serikali ipo kazini kulinda rasilimali za Taifa muda wote.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Chato,  Mtemi Simeoni akizungumza katika ziara hiyo  alisema kuwa  baadhi ya wananchi kutoka nje ya wilaya hiyo wamekua wakivamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba hilo, suala ambalo ni kinyume cha sheria.

Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa wananchi katika maenro hayo wana mahitaji makubwa ardhi na kuiomba Wizara iangalie  namna ya kuwasaidia  hekari 5000 ili wapate maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba hilo Bw. Thadeus Shirima  amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa hadi sasa zaidi ya hekari 900 zimepandwa miti licha ya Shamba hilo  kukabiliwa  na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendea kazi.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati)  akizungumza   na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe.  Mtemi Simeoni (kushoto)   wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa  ukubwa  wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita., Kulia ni Meneja wa shamba hilo, Edward Nyondo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Chato,  Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto)  alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo  kwa  ukubwa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine ni watumishi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  akizungumza na  wananchi pamoja na watumishi wa shamba la miti la Biharamulo ambalo mara baada ya kukamilika kwa kupandwa miti katika eneo lote litakuwa ndio  shamba la pili kwa ukubwa kati ya mashamba  20 yanayomilikiwa na Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania lililopo wilayani Chato mkoani Kagera.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipanda mti wakati alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa  hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
 Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni akipanda mti wakati alipoambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada  ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa  hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya na watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Baadhi ya watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika shamaba hilo hukuakiwasisitizan umuhimu wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wanaoishi karibu na shamba hilo. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

BREAKING NEWZZZZ: Askari Magereza Wanne Wasimamishwa kazi kwa Kuingiza Gereza la Ruanda mkoani Mbeya

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha kwa Waandishi wa habari baadhi ya simu zilizokamatwa kwa wafungwa katika Gereza La Ruanda jijini Mbeya.
Habari na Picha na Wizara
ya Mambo ya
Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amemuelekeza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi askari magereza wanne wanaotuhumiwa kuingiza simu za mikononi kwa wafungwa na kurahisisha mawasiliano kati ya wafungwa na watu walioko nje
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Mbeya Naibu Waziri Masauni amesema kumekuwepo na tabia ya kuingiza vitu visivyoruhusiwa magerezani ikiwemo simu, madawa ya kulevya huku baadhi ya askari wachache wasio waaminifu wakitumika katika mchezo huo.
“Nimefanya ziara katika Gereza la Ruanda, nimezungumza na wafungwa na kugundua kuwepo kwa simu ambazo mkuu wa gereza alizikamata. Maagizo ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli wakati akimuapisha Kamishna Jenerali wa Magereza ni kukomeshwa kwa tabia ya kuingiza simu magerezani ambalo Rias alisema limekuwa jambo la kawaida,sasa haiwezekani maagizo ya kiongozi wa juu kabisa yapuuzwe...Sasa namuelekeza Kamishna wa Magereza kuwasimamisha kazi askari hao wanne na aunde tume kuchunguza kwa kina zaidi tukio hilo” alisema Masauni
Aliwataja askari hao  na vyeo vyao kuwa ni  Longino Mwemezi (Inspekta),  Alexander Mwijano (Stafu Sajenti) Benjamini Malango (Sajenti)  na Ramadhani  Mhagama huku askari wengine wanne wakiendelea kuchunguzwa kutokana na tuhuma hizo.
Jumla ya simu za mkononi tisa zimekamatwa katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya huku zikishikiliwa kwa uchunguzi zaidi wa kubaini watu waliokuwa wanawasiliana na wafungwa hao na aina ipi ya mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika

Kikao Kazi Cha Pili Cha Serikali Mtandao 2019 Chuo Kikuu cha Dodoma

MJUE ALI CHOKI MZEE WA FARASI

Fursa kwa Makampuni ya Tanzania kupata soko China

$
0
0
Makampuni ya Tanzania yanayohitaji kuuza bidhaa katika soko la China yamekaribishwa kutumia mtandao ( E-commerce platform)- mall.ca-b2b.com/index ulioanzishwa mahususi kwa ajili ya kuyakutanisha makampuni yanayonunua na kuuza bidhaa mbalimbali  katika masoko ya China na Afrika

Fursa hiyo imeelelezwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya China-Africa E-Commerce ndugu Zhigang Hou alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki leo jijini Chengdu katika jimbo la Sichuan

Mtandao huo ulioanzishwa mwaka jana una makampuni 5000 yaliyosajiliwa kwa madhumuni ya kutafuta bidhaa mbalimbali zinazopatikana barani Afrika. Inatarajiwa kwamba ifikapo mwaka 2021 mtandao huo utaratibu biashara yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 200.

Balozi Kairuki ameyataka makampuni ya Tanzania yenye bidhaa zenye viwango na ubora  unaotakiwa na soko la kimataifa wajisajili katika mtandao huo ili waweze kukutana na makampuni yanayohitaji kununua bidhaa zao. Aidha, wafanyabiashara wanaotaka kununua bidhaa kutoka China pamoja na nchi nyingine za Afrika nao wanaweza kujisajili katika mtandoa huo ili waweze kukutana  na wauzaji mbalimbali.

