Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live

LEO NI SIKU YA EQUINOX. JE WAJUA MAANA YA SIKU HII?

$
0
0


Leo tarehe 21 mwezi March katika elimu ya Jiografia ni kwamba Jua lipo katika mstari wa Ikweta ambao unaigawa dunia katika sehemu mbili yaani hemispheres kwa maana ya upande wa Kaskazini na Kusini ... Northern Hemisphere and  Southern hemispheres . Kwa maana hiyo leo tarehe 21 mwezi Machi na tarehe 23 mwezi September jua linakuwa katika mstari wa Ikweta ambao unaigawa dunia katika sehemu mbili yaani Kaskazini na Kusini.
Hivyo leo sehemu zote duniani urefu wa mchana na usiku unalingana. Yaani kwa maana nyingine sehemu zote duniani zinapata urefu sawa wa mchana na usiku. Hali hii kijiografia inajulikana kama Equinox yaani maana yake equal night and equal day.

Hii inamaanisha nyakati zingine zote ukitoa hizi siku mbili yaani tarehe 21 Machi na 23 Septemba urefu wa usiku na mchana hutofautiana.  Nakutakia siku njema ya "Equinox" ambayo sehemu zote duniani urefu wa usiku na mchana unalingana. 

Pangani FM Community Radio among TOP 10 Media in Quality Study

$
0
0
By Mohammed Hammie Rajab
The Yearbook on Media Quality in Tanzania 2018, a research coordinated by the Media Council of Tanzania has now been published. The study was conducted by Spurk Media Consulting Ltd., Switzerland in collaboration with researchers of University Dar es Salaam between September and December, 2017.

The research analyzed a sample of 25 media outlets comprising of print, national radio, local radio, TV and Blogs/Forums applying specific quality criteria which were developed by key media stakeholders in Tanzania. They included:

1. Professionalism (use of multiple sources and coverage of topics beyond official calendar of events);   2. Comprehensiveness (presence of perspectives in a media piece, root-causes and historical background); 3. Understandability (quality of reporting structure and ability to contextualize figures); and 4. Ethics (right to reply conceded to the accused).

A total of 1,886 journalistic units were analyzed from Tanzania Mainland and Zanzibar.

One of the most salient results indicates that local radios’ performance outweighs that of national radios in many quality indicators.  Pangani FM has been one of them ranking eight out of the 25 media institutions including the largest media houses in the country.

Pangani FM is run by UZIKWASA, a local NGO that engages rural communities to find their own solutions to social problems through empowerment and committed leadership. Pangani FM is a key tool in UZIKWASA’s media campaigns that assist Pangani leaders to address problems identified by communities themselves—from oppressive gender norms, sexual violence to rights of education and poor leadership.  Being part of UZIKWASA’s community interventions Pangani FM journalists have continuous access to highly relevant content from local villages.

Through interactive programs the radio engages the people in an ongoing dialogue on social issues. This is reflected in very active community participation through calls and SMS to the station. Pangani FM is trusted by the community who are eager to volunteer to provide information enabling multiple and diverse sources on an issue of concern.

Apart from strong skills in journalism Pangani FM staffs have been trained as facilitators of change who apply reflective methodologies and strategic questioning when they interact with a source.

This has been one of the ‘secrets’ for a meaningful and sensitive dialogue with the community. Regular reflective learning meetings with the radio team enable self-assessment and continuous performance improvement among Pangani FM staff.

UZIKWASA has been providing learning opportunities for a large number of local youth that combine   basic journalism with organizational purpose, values and reflective intervention approaches for social change. Each trainee takes part in the radio’s daily work schedule under the mentorship of a senior radio staff and the Leadership program team.

The young trainees, apart from learning technical skills in journalism, are engaged in UZIKWASA’s gender and transformative leadership program and participate in reflective trainings for their personal development and growth.

MJUE KIUNDANI WAZIRI ALLY KIONGOZI WA WANA NJENJE

Tanzania yakaribia kuwa taifa la uchumi wa kati

$
0
0
Ndoto ya Tanzania kuwa nchi ya uchuni wa kati ifikapo mwaka 2025 ipo karibu kutimia.
 Hayo yalisemwa jana na Dkt. Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi na Jamii (Economic and Social Research Foundation- ESRF) katika semina iliyoandaliwa kwa pamoja baina ya taasisi hiyo na Benki ya Dunia kujadili safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati. 
Akizungumza katika semina hiyo, Dkt. Tausi Kida alisema kuwa hadi kufikia sasa pato la wastani la mtanzania ni dola za kimarekani (USD) 910 wakati inahitajika kwa taifa kufikisha kiwango cha pato la wastani la USD 995 kuwa taifa la uchumi wa kati.
 “We are almost there – tumekaribia kabisa kufika” Kinachotakiwa sasa ni kuzidisha juhudi ili kasi ya ukuaji wa uchumi usishuke bali izidi kuongezeka – alisema.
 Ili kuifikia lengo hilo, Dkt. Tausi Kida alishauri pia kufanyika mageuzi katika sekta ya kilimo kwa kuongeza tija sambamba na kuongeza usindikaji wa mazao ya kilimo hii ikiwa ni katika jitihada za kuondokana na kilimo cha kujikimu na kujikita zaidi katika kilimo cha kibiashara chenye kulenga mahitaji ya soko la ndani na nje. 
Sambamba na hilo, Dkt Tausi Kida alishauri pia kuongeza uwekezaji katika rasilimali watu hususani kuboresha upatikaji wa huduma za afya, elimu na maji kama njia ya uhakika ya kuondokana na umaskini ifikapo mwaka 2025. 
Akifafanua zaidi, Dkt Tausi Kida alieleza kwamba tangu mwaka 2000, Tanzania imekuwa ikitekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa (Development Vision 2025) inayolenga kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.  
Dkt. Tausi Kida aliwaeleza washiriki wa semina kuwa dira hiyo imelenga kubadili uchumi wa Tanzania kutoka kutegemea sekta ya kilimo yenye tija ndogo na kuwa taifa lenye kutegemea zaidi uchumi wa viwanda na hasa viwanda vyenye kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kumudu ushindani wa soko la kimataifa. 
Akifafanua zaidi, Dkt Kida alisema kuwa Dira hii ya Maendeleo ya Taifa inalenga pia kuondoa kabisa umaskini nchini Tanzania ifikapo mwaka 2025. “It is envisioned that by 2025 abject poverty shall be something of the past – ni ndoto yetu kwamba ifikapo mwaka 2025 suala la umaskini litakuwa ni jambo lilipitwa na wakati nchini Tanzania” alisema. 
Alieleza kwamba Tanzania imekuwa ikitekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa kupitia mikakati mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mkakati wa Kwanza na wa Pili wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini nchini Tanzania – mikakati ambayo ilifahamika zaidi kwa jina la MKUKUTA na Mipango ya Miaka mitano mitano ya Maendeleo ya Taifa ambapo kwa sasa taifa linatekeleza mpango wa pili kwa kipindi cha miaka ya 2016/17 – 2020/21 alisema. 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird alisema kwamba Benki ya Dunia itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania uliojengeka kwa zaidi ya miaka 54 sasa. 
Ushirikiano huu unalenga kuiwezesha Tanzania kuwa moja ya mataifa yenye uchumi mkubwa duniani. Bi Bella aliuambia mkutano kwamba katika miaka hiyo yote, Benki ya Dunia imekuwa ikitoa misaada ya kifedha kwa Tanzania hasa kupitia Shirika lake la Kimataifa la Fedha (International Development Association – IDA) ambalo limekuwa likitoa misaada katika nyanja mbali mbali hususani afya, elimu, hifadhi ya jamii, maji, nishati, uchukuzi, miji, mazingira, sekta za fedha na utawala bora.
Semina hiyo ilifanyika jana, Jumatano tarehe 21 mwezi wa 3 mwaka 2019 katika ukumbi wa mkutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. 
Dhumuni kuu ya semina hiyo lilikuwa ni kujadili safari ya Tanzania katika kuekea uchumi wa kati. Semina hiyo ilichagizwa na mada iliyotolewa na ndugu Yutaka Yoshino, mchumi mwandamizi wa Benki ya Dunia ambaye alitoa mada juu ya uzoefu wa mataifa ya Vietnam na Bangladesh katika kufanya mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya viwanda ambapo yamefanikiwa kupiga hatua na kuwa mataiafa ya uchumi wa kati katika miaka ya hivi karibuni. 
“Both countries were at the same level of per capita income as Tanzania in early 1990s - pato la wastani kwa mataifa haya lilikuwa sawa na lile la Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1990” alisema.
 Baadhi ya mataifa ya Afrika yaliyofanikiwa kutoka katika kundi la nchi maskini zaidi duniani na kuwa mataifa yenye uchumi wa katika miaka ya hivi karibuni ni pamoja na Ghana, Nigeria, Sudan na Zambia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (kulia) akisalimiana na baadhi ya washiriki kutoka Ubalozi wa Ufaransa wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)-juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akiongozana na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano mara baada ya kuwasili kushiriki semina ya pamoja kati ya Benki hiyo na Taasisi hiyo juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akitoa neno la ufunguzi wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

