Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWILI WA MAMA YAKE VICKY KAMATA JIJINI MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mbunge wa Viti Maalum, Vicky Kamata kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati aliposhiriki katika mapokezi ya mwili wa Paulina Kasama Selemani ambaye ni mama mzazi wa Mbunge huyo, uliosafirishwa kwa Ndege kutoka Dar es salaam kwenda Geita kwa mazishi, Machi 19, 2019. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo ambaye ni kaka wa marehemu na kulia ni Mume wa Mbunge huyo, Dkt. Servicius Likwelile. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANAWAKE KUPATA FURSA KATIKA MASUALA YA KIUCHUMI KUPITIA SEKTA BINAFSI

$
0
0
* Washauriwa kutumia fursa za kiuchumi na biashara  zinazojitokeza 

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
JUKWAA la nane la Canada linalofanyika nchini kila mwaka limeadhimishwa leo jijini Dar es Salaam huku likijadili ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi na namna zinavyochangia maendeleo yao pamoja na changamoto wanazokumbana nazo.

Akifungua jukwaa hilo ambalo limeandaliwa na mtandao wa Haki rasilimali, ubalozi wa Canada, taasisi ya sekta binafsi nchini (TPFS)na Policy Forum Tanzania, balozi wa Canada nchini Pamela O'Donnel amewashukuru washiriki wa  jukwaa hilo ambalo litanyanyua wanawake wengi katika kufikia malengo yao, amesema kuwa jukwaa hilo pia litaweka mazingira bora ya biashara na uchumi kwa wanawake.

Amesema kuwa Canada itaendelea kushiriki katika masuala ya kuwainua wanawake ikiwa ni pamoja na masuala ya usawa wa kijinsia, pia ameeleza kuwa wataendelea kushauri na kuhakikisha haki za mabinti na wanawake zinakuwa na thamani.

Akimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC,) Mkurugenzi wa idara ya Uhamasishaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini John Mnali amesema kuwa semina hiyo italeta matunda bora kwa wanawake hasa katika fursa za uwekezaji na upatikanaji wa mikopo na masoko.

Amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo wanawake katika sekta binafsi ni kutopata fursa za ushiriki wa kutosha pamoja na uchache wa mitaji na amezishauri taasisi za kiserikali na binafsi kuzidi kuongeza na kuendeleza ushiriki wao kwa wanawake katika fursa mbalimbali.

Pia Mkurugenzi wa huduma kwa wanachama kutoka taasisi za sekta binafsi nchini (TPSF) Louis Accaro amesema kuwa lazima wanawake wapate nafasi katika biashara  na kupata huduma stahili kutoka kwa watoa huduma na wao kama TPSF watasukuma na  kuhakikisha  wanawake wanashiriki katika shughuli za kiuchumi na uzinduaji.

Amesema kuwa katika sekta ya madini kuna wachimbaji wadogowadogo wapatao milioni 6 huku akihoji ni idadi ngapi ya wanawake wanashirikishwa.

Accaro amesema kuwa mabaraza ya taifa ya uchumi yaliyoko katika Mikoa na Wilaya zote nchini yatumike vyema katika kuweka mazingira bora ya biashara hasa kwa wanawake.

Vilevile  Mratibu wa mtandao wa haki rasilimali nchini  Rachel Chagonja amesema kuwa sasa ni wakati wa kujadili nafasi ya mwanamke katika manufaa ya mnyororo wa thamani katika mambo yatakayowapeleka mbele yakiwemo masuala ya mafuta, gesi pamoja na madini.

Rachel amesema  kuwa sekta  uzinduaji inaonekana kuwa ngumu kutokana na changamoto za uendeshaji wake ila amewataka wanawake kuwekeza nguvu zao katika shuguli hizo na kuwashauri  kutumia fursa hizo na kuonesha ujuzi wao katika sekta hizo za madini, mafuta na gesi katika kujenga uchumi wao na taifa kwa ujumla.
 Balozi wa Canada nchini Tanzania, Pamela O'Donell akizungumza na wadau wa sekta binafsi katika jukwaa la Canada la miaka nane ambalo limejadili ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi, ambazo ni pamoja na Mafuta, Madini, gesi,  lililoandaliwa na TPSF Policy Forum, ubalozi wa Canada nchini Tanzania pamoja na Haki Rasilimali.
Washiriki wa mjadala wa Jukwaa la Canada la miaka nane ambalo limejadili ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi, ambazo ni Mafuta, Madini, gesi na ICT, wakisikiliza Hotuba ya mgeni rasmi, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini, John Mnali hayupo pichani kwa niaba ya  Mkurugenzi wa kituo cha hicho cha uwekezaji.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini, John Mnali akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya  Jukwaa hilo na kuahidi wanawake kupatiwa fursa za uwekezaji ikiwa ni pamoja na kupatiwa mikopo na amezitaka taasisi Mbali Mbali kuongeza ushiriki wa wanawake katika njanja Mbali Mbali  za kiuchumi.
 Mratibu wa Mtandao wa haki Rasilimali Rachael Chagonja akiwaeleza  wanahabari namna mwanamke anavyoweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kiuchumi Inayoonekana kuwa ngumu katika kuleta maendeleo. Aidha amewashauri wanawake kutumia fursa zinazojitokeza.

