Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

WITO WATOLEWA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM NA PWANI KUTEMBELEA MAONESHO WIKI YA MAJI MNAZI MMOJA

0
0
Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Ilala,Upendo Omary akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Uzinduzi wa wiki ya Maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, DAWASA Inafanya Maadhimisho hayo kwa kutoa elimu kwa wakazi wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo wadau mbalimbali wameshiriki
Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Ilala,Upendo Omaryakizungumza na Waandishgi wa Habari juu ya Uzinduzi wa wiki ya Maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, DAWASA Inafanya Maadhimisho hayo kwa kutoa elimu kwa wakazi wa Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASA wakimsikiliza Mmoja wa Wakazi wa Dar es Salaam ambae amefika katika Maonyesho ya Wiki ya Maji yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam
Mwanamama akipata Maelezo kutoka kwa mmoja wa wato huduma kwa wateja juu ya huduma za DAWASA Katika Maonyesho ya Wiki ya Maji yanayoendeea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS SHEIN

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na wanawake kwa ujumla kuchapa kazi zaidi na kushikamana katika kuleta maendeleo kwa jamii nzima.

Makamu wa Rais ameyasema hayo kwenye Kongamano la Wanawake la Kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  kwa kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hoteli ya Verde, wilaya ya Magharibi A, mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

“Sisi ni sehemu muhimu sana ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, hivyo Kongamano hili liwe chachu yetu katika kuchapa kazi zaidi”alisema Makamu wa Rais.

Aidha, aliwasihi wanawake kuchukua jukumu la kuzisemea na kuzitangaza kwa sauti kubwa kazi nzuri zinazofanywa na viongozi  wa Serikali zetu mbili ili wananchi wazijue na wasipotoshwe.

“Sote ni mashuhuda wa kazi kubwa na nzuri iliyofanyika hapa Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitatu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi mahiri wa Dokta Shein imefanya kila liwezekanalo kuboresha hali ya maisha ya wananchi wa Zanzibar kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi.”Alisisitiza Makamu wa Rais.

 Rais Shein ametekeleza kwa umahiri mkubwa ilani ya Uchaguzi na kuweza kuleta mafanikio makubwa katika Uimarishaji wa Huduma za afya, Elimu , ujenzi wa miundombinu,Kilimo, ufugaji, uvuvi na Ushirika, kuwawezesha Wazee, wanawake na Walemavu na kuwateua wanawake kwenye nafasi za Uongozi.

Makamu wa Rais ameupongeza uongozi wa UWT Taifa pamoja na Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar kwa kuandaa kongamano hilo ambalo sit u la kumpongeza Dkt. Shein kwa kazi kubwa aliyofanya kwa kipindi cha miaka mitatu, bali Kongamano la kutoa ushuhuda kwa wananchi kuhusu kazi nzuri inayofanywa na Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia maendeleo ya wananchi.

Mawaziri wa SMZ , Wawakilishi wa Viongozi na Naibu Waziri wa Nishati kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano walipata nafasi ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Kongamano hilo.

Kongamano hili lilifanyika Pemba tarehe 9, Machi 2019 ambapo lilitanguliwa na ziara liyoanza tarehe 6-8 mwezi Machi 2019 na ziara kama hiyo imefanyika Unguja kuanzia tarehe 11-14 Machi 2019 ambapo tarehe 15 Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa ilikutana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Kongamano la UWT la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hotel ya Verde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka akihutubia kwenye Kongamano la UWT la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hotel ya Verde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Sehemu ya Waliohudhuria Kongamano la UWT la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hotel ya Verde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RC MAKONDA -KWA KASI HII YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO, IFIKAPO 2020 MIGOGORO YA ARDHI DAR ITABAKI KUWA HISTORIA

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi Mhe. William Lukuvi leo amezindua Mpango wa kutambua na kusajili kila kipande cha Ardhi Mijini  ambapo licha ya mpango huo kuwawezesha wananchi kutumia leseni za Makazi kama dhamana ya kuchukulia mikopo pia itawawezesha kutambulika kama wamiliki halali wa maeneo yao.

Waziri Lukuvi amesema Mpango huo wa kutoa Leseni na Makazi ni mkakati wa serikali kuwakwamua wananchi kiuchumi ambapo mwananchi atahitajika kuchangia kiasi cha Shilingi 5,000 pekee ili kupata leseni ya makazi kwa Muda wa miaka mitano na baada ya hapo mwananchi atapatiwa Hati ya makazi kwakuwa tayari atakuwa anatambukika na serikali.

Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amesema anaamini kwa utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda mpango huo unaenda kufanyika kwa ufanisi mkubwa na kuleta manufaa kwa wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema mpango huo ni zaidi ya ufumbuzi na utatuzi wa kero ya migogoro ya ardhi iliyokuwa ikitumika kama kichaka cha wajanja wenye pesa kuwakandamiza wananchi wanyonge kwa kuwapora maeneo yao jambo ambalo ameahidi kulisimamia kidete.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuwa na leseni za makazi kwakuwa hadi sasa takriban 70% ya maeneo ya jiji hilo hayana hati wala leseni za makazi ambapo amewataka watendaji wa kata na mitaa kutoa ushirikiano wa kutosha wataalamu wa ardhi watakaokuwa wakipita kwenye mitaa kuanzia wiki ijayo.

WAKANDARASI ACHENI KULIPUA KAZI ZINGATIENI VIWANGO-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi wanaojenga majengo mbalimbali nchini yakiwemo na ya Serikali wahakikishe wanazingatia viwango na waache kulipua kazi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wawafundishe kazi mafundi wasaidizi wanaowatumia katika ujenzi wa miradi malimbali ili waweze kunufaika kwa kuongeza ujuzi.

Ametoa wito huo  leo mchana (Jumamosi, Machi 16, 2019), alipotembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wilayani Ruangwa mkoani Lindi, ukiwemo wa Hospitali ya wilaya.

Amesema Serikali inatoa pesa kulingana na kazi inayotakiwa kufanyika, hivyo amewataka wakandarasi wafanyekazi wanazopewa kwa kufauata taratibu za kiufundi na si ‘kulipua lipua’.

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi hao kuwatumia mafundi wasaidizi waliopo kwenye maeneo ya karibu na miradi husika ili nao waweze kupata ajira.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka mafundi wasaidizi wahakikishe wanafanyakazi kwa bidii na uadilifu ili wawe mabalozi wazuri, jambo litalalowawezesha wengine kupata kazi.

"Nataka niwaambie mkifanya kazi kwa uaminifu wakandarasi.

watawachukua na kuwapeleka katika maeneo mengine wanayopata mradi. Jitumeni acheni uvivu mtafika mbali."

Amesema Serikali inatengeneza ajira kwa vijana kupitia wakandarasi wanaotekeleza miradi, hivyo wakandarasi wanatakiwa wawatumie mafundi wasaidizi walioko kwenye maeneo ya miradi.

Waziri Mkuu amesema amefarijika sana kuona vijana wanapata ajira na amewataka  watumie nafasi hizo kujifunza ufundi ili nao waje kuwa mafundi wakubwa na kuajiri wenzao.