Makampuni yenye nia ya kupata taarifa za kujiunga na mtandao huo yanaweza kuwasiliana na mratibu:  zhounana@ca-b2b.com











Jinsi ya kupata nakala ya Kitambulisho cha Taifa inayoweza kukusaidia kutambulika bila kuwa na Kitambulisho halisi.

WATOTO WA TAIFA STARS KUTOKA TABATA WATAKUWEPO TAIFA KUHAMASISHA

TANZANIA, UGANDA ZAJADILIANA ULINZI BOMBA LA MAFUTA

$
0
0
Ikiwa ni muendelezo wa majadiliano mbalimbali kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania (EACOP), Kamati za Ulinzi na Usalama za mradi kutoka  nchi hizo zimekutana jijini Kampala kwa lengo kujadili masuala ya usalama ya mradi huo.

Kikao kati ya pande hizo mbili kilianza tarehe 18/3/2019 na kuhitimishwa tarehe 20 mwezi huu  na Wawakilishi wa Wakuu  wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa nchi hizo mbili ambapo  kuliandaliwa Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi wa Bomba la Mafuta. 

Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi huo yanatarajiwa kusainiwa katika vikao vijavyo vya ngazi ya Mawaziri wa nchi husika.
Watendaji kutoka Tanzania na Uganda wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao chao kilichohusu masuala ya usalama katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
 Watendaji kutoka Tanzania na Uganda wakiwa katika kikao cha majadiliano kilichohusu masuala ya usalama katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.
Wataalam kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha majadiliano kilichohusu masuala ya usalama katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania.

JIMMY CARTER APEWA CHEO KIPYA BAADA YA KULA CHUMVI KUMZIDI GEORGE H.W

$
0
0
Awa Rais Mkongwe zaidi anayeishi nchini Marekani, Avunja rekodi ya Rais George H.W Bush aliyefariki akiwa na miaka 94 na siku 171

Na Leandra Gabriel, Blogu yajamii
ALIYEKUWA Rais wa 39 wa  Marekani Jimmy Carter amevunja rekodi kwa kuwa Rais mzee zaidi anayeishi nchini humo.

Amepewa cheo hicho leo Machi 22 mara baada ya kufikisha miaka 94 na siku 172 akivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya  41 George H.W Bush ambaye alifariki  mwezi Novemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 94 na siku 171.

Catter alizaliwa October 1, 1924 na alihudumu kama Rais wa 39 wa Marekani kuanzia 1977 hadi 1981 na kabla ya kuhudumu nafasi hiyo amewahi kushika nyadhifa katika ngazi za Bunge kwa miaka ipatayo 10.

RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI SHEREHE ZA MEI MOSI MBEYA

$
0
0
Na Emanuel Madafa, Mbeya 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Albert Chalamila amesema Rais Dkt Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Meimosi  nchini ambazo kitaifa zinatarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo jijini Mbeya katika kikao cha kwanza cha Maandalizi kwa ajili ya sherehe hizo za wiku ya wafanyakazi Nnhini ambacho kimehudhuliwa na viongozi wa shirikisho la vyama vya vya wafanyakazi Nchini TUKTA.

Chalamila amesema kuanzia tarehe moja watakuwa na ugeni wa Rais Dkt Magufuli hivyo wanacho subiri kwa sasa ni taratibu na taarifa Kutoka kwenye Ofisi yake ambayo itaweka bayana ujio wa Rais Magufuli katika sherehe hizo za Mei Mosi Mkoani hapa .

“Rais amekubali kuwa mgeni rasmi kwahiyo tunatarajja kwamba kuanzia tarehe moja tutakuwa nae ,ni lini atafika mkoani mbeya hii tunasubiri taarifa na taratibu kutoka katika ofisi yake na tutapewa kwa maandishi kwamba sasa Rais magufuli anakuja lini na wakati gani “RC Chalamila.

Aidha kuhusu ushiriki wa vyama vya kisiasa katika sherehe hizo za Mei Mosi Mkuu huyo wa Mkoa amesema wanachokitaka nikuona sherehe hizo haziegemei katika upande mmoja wa chama cha kisiasa kwani tukio hilo ni kubwa na linabeba  taswira ya watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa kitaifa wa serikali na vyama .

“Vyama vya kisiasa vinavyama  vyao hivyo vitashiriki  vizuri kabisa tunachokitaka sisi nikwamba hatupendi tukio hilo lionekane linaegemea upande mmoja wa chama  cha kisiasa,bali ni tukio ambalo litakuwa na malengo ,hisia na matarajio ya kitaifa ambapo wageni mbalimbali watakuwa hapa.”Amesema Chalamila.

Wakati huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo nakwamba serikali haita zuia mtu yeyote kuandika bango lolote ili mradi liwe limeandika kitu che haki .

Sherehe hizo za Mei Mosi zilifanyika Mkoani hapa 2013 na kuhudhuliwa na Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images