Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WALIPA KODI TUMIENI MFUMO WA TEKNOLOJIA YA MTANDAO KULIPA KODI-TRA

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha.

Mamlaka ya Mapato nchini TRA imewataka wafanyabiashara wakubwa mkoani Arusha, kutumia teknolojia za kisasa kwa mtandao kwaajili ya kulipa kodi zao ili kuongeza uwazi na kutunza kumbukumbu zao. 

Wito huo umetolewa na Kaimu Kamishna wa Idara ya walipakodi wakubwa wa TRA, Yeremiah Mbaghi katika warsha ya walipa kodi wakubwa juu ya mifumo ya kulipa kodi na sheria na kanuni mbali mbali za kodi ambazo zimepitishwa na serikali.

Amesema kuwa Matumizi ya mtandao katika malipo ya kodi, yanarahisisha ulipaji wa kodi na yanapunguza gharama kwa wafanyabiashara hao kwenda ofisi ya TRA."TRA imefanya maboresho makubwa katika mfumo wake wa kulipa kodi kupitia mtandao na tumeongeza ufanisi katika utunzaji wa kumbukumbu za kodi ya zuio kwani sasa malipo yote ya kodi zuio hungia moja kwa moja kwenye akaunti ya mlipakodi husika"alisema

Amewataka walipa kodi hao kuzingatia sheria ya fedha ya mwaka 2018 na maboresho ya kanuni, ikiwepo kuwasilisa taarifa za miamala baina yake na washirika kwa kamishna mkuu pale anapowasilisha ritani ya mapato kwa mwaka.

Akifungua warsha hiyo, Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Mrisho, Gambo, amesema serikali mkoani Arusha, itaendelea ushirikiana na TRA na walipa kodi ili kuhakikisha mapato ya serikali yanaimarika.

Amesema upatikanaji wa mapato yataiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendelo ambapo serikali ya awamu ya tano imejikita katika kutekeleza miradi endelevu katika kutatua kero za wananchi,kubadili mfumo wa uchumi na kuwa wa kati kwa kukuza sekta ya viwanda.

"kodi ambazo zinalipwa pia zinasaidia sana katika miradi ya huduma za kijamii, maji, barabara, umeme pembejeo na kupatikana huduma bora za afya"alisema.Hata hivyo, amesema kuwa serikali itaendelea kujenga mazingira bora ya biashara nchini, ili kuhakikisha wafanyabiashara wananufaika, serikali inapata kodi na wananchi wanapata mahitaji yao.

Mfanyabiashara Peter Minja alipongeza TRA kuanza kuwatembelea na kutoa elimu juu ya sheria mpya zilizopitishwa na serikali lakini pia juu ya mifumo sahihi ya malipo ya kodi, ikiwepo kodi za mabango.

INTRODUCING BRAND NEW RELEASE #YAMOTOBAND THE SOUL - "BWEGE"

SPIKA WA BUNGE AIPONGEZA TIMU YA SIMBA KWA USHINDI

UVCCM Dar, yazindua kwa kishindo Dar ya Kijani

$
0
0
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, akizungumza kwenye uzinduzi wa Dar es Salaamya Kijani. Hlafa hiyo ilifanyika Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), na kuhudhuhuriwa na vijana wote wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala (kushoto), akiwa na mgeni rasmi katika uzinduzi wa Dar es Salaam ya Kijani, Katibu Mkuu wa UVCCM Mwal. Raymond Mwangwala (kulia).
Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala (kushoto), akiwa na mgeni rasmi katika uzinduzi wa Dar es Salaam ya Kijani, Katibu Mkuu wa UVCCM Mwal. Raymond Mwangwala (kulia). 

Baadhi ya Vijana wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa Dar es Salaam ya Kijani 

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, umezindua kampeni ya ‘Dar es Salaam ya Kijani’ ikiwa na lengo la kurudisha mitaa na majimbo yaliyokwenda upinzani.

Kampeni hiyo inalenga kuweka mikakati kwa kuanzia ngazi za jumuiya zote za mkoa huo, kuanza kujipanga kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa kampeni hiyo itachochea ustawi zaidi wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuzidi kukita mizizi katika ngazi zote kuanzia mkoa hadi majimbo, wilaya hadi kata, na matawi hadi mitaa.

“Leo tunazindua kampeni yetu ya “Dar es Salaam ya Kijani kuelekea serikali za mitaa 2019”, kampeni kabambe kwa ajili ya kuirejeshea CCM mitaa iliyopotea katika uchaguzi uliopita ambayo kwayo itatusaidia kupata ushindi mkubwa kimkoa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 wa udiwani, ubunge na urais.

“Sote tu-mashuhuda kwamba katika uchaguzi uliopita wa 2014 wa Serikali za Mitaa na ule Mkuu wa 2015 tulipoteza baadhi ya mitaa, kata na majimbo yaliyokuwa yakishikiliwa na CCM.

“Na sababu za kupoteza huko zinajulikana, sina haja ya kuzirejea sasa. Hivyo sisi vijana wa CCM tunatambua kuwa ndiyo damu na roho ya chama chetu, na kwamba tunao wajibu wa asili wa kusafisha njia katika kutimiza malengo ya uwepo wa vyama vya siasa kikatiba ya kushika dola,” amesema Kilakala

Mwenyekiti huyo wa UVCCM, amesema kuwa CCM inahitaji ushindi mkubwa kwa kuweka mikakati ya awali kwa kuwahusisha wanachama wa chama hicho wa ngazi zote.