Naye,  fundi msaidizi wa jengo la utawala katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa,Hamisi Ali amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwapelekea miradi mkubwa ambayo inawapatia ajira.

Ali ametoa wito kwa vijana wengine waache kukaa mitaani na badala yake wajitokeze na wachangamkie fursa za ajira zilizopo kwenye maeneo yao na wafanye kazi hizo kwa bidii.

Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa hospitali ya wilaya, ghala, Ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Shule ya Seondari ya  Wasichana Lucas Maria.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mamantilie Asha Livembe (aliyesimama) na Asha Mluki (kushoto) baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa hospitali ya Wilaya Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mhandisi Mshauri Edgar Rugemalila, wakati akimuonesha mchoro wa ghala la Wilaya ya Ruangwa kabla ya kukagua ujenzi wa ghala hilo wilayani Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa ghala wilayani Ruangwa Machi 16.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUFA NA KUPONA YA SIMBA NA AS VITA, NGOMA BADO NZITO 1-1 MPIRA UNAENDELEA

SIMBA YAUNGURUMA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO, YAIFUNGISHA VIRAGO AS VITA MATAIFA YA AFRIKA

0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Klabu ya Simba inafanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga timu ya As Vita goli 2-1  na kushika nafasi ya pili kwenye Kundi D.

Mechi hiyo imechezwa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa na msumari wa ushindi uliwekwa na Clotous Chota Chama na kuivusha Simba kwenye hatua ya Makundi.

Ilikua dakika ya 12, As Vita wanaandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Fabrice Ngoma na kuipa timu yake uongozi.

Katika dakika ya 32, Mohamed Hussein anaipatia Simba goli la kusawazisha na kwenda mapumziko wakiwa 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Simba wakisaka goli la ushindi  na As Vita nao wakitafuta namna ya kupenya katika ngome ya ulinzi ya Simba.

Simba wanalisakama lango la As vita na wakipoteza nafasi nyingi za wazi mabadiliko ya kumtoa Emanuel Okwi na kuingia Haruna Niyonzima yaliweza kuzaa matunda na kurejesha uhai katika kikosi hicho.

Katika dakika ya 86, Simba wanafanya shambulizi langoni mwa As Vita na kumalizia pasi ya Zana Coulibaly na kuzima matumiani ya As vita kwenda hatua ya robo fainali.

Filimbi ya mwisho inapigwa Simba wanavyka hatua hiyo kwa alama 9 akiwa nyuma ya Alhly mwenye alama 10 baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi JS Saoura.










































Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini yakagua ujenzi wa kituo cha umahiri songea

0
0
Na Issa Mtuwa, Songea
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Akiongea na waandishi wa habari mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa Ruvuma, Mzuzuri amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na wataendelea kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.
“Tunawapongeza sana Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema Mzuzuri.
Naibu Wziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa kuzingatia ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata hivyo kituo cha songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo ambalo lilisha tatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.
Nae Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma ulikumbwa na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto mkoa nzima, mara baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.
Kituo cha Umahiri Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika maeneo mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala mbalimbali madini.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alie mbele akikagua na kutoa maelekezo kwa Meja Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini kulia kwa Meja ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu  wa Wizara ya Madini Issa Nchasi kabla ya kuwasili kwa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
 Meneja wa Kanda ya Ujenzi SUMA JKT, Meja Atupele Mwamfup akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kituo na kutafsiri michoro mbalimbali ya jengo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Makamu Mwenyekiti Mhe. Mriam Mzuzuri na wajumbe wengine.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitoa maelezo ya ujenzi wa kituo cha umahiri songea kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati Mhe. Mariam Mzuzuri kushoto kwake. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi na Meja Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mariam Mzuzuri akimueleza jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wa kulia kwake mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri.

KONGAMANO UWT TAIFA ZANZIBAR LAFANA,MAKAMU WA RAIS ATOA NENO

0
0

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka akimkabidhi zawadi ya Saa yenye picha yake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan (Kulia) katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.Picha Zote na Elisa Shunda

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AWAONGOZA WANAWAKE WA UWT TANZANIA KATIKA KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS DK.SHEIN KWA KUTIMIZA MIAKA MITATU YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA MWAKA 2015/2018 MJINI UNGUJA.

 Pwani Kucheleeeeeeeeeee

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka akiongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan (Kulia) katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

  Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

 Viongozi Wakiongozwa na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan (katikati) wakiimba wimbo wa taifa katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.


 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan (Kulia) katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

 Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu Uwt Taifa,Mwalimu Queen Mlozi (wa tatu kutoka kushoto) katika kongamano hilo.

  Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

 Viongozi Mbalimbali wa Serikali Mawaziri,Manaibu Mawaziri,Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi toka Sekta Mbalimbali wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

  Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

  Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

  Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi (katikati) na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Uwt Wilaya ya Kibaha Mjini,Mwalimu Joyce Francis (kushoto) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Dk.Gaudentia Kabaka (aliyekaa chini)  katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

  Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokea Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakifuatilia kwa umakini wakati Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 likiendelea katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.

Mwenyekiti wa Uwt Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka (kulia) akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana. Kulia ni Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan.

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akijadiliana Jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Abdallah Juma Mabodi (katikati) na Katibu Mkuu wa Uwt Taifa,Mwalimu Queen Mlozi (Kulia) wakati wa Kongamano hilo likiendelea.

 Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume, Mama Fatuma Karume akitafakari jambo wakati wa Kongamano hilo likiendelea kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar jana.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Taifa,Dk.Gauedentia Kabaka.

 Katibu Mkuu wa UWT Taifa,Mwalimu Queen Mlozi akizungumza katika Kongamano hilo.

Naibu Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Subira Mgalu,akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ushirikiano uliopo kati ya Shirika la Umeme la Tanesco na Shirika la Umeme la Zanzibar katika kuhakikisha umeme unapatikana na Kuelezea wizaara hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika sekta ya Nishati nchini katika Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka.

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Mwenyekiti wa Uwt Taifa,Dk.Gaudentia Kabaka (kulia) baada ya Kongamano la Wanawake Zanzibar la Kumpongeza Rais Dk.Shein kwa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka 3 kuanzia Mwaka 2015/2018 katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hotel ya Verde Mjini Unguja Zanzibar Jana.



NA:ELISA SHUNDA,UNGUJA,ZANZIBAR.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
amesema Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein ameitendea haki ilani ya uchaguzi wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2015/2018 katika kipindi cha miaka mitatu
aliyoongoza Zanzibar.

Pia, amesema utendaji huo umejidhihirisha katika jitihada zake za
kuendeleza na kuimarisha kwa ufanisi mkubwa azma ya machi 3 mwaka 1965
ya Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hayati Abeid
Aman Karume ya kutoa huduma za matibabu bure kwa wananchi.

Kauli hiyo ameitoa jana katika kongamano la wanawake la kumpongeza
Rais Dk.Ali Mohamed Shein kwa kutimiza miaka mitatu ya utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya CCM iliofanyika mjini Unguja liloandaliwa na
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) ya Chama cha CCM.

Makamu huyo wa Rais alisema katika uongozi wa Rais Dk.Shein
ametekeleza zaidi katika azma hiyo kwa kuhakikisha anaongeza bajeti ya
dawa kwa kila mwaka ambapo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ametenga
sh.bilioni 12.7 huku akiongeza watumishi wa afya pamoja na upatikanaji
wa vifaa tiba vya kisasa.