ANGELIQUE KIDJO ALIYEPINGA UKEKETAJI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Historia ya muziki katika nchi za Afrika Magharibi, haziwezi kumuengua Angelique Kidjo, ambaye ni raia wa nchi ya Benin.

Katika harakati zake za ushindani, Kidjo ameshinda tuzo ya Grammy pamoja na wanaharakati watatu kutoka barani Afrika, walituzwa tuzo ya haki za kibinaadamu mwaka 2016 kwa kusimamia haki na shirika la Amnesty International.

Wengine walioshinda ni pamoja na Yen a Marre wa Senegal, Le Bali Citoyen kutoka Burkina Faso na Lucha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katibu Mkuu wa Amnesty International Salil Shetty alitangaza katika taarifa yake kwamba wote wameonyesha ujasiri, shirika hilo la haki za kibinaadamu kwamba wanapigania haki za kibinaadamu kwa kutumia vipaji vyao kuwashiwishi wengine.

Msanii huyo amejiunga na orodha ya watu maarufu ambao wameshinda tuzo ya ubalozi wa watu walio na dhamira ya kubadilisha uovu katika jamii, akiwemo rais wa kwanza Afrika kusini Nelson Mandela na msanii wa China Ai Weiwei.

Msomaji wa makala haya itakuwa vyema kuufahamu wasifu wa mwanamama huyo Angelique Kidjo.Alijulikana sana kwa kampeni yake kwa uhuru wa kujieleza pamoja na vita dhidi ya ukeketaji.

Wakati akiwa na umri wa miaka sita, Kidjo alianza kijihusisha na kikundi cha Kibisa kilichokuwa kinamilikiwa na mama yake mzazi. Mama huyo ndiye akawa anampa kipaumbele sana katika muziki na kucheza pia.Kidjo ni msanii mashuhuri aliyejizolea sifa lukuki katika umahiri wa kutunga na kuimba nyimbo zenye maudhui yanayokubalika katika jamii.

Anafahamika sana kwa mtindo wake wa kuchanganya miondoko mbalimbali ya kimuziki ya Afro pop, Afro beat, Reggae, muziki wa dunia, Jazz, muziki wa Injili na Latin.

Kidjo katika wasifu wake unaeleza kuwa hivi sasa ni mtu mzima kwa umri ambae Julai 14, 2019 atatimiza miaka 59 tangu azaliwe Julai 14, 1960 katika mji wa Ouidah huko Jamhuri ya Benin, Afrika ya Magharibi.

Kwa wale wanaojua Jiografia vizuri watabaini kuwa nchi hiyo zamani ilikuwa ikiitwa Dahomey. Alianza kama mwimbaji wa bendi za vichochoroni kabla ya kuanzisha bendi yake mwenyewe, na mwishoni mwa miaka ya 1980.

Lakini kuendelea kwa machafuko ya kisiasa nchini Benin, kulipelekea Kidjo kukimbilia katika jiji la Paris nchini Ufaransa, mwaka ya 1982.Mwaka huo huo ndipo mkongwe huyo alipoianza kazi rasmi ya muziki mpaka hivi sasa bado anaendeleza talanta yake.Kidjo akawa mmoja kati waimbaji maarufu wa jukwaani huko Paris na amewahi kushinda mara tano tuzo ya Grammy kama mtunzi na mwimbaji bora. 

Aidha Angelique pia talanta ya ubunifu mzuri wa ‘sini’ za video.Kidjo ni mke wa mtu ambapo mumewe aitwae Jean Hebrail, pia ni mwanamuziki na mtayarishaji.Wamebahatika kupata mtoto mmoja aitwae Naïma, aliyezaliwa mwaka 1993.Kama walivyo wanamuziki wengi wenye wasanii wazuri, Kidjo kwa sasa anaishi New York, huko Marekani akifanya shughuli za muziki na zinginezo.

Nguli huyo amekuwa balozi wa kujitolea wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF tangu 2002.Kidjo katika juhudi zake za maendeleo zilipelekea kuanzisha mfuko uitwao Batonga Foundation.Mfuko ambao una lengo kubwa la kutoa elimu ya juu ya sekondari kwa wasichana kwa madhumuni ya kuwapa mwongozo wa maisha katika kuibadilisha Afrika. 

Batonga Foundation pia unakubali ufadhili wa wanafunzi, kujenga shule za sekondari, kuongeza uandikishaji zaidi, kuboresha viwango vya ufundishaji, na kukimu uenezaji wa shule. Adiha mfuko huo husaidia mipango endelevu katika elimu, kutafuta njia ya mbadala ya elimu na kuiwakilisha katika jumuiya kama ndio kuitambua thamani ya elimu kwa wasichana.

Angelique Kidjo aliwahi kutamba kwa wimbo uliomuongezea umaarufu ni wa ‘Agollo’.Katika video ya wimbo huo anaonekana akitamba jukwaani huku akiwa kanyoa kipara kichwani.Mwanamama huyo amekwisha fyatua albamu nyingi zikiwemo za ‘Parakou’ aliyoitoa mwaka 1990, ‘Longozo’ ya 1991, ‘Aye’ ilitoka mwaka 1994 , ‘Fifa’ ya mwaka 1996 na ‘Oremi’ ya mwaka 1998.

