Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

14 WAKAMATWA NA BANGI,WENGINE WAWILI KETE TANO ZA COCAINE MKOANI PWANI

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WATU 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Pwani, baada ya kukamatwa na wakiwa na kete 173, puli 19 ,misokoto 88  ya bangi pamoja na wengine wawili wakiwa na kete tano za madawa ya kulevya aina ya cocaine  .

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema, watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako unaoendelea mkoani hapo. 

Alieleza, huko Kwamfipa kata ya Kongowe walikamatwa Ramadhani Salehe na Frank Lusasi wakazi wa Mwendapole wakiwa na kete za madawa ya kulevya aina ya cocaine ambapo walikiri kujihusisha na uuzaji wa madawa hayo. Wankyo alisema kwamba, baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika wote watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. 

Aidha watu watano wanashikiliwa na jeshi hilo, kwa kosa la kupatikana na mitambo miwili ya kutengeneza pombe aina ya gongo na lita 65 za pombe hiyo.   Wankyo alitoa rai kwa jamii hususan kundi la vijana kuacha kujiingiza katika uuzaji wa madawa ya kulevya na bangi na kuacha kuvuta bangi kwani ina madhara kwao kiafya. 

Aliwaasa wafanye kazi nyingine ikiwemo ujasiriamali ili kujiepusha na biashara zisizo na tija kwao na ambazo haziruhusiwi kisheria. Pia aliisa jamii kufichua wale ambao wanawatilia shaka kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu ili sheria ichukue mkondo wake.

WAZIRI LUGOLA AONGOZA KIKAO CHA WAKUU WA IDARA WA WIZARA YAKE KUPITIA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza katika Kikao cha kupitia Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara yake, ya Mwaka wa Fedha wa 2018/19, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto meza kuu) akizungumza na Wakuu wa Idara wa Wizara yake katika Kikao cha kupitia Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo, ya Mwaka wa Fedha wa 2018/19, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto meza kuu) akizungumza na Wakuu wa Idara wa Wizara yake katika Kikao cha kupitia Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo, ya Mwaka wa Fedha wa 2018/19, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI HASSAN SIMBA YAHYA,AAGANA NAYE.

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya mteule wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi mpya mteule wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mgomo wa Daladala jijini Mbeya wazua tafrani

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 18.03.2019

TAASISI ZA USANIFU NA UHANDISI WATAKIWA KUWA WABUNIFU

0
0
Na Woinde Shizza,Arusha
Naibu waziri wa viwanda,baishara na uwekezaji mhandisi Stela Manyanya ameitaka taasisi ya  uhandisi na usanifu wa mitambo Tanzania(temdo )kuendelea kuwa  wabunifu  zaidi  katika uzalishaji wao  wa teknolojia ili  wawweze kusanifu mitambo inayokidhi malengo ya serikali  ya kuanzisha taasisi hiyo.
Injinia manyanya aliyasema hayo wakati kamati  ya  bunge  ya viwanda,biashara na mazingira ilipotembelea taasisi ya TEMDO kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi.
Amesema kwa kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa Temdo katika kusanifu mitambo ni vema tasisi hiyo ikaongeza ubunifu zaidi katika uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya serikali ya kuzalisha bidhaa zinazoenda na wakati
Ameongeza kuwa serikali itaangalia namna ya kuendelea kuziwezesha taasisi hizo za utengenezaji wa zana za kilomo na mashine   kwa kuzitolea fedha za bajeti ili ziendelee kuzalisha zana na mitambo yenye kukidhi mahitaji ya wananchi na viwanda.
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa kamati yakudunu ya bunge viwanda ,biashara na Mazingira aliwataka pia taasisi hiyo kujiendesha kibiashara  zaidi ,wazalishe fedha za ndani.
"Nendi kibiashara zaidi mtazalisha fedha zenu wenyewe ambazo zitawasaidia kuendelea kujiendesha hata kama fedha za bajeti za serikalini zikichelewa kuwafikia nyie mnaendelea kujiendesha wenyewe sio kukaa na kusubiri tu fedha za bajeti zije" alisema Mwenyekiti.
Kaimu meneja wa ushauri viwandani   kutoka taasisi ya TEMDO Alexander Komba   amesema ujio wa kamati ya bunge katika tassisi hiyo kunaiwezesha serikali kuweza kuongeza nguvu zaidi iliwaweze kuwa wabunifu  katika  teknolojia zenye kukidhi mahitaji ya soko kufuatia vitendea kazi wanavyonunua kupitia fedha wanazopewa za bajeti.
Kamati ya Kudumu  Bunge  ya viwanda ,biashara na mazingira ikikagua mashine zilizopo katika taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO) iliopo jijini Arusha (Picha na Woinde Shizza).


RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU DKT KIKWETE IKULU DAR ES SALAAM

ZAINABU VULU AFUNGUA OFISI YA UWT KISARAWE.

0
0

 Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani,Zainabu Vulu akizungumza na wajumbe wa kata ya Kisarawe ambapo alisema Msingi wa kuwa na maisha bora ni kufanya kazi kwa bidii na ameahidi kuendelea kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanasonga mbele bila  kurudi nyuma.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani,Zainabu Vulu akikabidhi viti kwa Katibu wa UWT kata ya Kisarawe,Moshi Litatilo kwaajili ya ofisi  ya kata hiyo.


Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani,Zainabu Vulu akifungua ofisi  ya kata UWT  Kisarawe mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


JAMII IACHE KUFUNGIA WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI –NURU

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh amesema kuwa jamii iache kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwani watu wenye ulemavu wanaweza kufanya vitu vikubwa na kusaidia nchi katika maendeleo mbalimbali.

