Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

TAA WAJIDHATITI NA UENDESHAJI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA

$
0
0
 Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.

 Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.

 Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.

 Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.

 Baadhi ya Maeneo ya Jengo la III la abiria yanavyoonekana ikiwa ujenzi umefikia kiwango cha asilimia 95.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Bw, Paul Rwegwasha akitoa taarifa fupi ya Mamlaka kuhusu mpango wa  usimamizi na uendeshaji jengo la III la abiria kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo mapema leo.

 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu  ambaye ni Mbunge wa Kasulu mjini Mhe, Daniel Nsanzugwako (mwenye kofia) akiuliza swali mara baada ya kusomwa taarifa ya mradi wa Jengo la III la abiria wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo mapema leo.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa (Mb) akijibu hoja maswali mbalimbali ya kisera kwa wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria  mapema leo.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye alipokuwa akijibu maswali kwa wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la III la abiria  mapema leo aliekaa kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi Selemani Kakoso. 


Mhandisi Burton Komba kutoka Wakala wa Barabara akitoa maelezo ya Ujenzi wa Jengo la III la abiria kwa Wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara katika Jengo hilo mapema leo.




MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imebainisha kwamba itakua tayari kwa ajili ya utoaji wa huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria pale mradi wa Ujenzi utakapokuwa umekamilika.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha alipokua akitoa taarifa fupi ya TAA kwa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu ilipofanya ziara katika eneo la Ujenzi huo.

Bw. Rwegasha amesema hatua mbalimbali za Maandalizi tayari zimeshachukuliwa kwa kushirikiana na wadau wa huduma hizo, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo yanayohitajika kwa watendaji wa ngazi mbalimbali.

“Mamlaka inaendelea kufanya taratibu za maandalizi ya utoaji huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria, katika mpango huo tayari mafunzo kwa watendaji mbalimbali yameanza na hivi sasa watendaji 40 wapo Korea ya kusini katika mafunzo” amesema Bw. Rwegasha.

Aidha Bw. Rwegasha amebainisha kwamba katika utekelezaji mpango wa uhamishaji shughuli, Mamlaka imejipanga kuhakikisha hakuna madhara yeyote ya kiuendeshaji yanajitokeza.

“Mamlaka itahakikisha kwamba inazuia athari zote zinazoweza kutokana na zoezi la uhamishaji wa shughuli za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa Ndege na abiria, uharibifu wa mitambo,madhara ya kiusalama na kadhalika.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Idara ya Viwanja vya Ndege katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Emmanuel Raphael amebainisha kwamba hadi kufika mwezi February 2019 utekelezaji wa kazi zote ulifikia asilimia 95.

“Ujenzi wa kazi zote za Ujenzi umefikia 95%, ambapo mchanganuo unaonesha kwamba ujenzi wa jengo umefikia 96%, maegesho ya magari 92%, maegesho ya ndege 98% na kwa ujumla kazi zinaenda vizuri na zinatarajiwa kukamilika Mei 31, 2019”, alisema Mhandisi Raphael.

Naye, Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amebainisha kwamba mpaka sasa Wananchi wa Kipawa waliopisha upanuzi wa Kiwanja wameshalipwa fidia na kwamba mpaka sasa hamna mgogoro wa fidia.

Akitoa majumuisho baada ya ziara ya kamati katika eneo la ujenzi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Mhe. Seleman Kakoso amesema kwa ujumla Kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kwamba wameridhishwa na namna pesa ya serikali ilivyotumika.

“Kwa ujumla Kamati imeridhishwa na hatua ya Ujenzi iliyofikiwa, matumizi ya pesa ya Serikali yanaonekana ni mazuri, lakini natoa wito kwa TAA kuongeza kasi ya maandalizi ili kwenda sawa na kasi ya ujezi huu, lakini pia mjipange kuongeza wafanyakazi ili kuhakikisha kwamba watendaji wa huduma za uendeshaji wanajitosheleza”, amesema Mhe. Kakoso.

TCRA Kanda ya Mashariki yatoa elimu Shule ya Sekondari Minaki

$
0
0
 Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mashariki imesema kuwa njia ya bora ya kufanya watumiaji wa mawasiliano kufuata sheria na taratibu za mawasiliano hayo ni kuwapa elimu.

Hayo aliyasema Mkuu wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mlaji Duniani ambapo Kanda hiyo ilitoa elimu katika shule ya Sekondari Minaki iliyopo Kisarawe mkoani Pwani amesema wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita ndio wanaingia katika utumiaji wa mawasiliano hivyo lazima wapewe elimu ya kutosha katika kutumia mawasiliano hayo.

Odiero amesema wanafunzi wakipata njia bora ya utumiaji wa mawasiliano wanakuwa chachu katika kuelimisha watu wengine kutokana na uelewa wao kuwa mkubwa.Amesema katika maadhimisho ya siku ya haki ya walaji duniani inatoa fursa katika TCRA kuwa na muendelezo ws kutoa elimu ya mawasiliano kwa wadau ili wajue sharia mbalimbali za mawasiliano hayo ili yasitumike visivyo na kuondoa maana ya mawasiliano.

Amesema katika kuelekea uchumi wa viwanda mawasiliano ni njia ya kufungua fursa ya watumiaji wa mawasiliano hayo kutengeneza ajira kutokana na teknolojia iliyopo katika mitandao ya simu.Aidha amesema kuwa sheria iliyopo kwa kampuni za simu ni kuhakikisha wanatoa huduma bora ya mawasiliano na wale ambao wanakiuka sheria kushika mkondo wake.

Amesema watumiaji wa mawasiliano wanatakiwa kutuma ujumbe wenye maadili na wanaofanya kutuma ujumbe wa uchochezi,matusi kufunguliwa mashitaka mahakamani lengo ni kufanya mawasiliano kuwa salama.

"Dunia hii imekuwa kijiji kutokana na mawasiliano hivyo kila kitu kinachofanyika kiendane na maadili yetu nchini pamoja na watu wengine wajifunze kwani sio kila kitu kiwekwe katika mawasiliano na njia rahisi kila mtu anayepata ujumbe usiofaata maadili hayo ni kufuta"amesema Odiero.

Nae Mwalimu wa Shule ya Sekondari Minaki Sweatbert Kijumba amesema wanafunzi wakipewa elimu ndio nguzo ya kufanya nchi kuwa na mawasiliano salama kwani wenyewe ndio wanaingia kwa kasi katika utumiaji wa mawasiliano.

Amesema Teknolojia ya mawasiliano inabadilika hivyo TCRA iendelee kutoa elimu katika makundi mbalimbali ili watumiaji wajue sheria za mitandao kwa kuwafikia moja kwa moja.Kwa upande wa Afisa Masoko wa TCRA Joyce Paul amesema kuwa wanafunzi wakipata uelewa wa matumizi ya simu ndio mabalozi wa kuelimisha jamii katika ngazi za familia.

 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ikiwa ni maadhimisho ya Siku Haki ya Walaji ambayo hufanyika kila Machi 15 ya kila Mwaka.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakiwasikiliza TCRA Kanda ya Mashariki wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani ambayo hufanyika Machi 15 ya Kila Mwaka.
 Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Joyce Paul akitoa maelezo kuhusiana utendaji wa mamlaka katika udhibiti wa mawasiliano wakati Kanda ya Mashariki TCRA ilipokwenda kutoa elimu katkka shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
 Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TCRA Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyofatilia mawasiliano wakati akitoa elimu katika Shule ya Sekondari Minaki ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.
 Mwalimu wa Shule ya Sekindari Minaki Sweatbert Kijumba akitoa maelezo juu ya ujio wa TCRA Kanda ya Mashariki katika shule hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Haki Mlaji Duniani.