“Kampeni yetu hii itashuka katika wilaya, kata na matawi yote katika Mkoa wetu ili kuwa na ufahamu wa pamoja na kuhakikisha kila Kijana wa UVCCM anawajibika ipasavyo kuhakikisha falsafa ya Dar es Salaam ya kijani yaani Dar es Salaam ya CCM inaenea kwa wanachama na wananchi ili ikifika wakati wa uchaguzi tuvune wapiga kura wa kutosha.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitatoa pongezi zangu za dhati kwa niaba ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais Dk. John Magufuli kwa kutuongoza vyema kupitia Serikali yetu ya CCM katika jukumu la kutatua changamoto za watanzania na kuwaletea maendeleo.

“Tumejionea dhahiri shahiri namna yale yaliyochelewa yakiwahishwa, yaliyoshindikana yakiwezekana, magumu yakiwa mepesi, yaliyokwama yakikwamuliwa,”amesema Kilakala

Kwa upande wake mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa UVCCM, Mwal. Raymond Mwangwala, amesema ameridhishwa na kasi kubwa inayofanywa na vijana wa Dar es Salaam ya kuhakikisha chama kinapata heshima katika chaguzi zote.

“Leo ninachokiona hapa, hii ndiyo UVCCM ninayoijua na sina shaka na uongozi wa mkoa kwani unafanyakazi kubwa na nzuri, ninachoweza kusema kwenu ninawaomba sana vijana tukilinde chama na kuhakikisha tunapata ushindi katika chaguzi zote. “Na ikiwezekana si waachieni (upinzani) asimilia mbili tu ya mitaa na pindi ikibidi hata hakikisheni tunachukua asilimia yote 100. Vijana tushikamane na tulinde heshima ya chama chetu,” amesema Mwal. Mwangwala

ATCL YAFUNGUA OFISI ZAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakichukua mkasi tayari kwa uzinduzi.
Spika wa Bunge Job Ndugai na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakiwa tayari wamekata utepe kuzindua ofisi za ATCL jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Job Ndugai (kushoto) akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele wakichukua mkasi tayari kwa uzinduzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akisalimiana na mmoja wa wahudumu wa ofisi hiyo ya ATCL jijini Dodoma. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa ofisi za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) jijini Dodoma leo. Baada ya maboresho makubwa ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege mpya za kisasa na kuongeza wigo wa safari zake, ATCL imeamua kufungua ofisi zake jijini humo badala ya kuendelea kutumia mawakala pekee.
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewataka wabunge, Maofisa wa Serikali, wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia huduma za ATCL popote zilipo ndani na nje ya nchi ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kufufua na kulijengea uwezo shirika hilo.

Akifungua ofisi ya ATCL mkoani hapa, Ndugai alisema Watanzania wote kwa ujumla wao wakiwemo wanatakiwa kutumia huduma za ndege hizo ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kuinua usafiri wa shirika hilo ambalo asilimia 100 ni mali ya Tanzania.

Alisema kwa kutumia usafiri ATCL wa ndani na nje ya nchi na katika nchi mbalimbali inakofika, ni uzalendo ambao hata mashirika ya ndege ya nje yanafanya hivyo, isipokuwa inapokuwa kuna sababu maalumu zinazochangia kutotumia usafiri huo.

Ndugai alitoa rai kwa mawakala 300 wa shirika hilo waliosambaa ndani na nje ya nchi, kuzitangaza huduma nzuri na bora za ATCL popote zinapotolewa na kuzionesha kwamba ni za ubora wa hali ya juu na za daraja la juu. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akizungumza katika hafla hiyo na kuwataka watendaji wa shirika hilo kuendelea kupanua na kuboresha huduma za usafiri wa ndani na nje ili kushinda katika soko la usafiri wa anga katika maeneo hayo.

Aliwatoa hofu Watanzania na akawataka waendelee kutumia huduma za ATCL kutokana na mkakati wa kutunza rekodi za usalama wa anga kwani huduma za shirika hizo ni za kiwango cha juu.
Baadhi ya watumishi wa ATCL na wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo wa ofisi za ATCL jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard M. Mayongela akizungumzia huduma za ATCL katika viwanja mbalimbali nchini. 
Mmiliki wa Kiwanda Mvinyo cha Alko Vintage cha jijini Dodoma, Archard Kato akionesha bidhaa za kiwanda chake ambazo zinapatikana katika Ndege za ATCL jambo ambalo linachangia ukuaji wa soko la zabibu jijini Dodoma.

BUNGE LATOA TAMKO KUFUATIA KAULI ZILIZOTOLEWA NA MBUNGE LIJUALIKALI

MASHINA YENYE BENDERA YA CUF ZANZIBAR YAANZA KUBADILISHWA RANGI NA KUPAKWA YA ACT-WAZALENDO

$
0
0


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MOTO umewaka CUF!Ndio maneno unayoweza kuelezea mgogoro unaondelea ndani ya Chama cha Wananchi(CUF) ambapo imefikia hatua ya kufuta rangi ya chama hicho katika vijiwe vya matawi na kupaka rangi ya ACT-Wazalendo.

