Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Maandalizi ya fainal za AFCON U-17 yanaendelea vizuri

0
0
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Fainali za AFCON U-17 Bw.Leodigar C.Tenga akiongoza Kikao cha Maandalizi ya Fainali hizo leo Jijini Dar es Salaam zinazotarajiwa kufanyika hapa nchini kuanzia Aprili 14 – 28 2019 ambapo timu ya Serengeti Boys itashiriki.
Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia Kikao cha Maandalizi ya Fainali za AFON U-17.kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Fainal hizo  Bw.Leodigar C.Tenga hizo leo Jijini Dar es Salaam zinazotarajiwa kufanyika hapa nchini kuanzia Aprili 14 – 28 2019 ambapo timu ya Serengeti Boys itashiriki.

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MECHI YA TAIFA STARS NA THE UGANDA CRANES JUMAPILI TAIFA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia Taifa Stars akitoa wito kwa wadau na wakazi wa Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi kushangilia Taifa Stars wakiungana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhakikisha tunapata ushindi
 Msanii wa Filamu na Aliyekuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu akitoa wito kwa Mashabiki na Team Wema Wote kufika kwa Wingi kuipa sapoti Taifa Stars .
 Mtaalamu wa Masuala ya Mitandao ya Kijamii,William Malecela Le Mutuz Super Brand akiwataka watu wote wanaotumia Mitandao ya kijamii kutumia simu zao kwa muda wa siku hizi tatu kutoa hamasa kwa ajili ya kuisapoti timu ya Taifa ya Tanzania.
 Mwenyekiti wa Bongo Movie Tanzania  Steve Nyerere akitoa wito kwa wapenzi wa Filamu kujitokeza kwa wingi

 Mchambuzi wa mpira wa Miguu, Eddo Kumwembe akizungumza na namna tunavyoweza kushinda.
 Mwandishi na mchora Vibonzo Maarufu Nchini, Nathan Mpangala (Kijasti) akieleza namna wachora Vibonzo walivyojipanga kuisadia Taifa Stars
Sehemu ya Waandishi wa Habari na Watu Maharufu walioshiriki mkutano wa kuhamasisha Taifa Stars Ishinde

Honda Motor Southern Africa Proprietary Limited's Public Notice

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 22,2019

Special Olympics kuwasili nchini leo na medali lukuki

0
0
TIMU ya Taifa ya walemavu wa akili, wanatarajia kuwasili nchini leo mchana ikiwa na medali 15 kutoka katika michezo ya Dunia ya walemavu wa akili iliyomalizika Falme za Kiarabu (UAE).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays katika medali hizo, 12 za dhahabu, fedha moja na Shaba 2 zilizopatikana katika Riadha na Mpira wa Wavu.

Rays alisema michezo hiyo iliyochezwa UEA, michezo ya Riadha ilichezwa Abu Dhabi huku Mpira wa Wavu michezo hiyo ilifanyika Dubai.

Katika mpira wa Kikapu, Tanzania imeibuka mabingwa baada ya kuiadhibu Italia kwa seti 2-1 katika fainali.

Rays alisema katika riadha Tanzania imezoa medali 9 za dhahabu , Fedha moja na shaba 2 ambako Boniventura Anga wa Mtwara alipata medali ya dhahabu.

Aidha katika michezo hiyo, Tanzania ilishiriki michezo hiyo sambamba na wachezaji kutoka kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nyarugusu.

Katika mapokezi hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Nkenyenge anatarajia kuwapokea wanamichezo hao ambao wameiletea heshima Tanzania katika michezo hiyo.

Michezo ya dunia ya majira ya kiangazi yalianza Machi 14 na kumalizika Machi 21 (UAE).


  Mwanariadha Boniventura Anga kutoka Mtwara akionesha medali yake ya dhahabu baada ya kufanya vizuri katika michezo ya dunia iliyomalizika Falme za Kiarabu.
 Picha ya pamoja
 Mkurugenzi wa Special Olympics International (SOI), Tim Shriver akipunga mikono juu na timu ya Taifa ya Tanzania katika michezo ya dunia nchini UAE



PAC yajiridhisha mtambo wa TTMS wa TCRA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema kuwa imeridhishwa na mtambo wa TTMS wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) unavyofanya kazi katika katika kulinda usalama wa Mawasiliano nchini.

Akizungumza wakati Kamati hiyo ilivyotembelea Mamlaka Hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Naghenjwa Kaboyoka amesema kuwa wamejiridhisha katika mtambo huo kwa umerahisisha TCRA kufanya kazi kwa ufanisi katika kuweza kusaidia serikali kupata mapato.

Amesema walikuwa na shaka kuhusiana na mtambo huo lakini wamejiridhisha kwa na kuondoa mashaka hayo kwa kamati na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) nao wamejiridhisha na mtambo huo.