"Huduma hizi zimeendelea kuboreshwa zaidi hususan kwa wazee nampongeza
kwa hatua ya kuwapatia vitambulishi 2,314 wazee kwa lengo la kuwapatia
pensheni ili kuhakikisha wanapata huduma za matibabu bure,"alisema
Makamau huyo wa Rais

Katika maelezo yake Samia alisema wanzanzibar ni mashahidia wa namna
utekelezaji wa ilani ambao Dk.Shein ameufanya kwa kiwango cha juu
ambapo shule za maandalizi zimeongezeka kwa mara 272 baada ya kipindi
cha mapinduzi.

Alisema kwa upande wa shule za msingi zimeongezeka mara 7 huku kwa
sekondari zikiongezeka kwa mara 67 na kwamba katika kipindi cha miaka
mitatu mbali na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo
madarasa,maabara na matundu ya vyoo.

"Pia Rais Dk.Shein amewaondolea wazazi na walezi mzigo wa kuchangia
elimu ya msingi mwaka 2016 na ya sekondari mwaka 2018 na hatua hii
itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mahudhurio na kuondoa ujinga na
kuongeza idadi ya watu walioelimika,"alisema

Makamu huyo wa Rais alisema katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
CCM Dk.Shein ameendelea kuwajali watu wa iana zote bila ya ubaguzi
ambapo wazee ambao wamefikisha miaka 70 na kuendelea wanapewa fedha za
kujikimu ya sh.20,000 kwa kila mwezi.

"Kwa upande wa sekta ya uvuvi ambayo bado hatujaitumia ipasavyo kwa
dhati jitihada za kutengeneza meli mbili ambazo zitakuwa na uwezo wa
kuhifadhi tani 86 za samaki kwa kipindi cha wiki mbili wakiwa baharini
pamoja na mapitio ya sheria ya vyama vya ushirika na uandaaji wa mfumo
wa kietroniki wa kukusanya,kuchambua na kutoa takwimu za vyama vya
ushirika vitaleta matokeo chanya,"alisema Makamu huyo wa Rais

Samia aliongeza kuwa anampongeza Rais Dk.Shein kuendelea na jitihada
zake za kutoa ruzuku kwa wakulima hususan kwa zao la mpunga na kwamba
zimeongeza uzalishaji na kuongeza kipato kwa wananchi na mapato kwa
serikali ya SMZ.

"Pia nampongeza kwa kuendeleea kuhakikisha kuwa zao letu la karafuu
linasimamiwa vizuri na wananchi wanafaidika na kilimo hichi na wazo la
kuanzisha Taasisi ya utafiti wa mifugo na kwamba wazo hili limekuja
kwa wakati kipindi ambacho tayari kiwanda kikubwa cha kuzalisha maziwa
kimeshafunguliwa Zanzibar,"alisema

Makamu huyo wa Rais aliongeza kuwa Dk.Shein ameendelea kutendea haki
katika utekelezaji wa ilani kwa upande wa ujenzi wa viwanja vya ndege
ambapo ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa Abeid Karume mjini Unguja
unaendelea kutekelezwa na uwanja wa ndege wa Pemba unatarajia kuanza
ujenzi wake hivi karibuni.

Hata hivyo, Samia aliwataka wanawake visiwani humu kuchukua jukumu la
kuzisemea na kuzitangaza kwa sauti kazi kubwa nzuri zinazofanywa na
viongozi wa serikali mbili ili wananchi wazijue na wasipotoshwe.

Kwa upande wa Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya Umoja wa
Wanawake(UWT),Gaudencia Kabaka alisema katika kipindi cha hivi
karibuni jumuiya hiyo imefanya ziara kwa upande wa Unguja na Pemba kwa
ajili ya kuelezea namna CCM ilivyotekeleza ilani yake.

Alisema kwa asilimia kubwa CCM imetekeleza ilani yake visiwani humu
ambapo hali hiyo inatokana na ushirikiano mkubwa na wa karibu uliopo
kati ya serikali ya SMZ na CCM.

"Nimejifunza mambo mengi hasa nilipofika kwenye ziara zangu ikiwemo
ushirikiano mkubwa ulioko kati ya Serikali ya SMZ na chama na kwamba
kila tulipoenda tulikutana na watendaji wa serikali ambao ndio
watekelezaji wa ilani huku wakitueleza mambo yalivyotekelezwa,"alisema

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UWT,Queen Mlozi alisema jumuiya hiyo
itaendelea kushirikiana na viongozi wa CCM ambao kwa kiasi kikubwa
wameendelea kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi wa CCM.

Alisema kupitia viongozi hao wameendelea kuwapatia wanawake nafasi
mbalimbali za uongozi ikiwemo nafasi za Uwakilishi,Ubunge na katika
ngazi za serikali za SMZ na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

"Kwa mfano Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi ni mwanamke na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ni mwanamke nataka niseme na
hiyo inatokana na kujitambua na kujiamini kwetu hivyo tupo bega kwa
bega kuhakikisha CCM inaendelea kuongoza kwa upande wa Zanzibar na
Tanzania,"alisema


Akizungumza kwa niaba ya Uwt Mkoa wa Pwani,Farida Mgomi,alimpongeza Rais Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM katika miaka 3 tokea 2015 hadi 2018 kupitia mawaziri wake waliowasilisha maelezo ya utendaji kutoka kwenye wizara zao na amemshukuru katibu mkuu wa Uwt Taifa,Queen Mlozi kwa mwaliko na amewakumbusha viongozi wenzake ngazi ya mkoa na wilaya kuandaa makongamano katika ngazi zao kuisemea serikali yao kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.



NCHI KUSIMAMA KWA DAKIKA 90 MCHEZO WA SIMBA NA AS VITA KUANZIA SAA MOJA YA USIKU

0
0
*Uwanja wa Taifa kwa Mkapa kumenoga...Simba full tambo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UWANJA wa Taifa jijini Dar es Salaam kumenoga!Hakuna maneno mengine ya kuelezea zaidi ya hayo wakati Tanzania ikitarajia kusimama kwa dakika 90 kushuhudia mechi kati ya Simba FC na AS Vita ya nchini Congo.

Wakati mchezo huo ukitarajiwa kuanza saa 1:00 kamili ya usiku ya leo Machi 16,2019 idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa soka hasa wa Simba wamejitokeza kwa wingi kwani licha ya mchezo huo kuanza muda huo sehemu kubwa ya uwanja  umeanza kujaa.

Shangwe na nderembo zilizoambatana na tambo kwa mashabiki wa Simba zimetawala uwanjani hapa .Mashabiki wa Simba wakijipa matumaini wa kuondoka na alama tatu muhimu za mchezo  huo.

Kwa kukumbusha wakati Simba wakijigamba kushinda mechi ya leo katika mchezo wa awali uliofanyika nchini Congo Simba walipokea kichapo cha mabao 5-0.Hata hivyo mashabiki wa Simba wanasema uzuri wa mechi hizi  kila timu inauhakika wa kushinda nyumbani.Acha tusubiri.Simba shusheni presha.