Nuru aliyasema hayo wakati  wa hafla ya Tuzo ya I Can  ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee  hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 Nuru amesema Tuzo mbili alizozipata zimetokana na kuwa na mchango katika jamii licha ya kuwa na ulemavu wa kuona lakini ameweza kutumia kipaji chake na kuiletea maendeleo nchi pamoja na wananchi.

Amesema kuwa yeye angefungiwa ndani asingeweza kupata elimu na kufanya maisha yake ya ulemavu kufunga kipaji pamoja na ndoto zake ambapo leo anaongoza watu wa makundi mbalimbali na wanamuamini katika uongozi.

‘’Namshukuru Rais Dkt. John Pombe Mgufuli kwa kuteua viongozi mbalimbali wenye ulemavu katika serikali yake ni kutokana na kutambua mchango wa wenye ulemavu kushiriki katika ngazi za maamuzi na sasa kufanya walemavu kijiamini kwa kupita kifua mbele”.amesema Nuru.

Nuru amesema watu wenye ulemavu wana kipaji kikubwa huvyo jamii iache kuwafungia ndani kwa kuona hawawezi kufanya chochote katika jamii yao wanayoishi.

Aidha amesema kuwa watu wenye uleamvu kwa vijana wanaosoma wasife moyo kwa ulemavu wao wasome kwa bidii kwani elimu ndio mkombozi kwa mtu mwenye ulemavu.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akipongeza Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee kwenye hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akipokea hundi ya sh.milioni mbili kutoka kwa mwakilishi wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akizungumza na Michuzi Blog wakati hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka.MMG)
 Makamu  wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na watu wenye ulemavu mara baada ya ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akiwa katika picha ya pamoja na Familia yake  katika ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka.MMG)

TBS YATOA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI WILAYANI LUSHOTO

0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na Semina kwa wajasiliamali wadogo katika Wilaya ya Lushoto ya kutoa Elimu kwa walengwa, kuhusu utekelezaji wa viwango vya kitaifa vya bidhaa zinazozalishwa na zinazosindikwa, pamoja na namna ya kupata alama ya ubora kwenye bidhaa wanazozalisha,Sambamba na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Semina hiyo kwa wajasiliamali wadogo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, huku wajasiriamali 33 wakijitokeza kupata elimu hiyo sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa. Wajasiriamali hao wanazalisha bidhaa za maziwa, siagi, mtindi, asali, jam, juisi, mbogamboga, wasindikaji wa nyanya na vitunguu saumu.

TBS katika semina hizi inashirikiana na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na ofisi ya Afisa Biashara.

Akifungua Semina hiyo Mhe. January Lugangika, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, amesisitiza washiriki kutumia hii fursa kwa kusikiliza kwa makini ili kutumia elimu watakayopata katika kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa, kwani vita dhidi ya umaskini ni yetu sote. Aidha Mh. January ameongeza kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima kuzingatia viwango kwani vita dhidi ya umaskini ni yetu sote.

Akifunga semina hiyo, Afisa Udhibiti Ubora Mkuu, Cunbert Kapilima (TBS), alisisitiza kuwa TBS inatambua mchango wa wajasiriamali katika kukuza pato la taifa na kutengeneza ajira kwa wananchi walio wengi. Hivyo TBS ina mchakato endekevu kutoa elimu kwa wajasiliamali kwa kuwa ni mojawapo ya majukumu yake ya kila siku. 

TBS mpaka sasa imeshatoa semina na mafunzo kwa bidhaa mbalimbali kwa washiriki kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Katavi, Kagera, Kigoma, Tanga, Tabora, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya  Lushoto, Mhe. January Lugangika akifungua Semina ya wajasiliamali katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Lushoto, Machi 18, 2019. Kushoto ni Bw. Cunbert Kapilima, Afisa udhibiti ubora mkuu(TBS) na kulia ni   Bw. Faustine January, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TBS).
 Bi. Gladness Foya, Afisa maendeleo ya biashara (SIDO), akiwasilisha mada ya teknolojia za usindikaji bidhaa za vyakula kwa wajasiliamali wa Wilaya ya  Lushoto.
Bw. Cunbert Kapilima, Afisa udhibiti ubora mkuu(TBS), akiwasilisha mada ya elimu ya ufungashaji kwa wajasiliamali wa Lushoto (w).
 Bw.Halfa Sume, Mkaguzi wa Chakula (TFDA), akiwasilisha mada ya usajili wa jengo na bidhaa za chakula kwa wajasiliamali wa Lushoto (W).
 Wajasiliamali wilayani Lushoto (W), wakisikiliza mada mbalimbali katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya lushoto.
Bw.Stephen Rwabunywenge, Afisa Viwango Mwandamizi (TBS), akiwasilisha mada ya viwango vya chakula, matumizi na faida za viwango kwa wajasiliamali wa Lushoto (W).

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 19,2019

'WINGU JEUSI’ KUMKUMBA KOFFI OLOMIDE ‘MOPAO’

0
0
Na: Moshy Kiyungi,Dar es Salaam

Jeuri ya pesa inaweza ikampandisha au kumshushia mtu umaarufu, hadhi hata heshima iliyoisaka kwa kipindi kirefu.

Pesa zikiwa nyingi kibindoni, husabisha dharau kwa mwingine asiyenacho, yupo radhi hata kumtemea mate utosini!

Tunashuhudia baadhi ya Watanzania wenzetu wanaopelekwa Ughaibuni, wakiahidiwa kupata ajira murua, lakini huko huambulia kufanyishwa kazi za ndani mithiri ya watumwa.Humu nchini wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiwaajiri kaka na dada wa ndani wakiwafanyisha kazi nyingi kwa ujira mdogo pasi soni wala huruma.