KAMATI YA BUNGE UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YAKAGUA MAENDELEO MIRADI YA GESI ASILIA JIJINI DAR

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakipokea taarifa za maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba (mwenye overall ya bluu) akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya PIC kazi ya kusambaza gesi asilia kwa wateja kwa matumizi ya majumbani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni. 
Mhandisi Dora Ernest (alieshika mic ya TBC) akitoa maelezo ya huduma ya kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC). 


Kamati ya Bunge inayosimamia uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mhe. Dkt. Raphael Chengeni ilitembelea kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi na kujionea kazi za kitaalam zinazofanywa na wazawa katika kupokea gesi na kuisambaza kwa wateja mbalimbali wakiwemo wazalishaji umeme. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba akitoa wasilisho juu ya mikakati ya TPDC katika kujiendesha kibiashara alisema “katika mwaka huu wa fedha tunategemea kuanza kutoa gawio Serikalini”. Mhandisi Musomba aliieleza Kamati ya PIC kwamba kwa sasa Shirika liko katika mageuzi makubwa ya kiutendaji nia ikiwa ni kuongeza ufanisi na hatimaye kutengeneza faida itakayoruhusu kutoa gawio kubwa Serikalini. 

Katika kipindi cha miaka mitatu TPDC imekuwa ikijeindesha kwa hasara kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia. 

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Mh. Dkt. Raphael Chengeni alisema “Sisi kama Kamati tumefurahishwa sana na mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika TPDC kwani hili lilikuwa moja ya Shirika ambalo linaonekana kuwa mzigo kwa Serikali kwa kushindwa kutoa gawio kwa Serikali”. 

Dk. Chengeni aliongeza kwamba kwa taarifa waliyopokea TPDC sasa wanaamini mambo yatakuwa mazuri katika Shirika hili ambalo linategemewa sana katika kufikia Tanzania ya viwanda kwa kuzingatia upekee wa bidhaa wanayozalisha, gesi asilia. Wajumbe wengine wa PIC pia walionekana kuridhishwa na utekelezaji wa miradi na mageuzi ambayo TPDC imeshaanza kuyafanya.

Katika ziara hiyo Wabunge walipata nafasi ya kutembelea eneo la Ubungo na kujionea wa mtambo wa kupunguza mgandamizo wa gesi kwa ajili ya kusambaza kwa wateja wa majumbani na viwandani. Pia walitembelea maeneo ya Mlimani City na kujionea zoezi la kuunganisha gesi kwa wateja wa majumbani na baadae kiwanda cha Coca-Cola maeneo ya Mikocheni ambao nao wanatarajiwa kuanza kutumia gesi baada ya kazi ya kuunganisha kukamilika. 

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma inaangalia mambo matatu makubwa, kwanza gawio linalokwenda Serikalini, kupokea mtaji unaozidi na suala la mapato ghafi ambayo ni 15%, alieleza Mwenyekiti wa Kamati, Dk. Raphael Chegeni.

TANROAD WAANZA UPEMBUZI YAKINIFU UJENZI WA BARA BARA YA IGAWA-TUNDUMA.

$
0
0
Na Emanuel Madafa,Mbeya.

Serikali ya Mkoa wa Mbeya,  imesema  wataalamu  kutoka TANROAD, wameanza zoezi laupembuzi yakinifu wa ujenzi wa Barabara ya Igawa-Tunduma.

Imesema tayari tmu ya wataalamu inaendelea na zoezi hilo na kwamba ujenzi huo wa barabara unatarajia kutumia miezi 14.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, ameyasema hayo leo, wakati akielezea hatua mbalimbali ambazo serikali inazifanya kwenye utatuzi wa changamoto za miundombinu ya barabara.

 “Tayari ujenzi wa barabara kipande cha Igawa hadi Mafinga kimekwisha kamilika,  kwahiyo hata hii ambayo imeanza kufanyiwa upembuzi nayo itakamilika kwa wakati “

Hata hivyo kwa mujibu wa Chalamila, amesema pia mchakato wa ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Inyara -Mbalizi  kwa ajili ya matumizi ya magari makubwa ya mizigo unaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila,

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKISALIMIA WANANCHI KIJIJINI KWAKE NANDAGALA WILAYANI RUANGWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na dada yake, Fatma Majaliwa kijijini kwake Nandagala Machi 15.2019, kushoto ni mtoto wa dada yake Hidaya Rashid.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na vijana waendesha bodaboda kijijini Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi bakora mwanakijijini wa Nandagala Mzee Khamis Kandege Machi 15.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kisima cha maji safi, katikakijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru Halima Athumani (kulia) na Zuena Bakari (katikati) kwa zawadi yamahindi, katika kijiji cha Nandagala Wilayani Ruangwa Machi 15.2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia watoto, katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na vijana kijijini kwake Nandagala wilayani Ruangwa Machi 15.2019

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Bi. Fatu Omar kijijini kwake Nandagala Machi 15.2019, aliye soma nae darasa moja shule ya msingi
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na mmoja wa Watoto waliopo kijijini kwake Nandagala 

LUGOLA AWATULIZA WANANCHI WENYE HASIRA WANAOGOMBEA ARDHI KILOSA, ASEMA WANASHERIA FEKI CHANZO CHA MIGOGORO HIYO

$
0
0
 WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto), akisoma moja ya bango liloandikwa na wananachi kabla ya kuanza mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, alipofika katika tarafa hiyo kwa lengo ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo inaleta uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Adamu Mgoyi. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akizungumza na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, alipofika katika tarafa hiyo kwa lengo ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo inaleta uvunjifu wa amani katika eneo hilo. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi.
 WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza mwakilishi wa wananchi katika Tarafa ya Kimamba, Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro, akisoma hukumu zilizotolewa na mahakama kuu na ya rufaa ambayo inaonyesha Mfuaji Lipasio Mbokoso (hayupo pichani) wa Tarafa hiyo alishinda kesi hiyo dhidi ya wananchi wachache waliofungua kesi ya ardhi wakidai ni mali yao. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mkazi wa Tarafa ya Kimamba, Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro, Iris Diamond, akitoa kero yake kuhusiana na mgogoro wa ardhi kati yake na wananchi wa Tarafa hiyo. Lugola alisema chanzo ya migogoro ya ardhi Wilayani humo ni kutokana na kuibuka wanasheria feki ambao wanawarubuni wananchi kushindwa kufauata sheria za nchi  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.




Na Felix Mwagara, Kilosa

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ametumia saa tano kuwatuliza wananchi wa Tarafa ya Kimamba Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, ambao walikuwa na hasira kali wakilalamika kunyang’anywa ardhi na wafugaji pamoja na Polisi kuwanyanyasa wananchi hao kwa kuwaweka ndani.

Waziri Lugola ambaye aliwasili saa sita mchana akitokea mjini Morogoro kwa ajili ya kutekeleza ahadi yake kwa wananchi hao baada ya kuwaahidi wiki iliyopita alipofanya ziara katika Tarafa hiyo ambayo ina wakazi zaidi ya elfu hamsini, ili aweze kutatua kero zao za ardhi wakiwa na nyaraka zao za uthibitisho.

Kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi hao, Waziri huyo alifanya kikao cha ndani na viongozi wa Wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya, kwa lengo viongozi hao kumpa sura halisi ya mgogoro huo ambao unaelekea katika uvunjifu wa amani.

Lugola aliwasili eneo la mkutano mara baada ya kumaliza kikao cha ndani, ambapo alipokelewa na mabango ya wananchi ambayo yalikuwa yameandikwa ujumbe mbalimbali ikiwemo ‘Polisi wa Dumila wanatumika kuwanyanyasa wananchi na polisi wa Chanzulu wanakamata watu na kuwaweka ndani wananchi wanaotafuta haki ya ardhi’, wafugaji wanapora ardhi zetu, polisi wanapewa rushwa na wafugaji kutuweka ndani’. 

Akizungumza na mamia ya wananchi hao, Lugola alisema amekuja kusikiliza kero za wananchi hao baada ya kutoa ahadi yake wiki iliyopita, hivyo anatumaini wananchi hao wanavielelezo kama alivyowaagiza waje nazo katika mkutano huo.

Lugola alisema Jeshi la Polisi alihusiki na masuala ya ardhi isipokuwa limekua likichukua hatua pale migogoro hiyo inapopelekea kwenye uhalifu ama uvunjifu wa amani.

Lugola alishangiliwa na wananchi hao alipowaita waje mbele ya meza kuu ili waweze kutoa kero zao, ndipo idadi kubwa ya wananchi hao waliitikia wito huku baadhi yao wakiwa na nyaraka mbalimbali kama walivyoelekezwa na Waziri huyo waje nazo katika mkutano huo.

Licha ya wananchi hao kutoa kero mbalimbali lakini tatizo kubwa walikuwa wanamtuhumu mfugaji maarufu ambaye ni Mmasai katika Wilaya hiyo, Lipasio Mbokoso, anayedaiwa kunyang’anya ardhi zaidi ekari 270 ambazo wanadai sio zake lakini anatumia nguvu ya fedha kuichukua ardhi ya wananchi hao.

Waziri Lugola alimwita Mbokoso katika mkutano huo ili aweze kujitetea kwa nyaraka zake, ndipo ikajulikana kuwa Mmasai huyo ardhi hiyo ni mali yake halali baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa na wananchi hao mahakamani. 

“Nyaraka zinaonyesha Mbokoso ni mmiliki halali wa ardhi hii, na pia wananchi ambao nimewataja walifungua kesi, na Mbokoso akashinda kesi hiyo mahakama kuu, baadaye mkakata rufaa mkaenda mahakama ya rufaa, pia akashinda, ndugu wananchi naomba mueleze na hakuna haja ya malumbano, huyu ni mmiliki halali wa mali hiyo, musidanganywe na mtu yeyote, fuateni sheria pamoja na kuiheshimu hukumu ya mahakama,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, kuna baadhi ya wanasheria feki katika eneo hilo wanawarubuni wananchi kwa kuwapotosha na kuwasababisha munaingia katika migogoro ya ardhi na amani inatoweka katika eneo hilo kwasababu tu ya watu wachache ambao wanawapotosha. 

“Wanasheria feki ndio wanaochangia migogoro ya ardhi katika sehemu mbalimbali ya Wilaya ya Kilosa, nawataka wananchi kutowatumia badala yake mufuate sheria kama inavyoelekeza,” alisema Lugola.

Kutokana na matatizo ya ardhi kuendelea kutokea katika eneo hilo, Waziri Lugola amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Wilbroad Mutafungwa kuchunguza nyaraka zote za migogoro ya ardhi inayowasilishwa na wananchi ili kujua kama ni halali au zimeghushiwa.

Sambamba na hilo, Lugola amemtaka Kamanda huyo kuwachukulia hatua kali za kinidhamu askari wote wasiokuwa waadilifu katika eneo hilo na Mkoa kwa jumla, watakaohusika kuwanyanyasa wananchi hasa katika masuala ya ardhi. 

Kauli ya Waziri huyo ilileta furaha kwa sehemu kubwa ya wananchi hao licha ya kuwa baadhi yao wakilalamika kuwa, Polisi wameshindwa kutatua kero zao na kuwadharau wakulikuma na kuwathamini wafugaji, hata hivyo Waziri huyo aliahidi kufuatilia mara kwa mara amani ya eneo hilo.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA KONGAMANO LA KUMPONGEZA DKT SHEIN

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tayari amewasili kwenye Kongamano la Kumpongeza Dkt. Ali Mohammed Shein Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika uwanja wa Hoteli ya Verde, leo tarehe 16 Machi, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka ,wakati akiwasili kwenye Kongamano la Kumpongeza Dkt. Ali Mohammed Shein Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika uwanja wa Hoteli ya Verde, leo tarehe 16 Machi, 2019.

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAVUTIWA NA MAFANIKIO YA TASAF MKOANI MTWARA.

$
0
0
Na Estom Sanga- Mtwara 

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wameridhishwa na mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ambao umeleta hamasa kubwa kwa Walengwa wake kupambana na umaskini. 

Wajumbe wa Kamati hiyo ambao wametembelea kijiji cha Namela katika wilaya ya Mtwara ambako wamepata fursa ya kuonana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kushuhudia namna Walengwa hao wanavyotumia fursa za Mpango huo kujiletea maendeleo. 

Wakiwa kijijini hapo Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wamepata ushuhuda kutoka kwa baadhi ya Walengwa wa TASAF ambao wametumia fursa ya kuwepo kwenye Mpango huo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa mbuzi na Kuku wa Kienyeji kuhamasisha watoto wao kuhudhuria masomo huku wengine wakiboresha makazi yao na kununua vifaa vya umeme jua ( solar systems. 

‘’…….nimetumia fursa ya kuorodheshwa na TASAF kwa kununua mbuzi ambapo hadi sasa nina zaidi ya mbuzi kumi” ninaishukuru sana serikali kwa kuniwezesha kujikomboa amesisitiza mmoja wa walengwa mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo ya bunge. 

Taarifa ya mkoa wa Mtwara imeonyesha kumekuwapo na manufaa ya kujivunia ambayo yamepatikana kutokana na utekelezaji wa shughuli za TASAF mkoani humo hususani katika sekta za Afya, Elimu,Miundombinu,uundaji wa vikundi vya kuweka na kuwekeza akiba na kujiongezea kipato kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi. 

Walengwa hao wa TASAF mkoani Mtwara pia wamehamasishwa kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana vipatavyo 3,070 vyenye jumla ya wanachama 43,872 ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita vikundi hivyo vimefanikiwa kujiwekea akiba ya zaidi ya shilingi milioni 537 na kukopeshana kiasi cha shilingi milioni 409 kwa ajili ya kuwekeza kwenye shughuli za kiuchumi hususani kilimo na ufugaji. 

Akizungumza kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati hiyo Mwenyekiti wake Mheshimiwa Steven Rweikiza amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwapunguzia Wananchi na adha ya umaskini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF. 

Hata hivyo kilio kikubwa ambacho kimekuwa kikipazwa sauti na Wajumbe wa Kamati ,Viongozi na Wanachi kwenye maeneo mengi nchini ni sehemu ya Wananchi ambao bado wanaishi kwenye hali ya umaskini ambao bado hajapata fursa ya kujumuishwa kwenye huduma za Mpango wa Kunusuru Kasya Maskini. 