 Mchumi wa Benki ya Dunia, Bw Yutaka Yoshino akitoa mada kuhusu safari ya Tanzania kuelekea uchumi kati wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Dr Jehovaness Aikaeli kutoka Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akielezea umuhimu wa umma na sekta binafsi kushirikiana kutokana uhaba wa rasilimali wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark tawi la Tanzania, Bw John Ulanga (wa pili kushoto) akizungumzia ukosefu wa masoko nchini Tanzania ambao unakwaza ukuaji wa kilimo ambao ndio uti wa mgongo kwenye viwanda wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (kulia) akizungumzia umuhimu wa kuangalia rasilimali watu kwa kuzingatia weledi na elimu yao katika ushiriki wa kujenga uchumi wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania CTI Bw. Subhash Patel (wa pili kulia) akizungumza sheria na vikwazo mbalimbali vinachangia kukwamisha ukuaji wa sekta binafsi wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Bi. True Schedvin (kulia) kutoka Ubalozi wa Sweden alisema katika safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati ni vyema Tanzania kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo kazi, afya elimu na masoko wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa washiriki akiuliza swali kwa wajadili wa mada wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano akifuatilia kwa umakini maoni yaliyokuwa yakiwasilishwa wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akifunga semina hiyo ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa maendeleo,sekta binafsi pamoja na taasisi mbalimbali za serikali waliohudhuria semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

WANANCHI WAISHIO MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA WAAHIDI KUTOA USHIRIKIANO KUPAMBANA NA WAHAMIAJI HARAMU SIRARI

$
0
0
WAKAZI na viongozi wa Kata za Sirari, Gwitiryo, Pemba na Mbogi pamoja na wakazi wa Kata ya Isebania (Kenya) wameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo mpakani ili kupambana na wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia katika nchini Tanzania na Kenya.

Hayo wameyasema wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Tarafa ya  Kijiji cha Sirari, Wilayani Tarime. Mkutano huo ambao ni sehemu ya Warsha ya “Ushirikishwaji Wananchi katika Ulinzi na Usimamizi wa Mipaka” unasimamiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) ni muendelezo wa kuwajengea uelewa wananchi waishio maeneo ya mipakani ili kushiriki katika suala zima la Ulinzi na Usimamizi wa mpaka katika maeneo yao.

Akifungua mkutano huo, Mgeni rasmi  Kemore Kemore ambaye ni Katibu Tarafa wa Inchugu ameishukuru Idara ya Uhamiaji na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji kwa kuamua kukutana na wananchi wa pande zote mbili kupawatia elimu juu ya Uhamiaji Haramu, Usafirishaji Haramu, Usafirishaji wa Magendo wa Binadamu, na athari zake kwa Usalama wa Nchi.

“Nashukuru sana kwa Uhamiaji na IOM kuja hapa na kufanya mkutano na wananchi. Wananchi wakielimika basi hata hizi changamoto za mpakani zitapungua au kwisha kabisa, na niwaombe viongozi wenzangu na wananchi wote mliohudhuria hapa, yote mtakayofundishwa basi nanyi muwe walimu kwa wengine ambao hawakufika hapa’’ Ameeleza  Kemore.

Mkutano huo ulishirikisha wananchi wa kawaida, madereva bodaboda na mabasi, wafanyabiashara, mamalishe, wajasiriamali, vijana, Viongozi wa vitongoji, vijiji, na Kata pamoja na wawakilishi wa taasisi na idara za serikalini zilizopo mpakani kwa pande zote mbili (Kenya na Tanzania).

Mzee Chacha Magatti, mkazi wa Kijiji cha Sirari alisema kuwa baada ya kupata elimu juu ya madhara ya wahamiaji haramu kwa usalama na uchumi wa nchi sasa yuko tayari kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi.

“Kwa kweli inabidi wananchi wa maeneo ya mipakani tuwe wazalendo kwa nchi zetu. Unakuta watu hawatambuliki wametokea wapi, wanapita vijijini kwetu, wanapitishwa na bodaboda na mafuso kwenda Tarime. Ukichunguza unaweza kusema watu hao ni wasomali au waethiopia. Sasa kwa jinsi tulivyoelimishwa katika mkutano huu, nimeona kuanzia sasa si vyema kukaa kimya. Nikiwaona lazima nitoe taarifa kwa wahusika ili wajiridhishe kama hawa watu wameingia kihalali.” Alisema Mzee Magatti.

kwa upande wake Diwani wa Kata ya Sirari  Nyangoko amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwa na mikutano kama hii angalau mara mbili kwa mwaka ili kujenga uelewa kwa wananchi na kuwakumbusha wajibu wao kwa nchi yao kwani ulinzi wa nchi unaanzia ngazi ya familia, kitongoji, Kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akichangia mada ya Magendo ya binadamu na bidhaa, Afisa kutoka TRA alisema kwamba pamoja na juhudi zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kudhibiti uingizaji na usafirishaji nje bidhaa zinazotakiwa kulipiwa kodi, bado kuna baadhi ya watu wanashiriki katika magendo lakini juhudi zinaendelea kuwadhibiti.

Pia mtoa mada kutoka Polisi, Mkaguzi Msaidizi Juma alisema suala la uhalifu mpakani japo kwa sasa limepungua lakini bado ni changamoto ambayo polisi wanaendelea kupambana nayo. Wahalifu wakifanya matukio Tanzania wanakimbilia upande wa pili (Kenya).

Aidha maafisa Uhamiaji na wale wa Mamlaka ya Mapato kutoka Kenya wamewaasa wananchi kufuata sheria wakati wa kuvuka mpaka ili kuepuka kuingia matatani kwani mtu anaevuka mpaka ni lazima apite kituo cha uhamiaji na kama ana mizigo lazima apite KRA kwa ukaguzi.

Diwani wa Kata ya Gutiryo Mheshimiwa Adam Nyawambura aliungana na viongozi wengine katika kuishukuru Idara ya Uhamiaji kwa kuandaa warsha na mikutano na wananchi kwa kuwajengea uelewa wa mambo ambayo kwa mpakani yanaonekana kero kwa wananchi lakini yanatakiwa kufuatwa kwa mujibu wa sheria.