Makala hii inamzungumzia mwanamuziki mkubwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide.Nguli huyu anayemiliki utajiri wa sawaswa na shilingi bilioni 40 za Kitanzania, yaelezwa kuwa ukiwataja wanamuziki matajiri, Koffi ni mmoja wao.

Olomide anamiliki hoteli yenye hadhi ya nyota 5, ana hisa kwenye Kampuni kadhaa ndani ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nje.Ukwasi huo huenda ndiyo sababu ya ‘Wingu jeusi’ kumyemelea.

Mwaka jana aliingia kwenye mlolongo wa matajiri wasio na huruma wala staha kwa wafanyakazi wao.Koffi Olomide anakabiliwa na misukosuko lukuki iliyoisababisha mwenyewe kwa vitendo vyake vya kujichukulia sheria mkononi.

Mwanamuziki huyo mwaka jana alikataliwa kuingia nchini Zambia, ambako alitaka kufanya maonesho ya muziki kutokana na makosa mengi aliyoyafanya nchini Ufaransa.

Kuzuiliwa kwa Koffi Olomide kunatokana na ushawishi mkubwa wa Balozi wa Ufaransa nchini Zambia, Bwana Sylvain Berger, aliyesema kuwa mwanamuziki huyo anayo mashitaka nchini Ufaransa yanayomtuhumu kumshambulia mpigapicha wakati alipofanya ziara nchini humo.

Balozi Berger alitishia kuwatumia maofisa wa Polisi wa Kimataifa (Interpol), kumkamata mwanamuziki huyo, akisema kuwa mashitaka yake bado hayajafutwa nchini Ufaransa.Berger alijinasibu kwa kusema kuwa atashirikiana na serikali ya Zambia, kumkamata Olomide, iwapo atathubutu kuingia nchini humo.

Hata hivyo, kabla ya kupigwa marufuku, Koffi alijinasibu kuwa anaipenda nchi ya Zambia, huku akisema anataka hapo ndiko yawe makazi yake ya pili baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mopao alikaririwa na kituo kimoja cha redio nchini Zambia, akiomba msamaha kuahirishwa kwa onesho la hilo kutokana na marufuku hiyo.Pamoja na hayo, alikana mashitaka yaliyosababisha apigwe marufuku kuingia nchini humo, bila kuingia kiundani kuhusu tuhuma zinazombabili.

Nyota huyo anayevuma kwa kupiga muziki mzuri na utanashati wa mitindo ya mavazi yake na maisha ya kifahari, amewahi kukumbwa na kashfa kama hizo katika miaka iliyopita.

Kumbukumbu zinaonesha mwaka 2008, alidaiwa kumpiga na kumvunjia kamera kibabe mpigapicha wa shirika la habari la RTGA!Olomide alifanya hivyo baada mpigapicha huyo kuingia sehemu moja ya burudani katika mji wa Kinshasa nchini DRC, kutofautiana kuhusu vibali vya kupiga picha.

Sakata hilo lilikuwa kubwa kiasi cha uongozi wa Bunge la Kitaifa kuingilia kati na kusulihisha mgogoro uliokuwepo kati ya mwanamuziki huyo na mmiliki wa kituo cha luninga hiyo.Olomide aliwahi pia kupigwa marufuku kufanya onesho Ulaya kutokana na kesi nyingine ya kuhangaisha wasakataji densi wake.

Aidha mwaka 2016, Koffi Olomide alinaswa kwenye kamera akimdharirisha mmoja wa wanenguaji wake kwa kumpiga teke baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata nchini Kenya.

Kutokana na tukio hilo serikali ya nchi hiyo, ilimuamuru mwanamuziki huyo kuondoka mara moja nchini humo, kutokana na kutokubaliana na vitendo vya udharirishaji kwa wanawake.Onesho lililokuwa limepangwa kufanya jijini Nairobi lilifutwa, huku wapenzi na mashabiki wake wakibaki wakisubiri kwa hamu.

Kama hiyo haitoshi, mwaka 2012, Koffi alipatikana na hatia ya kumshambulia na kumjeruhi msimamizi wake wa karibu, Diego Lubaki, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Katika shambulio hilo, Olomide alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Lakini hakukitumikia kifungo hicho gerezani baada ya kulipa faini.Ilidaiwa kuwa mwanamziki huyo alimshambulia Lubaki, kutokana na ubishani baina yao juu ya deni la dola 3,700.

Kisa kingine cha nguli huyu wakati mmoja alilighadhabisha Kanisa Katoliki alipojiongezea jina “Benedict wa 16 wa Kongo”, jina ambalo lilikuwa jina la Papa Benedict wa 16 wakati huo.

Koffi ni nani?

Wasifu wa mwanamuziki huyu unaeleza kuwa majina yake halisi anaitwa Antonie Christophe Agbepa Mumba. Alizaliwa Julai 13, 1956 katika mji wa Kisangani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Olomide ana asili wa nchi mbili za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sierra Leone.Mama yake ni raia wa Kongo DRC, akitokea katika kabila la Songye ambalo linapatikana katika mkoa wa Kasai. Baba yake ni mwenye asili ya nchi ya Sierra Leone.

Kwa mujibu wa mila na utamaduni wa kabila la babu zake, mama yake alimpa jina la ‘Koffi’ kutokana kuwa alizaliwa siku ya ijumaa.Olomide kuna kipindi alijartibu kuiingia katika uringo wa siasa nchini DRC, lakini alikumbana na vikwazo lukuki kikiwamo cha uraia wake kutiliwa mashaka.

Akiwa bado ‘kinda’ Koffi alipachikwa jina bandia la ‘Antoine Makila Mabe' likiwa na maana ya 'damu mbaya ya Antony’.Alianza safari ya muziki mwanzoni mwa miaka ya 1970, katika bendi ya Viva la Musica, iliyokuwa na wanamuziki magwiji akiwemo kiongozi wa bendi hiyo, Papa Wemba.