Kaboyoka amesema TCRA imepiga hatua nzuri katika mawasiliano kwa kuwa na watendaji mahiri wa kuendesha mtambo huo.

"Uzuri wa mtambo TTMS unasimamiwa na wazawa hii inaoyesha kuwa kila kinachofanyika kitakwenda sawa kuliko mtambo huo ungesimamiwa na watu wa nje"amesema Kaboyoka.Aidha amesema kuwa TCRA iendelee kudhibiti mawasiliano ikiwa ni pamoja na kwenda kukuza uchumi wa nchi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema kuwa mtambo huo unaweza kukokotoa takwimu zote miamala ya fedha unavyofanywa na kampuni za simu kutoka na moja kwenda Mtandao mwingine.Amesema kazi nyingine ni kusimamia simu ndani na nje sambasamba na kutambua simu za ulaghai, uhakiki wa mapato na ubora wa mawasiliano.

Amesema kuanza kwa mfumo huo umesaidia kupunguza simu za ulaghai kutoka asilimia 65 hadi kufikia asilimia 10 ikiwa ni pamoja kuongeza pato la Taifa kwa asilimia 9.8.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipotembelea Mamlaka hiyo.
 Afisa wa Makumbusho wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Abdulrahman Milasi akitoa maelezo wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo katika Makumbusho ya vitu vilivyotumika zamani katika mawasiliano.
 Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA Dkt Jonas Kilimbe akitoa maelezo kuhusiana na utendaji wa TCRA wakati Kamati ya PAC Ilipotembelea Mamlaka hiyo.
 Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)Jumanne Ikuja akitoa maelezo katika gari la kuangalia masafa wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC)  Naghenjwa Kaboyoka akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA).

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUTOKEA TETEMEKO LA ARDHI MKOA WA RUKWA.

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI YATAKAYOWEZESHA UTEKELEZAJI WA UJUMUISHWAJI WA MASUALA YA KIJINSIA SEHEMU ZA KAZI

0
0
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akitoa maelekezo kuhusu maazimio wakati wa kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro. 

Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akifunga kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro. 


Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakijadiliana maazimio wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Christina Mangwai akichangia mada wakati wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.


Mkurugenzi Msaidizi, Idara wa Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta akitoa mada kuhusu uzoefu wa taasisi yake katika masuala ya kijinsia kwenye kikao cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.

………………….

Taasisi za umma nchini zimetakiwa kuweka mazingira rafiki sehemu za kazi ili kuwezesha utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa ufanisi na hatimaye kufikia usawa wa kijinsia utakaokuwa na tija kwa maendeleo ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengo la kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika taasisi za umma.

Bi. Leila amesema kuwa, mazingira rafiki ya ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi yanategemea menejimenti za taasisi za umma kutoa kipaumbele kwa masuala ya anuai za jamii kuwa ni sehemu ya shughuli za uendeshaji wa ofisi za kila siku.

Bi. Leila ameainisha kuwa, ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia utafanikiwa iwapo kutakuwa na uelewa wa pamoja wa masuala ya kijinsia kwa watumishi wa umma na menejimenti zao ambao utasaidia kuepuka ubaguzi na unyanyapaa mahala pa kazi na kuongeza kuwa, taasisi za umma zikijenga majengo jumuishi yenye miundombinu inayofikika kwa urahisi na wadau wote hususan watu wenye ulemavu wa viungo, zitawezesha jinsia zote kupata huduma bora bila kikwazo cha aina yoyote.

“Ni vema taasisi zikaweka mifumo thabiti itakayoweka mazingira rafiki, wezeshi na mifumo rejeshi inayotoa fursa kwa wananchi kutoa taarifa za masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na ukiukwaji wa maadili kwa ujumla” amesema Bi. Leila.

Bi. Leila amezitaka taasisi zote za umma kuhakikisha kwamba, zinatenga bajeti kwa ajili ya ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi na kuyafanya masuala ya kijinsia kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya kitaasisi vya ndani na nje.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hamidi Mbegu amesema kuwa, kikao kazi hicho cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kitakuwa ni chachu ya kuboresha utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika wizara yake na taasisi zote za umma.

Aidha, Bw. Mbegu amesema, kikao hicho kimeazimia kuwepo mwongozo rasmi utakaowezesha utekelezaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi, ambao utasaidia uanzishaji wa madawati ya kijinsia sehemu za kazi ambayo yatarahisisha utekelezaji na ufuatiliaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi.