“Ni jambo jema kuja kwa wananchi na kuwaelimisha mambo yanayotakiwa kufuatwa kwa mujibu wa sheria za nchi, kuna mambo mengi wananchi wanadhani wanaonewa. Kumbe wanakuwa hajui sheria inasemaje, mfano mtu anaona shule ipo mita mia hapo Kenya anampeleka mtoto wake shule bila kufuata taratibu kwa kuwa hajui anatakiwa afanye nini, kumbe leo wananchi hasa wazazi wenye Watoto wao hapo Isebania watafuata utaratibu wa kupata vibali vya masomo kwa Watoto wao. Bila mkutano huu hii elimu tusingekuwa nayo.” Ameeleza Nyawambura.
Afisa Uhamiaji Mkoa Mara na Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Fredrick Kiondo akiongea katika hadhara  ambayo ni sehemu ya Warsha ya “Ushirikishwaji Wananchi katika Ulinzi na Usimamizi wa Mipaka” iyosimamiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) iliyofanyika katika uwanja wa Tarafa Kijiji cha Sirari, Wilayani Tarime.
Mwezeshaji katika mkutano huo, Mrakibu Allya Mtanda akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika Kijiji cha Sirari, Wilayani Tarime.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa “Ushirikishwaji Wananchi katika Ulinzi na Usimamizi wa Mipaka” iyosimamiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM).
Wananchi wakigawiwa vipeperushi  wakati wa mkutano wa “Ushirikishwaji Wananchi katika Ulinzi na Usimamizi wa Mipaka” iyosimamiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM).

FAHAMU VIJIJI MAARUFU NA TAJIRI ZAIDI NCHINI CHINA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
CHINA ni moja ya nchi ambayo imekua mstari wa mbele  katika kukuza uchumi wake ikiwa ni pamoja na kujenga mazingira ya kuvutia na tofauti zaidi duniani, vitu vingi vya kustaajabisha na kushangaza vimekuwa vikitokea nchini humo na hiyo ni kutokana na kukua kwa teknolojia nchini.

Mtandao wa Chinawhispers wa nchi humo umetoa orodha ya vijiji kumi ambavyo ni tajiri zaidi nchini humo.

1. Kijiji cha Daqiuzhuang
Kijiji hiki kinapatikana katika Mji wa Tianjin na imeelezwa kuwa awali kilikuwa kijiji tajiri zaidi nchini humo, na ilipofika mwaka 1976 mwenyekiti wa kijiji hicho Yu Zuomin aliongoza wakulima katika ujenzi wa viwanda hapo ndipo kijiji hicho kilipoanza kupata utajiri lakini mwaka 1993 kiongozi huyo Yu Zuomin alikamatwa na kufungwa jela hapo ndipo uchumi wa kijiji hicho ukaporomoka. Uchumi wa kijiji hicho umefikia dola za kimarekani 180.

2. Kijiji cha Huaxi
Kijiji hiki kinapatikana katika Mji wa Jiangsu na kinafahamika zaidi kama "kijiji namba moja chini ya anga" na imewahi kuelezwa kuwa ndicho kijiji tajiri zaidi nchini humo, kilianzishwa mwaka 1961 huku ikielezwa wenyeji wa kijiji hicho  wana utajiri wa yuan 1500  na zaidi.Kijiji hicho kina sekta mbalimbali ikiwemo viwanda pamoja na makampuni ya kubadilisha fedha na tayari wamenunua ndege na kupanga kununua meli yao binafsi pamoja na kufungua hoteli ya kimataifa  ambayo ilifunguliwa wakati kijiji hicho kikisherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

3. Kijiji cha Liuzhuang
Kinapatikana katika eneo la Henan na kilijulikana kwa kuwa kijiji maskini zaidi miaka iliyopita, kwa sasa kinamiliki zaidi ya dola milioni 120  na kina utajiri zaidi  katika sekta za makazi, shule nzuri, pamoja na huduma za afya ambazo hutolewa bure na kila familia kijijini humo kinamiliki takriban dola 24,000.

4. Kijiji cha Nanling
Hiki kinafahamika kama kijiji cha kwanza nchini China na viongozi wakubwa nchini humo Jiang Zemin na Hu Jintao waliwahi kutembelea kijiji hicho mwaka 2008, huku mali zao zikifikia Yuan 1.3 bilioni na mapato kwa wanakijiji yakifikia Yuan 150,000.

5. Kijiji Tengtou
Ni kijiji tajiri zaidi katika eneo la Zhejiang na hadi sasa zaidi ya watu 800 wanaishi kijijini hapo, na hadi kufikia mwaka 2009 uchumi wake ulikua hadi kufikia Yuan 5.5 bilioni.

6.Kijiji cha Nanjie
Kinapatika katika eneo la Henan kikiwa na makazi zaidi ya 3100 na idadi kubwa ya wakomunisti pamoja na huduma zinazotolewa bure zikiwemo elimu, afya,makazi, chakula pamoja na mishahara kwa wafanyakazi wa viwanda wanaolipwa dola 400.

7. Kijiji cha Huayuan
Kinapatikana katika Mji wa Jinhua huko Zhejiang, ni kijiji maarufu nchini humo, mapato ya wanakijiji ni Yuan 16,520 na mwaka 2005 kijiji kilitengeneza mapato ya  zaidi ya Yuan bilioni 1.729.

8. Kijiji cha Dazhai
Ni kijiji maarufu zaidi kikiwa na vivutio vya kutosha pamoja na kupata zaidi ya watalii 200,00 kwa mwaka huku mapato ya mwaka 2005 yakifika jumla ya Yuan milioni 116  huku mapato ya mwaka yakifikia Yuan milioni 5500.

9. Kijiji cha Shenquanzhuang
Kinapatikana karibu na eneo la Shandong likiwa na wanakijiji 1600 mwaka 2002 likiwa na mapato ya zaidi ya Yuan bilioni 2.69 kwa mwaka.

10.Kijiji cha Hangmin
Kinapatikana karibu na Zhejiang na kijiji tajiri zaidi Zheijiang, huku ikielezwa mapato ya wanakijiji  ni Yuan 35,000 na wanakijiji wakiwa na maisha bora zaidi.

Nini Maoni yako kuhusu vijiji bora na tajiri zaidi nchini?

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA QATAR IKULU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than aliyeambatana na ujumbe wake  mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kinyago Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi wanne kutoka kulia, Balozi wa Tanzania kutoka Qatar Fatma Rajab watatu kutoka kushoto pamoja na Balozi Zuhura Bundala wakwanza kushoto.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al Than mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

KESI YA KUTUMIA LUGHA CHAFU YA MATUSI INAYOMKABILI HALIMA MDEE KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 16

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha chafu ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuhakikisha tarehe ijayo kesi hiyo inasikilizwa.

Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ameyasema hayo leo Machi 21, mwaka huu kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa na wakili wa serikali Dasy Makakala ambayo ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa kuwa faili hilo lilikuwa kwa wakili mwingine na bado hajalipitia.
Wakili wa utetezi, Hekima Mwesipu alidai, shauri hilo ni la muda mrefu kwani limebakiza miezi minne tu kufikisha miaka miwili huku ikiwa haijamaliza kusikilizwa hivyo ameomba hili liwe ahirisho la mwisho.

Baada ya kusema hayo, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 16, 2019.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi akiwamo  mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki”  na kwamba kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.  

Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.