Kwa nyakati tofauti Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Kapteini Mstaafu George Mkuchika amekuwa akisisitiza azma ya serikali ya kuhakikisha kuwa katika utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru kaya maskini vijiji /shehia na wananchi ambao watakidhi vigezo vya kuorodheshwa kwenye Mpango wanapata fursa hiyo . 

 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya bunge ya kudumu ya bunge ua utawala na serikali za mitaa wakifurahia maelezo baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Namela mkoani Mtwara.

 Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe.Venance Mwamoto (aliyevaa shati jeupe) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga aliyenyoosha mkono wakiwa na mmoja wa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Namela wilaya ya Mtwara mbele ya nyumba aliyoijengwa kwa kutumia fursa za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.




 
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu ya Utawala na serikali za mitaa Mhe. Steven Rweikiza (mwenye Kaunda suti) akiwasikiliza  Walengwa wa TASAF wakielezea mafanikio waliyoyapata baada ya kujumuishwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Namela mkoani Mtwara.


Wanafunzi watembelea ofisi za Vodacom Tanzania kupata mafunzo ya ufanyaji kazi kidigitali

$
0
0

Meneja Mawasiliano na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Christina Murimi, akigawa vifaa kwa wanafunzi waliotembelea ofisi za Vodacom kujifunza juu ya utendaji kazi wa kidijitali wa kampuni hiyo. Katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao wa kike kutoka shule mbalimbali na kuwapatia mafunzo ya ufanyaji kazi wa kidijitali katika idara na vitengo vya kampuni hiyo.
Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania PLC, Grace Chambua akizungumza juu ya umuhimu wa elimu kwa wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za kanda ya kati walipotembelea ofisi za kampuni ya Vodacom jijini Dodoma. Katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Vodacom iliwakaribisha wanafunzi hao na kuwapatia mafunzo juu ya ufanyaji kazi wa idara na vitengo mbalimbali katika sekta ya mawasiliano.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya VodaCom Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Macfydene Minja (kushoto) akionesha bango lenye orodha ya viwango vya kutoa pesa vinavyotozwa wakati wa kutoa fedha kwenye Mpesa kwa wanafunzi wa Sekondari kutoka mikoa saba ya kanda hiyo ambao wamechaguliwa katika mradi wa Interantional Girls in ICT kwa ajili ya kushindani katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Wasichana ya TEHAMA, walipofika katika makao makuu ya Vodacom kanda hiyo zilizopo Uhindini Jijini Mbeya ili kujifunza.


RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA AMBAYE NI MJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS WA UGANDA

$
0
0
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni iliyowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa wapili kutoka kushoto, Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero pamoja na Balozi Zuhura Bundala mara baada ya mazungumzo na mjumbe huyo maalum Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa ambaye pia ni mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. wakwanza kushoto Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Kabonero.  PICHA NA IKULU

Soko kubwa la bidhaa za kilimo EAC chachu ya maendeleo

$
0
0
WATANZANIA wametakiwa kutumia ukubwa wa soko la Afrika Mashariki kujiinua kiuchumi kupitia bidhaa zilizoboreshwa za kilimo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji),Dk. Doroth Mwaluko kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo (7th NRG) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF.
Katika hotuba yake hiyo kwenye Mkutano  huo uliokuwa unazungumzia mnyororo wa thamani katika kilimo kwa Afrika Mashariki,iliyosomwa na Ezamo Maponde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maendeleo ya Sekta Binafsi alisema ukubwa wa soko unaleta maana zaidi kama mifumo itaoanisha kuwezesha ukuaji wa soko na huduma zake.
Alisema katika mkutano huo kwamba Afrika Mashariki ina jumla ya wananchi milioni 172 huku asilimia 22 ya wananchi wake wakiishi katika miji.
Aidha alisema takwimu zinaonesha kwamba nchi hizo zina pato la taifa za dola za Marekani bilioni 172 kufikia Desemba 2017, linatosha kukuza mnyororo wa thamani wa bidhaa za kilimo.
Alisema katika mkutano huo unaozungumzia utafiti kuhusu maendeleo endelevu ya mchakato wa kuongeza mnyororo wa thamani Afrika Mashariki na kuimarisha mahusiano ya kinchi, kwamba kuna changamoto nyingi zinazokumbwa juhudi hizo na lazima zitafutiwe tiba.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni tamaduni na namna ya kizamani ya kuchakata bidhaa, kuingizwa kwa bidhaa zilizochakatwa kutoka ughaibuni, uzalishaji mdogo wa wakulima unaotokana na matumizi hafifu ya pembejeo, ukosefu wa taarifa za masoko na bei ya bidhaa zisizo na tija.
Dk Mwaluko alisema kwamba mkutano huo una maana kubwa kwa kuwa unasaidia kuianisha mambo, kuyatambua na kuyatafutia suluhu ili kutekeleza Azimio la Malabo la kuongeza tija katika kilimo na pia matumizi ya soko la ndani kuinua kilimo.
Alisema kwa sasa taifa kama la Tanzania lenye uzalishaji mkubwa wa mahindi, muhogo, viazi mbatata, viazi vitamu, ndizi, mtama na sukari halina sababu ya kuwa na wakulima maskini kwa kuwa soko lipo.
Alisema ili kuweza kufanikiwa ni vyema kuunganisha nguvu katika jumuiya kuondoa vikwazo na kuiweka sekta ya uchakataji imara kwa kuwezesha maendeleo ya kilimo na uchumi wa mataifa ya Afrika Mashariki.
Dk Mwaluko alisema mkutano huo ambao unafanyika kipindi cha pili cha uboreshaji wa kilimo wakati wa mabadiliko ya tabia nchi, wataalamu wanatakiwa kujikita kukabili changamoto zilizopo ili kuikuza sekta ya kilimo na kuwezesha viwanda vinavyotegemea mazao ya kilimo kukua.
Alisema kukosekana kwa taratibu mtambuka kunachochea changamoto zilizopo katika kilimo na hivyo ipo haja ya kuangalia sera na kushawsihi mabadiliko ili kukiidhi mahitaji ya sasa.
Alitaka katika maamuzi pia kutosahau nafasi ya kibiashara ya kimataifa katika ukuzaji wa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania.
Mkutano huo ulioendeshwa na ESRF kwa ushirikiano na taasisi ya CUTS International ya Geneva  ulijadili mada mbili zinazohusu uwekaji wa maunganiko katika mifumo inayoinua sekta ya kilimo na uchakataji wa bidhaa.
Akimkaribisha Mwakilishi wa Dk Mwaluko kuzungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida alisema kwamba mkutano huo ni matokeo ya tafiti zinazofanyika kuhusu maendeleo ya kilimo.
Alisema kwamba hakuna maunganiko ya moja kwa moja katika sera na sheria zinazogusa kilimo cha uchumi na kusema ipo haja ya wataalamu kuangalia na kushawishi masuala mtambuka ya kilimo kuangaliwa kwa pamoja.
 Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida wakati wa ufunguzi wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa-CUTS International Bw. Rashid Kaukab akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.
 Bw. Ezamo Maponde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maendeleo ya Sekta Binafsi akifungua mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji),Dk Doroth Mwaluko uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa-CUTS International Bw. Rashid Kaukab, Bw. Ezamo Maponde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maendeleo ya Sekta Binafsi akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji),Dk Doroth Mwaluko pamoja na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene wakati wa ufunguzi wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa TCCIA, Peter Lanya akishiriki kwenye mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.
 Bw. Ezamo Maponde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maendeleo ya Sekta Binafsi akichangia maoni wakati wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mtafiti mshiriki wa ESRF, John Shilinde (kushoto) akichangia maoni wakati wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF jijini Dar es Salaam.