Kufutwa kwa rangi ya CUF kwenye mashina hayo kuna baada ya Mahakama kutoa uamuzi unamtambua Profesa Ibrahim Lupumba kama Mwenyekiti halali wa Chama hicho.

Baadhi ya mashina ya CUF ambayo yameonekana yakifutwa ni yale yaliyokuwa visiwani Pemba katika tawi la Jows Corner Stone Town ambapo baadhi ya wanachama wameamua kufuta rangi ya CUF na kukapa rangi ya bendera ya ACT-Wazalendo.

Hata hivyo inaelezwa kuna tetesi zinazodai huenda Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akahamia Chama cha ACT-Wazalendo ambacho kiongozi wake ni Mbunge Kigoma Mjini Zitto Kabwe.

Michuzi Blog itaendelea kukupa taarifa zaidi ya kinachoendelea ndani ya CUF kwa sasa...

Benki ya Exim yaandaa hafla ya chakula cha jioni kwa wateja wake Tanga.

$
0
0
Tanga; March 18th, 2019: Benki ya Exim mwishoni mwa wiki iliandaa chakula maalum kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga ili kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika jiji hilo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu alisema kupitia hafla hiyo  walilenga pia  kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.
“Pamoja na kushukuru kwa namna ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio ya kuikuaji na ubora wa huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia kufahamiana wao kwa wao na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema Matundu.
Alisema ukuaji wa benki hiyo unaoshuhudiwa kwasasa ni matokeo ya ushirikiano baina yake na wateja wake ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani kubwa kwa benki hiyo hali ambayo imekuwa ikiiwezesha benki hiyo kubuni huduma bora na rafiki za kibenki ili kulinda na kurejesha imani hiyo kwa wateja wa benki hiyo.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 benki hiyo imezidi kujitanua ndani na nje ya nchi ambapo hivi karibuni ilionesha nia na utayari wa kuinunua  rasmi benki ya UBL Tanzania Limited (UBTL) kwa asilimia 100 baada ya kusainishana barua ya kuonesha nia (Letter of Intent).
“Kwa muda wote wa uwepo wake ndani na nje ya nchi benki ya Exim imekuwa ikijipambanua kwa ubora wa huduma ikilenga kujenga thamani ya uwekezaji kwa wadau wake  na kufikia ukuaji wake kwa kutoa huduma kwa upekee na iliyoboreshwa. Haya yote yamekuwa yakifanikiwa kwa urahisi sababu utekelezaji wake umekuwa ni jumuishi kwa kuwa unahusisha wadau wote kwa majadiliano na wateja wetu kama hivi,’’ alisema.
 Pamoja na mambo mengine hafla hiyo ilipambwa na shuhuda mbalimbali kuhusu ubora wa huduma za benki hiyo kutoka kwa wateja mbalimbali wa benki hiyo.
Meneja Uendeshaji wa Benki ya Exim Bi Doreen Mcharo (katikati)  akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo  wakati wa tafrija ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki yaExim  kwa ajili ya wateja wake wa jiji la Tanga  iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.

Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani)  wakati wa tafrija ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki yaExim  kwa ajili ya wateja wake wa jiji la Tanga  iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Mmoja wa wateja wa benki ya Exim Tanzania jijini Tanga Bi Anna Saimo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wateja wa benki ya Exim Tanzania jijini Tanga Bw Sifaeli Mafunga  akizungumza kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa banki  ya Exim tawi la Tanga pamoja na Naibu Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim Bw Jaffari Matundu, kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.

Welcome to Ngorongoro Race 2019 - Half Marathon, Karatu Arusha.

$
0
0
Welcome to Ngorongoro Race 2019 - Half Marathon, Karatu Arusha. 

20th April 2019, Register Now, Online through M-Pesa ; 0754 82 13 80 (Meta Petro Bare ) .

TICKETS :
Will be Sold from 16 March - 15 April, 2019 at |Sheikh Amri Abeid Arusha Grounds |Gidabuday Sports Foundation Office,Namvua Plaza @gidabudaysfoundation | Karatu Ngorongoro race Office. .
.
√ 21 K (20,000/= Tshs) | √ 5 K (10,000/=Tshs) | √ 2.5K (5,000/=Tshs). " The Race Against Poaching 
".

DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Tanki la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi Lita 150,000 kwa siku katika Mtaa wa Kichangani Majohe Jijini Dar es Salaam.

Akiweka jiwe la Msingi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Katibu Tawala DAS Sheila Edward amesema kuwa mradi huu utawasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kuwapunguzia kero ya maji waliyonayo kwa muda mrefu.

Amesema, serikai inaendelea kutekeleza ahadi za serikali ya mapinduzi ili kufikia malengo ya kumtua mama ndoo kichwani na wamekuwa wanashirikiana na madiwani kwani marndeleo hayana chama.

DAS amesema, Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa maji Mtaa wa Kichangani Majohe utasaidia wananchi takribani laki saba (700,000) na amezitaka mamlaka husika kusimamia mradi huo pindi utakapomalizika ili uweze kujiendeleza.

Kaimu Mkurugenzi Wa Manispaa ya Ilala Mhandisi Upendo Lugongo amesema kuwa mradi huo wa maji umejengwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA na utawasaidia wananchi wote wanaoishi mtaa wa Kichangani Mahoje.