MAKAMU WA RAISA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA UN WOMEN

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa  linaloshughulikia Masuala ya Wanawake (UN-Women) Hodan Addou aliyeambatana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine Mwakilishi huyo wa UN-Women alizungumzia kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini hususani katika kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ikiwemo Mkakati wa Kukuza Uchumi na kupumguza Umasikini Tanzania(MKUKUTA) na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akisalimia na Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja  wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women), mwingine pichani ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja  wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women), pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa  Alvaro Rodriguez (katikati) ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja  wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women),pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez (kushoto) ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akitwa kwenye picha ya pamoja na Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja  wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women), mara baada ya kumaliza mazungumzo leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa  Alvaro Rodriguez mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

ARUSHA UNITED YAJITOA RASMI LIGI DARAJA LA KWANZA

$
0
0

Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha

Timu ya mpira Wa miguu ya mkoani Arusha ijulikanayo kwa jina la Arusha United (wana utalii), Leo imetangaza rasmi kujitoa katika mashindano ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara kwa kile kichodaiwa vurugu za Mara kwa Mara zinazotokea katika ligi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Murugenzi mtendaji wa timu hiyo Otte Ndauka alisema kuwa timu hiyo imeamua kujitoa rasmi katika mashindano hayo kutokana na vurugu wanazofanyiwa Mara kwa Mara viwanjani wakati wakicheza michezo mbalimbali.

Alisema kuwa timu yao ya Arusha United imefanyiwa vurugu katika mechi mbalimbali ikiwemo mchezo nambari 69 Wa ligi daraja LA kwanza uliochezwa mjini Tabora mnamo February 2 mchezo uliochezwa katika kiwanja cha All Hassan Mwinyi.

"Mchezo huu tulienda tulifika sikumoja kabla kwa mujibu Wa sheria tulitakiwa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo husikalakini jambo LA kusikitisha sana na lisilo lakiugwana viongozi Wa Rhino Rangers kwa kushirikiana na Meneja Wa uwanja walifanya kula jitiada kuhakikisha hatufanyi mazoezi,Aisha pia katika mechi ingine tuliocheza na kilabu ya Polisi pia tulifanyiwa vurugu na sio timu tu au wachezaji wanafanyiwa vurugu hapana lakini pia waandishi wetu wanapigwa na hata kunammoja aliaribiwa vifaa vyake vya Kazi" alisema Ndauka.

Alisema kuwa matukio yote ambayo yametokea wameandika barua TFF kulalamika pamoja na Bodi ya ligi lakini hakuna uamuzi wowote Wa kinithamu ambalo wameuchukua hivyo ndio maana wameamua kujitoa katika ligi hiyo.

Kuhusiana na swala La mikataba ya wacheza pamoja na Mali za klabu hiyo walisema kuwa bodi ya timu hiyo inakaa chini na wachezaji kujadili kuhusiana na mikataba hiyo pia wanampango Wa kuketi na bodi kujadili kuhusiana na Mali hizo.

Akizungumzia suala hilo Katibu wa chama cha mpira Wa miguu mkoa Wa Arusha Zakayo Mjema alisema kuwa wao kama chama cha mpira Wa miguu Mkoa Wa Arusha awajapata taarifa yoyote kuhusiana na timu hiyo kujitoa
Mkurugenzi mtendaji Wa timu ya Arusha United (WANAUTALII) Otte Ndauka 

MWAKINYO KUPIGANA NA BONDIA KUTOKA ARGENTINA

$
0
0
KIPAJI CHA MWAKINYO CHAMVUTIA KOCHA BELLEW WA UINGEREZA, KUPIGANA NA M'ARGENTINA MARCH 23. 

Na Mwandishi Wetu, Globu ya Jamii

Bondia nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amewasili mjini, Nairobi 

Kenya tayari kwa pambano lake la Kimataifa dhidi ya bondia kutoka Argentina, Eduardo Gonzalez lililopangwa kufanyika Machi 23 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (Kenyatta International Conference Centre).
Mwakinyo kwa sasa ananoa makali yake chini kocha Tony Bellew kutoka Liverpool, Uingereza ambako alikuwa kambini chini ya ufadhili wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.

Mbali ya Mwakinyo, pia Bellew anamfundisha bondia Fatuma Zarika ambaye atapambana na Catherine Phiri wa Zambia katika pambamo la ubingwa wa dunia wa uzito wa Super Bantamweight wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC).

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Kampuni ya Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema kuwa bondia Mwakinyo atafanya mazoezi chini ya kocha huyo chini ya uwezeshaji wa kampuni yao.

Tarimba alisema kuwa mbali ya kampuni yao kuwezesha kambi ya Mwakinyo na Zarika, Pia Bellew amevutiwa sana na viwango vya mabondia hao na wanaamini kuwa watafanya vizuri katika pambano hilo.

Alisema kuwa mabondia hao wamepata mafunzo bora na ya kisasa kutokana na umuhimu wa pambano hilo. “Wakiwa mjini Liverpool, Mwakinyo na Zarika walijiandaa vyema kwa kuwa wanajua ugumu wa mapambano yao. Kampuni ya SportPesa imeona umuhimu huo na lengo letu kubwa ni kuona mabondia hao wanapata matokeo mazuri na kuwafurahisha wadau wa ngumi za kulipwa katika nchi za ukanda wa Afrika 
Mashariki,” alisema Tarimba.

Alisema kuwa Gonzalez atawasili Kenya kesho (Machi 20) ambapo Ijumaa (Machi 22) mabondia wote hao watapima uzito kwenye hotel ya The Stanley.
Pia mabondia hao watatembelea ofisi za SportPesa na kufanya mahojiano kwenye vituo mbali mbali vya televisheni na redio mbali ya kula chakula cha jioni na wafanyakazi wa kampuni yao.

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA LA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

WAZIRI mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wadau kuunganisha juhudi za pamoja kukabiliana na ukatili dhidi ya makundi ya wanawake na watoto.

Hayo yamesemwa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Majaliwa amesema serikali imeandaa mwongozo na utaratibu wa usimamizi na ufuatiliaji unaotoa maelezo kuhusu uundwaji wa kamati mbalimbali za mfumo wa mawasiliano na uwasilishaji wa taarifa.

“Lengo kuu la serikali ni kuhakikisha ukatili dhidi ya wanawake na watoto na makundi kengine unatokomezwa na haki zote zinalindwabna kuheshimiwa,”amesema Majaliwa.

Pia, amesema kutakuwa na kamati za kijinsia na ustawi wa wanawake na kwenye kuunga mkono serikali imefanya jitihada mbalimbali za kufanya kampeni za kitaifa ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni ikiongozwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa mtoto (CDF).

“Suala la ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni jambo mtambuka na linahitaji ushitikishwaji wa wadau katika kutokomeza janga hili linaloikabili nchini yetu.”amesema Majaliwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF)Bwn Koshuma Mtengeti ameiomba serikali kutoa ushirikiano pamoja na kutenga bajeti ya kutosha katika kuendesha mikakati ya kupinga ukatili wa kinjisia nchini.

"Mwezi Mei mwaka 2018, mwalimu wa shule ya msingi hapa jijini Dar es Salaam alituhumiwa kuwadhalilisha kingono wanafunzi wake wanne wa kike wa darasa la saba kwa kuwageuza kuwa wake zake na kufanya nao ngono,”amesema Mtengeti.

Tunakushukuru sana Mh. Raisi John P. Magufuli kwa salamu zako kutoka kwa Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa. Tumefarijika kujua kwamba uko nasi bega kwa bega katika kongamano hili la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Prof. William Anangisye amesema Suala la Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake ni nyanja pana, ni tatizo linalozikabili nchi zote Duniani ingawa viwango vya Ukataili hutofautiana.