Alipiga nyimbo mchanganyiko zikiwemo za Black Ivory Soul ya mwaka 2002, Oyaya ya mwaka 2004 na Djin Djini ya 2007.Aidha Kidjo aliwahi kurekodi nyimbo nyingi kwa ajili ya filamu mbalimbali.Amekwisha tunukiwa tuzo zikiwemo za Octave RFI na Prix Afrique en Creation alizopokea mwaka 1992. 

Alipata tuzo ya uimbaji bora wa kike mwaka 1995, kwenye Kora Music Awards, mwimbaji bora kike wa Afrika mwaka 1997 na tuzo ya Mobo ya mwaka 2002.

Grammy ilimtunuku tuzo kupitia kipengele cha wimbo bora ya Video ya mwaka 1995 na albamu bora ya dunia kwa miaka ya 1999, 2003 na 2005. 

MFAHAMU HAMZA BENDELLADJ ALIYEDUKUA BENKI 217 NA KUSAIDIA PALESTINA NA AFRIKA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

AKIWA anatumikia kifungo cha miaka 15 gerezani alichokianza mwaka 2013  Hamza Bendelladj aliyepewa jina la "Mdukuaji anayetabasamu", anatumikia kifungo hicho  kwa makosa ya udukuzi katika benki 217 nchini Marekani na kuathiri zaidi ya kompyuta milioni 50 za watumiaji na kuweka rekodi ya kuwa mmoja kati ya wadukuaji 10 katika orodha ya mashirika ya upelelezi ya FBI na Interpol.

Hamza raia wa Algeria alizaliwa mwaka 1988 kwa sasa ana miaka 31 na   anazungumza lugha zaidi ya tano zikiwemo Kiingereza, kiarabu na kifaransa huku akiwa na Shahada ya sayansi na teknolojia ya komputa katika chuo kikuu cha Bab Ezzouar.

 Hamza amekuwa akifanya udukuzi na kutumia fedha hizo kwa kuwasaidia watu wenye matatizo , aliwahi kudukua mtandao rasmi wa serikali ya Israeli na kuhamisha zaidi ya dola milioni 280 za kuzigawa katika taasisi zisizo za kiserikali (NGO'S) nchini Palestina ili kuwasaidia wahitaji.

Alikamatwa Januari 8, 2013 mpakani mwa Malaysia na Misri na hakukataa kukamatwa kwake, alitabasamu kila alipopelekwa mbele ya vyombo vya habari na mkewe pamoja na binti yake walikuwa naye pamoja na kila hatua na hata alipoulizwa ni wapi alipopeleka fedha hizo alijibu amepeleka kusaidia Palentina na nchi za Afrika.

Yanayowavuta wengi kumuhusu ni pamoja na  kuwa na matukio mbalimbali ikiwemo ya kutengeneza maunzi laini(software) aina ya SpyEye na kuitumia katika kuiba fedha pamoja na  kuiuza kwa wadukuzi wengine hali iliyopelekea kuathirika kwa  watumiaji milioni 50 wa kompyuta baada ya nywila zao kudukuliwa.

Pia aliwahi kuwa mmoja wa wanachama cha wadukuzi cha Darkode.com pamoja na mdukuzi kutoka nchini Urusi Aleksandr Andereevich aliyehukumiwa jela miaka 8 na nusu jela.

Licha ya taarifa za kusambaa kuwa kijana huyo amenyongwa mamlaka husika ilikanusha taarifa hizo.

SERIKALI YA TANZANIA YATOA MISAADA YA MADAWA NA CHAKULA KWA MALAWI, MSUMBIJI NA ZIMBABWE ZILIZOKUMBWA NA MAFURIKO

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakipokea misaada ya madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika wakagua madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Sehemu ya misaada iliyotolewa na serikali ya Tanzania na madawa na chakula ikiwa tayari kupelekwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba
 Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha misaada ya madawa na chakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.

 Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha misaada ya madawa na chakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
 Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha misaada ya madawa na chakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Glad Chembe Munthali, Balozi wa Msumbiji Mhe. Monica D.C. Mussa na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini Mhe. Martin Tavenyika baada ya kuwakabidhi misaada ya madawa na vyakula ambavyo serikali ya Tanzania imetoa kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
Brigedia General Francis Shirima  wa kikosi cha anga cha JWTZ akiongea na wanahabari baada ya kukabidhiwa misaada ya madawa na chakula ili kuipeleka nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe  ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba

SIKU FILBERT BAYI ALIPOVUNJA REKODI YA DUNIA MJINI CHRISTCHURCH, NEW ZEALAND MWAKA 1974

KAMATI YA KUDUMU YA MIUNDOMBINU YATOA NENO KWA WIZARA

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupeleka fedha kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Mtwara - Newala - Masasi (KM 210), sehemu ya Mtwara - Mnivata yenye urefu wa KM 50 ili kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo.

Kamati hiyo imeonesha kutokuridhishwa na kasi ya mradi huo ambao mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 47 kwa sababu changamoto ya fedha kutolipwa kwa wakati.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Selemani Kakoso, amezungumza hayo wakati wa majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa miundombinu mkoani Mtwara jana ambapo walitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unaojengwa na mkandarasi Dott Services kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 89.