Pamoja na tambo za Simba ukweli utabaki kwamba dakika 90 zitaamua nani anakwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wameiambia Michuzi Blog jioni hii uwanjani hapa kwamba kwa mapenzi ya Mungu watashinda mechi yao dhidi ya AS Vita na kushinda kwao kutaongeza idadi ya timu zitakazoshiriki mwakani na kubwa zaidi in heshima kwa nchi.

Wakati Simba wakijiaminisha hivyo baadhi ya mashabiki wa Yanga walioko uwanjani hapa akiwemo Moses John na Idd Athuman wamesema Simba kushinda mechi ya leo ni sawa na  Ngamia kupenya kwenye tundu za sindano.Mbona mtihani!Kha!

Nje ya uwanjani idadi ya mashabiki walioko kwenye foleni ya kuingia uwanjani ni kubwa .

Kauli mbiu ya Simba katika mchezo wa leo inasema Do or Die wakiwa na maana kufa au kupona wakiamini kwamba ushindi ndilo jambo pekee wanalolitarajia kuona.

Kwa kukumbisha katika mchezo huo Simba inahitaji kushinda ushindi wa magoli yoyote kwani sare kwao haina maana yoyote na iwapo itatokea watakuwa wameaga mashindano hayo yenye heshima kubwa barani Afrika.

MTANZANIA ANTU MANDOZA KUIGIZA FILAMU YA PAMOJA NA NYOTA WA FILAMU WA NIGERIA,RAMSEY NOAH NCHINI GHANA

0
0
 Antu mandoza,Binti wa makamo hivi,anaejishughulisha na Ujasiliamali, muigizaji kutoka Tanzania ambae alionekana kwa mara ya kwanza katika filamu ya Kiumeni 2017 ,amepata 'shavu' la kucheza tamthilia moja na mkali kutoka Nigeria Ramsey Noah, katika tamthilia hiyo itaongozwa na Mwigazi Mkongwe Desmond Eliot inayorekodiwa hivi sasa nchini Ghana ,Desmond Eliot kwa sasa pia anafanya vyema kwenye duru la siasa Nchini Nigeria. Tamthilia hiyo inategemewa kurushwa Africa Magic na ving'amuzi vingine vya Africa kuanzia April,2019 

TUTAENDELEA KUIUNGA MKONO WIZARA YA MADINI-MWENYEKITI WA MADINI

0
0


 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alie mbele akikagua na kutoa maelekezo kwa Meja Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini kulia kwa Meja ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu  wa Wizara ya Madini Issa Nchasi kabla ya kuwasili kwa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
IMG_20190316_143451_8
Meneja wa Kanda ya Ujenzi SUMA JKT, Meja Atupele Mwamfup akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kituo na kutafsiri michoro mbalimbali ya jengo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Makamu Mwenyekiti Mhe. Mriam Mzuzuri na wajumbe wengine.
IMG_20190316_143702_4
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitoa maelezo ya ujenzi wa kituo cha umahiri songea kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati Mhe. Mariam Mzuzuri kushoto kwake. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi na Meja Atupele Mwamfupe Meneja wa Ujenzi SUMA JKT Kanda ya Kusini.
IMG_20190316_145341_9
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mariam Mzuzuri akimueleza jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wa kulia kwake mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umairi.
…………………….
Na Issa Mtuwa Songea.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Akiongea na waandishi wa habari mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa ruvuma, Mzuzuri amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na wataendelea kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.

“Tunawapongeza sana Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema Mzuzuri.

Naibu Wziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa kuzingatia ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata hivyo kituo cha songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo ambalo lilisha tatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.

Nae Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma ulikumbwa na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto mkoa nzima, mara baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.

Kituo cha Umahiri Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika maeneo mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala mbalimbali madini.

Bilioni 1.27 Kukarabati Vyuo vya Polisi Nchini

0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipowasili katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali.Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya Ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Shamsi Vuai Nahodha akiuliza swali wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Chuo cha Polisi Kidatu, lengo ikiwa ni kukagua na kutoa ushauri kwa miradi inayotekelezwa na serikali. Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Richard Marika, akifafanua hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa kikao katika Chuo cha Polisi Kidatu kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa miradi ya serikali.Ziara hiyo imefanyika leo, Mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Serikali imetenga jumla ya Shilingi Trilioni 1 .27 kwa ajili ya ukarabati wa Vyuo vitano vya Polisi nchini katika bajeti ya mwaka 2018/2019 gharama hiyo ikijumuisha ukarabati wa majengo ya ofisi, mabweni, makazi ya wakufunzi na maeneo mengine yaliyoanza kuchakaa.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea Chuo cha Polisi Kidatu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhnadisi Hamad Masauni alisema hali ya miundombinu ya majengo kwa vyuo vyote ni chakavu,nia ya Serikali na Jeshi la Polisi ni kukarabati majengo hayo ili yaweze kukidhi mahitaji.

“Tuna vyuo vitano vya polisi nchini;Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Dar es Salaam,Shule ya Polisi Moshi, Chuo cha Polisi Zanzibar, Chuo cha Maafisa Kidatu na Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza hivi vyote vinahitaji ukarabati na tumetenga jumla ya Shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya ukarabati huo na tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli ameshatoa milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo kimojawapo kati ya hivyo nilivyovitaja” alisema Masauni

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho wajumbe wa kamati hiyo ya bunge waliitaka serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kusimamia mafunzo yanayotolewa vyuoni humo ikiwemo suala la wapelelezi kubambikia kesi wananchi ikiwa ni kinyume na wanchofundishwa vyuoni huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mussa Azzan Zungu akiitaka serikali kuwachukulia hatua askari polisi wachache wanaolichafua jeshi na kuivunjia heshima nchi kwa matendo yao ambayo yako kinyume na maadili.

“suala la kubambikiwa kesi lipo , natoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua askari dhidi ya tuhuma hizo ambao ni wachache wanakiuka taratibu na ueledi katika shughuli zao za kuhudumia wananchi” alisema Zungu.

MACHI 31 MALIPO YA WAKULIMA WA KOROSHO YATAKUWA YAMEKAMILIKA - MHE HASUNGA

0
0
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakikagua kiwanda cha kubangua Korosho katika eneo la Mnazimmoja  wakati wakiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Lindi, Leo tarehe 16 Machi 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya wakulima wa Korosho wakati akizungumza katika ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Leo tarehe 16 Machi 2019. (Picha zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wakulima wa korosho Mkoani Lindi wakifatilia ufafanuzi wa malipo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza katika ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Leo tarehe 16 Machi 2019. 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akitoa maelezo ya awali kuhusu sekta ya kilimo, mifugo na maji mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Leo tarehe 16 Machi 2019. 
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakikagua mtambo wa kutengeneza kimininika cha Nitrojeni inayohifadhi Mbegu wakati wakiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Lindi, Leo tarehe 16 Machi 2019. 
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakikagua chanzo cha Maji na mfumo wa kutibu maji katika kijiji cha Ng'apa wakati wakiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Lindi, Leo tarehe 16 Machi 2019. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Lindi


Serikali imewahakikishia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa kufikia tarehe 31 Machi 2019 wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.