Koffi alianza kupiga muziki katika bendi hiyo akiwa kama mtunzi wa nyimbo na baadaye aligeukia katika uimbaji.Olomide pamoja na kupenda muziki tangu akiwa mtoto, ndoto zake kubwa zilikuwa awe mchezaji wa mpira wa miguu.

Kama Wahenga wasemavyo kuwa “Atafutaye hachoki, akichoka ujue kaisha pata”, mwaka 1986 alianzisha bendi iliyofahamika kwa majina ya Quartier Latin International.Baada ya miaka kadhaa kupita, bendi hiyo alijizolea umaarufu Kimataifa hususan katika Bara la Afrika na Ulaya.
Baadhi ya albamu zake zilizotoka ni Tcha Tcho ya mwaka 1990, Haut da gamme ya mwaka 1992, Noblesse Oblige ya mwaka 1994 na Magie ya mwaka 1995.

Zingine ni pamoja na Gagi ya Film Diva ya mwaka 1995, V 12 ya mwaka 1996, Loi ya mwaka 1997, Droit de Veto ya 1998, Attent ya mwaka 1999, Force de frappe ya mwaka 2000, Efrakata ya mwaka 2001, Affaire d’ Etat ya mwaka 2003, Monde arabe ya 2004 na Bord Ezang Kombo ya 2008.

Antoine Koffi Olomide alikulia katika familia ya watu wenye uwezo wa kati na mahali ambapo elimu ilikuwa ikipewa kipaumbeleAlipoanza kupevuka akiwa na umri wa miaka 18, wakati huo akiwa mwanafunzi kijana, alivutiwa sana na usanii pamoja na muziki, ndipo alipoanza kutunga na kuimba nyimbo.

Kwa mujibu wa historia hiyo, Koffi alikuwa ana akili sana darasani hali ambayo ilimfanya apate wadhamini wa kumlipia kwenda kusoma mjini Bordeaux, Ufaransa ambapo alipata Shahada yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi.

Mbali na shahada hiyo inaeleza pia ana shahada ya pili katika masuala ya hisabati kutoka chuo kikuu cha Paris, Ufaransa. Akiwa Paris alianza kujifunza kupiga gitaa na kuandika nyimbo na aliporudi drc alijiunga na bendi ya muziki ya muziki ya viva la musica ambayo ilikuwa ikiongozwa na Papa Wemba.

Baada ya kujiunga na bendi hiyo Koffi aliimarisha mtindo wa polepole wa soukous uliokuwa umeisha umaarufu aliouita Tcha Tcho.Baadaye aliamua kujitenga na kundi hilo na kuanza kuimba kama mwanamuziki wa peke yake ‘soloist’ na hadi mwaka 1986, alipounda bendi yake aliyoipa jina la Quartier Latin.

Baada ya miaka kumi ya mafaniko yake, akatamani kuwa mwanamuziki wa Kimataifa. Ilipofika mwaka 1988 wimbo wa 'Henriquet' ukatokea kuwa mkali uliopelekea kupachikwa jina bandia la ‘Golden Star'.

Koffi olomide aliyafurahia mafanikio zaidi baada ya kuandika wimbo akiwa na binti yake pekee Minou, ukiitwa D'elle et Moi' miaka ya 1990.Koffi toka mwaka 1990 hadi 1994, alifurahia kukua kwa mafaniko yake ambayo kwa kipindi cha miaka chini ya minne, alifyatua zaidi ya album saba zikiwa chini ya jina lake na kundi lake la 'Quartier Latin’.

Mwaka 1992 alichaguliwa kuwa mwimbaji bora wa kiume na mshindi wa video bora katika shindano la African Music Awards mjini Abidjan, Ivory Coast.Yaelezwa kwamba ujuzi wa aina yake, mpangilio mzuri wa muziki kumempa umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Antoine koffi Olomide alifyatua albam yake kali inayotamba ya Abracadabra, iliyonguliwa na albam za Ngounda, Efrakata, Tcha Tcho, Haute de Gamme – Koweit, Rive Gauche.

Baadhi ya nyimbo za nguli huyu ni pamoja na loi, Magie, Stila, Sexy Pop, Rounge A Levre, Etant Civil, Round Poit, San suit, Respect 2, l Autre la, Miss Dess, Nolesse Oblige na Escola Phamacien. Wimbo wa Phamacien sehemu kubwa ya uimbaji ametamba aliyekuwa mwimbaji wake Fally Ipupa.

Mwaka 1998, Koffi akiwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa, alikimbiwa na wanamuziki takribani wote, baada ya onesho kubwa lilofanyika katika ukumbi wa Olympia.

Bendi hiyo ilisambaratika na baadhi ya wanamuziki wake wakaenda kuunda bendi yao ya Orchestra ‘Quartier Latin Academia.Baada ya tukio hilo, Olomide hakuteteleka kabisa kwani haikuchukuwa kipindi kirefu akaibua tena vijana wengine wenye vipaji toka sehemu mbalimbali nchini humo.

Amewafundisha wanamuziki wengi chipukizi ambapo wengine wameamua kujitegemea na kusimama wenyewe katika kazi za muziki na wengine bado wapo na bendi hiyo hiyo .Baadhi ya wanamuziki ambao ameshawatoa ni Fele Mudogo, Motana Kamenga, ambaye alitimka kwenda kujiunga bendi ya Big Star ya General Defao.

Wengine ni pamoja na Bruno Mpela, Soleil Wanga, Sam Tshintu, Suzuki 4 by 4, Ferre Gola na Fally Ipupa.