WAAJIRI WASHAURIWA KUTOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WAPYA WA MABARAZA YA WAFANYAKAZI SERIKALINI

$
0
0
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael  akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la ofisi yake (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Lilian Denis.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael  akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la ofisi yake katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael  akikabidhi moja ya hati ya kiwanja kwa mtumishi wa ofisi yake,Bw. Jumbe Mgoha wakati wa kikao cha baraza  la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
 Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (kulia) akikabidhi moja ya hati ya kiwanja kwa mtumishi wa ofisi yake, Anna Zahoro  wakati wa kikao cha baraza  la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (wa pili kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora baada ya kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi yake  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA KUKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA UKONGA NA MAGOMENI KOTA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na baadhi ya wazee waliokuwa wakaazi wa nyumba za Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuona maendeleo ya ujenzi wa nyumba za ghorofa alizoziwekea jiwe  la msingi Aprili 15, 2017 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umesimama kwa sababu ambazo hazikuweza kujulikana mara moja.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alikofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwangalia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza  Julius Ntembala akipima nguzo wakati akikagua  maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za ghorofa za Magomeni Kota jijini Dar es salaam alizoziwekea jiwe  la msingi Aprili 15, 2017 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za ghorofa za Magomeni Kota jijini Dar es salaam alizoziwekea mnamo  Aprili 15, 2017 ambapo mpaka sasa ujenzi wake umesimama alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alikofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wana familia ya moja ya nyumba za askari Magereza huko Ukonga jijini Dar es salaam alikotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari hao alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumamosi Machi 16, 2019.PICHA NA IKULU.






JAJI SAMMATA AWAASA WANASHERIA KUKEMEA RUSHWA NA KUWA WAAMINIFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO

$
0
0
*Awataka kuwa mstari wa mbele kukemea rushwa na kuwa wawajibikaji

* Mkurugenzi wa WAJIBU ampongeza Rais Magufuli katika ufuatiliaji na utekelezaji

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
TAASISI ya WAJIBU inayojishughulisha na fikra ya uwajibikaji wa Umma leo Machi 16 imefanya mdahalo mkubwa uliokuwa na mada ya Mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma na mahakama uliowakutanisha wanafunzi wa sheria kutoka chuo cha sheria nchini pamoja na Jaji mkuu mstaafu Barnabas Sammata wakiongozwa na Mkurugenzi wa taasisi ya WAJIBU na CAG mstaafu Ludovick Utouh pamoja na viongozi kutoka TAKUKURU na Azaki mbalimbali.

Akizungumza katika mdahalo huo na wanafunzi wa chuo cha sheria nchini jaji mkuu mstaafu Barnabas Sammata amesema kuwa kuwepo kwa kansa ya rushwa nchini kunasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo kurahisha upatikanaji wa huduma,bidhaa na mapato, kupata usichostahili ili kumuumiza mpinzani, kukwepa kupunguziwa kulipa mapato, kodi au faini pamoja na kupata msaada wa kisheria.

Akieleza madhara ya rushwa Jaji Sammata amesema kuwa kansa hiyo ni kuwanyang'ganya wananchi haki yao hasa matarajio yao ya baadaye ikiwemo maisha bora na maendeleo waliojiwekea, amesema kuwa rushwa  hujenga chuki kwa kuwa huvunja haki na waathirika huchukua sheria mkononi wakiona vyombo husika havijatenda haki.

Jaji Sammata ametoa maoni yake na kusema kuwa ili kuepuka hayo yote lazima elimu zaidi kwa umma itolewe na kushauri vyama vya siasa hasa chama tawala na vyombo vya dola kukemea vitendo hivyo huku akihimiza taasisi za dini zishiriki katika kupinga kampeni hiyo kwa kutoruhusu mapato ya rushwa kutunisha kampeni hizo.

Aidha amewataka wanasheria nchini kote kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo hivyo na kuwa waaminifu kwani rushwa bila kujali ukubwa au udogo wake zinaathiri maendeleo ya jamii huku akisisitiza watakaokiuka taratibu za kisheria kuchukuliwa hatua kali kwa watakaokutwa na vitendo vya aina hiyo wakiwemo wanasheria na waandishi wa habari watakaokutwa na hatia dhidi ya rushwa kwani wao ndio ngao muhimu katika kumulika vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa taasisi WAJIBU Ludovick Utouh amesema kuwa taasisi hiyo ni changa na alianzisha baada ya kuona uwajibikaji haukuwa imara na hakukuwa na ushirikishwaji wa wananchi moja kwa moja.

Ameeleza kuwa amefurahishwa na kazi ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli kwa kuangalia kwa umakini suala la wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika mbalimbali hali inayoleta mgongano wa kimaslahi, Utouh amesema kuwa suala hilo amepambana nalo alipokuwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) lakini wengi hawakumwelewa ila Rais Magufuli amelitendea kazi mara tu baada ya kuingia madarakani.

Pia Kaimu mkuu wa Chuo cha Sheria nchini Dkt Luqman Zakayo amesema kuwa mada hiyo ni muhimu sana katika kujenga dhana nzima ya uwajibikaji kwa wanafunzi hao ambao ndio viongozi wa kesho na amewashukuru wanafunzi waliojitokeza katika mjadala huo.

Aidha amemshukuru jaji mkuu mstaafu Barnabas Sammata kwa kuwatengeneza vijana wengine wengi wanaofuata nyayo zake hasa katika kuwarithisha vijana hao mambo mazuri yanayozidi kujengwa miongoni mwao.

Vilevile ameipongeza taasisi wa WAJIBU kwa shughuli wanazozifanya ambazo kwa ukubwa wake zinagusa kila sekta katika jamii.

 Jaji Mkuu mstaafu na Mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama na amewaasa wanasheria hao kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo hivyo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya WAJIBU na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Seeikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama, Leo jijini Dar es salaam.
 Makamu mkuu wa chuo cha Sheria nchini Dkt. Luqman Zakayo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama,na ameishukuru taasisi ya WAJIBU kwa kuendelea kuandaa viongozi wa baadae kupitia midahalo ya namna hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Mkuu mstaafu na Mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata(kushoto) akimkabidhi zawadi ya vitabu Makamu mkuu wa chuo cha Sheria nchini Dkt. Luqman Zakayo(kulia) wakati wa mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama,na ameishukuru taasisi ya WAJIBU kwa kuendelea kuandaa viongozi wa baadae kupitia midahalo ya namna hiyo, leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya WAJIBU na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Seeikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh.
 Mwakilishi wa taasisi ya TWAWEZA Anastazia Lugaba  akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama, ambapo amesema kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni ya wote na amewataka wanasheria hao kuhudumia wananchi kwa haki na usawa  leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha sheria nchini wakichangia mada na kuuliza maswali katika mjadala huo uliolenga kujadili mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma za haki na mahakama, leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya washiriki waliohudhuria mdahalo huo ambao ni wanafunzi wa chuo cha sheria nchini wakifuatilia mjadala huo uliohusu  Mapambano ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama, leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI NCHINI WATAKIWA KUHAKIKISHA FEDHA ZA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI ZINAWAFIKIA WALENGWA

$
0
0
Wakurugenzi Watendaji katika halmashauri za wilaya nchini wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vema fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini zinawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) wakati wa ziara ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo mkoani Mtwara ikiwa ni pamoja na kujiridhisha namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unavyotekelezwa.