Amesema kuwa, gharama za mradi huo ni takribani milioni 230 na unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa nne na lengo kuu ni kupunguza kero ya maji kwa wananchi.

Upendo amesema, serikali kwa kushirikiana na mamlaka za maji wanaendelea kushirikiana kwa pamoja kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mtandao wa maji na kufikia lengo la asilimia 95 mwaka 2020.

“Kuna mradi mwingine wa maji unaosimamiwa na DAWASA wa Ujenzi wa tanki la Kisarawe ambapk kufikia mwishoni mwa mwaka huu wananchi wote wa Majohe na Gongo la Mboto kaa ujumla watapata majisafi na salama,”amesema Upendo.


Diwani wa Kata ya Kichangani Mwanevyale Waziri ameishukuru ofisi ya Mkurugenzi kwa kufanikisha kuja kwa mradi huo kwani wana muda mrefu wananchi wa eneo hilo hawajapta majisafi na salama.

Mradi huo wa maji wa Mtaa wa Kichangani utakapomalizika kutajengwa vizima saba vya kuchotea maji kwa ajili ya kuwarahishia wananchi wa maeneo hayo.

DAWASA wanaendelea kuadhimisha wiki ya maji iliyoanza Machi 16 na itamalizika Machi 22 ikiwa na kauli mbiu ya Hakuna atakayeachwa.
 Katibu Tawala DAS Ilala Sheila Edward akiwa sambamba na Diwani wa Mtaa Kichangani Mwanevyale Waziri wakiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Ilala Upendo Lugongo akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza na wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam

MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AONDOKA CUF ...AHAMIA ACT-WAZALENDO

$
0
0

*Asema yeye na wenzake wameutua mzigo wa CUF na wala hawana habari tena

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

HATIMAYE Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF) Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi wenzake wametangaza rasmi kuondoka Chama hicho na kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo leo Machi 18,2019.

Ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema baada ya kutafakari kwa kina wameona wanayo nafasi ya kuendelea na mapambano ya kisiasa na hivyo wamejiunga ACT-Wazalendo kuendeleza mapambano hayo.

Uamuzi wa Maalim Seif na wenzake umekuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi kutoa uamuzi wa kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF.

"Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa uamuzi wa kesi 23 ya mwaka 2016 ambayo tuliifungua kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kuingia maamuzi ya Chama ya kutomtambua Lipumba.

"Kwa mujibu wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni kwamba Msajili kumtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF.Tunajua sababu za kutolewa kwa uamuzi huo ni kuihujumu CUF pamoja na demokrasia nchini.Mahakama ilichelewa kutoa uamuzi kwasababu ya kutoa nafasi kwa Lipumba kusajili Bodi ya Wadhamini,"amesema.

Akifafanua zaidi Maalim Seif anasema wanahamia ACT wakiamini umma wa Watanzania haujawahi kushindwa mahali popote na kusisitiza wana-CUF wote na wananchi kuwaunga mkono na sasa ni wakati wa shusha Tanga pandisha Tanga.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuna watu walijitolea nyumba zao kwa ajili ya Ofisi za CUF na ombi lake kwao waendelee na moyo huo huo kwa kuzifanya nyumba hizo kuwa ofisi za ACT-Wazalendo na safari inaendelea.

Pia amesema kitendo cha wao kuhama katika Chama ambacho wamepambana kukijenga inakwenda kuandika historia mpya kuelekea Tanzania mpya ambayo itasimamia haki kwa Watanzania wote na kwamba huko wanakokwenda wanakwenda wakiwa wanachama wa kawaida.

Ameongeza mzigo wa CUF kwa sasa wameutua na hawana habari tena na Chama hicho , kwani wao wameshamalizana nao na ni mwendo wa kusonga mbele na Watanzania wafahamu kabla ya kujiunga na Chama hicho wamefanya upembezi wa kutosha kwa kupitia Katiba ya chama kimoja baada ya kingine na wamejiridhisha ACT ndio sehemu sahihi ya wao kwenda.
 
"Eneo ambalo tunaamini mapambano yetu yataendelea ni ACT- Wazalendo, tunakwenda huko kupigania wananchi na si kutafuta vyeo.Hatuendi na masharti ya aina yoyote yale.Tunajua wanachama wa CUF wakiwamo wabunge wanatuunga mkono sana lakini tunaacha wachukue maamuzi wenyewe na sio sisi,"amesema Maalim Seif.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT. JAKAYA KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wakielekea kwenye mazungumzo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 18/03/2019. PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULI AAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA MBUNGE WA VITI MAALUMU GEITA VICKY KAMATA NA DADA WA MKUU WA MKOA WA PWANI DKT. EVARIST NDIKILO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa wameungana na familia ya marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata (wa tatu kushoto) ambaye  pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia) kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (anayepeana naye mikono) kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata ambaye ni mtoto wa marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa Dkt Servacius Likwelile, mkwe wa marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa  marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa  marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa wameungana na familia ya marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakitoa sadaka wakati walipoungana na  familia ya marehemu Mama Paulina Kasama Selemani ambaye ni Mama Mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu wa Geita Mhe. Vicky Kamata (wa tatu kushoto) na pia ni dada yake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia) kwenye misa ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Machi 18, 2019.