Naye, Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Mradi wa SAUTI kutoka Shirika la Jhpiego, Bi. Grace Munisi amesema kuwa, serikali imekuwa ikishirikiana na mradi huo katika utekelezaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kupitia udhamini wa warsha mbalimbali zinazosaidia kuwapa uelewa watendaji juu ya mahusiano ya kijinsia yanavyoweza kusababisha maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kuepuka mila potofu zinazosababisha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI sehemu za kazi na kwenye jamii kwa ujumla.

Kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi katika Taasisi za Umma kilijumuisha Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka katika Wizara, kwa lengo la kujadili fursa na changamoto za masuala ya kijinsia katika utumishi wa umma ili kuweka mikakati endelevu itakayofanikisha uwepo wa Usawa wa Jinsia mahala pa kazi utakaowezesha maendeleo endelevu.

RAMA AKUDO ASIMULIA MACHUNGU AKIPIGANIA UHAI WAKE

0
0
 Pichani kati Meneja wa bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Ramadhani Pesambili ‘Rama Akudo’, akiendelea kujiuguza,pichani kushoni mi Mwandishi wa Makala hii Rhobi Chacha
Pichani Meneja wa bendi vya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Ramadhani Pesambili ‘Rama Akudo’, kabla hajaanza kuumwa


NA RHOBI CHACHA

Kweli hujafa hujaumbika, leo mzima kesho kitandani. Hii imemkuta Meneja wa bendi vya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Ramadhani Pesambili ‘Rama Akudo’, ambaye kwa sasa yuko kitandani akipigania uhai wake baada ya kufanyiwa operesheni tatu.

Mwanaspoti ni mdau mkubwa wa burudani na lilimtembelea nyumbani kwake Mwananyamala Komakoma maeneo ya Kopa Kabana jijini Dar es Salaam ili kufahamu tatizo lililomkumba na anasema alianza kuumwa akiwa Dodoma kwenye shoo ya Akudo Impact Februari mwaka jana, ambako alihisi mguu kama umestuka na kupata maumivu makali.

 Hata hivyo, baada ya muda yalipungua na kurudi Dar es Salaam akiwa salama kabisa.

“Sasa kuna siku nimetoka katika matembezi yangu, nikiwa narudi nyumbani nikafika Mwananyamala A, nikaona kama mguu umepigwa shoti, nikawa nashindwa kutembea, nilitulia kidogo, mara akatokea rafiki yangu mmoja akanipa msaada wa kunikokota hadi kunifikisha nyumbani kwangu. 

Huwezi kuamini, nilitumia takriban saa tatu hadi kufika ilhali hapo Mwananyamala A hadi kwangu ni mwendo wa dakika tano tu. Nilipofika nyumbani yule rafiki yangu aliyenisindikiza akanishauri niende hospitali. 

Tukaenda Hospitali ya Taifa Muhimbili. Baada ya kupata matibabu majibu yalikuja kuwa nimegundulika nina usaha kwenye nyonga, nikapewa dawa za kutumia.Hali ikazidi kuwa mbaya ndipo nikafanyiwa upasuaji kwenye nyonga na kutolewa usaha nusu kisado.”

Rama Akudo ambaye alianza umeneja katika bendi ya Akudo mwaka 2012, aliongeza; “Baada ya upasuaji huo wa kwanza, nilipata nafuu kidogo tofauti na yale maumivu ya mwanzo niliyokuwa nayasikia.

 Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda hali ilibadilika tena ikabidi nipelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Tawi la Mloganzila iliyopo Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam, pale nilianza kuchukuliwa vipimo upya. Wakachukua kinyama sehemu ya nyonga na kuambiwa nisubiri majibu baada ya wiki. 

Lakini kila nikifuatilia majibu ikawa naambiwa bado-bado, ndipo nikaamua kwenda hospitali nyingine ya Ibrahim Hajj iliyoko Posta jijini Dar es Salaam baada ya kuona majibu yangu yanachelewa na maumivu yanazidi.

“Hapo Ibrahim Hajj nilipata vipimo na kuambiwa natakiwa kufanyiwa upasuaji ili nikamuliwe tena usaha, hivyo sikuwa na ubishi kwani maumivu niliyokuwa nayapata Mungu ndiyo anajua, hiyo sasa ikawa ni upasuaji wa pili. 

Kiukweli ilikuwa kila nikikamuliwa usaha ndiyo napata nafuu.
“Sasa nikawa najiuliza, haya maisha ni hadi lini? Nimekosa nini mimi maana hata ugonjwa sijui ninachoumwa daah! Sijui kwa kweli uhai wangu mimi Rama Pesambili. 

Ila baada ya kutolewa huo usaha tena nikawa naendelea na matibabu lakini maumivu yalikuwa yanazidi kadri siku zinavyozidi kwenda na miguuni nikawa nakosa nguvu hata ya kutembea, siku moja nilizidiwa sana nikarudishwa hospitalini tena.