Mhe. Rweikiza amekemea tabia ya baadhi ya Wakurugenzi Watendaji katika halmashauri kuelekeza fedha zilizotengwa kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika matumizi mengine badala ya kuwanufaisha walengwa ambao ni kaya maskini na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja.
“Wakurugenzi Watendaji, mnao wajibu wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha maisha ya kaya maskini zote nchini kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini,” Mhe. Rweikiza amesisitiza.

Aidha, amewapongeza wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Namela, Manispaa ya Mtwara kwa kutumia vizuri ruzuku wanayopata katika kuboresha maisha yao ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za kisasa na kujishughulisha na ufugaji wa mbuzi na kuku. Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka wanufaika wa Mpango kuendelea kutumia vema ruzuku wanayopata ili waweze kuondokana na umaskini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewaasa wanufaika hao kuwekeza ruzuku hiyo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazowaongezea kipato na kuondokana na umaskini. Kwa upande wao, wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kijiji cha Namela, wameishukuru Serikali kuwawezesha kupitia TASAF kwani wameweza kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Mmoja wa wanufaika hao, Bw. Abdallah Chingwalu amesema, ametumia ruzuku aliyoipata kujenga nyumba ya kisasa, kununua mbuzi wawili ambao amewafuga na kufikia mbuzi 17, kufuga kuku ambao wamefikia 20 hivi sasa. Mnufaika mwingine, Bi. Fatuma Shamte, ametoa ushuhuda kuwa, ruzuku anayoipata imemsaidia kupata milo mitatu kwa siku tofauti na awali, kusomesha wajukuu na kufanya ukarabati nyumba yake ambayo haikuwa katika hali nzuri.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umelenga kuziwezesha kaya zote maskini kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu katika kuendesha maisha ya kila siku.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Namela Manispaa ya Mtwara wakati wa ziara ya kamati yake ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwahimiza wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuzitumia vizuri ruzuku wanayoipata.
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Namela Manispaa ya Mtwara wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) alipokuwa akizungumza nao kuhusu umuhimu wa TASAF wakati wa ziara ya kamati yake ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Mtwara.

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKEZA ZAIDI CHUO CHA NIT

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
SERIKALI imeshauriwa kuwekeza fedha nyingi kwa ajili ya kusaidia Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT), ili kukiwezesha chuo hicho kuzalisha wataalamu wa ndani watakaojenga viwanja, reli na kupata madereva wa treni na utengenezaji wa mabehewa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na NIT  leo Machi 16.2019  jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso amesema,  chuo hicho kimekuwa kikifanya ubunifu mkubwa utakaoleta mapunduzi kwa maendeleo ya nchi.

Amesema, pamoja na kazi nzuri wanayoifanya  ya kuzalisha wataalamu katika sekta hiyo, lakini bado  wanakabiliwa na  changamoto ya fedha ambayo serikali inapaswa kuitatua ili kuongeza ubunifu katika vitu mbali mbali.

Amesema, kama serikali itaweekeza fedha nyingi kwa ajili ya bunifu zinazofanywa na wanachuo hicho, basi hakutakuwa na haja ya kuwapeleka wakufunzi nje ya nchi ili kupata mafunzo badala yake tutakuwa tumezalisha wataalamu wetu wa ndani, na kuipunguzia nchi ya Tanzania garama kubwa.

"Uwekezaji mkubwa utasaidia kupata wataalamu watakaojenga reli ya kati, ujenzi wa meli, kukarabati mabehewa na vichwa vya treni", amesema Kakoso


Amesema, mtaalamu mmoja akipelekwa nje ya nchi hutumia Sh milioni 300 garama ambayo ni kubwa saba tunapaswa kuipunguza  sisi wenyewe kuwekeza hapa nchini  ili tupate wataalamu wa kutosha  kuliko kusubiri wanaotoka nje ya nchi ambao gharama yao ni kubwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (anayeshughulikia Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye amesema serikali imetoa kipaumbele kwa sekta ya uchukuzi na usafirishaji hivyo zimekuwa tegemezi nchini.

Nditiye amesema kupitia chuo hicho pekee Afrika Mashariki na Kikanda, kuna malengo makubwa ya kuhakikisha kuwa chuo kinazalisha wataalamu wengi watakaosaidia ujenzi wa reli ya kati, wahudumu ndani ya ndege, wahudumu katika mabehewa na madereva wazuri wa treni.

Ameongeza, serikali imeingia dhamana ya kutekeleza miradi mikubwa miwili inayofanywa chuoni hapo ambayo ni mkopo wa Benki ya Dunia (WB) na kutoka China ikiwa na lengo la kuwezesha shule ya mamlaka ya anga.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa amesema miradi hiyo miwili ambayo serikali imewadhamini ni mikopo ya masharti nafuu ambapo  WB imetoa Sh bilioni 50.
Alisema fedha hizo ni maalum kwa ajili ya kuwafundisha wataalamu wa anga, marubani, wahandisi, wahudumu wa ndege, wataalamu wa masoko na menejimenti ya anga.

Pia alisema mkopo uliotolewa na China ambao ni Sh bilioni 150, unalenga kukisaidia kuwa Chuo Kikuu cha  Kikanda kwa kutoa mafunzo ya reli, kuboresha wahandisi wa relii, wahudumu, Mawasiliano na menejimenti ya usafiri wa reli ya kisasa. Aidha amesema, chuo kinatarajia kuanza kutoa mafunzo ya sayansi ya bahari na eneo kutoka mkoani Lindi limepatikana  ambako watakuwa wanajenga meli na kufanya matengenezo. Huku kwa upande wa usafiri wa anga, wataalamu tunawazalisha kwa gharama nafuu," alieleza Profesa Mganilwa.