"Kama kamati sijaridhishwa na maendeleo ya mradi huu na sababu kubwa ya kucheleweshwa imesemwa hapa ni kuchelewa kwa malipo ya mradi huu, hali hii itachelewesha maendeleo katika mikoa hii hivyo Wizara mjitahidi fedha zije ili mradi ukamilike na wananchi wapate maendeleo' amesema Mwenyekiti Kakoso.

Aidha kamati imetoa wito kwa Serikali katika kuuendeleza mkoa huo hasa katika uimarishaji wa miundombinu ya barabara ili kuunganisha mkoa huo na mikoa jirani na kurahisisha usafirishaji wa korosho zinazolimwa mkoani humo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo anayesimamia masuala ya ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa ameihakikishia kamati hiyo wizara itatenga fedha katika bajeti ya mwaka 2019/20 ili ziweze kulipa madeni yanayodaiwa na mkandarasi huyo na mradi huo ukamilike ili kukuza uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla kupitia barabara hiyo.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo kwa kamati, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Barabara na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi John Ngowi, ameieleza kamati hiyo kuwa mkandarasi huyo anatakiwa kumaliza mradi mwezi Agosti mwaka huu na ameshaweka tabaka la kwanza la lami KM 8.5 na la tabaka la pili la lami KM 4.

Ameongeza kuwa mkandarasi amemaliza kazi ya ujenzi wa makalvati madogo 31, makalvati makubwa 4 na kazi zinaendelea ili kuhakikisha anakamilisha kwa kipindi cha mkataba.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imetembelea na kukagua kiwanja cha ndege cha mtwara ambacho kipo katika hatua za awali za uboreshwaji wake ambapo Serikali imepandisha hadhi ya kiwanja hicho kutoka Daraja 3C kwenda Daraja 4E kwa viwango vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Kakoso ameiagiza Seikali kumsimamia na kuhakikisha mkandarasi M/S Beijing Construction Engineering Group anaongeza kasi ya ujenzi ili aweze kukamilisha kwa wakati ambapo kazi zote zinatarajiwa kukamilika Mwezi Septemba, 2020.

Kamati pia imeielekeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuhakiisha wanapata hati miliki ya viwanja vyote hapa nchini ili kuepusha migogoro na wananchi wanaovamia maeneo ya viwanja vya ndege.

Uboreshwaji wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara ukikamilika utaimarisha usafiri wa anga, huduma za kibiashara, na kuchochea shughuli mbalimbali za ukuaji wa kiuchumi na kijamii katika ukanda wa kusini mwa nchi.

Kamati imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kutekeleza mradi wa upanuzi wa gati ya mtwara na kusisitiza mradi huo usimamiwe kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utekelezaji wa mradi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Barabara na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi John Ngowi, akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo, Mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu hatua za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo, Mkoani Mtwara.
Muonekano wa hatua ya ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 kwa kiwango cha lami. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 47 na utagharamu zaidi ya shilingi bilioni 89.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mtwara, Eng. Dotto Chacha, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 kwa kiwango cha lami, mkoani humo. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Selemani Kakoso.
Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng Emmanuel Raphael, akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu hatua za awali za uboreshwaji wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara kutoka Daraja 3C kwenda Daraja 4E, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eng. Desusdedit Kakoko, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu maendeleo ya upanuzi wa bandari ya Mtwara, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo, Mkoani Mtwara.


JAJI BARNABAS SAMMATA ASHAURI KUBADILISHA JINA LA MAHAKAMA YA MAFISADI

$
0
0
*Ahoji kuhusu Mahakama ya mafisadi, ahoji kuhusu jina hilo la Mahakama  mafisadi ni nani katika mahakama hiyo, je ni majaji? Mawakili? Washtakiwa au mashahidi? apendekeza jina hilo kubadilishwa

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
JAJI mkuu mstaafu na Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata ameshauri kubadilishwa kwa jina la mahakama ya mafisadi na litafutwe jina ambalo litasadifu wanaopelekwa katika mahakama hiyo ni washtakiwa.

Akizungumza katika mdahalo uliowakutanisha na wanafunzi wa chuo cha sheria nchini na kujadili mada kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya mahakama jaji Sammata amesema kuwa jina la mahakama ya mafisadi halisadifu wanaopelekwa katika mahakama hiyo kwa kuwa haifamiki mafisadi ni akina nani?, majaji? Mawakili? au mashahidi? na akashauri jina mbadala litafutwe ili kusadifu wanaopelekwa katika mahakama hiyo.

Katika mdahalo huo jaji Sammata alitoa rai kwa wanasheria kote nchini kuwa mstari wa mbele kupinga kansa ya rushwa wakati wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Jaji Mkuu mstaafu na Mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama.