Olomide aliwahi kufika hapa nchini mwezi Desemba 2012 ambapo ‘alimwaga’ burudani kamambe zilizokonga nyoyo za Watanzania walihudhuria onesho lake lililofanyika katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es salaam.

Nyimbo zake mpya zinazotamba hivi sasa ni Tshou Tshou, Nyataquance, Selfie, Mbirime, Afrakata, Charisma, Salopette, L’amour N’existe pas, Diaspora na Sixieme.

Koffi Olomide ni baba wa familia ya mke na watoto saba. 

Koffi Olomide Julai 13, 2018 alitimiza miaka 62, huku akiendelea na shughuli za muziki licha misukosuko hiyo kumharibia kazi yake. 

Hata hivyo nguli huyo Koffi ametangaza kung’atuka kwenye shughuli ya muziki baada ya kutoa albamu yake mpya ambayo iko studio kwa sasa, Hii itakuwa ni Albamu ya 20 ya mwanamuziki huyu ambaye anamaliza akiwa na mafanikio na mpaka sasa albamu zake tatu zimeorodheshwa kwenye orodha ya albamu 1,000.

WAANDISHI JIENDELEZENI NA KUZINGATIA MAADILI

0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha

Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa jangwa la Sahara( MISA) imeendesha mjadala wa siku moja wawaandishi wa habari, na wadau mbalimbali vya habari Jijini Arusha katika chuo cha Uandishi wa habari cha Fanikiwa ikiwa na lengo la kujadili changamoto zilizopo kwenye vyombo vya habari.

Gasirigwa Sengiyumva ni Mkurugenzi wa MISA nchini amesema kuwa lengo kuu la mjadala huo ni kuboresha namna ambayo vyombo vya habari vinafanya kazi, kukuza uhuru wa habari, kupata habari, uhuru wa vyombo vya habari

Amesema kuwa upo umuhimu wa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi, kuendana na sheria ya habari ya mwaka 2016 na kumtaka kila mwandishi kutimiza wajibu wake kwa kutafuta ukweli wa habari na uripoti ukweli sahihi, na kuepuka kuandika habari zinazodanganya jamii

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya MISA nchini Tanzania Mussa Juma amesema kuwa ni vyema waandishi wa habari kuepuka uchochezi unaokinzana na maslahi ya Taifa kwani kulingana na sheria ya habari ya mwaka 2016 kosa la mwandishi ni faini ya shilingi milioni 3,na kifungo hadi miaka 3

Pia amesisitiza waandishi kujiongeza Kielimu kwani serikali ilitoa kipindi cha miaka mitano kuanzia januari 01,2017 ndipo ilipitiswa kuwa kila mwandishi wa habari kuwaanzia kiwango cha diploma ya uandishi wa habari kutoka vyuo vinavyotambulika.

Wakichangia mjadala huo, Mwenyekiti wa Arusha Press Klabu, Claud Gwandu kushirikiana na wadau kudai mabadiliko ya sheria ya huduma za habari amesema kuwa sheria hiyo ina mapungufu kadhaa, ikiwepo kutotambua kada za chini katika vyombo vya habari, ambazo hazihitaji kuwa na elimu ya diploma na pia kufanya makosa ya habari kuwa makosa ya jinai.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari cha Fanikiwa Bwana Andrea Ngobole amesema kuwa siyo kweli kwamba hawatoi elimu ya kutoshawaandishi watarajiwa katika vyuo vyao bali wanatoa sawasawa na mtaala toka Nacte ila wanapokwenda nje ya chuo wanakutana na shinikizo la muda na kiuchumi wa habari tofauti ambazo kile jamii inahitaji kusikia.

Amekubaliana hoja wadau wa mkutano huo wa kuwachukua wataalamu wa habari wenye uzoefu wa muda mrefu ili waweze kutoa mafunzo yenye uhalisia katika tasnia ya habari ili waweze kutoa taarifa zenye uhalisia wa maisha ya watu wengi.

Kwa upande wake Inspekta wa polisi Rashid Nchimbi ambae amemuwakilisha RPC Jonathan Shana amesema jeshi polisi wanaushirikiano na waandishi hivyo yapo madawati mengi ambayo wanaweza kupata habari za kipolisi kila leo wakihitaji wasikariri sehemu moja.

Pia amewashauri vyuo vya uandishi wa habari kutafuta waalimu wenye uzoefu na kazi hiyo kwaajili ya kutoa mafunzo kwani asilimia kubwa wanakauwa na uzoefu mkubwa na kazi wanayoifanya.Nae Mkurugenzi Civic and Legal Aid Organization (CiLAO)amesema kuwa wanajiandaa kufanya mkutano na wadau wa Habari, haki za binadamu, tume ya uchaguzi nchini na Tamisemi ili kuona namna Waandishi wa Habari watashiriki kwenye uchaguzi kama waangalizi wa uchaguzi.

''Tayari tumefanya utafiti kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya ambako Vyombo vya Habari vina haki ya kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia upigaji, uhesabuji wakiwa ndani kama ambavyo waangalizi wa uchaguzi walivyo na haki hiyo"alisema Odero Odero

Gasirigwa Sengiyumva ni Mkurugenzi wa MISA nchini akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa habari
Baadhi ya washiriki wa mjadala wa changamoto za vyombo vya habari na namna vinavyofanya kazi
Baadhi ya washiriki wa mjadala wa changamoto za vyombo vya habari na namna vinavyofanya kazi
Mjumbe wa bodi ya MISA nchini Tanzania Mussa Juma akifafanua juu ua sheria mpya ya habari ya mwaka 2016
Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari cha Fanikiwa Bwana Andrea Ngobole akuchangia mjadala kuhusiana na elimu kwa wanaandishi

WATU NANE WAPATA MAJERAHA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA VIGWAZA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

WATU nane wapata majeraha baada ya gari la abiria , mali ya kampuni ya Friends ikitokea Dar es salaam kuelekea Kampala nchini Uganda kupata ajali ,eneo la Kwazoka, kata ya Vigwaza, Chalinze mkoani Pwani. 