"Tunazidi kuwahamasisha wasichana kusoma masomo ya sayansi ili wajiunge nasi katika sekta hii ya usafirishaji kwani hivi sasa ni asilimia 35 tu ya wanawake ambao wanachukua masomo haya chuoni hapa," alieleza. Kamati hiyo ilitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo kuona gari yenye uwezo wa kutembea  umbali wa kilometa 90 bila kutumia mafuta na Kitengo kinachoshughulikia masuala ya anga na urubani.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakosa akizungumza na  waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya siku moja ambapoh wametembelea miradi mbali mbali ya chuo cha NIT na  kukagua maendeleo na changamoto  katika chuo cha hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji NIT,  Profesa Zacharia Mganilwa, akiwaeleza waandishi wa habari mafanikio na changamoto za miradi mbali mbali inayofanywa na chuo hicho cha NIT, wakati wa ziara ya Kamati ya ya kudumu ya binge ya Miundombinu.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakosa aliyekaa kulia akikagua gari lililotengenezwa na wahitimu wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT),  wakati wa ziara ya siku moja ya kamati hiyo shuleni iliyofanyika leo katika chuo hicho cha jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni mbunifu wa gari hilo Gabriely Jeremia na wanaoshuhudia ni baadhi ya wabunge wa kamati hiyo.
 Mbunge wa Vunjo, kupitia tiketi ya NCCR, James Mbatia akiendesha gari lililobuniwa na wahitimu wa chuo cha Usafirishaji, Gabriely Jeremia, hayupo pichani na Mtatiro Boniphace kulia wakati wa ziara ya Kamati ya ya kudumu ya bunge ya Miundombinu iliyofanyika leo chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

WASOMI NCHINI KUANDIKA HISTORIA UPYA HISTORIA YA UKOMBOZI WA TANZANIA

$
0
0
Na Tiganya Vincent
WASOMI wa Kitanzania kutoka  Vyuo Vikuu wametakiwa kuandika historia ya Watanzania mbalimbali waliotoa mchango mkubwa katika kupinga ukoloni nchini ili vijana waweze kupata picha halisi ya harakati za mapambani dhidi ya wakoloni.

Kauli hiyo imetolewa leo wilayani Urambo na Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo ya urithi wa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.

Alisema waandishi wengi waliondika historia ya Tanzania ikiwemo mapambano dhidi ya ukoloni walitoka nje ya nchi na kuandika kwa matakwa yao na hivyo kuacha baadhi ya mashujaa wengi waliopinga kutawaliwa na wakoloni bila kuandikwa.

Dkt. Mwakyembe alisema katika mikoa mbalimbali imebainika kuwepo kwa watu walitoa upinzani mkali kwa Wajerumani na Waingereza lakini hakuna sehemu wanapotajwa katika vitabu wa historia za nchi ya Tanzania.

“Kuna mama Liti kutoka Singida alipambana na Wajerumani kwa kutumia nyuki lakini hakuna vitabu wa historia vinavyomzungumzia…kuna mama mmoja Manyoni ambaye yupo hai hadi leo alimuokoa Mwalimu Nyerere asikamatwe na Waingereza baada ya kumvalisha baibui na kisha kuungana naye lakini hakuna alipoandikwa” alisema.

“Mtemi Isike ni miongoni wa viongozi waliotoa upinzani mkubwa kwa Wajerumani na baadae akajipiga risasi kwa kukataa kukamatwa na Wajerumani , lakini hakuna vitabu vya historia vinapoeleza…tuna utajiri wa historia kubwa lakini iliyosndikwa ni sehemu kidogo sana” aliongeza.

Alisema hatua hiyo imesababisha vijana wengi kutokuwa na historia kubwa ya wapigania uhuru hapa nchini.

Dkt.Mwakyembe alisema wakati umefika wa Wasomi na wataalamu waliopo katika Vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kukaa chini na kufanya utafiti na kuandika historia ya urithi wa ukombozi hapa nchini kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mmoja wa Wazee wa Urambo John Samwel alisema Serikali imefanya vizuri kuanza kuyatambua maeneo ya urithi wa kihistoria ya ukumbozi kwa ajili ya kuandika historia ya pana ya mapambano dhidi ya ukoloni nchini Tanzania.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuondoa upotoshaji uliofanywa na waandishi kutoka mataifa ya nje ya bara la Afrika ikiwemo kudai uvumbuzi wa Ziwa Victoria , Mlima Kilimanjaro kugunduliwa na wazungu wakati walikuwepo Watanzania wenyeji wa maeneo hayo.

Samwel alisema ni vema historia iandike ukweli ili kuepuka kuwapotosha vijana na vizazi vijavyo.
 Nyumba ambayo wanaharakati wa kudai Uhuru nchini kutoka Wilayani Urambo walikuwa wakiendeshea vikao vyao vya siri na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
 Mratibu wa Programu yaUurithi wa Ukombozi wa bara la Afrika Ingiahedi Mduma akijibu hoja mbalimbali kwenye  mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wadau mbalimbali wakati wa ziara ya kikazi  leo wilayani Urambo ya kutembelea maeneo ya urithi wa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.
 Katibu Tawala Wilaya ya Urambo Pascal   Byemelwa akichangia hoja kwenye    mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wadau mbalimbali wakati wa ziara ya kikazi  leo wilayani Urambo ya kutembelea maeneo ya urithi wa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.
 Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa( kushoto)  akitoa taarifa ya Wilaya kuhusu masuala ya harakati za uhuru  kwenye  mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe( wa pili kutoka kushoto)  na wadau mbalimbali wakati wa ziara ya kikazi  leo wilayani Urambo ya kutembelea maeneo ya urithi wa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Urambo Mussa Shaban (wa pili kutoka kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adamu Malunkwi( kulia) 
 Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe( wa pili kutoka kushoto) akizungumza  na wadau mbalimbali wakati wa ziara ya kikazi  leo wilayani Urambo ya kutembelea maeneo ya urithi wa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.
 Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye kaunda suti nyeusi) akizungumza na wazee waharakati wa kudai uhuru wa Tanganyika kutoka wilayani Urambo wakati wa ziara ya kikazi  leo wilayani Urambo ya kutembelea maeneo ya urithi wa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika.
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto ) akianga na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Urambo Mussa Shaban (kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adamu Malunkwi( wa pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa ( kushoto) mara baada ya n ziara ya kikazi  leo wilayani Urambo ya kutembelea maeneo ya urithi wa historia ya ukombozi wa Bara la Afrika. Picha na Tiganya Vincent

RAIS DKT.SHEIN AFUNGUA SEMINA YA KITAIFA KUHUSU MASUALA YA ARDHI NA RASILIMALI ZISIZOREJESHEKA ZANZIBAR

$
0
0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Semina ya Kitaifa Kuhusiana na Masuala ya Ardhi na Rasilimali Zisizorejesheka  Zanzibar, ikiwashirikisha Wadau wa Ardhi na Sheria , inliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni , leo 16-302019.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kulia.Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabti Kombo, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim na Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Mhe. Juma Ali Khatib, wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Semina Kitaifa Kuhusu Masuala ya Ardhi na Rasilimali Zisizohamishika Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
 WAZIRI wa Ardhi Maji Nyumba na Nishati Mhe. Salama Aboud Talib, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindsuzi Mhe,. Dk.Ali Mohamed Shein, kufungua Semina hiyo ya Siku moja kwa Watendaji wa Serikali iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed, akichangia Mada iliowasilishwa kuhusu Matumizi ya Ardhi Zanzibar wakati wa Semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MWANASHERIA Mkuu wa Serekali Mhe. Said Hassan Said, akichangia Mada ya kutowa ufafanuzi wa Kisheria wakati wa Semina ya Kitaifa Kuhusu Masuala ya Ardhi na Rasilimali Zisizorejesheka Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MKURUGENZI wa ZIPA Ndg Salum Nassor Khamis, akichangia Mada kuhusiana na Matumizi ya Ardhi wakati wa semina hiyo iliowashirikisha Wadau kutoka sehemu mbalambali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.(Picha na Ikulu)
 JAJI wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe. Rabia Mohammed, akichangia wakati wa Semina hiyo iliowashirikisha Wadau mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuzungumzia Matumizi ya Ardhi Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 KATIBU Mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh.Abdallah Talib, akichangia Mada kuhusiana na Matumizi ya Ardhi wakati wa semina hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
 AADHI ya Washiriki wa Semina ya Kitaifa ya Kuhusiana na Masuala ya Ardhi na Rasilimali Zisizorejesheka Zanzibar, wakifuatilia hafla hiyo katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar  leo.16-3-2019.(Picha na Ikulu)

WAKUU WA IDARA ZA ARDHI WATAKAOKALIA HATI ZA ARDHI OFISINI SASA KUKIONA

$
0
0
Na Munir Shemweta, MISENYI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema kuanzia sasa Mkuu wa Idara ya Ardhi atakayekutwa amekaa na hati ya ardhi kwa muda mrefu   bila kuipeleka ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda kwa ajili ya kukamilisha taratibu za utolewaji hati hiyo basi Mkuu huyo ataondolewa katika nafasi yake.