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MKOA WA DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge alipomtembelea leo tarehe 19 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu wa Spika, Said Yakubu na kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (katikati) alipomtembelea leo tarehe 19 Machi, 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akifurahi jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka nje ya Ofisi ya Bunge leo tarehe 19 Machi, 2019 Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akifurahi jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka (kulia) nje ya Ofisi ya Bunge leo tarehe 19 Machi, 2019 Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (kushoto) nje ya Ofisi ya Bunge leo tarehe 19 Machi, 2019 Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA WA MJI WA MISUNGWI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa   (kulia) wakimsikiliza, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji  na Usafi wa Mazingira  Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) alipotoa maelezo kuhusu ujenzi wa Mradi wa Maji na Usafi  wa Mazingira  wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mji  wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti mkoani Mwanza, Machi 19, 2019. Kushoto  kwake ni Waziri wa Maji, Profesa, Makame Mbarawa na  kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira  Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga kuhusu michoro ya Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira  wa Mji wa Misungwi kabla ya kuweka jiwe la msingi la Mradi huo, Machi 19, 2019.  Wa pili kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na wa pili kushoto ni  Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua mashine za  za kusukuma maji kabla ya kuweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa  Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti mkoani Mwanza, Machi 19, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Maji  na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.  Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Anthony Daallo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

UWT KATA YA SARANGA WATAKIWA KUJITOKEZA KUCHUKUA NAFASI ZA UONGOZI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Dar es Salaam, Dorothy Kilave akizungumza na Wanawake Kata ya Saranga kwenye ziara ya kikazi kwa kata zote za Wilaya ya Ubungo ambapo amewaagiza Wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Dar es Salaam,Dorothy Kilave,akikagua Maonesho ya Wanawake wajasiriamali wa kata ya Saranga
 Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongea na Wanawake wa kata ya Saranga kwenye ziara ya Mwenyekiti wa wa UWT Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Dar es Salaam,Dorothy Kilave, akicheza na Wanawake wa kata ya Saranga
 Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ubungo akimkaribisha Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Dar es Salaam,Dorothy Kilave, akikabidhi kadi kwa Wanachama wapya wa UWT Wilaya ya Dar es Salaam.
 Wanachama wa Umoja wa  Wanawake wa Kata ya Saranga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Dar es Salaam,Dorothy Kilave

PRESHA YA MO YA DAKIKA TATU ZA MWISHO ZA MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA ZILIVYOGEUKA FURAHA ILIYOPITILIZA

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii  
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwekezaji wa Klabu ya Soka ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ kwa mara ya kwanza ameonyesha hisia zake na mapenzi kwa klabu hiyo katika mchezo wa mwisho wa Kundi D la Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo, ambapo Simba SC iliondoka na ushindi wa bao 2-1 na kufuzu Robo Fainali ya Michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.

Katika mchezo huo uliopigwa dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam majira ya Saa 1 Usiku, Simba SC ilionyesha kiwango bora na kupata ushindi huo mbele ya timu ngumu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vita Club.

Mohammed Dewji ‘MO’ akiwa na furaha iliyoje! siku hiyo baada ya ushindi huo wa Simba SC, MO ametuma picha yenye ujumbe iliyojawa na hisia ya huzuni na masikitiko kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram wakati huo kabla pambano kumalizika.

Ujumbe huo umeandikwa hivi: ‘’Hizi Picha zilipigwa zikiwa zimebaki dakika 3 kabla ya mpira kuisha. Tulikuwa na wasiwasi, Pressure ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba vidole vilikuwa na ganzi. Somo: Usikate tama. Mipango ya Mungu haina makosa! AMEEN’’

Baada ya matokeo hayo, Simba SC imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo, hata hivyo itasubiri March 20  droo ya Robo Fainali itakayofanyika nchini Misri.

BAGAMOYO YANUFAIKA NA MRADI WA MAJI KATIKA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0

Serikali imesema itahakikisha kuwa inaandaa miradi mbalimbali ili kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi hapa Nchini. Rai hiyo imetolewa  na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kutembelea moja ya Mradi wa Visima na Miundombinu ya kuvuna maji ya mvua katika Wilaya ya Bagamoyo inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Naibu Waziri Sima amesema kuwa Mradi huo umelenga hasa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi zitokanazo na maji ya bahari kuchangamana na maji ya visima. “Katika maeneo haya mradi umechimba visima kumi (10) na kuvijengea matanki ya lita 15,000 kwa lengo la kuwapatia maji safi  wakazi wa maeneo haya ambao visima vyao vya zamani vimeathiriwa na maji ya chumvi”.  Sima alisisitiza.

Aidha mradi huu umejenga miundombinu ya kuvuna maji ya mvua katika shule za Sekondari za Kingani na Matipwili zote za Wilayani Bagamoyo ambapo kwa kila shule takriban lita 147,000 hukusanywa katika matanki na huhudumia takriban wanafunzi 800. 

Mradi huu tofauti na miradi mingine ya maji umelenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi zinazosababisha watu kulazimika kutumia maji ya chumvi kutokana na visima vingi vya awali kuingia maji ya chumvi hali inayosababishwa na kuongezeka kwa ujazo wa bahari. “Lengo hasa ni kuwapatia vyanzo mbadala vya maji ikiwa ni hatua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo haya” Sima alisisitiza.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Murad Sadick ameipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi huo na kuishauri Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupitia kamati ya Maji kuhakikisha kuwa wanalinda miundombinu ya mradi huo ili uweze kunufaisha wakazi wengi zaidi na kuangalia namna bora ya uendashaji wa mradi huo ili kuwapunguzia gharama wananchi.