Hakikisho hilo mbele ya kamati hiyo limetolewa leo Tarehe 16 Machi 2019 na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) katika ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akitoa ufafanuzi katika mkutano uliowakutanisha wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wake Dkt Christine Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, wataalamu serikalini sambamba na wakulima.


"Kumekuwa na urasimu mkubwa tangu kuanza kwa zoezi hili la uhakiki lakini sasa tumeamua kama serikali kabla ya mwisho wa mwezi huu wa tatu wakulima wote wawe wamelipwa malipo yao ili kuondoa adha wanazokumbana nazo" alikaririwa Mhe Hasunga


Alisema pamoja na kwamba malipo ni mchakato unaohitaji kupitia katika hatua nyingi za mchakato ikiwemo uhakiki lakini kila jambo lenye mwanzo ni lazima kuwa na ukomo.


Alisema mpaka sasa Tani 222,684 zimekwisha kusanywa huku hadi kufikia tarehe 14 Machi 2019 tayari jumla ya Shilingi Bilioni 596.9 zimekwishalipwa kwa wakulima kati ya Shilingi Bilioni 723


Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amewahakikishia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa pamoja na mchakato huo wa malipo ya Korosho kuendelea lakini pia Wizara imepitia katika michakato mbalimbali ya kumpata Mkurugenzi mpya wa Bodi ya Korosho ili kuendelea na majukumu ya Bodi hiyo.


Kuhusu wanaofanya biashara ya zao hilo kinyume na sheria maarufu kama Kangomba Waziri Hasunga alisema kuwa tayari serikali imewabaini na wote watachukuliwa hatua za kisheria.


Akizungumzia Pembejeo feki Mhe Hasunga alisema kuwa tayari hatua zimeanza kuchukuliwa kwa wafanyabiashara wote waliofanya hujuma kwa kuwauzia wakulima Mbegu na mbolea feki ambapo hatua kali zimeanza kuchukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kutolipwa fedha wanazodai kwa kusambaza Pembejeo hizo.


Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu Vya Tropiki (TPRI) kutuma wataalamu Mkoani Lindi ili kuchukua sampuli za viuatilifu kwa wakulima na kuvipima ili kubaini kadhia ya usambazaji wa viuatilifu feki kwa wakulima.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Dkt Christine Ishengoma (Mb) amemuagiza Waziri wa Kilimo kuhakikisha kuwa taarifa ya malipo ya wakulima wote wa Korosho inafika bungeni tarehe 2 Aprili 2019.


KILIMANJARO WAANZA MAADHIMISHO WIKI YA MAJI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI

0
0
Mkurugenzi wa Halmashaur ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi(katikati) akiwa na Afisa wa Bonde la Pangani , Segule Segule (Kushoto) kwa pamoja wakishiriki zoezi la kufanya usafi katika soko la Mbuyuni ikiwa ni uzinduzi rasmi ya wiki ya Maji .
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi,Bonde la Maji la Pangani,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakishiriki katika zoezi hilo lililofanyika katika masoko ya Manyema na Mbuyuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michae Mwandezi akifagia katika neo la soko la Mbuyuni.
Afisa wa Maji ,Bonde la Pangani,Segule Segule akifanya usafi katika soko la Mbuyuni .
Afisa wa Maji ,Bonde la Pangani ambao ndio waratibu wa Wiki ya Maji kwa mkoa wa Kilimanjaro ,Segule Segule akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi la usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema.
Baadhi ya  watumishi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi,Bonde la Maji la Pangani,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) walioshirki katika zoezi la usafi kwenye masoko hayo.
Biashara zikiendelea katika soko la Mbuyuni mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Michael Mwandezi pamoja na Afisa wa Maji ,Bonde la Pangani Segule Segule wamewaongoza watumishi kutoka Halmashauri,Bonde la Pangani na Mamlaka ya Maji mjini Moshi (MUWSA) kufanya usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema.

Zoezi hilo lililoanza majira ya saa 12:00 za asubuhi na kudumu kwa saa sita limefanyika ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi Wiki ya Maji Duniani ambayo hufanyika kila mwaka na kuadhimishwa  katika maneo mbalimbali nchini.

Tofauti na miaka iliyopita ,mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro kupitia Ofisi za Bonde la Maji la Pangani ambao ndi waratibu kwa mwaka huu wameanza katika eneo la Mazingira ambalo pia ni sehemu ya kazi zinazotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira  na Ofisi za Bonde
kwa kushirikiana na ofisi za Halmashauri.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika masoko ya Mbuyuni na Manyema ,Ofisa wa Bonde la Maji,Pangani Segule Segule alisema wamechaguliwa kama taasisi itayoongoza maadhimisho ya wiki ya Maji na kwa kuanza limefanyika zoezi la usafi na baadae matukio mengine yatafuata.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi alisema manispaa ya Moshi imekua yenye bahati kutokana na uwepo wa vyanzo vya maji vinavyotosheleza mahitaji ya mji wa Moshi.

"Mwishoni mwa mwaka jana manispaa ya Moshi ilipata ushindi sio kwa Tanzania pekee bali kwa nchi za Afrika MAshariki kuwa ni manispaa inayotoa maji ya kutosha safi na salama,sisi tunabaraka hiyo lazima tumshukuru Mungu"alisema Mwandezi.

Alisema kama ishara ya kuadhimisha wiki ya maji Duniani wameanza kwa kufanya usafi katika masoko na kwamba hali hii ndiyo imekuwa ikiuweka mji wa Moshi kwenye ramani ya miji misafi Afrika.

Katibu Mkuu Susan Mlawi Atoa Maagizo kwa Chuo cha Michezo

0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kulia) akitoa maelekezo kwa uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kuweka alama za mipaka madhubuti badala ya Mawe katika mipaka ya maeneo ya Chuo hicho, alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana kwa lengo la kutambua mipaka ya Chuo hicho pamoja na kuzungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo hicho,wakwanza kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya BW.Richard Mganga.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kushoto) akifanya ziara ya kukagua mazingira ya hostel za wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana,watatu kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi.



Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wapili kulia) akiwa anatoka kukagua mazingira ya choo katika moja ya hosteli za Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana, anayeongoza kutoka ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga.


Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (wakwanza kulia) akikagua mipaka ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza alipofanya ziara ya kikazi Chuoni hapo jana, katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo jijini Mwanza (hawapo pichani) jana alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga,na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi.
Mhasibu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Mustapha Majura akimwomba Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (hayupo pichani) kupatiwa nafasi ya kusoma kozi fupi kwa mwaka ujao wa fedha za masuala ya uhasibu kufuatia mifumo utendaji wa kazi za uhasibu sasa kubadilika na kuwa za kieletroniki wakati wa kikao cha Wafanyakazi wa chuo hicho na Katibu Mkuu huyo jana alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (aliyeketi wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza mara baada ya kumaliza kikao na Wafanyakazi hao jana alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho kilichopo jijini Mwanza,aliyeketi( wa tatu kushoto ) ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Richard Mganga na (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw.Orest Mushi kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya alipofanya ziara ya kikazi katika Chuo hicho kilichopo Jijini Mwanza jana.

