Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 279 | 280 | (Page 281) | 282 | 283 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Timu ya Taifa, kilimanjaro Stars Leo imecheza mechi yake ya kwanza ya CECAFA Challenge Cup  na timu ya Taifa ya Zambia katika mji wa Machakos, ambao uko takriban kilometa 60 kutoka Nairobi. Timu hizo zimefungana 1-1. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua sana, Katika mechi iliyotangulia ambayo iliwakutanisha Burundi NA Somalia, Burundi iliwafunga Somalia goli 2. Yafuatayo ni matukio katika picha
   Hapa vijana wetu wakiwa katika Picha ya Pamoja Kabla ya kwanza kwa kipindi cha kwanza
   Bwana shiyo Pamoja na Gavana wa Machakos wakiwasalimia wachezaji.
   Mtanange ukiendelea uwanja wa Machakos.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  WAAFRIKA wametakiwa kukataa utumwa na kuiga neno la ‘WOOD’, kwenye soko la filamu hasa baada ya nchi nyingi kukopi jina la ‘HOLLYWOOD’ ambalo ni eneo lililopata umaarufu mkubwa kwenye soko la filamu Duniani kwa kuwa na wasanii nyota na studio za kisasa, za masuala ya filamu. 
  Akielezea mapema leo kwenye semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu za Kiafrika la Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia, kilichopo Pensylvania, Marekani , Mr. Akpor Otebele, alisema Waafrika waache dhana ya kuendelea kutumia jina hilo ambalo nchi nyingi wamekuwa wakitumia viunganishi vya neon hilo la ‘Wood’ bila kujua maana hasa la kuendelea kulitumia. 
  Hii haina maana, ni la kuliacha na Nigeria kule waigizaji wengi wanatafakari maana ya hili neno lakini jibu hakuna, lakini bado wanaendelea kulitumia” alisema. Akitolea mfano wa baadhi ya nchi zinazotumia jina hilo kutoka Hollywood, ni pamoja na : Bongowood/ Swahiliwood (Tanzania), Nollywood (Nigeria), Riverwood (Kenya), Ghollywood (Ghana), SierraWood (Sierra Leone)na Congowood (Kongo) na mengine mengi. 
  Akpor Otebele aliongeza kuwa, kuendelea kutumia viunganishi hivyo ni kuwanufaisha watu wa Magharibi na kuupamba Mji wa Hollywood unaoishi mastaa na studio maalufu huko Lose Angels nchini Marekani, ambapo kwa dhana hii inafanya Waafrika kuwa watu wasiojua wanachokifanya. …”Swahiliwood, its means, Swahili ubao? Is that sure? So why to use ‘Wood’?? in Swahili meaning ‘UBAO’?? Alisema Akpor Otebele.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia, kilichopo Pensylvania, Marekani Bw.  Akpor Otebele, akiongea kwenye semina hiyo jijini Arusha leo 
  Juu na chini ni washiriki wa semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, iliyoandaliwa na Tamasha la Filamu za Kiafrika la  Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013)


  0 0

   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 'akitoa dozi' alipohutubia katika mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo.
   Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano uliofanyika  Uanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma,leo
   Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye mkutano huo wa hadhara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye aliwakonga nyoyo wakazi wa eneo hilo wakiwemo wapinzani kwa kusema kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia viongozi wanaoshindwa kutatua kero za wananchi,waliojawa na umangimeza na urasimu.


  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  MAXCOM Africa intends to create 20,000 job opportunities and increase the quality of life in 20,000 homesteads by December 2015. While presenting a paper titled ‘Innovative use of technology in changing local challenges into opportunities for development using the MaxMalipo Experience’, Ahmed Lussasi, the company’s Chief Operations Officer said the beneficiaries would be both individuals and group entrepreneurs.

  Lussasi said his company has since inception in 2010 created 85 direct employments and 6,000 indirect job opportunities thus impacting the lives of 6,000 homesteads country wide.

  He was speaking in Dar es Salaam during the recently concluded first season of ‘Fursa Campaign’ where he reiterated his company’s commitment to help the government achieve the 2015 Millennium Development Goals.

  As a huge beneficiary of the Dar Technohama Business Incubator (DTBi), Maxcom Africa, trading as MaxMalipo is credited with bringing a durable solution in the distribution of prepaid electricity services TANESCO Luku countrywide as well as bringing electronic payment services closer to the people.