Dkt Mabula alisema hayo jana tarehe 15 Machi 2019 alipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.

Kauli hiyo ya Dkt Mabula inafuatia kukuta baadhi ya hati katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi zikiwa kwenye masijala ya ardhi tangu mwaka 2017 bila kupelekwa ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukamilishwa ili wahusika wapatiwe hati.

Alisema, baadhi ya halmashauri alizozitembelea wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi amebaini wakuu wengi wa idara ya ardhi wakiwa na hati kwenye ofisi zao kwa muda mrefu bila kufanya jitihada zozote za kuhakikisha hati hizo zinaenda ofisi ya Kamishna kwa ajili ya kukamilishwa ili wahusika wapatiwe hati.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi, ucheleweshaji utoaji hati miliki za viwanja na mashamba siyo tu unawakera wananchi bali unaikosesha serikali mapato ya kodi ya ardhi kwa kuwa wananchi wanakuwa hawajamilikishwa ardhi kwa mujibu wa sheria.

Dkt. Mabula ametoa onyo kali kwa Mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera kwa kukaa na hati kwa zaidi ya miaka miwili kwenye ofisi yake bila kuwasilisha  hati hizo ofisi ya Kamishna Msaidizi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukamilishwa na hatimaye kukabidhiwa kwa wahusika  kwa haraka na wakati.

Katika hatua nyingine Dkt Mabula amewataka wananchi wa miji ya Kyaka na Mtukula katika wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera kuchangamkia zoezi la urasimishaji makazi holela ambalo limeonekana kusuasua katika miji hiyo.

Akizungumza na wakazi wa Kyaka na Mtukula kwa nyakati tofauti Dkt Mabula alisema kuwa, haridhishwi kabisa na namna kasi ya urasimishaji inavyoendelea katika miji hiyo ambapo takwimu zinaonesha wananchi waliojitokeza kwenye zoezi hilo ni ndogo ukilinganisha na wakazi wa miji hiyo.

Dkt Mabula ametolea mfano wa Mji wa Mtukula katika kitongoji cha Katede kuwa, pamoja na eneo hilo kuwa na Kaya 842 zenye wakazi zaidi ya 3000 lakini ni watu 13 tu waliolipia fedha za kurasimishiwa maeneo yao na watu hao wamechangia jumla ya shilingi milioni moja na laki nane.

Aidha, Naibu Waziri Mabula amewataka wananchi wa miji ya Kyaka na Mtukula kutofanya maendelezo katika eneo lolote ambalo hawajajua mipango yake ili kuepuka kubomolewa na kupoteza haki zao kwa kujenga katika maeneo yasiyo ruhusiwa ambapo ameitaka halmashauri ya wilaya ya Misenyi kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa lengo la kuwa na miji iliyopangika.

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mji wa Mtukula wilayani Misenyi mkoa wa Kagera wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia sekta ya ardhi.
 Sehemu ya wananchi wa Mji wa Mtukula wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia sekta ya ardhi.
  Sehemu ya wananchi wa Mji wa Kyaka wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya majalada ya ardhi aliyoyakuta katika ofisi ya halmashauri ya Misenyi mkoa wa Kagera wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia sekta ya ardhi. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denis Mwila na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Elia Kamyanda na kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Misenyi Emanuel Samson.

QNET yatoa fursa ya ‘kufanya kazi kwa bidii na kuleta mabadiliko chanya

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda (katikati) na Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika Biram Fall (kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya bidhaa za QNET 2019 jijini humo. Kulia ni Mshauri wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wawakilishi, wafanyakazi na waalikwa wa QNET kuhusu maadili ya kazi kwenye uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za QNET jijini Dar Es Salaam jana.

………………………………………………………………………….

*Maelfu wa hudhuria maonyesho ya QNET Dar es salaam

*Watanzania kunufaika na bidhaa mbalimbali pamoja na fursa za biashara

Kampuni yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja QNET imeendesha maonyesho ya bidhaa na huduma zake jijini Dar es salaam siku ya tarehe 16 na 17 Machi 2019. 

Maonyesho yenye jina la Absolute Living, (Kuishi kikamilifu) sambamba na falsafa ya bidhaa za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja, huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa zake na huduma kwenye masoko mapya. Onyesho hilo pia ilikuwa kama jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kufahamu kuhusu QNET na mtindo wake wa biashara. 

Nadharia ya Absolute Living (Kuishi kikamilifu) inaakisi juhudi za QNET za kukuza mwendendo wa kujali afya, mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, ikiwa inatilia mkazo katika Afya, ustawi na elimu. 

Mgeni rasmi katika hfla hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda alisema ‘Maisha yangu ni mfano wa kufanya kazi kwa bidi na kujiamini katika kitu chochote unachokifanya. Hii ndiyo njia pekee yakuleta mabadiliko na maendeleo kwa mtu, familia na jamii”. 

Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari Meneja Mkuu wa QNET kwa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall alisema kwamba, “Tunatoa aina mbalimbali za bidhaa za kiwango cha juu na huduma kwa wateja wetu kuwasaidia waweze kuishi maisha yenye uwiano sahihi, na pia kutatua tatizo la msingi kama vile elimu, ufahamu, na maendeleo binafsi kupitia program za mafunzo yetu, ambayo yanawasaidia katika safari yao ya kujiajiri mwenyewe. 
 
Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao kama vile SELI/qLearn, mpaka katika vifurushi vya sikukuu kama vile Tripsavr, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu kama vile Bio Disc3, virutubisho kama EDGE, na saa za mkononi kama Bernhard H. Mayer, QNET ina aina mbalimbali za kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu. Katika kitovu cha yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya Kuishi Kikamilifu “Absolute Living”


Zaidi ya watu elfu mbili walipata fursa ya kuona bidhaa za mfano katika onyesho hilo na kufundishwa namna ya matumizi ya bidhaa na faida zake kwa wateja na watumizji wa mwisho. Kwa kuongezea, wataalamu wa bidhaa na biashara walikuwepo kwaajili ya kujibu swali lolote kutoka kwa wageni ili kuelewa vizuri ulimwengu wa QNET.

Maonyesho ya Dar es salaam yanafuata mfululizo wa maonyesho kama hayo yaliyofanikiwa nchini Togo, Guinea, Ivory Coast, Senegali, Burkina Faso na Cameroon mwaka jana.

Msafara wa maonyesho utasisimama katika mji wa Kumasi, Ghana, baada ya Dar es salaam kuanzia tarehe 23 mpaka 24 Machi mwaka 2019.
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images