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA KAZI WA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza kufungua mkutano wa Kazi wa Siku Tano wa Maafisa hao , Machi 18, 2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungau Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku tano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao wa siku tano kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi , Afisa wa Mawasiliano wa NSSF, Lulu Mengele, Cheti cha Shukuruani kwa udhamini wa  NSSF  wa Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini alioufungua kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019.  Kushoto ni Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukurani ya udhamini wa Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa baaada ya kufungua Mkutano wa siku tano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini, Kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. Kushoto ni Waziri wa Habari, Umaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.  Harrison Mwakyembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kaimu Mhariri Mtendaji wa  Magazeti ya Serikali ya Daily News  na Habari Leo (TSN), Tuma Abdallah cheti cha shukurani ya udhamini  wa Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini uliofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisindikizwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kufungua Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikalini kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HASUNGA AAGIZA MAJINA YA WAKULIMA WA KOROSHO WALIOLIPWA YABANDIKWE KWENYE OFISI ZA VIJIJI

$
0
0

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara


Kumekuwa na dhana ya kila mkulima wa korosho kulalamika kuwa hajalipwa fedha za korosho zake jambo hili limeibua sintofahamu katika jamii.


Katika hali hiyo serikali sasa imeamua kuja na mkakati kabambe wa kubandika majina ya wakulima wote waliolipwa fedha zao ili kuondokana na kadhia ya lawama za wakulima wasioitakia mema serikali.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa agizo hilo leo tarehe 18 Machi 2019 wakati akizungumza mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge, Mifugo na Maji kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.


Agizo hilo limetolewa kwa wataalamu wanaoongoza timu ya Oparesheni Korosho kubandika majina ya wakulima wote waliolipwa ili kuondoa sintofahamu katika jamii.


“ Mimi nashangaa sana kila mkulima akiulizwa anasema hajalipwa jambo hili sio sawa nadhani wanafanya hivi kukwepa madeni wanayodaiana huko vijiji, sasa naitaka timu ya wataalamu wa Oparesheni korosho kuhakikisha majina yote ya wakulima waliolipwa yanabandiikwa kwenye ofisi za vijiji ” Alikaririwa Mhe Hasunga


Alisema kuwa wanapaswa kubandika orodha ya majina ya watu waliolipwa na kiasi cha korosho walicholipwa.“Mpaka sasa Tani 222,684 zimekwisha kusanywa huku hadi kufikia tarehe 14 Machi 2019 tayari jumla ya Shilingi Bilioni 596.9 zilikuwa zimekwishalipwa kwa wakulima kati ya Shilingi Bilioni 723 

lakini nashangaa wakulima wanasema hawajalipwa hili sio sawa” Alisema Mhe Hasunga

Sambamba na hayo Waziri Hasunga alisema kuwa Serikali imejipanga hadi kufikia tarehe 31 Machi 2019 wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.


Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli inapaswa kuungwa mkono kwa maamuzi magumu kwenye korosho kwa kuamua kuwalipa wakulima shilingi 3300 kwa kila kilo moja ya korosho.


Kadhalika, ameshangazwa na Mkoa wa Mtwara ambao unazalisha kwa karibu nusu ya korosho zote nchini lakini imebaini idadi ndogo ya wafanyabiashara wanaofanya biashara ya Korosho kinyume na sheria maarufu kama kangomba ukilinganisha na mkoa wa Lindi ambao una idadi kubwa ya Kangomba.


“ Nashangaa sana Mkoa wa Mtwara una Kangomba 10 lakini ndio wazalishaji wakubwa wa korosho huku Mkoa wa Lindi ambao unafuatia kwa uzalishaji wa korosho ukiwa na idadi kubwa ya Kangomba ambao wapo zaidi ya 400” Alisema


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Dkt Christine Ishengoma amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kwa kuanzisha zoezi la usajili wa wakulima nchini.


“ Nakupongeza sana Waziri Hasunga kwa hili lakini hakikisha unalisimamia kwa weledi jambo hili ili liwe na matokeo chanya na wakulima waweze kutambulika kote nchini kwani kufanya hivyo serikali itakuwa na uwezo wa kuwahudumia kwa ufasaha” Alisema


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiongozwa na Mhe Dkt Christine Ishengoma wameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara wakikagua miradi ya maendeleo katika sekta husika za Kilimo, Mifugo na Maji.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA KAZI WA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza kufungua mkutano wa Kazi wa Siku Tano wa Maafisa hao , Machi 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungau Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku tano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao wa siku tano kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi , Afisa wa Mawasiliano wa NSSF, Lulu Mengele, Cheti cha Shukuruani kwa udhamini wa  NSSF  wa Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini alioufungua kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019.  Kushoto ni Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukurani ya udhamini wa Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa baaada ya kufungua Mkutano wa siku tano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini, Kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. Kushoto ni Waziri wa Habari, Umaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.  Harrison Mwakyembe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kaimu Mhariri Mtendaji wa  Magazeti ya Serikali ya Daily News  na Habari Leo (TSN), Tuma Abdallah cheti cha shukurani ya udhamini  wa Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini uliofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisindikizwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kufungua Mkutano wa Kazi wa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikalini kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YATOA ONYO KWA VIONGOZI WA WIZARA NA MIKOA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa wizara, taasisi au mikoa kuacha mara moja tabia ya kuwatumia waandishi wa habari binafsi katika utekelezaji wa majukumu yao ya Kiserikali na kuwaacha wale ambao wameajiriwa na Serikali katika ofisi zao kwa kazi hiyo.