“Hakikisheni kuwa miradi hii inakuwa endelevu, kamati ya maji angalieni namna bora ya uendeshaji wa mradi huu, kiwango cha Shilingi 50 kwa ndoo bado ni kikubwa, kaeni mje na namna bora zaidi ili kuwaondolea wananchi hawa kero na tozo ya maji” Alisisitiza Mhe. Sadick

Mradi huu wa Kujenga Uwezo wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi ambao umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kupata fedha takriban dola milioni 3.3 kutoka Mfuko wa Nchi Maskini Duniani chini ya Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi ulitanguliwa na tathmini ya hali ya maji ya ardhini kwa lengo la kuainisha maeneo ambayo hayajaathirika na  maji ya chumvi kutoka baharini. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge wa Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Murad Sadick (wa tatu kutoka kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Luise Lugata Mtaalamu Mwelekezi kutoka Kampuni ya WEMA Contractors juu ya hali ya uchimbaji wa visima katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Wengine pichani, ni sehemu wa waheshimiwa wabunge, wajumbe wa Kamati hiyo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge wa Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Murad Sadick (aliyesimama) akiongea na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kingani katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Kingani ni miongoni mwa shule zilizonufaika na mradi wa kuchimba visima na kujenga miundombinu ya kuvunaji maji ya mvua chini ya Mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi katika Ukanda wa Pwani unaosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akimtwisha ndoo ya maji Bi Kulwa Mohamed mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara ya kikazi ya kukagua mradi wa uchimbaji wa visima na uvunaji wa maji ya mvua katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo katika eneo la Magomeni ikiwa ni  njia mojawapo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo ya Pwani.

TEF kutangaza watakaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali Nigeria mwaka 2019

$
0
0

LAGOS, NIGERIA

TAASISI ya Hisani la Tony Elumelu Foundation (TEF), ambayo inaongoza kwa uwezeshaji wajasiriamali wa Afrika, linatarajia kutangaza majina ya waombaji waliopitishwa kushiriki programu ya ujasiriamali Machi 22, mwaka huu.

Tukio hilo, ambalo litaashiria awamu ya tano ya programu ya uwezeshaji ya shirika hilo, itafanyika kwenye Hoteli ya Transcorp Hilton Hotel, mjini Abuja Nigeria.

Kila mwaka TEF hukaribisha maombi ya uwezeshaji kwa wajasiriamali wa Afrika, wenye biashara zenye umri usiozidi miaka mitatu.

Kupitia programu yake yenye thamani ya dola milioni 100, taasisi hiyo huwezesha wajasiriamali 1,000 kila mwaka, ambao hupokea dola 5,000 kama mtaji wa kuchochea biashara zao.

Aidha hukutana na wataalamu, programu ya mafunzo ya wiki 12 na fursa za kutangaza biashara zao kwa ulimwengu wa kibiashara.

Waombaji wote hupata fursa ya kuunganishwa na mtandao wa kidijitali wa TEFConnect, ambao ni kitovu cha dijitali ya ujasiriamali barani Afrika, ukitoa fursa ya kuunganishwa na mitandao, mafunzo na vyanzo zaidi vya mitaji na fursa za kibiashara.

Katika miaka mitano tangu taasisi hiyo izindue programu ya ujasiriamali, imewezesha moja kwa moja wajasiliamali 4,000 wa Afrika na wengine 470 wakisaidiwa na wabia wa TEF.

Akizungumzia programu hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa TEF, Ifeyinwa Ugochukwu, ambaye anachukua nafasi ya Parminder Vir, atakayebakia katika bodi ya ushauri kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu, alisema kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya wanufaika wa kila mwaka kutoka 1,000 ya sasa.

“Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la waombaji hivyo idadi ya wanufaika itapaswa kuongezeka. Mbia wetu, Accenture Development Partnerships, kwa sasa anatathimini na kupitisha waombaji.

“Zaidi ya wajasiliamali 215,000 wa Afrika kutoka mataifa 54 waliwasilisha maombi likiwa ongezeko kutoka waombaji 151,000 wa mwaka jana na kutoka 62,000 mwaka 2018 hadi 90,000 mwaka 2019 kwa pande wa wanawake. “Kupanda kwa takwimu hizi kunaonesha dhamira tya mjasiriamali wa Afrika kuendeleza bara letu na tunatakiwa kugeuza dhamira hii kuwa fursa ya biashara itakayochochea maendeleo ya bara letu,” alisema Ugochukwu.
 
 Baadhi ya wajasiriamali kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mafunzo mwaka jana
 
 

Jeshi la polisi Arusha lazindua Mfumo mpya wa kukusanya madeni

$
0
0
Na Woinde Shizza Globu ya Jamii.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetambulisha mfumo mpya wa ukusanyaji wa Madeni ya Makosa ya usalama barabarani unaotumia kamera maalumu zenye uwezo wa kupiga picha na kutambua gari linalodaiwa.

Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana amesema kuwa mfumo huo mpya utarahisisha kutambua Magari yote yanayodaiwa kupitia kamera maalumu zilizofungwa barabarani zitakazo kuwa zikipiga picha na kuonyesha kiasi ambacho gari linadaiwa.