  Lussasi said his company has already partnered with the Kinondoni Municipal Council in the collection of local government levies, a project that would employ over 200 youth.

  The most recent achievement by MaxMalipo is the partnership with TEMESA in the provision of electronic ticketing services for the Magongoni – Kigamboni Ferry. The company has also been trusted with the distribution of the second phase TRA approved EFDs but also with the collection of road license levies by TRA.

  Lussasi notes: “We have developed a strong and trusted electronic payment platform that enhances peoples lifestyles. We are proud to have worked with both the government and private companies especially in projects that effectively improve quality of live among Tanzanians.”

  And continued: “We are working closely with the parliamentary committees regarding the use of electronic payment platforms in improving revenue collections in ministries and government corporations.

  HE President Jakaya Kikwete pose for a group with local entrepreneurs during the climax of the first edition of Fursa Campaign in Dar es Salaam. The president reiterated on the government’s commitment to support youth economic initiatives saying ‘I Trust In The Youth’ as engineers of economic development.

  A section of entrepreneurs that turned up in a packed Diamond Jubilee Hall during the climax of the first edition of Fursa Campaign in Dar es Salaam.

  0 0

  TAHADHARI:- KUNA TAPELI MWENYE ASILI YA KIZUNGU ANADAI YEYE NI RAIA WA AFRICA KUSINI. Ni  MREFU, ANAONEKANA SANA MITAA YA KINONDONI KWA MANYANYA JIJINI DAR MIDA YA USIKU. AMETAPELI WATU WENGI SANA AKIDAI KUA AMEIBIWA HOTELINI NA MWANAMKE NA ANADAI ANAISHI MBEZI KIMARA. KWA WENYEJI WENGI WA KINONDONI WANAMFAHAMU NA WENGI WAMESHAMSIKIA NA WANADAI NI MSWAHILI. CHUKUENI TAHADHARI NA TUKO KWENYE HARAKATI ZA KUMKAMATA KWA SABABU AMESHA TAPELI WENGI AKIJIFANYA KUCHUKUA NAMBA ZA SIMU KWA AJILI YA KUREJESHA FEDHA HIZO TUNAOMBA WENYE TARIFAA ZAIDI WATUSAIDIE KWA USHIRIKIANO NA POLISI KUMTIA MBARONI IMETOLEWA NA MMOJA YA WALIOLIZWA  

  0 0
 • 11/28/13--23:23: Article 22


 • 0 0

  WABUNGE WA MUUNGANO AMBAO WAKO ZIARANI UK WALIPATA FURSA YA KUTEMBELEA OFISI ZA WAZEE WA KAZI SERENGETI, KAMPUNI AMBAYO INAMILIKIWA NA WATANZANIA WAISHIO UK. PAMOJA NA MENGI WALIYOYAONA OFISINI HAPO, PIA WALIWEZA KUSHUDIA JINSI UKAGUZI WA MAGARI UNAVYOFANYIKA KWA KUTUMIA MASHINE ZA KISASA.
  MSAFARA HUO WA WABUNGE KUMI ULIONGOZWA NA MHESHIMIWA HAMIS KIGWANGALLA AMBAYE MBUNGE WA NZEGA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA SERIKALI ZA MITAA.
  KATIKA TUKIO AMBALO LILIVUTIA WENGI NI PALE MBUNGE WA SERENGETI MHSEHIMIWA DR KEBWE ALIPOSEMA ANAJISIKIA YUKO JIMBONI KWAKE NA KUFURAHI SANA KUONA JINA LA SERENGETI LINAVUMA KILA KONA ZA UK. WABUNGE WALIFURAHISHWA KUONA JINSI VIJANA WA KITANZANIA WALIVYOWEZA KUJITENGENEZEA AJIRA WENYEWE WAKIWA UGENINI
  Mbunge wa Serengeti akiwa na Wazee wa kazi
  Wazee wa Kazi wakiwa na Mhe Hamisi Kigwangala
  Waheshimiwa wakiangalia gari linavyokaguliwa kitaalamu kabla ya kusafirishwa kwenda Afrika Mashariki
  Waheshimiwa wakiwa na Wazee wa Kazi
  Waheshimiwa wakiangalia ukaguzi wa gari linalokaribia kusafirishwa kwenda Afrika Mashariki
   


  0 0

  spsl-1
  Seattle Stars FC players wear their SPSL Champions t-shirts after a 1:0 win over Pars Lions FC earned them the crown Sunday night at Starfire. (Club photo)
  Stars head coach Alex Kajumulo with the SPSL trophy. (club photo)
  Stars head coach Alex Kajumulo with the SPSL trophy. (club photo)