Ripoti mbalimbali za haki za binadamu zimeweza kuonyesha kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha mwaka 2018 ukilinganishwa na mwaka 2017 nchini.

Aidha, kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kudadavua ukubwa wa sura za ukatili yanayowasibu wanawake na watoto  na litasaidia juhudi za kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia, kukabili na kuanzisha utaratibu wa kuboresha huduma kwa watoto na wanawake waathirika wa ukatili.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE), Machi 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE), Machi 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Tanzania Mstaafu, Bibi Helen Kijo Bisimba baada ya kufungua Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE) Machi 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HDIF, UKaid na COSTECH kukutanisha wadau wa ubunifu kujadili, kukuza na kuendeleza ubunifu

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MFUKO wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Binadamu (HDIF) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeandaa wiki ya ubunifu inayotarajia kuwaleta pamoja wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa ili kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini.

Wiki hiyo ya ubunifu,  imelenga kuwakutanisha wataalamu, watafiti na wabunifu  ili kujadiliana namna ya kukuza na kuendeleza masuala ya ubunifu nchini.

Wiki hiyo, itakayoanza Machi 25-30 mwaka huu,  inafanyika kwa mara ya tano nchini Tanzania  ambapo mwa huu,  imefanikisha kuwafikia mpaka wadau walio nje ya Dar katika Mikoa ya Iringa na Arusha tofauti na awali ambapo wiki hii ilikuwa ikifanyika Dar es Salaam pekee.

Akizungumza na wanahabari leo Machi 21.2019 Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu amsema kauli mbiu ya wiki ya ubunifu mwaka huu ni ya kukuza na kuendeleza Bunifu kwa maendeleo ya Watu'. Ambapo amesema  Tume  kupitia Mfuko wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia wamefungua milango kwa wabunifu mbalimbali na kutoa fursa za kuendeleza ubunifu nchini.

Amesema, kwa kushirikiana na HDIF na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA), wametoa Sh bilioni 1.9 kwa wabunifu bora 32 na kumbi za Bunifu 15, zilizoshinda mashindano ya COSTECH ya mwaka 2018.

Dk. Nungu ameongeza kuwa,  wameandaa utaratibu wa kuwatambua wabunifu wote nchini na kuweka kwenye makundi kulingana na viwango vya ubunifu wao "Mwanzoni mwa mwezi Machi, tume ilifanikiwa kuratibu mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) ambapo wabunifu 60 walichaguliwa kiushandani katika nyanja mbali mbali.

Ameongeza, kwa miaka mitano mfululizo HDIF na COSTECH wamekuwa wakishirikiana kuinua ubunifu nchini kupitia sekta za afya, maji na elimu na kuboresha mfumo mzima wa ubunifu ikiwemo uwezeshaji na miundombinu.

"Tunalenga Tanzania kuwa na mfumo thabiti wa ubunifu kwa kuhakikisha kuwa wabunifu, wataalamu mbalimbali na jamii inakutana ili kujifunza vitu ambavyo wabunifu hao wanavifanya," amesisitiza.

"Maonesho haya yanatoa fursa kwa wabunifu, watafiti kutoka vyuo vikuu nchini, wajasiriamali na jamii kwa ujumla kuona namna ya kukuza uchumi wa viwanda kupitia ubunifu kwani katika kutekeleza lengo la kufikia uchumi wa viwanda, sekta yetu ya ubunifu yenyewe ina mchango mkubwa kwani inazalisha ajira na kutangaza bidhaa zetu ndani na nje ya nchi," amesema

Alisema maboresho ya mwaka huu ya ubunifu yatawaunganisha wadau wa sekta binafsi, wafanyabiashsra, serikali na wabunifu ili kushirikiana kuingiza bidhaa za ubunifu sokoni lengo ni kukuza uchumi wa viwanda kwa uhalisia.

Kwa upande wake, Kiongozi Mkuu wa HDIF, David McGinty amesema katika kipindi cha miaka mitano ya uendeshaji wa ubunifu huo, matokeo chanya yamejidhihirisha kwa   ongezeka la washiriki kukuza kwa zaidi ya asilimia 50 na Tanzania inaonekana ikipanda kwa nafasi 31 huu katika rekodi za kipimo cha Ubunifu cha Dunia.

Aidha amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho hayo ili kuona kazi zinazofanywa na watanzania katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kupitia ubunifu.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller amesema wiki hiyo inatoa fursa kwa wabunifu, wafadhili na sekta binafsi kubadilishana mawazo na kuhamasisha masuala ya ubunifu.

Amesema, wadau watakaoshiriki katika maonesho hayo ni Digital Impact Alliance (DIAL), Ubalozi wa Uswisi, 10 School of TECH, Buni, Ndoto na Digital Opportunities Trust na wengine watakaoendesha maonesho hayo.

Ameongeza, katika wiki hii ya ubunifu kutakuwa na shughuli zaidi ya 60 ambazo zitakuwa zikiendelea kwa pamoja na maonyesho 30 katika kumbi kuu za COSTECH na Dlab Kijitonyama Sayansi. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu wa katikati akizungumza na waandishi wa Habari  juu ya wiki ya ubunifu itakayoganza Machi 25-30 mwaka huu ambapo wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa na wanatarajiwa kukutana pamoja kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini. Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller na kushoto ni Kiongozi Mkuu wa mfuko wa ubunifu wa maendeleo, (HDIF)David McGinty.
 Makamu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, Jane Miller akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano huo ambapo amesema wiki hiyo inatoa fursa kwa wabunifu, wafadhili na sekta binafsi kubadilishana mawazo na kuhamasisha masuala ya ubunifu.
 Kiongozi Mkuu wa mfuko wa ubunifu wa maendeleo, (HDIF)David McGinty  ambao ndio waandaaji wa wiki ya ubunifu akifafanua jambo kwa waandishi wa  Habari juu ya wiki hiyo ambayo25-30 ambayo inatarajia kuwaleta pamoja wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa ili kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu alipokuwa akieleza dhima ya ya wiki ya ubunifu itakayoanza Machi 25-30.2019  ambayo inatarajia kuwaleta pamoja wabunifu zaidi ya 3000 wa mikoa ya Arusha Dar es Salaam na Iringa ili kubadilishana uwezo kwa lengo la kukuza ubunifu nchini.

SERIKALI YA MAREKANI YACHANGIA DOLA 500,000, KUWEZESHA WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA SIASA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SERIKALI ya Marekani imechangia Dola 500,000 kwa ajili ya kuchangia ushiriki zaidi wa wanawake kwenye mchakato wa kisiasa ambapo mchango huo utawanufaisha wanawake wa Tanzania 500 ambao watapenda kujishughulisha na mambo ya siasa.

Imefafanuliwa fedha hizo zitajumuisha mafunzo ya masuala ya kisiasa kiujumla na michakato ya uchaguzi , kutimiza malengo ya muda na jinsi ya kumudu ratiba za chama na uteuzi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Dk.Inmi Patterson wakati akizindua awamu ya pili ya mradi wa USAID/UN Women Wanawake Wanaweza wenye lengo la kuwawezesha wanawake ambapo amesema Serikali ya Marekani inachangia kulea na kutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa kampeni ,jinsi ya kuandaa ujumbe, kutunga sera na kuchangisha fedha.

Amesema ukweli ni kwamba wanawake wengi wanabaki na uwakilishi hafifu kwenye michakato ya kisiasa na uchaguzi."Naamanisha ushiriki wao kama wapiga kura , wagombea na kama wawakilishi waliochaguliwa .Hii si tatizo la Tanzania pekee lakini inaonesha kwa kiasi kikubwa jinsi wanawake wanavyotengwa kwenye nafasi nyingi za juu za kufanya maamuzi kwenye Serikali Kuu na vyama vya siasa".