Kamanda Shana amesema kuwa Jiji la Arusha limepata  kamera tatu za kisasa zinazotembea na zimefungwa katika maeneo mbalimbali katika Jiji la Arusha na kwamba machine hizo zinauwezo wa kutambua  namba za Magari ya aina mbali mbali.

Mtaalamu wa kitengo cha IT kutoka makao Makuu ya jeshi la polisi nchini,ACP Mayala Towo amesema mfumo huo umeanza kutumika  jijini dar es salaam tangu mwaka 2015, na sasa unasambaa nchi nzima na lengo ni kuhakikisha fedha ya serikali zinakusanywa kwa wakati.
Mmoja ya askari wa usalama barabarani anayeendesha mfumo huo wa kamera, Pc Masalu Yamala amesema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa kwani imerahisisha utambuzi wa Magari yanayodaiwa tofauti na hapo awali kwa kuwa lilikuwa likipoteza muda mwingi.

kamanda Shana alitumia wasaa huo kujitambulisha kwa waandishi wa habari na kueleza vipaumbele vyake vya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kupambana na uingizaji na utumiaji wa Dawa za kulevya ikiwemo Cocaine, Mirungi na Bangi.7

Picha ikionyesha Mmoja ya askari wa usalama barabarani anayeendesha mfumo huo wa kamera, Pc Masalu Yamala akiwaonyesha waandishi  Wa habari na wananchi jinsi kamera hiyo inavyofanya Kazi(Picha na Woinde Shizza globu ya jamii ).

TWIGA STARS KUINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA MCHEZO WAKE DHIDI YA DRC CONGO

$
0
0
Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” inatarajia kuingia kambini Machi 21,2019 kujiandaa na mchezo wa kufuzu Olympic dhidi ya DR Congo.

Mchezo wa kwanza utachezwa Aprili 5,2019 Nyumbani kabla ya kurudiana Aprili 9,2019 ugenini DR Congo.

Kocha Mkuu wa kikosi hicho Bakar Shime ametaja kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo huo.

Kikosi kilichotajwa :

1.Fatuma Omar Jawadu(JKT Queens) 
2.Najiath Abbas Idrissa(JKT Queens)
3. Gelwa Lugomba Yona( Kigoma Sisters) 
4.Wema Richard Maile(Mlandizi Queens) 
5.Maimuna Hamis Kaimu(JKT Queens)
6. Enekia Yona Kasonga(Alliance Queens)
7. Fatuma Issa Maonyo(Evergreen)
8. Fatuma Khatibu Salumu(JKT Queens)
9. Happyness Hezron Mwaipaja(JKT Queens)
10. Stumai Abdallah Athumani(JKT Queens)
11. Anastazia Antony Katunzi.(JKT Queens) 
12. Fatuma Bushir Makusanya(JKT Queens) )
13. Zena khamis Rashid(JKT Queens) 
14. Grace Tony Mbelay (Yanga Princess) 
15. Mwanahamis Omari Shurua (Simba Queens) 
16. Donisia Daniel Minja(JKT Queens) 
17. Asha Shaban Hamza(Kigoma Sisters) 
18. Asha Rashid Sada(JKT Queens) 
19. Amina  Ally Bilali( Simba Queens) 
20. Irene Elias Kisisa( Kigoma Sisters) 
21. Fatuma Mustapha Swalehe (JKT Queens) 
22. Dotto evalist Tossy (Simba Queens) 
23. Aisha khamis Masaka (Alliance Queens) 
24. Ester Mabanza Gindlya (Alliance Queens)
25. Tausi Abdalah Salehe (Mlandizi Queens) 
26. Niwael khalfan Makuruta (Marsh academy)
27.Amina Abdallah (Simba)

VITAMBULISHO VYA 'WAMACHINGA' VYANOGESHA BIASHARA YA MATUNDA KATIKATI YA JIJI LA DAR

$
0
0
Baadhi ya wafanyabiashara ya matunda katika Jiji la Dar es Salaam wakiendelea na biashara zao ambapo wameimbia Michuzi Blog kuwa wanamshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kutaka wafanyabiashara ndogondogo kuwa na vitambulisho na kutamulika rasmi.

Wafanyabiashara hao walieleza kuwa kwa sasa  wanaheshimika na usumbufu waliokuwa wakiupata hapo awali kabla ya kuwa na vitambulisho haupo,"kwakweli utulivu wa biashara zetu umesaidia hata kuongeza wateja kwani yale mambo ya kukimbiakimbia yamekwisha,hivyo kwa hakika tunamshukuru Rais Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya  Tano kwa namna ambavyo imekuwa ikiwajali wanyonge",alisema Fredi Nyasiki mkazi wa Kimara ambaye hufanya biashara zake za matunda katikati ya jiji la Dar.
Wafanyabiashara wa matunda mbalimbali wanaotumia baiskeli wakiwahudumia wateja, kama walivyokutwa na Kamera ya Michuzi blog kando ya Barabara ya Samora, Dar es Salaam leo,vijana wengi kwa sasa wana vitambulisho vya wajasiliamali almaarifu kwa jina la vitambulisho vya Wamachinga vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuli hivi karibu kwa Wakuu wa mikoa yote nchini .  (Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


wafanyabiashara wakiendelea kukatiza katika viunga vya Jiji la Dar es Salaam.