  0 0

  Hello  Kaka  Michuzi.Pole sana na kazi mjomba...mimi ni mdau wa hapa  MO,ST LOUIS......USA.Naomba  unisaidie kupost hii message ubaoni.
  I just drove here  few days  ago from  CA.Naomba unisaidie kupost  nahitaji kuwajua watanzania  wowote waishio  ST LOUIS-MO.
  Anyone  interested for  chit chat please  inbox me my E-mail: colleenfra06@gmail.com.
  Thank  you  very much
   
  Mdau Collen

  0 0
 • 11/28/13--23:41: Article 18
 • Upinzani wa dancing uliodumu tangia miaka ya 90 kati ya Athumani Diga Diga vs Bosco Cool J nani zaidi? Ufumbuzi kupatikana jumamosi hii ndani ya isumba lounge jollies club


  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Morogoro. Waziri Nchimbi aliwasikiliza maoni yao pamoja na maswali ambayo yalilenga kuimarisha chama chao mkoani humo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (Watatu kulia-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Morogoro. Waziri Nchimbi aliyasikiliza maoni pamoja na maswali yao ambayo yalilenga kuimarisha chama chao mkoani humo. Kikao cha kuimarisha chama chao kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro. Picha zote na Felix Mwagara.


  0 0


   Pichani kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,mara baada ya kuwasili mapema leo asubuhi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya..Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko ziarani mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM,kusikiliza kero za Wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
  Pichani kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro akisalimiana na Katibu wa NEC,Siasa  na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.Rose Migiro akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,mara baada ya kuwasili mapema leo asubuhi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya..Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko ziarani mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM,kusikiliza kero za Wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi.

  Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mbozi mapema leo asubuhi,ndani ya ofisi za CCM Wilaya ya Mbozi,mkoani Mbeya.

  Pichani ni baadhi ya Wanachama wa CCM na Wananchi wakiupokea ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipowasili mapema leo asubuhi kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko ziarani mkoani Mbeya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM,kusikiliza kero za Wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi.

  0 0

  Benki ya NMB inazidi kuwa karibu yako na sasa inakuletea akaunti mpya inayoitwa NMB Business Account Plus maalum kwa ajili ya wafanyabiashara.

  NMB Business Account Plus ni akaunti inayoruhusu kutumia kadi ya ATM katika mashine za ATM zaidi ya 500 nchi nzima, kumwezesha mteja kupata huduma ya ‘overdraft’ kusaidia biashara yake kwenda vizuri, ina gharama nafuu za uendeshaji, inamwezesha kupata statimenti ya bure ya kila mwezi, kufungua akaunti kwa kiwango nafuu na aweze kupata huduma ya hundi inayotambulika na benki nyingine.

  Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Mwanza, Mkuu wa kitengo cha Bishara wa NMB, Filbert Mponzi alisema “NMB imekopesha wajasiriliamali zaidi ya 55,000 kupitia matawi yake zaidi ya 150 yaliotapakaa nchi nzima. hivyo basi, uzinduzi wa akaunti ya NMB Business Account Plus utawawezesha wafanyabiashara kutumia kadi za ATM, vitabu cha hundi pamoja na kufurahia huduma za NMB mobile”

  Ili kufaidika na akaunti hii mpya kutoka NMB. Fungua NMB Business akaunti Plus leo.

  Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Waziri Barnabas wakipeana mkono na mwenyekiti wa kituo cha biashara Mwanza (NMB Business Club) baada ya uzinduzi wa NMB Business Account Plus. wakishuhudia kutoka kulia ni Mkuu wa kitengo cha Bishara wa NMB, Filbert Mponzi na Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Straton Chilongola

  Sehemu ya wafanyakazi wa NMB waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika kituo cha Biashara Mwanza (NMB Business Center) wakiwa katika picha ya pamoja.

  Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akimweleza jambo Meneja kituo cha biashara Mwanza (NMB Business Center), Mike Grata wakati wa uzinduzi wa NMB Business Account Plus

  Sehemu ya wateja wa NMB waliohudhuria uzinduzi huo

  0 0

  MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili nchini Kenya, Anastazia Mukabwa, aliyethibitisha kuwa miongoni mwa watakaotumbuiza katika Tamasha la Krismasi litakalorindima Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu, pia katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.