“Kwanza tabia hii ni hatari kwa usalama wa taarifa za Serikali. Nitumie nafasi hii kukemea viongozi na watendaji wenye tabia za namna hii kuacha mara moja tabia hizo zisizo kinyume na matakwa ya maadili ya utumishi wa umma.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Machi 18, 2019)katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini, kinachofanyika katika ukumbi wa BOT jijini Mwanza. Kikao hicho kinahudhuriwa na Maafisa Habari na Mawasiliano takbaribani 400.

Katika kuhakikisha suala hilo linakomeshwa Serikalini, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo umpelekee  majina ya kiongozi au mtendaji wa ngazi yeyote ile ambaye bila sababu zozote anawapuuza waliajiriwa na Serikali kufanya kazi hiyo.


Waziri Mkuu amesema Serikali inatumia rasilimali nyingi kuajiri, kuanzisha, kuiendeleza na kuitunza kada ya maafisa habari Serikalini, hivyo, maafisa habari waliopo wapewe nafasi ya kutekeleza majukumu yao kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Waziri Mkuu amesema maafisa hao wanatakiwa wapewe ushirikiano na viongozi wa taasisi wanazozitumikia ili habari za utekelezaji wa Serikali ziwafikie wananchi badala ya viongozi na wataalamu wengine kukalia habari hizo. “Mawaziri na Wakuu wa Mikoa, simamieni Maafisa Habari kutimiza wajibu wao”.

Waziri Mkuu amesema anafahamu changamoto nyingine kwa maafisa habari ambazo husababishwa na viongozi au watendaji katika taasisi za umma na hasa katika ngazi za Wizara, Mikoa na Halmashauri za kutotambua mchango wa sekta ya habari katika maendeleo ya nchi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema anazo taarifa za baadhi ya maafisa habari ambao wana vifaa vyote pamoja na ofisi nzuri zenye kuvutia lakini bado hawatimizi wajibu wao ipasavyo katika kutangaza shughuli za Serikali. 

“Wengine hawajui shughuli zinazofanywa na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakuu wa Sekta kwa siku, wiki hata mwezi…Taasisi haina taarifa. Badilikeni, nenda mkakusanye taarifa na mzitoe hadharani”. 

“Tambueni kwamba Serikali haitowavumilia Maafisa Habari wa namna hii kwani ni wazi kabisa kuwa hawatufai na ni mzigo kwa Serikali. Basi, wale wote wenye mienendo ya namna hiyo chukueni hatua, mjitathmini na mjirekebishe mara moja. 


Amesema maafisa hao ambao wamepata mafunzo ni lazima utendaji wao ukazingatia maadili na weledi na wakati wote utekelezaji wa majukumu yao ujikite katika kuboresha masilahi ya umma, kuepuka uchochezi, ushabiki, vijembe na kuepuka kuandika habari zinazopandikiza chuki katika jamii. 

Pia, ameielekeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Idara ya Habari-MAELEZO ifanye tathmini ya kina kuhusu utendaji wa maafisa habari hasa wale wanaoongoza vitengo na watakaoonekana kuwa hawaisaidii Serikali waondolewe mmoja baada ya mwingine bila kupepesa macho.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema kila nchi inayo misingi, utamaduni na tunu zake, hivyo amewataka maafisa hao  watambue kuwa wao ni sehemu muhimu katika kusimamia na kuendeleza misingi,utamaduni na tunu za Taifa. 

Amesema maafisa hao hawana budi kuhakikisha wanabeba agenda za Kitaifa katika utekelezaji wa majukumu yao kwani yapo mambo ambayo ni msukumo wa kitaifa kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. 

“Kutokana na haya kila tunachoandika ni lazima kiwiane na agenda zetu kitaifa katika sekta mbalimbali. Kwa mfano: Kisiasa msukumo wetu ni amani na utulivu, kiuchumi msukumo wetu sasa ni ujenzi wa viwanda na kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati. Kiutamaduni msukumo wetu ni kulinda na kudumisha mila na tamaduni zetu”. 

Waziri Mkuu amesema mambo hayo wao wana wajibu wa kuyapa kipaumbele ili jamii iweze kuhabarishwa vizuri. Vyombo vingine vya nje haviwezi kuyaandika na kuyatangaza mambo hayo vizuri na kwa msukumo wa Kitaifa kama wao. Nawasihi chukueni nafasi yenu katika kuzibeba agenda zetu za Kitaifa. 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza leo kwenye mkutano wa viongozi wa wizara, taasisi au mikoa kuacha mara moja tabia ya kuwatumia waandishi wa habari binafsi katika utekelezaji wa majukumu yao ya Kiserikali na kuwaacha wale ambao wameajiriwa na Serikali katika ofisi zao kwa kazi hiyo.

DAS ILALA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TANKI LA MAJI MAJOHE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Tanki la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi Lita 150,000 kwa siku katika Mtaa wa Kichangani Majohe Jijini Dar es Salaam.