Jarida la Kitaalam Kuhusu Sekta ya Maji Laanzishwa

$
0
0
Wataalam katika sekta ya maji wanaohuduhuria Kongamano la Kisayansi Kuhusu Sekta ya Maji nchini wametakiwa kutoa elimu kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji ambayo haiongezeki ilhali mahitaji yake yanaongezeka kila siku. 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema hayo jijini Dodoma wakati akiongea na Wataalam na washiriki wa kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili ikiwa ni moja ya matukio ya Wiki ya Maji kitaifa kwa mwaka 2019. 

Prof. Mkumbo amesema miongoni mwa miji inayokua kwa kasi hivi sasa ipo Barani Afrika na kama hatua hazichukuliwa mapema uhaba wa maji utaikumbuka baadhi ya miji ifikapo mwaka 2050. Amesema ni vizuri wataalam wakatumia elimu yao kuwashirikisha wananchi na kutoa elimisha zaidi kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji. 

Prof. Mkumbo amesema ni vizuri kujenga utamaduni wa kuwa na jukwaa la kuwashirikisha watu wengine kuhusu uzoefu na utaalam pamoja na utafiti katika sekta ya maji ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utendaji kazi, na kuhudumia wananchi vizuri zaidi. 

Kufuatia wazo hilo, wataalam na washiriki wa Kongamano la Kisayansi wameazimia kuanzisha chapisho la kitaalam, Jarida la Sekta ya Maji, na kumpitisha Prof. Tolly Mbwete kuwa Mhariri Mkuu mwanzilishi, na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo kuwa mlezi wa jarida hilo. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 

MSHAMA AWACHARUKIA WAFUGAJI WASIOPELEKA WATOTO WAO SHULE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 
MKUU wa wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Assumpter Mshama amewaagiza watendaji wa vijiji na kata, kuhakikisha watoto wa wafugaji walio na umri wa kwenda shule, wanakwenda ili wapate haki ya elimu kama ilivyo kwa watoto wa jamii nyingine. 

Aidha ameeleza, wilaya inatarajia kuchukua sensa ya watoto wa wafugaji ili kupata idadi kamili ya watoto hao ambao hawaendi shule hadi sasa. 

Assumpter alitoa agizo hilo, wakati akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wafugaji na wakulima, kijiji cha Kwala, Kibaha Vijijini. 

Aliwataka ,wafugaji kuacha kuwatumikisha watoto wao kuchunga mifugo hasa ng'ombe badala ya kuwapeleka shule kupata elimu. 

"Watendaji nendeni mkahakikishe hakuna mtoto wa mfugaji anaefuga, hawa ndio Sokoine wa kesho, kwenye maziwa kuna akili, wanarubuniwa tuu, ila wafugaji watie akilini kwamba mtoto akizaliwa sio wako ni mali ya serikali "

"Haiwezekani wewe unaenjoy, mnakaa kujiolea wanawake 30, wakati watoto wako hawaendi shule, baadae hawa hawajui kama wataweza kuoa wake wengi hivyo kutokana na uchumi na maisha yanavyobadilika ""alisema Assumpter. 

Mkuu huyo wa wilaya alielezea, serikali inajitahidi kujenga mazingira bora ya kielimu na kusomesha watoto bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne lakini jamii hiyo haijatambua umuhimu wa fursa hiyo. 

Pamoja na hayo,Assumpter aliwaomba waendelee kuheshimiana ,kuishi kwa upendo kati ya jamii ya wafugaji na wakulima .

Nae makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Esta Moreto aliiasa jamii hiyo kujenga utamaduni wa kusomesha watoto wao badala ya kuwageuza wachungaji wa mifugo ya familia, bali wafanye shughuli hiyo baada ya kutoka masomoni. 
MKUU wa wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Assumpter Mshama 

EFM YAKABIDHI BODABODA MBILI UFUNGUZI PAZIA LA SHIKA NDINGA MSIMU WA TANO

$
0
0
 Meneja wa Kituo Cha Radio Cha Efm, Dennis Busolwa(Sebo), Akitangaza Majina ya Washindi wa shindano la shika ndiga lililozinduliwa katika Viwanja vya Temeke Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam, ambapo Sebo alitumia muda huo kuwashukuru wasikilizaji wa Efm Kanda ya Pwani na Dar es Salaam

 Meneja huduma za Bima Kutoka Benki ya NBC, Benjamini Nkaka, akikabidhi kadi ya gari kwa Mshindi wa shika ndinga upande wa Wanawake.
 Meneja Huduma za Bima Kutoka Benki ya NBC, Benjamini Nkaka, akikabidhi kadi ya gari kwa Mshindi wa shika ndinga upande wa Wanaume, Masudi Said
 Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Shika Ndinga wakiwa wameshikilia gari hilo kuelekea hatua ya fainali
 Msanii wa Muziki wa Singeli Maarufu kwa jina la Mzee wa Bwax akitoa Burudani kwa wakazi wa Temeke Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam
baadhi ya Wakazi wa Wilaya ya Temeke waliofika kushuhudia ufunguzi wa pazia la shindano la shika ndinga kwa Wilaya ya Temeke.
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images