“Nilirudishwa katika hospitali ya Ibrahim Hajj ambao walinifanyia upasuaji wa pili.

 Nilipofika wakanilaza na kuanza kuchukua vipimo na kuendelea na dawa. Majibu yao walikuja kuniambia kuwa natakiwa kufanyiwa upasuaji mwingine wa kukatwa korodani moja, niliumia sana na kuyasikitikia maisha yangu, kwa nini chanzo cha kichomi na mguu kushtuka yamefika hapa! Kiukweli niligoma lakini baada ya muda maumivu yalizidi kuwa makali, ikabidi nikubali kutolewa korodani moja, hapa kwa sasa nimebaki na korodani moja.”

Rama Akudo anasema tangu aondolewe korodani moja, hali yake imekuwa na nafuu yaliyobaki ni maumivu ya mguu tu, ambayo kwa sasa anatembelea magongo.“Nina nafuu, japo maumivu yaliyobaki ni kwenye mguu ambao umesababisha kwa sasa natembelea magongo, na hivi ulivyonikuta ndio maisha yangu nashinda ndani tu na muda mwingi nalala kwa ajili ya kunyoosha miguu,” anasema.

 Gharama za matibabu 

“Niwe tu mkweli, sina kitega uchumi chochote ninachotegemea kupata pesa zaidi ya misaada kutoka kwa watu wangu wa karibu.

 Nilipoanza kuumwa Mh. Kapuya alitoa pesa za kufanyiwa upasuaji mara ya kwanza na siku zilivyoendelea kuna kundi moja la muziki wa dansi linaitwa Cheza Kidansi lilijichangisha pesa na kunipatia.

 Pia kuna mdau mmoja wa muziki wa dansi, Jimmy Kamuzora, alikuja kunitembelea hapa nyumbani na kuniachia pesa. Wapo watu wananipa msaada japo wengi hawajui kama naumwa, ila nadhani wakiona wewe ukienda kuandika gazetini, ndio watajua, sababu hakuna mwandishi yeyote aliyekuja kuniona.

Rama Akudo anasema watakaoguswa na hali ngumu anayopitia hivi sasa watamfariji sana kama wakimchangia ili aweze kuendelea kupambana kujaribu kuokoa maisha yake.

 Nani anamuuguza ?

Tangu ameanza kuumwa, Rama Akudo anasema anauguzwa na kaka yake ambaye ametoka Tabora, akishirikiana na mke wake, ambaye wamejaaliwa kupata mtoto mmoja.

 Siku Mwanaspoti lilivyoenda nyumbani kwake lilimkuta kaka yake akimhudumia.

 Atimkia Tabora 

Wiki moja baada ya mahojiano na Mwanaspoti, Rama alilipigia simu Mwanaspoti na kutaarifu amesafiri kwenda nyumbani kwa Mh Kapuya, Tabora Wilaya ya Kaliua kwa ajili ya kwenda kuugulia huko.

“Mimi naomba tu kitu kimoja kwa watu wangu wote wa karibu, wadau wa muziki wa dansi na hata wasio karibu na mimi wala wasio wadau wa dansi, kinachoendelea kuhusu afya yangu, wazidi tu kuniombea ili nirudi katika hali yangu ya kawaida na kwa watakaoguswa na kutaka kunipatia msaada basi watume tu kwenye namba hizi 0715-862051 hii ni Tigo na Voda ni 0764888840 jina ni Rama Pesambili. Mungu aendelee kuwabariki sana na naomba maombi yenu,” anasema Rama Akudo.

HABARI HII KWA HISA YA GAZETI LA  MWANASPOTI.

MAOFISA USTAWI WA JAMII SHINYANGA WATINGA GEREZANI KUSHEREHEKEA SIKU YA USTAWI WA JAMII

0
0
Maofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga wameungana na wenzao duniani kote kuadhimisha Siku ya Ustawi wa Jamii kwa kutembelea wafungwa wanawake katika gereza la Shinyanga,kutoa chakula kwa kaya maskini na kutoa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya watoto kwa wanafunzi.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo mkoani Machi 21,2019 ,Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa, Lidya Kwezigabo, alisema wameamua kutembelea wafungwa wanawake kwenye gereza la Mjini Shinyanga ambao wamefungwa na watoto wao, ili kutoa elimu ya ulinzi wa mtoto na kuweza kupata haki zao za msingi. 

Alisema mbali na kutembelea wafungwa hao, pia wameona ni vyema kwenda kutoa elimu ya ukatili na kujitambua kwa wanafunzi mashuleni kwani wanafunzi ndiyo waathirika wakubwa wa vitendo hivyo, lengo likiwa ni kutokomeza matukio hayo ndani ya jamii. “Sisi Maofisa Ustawi wa Jamii mkoa Shinyanga kwa pamoja tumeamua kuadhimisha siku yetu hii kwa kutoa elimu zaidi juu ya kutomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwamo kutimiza malengo yao ya kielimu,”alisema Kwezigabo. 