Akiweka jiwe la Msingi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Katibu Tawala DAS Sheila Edward amesema kuwa mradi huu utawasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kuwapunguzia kero ya maji waliyonayo kwa muda mrefu.

Amesema, serikai inaendelea kutekeleza ahadi za serikali ya mapinduzi ili kufikia malengo ya kumtua mama ndoo kichwani na wamekuwa wanashirikiana na madiwani kwani marndeleo hayana chama.

DAS amesema, Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa maji Mtaa wa Kichangani Majohe utasaidia wananchi takribani laki saba (700,000) na amezitaka mamlaka husika kusimamia mradi huo pindi utakapomalizika ili uweze kujiendeleza.

Kaimu Mkurugenzi Wa Manispaa ya Ilala Mhandisi Upendo Lugongo amesema kuwa mradi huo wa maji umejengwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA na utawasaidia wananchi wote wanaoishi mtaa wa Kichangani Mahoje.

Amesema kuwa, gharama za mradi huo ni takribani milioni 230 na unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa nne na lengo kuu ni kupunguza kero ya maji kwa wananchi.

Upendo amesema, serikali kwa kushirikiana na mamlaka za maji wanaendelea kushirikiana kwa pamoja kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mtandao wa maji na kufikia lengo la asilimia 95 mwaka 2020.

“Kuna mradi mwingine wa maji unaosimamiwa na DAWASA wa Ujenzi wa tanki la Kisarawe ambapk kufikia mwishoni mwa mwaka huu wananchi wote wa Majohe na Gongo la Mboto kaa ujumla watapata majisafi na salama,”amesema Upendo.


Diwani wa Kata ya Kichangani Mwanevyale Waziri ameishukuru ofisi ya Mkurugenzi kwa kufanikisha kuja kwa mradi huo kwani wana muda mrefu wananchi wa eneo hilo hawajapta majisafi na salama.

Mradi huo wa maji wa Mtaa wa Kichangani utakapomalizika kutajengwa vizima saba vya kuchotea maji kwa ajili ya kuwarahishia wananchi wa maeneo hayo.

DAWASA wanaendelea kuadhimisha wiki ya maji iliyoanza Machi 16 na itamalizika Machi 22 ikiwa na kauli mbiu ya Hakuna atakayeachwa.
 Katibu Tawala DAS Ilala Sheila Edward akiwa sambamba na Diwani wa Mtaa Kichangani Mwanevyale Waziri wakiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Ilala Upendo Lugongo akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza na wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI AIOMBA KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA KUSAIDIA UTOLEWAJI WA ELIMU YA USALAMA BARABARANI

$
0
0


*Ni baada ya kufurahishwa na mafunzo yanayotolewa na Puma Energy Tanzania kwa wanafunzi wa shule za msingi

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy, imezindua mafunzo na uchoraji la usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi, mafunzo ambayo yatawapa uelewa wa usalama huku Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni akitoa ombi kwa Puma kutoa elimu hiyo kwa shule zote nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 18 , 2019 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Yussuf Masauni, ambapo Mkurugenzi wa Puma, Dominic Dhanah, amefafanua mafunzo hayo yanakwenda sambamba pia kwa wanafunzi waliowahi kufundishwa.

Amesema madhumuni ya kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi ni kutokana na imani yao kwamba, watoto hao wanakabiliwa na hatari za ajali za barabarani na kuhitaji mafunzo ya usalama barabarani ili kuepukana na ajali.

“Usalama barabarani ni kipaumbele namba moja katika Kampuni ya Mafuta Puma na tumeamua kuwafundisha watoto wadogo kwani tunfahamu hatari za barabarani wanazokabiliana nazo. Kampuni ya Puma inafanya biashara ya mafuta katika nchi 49 duniani na kwa Afrika tupo katika nchi 19. Mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi yalianza mwaka 2013 hapa Tanzania na mpaka sasa shule 75 zimenufaika na mafunzo haya wakati wanafunzi 80,000 wamepata mafunzo haya,"amesema

Ameongeza kuwa "Tumefanya utafiti na kugundua kuwa shule tulizoendesha mafunzo haya , ajali kwa wanafunzi zimepungua na hivyo basi kwa mwaka 2019 mafunzo haya yataendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar,” alisema Dhanah

Kwa upande wake Naibu Waziri Masauni, amesema Serikali inafarijika na kazi inayofanywa na Kampuni ya Puma kwa kurudisha faida inayopatikana kwa jamii ikiwamo kutoa mafunzo muhimu ya usalama barabarani.

Amesema elimu ni suala la kipaumbele kwa jamii na mkakati wa wao Wizara ya Mambo ya Ndani na Serikali kwa ujumla ni kupunguza ajali za barabarani na Puma inafanyakazi hii kwa karibu na Machi 30, mwaka huu tutakuwa na kongamano la wiki ya usalama barabarani pia tujadili hili kwa kina.

"Serikali tunatambua kazi nzuri ambayo inafanywa na Puma Energy Tanzania katika kutoa elimu hii inayohusu usalama barabarani.Ni jukumu letu na wananchi kwa ujumla kuunga mkono jitihada hizi.,” alisema Masauni

Akifafanua zaidi Mhandisi Masauni amesema kitendo cha Puma kuwa na programu hiyo kinaonesha namna ambavyo wanakataa ajali za barabarani kwa vitendo na kwamba wanafunzi ambao wanapata elimu hiyo anauhakika watakuwa mabalozi wazuri wa kuelezea kwa usahihi mtembea kwa miguu anatakiwa kufanya nini akiwa barabarani.

"Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani wana program nyingi za kusaidia kutoa mafunzo kwa shule zote zilipo kwenye mazingira hatarishi na zisizo kwenye mazingira hayo pia. Programu hizo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali za kifedha. Ninaomba kutumia fursa hii kuomba uongozi wa Puma kukisaidia Kikosi cha Usalama Barabarani kuzifikia shule zote nchini kwa kupitia askati walioko kwenye maeneo yote nchini,"amesema Pia amemuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani kuanza mchakato wa kuandaa andiko la kutoa mafunzo kwa shule zote nchini na kuliwasilisha kwenu (Puma) ili muone namna yambavyo mnaweza kusaidia kuokoa kizazi chetu cha kesho,” amesema Masauni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akimpa zawadi mmoja wa Wanafunzi wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,mara baada kujibu vizuri swali lililohusu mambo ya usalama barabarani,kabla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania iishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
Mmoja wa Watoa Mafunzo ya Usalama barabarani kwa Wanafunzi wa shule ya msingi chini ya Ufadhili wa kampuni ya Puma Energy Tanzania,Neema Swai kutoka taasisi ya AMEND akionesha moja ya mchoro ulioshinda kwenye shindano la Wachoraji kuhusu Usalama barabarani mwaka 2018,mbele ya mbele ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi ( wa pili kulia ) Mhandisi Hamad Masauni,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania
Ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ukiendelea leo jijini Dar

Mwanafunzi Shule ya Msingi Bunge jijini Dar, Omari akifafanua kuhusu namna ya matumizi sahihi kwa watembea kwa miguu mbele ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchi ( wa tatu kulia ) Mhandisi Hamad Masauni,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania,Dominic Dhannah akizungumza leo jijini Dar wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni hiyo,ambapo mgeni rasmi ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi ( wa kwanza kulia ) Mhandisi Hamad Masauni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akiwa na baadhi ya Wanafunzi ambao ni pia ni Mabalozi wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,ambao wamehudhuria ufunguzi wa mafunzo ya usalama barabarani yanayotolewa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni akiwaaaga baadhi ya wanafunzi ambao ni pia ni Mabalozi wa Usalama barabarani wa shule ya msingi Bunge jijini Dar,mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya Usalama barabarani yanayotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania kishirikiana na wadau wengine ikiwemo taasisi ya AMEND.

MASAUNI AAGIZA TRAFIKI WALIOMSHAMBULIA , KUMTUSI DEREVA NA ABIRIA WAKE WACHUKULIWE HATUA KWA MUJIBU WA SHERIA

$
0
0
 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameonesha kukerwa na kitendo cha askari wa wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani, ambao wameonekana kwenye video kupitia mitandao ya kijamii wakimtukana dereva na kumpiga yeye na abiria wake  huku akieleza kuwa tayari wamekamatwa na kuwekwa ndani ili sheria ichukue mkondo wake.
Kukamatwa kwa askari hao kumetokana na agizo lililotolewa na Mhandisi Masauni ambapo amesema katu Serikali haiko tayari kuona Jeshi la Polisi likichafuliwa na baadhi ya askari waliokosa uadilifu.
Akizungumza leo ijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uchoraji la usalama barabarani, Masauni amesema kumekuwa na malalamiko mengi ya madereva kubambikiwa makosa au askari kufanya vitendo vilivyo kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la polisi.
“Kuna video ambayo tangu jana imeonekana ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha askari wakimtukana dereva pamoja na abiria waliokuwamo na si hivyo tu ilifika hadi kumpiga. Baada ya tukio hili nilimuagiza Kamanda wa Kiko cha Usalama Barabarani achukue hatua kwa suala hili. Kwa taarifa ambazo ninazo tayari wamekamatwa,"amesema.
 Amesema ikitokea mtumiaji yoyote wa barabara amefanyiwa vitendo vyovyote asisite kuwasiliana na uongozi wa askari aliyefanya vitendo hivyo.“Na ikitokezea uongozi wa askari husika anatetea au kutochukua hatua muafaka, mlalamikaji apande kwa uongozi wa juu na ikibidi afike hata kwangu nani mitachukua hatua stahiki na utapata mrejesho.
 Kuhusu suala la usalama barabarani, Mhandisi Masauni amesema anaipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma kwa kuendesha program hiyo ambapo pia alizitaka kampuni zingine kuiga mfano huo kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama wa watoto kwani ni Taifa leo kesho na wateja wa kesho pia.
 “Programu hizo zimekuwa zikikabiliw na changamoto mbalimbali za kifedha. Ninaomba kutumia fursa hii kuomba uongozi wa Puma kukisaidia Kikosi cha Usalama Barabarani kuzifikia shule zote nchini kwa kupitia askati walioko kwenye maeneo yote nchini.Namuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani kuanza mchakato wa kuandaa andiko la kutoa mafunzo kwa shule zote nchini na kuliwasilisha kwenu (Puma) ili muone namna yambavyo mnaweza kusaidia kuokoa kizazi chetu cha kesho,” alisema Masauni
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images