Amefafanua hivi karibuni iliadhimishwa Siku ya Wanawake Duniani kwa kauli mbiu ya 'Usawa Bora', kauli ambayo inaendana na mazingira ya Tanzania kwa sasa , wakati ikiongeza kasi ya maendeleo yake kuelekea kwenye viwanda na nchi zisipotilia mkazo kujenga uwezo wa wasichana na wanawake , zinasahau kuwa wanawake waliojengewa uwezo wana wanaweza kuleta mageuzi kwenye jamii.

"Sisi tunajua pale ambapo wasichana wa rika balehe na wanawake vijana wanapotunzwa vizuri inaashiria nchi iko mahali pazuri .Wao ni akina mama watarajiwa watakaoelimisha kizazi kijacho na pia ni sehemu ya injini ya baadae kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania.

"Vikwazo gani vinawafanya wasichana na wanawake washindwe kuishi maisha ya kujitosheleza , vinavyosababisha kutokuwepo na usawa kwenye jamii yetu?Kwanza kabisa ni ukosefu wa elimu na ukosefu wa kupata huduma za afya.Changamoto kubwa kabisa wanawake wengi wanakosa nguvu ya kufanya maamuzi muhimu yanayohusu maisha yao na kutenda kwa uhuru bila adhabu, wasiwasi au hofu.

"Tunaweza kuona jinsi hali kama hizi zinavyoweza kujitokeza nchini Tanzania , katika baadhi ya maeneo hata ukatili wa kijinsia unahalalishwa kwa kisingizio cha utamaduni,"amesema Dk.Petterson huku akiwataka wanawake kushiriki kikamilifu katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo na kijamii.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Juma Hassan amesema kuwa kupitia awamu ya kwanza ya mradi huo yeye binafsi amenufaika na mradi huo na sasa amekuwa mfano kwa wanawake wa Zanzibar.

"Kupiti mradi huu wa UN Women Wanawake Wanaweza, nimekuwa mmoja wa wanufaika kwani kupitia programu zao mbalimbali za kimafunzo nimeweza kuwa imara na kufikia malengo yangu kisiasa.Kazi ambayo ninandelea kuifanya ni kushirikiana na wanawake wa Zanzibar katika kuleta maendeleo yetu na jamii nzima kwa ujumla,"amesema.

Amesema hata katika Baraza la Wawakilishi amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake waliko ndani ya baraza hilo wanapata pia nafasi ya kuwemo kwenye kamati mbalimbali za maamuzi.

Mgeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wawakilishi Zanzibar (WAWAZA) amesema wamekuwa na mipango mingi ya kumsaidia mwanamke wa Zanzibar na kwa sehemu kubwa wanakwenda vizuri kwani hata idadi ya wanawake inaongezeka katika nafasi za uongozi siku hadi siku.

Wakati huo huo Mbunge wa Tarime Vijijini Ester Matiku amesema kupitia mradi wa kuwawezesha wanawake kisiasa umemuwezesha hata yeye kufika hapo alipo kwani alipata nafasi ya kujengewa uwezo . "Hizi fedha ambazo zimetolewa tuwahakikishie zitatumika kwa malengo ambayo yamekusudiwa.Bnafsi nimefika hapa kwasababu ya miradi ya aina hii,"amesema Matiku.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Sofia Mwakagenda ametoa shukrani kwa USAID/UN Women Wanawake Wanaweza kwani kupitia mradi wao umeibua na yeye na leo ni mbunge.Mbali ya kumuwezesha kuwa mbunge amefanikiwa kuanzisha asasi yake ambayo imesaidia wanawake 500 kwa kuwawezesha kimaendeleo na kiuchumi.
 Baadhi ya washiriki waliohudhuria uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa UN Women Wanawake Wanaweza wakifuatilia hotuba kutoka kwa mgeni rasmi Dk.Inmi Petterson
Mbunge wa Tarime Vijijini Ester Matiko (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa kuwawezesha wanawake kupitia Usaid/Un Women wanawake Wanaweza.Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Sofia Mwakagenda

RAIA WA KENYA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
RAIA wa Kenya, ambae ni mtaalamu IT, Brian Lusiola na Meneja Uwendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya Inventure Mob Tanzania Ltd, Ahmed Ngassa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, likiwemo la kuingiza  kifaa cha mawasiliano nchini bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 64.2.

Mbali na Lusiola na Ngassa mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Kampuni ya Inventure Mobile Tanzania Ltd inayowafanya biashara na Tala Tanzania.

Akisoma hati ya mashtaka leo Machi 21,2019,  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Jackline Nyantori amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kuwa, washtakiwa wametenda makosa hayo, wakiwa katika jengo la Tanzanite Park, lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku wakijua ni kinyume cha sheria.
Imedaiwa, katika shtaka la kwanza kuwa, katika tarehe isiyofahamika kati ya Januari Mosi na Desemba 31, 2018 washtakiwa wakiwa katika jengo hilo kinyume na sheria waliingiza kifaa cha mawasiliano kinachoitwa Proliant MLI GEN 9 Server (PABX Virtual Mashine yenye serial number 76520D88838129_425) bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Katika shtaka la pili,  imedaiwa siku na mahali hapo,  washtakiwa pamoja na kampuni hiyo, walisimika kNa Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
RAIA wa Kenya, ambae ni mtaalamu IT, Brian Lusiola na Meneja Uwendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya Inventure Mob Tanzania Ltd, Ahmed Ngassa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, likiwemo la kuingiza  kifaa cha mawasiliano nchini bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 64.2.

Mbali na Lusiola na Ngassa mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Kampuni ya Inventure Mobile Tanzania Ltd inayowafanya biashara na Tala Tanzania.

Akisoma hati ya mashtaka leo Machi 21,2019,  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Jackline Nyantori amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kuwa, washtakiwa wametenda makosa hayo, wakiwa katika jengo la Tanzanite Park, lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku wakijua ni kinyume cha sheria.

Imedaiwa, katika shtaka la kwanza kuwa, katika tarehe isiyofahamika kati ya Januari Mosi na Desemba 31, 2018 washtakiwa wakiwa katika jengo hilo kinyume na sheria waliingiza kifaa cha mawasiliano kinachoitwa Proliant MLI GEN 9 Server (PABX Virtual Mashine yenye serial number 76520D88838129_425) bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Katika shtaka la pili,  imedaiwa siku na mahali hapo,  washtakiwa pamoja na kampuni hiyo, walisimika kifaa hicho na kuendesha mtambo huo wa mawasiliano bila kuwa na leseni inayotolewa na TCRA.

Aidha  washtakiwa wanadaiwa, kutoka Januari 2 hadi  Machi 11,2019 waliendesha kifaa hicho cha kieletroniki cha mawasiliano kwa kurusu simu za kimataifa zilizoingia nchini bila kibali cha TCRA.

Katika shtaka la nne, washtakiwa hao wanadaiwa kumiliki kifaa hicho kilaghai, ambapo wakiwa na nia ya kukwepa gharama za uendeshaji wa kifaa kwa ajili ya kupokea na kusambaza mawasiliano, walisambaza simu hizo za kimataifa nchini.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutumia kifaa hicho kilichounganishwa na mawasiliano kwa nia ya kupokea na kusambaza mawasiliano bila kupata kibali cha TCRA

Katika shtaka la sita, wakili Nyantori amedai kwa  matendo yao hayo ya makusudi, washtakiwa wameisababishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na TCRA hasara ya Sh 64,260.000/-

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mhakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ispokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.
kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi  Aprili 3,2019 kwa kutajwa.ifaa hicho na kuendesha mtambo huo wa mawasiliano bila kuwa na leseni inayotolewa na TCRA.