“Pamoja na kutoa elimu ya ukatili pia tumetoa msaada wa sabuni za kufulia, kuogea na dawa za mswaki kwa wanawake ambao wamefungwa kwenye Magereza ya Shinyanga pamoja na msaada wa chakula kwenye kaya maskini iliyopo kata ya Mwasele katika Manispaa ya Shinyanga,”aliongeza. 

Naye Ofisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Elizabeth Mweyo aliwataka wanafunzi hao pale wanapofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ama mwenzao, wawe wanatoa taarifa kwa walimu au viongozi wa Serikali ili waweze kusaidiwa na kupata haki zao kwa mujibu wa sheria. Pia aliwataka kuacha kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa bado wanafunzi na kutopenda vitu vya dezo ikiwamo Lifti, vitu ambavyo vimekuwa vikiwaingiza kwenye vishawishi na kujikuta wakiambulia kupewa ujauzito na kuachishwa masomo yao. 

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Sekondari Chamaguha ambayo ilitembelewa na Maofisa Ustawi wa Jamii Abdalla Lidyati, alipongeza utolewaji wa elimu hiyo ya ukatili na kujitambua kwa wanafunzi hali ambayo itasaidia kuondokana na mimba mashuleni. Maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii kitaifa yamefanyika Machi 21,3,2019 Jijini Arusha.  
Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga, Lidya Kwezigabo akizungumza kabla ya kuanza kugawa msaada wa sabuni za kufulia na kuogea pamoja na dawa za meno kwa ajili ya matumizi ya wafungwa wanawake ambao wamefungwa na watoto wao katika gereza la Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Mkuu wa Gereza la Shinyanga Paulo sabuni Kamole (kulia) akipokea msaada wa sabuni za kufulia na kuogea pamoja na dawa za meno kutoka kwa Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwezigabo. Mkuu wa Gereza la Shinyanga Paulo Sabuni Kamole, akishukuru msaada huo kutoka kwa Maofisa Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kuwatatulia changamoto ndogo ndogo wafungwa wanawake pamoja na kuwapatia elimu ya ulinzi wa mtoto. Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwezigabo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha na kuwataka wapinge masuala ya ukatili ndani ya jamii kwa kuanza na wao wenyewe. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Chamaguha Shinyanga mjini wakisikiliza kwa makini elimu ya makuzi na kupinga masuala ya ukatili ambayo yamekuwa yakizima ndoto zao. Wanafunzi wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga ukatili. Ofisa ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo, akiwataka wanafunzi hao hasa wa kike waache kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa katika umri mdogo na kuacha tamaa ya kupenda chips na Lift, ili wapate kutimiza ndoto zao. Ofisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Agnes Cinethon akiwataka wanafunzi hao hasa wa kike pale wanapobakwa wawahi kwenye vituo vya afya ili waweze kupatiwa matibabu ya haraka na kuwazuia kutopatwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Ofisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Sophia Kang'ombe ambaye huwa ana hudumia Kambi ya wazee Kolandoto akiwataka wanafunzi hao kupenda Babu na Bibi zao wakiwamo na wazazi ili kujenga mahusiano mazuri ambayo yatawasaidia kuwa wanatatuliwa shida zao, ikiwamo na kutoa taarifa za watu kutaka kuwafanyia ukatili na kuweza kutatuliwa. Wanafunzi wakiendelea na upewaji wa elimu ya makuzi na ukatili. Mwanafunzi Naomi Geogre akiuliza swali namna kesi za ukatili zitakavyoshughulikiwa pale watakapokuwa wakitoa taarifa za matukio hayo. Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari Chamaguha Abdalla Lidyati, akielezea kufurahishwa na ujio wa mofisa ustawi kwenye shule hiyo na kutoa elimu ya makuzi na ukatili, hali ambayo itasaidia kusiwepo na mimba shuleni hapo. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ushirika nao wakisikiliza elimu ya ukatili na kutakiwa wawe wanatoa taarifa mapema pale wanapoona kutaka kufanyiwa vitendo hivyo, ili vipate kushughulikiwa kabla ya kuwaletea madhara. Ofisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo akitoa elimu ya kupinga ukatili kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika. . Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

DKT. MAHIGA AZINDUA KAMPENI YA USAJILI NA UTOAJI VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO KWA MIKOA YA SINGIDA NA DODOMA

0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mtoto cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili watoto katika viwanja vya stand mjini Singida baada ya akizindua kampeni ya kitaifa ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Singida na Dodoma Machi 21,2019.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mzazi wa mtoto aliesajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa katika viwanja vya stand mjini Singida
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mtoto cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili watoto katika viwanja vya stand mjini Singida baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Singida na Dodoma Machi 21,2019.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wananchi mbalibali , wazazi na watoto waliopata vyeti vya kuzaliwa na watendaji wa RITA baada ya kuzindua usajili wa watoto kwa mikoa ya Singida na Dodoma katika viwanja vya stendi mjini Singida
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionyesha kitabu kinachotumika kusajili watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa baada ya kuzindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Singida na Dodomajini Singida leo

……………………

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amezindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Dodoma na Singida.