Aidha dereva wa gari hilo lenye namba za usajili, UAY 458 F aina ya Scania ,Bashiru Telu mkazi wa nchini Uganda amekimbia baada ya kutokea ajali hiyo. 

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mchana march 18,mwaka huu na kusema gari hiyo ilikuwa na abiria 42.

Alieleza, gari hiyo iliacha njia na kupinduka na kusababisha majeruhi hao ambapo chanzo cha ajali ni dereva huyo kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari. 

Wankyo aliwataja waliopata majeraha kuwa ni Kubo Zuberi (24) aliyepata jeraha katika mkono wa kulia mkazi wa Uganda ,Rudigo Benjamin (24) na Aisha Salin (34) mkazi wa Dar es salaam ameumia kichwa.

Wengine ni Theonestina Gedioni (29) mkazi wa Tabata ,Baiga Jacquie (30) mkazi wa Uganda, Nasra Amani (12) mkazi wa Dar es salaam, Farouqs Natkunda (22)mkazi wa Uganda na Hassan Omary mkazi wa Mbezi Dar es salaam. 

"Majeruhi hao walikimbizwa katika kituo cha afya Mlandizi, ambapo wanaendelea na matibabu "alifafanua Wankyo. 

Kamanda huyo alitoa rai kwa madereva wa vyombo vya moto kutii sheria za usalama barabarani. 

Vile vile wasafiri wanaotumia vyombo hivyo kuendelea kuwafichua madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani ili waweze kuchukuliwa hatua kwa kupiga namba za makamanda wa mkoa wa wakuu wa usalama barabarani.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa

Kamati ya Bunge yakagua mradi wa umeme mkoani Iringa na kupongeza Wizara ya Nishati

0
0





Na Teresia Mhagama,

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya uenyekiti wa Mariamu Ditopile Mzuzuri, imefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa iliyokuwa na lengo na kukagua kazi ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini ili kijiridhisha endapo fedha zinazoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Kamati hiyo ilikagua utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika Kijiji cha Ngano, wilayani Iringa na katika Kitongoji cha Ikuvala kilichopo wilayani Kilolo ambapo waliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga na watendaji kutoka TANESCO.

Pamoja na kukagua utekelezaji wa mradi huo, Kamati hiyo ilipata fursa ya kuwasha rasmi umeme katika Kisima cha Maji, Shule ya Msingi na Zahanati katika Kijiji cha Ngano wilayani Iringa pamoja na kuwasha umeme katika Kitongoji cha Ikuvala, wilayani Kilolo.

“ Tunaipongea Wizara kwa kuzingatia agizo la Kamati ya Bunge la kuhakikisha kuwa umeme unafika katika Taasisi za Umma na Kijamii, kwani wakati tunakagua mradi huu mwaka jana, tuliongelea suala la wigo wa wakandarasi na tuliwashauri kwamba umeme ufike katika Taasisi za kijamii ikiwemo zahanati na Shule,” alisema Mzuzuri.

Mzuzuri alisema kuwa, haitaleta maana kama Wakandarasi wa umeme wa vijijini watasambaza umeme katika makazi ya watu pekee kisa tu wako katika wigo waliopangiwa na kuacha Taasisi muhimu za kijamii hivyo aliipongeza Wizara ya Nishati kwa kuitikia agizo hilo la Kamati na kulifanyia kazi.

Aidha, Kamati hiyo ya Bunge imeipongeza Wizara ya Nishati, kwa kufanyia kazi ushauri wa kupunguza bei za umeme ambapo sasa bei ya kuunganisha umeme vijijini ni 27,000 tu, iwe kwa miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) au TANESCO.

“ Sisi kama Kamati tunapata faraja, pale tunapotoa ushauri na nyie mnaufanyia kazi, tunawatia moyo muendelee kufanya kazi kwa bidii ili mradi yale tunayoyapanga kwa pamoja yaweze kufanikiwa zaidi na zaidi,” alisema Mzuzuri.

Akitoa taarifa ya usambazaji umeme vijijini mkoani Iringa, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alisema kuwa vijiji 179 mkoani humo vimepangwa kupelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali ikiwemo wa REA III na mradi wa Backbone ambapo gharama zake ni takriban shilingi bilioni 30.

Naibu Waiziri alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa bei ya kuunganisha umeme vijijini ni shilingi 27,000 tu bila kujali kama mradi unatekelezwa na TANESCO au Wakala wa Nishati Vijijini kwani Serikali imedhamiria kurahisisha zoezi la kuwapelekea wananchi umeme.

Aidha, alilisisitiza kuhusu matumizi ya vifaa vya UMETA kwa wananchi vijijini na kuwataka wakandarasi kuhakikisha kuwa wanawapatia wananchi vifaa hivyo kwani baada ya kukamilika kwa mradi, Serikali itakagua endapo wakandarasi hao wametekeleza agizo hilo la Serikali.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme katika Kitongoji wa Ikuvala wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (katikati), akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati walipofika katika Kijiji cha Ngano wilayani Iringa kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu. Wa Pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mariamu Ditopile Mzuzuri na Wa Tatu kulia ni Kaimu Kamisha wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mariamu Ditopile Mzuzuri akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa umeme katika Kitongoji wa Ikuvala wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.