……………………………

Anitha Jonas – WHUSM ,Mwanza

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ameutaka uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kupanda miti ya mbao kwa maeneo ya wazi ya chuo hicho badala ya kuacha ardhi hiyo bila matumizi rasmi.

Katibu Mkuu Mlawi ametoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo Mkoani Mwanza kwa lengo la kuzungumza na uongozi na wafanyakazi wa chuo hicho mambo mbalimbali ikiwemo kuweka mikakati ya kuboresha chuo hicho pamoja na kujua mipaka ya chuo hicho.

“Chuo hichi kina eneo kubwa sana ekari 161 ni nyingi na eneo hili lote haliwezi kuendelezwa sasa hivi hivyo ni vyema mkapanda miti ya mbao itakayo wasaidia kuongeza kipato cha chuo na kupata rasilimali fedha itakayo wasaidia kufanya maendeleo katika chuo hichi wasalianeni na Wakala wa Misitu Tanzania watawashauri aina ya miti inayofaa kwa ardhi hii,”alisema Bibi.Mlawi.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ameusistiza uongozi wa Chuo hicho kufanya vikao na wafanyakazi wake pamoja na wanafunzi wa chuo hicho mara kwa mara ilikuweza kusikiliza kero zao na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali,pia amewasihi watumishi hao kuzingatia maadili ya utumishi wa umma pamoja na kuwa na nidhamu kazini.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Richard Mganga hicho alieleza kuwa Chuo hicho kimekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madai mbalimbali ya watumishi ,uhitaji wa kuchimba kisima cha maji ilikuweza kuwa na maji ya kutosha kufuatia ongezeko la wanafunzi wa Chuo hicho.

“Udahili wa Wanafunzi kwa Mwaka huu umeongezeka na kufikia 261 na hivyo kulingana na miundo mbinu tuliyokuwa nayo awali kuwa na uwezo mdogo tumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ya kutosha,hivyo tunaomba tusaidiwe kupata fedha za kuchimba kisima cha maji mapema ili kuondokana na kero hii,”alisema Mganga.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Chuo alitoa wito kwa watu kujitokeza kujakusoma Kozi mbalimbali za Michezo kwani Chuo hicho kinafundisha Diploma ya Uongozi na Utawala katika Michezo,Diploma ya Elimu ya Michezo pamoja na Diploma ya Ufundishaji Michezo

Pamoja na hayo nae Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Orest Mushi aliwatoa hofu watumishi wa Chuo hicho waliyokuwa na madeni ya malipo ya stahili mbalimbali kuwa hivi karibuni malipo hayo ya madeni yatafanyika kwa hazina wanatoa fedha hizo.

Vilevile nae Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Steven Dalasia aliusistiza uongozi huo kuandaa mpango wa manunuzi kwa bajeti ya 2019/2020 ili kupunguza hoja wakati wa ukaguzi wa mahesabu.

Halikadahali nae Mkufunzi wa Chuo hicho Bw.Omari Mataka aliupongeza uongozi wa wizara kwa kufanya ziara chuo hapo pamoja na kuwasililiza kero zao na kutoa majibu ya hoja zao mbalimbali

UTEUZI WA WAKUU WA CHUO KIKUU CHA DODOMA

LUGOLA AKAGUA NA KUPIMA ULEVI MADEREVA WA MABASI, MALORI MJINI MOROGORO, AZUNGUMZA NA ABIRIA, WAPIGA DEBE KITUO KIKUU CHA MSAMVU

0
0



 Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (wapili kulia) akiwa ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu, mjini Morogoro, wakati alipokuwa anafanya ukaguzi na kupima kilevi kwa madereva wa mabasi kituoni hapo pamoja na wa malori katika barabara ya Morogoro-Dodoma. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.
B
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kulia) akiangalia zoezi la upimaji wa kilevi kwa dereva wa basi la Kimbinyiko, Omary Sauli (katikati). Dereva huyo hakuwa na kilevi chochote na aliruhusiwa aendelee na safari yake
C
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akiwauliza maswali abiria wa basi la Kimbinyiko kuhusiana na mwendokasi wa dereva wa basi hilo, na pia kuwapa elimu kuhusiana na kujua haki zao wanapokuwa safarini. Abiria hao walimweleza Waziri huyo dereva huyo yupo makini na pia walimshukuru kwa kufanya ukaguzi kwa mabasi mbalimbali nchini.
D
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akitoka ndani ya basi la Kimbinyiko kufanya ukaguzi na kuzungumza na abiria wa basi hilo, mjini Morogoro, leo. Abiria hao walimweleza Waziri huyo dereva huyo wa basi hilo yupo makini na pia walimshukuru kwa kufanya ukaguzi kwa mabasi mbalimbali nchini.
E
  1. Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na madereva wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu, Mjini Morogoro, leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kituo hapo kwa ajili ya kukagua na kupima kilevi kwa madereva wa mabasi kituoni hapo. Pia Lugola aliwapima madereva wa malori barabara kuu ya Morogoro Dodoma. Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………………..

Na Felix Mwagara, MOHA, Morogoro.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amefanya operesheni kubwa ya kukagua na kupima ulevi wa pombe kwa madeveva wa mabasi na malori mjini Morogoro, leo.

Lugola pia alizungumza na abiria wa mabasi hayo, pamoja na viongozi wa madereva waliopo stendi kuu ya mabasi Msamvu, mjini humo, ambapo walimwelezea kero mbalimbali zinazowakabili.

Ukaguzi wa mabasi na malori hayo ulifanyika barabara kuu itokayo Dodoma kuja Morogoro-Dar es Salaam ambapo Waziri huyo akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa huo (RPC), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa huo (RTO), alisimamisha vyombo hivyo vya moto vilivyokuwa vinaingia Mizani iliyopo eneo la Kihonda, nje kidogo ya Mji wa Morogoro.

Akizungumza na madereva, kondakta, wapiga debe na abiria mara baada ya kufanya ukaguzi huo, Lugola alisema ni wajibu wake kufanya hivyo katika hatua ya kupunguza kwa kasi ajali mbalimbali zinatokana kwa uzembe wa madereva nchini.

“Mimi ni Waziri wa vitendo, nikiagiza nataka nitekelezwe, na pia nikiahidi lazima nilifuatilie, niliwaambia nitakua nakuja kufanya ukaguzi muda wowote ambao hamuujui, na ninafanya hivi kwa lengo moja tu, kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa ikiwa ni hatua ya kumaliza kupunguza au kumaliza kabisa ajali za barabarani hapa nchini,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, kwasasa ajali zimepungua nchini, hasa Mkoa wa Morogoro, kwasababu ya askari wa usalama barabarani kufanya kazi zao kiweledi, na pia madereva kufuata sheria za usalama barabarani.

Lugola aliwataka madereva nchini, kuacha uendeshaji wa mashindano, kuwa na leseni na pia kuhakikisha wanapokuwa barabarani wanakua makini kwasababu ya kuwabeba abiria au mizigo mbalimbali wanayoisafirisha sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi.