Akizindua kampeni hiyo, Dkt. Mahiga ameitaka RITA kuhakikisha inatunza taarifa za watoto wanazozichukua kupitia mtandao wa simu na kuhakikisha zinapatikana pale zitakapohitajika.

“Kuwasajili watoto hawa kwa kasi hii ni vizuri lakini kazi kubwa ni kuhakikisha taarifa hizo zinawekwa na kutunzwa kule zinakostahili na zinapatikana wakati wote”, alisema Dkt Mahiga.

Amesema Serikali itaendelea kulinda haki za msingi za raia wake na ndio maana umeamua kutekeleza mpango wa Usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwa kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto.

Amesema cheti cha kuzaliwa ni alama na vitambulisho wa uraia wa kila mtu na kwamba Tanzania imeamua raia wake wote wawe na utambulisho wao.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa RITA bibi Emmy Hudson amesema tangu kuanza kwa awamu ya kwanza ya kampeni hiyo jumla ya watoto milioni tatu wamesajiliwa na kupewa vyeti katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Simiyu, Geita, Njombe, Iringa, Songwe, Mara, Musoma, Lindi, Mtwara, Dodoma na Singida na inakadiriwa hadi kampeni hiyo itakapokamilika mwisho ni mwa mwezi huu zaidi ya watoto milioni tatu na nusu watakuwa wamesajiliwa.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi aliahidi kukusimamia Mkoa wa Singida ili uweze kufanya usajili kwa watoto zaidi ya lengo lililorekebishwa la watoto 280,000 ndani ya wiki mbili ambapo alisema hadi kufikia Machi 20 mkoa wake ulikuwa umesajili zaidi ya watoto 180,000

Kazi ya usajili wa watoto hao inafanywa na wasajili wasaidizi ambao wamepewa Mafunzo maalum ya kuingiza taarifa za watoto kwa kutumia simu ya Mkononi na inafanyika katika vituo vyote vya afya na katika ofisi za kata ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi mjini Singida na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji wa serikali kutoka mikoa ya Singida na Dodoma wadau wa maendeleo wa UNICEF, CANADA na kampuni ya TIGO ambayo imetoa simu na mtandao wa simu wake unaothmika kufanya usajili wa watoto katika mikoa hiyo nchini.

TRAILER YA FILAMU YA "SIVYO TULIVYO" INAYOZINDULIWA APRILI 13, 2019 NCHINI SWEDEN

MAAFISA HABARI WA SERIKALI WATOA MSAADA WA WA MIL. 7.5 KUWASAIDIA WAZEE BUKUMBI

TAARIFA KUHUSU DUA YA KUOMBA MVUA NCHINI

Bridging the water supply gap in Tanzania through ICT

0
0
 Availability of clean water is still a challenge in many developing countries. According to the Ministry of Water and Irrigation, in Tanzania, only 64% of rural dwellers have access to clean water compared to nearly 80% of urban residents. Challenges such as access to clean water sources, poor management of the water sources and incomplete water projects still impede the public and private partner’s strides in achieving availability of sustainable water supply and management of water sources


Various initiatives are underway to close the water supply gap and technology is playing a significant role to expedite the bridging process. Every March 22, the world commemorates the International Water Day, to commend the global efforts, partners and initiatives that ensure sustainable supply of water.


Revolutionizing Remittance Recovery in Water (R3W), is a project funded by Human Development Innovation Fund (HDIF) in partnership with Catholic Relief Services (CRS), to empower communities in Tanzania by building their capacity to reduce water wastage and improve revenue collection. R3W launched a first in the country, electronic water machine called AQtab that is housed in a local kiosk and uses a smart card to monitor and utilize water more efficiently. 

The project partnered with local water vendors such as Community Owned Water Supply Organizations (COWSOs), the Karatu Village Water Supply (KAVIWASU) and Endamarariek/Endabash Water Supply (ENDAWASU) and significantly ensured reliable and sustainable water supply in the communities. 