  Tamasha hilo la Krismasi limepangwa kusheheni waimbaji kochokocho wa nyimbo za Injili, miongoni mwao akiwamo mwimbaji huyo galacha wa nyimbo za Injili, Mukabwa.

  Mukabwa anatoa mwito kwa watu kujitokeza kwa wingi ili 'wavue viatu' siku hiyo aliyopania kukonga nyoyo za mashabiki atakapopanda jukwaani katika tamasha hilo. Kulingana na taarifa yake iliyotolewa na waandaaji wa tamasha hilo, msanii huyo amepanga kuwapa mashabiki raha na kuwataka wake mkao wa kula wakisubiri vitu vyake.

  “Nimejipanga, najua mashabiki wa Tanzania wanataka kitu gani, nitawapa raha, mambo ya Kuvua Viatu watayasikia na mengine, watafurahi sana. “Kwa vile Rose (Muhando) atakuwepo, nitashirikiana kwenye wimbo huo na nyimbo zangu mpya nitazitoa huko kwa mara ya kwanza, ni mambo mazuri yatakuwepo,” alitamba.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama alisema Mukabwa aliyeimba kwa kumshirikisha mwimbaji nguli wa Tanzania, Rose Muhando katika wimbo wa Vua Kiatu, ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Imelda Ishuza ( kulia) akipokea cheti ya kuhitimu matunzo toka kwa RC Moro, Joel Bendera.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ( kulia) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo Mkuu wa Wilaya ya Makete, Josephine Matiro.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Norman Sigalla.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (aliyesimama) akitoa hutuba ya kufunga mafunzo ya Utaalamu wa kilimo cha mazao ya matunda, mboga na mauwa , mjini Morogoro.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera ( wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo ya utaalamu wa kilimo cha mazao ya ' Horticulture' mjini Morogoro, wakiwemo pia Wakuu wa Wilaya.

  Na John Nditi, Morogoro

  TAASISI  Kilele ya Mazao ya Matunda, Mboga na Maua ‘ Horticulture’( TAHA),imewapatia  mafunzo Wakuu wa Wilaya na Wataalamu wa kilimo  wa  Mikoa ya Kanda ya Kati, Mashariki na Nyanda za Juu kusini juu ya  mbinu bora na sahihi za  kuboresha na kuendeleza kilimo cha mazao hayo ili kuongeza uzalishaji , kukuza soko la ndani na nje ili kuinua uchumi wa taifa.

  Maneja wa Ufundi wa TAHA, Isack Ndamanyere, alisema hayo  Novemba  21, mwaka huu  mjini hapa , kabla ya kukaribishwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, kufunga mafuzo  ya nadharia na vitendo yaliyochukua muda wa  tatu ambayo  yalindaliwa na Taasisi hiyo na kuwashirikisha washiriki 25.


  0 0

  WAZIRI wa Viwanda Biashara ambaye pia ndio mbunge wa Handeni, Dkt Abdallah Kigoda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Utamaduni, lililopangwa kufanyika Katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.

  Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani hapa, huku likitarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayoendelea kushika kasi, ambapo kwenye uwanja huo, Tamasha hilo litaanza saa 2 asubuhi hadi saa 12 za jioni.

  Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema maandalizi yamezidi kushika kasi kwa kuangalia mazoezi ya vikundi kadhaa vitakavyotoa burudani katika tukio hilo.

  “Tunashukuru Mungu kuona mambo yanazidi kuwa mazuri kwa kuhakikisha kuwa Desemba 14 mwaka huu tunafanya tamasha lenye mguso na kila mmoja wetu kufaidishwa.

  “Huu ni wakati wa kila mtu kujipanga ili aje kushiriki kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa juhudi hizi zote zipo kwa ajili ya kujenga ushirikiano kwa watu wote,” alisema Mbwana.

  Wadhamini katika tamasha hilo ni pamoja na gazeti la Mwananchi, Clouds Media Group, ni Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog, Pamoja Pure Blog na Taifa Letu.com.

  0 0
 • 11/29/13--10:02: KUMBUKUMBU
 • Marehemu KANAEL NTALIMA
  LEO Tarehe 29 NOVEMBER 2013 Ni miaka 25 kamili tangu mungu alipokuchukua Mama yetu Mpendwa,tunakukumbuka sana Mama yetu na mungu akurehemu.

  Unakumbukwa sana na wanao GEORGE, PRICILLA NA MATTY. Wakwe zako wote na wajukuu wote, mungu ametoa na mungu ametwaa jinalake lihimidiwe...