“Madereva wa mabasi na malori ambao nimefanikiwa kuwapima kilevi leo, ambao wasiopungua sita, sijawakuta na kilevi, wapo makini na hii inaleta nguvu na imani kuwa madereva wanaelewa na kuzingatia sheria za usalama barabarani, na pia ndani ya mabasi niliyokuwa nayakagua nimezungumza na abiria wakaniambia madereva wanaendesha vizuri na pia niliwakuta wamevaa mikanda, naamini safari yetu ya kuondoa ajali za barabarani tunazidi kufanikiwa,” alisema Lugola.

Wakizungumza kwa wakati tofauti katika stendi kuu ya mabasi, madereva walilipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kwa usimamizi mzuri ambao umewaunganisha na kuwafanya waifurahie kazi wanayoifanya.
Dereva Juma Rashidi wa basi linalosafiri kutoka Ifakara kuja Morogoro, alisema wanajisikia furaha kubwa kwa uongozi mpya wa Jeshi la Polisi ulioletwa Mkoani Morogoro hivi karibuni.  

“Naomba niseme ukweli, RPC na RTO hakika wanatuongoza vizuri, hakuna kero za ajabu kama zamani, tupo huru kufanya kazi zetu, hii inaonyesha viongozi hawa wanataka tufanye kazi ili tuweze kupata riziki zetu kwa njia halali bila usumbufu wa kusumbuana kama ulivyokuwa siku za nyuma,” alisema Rashidi.

Lugola alifanya ziara katika kituo hicho, na baadaye kutoka nje ya kituo hicho kuyakagua mabasi na malori, mara baada ya kumaliza ziara yake aliyoifanya Wilayani Kilosa ya kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Tarafa ya Kimamba wilayani humo, juzi.

WANAFUNZI WA KIKE WATAKIWA KUJIKINGA NA MIMBA ZA UTOTONI MKOANI IRINGA

0
0
Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi akipokea taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus wakati wa mahafali ya klub za FEMA yaliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana ya Ifunda mkoani Iringa.
Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza kwenye mahafali hayo ya klabu za FEMA 
Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi akiwa katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus pamoja na wageni wengine wakelekea ukumbini kwenye sherehe za mahafali ya klabu za FEMA mkoani Iringa. 



Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi amewataka wanafunzi wa kike kujikinga na mimba za utotoni ili kujijenga malengo mazuri ya hapo baada yenye tija kwa taifa na wao binafsi.

Akizungumza wakati wa mahafali ya club za FEMA yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Ifunda Girls,Ngowi alisema wanafunzi wengi wa kike huacha masomo mapema kutokana na kupata mimba wakiwa bado wapo masomoni hivyo ni lazima mjijengee malengo.

“nimetembea sehemu nyingi nimekuta nimekutana na watoto wakike wengi wameacha shule kwa sababu ya kupata mimba wakiwa shuleni,hivyo hata nyie mnatakiwa kujitunza na kuwa na maisha mazuri na bora kama ambavyo mnatuana baadhi ya wanawake tunafanya vizuri kwa kuwa tulijitunza toka tukiwa shuleni” alisema

Ngowi aliwaambia,starehe na mapenzi vipo siku zote za maisha hivyo lazima mjitambue katika umri huu ndio muda wa kutengeneza dira ya maisha yenu hapo baadae kwa faida yenu.

“Kila mwanamke ambaye mnamuna hivi sasa amefanikiwa ni kutokana na kujitunza walipokuwa wanasoma kama ambavyo nyie mpo hivi sasa,mnatakiwa kujifunza kutoka kwa wanawake walifanikiwa” alisema 

Aidha Ngowi aliwataka wanafunzi kuwa wazalendo na maendeleo ya nchi yao kuwa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa kuwapotosha juu ya ukweli ambao unaendelea kwenye nchi hii,hivyo lazima muwe wazalendo wa kweli kwa kuipenda nchi yetu na kuilinda isiingie kwenye machafuko.

“Ili uweze kufanikiwa katika maisha uzalendo ni japo la kwanza na la msingi kabisa kwenu nyie wanafunzi kwa kuwa ndio taifa la sasa na baadae kwa kuwa mtakuja kuwa viongozi wa kuongaza nchi hii na siwa watu wengi hata sisi ni viongozi ambao tulisoma katika shule kama hizi ambazo nyie mnasoma hivi sasa” alisema 

Akiwa katika mahafali hayo mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi aliwachangia viongozi shilingi laki mbili kwa ajili ya kuwawezesha kuweza kufika katika maeneno ambayo wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanafunzi hao zaidi ya mia nane wa mkoani Iringa.

Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi, katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus alisema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za kuendeshea semina mbalimbali wa walimu walezi wa mkaoni Iringa.

“Tunakosa pia fedha za kuendeshea matamasha mbalimbali yenye kubeba ujumbe mzuri katika jamii,ukosefu wa ofisi ya FEMA mkoa wa Iringa” alisema .Tunus alisema kuwa mikakati yao ni kuhakikisha wanaandaa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi wananchama wa FEMA yatakayo kuwa yanahusisha shule za sekondari tano za mkoa wa Iringa.

“Tutaendelea kushirikiana na serikali katika kuwalea vijana katika maadili mema na kuhakikisha FEMA klabu zinaenea katika shule zote za sekondari hapa mkopani iringa” alima Tunus

MAJALIWA AFUNGUA SOKO LA DHAHABU MJINI GEITA

0
0
WazirI Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika kipande cha dhahabu mali Mchimbaji Mdogo Bw. Christopher Thadeo (kushoto) chenye uzito wa gramu 141.01 kikiwa na thamani ya sh. 13,537, 439/= wakati alipofungua Soko la Dhahabu mjini Geita, Machi 17, 2019. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (kulia) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kufungua Soko la Dhahabu mjini Geita, Machi 17, 2017. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaji Said Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko baada ya kufungua Soko la Dhahabu mjini Geita, Machi 17, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita, Alhaji Said Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



WAZIRI MKUU AWATAHADHARISHA WADAU WA MADINI

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa atakayekamatwa anatorosha madini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha. 

Pia amewataka viongozi na watendaji wote wa Serikali wasimamie kwa weledi, uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo kuhusu sekta ya madini kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa madini hususan dhahabu kwenda nje ya nchi.

Waziri Mkuu ametoa tahadhari hiyo leo (Jumapili, Machi 17, 2019) wakati akifungua soko la madini la Mkoa wa Geita. Ufunguzi wa soko hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilotoa tarehe 22.01.2019 la kuitaka mikoa yote ianzishe masoko ya madini.

Waziri Mkuu ameitakaWizara ya Madini, Tume ya Madini, Serikali ya Mkoa, Idara na Taasisi nyingine za Serikali zinazohusika na maendeleo ya sekta ya madini waheshimu mipaka ya majukumu yao ili waweze kulisimamia vizuri soko hilo na kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

“Wizara ya Madini ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuandaa mpango kazi mahsusi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya soko hili ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya kwa wachimbaji na wafanyabishara wa madini”

Waziri Mkuu ameviagizaVyombo vya Ulinzi na Usalama vihakishe soko hilo linapata ulinzi wa kutosha muda wote ili watendaji, mali zitakazokuwemo, vitendea kazi na miundombinu yote iwe salama muda wote. “Mkuu wa mkoa na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, nawaagiza hakikisheni Suala hili mnaliandalia utaratibu haraka iwezekanavyo”.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuielekeza mikoa mingine yenye kiwango kikubwa cha uzalishaji wa madini hususan ya metali na vito iharakishe uanzishwaji wa masoko ya madini sanjari na miundombinu yote muhimu ili masoko hayo yaanze kufanya kazi kabla ya kwisha kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Amesema anaamini kwamba, usimamizi mzuri wa soko hilo na masoko mengine ya madini yanayoendelea kuanzishwa nchini utaimarisha makusanyo ya kodi za Serikali na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa. Vilevile, amesema wafanyabiashara wa madini, hususan kutoka nje ya nchi wataongezeka kwa sababu tutakuwa tumewaepusha na matapeli na vikwazo vingine vya kibiashara. “Uimara wa soko hili pia, utaboresha uhusiano kati ya wadau wa biashara ya madini na Serikali”.