“Until mid-2018, 1,400 smart cards were disbursed to the community members and made a tremendous impact to the communities especially women whom prior to the invention, spent up to three hours waling to fetch water” said Engineer Ephraim Tonya, the Project manager.


Gongali Nanofilter is another organization that provides safe and clean water to communities across Arusha. With an objective of redirecting the amount of time spent fetching water to productive economic activities, Dr. Askwar Hilonga, the founder of Nanofilter, innovated the tech and assembled 30 Nanofilter stations to provide sustainable supply of water in the communities outside Arusha town. 

Also funded by Human Development Innovation Fund (HDIF), the project currently has 100 stations that have significantly bridge the water supply gap across Arusha and enabled the community members to invest their time in more productive economic activities such as small scale agricultural, and livestock keeping.


Given the population growth and increase in water consumption, the Government is accelerating its partner’s efforts by implementing the Water Supply Development Plan (WSDP) which is on its second phase from 2014 to 2019 and also through implementing the right policies to enable successful water projects in Tanzania. 

WSDP constitutes of programs intended to strengthen institutions in integrated water resources management and improve access to water supply and sanitation services across Tanzania. The Permanent Secretary of in the Ministry of Water and Irrigation, Professor Kitila Mkumbo recently affirmed scientists and innovators of the government’s support, assuring them that they will enact the right policies towards achieving the mutual objective of sustainable water supply in Tanzania.



The future of a cashless economy

0
0
Across the globe, new technologies are rapidly replacing coins and notes, with variations among countries. According to the World Payment Report (2018), non - cash transaction global volumes continue to grow at a double-digit rate of 10.1% within an ecosystem of 482.6 billion people. 

Multiple reports have also shown that the emergence of digital technologies is driving unprecedented change across African countries and Tanzania has joined the bandwagon of nations experiencing robust shifts in digital technology. These paradigm shifts include liberalisation of financial systems, improvements in infrastructure technology and innovations in payment systems. 

Prior to Tanzania’s independence, people paid for goods and services using various currencies such as: The East African rupee, the Zanzibari rupee, the Zanzibari riyal, British East Africa Florin and the German East African rupee. Since the government issued its first Tanzanian shillings in 1966, the country has by and large been a cash-based economy where the majority of businesses and transactions operate on a cash basis only. The introduction of M-Pesa in 2008 revolutionized the payment/transaction landscape in Tanzania; coupled with the advent of the Internet of Things, the rise of e-commerce will disrupt the way business is conducted. 
In the last decade, the country has seen ground breaking innovation of electronic payment methods ranging from mobile money, online banking, credit and debit cards, charge card e-wallet or QR scan to the Government e-Payment Gateway System (GePG). Recently, the Bank of Tanzania (BoT) launched an Instant Payment System (TIPS) which is set to create a shared platform for payments originating from different delivery sources to facilitate inter-provider payment for electronic systems and the use of digital financial services among payment service providers. The TIPS ecosystem includes traditional banking services, mobile money and telco network operators providing financial services. 

According to the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA), the use of mobile money in the country has recorded a robust growth in recent years, with the value of transactions averaging USD 1.6 billion per month, with over 45 million registered mobile money accounts. Mobile money platforms such as M-Pesa, continue to innovate and simplify the transfer of money across geographical boundaries as well as narrowing financial inclusion gap between men and women. 

There has also been an increase in the uptake by businesses in the utilization of online payment solutions and the landscape continues to evolve, ensuring safety, security and convenience for consumers to transact online. Vodacom Tanzania limited has been on this journey since it launched M-Pesa in 2008, the platform has combined versatile digital products such as M-Pesa app, M- Pesa Mastercard, M-Pawa, and a newly launched Vikoba digital platform – M-Koba, all these platforms enable Vodacom universal customers to perform transactions without the need of cash, in a more safe and convenient way.

 “With the wider variety of payment options at consumers’ fingertips, the broader objective is to pursue the national cashless payments agenda, in which M-Pesa system will be a driving force in ensuring that over 60 percent of our transaction will be digitized by the M-Pesa cashless platform come 2025” said Vodacom Director of M-Commerce Epimack Mbeteni. 

Tanzania is on the path to a cashless community and mobile companies like Vodacom are playing an integral role through the use of the digital technologies which allows all people, even in rural areas, to become a part of his cashless society though money transfers, e-payments to businesses and government agencies but also saving and access to loans. Going cashless is becoming increasingly popular among small and medium business all over the country who want to reap the benefits which include faster service, easier financial reconciliation, reduced risk of theft, and appeal to customers who don't carry cash. 

A whole new suite of value-add services is possible when cash is replaced by electronic-based payment. This presents an opportunity for an inclusive cashless economy without the inconvenience of cash and geographical boundaries. Cash handling is expensive, and in today’s connected world, unnecessary. With 60% of transactions already taking place on mobile platforms, the future is undoubtedly cashless using mobile devices that over 40 million Tanzanians own.