Aidha  washtakiwa wanadaiwa, kutoka Januari 2 hadi  Machi 11,2019 waliendesha kifaa hicho cha kieletroniki cha mawasiliano kwa kurusu simu za kimataifa zilizoingia nchini bila kibali cha TCRA.

Katika shtaka la nne, washtakiwa hao wanadaiwa kumiliki kifaa hicho kilaghai, ambapo wakiwa na nia ya kukwepa gharama za uendeshaji wa kifaa kwa ajili ya kupokea na kusambaza mawasiliano, walisambaza simu hizo za kimataifa nchini.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutumia kifaa hicho kilichounganishwa na mawasiliano kwa nia ya kupokea na kusambaza mawasiliano bila kupata kibali cha TCRA

Katika shtaka la sita, wakili Nyantori amedai kwa  matendo yao hayo ya makusudi, washtakiwa wameisababishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na TCRA hasara ya Sh 64,260.000/-

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mhakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ispokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi  Aprili 3,2019 kwa kutajwa.

WATALAAM NCHI ZA SADC WAKUTANA DAR KUJADILI NA KUWEKA MUONGOZO MFUMO WA UNUNUZI DAWA WA PAMOJA KUPITIA MSD

$
0
0
 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WATALAAM wa sekta ya afya na hasa katika upande wa ununuzi wa dawa kutoka nchi za SADC wamekutana nchini Tanzania kwa lengo la kujadili pamoja na kutoa muongozo  utakaosaidia kufanikisha mfumo wa ununuzi wa dawa kwa pamoja kwa nchi hizo.

Jukumu la kununua na kusambaza dawa hizo kwa nchi za SADC limekabidhiwa kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) nchini ya Tanzania baada ya kukidhi vigezo na sifa ambazo zilikuwa zimewekwa na nchi hizo.

Akizungumza leo Machi 21,2019 jijini Dar es Salaam Mgeni rasmi wa mkutano huo wa watalaam wa sekta ya afya kwa nchi za SADC na hasa upande wa manunuzi ya dawa, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi amesema mkutano huo ni muhimu kwani utatoa muongozo wa namna bora ya kufanikisha ununuzi wa dawa wa pamoja.

Amesema jukumu la kununua dawa hizo na kuzisambaza kwa nchi za SADC lipo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na hivyo kabla ya kuanza kwa utaratibu huo watalaam wamekutana kuweka mkakati utakaofanikisha ili kufikia lengo.

 "Hiki nikao cha kitalaam ambacho lengo lake ni kujadili namna bora ya kufanikisha ununuzi wa dawa kwa pamoja.Pia ni kikao kitakachotoa muongozo ili kufanikisha mfumo huo ambao ni mpya ingawa kwa nchi nyingine duniani wamekuwa wakiutumia kwa baadhi ya dawa,"amesema.

Kuhusu lini mfumo huo utaanza, Msasi amejibu utaanza baada ya kikao hicho cha watalaam kujadiliana na kwa upande wa MSD ipo tayari kwani walishajipanga kwa kazi hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD Abdul  Mwanja amesema wao wamejipanga na wako tayari kuanza kazi hiyo  ya ununuzi wa dawa wa pamoja ambao faida ya nyingi na kubwa utasaidia kukunua dawa kwa bei nafuu.

"Mnaponunua dawa kwa pamoja, wenye viwanda vya kuzalisha dawa watapunguza bei na hivyo kumuwezesha mwanchi anayehitaji dawa kuzipata kwa gharama ya chini. Hivyo ni mfumo ambao utasaidia nchi hizo kununua dawa wa gharama ya chini,"amesema.

Alipoulizwa kuhusu MSD wamewezaje kuaminiwa na kupewa jukumu hilo, amejibu kulikuwa na vigezo ambavyo viliwekwa na kazi nzuri ambayo imefanywa na MSD ikiwemo ya kusambaza dawa katika hospitali zote nchini Tanzania imewapa nafasi ya kupewa kazi hiyo.

Kuhusu changamoto za mfumo huo,amesema kwa sasa ni mapema mno maana bado hawajaanza , hivyo iwapo zitajitokeza wataangalia namna ya kukabiliana nazo lakini kwa namna ambavyo wamejipanga wana matumaini watatimiza jukumu hilo kikamilifu."Na kwa uwekezaji ambao umefanyika MSD inaweza kuifanya kazi hiyo kwa miaka mitano."


Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa MSD miaka miwili iliyopita walikuwa wananunua dawa kwa wazalishaji wa dawa 10 lakini sasa hivi wananunua kwa wazalishaji  148 ambao wameingia nao mkataba."Hii  itasaidia kupata dawa kwa gharama nafuu kwani hakuna mtu wa kati tena na tumekubaliana kila nchi itakuwa na fedha zake lakini anayenunua kwa niaba ya nchi hizo ni MSD."
Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kufungua mkutano wa kujadili mwongozo wa huduma ya ununuzi wa pamoja wa dawa kupitia kupitia MSD.

 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa wataalamu kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo (SADC)wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam leo ili kujadili mwongozo wa huduma ya ununuzi wa pamoja wa dawa kupitia MSD. 

Dkt. Abbas atolea ufafanuzi Suala la Viongozi wa Serikali Kuwashirikisha wanahabari

ARUSHA UNITED WATANGAZA KUJITOA LIGI DARAJA LA KWANZA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha United Sports Club Otte Beda Ndaweka.

TIMU ya Arusha United Sports Club, inayoshiriki ligi daraja la kwanza imetangaza kujitoa rasmi katika ligi hiyo kwa madai  ya kuchoshwa na vitendo ambavyo si vya kimichezo huku TFF kupitia bodi ya ligi ikishindwa kuchukua hatua stahiki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo Otte Beda Ndaweka amesema kuwa licha ya timu hiyo kuwa katika nafasi nzuri katika kundi B imeona si buasara kuendelea na ligi hiyo kufuatia matukio mbalimbali ikiwemo kufanyiwa vurugu wakati ikicheza na timu kadhaa tangu timu hiyo ianze kushiriki ligi hiyo msimu wa mwaka 2018-2019.

Aidha Ndaweka amesema licha ya timu hiyo kuwa na vibali vya kurekodi michezo yake yote ya ligi kuanzia mchezo wake dhidi ya Dodoma Fc uliofanyika mjini Dodoma bodi hiyo pia imeshindwa kuhakikisha maelekezo,miongozo au vibali vyake vinaheshimiwa na au kuchukua hatua pale ambapo haviheshimiwi.

Timu ya Arusha United ni moja ya timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara kwa kundi B,kwa sasa ikiwa imekwisha cheza michezo 17 kukusanya jumla ya point 28 huku ikishika nafasi ya tano ambapo timu ya Geita gold FC ikiongoza ligi hiyo ikiwa na point 33.

NAIBU MEYA ILALA AZINDUA MRADI WA MAJI VINGUNGUTI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala Omar Kumbilamoto amezindua mradi wa maji Mtaa wa Majengo Kata ya Vingunguti utakaohudumia wananchi 1440 kwa siku.

Mradi huo uliogharimu milioni 28 kuanzia uchimbaji wa kisima, ujengaji wa Vizimba vya kuchotea maji na tanki utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita 4800 kwa siku  na kuondoa kero ya maji kwa kwa wananchi wa mtaa wa Majengo.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Kumbilamoto amesema pongezi kubwa zinaenda kwa Mhandisi wa Maji Manispaa ya Ilala kwa jitihada kubwa alizofanya za kuwezesha kupatikana kwa mradi huo na kumalizika kwa wakati.