Waziri Mkuu amesema Serikali imefuta baadhi ya tozo na kodi ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo. Miongoni mwa tozo zilizofutwa ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio ya asilimia tano ya mwisho (final withholding tax) inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote.

Amesema baada ya kufutwa kwa kodi na tozo hizo Serikali inatarajia kuwa utoroshwaji wa madini utapungua, pia kutasaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini; kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato kwa nchi. 

“Nitoe wito kwa wachimbaji wote wadogo kwamba endeleeni kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yenu kwa kufuata taratibu, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali”. AmesemaSerikali inachukua hatua zote hizo si kwa lengo jingine bali kuziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi, na hivyo, kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi yetu. 

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vema katika kuhakikisha vikwazo vyote vilivyomo katika mnyororo wa biashara ya madini vinaondolewa kwa lengo la kukuza sekta hiyo na kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla. Amesema Serikali imeamua kutoa mwelekeo mpya katika usimamizi na maendeleo ya sekta ya madini. “Utekelezaji wa dhamira hii unakwenda sambamba na kuweka mazingira mazuri na miundombinu itakayowezesha kuimarika kwa sekta ya madini nchini”. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa masoko ya uhakika ya madini ambao umekuwa sababu ya utoroshwaji madini, hivyo kuanzishwa kwa soko hili kunawahakikishia wachimbaji wadogo masoko na kukua kwa kipato kutokana na shughuli za madini.

Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na malalamiko ya kudhulumiwa au kupunjwa kutoka kwa baadhi ya wachimbaji wadogo, vitendo hivyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu. “Ndugu wachimbaji wadogo, soko hili linakwenda kuwa mwarobaini wa tatizo hilo kwani litasheheni vifaa vya kupimia uzito na ubora wa madini kabla hayajauzwa. Naielekeza Tume ya Madini, isimamie ipasavyo vifaa na taratibu za vipimo kwenye soko hili na kuhakikisha hakuna manung’uniko juu ya utendaji kazi wa vifaa hivyo”. 

Waziri Mkuu ameongeza kuwa soko hilo pia litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana. “Nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko hili kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli”.

Pia ameiagiza Tume ya Madini kuratibu bei za madini ndani ya soko hilo na ihakikishe mchimbaji anapata stahiki zake, Serikali inapata mapato yake na mfanyabiashara naye ananufaika. “Tunaimani kabisa tatizo la kudhulumiana na kupunjana linaenda kwisha kabisa. Na kwa kweli ikitokea mtu amepunjwa, atakuwa amejitakia mwenyewe”.

“Ndani ya soko hili kutakuwa na huduma zote muhimu kwa mfanyabiashara ikiwemo huduma za Tume ya Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mabenki na nyinginezo, hivyo kuokoa muda na gharama nyingine katika kuendesha biashara hii ya madini. 

Amesema soko hilo litasaidia sana katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na takwimu za biashara ya madini. Hivyo, niwasihi wachimbaji wa madini kulitumia soko hili na kuacha vitendo vya utoroshaji wa madini. Serikali kwa upande wake, haitomvumilia mtu yeyote yule atakaye jihusisha na utoroshaji wa madini. 

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Wabunge wa mkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robertt Gabriel, wakuu wa mikoa jirani na maafisa wa Serikali.

RMO SIMANJIRO AWAASA WENYEVITI

0
0
WENYEVITI wa Vitongoji na Vijiji wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wametakiwa kutokwamisha shughuli za serikali kwa kutoa matamko yasiyo na tija kwenye machimbo ya madini.

Ofisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima aliyasema hayo wakati akizungumza na wachimbaji wa madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo.

Ntalima alisema wenyeviti hao wanapaswa kutambua kuwa Rais John Magufuli akishatoa maelekezo hawapaswi kuyakwamisha kwa kutoa kauli tofauti. Alisema baadhi ya wenyevi wanatoa maagizo yasiyo na tija ambayo yanakinzana na kauli ya Rais Magufuli ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. 

"Hili ni eneo la uchimbaji madini, Mwenyekiti wa kijiji au kitongoji hana mamlaka ya kutoa matamko ya kuwachangisha watu sh15,000 au kuwaagiza waendelee kwenye mkutano kilomita 18 kutoka hapa," alisema Ntalima. Alisema viongozi hao wanapaswa kushirikiana na ofisi ya madini endapo kuna jambo wanataka kulifanya kwenye maeneo ya madini yenye leseni kuliko kujiamulia wao wenyewe. 

"Rais Magufuli amewapa unafuu wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwasamehe kodi sasa anapotokea mwenyekiti wa kijiji anawachangisha fedha lazima tuingilie kati," alisema Ntalima. 

Mwenyekiti wa chama cha wachimba madini mkoa wa Manyara (Marema) Tawi la Lemshuku, Bernard Kasanu alisema wenyewe wana haki ya kuchimba na siyo kuwekewa vikwazo vya kisiasa visivyo na tija. Kasanu alisema wamekuwa wakipata vikwazo vingi kutoka kwa uongozi wa kijiji ikiwemo huduma ya maji ambayo hivi sasa imesimama. 

Mchimbaji wa madini ya Green, Charles Shoo alisema viongozi wa wizara ya madini na kijiji wangekutana ili wapeane utaratibu wa suala hilo kwani wananchi wamebakia njia panda. Shoo alisema tatizo hilo ni la muda mrefu hivyo ni wakati muafaka wa kufanyiwa kazi ili lipatiwe ufumbuzi wa kudumu. 

Hata hivyo, mmoja kati ya wachekechaji wa madini hayo Shedrack Ibrahim alisema viongozi wa vijiji na vitongoji wanapaswa kutoa kipaumbele kwenye huduma za kijamii kuliko kuwachangisha fedha bila utaratibu wowote. 

Ibrahim alisema machimbo hayo hayana sehemu za kuwazikia wenzao wanapokufa hivyo wanaomba serikali iwatengee sehemu ya maziko machimboni. Mkoa wa kimadini wa Simanjiro unaongoza kwa kuwa na madini mengi katika mkoa wa Manyara, ikiwemo Tanzanite, Rubby na Green.
Ofisa madini mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima akikagua migodi ya madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo. 
Maofisa wa Tume ya madini, wakikagua migodi ya madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. 
Ofisa madini mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima akizungumza na wachimbaji madini ya Green kwenye machimbo ya Lemshuku Kata ya Komolo. 
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images