MKURUGENZI HALMASHAURI YA CHEMBA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI,ATOA AGIZO KWA WATENDAJI

0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Dkt.Semistatus   Mashimba amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya shule za msingi za Chemba ikiwemo Songoro,Mapango na Chandama na kuangalia mazingira ya shule hizo ikiwemo kukagua taaluma na miundombinu ya shule hizo pamoja na  changamoto wanazozikabili na namna ya kuzitatua,Pichani ni Mkurugenzi Dkt Mashimba akizungumza na baadhi ya Wafunzi wakati wa ziara yake.
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya chemba Dkt.Semistatus Mashimba akipata maelezo kidogo kutoka kwa mmoja wa mafundi ujenzi alipotembelea na kufanya ukaguzi wa ujenzi  unavyoendelea katika hospitali ya wilaya ya Chemba.Dkt Mashimba amefanya ziara kwenye  moja wapo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chemba hatua kwa hatua,ambapo alieleza na kutoa maagizo kwa Wakandarasi kuwa  ifikapo Machi 31/2019 majengo ya Chemba yote yawe yamefikia hatua ya renta 

JAMII IACHE KUWAFUNGIA WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI –NURU

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh amesema kuwa jamii iache kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwani watu wenye ulemavu wanaweza kufanya vitu vikubwa na kusaidia nchi katika maendeleo mbalimbali.

Nuru aliyasema hayo wakati wa hafla ya Tuzo ya I Can ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Nuru amesema Tuzo mbili alizozipata zimetokana na kuwa na mchango katika jamii licha ya kuwa na ulemavu wa kuona lakini ameweza kutumia kipaji chake na kuiletea maendeleo nchi pamoja na wananchi.

Amesema kuwa yeye angefungiwa ndani asingeweza kupata elimu na kufanya maisha yake ya ulemavu kufunga kipaji pamoja na ndoto zake ambapo leo anaongoza watu wa makundi mbalimbali na wanamuamini katika uongozi.

‘’Namshukuru Rais Dkt. John Pombe Mgufuli kwa kuteua viongozi mbalimbali wenye ulemavu katika serikali yake ni kutokana na kutambua mchango wa wenye ulemavu kushiriki katika ngazi za maamuzi na sasa kufanya walemavu kijiamini kwa kupita kifua mbele”.amesema Nuru.

Nuru amesema watu wenye ulemavu wana kipaji kikubwa huvyo jamii iache kuwafungia ndani kwa kuona hawawezi kufanya chochote katika jamii yao wanayoishi.

Aidha amesema kuwa watu wenye uleamvu kwa vijana wanaosoma wasife moyo kwa ulemavu wao wasome kwa bidii kwani elimu ndio mkombozi kwa mtu mwenye ulemavu.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongeza Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya I CAN ya Mafanikio katika Ujuzi wa Kipekee kwenye hafla ilioandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akipokea hundi ya sh.milioni mbili kutoka kwa mwakilishi wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akizungumza na Michuzi Blog wakati hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka.MMG)
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na watu wenye ulemavu mara baada ya ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Nuru Awadh akiwa katika picha ya pamoja na Familia yake katika ya utoaji wa Tuzo ya Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation iliyofanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka.MMG)

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YADHAMINI WASICHANA MKOANI LINDI KUPEWA ELIMU YA AFYA YA UZAZI

0
0
 Meneja wa Vodacom mkoa wa Lindi, Omary Kilumanga akikabidhi baadhi ya taulo za kike kwa mkuwa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga kwa ajili ya kugawa kwa wanawake wa wilaya hiyo hivi karibuni kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Sherehe hizi ziliandaliwa na taasisi ya T-Marc Tanzania chini ya mradi wa Hakuna wasichoweza unaotoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana kwa kudhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation.
Meneja wa Vodacom mkoa wa Lindi, Omary Kilumanga akikabidhi taulo za kike kwa wanawake wa Lindi hivi karibuni kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani chini ya mradi unaotekelezwa na taasisi ya T-Marc Tanzania wa Hakuna wasichoweza unaotoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana kwa udhamini wa Vodacom Tanzania Foundation. 