Amesema, baada ya kukamilika kwa mradi huu ambao ulikuwa unasubiriwa na wananchi kwa muda mrefu, jumuiya ya watumia maji wajiongeze kwa kuweza kusimamia mradi huu kwa uweledi na uweze kujiendesha ikiwemo kuzalisha miradi mingine.

“Tunajua kunakuwa na changamoto hususani kwenye jumuiya za maji kwa kushindwa kusimamia miradi iliyopo kwenye mitaa ila napenda kuwaambia kuwa jumuiya mjiongeze kwa kusimamia miradi hii ili iweze kujiendesha yenyewe na kuzalisha mingine kwani visima vya watu binafsi vimekuwa na maendeleo mazuri kuliko vya serikali,”amesema Kumbilamoto.

Kumbilato amewataka Manispaa kuangalia beinza maji na kuweka utofauti kati ya bei ya visima vya watu binafsi na vya serikali ili wananchi wengi wapate maji safi na salama.

“Wananchi pia watunze miundo mbinu ya maji ili iweze kudumu na wapate maji safi na salama kwani lengo la serikali ya awamu ya tano kama inavyoanishwa na makamu wa Rais Samia Suluhu ni kumtua mama ndoo Kichwani,”amesema Kumbilamoto.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Mhandisi Upendo Lugongo amesema eneo lililojengwa mradi huo litasaidia wananchi 1440 na maji yatapatikana kwa saa 24.

Aidha, ameeleza kuwa sheria mpya iliyopotishwa ni kuwa watumishi wote wa maji katika manispaa pamoja na miradi ya maji ya Halmashauri na mitaa kwa sasa itaungana na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA).

Upendo amewaomba wananchi kuendelea kulinda miundo mbinu pamoja na kutumia maji hayo kwa manufaa yao wote.

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Majengo Chande Msoke ameishukuru serikali pamoja na Kamati ya Utendaji kwa kupitisha bajeti na kufanikiwa kwa kumalizika kwa mradi huo ndani ya wakati na kuwa kwa sasa kero ya maji kwenye mtaa wake umemalizika.

Katika kusherehekea wiki ya maji iliyoanza Machi 16 na kumalizika Machi 22, miradi mbalimbali ya maji imezinduliwa ikiwa ni mikakati ya kuhakikisha kufiki 2020 asilimia 95 ya wananchi wanapata maji safi na salama kwa mjini na asilimia 85 kwa upande wa vijijini.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omar Kumbilamoto akizundua mradi wa maji mtaa wa Majengo Vingunguti leo Jijini Dar es Salaam utakaohudumia wananchi 1440 kwa siku ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza Machi 16-22.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omar Kumbilamoto akimtua mama ndoo kichwani baada ya kuzindua mradi wa maji mtaa wa Majengo Vingunguti leo Jijini Dar es Salaam utakaohudumia wananchi 1440 kwa siku ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza Machi 16-22.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omar Kumbilamoto akifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji mtaa wa Majengo Vingunguti leo Jijini Dar es Salaam utakaohudumia wananchi 1440 kwa siku ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza Machi 16-22.

Lishe Endelevu kumaliza tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amepongeza ufadhili wa mfuko wa watu wa Marekani (USAID) kwa kuujumuisha Mkoa wa Rukwa katika mradi wa Lishe Endelevu, ili kupunguza na kuondoa hali ya udumavu, Ukondefu, upungufu wa damu kwa watoto na wanawake pamoja na upungufu wa uzito kwa watoto wachanga katika Mkoa.

Amesema kuwa kwa muda mrefu mkoa wa Rukwa umeendelea kusikitishwa na takwimu za Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu Tanzania (TDHS) chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) za mwaka 2015/2016 zinazoonyesha Mkoa wa Rukwa kuwa na kiwango cha asilimia 56.3 ya udumavu kwa watoto walio chini ya miaka mitano huku asilimia 5.3 wakiwa na ukondefu na asilimia 23 wakiwa na uzito mdogo.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha mkoa unajipanga kukabiliana na hali hiyo hadi sasa Mkoa tayari umefanikiwa kuandaa mpango mkakati wa lishe wa mkoa wa miaka mitatu ambao umeanza utekelezaji wake mwaka 2018 na kutegemewa kukamilika mwaka 2021, amabapo mpango huo umeainisha vipaumbele vya mkoa katika kukabuliana na utapiamlo ili kuondokana na udumavu.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amesaini Mkataba wa usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za lishe na wakuu wa wilaya. Kwa kila robo mwaka taarifa za utekelezaji wa Mkataba huu hujadiliwa katika Kikao cha mapato na Matumizi cha mkoa. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ndio mwenyekiti wa kikao hichi na pia agenda ya lishe imekuwa ni ya kudumu katika vikao vya kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na vikao vya kamati za ushauri za Wilaya (DCC),” Alisema.

Ameyasema hayo katika kikao cha utambulisho mradi wa Lishe Endelevu unaofadhiliwa kwa msaada wa watu wa Marekani unaosimamiwa na shirikia lisilo la Kiserikali la Save the Children kwa kushirikiana na Delloitee, PANITA, Manoff, na AAPH ambapo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyepaswa kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho kilichowajumuisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wenyeviti wa halmashauri waganga wakuu wa wilaya na wataalamu kutoka ofisi ya Mkoa na wawakilishi wa mashirika yanayojihusisha na maendeleo ya afya katika mkoa.

Akielezea namna ya kushirkiana na uongozi wa Mkoa pamoja na wasimamizi wa mradi Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Kalambo Mh. Daudi Sichone alilisisitiza kutomuangusha mkuu wa wilaya katika kutekeleza malengo ya mkoa kuhakikisha udumavu unapungua ili watoto waweze kulisaidia taifa katika miaka ijayo na hivyo kuwaasa wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu.

“Ntawataka wananchi wote katika halmashauri ya wilaya ya Kalambo na maeneo mengine ambapo mradi huu utapita tuhakikishe tunafuata taratibu ambazo tutaelekezwa na wataalamu kwamba vyakula hivi ndivyo vinaweza vikatutoa katika hali tuliyonayo na kwenda katika hali ambayo ni salama 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mradi huo Bi. Joyceline Kaganda alisema kuwa mradi huo tayari umeshatambulishwa katika mikoa mingine mitatu ya Dodoma, Iringa na Morogoro na hivyo kuja kumalizia katika Mkoa wa Rukwa ambapo uzinduzi rasmi wa mradi huo kitaifa utafanyika Mkoani Rukwa.

“Asilimia 56.3 ya watoto chini ya Miaka mitano wamedumaa hiyo siyo hali nzuri hata kidogo, hicho ndio kizazi ambacho tunategemea kitakutana na uchumi wa viwanda, Tanzania inataka kufikia Uchumi wa Kati, tunataka kwenda kwenye uchumi wa Viwanda, sasa kama hawa watoto wamedumaa, nani atafanya kazi kwenye hivyo viwanda? Tutafika kwenye lengo? Ndio maana mkoa umechukulia katika hali ya Uzito,” Alisema. 

Malengo ya mradi huo ni kupunguza udumavu kwa asilimia 15 huku malengo ya mkakati wa lishe wa Mkoa ni kuhakikisha mkoa unashuka kutoka asilimia 56.3 hadi kufikia asilimia 40 ya udumavu ifikapo mwaka 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha utambulisho wa mradi wa Lishe Endelevu unaofadhiliwa na watu wa Marekani (USAID).
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live


Latest Images