Introducing "Naiona" by Mtafya Ft. Nay Wa Mitego

Jumia kuja na kampeni kubwa ya Mauzo ya Simu!

0
0

Ni ajabu namna ambavyo simu ya mkononi ilivyobadili maisha ya kila siku ya binadamu. Miongo kadhaa iliyopita, simu ilionekana kama kifaa cha anasa ambacho watu wachache wenye uwezo wa kifedha ndiyo walikuwa wanamiliki.
Lakini leo hii, simu ya mkononi imekuwa ni kifaa muhimu ambacho asilimia kubwa ya binadamu hawawezi kufanya shughuli zao bila ya kuwa nacho. Simu haitumiki tena kwa matumizi ya kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa maneno bali ni kifaa ambacho kinarahisisha shughuli kadha wa kadha za maisha ya kila siku ya binadamu.

Kupitia simu ya mkononi mtu anaweza kupata huduma za intaneti - kutumia barua pepe, kupata habari, kuperuzi mitandao ya kijamii, huduma za kibenki, kulipia huduma tofauti, kufanya manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandaoni, kusikiliza muziki, kutazama video, burudani na masuala chungu mzima ambayo yanazidi kuvumbuliwa kadri siku zinavyosonga mbele.

Kutokana na umuhimu wa simu ya mkononi kumekuwepo na ongezeko kubwa la idadi ya watumiaji wa simu duniani. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwenye mtandao wa GSMA, watumiaji wa simu duniani wamefikia zaidi ya bilioni 5. Hii inamaanisha kwamba zaidi ya nusu ya watu duniani, ambayo ni zaidi ya bilioni 7.5, wanatumia simu katika shughuli zao za kila siku.

Tanzania nayo haiko nyuma katika matumizi ya simu za mkononi. Ikiwa na watu zaidi ya milioni 54, idadi ya wananchi wanaotumia simu za mkononi inazidi kuongezeka kila mwaka. Hivi sasa, ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa ripoti ya Takwimu za Mawasiliano iliyotolewa na TCRA ya kuanzia mwezi Oktoba mpaka Desemba 2018, inaonyesha kwamba idadi ya watumiaji wa simu wameongezeka na kufikia zaidi ya milioni 43 mwaka 2018 kutoka milioni 40 mwaka 2017. Hii ni sawa na ueneaji wa asilimia 81 ya Watanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi nchini.



Ongezeko la umiliki na utumiaji wa simu za mkononi linasababishwa na sababu kadhaa zikiwemo; ongezeko la makampuni ya mitandao ya simu - ambayo yamepelekea unafuu kwenye upatikanaji wa huduma za mawasiliano, vifurushi vya mtandao wa intaneti pamoja na huduma za kifedha, ongezeko la makampuni yanayouza simu - ambayo yamepelekea simu za mkononi kupatikana kwa urahisi na bei nafuu miongoni mwa Watanzania wengi.

Katika kuhakikisha watumiaji na wamiliki wa simu za mkononi wanazidi kuongezeka, Jumia imekuwa mstari wa mbele katika kurahisisha upatikanaji wake kwa kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi kwa njia ya mtandaoni. Njia hii itawapatia uwanja mpana wateja kunufaika kwa kuweza kuperuzi maelfu ya bidhaa za simu kutoka kwa wauzaji mbalimbali wa simu mtandaoni, kununua na kupelekewa mpaka mahali walipo.
Kila mwaka, Jumia huwa na kawaida ya kuwa na kampeni kubwa ya mauzo ya bidhaa za simu pekee kwa muda wa wiki nzima! Wakati wa kampeni hii, wateja hufurahia mauzo ya simu za aina zote kwa gharama nafuu, kupatiwa punguzo kubwa la bei, vocha za bure za manunuzi, pamoja na kuzawadiwa zawadi lukuki pindi wanapofanya manunuzi yao ya kila siku.

Zimebaki siku chache kabla ya kampeni hii kutangazwa na kuanza rasmi. Kwa sasa, unaweza kutembelea mtandao wa Jumia kujionea bidhaa zilizopo huku ukifuatilia kwa ukaribu kurasa zake za mitandao ya kijamii kupata taarifa mbalimbali. Usicheze mbali, kaa mkao wa kula!

STEVE NYERERE AHAMASISHA WANANCHI KUISHANGILIA TAIFA STARS DHIDI YA UGANDA CRANES JUMAPILI

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA LA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE), Machi 21, 2019.
  Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE), Machi 21, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Tanzania Mstaafu, Bibi Helen Kijo Bisimba baada ya kufungua Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE) Machi 19, 2019. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images