Julai Tanzania kuzindua mpango wa uendelezaji miji

0
0
UZINDUZI wa mpango njia wa uendelezaji wa miji nchini (urbanisation road map) unatarajiwa kufanyika Julai mwaka huu baada ya kukamilika kwa uchambuaji wa maoni kutoka kwa wadau kuhusiana na mpango huo.
Hayo yameelezwa na Dk Lorah Madete, Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa kufungua mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) katika ukumbi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Alisema wakati taifa linatekeleza mipango yake ya maendeleo kuelekea uchumi wa kati unaotegemea viwanda, ni dhahiri kwamba suala la mipango miji ni lazima kutiliwa maanani.
Alisema kwamba miji yetu inatakiwa kukua kwa utaratibu ili kulingana na mahitaji ya uchumi wa viwanda.
Alisema kwa sasa kutokana na watu kutaka maisha bora wamekuwa wakitoka vijijini na kukimbilia mjini na hivyo kuleta shinikizo katika menejimenti ya miji.
Alisema kutokana na mazingira ya sasa katika miji yetu, ushiriki wa sekta binafsi katika kuboresha  miji ni muhimu ili kukabiliana na kasi ya ukuaji wa miji.
Alitaka wataalamu wanaopitia mpango huo na kutoa maoni yao kuhakikisha kwamba wanawezesha Tanzania kuwa na miji inayokidhi mahitaji ya makazi; kwa kuwa miji iliyopangwa vyema ikifuata kanuni zote ikiwa ni pamoja kuwa na njia bora za kudhibiti uchafu, menejimenti na matumizi ya usafiri endelevu na kutumia nishati iliyo safi.
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kuanzia mwaka 2017 kwa msaada wa Wizara ya misaada ya kimataifa ya Uingereza (DFID) na kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha ya Tanzania walianzisha TUlab kwa lengo la kuangalia ukuaji wa miji endelevu, unaojali watu wake.
“Tunapoenda kwenye uchumi wa viwanda ni lazima tujiandae kwa uchipukaji na ukuaji wa miji, hivyo ni lazima tuingize mipango hiyo katika mpango huo mkubwa wa maendeleo kuelekea uchumi wa kati unaotegemea viwanda ‘Tanzania Development Vision 2025’ ” alisema Dk Madete.
Alisema wakati serikali kwa sasa inatekeleza awamu ya pili ya mpango wa maendeleo wenye lengo la kuweka msingi wa mapinduzi ya viwanda, ipo hatari kubwa kwamba Tanzania ipo katika hatari ya wananchi wake kutofaidika kiuchumi, kijamii na kimazingira kutokana na mlipuko wa ukuaji wa miji usiozingatia taratibu.
Hata hivyo alisema kwamba pamoja na kuwa na mpango wa ukuaji wa miji, mipango hiyo lazima iambatane na makubaliano ambayo taifa hili limetia saini ikiwamo Makubaliano ya Paris, Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, Ajenda Mpya ya Miji na Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063.
 Mikataba mingine ni ya Afrika Mashariki (EAC) 2050 na Jumuiya ya Ushirikiano ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC 2050.
Alisema kwamba ili kuwepo na mwenendo mzuri ni lazima wataalamu kuangalia namna ya kuendana na ukuaji wa miji ulio endelevu na salama na kujiongezea tija na ufanisi.
Alisema ni umuhimu huo ndio ulifanya Agosti 2017, Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na ESRF na taasisi ya Coalition for Urban Transitions (CUT) kuanzisha TULab ili kusaidia kuwa na mipango  madhubuti ya maendeleo ya miji.
”Hatuwezi kufanikiwa bila uhusiano mzuri wa kiutendaji na hapo ndipo TULab inapoingia kusaidia mipango endelevu ya miji kwa kuwezesha jukwaa la majadiliano jinsi ya kuiendeleza miji yetu”
Awali akimkaribisha Dk Madete, Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida alisema kwamba mkutano huo wa Saba ni muhimu kwani ndio wanaingia katika kipindi ushindani mkubwa wa kuweka sawa mawazo yatakayotumika kama ramani kuelekea miji yenye utaratibu.
Alisema tangu kuanzishwa kwa TUlab Agosti 2017, imewezesha kufanyika kwa tafiti nne zenye lengo la kuangalia ukuaji wa miji na huduma zake. Aidha tafiti nyingine zilikuwa za kuona kinachokosekana katika uendelezaji wa miji na mahusiano kati ya serikali kuu na serikali za mitaa katika utoaji wa huduma kwa miji.
Tafiti hizo na nyingine zimewezesha kutengeneza mfumo wa maendeleo ya miji ambao bado unajaziwa nyama baada ya uzinduzi wa mazungumzo uliofanywa na Naibu katibu Mkuu, Menejimenti ya uchumi wa wizara ya fedha na Mipango Dk. Khatibu M. Kazungu, mjijini Dodoma hapo Novemba 28,2018.
Pamoja na kushukuru uwapo wa mkutano huo wa saba wa majadiliano, Dk Kida pia alishukuru Wizara ya Fedha na Mipango, Coalition for Urban Transitions (CUT), World Resource Institute (WRI) na African Centre for Cities (ACC) kwa kuwezesha mkutano huo.
Alisema ni matumaini yake kwamba wataalamu watafikia muafaka wa kuwezesha taifa la Tanzania kuwa na ukuaji bora wa miji kuelekea uchumi wa viwanda na kipato cha kati.
“Naamini kwamba TULab  ni jukwaa jema na salama ambalo linaweza kujadili na kuchambua masuala ya kila siku  ya ukuaji wa miji nchini Tanzania na kuja na hoja bora zaidi ya kuwezesha ukuaji wenye kukidhi matakwa ya wakazi” alisema Dk Kida katika hotuba iliyosomwa na Bw Sango.
Alisema  pia TULab lengo lake ni kuangalia, kuchambua kwa undani juu ya sera za mipango miji na pia kuona changamoto za maendeleo na namna ya kukabiliana nayo.
 Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF).
 Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida wakati wa mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF) .
 Bw. Anton Cartwright kutoka Taasisi ya Miji ya Afrika iliyopo Afrika Kusini, akielezea kilichojiri kwenye mpango wa taifa wa uratibu wa miji wakati wa mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF).
 Bw Brent Cloete kutoka Afrika Kusini akiwasilisha utafiti unaolinganisha njia mbili za kiuchumi zilizochukuliwa na Tanzania kuelekea uchumi wa viwanda wakati wa mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF) .
 Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa maoni wakati wa mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji (TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF).
 Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Madete akitoa neno la kufunga mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF).
 Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki waliohudhuria mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF).


Mwanamuziki Joshua Meshack Ringo akitoa burudani ya wimbo wa Upendo wa Kweli alioimba Ambwene Mwasongwe wakati wa mkutano wa saba wa Maabara ya Mipango Miji ( TULab) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Jamii na Uchumi (ESRF).

Rais wa Zanzibar Dk.Shein Azungumza na Executive Coordinotor wa Program ya Kujitolea ya "United Nations Volunteers"

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mratibu Mkuu wa Program ya Kujitolea ya "United Nations Volunteers " (UNV) Bw,Oliver Adam kushoto,alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo 19-3-2019.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mratibu Mkuu wa Programu ya Kujitolea ya (UNV) " United Nations Volunteers "Bw.Oliver Adam, kushoto akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar  leo kwa mazungumzo leo 19-3-2019.(Picha na Ikulu)
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images