  AMEENA.

  0 0

  Na Richard Bagolele

  Serikali Wilayani Chato imesema haitavumulia vitendo vya imani potofu hasa zile za kishirikina zinazoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hii.

  Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo ameyasema hayo leo wakati akihutubia kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo. 

  Mhe. Mpongolo amesema matukio mengi yanayotokea katika Wilaya ya Chato hasa yale ya kishirikina kama mauaji ya vikongwe na mauaji mengine kwa imani potofu yanatokana na jamii kutokuwa na elimu na kuendekeza imani potofu “haya matukio ya mauaji ya vikongwe tunayoyashuhudia katika wilaya hii ni kwa sababu ya jamii kutokuwa na elimu, ni wajibu wetu kuwaelimisha wananchi” amesesisitiza Mkuu wa Wilaya.

  Amelitaka Baraza la Madiwani kushirikiana na wataalamu kutoa elimu kwa Jamii ya wananchi kupeleka watoto shule kwa hiari.

  Amesema kutokana na taarifa za Mkoa wa Geita kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefanya ziara hivi karibuni zinaonyesha kwa Mkoani Geita kuna mdondoko mkubwa wa wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza na kumaliza darasa la saba,  hata mtihani wa kumaliza kidato cha nne katika wilaya ya Chato zaidi ya wananfunzi 1000 hawakufanya mtihani huo na kusema jambo hilo si la kuvumiliwa na kila mtu lazima atimize wajibu wake.

  Kutokana na tatizo hilo Mkuu wa Wilaya ameitaka Halmashauri hiyo kutunga sheria ndogo ambazo zitasimamia masuala ya elimu  Wilayani hapa.

  Kwa mujibu wa Taarifa ya  mkoa wa Geita kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefanya ziara hivi karibuni watoto  walioandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka 2007 ni 52355 na waliofanya mtihani mwaka huu ni 30367 ambao hakumaliza shule wakiwa 21988 hali iliyomshtua sana Mhe. Rais.

  Kutokana na Taarifa hiyo Mkuu wa Wilaya amewaomba viongozi wote, wazazi na walimu kushirikiana katika kuhakikisha wanafunzi wote wanaoandikishwa kuanza darasa la kwanza wanamaliza darasa la saba na wale wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanamaliza kidato cha nne.

  0 0

   MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA KUUNGANA NA RAIS MUSTAAFU ALI HASSAN MWINYI SHEREHE YA UHURU CALIFORNIA
   tiketi zinapatikana online au Piga simu kwa Dj Luke 301 661 6696,  Dj Seif  202 286 6595 na Baraka Daudi 301 792 8562 
  Hawa ndio watakaopendezesha Uhuru  Bar
  Kristina                             Sonia                                        Nina
  Uhuru Red Carpet

  VIJIMAMBO Blog inakuletea TANZANIA UHURU NIGHT siku ya Jumamosi December 7, 2013 Ukumbi wa THE FRIENDSHIP CENTER, 9055C Maier road, Laurel, MD 20723 Balozi Mhe. Liberata Mulamula atakuwa mgeni rasmi
  Ni usiku wa Uhuru wa Tanzania, kula, kunywa mpaka unasaza kwa $60 tu na muziki ni mpaka asubuhi nunua tiketi yako mapema nafasi za kukaa ni watu 200 tu na 
  Mimi ni mtanzania, natoka Tanzania, nchi yangu Tanzania, MIAKA 52 ya UHURU wa TANZANIA.
  TANZANIA UHURU NIGHT Itaanza saa 12 jioni (6pm) kwa COCKTAIL

  Tega sikio tutazidi kuwajuza mambo mazuri yakayojiri siku hii ya Tanzania Uhuru Night


  ALL YOU CAN EAT AND DRINK ALL NIGHT FOR $60 ONLY

  KARIBUNI WOTE

  0 0

  Mmoja wa machifu wa Kisukuma eneo la Bariadi ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki Andrew Chenge akimvika vazi la kijadi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kumpa uchifu Rais Kikwete iliyofanyika mjini Bariadi,Mkoa mpya wa Simiyu leo.Rais Kikwete alipewa jina la kisukuma la Chifu Ng’humbu Banhu lenye maana ya Anayekumbuka na kuthamini Watu.

older | 1 | .... | 279 | 280 | (Page 281) | 282 | 283 | .... | 3278 | newer